Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48979 articles
Browse latest View live

CCM YAFANYA UTEUZI WA MAJINA YA WANACHAMA WATAKAOGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA HICHO NA JUMUIYA ZAKE NGAZI YA MKOA NA TAIFA

$
0
0

 


Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) imekutana kikao cha kawaida Jumapili 13 Novemba, 2022 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Chama, Dodoma.

Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imefanya uteuzi wa majina ya wanachama watakaogombea nafasi za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake katika ngazi ya Mkoa na Taifa kwa mujibu wa katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2022 Ibara ya 82(1). Kwa upande wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya za CCM ngazi ya Taifa walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-


NAFASI: MWENYEKITI UVCCM TAIFA

1.  Farid Mohamed HAJI

2.  Kassim Haji KASSU

3.  Mohamed Ali MOHAMED (KAWAIDA)

4.  Abdallah Ibrahim NATEPE


NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA

1.  Khadija Khalid ISMAIL

2.  Dorice John MGETTA

3.  Victoria Charles MWANZIVA

4.  Rehema Sombi OMARY


NAFASI: MWENYEKITI UWT TAIFA

1.  Gaudentia Mugosi KABAKA

2.  Kate Sylvia KAMBA

3.  Dkt. Wemael Allen CHAMSHAMA

4.  Mariam Mohamed LULIDA

5.  Mary Pius CHATANDA

 

NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI UWT TAIFA

1.  Latifa Nasser AHMED

2.  Thuwaybah Edington KISSASI

3.  Hafsa Said KHAMIS

4.  Zainab Khamis SHOMARI

 

NAFASI: MWENYEKITI WAZAZI TAIFA

1.  Dkt. CPA. Edmund Bernard MNDOLWA

2.  Fadhili Rajabu MAGANYA

3.  Bakari Nampenya KALEMBO

4.  Said Mohamed MOHAMED (DIMWA)

5.  Mwanamanga Juma MWADUGA

6.  Ally Maulid OTHMAN

7.  Ali Khamis MASUDI

8.  Hassan Haji ZAHARA

 

NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI WAZAZI TAIFA

1.  Haidar Haji ABDALLA

2.  Dkt. Wemael Allen CHAMSHANA

3.  Fatma Abeid HAJI

4.  Rachel Ntiganyigwa KABUNDA

5.  Neema George MTURO

6.  Zahoro Salehe MOHAMED

7.  Dogo Idd MABROUK

 

Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hizo kwa ngazi ya Taifa utafanyika tarehe 24-29 Novemba, 2022. Wagombea wote wanakumbushwa kuheshimu Kanuni za uchaguzi za CCM na misingi ya chama kwa kufanya siasa safi na kuzingatia maadili ya Chama wakati wote.

Aidha Orodha ya majina ya wagombea uongozi Chama na Jumuiya zake ngazi ya Mkoa yatatumwa katika mikoa husika.

 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

 

Shaka Hamdu Shaka

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa

Itikadi na Uenezi.

13 Novemba, 2022


Washindi 75 wa NMB MastaBata KoteKote wamechomoka na Laki moja kila mmoja na Pikipiki

$
0
0

 


Zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 10.5 za droo ya kwanza ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ zimepata wenyewe mwishoni mwa wiki, ambapo washindi 76 walipatikana, 75 kati yao wakijishindia fedha kiasi cha Sh. Mil. 7.5, huku Asumwisye Stallone akiibuka na zawadi ya bodaboda yenye thamani ya Sh. Mil. 3.
 
Kampeni hiyo, ambayo inaendeshwa na Benki ya NMB kwa ushirikiano na Mastercard International, ikilenga kuhamasisha matumizi ya NMB Mastercard kufanya malipo, Lipa Mkononi kwa kuskani QR na kufanya malipo mtandaoni huku zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 350 zitatolewa katika miezi mitatu ya kinyang’anyiro hicho.
 
Akizungumza kabla ya droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa NMB, Manfredy Kayala, alisema malengo makuu ya kampeni hiyo iliyoanzishwa mwaka 2018, ni kuihamasisha jamii katika kuachana na matumizi ya pesa taslimu ‘cashless’, lakini pia ikilenga kurejesha sehemu ya faida yao kwa wateja wao.
 
Kayala alifafanua kuwa, ukiondoa bodaboda moja na pesa taslimu kwa washindi 75 wa kila wiki, NMB MastaBata Kote Kote itatoa zawadi kwa washindi 49 wa droo za mwisho wa mwezi, sambamba na bodaboda mbili, na droo ya fainali itazawadia safari za Dubai kwa washindi na wenza wao kwa siku nne.
 
Mbele ya Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema NMB MastaBata Kote Kote ni muendelezo wa benki yake katika kuwafanya wateja na Watanzania kugeukia utamaduni chanya wa matumizi yasiyohusisha pesa taslimu.
 
Alifafanua kuwa, MastaBata Kote Kote inagusa wateja wote wa ndani na nje ya nchi wanaotumia kadi za Mastercard au Lipa Mkononi kaa kuscan QR na kutoa wito kwa Watanzania kuhakikisha wanatumia kadi zao katika kufanya malipo na miamala mbalimbali ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda.
 
Kampeni hii ya NMB MastaBata KoteKote itaendelea kwa takribani miezi mitatu. Kutakuwa na washindi wa kila wiki, kila mwezi na na wale wa Grand Finale. Wateja wanapaswa kufanya malipo kwa kadi Ya NMB Mastercard au Lipa Mkononi (mastercard QR) ili kujiwekea nafasi ya kushinda.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, akibonyeza kitufe cha kompyuta kuchezesha droo ya kwanza ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ inayohamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mlimani City, Deogratius Kawonga na Kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi na Biashara wa NMB, Manfredy Kayala.

HUYU NI MFALME WA USSD BETI NA KITOCHI

$
0
0

 


HAIJALISHI unatoka familia gani ili uwe Mfalme, Yeyote aliyepo kwenye famila ya Meridianbet ni mfalme wa Maisha yake, na Leo Meridianbet wanamleta kwenu Mfalme wa Beti na Kitochi kwa USSD.

Mfalme huyu anaitwa Zamiru Mohammed kutoka Chalinze, Gwiji aliyejishindia Pesa Taslimu TZS 1,324,878/= Milioni moja, Laki tatu na Elfu Ishirini na nne, Mia nane sabini na nane, alibeti kwa dau la 2,500/= na mkeka wake ulikuwa na Odds kubwa ya 529.95.

Kwake haikuwa ngumu kumuua Manchester City aliyekuwa Etihad dhidi ya Brentford, huu ni ujasiri mkubwa sana, hakuishia hapo alimfuata RB Leipzig akiwa ugenini na kumpa ushindi. Napoli na Udinese akaweka GG, Kupanga ni kuchagua Beti na kitochi sasa na uwe Mfalme.

Mfalme Zamiru yeye anajishughulisha na biashara ndogo ndogo za uwakala wa kutuma na kutoa pesa kwa mitandao ya simu, alipopigiwa simu ya ushindi alikuwa na haya ya kusema;

“Mimi huwa nabeti pesa nyingi kuanzia Elfu kumi, lakini safari hii sikuwa najiamini ikanibidi nibeti kwa 2,500/= na kweli mkeka wakati ukatiki. Nina furaha kushinda pesa hizi nitazitumia kuongezea msingi wa biashara yangu”

“Mara ya mwisho nilikuja na Rafiki yangu kwenye ofisini za Meridianbet makao makuu, nilimsindikiza kuja kuchukua Bodaboda yake aliyoshinda kwenye promosheni ya mwezi uliopita, na mimi nikatamani kubeti na kitochi, hatimaye bahati imekuwa kwangu nimeshinda Milioni Moja na Laki tatu”. Alisema Mfalme wa beti na kitochi- Zamiru.

Beti na kitochi ni rahisi sana kujishindia kwani haina machaguo mengi yanayochanganya na pia dau lake ni kuanzia 250/= TZS unatandika mkeka wako wa timu unazozitaka. Piga *149*10# Kubeti sasa na Kitochi, ujipatie odds kubwa.

N.B Meridianbet wana promosheni nyingi zinazoendelea hivi sasa, Ukibeti kwa kitochi kwa kupiga *149*10# kwa dau la kuanzia 250/=TZS unaweza kujishindia Bajaji Mpyaa au TV ya kisasa yenye Inchi 50. Beti na kitochi sasa uwe Mfalme wa Maisha yako.

MJI WA KIBAHA WAIMARISHA MAHUSIANO NA GOTLAND KWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA USAWA WA JINSIA

$
0
0

 

Picha ya Pamoja
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina Wilson akizungumza wakati wa Kikao cha Madiwani Kibaha.

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani kwa kushirikiana na Shirika la Elimu Kibaha pamoja na Mji wa Gotland ya nchini Sweden zinatekeleza mradi wa Usawa wa jinsia ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Dunia.

Katika utekelezaji wa malengo hayo Tanzania ni nchi moja wapo kati ya nchi 196 wanachama wa Umoja wa Mataifa zinazotakiwa kutekeleza malengo hayo.

Akizungumzia mahusiano kati ya halmashauri ya Mji wa Kibaha na Mji wa Gotland ,katika kikao Cha madiwani ,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina Wilson alieleza, wamejikita katika Mradi wa jinsia ni Lengo namba 5 ambalo linataka kuwe na usawa ambao hautomuacha nyuma msichana Wala mvulana.


Selina alieleza, mradi mwingine ni mradi wa Sekondari kwa Mji na Shirika la Elimu ili kuwawezesha wanafunzi kuelewa nchi inatekeleza malengo ya maendeleo endelevu.


"Lipo lengo linalosisitiza usawa katika elimu na kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike kujiamini na kuhakikisha wanakuwa miongoni mwa sehemu ya kuleta mabadiliko."

Nae mratibu kutoka Mji wa Gotland Eva Flemming alisema, wamekuja ujumbe wa watu nane ili kujifunza masuala mbalimbali ya shughuli za Halmashauri kwa kulinganisha na kwao.

Alisema,wametembelea pia shule ya Bundikani na Kibaha Sekondari kujionea mradi wa usawa wa jinsia na elimu Sekondari.

Awali mratibu wa safari kutoka maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji Kibaha, Anita Lyoka alifafanua tarehe 18-23 September mwaka huu timu kutoka Halmashauri hiyo ilisafiri kwa ajili ya kwenda kuhudhuria kikao Cha kamati tendaji ya usimamizi wa miradi ya uhusiano baina ya Mji wa Gotland na Kibaha.

"Tumejifunza mambo mengi ikiwemo kutokaa na utekelezaji wa Jambo ,hakuna masuala ya tunasubiri mchakato,"upangaji mzuri wa masoko mfano masoko ya mitumba ambayo mtu yeyote anaweza kwenda kuuza ama kutoa vitu asivyohitaji kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji"Hii inatunza Mazingira kwasababu watu hawachomi wala kutupa vitu hivyo"alieleza Anita.

Alitaja mambo mengine kuwa ni jamii ikielemishwa inaweza kubadilika na kutunza urithi wa rasilimali kwa faida ya vizazi vijavyo.

Anita alibainisha, mipango miji inazingatia utekelezaji wa Maendeleo endelevu ambapo Vijijini na mjini kumepangwa vizuri kwa nafasi na miundombinu ya barabara imeunganishwa maeneo yote, matumizi ya mabasi yanayotumia Nishati ya umeme yanasaidia utunzaji wa Mazingira na ushirikiano mzuri wa wafanyakazi na watendaji katika idara mbalimbali katika mji wa Gotland.

Mji wa Kibaha na Gotland Sweden ulianza mahusiano toka mwaka 2006.

RAIS SAMIA KUKUTANA NA MABALOZI ZANZIBAR

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akitoa tathmini ya mkutano wa mabalozi unaoendelea Zanzibar. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika mkutano wa Mabalozi unaoendelea Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwasilisha hotuba yake kwa mabalozi (hawapo pichani). Mkutano huo umeanza leo Zanzzibar na utamalizika tarehe 21 Novemba, 2022.
Sehemu ya mabalozi wakifuatilia kikao.
Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakiongozwa na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Amani, Balozi Stephen Mbundi wakifuatilia kikao.


Emirates Skyward watamba katika msimu wa sikukuu wakiwa na ofa ya maelfu ya maili

$
0
0

 


EMIRATES Skywards imeanza msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka kwa ofa za kushangaza mwaka huu. Mpango wa uaminifu utakuwa ukitoa ofa maalum kila mwezi ili kuwapa wanachama njia zaidi za kuchuma maelfu ya maili kwa kila safari ya ndege, hoteli, kukodisha magari, misururu ya ununuzi na zaidi.

Kwa sasa hivi, hadi tarehe 18 Novemba, wanachama wanaweza kuchuma maelfu ya maili na washirika wafuatao kama vile Rotana Hotels na kupata maili mara mbili kwa kukaa hotelini kote Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya Mashariki na Uturuki. Hoteli nyingine za Rotana zinazopatikana barani humo pamoja na Johari Rotana jijini Dar es Salaam, ziko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri na Morocco.

Wanachama wa Emirates Skywards wana sababu zaidi za kusherehekea mwaka huu, na karibu wanachama milioni 30 duniani kote mpango wa uaminifu hutoa madaraja manne ya uanachama; Bluu, Fedha, Dhahabu na Platinamu, huku kila daraja ikipata mapendeleo ya kipekee.

Wanachama wanaweza kuchuma maili ya Skyward na washirika mbalimbali kutoka kwa mashirika ya ndege, hoteli na kukodisha magari hadi biashara za kifedha, burudani na mtindo wa maisha. Maili za Skywards zinaweza kutumika kwa zawadi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tiketi za ndege kwa mashirika ya ndege washirika, uboreshaji wa safari za ndege, kukaa hotelini, tiketi, ukarimu katika hafla za michezo na kitamaduni, ziara na uzoefu usioweza kununua pesa.

Wanachama wa Emirates Skywards wana sababu zaidi za kusherehekea mwaka huu, na karibu wanachama milioni 30 duniani kote mpango wa uaminifu hutoa madaraja manne ya uanachama; Bluu, Fedha, Dhahabu na Platinamu, huku kila daraja ikipata mapendeleo ya kipekee.


Huawei at AfricaCom2022: Nonstop innovation to fuel Africa's digital future

$
0
0

[Cape Town, 09 November 2022] - After two years of virtual gatherings, the prestigious annual AfricaCom event – Africa’s largest technology conference – made its in-person return this year. Taking place at the Cape Town International Conference Centre (CTICC) from 7 to 11 November, the event brought together African operators, industry elites, and opinion leaders.

As a leading industry player, Huawei had a big presence at the event. With the theme “Lighting up the Future,” it shared insight on cutting-edge trends in the telecom industry, including 4G/5G co-development, FMC intelligent connectivity, digital operations transformation, and green development leading the future of digital networks in Africa.

During the conference’s opening session, Leo Chen, President of Huawei Sub-Saharan Africa Region delivered a presentation entitled "Lighting up the Future with Nonstop Innovation". In it, he outlined Huawei’s latest ICT development concepts and successful digital transformation solutions.

“The high resilience and rapid growth of the continent’s digital economy, technologies such as 5G, artificial intelligence, and cloud are evolving rapidly and the adoption of ICT in a wide range of industries is growing,” said Chen. “They are supporting Africa in advancing the technical revolution, boosting productivity and increasing jobs.”

He pointed out that over the last two decades, Africa has made significant progress in digitalization. It has established the first-mile infrastructure, connecting countries on the continent to the global internet. Additionally, it has tripled its middle-mile internet infrastructures that expands the connection within and between countries. However, there are still challenges to be overcome.

“Today, we still need to improve the last-mile broadband infrastructure and bridge the digital divide between urban and rural areas,” Chen said.

Whilst there is appetite for a greater uptake of digital technologies, constraints including a skills deficit, and lack of viable technology solutions are impeding the advance of ICT adoption. Chen pointed out there are three major ways to break through these bottlenecks.

“We need to further deepen connectivity to connect more people, enterprises, and scenarios; unleash digital productivity and enable digital transformation in multiple industries; increase the ICT industry’s energy-efficiency and leverage ICT technologies to reduce emissions across all industries,” he added.

Of particular relevance to the African context were case studies around the digital transformation of the port and mining sectors in China which have attracted wide attention from its African counterparts. These case studies provide a good example and reference for the potential of the development of the digital economy in Africa, as 90% of Africa’s imports and exports travels by sea, and mining is an important source of wealth creation for many African countries.

As Africa's digital ship sails into the future, it requires a strong tail wind to propel it forward. Chen called for more favourable industrial policies, and more cooperation between public and private sectors. To this end, Huawei has set up four innovation centres in Africa, launched several plans to support the development of small and medium-sized enterprises (SMEs), and will train 100 000 digital champions in Africa over the next three years.

At AfricaCom, Huawei also showcased a range of innovative technologies and solutions, including the Very Large Scale Antenna Array (ELAA), and solutions such as Ultra-Wideband RRU, that effectively and cost effectively address some of the obstacles such as inconsistent spectrum resources and insufficient fibreoptic network reach that are holding Africa back.

Leo Chen, President of Huawei Sub-Saharan Africa Region


UCHUNGUZI AJALI YA NDEGE YA PRECISION AIR KUFANYIKA KIMATAIFA

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV - Dodoma 

Serikali imesema kuwa uchunguzi wa ajali ya  Ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, mwaka huu unaendelea na ulianza tangu siku ya kwanza ilipotokea ajali hiyo katika Ziwa Victoria mjini Bukoba mkoani Kagera.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa Baraza la Mawaziri lililokutana leo (Novemba 14, 2022) limeagiza uchunguzi wa ajali hiyo ufanyike baina na Wataalamu wa ndani kwa kushirikiana na Waatalamu kutoka nje ya nchi ili kutoa taarifa ya chanzo chake.

“Nchi yetu imetiliana saini za makubaliano katika mikataba mbalimbali ya Kimataifa ambayo inasimamia usafiri wa Anga, na hivyo kuhakikisha hatua stahiki zitachukuliwa baada ya ajali za Ndege kutokea”, amesema Msigwa baada ya Baraza la Mawaziri kutoa tamko.

Aidha, Msigwa amesema Baraza hilo la Mawaziri limeagiza kuimarishwa Vitengo vyote vinavyokabiliana na majanga nchini ili kuchukua tahadhari dhidi ya ajali kama hiyo iliyosababisha idadi kubwa ya vifo vya watu.

Msigwa amesema timu hiyo ya uchunguzi kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka nje, itatoa ripoti ya awali ya ajali hiyo katika siku 14, pia itatoa ripoti ya ajali hiyo ndani ya siku 30 na mwisho itatoa ripoti ndani ya miezi 12 baada ya ajali kutokea.

Serikali imewataka Wananchi kuwa na utulivu katika kipindi cha uchunguzi wa ajali hiyo, huku ikiwahakikishia Wananchi kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inachukua tahadhari na kuzuia ajali na majanga mbalimbali yanayotokea nchini

Ajali ya Ndege ya Kampuni ya Precision Air ilitokea Jumapili ya Novemba 6, 2022 katika Ziwa Victoria, ilibeba watu 43 ambapo ilisababisha vifo vya watu 19 wakiwemo Marubani wawili na wengine 24 kujeruhiwa kati ya majeruhi hao Wahudumu wa Ndege hiyo walikuwa wawili.




ATU and ICT ministers underscore importance of a digital economy for Africa’s resilient growth

$
0
0

  The African Telecommunications Union (ATU) held a ministerial forum on Day 0 of AfricaCom 2022, bringing together participants from Malawi, Namibia, Uganda, and Zambia. The session focused on methods to engineer a new sense of hope for Africa’s digital economy journey.


Under the theme ‘Rise Stronger with Digital Economy: New Paths towards a Resilient Recovery and Growth’, the forum was supported by Huawei.

Introducing the session, the General Secretary of the ATU, John Omo spoke about digital transformation as the driver of inclusive economic growth, job creation, the improvement of public service delivery, and the optimisation of business services in Africa.

“Africa needs digital innovation to spill over into all segments of business and society if we are to strengthen our digital economy,” he said. “According to the World Bank, Africa requires US$100 trillion to achieve full digital transformation, and no one, in the public or private sector, has the capacity to do this alone. Through the power of investment and of regulation, together we can craft a framework that will give effect to the growth and development we want to see.”

Leo Chen, Huawei President of Sub-Saharan Africa Region, in his address, emphasized the three major elements of digital transformation: digital infrastructure, digital services and digital skills.

“If we do these three things well, we can connect the unconnected people and businesses, fully unleash digital productivity, and develop the digital economy, no matter what its definition is,” he said.

“To achieve this, Huawei innovates to impact with local partners, to find local solutions to local problems,” Chen said. “We are a leading global ICT company, and technology is our most important asset. We want to keep what matters the most in Africa. That is why we have made significant investments in people and skills transfer, through training, certification, and joint innovation.”

Forum guests were in consensus that digital infrastructure is fundamental to ensuring the digital transformation of their respective countries. In Malawi, according to Francis Bisika, Principal Secretary of e-Government, 2,300 km of fibre network has been installed across the country including to the remote rural areas.

“We are addressing the issue of connectivity, especially in rural areas, we are also bringing fiber to the home, as well as business. Once we have the connectivity, we can address the issue of digital literacy,” he said. “We have also built a government data centre in which we are accommodating businesses and individual’s request for networking and storage, making ICT facilities available to as many Malawians as possible.”

What the guests also have in common is the integration though all government ministries, departments and agencies of the digitisation process, for example in issues around agriculture and education - technology is being incorporated through their systems.

“The digital sector has been given authority in Zambia,” said Zambia’s National Coordinator of SMART Zambia Institute, Percy Chinyama “We are working to maximise the work of revenue generating departments and to reduce duplications of work and now have 240 government services online.”

ICT and climate change share equal importance in Namibia, according to Emma Theofelus, Deputy Minister of Information and Communication technology. “Digitisation and energy efficiency go hand in hand,” she said, “and we are committed to working to increase levels of digitization and reducing our impact on climate change.”

Another theme was that of the inclusion of youth in the continent’s digital transformation. Given that 60% Africa’s population is under 25, harnessing and retaining the innovation of its young people is critical for the future of Africa.

“Even as we have increased the number of tertiary education institutions, levels of unemployment remain a problem, and so we are working towards greater job creation for graduates,” said Ugandan Minister for ICT and National Guidance, Chris Baryomunsi.

The forum closed with the signature of a joint communique where all participants agreed that the development of the digital economy is measurable. In order to develop the digital economy, countries need to have in place a top-level strategy and an implementation roadmap, with clear objectives, indicators and milestones. They also need favourable policies to encourage investment, improve efficiency, and enable the infrastructure, skills, digital ecology, and innovation needed to grow the digital economy and create a fair business environment for all investors.

Under the theme ‘Rise Stronger with Digital Economy: New Paths towards a Resilient Recovery and Growth’, the forum was supported by Huawei.


HIVI NDIVYO MKAZI WA KILOSA ALIVYOJISHINDIA MILIONI NANE ZA BIKOSPORTS

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Kilosa

KAZI wa Magulu, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, Bahati Rajabu Ally, amefanikiwa kupenya kwenye duara la Bongebonasi ya mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali ya bikosports kwa kushinda sh milioni 8.

Akizungumzia ushindi wake, Ally anayejishughulisha na kilimo, alisema fedha zake hizo zitamsaidia katika gurudumu la maisha yake, sanjari na kuwekeza kwenye kilimo kwa ujumla.

Alisema amepata fedha zake za bikosports bila usumbufu wowote, jambo linaloufanya mchezo huo uwe na tija kwa Watanzania wote.
“Niliweka mkeka wa Bikosports nikashinda sh Milioni 8 ambazo zimekuja wakati ambao nazihitaji fedha hizi kwa ajili ya kurahisisha maisha yangu ya kila siku.

“Naomba Watanzania wenzangu nao wabashiri matokeo ya michezo kwa kupitia bikosports ili nao wavune fedha kama nilivyoshinda mimi, ambao unapokea ushindi wako mara baada ya mkeka wako kutiki, huku namba yangu ya kampuni ikiwa ni 101010.

Watanzania wanaweza kubeti moja kwa moja kwa kupitia mtandao ambao ni kwa www.bikosports.co.tz bila kusahau wanaobeti kwa kwa kucheza *149*89# ambapo namba ya kampuni ni 101010 na kutoa nafasi kubwa kwa watu wote kubashiri na kupata ushindi kwa asilimis kubwa nchini.

Mkazi wa Magulu wilayani Kilosa, mkoani Morogoro (katikati) akionyesha shauku yake baada ya kupokea fedha zake sh milioni 8 alizoshinda kutoka kwenye mchezo wa kubashiri matokeo wa bikosports kutoka kwenye kilele chake cha bongebonasi.



NSSF ILIVYOSHIRIKI KATIKA MAONESHO YA UTALII KARIBU KUSINI MKOANI IRINGA

$
0
0

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulishiriki katika Maonesho ya Utalii Karibu Kusini  yaliyofanyika katika viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani Iringa, maonesho hayo yalifungwa  na Mgeni Rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud.

NSSF ilitumia  maonesho haya kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi,kuandikisha wanachama, kusikiliza na kutatua kero za wanachama.











WANAWAKE WANOLEWA, TGNP YATOA WITO

$
0
0

 

Mwanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha Ardhi jijini Dar es Salaam, Nyanzobe Makwaiya akizungumza leo Novemba, 14 2022 akizungumza alipozindua warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.
Mtoa mada, Scholastica Makwaia akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.



Washiriki wa warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake wakisikiliza mtoa mada jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2022.
Picha ya Pamoja.

MWANAMKE ni Mama Mwanamke ni Kiongozi muungoza njia ndivyo " ndivyo ambavyo unaweza kueleza kwa vielelezo mbalimbali pamoja na mfano wa wazi wa Rais Samia Suluhu Hassan amiri jeshi Mkuu wa Tanzania.

Rais Samia amewapa ujasiri wanawake wengi kuamini kuwa Mwanamke ni kiongozi bora kutokana na kurejesha matumaini nchini.

Mwanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha Ardhi jijini Dar es Salaam, Nyanzobe Makwaiya kwenye shahada ya kwanza ya Usimamizi wa Mazingira pia ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho anasema kuwa anaamini anaweza na kuwasihi wanawake wengine kusimama kwa kuwa tayati Rais Samia ameshatoa njia.

Hayo ameyasema leo Novemba, 14 2022 alipozindua warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.

"Nimekuja hapa kama Mgeni rasmi kwa ajili ya kufungua mafunzo ya uongozi kwa Wanawake ".

Anaeleza kuwa historia yake ya uongozi imeenza tangu alipoanza elimu yake ya awali mpaka sasa yupo Chuo kikuu akihudumu nafasi ya Uwaziri Mkuu.

Amesema kuwa amepata wito kutoka ndani ya nafsi yake lakini pia kutoka kwa watu wanaomzunguka.

"Kinachonisukuma kuwa kiongozi ni kuona kwama kunavitu vinafanyika katika namna ambayo pengine sio sahihi au sahihi lakini naweza kuboresha zaidi utendaji wangu ambapo watu waliokaribu yangu wanaona nafaa kuwania nafasi hiyo kwa hiyo nimepata msukumu kutoka ndani na kutoka kwa watu wanaonizunguka kuona kwamba ninafaa na kuona uwezo wangu katika kazi ninazozifanya." Amesema.

Ameleza mafanikio yake ni pamoja na kushiriki warsha mbalimbali na kitengeneza mtandao mkubwa wa kufahamiana na watu.

"Pia nimepata mafanikio ya kusaidia watu wengine kwa kuwa ukiwa kiongozi unatarajiwa kuwasaidia watu."

Ameeleza changamoto ni pamoja mifumo ya uongozi bado haijawa rafiki kwa mwanamke kwa kuwa anaongoza wanaume wenye fikra za kimfumo dume.

"Nafasi za uongozi nyingi zinachukuliwa na wanaume kuliko wanawake"

Changamoto nyingine ameeleza kuwa ni muda na fedha za kufanya kampeni.

Pamoja na changamoto zote hizo anasema kuwa wanawake wanaweza " wanawake ni jeshi kubwa wanaweka tunaweza hajalishi kuwa wewe ni kiongozi kwa sasa au sio kiongozi wanaweke tushaonesha nia na njia haijalishi umri wako unaweza unaweza kuamua leo kuanza na unaweza kufika unapotaka".

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Lihundi amesema kuwa Wanawake wapewa wito wa kuingia kwenye siasa ili kuingia kwenye nafasi mbalimbali za uamuzi nchini.

Amesema kuwa idadi ya wanawake kwenye ngazi za uamuzi hairidhishi hivyo amewataka wanawake wajitokeze kwenye nafasi za uongozi ili kuleta maendeleo kwenye jamii.

Amesema kuwa Mwanamke ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuleta maendeleo kwenye jamii kwa kuwa wapo karibu zaidi kwenye jamii.

"Wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya wananchi Tanzania ndio maana tunasisitiza vijana wa kike na wanawake kwa ujumla wao washiriki kupata fursa au rasilimali hii ya uongozi.

Tumeambiwa na tafiti mbalimbali kuwa uongozi unaohusisha wanawake na wanaume unakuwa na tija kwa sababu macho ya wanawake yanaona vitu vingi zaidi kuliko macho ya wanaume unapozungumzia ukatili wa kijinsia kiongozi mwanamke atauona zaidi kuliko kiongozi Mwanamme unapozungumzia rushwa ya ngono kiongozi Mwanamke ataiona zaidi kuliko kuliko kiongozi mwanamme kwa sababu kiongozi mwanamke ndiye inayemuathiri Zaidi." Amesema Lilian.

Lakini kuna matatizo ya watoto na hata watu wazima kutokana na ile fursa mungu aliyotupa ya kuzalisha nguvu kazi na tunalea kwa hiyo unapomlea mtoto wa kike unapomlea mtoto wa kiume unawafahamu zaidi kwa hiyo unalea mtoto wa kike unalea mtoto wa kiume na unaishi na mwanamme ambaye ni mume wako ndugu zako kwa hiyo sisi wanawake tumepata bahati ya kuwajua wote ni rahisi kuzijua changamoto zao kiundani zaidi.

Amesema kuwa kuna changamoto ya wanawake kuwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi "kuna mila na Desturi zinazomfanya mwanamke asiwe kiongozi hata mfumo wa elimu ulivyotengenezwa hata kwenye vyuo vyetu hapa nchi kwenye nafasi za uongozi katika serikali za wanafunzi wapo wangapi, ukiingalia kwenye shule zetu za msingi na sekondari viongozi wa kike wapo wachache."

Amesema kuwa nafasi ya mwanamke kwenye uongozi kidunia hairidhishi kwa kuwa wapo viongozi wa juu wachache kwenye nchi zote duniani.

"Hata kwenye nafasi ya Urais unaona ni marais 21 tu kwenye nchi zote duniani ambapo ni wanawake akiwemo na Rais Samia kwa hiyo bado ni wachache mno"

Ameitaja nafasi ya kulisimamia bunge kwa wanawake kidunia amesema kuwa wanawake maspika wa Bunge duniani kote ni asilimia 20.9 huku manaibu Spika wakiwa 28.3 huku kwa wabunge wote duniani wanawake ni asimilia 25.5.

Amesema kuwa Tanzania imebahatika kuwa na wabunge wanawake asilimia 36.7 kutokana na kuridhia mikataba ya kimataifa pamoja na jitihada za wanaharakati.

Amesema kuwa Tanzania imepata bahati ya kipekee kwa kuwa na Viongozi wa Mihimili miwili ule wa Serikali yaani Rais ni Mwanamke (Rais Samia Suluhu Hassan) na ule wa Bunge (Spika ni Dk. Tulia Ackson).

Amesema kuwa asilimia ya wanawake kwenye ngazi ya maamuzi muhimu serikali za mitaa ni asilimia 2 tu.

VYUO VIKUU 7 KUTOKA UFARANSA VYAKUTANA NA WANAVYUO TANZANIA

$
0
0

 

 

USHIRIKIANO baina ya Tanzania na Ufaransa umeendelea kuimarika zaidi hasa katika sekta ya elimu ambapo Ufaransa kupitia Ubalozi wake nchini umezindua maonesho ya Elimu ya Juu kwa mwaka 2022 kwa vyuo vikuu 7 vya nchini Ufaransa kukutana na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Tanzania na kueleza program zinazotolewa katika vyuo vikuu vya Ufaransa kwa lugha ya Kiingereza.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC,) jijini Dar es Salaam Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kupitia fursa hiyo vijana wa Tanzania watapata ujuzi ambao utasaidia katika masuala ya Teknlojia, Fizika, Sayansi pamoja na biashara.

 

‘’Mje kama watanzania mkiwa mnazungumza Kiswahili na Kingereza mtapata ujuzi kwa lugha ya Kiingereza…Tunahitaji watanzania wengi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania ambavyo tunashirikiana navyo kwa ukaribu zaidi na mkiwa Ufaransa mtafahamu pia tamaduni na lugha ya Kifaransa.’’ Amesema.

 

Balozi Nabil amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron walikubaliana kubadilishana ujuzi katika masuala ya Sayansi na Teknolojia ambapo kupitia fursa hizo za elimu katika kada mbalimbali zinazotolewa nchini Ufaransa ni moja ya nyenzo muhimu kwa vijana wa kitanzania katika kukuza Sayansi na Teknolojia nchini.

 

Aidha amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na vyuo vikuu vya Tanzania ili kujenga mahusiano mazuri  kwa pande zote mbili.

 

‘’Vijana wa Afrika wakiwemo wa hapa Tanzania wakitoka Ufaransa kupata mafunzo na ujuzi wamekuwa mstari katika nchi zao katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya teknolojia na Nchi kwa ujumla tunawahimiza vijana wa Tanzania kuendelea kuchangamkia fursa hii.’’ Amesema.

 

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kitengo cha Afrika, Kitengo cha Campus France Matthiew Bragato amewataka wanafunzi hao kutumia fursa hiyo ya kusoma nchini Ufaransa, na kuwatoa hofu kwa kuwaeleza kuwa masomo yanafundishwa kwa lugha ya kiingereza.

 

‘’Tutumie fursa hii ili kuweza kubadilishana uzoefu wa Sayansi na Teknolojia kupitia elimu ambayo ujuzi unatolewa kwa lugha ya Kiingereza.’’ Amesema.

 

Bragato amesema, wawakilishi kutoka vyuo vikuu 7 kutoka nchini Ufaransa watawasilisha program bora zinazofundishwa kwa lugha ya Kiingereza na Kifaransa kwa wanafunzi wa vyuo Tanzania na  watakuwa nchini kwa kushirikiana na Kituo cha Campus France, Kiongozi wa Kifaransa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa anayeshughulikia uwezeshaji wa masomo nchini Ufaransa kwa wanafunzi wa kigeni.

 

Mkutano huo uliojikita katika mada mbalimbali ikiwemo masomo ya uhusiano wa kimataifa, masomo ya Kifaransa, masomo ya PhD, fursa za Erasmus Mundus na masomo ya biashara, pia jinsi ya kujiunga na kushiriki nafasi za masomo nchini Ufaransa pamoja na kujadili nafasi za kazi katika Nyanja hizo kwa nchi za Ufaransa na Tanzania.

 

Vyuo vikuu kutoka Ufaransa vilivyoshiriki na kuwasilisha program zao ni pamoja na Chuo Kikuu cha masomo ya kimataifa na siasa, shule tatu za uhandisi za IMT Ales, IMT Atlantique na ISEA- SUPAERO, shule mbili za biashara za Excelia na SKEMA pamoja na shule moja ya kilimo ya Institut Agro huku mamia ya wanavyuo kutoka Tanzania walitoka katika vyuo vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Morogoro, Iringa, Zanzibar na Mwanza.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Elimu ya Juu kwa mwaka 2022 na kueleza kuwa kupitia fursa hiyo ya elimu nje ya Nchi vijana wa Tanzania watapata ujuzi ambao utasaidia katika masuala ya Teknlojia, Fizika, Sayansi pamoja na biashara.
Meneja Masoko wa Kitengo cha Afrika, Kituo cha Campus France Matthiew Bragato akizungumza wakati wa uzinduzi huo na kuwataka wanavyuo hao kutumia fursa hiyo ya kusoma nchini Ufaransa, na kuwatoa hofu kwa kuwaeleza kuwa masomo yanafundishwa kwa lugha ya kiingereza.


Baadhi ya wanavyuo wakipata mafunzo kutoka kwa wawakilishi wa vyuo vikuu saba kutoka nchini Ufaransa juu ya kunufaika na fursa ya kupata ujuzi kupitia vyuo vikuu vya Ufaransa, Leo Jijini Dar es Salaam.

 

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (Kulia,) akikagua maonesho hayo.



Mkutano ukiendelea.


Maonesho yakiendelea.
 


 
 

Absa buttresses status with four awards at Consumer Choice Awards Africa 2022

$
0
0

Absa Bank Tanzania Limited has reinstated its position as a digital innovation pioneer in the industry and preferred bank of choice after scooping four different awards during the Consumer Choice Awards Africa Gala held at Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam over the weekend.

Absa Bank was awarded The Most Advanced Digital Banking Service in Southern Africa, The Most Preferred International Bank (Large Size) at Customer Service, The Most Consumer Preferred Extended and Accessible Bank in Africa, and The Most Advanced Digital Banking Service in Southern Africa.

Representing the Bank’s MD, Absa’s Finance Director, Mr. Obedi Laiser, said “One of our core values as a bank is our obsession with the customer. And throng our customer centricity approach, we have become a truly digitally lead bank that is in tune with the changing needs and wants of our customers. We continuously deploy innovative banking solutions that are “a-first in the market” offering unrivaled customer convenience, and this is evidently the reason we have been voted as the best in the different awards categories we have won today.”

The official noted that in 2015 the bank made a deliberate decision to become a truly digital bank and went paperless bank in order to deliver the best banking experience for customer, enabling customers to walk into branches and access service like deposit and withdrawal without having to fill papers.

Hand in hand with this, Absa has introduced a unique Queue Management System that allows customers to interact with the bank’s tellers directly and privately through their phone either via WhatsApp or SMS.

He noted that the bank has also enhanced its Mobile Banking App to allow customers access virtually every banking service through Mobile Banking App and also manage their cards and banking details conveniently. Customer can change their email addresses, update their mobile numbers, block or unblock their cards at their convenience without needing to visit any of the branches or filling any papers.

“ Recently we also launched a QR Code ATM Withdraw Solution that allows customers to withdraw cash from any Absa ATM through the Absa Mobile Baking App using a QR code, discarding the need to have an ATM card with them,” noted Obedi Laiser.

“Our ATMs have also been enhanced to accept cash deposits. Through these Cash Deposit ATMs our customers do not need to visit a branch in order to make deposits. They can deposit their cash on any of our Cash Deposit ATM near them conveniently without the limit of time.”

According to the Absa official the bank’s has not stopped at individual customers segments only. To serve better the business clients the bank has partnered with Visa and introduce a debit card targeted at businesses in Tanzania. The Absa Visa Business Debit Card, which is linked to the business’ transaction account, is more than a payment tool. It is a solution aimed at helping businesses track and manage their operational expenses efficiently, access cost saving benefits and make easy and secure online transactions.

“ Most of these innovations are “firsts” in the market, and we are very proud to be the bank that is always ahead of the curve when it comes to introducing cutting edge digital solutions to our customers in Tanzania, ” Said Obedi Laiser in his concluding remarks.

“Despite the many innovations we have already introduced, we remain dedicated to finding new differentiated banking solutions to meet the evolving needs of our customers by providing innovative, digitised products delivered through personalised service.”


Deputy Minister for Industry, Trade and Investment, Exaud Kigahe (second left), presents a certificate of appreciation to Absa Bank Tanzania Chief Financial Officer, Obedi Laiser (second right), during the 2022 edition of the Customer Choice Award Africa (CCAA), grand finale in Dar es Salaam over the weekend.

GF TRUCKS & EQUIPMENTS YASAIDIA JANGA LA MOTO MLIMA KILIMANJARO

$
0
0

Na mwandishi wetu Kilimanjaro

Licha ya zoezi la uzimaji moto mlima Kilimanjaro kukamilika kwa asilimia 99 lakini vikosi mbali mbali vya jeshi la akiba pamoja na askari wa wanyamapori bado wapo eneo la tukio kuzunguka mlima kwa ajili ya doria na kuhakikisha masalia ya moto ulipo kwenye visiki wana udhibiti kwa haraka ili usilete madhara Zaidi.

Akizungumza wakati wa kupokea misaada iliyotolewa na kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd ,Kiongozi wa Geti ya Mweka Afisa mfawidhi daraja la kwanza Denis Simion aliishukurun kampuni ya GF kwa kuguswa na kupeleka misaada mbalimmbali ya vyakula kwa ajili ya askari hao wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto

Unajua ndugu Mwandishi moto ni kama umedhibitiwa kwa asilimia 99 lakini hatuwezi viondoa vikosi vya askari wetu katika eneo la mlima kwani lolote lina weza kutokea kwa hiyo kuwa tyr kukabilianja na dharula inatakiwa askari wetu wawe doria muda wote alimaliza Denis

Nae Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Smart Deus Iliguswa kutokana na ajali ya moto ya mlima Kilimanjaro hivyo wakaamua kujikusanya na kutafuta utaratiobu wa kuja kukabidhi sehemu ya mchango wao kwa wapiganaji hao ambao bado wapo eneomla tukio kwa ajili ya doria ,miongoni wa vitu ni pamoja na maji ,soda mikate sukari na vingine vingi ikiwa nisehemu ya kurudisha kwa jamii faida waliyoipata katika biashara zao

GF Ni wauzaji wa magari ya FAW ,Hong Yang na mitambo aina ya XCMG pia kamuni hiyo inaoutaratibun maalumu wa kuwakopesha magari na mitambo kwa wakandarasi wa kizalendo wenye miradi mikubwa mkononi ilikukabiliana na ushindani na makampuni makubwa ya kigeni
Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deius akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vifaa kwa Afisa mfawidhi daraja la kwanza na Kiongozi wa Geti ya Mweka Denis Simion wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya askari wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto katika mlima Kilimajaro.Picha na GF


Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deius (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa askari wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya askari wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto katika mlima Kilimajaro .Picha na GF




Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deius akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vifaa kwa Afisa mfawidhi daraja la kwanza na Kiongozi wa Geti ya Mweka , Denis Simion wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya askari wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto katika mlima Kilimajaro.Picha na GF


BENKI YA NBC YACHANGIA MILIONI 15 UJENZI WA UWANJA WA GOLF IRINGA , RC AWAPONGEZA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na Wateja Wadogo Benki ya NBC Bwn. Elibariki Masuke akikabidhi Mfano wa Hundi ya Milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Golf kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego . Kushoto ni Bwn. Edmund Mkwawa - Mwenyekiti wa Mkwawa University Golf Club Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na Wateja Wadogo Benki ya NBC Bwn. Elibariki Masuke akikabidhi Mfano wa Hundi ya Milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Golf kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego . Kushoto ni Bwn. Edmund Mkwawa - Mwenyekiti wa Mkwawa University Golf Club.


Benki ya Taifa ya Biashara NBC , Novemba 13, 2022 imeidhamini Club ya Golf ya Mkwawa University Golf Club Shilingi Milioni 15 , kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Golf ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali na Mkoa wa Iringa kwa Ujumla katika kutangaza utalii wa Kusini maarufu kama " UTALII KARIBU KUSINI " ambao maadhimisho yake yamefungwa leo hii katika viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani humo.


Akizungumza baada ya kupokea mfano wa Hundi ya Milioni 15 kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na Wateja Wadogo Benki ya NBC Bwn. Elibariki Masuke , Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameipongeza Benki ya NBC kwa jinsi inavyojitoa katika kuunga mkono masuala mbalimbali ya kijamii pamoja na michezo " Hakika Benki ya NBC tunajivunia sana uwepo wenu , asante sana kwa jitihada zenu katika kukuza sekta ya michezo nchini lakini pia kwa umuhimu mkubwa niwashukuru sana kwa kuiunga mkono klabu yetu ya Golf ya " Mkwawa University Golf Club " asanteni sana kianzio icho kitasaidia sana katika kuendeleza mchezo wa Golf hapa Iringa na moja kwa moja kutengeneza fursa zaidi za utalii asanteni sana " Alimalizia. Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na Wateja wadogo wa Benki ya NBC Bwn. Elibariki Masuke amesema kuwa " Kama kawaida yetu Benki ya NBC tunapenda sana kuunga mkono sekta ya michezo hapa nchini , kama mnavyojua sisi ni wadhamini wakuu wa Ligi ya mpira wa miguu maarufu kama NBC PREMIER LEAGUE lakini tumekua tukiendesha mashindano ya Marathon Maarufu kama NBC DODOMA MARATHON ambapo fedha zinazopatikana katika mashindano hayo ya mbio huenda moja kwa moja kuwasaidia akina mama wenye matatizo ya kansa ya Kizazi , Kwahiyo tupo hapa kujumuika na wana Iringa hasa katika tamasha hili kubwa lililofungwa leo Tamasha la " Karibu Utalii Kusini " ambalo limehusisha watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na sisi tumekuja kama wadhamini wa uwanja wa Golf ambapo tunaamini ukiwepo uwanja wa Golf hapa basi utavutia watalii zaidi na zaidi kwa maana Watalii watapata sehemu nzuri ya kujiburudisha baada ya kumaliza shughuli zao mbalimbali huko hifadhini " Alimalizia .

Kwa upande Mwingine , akizungumza kwa Niaba ya Bwn. Edmund Mkwawa Mwenyekiti wa Mkwawa University Golf Club , Yohannes Chavala ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo ameipongeza Benki ya NBC kwa mchango wao uliotukuka wa milioni 15 , na kuongezea kuwa ujenzi wa uwanja huo wa Golf utavutia watalii wengi na kukuza Utalii wa Kusini na Tanzania nzima kwa Ujumla. Mwisho. Wateja wakiendelea kupata huduma mbalimbali kwenye banda la Nbc

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Uwekezaji (UNCDF) limeteua Benki ya NBC kuwa Mtaalam Mshauri wa kukamilisha Hati Fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga

$
0
0

Picha ya pamoja kwenye makabidhiano ya mkataba wa maridhiano,taasisi ya maji safi na taka ya Tanga-UWASA juu ya uanzilishwaji wa hati fungani za kukusanya fedha kwaajili ya kuboresha mfumo wa maji jijini Tanga,kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Sera na Mipango-Tamisemi John Cheyo, Mkuu wa UNCDF-Tanzania Peter Malika,Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa benki ya NBC, Bw. James Meitaroni James Meitaron na Mkurugenzi kutoka Tanga-UWASA Geofrey Hill.

– Leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Uwekezaji (UN Capital Development Fund -UNCDF) limetangaza rasmi uteuzi wa Benki ya NBC kuwa mtaalam mshauri atakayekamilisha hatua za msingi kuwezesha kuuzwa kwa Hati fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga UWASA) ambayo itakuwa ya kwanza kuwahi kutolewa na taasisi ya Serikali nchini.



Tangazo hilo la uteuzi limeambatana na utiaji saini wa makubaliano ya kimkakati baina ya UNCDF na Benki ya NBC ambayo itaongoza timu ya wataalamu washauri inayojumuisha taasisi tano zinazotoa huduma za ushauri wa kifedha na uwekezaji na kusajiliwa na Mamlaka ya soko la hisa na mitaji (Capital Market and Securities Authority-CMSA). Hatua hii ya uteuzi ni kwa mujibu wa matakwa na miongozo ya CMSA ambapo timu hiyo inatarajiwa kuhakikisha hati fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga inaorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ifikapo robo ya kwanza ya mwaka 2023. Mkurugenzi wa Tanga UWASA, Bw. Geofrey Hill Akiongea katika hafla hiyo ya utiaji Saini, Mkurugenzi wa Tanga UWASA, Bw. Geofrey Hill, amesema, “Siku hii muhimu imefikiwa kutokana na ushirikiano wetu na UNCDF na kwa kuzingatia miongozo na maelekezo ya Serikali ya kutafuta vyanzo mbadala vya fedha ili kutekeleza miradi ya maendeleo. Tunatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na NBC ili kuharakisha hatua zilizobaki kuwezesha upatikanaji wa fedha zitakazotumika kuboresha na kuongeza uwezo wetu wa kusambaza maji kwa wananchi na maeneo yasiyo na huduma hiyo”.


Kadhalika, akitoa salamu zake Mkuu wa Shirika la UNCDF Tanzania Bw. Peter Malika, alieleza kuwa “Tunajivunia kuwateua NBC ambayo ni taasisi ya kitanzania kukamilisha suala hili la kihistoria. Hii ni njia mojawapo ya kuimarisha na kujenga uwezo wa ndani (national capacities) kuibua na kutumia vyanzo bunifu vya fedha kugharamia maendeleo. UNCDF kama mdau wa maendeleo ina nafasi muhimu ya kusaidia kutatua changamoto za upatikanaji wa fedha hususani kwenye nchi zinazoendelea ambazo masoko ya fedha ni machanga.”



Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa benki ya NBC, Bw. James Meitaroni alisema “Tukiwa kama Benki ya kizalendo, tunajivunia kuwa taasisi ya kifedha ya kwanza nchini kushiriki kama kiongozi wa mchakato na mtaalam mshauri, katika kuhakikisha ukamilifu na uuzwaji wa hati fungani hii ambayo itakuwa ni ya kwanza kutokea nchini Tanzania. Leo tumeshuhudia historia ikiandikwa ambapo kwa mara ya kwanza nchini, Mamlaka ya Umma imefungua milango mipya ya kupata fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

 Fedha zitakazopatikana kutoka kwenye mauzo ya hati fungani zitaenda moja kwa moja kurekebisha miundombinu ya maji ya mji wa Tanga na hivyo kuongeza tija ya upatikanaji na usambazaji maji jijini Tanga. 

Tunajivunia kuwa Benki washauri na kutumia uzoefu wetu katika kuleta suluhu ya changamoto zinazokabili jamii. Kupitia hati fungani hizi tunaenda kupata suluhu kubwa ya tatizo la upungufu wa mji mkoani Tanga na vijiji vya jirani. Tunaishukuru sana serikali na wadau wengine kama UNCDF kwa kuendelea kuweka mazingira bora yanayofanya taasisi za kifedha kama sisi NBC kushiriki katika shughuli za kutatua changamoto za jamii inayotuzunguka”










Benki Ya NBC Yasisitiza Dhamira Yake ya Kuboresha Ligi Kuu ya NBC, Yamwaga Mikopo ya Mabasi Kwa Vilabu.

$
0
0

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League imesisitiza kuhusu dhamira yake ya kuboresha zaidi ligi hiyo kwa kuendelea kuziwezesha timu zinazoshiriki ligi hiyo ili ziweze kujenga uwezo wa kujitegemea.

Dhamira hiyo imesisitizwa na Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Bw Waziri Barnabas mapema jana wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa 17 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) uliofanyika jijini Mwanza.

“Kimsingi ni kwamba sisi kama wadhamini wa ligi hii tunajivunia sana kuona ligi yenye ushindani na viwango bora vya kiuchezaji vinavyoendelea kuonekana kwenye ligi hii. Hii inatokana na timu zinazoshiriki ligi hii kuweza kusajili na wachezaji wazuri kutoka ndani na nje ya nchi sambamba na kuweza kuwahudumia vema wachezaji hao ikiwemo kuwapatia maslahi yao.’’ alisema

Kwa mujibu wa Bw Waziri, mbali na udhamini wa ligi hiyo benki hiyo imebuni mikakati mbalimbali inayolenga kufanikisha dhamira hiyo muhimu ikiwemo mikopo ya mabasi kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi hiyo ili kurahisha usafiri kwa vilabu hivyo.

“Ligi hii inahusisha suala zima la usafiri kwa vilabu husika na wakati mwingine timu zinasafiri kwa umbali mrefu sana na hivyo kusababisha uchovu kwa wachezaji. Upatikanaji wa mabasi mazuri ya kisasa utasaidia kupunguza uchovu kwa wacheza ili waweze kuleta ushindani unaohitajika wakiwa viwanjani. Tupo kwenye hatua nzuri na hivi karibuni baadhi ya timu zitapatiwa mabasi yao,’’ alisema.

Zaidi Bw Waziri alitaja huduma nyingine kuwa ni pamoja na utoaji wa Bima kwa wachezaji, benchi za ufundi na familia za wachezaji wote wa ligi hii ya NBC Premier League.

“Tunaamini kuwa Bima hizi ambazo tunazitoa kupitia kampuni washirika za Britam na Sanlam, zimekuwa chachu kubwa kwa kuwaondolea wachezaji hofu za kucheza kwa woga wakihofia kupata majeraha yanayoweza kuathiri ajira zao. Hili limechochea sana wachezaji wetu kuonyesha viwango vyao.’’ Alisema.

Aidha Bw Waziri aliwaomba wadau hao wamichezo vikiwemo vilabu, viongozi wa mchezo huo na wachezaji mmoja mmoja kuhakikisha wanachangamkia fursa ya kuwekeza kwenye Hati Fungani ya NBC Twiga Bond ili waweze kunufaika na faida mbalimbali zitokazo na Hati fungani hiyo.

“Kiasi cha chini cha ununuzi wa hati fungani hiyo ni TZS 500,000. Kupitia uwekezaji huu wahusika wataweza kupata riba kubwa ya 10% kwa mwaka, inayolipwa nusu mwaka katika kipindi chote cha miaka mitano hadi Novemba 2027. Kiwango cha riba kinacholipwa hakina punguzo la kodi. Hivyo nawakaribisha sana wadau wa michezo’’ Alisema.


Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya NBC Bw Waziri Barnabas akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa 17 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) uliofanyika jijini Mwanza hii leo. Alisisitiza kuhusu dhamira yake ya benki hiyo kuboresha zaidi ligi hiyo kwa kuendelea kuziwezesha timu zinazoshiriki ligi hiyo ili ziweze kujenga uwezo wa kujitegemea.



Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya NBC Bw Waziri Barnabas (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa mchezo wa soka nchini akiwemo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw Wallace Karia wakati wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa 17 wa Shirikisho hilo uliofanyika jijini Mwanza hii leo.





Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa 17 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) uliofanyika jijini Mwanza hii leo wakijadili mada mbalimbali wakati wa mkutano huo.

NMB yapongezwa kusaidia Wakandarasi- Zanzibar

$
0
0

 


Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi -Zanzibar imeipongeza Benki ya NMB kwa kuleta masuluhisho maalum yalio rafiki kwaajili ya wakandarasi huku akiamini ndio njia rahisi ya kusaidia kuwakuza wakandarasi wazawa kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed alipokuwa anazindua rasmi warsha ya Benki ya NMB pamoja na wakandarasi wa Zanzibar ikiwa na lengo la kuwatambulishia suluhisho mpya kwaajili ya wakandarasi na kuwasihi wachangamkie fursa hizo.

Mbali na hilo, Waziri huyo aliwasihi pia wakandarasi kutumia fedha za mikopo wanaopata kutoka kwa mabenki kwaajili ya kazi waliokopea na sio kwa shuguli zingine kwa inaweza wapa ugumu katika kurejesha mkopo huo.

Akizungumza katika warsha hiyo, mwakilishi wa Benki ya NMB ambae ni Mkuu wa Idara ya Miamala wa Benki hiyo, Bi. Linda Teggisa alisema kuwa Benki ya NMB imesimama katika nafasi ya kuendelea kuongeza fursa ya upatikanaji wa huduma za kifedha ili kuendelea kuwawezesha wakandarasi kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za dhamana za zabuni kwaajili ya miradi au manunuzi (unsecured bid bond) pamoja na dhamana za utekelezaji (performance guarantee) au dhamana za malipo ya awali (advance payment guarantee), zote ambazo hazihitaji dhamana.

Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu, Mkuu wa wilaya ya Mjini, Mhe. Komred Rashid Simai Msaraka alisema kuwa sekta ya ujenzi imekuwa ni sekta ya muhimu sana kwa Zanzibar kwa sasa kwani ni miongoni mwa Sekta ambazo zinaongeza ajira zilizo na zisizo rasmi kwa wananchi wa Zanzibar na kupongeza taasisi za fedha kuamua kuongeza nguvu kwa sekta hii sio tu kuwanyayua wakandarasi lakini linaenda kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa Zanzibar

Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar, Bi. Naima Shaame (Kushoto) akizungumza katika warsha maalum ya Benki ya NMB pamoja na wakandarasi iliyolenga kuzitambulisha suluhisho mpya za benki ya NMB kwa wakandarasi. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano a Uchukuzi, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, wapili kulia ni waziri wa Ardhi, Mhe. Rahma Kassim Ali, kulia ni naibu waziri wa Ardhi, Mhe. Juma Makungu Juma na wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Miamala ya Benki ya NMB, Bi. Linda Teggisa. 

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA TAWI JIPYA KUFANYA KAZI MASAA24

$
0
0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la benki hiyo lililozinduliwa leo katika Jengo la makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo posta jijini Dar es Salaam ambapo tawi hilo litakuwa likifanya kazi masaa 24 ili kuhakikisha wafanya biashara wanapata huduma ya kifedha muda wote wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta,Mkurugenzi wa Masoko Deo Kwiyuka, Meneja wa TCB Tawi la TPA, Anastela Kabudi, Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Mkurugenzi wa Hazina wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Wenceslaus Fungamtama pamoja na maa fisa wengine wa TCBAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi (kushoto), akifungua kisanduku maalum kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la benki hiyo lililozinduliwa leo katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo posta jijini Dar es Salaamambapo tawi hilo litakuwa likifanya kazi masaa 24 ili kuhakikisha wafanya biashara wanapata huduma ya kifedha muda wote wengine pichani Mkurugenzi wa Masoko wa benki hiyo Deo Kwiyuka, pamoja na Meneja wa TCB Tawi la TPA, Anastela KabudiAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo lililozinduliwa leo katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo posta jijini Dar es Salaam ambapo tawi hilo litakuwa likifanya kazi masaa 24 ili kuhakikisha wafanya biashara wanapata huduma ya kifedha muda wote Meneja Tanzania Commercial Bnk TCB Tawi la TPA, Anastela Kabudi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo lililozinduliwa leo katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo posta jijini Dar es Salaam ambapo tawi hilo litakuwa likifanya kazi masaa 24 ili kuhakikisha wafanya biashara wanapata huduma ya kifedha muda wote

Viewing all 48979 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>