Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48993 articles
Browse latest View live

BENKI YA BIASHARA YA DCB YAZINDUA MUONEKANO MPYA

$
0
0

  

Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya Biashara ya DCB leo imezindua muonekano wake mpya , ambao  unaenda sambamba na mikakati ya benki hiyo  ya kuboresha huduma zake na kukidhi malengo na maono iliyojiwekea mara baada ya kupewa leseni ya kujiendesha kama benki kamili ya biashara.

 

" Muonekano huu mpya unawiana na mabadiliko na mafanikio yatokeayo kwenye benki hii yanayolenga kuisimika DCB kwenye  njia ya ukuwaji na utowaji wa huduma bora zinazorandana na mabadiliko ya soko la kibenki,'  alisema Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa, kwenye uzinduzi leo jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa 19 wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo Ndalahwa alisema, muonekano huo mpya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango kazi wa DCB wa miaka mitano 2018-2022, unaolenga kuikuza na kuibadilisha benki  ili kwenda sawia na hali ya soko.

 

Akifafanua, Ndalahwa alisema muonekano huo mpya utalenga kuwezesha benki hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi nchi nzima, kutoa huduma bora zaidi za kiubunifu  na zenye gharama nafuu katika mrengo wa kidigitali, kuendelea kuongeza thamani ya uwekezaji ili kukuza mapato ya wanahisa, kuimarisha benki, na kuhakikisha fedha za wateja zipo salama.

 

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa nembo mpya ya DCB ina mistari sambamba miwili inayoakisi dhana ya kuwa DCB ni benki ya biashara inayoongozwa kwa misingi imara na uzoefu na uthibitisho wa mafanikio makubwa toka kuanzishwa kwake, na ina doti jekundu kuashiria safari ya benki hiyo katika kuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kidigitali na kuwafikia wateja wengi zaidi.

 

" Vilevile, benki pia imebadili rangi kwenda nyekundu na bluu ikiwakilisha uwezo na nguvu ya kutoa huduma, uzoefu katika soko, utulivu tunapohudumia wateja wetu, uimara wa misingi tuliojiwekea, uaminifu kwa wateja wetu na shauku ya kutoa huduma bora kwa wateja wetu,' alisema Ndalahwa.

 

" Muonekano huo mpya wa DCB utaonekana  kwenye vituo vyetu vyote vya kutolea huduma, matawi, ATM, mawakala, huduma za mtandao wa simu (DCB Digital), mitandao ya kijamii, tovuti na sehemu nyingine zote."

 

Benki ya Biashara ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 kuitikia kilio cha wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam cha kukosa chanzo cha mitaji midogo ya biashara, hali  iliyokuwa changamoto kubwa kwa wajasiriamali wadogo katika jitihada za kuboresha maisha yao, hasa kwa kuzingatia masharti magumu ambayo  yalikuwa yanawekwa na benki nyingi za kibiashara.

 

 " Kwa kipindi chote cha miaka 19 ya uendeshaji, jukumu mama la benki hii limeendelea kuwa ni kutoa huduma bora za kifedha huku ikijikita zaidi katika kutengeneza miradi endelevu ya kupunguza umaskini na kuendeleza jamii.Benki imeendelea kushindana kwenye soko kwa kuhakikisha inatoa huduma bora na bidhaa zenye ubunifu kwa wateja wake," a lisema Ndalahwa.  

 

Alitaja mafanikio makubwa kuwa ni, kuboresha leseni  na kupanda hadhi kutoka benki ya mkoa hadi kuwa benki kamili ya biashara, kuwa  benki ya kwanza kujiunga na Soko la Hisa la Dar es salaam, kulipa gawio mfululizo  tangia kuanzishwa kwake, kutoa huduma na bidhaa zinazokidhi viwango vya ushindani, na kufungua matawi 8 na vituo vya kutolea huduma 12

 

Pamoja na hayo, alisema DCB imekuwa ikitoa huduma bora kwa wateja mbalimbali wadogo, wa kati na wakubwa, ambao hadi sasa benki ina wateja zaidi ya 200,000; imeweza kufikia mizania inayokaribia billioni 200; ina huduma za simu ya mkononi (DCB DIGITAL); ina huduma za internet banking na Visa, na ATM  zinazounganishwa  kwenye huduma za Umoja Switch zinazopatikana kwenye ATM 300 nchi nzima.

 

Ndalahwa alibainisha azma ya dhati ya Benki ya Biashara ya DCB ya kuendelea kubuni huduma bora kwa lengo la kupanua wigo wa  upatikanaji wa huduma za benki hiyo nchini kote.

 

" Tumeimarisha huduma zetu, na sasa mteja anaweza kupata huduma za kibenki popote alipo kupitia DCB Digital, huduma za kibenki kwa njia ya intaneti na simu za mkononi, mawakala nchi nzima na matawi yetu ili kuondoa usumbufu  wa wateja wetu kuja matawini. Tunawaahidi kuendelea kuwa wabunifu na kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wetu kulingana na matakwa na matarajio yao," alisema."

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wanahisa wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa benki hiyo uliofanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wanahisa wa DCB jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa nne kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Maharage Chande (kushoto kwake), pamoja na wakurugenzi wa benki hiyo, wakishangilia wakati wa uzinduzi rasmi  wa muonekano mpya wa benki hiyo uliofanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wanahisa wa DCB jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya wakurugenzi wa DCB pamoja na waalikwa wengine wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mtandaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa wakati wa uzinduzi rasmi  wa muonekano mpya wa benki hiyo uliofanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wanahisa wa DCB jijini Dar es Salaam leo.


SPIKA NDUGAI ASHIRIKI SEMINA KUHUSU UFANISI WA RANCHI ZA TAIFA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza wakati wa Semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu majukumu, muundo, mafanikio, changamoto na mikakati ya kutatua changamoto zinazoikabili Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) iliyofanyika bungeni jijini Dodoma. Wa pili kutoka kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa Semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu majukumu, muundo, mafanikio, changamoto na mikakati ya kutatua changamoto zinazoikabili Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) iliyofanyika bungeni jijini Dodoma



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Dkt. Christine Ishengoma,akizungumza na wajumbe pamoja na washiriki wakati wa Semina ya Kamati hiyo kuhusu majukumu, muundo, mafanikio, changamoto na mikakati ya kutatua changamoto zinazoikabili Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) iliyofanyika bungeni jijini Dodoma



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Viongozi na Wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) wakati wa semina iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Kunti Majala,akiuliza swali baada ya kumalizika kwa uwasilishaji wa taarifa kuhusu Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) wakati wa semina iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa (CCM) Dkt.Bashiru Ally akichagia mada mara baada ya kumalizika kwa uwasilishaji wa taarifa kuhusu Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) wakati wa semina iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM) Prof.Patrick Ndakidemi akichagia mada mara baada ya kumalizika kwa uwasilishaji wa taarifa kuhusu Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) wakati wa semina iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………….

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imepewa semina kuhusu Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kwa malengo ya kujua majukumu yake, muundo wake, utekelezaji wa bajeti, mafanikio, changamoto na mikakati ya kutatua changamoto hizo.

Kamati imepatiwa semina hiyo bungeni jijini Dodoma katika ukumbi wa Msekwa D ambapo viongozi wa Wizara waliongozwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.

Akizungumza kuhusu semina hiyo Mhe. Ulega amesema kuwa wizara imeona ni wakati muafaka kufanya semina kuhusu NARCO ili wajumbe wa kamati hiyo waweze kuielewa na kutoa maoni yao ambayo yatasaidia sana katika kuhakikisha kampuni hiyo inaendelea kuimarika kwa kuongeza uzalishaji wa mitamba, nyama na kuzidi kuchangia kwenye pato la taifa.

Mhe. Ulega amesema kuwa Kampuni hiyo ya Ranchi za Taifa ilipita katika kipindi kigumu na hivyo kushindwa kujiendesha lakini kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na wizara kwa sasa Kampuni hiyo inajiendesha yenyewe.

Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye Kamati hiyo, imeainisha mafanikio yaliyopatikana, mipango iliyopo ya kuongeza uzalishaji na maeneo ya vipaumbele yaliyopo katika bajeti ya mwaka 2020/2021. Maeneo hayo ni Kuboresha Ranchi tano (5) za Kongwa, Ruvu, Kalambo, Missenyi na West Kilimanjaro ili kuongeza tija katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Mifugo, Kuongeza uzalishaji wa ng’ombe kwa njia ya Uhimilishaji (AI) – kwa kutumia mbegu bora za ng’ombe wa nyama kama vile Boran na Simental.

Maeneo mengine ni Kudhibiti vifo vya mifugo kwa kiwango kisichozidi 2% ya wastani wa mifugo, Kuongeza na kuboresha nyanda za malisho kwa kudhibiti na kuondoa vichaka na kuimarisha vyanzo vya maji na Kuweka alama za kuonekana katika mipaka ya ranchi, kuondoa wavamizi na kuimarisha ulinzi wa mipaka.

Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Dkt. Christina Ishengoma amesema sasa ni wakati muafaka kwa Ranchi za Taifa kuanza kuzalisha malisho kwa ajili ya mifugo ambayo yataweza kuwasaidia hata wafugaji wanaozizunguka ranchi hizo. Vilevile ameshauri ranchi hizo ziweze kutumika kama mashamba darasa ambapo wafugaji hasa wa maeneo ya jirani wataweza kupata elimu juu ya ufugaji bora.

Akichangia baada ya taarifa kuwasilishwa mjumbe wa kamati hiyo, Mhe. Prof. Patrick Ndakidemi amesema kuwa ni wakati muafaka kwa kamati kuisaidia NARCO.

Prof. Ndakidemi amesema kwa kuwa tayari kampuni hiyo imeshaandaa andiko mradi, ni vema wajumbe hao wakalisoma hilo andiko na kuona ni maeneo yapi kamati inaweza kuisaidia kampuni hiyo. Vilevile amewasihi NARCO kuendelea kuyatunza na kuyalinda maeneo yao kwani yanawasaidia wafugaji wenye changamoto ya maeneo ya malisho kwa kuwakodishia.

RAIS SAMIA AWASILI JIJINI MWANZA NA KUZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY LIMITED

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Madini Doto Biteko, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mwanza Antony Dialo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi pamoja na viongozi mbalimbali, akivuta utepe kuzindua Kiwanda cha kusafisha Dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery Limited kilichopo Sabasaba mkoani Mwanza leo tarehe 13 Juni, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Madini Doto Biteko, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mwanza Antony Dialo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi pamoja na viongozi mbalimbali, akikata utepe kuzindua Kiwanda cha kusafisha Dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery Limited kilichopo Sabasaba mkoani Mwanza leo tarehe 13 Juni, 2021.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea kiwanda cha kusafisha Dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery Limited kujionea hatua mbalimbali za upokeaji malighafi, usafishaji pamoja na upatikanaji wa Dhahabu iliyosafishwa.PICHA NA IKULU

SHEIKH SHABANI MKANGA ATANGAZWA KUWA KADHI MKOA WA SINGIDA

$
0
0

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro,akizungumza na Waislamu  katika dua ya arobaini ya Sheikh Mohamed Makula iliyofanyika Iguguno wilayani Mkalama mwishoni mwa wiki. 

Sheikh wa Wilaya ya Singida Issa  Simba,akizungumza kwenye dua hiyo.

Dua ikiendelea.
Dua ikiendelea.
Dua ikiendelea.
Dua ikiendelea.
Wakina Mama wakiwa katika Arobaini ya Marehemu Mohamed Makula.

 Wakina Mama wakiwa katika Arobaini ya Marehemu Mohamed Makula.

Dufu likipigwa  katika mkutano huo.

Picha zikipigwa.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akiongoza kuomba dua kwenye arobaini hiyo.
 Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida Sheikh Burhan Mlau  akizungumza katika dua hiyo.

Utambulisho ukifanyika.
Walimu wa dini wakitambulishwa.
Utambulisho ukifanyika.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)  Mkoa wa Singida, Jumanne Nkii, akizungumza katika dua hiyo.
Sheikh wa Kata ya Mungu Maji, Juma Sungi, akizungumza katika dua hiyo.
Sheikh wa Wilaya ya Mkalama,Miraji Miraji, akizungumza katika dua hiyo.
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akisalimiana na Waislamu waliofika kwenye dua hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Singida Mjini, Sheikh Hamisi Kisuke,akizungumza katika dua hiyo.
Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Mkalama, Muadh Musa Ntoga, akizungumza katika dua hiyo.

Dua katika arobaini ya Marehemu Mohamed Makula, ikiendelea.


 Na Dotto Mwaibale, Singida


KAIMU Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amemtangaza Sheikh Shabani Mkanga kuwa Kadhi wa mkoa huo kuanzia sasa.

Sheikh Nassoro alitoa tangazo hilo katika dua ya arobaini ya Sheikh Mohamed Makula iliyofanyika Iguguno wilayani Mkalama mwishoni mwa wiki.


" Muda mchache tangu tuanze dua hii ya Mzee wetu Makula Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida Sheikh Burhan Mlau amenipa nakala ya uteuzi wa Sheikh Shabani Mkanga kuwa umekamilika sasa ndio Kadhi nikiwa kama Kaimu Sheikh wa mkoa nimeipokea hiyo nakala na mbele ya shughuli hii namtangaza rasmi kuwa Kadhi wa Mkoa wa Singida na ninakuagiza Katibu wangu  Sheikh Mlau kuanzia sasa ufanye kazi na kadhi huyo mteule," alisema Nassoro.

Alisema kesi zote zilizokwishafunguliwa sasa zielekezwe kwa Sheikh Shabani Mkanga na si vinginevyo na aliyekuwepo kwenye nafasi hiyo sasa ataitwa kadhi mstaafu na hana mamlaka ya kufanya kazi hiyo tena.

Alisema mambo hayo ndio yanayotakiwa kufuatwa na Waislamu kwani mamlaka za juu zimemteua na wao wajibu wao ni kumsikiliza na ku mfuata.

Sheikh Nassoro alitumia nafasi hiyo kuwaomba waislamu wafike mahala waseme migogoro sasa basi kwani wana migogoro mingi ambayo haina tija na kuwa haiwafai.

"Tuna fursa nyingi tunaziacha ambazo wajibu wetu kuzitumia lakini hatuzitumii, wasio na migogoro wanazitumia fursa hizi moja ya fursa ambayo nataka Waislamu wa Mkalama waitumie ni eneo la uwanja lililotangazwa wakati wa mazishi ya Sheikh Makula kuwa ufanyiwe kazi na kwa kuwa viongozi wote mpo hapa natoa agizo kuwa uwanja huo ujengwe chuo au Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ikiwa namna ya kumuenzi marehemu na ipewe jina lake," alisema Nassoro.

Alisema wamuenzi mzee huyo kwa kuweka alama na watu waanze ujenzi kwa kutumia fursa ya ujenzi huo kama wanavyotumia wenzao wa kristo misamaha ya kodi ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi ambayo waislamu hawaitumii hasa wanapo jenga misikiti na madrasa zao wampelekee Katibu wa Bakwata barua za maombi hayo badala ya kumpelekea barua za majungu na vitina ambazo zimejaa ofisini kwa katibu huyo.

Aidha Sheikh Nassoro aliwataka waislamu wa Msikiti wa Mariam Iguguno aliokuwa akiongoza Sheikh Mohamed Makula kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba na mchakato wa kumpata Sheikh mwingine na pindi atakapopatika atakaye teuliwa na mamlaka husika wampe ushirikiano.

UMOJA WA WATENGENEZA MAGARI DUNIANI WATEMBELEA KIWANDA CHA GFA WILAYANI KIBAHA,WAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV


KIWANDA cha Magari cha GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimepata ugeni mkubwa baada ya kutembelewa na wanachama wa Umoja wa Watengenezaji Magari Duniani(AAAM).

Wakiwa kwenye kiwanda hicho wanachama wa umoja huo wamepata fursa ya kuzungunza na kubadilishana mawazo na viongozi wa kiwanda cha GFA ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia pia kuimarisha uhusiano.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema kwamba Kiongozi wa Msafara wa AAAM ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Nissan ukanda wa Afrika Mike Whitfield  amesema watashirikiana na kiwanda hicho cha GFA katika nyanga mbali mbali na kuweza kujitegemea na suala la uunganishwaji wa magari na Tanzania inakuwa  kama nchi zingine zinazotengeneza magari kama ilivyokuwa nchi ya Afrika Kusini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa  wa kampuni ya GFA Assemblers ,Mehbooub Karmali ameushukuru ujio huo wa msafara wa viongozi hao na kusisitiza ujio wao ni neema kwao na mambo yakienda  vizuri basi Serikali itakuwa inapata fedha za kigeni kutokana na magari kutengenezwa nchini hali itakayoongeza soko la ajira kwa vijana wengi wanao hitimu katika vyuo vyetu.

Wakati huo huo wanachama hao wakiwa nchini Tanzania wamekutana  na viongozi wa Serikali na kuzungumza mambo kadha katika kuhakikisha lengo la Tanzania ya Viwanda linatimia kwa vitendo

Miongoni mwa wanachama wa umoja huo ambao wametembelea kiwanda hicho na kufanya mazungumzo na Serikali wanatoka katika kampuni za Nisani,Ford, BMW, Isusu, Toyota na Volkswagen.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa GFA Assemblers, Mehbooub Karmali (kulia) akimtembeza moja ya wageni katika kiwanda hicho Kibaha mkoni Pwani
-Mshauri mkuu wa Waziri wa viwanda nchini Afrika ya kusini, Alec Erwin  akizungumza jambo wakati wa ujumbe wa Umoja wa Watengenezaji wa magari Dunia(Association of African Automobile Segment (AAAM) walipotembelea kiwanda cha kuunganisha magari nchini kilichopo Kibaha mkoni Pwani .Kati kati ni Mwenyekiti wa bodi ya GFA Assemblers, Mehbooub Karmal  na kulia ni Mwenyekiti wa umoja wa watoa huduma za mafuta na gesi nchini (ATOGS), Abdulsamad Abdulrahim.
Jopo la viongozi wa  Umoja wa Watengenezaji wa magari Dunia(Association of African Automobile Segment (AAAM) wakiangalia moja ya gari inavyotengenezwa katika kiwanda hicho

Absa Bank Tanzania injects TZS 15m bankroll war against Covid 19 pandemic

$
0
0
Absa Bank Tanzania has last weekend in Dar es Salaam, donated TZS 15m to EngenderHealth in support of procuring Personal Protective Equipment (PPE) to boost the on-going fight against the Covid 19 pandemic.

Speaking about the donation, the bank’s Head of Marketing and Corporate Relations, Mr. Aron Luhanga, said, “We realize that this has been the most difficult time for most of our communities and businesses whose financial means are being negatively affected. As such, being responsible financial partners, we are happy to support our communities through Engender Health in order to continue bringing their possibilities to life despite the present challenges.”

Receiving the financial support, EngenderHealth Country Representative, Prudence Masako, said the NGO had been working in Tanzania for over 30 years, in partnership with the government and private sector to strengthen capacity of the health system to provide Reproductive Health services, providing technical and logistic assistance.

Said Masako:” Today, EngenderHealth is proud to partner with Absa to support PPE distribution to some of our supported health facilities in Dar es Salaam as part of Covid 19 response measures. Engenderhealth have worked with local government authorities to support our frontline workers to have the necessary equipment to ensure services are not interrupted. We will continue to support government in this area and work with other partners to mobilize resources for PPE procurement as part of Covid -19 response.”

The EngenderHealth representative added: “This is not the end of this partnership; I believe our two organizations will continue to work together in investing in health care and enable our front-line workers to continue to provide quality services even during this challenging time.”

The bank’s Acting Corporate Director, Ms. Nellyana Mmanyi said: “Our passion for our communities is as strong as ever and our commitment to serve and protect them is unwavering. Therefore, we continue to invest in our customers’ wellbeing as we adhere with the guidelines and protocols set out by the Ministry of Health in the wake of Covid 19 pandemic. EngenderHealth being our client we keep on investing in our business relationship while ensuring we play a role in the society we serve”.

Ms Mmanyi added that Absa, ‘ maintained strong relationship with organizations such as EngenderHealth with purpose of bringing change to the community and providing support to the ongoing efforts of the government plays in developing the country at all levels.’

Summing up the bank’s social investment endevour, Mr. Luhanga noted: “Absa is a key role player in advancing several sectors in the country some of them being education, entrepreneurship, financial literacy, environment and social wellbeing. The bank ensures that every society investment is aligned with strengthening our relationship with the community, the organization we work with and the government.”

 

Absa Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (right) hands over a dummy check for Tsh 15m to EngenderHealth Country Representative, Prudence Masako, donated by Absa to the charity  for procurement of personal protective gear to shore up the fight against Covid 19 plague. The occasion was held in Dar es Salaam recently. Looking on is Absa’s Acting Corporate Affairs Director, Nellyana Mmanyi.
EngenderHealth Country Representative, Prudence Masako (left), gives a vote of thanks after receiving a donation of Tsh 15m from Absa Bank Tanzania to finance purchase of personal protective equipment to buttress the fight against Covid 19. The hand-over was held in Dar es Salaam recently. The grant was handed by ABT Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (second left).

 Absa Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (second left), addresses the press during the bank’s  donation of Tsh 15m to EngenderHealth  for acquisition of protective kits to shield frontline workers in the fight against  covid-19. The brief occasion was held in Dar es Salaam recently. Left is EngenderHealth Country Representative, Prudence Masako.

 

Absa Bank Tanzania  Head of Global Markets Sales,  Irene Rwegalulira (right), talks to  attendees during the hand-over ceremony of some Tsh 15m granted by the bank to EngenderHealth to help the charity purchase protective gear destined for front-line workers  in fight against the covid-19 scourge. The brief occasion was held in Dar es Salaam recently.

EngenderHealth  Senior Manager, Programs and Partnership EngenderHealth Yisambi Mwanshemile (right), talks to journalists and invited guests during the hand-over ceremony for Tsh 15 million the bank granted the charity for procurement of personal protective equipment intended for frontline workers in the fight against Covid-19 outbreak. The brief occasion was held in Dar es Salaam recently.

VIONGOZI WA DINI WAMSHUKURU MUNGU KUIFANYA TANZANIA KWA MARA YA KWANZA KUWA NA RAIS MWANAMKE, NCHI KUWA SALAMA

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

VIONGOZI wa dini nchini wamekutana kwa ajili ya kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu mustakali wa Taifa la Tanzania huku wakitumia nafasi hiyo kumshukuru Mungu neema yake ya kuifanya nchi kwa mara ya kwanza kuwa na Rais mwanamke.

Aidha wamesema wanamshukuru Mungu kwa jinsi ambavyo Katiba ya Tanzania imetekelezwa bila kuwepo na uvunjifu wa amani baada ya aliyekuwa Rais Dk.John Magufuli kufariki dunia akiwa madarakani na hivyo ikalazimika Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kushika nchi kwa amani na utulivu mkubwa, kitu ambacho kwa nchi nyingine kisingewezekana.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Askofu Nelson Kisare ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu ,Kanisa la Mennonite Tanzania amesema pamoja na mambo mengine ambayo wameyajadili kwenye kikao hicho, kuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kufanya mambo makubwa mawili ndani ya nchi yetu na Watanzania wamebakia salama.

"Katika siku za karibuni, ni mara ya kwanza katika Taifa letu Katiba yetu imeonesha kama inafanya kazi au haifanyi kazi.Rais wetu alitwalia na Mungu akiwa madarakani, tumeona Katiba yetu imefanya kazi, tumetoka kwenye utawala mmoja kwenda mwingine kwa amani na utulivu.

"Tunayo kila sababu kumshukuru Mungu na kuliombea Taifa na viongozi kwa yale ambayo yametokea, katika nchi nyingine za wenzetu ikitokea kitu kama kilichotokea kwetu, Rais aliyekuwa madarakani ametwaliwa na Bwana inaweza kutoa vurugu lakini kwetu Tanzania hakuna vurugu iliyotokea.

"Hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu na sisi mahusiano yetu na Mungu ni ya kila siku , kila wakati na muda wote.Pia ni jambo la kumshukuru Mungu kwani ni kwa mara ya Kwanza kuwa na Rais mwanamke jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye nchi yetu,"amesema Askofu Kisare

Ameongeza ndio sababu ya wao viongozi wa dini wamekutana na kufanya dua na sala kwa ajili ya kushukuru kwa mambo makubwa mawili ambayo yametokea kwenye nchi yetu.

Akizungumza sababu za kukutana kwa viongozi hao wa dini na kufanya kikao hicho, Mwenyekiti wa kikao hicho, Sheikh Mkuu wa Tanzania Aboubakari Zubeir amesema wamekuwa na kawaida ya kukutana na kujadiliana mambo yanayohusu dini zao , waumini wao na mustakali wa nchi kwa ujumla.

"Viongozi wa dini tunakawaida ya kukutana kuzungumza masuala yanayohusu dini zetu, kama vile kujenga mahusiano mema,kuzungumzia amani ,kujenga maadili kwenye jamii na wakati mwingine kutoa muelekeo wa waumini wetu katika mambo yanayohusu waumini wetu na Taifa letu.

"Wakati mwingine tunazungumza mambo yenye mahusiano kama wana dini lakini na Serikali vile vile , kwasababu dini ni kitu kikubwa , kimechukua jamii kubwa sana na karibu watu woote atakuwepo mmoja kwenye upande mmojawapo wa dini , kwa hiyo tabia hii ya kukutana mara kwa mara haikuanza sasa imeanza miaka mingi huko nyuma.

Wakati huo huo Askofu Alex Malasusa amesema wanashukuru ushirikiano uliopo kwenye dini na madhehebu mbalimbali katika Taifa hili."Ushirikiano huu umekuwa ukituletea sifa sio tu kwa Bara letu la Afrika, bali duniani, kwamba viongozi wa dini wanaweza kukaa pamoja.

"Ni jukumu la vyombo vya habari kusaidia kueleza kuwa watu wanaweza kuwa na dini tofauti, madhehebu tofauti na bado wakakaa pamoja, kwababu yako mambo yanatuunganisha moja kwa moja.

"Unapozungumzia suala la amani , sisi sote tunatamani kuwa na amani kama watanzania, sisi sote tunalo jukumu la kuhakikisha tunakuwa na amani, tunapozungumzia uchumi wote tunahitaji kuwa na uchumi ili kila mtu aweze kuona hii ni nchi nzuri.

"Kila mtu apate chakula cha kila siku, tunajua tuna dini tofauti lakini kuna mambo yale yanayotuunganisha, tunapozungumzia maji tena maji safi na salama, hayahusiani na dini lakini yanatukusanya pamoja , tunapozungumzia afya , miundombinu, vitu kama hivyo lazima tuendelee kuvizungumza.Ni vikao vyetu vya kawaida,"amesema Askofu Malasusa.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Aboubakari Zubeir akizungumza jambo na viongozi wenzake wa Dini wakati wakielekea kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mambo mbalimbali leo mkoani Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Aboubakari Zubeir  akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo mkoani Dar es Salaam
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwasikiliza Viongozi vya Dini walipokuwa wakizungumza mambo mbalimbali leo mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) Askofu Peter Konki (wa pili kushoto) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) akifafanua umuhimu wa kuwalinda viongozi wetu Wastaafu na hata walioko madarakani kwa wale wanaosambaza maneno mabaya kwa viongozi wa Kitaifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii.
Askofu Alex Malasusa akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu unyanyasaji na ukatili kwa Watoto ambao umekuwa ukiendelea kufanyika katika jamii
Askofu Nelson Kisare ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu ,Kanisa la Mennonite Tanzania akifafanua kwa ufupi mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mambo mbalimbali waliyoyajadili kwenye kikao cha pamoja walichokifanya kabla ya kuzungumza na Vyombo vya Habari leo mkoani Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

MECHI ZA EUR0 2020 KUENDELEA WIKI HII

$
0
0

 

*Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!

TiMU nyingi zimerusha karata zao kwenye michezo ya kwanza ya michuano ya EURO 2020, wa kufungwa, amefungwa, wakutoka sare vile vile. Mwezi mzima huu mechi za kibabe kuendelea na ndani ya wiki hii kutakuwa na mechi kubwa zenye odds bomba sana kutoka Meridianbet, bashiri sasa!


Jumanne hii, kutakuwa na mechi ya kati ya Hungary na Portugal, Hungary wapo kwenye kundi la kifo na hawapewi uzito sana, je wataweza kuwashangaza kina Ronaldo? Meridianbet imekuwekea odds ya 1.53 kwa Portugal kwa ajili yako. 


Jumanne hiyo hiyo, kutakuwa na mechi kubwa kuliko, France iliyo na mastaa kibao watakuwa wenyeji dhidi ya Ujerumani yenye mastaa vilevile. Meridianbet imekuwekea odds ya 2.65 kwa France. Nani atashinda mechi hii? Bashiri sasa!


Jumatano hii, baada ya kupigwa 3-0 na Belgium mechi ya kwanza, Russia watakuwa kibaruani kucheza na Finland ambao walishinda mechi ya kwanza, Meridianbet wameweka odds ya 1.75 kwa Russia ili uwe Tajiri. 


Usiku huo huo wa Jumatano, Italy watakuwa kibaruani dhidi ya Switzerland kutafuta ushindi wa pili. Italy wamewekewa Odds ya 1.62 na Meridianbet kwa ajili yako! 


Alhamis nako kuna makubwa, Belgium watakuwa ugenini kucheza na Denmark, Denmark watafanikiwa kushinda au watawaacha Belgium waendelee ubabe wa kundi? Belgium wamewekewa Odds ya 2.10 ili kukufaidisha!


Ni rahisi sana kuwa bingwa wikiendi hii, cha kufanya nikuchangamkia fursa tu. Piga *149*10# kujiunga au tembelea www.meridianbet.co.tz na ujiunge na familia ya mabingwa!


Article 1

WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO KUFANIKISHA KILIMO CHA ALIZETI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mabanda ya wadau wa Wakala za Mbegu na Makampuni yaliyopo kwenye mnyororo wa uzalishaji kwenye kilimo cha zao la alizeti, alipozindua kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha kilimo cha zao hilo mkoani hapa juzi kwa kuanza na mikoa ya Singida, Dodoma na Simiyu. 

Na Godwin Myovela, Singida

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza sehemu zote zinazolima zao la alizeti ikiwemo mikoa ya Singida, Dodoma na Simiyu kutumia asilimia 10 ya mikopo inayotengwa kwa makundi ya vijana, wanawake na wenye ulemavu kwa kuwapatia mitaji ya mbegu za zao hilo badala ya fedha ili kupanua wigo wa uzalishaji wake, sanjari na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja kupitia kilimo.

Waziri Mkuu aliyasema hayo juzi mkoani hapa wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha kilimo cha alizeti alipokutana na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani ya zao hilo kutoka mikoa ya Singida, Dodoma na Simiyu.  

"Toeni mitaji ya mbegu kwa makundi haya badala ya fedha. Mana hata wengine mnaowapatia mikopo ya fedha hizo hawarudishi, wapeni mbegu na wasimamieni hii italeta tija kubwa," alisema.

Waziri Mkuu aliweka bayana faida kubwa ambayo mkulima atanufaika nayo endapo atajikita kwenye kilimo cha alizeti, kuwa pamoja na mambo mengine, mkulima atakayelima ekari moja atatumia wastani wa shilingi 250,000 lakini atakwenda kupata takribani shilingi 1,350,000.

"Mathalani ukilima zao hili Kwa ekari moja utatumia mbegu kilo 2 kwa gharama ya elfu 70, utavuna magunia 15 ya takribani kilo 65 na kwa kila gunia utapata lita 18 za mafuta, na kila Lita Kwa bei ya soko ni shilingi 5000...kwaiyo unakuta unakwenda kupata takribani 1,350,000 ukitoa 250,000 za maandalizi ya shamba hadi kuvuna unajikuta na faida kubwa," Alisema Waziri Mkuu.

Alihamasisha wakulima kuchangamkia fursa hiyo ili kuinua hali ya vipato vyao lakini pia kutumia zao kama suluhisho la kukabiliana na uhaba wa mafuta ya kula nchini ambapo takribani tani 400,000 hulazimika kuagizwa nje ya nchi ili kutosheleza mahitaji.

Alisema uwezo wa nchi kwa sasa ni kuzalisha tani 290,000 pekee huku akisisitiza kiasi hicho ni sawa na asilimia 45 ya jumla ya tani zipatazo 650,000 zinazohitajika nchini.

"Nchi huagiza tani zipatazo 400,000 kufidia upungufu wa mafuta ya kula kwa gharama ya shilingi bilioni 474 kila mwaka kwa takwimu za sasa," Alisema Waziri Mkuu.

Alisema mkakati wa Serikali uliopo ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya mafuta yakiwemo alizeti, chikichi, pamba, karanga na ufuta ili kujitosheleza na kuondokana ya adha ya uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje.

Kuhusu mkakati uliopo wa kuinua tija ya kilimo cha alizeti, pamoja na mambo mengine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa kuandaa mpango mkakati ikiwemo kutenga maeneo mahususi kwa ajili ya kilimo cha zao hilo.

Aidha, aliwaagiza wakuu hao wa Mikoa kuhakikisha kila Taasisi na mashule wanaweka mara moja utaratibu wa  kuanza kuzalisha alizeti, jambo ambalo anaamini litasaidia hata kuwajenga kiujuzi wanafunzi kuweza kutumia mafunzo hayo ili kujitegemea hapo baadaye.

Alisema mkulima, mwekezaji au yeyote kwenye mnyororo wa kilimo hicho anayehitaji kuwekeza kwenye alizeti serikali itamlinda na kumhakikishia kila aina ya ushirikiano.

Hata hivyo, aliwakumbusha Wizara ya Kilimo kuandaa kalenda ya kilimo cha zao hilo na kuisambaza kwa wakulima kabla ya msimu mwingine kuanza sambamba na kuongeza idadi ya maafisa ugani kwenye Vijiji na Kata ili kuongeza tija.

Waziri Mkuu pia aliwaagiza Wakuu wa Wilaya ambazo alizeti inalimwa kuandaa vitalu vya mashamba darasa ya mbegu bora kama mwendelezo wa uzalishaji wake baada ya Utafiti, ili kurahisisha upatikanaji wake.

Suala la mkoa husika kuwa na kanzi data (database) ya wakulima na hali halisi ya kilimo hicho ni miongoni mwa maagizo yaliyopewa mkazo lengo ni kufanya kilimo cha alizeti kuwa tegemeo, na hatimaye kuweza kusambaza uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Agizo lingine ni kuanza kuunda vikundi vya ushirika ili kurahisisha usambazaji elimu ya mbinu bora za kilimo, lakini zaidi kupeleka huduma za kiugani kwa mkulima kwa wakati.

Pia aliwataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kila Afisa Ugani anapimwa Kwa matokeo Kwa kupewa eneo na kulima yeye mwenyewe shamba lake la mfano kulingana na zao la mahali husika, ili wakulima wanaomzunguka waende kujifunza kwake, na endapo shamba hilo litashindwa kutoa matokeo mazuri basi aondolewe kwenye halmashauri husika.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alizitaka Taasisi mbalimbali za Fedha, ikiwemo Benki ya Kilimo kujitambulisha kwa wakulima na kusambaza elimu ya namna ya kunufaika na mikopo ya kilimo suala ambalo wengi hawalifahamu.

Pia aliagiza Wizara ya Kilimo kuanza mkakati wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia alizeti sambamba na Wizara ya Viwanda kwenda mara moja kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wenye viwanda vya ukamuaji mafuta ya zao hilo.

"Tutahakikisha mtandao wote wa wanaojihusisha na kilimo cha alizeti tunausimamia ipasavyo. Na naagiza kila kiongozi au taasisi itakayofanya mkutano wowote kwenye mikoa inayolima zao hili kuwe na ajenda ya kuhamasisha alizeti," alisema Waziri Mkuu na akaongeza;

"Kikao hiki sio mwisho nitarudi tena Kwa tathmini kabla ya msimu kuanza ili kuangalia je tulijipanga kwenye kuhamasisha?, pembejeo zimefika kwa wakati? je tuko tayari kulima?, tumeandaa ekari ngapi kwa kilimo hiki? ili tuone kama tutafikia shabaha yetu," alisema kupitia kampeni hiyo ya Twende Tukalime Alizeti ina Faida.

LIVE : RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIWA KATIKA SIKU YA TATU YA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 3 MKOANI MWANZA

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU 3 MKOANI MWANZA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza, mikoa jirani, pamoja na Wabunge mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku 3 na kuondoka mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi wakati akiondoka mkoani Mwanza leo tarehe 15 Juni, 2021. PICHA NA IKULU










Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma za asili cha mkoa wa Mwanza wakati akielekea kuagana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Mkoa mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku 3 mkoani Mwanza.

TANGAZO MAALUM KUTOKA TCRA

RC KUNENGE AZINDUA MAGARI MAPYA YA HONG YANG KIBAHA MKAONI PWANI

$
0
0

  

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezindua awamu ya  pili ya utengenezaji wa magari aina ya HONG YANG katika kiwanda cha GF Assemblers Kibaha mkoni Pwani

Akizungumza baada ya uzinduzi wa magari hayo, Kunenge alikemea baadhi ya tabia za watendaji wa serikali za kupishana katika ofisi za wawekezaji kwa visingizio mbali mbali mbali

 Ikiwamo kulazimisha kuonana na wamiliki ama kwa visingizio vya kutaka kufanya ukaguzi  hali inayowafanya wawekezaji kuwa na hofu na kujikuta wanashindwa kutimiza majukumu yao

Kunenge alisema Serikali ya mkoa wa Pwani inahakikisha inapata maendeleo kwa kuongeza fursa ya biashara na uwekezaji wenye mazingira rafiki na utawala bora kwa hiyo hataki kusikia ama kuona watendaji wanakua kikwazo katika kufanikisha mpango huo na kwamba hatawavumilia.

" wakati Serikali ikijenga mazingira rafiki na wawekezaji sisi wenyewe mafisa wa Serikali tumekuwa kikwazo ,   Nae Meneja wa kampuni  GF Vehcle Assemblers , Ezra Mereng alisema lengo  lao ni kuunda kila aina ya chapa (brand ) ya magari kwa kuwa teknolojia na mitambo waliyonayo inauwezo wa kuunganisha magari aina zote zenye viwango na vigezo vya kitaifa na kimataifa.

 Mereng alisema kiwanda hicho kilianza kwa kuunda magari chapa aina ya FAW na sasa  wamezindua  chapa ingine  ya Hongyan  na kuwataka wadau na makampuni mengine  ya magari kuacha kuagiza badala yake walete GFA kuundiwa (Assembling) kwa zingatia vigezo vyoote vya kimataifa.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari mpya ya kubebea mizigo aina ya Hong Yang katika kiwanda cha GF  leo mkoani Pwani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge  akipokea zawadi ya kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya GF Assemblers Imrani Karmali wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari jipya ya kubebea mizigo anina ya Hong Yang katika kiwanda hicho leo mkoani Pwani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifurahia jambo na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha GF Assemblers,Imrani Karmali  baada ya  uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari mpya ya kubebea mizigo aina ya  Hong Yan katika kiwanda hicho mkoani Pwani

TAASISI YA WAJIBU YACHAMBUA BAJETI YA SERIKALI, WAPONGEZA UWEPO VYANZO VIPYA UKUSANYAJI MAPATO

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

TAASISI ya Wajibu imesema kwamba imepitia na kuchambua Bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/2022 ambapo kwa sehemu kubwa wameipongeza kwa kuja na vyanzo vipya vya ukusanyaji mapato ikilinganishwa na bajeti za miaka iliyopita.

Akizungumza leo Juni 16,2021, kuhusu uchambuzi wa bajeti ya Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu Ludovick Utouh amesema taasisi hiyo aliianzisha mwaka 2015 ikiwa na malengo ya kujenga uwezo wa wananchi kufahamu mambo yanayowahusu uwajibikaji wa rasilimali za Taifa. 

"Sisi wajibu tunajikita zaidi kwenye uwajibikaji kwenye rasilimali za taifa,niseme ni mara ya kwanza leo WAJIBU imeingia kwenye kuchambua bajeti ya Taifa kwa jicho la uwajibikaji.Tunafahamu Juni 10 mwaka huu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Mwigulu Nchemba aliwasilisha bajeti ya Serikali bungeni.

"Ni bajeti ya mwaka 2021/2022 ni bajeti ya kwanza chini ya mpango wa tatu wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano na ni bajeti ya kwanza pia kwa awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan na bajeti hii na mpango huu inachukua dhima inayosema kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu,"amesema Utouh.

Amefafanua taasisi ya Wajibu imefanya uchambuzi wa bajeti pendekezwa kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na utawala bora, hivyo imekuja na maoni, changamoto na mapendekezo yanayolenga kuboresha ukamilishaji wa bajeti ya taifa ya mwaka 2021/2022.

"Kama  tulivyoona na tulivyosoma , makadirio ya bajeti ya Serikali ya mapato na matumizi yameweka malengo ya jumla kwa kuanza na lengo la kwanza la kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa kuweka mazingira rafiki kwa mlipa kodi.

"Kwa lengo la kuvutia uwekezaji, ukuaji wa biashara ndogondogo na zakati  ili kapunia wigo wa kodi.Pili kuboresha mifumo ya usimamizi na ukusanyaji wa kodi ili kupanua wigo wa kodi.Kwa kweli bajeti hii imekuja na vyanzo vipya vya mapato ya Serikali ambavyo huko nyuma havijakuwepo.

"Zamani mabajeti mengi ya Serikali yakuliwa ni marudio ya yaliyofanyika huko nyuma, lakini safari hii tunaona Serikali imekuja na taratibu za kukusanya mapato kwa kutumia ufumo wa ununuzi wa umeme LUKU, mfumo ambao hakuwepo nyuma.

"Wamekuja kwenye kodi ya laini za simu ambayo ni kitu kipya na vile vile Waziri ametuambia Serikali inaingia kwenye hati fungani za manispaa kama njia ya mapato ya Serikali, tunapaswa kuipongeza Serikali kwa ubunifu huo,"amesema.

Ameongeza pia bajeti inalenga kuimarisha uendeshaji wa mashirika ya umma ili kuendelea kufanya kazi kibiashara, kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.Pia kuboresha kilimo cha umwagiliaji, kuogeza mnyororo wa thamani na masoko ya mazao ya kilimo, kuchochea uvumbuzi na uhuhishaji wa teknolojia kutoka nje.

"Kuchochea uwekezaji kwenye viwanda hasa zinazotumia malighafi zinazotoka hapa nchini, kudhibiti utoroshaji madini na kujenga mitambo ya uchenjuaji madini nchini pamoja na viwanda vya kuongeza thamani kwenye madini yanayozalishwa nchini.

"Ikiwemo jitihada za maksudi za kuwajengea uwezo zaidi wachimbaji wadogo katika ushiriki wao sekta hii, uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya usafirishaji wa nishati , kuboresha utoaji huduma za kijamii hasa katika sekta ya afya,elimu na maji.

"Na kuimarisha ushirikiano wa nchi yetu na nchi jirani,kanda na kimataifa. Haya ndio malengo makuu ya bajeti inayozungumziwa sasa hivi bungeni.Hivyo uchambuzi wa bajeti hii tuliofanya tumeona kuna masuala matano ambayo bajeti imeyataja, ukweli ukienda kwenye ripoti za CAG za miaka ya nyuma zilikuwa ni mapendekezo.

"Kwa ajili ya utekelezaji wa Serikali, nitaeleza mabadiliko ya sheria ya ukaguzi wa umma sura ya 418, kama mtakumbuka mwaka 2013 Serikali ilileta mabadiliko ya sheria ya ukaguzi ya mwaka 2008 ambapo sheria ilitaka CAG anawapasilisha ripoti zake bungeni kama alivyowasilisha Aprili mwaka huu, serikali nayo inatakiwa kwenda sambamba siku hiyo hiyo iwasilishe  majibu,"amesema.

Ameongeza hiyo kitu ilipingwa sana lakini ilipita, hivyo kwa wao watalaamu wa ukaguzi walijua haitekelezeki.Bahati nzuri Serikali imetambua hilo na imekuja na mapendekezo ya kubadilisha yale marekebisho yaliyofanyika mwaka 2013 .

"Pili kuna mabadiliko ya sheria ya mikopo , dhamana na misaada sura ya 134, nayo hii mabadiliko haya yatairusu Serikali kuidhamini kampuni au taasisi yoyote ya umma kukopa kiasi kisichozidi hisa za serikali au taasis husika.

"Ambapo hii inaenda kujibu pendekezo la CAG ambapo amekuwa anahoji mara nyingi kuhusu upungufu wa mitaji kwa mashirika yanayosimamiwa na Serikali .Tatu kuna kumekuwa na kelele kuhusu mikopo ya Serikali kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Ukweli Serikali inakopa hailipi na wakati mwingine hailipi riba , kwa hiyo mara nyingi inapochukua miaka mingi kwa kulipa madeni yale inaathiri utendaji kazi wa mifuko hiyo.Kwa hiyo bajeti hii inatuambia Serikali italipa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kutenga fedha kwenye bajeti na kutumia hatifungani zitakazoiva kwa nyakati tofauti kuanzia miaka miwili hadi miaka 25.

"Hii itasaidia kuyajumuisha madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwenye deni la taifa, mara nyingi madeni hayo yalikuwa hayaingizwi kwenye deni la taita.Utaratibu huo sasa madeni hayo yatakuwa yanaingizwa kwenye deni la taifa, itasaidia mifuko hii kuwa na fedha za kuwekeza na kujiendesha kwa ufanisi zaidi,"amesema.

Aidha amesema jambo la nne katika baheri hiyo ni Serikali kuongeza mapambano zaidi dhidi ya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu wa mali za umma."Kama mnavyojua ile lugha ya ufisadi huko nyuma , pesa kupigwa huko na huko kitu ambacho CAG amekuwa akikizungumza kila wakati.

"Serikali kusema kweli imedhamiria kukaza uzi , na kuweka mazingira magumu zaidi ya upotevu au matumizi mabaya ya fedha na serikali za taifa. Kuna mfano wa mwenendo wa fedha na makusanyo ya serikali yenye viashiria vya rushwa kwa miaka mitatu iliyopita.

"Na tano ni mapato ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) na Wakala wa Meli Tanzania(TASAC) kuanzia mwaka 2021/2022 yatakusanywa na mfumo huo kupitia GPE na kuingizwa kwenye akaunti ya makusanyo zilizopo Benki Kuu.

"Nafikiri hizi zimetokana na maoni ya CAG kwenye ripoti yake ya mwaka 2019 ambapo kuliokana kuna upotevu Sh.bilioni 3.9 kutokana na udanganyifu katika Bandari ya Kigoma na Mwanza ambao ulitokana na udhaifu wa mifumo ya ndani katika usimamizi wa malipo, hivi kwa upande wa CAG ni furaha, tunaona utekelezaji wa mapendekezo yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe tawi la Dar es Salaam Profesa Honest Ngowi amesema bajeti ya mwaka huu kuna aina mpya za ukusanyaji kodi ambazo zinaweza kuwa na mjadala kwa mfano kutoza kupitia umeme ina mjadala wake lakini ni aina tofauti ya kutoza hiyo kodi ukilinganisha na ilivyozoeleka.

"Njia ya kwanza ni kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara , hapo ndipo tunapozungumzia wigo wa kupanua kodi, na hii muhimu kwasababu kodi zote hizi zinatokana na uzalishaji wa bidhaa na huduma usipopanua wigo na uwekezaji zaidi utazikosa.

"Lakini kuboresha mazingira yatakayochochea ulipaji kodi wa hiyari, hiyo muhimu sana.Ulipaji kodi wa kushurutishana ni gharama sana na unaweza kuangukia fedha nyingi kupotea lakini utumiaji wa TEHAMA unarahisisha ukusanyaji wa kodi.

"Siku hizi kuna mfumo wa kulipia kodi zako kiganjani, msingi wake kuna watu wanataka kulipa kodi lakini kwenda kupanga foleni kwenye mabenki inapoteza muda lakini kufanya kiganjani ndio kinazungumziwa hapa,"amesema Prof.Ngowi.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU , Ludovick Utouh akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo mkoani Dar es Salaam kuhusu uchambuzi wa bajeti ya Serikali,ambapo Taasisi ya WAJIBU imesema kuwa imepitia na kuchambua Bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/2022 na kwamba sehemu kubwa wameipongeza kwa kuja na vyanzo vipya vya ukusanyaji mapato ikilinganishwa na bajeti za miaka iliyopita,Pichani kulia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe tawi la Dar es Salaam Profesa Honest Ngowi .

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe tawi la Dar es Salaam Profesa Honest Ngowi akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo mkoani Dar es Salaam,wakati akifafanua kuhusu Bajeti ya Mwaka huu na uwepo wa aina mpya za ukusanyaji kodi tofauti  na ilivyozoeleka hapo awali


DKT. NCHEMBA ATOA UFAFANUZI WA TOZO ALIZOWASILISHA BUNGENI

$
0
0

 


Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha bungeni wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 na kuleta mkanganyiko kwa wananchi ikiwemo makato ya miamala ya simu, kodi ya majengo kwa njia ya Luku na Makato yanayopendekezwa ya mafuta kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokutana na kuzungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini kupitia Jukwaa la Wahariri (TEF), katika kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kodi hizo zimetafsiriwa kinyume na lengo la Serikali, ambapo kwenye kodi ya kuongeza salio mtu akiweka kuanzia Sh. 1000 hadi Sh. 2500, atatozwa shilingi 10, shilingi 2500 hadi 5000 atatozwa Sh. 21, shilingi 50,000 hadi 100,000 atatozwa shilingi 186 na shilingi 100,000 kwenda juu anatozwa shilingi 200 na sio kila siku ni pale anapoweka mud awa maongezi.

“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

Akielezea kuhusu kodi ya miamala ya simu Dkt. Nchemba alisema kuwa kila mwananchi atakaopofanya miamala kwenye simu chini ya shilingi 1000 kodi hiyo haiwahusu, kuanzia shilingi 1000 hadi 2000 atatozwa shilingi 10, shilingi 10,000 hadi 15, 000 atatozwa shilingi 300, shilingi 30,000 na kuendelea atatozwa shilingi 1000 na shilingi milioni tatu na kuendelea watatozwa shilingi 10,000.

Kuhusu Kodi ya Majengo kwa kutumia LUKU alisema kuwa mfumo huo mpya unatumika katika nchi nyingi Duniani na unarahisisha ukusanyaji wa mapato kuliko mfumo ulikuwepo ambao unawafanya watu kutumia muda mwingi kwenye foleni.

Kwa upande wa kodi katika mafuta, alisema ongezeko la kodi hiyo itasaidia kukarabati, kujenga na kufufua barabara ambazo ni muhimu katika usafiri na usafirishaji.

Alisema kutumia barabara mbovu ni gharama kubwa kuliko ongezeko la kodi hiyo kwenye mafuta, akitolea mfano wa vifo vya wakinamama wajawazito wanopokwenda kujifungua kutokana na ubovu wa barabara hizo.

Kwa kuwafuata walipa kodi kwa njia ya kawaida hatuzidi watu laki mbili, kwa kutumia Mita za umeme watu wamezidi milioni tatu kwa hiyo tukaona kwa nini tusitumie utaratibu huu wa digitali ili kuwaondolea watu usumbufu.

Waziri Dkt. Nchemba alisema kuwa fedha zitakazopatikana katika kodi hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika kama mfuko wa Barabara na elimu hivyo kutumika kwa kusudi lililowekwa.

Kwa upande wao wahariri walioshiriki semina hiyo wamempongeza Waziri Dkt. Nchemba pamoja na uongozi wa Wizara kwa kutoa ufafanuzi huo na kuomba kuendelea na utaratibu huo ili kuondoa mikanganyiko kwa wananchi. 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza katika semina ya Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya habari nchini (TEF) iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, jijini Dodoma.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb), akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayumo pichani), kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, jijini Dodoma.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb), na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Deodatus Balile, wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini iliyoandaliwa na Wizara hiyo jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya tozo alizowasilisha bungeni ambazo zimeleta mkanganyiko kwa wananchi ikiwemo kodi za miamala ya simu na kodi ya majengo, jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bw. Deodatus Balile, akitoa neno la shukrani baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuzungumza na washiriki wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, jijini Dodoma.

Mmoja wa washiriki wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Allen Lawa, akiuliza swali baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kutoa ufafanuzi wa tozo zilizoibua mkanganyiko katika hotuba aliyoiwasilisha bungeni, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na baadhi ya washiriki wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , jijini Dodoma

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

 

Benki Ya Exim Yakamilisha Ukarabati Vyoo Vya Shule Zanzibar.

$
0
0

 




Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Sadifa Juma akikagua moja ya chumba cha vyoo vya Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi iliyoko Unguja, Zanzibar baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF) kwa hisani ya Benki ya Exim.Ukarabati huo umegharimu takriban sh. milioni 10. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja Mwandamizi wa benki ya Exim Zanzibar, Mwinyimkuu Ngalima (Kulia) na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF), Asma Mwinyi (Katikati)





Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Sadifa Juma (Kulia) akizungumza na wananchi wakati wa makabidhiano ya vyoo vya Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi iliyoko Unguja, Zanzibar vilivyofanyiwa ukarabati mkubwa na taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF) kwa hisani ya Benki ya Exim. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF), Asma Mwinyi (Kulia kwake), Meneja Mwandamizi wa benki ya Exim Zanzibar, Mwinyimkuu Ngalima (wan ne kushoto) pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo.





Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Sadifa Juma akizungumza na wananchi wakati wa makabidhiano ya vyoo vya Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi iliyoko Unguja, Zanzibar vilivyofanyiwa ukarabati mkubwa na taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF) kwa hisani ya Benki ya Exim.

Nipe Fagio yasisitiza umuhimu wa Mazingira Safi na Salama kwa Mtoto

$
0
0

KATIKA kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, taasisi isiyo ya kiserikali ya Nipe Fagio imesisitiza kuwa ni muhimu serikali, taasisi, makampuni yanayozalisha taka na jamii kwa ujumla kuongeza jitihada katika utunzaji wa mazingira ili kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.

 

Hayo yamezungumzwa na Mratibu Sera wa taasisi ya Nipe Fagio, Bi Veronica Hollela wakati wa tukio maalum lililofanyika katika Shule ya Msingi Bonyokwa la kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 16 mwezi Juni kila mwaka.

 

Bi Veronica amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa mtoto anaishi na anasema katika mazingira Safi na Salama ni lazima jamii, serikali na wadau mbali mbali waupokee mfumo wa Taka Sifuri ambao ni mfumo endelevu na jumuishi wa usimamizi na udhibiti wa Taka ngumu kuanzia kwenye uzalishaji uhifadhi, usafirishaji na utumiaji wa bidhaa.

 

"Ni muhimu jamii ijifunze kutenganisha taka kwa ajili ya kurahisisha uhifadhi na utumiaji wa taka kama rasilimali ikiwemo utengenezaji wa mbolea ya mboji itokanayo na taka ozo na urejelezaji wa taka," alisema Bi. Veronica.

 

Aliongeza kuwa mfumo huu wa Taka Sifuri ni muhimu sana kwa sababu ni mfumo unaotoa fursa ya ajira kwa jamii, na pia ni mfumo unaohakikisha mtaa unakuwa na safi na salama kwa watoto na jamii kwa ujumla. Huu ni mfumo unaomilikiwa na jamii kwa asilimia mia moja wakiwemo watoto ambao ni taifa la leo.

 

Aidha naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Bonyokwa Bw. Shabani Maliyatabu katika tukio hilo alisema kuwa jambo la muhimu ni kuwasisitiza wazazi na walezi kwamba nyumbani pawe chou cha mambo na matendo mema, ugomvi na vurugu nyumbani upelekea kuharibu mienendo na tabia za watoto wengi.

 

“Mzazi au mlezi ukiwa rafiki kwa mtoto na mtoto atakuwa rafiki kwa familia na kuwa na matendo na maadili mazuri,” alisema Bw. Maliyatabu.

 

Bw. Maliyatabu aliishukuru taasisi ya Nipe Fagio kwa kushiriki maadhimisho hayo lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za maendeleo za kata yake ya Bonyokwa hususani katika sekta ya mazingira kwa kuhakikisha Bonyokwa inakuwa safi na salama kwa Watoto na jamii nzima.

Mratibu Sera kutoka taasisi isiyo ya kiserikali Nipe Fagio, Bi Veronica Hollela (Kulia) akizungumza kuitambulisha taasisi wakati sherehe za kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika zilizofanyika katika Shule ya Msingi Bonyokwa katika manispaa ya Ilala.  Katikati ni Mratibu Mawasiliano wa taasisi hiyo Muddy Kimwery na Afisa Uhamasishaji Jamii Abdallah Mikulu (Kushoto).

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bonyokwa uliopo katika Manispaa ya Ilala, Bw. Shabani Maliyatabu akizungumza kuwakaribisha wageni waalikwa wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika zilizofanyika katika Shule ya Msingi Bonyokwa katika manispaa ya Ilala.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Nipe Fagio wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Bonyokwa uliopo katika Manispaa ya Ilala, Bw. Shabani Maliyatabu (wapili kushoto) wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika zilizofanyika katika Shule ya Msingi Bonyokwa katika manispaa ya Ilala.


MZUKO WA PILI NA TATU KUNAKO HATUA YA MAKUNDI KUENDELEA WIKIENDI HII

$
0
0

 

*Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!
BAADA ya kukuru kakara za hapa na pale kwenye mzunguko wa kwanza, Euro 2020 kuendelea wikiendi hii ikiwa ni mzunguko wa pili. Italia, Uholanzi na Ubelgiji wameshafuzu hatua ya 16 bora. Timu zipi zitaungana nao?

Ijumaa hii, Sweden atakutana na Slovakia, mchezo wa kwanza Sweden walitoka sare na Hispania huku Slovakia akimshindilia kipigo Poland. Ushindi ndio kitu cha msingi kwa timu zote mbili. Meridianbet tumekuwekea Odds ya 1.95 kwa Sweden.

Uingereza atakua pale Wembley kuchuana na Scotland, hii inaitwa “All British Fight”. Hizi timu ni ndugu kiutawala na geografia lakini kwenye mashindano ni mahasimu. Pointi 3 muhimu zinaweza kubadilisha muonekano wa Kundi D. Zifuate Odds ya 1.34 kwa Uingereza kwenye mchezo huu.

Jumamosi, macho na masikio ya mashabiki wa Soka yatakuwa pale kwenye Kundi F, ni Ureno vs Ujerumani. Machungu ya Ujerumani kupoteza mchezo wa kwanza, yalipeleka furaha kwa Ureno aliyeshinda mchezo wa kwanza, dakika 90 zitaamua nani afurahie au ahuzunike? Meridianbet tumekupatia Odds ya 2.45 kwa Ujerumani.

Jumapili mchongo utakua kwenye Kundi A. Switzerland vs Uturuki, timu hizi zinashika nafasi ya 3 na 4 kwenye msimamo wa kundi lao. Kuhakikisha nafasi ya kusonga mbele, ushindi ndio kitu pekee kinachohitajika kwa timu zote mbili. Meridianbet tumekusogezea Odds ya 1.80 kwa Switzerland.

Jumatatu tunauanza mzungo wa 3 kwa mtanange wa Russia vs Denmark. Kimahesabu, Denmark wameshayaaga mashindano baada ya kupoteza michezo 2 ya mwanzo kwenye hatua ya makundi. Lakini hawajaondoka kinyonge, bado wanaweza kufanya kitu kwenye mchezo wa 3. Odds ya 1.95 kwa Denmark inaweza kukupa faida kupitia Meridianbet.

Hakika, ukiwa na Meridianbet – huna sababu ya kuwaza sana kuhusu ushindi. Karibu kwenye familia ya Mabingwa!

RAS AAGIZA MADIWANI WA UYUI KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WANAOISHI NJE YA VITUO VYAO

$
0
0

 

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maagizo jana wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui la kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)

Na Tiganya Vicent
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Uyui limeagiza kuwachukulia hatua za kinidhamu Watumishi wote ambao wanaosihi nje ya vituo vyao vya kazi na kuendelea kuisababishia Serikali hasara na kuzorotesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui la kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Alisema tayari kuna orodha ya Watumishi ambao bado wanaishi Tabora mjini badala ya kukaa katika eneo la Isikizya ambayo ni ndio Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Uyui

Makungu alisema kuwa hivi sasa hakuna kisingizio kwa sababu upatikanaji wa huduma zote muhimu kama vile maji ya uhakika, umeme na afya zipo katika Makao Makuu ya Halmashauri hiyo.

Alisema kuendelea kwa Watumishi kuishi Tabora mjini huku wakifanyakazi Uyui ni dharau dhidi ya maagizo ya viongozi wa juu waliyoyatoa katika nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali hapa nchini ya kuzitaka Halmashauri zote ambazo Ofisi zake ziko katika Halmashauri nyingine kuondoka na kwenda kwenye makao makuu yao na watumishi wake.


Makungu alisema kama Madiwani wakishindwa kuwachukulia hatua Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatarajia kuchukua hatua kali.


Aliongeza sanjari na Watendaji wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Uyui na watumishi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya wanatakiwa kuishi maeneo yao ya kazi.

Makungu alisema lengo la kuwataka Watumishi wote katika maeneo yao ni kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu wakitaka huduma kutoka kwa watumishi kwa kisingizio ya kuishi mbali na Ofisi zao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Said Ntahondi alimtaka Mkurugenzi Mtendaji kuorodhesha majina ya watumishi wote ambao hadi hivi wanaishi nje ya Isikizya ili Baraza la Madiwani liweze kuwachukulia hatua za kinidhamu.
Viewing all 48993 articles
Browse latest View live