Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Tanzania, Prof. Makame Mbarawa na Mawaziri wa Miundombinu na Uchukuzi Alexis Gusaro na Cherubin Senga wa DRC wakisaini Makubaliano ya ujenzi wa miundombinu ya Reli, Meli, Bandari na barabara baina ya nchi hizo jijini Dar leo.
TANZANIA NA DRC ZAJA KIVINGINE...!
Spika Dk Tulia Aguswa na Jitihada za Wanawake Benki ya NBC kuwanoa wenzao kiuchumi, atoa angalizo
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya NBC kupitia Chama cha wanawake Wafanyakazi wa NBC (Women Network Forum) katika kuendesha mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwakomboa wanawake dhidi ya changamoto za kiuchumi.
Kwa mujibu wa Dk Tulia jitihada mbalimbali zinazofanywa ili kuwakomboa wanawake kijamii zinaweza zisifanikiwe vema iwapo kipaumbele hakitawekwa katika kuwapatia mafunzo yanayolenga kuwajenga kiuchumi.
Spika Dk. Tulia alitoa rai hiyo jijini Dodoma leo wakati akifungua semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofahamika kama “Pamoja na NBC Bank” .
Kwa mujibu wa Dk. Tulia, kupitia mafunzo hayo wanawake wataweza kubadili fikra zao kuhusu vipaumbele vyao pindi wanapofanya maamuzi mbalimbali ya kiuchumi kwa kuwa licha ya jitihada mbalimbali za wanawake nchini katika kujiongezea kipato bado changamoto imebaki kwenye namna ambavyo wanatumia kipato chao.
“Nitolee mfano mdogo tu kwenye VICOBA, ni kweli wananawake tunafanikiwa kujiongezea kipato lakini sehemu kubwa ya kipato hiki mara nyingi imekuwa ikielekezwa kwenye matumizi yasiyo ya kipaumbele ikiwemo manunuzi ya mavazi mengi zikiwemo sare nyingi tunazoshona au kununua kwa ajili ya kila tukio tunalolifanya kina mama. Ndio maana nawapongeza Benki ya NBC kwasababu kupitia wabunge hawa elimu hii itawafikia wanawake kote nchini.’’ Alisema.
Alisema mbali na kuwasaidia wabunge wanawake ambao pia baadhi yao wamekuwa na udhaifu kwenye nidhamu ya matumizi ya fedha zao, semina hiyo pia itasaidia kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya kiuchumi wabunge hao hususani pale wanaposhiriki kwenye mijadala ya kibunge inayolenga kuishauri serikali kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi yanayowahusu wanawake na nidhamu katika matumizi ya fedha za umma.
“Hivyo natarajia kuona matunda ya semina hii kwenye mijadala mbalimbali inayoendelea hususani kwenye vikao vya Bunge vinavyoendelea…nashukuru sana NBC mmefanya kitu sahihi wakati sahihi,’’ alisema.
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw Theobald Sabi, Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa alisema semina hiyo iliwalenga wabunge hao kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi na wenye ushawishi mkubwa kwa jamii, hususan makundi ya wanawake, ili nao wafikishe ujumbe kwa walengwa.
Akizungumiza kuhusu Chama cha wanawake Wafanyakazi wa NBC (Women Network Forum) ambacho ndicho kilichoratibu semina hiyo, Bi Lowassa alisema kinalenga kuwanganisha na pia kukuza elimu ya kifedha miongoni mwa wanachama wake ili wakawe mabalozi kwa wanawake wengine.
“Chama hiki pia kimeenda mbali kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi ya wanawake katika maeneo mbalimbali nchini.Kupitia chama hiki, Benki pia imeweka utaratibu maalum wa kuwapa nafasi wafanyakazi wanawake ili kushika nafasi za uongozi.’’ Alisema huku akibainisha kuwa kwasasa benki hiyo ina wafanyakazi zaidi ya 900 ambapo asilimia 47% kati yao ni wanawake.
Katika semina hiyo ilishuhudiwa maofisa mbalimbali wanawake kutoka benki ya NBC wakitoa elimu kwa wabunge hao kuhusu mada mbalimbali za kiuchumi ikiwemo usimamizi wa fedha, mafunzo kuhusu bima za biashara na maisha na pamoja na Hati fungani ya NBC.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), (Kulia – meza kuu) akifurahia pamoja na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma. Wengine ni pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (katikati
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa akizungumza na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake akiwemo Mbunge wa Mchinga ambae pia ni mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (Pichani) wakichangia mada wakati wa semina hiyo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), (wanne kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (katikati) wakati wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mbunge wa Mchinga ambae pia ni mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (wa tatu kushoto) wakati wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mbunge wa Mchinga ambae pia ni mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (wa tano kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Kwa heri! Maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (katikati) wakimuaga Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI MABULA ASITISHA VIBALI VYA UJENZI WA VITUO VYA MAFUTA
MECHI ZENYE ODDS KUBWA MERIDIANBET WIKIENDI HII
REGINA NDEGE-TUMUUNGE MKONO RAIS SAMIA
MATUKIO; MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIANCHI MISRI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi akitoa ufafanuzi kwa wageni waliotembelea banda la banda la maonesho la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
MERIDIANBET YAWASHIKA MKONO HOSPITALI YA TUMBI
KAMPUNI ya Meridianbet iliyoambatana na timu nzima ya masoko, akiwemo meneja masoko wa kampuni hiyo Ndugu Matina Nkurlu, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Maudhui Bw Twaha Ibrahimu, leo Novemba 11, 2022 ilitembelea Hospital ya Rufaa ya Tumbi mkoa wa Pwani, kwaajili ya kutoa msaada wa vifaa kwa matumizi ya wagonjwa katika hospitali hiyo.
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya chini ya Waziri mwenye dhamana hiyo Mhe Ummy Mwalimu, Meridianbet iliguswa na mahitaji ya hospital hiyo na hivyo waliamua kuchangia neti, barakoa na vifaa vingine ikiwa ni sehemu ya utamaduni wao wa kurudisha kwa jamii kile kidogo wanachokipata.
Meridianbet pamoja na uongozi wa Hospitali ya Tumbi walishiriki owa pamoja katika zoezi hilo la kukabidhiana vifaa hivyo, na mara ya kukamilika kwa zoezi la kutoa msaada huo, mwakilishi kutoka Hospitali hiyo, Christina Salusi alitoa shukrani zake kwa kampuni ya Meridianbet kwa msaada huo.
"Kwa niaba ya Uongozi na Menejimenti nzima ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, napenda kuwashukuru kampuni ya Meridianbet kwa kuguswa na kuamua kutoa msaada huu mkubwa wa vifaa vya matibabu, hakika hili ni jambo kubwa kwetu na kwa jamii nzima" alisema Christina Salusi- Muuguzi.
Aidha timu nzima ya Meridianbet walioambatana na Meneja Masoko Matina Nkurlu hawakusita kuzungumza kile kilichowasukuma kutoa msaada huo tena kwa mara ya kwanza kwa Hospitali ya Mkoa wa Pwani-Tumbi.
"Sisi kama Meridianbet huwa tuna utamaduni wa kutoa kwa jamii kile kidogo tulichopata kama faida kwenye biashara yetu, na hii sio mara ya kwanza tumewahi kufanya kwenye hospitali ya Mwananyamala, Amana n.k
“Na tumeamua kuja hapa Hospitali ya Tumbi ili kuwashika mkono katika juhudi zenu za kuokoa maisha ya wapendwa wetu, hivyo tunawaahidi kuendelea kushirikiana nanyi" Twaha Ibrahimu
Hata hivyo, Muuguzi ndugu Salusi alitoa nafasi ya wawakilishibwa Meridianbet kutembelea baadhi ya maeneo katika Hospitali hiyo ili kuwajulia hali wagonjwa waliofika kutibiwa. Moja ya eneo lililotembelewa ni wodi ya wajawazito ambao nao hawakusita kutoa neno lao kwa kampuni hiyo namba moja Tanzania na Afrika Mashariki kwa michezo ya kubashiri kutokana na msaada huo.
Mmoja ya wazazi waliojifungua katika hospitali hiyo, Bi Zuwena Rashi mara baada ya kupokea msaada huo hakusita kuonesha hisia zake za furaha.
"Kwakweli mimi kama mzazi nimefurahishwa na hiki mlichokifanya kwetu, nawashukuru sana kampuni ya Meridianbet kwa kugusa maisha yetu, hususani ya mama wajawazito na wagonjwa wengine, msaada huu utasaidia wagonjwa wengi wanaotibiwa kwenye Hospitali ya Tumbi" -Zuwena Rashid
Kampuni ya Meridianbet inapenda kuushukuru Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Mkoa wa Pwani, kwa ushirikiano wao walioutoa mwanzo wa zoezi mpaka mwisho, na unapongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali hiyo kuokoa maisha ya watanzania wengi na kurejesha matumaini zaidi. Unaweza kubeti Meridianbet kwa dau dogo la kuanzia TZS 250/= kwa kupiga *149*10#.
Mbali na michezo ya kubashiri, pia Meridianbet wana michezo mingine mingi ya kasino mtandaoni, unaweza kucheza mchezo wa Aviator ukawa rubani wa maisha yako, kuna mchezo wa Roulette, Poker, n.k. Pia Kampuni hiyo inaendesha promosheni kibao ya michezo ya kubashiri, ambapo unaweza kujishindia Bajaji droo hii itatangazwa Novemba 22 mwaka huu, lakini pia kuna promosheni ya SHINDA TV ya Inchi 50 kubeti kwa USSD Code.
DKT. KIRUSWA ATATUA MGOGORO BAINA YA MWEKEZAJI NA JAMII BUTIAMA
KINGAI, KAGANDA, MWAMBASHI WALA KIAPO KUWA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISII DODOMA LEO
DCI KINGAI, KAMISHNA KAGANDA NA SACP MWAMBASHI WALA VIAPO KUWA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI, MAGEREZA, ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA UHAMIAJI JIJINI DODOMA LEO NOVEMBA 11, 2022.
Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu wa Jeshi la Polisi, Suzan Kaganda akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Gerson Mdemu, jijini Dodoma leo Novemba 11, 2022. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
TPSF yazindua maadhimisho ya Siku ya Sekta Binafsi
MELI KUBWA YENYE WATALII ZAIDI YA 1500 KUTOKA MAREKANI IMEWASILI NCHINI TANZANIA
BILIONI 200 ZIMETENGWA KWAAJILI YA UNUNUZI WA DAWA NA VIFAA TIBA- DKT.MOLLEL

KIKAO CHA TATHMINI YA USAJILI WA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA MITANO- TABORA
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani ameongoza Kikao cha Tathmini ya Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya Miaka Mitano ulioanza kutekelezwa mkoani Tabora Mwezi June 2022.
Katika hotuba yake Dkt. Buriani amesema kwamba Usajili kupitia mpango huu umeweza kuongeza kiwango cha Usajii wa Watoto kwa Mkoa wa Tabora kutoka asilimia 9 mpaka asilimia 49 hivyo kuna ongezeko la asilimia 40.
Ameongeza kwamba Mkoa utahakikisha kwamba watoto wote ambao hawajapata huduma wanasajiliwa kwani ni haki yao ya Msingi ya Kutambuliwa na kuwataka Wasajili wasaidizi wote waendelee kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu ili kuhakikisha watoto wanaopata vyeti vya kuzaliwa ni wale tu wanaostahili.
Akiwasilisha salamu za Wizara ya Katiba na Sheria, Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuleta maboresho ya mfumo wa usajili kupitia Mkakati wa Kitaifa wa Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu na kuongeza kwamba Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya Miaka Mitano ni uthibitisho wa sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha watoto wanasajiliwa na kupata nyaraka ya awali na ya msingi ya utambulisho ambayo ni cheti cha kuzaliwa.
Naye Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi. Angela Anatory ameeleza kwamba Mpaka sasa Mpango huu unatekelezwa katika Mikoa 23 ya Tanzania Bara ambapo zaidi ya watoto 8,106,469 wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa hivyo kuongeza kiwango cha usajili wa watoto nchini kutoka asilimia 13 na kufikia asilimia 65 hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano katika kuleta mageuzi makubwa katika usajili barani Afrika.


.jpeg)
NUNUA TIKETI YA USHINDI KWENYE KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET
Maji ya kuingia Mto Ruaha yamezuiliwa na shughuli za Kibinadamu
Uvuvi haramu changamoto nyingine kwenye mto Ruaha kukauka
Mfuko wa Samaki zilizoharibika zilizotelekezwa wakati operesheni wa Askari wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Ruaha wakati walivyofanya operesheni eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi 'Afande Sele' akionesha Mtumbwi ulioharabiwa na Askari wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Ruaha wakati walivyofanya operesheni eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi akizungumza na waandishi habari kuhusiana Uvuvi haramu unaofanyika kwenye Mto Ruaha na Hifadhi ya Ruaha katika eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
DKT.JAFO-TANZANIA YAFANYA VIZURI MWONGOZO HEWA UKAA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu maswali ya Waandishi wa Habari pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini China na Misri kwenye Mkutano uliofanyika leo Novemba 12, 2020 Ikulu Jijini Dar es Salaam
BIRIANI FESTIVAL NA COCA-COLA AWAMU YA PILI KUFANYIKA DODOMA
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutangaza Tamasha hilo la Birian Friday na Coke, Meneja Biashara na Masoko Coca-Cola Kwanza Wahida Mbaraka alisema kuwa tamasha la Birian Festival na Coke awamu ya pili itafanyika Dodoma mnamo tarehe 26 Novemba mwaka huu.
‘Kwenye tamasha ili, tutawakutanisha kwa Pamoja wapishi wa Biriani wa mkoa huu na wateja wao, tamasha la mwaka huu litakuwa ni la kipekee kabisa na utofauti mkubwa, sababu tutaweza kupata Ladha pia ya vyakula vya asili vya Dodoma, Vionjo vingi vya kiasili ambavyo vinabeba utaifa wetu, na vile vile kuangalia mechi za Kombe la Dunia’, Mbaraka alisema.
Mbaraka aliongeza kuwa kutakuwa na Migahawa Zaidi ya 15, Michezo ya Watoto wetu, tukiburudishwa na Bendi ya Bushoke na Dj mkali Dj D-ommy Pamoja na burudani nyengine nyingi, na zawadi mbali mbali.
Kupitia jukwaa hili napeda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watanzania wote, wapenzi na wadau wa biriani na Coca-Cola, Familia, Marafiki kuja kujionea na kushiriki kwenye utamaduni huu, Tanzania nchi yetu, Dodoma ndio makao makuu yetu, Biriani na Coca-Cola ndio chaguo letu na Mpira wa Kombe la dunia ndio raha yetu.Tarehe ni 26/11/22 ( Jumamosi), Mahali ni viwanja vya wajenzi Maili Mbili Dodoma,kuanzia saa nne asubuhi, aliongeza Mbaraka.


DCB yashinda Tuzo ya Benki Bora kwa Kutoa huduma Bora kwa Wateja Nchini.
BENKI ya Biashara ya DCB imesema ushindi wa benki bora katika utoaji huduma kwa benki zenye ukubwa wa kati ilioupata, umetokana na mabadiliko makubwa iliyoyafanya katika mfumo mzima wa utoaji wa huduma kwa wateja wao.
Akizungumza katika hafla za utoaji zawadi za Tuzo za Chaguo la Mlaji Afrika (CCAA) jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema ushindi huo uliotokana na uboreshaji mkubwa walioufanya katika huduma zao umekuja kwa wakati mzuri kipindi hiki DCB ikisherehekea miaka 20 tokea ilipoanzishwa.
“Kwa niaba ya familia ya DCB, napenda kushukuru sana wateja wetu na wasio wateja wetu kwa kutupigia kura kwa kuwa benki bora kabisa nchini kwa kutoa huduma bora, kupata tuzo hii kunazidisha furaha yetu wakati tukiendelea kusherehekea miaka 20 ya benki yetu.
“Mimi na wafanyakazi wenzangu tunafuraha kuona wateja wetu wameweza kuona uboreshaji mkubwa tulioufanya wa jinsi tunavyowahudumia, hii ni safari tuliyoanza miaka minne iliyopita na tunashukuru kuona matunda yake yanaonekana na wateja wameweza kuyaona,” alisema Bwana Ndalahwa.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mafanikio hayo wao kama wanafamilia wa DCB wanayachukulia kama changamoto ya wao kuzidi kuboresha zaidi huduma zao na kuwa zaidi ya mahali walipo.
Hii ni mara ya pili kwa DCB kushinda tuzo hii japo kwa mara ya kwanza mwaka 2021 ilitwaa ushindi wa pili wa tuzo hizi zenye lengo la kuleta ushindani kati ya makamapuni na biashara mbali mbali barani Afrika, kuhamasisha utoaji huduma na bidhaa bora kwa wateja pamoja na kutambua kazi bora za watoa huduma.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB, Dk. Amina Baamary (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa (wa nne kushoto), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakishangilia mara baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa kwanza ya Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora kwa Wateja nchini kwa mwaka 2022 katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa Tuzo za Chaguo la Mlaji Afrika (CCAA) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
MWENYEKITI WA CCM, RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (NEC), MAKAO MAKUU YA CCM JIJINI DODOMA LEO
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Makao Makuu ya CCM (White House) jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA CCM MAKAO MAKUU)
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo akizungumza katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu, Makao Makuu ya CCM (White House) jijini Dodoma.Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu, Makao Makuu ya CCM (White House) jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Makao Makuu ya CCM (White House) jijini Dodoma. Kushoto wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia kwa karibu.