Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48994 articles
Browse latest View live

RC KUNENGE AGEUKA MBOGO, AWAJIA JUU WATUMISHI WANAOKUTWA NA TUHUMA MBALIMBALI

$
0
0

 

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
SERIKALI Mkoani Pwani ,imeziagiza halmashauri zote mkoani Pwani ,kuwachukulia hatua ikiwemo kutumia vyombo vya dola ili vifanye kazi yake kwa watumishi wanaobainika kuwa na tuhuma mbalimbali .

Aidha imeiagiza ,halmashauri ya Mji wa Kibaha na halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,kuhakikisha zinafunga hoja zote ambazo hazijafungwa katika ukaguzi wa hesabu za Serikali ,kwa mwaka 2019/2020, ifikapo September 30 mwaka huu.

Akitoa maagizo hayo mkuu wa mkoa wa Pwani ,Aboubakar Kunenge ,wakati wa baraza la madiwani kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG )mwaka 2019/2020, alisema ,ni wakati wa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi ambao watabainika kujinufaisha kwa mapato ama kusababisha hasara kwa halmashauri.

Aliongeza ,adhabu itakayotolewa ilingane na ukubwa wa tuhuma husika aliyosababisha mtumishi lengwa ili kusaidia kulinda maadili na uwajibikaji.

Pamoja na hilo ,Kunenge alitaka hoja ambazo hazijafungwa zifungwe na kama watakwama watoe taarifa.

Alibainisha pia hoja zinazohusisha taasisi nyingine zishughulikiwe na kuhakikisha hazijirudii katika mwaka mwingine.

Pamoja na hayo,aliwaasa kuacha kuridhika na vyanzo walivyovizoea ,badala yake wabuni vyanzo vipya vya mapato ,pamoja na miradi ya kimkakati itakayowawezesha kuinua mapato yao ya ndani .


"Epukeni kuzalisha hoja ,ongezeni wigo wa ukusanyaji mapato na halmashauri ibueni vyanzo vipya vya mapato ili kuinua mapato ." alisema Kunenge.


Nae mkaguzi mkuu wa hesabu ,Mkoani Pwani Mary Dibogo ,alisema wao wapo kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwa maslahi ya jamii na serikali hivyo CAG haiwezi kuonea halmashauri yoyote .


Alitaka fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi zifanyiwe kazi husika na ijengwe kwa thamani inayolingana na fedha iliyotolewa bila miradi hiyo kukaa kwa muda mrefu pasipo kukamilishwa.

Alizitaka halmashauri hizo,kusimamia ukusanyaji wa mapato ,na kuhakikisha yanafika sehemu sahihi .

Kwa upande wake ,Katibu tawala Mkoani Pwani ,Mwanasha Tumbo alitoa rai kwa watumishi na watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea .

Mwanasha aliwaasa kufuata sheria ,kanuni na muongozo katika masuala ya ukaguzi ili kuondokana na dosari ndogondogo.

Akiwa kibaha mji ,mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha ,Jeniffer Omolo yeye alisema ,kati ya hoja 38 kufikia juni 2 mwaka huu 22 zilifungwa ambapo hoja 16 hazijafungwa.


DKT.SENGATI KUKUTANA NA FAMILIA ZINAZOTELEKEZA WAZEE WAO

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongea na baadhi ya wazee waliofika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga na kujadiliana nao kuhusu masuala mabalimbali yahusuyo wazee hao.Baadhi ya wazee wa Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza hoja mbalimbali za viongozi wa mkoa wa Shinyanga jana mkoani Shinyanga.


Na Anthony Ishengoma -Shinyanga
MKUU wa mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati amehaidi kulifanyia kazi suala la wazee wanaotelekezwa na watoto wao kwa kuitisha vikao vya familia kwa lengo la kuzitaka familia hizo kubeba jukumu la kutunza wazee lakini pia kurejesha mahusiano yao.

Dkt. Sengati alitoa ahadi hiyo baada ya baadhi ya wazee wa Mkao wa Shinyanga kudai kuwa baadhi yao wametekelezwa na watoto wao na wengine kuachiwa kulea wajukuu na watoto wao ambao wana nguvu za kutosha kuwatunza watoto pamoja na wazee.

Dkt. Sengati alisema hayo jana alipofanya kikao cha pamoja na wazee wa mkoa wa Shinyanga ikiwa ni hatua yake muhimu ya kukutana na kusikiliza makundi tofauti ya jamii katika Mkoa wa Shinyanga.

Adha Dkt. Sengati aliwambia wazee hao kuwa ataendelea kuimarisha mabaraza ya wazee mkoani humo kwani baadhi ya mabaraza hayo hayafanyi kazi vizuri na kuziagiza Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kufanyia kazi changamoto za kibajeti ili wazee hao waweze pia kupata mikopo ya Halmashauri kama ilivyo kwa makundi mengine.

‘’Tutaendelea kushughulikia changamoto za kibajeti hasa ile asilimia mbili ambayo huwa ni lazima itengwe kutoka mapato ya ndani kwa lengo la kuwahudumia wazee kama kundi maalum lakini imekuwa haiwekwi na kwa namna moja au nyingine mmekuwa hamuipati.’’Aliongeza kiongozi huyo wa Mkoa wa Shinyanga.

Aidha Dkt. Sengati ametaka kila mwana Shinyanga kujielimisha lakini pia kutoa elimu kuhusu mira na desturi na imani potofu ya mahuaji ya wazee na kuwa na mtazamo chanya kwa kundi hili la wananchi hodari.

Katika hatua nyingine Dkt. Sengati alizitika Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kuendelea kuelemisha wazee hao namna bora ya kupata mikopo kutoka katika Taasisi za fedha na Halmashauri ili wazee waweze kijihimarisha kiuchumi na kuchangia katika Maendeleo ya Taifa.

Naye Mzee Mohamedi Mkambala mkazi wa Manispaa ya Shinyanga alimwambia Mkuu wa Mkoa kusaidia wazee katika suala zima la kimatibabu kwani wazee hao mara kwa mara wamekuwa wakiandikiwa madawa ambayo yamekuwa hayapatikani hospitalini.

‘’Kuhusu suala la Afya wazee wanapewa dawa za bure lakini wamekuwa wakiandikiwa kwenda kununua dawa izo hela watapata wapi wakati wana andikiwa dawa za bure?Alihoji Mzee Mkambala.

Katika madai tofauti tofauti ya wazee hao Bi. Judithi Kalwalala aliangazia suala la usalama na kuomba msaada wa Jeshi la Polisi kuingilia kati kwani vibaka wamekuwa wakivamia nyumba zao wakiwa wamevalia madera na kuwabia mali zao huku wakijua hakuna wanaume wakuwalinda.

Dkt. Sengati jana alifanya kikao cha pamoja na wazee wa mkoa wa Shinyanga ikiwa ni hatua yake muhimu ya kukutana na kusikiliza makundi tofauti ya jamii na atakutana na makundi mengine kama hayo kwa lengo la kuona namna bora kufanyia kazi matatizo ya wananchi mkoani Shinyanga.

UBALOZI WA FINLAND WACHANGIA PICHA, VITABU MAKUMBUSHO YA TAIFA

$
0
0

 

Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe Riitta Swan akimkabidhi kitabu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga.
Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe Riitta Swan akimkabidhi picha Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga.
Kushoto ni Balozi wa Finland nchini Mhe Riitta Swan, akijaza fomu maalumu ya Makumbusho ya Taifa ya kukabidhi mikusanyo, huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure (watatu kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Makumbusho ya Taifa Bi Joyce Mkunga (wa kwanza kulia) pamoja na afisa kutoka ubalozi wa Finland.

Na Sixmund J. Begashe
UBALOZI wa Finland nchini Tanzania umechangia picha 23 na vitabu viwili kwa Makumbusho ya Taifa la Tanzania ili viweze kuhifadhiwa kwenye taasisi yenye dhamana ya Uhifadhi, Utafiti, Ukusanyaji, na Utoaji elimu kupitia matokeo ya tafiti na Mikusanyo mbali mbali.

Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe Riitta Swan, alikabidhi picha na vitabu hivyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Mhe Balozi Swan ameeleza kuwa nchi yake imekuwa ikijihusisha sana na uhifadhi wa mazingira kwa faida ya viumbe hivyo, wamesukumwa kuchangia picha hizo ili zitumike kuelemishia jamii juu ya umuhimu wa mazingira salama kwa watu, mimea na viumbe vingine.

Picha hizi zilipigwa na Prof. Olli Marttla, ambaye ameishi miaka mingi nchini na kusafiri sehemu mbali mbali za Tanzania akipiga picha na kuandika vitabu vya mazingira, alisema Mhe. Balozi na kuongeza kuwa kupitia picha hizo zitkazohifadhiwa kitaalamu Makumbusho ya Taifa, watu wengi watapata elimu ya Mazingira na umuhimu wake ili dunia yote iwe salama kwa kila mtu na viumbe wengine.

“Ni Imani yetu kwamba picha hizi zitawafikia watu wengi zaidi hapa Makumbusho ya Taifa kuliko kuzihifadhi Ubalozi” amesema Mhe. Swan.

Akipokea picha hizo na vitabu, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa nchini, Dkt. Noel Lwoga aliushukuru Ubalozi wa Finland kwa mchango huo mkubwa na muhimu na kusema kuwa Taasisi yake inatarajia kuwa na Makumbusho nyingine ya Elimu Viumbe, hivyo, picha hizo zitatumika huko na hata kuboresha maonesho ya Baolijia yaliyopo sasa.

“Ukiachana na ile tuliyonayo pale Jijini Arusha, pia tuanatarajia kuwa na Makumbusho nyingine ya Elimu Viumbe, hivyo kwa picha hizi nzuri tulizo zipata leo zitasaidia kwenye Makumbusho hiyo.” Alisema Dkt. Lwoga

Dkt Lwoga aliongeza ametoa wito kwa wadau mbali mbali kuendelea kuchangia mikusanyo ya kimakubusho na kwa jamii kutembelea Makumbusho ya Taifa ili kupata elimu ya mazingira na nyinginezo kwani watapanua wigo wa uwelewa juu ya nchi ya Tanzania na dunia kwa ujumla.

Bw. Pius Gondeka, ambaye ni mdau wa Makumbusho ya Taifa, amepongeza kitendo cha Ubalozi wa Finland kuipatia Makumbusho ya Taifa picha ambazo yeye kama mwananchi na wananchi wengine watapata fusra ya kujionea uzuri wa Tanzania kupitia picha hizo lakini pia zitawawezesha kuwakumbusha umuhimu wa uhifadhi wa Mazingira.

Mkuu wa Idara ya Mikusanyo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Dar es Salaam Bi Flower Manase amesema Idara yake imejipanga vyema kuhakikisha picha hizo zinahifadhiwa kwa umakini mkubwa na utaalam wa hali ya juu ili ziweze kuishi miaka mingi na kuwafaidisha watanzania waliopo sasa na vizazi vijavyo.

UONGOZI INSTITUTE KUWAPIKA VIONGOZI WA UMMA NA WATEULE RAIS

$
0
0

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Uongozi Institute, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi Institute Dk.Stergomena Tax(watatu kushoto waliokaa)viongozi wa Serikali, wafanyakazi pamoja na wajumbe wa bodi hiyo baada ya kuzinduliwa rasmi leo Juni 18,2021.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa akizungumza wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Uongozi Institute leo Juni 18,2021 jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Samia Suluhu Hassan kumteua Dk.Stergomena Tax kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Uongozi Institute wakiwa kwenye tukio hilo la kuzinduliwa kwa Bodi ya Tatu ya Wakurugenzi ya Uongozi Institute iliyofanyika leo Juni 18,2021 jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Uongozi Istitute Dkt.Kadari Singo akizungumza kuhusu taasisi hiyo leo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Tatu ya Wakurugenzi ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa.Pia walikuwepo viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa(katikati) akiwa kwenye meza kuu na viongozi wengine wa Uongozi Insitute akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dk.Stergomena Tax(wa pili kushoto)Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Said( wa pili kulia).
Katibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Saidi(kushoto) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uongozi Institute Dk.Kadari Singo(kulia) wakipiga makofi wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa akitoa hotuba yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Uongozi Institute pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa(wa pili kushoto) akiwa na viongozi wengine baada ya kumkabidhi rasmi moja ya vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Uongozi Institute Dk.Stergomena Tax( wa tatu kushoto.)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt.Stergomena Tax akizungumza baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohemed Mchengerwa(hayupo pichani) kuzindua bodi hiyo leo Juni 18,2021.






 Matukio mbalimbali katika picha wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tatu ya Wakurugenzi wa Uongozi Institute leo Juni 18,2021.(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE - MICHUZI TV.)


*Serikali yaeleza kutotegemea viongozi kwenda kinyume na maadili na haki baada ya mafunzo hayo

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI wa nchi, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa amesema kuwa viongozi wote walioteuliwa wakiwemo wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakurugenzi lazima wapitie mafunzo wa Uongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) taasisi ambayo imekuwa ikiwaandaa na kuwapika viongozi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia haki, maadili na weledi.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam wakati akizundua bodi ya tatu ya wakurugenzi ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,)  Waziri Mchengerwa amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo hayo kwa viongozi wote wa Umma wakiwemo wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi, wakurugenzi wa Wizara, viongozi walioteuliwa na Mawaziri kupata programu za mafunzo maalumu ya uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi ambayo imerejesha sifa ya kupika viongozi.

'' Ili watendaji wafanye kazi kwa weledi katika nafasi zao walizoteuliwa na wanazozitumikia wakiwemo vijana lazima wapite katika mikono ya Taasisi ya Uongozi ili watumikie nafasi zao kwa kuzingatia maadili, haki na weledi.'' Amesema.

Waziri Mchengerwa amesema, Hakuna kiongozi yeyote wa Umma na kuteuliwa ambaye hawatapitia mafunzo hayo na hawategemei baada ya mafunzo hayo viongozi hao kwenda kinyume na haki na maadili wa uongozi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Pia amesema, Bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Uongozi iliyozinduliwa leo imesheheni wataalamu wa elimu na viongozi wabobevu ambao watashirikiana na Taasisi hiyo ambayo Serikali inatambua mchango wake wa kuikuza Taasisi ya Uongozi ndani na nje ya nchi.

kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC,) Dkt. Stergomena Tax amesema, bodi mpya ya Taasisi ya Uongozi inamshukuru Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi huo na watafanya kazi na kuhakikisha wanafikia lengo kuu la kujenga viongozi watakaoleta maendeleo endelevu nchini.

Dkt. Tax amesema, Wanatambua umuhimu wa viongozi mahiri na watasimamia jukumu hilo katika kuhakikisha viongozi wanajengwa katikla miiko ya maadili na kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi.

''Sio kwamba viongozi hawapo....Wapo ila mambo yanabadilika kila siku lazima viongozi waende na maendeleo ya kidunia.'' Amesema Dkt. Tax.

Awali akieleza majukumu ya Taasisi hiyo Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) Dkt. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo kwa viongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam na kuzisaidia taasisi mbalimbali pamoja  na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) ilianzishwa Julai, 2010 kwa malengo ya  kuwa na kituo cha utalaam wa juu cha kuendeleza viongozi barani Afrika kwa kuanzia nchini Tanzania, Kanda za Afrika Mashariki na hatimaye Afrika nzima.


RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA WILMAR INTERNATIONAL, IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya Wilmar International ya Singapore, Kuok Khoon Hong mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Juni, 2021.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Wilmar International ya Singapore Kuok Khoon Hong akizungumza na Wanahabari Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Juni, 2021.
 



 

Makinda amrithi Salim Ahmed Salim HKMU

$
0
0

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), wakiongoza maandamano ya kwenda kumsimika rasmi mkuu mpya wa chuo hicho, Anne Makinda kwenye hafla iliyofanyika  jana chuoni hapo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki (HKMU), John Ulanga akimvalisha kofia Mkuu mpya wa  Chuo hicho, Anne Makinda kama ishara ya kumsimika rasmi kwenye nafasi hiyo. Makinda anachukua nafasi ya Salim Ahmed Salim. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki, Kokushubila Kairuki.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Spika mstaafu Anne Makinda akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa HKMU mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mkuu wa chuo hicho kwenye hafla iliyofanyika jana Mikocheni jijini Dar es Salaam..
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Spika mstaafu Anne Makinda akiongoza kwenda kwenye hafla ya kumsimika rasmi kuwa mkuu wa chuo hicho jana jijini Dar es Salaam Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, John Ulanga na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa Shirika la Afya na Elimu

WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA POLISI KUDHIBITI UTOAJI, UKAGUZI WA SILAHA NCHINI

$
0
0

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Tatu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, jijini Dodoma, leo, kabla ya kuizindua Bodi hiyo. Ameitaka Polisi kudhibiti Utoaji na ukaguzi Nchini na pia ishirikiani na sekta binafsi za ulinzi ili kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi. Wapili kulia ni Kamishina wa Polisi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Benedict Wakulyamba.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akimsikiliza Kamishina wa Polisi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Benedict Wakulyamba, akizungumza katika Kikao cha Wajumbe wa Bodi ya Tatu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, jijini Dodoma, leo, kabla ya Bodi hiyo haijazinduliwa. Waziri huyo ameitaka Polisi kudhibiti Utoaji na ukaguzi Nchini na pia ishirikiani na sekta binafsi za ulinzi ili kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tatu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, Toyi Ruvumbangu, jijini Dodoma, leo, kabla ya Waziri huyo hajaizindua Bodi hiyo. Waziri huyo ameitaka Polisi kudhibiti Utoaji na ukaguzi Nchini na pia ishirikiani na sekta binafsi za ulinzi ili kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Katibu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Massawe, jijini Dodoma, leo, kabla ya Waziri huyo hajaizindua Bodi hiyo. Waziri huyo ameitaka Polisi kudhibiti Utoaji na ukaguzi Nchini na pia ishirikiani na sekta binafsi za ulinzi ili kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi. Katikati ni Kamishina wa Polisi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Benedict Wakulyamba.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Tatu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, jijini Dodoma, leo, baada ya Waziri huyo kuizindua Bodi hiyo. Ameitaka Polisi kudhibiti Utoaji na ukaguzi Nchini na pia ishirikiani na sekta binafsi za ulinzi ili kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi. Wapili kushoto waliokaa ni Kamishina wa Polisi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Benedict Wakulyamba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NMB YAKABIDHI SERIKALI HUNDI YA ZAIDI YA BILIONI 21.7

$
0
0
Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango (wapili toka kulia) akionesha mfano wa hundi ya zaidi ya sh Bilioni 21.8 iliyokabidhiwa Serikali ikiwa ni gawio kutoka Benki ya NMB,kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori .

*************************

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh21.8 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 ya gawio la mwaka jana ambalo lilikuwa Sh15.25 bilioni.


Akipokea mfano wa hundi, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema kiasi hicho kimemridhisha kwa mwaka huu lakini akataka waongeze maarifa zaidi ili kutoa gawio la juu ikiwemo kuwekeza katika nchi majirani.

Dk Mpango alisema kiwango kilichotolewa mwaka jana hakikumfurahisha ndiyo maana akaagiza lazima waongeze juhudi lakini kwa mwaka huu amebarikiwa.Gawio lililotolewa jana ni sehemu ya faida ya Sh206 bilioni ambazo benki hiyo ilipata katika msimu wa kuishia desemba 2020 baada ya kuondoka kodi.

Serikali inapokea gawio hilo kutokana na umiliki wake wa hisa asilimia 31.8 ndani ya benki hiyo ambayo kwa miaka 8 mfululizo imekuwa ikipata tuzo ya benki bora nchini.

“Nimefurahishwa sana na hiki mlichotoa, pamoja na mafanikio haya lakini nataka muongeze ubunifu ili mwaka muwe zaidi ya hapa, hata hivyo nakuagiza Waziri wa Fedha kwamba kiasi hiki kikafanye kazi nzuri kwa wananchi ambayo imekusudiwa,” amesema Dk Mpango.

Kuhusu NMB aliwataka kushirikiana na Taasisi zingine ili wakae na benki Kuu (BoT) kujadili kuhusu riba kubwa ambayo bado inatozwa na mabenki na hivyo kusababisha watu washindwe kukopa.

Aliwataka viongozi wa taasisi ambazo Serikali ina hisa lakini hawatoi gawio kwamba wajitathimini vinginevyo watachunguzwa na watakaokuwa wamekiuka kanuni Serikali itawapeleka Segerea hata kama kumejaa.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NMB Edwin Mhede alisema tayari fedha hizo zilishawekwa katika akaunti ya msajili wa Hazina na kwamba mwakani watakuwa na kiasi kikubwa zaidi kutokana na mwenendo wavyoona.

Mhede alitaja siri kubwa ya mafanikio ya NMB ni ubunifu na kutljituma kwa watumishi wao katika kuutafuta masoko lakini utoaji bora wa huduma unaowabutia watu kuitumia benki hiyo.

Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna alisema mbali na gawio hilo,lakini wamelipa Serikalini Sh245 bilioni kama kodi za tozo mbalimbali na kutumia asilimia moja ambayo ni zaidi ya Sh2 bilioni kwenye huduma za kijamii.

Bi. Zaipuna alisema benki hiyo imefikia mtaji was Sh1.1 trilioni kutoka Sh660 bilioni kwa mwaka 2015 hivyo ukuaji wake unatia matumaini kwamba itaendelea kuwa ni benki bora yenye kutoa huduma kwa viwango vinavyotakiwa.

SERIKALI IPO TAYARI KUPOKEA MAONI YA WADAU ILI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU - WAZIRI NDALICHAKO

$
0
0
SERIKALI ipo tayari kupokea maoni ya wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya Elimu ili kupata wahitimu wenye ujuzi wa kujiajiri, kuajiriwa na kukidhi mahitaji ya uchumi wa kati na viwanda.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo Mkoani Dar es Salaam katika mkutano wa pamoja uliowakutanisha na wadau elimu na kujadili kwa pamoja namna gani kuboresha mitaala ya elimu kwa ngazi ya awali, msingi na sekondari.

Waziri Ndalichako amesema, Mkutano huo ni matokeo ya maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Serikali ya awamu ya sita Samia Suluhu Hassan na ambayo amekuwa akiyatoa kwa nyakati tofauti kuhusu mapitio ya elimu inayotolewa kuzingatia inajenga ujuzi na stadi za kazi kwa watoto wa kitanzania.

Amesema katika kutekeleza maelekezo ya Rais wamekutana na wadau hao na kupitia mitaala kwa kujikita zaidi katika kutoa maoni yenye kuimarisha mitaala hiyo ambayo italenga kujenga ujuzi na stadi za kazi na mwelekeo chanya kwa watoto wa kitanzania.

Amesema, kupitia mkutano huo maoni yatakayotolewa na wadau hao yatatumiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET,) katika kuboresha mitaala katika ngazi msingi kwa mlengo wa ujuzi, maarifa na misingi madhubuti ya uendelezaji wa elimu nchini.

"Msingi imara wa uboreshaji wa mitaala kwa elimu ya msingi ni nguzo imara katika ngazi za elimu zinazofuata na kuwawezesha wahitimu kumudu mazingira na shughuli za maendeleo zinazowazunguka, na niwaombe maoni tutakayoyatoa yawalenge watoto/wahitimu wa ndoto zetu ambao tunasema wakimaliza darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita hawajui chochote.'' Amesema.

Pia Ndalichako amesema Rais Samia amekuwa akisisitiza kuhusu sekta ya elimu kupitia hotuba zake hasa katika suala la mitaala kwa kuangalia mitaala itakayokuza elimu nchini.

"Niwaombe wadau mliojitokeza leo tujadili suala hili tumuunge mkono Rais wetu katika kutoa mapendekezo na maboresho bora katika mitaala itakayojenga ujuzi, maarifa na kujitegemea kwa wahitimu pamoja na kutumia fursa zinazopatikana nchini kwa kuajiriwa na kujiajiri." Amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba amesema kuwa matarajio ya mkutano huo, ni kupatikana kwa uelewa wa pamoja wa Mitaala iliyopo sasa na kupokea maoni ya Elimu na Mitaala itakayorekebishwa.

“Na imani kuwa tutapata maoni mengi yatakayoboresha Elimu yetu nchini,hivyo tushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha tunafanikisha ubora wa Elimu” alisema Dkt.Aneth.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadetha Kilian, amesema taasisi hiyo imejipanga vyema kuhakikisha inaboresha mitaala kuendana na mahitaji ya sasa.

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET,) umelenga kukutana na kupokea maoni ya wadau kuhusu mchakato wa kuboresha mitaala ya ngazi ya elimu ya awali, msingi na sekondari, mitaala iliyopo na mwelekeo wa Elimu nchini.
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mh. Prof.Joyce Ndalichako akizungumza mbele ya Wadau wa Elimu (hawapo pichani) wakati akifungua mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City,mkoani Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mkoani Dar es Salaam
Sehemu ya Meza kuu ikifurahia jambo .
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba, akizungumza katika mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadetha Kilian akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mkoani Dar es Salaam
Sehemu ya Wadau wa Elimu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mh. Prof.Joyce Ndalichako,Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo pamoja na Wadau wengine wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa ukumbini humo kuhusu mchakato mzima wa kuleta mabadiliko makubwa katika mitaala ya elimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba, akizungumza katika mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini.
Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Jijini Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Jijini Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Jijini Dar es Salaam

SERIKALI KUFUNGA KAMERA ZA USALAMA DODOMA

$
0
0

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka(wapili kushoto), akisikiliza maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Zakaria Senso baada ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa kituo hicho leo, kinachojengwa katika Kata ya Chang’ombe, jijini Dodoma.Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ramadhani Kailima.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (wapili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka mifuko ya saruji ikiwa ni mchango wake katika Ujenzi wa Kituo Kipya cha Polisi Chang’ombe lengo ikiwa kudhibiti uhalifu katika maeneo ya Changombe.Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ramadhani Kailima.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

*************************

Abubakari Akida, Dodoma

Serikali imedhamiria kufunga kamera za usalama katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kupunguza uhalifu ambao umeanza kushamiri katika maeneo ya jiji hilo baada ya Serikali kuhamia Dodoma huku wimbi la watu likichagiza hali hiyo ya uhalifu.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka wakati wa Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe kinachojengwa katika eneo la Chang’ombe, jijini Dodoma.

Adhma hiyo ya kujenga kituo imekuja baada ya matendo ya uhalifu ikiwemo uporaji, ubakaji, udhalilishaji, matumizi ya dawa za kulevya kushamiri katika maeneo ya Chang’ombe hali inayopelekea wananchi wa maeneo hayo kuishi kwa wasiwasi wakihofia matendo hayo ya uhalifu.

“Maeneo mengi ya jiji la Dodoma tutafunga kamera za usalama barabarani, hatuwezi kuwa na jiji ambalo  polisi wetu wanakimbizana na wahalifu muda wote, tutatumia teknolojia hiyo kudhibiti uhalifu wa aina mbalimbali, Dodoma ni Makao Makuu ya nchi lazima pawe salama nawashauri wahalifu watafute shughuli nyingine ya kufanya hapa si salama tena kwa kazi zao” alisema Mtaka

Akizungumzia Ujenzi wa Kituo hicho cha Polisi, Mkuu wa Mkoa huyo aliwataka wananchi kushirikiana na serikali kuhakikisha kituo hicho ujenzi wake unakamilika mapema ili kianze kutoa huduma za kiusalama katika maeneo hayo.

“Chang’ombe inakua inahitaji kituo kikubwa kitakachofanya kazi saa ishirini na nne ili wafanyabiashara na wananchi wafanye shughuli zao kwa muda wote na sio biashara zifungwe kwa kuhofia uhalifu, sasa kazi ya serikali sio kukwambia ufunge biashara yako muda gani kazi ya serikali ni kukulinda ili kuwepo na  uhuru wa kutoa huduma, kwahiyo wananchi tushirikiane ili kituo kimalizike haraka” alisema Mtaka

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Naibu Katibu Mkuu Ramadhani Kailima alisema wizara imetoa kiasi cha shilingi milioni 10/= kama mchango wake katika ujenzi wa kituo hicho na kikikamilika  kitaweza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo upelelezi wa matukio, upelekaji wa majarada ya kesi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ambayo yatapelekwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Katika hafla hiyo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alichangia papo hapo mifuko hamsini ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka.

SERIKALI YAJIPANGA KIMKAKATI KUVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI - WAZIRI MKUMBO

$
0
0

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo(kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje(EPZA) John Mnali wakiteta jambo wakati wadau walipokutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uwekezaji nchini.
Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati akifungua majadiliano yaliyohusu uhusiano baina ya maeneo maalum ya uwekezaji na uchumi wa ndani ambapo wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya uwekezaji wameshiriki.
Wadau wa uwekezaji, wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi pamoja na wafanyakazi wa EPZA wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo(hayupo pichani.)
Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi pamoja na wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje(EPZA.)
Mmoja ya wadau akiwa makini kusoma kijarida cha EPZA wakati wa majadiliano hayo yakiendelea.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Mku wa TPSF Godfrey Sembeye akiandika jambo wakati wa majadiliano hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo(hayupo pichani.)
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwezeshaji wa Uwekezaji wa EPZA akitoa mada iliyohusu fursa zinatolewa na maeneo maalum ya uwekezaji na namna ambavyo Serikali za mitaa na biashara ndogo na za kati zinavyoweza kunufaika.









Matukio mbalimbali katika picha wakati wa majadiliano yaliyohusu uhusiano baina ya maeneo maalum ya uwekezaji na uchumi wa ndani.(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE- MICHUZI TV.)

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

SERIKALI imesema imejipanga  kisera na kutoa huduma muhimu na sheria rafiki zinazokidhi na kuvutia wawekezaji wa nje na ndani ya nje ya nchi ili kuwezesha ukuaji wa biashara ndani ya bara la Afrika na nje ya nchi.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo wakati akizindua kongamano la uhusiano baina ya maeneo maalumu ya uwekezaji na uchumi wa ndani lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi Tanzania (Uongozi Institute,) pamoja na Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA,) na kuwakutanisha wawekezaji wa ndani na nje na kujadili namna ya kuunganisha maeneo muhimu ya uwekezaji na uchumi wa ndani pamoja na kuangalia namna ya kushirikisha wawekezaji wa ndani hasa wajasiriamali.

prof. Mkumbo amesema, katika kuhakikisha uchumi wa nchi unashindana kimataifa Serikali na taifa kwa ujumla linaendelea kujiunga na jumuiya mbalimbali za kikanda na kimataifa ili kushindana kimataifa kama ilivyoelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan juu ya msingi wa kuimarisha biashara ndani ya Afrika na nje ya mipaka kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wa taifa.

''Serikali imejipanga kisera, huduma muhimu katika maeneo ya uwekezaji, skills muhimu katika elimu ili kwenda na matakwa ya soko kwa ujumla pamoja na sheria za kodi katika kuhakikisha uwepo wa uzalishaji wenye tija katika maeneo ya viwanda.'' Amesema.

Aidha amesema, Serikali imejipanga Katika ujenzi wa mitaa ya viwanda "Industrial parts" pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika maeneo ya uwekezaj ya Kurasini, Bagamoyo na Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam.

Kwa upande wake kaimu mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA,) John Mnali amesema mamlaka hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu katika maeneo ya uwekezaji kwa niaba ya Serikali kwa kuhakikisha maeneo yote ya uwekezaji yanapata huduma muhimu hasa  miundombinu ya maji, umeme na barabara pamoja na kutoa leseni za uwekezaji kwa wawekezaji hao.

Amesema, wamekuwa wakishirikiana na Wizara ya viwanda na biashara pamoja na wadau wengine wa uwekezaji kwa kuhakikisha wanayafikia mafanikio kwa kiwango kikubwa na hadi sasa wamesajili kampuni zipatazo 176 zenye uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 2.5 na watanzania 58198 wamenufaika kwa kupata ajira za moja kwa moja hadi kufikia Machi, 2021.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi (Uongoz Institute,) kwa kushirikiana na EPZA liliwakutanisha wawakilishi wa Serikali za mitaa, wawakilishi wa biashara ndogondogo na kati, kampuni za uwekezaji, Taasisi za Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.


 

Benki ya UBA yatoa vitabu vya fasihi kwa vituo vya watoto yatima Dar es Salaam

$
0
0

Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali zaa kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne wanapata elimu bure, benki ya UBA Tanzania kupitia kitengo cha UBA Foundation umetoa msaada wa vitabu vya fasihi kwa vituo vya watoto yatima vya UMRA na Babu na Bibi vya jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Muasisi wa kituo cha UMRA Orphanage Center Rahma Juma alisema “Ni muhimu kutambua mchango wa makampuni binafsi kama benki ya UBA Tanzania kwa juhudi za dhati za kuunga mkononi na kuinus sekta ya elimu hapa nchini. Zote tunajua ya kwamba serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda. Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wasomi wazuri kutoka kwenye jamii yetu, hiyo basi vitabu hivi vitaongeza chachu kwa watoto ambao tunawale hapa kwani wote ni wanafunzi na hivyo kufanya vizuri katika masomo yao na hatimaye kufanikisha ndoto zao pamoja na serikali”.

Rahma aliongeza “nawaomba benki ya UBA na wadau wengine waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali ili kuendelea kutengeneza mazingira bora kwa watoto hawa kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Digitali UBA Tanzania Asupya Bussi“ Sisi benki ya UBA tunaamini jamii iliyoelimika inajengwa kutoka katika watoto pamoja na wanafunzi kuwa na vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani vitabu, ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu kwa shule hizi”.

Benki ya UBA imekuwa kwa muda mrefu ikisaidia sekta ya elimu hapa nchini kwenye Nyanja mbali mbali. Kwa maana hiyo, uongozi wa benki hii ulianzisha kitengo maalum kijulikanacho kama UBA Foundation kwa ajili ya kuendesha zoezi hili. Na kwa kutimizi hili, tumekuwa tukifanya kazi na serikali na naomba nitoe pongezi za dhati kwani serikali imekuwa ikituunga mkono kwa hili, Asupya alisema huku akiongeza kuwa benki ya UBA itaendelea kusaidia kwenye sekta ya elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi wetu.

Tunaamini ya kwamba msaada wa vitabu utachochea ufaulu mzuri kwa wanafunzi katika masomo yao na pia kuongeza ufaulu kwa shule zote hizi, alisema Asupya.

Kwa upande wake, Muasisi wa kituo cha watoto yatima cha Babu na Bibi Apolinary Mutalemwa alisema kuwa msaada wa vitabu hivi umekuja wakati muafaka wakati kituo hicho kilikuwa hakina vitabu kabisa licha ya kuwa watoto wote wanaolelewa hapo na wanafunzi na hivyo tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".

Aliongeza, watoto wote hawa hapa ni mayatima. Licha ya msaada wa vitabu hivi, lakini kufika kwenu kumekuwa ni faraja sana. Tunatoa pongezi za dhati kwa uongozi wa UBA Tanzania kwa kuamua kuja kututembela. Vitabu hivi vitajenga hali ya kujisomea kwa watoto wetu na kwa vyovyote ufaulu wao kwenye shule utaongezeka, alisema Mutalemwa.

Mkuu wa Kitengo cha digitali kutoka Benk ya UBA, Asupya Bussi Nalingigwa (kulia) akikabidhi vitabu kwa Muasisi wa Kituo cha kulea watoto wanaishi katika mazingira magumu cha Babu na Bibi Apolinary Mutalemwa kwa ajili ya wanafunzi wanaolelewa kituoni hapo. Benki ya UBA Tanzania kupitia UBA Foundation ilitoa vitabu hivyo kwa ajili ya kusaidia watoto kituoni hapo kupata vifaa vya kujisomea.
Mkuu wa Kitengo cha Digitali kutoka benki ya UBA Tanzania Asupya Bussi akiongea na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha watoto yatima cha Babu na Bibi cha jijini Dar es Salaam. Benki ya UBA Tanzania kupitia UBA Foundation ilitoa vitabu vya vituo vya UMRA na Babu na Bibi vyote vya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia watoto kituoni hapo kupata vifaa vya kujisomea.
Mkuu wa Kitengo cha digitali kutoka Benk ya UBA, Asupya Bussi Nalingigwa akikabidhi vitabu kwa Muasisi wa Kituo cha kulea watoto wanaishi katika mazingira magumu (UMRA), Rahma Juma Kishumba kwa ajili ya wanafunzi wanaolelewa kituoni hapo. Benki ya UBA Tanzania kupitia UBA Foundation ilitoa vitabu hivyo kwa ajili ya kusaidia watoto kituoni hapo kupata vifaa vya kujisomea.

Mkutano Mkuu Wadau wa Kahawa: Serikali Yaviasa Vyama Vya Ushirika Matumizi Bora Ya Mikopo, NBC Yaelezea Suluhisho.

$
0
0
Naibu waziri wa kilimo, Husein Bashe ameviagiza vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri mikopo inayokopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali ili ilete tija kwa wakulima wanachama badala kuitumia mikopo hiyo kwenye shughuli za uendeshaji wa miradi isiyo na tija kwa wanachama hao.

Bashe alitoa agizo hilo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.

Alibainisha kuwa kwasasa baadhi ya vyama hivyo vinapitia wakati mgumu na kukosa tija kwa wakulima kwa kuwa vimeandamwa na madeni kutoka kwa baadhi ya benki, madeni ambayo kimsingi yametokana na matumizi yasiyo na tija kwa vyama hivyo bila kuwashirikisha wanachama.

“Na hii ndio sababu vyama vya ushirika vimekuwa mzigo kwa wakulima ambao kwa sasa wanalazimika kubeba mzigo wa kulipa madeni ambayo hawajahusika kuyatengeneza. ’’ alisema Bashe ambae pia alitaka vyama hivyo kuanzia mwakani vianze kuwanufaisha wakulima badala ya kuendelea kuwekeza fedha kwenye miradi isiyo na tija.

“Mnajua haiingii akilini kabisa kuona kwamba vyama vya ushirika vinatengeneza mabilioni kupitia makato ya wakulima lakini vinashindwa kuwasaidia pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo hata zile muhimu za kifamilia. Fedha zote zinaenda kulipa madeni ambayo kimsingi yamezalishwa na viongozi wanaoongoza vyama hivi kwa maslahi yao binafsi…naomba hili lifike mwisho sasa.’’ Alisema.

Akizungumzia changamoto ya matumizi mabaya ya mikopo kwenye vyama vya ushirika, Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kuendesha mafunzo kuhusu namna bora ya kutumia mikopo kabla ya kuwapatia walengwa hatua ambayo imesaidia sana kupunguza tatizo hilo.

“Pamoja na mambo mengine lengo la mikopo yetu huwa kuhakikisha tunamsaidia mlengwa kukuza mtaji wake na kufanya shughuli zake kwa ufanisi na ushindani ili atengeneze faida itakayomuwezesha kurejesha fedha kwetu bila changamoto. Hili kufanikisha hili wateja weteja wetu zikiwemo AMCOS wamekuwa wakipata mafunzo ya namna bora ya kuendesha shughuli zao kutoka kwa wataalam tunaoshirikiana nao…hii imesaidia sana!’’ alitaja.

Benki hiyo mbali na kuwa moja ya wadhamini muhimu wa mkutano huo, ilipata fursa ya kuelezea huduma zake mbalimbali kwa wadau hao ikiwemo huduma ya NBC Shambani inayolenga wadau wote wanaojihusisha na biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazaji wa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo.

“Lengo hasa la huduma hii ya NBC Shambani ni kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja,’’ alisema.

“Akaunti ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezesha kuweka fedha bila ada ya uendeshaji wa akaunti huku pia vikundi vikifaidika kwa faida nyingi ikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifa za akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamisha fedha wakati wa kulipa wakulima wenye akaunti NBC,’’ alifafanua.

Wakizungumzia huduma za kifedha, baadhi ya wadau wa kilimo walisema huduma hizo ni muhimu kwa kuwa kwasasa taifa linapitia mageuzi ya kilimo biashara ambacho ustawi wake kwa kiasi kikubwa unategemea uwepo wa huduma bora za kibenki zinaenda sambamba na mahitaji wa wadau hao.

“Huduma kama NBC Shambani zinatugusa wadau wote tukiwemo hata sisi wafanyabiashara wa mazao ya kilimo na usindikaji. Hii ni moja ya mfano wa huduma ambazo wadau wa kilimo tunahitaji haswa!,’’ alisema Bw Shakiru Kyetema, Mkurugenzi wa Kampuni ya Shayakye Trading Company inayojihusisha na uuzaji wa kahawa.
Naibu waziri wa kilimo, Husein Bashe (Aliesimama) akizungumza na washiriki Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa ulifanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Primus Kimaryo (Kushoto walioketi)
Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira (Aliesimama) akizungumza na washiriki Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa kuhusu huduma za benki hiyo kwa wadau hao.Mkutano huo wa siku mbili ulifanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.
Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira (katikati akifuatilia mkutano huo).
Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira (Kushoto) akizungumza na mmoja wa wadau wa zao la kahawa Bw Shakiru Kyetema, Mkurugenzi wa Kampuni ya Shayakye Trading Company wakati wa mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa ulifanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma. Benki hiyo ilikuwa moja ya wadhamini muhimu wa mkutano huo.
Baadhi ya wadau wa zao kahawa nchini wakifuatilia moja ya agenda kuhusu ustawi wa zao hilo wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.

MSISUBIRI DAKTARI AWAANDIKIE MAFANYE MAZOEZI- DKT MGAYA

$
0
0

 

Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakiendelea kufanya mazoezi mbalimbali ya viungo.


Na Avila Kakingo

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimeadhimisha wiki ya utumishi Umma kwa wafanyakazi wake (Bonanza Staff ) kwa kufanya mazoezi ya viuongo ili kutunza Afya zao

Naibu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Dkt. Profesa Prosper Mgaya, ameyasema hayo leo Juni 19, 2021 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzunduzi wa bonanza hilo kwa watumishi wote wa chuo lililofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho eneo la Mabibo Mkoani Dar es Salaam. Amesema kuwa wameona kuadhimisha wiki hiyo kwa vitendo kwa kufanya bonanza la michezo.

"Lengo la bonanza hili la Michezo ni kuwaonesha wafanyakazi wetu kuwa ni mhimu kufanya mazoezi ili kuweka afya yako katika hali nzuri."

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassani Suluhu amelisisitiza sana hili kwamba ni Vizuri na inapendeza watu wakafanya mazoezi. " Amesema

Amesema kuwa kufanya mazoezi ni vizuri zaidi sio mpaka Daktari akuambie au akuandikie kuwa ufanye mazoezi, lakini wafanyakazi wa Chuo Cha Usafirishaji cha NIT wamelitambua hilo na wameanza kuhamasisha kufanya mazoezi.

Amesema kuwa viongozi wa juu wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji wameona wahamasishe wafanyakazi wenzao kufanya mazoezi kwa kila baada ya robo mwaka ili kujiimarisha kimwili, kiakili na kitamaduni wa kufanya mazoezi kila siku.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kufanya mazoezi kwani ni mazuri kwa kila mtu. "Kwahiyo natoa wito kwa watanzania wote kwamba tufanye mazoezi mazoezi ni dawa ya kuweka mwili wako ukiwa katika afya njema na kwa kufanya mazoezi tunaweza kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza na mangonjwa mengine ambayo hayana msingi wa kukupata.

Kwa upande wa Mkufunzi wa Michezo Chuo Cha NIT Agustino Sakwale amesema kuwa michezo ni burudani michezo ni afya kwani watumishi wote wa NIT wameshiriki bonanza la michezo ili kuendelea kulindaa afya zao.

"Ushiriki wa watumishi wa Chuo cha NITutaimarisha afya zao na pia huongeza ati katika utendaji wa majukumu yao." Amesema Sakwale.

Licha ya hao Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Sara Mwakyusa amesema kuwa amefurahishwa na bonaza kwani watumishi wanatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya afya zao.

"Mazoezi haya ni mhimu na mazuri kwani yanawajuisha wote pamoja, tunafurahi pamoja, inatuweka pamoja na tunashirikiana pamoja." Amesema Sara.

Michezo mbalimbali imeshindaniwa katika kuadhimisha bonanza hilo ikiwemo ya Kukimbiza Kuku, kukimbi na yai kwenye kijiko, kukimbia na maguni, mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa wavu na mbio za vikwazo na kutunga uzi kwenye sindano huku ukikimbia. Washindi wa michezo hito walijishindia zawadi kemkem zikiwamo pesa taslimu.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT)wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo ikiwa ni njia moja wapo ya kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma katika chuo hicho.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakikimbia na magunia.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakivuta kamba.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakifanya mzoezi mbalimbali ya viungo.




Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo.

NMB ups its stake in Zanzibar’s tourism as hoteliers unite

$
0
0

 Zanzibar. NMB Bank Plc is upping its stake in Zanzibar tourism in an effort to play an increasingly important role in the growth of the most important economic sector in the Isles’ economy.


Through its involvement with the newly-formed Hotel Association Zanzibar (HAZ), NMB Bank Plc said at the weekend that apart from several tourism-related products that were already on offer in Zanzibar, the lender was also bringing several others in the coming few weeks.

“You shall recall that we launched our E-Commerce Payment Gateway and our UnionPay products right here in Zanzibar. The products are meant to aid transactions associated with tourism. With our partnership with HAZ, we are soon going to do much more, including a special card for tourists,” said the bank’s chief of retail banking, Mr Filbert Mponzi.

He was speaking during an event to officially launch HAZ which was graced by Zanzibar’s Second Vice President, Mr Hemed Suleiman Abdulla.

With its bancassurance products, the bank has entered into partnerships with ten insurance firms, including the Zanzibar Insurance Corporation.

“If taken seriously in Zanzibar, this could offer a lasting solution to such accidents as fire that raze hotels time and again and other risks associated with the tourism sector…Hotels could look up to using bancassurance to mitigate risks associated with damage of properties such as hotels, boats and yacht among others,” he said.

NMB Bank Plc’s ATM machine that has the ability to exchange foreign currency will soon be set up at Amani Karume International Airport Zanzibar.Gracing the event, Mr Hemed Suleiman Abdulla said the coming of HAZ should help to invigorate the tourism industry which had been facing several challenges associated with the Covid-19 pandemic.

“HAZ members should also join hands with the government in preparing a comprehensive recovery plan,” he said.

He said when he inaugurated the House of Representatives in November last year, President Dr Hussein Mwinyi assured investors that his country would leave the doors open for their engagement in creating jobs in line with the government’s Blue Economic model.

HAZ, he said, must work with Zanzibar Association of Tourism Investors (Zati) and Zanzibar Association of Tour Operators in promoting the Isles’ attractions globally.According to the HAZ chairman, Mr Paolo Rosso, last year, Zanzibar received 528,425 tourists who earned the country a total of $426 million in forex earnings.

There were 582 hotels with a total of 9,860 rooms in Zanzibar.

Tourism accounted for 82.1 percent of Foreign Direct Investment (FDI) in Zanzibar, he said, noting that each year, ten new hotels were being built in the Isles, each consuming $30 million in average investment.

“The amount that each tourist spends in Zanzibar has also gone up from an average of $80 per day in 2015 to $206 in 2020,” he said.

HAZ will be the principal voice of all hotels in Zanzibar on issues pertaining to the sectors’ engagement with the government and other agencies.

NMB Bank employees in a group photo with the guest of honor and HAZ Board of Directors.

NMB Bank Chief of Retail Banking receives a certificate of appreciation from Zanzibar’s second vice president, Hon. Hemed Abdulla to recognize the bank’s role towards the development of the tourism sector in the isles.

NMB Bank Chief of Retail Banking, Filbert Mponzi speaks during the launch of Hotel Association of Zanzibar at an event held in the isles over the weekend.

NMB Bank Chief of Retail Banking, Filbert Mponzi welcomes Zanzibar’s Second Vice President, Hon. Hemed Suleiman Abdulla who was the guest of honor at the launch event.


Shule ya sekondari Academic Achievement yafanya mahafali ya kidato Cha sita.

$
0
0

Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi, Salma Kikwete amehimiza wanafunzi kusoma masomo ya sanyansi na hisabati akisema ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
 
Alisema mafanikio katika masomo ya sayansi na hisabati ndiyo yakatayotengeneza nguvu kazi nzuri na madhubuti ya kuleta maendeleo ya uhakika.
 
Mama Salma alieleza hayo jana katika hotuba yake iliyosomwa na mbunge mstaafu, Zakia Meghji  wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya Academic Archievement Open School (AAOS) ya Dar es Salaam. Shule hiyo ya kimataifa inatumia mfumo Cambridge katika utoaji wa elimu yake.
 
Katika mahafali hayo, mke huyo wa rais mstaafu, Jakaya Kikwete, “masomo ya sayansi ndiyo yanayochochea maendeleo na maisha ya watu, ujenzi wa barabara, umeme, kompyuta yote kazi ya uanasayansi,” alisema.
 
Katika hatua nyingine,  alieleza kufurahishwa na namna shule hiyo ilitilia mkazo masomo ya sayansi na hisabati, akiwataka kuendelea kukaza buti katika kufundisha masomo hayo kwa wanafunzi kwa maslahi Taifa.
 
Meghji aliupongeza uongozi wa shule kwa hatua hiyo, akisema ina miaka miwili lakini imeonyesha mafanikio makubwa, huku akiwataka kutombweta katika utekelezaji wa majukumu yao.
 
“Kitu kitakachoweza kuwarudisha nyumba ni endapo ufundishaji na uendeshaji wa  shule hautakuwa mzuri. Lakini kwa taarifa yenu ilivyo na nilivyotembelea shule sitegemei matatizo hayo kujitokeza,” alisema Mama Salma katika hotuba yake ilisomwa na Meghji.
 
Aliwataka viongozi na wafanyakazi wa AAOS kuwa na ushirikiano na mshikamano katika uendeshaji wa shule hiyo, ili kufikia malengo yao na kwamba hakuna jambo litakaloharibika bali mafanikio.
 
Ofisa  Mtendaji  Mkuu wa  AAOS, Rana Ahmed Saada, shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kujiendesha ikiw ni pamoja  kuchelewesha kwa majibu ya kutambuliwa na kituo chao cha mitihani ya Cambridge na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta).
 
“Tumejitahidi kuandika barua ya kuomba kutambuliwa kama kituo cha mtihani cha Cambridge ili vyeti vya wanafunzi wetu vitambuliwe kitaifa wanapoitimu mitihani yao lakini hatujajibiwa hadi sasa. Lengo letu ni kufungua fursa kwa wanafunzi wa kitanzania na mataifa mengine kusoma vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi,” alisema Rana.
 
Alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2019 kama shule huria, lakini wana mpango wa kuanzisha program za ufundishaji kwa wanafunzi QT pamoja na watahiniwa binafsi.

Wanafunzi wa kiume Sekondari ya Academic Achievement wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza mahafali ya kuhitimu kidato cha Sita.

Wanafunzi wa kike Sekondari ya Academic Achievement wakiwa kwenye mahafali ya kuhitimu kidato cha Sita.

Mbunge mstaafu Zakia Meghji akiwa katika mahafali ya shule ya sekondari Academic Achievement akiwa na (kushoto) mkurugenzi wa shule ya Academic Achievement Rana Saada (kulia) ni Mshauri na Msimizi shirika la Maendeleo (WAMA) Johari Kandoro.

Wasanii watia fora uzinduzi wa UMISSETA LEO

$
0
0


Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Chege  Chigunda  akitumbuiza  pamoja na wanafunzi kwenye  uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA leo Juni 21, 2021 kwenye viwanja vya Nangwanda Sijaona  Mjini Mtwara.
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Maua Sama akitumbuiza jukwaani wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

************************

Na John Mapepele, Mtwara

Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, wakiongozwa na Maua Sama na Chegi wamekonga nyoyo za wanamichezo wa UMISSETA na kuleta hamasa kubwa kwa wanamichezo na wadau mbalimbali wa mkoa wa Mtwara walipotumbuiza jukwaani leo Juni 2021 kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Katika ufunguzi wa leo wa UMISSETA vikundi mbalimbali vya kwaya na ngoma vimetumbuiza na kuufanya umati wa watazamaji kupanda jukwaani na kuimba pamoja na wasanii mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza.

Akisoma hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo Profesa Nombo amepongeza ubunifu wa waandaji wa mashindano ya mwaka huu kwa kuwashirikisha wasanii ili kuja kutoa burudani katika kipindi cha mashindano haya na kuonesha vipaji na vipawa walivyopewa na Mwenyezi Mungu.

“Pia ninawashukuru na kuwapongeza wasanii mbalimbali wanaoendelea kusherehesha wakiwemo Maua Sama na Chege. Wanahabari na wasanii hawa wanasaidia kuitangaza michezo hii na wameongeza hamasa kwa jamii kuifuatilia nchi nzima wakiwemo wazazi, walezi wa wanafunzi na Viongozi wa Vyama vya Siasa na viongozi wa Serikali popote walipo”. Aliongeza Profesa Nombo

Profesa Nomba alitumia ufunguzi wa mashindano haya kuwaagiza wadhibiti ubora wa Shule kote nchini kuanzia ngazi ya wilaya, kanda na Makao makuu ya Wizara kufanya tathmini na kutoa ushauri wa kuimarisha ufundishaji wa michezo, elimu kwa michezo na sanaa katika taasisi zote hapa nchini

Amesema katika kipindi hiki Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa shule zinatenga maeneo maalum kwa ajili ya michezo na Sanaa ili kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi.

Amesisistiza kuwa michezo ya UMISSETA na ile ya vyuo vya ualimu (UMISAVUTA) imekuwa ikiibua vipaji vya wanamichezo wengi ambao miongoni mwao wamefanikiwa kung’ara kitaifa na kimataifa ambapo amesema kutokana na hilo Serikali imeamua kurejesha mashindano yaVyuoi vya Ualimu pia kwa kuzingatia agizio la Mkuu alilolitoa mwaka 2019 wakati wa kufungua mashindanio ya UMISSETA na UMITASHUMTA la kutaka mashindano hayo yarejeshwe.

Aidha amesema wachezaji wenye mafanikio duniani ni wale wenye nidhamu viwanjani na nje ya uwanja na kuwataka wanamichezo wote kuwa na nidhamu ili kufika katika kiwango cha juu.

“ Mfano wa wachezaji hao ni Mbwana Samatta, Hashimu Thabiti, Saimoni Msuva, Usain Bolt Lionel Messi, Christian Ronaldo na wengine wengi . ni matarajio ya kila mmoja wetu kuona mkishindana kwa ujuzi na maarifa ya hali ya juu ili kupata washindi mahiri wenye vigezo vya kuweza kushindana kitaifa na kimataifa” alifafanua

Mashindano yameandaliwa na Wizara tatu zinazohusika na Elimu, Michezo na TAMISEMI chini ya Kamati ya Uratibu ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.

Mashindano haya yalitanguliwa na Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa Juni 8, mwaka huu mjini Mtwara na kufungwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekul Juni 18, 2021.Mashindano ya UMISSETA yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 3, mwaka huu.

Rais Samia azungumza kwa njia ya simuna Rais Xi Jinping wa China.

$
0
0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya Simu na Rais wa China Xi Jinping Ofisini kwake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Juni, 2021. PICHA NA IKULU


 

PSSSF, BENKI YA AZANIA WAINGIA MAKUBALIANO KUUZA NYUMBA,VIWANJA KWA MKOPO WA RIBA YA ASILIMIA 10

$
0
0

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF) pamoja na Benki ya Azania wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa mfuko huo na wananchi wengine kukopa kwenye benki hiyo kwa kupata riba nafuu.

Akizungumza leo Juni 21,2021 mkoani Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba amesema taasisi hizo zina dhima ya kuhakikisha wanaendana na azma ya Serikali ya kutekeleza kwa vitendo malengo yaliyomo kwenye dira ya Taifa ya 2025.

Na vipaumbele vya Ilani ya CCM inayohimiza kupatikana kwa huduma bora za afya, elimu , maji,makazi na umeme mijini na vijijini ambapo lengo lake kuu ni kustawisha maisha ya kila mtanzania.

"Ikumbukwe PSSSF kupitia jukumu lake la kisheria la uwekezaji umeendelea kutekeleza miradi ya kuuza nyumba za gharama nafuu pamoja na viwanja vya makazi.Madhumuni ya miradi hii ni kuwezesha wafanyakazi ambao ni wanachama wa mfuko na watanzania kwa ujumla kupata makazi bora na salama.

"Kwa kununua nyumba na viwanja vilivyopima kwa kulipia kwa njia rafiki ikiwemo mikopo ya makazi , aidha mradi wa nyumba za gharama nafuu upo katika Mkoa wa Dar es Salaam , Morogoro, Shinyanga, Tabora ,Mtwara na Iringa.

"Pia mradi wa viwanja vya gharama nafuu upo mikoa ya Ruvuma ,Kagera, Tabora Iringa,Katavi Morogoro ,Dar es Salaam, Kigamboni kule Kimbiji ,Rukwa, Lindi na Mtwara."amesema.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru benki ya Azania akiwemo Mkurugenzi Mtendaji na timu yake kwa kuwa wa kwanza kuonesha utayari wa kushirikiana nao kukubali kutoa mikopo hiyo yenye riba na masharti nafuu.

Ameongeza kwa kufanya hivyo wanatekeleza azma ya Serikali ya kuongeza idadi ya wafaidika wa mikopo kwa ajili ya makazi bila mzigo wa riba kwa kuendelea kushusha viwango vya  riba hadi kufikia kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka ambacho ni kiwango nafuu.

"Miongoni mwa maeneo yaliyoonesha mafanikio katika dira ya uwekezaji ya mwaka 2025 na Ilani ya CCM ni kuendelea kushusha kwa riba iliyokuwepo ya kati ya asilimia 21 hadi asilimia 25 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 13 na 18 mwaka 2020.

PSSSF na Benki ya Azania tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha azma hii inatekelezwa kwa vitendo,kupitia makubaliano haya wananchi watafaidika kwa kukopesha nyumba na viwanja,hivyo kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi walioko maeneo yote nchini ili wawe na makazi bora na kutimiza kauli mbiu ya Serikali nyumba bora kwa wananchi wote inawezekana.

"Makubaliano haya yatamuwezesha mkopaji kulipa mkopo wake taratibu huku akiendelea kutimiza majukumu mengine ya kimaisha.PSSSF na Benki ya Azania tumeenda hatua zaidi kwa kuhakikisha tunawalinda wakopaji dhidi ya majanga kama vile moto , mafuriko, kimbunga na majanga mengine ya kibima wakati wote wa mkopo ili kulinda thamani ya uwekezaji ambao umefanywa,"amefafanua.

Kashimba amesema benki ya Azania imeshaandaa utaratibu wa kibima ili kuwalinda wakopaji dhidi ya majanga hayo na kwamba mteja atakapokamilisha mkopo wake atakabidhiwa hati yake ya nyumba na benki ya Azania.

"Muda wa marejesho ya mkopo huu ni kipindi kisichozidi miaka 15 kwa mkopo wa nyumba na miaka miwili kwa mkopo wa kiwanja .Masharti mengine ya msingi kwa mkopaji ni kuweka asilimia 10 ya thamani ya mkopo au mali yenye thamani hiyo kwa dhamana ya mkopo.

"Kiwango cha juu kabisa ambacho mteja anaweza kukopeshwa ni asilimia 90 ya thamani yote ya nyumba au kiwanja.Aidha taratibu zote na maelekezo ya masharti na vigezo vingine vya mkopo utakavyopatikana vitatolewa kwa wakopaji pindi watakapofika kwenye ofisi za PSSSF na Benki ya Azania,"amesema.

Aidha jumla ya nyumba 192 na viwanja 886 vyenye hati vitakuwa sokoni na vitauzwa kwa njia ya mkopo wenye riba nafuu utakaotolewa kwa wanachama na wananchi wote kwa kutegemea vigezo na masharti mepesi yaliyowekwa.

Amesema utaratibu wa kuviona, na kutoa mikopo utaratibiwa kupitia ushirikiano kati ya PSSSF na benki ya Azania pamoja na benki nyingine zitajitokeza baadae kwa kuzingatia idadi ya nyumba na viwanja.

"Mikoa ambayo nyumba za miradi zipo ni Dar es Salaam eneo la Chanika Buyuni, ambalo lina nyumba 106.Morogoro eneo la Lukobe nyumba moja, Tabora eneo la Usule kuna nyumba 25 ,Mtwara eneo la Mang'amba nyumba sita ,Shinyanga eneo la Ibadakuli nyumba 46, na Iringa eneo la Mawelewele kuna nyumba nane.

"Aidha nyumba ziko za aina nne zenye ukubwa tofauti kuanzia nyumba za vyumba viwili hadi vyumba vinne , bei ya nyumba ni kati ya Sh.milioni 36 hadi Sh.milioni 61 kulinagana na aina na ukubwa wa nyumba husika.

"Bei hizi zimejumuisha kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT .Makubaliano haya na  benki ya Azania ni pamoja na uuzaji wa viwanja kwa njia ya mkopo ambapo vinapatikana mikoa ya Ruvuma viwanja 128.

"Kagera viwanja 192,Tabora kiwanja kimoja ,Iringa viwanja vinne, Katavi viwanja 50, Morogoro kiwanja kimoja ,Singida viwanja 211, Dar es Salaam eneo la Kigamboni kule Kimbiji viwanja 87,Rukwa viwanja 54,Lindi viwanja 70 na Mtwara viwanja 70"amesema.

Amesisitiza viwanja hivyo vina hati na vina ukubwa kati ya mita za mraba 450 hadi mita za mraba 1500 na vinapatikana kwa kati ya Sh.2500 hadi Sh.15000 za mita za mraba.Hata hivyo mfuko huo bado una uhuru wa kuuza kwa muuzaji mwingine.

Pia PSSSF itaendelea kuandaa mipango kama hiyo  ya kuwapatia wanachama wake fursa ya kumiliki makazi yao pindi wakiwa bado kwenye ajira.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania, Bw. Charles Itembe...amesema benki yao inaona faraja kuwa sehemu ya mradi huo mkubwa na kwamba benki hiyo ilikuwa ya kwanza na kinara wa ukopeshaji wa nyumba kwa riba nafuu.

"Kwa hiyo ni jambo ambalo tunauozoefu nalo kwa miaka mingi sana,tulikuwa ni benki ya kwanza kabisa kutoa mikopo ya nyumba toka miaka 2005 na mwaka 2016 wakati benki nyingine zikiwa bado hazijaanza kufanya kazi hiyo.

"Ukiangalia benki hii kwa kiasi kikubwa huduma ya mikopo ya nyumba imechukua asilimia kubwa, hivyo kwetu hili si jambo la kwenda kuiga bali tumeshalifanya na wengi wamefaidika hasa wafanyakazi wa sekta ya umma ukiondoa wa sekta binafsi.

"Na jambo hili kimsingi limetujengea heshima kubwa mtaani, ukisikia watu wengi wana nyumba za kuishi watakwambia ni kwasababu ya benki ya Azania, hivyo watanzania wanaokwenda kuomba mikopo ya nyumba au viwanja, basi benki hiyo iko  tayari kuwahudumia, na mikopo hiyo inatolewa kwa riba ya asilimia 10.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania, Bw. Charles Itembe wakisaini makubaliano yatakayowawezesha wananchama wa PSSSF na wananchi wengine kukopa fedha kwenye Benki ya AZANIA kununua nyumba za gharama nafuu na viwanja zilizojengwa na Mfuko sehemu mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania, Bw. Charles Itembe wakibadilishana nyaraka za makubaliano yatakayowawezesha wananchama wa PSSSF na wananchi wengine kukopa fedha kwenye Benki ya AZANIA kununua nyumba za gharama nafuu na viwanja zilizojengwa na Mfuko sehemu mbalimbali nchini.Wanaoshuhudia pichani  kulai ni Mkurugenzi wa Mipango PSSSF Fortunatus Magambo na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Wateja  Binafsi Jackson Lolai 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania, Bw. Charles Itembe wakiwaonesha Waanishi wa Habari (hawapo pichani) nyaraka za makubaliano yatakayowawezesha wananchama wa PSSSF na wananchi wengine kukopa fedha kwenye Benki ya AZANIA kununua nyumba za gharama nafuu na viwanja zilizojengwa na Mfuko sehemu mbalimbali nchini.
Picha ya pamoja



TAARIFA YA KUUZWA KWA SHAMBA

$
0
0

 


Shamba lenye jumla ya Heka 165 ambalo tayari limeishapimwa linauzwa .


Mahali: Shungumbweni, Mkuranga karibu na Kiwanda cha Chumvi Neel Salt


Bei: Shamba hilo linauzwa kwa kila Heka moja ni shilingi 1,500,000/= (Milioni moja na Laki tano)..


Umbali: Kilomita 5 kutoka baharini, Kilomita 26 kutoka barabara kuu ya Dar-Lindi, (Unaweza Ingilia kwa njia ya Kibada-Mwasonga pia).


Shamba lina miti ya mikorosho iliyopandwa kwa heka 20,Mianzi,kisima cha maji safi mita 72, kinatoa lita 20,000 kwa saa.

 

Kwa aliye SERIOUS kununua anakaribishwa sana.


KWA MAWASILIANO ZAIDI  0763000053



 

Viewing all 48994 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>