Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48983 articles
Browse latest View live

TUME YA UCHAGUZI YAENDESHA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UCHAGUZI MDOGO MOROGORO

$
0
0

 

 Na Mwandishi Maalum, Morogoro

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka  katika Kata zinazotaraji kufanya uchaguzi mdogo wa udiwani Desemba 17, 2022 kutofanya kazi ya uchaguzi kwa mazoea, badala yake wazingatie sheria, kanuni za uchaguzi pamoja na maelekezo ya Tume katika utendaji wao.
 
Tume pia imewataka wasimamizi wa nchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuhakikisha wanavishirikisha Vyama vyote vya  Siasa na wadau wengine wa uchaguzi ili kurahisha utekelezaji wa majukumu yao.
 
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adv. Magdalena Rwebangira wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi wa Uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata yanayofanyika Mkoani Morogoro.
 
Adv. Rwebangira amesema Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha, hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kupunguza kama siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
 
“Nachukua nafasi hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa  uchaguzi, ni vyema mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea”,alisema Adv. Rwebangira.
 
Aidha amewataka kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, na kwamba katika utendaji wa majukumu yao wanapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume na kuongeza kua jambo hilo lisiishie katika mafunzo na nadharia bali ionekane kufuatiwa katika kutenda.
 
“Sanjari na hilo nawaasa kukumbuka kuvishirikisha Vyama vya Siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika  maeneo yenu katika masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia sana  utekelezaji wa majukumu yenu,”alisema Adv Rwebangira.
 
Wasimamizi hao wametakiwa kuhakikisha wanayatambua na kuyajua  vizuri maeneo ambayo chaguzi utaendeshwa ikiwemo hali ya miundombinu ya kufika katika Kata na hasa Vituo vya kupigia kura.
 
“Mfanye utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo husika kwa lengo la  kuhakikisha mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani,”alisema Adv. Rwebangira.
 
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adv. Magdalena Rwebangira pia amewataka wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanaajiri watendaji wa vituo wenye weledi, wanaojitambua na kwa kadri inavyowezekana kuacha undugu au upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi.
 
Alisema jambo muhimu wanalotakiwa kuzingatia Wasimamizi hao wa uchaguzi ni kujiamini, kufanya kazi kwa weredi na kuzingatia Katiba ya nchi, sheria za uchaguzi na kanuni zake, maadili ya uchaguzi pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume.
 
Aidha Mjumbe wa Tume hiyo ya uchaguzi, aliwasisitizia wasimamizi hao wa uchaguzi kuhakikisha wanafanya utambuzi wa vituo vya uchaguzi mapema kwa lengo la kuhakikisha mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.
 
Naye  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Stephen Elisante, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi alisema uchaguzi huo mdogo wa udiwani utafanyika  katika Kata 12 za Tanzania Bara ila waliopo katika mafunzo hayo Mkoani Morogoro ni kutoka katika Kata sita za Vibaoni – Halmashauri ya Mji wa Handeni, Lukozi – Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Misugusugu – Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Majohe - Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mnyanjani - Halmashauri ya Jiji la Tanga na Dunda -  Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
 
Mapema kabla ya ufunguzi wa Mafunzo hayo watendaji w uchaguzi hao walikula kiapo cha kutunza siri na kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vyao vya siasa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro, Mhe. Japhet Bwire Manyama.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adv. Magdalena Rwebangira akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi Uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi pamoja na watendaji wengine wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa udiwani unaotaraji kufanyika tarehe 17 Desemba, 2022. Mafunzo hayo yanayohusisha washiriki 42 kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na  Lushoto yanafanyika Mkoani Morogoro. 

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adv. Magdalena Rwebangira akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi Uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi pamoja na watendaji wengine wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa udiwani unaotaraji kufanyika tarehe 17 Desemba, 2022. Mafunzo hayo yanayohusisha washiriki 42 kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na  Lushoto yanafanyika Mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi, Stephen Elisante na wengine kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Tume, Felister Ishuza na Mwenyekiti wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Handeni, Maryam Ahmad Ukwaju. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. 
Mwenyekiti wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Handeni, Maryam Ahmad Ukwaju akizungumza wakati wa mafunzo hayo. 
Sehemu ya washiriki ambao ni Wasimimizi wa uchaguzi na Wasimamizi wasaidi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na  Lushoto yanafanyika Mkoani Morogoro wbakifuatilia mafunzo hayo. 
Sehemu ya washiriki ambao ni Wasimimizi wa uchaguzi na Wasimamizi wasaidi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na  Lushoto yanafanyika Mkoani Morogoro wbakifuatilia mafunzo hayo. 
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Japhet Bwire Manyama akiongoza kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri kwa wazimamizi na wasimamizi wasaidi wa uchaguzi wakati wa mafunzo ya wasimamizi hao kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Tanga Jiji na  Lushoto ambao wanataraji kufanya uchaguzi mdogo katika kata zao Desemba 17,2022. 
Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wakilakiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Japhet Bwire Manyama wakati wa mafunzo ya wasimamizi hao kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Tanga Jiji na  Lushoto ambao wanataraji kufanya uchaguzi mdogo katika kata zao Desemba 17,2022. 

Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wakilakiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Japhet Bwire Manyama wakati wa mafunzo ya wasimamizi hao kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Tanga Jiji na  Lushoto ambao wanataraji kufanya uchaguzi mdogo katika kata zao Desemba 17,2022.



JAFO: WOTE WALIOVAMIA VYANZO VYA MAJI WAONDOKE MARA MOJA.

$
0
0

 


Na. Jacob Kasiri -Ruaha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) amewataka wananchi wote waliovamia bonde la Ihefu ambalo ni chanzo cha mto Ruaha Mkuu kuondoka mara moja ili kuondokana na athari zilizopelekea mto Ruaha Mkuu kutotiririsha maji kwa miezi mitatu mfululizo.

Ameyasema hayo leo katika kikao kilichowahusisha Mawaziri nane wa Kisekta, Makatibu wakuu, wakuu wa Mikoa pamoja na wataalam kilichofanyika katika Hifadhi ya Taifa Ruaha iliyoko mkoani Iringa.

“Wale wote waliovamia vyanzo vya maji tumeazimia waondoke haraka iwezekanavyo, swala la kuondoka halina mjadala wa kusubiri mwezi au miezi miwili. Mara baada ya kikao hiki cha leo Novemba 15, 2022 wote waliovamia vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu mkubwa mnatakiwa kuondoka mara moja. Hii kauli tukisema mara moja ni kuanzia leo,” amesisitiza Waziri huyo.

Waziri Jafo ametaja sababu za kukauka kwa mto Ruaha Mkuu ni pamoja na uingizaji wa mifugo ndani ya bonde la Usangu na kwenye ardhi oevu ya Ihefu, uchepushaji wa maji toka kwenye mito inayoingiza maji bonde la Usangu unaofanywa na baadhi ya wakulima wasiofuata sheria na taratibu pamoja na ukataji na uchomaji wa misitu unaosababisha ukame na uharibifu wa mazingira.

Eneo la darajani ambalo Mawaziri, wakuu wa Mikoa na wataalamu hao wamelitembelea ni moja ya kivutio ndani ya hifadhi hii pindi mto Ruaha Mkuu unapokuwa unatiririsha maji yake ambapo watalii hushuka na kupiga picha mbalimbali kutokana na mandhari nzuri ya beta (meanders) za mto huo, sasa hivi yamesalia madimbwi yenye maji machache na machafu yanayopelekea maisha ya viboko, mamba, samaki na wanyama wengine wanaotegemea maji hayo kuwa hatarini.

“Mambo ya haraka ili kunusuru hali hii ni pamoja na Mamlaka ya bonde za maji kusimamia sheria iliyopitishwa na Bunge 2022 inayoelekeza wale wote wanaochepusha maji kinyume cha sheria kuchukuliwa hatua. Pia naelekeza Mamlaka ya bonde za maji pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kubaini wale wote waliovamia vyanzo vya maji waondoke haraka”, aliongeza Waziri huyo.

Uhai wa hifadhi ya taifa Ruaha hutegemea mto Ruaha Mkuu, hivyo kukauka kwake hakutaathiri tu hifadhi hii katika shughuli za utalii na uhifadhi bali pia itaathiri shughuli za kiuchumi kama vile uzalishaji wa umeme, kilimo na uvuvi unaofanyika katika bwawa la Mtera. Kama tujuavyo zaidi ya asilimia 65 ya umeme unaozalishwa kwa njia ya maji nchini Tanzania hutegemea maji yanayotokea bonde la Ihefu kupitia mto Ruaha Mkuu.





TADB KUWAJENGEA UWEZO WAKULIMA WA MAKUNDI MAALUM

$
0
0



Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeonyesha kwa vitendo nia yake ya kuinua wakulima wadogo wa makundi maalum nchini kwa kufanya mafunzo ya siku 3 kwa Kituo cha Wakulima Wafugaji Viziwi Tanzania (KIWAWAVITA) yaliyoandaliwa na TADB katika katika ukumbi wa Edema, mkoani Morogoro.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo kwa nadharia na vitendo wakulima hao wa kituo hicho cha Wakulima na Wafugaji Viziwi Tanzania ili wainuke kiuchumi na kuongeza uzalishaji wa tija.

Mafunzo hayo yalijumuisha mada kama:


Elimu ya Fedha na Biashara
Huduma zinazotolewa na TADB
Kilimo cha Mbogamboga
Kilimo cha Kisasa


Mafunzo hayo ni muendelezo wa mpango wa TADB katika kufikia wakulima wa makundi maalum ili kuwajengea uwezo wakulima wadogo nchini waweze kutoka katika kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha kibiashara.






Walioko kwenye vyanzo vya maji waondoke

$
0
0


Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika  la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) William Mwakilema akionesha kukauka Mto Ruaha wakati Mawaziri Nane waliofika hapi kuangalia Mto huo Msembe Iringa. *Ni kutokana na kuchangia Mto Ruaha kukauka na kuleta madhara

*Mwakilema :Ihefu ambayo ni tegemeo yaingiliwa na kilimo na ufugaji

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv, Msembe ,Iringa
SERIKALI imesema kuwa waliopo katika vyanzo vya Maji wasitishe shughuli zao za kilimo kutokana na kuchangia kukauka kwa mto Ruaha Mkuu.

Hayo ameyasema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dk.Seleman Jafo kwenye mkutano wa mawaziri nane uliofanyika Makao Makuu ya Hifadhi ya Ruaha iliyopo Msembe mkoani Iringa.

Kabla ya mkutano huo umechukua masaa matatu ya viongozi kujadiliana kutokana na hali waliokuta katika mto Ruaha ukiwa umekauka.

Dk.Jafo amesema kukauka mto Ruaha umeathiri shughuli za kiuchumi ikiwemo mgao wa umeme pamoja kutokuwa na maji ya matumizi ya nyumbani katika mkoa wa Dar es Salaam.

Dk.Jafo ameagiza bodi za bonde za maji na Baraza la Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira kusimamia vyanzo vya maji kwa wale waliochepusha na wale wanaotumia maji kwa mujibu wa vibali kuangalia suala hilo.

Amesema kuwa suala la Ruaha tangu 1994 maji yanaacha kutiririka mwezi wa tano hiyo ni kutokana na shughuli za kibidamu kuendelea kwenye vyanzo vya maji.

Aidha amesema kwa kipindi hiki wanyama wakiwemo viboko wako katika hali mbaya hivyo tuombe mvua zinyeshe kwa kipindi kifupi viboko hao waendelee kuishi vinginevyo watakufa.

Naye Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) William Mwakilema amesema ukame wa Mto Ruaha ni hatari kwa wanyama na hii ni kutokana bonde la Usangu/Ihefu kuendelea kwa shughuli za kilimo za kuzuia maji kwenye mto Ruaha.

Mwakilema amesema jitihada mbalimbali zinafanyika za kuweza Mto Ruaha kuwa na maji kwa vipindi vyote kutokana na mto huo kuwa na tegemeo kwa Taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa  Rais Mazingira na Muungano  Dk.Seleman Jafo akizungumza na mawaziri na viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa kujadili kukauka kwa mto Ruaha Mkuu na madhara yaliyotokea kwenye Mto huo Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Hifadhi ya Ruaha Msembe ,Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Pindi Chana akitoa maelezo kuhusiana na mto Ruaha Mkuu na madhara kwa wanyama kwenye Mkutano  wa Mawaziri Nane waliofika kujionea kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu uliofanyika Makao Makuu Hifadhi ya Ruaha Msembe,Iringa


KOMBE LA DUNIA NA MACHAGUO SPESHO MERIDIANBET TWEN'ZETU KIBINGWA QATAR

$
0
0

  


KILA baada ya miaka minne wapenda soka kote duniani huwa wanaungana na kushuhudia utamu wa burudani ya macho na moyo nikimaanisha hisia zote huwa uwanjani. Ndio Namaanisha Kombe la Dunia, ni jukwaa maalum kabisa la Mabingwa kuonesha ukali wao na Mabingwa wenzao.

Na wewe una nafasi ya kuonesha ubingwa wako kwa kubeti kwenye nyumba ya Mabingwa, Meridianbet ambao safari hii hawana jambo dogo kwenye Kombe la Dunia, kwani wamekuongezea machaguo spesho na rahisi.

Ni Mataifa 32 mechi 64 kutoka mabara 6 ambayo ni mwanachama wa FIFA, Afrika, Ulaya, Asia, Amerika Kusini na Kaskazini na nchi za Carribean. Meridianbet wanakupa Odds bomba na kubwa kuliko kawaida, msimu huu wa Kombe la Dunia, ndiyo maana wanakwambia Twendezetu Kibingwa Qatar. Machaguo spesho ya kombe la dunia.

Leo nataka kukwambia jambo jipya kutoka Meridianbet, lakini kabla ya yote nataka kukujuza kwa ufupi tu kuhusu Kombe la Dunia, hili ni Kombe la pili kutengenezwa baada ya lile la kwanza kuchukuliwa moja kwa moja na nchi yenye vipaji vingi na vya Soka ni Brazil mara ya mwisho wakilichukua mwaka 2002 na kuliweka kabitini na ndio nchi iliyochukua mara nyingi Zaidi, mara 7 wakifuatiwa na Ujerumani aliyechukua mara 4.


Si unawakumbuka magwiji hawa, Ronaldo Delima, Ronadinho, Kaka, Roberto Carlos, huko Brazil pia ndiko wanatoka nyota kama Neymar Jr, Vinicious Jr, Antony, Casemiro. Odds bomba za Kombe la dunia meridianbet.

Kombe la Dunia lina urefu wa sentimita 36.8 na uzito wa 6.1 kg, thamani yake ni dola za Marekani milioni 42 sawa na TZS Bilioni 96.6 ambazo mshindi wa kwanza anazinyakua. Hili ndio kombe lenye thamani kubwa zaidi kuliko makombe yote unayoyajua wewe. Machaguo spesho ya kombe la dunia yapo Meridianbet.


Ukiachana na Mabingwa wengine hata wewe pia ni bingwa wa maisha yako, itoshe kusema tu wewe ni mfalme, au wewe ni Malkia kwenye himaya yako na unaweza kuwa mfalme na Malkia ukibeti kwenye nyumba ya mabingwa ya Meridianbet ambao wamekuwekea machaguo spesho ya kombe la dunia na ni rahisi kushinda, na kujitengenezea utawala wako. Pia kuna michezo mingine ya kasino mtandaoni kama vile Aviator, Roulette na Poker. Beti sasa.


Nikudokezee tu kwa uchache bila kumaliza utamu wote, timu zinazoshiriki kombe la dunia zipo 32, unaweza kubeti timu gani itafuzu robo fainali, au timu gani itafuzu nusu fainali, timu gani itachukua kombe machaguo hayo yana odds bomba na kubwa zaidi.

Usisahau kuna timu zinatoka Afrika kama vile Senegal yenye Sadio Mane, Tunisia, Ghana n.k unaweza kubeti ni timu gani ya Afrika itafuzu robo fainali au hata kama unahisi itachukua ubingwa, nafasi ni yako tu na Machaguo spesho yapo kwaajili yako bingwa wa kubeti.

RATIBA YA KOMBE LA DUNI HII HAPA

$
0
0

 Ratiba ya Mashindano ya Kombe la Dunia FIFA imetoka.






Kishindo cha UWT Njombe, Mwenyekiti Scolastika Kevela atetea kiti chake sasa kuludi upya

$
0
0

Njombe
JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Njombe umemchagua Scolastika Kevela kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kura 242 kati ya kura 266.Scolastika Kevela ametetea kiti hicho mara baada ya kuwa mwenyekiti tangu alipochaguliwa March 2021 kutokana na aliyekuwa mwenyekiti kuwa diwani mjini Makambako.

Mara baada ya kuchaguliwa tena na kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyi Bi Kevela amesema.

“Sio kazi nyepesi lakini nimeshinda kwa kishindo,ninawashukuru wajumbe wa mkutano Mkuu wa mkoani wa Njombe kwa kunichagua lakini pia hata halmashauri kuu kwa kurudisha jina langu maana kuja kuwa mgombea ni mchakato ninashukuru kwa kuaminiwa”Scolastika Kevela Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe

Ameongeza kuwa “Ahadi yangu kwa UWT ni huduma zilizotukuka,tuna vipaumbele vinci kwa sasa ikiwemo kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha Sabuni ambapo kengo liko tayari na kilichobaki mwaka huu ni kufunga mashine ili uzalishaji uweze kuanza kwa ajili ya kukuza uchumi wa UWT”Scolastika Kevela Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe

Naye Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Julius Peter ameagiza kuvunjwa kwa makundi yote yaliyokuwapo katika jumuiya ya wanawake UWT mkoa wa Njombe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi ndani ya chama hicho na kwamba hivi sasa kinachotakiwa ni kuungana kufanyakazi.

Baadhi ya wanawake wa UWT akiwemo Esteria Mbwilo,Tumain Mtewa na Neema Mbanga wamesema wanamatumaini makubwa toka kwa Viongozi wao katika kuhakikisha maendeleo yanasonga.

Msimamizi wa uchaguzi huo Juma Sweda ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Makete amesema Wajumbe hao wamemchagua Scholastica Kevela kuwa mwenyekiti wao kwa kumpa zaidi ya kura 200.

TPDC YAZIGARAGAZA BENJAMINI MKAPA HOSPITALI, TPHPA MICHUANO YA SHIMUTA TANGA.

$
0
0

Kikosi cha timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanaume

Kikosi cha timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanawake

Na Oscar Assenga, TANGA

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya kuvuta kamba kwa upande wa wanaume leo wameibuka kidedea kwenye mchezo wa kuvuta kamba baada ya kuwavuta timu ya Benjamini Mkapa Hospitali kwa seti 2-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ulifanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly Jijini Tanga ambapo wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya TPDC walionekana kuwa makini jambo ambalo liliwawezesha kuibuka na ushindi huo

Baada ya timu hiyo ya wanaume kumaliza kuvuta kamba iliingia upande wa wanawake ambapo timu ya Shirika hilo nayo iliweza kuibuka kidedea baada ya kuwavuta wanawake wenzao wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu (TPHPA) kwa seti 2-0.

Timu ya TPDC ya kuvuta kamba iliwakilishwa vema na wachezaji wake mahiri ambapo kwa upande wa wanaume iliongozwa na Nahodha Joram Ndalahwa,Nnocent Mvamba,Adam Sajilo na Joseph Majebele.

Kwa upande wa timu ya wanawake iliwakilishwa vema na Rehema Saidi,Robi Chambiri,Catherine Madinda na nahodha wao Joyce Kiheka .

Naibu Waziri wa fedha Chande azindua Consortium ya mafuta na gesi

$
0
0

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Serikali imepongeza umoja wa makampuni 22 ya bima nchini ambao utafanya kazi kwenye miradi mikubwa ya mafuta na gesi na kuiwezesha serikali kupata pato la taifa kupitia ada ya kinga dhidi ya vihatarishi mbalimbali.

Pongezi hizo zilitolewa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Hamad Chande katika uzinduzi rasmi wa muungano huo ujulikanao kwa jina la Tanzania Energy co-insurance Consortium au Consortium ya mafuta na gesi uliofanyika juzi usiku kwenye hotel ya Johari Rotana jinini Dar es Salaam.

Bw Chande alisema kuwa umoja huo ni wa kwanza hapa nchini na serikali itaongeza pato la taifa kupitia ada za bima ambazo sasa zitabakia hapa nchini tofauti na zamani.

Alisema awali, uwezo mtaji wa kampuni mojamoja za bima nchini haukuweza kukidhi vigezo vya ada ya kinga dhidi ya vihatarishi na kufanya miradi mingi ya uwezekaji katika sekta hiyo kuingia mikataba na makampuni ya nje ya nchi.

“Kutokana na sababu hizom, pato la taifa upotea kwani fedha za ada ya bima uchukuliwa na makapuni ya nje kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha.

Kupitia umoja huu, sasa makampuni ya uwezekaji wa nje yataweza kukata bima zao hapa nchini ili kukikinga na vihatarishi katika sekta ya mafuta na gesi,” alisema Bw Chande.

Alifafanua kuwa muungano huo unaongeza uwezo wa kuhimili vihatarishi hivyo na kusaidia ubakishaji (retention)za fedha za ada nchini kwa maendeleo ya taifa.

“Uhitaji wa muungano huu ulianza uhitaji mwaka 2019 kuelekea mwaka 2020 baada ya miradi mikubwa kama East Africa Crude Oil Pipeline) wenye thamani ya Dola bilioni 3.5 na mradi wa LNG (Gas Processing Plant) wente thamani wa dola za Kimarekani Bilioni 30, miradi mikubwa ya madini na kilimo.

Kutokana na thamani ya miradi hiyo kuwa kubwa, bima ya kinga dhidi ya vihatarishi ulipelekea uhitaji wa bima mtawanyo ambayo kwa asilimia kubwa ilinunuliwa kwa kampuni ya bima mtawanyo za nje na hivyo kupelekea fedha nyingikama malipo ya ada ya kukinga miradi hiyo dhidi ya vihatarishi kuzinufaisha nchi hizo,”alisema Bw Chande.

Alisema kuwa “Kutokana na mtaji mdogo wa makampuni ya hapa nyumbani, ilipelekea uhitaji wa kuundwa kwa umoja huo ili kuunganisha uwezo wa kampuni za ndani dhidi ya vihatarishi maalum ili kuweza kuhimili vihatalishi hivyo na kubakisha ada na kuongeza pato la Taifa,” alisema.

Kwa upande wake, Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt Baghayo Saqware alisema kuwa umoja huo unazifanya kampuni hizo 22 kuunganisha mitaji na kuwa na uwezo wa kuhimili vihatarishi vya miradi hiyo mikubwa pamoja na mradi gesi asilia wa Lindi wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 30 ambao unatarajiwa kutekelezwa hivi karibuni.

Bw Saqware alisema kuwa muunganiko huo utaleta faida mbalimbali kama kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha na kitaaluma kwa kampuni za bima, kuongeza uhifadhi wa ndani na uendeshaji mzuri wa hatari miongoni mwa kampuni za bima na bima mtawanyo, kulinda maslahi ya watanzania na kuongeza uwezo wa ndani kulingana na mahitaji ya kisheria (local content requirement) na kuongeza ajira.

Alisema faida nyingine ni kutoa mpangilio wa haki, uwazi na wenye usawa kwa kushirikisha wadau wengine wa bima katika sekta ya mafuta na gesi na kuongeza ujuzi na utaalam wa kuandikisha bima ya vihatarishi maalum kwa kupitia uzoefu utakaopatikana katika umja huo wa mafuta na gesi.

Wakati huo huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bima ya Phoenix AssuranceBw Ashraf Musbally alisema kuwa ndani ya wiki chache zijazo watatoa muongozi kwa wadau mbalimbali kuhusiana na malengo yao ya muda mfupi na mrefu.

Bw Musbally alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kuona wazo lao limeungwa mkono na wadau wa sekta hiyo na wanaamini litaleta tija katika maendeleoya sekta ya bima hasa kwa upande wa gesi na mafuta.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Chande (wa nne kulia) akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bima ya Phoenix Assurance Bw Ashraf Musbally (wa pili kushoto)moja ya mikataba ya umoja wa ushirikiano wa makampuni 22 ya bima nchini kwa ajili ya miradi ya mafuta na gesi
nchini. Wanao shuhudia makabidhiano hayo ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Dk Baghayo Saqware (wa tatu kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Nauritius (MUA)Joerg Webe (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanre Rajab Kakusa (wa kwanza kulia). Pia katika picha ni Khamis Selemani (kushoto) ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni ya Bima nchini (ATI)



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Chande (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua umoja wa ushirikiano wa makampuni 22 ya bima nchini (Tanzania Energy co-insurance Consortium) kwa ajili ya miradi ya mafuta na gesi nchini. Wanao shuhudia uzinduzi huo ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Dk Baghayo Saqware (wa tatu kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Nauritius (MUA)Joerg Webe (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanre Rajab Kakusa (wa kwanza kulia). Pia katika picha ni Khadija Said ambaye ni Naibu Kamishna wa bima Tanzania




Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Chande (wa tatu kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa makampuni ya bima na viongozi wa mamlaka ya usimamizi wa sekta hiyo (TIRA) na wadau wengine mara baada ya kuzindua umoja wa ushirikiano wa makampuni 22 ya bima nchini (Tanzania Energy co-insurance Consortium) kwa ajili ya miradi ya mafuta na gesi nchini.

TMA YATOA TAARIFA JUU WA UWEPO WA ONGEZEKO LA JOTO NCHINI

$
0
0

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa  taarifa juu ya uwepo wa ongezeko la joto katika maeneo mbalimbali nchini kufuatia kusogea kwa jua la Utosi.

Katika taarifa iliyotolewa na TMA leo Novemba 17, 2022 imesema kuwepo kwa ongezeko la joto katika baadhi ya maeneo nchini  ni hali ambayo inasababishwa na kusogea kwa jua la utosi sambamba na upungufu wa mvua katika maeneo mengi hapa nchini.

Taarifa hiyo inasema kwa kawaida vipindi vya jua la utosi nchini hufikia kilele mwishoni mwa mwezi Novemba wakati jua la utosi likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena mwezi Februari wakati jua la utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa).

 Imeelezwa, jua la utosi huambatana na hali ya ongezeko la joto kwa sababu uso wa dunia katika eneo tajwa huwa karibu zaidi na jua kuliko maeneo mengine. 

"Katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2022, hali ya joto imeongezeka  katika maeneo mbali mbali nchini ambapo kiwango cha juu zaidi cha joto cha nyuzi joto 36.9 0C kiliripotiwa katika kituo cha Mpanda, Katavi mnamo tarehe 26 Oktoba, 2022. " imesema sehemu ya taarifa hiyo. 

Taarifa hiyo imesema, ongezeko hilo la nyuzi joto 4.0 0C ukilinganisha na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Oktoba. Aidha, baadhi ya maeneo mengine yaliyokuwa na ongezeko la joto kwa mwezi Oktoba, 2022 ni pamoja na mkoa wa Tabora nyuzi joto 35.7 (ongezeko la nyuzi joto 3.0), Moshi nyuzi joto 34.1 (ongezeko la nyuzi joto 3.2) na Dar es Salaam nyuzi joto 32.8 (ongezeko la nyuzi joto 1.4).

Aidha, katika wiki mbili za mwanzo za mwezi Novemba, 2022; hali ya ongezeko la joto iliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo ambapo Novemba 2,2022  kituo cha Mpanda kiliripoti nyuzi joto 35.4 0C ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 4.7 ukilinganisha na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Novemba. 

Kituo cha Tabora kiliripoti nyuzi joto 34.8 ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 3.7, Dar es Salaam nyuzi joto 33.7 ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 2.1 pamoja na Kilimanjaro nyuzi joto 34.3  (ongezeko la nyuzi joto 2.4). 

"Vipindi vya ongezeko la joto vinatarajiwa kuendelea kujitokeza katika mwezi Novemba, 2022 hususan katika maeneo yanayotarajiwa kuendelea kuwa na upungufu wa mvua na kupungua kidogo ifikapo mwezi Disemba, 2022 ambapo ongezeko la mtawanyiko wa mvua unatarajiwa." imeelezwa na TMA 

Hata hivyo, TMA inaendelea kutoa wito kwa wananchi kufuatilia taarifa za mwenendo wa hali ya hewa zinazotolewa pamoja na kutafuta, kupata na kutumia ushauri wa wataalamu wa kisekta ili kuepuka au kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na hali mbaya ya hewa ikiwemo ongezeko la joto.

FANYENI KAZI MSIBUBIRI VYEO - AG FELESHI

$
0
0

 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akisisitiza jambo wakati Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniface Luhende na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Sara Mwaipopo walipomtembelea Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma na kisha kuwa na mazungumzo ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mawakili Wakuu wa Serikali na Mawakili Waandamizi wa Serikali.

Na Mwandishi Maalum, Dodoma
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amerejea wito wake wa kuwataka Watumishi waliopo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza majumuku yao kwa weledi , uaminifu na uadilifu na siyo kusubiri teuzi au vyeo.

Ametoa rai hiyo leo, alhamisi wakati wa mazungumzo yake na Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Bonifance Luhende na Naibu Wakili Mkuu Bi. Sara Mwaipopo waliofika Ofisini kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo na ambayo pia yalihudhuriwa na Menejimenti, Mawakili Wakuu na Mawakili wa Waandamizi wote kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Feleshi amesema, uongozi hautafutwi ,uongozi unakuja kwa kufanya kazi.

“ Niwapongeze kwa kuaminiwa na kuteuliwa kwenu na Mhe. Rais kushika nafasi hizo za uongozi. Uongozi hautafutwi, tekeleza majukumu yako, jukumu ulilonalo mkononi ndilo lako, timiza wajibu wako na mengine yatafuata”. Amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesisitiza haja na umuhimu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuwa na ushirikiano wa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake ambayo kimsingi Ofisi hiyo inatekeleza kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali .

Akielezea Zaidi kuhuhusu haja na umuhimu wa Ofisi hizo mbili wa kufanya kazi kwa Karibu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amebainisha kuwa taratibu kadhaa zimeshawekwa zikiwamo za kuwa na maafisa dawati wanaoratibu mawasiliano na ubadilishanaji wa taarifa kwa haraka na kwa wakati baina ya Ofisi hizo mbili.

Naye Wakili Mkuu Mkuu wa Serikali Dkt. Bonifance Luhende amemhakikishia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba, yeye binafsi, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi yote wanalichukulia suala na uhusiano na Ushirikiano na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa ni jambo la kipaumbele.

Dkt Lunhede amesema, Ofisi hizo mbili ni kiungo muhimu katika kuisadia Serikali kufikia malengo yake yakiwamo ya kuwaleta wananchi maendeleo, lakini pia ni Ofisi ambazo mambo mengi na mazito yanapita kwenye Ofisi hizo, mambo ambayo wakati mwingine yanahitaji ushauri wa haraka au maamuzi ya haraka hivyo ushirikiano na mawasiliano kati yake ni jambo ambalo halikwepeki.

“Ofisi zetu hizi zina mambo mazito yanayopita mikononi mwetu, mambo yanayohitaji wakati mwingine kutoa ushauri na maamuzi ya haraka kwa Serikali ili mambo yaweze Kwenda. Kwa hiyo kwetu sisi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jambo la ushirikiano na Ofisi yako, Mhe Mwanasheria Mkuu wa Serikali tunalipa kipaumbele” amesisitiza Wakili Mkuu wa Serikali .

Amebainisha kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inatekeleza majukumu yake kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivyo ni muhimu kwa Ofisi hizo kuwa na mwelekeo na maono ya Pamoja ili kuisaidia Serikali .

“Tunatekeleza majukumu yetu kwa niaba yako Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tunapaswa kuwa na maono na uelewa wa Pamoja, tunapaswa kucheza kama timu moja, hakuna mchezaji anayeweza kushinda bila ya ushiriki wa wachezaji wengne , lengo letu si kushindana bali kuisaidia serikali ishinde” Akasema Wakili Mkuu wa Serikali.

Aidha katika mazungumzo hayo, Ofisi hizo mbili pia zimekubaliana kuwatumia Mawakili wa Serikali waliomo katika Kanzi Data ya Mawakili wa Serikali inayoratibiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale watakapohitajika kuisaidia serikali kwa mijibu wa taaluma zao, uwezo na uzoefu wako katika masuala mbalimbali.

Octoba 10, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwateua Dkt. Boniface Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali na alimteua Bi. Sara Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

SAMAHA ATETEA KITI CHAKE UVCCM PWANI-AWAASA VIJANA KUKOMAA KISIASA NA KUACHA KUFANYIANA CHUKI

$
0
0

 

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MWENYEKITI wa umoja wa vijana Mkoani Pwani ( UVCCM) aliyekuwa akitetea nafasi yake ,Samaha Said amewaasa vijana kukomaa kisiasa na kuachana na siasa za chuki na kuchafuana.

Aliyayasema hayo baada ya kumalizika uchaguzi wa vijana Mkoani humo uliofanyika Picha ya Ndege Mjini Kibaha.

Samaha alieleza, ni bora kutengeneza kwenye siasa na kufanya siasa lakini waache chuki na kuchafuana ili kujiimarisha Jumuiya.

"Siasa ya vijana ni ndefu hivyo wasipende kuchafuana maana hawajui yule wanae mchafua atakuwa nani hivyo chuki na fitina zisiwepo bora tusema twende salama,"alisema Samaha.

Hata hivyo alieleza, kwa upande wa vijana hakuna maslahi binafsi bali ni kwa ajili ya chama na kazi za chama zinajulikana na kuwa uchaguzi umeisha kilichobaki ni kuitengeneza jumuiya na chama.

"Tushirikiane kukijenga chama tusameheane kwani hii itatufikisha pale tunapotaka kufika mmenikopesha imani nitawalipa imani hiyo kwani mmenipa kura nyingi,"alisema Samaha.

Vilevile alieleza, ataendelea kuleta mabadiliko na kuunganisha Jumuiya ili kuleta maendeleo na kuwataka kuachana na makundi .

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi Fatuma Ndee alimtangaza Samaha Said kuwa mshindi kwa kupata kura 223, akifuatiwa Adam Salehe Athuman aliyepata kura 204, Tengeneza Abuu kura tatu na Mkongo Mauli kura mbili.

Naye mjumbe wa baraza kuu la mkoa kuwakilisha Taifa Juma Kwangaya alisema kuwa ajenda za vijana kutoka mkoa Pwani ataziwasilisha sehemu husika ili kuleta maendeleo.

Naye Katibu wa (UVCCM) Kisamba Kidando alifafanua, uchaguzi huo umefuata taratibu zote hadi kufanikiwa kupata viongozi na hakukuwa na malalamiko yoyote.

Kidando alisema, kikubwa ni kuwapa ushirikiano viongozi waliochaguliwa ili malengo waliyoyaweka yaweze kutimia na kuufanya umoja huo kuwa imara kwani ni nguzo imara ndani ya chama.

KMC NA MERIDIANBET WACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI

$
0
0

 

KLABU ya KMC, alimaarufu kama "KINO BOYS", kwa kushirikiana na Mdhamini mkuu wa klabu hiyo kampuni ya Meridianbet wametoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa kituo cha polisi, kilichopo Mtaa wa Tegeta A ambacho kinaendelea kujengwa ili kutoa msaada wa kiusalama kwa eneo hilo.

Vifaa hivyo vilivyotolewa ni mifuko ya Saruji "Cement" zaidi 50 pamoja na ndoo kubwa za rangi 16 na hivyo kuifanya timu hiyo na kampunia hiyo kuwa ni wadau wa kwanza kufika na kuunga juhudi za ujenzi wa mradi huo ambao unatarajia kuhudumia takribani wakazi 10,000 wa eneo hilo na wa maeneo jirani ambao walikuwa wanataabika kwa kukosa ulinzi wa uhakika.

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet, Matina Nkurlu alizungumzia kile kilichowasukuma kushirkiana na KMC kutoa msaada huo.

"Sisi kama Meridiabet kwa kushirikiana na timu ya KMC, tumetoa msaada huu wa zaidi ya mifuko 50 ya saruji 'Cement' pamoja na ndoo kubwa za rangi 17, ili kuunga juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuimarisha usalama wa raia na mali zao, hivyo tunaunga juhudi za ujenzi wa kituo hiki cha polisi.
“Pia niwaombe wadau mbalimbali waige mfano huu wa Meridianbet ambao inakuwa kampuni ya kwanza kufika hapa kutoa msaada, na ndio kampuni namba moja pia kwa michezo ya kubashiri hapa Tanzania, nao waguswe kuchangia maendeleo kama haya"-Matina Nkurlu.

Nae Inspekta Henry Mdalingwa ambaye alimwakilisha OCD wa polisi wilaya ya kimara, alipendezwa na hatua hiyo iliyofanywa na Klabu ya KMC kwa Kushirikiana na Mdhamini mkuu kampunia ya Meridianbet.

"Tunawashukuru Klabu ya KMC pamoja na Meridianbet kwa msaada huu ambao unaunga juhudi zilizoanzishwa, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi wote.

"Wananchi wa Tegeta wamekuwa ni wengi, tunahitaji kuwa na usalama wa kutosha ili shughuli za kuijenga nchi ziendelee vizuri, niwakaribishe wadau wengine wajitokeze kama jinsi walivyojitoa Meridianbet"- Inspekta H. Mdalingwa.

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa wa Tegeta-A Marco Vaginga, ambao ujenzi wa kituo hicho unafanyika, hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kuwaombea KMC pamoja na Meridianbet wazidi kufanikiwa zaidi.

"Kwa niaba ya wananchi na wakazi wa eneo hili, nawashukuru kwa msaada huu, sina cha kuongea ila nawaombea kwa Mwenyezi Mungu atawaongezea kwa hiki mlichokitoa, nasisitiza kwamba nawashukuru sana, kwa kutimiza kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kazi iendelee"

Meridianbet ni kampuni inayojihusisha na michezo ya kubashiri kwa zaidi ya miaka 10 sasa hapa Tanzania, mbali na michezo ya kubashiri pia wanaendesha michezo ya kasino mtandaoni yenye michezo mingi pendwa kama vile Aviator, Poker, Roulette ambayo ni rahisi kucheza. Pia ukibashiri kwa kitochi unaweza kujishindia zawadi nyingi kama Simu, TV n.k. Beti sasa na Meridianbet kuelekea michuano ya kombe la dunia wanatoa Machaguo Spesho na yenye odds kubwa.

DKT. NDIEGE AKAGUA MAGHALA YA KOROSHO TUNDURU, ATAKA USAWA KWA WATUNZA MAGHALA WALIOTEULIWA KWA HAKI

$
0
0

 

Mrajisi Mkuu wa vyama vya Ushirika nchini Dkt. Benson Ndiege kulia, na Mkurugenzi wa Usimamizi wa maghala Asangye Bangu wa pili kulia,wakimsikiliza meneja wa kampuni ya Splendors Control Limited Grace Tarimo wa kwanza kushoto kuhusu zoezi la upokeaji wa korosho katika ghala ya Export linavyoendelea ,wa pili kushoto Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika wilayani Tunduru(Tamcu) Imani Kalembo.
Sehemu ya shehena ya korosho zilizokusanywa kutoka kwenye vyama vya msingi vya ushirika wilayani Tunduru.

Na Muhidin Amri, Tunduru
MRAJISI Mkuu wa vyama vya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege amesema,watunza maghala watakaobainika kufanya udanganyifu katika msimu wa mauzo ya korosho watachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufungiwa na kutojihusisha na shughuli za ukusanyaji wa zao hilo.

Dkt Ndiege,ametoa kauli hiyo jana mara baada ya kukagua maghala mbalimbali ya kukusanya na kuhifadhi korosho katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Dkt Ndiege,amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko ya kutoka kwa baadhi ya wachukuzi wa ghala la Export linalotumiwa na kampuni ya Splendors Control Ltd kuwa ,shughuli za kupokea korosho zinafanyika taratibu ikilinganisha na maghala mengine.

Alisema, maghala yote yaliyoteuliwa yana haki sawa ya kupokea mzigo wa korosho na kuwaasa viongozi wa vyama vya msingi kuacha upendeleo kwa watunza maghala kwani wote wana haki ya kupokea korosho zinzotoka kwenye vyama vyao.

Amewataka viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika na Chama Kikuu cha Ushirika wilayani humo(Tamcu), kusimamia na kuweka mazingira mazuri ili zoezi hilo lifanyike kwa uwazi na usawa ili kuondoa malalamiko.

Awali mwakilishi wa wachukuzi katika ghala la Export Said Mohamed alisema, katika ghala hilo shughuli za kukusanya korosho zimesimama ikilinganisha na maeneo mengine, jambo linalowafanya kuishi maisha magumu za familia zao.

Naye meneja wa kampuni ya Splendors Control Ltd Grace Tarimo alisema, hadi sasa katika ghala hilo korosho zilizouzwa ni tani 1,193 na kilo 229 na ambazo hazijauzwa ni tani 9 na kilo 975.

Hata hivyo alieleza kuwa,changamoto kubwa wanayokutana nayo ni mapokezi ya mzigo kutokuwepo kwa usawa kwenye mgawanyo kwani baadhi ya maghala yanapokea mzigo kidogo na katika ghala hilo wanakaa hata siku mbili bila kupokea mzigo.

Alisema,hawafahamu sababu ya ghala hilo kazi ya kupokea korosho kwenda taratibu kwa kuwa wenye jukumu la kusimamia kazi hiyo ni Chama kikuu cha Ushirika wilayani humo (Tamcu).

Tarimo ameiomba serikali,kuangalia idadi ya maghala katika wilaya hiyo kulingana na uzalishaji na Chama kikuu kuweka usawa wa mzigo kwa kila ghala na kufahamu mzigo uliposhushwa kama ilivyoelekezwa na kufanya hivyo watapunguza tatizo hilo.

Kwa upande wake meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika(Tamcu)Iman Kalembo alisema, changamoto hiyo inatokana na baadhi ya vyama vya msingi kuchagua msafirishaji wa korosho kwenda ghalani na watunza maghala kutumia ujanja ili wapate mzigo mkubwa.

FATUMA TSEA AIBUKA KIDEDEA UWT MANYARA

$
0
0

 






Na Mwandishi wetu, Babati
KATIBU mstaafu wa UWT wa Wilaya za Babati, Kondoa na Arusha mjini na Mikoa ya Arusha na Rukwa Fatuma Tsea amechaguliwa kwa kura za kishindo kuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Manyara.


Fatuma Tsea mwenye uzoefu mkubwa wa uongozi uliobobea kwenye jumuiya ya UWT, amewabwaga wanawake wenzake wengine watatu waliokuwa wanawania nafasi hiyo.


Akizungumza baada ya kuchaguliwa kwa kura za kishindo Tsea ameahidi kuwatumikia wanawake wa Manyara ila ameomba wampe ushirikiano wa kutosha.

MWENYEKITI huyo wa UWT Mkoa wa Manyara, ambaye nyumbani kwao ni Wilaya ya Hanang' amesema wanawake wa Manyara wakiendeleza mshikamano watapiga hatua kubwa.

Hata hivyo, amewapongeza wabunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, kwa kutowaelekeza wajumbe ili kuwachagua wagombea wanaowataka wao.

Amesema wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Manyara, Regina Ndege na Yustina Rahhi hawakuwaelekeza wajumbe wawachague wagombea wao hivyo wanapaswa kupongezwa.

"Pia mbunge wa vijana Taifa kupitia mkoa wa Manyara, Asia Halamga ambaye ni mpiga kura wetu naye hakuwa na wagombea kwenye uchaguzi huu wote wamewaacha wanawake wachague mtu wanayempenda," amesema Tsea.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Sezaria Makota ambaye ni msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, amemtangaza Tsea kushika nafasi hiyo kwa kupata kura 284.

Makota amesema Claudia Haule amepata kura 38 Diana Kulo amepata kura 31 na Mariam Njavike amepata kura nne.

WAZIRI SORAGHA: ZANZIBAR NI ENEO BORA KWA UWEKEZAJI

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Abdallah Possi akichangia mada kuhusu uwekezaji katika uchumi wa buluu Zanzibar. Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe akitoa neno kuhusu uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu Zanzibar.

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea, Mhe. Togolany Mavura akichangia jambo kuhusu mada ya uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole akitoa neno kuhusu uwekezaji katika uchumi wa buluu Zanzibar.

RC MAKALLA ATOA MAELEKEZO MATATU KWA SHIRIKA LA DDC

$
0
0

 


* Asema Rais Samia ameelekeza Shirika kujiendesha kiuchumi na kibiashara Kama maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. 

*Ataka Mali zote za DDC zilizoporwa/kuvamiwa kuainishwa ili zikombolewe.

* Aelekeza Bodi na Menejimenti kubadilika kifikra na kimtazamo Shirika lijiendeshe kibiashara.

*Shirika liandae Mpango Mkakati wa Biashara wa muda mfupi, wa Kati na muda mrefu.

*Apongeza Maboresho yaliyoanza kufanyika Baada ya maelekezo aliyotoa.
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jiji la Dar es salaam DDC kubainisha Mali zote zilizovaniwa au kuporwa ili aweze kuweka Nguvu kuhakikisha zinarejeshwa kwa mujibu wa sheria.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa DDC Millennium Lounge Keko Temeke ametaka Bodi na Menejimenti ya Shirika kubadilika kifikra na kimtazamo Shirika lijiendeshe kibiashara.

Aidha RC Makalla ameelekeza Shirika kuandaa Mpango Mkakati wa kibiashara kwa kutumia Vizuri rasilimali zinazomilikiwa na Shirika kukuza Uchumi.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona DDC yenye mafanikio makubwa Kibiashara na kiuchumi kulingana na lengo la hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

NSSF YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amehudhuria katika Mkutano wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mabalozi wa Tanzania unaoendelea katika Hotel Verde, Zanzibar. Katika Mkutano huo Mshomba akiwa ni mjadili mada alipata muda wa kuzungumzia masuala ya uwekezaji na fursa zilizopo NSSF.

Mjadala huo ulitanguliwa na wasilisho kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba. Awali wageni mbalimbali walitembelea Banda la NSSF akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Stergomena Tax, Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia Mhe. Dkt. Ramadhan Dau na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi James Bwana.

NSSF inatumia Mkutano huo kwa ajili ya kutangaza Fursa mbalimbali za Uwekezaji ikiwa ni mradi wa nyumba za kisasa, miradi ya uwekezaji ya jengo la Mzizima Tower, jengo la hoteli Mwanza pamoja na viwanja.















Benki ya NMB yaibuka kinara tuzo za TRA

$
0
0

Benki ya NMB imeibuka kinara katika tuzo za mlipa kodi mkubwa zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).

Benki hiyo imeshinda tuzo tatu zinazoitambua kama mlipa Kodi Mkubwa nchini kwa mwaka 2021/2022.


Tuzo hizo ni:

1️⃣ Mshindi wa Kwanza; Taasisi inayozingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi.

2️⃣ Mshindi wa Kwanza; Mlipa kodi mkubwa zaidi katika kundi la taasisi za fedha nchini.

3️⃣ Mshindi wa Tatu; Taasisi inayolipa kodi kubwa zaidi nchini (sekta zote).


Mafanikio haya ni matokeo ya benki hiyo kuzingatia kanuni bora za ulipaji kodi, ufanisi katika kujiendesha na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha zenye manufaa kwa wateja.

Benki ya NMB imedhamiria kuendelea kuendesha biashara yake kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa


Afisa Mtendaji Mkuu - NMB, Bi. Ruth Zaipuna akipokea moja ya tuzo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Afisa Mkuu wa Fedha - NMB, Bw. Juma Kimori(wa tatu kulia) , Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii - NMB, Bi. Lilian Kisamba pamoja na Meneja wa Kodi - NMB, Bi. Janeth Buretta.









OMAN WASHEREHEKEA MIAKA 52 YA KUASISIWA KWAKE, WASIFU UONGOZI WA MTUKUFU SULTANI HAITHAM BIN TARIQ

$
0
0

 




TAIFA la Oman leo Ijumaa ya Novemba 18, 2022 linasherehekea miaka 52 ya kuasisiwa kwake pamoja na mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa katika muamko wake Mpya, na kipindi chake kitukufu, chini ya uongozi wa Mtukufu Sultani Haitham bin Tariq.

Kiongozi ambaye amekuwa akifanya juhudi kubwa bila kuchoka katika kuimarisha nafasi na hadhi ya Dola ya kisasa, kimaendeleo na kiuchumi, na ili kila Mwananchii wa Oman awe mshiriki wa kweli wa maendeleo jumuishi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo imefafanua kwa kina mafanikio ya Taifa hilo ambalo linasheherekea miaka 52 ya kuasisiwa kwake huku ikielezwa hatua kwa hatua mageuzi yanayoendelea sasa hivi Oman, kuelekea kwenye mfumo wa kidijatali wa Serekali, ni moja ya programu za utekelezaji wa uchumi wa kidijiti, na moja ya nyenzo kuu za kusaidia kufikia vipaumbele vya Dira ya "Oman 2040 ".

Kwa mujibu wa taarifa kwamba Mtazamo wa Mtukufu Sultani unajipambanua kama maono ya busara na yanayoangalia mbali kwani umejikita katika kuendeleza azma ya Oman ya kuwa na ushirikiano chanya na wote na katika nyanja anuwai zenye manufaa, na kwa namna ambayo itakuza masilahi ya pande zote, na matokeo ya mtazamo huo yamejitokeza katika ziara za viongozi mbalimbali duniani akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibari Dkt. Hussein Ali Mwinyi Raisi wa Zanzibar, ziara ambazo zimefikia kilele chake kwa kuanzishwa ubia wa aina mbalimbali na kusiniwa hati za maelewano na mipango ya utekelezaji katika nyanja kadhaa zikiwemo za uwekezaji na biashara.




Viewing all 48983 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>