Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48995 articles
Browse latest View live

MECHI ZA EUR0 2020 KUENDELEA WIKI HII

$
0
0

 

*Hatua ya Makundi Kumalizika Kibingwa, Changamkia Fursa!


HATUA ya Makundi ya michuano ya EURO 2020 kutamatika wiki hii. Timu kadhaa zimeshafuzu 16 bora, huku nyingine zikiendelea kujitafuta. Kwa kuthamini harakati za kutaka kufuzu kuingia 16 bora, Meridianbet imekuwekea Odds bomba katika mechi hizo, bashiri sasa!


Jumanne hii, Timu ya England ambayo imejaa mastaa kibao itakuwa kibaruani kuwakabili Czech Republic. Timu hizi zote zina alama 4 na ushindi ni muhimu kwa timu zote. Meridianbet imekuwekea Odds ya 1.75 kwa England katika mechi hii.


Siku ya Jumatano, kutakuwa na mechi ya mwisho katika kundi la kifo, Portugal watakuwa wakicheza na France. Portugal ina jukumu la kutetea taji lake France inahitaji ushindi. Meridianbet imeweka Odds ya 2.40 kwa France kwa ajili yako!


Alhamis hii, ile ligi ya Norway, Elliteserien itaendelea na kutakuwa na mechi kati ya Stabaek dhidi ya Valerenga. Stabaek wako nafasi ya pili kutoka mwisho na wanatafuta ushindi. Valerenga wamewekea Odds ya 2.15 na Meridianbet ili kukufaidisha!


Ni rahisi sana kuwa bingwa wikiendi hii, cha kufanya nikuchangamkia fursa tu. Piga *149*10# kujiunga au tembelea www.meridianbet.co.tz na ujiunge na familia ya mabingwa!


Meridianbet, Nyumba yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!


Milioni 130 kujenga Kituo cha Polisi

$
0
0
Na Abubakari Akida, Dodoma
KATIKA kukabiliana na matukio ya uhalifu ikiwemo uporaji. ukabaji na udhalilishaji, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limedhamiria kujenga Kituo cha Polisi katika Kata ya Chang’ombe ambapo mpaka kukamilika kwake kinatarajiwa kugharimu Shilingi Milioni 130.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mshauri Mkuu wa Miradi ya Ujenzi ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi,Richard Malika wakati wa kupokea jumla ya matofali 6700 yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ikiwa ni jitihada za mkuu wa mkoa huyo kukabiliana na matukio ya uhalifu yaliyoshamiri katika Kata ya Chang’ombe huku Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikitoa kiasi cha Shilingi Milioni 10 katika kuchangia ujenzi huo.

“Tunakadiria hadi kukamilika kwa kituo hiki jumla ya Shilingi Milioni 130 zitakua zimetumika kama gharama yam ujenzi wa jengo ukiachana na samani za ofisi na kitakua kituo cha pili kwa ukubwa kwa hapa Dodoma sambamba na kuzingatia haki za binadamu huku kila mahabusu zikiwa na sehemu ya choo na mabomba ya maji” alisema Naibu Kamishna Malika

Naibu Kamishna Malika pia aliwataka wahalifu pindi kituo hicho kitakapokamilika watafute taratibu nyingine za maisha kwani uhalifu sio kazi nzuri huku akiweka wazi kituo hicho kitakamilka ndani ya miezi sita.

Akizungumza baada ya makabidhiano ya matofali hayo, Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikira alisema wanaishukuru Wizara, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ambae amechangia mifuko mia moja ya saruji katika mradi huo.

“Uhalifu hapa kwetu umekua ni changamoto watu wanaporwa wanafanyiwa matendo ya kihalifu lakini viongozi tumeanza mipango kukomesha uhalifu huo ikiwemo dhana ya ulinzi shirikishi na sasa ujenzi wa kituo hiki utaenda kukomesha matendo ya uhalifu katika maeneo ya Chang’ombe, sisi kama viongozi tutahakikisha tunawahamasisha wananchi wetu wachangie katika mradi huu na tunawashukuru wahisani wote waliotuunga mkono na wanaoendelea kutuunga mkono katika ujenzi huu”alisema Diwani Bakari.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ramadhani Kailima(wapili kushoto), akimkabidhi tofali moja Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe,Seif Mohammed, ikiwa ni moja kati matofali 6700 yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka ikiwa ni mchango wa ofisi ya mkoa katika ujenzi huo.Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Vyama vya Siasa Kuendeleza Ushirikiano na Serikali, Vyawapongeza Rais Samia, Dkt. Mwinyi

$
0
0

 

Na Mwandishi Wetu ORPP
VYAMA vya Siasa nchini vya ahidi keendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambazo zinaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussen Ally Mwinyi, mtawalia.

Ahadi hiyo imetolewa juzi tarehe 20 Juni 2021 na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Magalle Shibuda kupitia Taarifa yake kwa umma akitoa maazimio ya Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza hilo kilichakaa tahere 3 Juni 2021 Jijini Dar es Salaam.

“Kamati kwa niaba ya Vyama vyote vya Siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo kimsingi vyote ni wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, ili ahidi kushirikiana na Serikali zote mbili,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuleta maendeleo ya Watanzania.” Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha kupitia taarifa hiyo Kamati ya uongozi imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu kwa uamuzi wake wa kutaka kukutana na viongozi wa Vyama vya siasa nchini.

Katika hatua nyingine Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa kwa pamoja iliazimia kutoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussen Ally Mwinyi kwa kuwa Rais wa Zanzibar wa awamu ya nane kutokana na ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Baraza hilo limeendelea kutoa pongezi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussen Ally Mwinyi kwa namna wanavyoendesha Serikali kwa kushirikisha vyama vya upinzani ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa hiyo ni ishara ya kudumisha Demokrasia ya Vyama vingi hapa nchini.

Baraza la Vyama vya Siasa ni chombo kinachoundwa chini ya kifungu 21B cha Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya Siasa namba 7 ya Mwaka 2009 ambalo linashirkisha wajumbe wawili ambao ni viongozi wa kitaifa kutoka vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu huku shughuli zake zikiratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

MUHIMBILI YASISITIZA UVAAJI WA BARAKO

RC MAKALLA AWAPA MATUMAINI MAPYA WAFANYABIASHARA SOKO LA MACHINGA COMPLEX

$
0
0


MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam kuja na Mpango Mkakati wa Kuendeleza na Soko la Machinga Complex ili Soko hilo liwe kimbilio kwa Wamachinga na Wateja.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko hilo na kusikiliza kero za Wafanyabiashara sokoni hapo ambao wamemueleza sababu zinazopelekea Wafanyabiashara kulikimbia Soko hilo na kwenda mitaani.

Miongoni mwa Kero zilizotolewa na Wafanyabiashara hao ni mazingira mabovu ya kufanya biashara, Utaratibu mbovu wa kupata vizimba, Kodi kubwa, Sheria kandamizi, Ushirikiano mbovu wa Viongozi, Umeme, Maji, Vyoo, Maji taka, Miundombinu isiyorafiki na utaratibu wa kulipa Kodi ya mwezi badala ya Ushuru wa siku.

Kutokana na Malalamiko hayo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji kuhitisha vikao vya Mara kwa Mara na Wafanyabiashara hao na kupeana Mrejesho wa utatuzi wa kero zao ili mwisho wa siku biashara zifanyike na Serikali ipate Mapato.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Soko hilo kuachana na tabia ya kufungia biashara za wapangaji wanaoshindwa kulipa Kodi na badala yake wakae mezani kuangalia namna Bora.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji kufuatilia fedha za NSSF zilizotolewa Kama mkopo wa Ujenzi wa jengo hilo lili kujua Kama mkopo umemalizika au bado Deni lipo.

Tanzania Mwenyeji Mashindano ya Mchezo wa Kabbadi

$
0
0

MASHINDANO ya Afrika ya mchezo wa Kabaddi kwa mwaka 2021 yanatarajiwa kufanyika hapa nchini  kuanza  Juni  29 hadi 5 Julai, 2021 katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam.

 

Mchezo huo ambao asili yake ni nchini India umekua ni miongoni mwa michezo inayokuwa hapa nchini kutokana na muingiliano wa mataifa hayo mawili.

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul Juni 21, 2021 ametembelea kambi ya timu ya taifa ya mchezo huo katika shule ya Sekondari Nguva wilayani Kigamboni Jijini Dar es Salaam, ambapo amewataka waratibu wa mchezo huo kutoa elimu ili jamii iutambue mchezo huo.

 

"Natoa rai kwenu kuzishirikisha sekta nyingine katika fursa hii muhimu, mfano sekta ya  Utalii, wanaweza kutumia fursa iliyopo kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini kwa mataifa ambayo yanakuja kushiriki mashindano haya," amesema Mhe. Gekul.

 

Aidha, Mhe. Gekul amewataka wachezaji waliopo kambini kufanya mazoezi kwa bidii ili kulibakisha kombe la mashindano hayo  nyumbani, huku akipongeza wadhamini waliojitokeza kudhamini kambi hiyo na kutoa rai kwa wadhamini zaidi kujitokeza.

 

Mhe. Gekul ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuipa kipaumbele michezo mbalimbali inayofanya vizuri ndani na nje  kwakuwa inasaidia kutangaza nchi, kuibua vipaji pamoja na kuzalisha ajira kwa vijana.

 

Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha nchi sita Kenya, Mauritius, Misri, Cameroon  Zimbambwe na wenyeji  Tanzania  ambapo wageni kutoka katika nchi zaidi ya 20 za Afrika wanatarijiwa kuwasili hapa nchini kwa ajili ya kuratibu na kushuhudia mashindano hayo.

MKAZI WA MOROGORO VIJINI ASHINDA GARI AINA YA TOYOTA FORTUNER KUTOKA NMB BONGE LA MPANGO

$
0
0

 

Wafanyakazi wa NMB wakifurahia baada ya kupatikana mshindi wa promosheni ya Bonge la Mpango – Abdallah Mohamed Abdallah, mkazi wa Morogoro vijijini  aliyejshindia Toyota Fortuner, baada ya droo ya mwisho kuchezeshwa Sengerema mkoani Mwanza, akishuhudia ni msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga.


Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Baraka Ladislaus akibonyeza kitufe ili kumpata mshindi wa mwisho wa promosheni ya Bonge la Mpango ambapo Abdallah Mohamed Abdallah aliibuka mshindi na kuondoka na Toyota Fortuner, mpya, akishuhudia ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga (kushoto), Maafisa wa NMB pamoja na wateja  wa benki hiyo. 

*************************

Abdallah Mohamed Abdallah, mfanyabiashara na mkazi wa Morogoro vijijini ameshida zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Fortuner yenye thamani ya sh. milioni 169 katika droo ya mwisho ya kampeni ya NMB Bonge la Mpango iliyochezeshwa mjini Sengerema Mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa droo hiyo mbele ya Msimamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Ladislaus Baraka alisema ushindi wa Abdallah umekamilisha orodha ya washindi 148 waliojishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh550 milioni tangu droo hiyo ilipozinduliwa mwezi Februari mwaka huu.

Kupitia kampeni hii, benki ya NMB imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa washindi 120, pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya LIFAN 24, magari matatu ya mizigo aina ya Tata ACE maarufu kama kirikuu na gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner.

Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kujishindia gari, Abdallah aliishukuru benki ya NMB kwa zawadi hiyo huku akiwahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha zao katika benki ya NMB. Alikiri kwani tangu aanze kuweka fedha NMB – ambayo ina matawi zaidi ya 225 nchini na machine za ATM zaidi ya 700 bila kusahau mawakala walitapakaa kila mahali, hajawahi kujuta kwani amekuwa mnufaika mkubwa wa huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo, na sasa amejishindia zawadi kubwa ya gari ambayo hakuitarajia.

“Bado sijaamini kama kweli nimeshinda zawadi ya gari kwa sababu hata sikujua kama kuna droo inachezeshwa leo; sina mengi zaidi ya kuishukuru NMB kwa zawadi hii,” alisema Abdallah.

SERIKALI YAKUSANYA TZS TRILIONI 5.9 KUPITIA MIFUMO YA KIDIJITALI YA NMB

$
0
0


Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango (kulia) akiagana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB, muda mfupi baada ya kupokea gawio la zaidi ya sh. bilioni 21.8 kwa niaba ya Serikali,mwishoni mwa juma Jijini Dodoma, Serikali ilipokea gawio hilo ikiwa ni kutokana na kuwa na hisa katika benki ya NMB.

*****************************

Ubora wa Benki ya NMB kiutendaji miaka ya hivikaribuni na mafanikio yake makubwa kifedha mwakajana ni miongoni mwa matokea ya ubunifu na uwekezajikatika mifumo ya kisasa hasa ile ya kidijitali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bi Ruth Zaipuna, amesema.

Akizungumza jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, kiongozihuyo alimwambia Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango, kuwa mifumo hiyo imekuwa na tija kubwa si tu kwataasisi hiyo kinara wa faida bali pia kwa serikali, wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2018, serikali imeweza kukusanya mapato yenye thamani ya takribani TZS trilioni 6 kupitia mifumo hii ambayo pia inamchango mkubwa kwenye ufanisi wa NMB kifedha.

Bi Ruth aliyasema hayo kabla ya kumkabidhi Dkt. Mpango hundi ya TZS 21.8 bilioni ambazo NMB imezitoa kwa serikali kama gawio la mwaka 2020 ikiwani ongezeko la asilimia 43 ya kiasi ilichokitoa mwaka2019.

Aidha, pamoja na kuwa mwanahisa mkubwa kwenyebenki hiyo, pia serikali ni mteja mzuri na mdau wakimkakati wa NMB kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“Pamoja na miradi hii, uwekezaji ambao Benki ya NMB imeufanya kwenye teknolojia, unaendelea kuiwezeshabenki kuunganisha mifumo yake na taasisi mbalimbaliza serikali na zisizo za kiserikali na hivyo kurahisishaukusanyaji wa mapato,” Bi Zaipuna alisema.

“Serikali, zaidi ya kuwa mbia, ni mteja mzuri na mkubwawa Benki ya NMB. Sisi tunalitambua hilo natumeendelea kuwekeza katika teknolojia inayotoasuluhisho kwa serikali,” alifafanua.

“Pamoja na kuunganisha mfumo wa malipo ya serikalikatika mifumo ya Benki ya NMB, tunaendelea kuwekezakuhakikisha miamala mingine mbalimbali inafanyika kwanjia ya kielekroniki,” kiongozi huyo aliongeza.

“Juhudi hizi zote zinachangia kuleta ufanisi na pia kupunguza gharama za uendeshaji katika ukusanyaji wamapato. Kwa miaka mitatu, 2018/20, jumla ya TZS trilioni 5.9 zimekusanywa kupitia mifumo ya Benki yaNMB ambayo imeunganishwa na taasisi mbalimbalizilizopo nchini.”

Mbali na malipo ya gawio, ambalo katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 yamefikia TZS bilioni 155.8, Dkt Mpangoalisema NMB kuiwezesha serikali kukusanya mapatokupitia mifumo yake ni mchango mwingine mkubwakutoka benki hiyo mahili.

Alisema serikali inajivunia mafanikio makubwa ya NMB na kuwa mbia kwenye taasisi hiyo kitu ambachokinaifanya kupata faida nyinji zenye tija kutokana nauwekezaji wake wa asilimia 31.8. Dr Mpangoaliwachagiza Watanzania kuhakikisha benki hiyo inazidikuwa imara kwani faida zake ni kubwa kwao na taifa kwa ujumla.

Katika kipindi cha miaka mitano, benki hiyo imewezakuukuza mtaji wa wanahisa wake kwa ongezeko la zaidi ya TZS bilioni 463, hivyo kuufanya mtaji wake kufikiaTZS trilioni 1.1 ukilinganisha na TZS bilioni 666 mnamomwaka 2015.

Pia NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia ajenda yakitaifa ya kufikisha huduma za kifedha kwa Watanzania. Bi. Zaipuna alisema wigo mpana wa bidhaa na hudumazake umeongeza upatikanaji wa suluhisho za kifedhakupitia njia za kawaida na njia mbadala za kibenki.

Mpaka Desemba ya mwaka 2020, Benki ya NMB ilikuwana akaunti za wateja zaidi ya milioni nne na mawakalazaidi ya 8,400 waliotapakaa nchi nzima.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede, alisema zaidi ya ubunifu wa kidijitali, siri kubwa ya mafanikio ni wafanyakazi ambao ndiyo silaha kubwa ya benki hiyo. Aidha, mchango mwingineunatokana na ushirikiano kutoka kwa wateja pamoja na mazingira wezesha ya biashara.



WATUMISHI MKIGOMBEA UONGOZI MKAKOSA RIDHIKENI-RAIS TUCTA

$
0
0

 

Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (Talgwu) Bw. Rashid Mtima akizungumza Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw.Tumaini Nyamhokya akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania (Talgwu) wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV,
WATUMISHI wa kutoka kada mbali mbali wanaogombea nafasi mbali za uongozi wa chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TAWLGU) wameaswa kuridhikaxs na matokeo badala ya kushindwa na kwenda kuanzisha chama chao kipya.

RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini,(TUCTA),Tumaini Nyamhokya ameyasema hayo leo Juni 22, 2021 wakati akifungua mkutano Mkuu wa TAWLGU mkoa wa Dar es Salaam ambao unaendana na uchaguzi wa viongozi wa mkoa huo, Nyamhokya alisema ni vema viongozi kukaa meza moja huku wakiimba wimbo mmoja ambao watakubaliana kwa hoja bila kwenda kwenye migomo au kuingia barabarani

Amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi wa viongozi wanaposhindwa katika chaguzi kuwa na makovu ya kushindwa uchaguzi hivyo kuunda makundi ndani ya Chama jambo ambalo hudhoofisha chama

Amesema kukaa kwa pamoja baina ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa ngazi ya mkoa na Taifa kwa pamoja na kuwa wamoja ni chachu mmojawapo kuwa wanauwezo wa kutatua changamoto zinazowakabili wanachama wake.

"Ni vema viongozi wakakaa meza moja huku wakiimba wimbo mmoja ambao watakubaliana kwa hoja bila kwenda kwenye migomo au kuingia barabarani." Amesema Nyamhokya.

"Hatuzuiwi kuingia kwenye migomo au kuingia barabarani lakini kukaa mezani, kujadiliana na kupata ufumbuzi wa mambo yetu ni mafanikio makubwa na kutafanya uwepo wa kusikilizana baina ya viongozi wa Taifa na Chama na kufanya vyama kuwa imara zaidi." Amesema

Ameongeza kuwa, ni matarajio yake makubwa kuwa katika uchaguzi wa leo watapatikana viongozi wazuri ambao watakiongoza Chama kwa kusikilizana na kukunaliana katika hoja mbali mbali watakazokuwa wanaafikiana.

Naye, Rashid Mtima Katibu Mkuu wa TAWLGU amesema mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano ni mkutano wa kikatiba ambao lengo lake ni kupitia taarifa za Chama za kazi na kifedha kwa miaka mitano iliyopita.

"Leo tutakaa na kupitia ripoti ya miaka mitano katika Mikoa wa Dar es Salaam pia tutachagua viongozi wapya wa a miaka mingine mitano akiwamo Mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam."Amesema Mtima.

" Katiba imeipa Mamlaka Chama kuanzisha mkoa tangu mwaka jana ambapo baraza kuu liliidhinisha Mikoa mitatu ya Dar es Salaam iianzishwe ikiwemo mkoa wa Temeke,ilala na Kinondoni hivyo leo wanafanya uchaguzi wa mkoa wa Dar es Salaam lakini wakitoka hapa wataenda kuchagua viongozi wa Mikoa mitatu ilihuduma kwa wanaachama ifike vizuri katika kuwahudumia."Alisema

"Kanuni za chama za mwaka 2018 zinazungumza kwamba viongozi wakichaguliwa wanapaswa kupewa mafunzo ya uongozi ya shughuli za Chama hivyo viongozi watakaochagulia leo hapa watapewa mafunzo ya Uongozi kwa shuguli zote Chama cha wafanyakazi." Amesem

UZINDUZI WA NMB HEALTHCARE CLUB,SERIKALI YAIPONGEZA NMB

$
0
0

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Klabu za afya ‘NMB Healthcare Club uliofanyka jijini Dar es Salaam

Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Klabu za afya ‘NMB Healthcare Club.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Klabu za afya ‘NMB Healthcare Club uliofanyka jijini Dar es Salaam.

………………………………………………………………..

Benki ya NMB, imekuwa ya kwanza nchini kuzindua Klabu za Afya ‘NMB Healthcare Club,’ mtandao unaowapa wadau wa Sekta ya Afya mikopo ya vifaa kazi, mitaji na uwekezaji, huduma inayokuja huku benki hiyo ikiwa imetumia zaidi ya Sh. Bilioni 32 kutoa mikopo kwa Sekta Binafsi ya Afya, kati ya Sh. Bilioni 112.5 ilizopanga kutumia hadi mwaka 2025.

NMB Healthcare Club imezinduliwa sambamba na Kongamano la Afya ‘Tanzania Health Summit 2021,’ uzinduzi uliowakutanisha wadau wa Sekta ya Afya zaidi ya 150, wakiwemo madaktari, wamafasia, wamiliki wa hospitali, zahanati, vituo na vyuo mbalimbali vya afya na viongozi wa vyama washirika.

Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ambako Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale, aliipongeza NMB kwa kuwaunganisha na kuwapa uwezeshaji wadau muhimu wa Sekta ya Afya nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dk. Sichwale alibainisha kuwa, uzinduzi wa Klabu hiyo una baraka zote za Serikali na wanawaunga mkono NMB kwa juhudi zeo za kuwaunganisha Madaktari na wadau wengine muhimu wa Sekta ya Afya hapa nchini.

Dk. Sichwale aliipongeza NMB sio tu kwa kuwaunganisha wadau hao muhimu, bali utayari wao wa kutoa bure elimu juu ya fedha ambayo mahali pengine wangeipata kwa gharama kubwa, hasa inayohusu; uwekaji akiba, uwekezaji, umuhimu wa kupitisha fedha zao kwenye akaunti ya benki, pamoja na huduma zinginezo zitolewazo na NMB.

Naye Kaimu Afisa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, aliwapongeza wadau wa Sekta ya Afya kwa kuona umuhimu wa Klabu hiyo na kuwaasa ambao bado hajajiung kufanya hivyo.

Aidha alibainisha kuwa NMB imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya afya, ambako wanatoa misaada ya vifaa tiba, vikiwamo vinavyolenga kuhudumia eneo lenye changamoto nyingi, la afya ya uzazi. Aliongezea kuwa, NMB imeingia kwa nguvu moja kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wote, ambapo kupitia huduma ya Asset Financing – inayotoa mikopo nafuu mahsusi kwa Sekta Binafsi ya Afya,ambapo walitumia zaidi ya Sh. Bilioni 32 kufikia Machi mwaka huu, kati ya Sh. Bilioni 112.5 walizopanga kutumia hadi mwaka 2025.

NMB Healthcare Club ni uthubutu mwingine kutoka NMB unaowapa nguvu za ziada wawekezaji na wadau muhimu waliopo katika sekta hiyo

WAFANYAKAZI TTCL WAJITOLEA KUFANYA USAFI DAR KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mtahiko Henry (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuzungumzia tukio la Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation kufanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma.

 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mtahiko Henry (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuzungumzia tukio la Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation kufanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma.

Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation wakizunguka kufanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Sehemu ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation wakisafisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Gari la Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation likiwa limejaa taka zilizokusanywa na Watumishi wa Shirika hilo mara baada ya kufanya usafi baadhi ya maeneo ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania wakipakia uchafu kwenye gari la TTCL walipokuwa wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.
Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation wakifanya usafi baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi kwa Umma leo.

Na Mwandishi Wetu, Dar
WAKATI Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi kwa Umma yakifikia kilele chake leo June 23, 2021 Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation wamefanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam kitendo walichokiita 'Matembezi ya Usafi' ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.

Katika matembezi hayo Watumishi wamepita katika maeneo ya Posta Mpya, IFM, Soko la Kimataifa la Feri ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa wakiokota taka zote zilizotupwa katika maeneo tajwa na kuyakusanya kwa ajili yakuyapeleka katika maeneo maalum ya kuhifadhi takataka.

Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma yanaratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Akizungumzia maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mtahiko Henry amesema Wiki ya Utumishi wa Umma inamkumbusha kila Mtumishi kwamba anawajibika kwa jamii na kumkumbusha kuwa utumishi wake haupaswi kuishia Ofisini bali unaenda mbali zaidi kwa wananchi.

Aidha Mtahiko amesema kupitia matembezi hayo Wananchi watapata fursa kuonana na Watendaji wa TTCL uso kwa uso, na kupata maelezo mbalimbali ya huduma na bidhaa zitolewazo na shirika hilo.

Pamoja na kupata maelezo hayo wananchi pia watapata nafasi ya kutoa maoni kuhusu huduma wanazozipata kutoka katika shirila lao la mawasiliano na kwamba maoni yao yatathaminiwa kwakufanyiwa kazi kwakuhakikisha kero itakayobainika inafanyiwa kazi.

“Sisi ni Watumishi wa Umma kama walivyo watumishi wengine hivyo tunawajibika kwa wananchi na ndiyo maana leo tumefanya shughuli ya kijamii ambapo katika maeneo yote tulipopita tumeahakikisha tunayaacha mazingira yakiwa safi.” Amesema Mtahiko

Ametoa rai kwa Watumishi wote wa TTCL kuhakikisha wanaendelea kuzingatia misingi ya utumishi wa Umma pindi wanapokuwa kazini na baada ya kazi kutokana na ukweli kwamba jamii ndiyo inayowapima tabia na utendaji wao wa kazi.

Katika hatua nyingine Mtahiko amesema TTCL inawatumikia Wananchi kwakuhakikisha inalipa kodi ya kila mwezi kwa wakati ambapo kupitia kodi hizo mwananchi ananufaika kwakupata huduma mbalimbali za jamii ikiwemo maji, barabara, elimu na Afya.

Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni wiki maalum ya Watumishi wa Umma na taasisi za Umma ambayo husherehekewa kuanzia tarehe 16 Juni hadi 23 Juni kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya Bara la Afrika.

Chimbuko la Sherehe hizi ni uamuzi wa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma uliofanyika Tangiers nchini Morocco mwaka 1994. Uamuzi huu ulizitaka nchi za Afrika kusherehekea sherehe hizo kwa kauli mbiu moja katika Bara zima la Afrika.

Malengo ya msingi ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni pamoja na kuwezesha watumishi wa Umma kutambua Dira, Dhima, na Malengo; Programu na Mikakati; na Mafanikio na Changamoto zinazokabili Utumishi wa Umma, kutambua mchango na umuhimu wa Watumishi wa Umma na umuhimu wao katika kuleta maendeleo nyanja mbalimbali katika Taifa.

Lingine ni kuhamasisha na kuwapa motisha Watumishi wa Umma ili waendelee na kazi yao nzuri ya ujenzi wa Taifa na kuendelea kuwa wabunifu ili kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, Kupata mrejesho kutoka kwa wateja na wadau wao juu ya huduma wanazozitoa na Kuwaandaa Watumishi wa Umma ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali.

SIKU YA WAJANE YAFANA MNAZI MMOJA DAR, SERIKALI KUFANYA MAREKEBISHO YA SHERIA, SERA ZINAZOLINDA HAKI ZA WAJANE

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wajane duniani yaliyofanyika Mkoani Dar es Salaam leo Juni 23,2021 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt John Jingu. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt John Jingu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya siku ya wajane duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo June 23, kila mwaka.
Wakili wa serikali kutoka RITA, Edna Kamala akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wajane duniani yaliyofanyika Mkoani Dar es Salaam leo Juni 23,2021 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Maafisa RITA wakitoa huduma kwa wajane waliofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kusheherekea siku ya wajane duniani ambayo ufanyika kila Juni 23 kila Mwaka.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TAKWIMU zinaonyesha kuwa idadi ya wajane Duniani ni takriban milioni 258 kati ya hao, wajane 115 milioni wanadhulumiwa, wanafanyiwa ukatili, wanakabiliwa na umasikini na kutengwa na jamii na mmoja kati ya wajane 10 anaishi katika umasikini uliokithiri.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis wakati akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wajane Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoani Dar es Salaam leo Juni 23,2021.

Amesema kuwa hapa nchini wajane wanakadiliwa kuwa laki 8.8 ambayo ni sawa na asilimia 3.1 ya wanawake wote nchini ambao wanakadiriwa kuwa milioni 28.5 kwa mwaka 2020.

"Katika baadhi ya jamii, hadhi ya mwanamke inahusishwa zaidi na maisha yake na mumewe, na hivyo mume anapofariki, mwanamke anakuwa hana nafasi yoyote kwenye jamii. Wengine hutakiwa kuolewa na ndugu wa mume bila ridhaa zao. Na huo ni mwanzo tu wa baadhi ya kero zinazo wakabili wajane." Amesema Mwanaidi

Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inawatambua na kuwaenzi wajane katika jamii ikiwajuhudi mbalimbali zimefanywa na Serikali ikiwa ni pamoja na Kuitambua Siku ya Wajane kitaifa na kuhamasisha wadau wote kuiadhimisha na hivyo kuweza kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wajane.

Aidha amesema kuwa jumla ya kodi, ada na tozo 108 kati ya 139 zimefutwa ili kupunguza kero kwa wanawake wajasiriamali wakiwemo wajane ili kuondoa kero kwa wajasiriamali wakiwemo Wajane, mama lishe na wauza mbogamboga kwa kupatiwa maeneo rasmi ya kufanyia biashara yenye ukubwa wa hekta 15,822.64 katika Halmashauri 150 nchini.

Hata hivyo amesema kuwa serikali itaweka na kuimarisha mifumo ya kulinda haki za Wanawake wakiwemo Wajane kwa Kuanzisha madawati ya jinsia na watoto 427 katika vituo vya polisi na vituo 153 katika Jeshi la Magereza kwa lengo la kutokomeza ukatili wa Kijinsia kwa Wahanga wakiwemo Wajane.

Pia serikali itaongeza huduma za msaada wa sheria kutokana na kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria Na. 1 ya mwaka 2017, ambayo imewezesha makundi maalum ikiwemo Wajane na watoto kupata haki zao katika vyombo vya usimamizi wa sheria. Aidha, taasisi 125 za kutoa huduma za msaada wa kisheria zimetambuliwa na Wasaidizi wa Kisheria 3,721 wamesajiliwa kote nchini.

Serikali inawawezesha Wanawake kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwapa fursa Wanawake Wajasiriamali wakiwemo Wajane kupatiwa mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri, mikopo hiyo ya asilimia 4 kwa Wanawake, 4 kwa Vijana na 2 kwa walemavu hutolewa iwapo walengwa watakuwa wamekidhi vigezo vinavyotolewa katika hamashauri ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha wanawake kuanzia watano hadi 10, wawe na umri isiozidi miaka 18 na kuendelea pamoja na kutimiza vigezo vingine vinavyohitajika.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt John Jingu amewaasa wajane na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa wa COVID-19 kwa ugonjwa huo ni hatari sana kwa jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Widows Association (TAWIA), Rose Sterwart amesema kuwa wajane ni kundi maalumu na maadhimisho yaliyofanyika leo ni kwaajili ya kutafakari changamoto zinazowakabiri wanawake hasa wajane.

Hata hivyo amewaasa wajane kutokukaa na changamoto zinazowakabiri na kuibua vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na wanadugu mara baada ya mume au kufariki dunia.

Licha ya hayo ameiomba serikali kufanya mabadiliko ya Sheria na sera zinazohusiana na kulinda haki za wajane kwa jamii nzima.

Tanzania huadhimisha Siku ya Wajane kwa lengo la kujenga hamasa, mshikamano na uelewa ndani ya Jamii kuhusu haki na Ustawi wa Wajane, maadhimisho yamwaka huu yanatoa fursa ya pamoja katika kubaini changamoto za wajane na namna ya kukabiliana nazo.

Mwaka huu Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani yameongozwa na Kaulimbiu “Mapambano Dhidi ya COVID-19, Wajane Washiriki Kikamilifu.”

Benki ya DCB yashiriki uzinduzi wa mpango wa kuwaandaa wanachuo katika soko la kibenki

$
0
0

 

 Baadhi ya viongozi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi na waalikwa wengine wakipiga picha ya kumbukumbuku muda mfupi baada ya uzinduzi wa  program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na shule hiyo, Dar es Salaam leo.

Kaimu Mkuu wa  Rasilimali Watu wa Benki ya DCB, Meshack Kayila (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), waliohudhuria uzinduzi huo chuoni hapo, Dar es Salaam, leo.

 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakihudhuria uzinduzi huo chuoni hapo, Mlimani, leo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mabenki Tanzania  (TBA), Tusekelege Joune (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Kituo Huduma za Kibenki na Fedha wa UDBS, Dk. Tobias Swai, Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Fedha wa UDBS, Dk. Evelyn Richard, Mkuu wa UDBS, Prof. Ulingeta Mbamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa. 

Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Fedha wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), Dk. Evelyn Richard, akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto kwake pichani ni, Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), Prof. Ulingeta Mbamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mabenki Tanzania  (TBA), Tusekelege Joune. 

Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), Prof. Ulingeta Mbamba, akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Kituo Huduma za Kibenki na Fedha wa UDBS, Dk. Tobias Swai, Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Fedha wa UDBS, Dk. Evelyn Richard, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mabenki Tanzania  (TBA), Tusekelege Joune.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Fedha wa UDBS, Dk. Evelyn Richard, Mkuu wa UDBS, Prof. Ulingeta Mbamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mabenki Tanzania  (TBA), Tusekelege Joune.

RAIS SAMIA AREJEA NCHI KUTOKA MSUMBIJI

$
0
0









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Juni 23,2021, akitokea Maputo Nchini Msumbiji alikohudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC. Ambapo kwenye Mkutano huo SADC imeridhia kuanzishwa kwa Kituo cha Haki za Binaadamu kitakachosaidia Nchi zinazokabiliwa na Athari za mabadiliko ya Tabia Nchi, kuweza kukabiliana na Janga la Covid 19 pamoja na kuangalia jinsi gani SADC itaweza kupambana na suala la Ugaidi.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Juni 23,2021, akitokea Maputo Nchini Msumbiji alikohudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC. Ambapo kwenye Mkutano huo SADC imeridhia kuanzishwa kwa Kituo cha Haki za Binaadamu kitakachosaidia Nchi zinazokabiliwa na Athari za mabadiliko ya Tabia Nchi, kuweza kukabiliana na Janga la Covid 19 pamoja na kuangalia jinsi gani SADC itaweza kupambana na suala la Ugaidi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Juni 23,2021, akitokea Maputo Nchini Msumbiji alikohudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC. Ambapo kwenye Mkutano huo SADC imeridhia kuanzishwa kwa Kituo cha Haki za Binaadamu kitakachosaidia Nchi zinazokabiliwa na Athari za mabadiliko ya Tabia Nchi, kuweza kukabiliana na Janga la Covid 19 pamoja na kuangalia jinsi gani SADC itaweza kupambana na suala la Ugaidi. (Picha na Ikulu)

BancABC yazindua kampeni ya kuweka fedha akaunti ya amana itakayowezesha wateja kupata riba hadi asilimia 14

$
0
0
BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara leo imetangaza kuzindua kampeni kabambe ya kuweka fedha katika akaunti ya amana (fixed deposit) kwa wateja wote, ambapo kwa sasa mteja ataweza kupata riba ya hadi asilimia 14 kwa mwaka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kampeni hiyo, Muendeshaji Mkuu wa Biashara wa BancABC Tanzania Joyce Malai amesema kuwa benki hiyo imeanzisha utaratibu wa kutoa riba ya hadi asilimia 14 kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana kuanzia leo mpaka mwishoni mwa mwezi Septemba na mteja atalipwa riba hiyo papo hapo huku fedha ikiendelea kusalia kwenye akaunti mpaka pale itapofikia muda wake uliokusudiwa (mwaka, miezi sita au miezi mitatu).

‘Hii ndio ofa kabambe na bora kwenye soko kwa sasa, kwa hiyo nachukua nafasi hii kuwahimiza wateja wetu na pia kwa wale ambao sio wateja wetu kuchangamkia fursa hii na kuwekeza kwenye akaunti ya amana ya BancABC kabla muda wa ofa hii haujaisha’, Malai alisema.

Malai alisema kuwa BancABC imedhamiria kuendelea kutimiza mahitaji ya wateja wake kwa kuhakikisha kuwa wote wanafaidika na wanakuwa kwa pamoja. Tunatoa riba papo hapo ili kufanya wateja wetu waendelee kuendesha biashara zao pamoja na shughuli zao za kila siku bila kusubiri muda wa uliokusudiwa wa akaunti ya amana ufike ndio wapate fedha zao. Hili la BancABC kutoa malipo ya riba mwanzoni ni jibu la ombi lililotolewa na wateja ikiwa ni hatua ya kufaidi mapema pato au mavuno yanayotokana na uwezekezaji wao kwa kipindi hicho.

‘Vile vile, tumetoa uhuru kwa mteja anayetaka kuchukua riba yake baada ya robo ya mwaka, nusu ya mwaka au hata baada ya mwaka ikiwa hataki kuchukua punde tu anapowekeza. Kwetu sisi BancABC, mteja ni mfalme na ndio sababu tumetoa uhuru huu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu wote’, alisema Malai.

Akizugumzia zaidi juu ya kampeni hii, kaimu mkuu wa kitengo cha Haina Luiza Paschal, aliongeza kuwa mteja anaweza kukopa kutokana na amana ya akaunti yake iwapo atahitaji mkopo. Tunaomba wateja wetu wote watumie fursa hii kabla ya muda wa ofa kuisha.

‘Unachotakiwa kufanya ni kupiga namba 0779 111 000 au tembelea matawi yetu yaliyopo Dar es Salaam (Uhuru, Tegeta na Kariakoo), Dodoma, Arusha na Mwanza, fungua akaunti ya amana kisha upate riba yako papo hapo’, Malai alisema.

Ofa hii ni kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana na BancABC Tanzania kwa mwaka mmoja kabla ya tarehe 30 Septemba 2021.
Muendeshaji Mkuu wa Biashara wa BancABC Tanzania Joyce Malai akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya benki hiyo kuzindua kampeni kabambe ya kuweka fedha katika akaunti ya amana (fixed deposit) kwa wateja wote, ambapo kwa sasa mteja ataweza kupata riba ya hadi asilimia 14 kwa mwaka. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Luiza Paschal.
Muendeshaji Mkuu wa Biashara wa BancABC Tanzania Joyce Malai (kulia) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Luiza Paschal wakionyesha bango baada ya benki hiyo kuzindua kampeni kabambe ya kuweka fedha katika akaunti ya amana (fixed deposit) kwa wateja wote, ambapo kwa sasa mteja ataweza kupata riba ya hadi asilimia 14 kwa mwaka.

TIC YAONGOZA KAMATI YA KUJADILI MASWALA YA MUWEKEZAJI DANGOTE

$
0
0

 Taasisi za serikali na Wizara zilizopo kwenye kamati ya kujadili maswala ya muwekezaji wa Kiwanda cha saruji cha Dangote (Dangote Cement (T) LTD) zakutana na kujadili namna bora ya kutatua changamoto mbalimbali za kiwanda hicho, kikao kazi hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Udzungwa kwenye ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tarehe 23 Juni, 2021.


Kikao hicho ni muendelezo wa kikao cha Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geoffrey Mwambe na wawakilishi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichofanyika tarehe 8 Juni, 2021 ambapo Mhe. Waziri Mwambe alielekeza kuwa changamoto zilizopo kwenye kiwanda hicho cha saruji ziwasilishwe Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili waweze kuratibu kikao na wadau kwa ajili ya kukamilisha changamoto hizo na kutoa mapendekezo kwa kikao cha ngazi ya Mawaziri wa Kisekta chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji.

Kutokana na muktadha huo Mkurugenzi Mtendaji wa (TIC) Dkt. Maduhu I. Kazi ameongoza kikao kazi hicho na kuelekeza kuwa kila taasisi ihakikishe inafanyia kazi makubaliano yaliyofikiwa ikiwa ni njia moja wapo ya kutatua changamoto hizo.

Wadau walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jeshi la Polisi Tanzania (TPF), Dangote Cement (T) Ltd, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Mawasiliano na Tehama na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA)















Wajumbe wa kamati kutoka Wizara na taasisi mbalimbali walioshiriki kikao cha kujadili na kutoa maoni kuhusiana na maswala ya muwekezaji wa kiwanda cha saruji cha Dangote.Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu I. Kazi Kushoto akipokea maoni toka kwa wajumbe wa kamati kutoka Wizara na taasisi mbalimbali walioshiriki kikao hicho.

Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumiliki pikipiki kupitia mkataba wangu na Bolt- Dizaya Damiano

$
0
0



“Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumiliki pikipiki kupitia mkataba wangu na Bolt. Sasa najivunia kumiliki pikipiki yangu mwenyewe, ndani ya kipindi cha miaka minne (4) kupitia mfumo wa usafiri kwa njia ya mtandao. Kwa kipindi hiki nimefanikiwa kuoa na kwa ninamtunza mke na binti yangu kupitia usafiri huu.

Pia nimeweza kutunza akiba ya kutosha na kununua kiwanja ambapo nina mpango wa kuanza kujenga nyumba yetu.

Kweli mfumo wa usafiri kupitia mtandao unawapatia vijana fursa nzuri ya kujiongezea kipato kizuri, na kupanga vyema muda wa kufanya kazi.

Nimeweza kuwapa fursa za ajira marafiki zangu wengi, ambao nao sasa wanafaidika kwa kufanya kazi na Bolt. Nina mengi ya kushukuru na yote ni kwa sababu ya Bolt”.

Huduma ya usafiri wa Bolt kupitia mtandao ipo kila sehemu na abiria wanapata huduma hii kiurahisi kupitia simu zao za mkononi, wakati wowote na mahali popote wanapohitaji huduma.

Kupitia Bolt, najisikia kuheshimiwa na jamii na nimebarikiwa pia kujua sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam. – Dereva Bolt - Dizaya Damiano Bugeraha (24), Tegeta - Dar es Salaam.

WADAU WA USAFIRISHAJI NCHINI WATOA NENO SHERIA UBEBAJI MIZIGO ZAMBIA KATIKA BANDARI YA DAR

$
0
0

 


*Waiomba Serikali kuchukua hatua haraka, kwani inaonesha ukandamizaji
 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WADAU wa usafirishaji katika bandari ya Dar es Salaam ukiwemo Uwakilishi wa Vyama vya usafirishaji na Chama cha Wakala wa Bandari wametoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikitatua changamoto zao kwa spidi ya kuridhisha.

Mbali ya pongezi hizo, wadau hao wametoa ombi kwa Serikali kuhakikisha inashughulikia changamoto ambayo imejitokeza baada ya wadau wenzao wa Zambia kuwa na sheria ambayo inaeleza wasifirishaji wa mizigo kutoka nchini Zambia ndio wanaotakiwa kusafirisha mizigo ya bandari ya Dar es Salaam inayokwenda nchini kwao kwa asilimia 50.

Wamesema ni vema Serikali ikatoa utatuzi wa changamoto hiyo huku wakiweka wazi , Watanzania wako tayari kushindana na majirani zao wa Zambia kwa ushindani wa bei, ubora wa huduma na usawa lakini sio kushindana kwa kutumia sheria inayokandamiza upande mmoja kwani hata Jumuiya ya SADC imeruhusu ushindani unaozingatia usawa katika kufanya biashara huru kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Akizungumza leo Juni 24,2021 jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Bw.Elias Lukumay   amesema wadau hao wanapongeza hatua ya Serikali kuboresha bandari hiyo ili iweze kubeba mizigo tani milioni 30 na spidi ambayo Rais Samia anakwenda nayo wanaamini hilo linawezekana.

Pamoja na mafanikio yaliyopo amesema  wadau hao wameona haja ya kuzungumzia mjadala unaondelea wa suala la SI ambalo haliko ndani ya Serikali ya Tanzania bali liko nje ya Serikali."Ni jambo ambalo limezungumzwa kwenye vyombo vya habari, hivyo nasi tunaona tuzungumze kidogo, wenzetu wa kule Zambia ni wadau wakubwa wa bandari ya Dar es Salaam, mizigo mingi inakwenda Congo na Zambia ambayo ni mtumiaji wa pili wa bandari yetu.

"Kwa hiyo ni mdau muhimu sana,lakini upande wa Zambia tumeona changamoto moja ambayo ni lazima kuisemea kwasababu ni ya kitaifa, Zambia ni wanachama wa jumuiya ya SADC na jumuiya hiyo ina taratibu zake,inataka kuwe na ufanyaji wa biashara wa soko huria, tushinde kwa huduma bora, bei nzuri, tusishindane kwa hila.

"Tunachokiona kwa wenzetu ni jambo ambalo linahitaji kutolewa ufafanuzi kidogo .Kitu kinachoitwa SI maana yake ni nini? Wazambia wanataka jinsi ya kubeba mzigo ya Zambia katika bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia na mzigo wa zambia kuja Dar. Wanasema mizigo ya Wazambia ambayo mingi ni mafuta na Copa asilimia 50 ibebebwe  na wao.

"Hii maana yake ni nini?Mzambia kwa maana ya ni Mzambia kwa uraia, awe amezaliwa kule au ameoa, hivyo ukienda kule huwezi kupata nafasi hiyo, asilimia 30 ya mizigo  ndio ibebwe na TAZARA na asilimia 20 iliyobakia ibebwe na wengine, kumbukeni hapa nyumbani kuna wasafirishaji ambao wamekuwa kwenye biashara hiyo  kwa muda mrefu,"amesema 

Ameongeza wadau hao waliopo nchni wamekopa fedha na wamewekeza kwenye biashara hiyo."Leo tukifika tunagawana biashara hii kwa asilimia maana yeke watanzania waliowekeza watafilisika na watakosa mizigo lakini Mungu aliyetupa bandari hii tutaona kama urembo, tutakuwa tunaona magari ya wenzetu tu yanapita. 

"Sisi hatupingani na mtu yoyote anayetaka kufanya biashara kwa soko hurua, tuko tayari kushinda kwa ubora wa huduma kwa bei lakini hatuko tayari kuona tunashinda kwa watu kutumia sheria kukandamiza wengine, kwa hiyo tukasema katika kuboresha huduma zetu ni vizuri tukaona Serikali inachukua hili jambo kama changamoto.

"Wasafirishaji wa tanzania wanatumia lita za mafuta milioni mbili wakiweka Zambia na kurudi na wanaporudi wanachukua mizigo ya nafaka kwa ajili ya kuleta Dar es Salaam na hivyo bei ya mazao ya nafaka kuwa chini kutokana na kusafirishwa na usafiri wa malori,hivyo tunahitaji kufanya biashara na wenzetu wa Zambia kwa ushindani wa kibiashara sio kutumia sheria kushindana kibiashara.

"Na hii tunaisema kwa nia njema tukiamini sisi kama nchi hatuwezi kuruhusu utaratibu huo lakini pia hatutaki kuwanyima Wazambia stahili yao ya msingi ya kuja kuchukua mzigo, tunachosema tushindane kwa huduma na hizi huduma ndizo zitakazoamua nani atafanya zaidi lakini sio kutumia sheria,"amesema.

 Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Forodha Elitunu Maramia amesema wao kama wadau wa usafirishiji ambao wanahusika na uchakati wa kuondosha mizigo inayoingia Tanzania na ile inayoondoka, wamekaa na wadau wenzao wa uchukuzi, usafirishaji na wamiliki wa malori na Chama cha Wamiliki wa usafirishaji (TOT) na wameamua kufanya tathimini ya sekta inavyokwenda.

Amesema wameona kuna mambo ambayo Serikali inapaswa kutekelezwa kwa spidi kubwa ambayo ndani ya miezi mitatu ya awamu ya sita wameiona na kikubwa wamekiona na kuthaminiwa, Serikali katika kipindi hicho imesogea karibu na wadau hao na kusikiliza changamoto walizonazo na kuzipatia ufumbuzi kwa spidi.

Pia amesema wameona jinsi Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye miundombinu ikiwemo upanuzi wa bandari , kuongeza kina cha bandari , ujenzi wa mindombinu ya barabara na reli."Tunamshukuru Rais Samia amejipanga kuindeleza sekta hii na kuikuza, sekta ya uchukuzi ni sekta wezeshi kwenye uchumi na inachangia kwa asilimia nane.

"Sasa kwenye uchumi na vile vile inasadia sekta nyingine ziweze kukua kwa kasi, tunavchokiona pia sisi kama nchi sio tu tunahudumia soko la ndani bali tunahudumia na soko la nchi jirani kam Zambia, Congo na nyinginezo na kwenye hili tunaona Serikali inatakiwa kama ambavyo tunashauri inapaswa kuiona sekta binafsi kama mbia.

"Sekta ya umma na sekta binafsi zinatakiwa kushirikiana kutatua changamoto na kupanga mipango ya pamoja, tani milioni 30 kupitia Bandari ya Dar es Salaam inawezekana na mambo ambayo tunashauri ili kufikia tani hizo milioni 30 za mizigo ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi,"amesema.

Pia amesema kuna haja ya Serikali kuiangalia kwa kina na kuifafanua sheria inayozungumzwa nchini Zambia kwani kama ikiachwa iendelee ilivyo inaweza kuathiri nchi yetu kwa maana ya kubeba mizigo inayopita hapa nchini.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Bw.Elias Lukumay akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam

Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Bw. Elitunu Mallamia akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.


NMB mkombozi wa maisha ya Wafanyakazi, Wastaafu Tanzania

$
0
0

 WATUMISHI wa umma nchini, hususani walimu, wamekumbushwa umuhimu wa kukopa kwa malengo, sambamba na kuepuka mikopo kandamizi, huku wakielezwa kuwa Benki ya NMB ni mkombozi, mshirika na rafiki sahihi wa maisha ya wafanyakazi kabla na baada ya kustaafu.


Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Dar es Salaam, Amos Makalla, wakati akizindua kongamano la siku moja la Walimu na NMB kwa mkoa wa Dar es Salaam 'Hatua kwa Hatua,' lililofanyika Jumatano, likiandaliwa na Benki ya NMB na kushirikisha walimu zaidi ya 300 toka wilaya za mkoa huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo, RC Makalla alibainisha kuwa, walimu na watumishi wengine wa umma wanapaswa kutambua umuhimu wa uwekezaji mdogo mdogo kwa ustawi wa maisha yao wawapo kazini na baada ya kustaafu na kutumia vema fursa za mikopo rafiki ya NMB.

"Tumieni falsafa ya 'I=C+S.' Maana yangu ni kuwa 'Income Can be Consumed or Saved.' Kwamba chochote unachopata unaweza kukitumia au kuweka akiba. Sasa tunakosea tunapogeuza pato lote kuwa 'Consumption.' Kadri unavyoweka akiba, ndivyo unavyoweza kufanya 'investment.'

"Ustawi wa maisha yenu ya sasa na baada ya kustaafu, unategemea na uwekezaji mtakaofanya, ikiwamo kukopa kwa malengo, kuepuka mikopo kandamizi na kutotumia pesa za mikopo kwa anasa. Mimi mwenzenu ni shuhuda wa hili na niwaibie siri, ukiondoa NMB, taasisi nyingi za fedha hazina madirisha yanayokidhi mahitaji ya watumishi.

"NMB ndio benki kinara wa kuwakomboa watumishi wa umma, benki inayoongoza katika kubuni na kutoa huduma rafiki kwa walimu na watumishi wengine kwa kuwapa mikopo yenye riba na masharti nafuu. Walimu mna fursa pana ya kunufaika na benki hii," alisema RC Makalla.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema walimu ni kada muhimu miongoni mwa makundi yanayo hudumiwa na benki yake, huku akiitaja kada hiyo kama iliyotoa mchango mkubwa wa kukuza pato la NMB kiasi cha kuongezeka kwa gawio lao kwa Serikali katika mwaka wa fedha uliopita.

"Niseme tu kwamba, walimu ni kundi muhimu kwa benki yetu, ndio maana tumeandaa Siku ya Walimu na NMB. Kupitia siku hii, tunapata fursa ya kuongea nanyi, kutambulisha huduma mpya na kupokea mawazo mazuri kutoka kwenu, kwani nyie mnayaona mengi huko kwenye jamii na mawazo yenu yana thamani kubwa.

"Majuzi NMB imekabidhi kwa Serikali gawio la Sh. Bilioni 21.8, mafanikio ambayo kimsingi yana mchango mkubwa wa walimu, kada ambayo bila uwepo wake, huenda NMB isingekuwa hapa ilipo. Ndio maana tuko makini kubuni huduma rafiki kwenu, zikiwamo za Kidijitali," alisema Mponzi.

Naye Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema NMB na Walimu ni jukwaa muhimu sio tu kwa kutoa elimu ya masuala ya fedha na kukusanya maoni yao, bali kunadi bidhaa mpya, ambako mwaka huu, pamoja na nyinginezo, wamekuja na Bima ya Vikundi.

Aidha, baadhi ya washiriki wa kongamano hilo walikiri kuvutiwa na ubunifu wa NMB sio tu katika huduma rafiki wanazotoa kwao, bali kwa namna inavyojitoa kutatua changamoto za Sekta ya Elimu, sambamba na kuwakutanisha walimu na kupokea mawazo na ushauri wao, kisha kuyafanyia kazi.

Mwalimu Victor Timbuka wa Shule ya Msingi Msasani, wilayani Kinondoni, aliipongeza kwa namna inavyopambana kuwaelimisha walimu nchini masuala ya uwekaji akiba, huku alikiri kuvutiwa na kauli ya RC Makalla juu ya umuhimu wa kuweka akiba na kufanya uwekezaji mdogo mdogo kwa ustawi wa maisha yao ya sasa na baada ya kustaafu.

"Kauli ya RC Makalla ina ukweli, kwa miaka mingi matatizo yetu yalitokana na kukosa elimu ya masuala ya fedha, madhara ya ukopaji usio na malengo, pamoja na matumizi ya pesa za mikopo kwa anasa. Lakini kupitia majukwaa kama haya, walimu hivi sasa wameelimika na hawafanyi makosa hayo tena," alisema Timbuka.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Walimu Tanzania, Fatuma Kalembo, alikiri kuwa wengi wao waliingia matatizoni kwa kuvamia mikopo kandamizi, isiyo na malengo na kutojibunia miradi midogo ya maendeleo na hivyo kuishi kwa kutegemea mishahara yao, lakini kwa sasa wanafanya ujasiriamali na kuongeza uwezo wa kujikumu na kujiendeleza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiongea kwenye kongamano la siku ya walimu na NMB lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. NMB Iliandaa siku ya walimu Dar es Salaam ambapo iliwapa mafunzo na elimu juu ya bidhaa za NMB zitakavyoweza kuwasaidia kwa Maisha ya baadae.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akikaribishwa na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati) na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard wakati wa Siku ya walimu na NMB (Teachers Day) iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.



MBIVU NA MBICHI KUELEKEA FAINALI YA EURO 2020

$
0
0

 

*Tumia Fursa ya Kubashiri na Meridianbet Sasa!
BAADA ya timu 24 kuoneshana uwezo kwenye hatua ya makundi, sasa ni timu 16 tu zitakazoendelea na mashindano ya Euro 2020. Mtanange unaanza upya, wikiendi hii mambo yapo hivi.

Ligi ya Norway itaendelea ambapo Lillestrom watachuana na Rosenborg, Meridianbet tunapatia Odds ya 2.15 kwa Rosenborg kwenye mtanange huu. Changamkia fursa hii.


Wales kumenyana na Denmark katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya Euro 2020. Itakumbukwa kuwa Wales walifika hatua ya nusu fainali msimu uliopita na wamemaliza katika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa Kundi A nyuma ya Italia msimu huu. Denmark wanamkosa Christian Eriksen lakini wameonesha namna gani sio timu ya kuibeza. Ukipata Meridianbet, utakuta Odds ya 1.95 kwa Denmark.


Jumapili mambo yatakuwa moto moto! Ubelgiji uso kwa uso na bingwa mtetezi wa Euro, Ureno. Hapa CR7 na Bruno Fernandez, kule Romelu Lukaku na Kevin De Bryune, hapatatosha! Unaweza kutengeneza faida kwenye mchezo huu kwa kuifuata Odds ya 2.55 kwa Ubelgiji ukiwa na Meridianbet.


Croatia kupambana na Hispania kwenye mchezo utakaochezwa Jumatatu. Hispania wameonesha kiwango cha chini kwenye michezo 2 ya mwanzo kunako hatua ya makundi lakini walimaliza hatua hiyo kwa ushindi wa 5-0. Luka Modric ameendelea kuwa nahodha hodari wa kikosi cha Croatia, Meridianbet inakupa Odds ya 1.70 kwa Hispania.

Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa! 

Viewing all 48995 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>