Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48963 articles
Browse latest View live

Rais Samia amteua Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB kuchakata Haki za Wanawake Kiuchumi

$
0
0

  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, kuwa mmoja wa wanawake watakaoshiriki mchakato wa kujadili na kupatia ufumbuzi Haki za Wanawake Kiuchumi.

 Rais Samia ameyasema hayo  jana , wakati akihutubia Mkutano wa Wanawake uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ulioshirikisha takribani wanawake 10,000, wakiwemo wabunge wanawake, madiwani, wajasiriamali na Mama Lishe, waliowawakilisha wanawake wote nchini.

 Akizungumza katika mkutano huo, Rais Samia alieleza mikakati mbalimbali ya Serikali yake inayolenga kuleta Usawa wa Kijinsia, moja ya eneo ambalo yeye aliposhiriki Mkutano wa Afrika na Ufaransa kwa njia ya video, alilichagua baada ya kupewa heshima ya kuchagua eneo la Kumjenga Mwanamke wa Afrika.

 "Wakati wa Mkutano wa Afrika na Ufaransa, uliofanyika kwa njia ya video, kwenye suala la Usawa wa Kijinsia, nilipewa heshima ya kuchagua eneo moja la Kumjenga Mwanamke ili tulisimamie na tuwe 'championi' wa eneo Hilo.

 "Tanzania tumepewa heshima hiyo na Mimi nikachagua eneo la Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke, kwa kutambua kuwa eneo hilo ni nguzo muhimu sana katika kuleta Usawa wa Kijinsia. 

 "Hivyo basi, naomba wadau tushirikiane katika hilo. Najua kati yetu hapa, nina vijana wazuri kwenye mabenki, wakiongozwa na ndugu yangu wa NMB (Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna). Huyu ni mmoja kati ya Wanawake niliowachagua watakaoshiriki jambo hili, sambamba na wengine walio kwenye Sekta ya Uchumi," alisema Rais Samia.

 Alibainisha kuwa, Zaipuna na wanawake wengine aliowachagua, jukumu lao kuu litakuwa ni kumsaidia Rais kufanya uchambuzi yakinifu na wa kina juu ya hali halisi ilivyo katika suala zima la Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke ndani ya Tanzania na Afrika kwa ujumla wake.

 Aliongeza kuwa, jopo hilo litapaswa kuangalia ni maeneo gani yana mapengo na maeneo gani Serikali za Afrika zingependa zisaidiwe na Ufaransa na mipango yao ni kwenda umbali gani, ambayo watayawasilisha kwa nchi hiyo ya Ulaya ili ione namna ya kuisaidia Afrika kufikia Usawa wa Kijinsia kupitia Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Bi. Ruth Zaipuna akipongezwa baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa mmoja wa wanawake watakaoshiriki mchakato wa kujadili na kupatia ufumbuzi Haki za Wanawake Kiuchumi.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Bi. Ruth Zaipuna akiwa miongoni mwa wanawake zaidi ya 10,000 walioshiriki katika mkutano wa Rais uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jiini Dodoma. 

 Afisa Mtendaji wa Benki ya NMB - Ruth Zaipuna akifurahia pamoja na wenzake mara baada ya kushiriki Mkutano wa Rais jijini Dodoma.


NANDY FESTIVAL SASA NI TTCL NANDY FESTIVAL 2021 WATAKAA TU

$
0
0

 

Msanii wa muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flava), Faustina Charles Mfinanga (Nandy) akisaini Makubaliano ya kudhamini Tamasha la TTCL Nandy Festival 2021 wakati wa hafla iliyofanyika katika Ofisi za Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto (anayesaini) ni Mkurugenzi wa Biashara kutoka TTCL Bw. Vedastus Mwita na wa pilikulia (aliyesimama) ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TTCL Bi Puyo Nzalayaimis.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Faustina Charles Mfinanga alimaarufu Nandy (katikati) akifunua kitambaa kuashiria makubaliano rasmi na Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, kuwa Mdhamini Mkuu wa Tamasha la Nandy Festival 2021.

Baadhi ya maofisa wa TTCL wakiwa katika hafla hiyo ya Msanii wa muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flava), Faustina Charles Mfinanga (Nandy) kukubaliana na Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation kuwa Mdhamini Mkuu wa Tamasha TTCL Nandy Festival 2021.

Msanii wa muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flava), Faustina Charles Mfinanga (Nandy) akikata utepe kuashiria kwamba Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation ni Mdhamini Mkuu wa Tamasha TTCL Nandy Festival 2021 wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo iliyofanyika katika Ofisi za TTCL Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara kutoka TTCL Bw. Vedastus Mwita na kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TTCL Bi Puyo Nzalayaimis.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TTCL Bi. Puyo Nzalayaimis (kushoto) akimwelekeza jambo msanii wa muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flava), Nandy wakati wa hafla ya kusaini Makubaliano ya kudhamini Tamasha la TTCL Nandy Festival 2021 katika Ofisi za Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Msanii wa muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flava), Nandy akitoka katika Ofisi za TTCL Kijitonyama Jijini Dar es Salaam mara baada ya hafla hiyo.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Faustina Charles Mfinanga alimaarufu Nandy (katikati) akipiga picha za kumbukumbu mara baada ya kusaini makubaliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, kuwa Mdhamini Mkuu wa Tamasha la Nandy Festival 2021.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Faustina Charles Mfinanga alimaarufu Nandy akiwa katika hafla ya makubaliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, kuwa Mdhamini Mkuu wa Tamasha la Nandy Festival 2021.

*Ofa Kabambe kutolewa kwa watakao Rudi Nyumbani

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania limesaini Makubaliano na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Faustina Charles Mfinanga alimaarufu Nandy yakuwa Mdhamini Mkuu wa Tamasha la Nandy Festival 2021.

Hafla ya makubaliano hayo ilifanyika katika ofisi za TTCL Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo Uongozi wa EASTWAVE MARKETING ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la hilo waliomba TTCL kushirikiana nao katika kufanikisha tukio hilo kubwa katika Tasnia ya Muziki hapa nchini na Afrika kwa ujumla.

Akizingumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Biashara kutoka TTCL Ndugu Vedastus Mwita alisema baada ya mchakato wa kibiashara kukamilika TTCL Corporation imekuwa Mdhamini Mkuu wa Tamasha la NANDY FESTIVAL 2021 ambapo, kuanzia sasa litaitwa TTCL Nandy Festival 2021- Watakaa tu.

Tamasha hili litafanyika katika Mikoa Kumi (10) ambayo ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Sumbawanga, Kigoma, Shinyanga, Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Zanzibar huku matarajio yakiwa ni kwamba Wananchi wa Mikoa hiyo na visiwa vya Zanzibar watapata burudani ya muziki yenye ubora na kiwango cha Kimataifa.

Katika udhamini huo TTCL inatarajia kufikia wateja wake ambapo katika kunogesha tamasha hilo inatoa ofa kwa Wateja wapya ambao watasajili laini zao katika kipindi chote cha tamasha hilo. Amesema kila Mteja mpya atakuwa na uwezo wa kupiga simu mitandao yote dakika 50, kupata MB 150 na SMS 50 bure kwa siku saba.

“tunapenda kuwakaribisha zaidi wananchi wajitokeze kwa wingi kuchukua laini zetu sambamba na kuingia uwanjani ambapo Tamasha litakapokuwa linafanyika ili kuweza kunufaika na huduma kutoka TTCL ambako ndiko nyumbani “alisema Mwita.

Aliongeza kuwa ili kuongeza radha za Tamasha hili, Mashabiki na wapenzi wa Muziki wa Nandy watakaonunua tiketi kupitia T-PESA watapata punguzo maalum hivyo hawapaswi kubaki nyuma ni vyema wakachangamkia fursa hiyo adhimu ya kumuona Msanii wao mubashara katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine Mwita alimpongeza Nandy kwa uthubutu wake wa kuanzisha Tamasha la kuwapa burudani mashabiki zake na wapenda burudani nchini na kwamba uthubutu huo ni ishara kuwa Wanawake kupitia sekta mbalimbali wanaouwezo mkubwa wa kuleta mageuzi makubwa kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Kwa upande wake Moko Biashara ambaye ni Meneja wa Nandy alisema anaishukuru TTCL kwakukubali kuitika wito wa kumuunga mkono Nandy katika Tamasha lake na kwamba tamasha hilo litakuwa chachu kwa wateja wa TTCL ambapo pamoja na mambo mengine Wananchi wataweza kujisajili na kujipatia laini ya TTCL, watanunua bidhaa na kupata elimu kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika hilo.

Naye Msanii Nandy amesema TTCL kujitoa na kuwa mdhamini mkuu si jambo dogo hivyo analishukuru shirika hilo kwakuona umuhimu wa kutumia Tamasha lake kuwarudisha Watanzania Nyumbani kupitia burudani atakayoitoa katika mikoa iliyoandaliwa.

Nandy aliviambia vyombo vya habari kuwa atahakikisha anafanya kazi kwa weledi mkubwa utakaosaidia TTCL kusajili wateja wengi zaidi wapya, kuuza bidhaa na kutoa elimu kuhusu mawasiliano kwa wananchi katika maeneo aliyopanga kutoa burudani.

“Mimi ni wahakikishie tu kwamba nitafanya kazi kwa uweledi wa hali ya juu na tumeishaonesha mfano katika Mkoa wa Kigoma ambapo si chini ya elfu kumi na nane ya mashabiki na wapenzi wa burudani waliingia katika tamasha letu na kupitia idadi hii tunayo matumaini ya kuwarudisha nyumbani waanze kutumia huduma zinazotolewa na TTCL,” alisema Nandy.

Tamasha hili linalobebwa na kauli mbiu ya TTCL Nandy FESTIVAL 2021, Watakaa tu, limeanza kwa mafanikio makubwa Mkoani Kigoma ambapo limewakutanisha mashabiki wengi na wapenda burudani mkoani humo na kuacha historia kutokana na Wasanii wakubwa nchini ambao wameshiriki katika Tamasha hilo.

Mkoa wa Ruvuma waridhia kupandisha hadhi hifadhi mbili za misitu

$
0
0


MKOA wa Ruvuma umeridhia kupandisha hadhi Hifadhi mbili za misitu kuwa mapori ya akiba (Game Reserve) kwa lengo la kuboresha sekta ya utalii kusini.

Mshauri wa Maliasili na Utalii Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe ameyataja mapori hayo kuwa ni Gesimasowa lenye ukubwa wa kilometa za mraba 764 lililopo Halmashauri ya Madaba wilayani Songea na pori la Litumbandyosi lenye ukubwa wa kilometa za mraba 494 lililopo wilayani Mbinga.

“Mapori yote mawili ni sehemu ya ekolojia ya ushoroba wa Selous-Niassa,hata hivyo hadi sasa bado hifadhi hizo haziajapata Tangazo rasmi la serikali la kuwa ni mapori ya akiba,ingawa mchakato wa kutangaza upo katika hatua za mwisho’’,alisisitiza.

Challe amesema Mkoa wa Ruvuma,una mpango wa kuanzisha mashamba ya wanyapori katika Jumuiya zote tano za uhifadhi,kikiwemo kisiwa cha Lundo ndani ya ziwa Nyasa na katika chuo cha Maliasili cha Likuyusekamaganga wilayani Namtumbo ili wananchi wajifunze na kuanzisha mashamba binafsi ya wanyamapori.

Akizungumzia fursa za utalii zilizopo katika Mkoa wa Ruvuma,amesema Mkoa una fursa za utalii wa kiutamaduni na kiikolojia ambapo amezitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni mapori ya akiba ya Selous,Mwambesi,ziwa Nyasa lenye samaki wa mapambo,visiwa,fukwe za kuvutia na vuvutio vingine lukuki.

Fursa nyingine amezitaja kuwa ni mto Ruvuma wenye maporomoko ya Nakatuta,Tulila na Sunda ambayo yamekuwa yanavutia watalii wengi wa ndani na nje ya nchi.

Challe amezitaja fursa za utalii wa kiutamaduni kuwa ni majengo ya kihistoria yakiwemo makanisa makongwe ya Peramiho,Lituhi na Lundu, makumbusho ya vita ya Majimaji,historia ya machifu wa kiyao,wangoni na historia ya biashara ya utumwa.

Fursa nyingine za utalii wa kiutamaduni amezitaja kuwa ni historia ya wapigania uhuru wa Afrika,jiwe la Mbuji,mapango ya wamatengo na pango la mlima Chandamali ambalo lilikuwa maficho ya Nduna Songea Mbano wakati wa Vita ya Majimaji.

Ili kuhakikisha vivutio vilivyopo vinaleta tija,Challe amesema Mkoa umeendelea kufanya jitihada za kuboresha miundombinu na matangazo katika vyombo vya habari ambayo yatawezesha fursa hizo kufahamika kitaifa na kimataifa.

Ameipongeza serikali kuu kwa kuboresha miundombinu ya barabara na anga hivyo kuvutia watalii na kuufungua Mkoa na ukanda wa kusini katika sekta ya utalii na uwekezaji.

Imeandikwa na Albano Midelo Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma Juni 9,2021

CHAGUA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA ZIKUFAIDISHE KWENYE SLOTI YA TITAN ROULETTE DELUXE

$
0
0

 

*Chagua kete zako, subiri gurudumu likupe ushindi na Titan Roulette Deluxe

*Sloti ya Titan Roulette Deluxe

UNAPENDELEA michezo ya bahati nasibu? Una namba ambazo unaamini ni za bahati kwako? Kama jibu ni ndiyo, basi usichelewe pitia duka la Meridianbet ili ujitengenezee pesa ndefu. Sloti ya Titan Roulette Deluxe kutoka kasino ya Mtaandaoni ya Meridianbet inakupa ushindi wa kutosha ukiwa huku ukipata mziki mzuri ukipigwa!


Titan Roulette Deluxe ni moja ya michezo pendwa kutoka kwa Expanse studios, ambayo inapatikana kasino za Meridianbet pekee! Mchezo huu unakupa fursa ya kipekee ya kushuhudia mzunguko wa roulette ukikamilika, huku ukiona sehemu ambapo mpira utatua. 


Kama wewe ni shabiki mzuri wa Roulette na unavutiwa na michezo hiyo, basi mchezo ni chaguo bora kwa ajili yako. Licha ya muonekano mzuri na muundo rafiki Titan Roulette Deluxe inakupa nafasi ya kuona sehemu za bashiri na majedwali mbalimbali yanayovutia unapotaka kuweka dau lako.


Namna ya Kucheza Sloti ya European Roulette

Ukiingia kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, chagua Titan Roulette Deluxe. Hapo utakuta mchezo wenye namba nyingi na muonekano mzuri uliojawa na rangi maridhawa kabisa. Chakufanya chagua namba unazoamini kete yako ya Roulette itaangukia kisha weka dau lako na ufurahie ushindi mnono. 


Baada ya kuchagua namba zako na kuweka dau, bonyeza kitufe chenye alama ya “play” ili uweze kushuhudia mzunguko unaoweza kukupa ubingwa! Ukiwa unajiamini Zaidi unaweza kuweka mara mbili ya ushindi wako kwa kubonyeza kitufe cha x2. 


Usidanganyike! Titan Roulette Deluxe kutoka Meridianbet inaweza kukufanya milionea! Licha ya hayo yote, utapata sehemu ya “demo” ili kujaribu kabla ya kuweka pesa yako. Ukichagua kete zako za bahati basi kwa hakika utapata ushindi mnono sana!


Jiunge sasa na Meridianbet na ufaidi odds, bonasi na promosheni kabambe!

TASAC KUNUNUA BOTI KUZUIA VITENDO VYA UCHAFUZI WA MAZINGIRA BAHARINI

$
0
0

MENEJA wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali amesema shirika hilo lipo kwenye utaratibu wa manunuzi ya boti ambayo itapita maeneo mbalimbali kuelimisha jamii ikiwa ni mkakati wa kuzuia vitendo vya uchafuzi wa mazingira kwenye bahari. MENEJA wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga hivi karibuni wakati wa maonyesho ya biashara.


Mlali aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kwenye maonyesho ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini hapa ambapo alisema kabla ya mwaka huu kwisha itapatikana ili waweze kushirikiana na taasisi nyengine.

Alisema taasisi ambazo watashirikiana nazo ni zile ambazo zinaangalia maeneo hayo kiusalama wa mazingira na pia kiusalama wa nchi kwa sababu bandari ni mipaka ya kimataifa.

Alisema kwa Tanzania uchafuzi wa mazingira kwenye pwani yao sio mkubwa kama zilivyo nchi nyengine huku akibaini changamoto zinazowakabili ni wananchi kutokufahamu shirika hilo na shughuli wanazofanya kwa sababu bado ni changa hivyo wapo kwenye utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi.

“Elimu hiyo itakuwa ni kuhusu biashara za kimataifa kupitia njia za maji zinazofanyika kwa hivyo tumekuwa tukifanya mikutano mbalimbali ya kuwapa uelewa mkubwa”Alisema

Hata hivyo alisema uingiaji wa meli nchini umeongezeka hasa kwa sababu ya madhara yaliyotokana na COVID 19 kwa nchi nyengine ambazo walikuwa wameweka vizuizi lakini kwa hapa nchini hatukujaweka na hivyo kuruhdu meli kuja kuleta shehena na kubadilisha mabaharia.

“Meli kutoka Dunia nzima zimekuwa zikiingia kwa mfano za mafuta zinazotoka ukanda wa Huba zinaleta mafuta ikiwemo Kuiwati,Saudi Arabia na nchi nyengine nyingi..,Meli za ngano kutoka Ulaya Mashariki na nyengine dunia nzima.”Alisema

Hata hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara wazingatia masuala ya usalama wanapotumia njia za usafiri wa majini na wanapopanda vyombo na wanaposafirisha mizigo huku akiwataka wamiliki wa vyombo wafuate utaratibu.

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AZUNGUMZA NA RAIS NDAYISHIMIYE WA BURUNDI

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, akiagana na Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali ya Burundi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melkior Ndadaye Bujumbura Burundi, alipokuwa akirejea Nchini Baada ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu Gitega Nchini wakati Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.

Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango Ofisini kwake Ikulu Gitega Burundi kwa ajili ya Mazungumzo. Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI ZANZIBAR IKULU LEO

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu wa Dini mbalimbali Zanzibar Askofu Dickson D.Kaganga, walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, Katibu wa Mufti.Sheikh. Khalid Ali Mfaume na Fr.Damas Mfoi wa Kanisha Katoliki Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa Dini mbalimbali Zanziubar wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) waipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo.9-6-2021.

Katibu wa Umoja wa Dini Mbalimbali Zanzibar Askofu Dickson D Kaganga akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kumaliza mazungumzo yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ujumbe huo wa Viongozi wa Dini ukiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh Saleh Omar Kabi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi wa Dini mbalimbali Zanzibar yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
(Picha na Ikulu)

VIONGOZI WANAWAKE WA VYAMA VYA SIASA WATEMBELEA NEC

$
0
0

 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera akizungumza na viongozi wanawake kutoka vyama vya Siasa 14 vyenye usajili wa kudumu, waliotembelea Ofisi za Tume, Njedengwa jijini Dodoma juzi kujionea shughuli zinazofanywa na Tume hiyo. Ujumbe huo uliratibiwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini kewa lengo la kuwajengea ufahamu wadau wake. (Picha na NEC).


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera akifafanua jambo wakati akiwatembeza katika maeneo mbalimbali ya jingo la Tume, viongozi wanawake kutoka vyama vya Siasa 14 vyenye usajili wa kudumu, waliotembelea Ofisi za Tume, Njedengwa jijini Dodoma juzi kujionea shughuli zinazofanywa na Tume hiyo. Ujumbe huo uliratibiwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini kewa lengo la kuwajengea ufahamu wadau wake. (Picha na NEC)



RAIS SAMIA AONGOZA VIONGOZI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZINDAKAYA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY MKOANI DAR ES SALAAM

$
0
0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya mara baada ya Misa ya kumuombea Marehemu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni 2021.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam mara baada ya kutoa Heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya leo tarehe 09 Juni, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.a Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Misa ya kumuombea Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni, 2021.

MCHAMBUZI WA SOKA OSCAR OSCAR ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS TFF

$
0
0

*Ameshauri kwa baadae Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kupiga asilimia 50, Vyombo vya Habari asilimia 25 na Wadau wa Mpira wa miguu asilimia 25.


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV


Mchambuzi wa Soka nchini, Oscar Oscar rasmi ameingia kwenye kinyang’iro cha kuwania urais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) baada ya leo kujitokeza katika Ofisi za Shirikisho hilo kuchukua Fomu ya kuwania Urais huo.

Akiongozana na Wachambuzi wengine, Jeof Leah, Tunu Hassan, Oscar Oscar aliingia kwenye Ofisi za Shirikisho hilo majira ya Saa 7 mchana akiwa na imani, furaha tele kuchukua fomu hiyo ya Uongozi wa juu wa TFF.

Baada ya kuchukua Fomu hiyo, Oscar Oscar amesema amefanya maamuzi hayo ya kuwania Urais wa TFF akiwa na malengo makubwa ya kuongoza Soka la Ulimwenguni lakini akianza na uongozi wa soka la nyumbani Tanzania kama atapata nafasi hiyo.

Oscar amesema anajivunia kuwania urais wa TFF akiwa tayari na uzoefu wa mpira wa Tanzania wakati akifanya kazi na timu ya Azam FC na kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara akiwa na timu hiyo iliyoweka rekodi yake msimu wa 2013-2014 chini ya Kocha Mkuu Joseph Omog.

“Ndoto inaendelea kubaki kuwa ndoto, kuota ndoto kubwa au ndogo, inaendelea kuwa na uzito ule ule, TFF kwangu mimi ni kama mwanzo lengo kuu ni kuongoza Mpira wa Dunia”, amesema Oscar Oscar.

Amesema hatanii kuwania nafasi hiyo kutokana na umuhimu wa nafasi yenyewe katika kuongoza masuala ya Soka la Tanzania, amesema anaamini ana uzoefu wa kutosha katika mpira wa miguu.

“Hakuna Chuo kinachofundisha watu kuwa Rais wa TFF, tumewaona akina Leodgar Tenga, Jamali Malinzi na Wallace Karia wameongoza Soka la Tanzania kwa Uongozi wa miaka minne na matokeo chanya”, ameeleza Oscar.

Hata hivyo, Oscar amesema hana tatizo na Wajumbe katika Shirikisho hilo kuelekea Uchaguzi huo, amesema anaweza kuwa mshauri mzuri wa Mifumo kupitia Shirikisho.

“Kwa mfano mchakato wa kumpata Mchezaji bora wa dunia (FIFA), wadau mbalimbali wanapiga kura kumchagua Mchezaji bora, natamani hata sisi tungeweza kumpata Rais wa TFF kwa kupiga kura Wajumbe wa Mkutano Mkuu, Vyombo vya Habari na hata Wadau wa Soka”, ameeleza.


NEWZ ALERT: Rais Samia amteua Bw. Jaffar Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu

Ongeza kipato chako: Kuwa dereva: masomo, gharama na vitu vya kujua.

$
0
0


Ikiwa unafikiria kuwa dereva wa Bolt, haya ni masomo na taarifa chache kuhusu gharama na vitu unavyohitaji kujua kabla ya kuanza.

Kuna faida nyingi za kuwa dereva wa Bolt. Unaweza kupata pesa wakati unataka, kuwa bosi wako wewe mwenyewe na una hiari maana hakuna ada ya kila mwezi unayohitaji kulipa!

Ikiwa unafikiria kuwa dereva wa Bolt, haya ni masomo na taarifa chache kuhusu gharama na vitu unavyohitaji kujua ili kuhakikisha kuwa unakuwa dereva wa Bolt kwa muda mrefu, wenye mafanikio na furaha!

Masomo ya udereva ili uanze

Kupata shule inayofaa ya udereva itakayokusaidia kujifunza jinsi ya kuendesha gari ni rahisi. Nenda kwenye mtandao na uandike "shule za kuendesha gari zilizo karibu" na utapata orodha ya shule hizo.

Gharama ya masomo ya udereva kwa ujumla ni nafuu sana na thamani ya ustadi utakaoupata ni kama dhahabu, maana itakuongezea ustadi wa juu wa usalama barabarani na fursa za kupokea takrima zaidi kutoka kwa wateja wako wenye furaha.

Tafadhali jua kwamba unahitaji kuwa na leseni halali ya udereva kabla ya kujisajili kama dereva wa Bolt nchini Tanzania.

Jiandikishe na ufanye biashara.

Huku tukifanya bidii kuhakikisha kuwa kila wakati tunapata washirika wanaofaa, kusajiliwa kwa dereva wa Bolt ni mchakato rahisi, ulioboreshwa.

Fomu yetu ya usajili wa udereva inakuchukua dakika 5 tu kukamilisha na kuwasilisha. Mara tu unapokubaliwa na kusajiliwa kama dereva, utahitaji kumaliza mafunzo yako ya udereva ama katika ofisi ya Bolt au mtandaoni.

Tutapitia nyaraka zinazohitajika na mara tu tutakapokamilisha, tutakufungulia akaunti ya dereva katika programu ya Dereva wa Bolt. Utahitaji kuwa na simu janja ‘smartphone’ inayofanya kazi ambayo angalau inatumia mfumo wa Android 9.0 au iOS 12, ili uweze kuchukua abiria na kuwafikisha mwisho wa safari yao.

Ikiwa huna simu mahiri, timu yetu inaweza kupendekeza simu ya bei nafuu ya Android ili uanze.

Weka gari yako katika hali nzuri.

Ikiwa tayari una gari, utahitaji kuifanya ionekane jinsi ilivyokuwa wakati ulipoinunua kutoka kwenye chumba cha maonyesho ya magari.

Moja ya vitu waendeshaji wa Bolt hutegemea katika ukadiriaji wao ni hali ya mambo ya ndani ya gari lako. Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa ni safi iwezekanavyo. Utahitaji kuwekeza katika usafishaji wa viti ikiwa havijasafishwa kwa muda mrefu na hakikisha kuondoa madoa yoyote na harufu mbaya.

Kumbuka kwamba uboreshaji mwingine wa mfumo wa hewa unaweza kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo uwe makini kabla ya kununua air freshener.

Je! Unafanyaje ikiwa hauna gari au gari lako halikidhi vigezo vya Bolt kwa safari inayokubalika?

Bolt inaweza kukusaidia kupata gari kutoka kwenye orodha ya magari yetu au kutoka kwa washirika wetu wenye huduma ya kukodisha ikiwa hauna gari linalofaa. Kuna anuwai ya gari mpya na zilizotumiwa kwa kuendesha kama mshirika wa Bolt. Unaweza kuchagua kukodisha gari kwa muda mfupi au mrefu kwa muda usiojulikana, kwa kiwango cha bei nafuu.

Ongeza kiwago chako cha kujichanganya na kijamii.

Hata kama wewe ni mpole, hiyo haimaanishi kuwa huwezi kuwa dereva mzuri. Ila, ni muhimu kukumbuka kuwa ingawa shughuli yako kuu ni udereva, bado uko kwenye biashara ya huduma kwa wateja.

Moja ya mambo muhimu zaidi unayoweza kufanya katika kila mwingiliano ni kuanzisha mazungumzo na abiria wako yanayolenga kuzuia kutokuelewana. Ni muhimu kuzingatia kwamba viwango vya chini vya udereva vinaweza kumaanisha kupoteza sifa za udereva na kufutwa kwenye mfumo ya Bolt.

Hakikisha kumsalimia abiria wako mara tu wanapoingia kwenye gari lako. Kuwa karibu zaidi na jamii, inaleta matokeo mazuri!

Hapa kuna zana za mazungumzo 101 ambazo unaweza kutumia kwenye safari yako ya Bolt ijayo.

Jaribu kufahamu kwamba wakati abiria wengine watafurahi zaidi kuwa na mazungumzo, wengine wanataka tu kupotea katika mawazo yao wakati wanaangalia ulimwengu ukipita. Jihadhari na baada ya muda mfupi utakuwa mtaalamu wa kusoma abiria wako ili uweze kupima kama wako kwenye hali ya gumzo au la.

Ikiwa unaendesha gari katika eneo lenye watalii wengi, inaweza kusaidia kujifunza misingi ya lugha chache na maneno ya kawaida ili kupunguza kizuizi cha mawasiliano. Kwa kuongezea, mwishoni mwa safari, hakikisha kumuaga abiria wako na kuwatakia mapumziko mema ya siku yao, ili uweze kuwa na hakika ya kuacha maoni mazuri ya kudumu kwa abiria.

Jihadhari mwenyewe

Kupata pesa kama dereva wa Bolt inaweza kuwa zoezi ya kufurahisha, lakini pia inaweza kuwa kazi ngumu, kwani inahitaji kutumia muda mwingi kukaa chini, wakati mwingine katika hali zenye mkazo ikiwa uko kwenye foleni ndefu, ukiendesha kwenye eneo mkanganyiko au una abiria aliechelewa safari yake kama kupanda ndege.

Kwa sababu hii, ni muhimu sana kutunza afya yako ya mwili na akili.

Hakikisha kuchukua mapumziko ya mara kwa mara wakati wa kuendesha gari ili uweze kutoka na kunyoosha miguu yako. Kunya maji mara kwa mara, kula kiafya na upate usingizi mzuri wa hali ya juu ili ubaki makini na uwe umepumzika vizuri ukirudi barabarani.

Kwa kuongezea, wakati inaweza kuvutia kufanya kazi kadri uwezavyo ili kuongeza mapato yako, hakikisha kuchukua muda wako na watu unaowapenda. Hii itahakikisha wakati wako wa kuendesha gari na Bolt ni mrefu, wenye furaha na ustawi!

Je, una kile kinachohitajika kufanikiwa kama dereva wa Bolt? Anza leo!

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA BOTSWANA KUKUZA SEKTA YA MADINI.

$
0
0

 

 Na. Georgina Misama- MAELEZO

Rais wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzaia itapeleka timu ya wataamu wa sekta ya madini nchini Botswana kujifunza mikakati ya namna ya kuendeleza madini  nchini kwaajili ya biashara duniani.

Akizunguma katika mkutano maalumu na waandishi wa habari uliofanyika leo Ikulu Dar es salaam wakati wa ziara ya Rais wa Botswana nchini, Mhe. Dkt. Mokgweetsi Keabetswe Masisi, Rais Samia amesema Botswana ni nchi inayofanya vizuri kiuchumi Afrika, ambapo uchumi wake unatokana na kuzalisha kwa wingi madini ya almasi na nyama.

“Botswana ni nchi yenye uchumi mzuri Afrika na inayoongoza duniani kwenye kuuza madini ya Almasi, hivyo mimi na mgeni wangu Mhe. Rais Mokgweetsi Masisi tumekubaliana Tanzaia ipeleke wataamu wa sekta ya madini kule, ili kujifunza uzoefu wao katika eneo hilo na  kuweza kufanya vizuri”, anasema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema kwamba katika mazungumzo yake ya faragha na Rais Masisi wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao wa kirafiki lakini pia wa kibiashara na uwekezaji ambapo uwekezaji wa Botswana nchini umekuwa ukiongezeka kutoka shilingi za kimarekani milioni 731 mwaka 2005 hadi kufikia bilioni 3.5 mwaka 2020.

Kutokana na Botswana kuwekeza kwenye miradi mbalimbali hapa nchini yenye thamani ya Dola za kimarekani shilingi milioni 31, kuna Watanzania wapatao  2,128 ambao wamenufaika na ajira kutoka kwenye miradi hiyo. Rais Samia anatoa wito kwa watanzania wote, kuchangamkia fursa za kibiashara zitakazotokana na uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wa Rais wa Botswana Mhe. Dkt. Mokgweetsi Masisi amesema kwamba Tanzania na Botswana zina uhusiano wa kihistoria tangu enzi za kupigania uhuru wa nchi mbalimbali Afrika, hivyo ushiriano baina ya nchi hizi mbili utaleta manufaa kwa pande zote mbili.

“Ushirikiano wetu utaongoza nchi zetu kwa manufaa kila nchi. Tumekubaliana mawaziri wetu wa Mambo ya Nje ndani ya miezi mitatu wakutane na kupanga utaratibu wa kifufua Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ya mwaka 2002 na kufanya mkutano wake wa mwisho mwaka 2009”

Rais Masisi pia alimkaribisha Rais Samia, kwenda kumtembelea nchini Botswana ili kuimarisha uhusiano wao na kupata uzoefu wa mambo mabalimbali, lakini pia alimuahidi kumuunga mkono hasa kwa kuzingatia historia ya nchi zao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Botswana Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi  wakishuhudia utiaji saini Tamko la pamoja zoezi ambalo lilifanywa na Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Tanzania na Botswana leo  Juni 10 ,2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Masisi yuko nchini kwa ziara ya siku mbili.

WADAU WA HAKI ZA WANAWAKE WAKUTANA KUFUATILIA MUBASHARA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKIWASILISHA BAJETI BUNGENI DODOMA

$
0
0

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeendesha Kijiwe cha Kahawa kwa ajili ya kuwapa fursa wadau mbalimbali wa haki za wanawake na masuala ya jinsia kufuatilia Hotuba ya Bajeti ya Taifa mwaka wa fedha 2021/2022 Mubashara ikiwasilishwa Bungeni na kutoa maoni, mitazamo yao juu ya bajeti na mapendekezo yao yatakayowezesha uboreshaji wa utekelezaji wake kwa mrengo wa kijinsia.

Mjadala huo ulioongozwa na Kauli Mbiu "Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia : Chachu ya uchumi Jumuishi, Viwanda na Maendeleo ya watu" umekutanisha pamoja na mashirika yanayohusika na kutetea haki za wanawake, wanachama wa Vituo vya Taarifa na Maarifa,Wanachama wa Semina za Jinsia na Maendeleo, Wanazuoni, Serikali za mitaa, Madiwani, Wana Jamii, Wawakilishi wa sekta binafsi,vyombo vya habari, Wafanyakazi na Wanachama wa TGNP na Wadau wa Maendeleo.

Akifungua Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022, uliofanyika leo katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema mjadala huo unalenga kutathamini Bajeti ya Taifa mwaka 2020/2021 kwa mtizamo wa kijinsia na kwa kuzingatia matarajio ya wananchi na kubainisha mapengo ya kijinsia yaliyopo katika bajeti na kutoa mapendekezo ya namna ya kuendelea kufuatilia mchakati wa utekelezaji wa bajeti ya matokeo yake.

“Jukwaa hili la Kijiwe cha Kahawa limewaleta pamoja wadau mbalimbali kutazama na kusikiliza Mubashara uwasilishwaji wa taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2020 kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Hotuba ya Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022”,amesema Lilian.

“Mjadala huu umelenga kuhamasisha nguvu na sauti za pamoja katika kudai utengwaji wa rasilimali ulio jumuishi ili kutatua changamoto za makundi mbalimbali katika jamii hasa ya walio pembezoni”,amefafanua Lilian.

Amesema Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa miaka mitano sasa umekuwa ukiandaa Jukwaa hilo ambalo ni mojawapo ya majukwaa ya TGNP ya kujenga nguvu za pamoja ili kuleta chachu ya mabadiliko chanya kisera, kiutendaji na kifikra kwa mrengo wa jinsia.

Katika hatua nyingine amesema kwa miaka 27 sasa TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kujenga uwezo na ushawishi juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia ambapo TGNP imekuwa ikijihusisha na mchakati wa bajeti kila mwaka kwa kuwawezesha wanawake na makundi yaliyo pembezoni katika ngazi za jamii kushiriki kikamilifu kupitia mchakato wa fursa na vikwazo unaofanyika katika ngazi ya jamii.

“Mchakato huu unawezesha wananchi kuibua vipaumbele vyao na pia kuwaunganisha na mjadala wa kitaifa ili kudai utengwaji wa rasilimali kwa ajili ya masuala ya jamii kwa ujumla. Kwa kushirikiana na wadau tumewezesha kwa pamoja uingizwaji wa masuala ya jinsia katika bajeti za baadhi ya halmashauri, Wizara na bajeti ya taifa”,ameongeza

Amesema Jukwaa hilo litaimarisha sauti za pamoja katika kuhamasisha bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa maendeleo endelevu.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa TGNP ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuyapa kipaumbele masuala ya Kijinsia.

“Masuala ya kijinsia yamekuwa kipaumbele katika uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafuatilia, inapofika mwaka 2025 tuone kuna mabadiliko kwa wanawake. Tuchukue fursa hii ya serikali ya awamu ya sita kuhakikisha tunakuwa mfano katika usawa wa kijinsia na watu wengine kutoka nchi zingine duniani zije kujifunza Tanzania”,amesema Lilian.

Naye Mwanachama wa TGNP Jovita Mlay amewataka wadau wa haki za wanawake na masuala ya jinsia kuendele kupaza sauti kwenye maeneo yenye changamoto ili serikali iweze kuzitafutia ufumbuzi  akibainisha kuwa Rais Samia ameonesha wazi kuwa anazingatia masuala ya usawa wa kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mchambuzi wa Masuala ya Kijinsia, Edward Mhina akiwasilisha masuala muhimu ya kijinsia kuhusu hali halisi ya uchumi wa taifa wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji Mubashara wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 Bungeni Dodoma  kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji Mubashara wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 Bungeni Dodoma  kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji Mubashara wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 Bungeni Dodoma  kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mwanachama wa TGNP, Jovita Mlay akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mwanachama wa TGNP, Maimuna Kanyamala akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji Mubashara wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 Bungeni Dodoma  kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakipiga picha ya kumbukumbu
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakipiga picha ya kumbukumbu
Wafanyakazi wa TGNP wakipiga picha ya kumbukumbu
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua Mjadala wa hali ya uchumi mwaka 2020 (Kijiwe cha kahawa) katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa Mjadala wa hali ya uchumi mwaka 2020 (Kijiwe cha kahawa) katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2020 kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mubashara kutoka Bungeni Dodoma kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kufuatilia Mubashara uwasilishwaji wa taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2020 kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mubashara kutoka Bungeni Dodoma kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

MECHI ZA EUR0 2020 KUTIMUA VUMBI RASMI WIKIENDI HII


RC IBUGE aagiza vituo vya kutolea huduma za afya vifungwe mfumo wa kukusanya mapato

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert, Ibuge akifungua kikao kazi kuhusu mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa viongozi wa serikali mkoani Ruvuma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa miezi mitatu kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha kuwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa umma vinafungwa mifumo ya kukusanya mapato (GOTHOMIS).

Brigedia Jenerali Ibuge ametoa agizo hilo wakati anafungua kikoa cha mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa viongozi wa serikali kutoka Halmashauri na wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo kutokana na vituo vingi vya serikali kukosa mifumo ya kukusanya mapato (GOTHOMIS) ambapo takwimu zinaonesha kuwa kati ya vituo 280 vya kutolea huduma za afya vilivyopo mkoani Ruvuma,ni vituo kumi tu ndivyo vimefungwa mifumo hiyo.

“Kufikia Septemba Mosi,2021,vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa umma,viwe vimefungwa mifumo ya GOTHOMIS bila kukosa,Septemba 2,2021,niwe nimepata taarifa ya utekelezaji na baada ya hapo,ukaguzi wa kushitukiza utaendelea na kuchukua hatua’’,amesisitiza RC Ibuge.

Mkuu wa Mkoa pia amewaagiza wakuu wa Wilaya na wakurugenzi katika Halmashauri zote,kuhakikisha mapato na matumizi ya vyanzo vyote katika Halmashauri yanajadiliwa kwenye vikao vya kisheria na amekitaja moja ya kigezo kitakachotumika kuangalia ufanisi wa ukusanyaji mapato katika Mkoa wa Ruvuma katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 ni lazima kufikia zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya vyanzo vya sekta ya afya.

RC Ibuge ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya kwa umma vinatuma kila mwezi kwa wakati madai ya huduma iliyotolewa kwa wanachama wa Mfuko wa Afya Jamii ulioboreshwa(iCHF) na Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya(NHIF).

Kutokana na asilimia ndogo ya wananchi waliojiunga na (iCHF) mkoani Ruvuma,RC Ibuge ameziagiza Halmashauri zote kufanya uhamasishaji mkubwa wa jamii kujiunga na mfuko huo ambapo hadi sasa Mkoa umeandikisha kaya zilizohai 11,820 sawa na asilimia 3.3 wakati lengo ni kufikia kaya 180,085 sawa na asilimia 50.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Jairy Kanga ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa,ikiwemo kuongeza ukusanyaji mapato kupitia mfumo wa GOTHOMIS na kuongeza uhamasishaji kwa jamii kujiunga na (iCHF).

Dr.Kanga amesema mfuko wa iCHF mkoani Ruvuma ulianza kutekelezwa mwaka 2019,ambapo kitaifa Mkoa ulishika nafasi ya mwisho ambapo hivi sasa Mkoa umepanda hadi kufikia nafasi ya 11 kitaifa na kwamba kikao kazi hicho kitaongeza ufanisi na tija.

Imeandikwa na Albano Midelo, Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Juni 11,2020

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Jairy Kanga akitoa taarifa ya mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa viongozi wa serikali mkoani Ruvuma.

SHAMBA LENYE EKARI 100 LINAUZWA WAHI MAPEMA

$
0
0

  Shamba lenye Ekari 100  ambalo tayari limeishapimwa linauzwa .

Mahali: Shungumbweni, Mkuranga karibu na Kiwanda cha Chumvi Neel Salt

Bei: Mil.150,000,000 (mazungumzo yapo) .

Umbali: Kilomita 5 kutoka baharini, Kilomita 26 kutoka barabara kuu ya Dar-Lindi, (Unaweza Ingilia kwa njia ya Kibada-Mwasonga pia).

Shamba lina miti ya mikorosho na mianzi,kisima cha maji safi mita 72, kinatoa lita 20,000 kwa saa.

Lakini pia kwa aliye SERIOUS kununua atapewa bei ya punguzo,NAFASI ipo pia kwa anaetaka kununua kwa malipo ya AWAMU ' Installment' anakaribishwa sana.

KWA MAWASILIANO ZAIDI 📞 0763000053











UFARANSA NA TANZANIA ZATILIANA SAINI MKOPO WA SH. BIL. 362 KUJENGA MRADI WA UMEME JUA MKOANI SHINYANGA

$
0
0

 

Na: Josephine Majura WFM Dodoma

 

Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la Ufaransa (AFD), imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 361. kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa jua.

 

Mkataba wa makubaliano ya msaada huo umesainiwa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Bw. Frederic Clavier Pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shitrika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stepanie Mouen Essombe, kwa niaba ya Serikali ya Ufaransa.

 

Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa Mkataba huo, Bw. Tutuba alisema kuwa mkopo huo utatumika kujenga mitambo ya kuzalisha umeme-jua kiasi cha Megawatt 50 katika Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga.

 

“Ni matumiani yangu kwamba AFD wataridhia kutupatia fedha kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ya mradi huo iliyopangwa kuzalisha Megawatt nyingine 100 ili kuweza kufikia kiwango cha uzalishaji kilichokusudiwa cha Megawatt 150”, alisisitiza Bw. Tutuba.

 

Alisema kuwa Shirika la Maendeleo la Ufaransa lilitoa pia msaada wa Euro milioni 7 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa mradi ambao utatekelezwaji wake utaanza Mwezi Machi 2022 hadi Machi mwaka 2023.

 

Bw. Tutuba alisema kuwa faida za mradi huo utaongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme  na kuiwezesha TANESCO kutimiza malengo yake ya kuzalisha umeme kupitia vyanzo mbalimbali kupitia nishati jadidifu, utapunguza utegemezi wa umeme wa nguvu za maji na kuzalisha umeme wa ziada utakao tumika majira ya ukame.

 

“Sehemu ya mkopo  uliosainiwa  utatumika kufanya maboresha na kuimarisha Grid ya Taifa ili kuifanya ya kisasa ili kupunguza upotevu wa umeme” aliongeza Bw. Tutuba

 

Bw. Tutuba aliishukuru Serikali ya Ufaransa kwa kuipatia Serikali ya Tanzania mkopo huo kwani utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika ambapo utachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine nchini.

 

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Bw. Frederic Clavier, alisema kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha Mpango wa Taifa wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26 unafikia malengo yake.

 

Mhe. Clavier alifafanua kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaifanya Tanzania kushika  nafasi ya 2 kwa ukubwa Afrika Mashariki katika uzalishaji wa umeme wa nguvu ya jua na kuifanya TANESCO kuwa na umeme wa uhakika kutoka katika chanzo rafiki wa mazingira.

 

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stephanie Mouen Essombe, alisema kuwa kati ya mwaka 2016 na 2020, Ufaransa imetoa zaidi ya Euro bilioni 6 kwa ajili ya Miradi ya Nishati sawa na shilingi za Tanzania trilioni 17 ambapo kati ya fedha hizo shilingi trilioni 2.8 zimetumika kwenye miradi ya umeme-jua.

 

Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo wa Umeme-Jua mkoani Shinyanga utaiwezesha TANESCO kuzuia zaidi ya tani 43,460 za hewa ya ukaa na kuchangia jitihada za Serikali ya Ufaransa za kuhifadhi mazingira duniani.

 

“Katika kipindi cha mwaka 2020, Ufaransa imetoa misaada na mikopo yenye thamani ya Euro milioni 330 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 932 na kwamba kusainiwa kwa kiasi kingine cha Euro milioni 130, kutaifanya jumla ya mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na Ufaransa kupitia shirika lake kufikia Euro 580 sawa na sh. Tril. 1.6.

 

Alisema kuwa mwaka huu, Shirika lake linaandaa mkakati ama mpango mpya wa namna ya kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo hifadhi ya mazingira na kilimo endelevu kwa upande wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, miradi ambayo imewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo.

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) Mhandisi Dkt. Titto Mwinuka, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, alisema kukamilika kwa mradi huo utachangia kufikia lengo la Taifa la upatikanaji wa umeme kufikia Megawatt 5,000 kufikia mwaka 2025.

 

Aliongeza kuwa mradi huo utasaidia kuwa na mchanganyiko wa vyanzo mbalimbali vya nishati kwa sababu lengo la Serikali ni kuwa na vyanzo vingi vya nishati ikiwemo maji, nyuklia na jua.

 

Dkt. Mwinuka aliahidi kusimamia kikamilifu mradi huo ili ikuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kufikia lengo lililokusudiwa.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Stephanie Mouen Essombe Mkurugenzi Mkuu Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) nchini Tanzania, wakisaini  hati za  mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na shilingi bilioni 361.71 kwa ajili mradi wa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua. Kushoto wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) nchini Tanzania Bi. Stephanie Mouen Essombe, Wanaoshuhudia nyuma ni Bw. Joguet Vicent Mratibu wa Miradi ya Nishati wa AFD na Bi. Loveness Msechu Mwanasheria Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Mhe. Bw. Frederic Clavier, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, wakisaini   mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na Shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya mradi wa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua. Wanaoshuhudia ni Bw. Joguet Vicent Mratibu wa Miradi ya Nishati wa AFD na Bi. Loveness Msechu Mwanasheria Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na  Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier, wakibadilishana hati za mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na Shilingi bilioni 361.71 kwa ajili mradi wa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa juakatika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) nchini Tanzania Bi. Stephanie Mouen Essombe, wakibadilishana hati za mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na Shilingi bilioni 361.71 kwa ajili mradi wa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa juakatika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Stephanie Mouen Essombe Mkurugenzi Mkuu Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) nchini Tanzaniawakionesha hati za mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na Shilingi bilioni 361.71 baada ya kusainiwa, kwa ajili ya mradi wa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa juakatika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.



Baadhi ya Wataalam kutoka Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) pamoja na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Fedha na  MIpango, wakiwa katika tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo nafuu wa zaidi ya shilingi bilioni 361.7 kwa ajili ya mradi wa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua, Megawati 150 wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, kati ya Tanzania na Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la AFD, Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, akihutubia baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na Shilingi bilioni 361.71 uliotolewa na Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la AF kwa ajili ya mradi wa umeme-jua utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, tukio hilo limefanyika Jijini Dodoma.



Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo na Kamisha Msaidizi wa Idara hiyo Bw. Melkizedeck Mbise, wakifuatilia kwa makini tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya sh. bilioni 361.71 uliotolewa na Ufaransa kwa ajili ya mradi wa umeme-jua utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, tukio hilo limefanyika Jijini Dodoma


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Titto Mwinuka, pamoja na maafisa wake wakiwa katika tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu uliotolewa na Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo (AFD) kwa ajili ya mradi wa umeme-jua utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, tukio hilo limefanyika Jijini Dodoma.uliotolewa na

 

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango – Dodoma)

 

 

SPIKA AFUNGUA MAJADILIANO YA WABUNGE KUHUSU UCHUMI

$
0
0


Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) akizungumza wakati akifungua majadiliano ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Mhe. Daniel Baran Sillo na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa Mwihambi,



Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mada wakati wa majadiliano ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Mada zilizotolewa ni pamoja na umuhimu wa takwimu katika kukuza uchumi, mchango wa taasisi za sera katika maedeleo ya uchumi wa jamii, sera za Kibajeti na Uchumi Jumuishi.



Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa mada umuhimu wa takwimu katika kukuza uchumi wa nchi wakati wa majadiliano ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.



Kamishna wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Ndg. William Mhoja, akitoa mada kuhusu Sera za kibajeti wakati wa majadiliano ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma


NDAHANI AWATAKA VIJANA WASICHANA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KATIKA MAENEO YAO

$
0
0

Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick  Ndahani, ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati akifunga mafunzo ya waelimishaji rika wa Mradi wa TIMIZA MALENGO unaotekelezwa na Amref Tanzania mkoani hapa jana.
Waelimishaji rika wa Mradi wa TIMIZA MALENGO unaotekelezwa na Amref Tanzania mkoani hapa wakimsikiliza, Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick  Ndahani, wakati akifunga mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yakifungwa.
Mafunzo yakifungwa.



Na Dotto Mwaibale, Singida


KAIMU Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick  Ndahani awewaomba vijana Wasichana ambao ni waelimisha rika kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa vijana wa mkoa wa singida.

Ombi hilo limetolewa na Ndahani ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga mafunzo ya waelimishaji rika wa Mradi wa TIMIZA MALENGO unaotekelezwa na Amref Tanzania ambapo jumla ya waelimishaji rika 51  wasichana waliozalia nyumbani  kutoka Halmashauri ya Iramba, Singidana Manispaaa wamepatiwa mafunzo ya malezi bora ya watoto na familia.

Ndahani alisema kuzaa nyumbani siyo mwisho wa mafanikio katika maisha ,vijana wanapaswa kutumia changamoto walizonazo na kuzibadili kuwa fursa kwani wasichana wengi wakishazaa hukataka tamaa na mwisho kushindwa kuhudumia watoto wao na familia kwa ujumla.

Kaimu Afisa Maendeleo huyo amewashauri wasichana kuunda vikundi vya ujasiriamali katika maeneo yao ili kujipatia kipato kwani mkoa wa singida unazo fursa nyingi za kiuchumi kama vile ufugaji wa kuku wa asili, nyuki na kilimo cha mboga na mazao mengine kama Alizeti, mahindi, mpunga na dengu.

" Hatupendi kuona wala kusikia msichana au mwanamke anakuwa maskini  katika nchi hii ili  hali Rais wa Tanzania ni   Mwanamke lazima wanawake hapa nchini wawe wa mfano katika Bara la Afrika kwa sababu tunaye Rais mwanamke ambaye ni mchapakazi na makini katika uogozi ambaye anawajali wanawake na katika kuonesha hilo mapema wiki hii alikutana nao mkoani Dodoma na kuzungumza nao," ,alisema Ndahani.

Aidha amewataka maafisa maendeleo wa wilaya zote kuwasaidia vijana katika kutimiza malengo yao kwa kuwapatia mafunzo na ujuzi wa kuanzisha shughuli za kiuchumi ikiwemo usimamizi wa miradi na uandishi wa maandiko ya biashara, kilimo na ufugaji katika  maeneo yao badala ya kukaa ofisini.

Ndahani amewakikishia vijana wanawake kuwa Serikali  ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu imejipanga na   kuhakikisha inatatua changamoto zote za kiuchumi na usawa wa kijinsia kwa wanawake ikiwemo kuanzisha mifuko maalumu ya kuwawezesha wanawake ikiwemo Benki ya Wanawake na asilimia kumi ya mapato ya ndani ambayo asilimia nne huenda kwa wanawake.

Afisa huyo alisema ataendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana ili kutimiza malengo ya serikali   ya kuwakwamua vijana katika dimbwi la umaskini katika Mkoa wa Singida.

Aidha ameishukuru Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuratibu vizuri mafunzo hayo kwa vijana yaliyofanyika Singida na mikoa mingine katika mradi wa TIMIZA MALENGO .

Kwa upande wake Afisa Mradi wa Amref Tanzania, Mkoa wa Singida  Johnstone John Sendama amewawataka vijana hao kwenda kuwaibua na kuwasidia wasichana wote waliozaa wakiwa nyumbani ili kuwapatia mafunzo ya malezi bora ya mtoto na familia kama walivyofundishwa  ili malengo ya mradi wa TIMIZA MALENGO yaweze kufanikiwa.

Vijana walionufaika na mradi huo wameishukuru serikali na Shirika la Amref Tanzania kwa kuwaona na kuamua kuwapatia mafunzo yatakayo wasaidia katika malezi bora ya familia na watoto wao hivyo kujenga kizazi bora katika Taifa letu.

Viewing all 48963 articles
Browse latest View live