Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48952 articles
Browse latest View live

MIRADI YA THAMANI YA TRILIONI MBILI YASAJILIWA TIC

$
0
0

 Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi 59 yenye thamani ya shilingi trilioni 2 kuanzia mwezi Aprili hadi Mei mwaka huu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Profesa Godius Kahyarara alipokuwa akizindua Baraza la Wafanyakazi wa TIC  4 Juni, 2021 amesema kwamba, usajili wa miradi hiyo umeongeza ajira takribani elfu kumi na mbili (12) nchini.


Katika uzinduzi huo Prof. Kahyarara amewataka wafanyakazi kutekeleza mpango wa kanda maalum za kiuchumi lengo likiwa ni kurahisisha kuwahudumia wawekezaji ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zao.

“Suala la Uwekezaji katika Kanda hizi za kiuchumi matarajio ya serikali ni tofauti na tulivyokuwa tunaona kwani ni muhimu sana kutekeleza maono ya namna hiyo. Ni jambo ambalo hatukutegemea Tanzania kuweza kuvutia wawekezaji na kupatikana kiasi cha shilingi trilioni 2 ndani ya miezi miwili (2) hivyo kwa muktadha huo kwa mwaka mmoja itakuwa trilioni ishirini na nne (24)” amesema Prof. Kahyarara.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi amesema  Kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu sana kati ya menejimenti ya TIC pamoja na wafanyakazi hivyo tumeona ufanisi umeongezeka kwa kasi sana, na miradi mingine iliyosajiliwa ni pamoja na kilimo na tehama” ameongeza Dkt. Maduhu.

Aidha, serikali imeanza kuboresha Uwekezaji kwakuwa imeanza mchakato wa kuwa na benki ya ardhi kwa kuunda timu inayohusisha Wizara ya Ardhi, Wizara ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na TAMISEMI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu I. Kazi.
Prof. Godius Kahyarara Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji
Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Prof. Godius Kahyarara wa nne kutoka kushoto.


Wajumbe wa baraza la wafanyakazi na menejimenti (TIC) walioshiriki katika kikao kazi hicho.

WAIATARA ATAKA WAKANDARASI WAZAWA KUCHANGAMKIA FURSA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akimsikiliza Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Wenceslaus Bavuma, akimweleza maendeleo ya mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Nduli mkoani Iringa, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi huo, hivi karibuni.

Muonekano wa moja ya tabaka la chini la barabara ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja cha ndege Nduli-Iringa.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, ameutaka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kufanya utafiti wa kwanini Wahandisi Wazawa hawakuomba kazi licha ya Mkandarasi Kampuni ya SINOHYDRO Corporation Limited kutangaza kazi kwa mradi wa upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Nduli mkoani, Iringa.


Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho Naibu Waziri Waitara amesema kutoshiriki kwenye miradi mikubwa ya ujenzi kunawanyima uzoefu wahandisi wazawa nchini, hali itakayosababisha kushindwa hata kufanya ukarabati baada ya mradi kukamilika.


“Kama nafasi zinatangazwa kwenye miradi na wahandisi wetu hawaombi kazi hizi, ipo haja ya kufanya utafiti kujua sababu ni ni nini, hivyo nawaagiza TANROADS kufanya  utafiti kuhusu suala hili’, amesema Naibu Waziri Waitara.


Aidha, Naibu Waziri Waitara amezitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na TANROADS kukaa pamoja ili kukubaliana namna ya kutekeleza awamu zote mbili za ujenzi kwa mara moja.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera amesisitiza utekelezaji wa awamu zote mbili za ujenzi kwani utapunguza muda wa utekelezaji na kufanya mradi kukamilika kwa muda mfupi.


Naye Msimamizi wa Mradi kutoka TANROADS Mhandisi, Wenceslaus Bavuma, amemuhakikishia Naibu Waziri Waitara kuwa Wakala unasimamia kwa karibu mradi huo na utahakikisha viwango vyote vinazingatiwa ili mradi ukamilike kwa wakati na viwango.


Mradi wa kiwanja cha Ndege cha Nduli mkoani Iringa utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 40 na utahusisha urefushaji wa barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, jengo la muda la abiria, jengo la zima moto, jengo la kuongozea ndege, taa za barabarani na kituo cha nishati.

MIRADI 59 YENYE THAMANI YA TRILIONI 2 YASAJILIWA TIC

$
0
0

 Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi 59 yenye thamani ya shilingi trilioni 2 kuanzia mwezi Aprili hadi Mei mwaka huu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Profesa Godius Kahyarara alipokuwa akizindua Baraza la Wafanyakazi wa TIC  4 Juni, 2021 amesema kwamba, usajili wa miradi hiyo umeongeza ajira takribani elfu kumi na mbili (12) nchini. 

Katika uzinduzi huo Prof. Kahyarara amewataka wafanyakazi kutekeleza mpango wa kanda maalum za kiuchumi lengo likiwa ni kurahisisha kuwahudumia wawekezaji ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zao.

“Suala la Uwekezaji katika Kanda hizi za kiuchumi matarajio ya serikali ni tofauti na tulivyokuwa tunaona kwani ni muhimu sana kutekeleza maono ya namna hiyo. Ni jambo ambalo hatukutegemea Tanzania kuweza kuvutia wawekezaji na kupatikana kiasi cha shilingi trilioni 2 ndani ya miezi miwili (2) hivyo kwa muktadha huo kwa mwaka mmoja itakuwa trilioni ishirini na nne (24)” amesema Prof. Kahyarara.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi amesema Kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu sana kati ya menejimenti ya TIC pamoja na wafanyakazi hivyo tumeona ufanisi umeongezeka.

Aidha, serikali imeanza kuboresha Uwekezaji kwakuwa imeanza mchakato wa kuwa na benki ya ardhi kwa kuunda timu inayohusisha Wizara ya Ardhi, Wizara ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na TAMISEMI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu I. Kazi.

Prof. Godius Kahyarara Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji

Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Prof. Godius Kahyarara wa nne kutoka kushoto.

Wajumbe wa baraza la wafanyakazi na menejimenti (TIC) walioshiriki katika kikao kazi hicho.

WAHARIRI WAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0

 

Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya akifundisha wahariri (hawapo pichani) kuhusu dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi walioshiriki semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, jijini Arusha.



Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya akifundisha wahariri kuhusu dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi walioshiriki semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, jijini Arusha.





Afisa kutoka Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Edwin Kachenje akifutalitia kwa makini wasilisho kwenye kompyuta mkapato wakati wa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.



hariri wa Gazeti la Jamvi la Habari Dkt. Bravious Kahyoza akisoma kanuni za Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wakati wa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia, jijini Arusha.



Kamishna Msaidizi wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Bashiru Taratibu akifafanua jambo wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu masuala ya ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.



Mhariri wa Star Tv Bw. Dotto Shashi (kulia) na mhariri wa redio Free Afrika Bw. Jilala Duttu wakifuatilia mada iliyowasilishwa wakati wa semina Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.



Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya, akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwenyekiti wa mkutano wa wahariri Bw. Ben Mwang’onda, baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi iliyofanyika jijini Arusha.



Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya, akimkabidhi cheti cha ushiriki mhariri wa Clouds Media Bi. Joyce Shebe baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi iliyofanyika jijini Arusha.

(Picha na Wizara ya Fedha na Mipango – Arusha)

************************

Na. Josephine Majura, WFM, Arusha

WAHARIRI wa vyombo vya habari wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali kutangaza miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ili wananchi wafahamu kazi kubwa inayofanywa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Ahadi hiyo wameitoa jijini Arusha wakati wa kufunga semina ya wahariri hao iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini lengo likiwa kuwajengea uwezo wahariri kuhusu dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

Mhariri wa Gazeti la Tanzanite Bi. Selina Mathew, Clouds Media Joyce Shebe, Habarileo Bakari Kingoba, wameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wahariri kwani yamewajengea uwezo mkubwa kuelewa dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ambayo bado ni changamoto kwa baadhi ya waandishi katika kuiripoti.

“Wataalamu wametupa shule ya kutosha mambo mengi tulikuwa hatuyafahamu lakini kupitia semina hii ya siku mbili tumejifunza mengi kwa kweli tunaipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mada ambazo zimekuwa na tija kwetu na zimetoa mwelekeo wa nini kinafanyika kwenye dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,” alisema Bi. Selina Mathew.

Waliahidi kwenda kuandika makala za kutosha ili kuelimisha jamii kuhusu dhana ya PPP na namna itakavyoleta matokeo chanya kwa nchi kupitia uwekezaji unaofanywa na Sekta Binafsi katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Aidha Wahariri hao walishauri serikali isichoke kutoa elimu na kutangaza miradi inayotekelezwa na serikali na kuongeza kuwa wao kama chombo cha kutoa taarifa kwa umma wataendelea kutoa taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio ya serikali ili dhana potofu ya kuwa serikali haitekelezi miradi kwa wakati iweze kufutika.

Kwa upande wake, Bi. Janeth Mushi aliwapongeza wataalamu kutoka Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa mada mbalimbali walizofundisha ikiwemo Dhana ya PPP, Sheria na Kanuni zake.

“Sisi ni chombo cha kutoa taarifa kwa umma ni wakati sasa kwa taasisi na wizara nyingne kuiga mfano huu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wa kutujengea uwezo ili tuwe na uelewa mpana wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili tuweze kuzitangaza na wananchi wajue kazi nzuri na kubwa inayofanywa na serikali”, alisisitiza Bi. Mushi.

Naye Mhariri wa Gazeti la Majira, Bw. Ruben Kagaruki alitoa ushauri kwa Wizara ya Fedha na Mipango iandae mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari kwa kuwa wao ndio wanaenda kuchukua taarifa hivyo ni vizuri nao pia wakapatiwa mafunzo ya masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili wawe na uelewa mpana katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake, Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema, Bw. John Daniel, aliishauri serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kusimamia kwa hali na mali utekelezaji wa Sheria na Kanuni za PPP, bila kuruhusu mianya ya rushwa na kupewa watu ambao hawana uwezo wa kutekeleza miradi hiyo na kusababisha ucheleweshwaji na miradi kutokamilika kwa wakati.

Bw. Daniel aliongeza kuwa ni vyema Wizara ya Fedha na Mipango ikaongeza muda wakati mwingine wakiandaa semina ili kutoa nafasi kwao kujifunza mambo mengi kwa weledi zaidi kwa kuwa elimu waliyoipata ni sehemu tu katika dhana nzima ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kimekuwa na utaratibu wa kufanya semina na wahariri wa vyombo vya habari nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutoa taarifa za wizara hiyo kwa usahihi.

Hadi sasa wizara imeshafanya semina kwa wahariri wakitokea kwenye vyombo vya habari zaidi ya 40 katika nyanja mbalimbali kuhusu majukumu yanayotekelezwa na wizara ikiwemo masuala ya Huduma Ndogo za Fedha, Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) na semina hii ya masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Kabla ya kufunga semina hiyo, Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Dkt. John Mboya, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, aliwakabidhi Wahariri vyeti vya kushiriki semina hiyo kwa ufanisi mkubwa.


NIT, KAMPUNI YA AVIC, KAMPUNI YA MALLOY, WASAINI MIKATABA KUKUZA SEKTA YA USAFIRISHAJI NCHINI

$
0
0

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Profesa Zacharia Mganilwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi pamoja na wanafunzi wanaosoma kozi ya Urubani katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo mara baada ya kusainiwa Mikataba miwili ya kupeleka vifaa vya kusomea masuala mazima ya Usafirishaji wa ndege pamoja na Vitabu vya sekta ya usafirishaji wa anga, Maji na Reli.


Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya chuo cha NIT, Rukia Shamte, akizungumza wakati wa kusaini mikataba leo katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa akibadilishana mkataba na mwakilishi wa kampuni ya Mallory International Limited mara baada ya kusaini Mkataba huo.
Picha ya pamoja.
Mwakilishi wa kampuni ya Mallory International Limited Wakibadilishana mikataba na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Prof. Zacharia Mganilwa mara baada ya kusaini leo katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji.
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji  (NIT) kimesaini Mikataba miwili na wazabuni kutoka kampuni ya Kichina inayojihusisha na biashara  ya vifaa vya usafiri wa anga Avic International Holding Company na kampuni ya Mallory International Limited kwa lengo la kununua Vifaa mbalimbali vya mafunzo na vitabu katika chuo hicho.

 Mkataba uliosainiwa na Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Avic international Holding unaogarimu zaidi ya USD milioni 1.2 ( bilioni 2.4) na ule wa Kampuni ya Mallory wa USD 300,000 000 (Milioni 700) ni sehemu ya kutekeleza mradi unaofadhiliwa na benki ya dunia chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam leo Juni 5, 2021, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa amesema kampuni ya Avic, ndio imeshinda zabuni ya kulete vifaa vya kutumika kufundisha wahudumu ndani ya ndege ambapo wahudumu hao watafundishwa usalama wa abiria kwenye ndege pamoja na vifaa vya kufundishiwa wahandisi wa matengenezo ya ndege hapa nchini.

"Vifaa hivi ni vya Kisasa kabisa ambavyo vinatumika duniani kote, Ulaya, Marekani nao wanatumia vifaa kama hivyo." Amesema Prof. Mganilwa.

Amesema vifaa hivyo vitawawezesha vijana wa kitanzania  kusoma hapa hapa nchini ambapo zamani mafunzo hayo walikuwa wakiyafuata nje ya nchi...."vifaa hivyo vikifika vijana wengi watajifunza hapa hapa na kuweza kuendesha mashirika yetu ya ndege kwa usalama na umahiri mkubwa, kuketa faida na kuwahudumia watanzania watakao kuwa wakitumia usafiri wa ndege". 

Aidha amesema, mkataba wa pili  waliousaini leo ni kati ya Chuo cha Usafirishaji na kampuni ya Mallory ambayo imeshinda zabuni ya kuwapelekea vitabu ambapo katika mkataba huo kampuni ya Mallory itatoa vitabu elfu 10 chuoni hapo kwa ajili ya kufundishia usafiri wa anga, usafiri wa Maji pamoja na usafiri wa reli.

"Tunatarajia vitabu hivyo vitakuwa katika maeneo ya Usafiri wa Anga, Usafiri wa Maji na usafiri wa Reli ambapo vitawawezesha  wanafunzi na watafiti wa masuala ya usafirishaji  kuweza kuvitumia na hivyo kuweza kutoa huduma ya kitaalamu katika Chuo Cha Usafirishaji amesema Profesa Mganilwa.

Profesa Mganilwa amesema,  upatikanaji wa vifaa hivyo, utasaidia sana katika miradi mbali mbali inayoendelea hapa nchini kwa sasa hasa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ununuzi na ujenzi wa Meli na ufufuaji wa sekta ya anga ambapo sasa wataalamu wataweza kuwa mahili na baada ya hapo nchi itegeme kuwa na mpango wa uchumi kutoka katika sekta ya Usafirishaji.

Kwa Upande wake Mhandisi wa Ndege na Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mhandisi Abubakar Noor amesema, mikataba hiyo iliyosainiwa leo wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP) umelenga kukuza vyuo vya Ufundi kuwa vyuo vya umahili.

Mhandisi Noor amesema kupitia mikataba hiyo, Chuo cha NIT kitakuwa na kituo cha Umahili katika anga ambapo watafundisha mafunzo mbalimbali yanayohusiana na usafiri wa anga ikiwemo urubani, uhudumu ndani ya ndege na uhandisi matengenezo ya ndege.

Amesema wanafunzi wataenda kupata uhalisia wa kazi ambazo wanapaswa kuifanya watakapokuwa wameajiriwa katika sekta ya usafiri wa anga.

"Tunatarajia mafunzo haya tutayafundisha kwa kiwango au kwa ngazi ya PPL. ambayo ni Private Pilot Licence, mafunzo hayo Rubani atapata mafunzo ya awali ya kurusha ndege, pia kutakuwa na mafunzo ya CPL ambayo Comercial pilot Licence ambapo Rubani atapata leseni ya kurusha ndege ya buashara." Amesema Mhandisi Noor.

Mafunzo hayo yatatolewa mara baada ya kukamilisha kununuliwa kwa ndege ndogo mbili ambapo moja wapo itakuwa na injini mbili kupitia mradi huo wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP).

Mhandisi Noor amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa katika Chuo Cha Taifa ya Usafirishaji tuu na sio vyuo vingine.

BENKI YA EXIM YAIBIKA KINARA UHIFADHI MAZINGIRA.

$
0
0

Benki ya Exim imeibuka kinara wa kutunza na kuhifadhi mazingira miongoni mwa taasisi za kifedha jijini Dar es Salaam na hivyo kukabidhiwa tuzo maalum ya kutambua jitihada hizo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Tuzo hiyo maalum imekabidhiwa hii leo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Amosi Makala katika serehe za kuadhimisha siku ya Mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Kupitia mkakati wake wa kutunza na kuhifadhi mazingira unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ benki hiyo imekuwa mstari mbele katika kampeni mbalimbali za kuhifadhi mazingira ikiwemo  upandaji miti ambapo hivi karibuni benki hiyo kwa kushirikiana na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ilipanda miti 10,0000 jijini Dodoma

Aidha, benki hiyo pia imekuwa imekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa bustani mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya majiji hapa nchini ikiwemo Dar es salaam.

Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Lameck Charles (Kushoto) akipokea tuzo maalum kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija  baada ya benki hiyo kuibuka kinara wa kutunza na kuhifadhi mazingira miongoni mwa taasisi za kifedha jijini Dar es Salaam katika serehe za kuadhimisha siku ya Mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam hii leo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Muonekano wa tuzo iliyotolewa na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa Benki ya Exim baada ya benki hiyo kuibuka kinara wa kutunza na kuhifadhi mazingira miongoni mwa taasisi za kifedha jijini Dar es Salaam katika serehe za kuadhimisha siku ya Mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam hii leo.

Stanbic Bank yaidhamini Taswa SC

$
0
0

   Benki ya Stanbic Tanzania imetoa msaada wa vifaa na fedha wenye thamani ya Sh9.2 millioni kwa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa SC).


Taswa SC inatarajia kucheza mchezo  wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge FC ambapo Mkuu wa Masoko wa benki ya Stanbic Tanzania, Desideria Mwegelo amesema msaada huo utafanikisha vyema ziara hiyo ya mkoa wa Dodoma.

Mwegelo amesema kuwa benki yao  inatambua mchango wa Taswa SC katika maendeleo ya michezo nchini pamoja na masuala ya afya.

“Michezo ni moja ya njia ya kujenga afya ya mwili katika jamii. Benki yetu mbali ya kusaidia michezo, pia inasaidia masuala ya afya, tunaamini kwa msaada huu, timu itafanya vizuri katika mchezo huo,” alisema Mwegelo.

Alisema kuwa benki yao inajisia fahari zaidi kushirikiana na Taswa SC kwani  wanafanya hivi kwa mara ya pili.

“Msaada huu pia ni sehemu ya benki ya Stanbic Tanzania kujishughulisha na masuala ya shughuli za kijamii. Tunawaomba wachezaji wa Taswa SC watuwakilishe vizuri siku ya mchezo huo,” alisisitiza Mwegelo.

Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza benki ya Stanbic Tanzania kwa msaada huo ambao utwafanya kufanya safari yao kwa uhakika zaidi mbali ya kucheza mechi.

Majuto alisema kuwa klabu ilikuwa njia panda kusafiri kwenda Dodoma na  maada huo umewahamasisha wachezaji kufanya vyema.

 “Msaada umekuja wakati muafaka ambapo klabu ilikuwa inahitaji kusafiri na kucheza mechi dhidi ya timu ya Wabunge. Naishukuru sana kwani ndoto yetu ya miaka mingi kucheza na Bunge FC mkoani Dodoma itatimia,” alisema Majuto.

 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano  cha benki ya Stanbic Tanzania, Desideria Mwegelo (Kulia)akikabidhi mfano wa hundi wenye thamani  ya Sh9.2 millioni  kwa mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa SC) Majuto Omary. Fedha hizi ni kwa ajili ya kugharimia vifaa na ziara ya Dodoma kucheza mechi dhidi ya timu ya Bunge FC. 

TAASISI YA ELIMU TANZANIA YAWAHIMIZA WAWEZESHAJI KUFUNDISHA ELIMU STADI ZA MAISHA ZA AFYA YA UZAZI, VVU NA JINSIA

$
0
0

 TAASI ya Elimu Tanzania (TET) imewataka wawezeshaji wa ujaribishaji wa mwongozo wa kufundisha elimu stadi za maisha za afya ya uzazi ,VVU/Ukimwi na jinsia kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kuwa na uzalendo katika kuifanya kazi yao.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba katika ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa siku sita ambapo amewaeleza washiriki mafunzo waliyoyapata yawe chachu katika utaoji wa elimu ya afya ukiwemo maambukizi ya VVU , ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.

“Ningependa ifahamike kwa sasa Miongozo hii ipo kwenye majaribio , wawezeshaji wakati mnapofanya ujaribishaji mnapaswa kufuatilia na kupata mrejesho ya kipi kinahitajika katika kufanyiwa marekebisho’ amesema Dkt.Komba.

Ameongeza TET kwa kushirikiana na Shirika la UNESCO,TACAIDS,Maria Stops na shirika la Room to Read watafuatilia kwa karibu ujaribishaji wa miongozo hiyo katika halmashauri zote 13 zilizopanga kufikiwa.

Kwa upande Mmwakilishi kutoka wizara ya TAMISEMI Teresia amesema miongozo hiyo itasaidia katika kupunguza au kumaliza kabisa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kwa wahusika watakaopatiwa elimu hii ya stadi za maisha itasaidia wanafunzi kuweza kupambana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo wanafunzi wengi kushindwa kumaliza Shule .

Ameongeza kuwa TAMISEMI imefurahishwa na kuona walimu wengi wameweza kupata mafunzo hayo ambayo kwa vitendo na kuwa kila Shule itaweza kuwa na walimu wawili wawilii kwa Shule za Msingi na Sekondari na wataweza kufundisha stadi za maisha kwa wanafunzi.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku sita na kuwashirikisha jumla ya washiriki 46 wakiwemo Walimu ,maofisa kutoka TAMISEMI, Wakufunzi na wataalamu wa afya ambapo jumla ya walimu 1696 wa shule za Sekondari na Msingi wanatarajiwa kuwezeshwa kwenye mafunzo hayo kwenye halmashauri 13.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba
Picha ya pamoja


Huawei yazindua Bidhaa Mpya Zinazoendeshwa na Mfumo wake wa HarmonyOS 2

$
0
0
[Shenzhen, China, Juni 6, 2021] Huawei imezindua simu janja (smartphones), saa janja(smartwatches) pamoja na kompyuta bapa(tablet) vinavyotumia mfumo wake mpya wa kiuendeshaji unaoitwa HarmonyOS 2 , utakao wapa wateja wake huduma bora na zinazoweza kujiendesha kutokana na matumizi ya mtu katika nyakati tofauti.

Mbali na mfumo huo, HUAWEI pia imetoa matoleo mapya ya HUAWEI Mate 40, HUAWEI Mate X2, HUAWEI WATCH series 3 na HUAWEI MatePad Pro.

"Kimoja kama vyote, vyote kama kimoja. Tunaishi kwenye ulimwengu ambao vitu vyote vimeunganishwa na vinaweza kujiendesha. Hakuna mtu hata mmoja anaeweza kuukwepa ulimwengu huu." Alisema Richard Yu, Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.

Katika hafla hiyo, Huawei pia imezindua HUAWEI FreeBuds 4, vishika sauti(wireless earphones) vya teknolojia ya kisasa vyenye uwezo wa kuzuia kelele za nje(Active Noise Cancellation) huku vikiunganishwa na simu kwa mfumo wa “Bluetooth”. Kampuni hiyo pia imezindua "monitors" mbili zenye ubora wa juu ambazo ni HUAWEI MateView na HUAWEI MateView GT.

HUAWEI ilichukua fursa hio kutangaza kuwa takribani vifaa 100 vya HUAWEI - simu pamoja na kompyuta bapa – vitaboreshwa ili viweze kutumia mfumo huu mpya wa HarmonyOS 2, huku ikiwapa watumiaji wake nafasi ya kufurahia mfumo huu unaoendeshwa kwa utashi na unaoweza kuunganisha vifaa vingi katika hali mbalimbali.

"Kuna vifaa janja(smart devices) vingi katika maisha yetu hivi sasa kuliko hapo awali, lakini ufanisi wake mara nyingi sio mzuri. Ni vigumu kuunganisha mifumo tofauti na kufanya kazi ipasavyo, jambo ambalo huupelekea watumiaji kutoridhika." Alisema

"HarmonyOS imetengenezwa kushughulikia tatizo hilo. Mfumo huu hutoa lugha ya kawaida kwa vifaa mbalimbali ili viweze kuunganishwa pamoja na kushirikiana, huku ikiwapa watumiaji ubora, ufarisi na usalama wa hali ya juu." Alisema Yu

HarmonyOS 2 hutumia teknolojia kukidhi mahitaji tofauti ya vifaa mbalimbali hivyo kuongeza urahisi katika matumizi. Mfumo huu pia hujumuisha vifaa vilivyokua vinajitegemea kwenye mfumo wake na kuvifanya kuwa kifaa kimoja chenye uwezo mkubwa ambacho huunganisha rasilimali zote na kuzielekeza kutokana na matumizi halisi ya mtu.

"Kwa watengenezaji wa programu, HarmonyOS 2 hutoa jukwaa la kutengeneza programu ambazo zinaweza kuingiliana na mifumo mingine na hivyo kufanya ukuaji wa program kuwa rahisi kuliko hapo awali." Alimalizia


TUNAONGEZA TIJA UZALISHAJI WA KOROSHO ILI UFIKIE KILO 35 KWA MTI MMOJA-WAZIRI MKENDA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo leo tarehe 6 Juni 2021 wakati akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kwenye Mkutano maalumu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unaofanyika katika hoteli ya Sea View Resort Mkoani Lindi.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geofrey Mwambe akisisitiza jambo leo tarehe 6 Juni 2021 wakati akizungumza kabla ya mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kwenye Mkutano maalumu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unaofanyika katika hoteli ya Sea View Resort Mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega akisisitiza jambo leo tarehe 6 Juni 2021 wakati akizungumza kabla ya mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kwenye Mkutano maalumu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unaofanyika katika hoteli ya Sea View Resort Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akikiwatambulisha washiriki wa mkutano maalumu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unaofanyika katika hoteli ya Sea View Resort Mkoani Lindi, Tarehe 6 Juni 2021.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe wakifatilia mkutano maalumu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unaofanyika katika hoteli ya Sea View Resort Mkoani Lindi, Tarehe 6 Juni 2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania akitoa wasilisho kuhusu mwenendo wa zao la Korosho nchini wakati akizungumza kwenye Mkutano maalumu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unaofanyika katika hoteli ya Sea View Resort Mkoani Lindi.





Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Lindi




Kiwango cha uzalishaji na tija kwenye mazao mengi hapa nchini bado kipo chini. Kwa mfano, uzalishaji wa korosho kwa sasa ni wastani wa kilo 5 hadi 10 kwa mti ikilinganishwa na tija ya juu ya kilo 35 kwa mti inayoweza kufikiwa kulingana na viwango vya kitaalam.




Baadhi ya sababu zinazosababisha kuwepo kwa tija ndogo kwenye mazao ni pamoja na Matumizi madogo na yasiyokuwa sahihi ya pembejeo, Uwekezaji mdogo kwenye tafiti za kimaendeleo, Huduma duni za ugani, na Kuyumba kwa masoko ya mazao kwenye baadhi ya misimu.




Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda amebainisha hayo leo tarehe 6 Juni 2021 wakati akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye Mkutano maalumu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unaofanyika katika hotel ya Sea View Resort Mkoani Lindi.




Amesema kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau imeendelea na jitihada za kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya kimkakati ikiwemo korosho ili kuongeza kipato cha mkulima na taifa kwa ujumla.




Katika zao la korosho, Waziri Mkenda amesema kuwa jitihada hizo ni pamoja na elimu ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima, uzalishaji wa miche bora ya korosho, matumizi ya pembejeo, kuimarisha shuguli za utafiti na usambazaji wa mabomba ya kupulizia viuatilifu, ambapo Vyama Vikuu vya Ushirika vinasambaza mabomba kwenye AMCOS zote 623 nchini.




“Hadi sasa mabomba 135 yameshasambazwa kwenye AMCOS. Mfano Mkoa wa Mtwara wenye wastani wa miche 23,918,206 ulizalishaji ukiongezeka kufikia tija ya kilo 35 kwa mti kwa mwaka mapato ya wakulima yataongezeka kutoka billion 279.8 za sasa hadi kufikia trilioni 1.971 kwa mwaka” Amekaririwa Prof Mkenda




Amesisitiza kuwa ili kuendelea na juhudi za kutatua changamoto za mazao nchini, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho ilifanya kikao cha wadau wa korosho tarehe 23 Aprili, 2021 jijini Dodoma kujadili changamoto za zao hili hapa nchini.




Katika kikao hicho, wadau walipata fursa ya kupokea mawasilisho kutoka kwa wataalam yaliyoelezea hali ya tasnia ya korosho hapa nchini na namna ya kuongeza tija na uzalishaji.




Miongoni mwa mawasilisho hayo ni utafiti wa hali ya uzalishaji wa korosho uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele ambao ulionesha mwenendo wa kushuka kwa uzalishaji wa korosho kutokana na matumizi madogo ya pembejeo na mabadiliko ya tabianchi.




AMesema kuwa ipo haja kama nchi kuwa na mpango wa uhakika wa ugharamiaji wa pembejeo za zao la korosho pamoja na kuendelea kufanya utafiti ili kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.




MWISHO

Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya DLight yafungua duka mjini Moshi

$
0
0

  

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu (wa pili toka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la kusambaza vifaa vya umeme wa jua (Solar) la D.Light , lililopo jengo la Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro  (KNCU) , Wengine katika picha kutoka kushoto ni Afisa mkuu Uwendeshaji wa D.Light Afrika, Jacob Okoth,  Mkurugenzi wa D.Light Tanzania , Charles Natai na kulia ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji  D.Light Tanzania, Hamis Mruta.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu akizungumza waandishi wa habari na wageni waalikwa  kwenye uzinduzi wa duka jipya la kisasa la DLight mjini Moshi. 


Mkurugenzi wa DLight Tanzania,  Charles Natai akizungumza waandishi wa habari na wageni waalikwa  kwenye uzinduzi wa duka jipya la kisasa la DLight mjini Moshi. Wengine kushoto kwake ni Mshahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu na Afisa Mkuu wa Uendeshaji DLight Afrika,  Jacob Okoth .

Serikali kuhakikisha kunakuwa na Usalama na Ubora wa huduma za mawasiliano nchini

$
0
0
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Kushoto) akisikiliza wasilisho kuhusu Kituo cha kuratibu Majanga ya kimtandao (TZ CERT) lililotolewa na Mkuu wa Kitengo hicho Mhandisi. Darius Luhaga (Kulia).

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwahimiza Wataalamu kutoka TCRA kuhusu uboreshaji wa Mifumo ya Huduma za Mawasiliano Nchini.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Jabiri Bakari, pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo vya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA alipotembelea Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Tarehe 04/06/2021.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulie akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (Kulia) mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya TCRA.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imehimiza uboreshaji wa Mifumo mbalimbali ya usimamizi wa huduma za Mawasiliano ili kuhakikisha kunakuwa na Usalama na Ubora wa Huduma Nchini.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea mifumo hiyo kwenye Taasisi ya Udhibiti, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar Es salaam, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine E. Ndugulile (Mb) amesema Wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.

“Upatikanaji wa huduma Bora, za Uhakika na Salama nijambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi na Taifa.” Amesema Mhe. Ndugulile.

Katika ziara hiyo Mhe. Ndugulile alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri K. Bakari na Menejimenti alipotembelea mifumo ya udhibiti wa Mawasiliano.

Dkt. Ndugulile aliipongeza TCRA kwa ubunifu wa kujenga Mifumo Wezeshi kwa huduma mbali-mbali za Mawasiliano Nchini, ambapo alisema uboreshaji wake nimuhimu sana.

Baadhi ya mifumo aliyotembelea Mhe. Waziri ni Mfumo wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT). TZ-CERT pia itatoa ushuri wa kitaalam-namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbali-mbali ya Kimtandao kwa Taasisi na makampuni mbali-mbali hapa Nchini.

Mhe. Waziri pia alitembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja ambapo alihimiza TCRA kuendeza kushirikiana na Taasisi zingine zikiwemo za Kiudhibiti kama Bank Kuu ya Tanzania (BOT).

Benki Ya NBC Yaitikia Wito Uwezeshaji Wajasiriamali, Wakulima Wadogo Jijini Tanga.

$
0
0
Benki ya NBC imeahidi kuendelea kutoa huduma zake kwa kuzingatia mikakati na mahitaji ya wateja wake wakiwemo wajasiriamali na wakulima kwa kuendelea kutoa mafunzo ya biashara na kilimo biashara kwa wakulima ili waweze kukuza mitaji yao sambamba na kuendesha shughuli zao kwa ushindani.

Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya NBC tawi la Tanga Bw Aljiran Mbwani wakati akielezea huduma za benki hiyo mbele ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bi Pili Hassani kwenye Maonesho ya nane ya biashara yaliyohitimishwa mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga.

Maonesho hayo yalihusisha wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, mamlaka na taasisi za serikali, wadau wa utalii, wakulima na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya jiji hilo.

Aidha Mbwani alibainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa wajasiriamali na wakulima jijini humo benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na makundi hayo kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kilimo biashara kabla ya kuwapatia mikopo.

“ Hata hivyo kwa jiji la Tanga ushirikiano tunaupata zaidi kutoka kwa wakulima wakubwa hususani wa mazao ya katani na viungo wakati tukiendelea kuwaamsha zaidi wafanyabiashara wadogo na wakulima wadogo. Uamshwaji huu unafanyika kupitia mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali na elimu kuhusu mikopo sahihi tunayoitoa kwa wakulima.’’ Alisema

Alizitaja baadhi ya huduma mbalimbali mahususi kwa makundi hayo kuwa ni pamoja na akaunti za NBC Shambani, Kua Nasi, akaunti ya malengo, akaunti ya Johari ambayo ni mahususi kwa ajili ya wanawake pamoja na huduma za mikopo.

Mbali na kushiriki maonesho hayo benki ya NBC ilikuwa ni moja ya wadhamini muhimu wa maonesho hayo yaliyofanyika kwa mafanikio makubwa ambapo yalivutia washiriki wengi zaidi huku pia ikishuhudiwa mamia ya wakazi wa jiji hilo wakijitokeza kutembelea maonesho hayo.








Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya NBC tawi la Tanga Bw Aljiran Mbwani (Kulia) akipokea cheti cha shukrani ya ushiriki na udhamini kutoka kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Bi Pili Hassan ikiwa ni utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha Maonesho ya nane ya biashara yaliyomalizika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga.





Ofisa Masoko Benki ya NBC tawi la Tanga Bw Alli Tupa (Kushoto) akieleza huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wageni waliotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya nane ya biashara yaliyomalizika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga.


Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya NBC tawi la Tanga Bw Aljiran Mbwani (Kushoto) akieleza huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa mmoja wa wageni waliotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya nane ya biashara yaliyomalizika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga.



Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya NBC tawi la Tanga Bw Aljiran Mbwani (Kulia) akieleza huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Bi Pili Hassan (wa pili kushoto) wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya nane ya biashara yaliyomalizika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga.



Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya NBC tawi la Tanga Bw Aljiran Mbwani (Kulia) akieleza huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa mmoja wa wageni waliotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya nane ya biashara yaliyomalizika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga.

WEKA KETE KWENYE NAMBA ZAKO ZA BAHATI KWENYE SLOTI EUROPEAN ROULETTE YA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET

$
0
0

  

*Chagua kete zako, subiri gurudumu likupe ushindi na European Roulette

Sloti ya European Roulette

Ukiwa unaelekea mwisho wa wiki yako, pitia duka la Meridianbet ili uweze kujiweka kwenye nafasi ya kutengeneza mkwanja mrefu. Sloti ya European Rouletteiliyopo kwenye Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, inaweza kukupa ushindi mkubwa.


European Rouletteni moja wa michezo rahisi na inayopendwa na wachezaji wengi wa michezo ya kasino, mchezo huu umetengenezwa na Habanero. Meridianbet imekusogezea sloti hii ili kukuletea ushindi mkubwa. Mchezo huu una gurudumu la Roulettelenye namba, mpira na meza yenye namba za kuchagua.  Chagua namba moja au kadhaa ambazo unahisi mpira utasimama, acha gurudumu lizunguke likuletee ushindi wa kibingwa! 


Namna ya Kucheza Sloti ya European Roulett

Ukiingia kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, chagua European Roulette. Hapo utakutana na gurudumu la Roulette linalozunguka, meza yenye namba 36.  Weka kete zako kwa kuchagua namba unazohisi mpira wa gurudumu utafikia, kisha weka dau lako. Unaweza kuchagua namba zote kulingana na dau lako. Katika gurudumu la namba za Roulette, utaona rangi nyekundu na nyeusi yenye namba tofauti tofauti, isipokuwa namba 0 tu ambayo ina rangi ya kijani. 


Baada ya kuona umechagua kete zako vizuri, bonyeza kitufe cha "play" kisha subiri mshindo wa kibingwa. Baada ya ushindi, unaweza kurudia mzunguko kwa kubonyeza "Rebet". 


Usidanganyike! European Roulette kutoka Meridianbet inaweza kurudishia mpaka 98.65% ya dau lako! Ukichagua kete zako za bahati basi kwa hakika utapata ushindi mnono sana!


Jiunge sasa na Meridianbet na ufaidi odds, bonasi na promosheni kabambe!

RAIS SAMIA AFUTA MASHAMBA 11 KILOSA

$
0
0
Wananchi wa kijiji cha Kimamba wakimsikiliza waziri wa Ardhi na maendeleo ya makazi, Wiliam Lukuvi.


Na Farida Said, Morogoro
RAIS wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suruhu Hassan amefuta mashamba 11 yenye ukubwa wa ekari 24119 na kufufua mashamba 49 yenye ekari 45788.3 ambayo yamefutwa hatimiliki yake wilayani kilosa Mkoa wa Morogoro na kuagiza mashamba hayo kugawiwa kwa wananchi ambao hawana mashamba ya kulima.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kimamba Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amesema Mhe Rais Samia ametoa Ekari 1000 kwa kijiji hicho kama kifuta jasho hivyo ardhi hiyo isitumike kuwa chanzo cha migogoro ya Ardhi.

“Ardhi hii imetolewa na Mhe Rais kwa ajili ya kulima katani na sisi tutafurahi zaidi kama mtawakaribisha wawekezaji wakubwa waje kulima katani hapa ili waweze kuinua uchumi wa wanakimamba”.alisema Waziri Lukuvi.

Aidha amesema wizara ya Ardhi imetuma tume itakayoongozwa na kaimu Kamishina wa Ardhi Mkoa wa morogoro katika kuhakikisha mashamba yote yaliotolewa na Mhe Rais yanapangiwa matumizi bora ya ardhi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Morogoro Bwana Martin Shigela amemuhakikishia Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kuwa atawashughulikia viongozi wote wa vijiji wanaosababisha migogoro ya Ardhi katika Wilaya ya Kilosa na Mkoa kwa ujumla

Ameongeza kuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya Ardhi ni viongozi wa vijiji ambao wanauza mashamba bila ya kufuata taratibu na kusababisha migogoro isiyokuwa ya lazima na kuutia doa Mkoa na kuufanya kuwa kitovu cha migogoro ya Ardhi.

Nae Mbunge wa Jimbo la Kilosa ambaye pia ni Waziri wa katiba na sharia Mhe Palamagamba Kabudi Akizungmza na wananchi wa vijiji vya Kimamba na Ilonga amewataka wananchi kutunza Ardhi waliopatiwa na Mhe Rais kwa ajili ya kilimo.

Nao wakazi wa Wilaya ya kilosa wamemshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hasan kwa kuwarudishia mashamba hayo kwa ajili ya kilimo cha katani kwani wengi walikuwa wanatamani kulima katani lakini hawana maeneo ya kulima kutokana na mshamba mengi kumilikiwa na Taasisi mbalimbali.

Kampuni ya LG Electronics yafungua duka jipya la pili Mlimani City jijini Dar

$
0
0

Kampuni ya LG Electronics imezindua duka jipya la pili na la kisasa katika eneo la Mlimani City Mall jijini Dar kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kupata vifaa vya kampuni hiyo kwa urahisi ambavyo ni rafiki kwa mazingira.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar na kushuhudiwa na umati wa watu mbalimbali waliohudhuria kujionea baadhi ya bidhaa hizo za kisasa na za kiteknolojia ambazo ni pamoja na friji, televisheni, mashine za kufua nguo na vifaa vingine.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim alisema duka hilo ni pili hapa Tanzania baada ya jana kuzindua duka la kwanza katika mitaa ya Posta karibu na Mnara wa saa jijini Dar.

“Posta na Mlimani City ni maeneo mwafaka kabisa kwa sababu ya wateja wengi wanatembelea maeneo hayo na tumejionea namna mazingira ya biashara Tanzanaia yalivyochangamka. Tunaahidi kuwapa wateja wetu huduma na bidhaa nzuri ili wajisikie fahari wakati wanafanya manunuzi kwani watahudumiwa na wafanyakazi wetu wenye utaalamu wa hali ya juu”

“Katika miaka michache iliyopita, tumekuwa tukitanua wigo na uwepo wetu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tuna mpango wa kuendelea kukuza bidhaa zenye hadhi ya premium na kuwapa wateja wetu bidhaa wanazotarajia wao binafsi na kama biashara kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa zaidi ya daraja la kwanza. Tutawapa wafanya biashara wa Tanzania fursa nzuri ya kufanya kazi na sisi mfano mzuri ukiwa ni MeTL ambaye ni msambazaji mkuu wa bidhaa zetu za LG hapa Tanzania pamoja na dealers kama F&S ambaye ni mfanyabiashara wa kwanza katika mpango wetu wa thamani wa Tanzanite Club Tanzania” alisema Kim.

Aidha, Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya MeLT, Fatema Dewji ametoa wito kwa Watanzania kutumia vifaa vya kielektroniki kutoka kampuni ya LG kwa kuwa ni vifaa ambavyo rafiki kwa mazingira.

Dewji ametoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa duka la pili la kampuni hiyo ya LG Electronics lililopo Mlimani City Mall jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alisema MeLT inashirikiana na LG katika usambazaji wa vifaa vya kielektroniki kutoka LG hapa nchini ambavyo ni pamoja na runinga, mashine za kufua nguo, friji na vifaa vingine.

“Vifaa hivi vina ubora wa juu lakini pia vinatumia teknolojia mpya ambayo inatumia umeme mdogo na rafiki kwa mazingira ndio maana hata sasa tunaona kuwa Watanzania wamekubali bidhaa za LG hii ina maanisha kuwa Tanzania kuna soko kubwa” alisema.

Kauli hiyo ya pia iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Mauzo wa MeLT, Hussein Dewji ambaye alitoa wito kwa Watanzania kutembelea maduka hayo ya LG ili kujionea bidhaa bora na kufanya uamuzi sahihi katika ununuzi wa bidhaa za majumbani mwao.

Kwa upande wake Henry Chami ambaye ni mwakilishi kampuni ya F&S inayojishughlisha na uuzaji na usambaji wa bidhaa za kielekroniki, alisema katika kipindi cha mwezi mmoja Watanzania watapa fursa ya kununua bidhaaza LG katika dula hilo la Mlimani City kwa bei punguzo hadi asilimia 25.

“Ofa hiyo inalenga kutoa motisha kwa Watanzania kupata bidhaa bora za LG kwa sababu mbali na ubora na teknolojia ya hali ya juu iliyotumika kutengeneza pia upatikanaji wake ni wa urahisi zaidi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa vya kielektroniki vya kampuni hiyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.

Mwakilishi wa kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kielektroniki-F&S, Henry Chami (katikati), akikata utepe kuashiri uzinduzi wa duka la pili la vifaa vya kielektroniki kutoka Kampuni ya LG Mlimani City jijini Dar. Kulia ni Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim na kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa MeLT, Hussein Dewji.

Meneja Masoko kutoka kampuni ya LG Electronics, David Kessy (wa kwanza kushoto), pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Masoko wa MeLT, Fatema Dewji ambao ni washirika wa usambazaji wa vifaa vya LG, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa hivyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.

Kampuni ya LG Electronics yafungua duka jipya la pili Mlimani City jijini Dar

$
0
0
Kampuni ya LG Electronics imezindua duka jipya la pili na la kisasa katika eneo la Mlimani City Mall jijini Dar kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kupata vifaa vya kampuni hiyo kwa urahisi ambavyo ni rafiki kwa mazingira.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar na kushuhudiwa na umati wa watu mbalimbali waliohudhuria kujionea baadhi ya bidhaa hizo za kisasa na za kiteknolojia ambazo ni pamoja na friji, televisheni, mashine za kufua nguo na vifaa vingine.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim alisema duka hilo ni pili hapa Tanzania baada ya jana kuzindua duka la kwanza katika mitaa ya Posta karibu na Mnara wa saa jijini Dar.

“Posta na Mlimani City ni maeneo mwafaka kabisa kwa sababu ya wateja wengi wanatembelea maeneo hayo na tumejionea namna mazingira ya biashara Tanzanaia yalivyochangamka. Tunaahidi kuwapa wateja wetu huduma na bidhaa nzuri ili wajisikie fahari wakati wanafanya manunuzi kwani watahudumiwa na wafanyakazi wetu wenye utaalamu wa hali ya juu”

“Katika miaka michache iliyopita, tumekuwa tukitanua wigo na uwepo wetu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tuna mpango wa kuendelea kukuza bidhaa zenye hadhi ya premium na kuwapa wateja wetu bidhaa wanazotarajia wao binafsi na kama biashara kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa zaidi ya daraja la kwanza. Tutawapa wafanya biashara wa Tanzania fursa nzuri ya kufanya kazi na sisi mfano mzuri ukiwa ni MeTL ambaye ni msambazaji mkuu wa bidhaa zetu za LG hapa Tanzania pamoja na dealers kama F&S ambaye ni mfanyabiashara wa kwanza katika mpango wetu wa thamani wa Tanzanite Club Tanzania” alisema Kim.

Aidha, Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya MeLT, Fatema Dewji ametoa wito kwa Watanzania kutumia vifaa vya kielektroniki kutoka kampuni ya LG kwa kuwa ni vifaa ambavyo rafiki kwa mazingira.

Dewji ametoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa duka la pili la kampuni hiyo ya LG Electronics lililopo Mlimani City Mall jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alisema MeLT inashirikiana na LG katika usambazaji wa vifaa vya kielektroniki kutoka LG hapa nchini ambavyo ni pamoja na runinga, mashine za kufua nguo, friji na vifaa vingine.

“Vifaa hivi vina ubora wa juu lakini pia vinatumia teknolojia mpya ambayo inatumia umeme mdogo na rafiki kwa mazingira ndio maana hata sasa tunaona kuwa Watanzania wamekubali bidhaa za LG hii ina maanisha kuwa Tanzania kuna soko kubwa” alisema.

Kauli hiyo ya pia iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Mauzo wa MeLT, Hussein Dewji ambaye alitoa wito kwa Watanzania kutembelea maduka hayo ya LG ili kujionea bidhaa bora na kufanya uamuzi sahihi katika ununuzi wa bidhaa za majumbani mwao.

Kwa upande wake Henry Chami ambaye ni mwakilishi kampuni ya F&S inayojishughlisha na uuzaji na usambaji wa bidhaa za kielekroniki, alisema katika kipindi cha mwezi mmoja Watanzania watapa fursa ya kununua bidhaaza LG katika dula hilo la Mlimani City kwa bei punguzo hadi asilimia 25.

“Ofa hiyo inalenga kutoa motisha kwa Watanzania kupata bidhaa bora za LG kwa sababu mbali na ubora na teknolojia ya hali ya juu iliyotumika kutengeneza pia upatikanaji wake ni wa urahisi zaidi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa vya kielektroniki vya kampuni hiyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.

Mwakilishi wa kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kielektroniki-F&S, Henry Chami (katikati), akikata utepe kuashiri uzinduzi wa duka la pili la vifaa vya kielektroniki kutoka Kampuni ya LG Mlimani City jijini Dar. Kulia ni Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim na kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa MeLT, Hussein Dewji.

Meneja Masoko kutoka kampuni ya LG Electronics, David Kessy (wa kwanza kushoto), pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Masoko wa MeLT, Fatema Dewji ambao ni washirika wa usambazaji wa vifaa vya LG, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa hivyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.

TBS YAWAFUNDA MAWAKALA WA FORODHA NA WAFANYABIASHARA WA MAHINDI MPAKANI HOROHORO TANGA

$
0
0

 SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wa mahindi na nafaka nyengine katika mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga Mkoani Tanga ikiwa ni kuwapa elimu ya namna taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafirisha mahindi kwenda nje ya mipaka nchi.


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga amesema wafanyabiashara hawana budi kuhakikisha mahindi wanayonunua kama yamezingatia kanuni bora za kulimo ili kuzuia fangasi wanaoweza kusababisha sumu kuvu kwenye mahindi.

Alisema wafanyabiashara hao wanatakiwa kujua mahindi wanayokuwa wakinunua yanayotoka wapi ili kuweza kuepuka hasara inayoweza kujitokeza pindi mahindi yatakapokuwa na sumu kuvu.

“Ni muhimu sana kwa wafanyabiashara kujua Mahindi wanayoyanunua yanazalishwaje kwani ni muhimu sana kujua yule anayekuuzia mahindi kwa lengo la kujua kama anafuata kanuni bora za kilimo kutokana na kwamba inakupa uhakika na ukinunua haitaleta shida kwenye usafirishaji”Alisema Msasalaga.

“Mafunzo haya yatawasaidia wafanyabiashara namna ya mahindi yanavyopokelewa,kuna taratibu za kupeleka mahindi nje ya Nchi na kila Nchi ina namna ya kulinda usalama wa wananchi wake”alisema Msasalaga.

Akielezea namna ya sumu kuvu iweze kuepukika,Msasalaga amesema ni lazima kanuni bora za usindikaji wa mahindi na mnyonyoro mzima wa uzalishaji uwe umefuatwa huku akiwataka wafanyabiashara wafuate taratibu ambazo zinatakiwa kwa kuwa nchi inayopokea bidhaa ndio inayotoa sharti ya kupokea mizigo.

Semina hiyo inafanyika katika Mikoa mitatu yenye Mipaka ya Holili mkoani Kilimanjaro,Namanga Mkoani Arusha na Horohoro Mkoani Tanga


Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga
akisistiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wa mahindi na nafaka nyengine katika mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga Mkoani Tanga ikiwa ni kuwapa elimu ya namna taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafirisha mahindi kwenda nje ya mipaka nchi kushoto ni Meneja wa TBS Kanda ya Kaskazini Happy Brown


Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga akisistiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wa mahindi na nafaka nyengine katika mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga Mkoani Tanga ikiwa ni kuwapa elimu ya namna taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafirisha mahindi kwenda nje ya mipaka nchi

DKT Candida Shirima kutoka TBS akitoa mada wakati wa semina hiyo kuhusu Sumu  kuvu,Visababishi,Madhara yake na namna ya kuhifadhi Mazao kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti
Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga

REQUEST FOR SUBMISSION OF BANKABLE PROJECTS FOR THE AFRICAN INVESTMENT FORUM 2021

$
0
0

  


 


Rais Samia amteua CEO NMB kuchakata Haki za Wanawake Kiuchumi

$
0
0

  

RAIS wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, kuwa mmoja wa wanawake watakaoshiriki mchakato wa kujadili na kupatia ufumbuzi Haki za Wanawake Kiuchumi.

Rais Samia ameyasema hayo leo, wakati akihutubia Mkutano wa Wanawake uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ulioshirikisha takribani wanawake 10,000, wakiwemo wabunge wanawake, madiwani, wajasiriamali na Mama Lishe, waliowawakilisha wanawake wote nchini.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Samia alieleza mikakati mbalimbali ya Serikali yake inayolenga kuleta Usawa wa Kijinsia, moja ya eneo ambalo yeye aliposhiriki Mkutano wa Afrika na Ufaransa kwa njia ya video, alilichagua baada ya kupewa heshima ya kuchagua eneo la Kumjenga Mwanamke wa Afrika.

"Wakati wa Mkutano wa Afrika na Ufaransa, uliofanyika kwa njia ya video, kwenye suala la Usawa wa Kijinsia, nilipewa heshima ya kuchagua eneo moja la Kumjenga Mwanamke ili tulisimamie na tuwe 'championi' wa eneo Hilo.

"Tanzania tumepewa heshima hiyo na Mimi nikachagua eneo la Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke, kwa kutambua kuwa eneo hilo ni nguzo muhimu sana katika kuleta Usawa wa Kijinsia.

"Hivyo basi, naomba wadau tushirikiane katika hilo. Najua kati yetu hapa, nina vijana wazuri kwenye mabenki, wakiongozwa na ndugu yangu wa NMB (Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna). Huyu ni mmoja kati ya Wanawake niliowachagua watakaoshiriki jambo hili, sambamba na wengine walio kwenye Sekta ya Uchumi," alisema Rais Samia.

Alibainisha kuwa, Zaipuna na wanawake wengine aliowachagua, jukumu lao kuu litakuwa ni kumsaidia Rais kufanya uchambuzi yakinifu na wa kina juu ya hali halisi ilivyo katika suala zima la Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke ndani ya Tanzania na Afrika kwa ujumla wake.

Aliongeza kuwa, jopo hilo litapaswa kuangalia ni maeneo gani yana mapengo na maeneo gani Serikali za Afrika zingependa zisaidiwe na Ufaransa na mipango yao ni kwenda umbali gani, ambayo watayawasilisha kwa nchi hiyo ya Ulaya ili ione namna ya kuisaidia Afrika kufikia Usawa wa Kijinsia kupitia Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke.

Viewing all 48952 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>