Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48950 articles
Browse latest View live

Brigedia Jenerali Ibuge akagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji

$
0
0

 MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefanya ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa kwa kukagua eneo la Mkenda lililopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kupitia wilaya ya Songea.

Brigedia Jenerali Ibuge amekagua daraja la Mkenda Mto Ruvuma linalotenganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji, amezungumza na askari wa Msumbiji waliopo mpakani,ametembelea kivuko cha Mitomoni,kupitia Mto Ruvuma,amekagua soko la kimataifa la Mkenda na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mkenda.

Akizungumza na watumishi wa Idara za uhamiaji,Mamlaka ya Mapato Tanzania,polisi na Usalama waliopo eneo la Mkenda,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amelitaja lengo la serikali kuwaweka watumishi hao mpakani ni kusimamia maslahi ya taifa.

 Amewataka watumishi hao kila mmoja katika Idara yake kushirikiana na kufanya kazi kwa tija na ufanisi kwa maslahi ya watanzania.

“Sasa hili la ushirikiano nataka kusisitiza,mpo mbele ya mpaka wetu ,kumbukeni kuna changamoto kubwa ya ugaidi inayotukabili kwenye mpaka wetu na Msumbiji ,huu sio wakati wa kuchukulia vitu poa’’,alisisitiza Brigedia Jenerali Ibuge.

Hata hivyo amewatahadharisha watumishi hao wasipokuwa na muunganiko wanapobaini watuhumiwa wakiwemo wahamiaji haramu, biashara zinazotia mashaka na vitendo vya rushwa wanaweza kuharibu mfumo mzima wa Mkoa na Taifa kwa ujumla kutokana na uzembe na ujinga wa mtumishi mmoja.

Kuhusu watumishi wa TRA waliopo mpakani,RC Ibuge amesema licha ya ukweli kuwa mapato ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,hata hivyo ametaka ushirikiano wa kuangalia mazingira ya kiforodha yaangaliwe kiulinzi na usalama kwa kudumisha mawasiliano na vyombo vingine vya usalama.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa pole na kuwafariji wananchi wa kijiji cha Mkenda kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali ya majini kwenye mto Ruvuma hivi karibuni.  

Hata hivyo ametoa rai kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mkenda na wananchi kwa ujumla kushirikiana na vyombo vya usalama vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ili  kujilinda kwa ajili ya usalama wa wananchi na Taifa kwa ujumla. 

Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Kituo cha Uhamiaji Mkenda,Mratibu Msaidizi wa Uhamiaji Upendo Kikudo amesema kituo hicho kinafanya kazi kwa ushirkiano na Idara nne ambazo ni  Uhamiaji,Polisi,TRA na Usalama wa Taifa.

Amezitaja changamoto zinazokikabili kituo hicho ni ukubwa wa mpaka kutokana na jiografia ya eneo lililozungukwa na Mto Ruvuma na misitu,hali ya machafuko inayoendelea nchini Msumbiji,uwepo wa vipenyo vingi vilivyo rasmi na visivyo rasmi,mawasiliano,miundombinu ya barabara,huduma za afya na ukosefu wa nishati ya umeme.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akikagua kivuko cha mto Ruvuma eneo la Mitomoni wilayani Songea

Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na wilaya ya Songea,kukagua daraja la Mkenda Mto Ruvuma wilayani Songea ambalo linatenganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji

Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akipata maelezo ofisi ya uhamiaji eneo la mpakani upande wa pili wa nchiMsumbiji.

MAKONGORO NYERERE AIPONGEZA SIMANJIRO KWA HATI SAFI

ZAWADI ZA KAMPENI YA 'TWENDE MJINI NA M- PESA' ZAANZA KUTOLEWA

$
0
0

 


KAMPENI ya 'Twende Mjini na M-Pesa' inayoendeshwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imeendesha droo ya kwanza na kuwapata washindi watano waliojishindia bodaboda mpya (Boxer BM 125X) na mmoja akijishindia bajaji mpya aina ya a TVS King GS.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo iliyodhuriwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha na wanahabari leo Mkoani Dar es Salaam Afisa wa Masoko wa M-pesa Fredrick Mwamyalla amesema, kama walivyotoa ufafanuzi katika uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba ndani ya wiki 8 watumiaji wa huduma ya M- PESA watapata fursa ya kujishindia bajaji, bodaboda na gari ya kisasa aina ya Toyota Corolla Cross (SUV) la mwaka 2021 ambalo litatolewa katika grand finale la kampeni hiyo.

Amesema kuwa kampeni ya Twende Mjini na M-Pesa ni ahadi ya Vodacom katika kuboresha maisha ya jamii na kampeni hiyo inawahusisha watumiaji wote wa M-pesa wakiwemo mawakala nchi nzima.

"Kampeni hii inawalenga watumiaji wote wa M-pesa ambao wataingia katika droo ya ushindani kwa kutumia huduma za M-Pesa kwa kutuma pesa kutoka akaunti ya benki kwenda M-Pesa, kutuma pesa kwa wateja wa Vodacom na wateja wa mitandao mingine, kulipa bili na huduma nyingine na moja kwa moja wataingia katika droo ya ushindi." Amesema.

Aidha amewataka wateja wa mtandao huo kupokea namba ya huduma kwa wateja 0754 100 100 ili kutopitwa na bahati zao na wataendeleza kampeni ya  kujitambulisha kwa wateja kupitia jumbe fupi 'Sms' pamoja na kupitia mitandao yao ya  jamii ili wateja na watumiaji wa huduma za M-Pesa wasipitwe na zawadi hizo.

Katika kampeni hiyo waliojishindia bodaboda ni Godfrey Mgeni (Morogoro,) Francis Kwale, Wakala wa huduma za M-Pesa (Dar es Salaam,)  Zanzibar gateway Wakala wa huduma za M-Pesa (Zanzibar,) Ramadhan Nkondo (Dar es Salaam) Pili Joseph (Dar es Salaam.) huku Bajaji mpya ikienda kwa Nyangije Basondole kutoka Dar es Salaam.



Mchakato wa kuwapata washindi wa zawadi kupitia kampeni ya Twende Mjini na M-PESA ukiendelea katika ofisi kuu za Vodacom Tanzania Dar es Salaam.




Benki Ya Exim Yakabidhi Vifaa Vya Usafi Kwa Halmashauri Ya Jiji Dar es Salaam

$
0
0
Maadhimisho Siku Ya Mazingira Duniani:

Benki Ya Exim Yakabidhi Vifaa Vya Usafi Kwa Halmashauri Ya Jiji Dar es Salaam.

Dar es Salaam; Juni 1, 2021:Benki ya Exim imekabidhi vifaa vya usafi kwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa Juni 5 mwaka huu.

Hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kutunza mazingira unaofahamika kama Exim Go Green Initiative.

Akipokea msaada huo jijini Dar es Salaam mapema hii leo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa msaada huo ,alitumia fursa hiyo kuzialika taasisi mbalimbali kushiriki kwenye utunzaji wa maeneo ya asili ikiwemo fukwe za bahari, kupanda miti na maua kwenye maeneo ya wazi na hifadhi za barabara pamoja kuhifadhi bustani zilizopo maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

“Jitihada kama hizi zinazooneshwa na benki ya Exim sambamba na shughuli nyingine nyingi zitaendelea wiki nzima kuanzia Juni mosi hadi Juni 5 ambayo ndio siku ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira.” Alibainisha Bw Ng’wilabuzu.huku akiwahimiza wakandarasi wanaotoa huduma ya uzoaji taka katika jiji hilo kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kutosha na kutoa huduma inayokidhi mahitaji ya wananchi kwa wakati.

Alisema maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali inayolenga kuongeza hamasa za utunzaji wa mazingira ikiwemo mikutano ya Kitaaluma juu ya masuala ya mazingira, matamasha ya maonyesho, kampeni za usafi wa mazingira, shughuli ambazo zitaendelea kwa wiki nzima kuanzia Juni mosi.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim, Bw Stanley Kafu alisema msaada huo unahusisha vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi ikiwemo matoroli ya kubebea takataka, vyombo vya kuhifadhi takataka, mafagio, reki pamoja na makoleo .

"Siku ya Mazingira Duniani ni siku ambayo inahitaji jitihada za pamoja ili kuhakikisha suala zima la usafi na muonekano wa mazingira linapatiwa ufumbuzi. Hiyo ndio sababu benki ya Exim tunaamini sana umuhimu wa kusaidia mipango ya mazingira ambayo ina faida za moja kwa moja kwa jamii. ’’ alisema Bw Kafu.

Mbali na kuongoza kampeni mbalimbali za upandaji miti ikiwemo ile ya upandaji miti 10,0000 iliyofanyika hivi karibuni jijini Dodoma kwa ushirikiano na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, benki hiyo pia imekuwa imekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa bustani mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya majiji hapa nchini ikiwemo Dar es salaam.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania Bw Stanley Kafu (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija (katikati) vifaa vya usafi vilivyotolewa na benki hiyo ili kuimarisha hali ya usafi katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa Juni 5 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi Charangwa Makwiro (wa tatu kushoto) na pamoja na wafanyakazi wa Exim Bank.

SAMATTA ATEMBELEA COCA-COLA TANZANIA, AZINDUA KAMPENI YA WASHA MDUNDO

$
0
0

Meneja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto), akimuonyesha nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta hatua za utengenezaji wa kinywaji cha Coca-Cola wakati alipotembelea kiwandani hapo. Samatta ambaye pia ni mwakilishi wa Coca-Cola Tanzania wa kuitangaza chapa ya kampuni hiyo katika kampeni zake ili kuwahamasisha Watanzania kufikia ndoto zao, alishirika kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO.’

 Nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta (Kulia), akipata maelekezo kutoka kwa Meneja wa Kitecho cha Ufungaji cha Coca-Cola Kwanza, Jamah Adam (Kushoto) kuhusu mchakato mzima wa utengenezaji wa kinywaji cha Coca-Cola wakati alipotembelea kiwandani hapo. Samatta ambaye pia ni mwakilishi wa Coca-Cola Tanzania wa kuitangaza chapa ya kampuni hiyo katika kampeni zake ili kuwahamasisha Watanzania kufikia ndoto zao, alishirika kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO.’

 

Menenja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto), akimkabidhi zawadi nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta wakati alipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kujionea mchakato mzima wa utengenezaji wa kinywaji cha Coca-Cola. Samatta ambaye pia ni mwakilishi wa Coca-Cola Tanzania wa kuitangaza chapa ya kampuni hiyo katika kampeni zake ili kuwahamasisha Watanzania kufikia ndoto zao, alishirika kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO.’        

 

Nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta (Katikati), akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mauzo wa Coca-Cola Kwanza, Eric Ongara (Kulia) kuhusu kinywaji cha Coca-Cola na shughuli zake nchini wakati alipotembelea kiwandani hapo. Aikuatilia kwa makini mazungumzo hayo kulia ni Mkurugenzi wa Uchukuzi wa Coca-Cola Kwanza, Haji Ally Samatta ambaye pia ni mwakilishi wa Coca-Cola Tanzania wa kuitangaza chapa ya kampuni hiyo katika kampeni zake ili kuwahamasisha Watanzania kufikia ndoto zao, alishirika kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO.’   

        

Nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta (Kushoto), akijibu maswali ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati alipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kujionea mchakato mzima wa utengenezaji wa kinywaji cha Coca-Cola. Pamoja naye kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Samatta, Habuna Habibu Makanyangiro. Samatta ambaye pia ni mwakilishi wa Coca-Cola Tanzania wa kuitangaza chapa ya kampuni hiyo katika kampeni zake ili kuwahamasisha Watanzania kufikia ndoto zao, alishirika kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO.’       

  

 DJ D Ommy au maarufu kama ‘The International DJ’ naye alikuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO’ ya kampuni ya Coca-Cola Tanzania ambayo ilihudhuriwa na kuzinduliwa rasmi na Nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta (hayupo pichani) wakati alipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kujionea mchakato mzima wa utengenezaji wa kinywaji cha Coca-Cola.   

 Ubao wa maelekezo ya namna ya Watanzania kushiriki katika kampeni ya ‘WASHA MDUNDO’ iliyozinduliwa na kinywaji cha Coca-Cola Tanzania. Uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo ulihudhuriwa na nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta (hayupo pichani) wakati alipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kujionea mchakato mzima wa utengenezaji wa kinywaji cha Coca-Cola.  

Menenja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto), akiwa amepozi katika picha na nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta wakati alipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kujionea mchakato mzima wa utengenezaji wa kinywaji cha Coca-Cola. Samatta ambaye pia ni mwakilishi wa Coca-Cola Tanzania wa kuitangaza chapa ya kampuni hiyo katika kampeni zake ili kuwahamasisha Watanzania kufikia ndoto zao, alishirika kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO.’          

 

JACKPOT ZA NGUVU NA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET

$
0
0

  C:\Users\user\Downloads\Wild-Hot-40_PR.png

*Jihakikishie Ushindi Mkubwa Kupitia Sloti ya Wild Hot 40.

Sloti ya Wild Hot 40 

Ushindi babkubwa na Meridianbet yenye kukuletea Odds Kubwa, Ofa na Bonasi za kukata na shoka. Wiki hii, Meridianbet kupitia kasino yake ya mtandaoni, inakuletea sloti bomba ya kizamani inayohusisha matunda iitwayo Wild Hot 40.

Wild Hot 40 ni sloti ambayo inawavutia watu wengi kutokana na muonekano wake. Sloti hii imetengenezwa na watengenezaji maarufu wa sloti za kizamani waitwao Fazi. Kasino hii ya mtandaoni ya Meridianbet, inakuhakikishia ushindi wa nguvu kwa kuwa ina jackpot3 kubwa zenye kukuletea faida ambazo ni Gold, Platinum na Diamond

Kazi ni kwako tu, unasubiri nini? Cheza sasa na Meridianbet ukijihakikishia ushindi mkubwa! Tembelea https://www.meridianbet.co.tz na ushinde.

Jinsi ya Kucheza Sloti ya Wild Hot 40

Sloti zenye maudhui ya kizamani zimekuwa maarufu karne na karne. Umaarufu wake umetokana na uchezaji wake kuwa rahisi na alama zake zisizosahaulika (alama za matunda) na muundo wa kolamu5 na mistari40 ya malipo.

Matunda hayo ni Ndizi, Tufaa (Apple) na Strawberry ambapo ukipata alama hizi 5, utapata mara2.5 ya dau uliloliweka. Ukipatia alama 5 za Kengele, unarudishiwa mara5 ya dau uliloliweka. Ukipatia alama ya namba 7 za bahati, utapata mara10 ya dau uliloliweka. Ukipatia alama5 za Wild, utarudishiwa mara 25 ya dau uliloliweka wakati ukipatia alama 5 za Scatter utarudishiwa zaidi ya mara 500 ya dau lako. 

Sio hayo tu, sloti ya Wild Hot 40 kupitia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuja na Jackpot zenye kukuletea faida babkubwa bila kusahau chaguo la Gamble ambalo litakuletea mara 2 ya faida ulioipata. 

Tunaposema Meridianbet ni Nyumba yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa, tunamaanisha! Jiunge Meridianbet na ushinde! Vigezo na masharti kuzingatiwa.

WASHIRIKI JUMA LA ELIMU WAENDESHA MIJADALA YA ELIMU NAKUHAMASISHA JAMII

$
0
0

 

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Rorya, Gerald Ng'ong'a (kushoto) walioshika chepe wakiwaongoza wadau wa TEN/MET Shule ya Msingi Obwere kukishiriki katika shughuli za nguvu kazi kwenye ujenzi wa madarasa shuleni hapo ikiwa ni kuhamasisha wana jamii kushiriki moja kwa moja ujenzi wa miundombinu ya elimu.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Rorya, Gerald Ng'ong'a (kushoto) walioshika chepe wakiwaongoza wadau wa TEN/MET Shule ya Msingi Obwere kukishiriki katika shughuli za nguvu kazi kwenye ujenzi wa madarasa shuleni hapo ikiwa ni kuhamasisha wana jamii kushiriki moja kwa moja ujenzi wa miundombinu ya elimu.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kushoto) akizungumza na wanafunzi, wazazi, walimu, viongozi anuai na wadau wa elimu Sekondari ya Profesa Philemon Sarungi ikiwa ni kushirikishana fursa na changamoto zilizopo katika elimu kwenye maeneo yao na namna ya kuzitatua kuanzia ngazi ya jamii.

Wanafunzi Shule ya Sekondari Profesa Philemon Sarungi wakishiriki katika mijadala hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct, Faraja Nyalandu (kushoto) akizungumza na wanafunzi, wazazi, walimu, viongozi anuai na wadau wa elimu Sekondari ya Profesa Philemon Sarungi ikiwa ni kushirikishana fursa na changamoto zilizopo katika elimu kwenye maeneo yao na namna ya kuzitatua kuanzia ngazi ya jamii.

Mikutano na mijadala ikiendelea na makundi mbalimbali kushirikishana changamoto.

Mikutano na mijadala ikiendelea na makundi mbalimbali kushirikishana changamoto.

Mikutano na mijadala na wanafunzi ikiendelea kushirikishana utatuzi wa changamoto za elimu.

Mikutano na mijadala na walimu ikiendelea kushirikishana mbinu za utatuzi wa changamoto za elimu.

Mikutano na mijadala na walimu ikiendelea kushirikishana utatuzi wa changamoto za elimu.

Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za nguvu kazi.

Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za ujenzi kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.

Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za ujenzi kwa kufyatua tofali kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.

Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za ujenzi kwa kufyatua tofali kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa Greison Mgoi akishiriki katika shughuli za ujenzi kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (katikati) akishiriki shughuli za ujenzi katika maadhimisho juma la elimu.

Na Mwandishi Wetu, Rorya
WANACHAMA wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) leo wameanza kufanya mikutano na wazazi, wanafunzi, walimu na pamoja na viongozi huku wakishiriki katika shughuli za nguvu kazi kwenye ujenzi wa madarasa ikiwa ni kuhamasisha wana jamii kushiriki moja kwa moja ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu.

Wakishirikiana na viongozi wa elimu kuanzia ngazi ya kata hadi Wilaya ya Rorya wamefanya shughuli hizo katika Shule ya Msingi Obwere pamoja na Sekondari ya Profesa Philemon Sarungi ikiwa ni kushirikishana fursa na changamoto zilizooo katika elimu kwenye maeneo yao na namna ya kuzitatua kuanzia ngazi ya jamii yenyewe.

Akizungumza na wanajamii katika mikutano hiyo, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga alisema utatuzi wa changamoto zilizopo katika elimu unaanzia katika ngazi ya jamii kwa kushirikishana kwenye mijadala kabla ya kuanga kupanda ngazi za juu.

Bw. Wayoga alisema mikutano na mijadala inayofanyika ni mwendelezo wa shughuli za Maadhimisho ya Juma la elimu ambazo kitaifa zinafanyika wilayani Rorya. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni; Uwekezaji katika mifumo ya Elimu kwa malengo ya maendeleo endelevu (Financing Education System for Sustainable Development Goals), kauli inayoikumbusha jamii umuhimu wa juhudi ya pamoja kama wadau wa elimu, yaani serikali, Asasi za Kiraia, sekta binafsi, wanafunzi, wazazi na wananchi kwa ujumla.

Miongoni mwa mashirika wanachama na wadau walioshiriki katika shughuli za leo ni pamoja na PCI, Uwezo Tanzania, Haki Elimu, ADD International, Shule Direct, Sense International, Child Support Tanzania, Malala Foundation, Right to Play, RELI Tanzania, CAMFED, WeWorld, Pestalozzi Children’s Foundation, OCODE, PWC, SAZANI TRUST-ZANZIBAR, SAWO na TEN/MET Secretariat.

Mikutano na mijadala na walimu ikiendelea kushirikishana utatuzi wa changamoto za elimu.

WAMI/RUVU yasisitiza Nishati Mbadala, Kuhifadhi Vyanzo vya Maji

$
0
0

 

Walimbwende wanaoshiriki Mashindano ya Miss Dodoma 2021 wakiwa wapozi kwa picha ya Pamoja na Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu, Baada ya Kutembelea Banda hilo na Kujifunza Mambo mbalimbali kuhusiana na Shughuli za Bodi hiyo kwenye Usimamizi wa Rasilimali za maji.


Machapisho mbalimbali yanayoelezea kwa kina kuhusiana na Rasilimali za maji na umuhimu wake, ambayo yanapatikana kwenye banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu.

Mhandisi wa Rasilimali za Maji wa Bodi ya Maji Bonde la  / Wami / Ruvu akitoa Elimu kwa Wananchi mbalimbali kuhusu umuhimu wa Kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji ambao wamefika Kwenye Banda la Bodi hiyo katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Mjini Dodoma, ambapo yanafanyika Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani.
Mhandisi wa Rasilimali za Maji wa Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu, John Kassambili akielezea Umuhimu wa kutunza Mazingira hususani kwenye vyanzo vya Maji, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Mjini Dodoma, ambapo yanafanyika Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani. WAMI / RUVU yasisitiza Nishati Mbadala ili Kulinda na Kuhifadhi Vyanzo vya Maji 

KUELEKEA Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, ambayo huadhimishwa kila ifikapo June 5, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeelezea kujikita hasa kwenye kuihamasisha Jamii kuhusiana na Suala zima la Utunzaji wa Mazingira Kwenye Vyanzo vya Maji.

Imesema pamoja na Msisitizo huo, itaendelea kutoa Elimu kwa Makundi mbalimbali ya Wananchi kuhusiana na Matumizi ya Nishati Mbadala ikiwemo Gesi ama Nishati Banifu.

Mhandisi wa Rasilimali za Maji wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu John Kassambili akizungumza Wakati wa Maonesho ya Wiki ya Mazingira inayofanyika Mjini Dodoma kwenye Viwanja vya Jakaya Kikwete, amesema matumizi ya Nishati Mbadala yatasaidia Kupunguza Uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo mbalimbali vya maji ama Rasilimali za maji.

“Ukataji wa miti hovyo ni miongoni mwa viashiria hatarishi kwenye suala la utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo hivyo vya maji, ambapo matumizi ya nishati mbadala ndio tiba sahihi ya kuendelea kutunza na kuimarisha rasilimali za maji” alisema Mhandisi Kassambili.

Kwa Upande wake Bwana Mashaka  Amrilok ni miongoni mwa Baadhi ya Wananchi Waliotembelea kwenye maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani, akizungumzia  kuhusiana na Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira kwenye vyanzo vya maji, amesema Baada ya kutembelea Banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu amekiri kuridhishwa na Elimu aliyoipata kuhusu Mazingira na Umuhimu wa Matumizi ya Nishati Mbadala katika mizania ya Uhifadhi Endelevu wa vyanzo vya maji.

“ Nimejifunza zaidi kuhusu namna Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu inavyoshiriki katika kuangalia vyanzo vya Maji katika Mto Wami lakini pia katika Maeneo mengine ya Mikoa Mbalimbali nchini ikiwemo wanavyofanya Tathmini ya Maji yaliyoko Chini ya Ardhi na Juu ya Ardhi”.

Maonesho ya Wiki ya Mazingira yanaendelea mjini Dodoma na yakitarajia kufikia kilele chake June 5, huku yakibeba Kauli mbiu inayosema Tutumie  Nishati Mbadala ili kuongoa Mifumo Ikolojia.


WANUFAIKA 395 WA MKURABITA MUFINDI WAFURAHIA MAFUNZO YA KUWAINUA KIUCHUMI

$
0
0

 

Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kiuchumi wanufaika wa mpango huo waliorasimishiwa ardhi yao kwa kupatiwa hati miliki za kimila katika Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa Juni Mosi, 2021.

Walioshiriki mafunzo hayo walikuwa 395 ambapo walifundishwa jinsi ya kutumia hati miliki kuweka kama dhamana kukopea fedha benki na taasisi zingine za fedha ii kuinua mitaji ya miradi yao, kanuni bora za kilimo ili kupata mavuno mengi kwa heka moja, kuthaminisha rasilimali zao na hasa ardhi, jinsi ya kuweka kumbukumbu za mahesabu ya miradi yao, umuhimu wa kujiunga na ushirika na faida zake na faida za kuweka akiba benki na mikopo inayotolewa na benki hizo.

Pia walifundishwa jinsi ya kufuga nyuki na mazao yake ikiwemo asali, nta, chavua, sumu ya nyunki na thamani yake kwenye masoko. Wakati wa mafunzo hayo kikundi cha watumia maji walikabidhiwa msaada wa mizinga 30 iliyotolewa na Mkurabita.

Maofisa walioshiriki kutoa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu ni;Maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambao ni Afisa Ardhi Mteule, Leonard Jaka, Afisa Ushirika, Pili Mwaipaja, Afisa Kilimo, Mwamini Mwakyaka, Afisa Ufugaji Nyuki, Hamisi Hassan,Afisa Maendeleo ya Jamii, Joha Kambala na Afisa Upimaji Ardhi Imamu Sherukindo.

Kwa upande wa benki waliotoa mafunzo ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Gasper Mlala, Afisa Mikopo wa Benki ya Posta, TPB, Japhet Peter na Prosper Peter wa Benki ya Mucoba ambao kila mmoja alieleza masharti ya kujiunga, masharti ya ukopaji na faida zake. Benki zote hizo zinaruhusu kuweka hati miliki za kimila kuweka kama dhamana kukopa fedha.

Awali mafunzo hayo ambayo wengi waliyafurahia na kuomba Mkurabita kuwapelekea tena siku nyingine, yalifunguliwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Sailas Kiwuyo na kupata baraka za mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Igombavanu,Veronica Kilongumtwa.
Wananchi wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa mafunzo hayo.



Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mufindi, Joha Kambala akitia dodoso kwenye simu janja kwa kutumia mfumo wa Kobo.
Msaidizi Upimaji Ardhi wa Kijiji cha Lugodalutali, Felister Choga akiingiza taarifa za dodoso kwenye simu janja kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa wa Kobo.
Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu akiingiza taarifa za dodoso kwenye simu janja kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa wa Kobo.
Kwaya ya Mashahidi wa Uganda ikitumbuiza wakati mafunzo hayo.
Prosper Peter wa Benki ya Mucoba akiwaeleza wananchi umuhimu wa kuwa na tabia ya kuweka akiba fedha zao benki, kutumia hati miliki za kimila kukopa kupanua wigo wa miradi yao.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Gasper Mlala akiwahamasisha wananchi kujiunga na benki hiyo kwa kutoa kiingilio cha sh. 5000 na kuahidi kufungua wakala wa benki hiyo katika kijiji hicho.
Afisa Mikopo wa Benki ya Posta, TPB, Japhet Peter akielezea masharti ya kujiunga na benki hiyo, mikopo wanayotoa na faida zake.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mafunzo hayo.
Afisa Ushirika, Pili Mwaipaja akiwaeleza sheria na masharti ya kujiunga na ushirika na faida zake.
Wazee wakisikiliza kwa makini mwenendo wa mafunzo hayo.

Wananchi wakijiorodhesha kuanzisha chama cha Ushirika katika kijiji hicho.
Afisa Kilimo, Mwamini Mwakyaka akiwafundisha kanuni za kilimo na hasa kilimo bora cha zao la alizeti.
Afisa Upimaji Ardhi Imamu Sherukindo. akielezea faida za kurasimisha ardhi kwa kuiongezea thamani pamoja na kupata hati miliki.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Joha Kambala akiwafundisha jinsi ya kuunda vikundi na faida zake ikiwemo urahisi wa kupata mikopo na misaada mbalimbali.

Afisa Ufugaji Nyuki, Hamisi Hassan akielezea faida ya ufugaji nyuki na kutaja mazao yatokanayo ambayo ni asali, chavua, nta pamoja na sumu ya nyuki.

MKOA WA PWANI YASHUSHA KIKOSI CHA WACHEZAJI 100 KUSHIRIKI MICHUANO YA TAIFA UMITASHUMTA MTWARA

$
0
0

 JUMLA ya wachezaji wapatao 100 wamechaguliwa kwa ajili ya kuweza kuunda kikosi cha timu ya Mkoa wa Pwani ambacho kitashiriki katika kinyanga’nyoro cha michezo mbali mbali kwenye kivumbi cha Mashindano ya umoja wa michezo na taalumu kwa shule ya za msingi (UMITASHUMTA) ngazi ya Taifa ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake mwanzoni mwa mwezi huu Mkoani Mtwara.


Hayo yamebainishwa na Afisa Michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta wakati wa kufunga rasmi michuano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa na kubainisha kuwa kabla ya kuchagua kikosi hicho cha wachezaji 100 kuliweza kufanyika mashindano katika michezo mbali mbali ambayo yaliweza kuwajumuisha wanamichezo kutoka halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani na ndipo jopo la kamati ya michezo kwa kushirikiana na maafisa michezo waliweza kuwachagua wachezaji kwa kuzingatia vigezo.

Buleta aliongeza kuwa hapo awali wachezaji ambao walishiriki katika mashindano ya ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata kikosi hicho walikuwa zaidi ya 650 lakini kwa sasa baada ya michuano hiyo kumalizika waliweza kuwachagua baadhi ya wachezaji ambao wana vipaji na uwezo kwa lengo la kuweza kuunda kikosi cha Mkoa kilichokuwa bora.

“Tunashukuru hii hatua ya mwanzo tumeweza kuikamilisha ya kupata wachezaji 100 ambao wataunda timu ya Mkoa wa Pwani na kwamba sio kwamba wengine hawana uwezo lakini tumehakikisha kwamba tunawachagua wale wachazaji ambao wameweza kuonyesha uwezo wao katika kipindi chote za mashindano hayo na nia yetu kubwa ni kufanya vizuri katika mashindano ya Taifa,”alisema Buleta.

Aidha Buleta alifafanua kuwa kwa sasa mipango ambayo wameiweka ni kuiweka timu ya Mkoa kambini kwanza kwa muda nne hadi kwa ajili ya kuweza kuwapa fursa walimu na makocha waweze kutoa maelekezo mbali mbali ambayo yatawasaidia wachezaji kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo sheria na taratibu ambazo zitakwenda kutumika katika mashindano ya Taifa.

“Zoezi la kuchagua kikosi cha timu ya Mkoa wa Pwani kwa upande wetu tumelifanya kwa kuzingatia usawa katika kila pande na kwamba katika michuano hii tumeweza kuwachagua wachezaji katika michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa mikono, netiboli, Riadha, mpira wa wavu, pamoja na fani mbali mbali za ndani ikiwemo ngoma na kwaya.”alifafanua Buleta.

Katika hatua nyingine Buleta aliongeza kwamba katika michuano ya msimu wa mwaka huu wa 2021 wamejipanga vizuri hivyo wanatarajia kuipeperusha vema bendera ya Mkoa wa Pwani na kurudi na ubingwa na kuwaomba wadau, mashirika na umma na taasisi binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa sapoti ya hali na mali kwa kikosi hicho kilichoundwa cha Mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha injinia Martine Ntemo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kufunga mashindano hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani amewataka wanamichezo hao kuhakikisha kwamba wanajitadi kwa uwezo wao wote kufanya vizuri katika mashindano hayo ya Taifa kwa lengo la kuweza kuibuka na ubingwa na kurudi na vikombe ili kuutangaza vema Mkoa wa Pwani katika Nyanja ya michezo.

Pia Ntemo aliwasisitizia kwamba wanamichezo ho hao kuhakikisha wanachukua tahadhari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa mbali mbali na kuziagiza halmashauri kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya viwanja vya michezo kwa wanafunzi hao sambamba na kuwanunulia sare za michezo na kuwataka pia wanafunzi hao kuwa na nidhani katika kipindi chote na michuano hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha Robert Shilingi akitoa salamu zake alisema kuwa wachezaji wote ambao wamechagulia kunda kikosi cha timu ya Mkoa kupambana vilivyo na kutumia fursa hiyo katika kuonyesha vipaji uwezo walionao katika michuano hiyo ya ngazi ya taifa ili kurudi na ubingwa ambao utaweza kuwa na tija zaidi katika sekta ya michezo ndani ya Mkoa wa Pwani.


Baaadhi ya wanafunzi kutoka katika shule mbali mbali kutoka halmashauri mbali mbali wakiwa wanashangia baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa wa Pwani ambayo yamefanyika katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha, na hatimaye kuchaguliwa kwa wachezaji wapatao 100 ambao wataunda kikosi cha timu ya Mkoa wa Pwani.
 wanafunzi wa shule za msingi UMITASHUMTA ambayo yamefungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Injinia Martine Ntemo.

Wajasiriamali wameaswa kulipa kodi

$
0
0
Wajasiriamali wameaswa kulipa kodi

*Kulipa kodi kuunga mkono serikali kuweza kupeleka maendeleo

Na Mwandishi Wetu
WAJASILIAMALI Nchini wametakiwa kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kuhakikisha inawaletea maendeleo makubwa wananchi wake pamoja na kuongeza mapato zaidi Nchini.

Wito huo ulitolewa na Mjasiliamali maalufu Charles Sabiniani maarufu kama Lowasa, alipokuwa akizungumza na Wajasiliamali wanaofanya shughuli hizo huko Wilayani Chato Mkoani Geita alipofika kwa ajili ya kusalimia wanachato wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara kwa nyakati tofauti tofauti.

"Nimetembelea wajasiriamali pamoja na dereva bodaboda nikiwa naongea nao nimewapa elimu kuusu ulipaji kodi za Serikari pamoja na sadaka zitolewazo kwenye nyumba za ibada lakini nimewaelewesha kwamba wakiwa na utaratibu wa kulipa kodi wataendelea kufanya shughuli zao kwa uhuru zaidi na bila kubughudhiwa na mtu," alisema Lowasa, na kuongeza;

"Nimewambia wajasiriamali wengi wanakwepa kodi za Serikari ndio maana hawafanikiwi, unapolipa kodi Serikali inatutengenezea Shule, Hospital, Vituo vya Police, Barabara na huduma nyingine nyingi za kijamii ambazo ni kwa manufaa yetu."

Lowasa ambaye pia ni Kada wa CCM alisema kuwa, kutokana na hali hiyo wajasiliamali watakubaliana kwamba kodi wanazolipa pamoja na wafanyabiashara wengine wakubwa zinawapatia watanzania na Taifa kwa ujumla huduma mzuri na zenye kuleta tija zaidi tofauti na pale anbapo kodi hizo zingekuwa zinakwepwa.

"Mfano watu wanapolipa kodi Shule zinajengwa na kwenye shule wanatoka madaktari, wachungaji, wabunge, mashehe na watu wengine wenye taaluma mbalimbali na hawa wakiwa wanashukuru kwa Mungu baraka zinaenda mpaka kwa walipa kodi za serikali." Alisema Lowasa.

Alisema anaamini kwamba Wajasiliamali wanazo changamoto nyingi wanazokumbana nazo ambazo nyingine zimekuwa zikitokana na baadhi yao kukwepa kulipa kodi.

"Mfano mtu anakopa milioni 10 pale pale anatoa sadaka ya shukrani kwa Mungu akija afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hawamwambii ukweli kwenye makadilio kwa mantiki hiyo tayari anakua kaharibu baraka zake kwa kusema uongo hivyo nawaomba muwe makini katika kulipa kodi za Serikari," alisema Lowasa.

Hata hivyo mjasiliamali huyo ambaye pia ni Kada aliwaomba Wajasiliamali hao pamoja na wafanyabiashara kuwa wakati wakiendelea kutekeleza hiyo adhima ya kulipa kodi kwa wakati pia waendelee kumuunga mkono Mama Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kubwa za kuwaletea maendeleo watanzania na Taifa kwa ujumla.

"Kwenye suala la ulipaji kodi naamini tutakua tunamuunga mkono mama yetu Samia Rais Mwanamke wa kwanza ambae ukifuatilia alitabiliwa miaka ya 1480 lakini pia amekua na Hayati magufuli na Magufuli kwenye kampeini aliwai kusema nimewaletea mama kama sipo mama yupo hivyo mimi kama viongozi wa Taasisi mbalimbali namuunga mkono Mama Rais Samia na kumuombea Baraka tele kama kiongozi.

Dondoo za Usalama kwa Watumiaji Wote wa Bolt

$
0
0

 


Bolt – Mfumo wa kuagiza usafiri kupitia mtandao ndio mojawapo ya mifumo ya usafiri inayotumiwa sana nchini, kutokana na urahisi, unafuu na usalama wake.

  Kama jukwaa linalokua kwa kasi zaidi la upatikanaji wa usafiri kupitia mtandaoni barani Afrika, Bolt hutoa vidokezo na taarifa za kwa abiria ambazo zitawafanya wasafiri kwa usalama kwa urahisi kabisa kupitia vidole tu.

 Nchini Tanzania, Bolt inapatikana katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Dodoma ambapo inakupatia huduma nzuri na kwa bei nafuu zaidi.

 Zifuatazo ni dondoo 5 ambazo zinakuwezesha wewe mtumiaji wa Bolt kufurahia huduma zetu kwa usalama zaidi.

 1.    Agiza usafiri na umsubiri dereva ukiwa katika sehemu salama – Unapoagiza usafiri, hakikisha upo katika sehemu salama. Huna sababu ya kutumia muda mrefu kusubiri usafiri huku ukiwa umesimama nje na simu yako mkononi. Bolt inakuonesha wakati dereva anawasili kwa hiyo subiri ndani hadi dereva atakapowasili. Kwa njia hii unakuwa salama zaidi hadi dereva wako atakapowasili.

 2.    Hakiki taarifa za aina ya gari na namba zake za usajili – Unapounganishwa na usafiri, unapokea ujumbe wenye taarifa kuhusu jina la dereva, aina ya gari na namba zake za usajili. Hakikisha kuwa taarifa za gari linalokuja kukuchukua zinafanana na taarifa uliyopokea katika simu yako ya mkononi. Ikiwa taarifa hizi haziendani, tafadhali usiingie kwenye gari. Toa taarifa kwa Bolt kupitia kitufe cha huduma kwa wateja kwenye app yako.

 3.    Vaa mkanda – Daima vaa mkanda! Haijalishi ikiwa umekaa katika kiti cha mbele au nyuma. Pia hakikisha kuwa huning’inizi mikono dirishani na kuwa viungo vyote vya mwili vinabaki ndani ya gari muda wote ambapo gari linatembea. Kuwa mtulivu hadi utakapowasili pale unapokwenda.

 4.    Wahusishe wapendwa wako: Wape ETA yako: Katika kujali usalama wako, tuna mfumo wa Share My ETA ambao unapatikana katika app yako chini ya taarifa za dereva. Unaweza kutumia mfumo huu kutoa taarifa za safari yako kwa watu unaowaamini kila mara unaposafiri. Mfumo huu unawawezesha wapendwa wako kufuatilia safari yako hatua kwa hatua hadi unapowasili pale unapokwenda.

 5.    Endapo abiria watataka kutoa taarifa ya tukio, wanaweza kufanya hivyo kupitia app support ya Bolt kwenye simu na pia kupitia barua pepe kwa tanzania@bolt.eu

  Ikifanya kazi katika miji zaidi ya 60 ya Kiafrika katika nchi saba, Bolt inapanua na inaboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji ya wateja kote barani.

 Wakati wowote unahitaji kusafiri au kuzunguka mjini, Bolt iko kwajili yako  wakati wowote.

 Jisikie huru kutumia vidokezo hapo juu kila wakati unapotumia Bolt.

 Kaa salama na ufurahie safari yako.

Vodacom Tanzania Plc yashiriki upandaji wa miti kuelekea kilele cha siku ya mazingira duniani

$
0
0

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (kulia), Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia (katikati) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la WWF Dkt Aman Ngusam wakishirikiana kupanda mti katika eneo la Medeli jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra kuelekea siku ya kimataifa ya mazingira duniani. Utanzaji wa mazingira ni moja ya malengo ya Vodacom Tanzania Plc ya kuhakikisha kuwa dunia inakuwa mahali salama pa kuishi kwa kupanda miti na kuboresha mazingira kwa ujumla. (Picha kwa Hisani ya Vodacom Tanzania.)


Wizara ya Fedha yawakutanisha Wahariri wa vyombo vya habari kuwajengea uwezo kuhusu dhana ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi jijini Arusha

$
0
0
Jumla ya miradi 41 imeandaliwa na kufanyiwa uchambuzi ambapo itagharimu kiasi cha shilingi trilioni 3.402, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Ndg. Emmanuel Tutuba amesema.

Ndg. Tutuba ameyasema hayo leo Juni 3, 2021 jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuwajengea uwezo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ubia kati ya serikali na sekta binafsi (PPP) katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Miradi 40, imeandaliwa na Mamlaka za Serikali kutoka sekta mbali mbali na mradi mmoja umeandaliwa na mwekezaji kutoka sekta binafsi.

Ndg. Tutuba alisema kuwa mpango huo una umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi miundombinu, Elimu, Afya, Mawasiliano, Maji, Michezo, Viwanda na biashara.

Ndugu Tutuba alisema kuwa serikali imeandaa programu hiyo ya PPP nchini ili kuwezesha sekta binafsi,kushirikiana na serikali kwa utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo, katika sekta mbali mbali ambazo ni

“Ndugu zangu mapato ya kodi peke yake hayatoshi kwa serikali kuweza kutekeleza na kuendeleza miradi yote hii,hivyo jitihada hizi zitachangia kujenga uchumi shindani,na wa viwanda kwa maendeleo ya watu ifikapo mwaka 2025/26”alisema Tutuba.

Kwa upande wake Kamishna wa PPP Dkt. John Mboya alisema kuwa faida nyingine ya kutumia utaratibu huu katika utekelezaji wa miradi na utoaji wa huduma ni pamoja na serikali kupata ubunifu,utaalamu na teknolojia kutoka kwa sekta binafsi na serikali kuhamasisha vihatarishi vya mradi vikiwemo vya kiufundi,kifedha na kiutendaji,ambavyo sekta binafsi ina nafasi nzuri ya kuvisimamia na kuongeza ubora wa huduma.

Alisema kuwa ili kuweka mazingira wezeshi ya kuishirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP Serikali iliamua kutunga sera ya PPP,ya mwaka 2009 na sheria ya PPP sura namba 103,na kanuni za PPP za mwaka 2020.

“Ndugu zangu ili kufikia azma ya kutekeleza Programu ya PPP na kwa kasi inayotakiwa ni jambo la msingi sana na kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana hiyo,ili wadau wetu washiriki kikamilifu kutekeleza sera na Sheria ya PPP,na elimu hii imekuwa ikitolewa ambapo kabla ya mwaka huu wa fedha jumla ya wadau 829 wamepatiwa elimu hii”alisema Dkt.Mboya.





Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari wakati akifungua semina ya siku 2 kwa wahariri hao kuhusu masuala ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha Juni 3, 2020




Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari wakati akifungua mafunzo ya siku 2 kwa wahariri hao kuhusu masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha Juni 3, 2020
Meza Kuu, ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba (katikati) wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiendelea wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu kuhusu masuala ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.

Kamishina wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Dkt. John Mboya akizungumza wakati wa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.










 Kamishina Msaidizi wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Bw. Bashiru Taratibu (kulia) akimsikiliza  Kamishina wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Dkt. John Mboya wakati wa mafunzo ya siku 2 kwa wahariri hao kuhusu masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi yaliyofanyika leo juni 3,2021 katika ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha



MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI KUPIGIKA WIKIENDI HII

$
0
0

 

*Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!

UKWELI ni kwamba kujipima nguvu kabla ya mechi kubwa ni muhimu! Wikiendi hii inaweza kukupa ushindi mkubwa sana endapo ukifuata mechi za kirafiki za kimataifa zilizowekewa odds rafiki kabisa ili zikufaidishe! Usisubiri kuhadithiwa na Jirani, bashiri sasa!

ijumaa hii, kutakuwa na mechi ya kirafiki kabla ya michuano ya EURO 2020, baada ya Italy kuwalaza Wales 3-0, sasa Italy watakuwa nyumbani kuwaalika Czech Republic. Meridianbet imekuwekea Odds ya kirafiki kabisa ya 1.73 kwa Italy ili kukufaidisha.

Siku ya Jumamosi, Kutakuwa na mchezo wa mzunguko wa pili wa nusu fainali ya La Liga 2. Almeria watakuwa nyumbani kucheza na Girona baada ya kukubali kipigo cha 3-0 ugenini. Meridianbet wanawapa nafasi ya kupindua matokeo, na wameweka Odds ya 2.05 kwa Almeria ili uwe bingwa!

Jumapili nako kuna mambo makubwa, Belgium chini ya Lukaku watakuwa na Croatia chini ya Modric kama nahodha katika mechi ya kirafiki kabla ya EURO 2020. Kutambua ukubwa wa mechi hii, Meridianbet imekuwekea Odds ya 1.93 kwa Belgium.

Ni rahisi sana kuwa bingwa wikiendi hii, cha kufanya nikuchangamkia fursa tu. Piga *149*10# kujiunga au tembelea www.meridianbet.co.tz na ujiunge na familia ya mabingwa!


ML 500 ZATOLEWA KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA MBINGA

$
0
0

 

Na Muhidin Amri, Mbinga
SERIKALI imeipatia Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya ikiwa ni mkakati wa kuimarisha na kuboresha huduma za Afya hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Mbinga Juma Mnwele alisema, tayari wamepokea fedha hizo kutoka Serikali Kuu na wameshaanza kujenga Hospitali hiyo katika kijiji cha Kigonsera kata ya Kigonsera.

Mnwele alisema, ujenzi wa Hospitali hiyo utafanyika kwa awamu kulingana na fedha zitakazoletwa na Serikali na kwa kuanzia wataanza kujenga majengo ya vipaumbele kama jengo la wagonjwa wa nje(OPD) na maabara na kichomea taka na majengo mengine yataendelea kujengwa kulingana mapato.

Alisema, kwa kazi zilizofanywa na wananchi wa Kigonsera kusafisha eneo zimesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zitasaidia kuongeza majengo mengine ya kutolea huduma na kuwaomba wananchi hao kuendelea kufanya kazi za kujitolea katika mradi huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinda Desdelius Haule, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutao fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo na miradi mingine ya maendeleo inayokwenda kuharakisha kukua kwa uchumi.

Alisema, ujenzi wa Hospitali hiyo ni matokeo mazuri ya utendaji wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kuimarisha na kuboresha huduma za Afya kwa wananchi.

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali Kuu,SerikaliI ya kijiji cha Kigonsera,imetoa zaidi ya ekari 35 za ardhi ili kujenga Hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Emanuel Ngongi alisema, kwa kutambua changamoto walizokabiliana nazo kwa muda mrefu serikali ya kijiji kupitia mkutano Mkuu wa kijiji uliowajumuisha wananchi wote umeridhia kutoa ardhi iliyotengwa baada ya Halmashauri ya wilaya kuwa na wazo la kujenga Hospitali.

Ngongi alisema, wameamua kutoa ardhi hiyo bure ili kutekeleza mradi huo ambao unakwenda kumaliza changamoto ya huduma za afya kwa wakazi wa kijiji hicho ambao sasa wanalazimika kwenda hadi Hospitali ya Misheni Peramiho na Hospitali ya Rufaa Songea mjini umbali wa km 100 kufuata huduma ya matibabu.

Alisema, ni heshima kubwa na fursa pekee kuona Halmashauri ya wilaya imeamua kujenga Hospitali kubwa katika kijiji hicho na kuishukuru serikali ya awamu ya sita kutoa fedha za ujenzi wa Hospitali hiyo.

Mtendaji wa kijiji hicho Kasiana Kapinga alisema, uwepo wa Hospitali ya wilaya katika kijiji hicho utasaidia sana wananchi hasa wale wenye kipato kidogo kupata matibabu karibu na hivyo kuokoa maisha yao hususani mama wajawazito pindi wanapotaka kujifungua.

Alisema, wananchi wa kijiji hicho wamepokea mradi huo kwa furaha na wameshiriki katika kazi za kusafisha eneo la ujenzi kwa kukata miti na kung’oa visiki wakiwa na matumaini kwamba kujengwa kwa Hospitali hiyo ni sehemu ya chachu ya kuharakisha maendeleo yao.

Alisema, kwa sasa wakazi wa kijiji hicho wanalazimika kupata huduma za matibabu katikazahanati ya kanisa katoriki Kigonsera kwa gharama kubwa na wengine kwenda nje ya wilaya ya Mbinga jambo linalorudisha nyuma maendeleo kwa kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Mbinga kwa kazi nzuri wanazofanya katika kutekeleza kazi za maendeleo na miradi mbalimbali inayokwenda kuchochea na kuhamasisha wananchi kufanya kazi za kujitolea.

Ameitaka Halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza majengo mengine, badala ya kujenga majengo matatu hasa kutokana na ushiriki mkubwa wa wananchi katika ujenzi huo.

Alisema, kama watajipanga vizuri fedha hizo zinaweza kujenga majengo mengi ya kutolea huduma za afya na kuhakikisha majengo yatakayojengwa yanakuwa na ubora mkubwa na yanakamilika haraka.

Nshenye,amewataka wananchi wa kijiji hicho kutumia uwepo wa Hospitali hiyo kujenga nyumba bora kwa ajili ya watumishi na kuboresha huduma mbalimbali kwa ajili ya jamii itakayoishi kuzunguka eneo hilo, badala ya kuwa waangaliaji kwa watu kutoka nje ya wilaya hiyo.

MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA ZATAKIWA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA HUDUMA ZA USTAWI

$
0
0

 Na Heri Shaaban, Morogoro

MAMLAKA za Serikali za Mitaa zimetakiwa kutenga bajeti kwa ajili ya utoaji elimu na usimamizi wa huduma za ustawi wa Jamii.

Hayo yalisemwa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro Bi. Jesca Kagunila wakati wa kikao kazi cha siku moja cha kuwajengea uwezo mafisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri zote za Mkoa huo kilichoandaliwa na Mkoa kwa kushirikiana na Mdau wa Mradi wa Kizazi kipya Kanda ya Kati kupitia Shirika la PACT TANZANIA

Akizungumza katika kikao kazi hicho Afisa Ustawi wa Jamii Jesca alisema Mamlaka za Serikali za Mitaa zitakapotenga bajeti ya kutosha Mamlaka rahisi kusimamia masuala ya Ustawi ya Jamii bila kuwepo changamoto zozote katika sehemu zao za kazi na kuwawezesha kutoa huduma kwa weledi na ufanisi

Jesca alisema Maafisa Ustawi wa Jamii wamekuwa wakishughulika na Jamii hivyo watakapotengewa bajeti ya kutosha itasaidia kuifikia jamii kwa ukubwa na wakati.

"Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kuhakikisha vikao vya mabaraza ya Wazee ,Watu Wenye Ulemavu na Kamati za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinafanya kila robo kama ilivyoainishwa kwenye sera, sheria na miongozo." Alisema Jesca .

Aidha aliwataka Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha takwimu za watoto ,wazee na watu wenye ulemavu zinahuishwa na utambuzi unafanyika kwa kuwashirikisha Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na kujadiliwa kwenye vikao vya vijiji, kata na halmashauri.

Pia wawe na ratiba ya utoaji wa vipindi kwenye vyombo vya habari sambamba na utoaji elimu mashuleni na vyuoni.

Akizungumzia suala la mimba/ndoa za utotoni na Ukatili wa Kijinsia amesisitiza umuhimu wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Halmashauri/Wilaya

kujadili masuala hayo na kuweka mikakati ya namna ya kuondoa au kupunguza matukio hayo kwenye Jamii.

Alisema kwamba masuala ya ukatili kwa watoto, mimba/ndoa za utotoni ni suala mtambuka si la kuwaachia Maafisa Ustawi wa Jamii pekee, kwa kuwa Maafisa wa kada hiyo ni wachache ukilinganisha na matukio hayo yanayojitokeza kila kukicha hivyo nguvu za pamoja zinahitajika.

“Natoa wito kwa Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi, kuwahimiza Maafisa Ustawi wa Jamii kuwapatia takwimu za matukio hayo ili ziweze kujadiliwa katika vikao vya WDC, CMT, CHMT na Kamati za Ulinzi na Usalama ili kuweka mpango mkakati wa kupunguza matukio hayo kwenye jamii." Alisema Jesca.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kusirye Ukio amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii kufanya kazi kwa juhudi na maarifa huku wakijijengea tabia ya kutathmini kazi zao kwa mujibu wa maelekezo yanayotolewa na serikali sambamba na kuwahimiza Waganga Wakuu wa wilaya kufanya ufuatiliaji wa fedha zilizotengwa kutumika kwa wakati kwa ajili ya kutekeleza majukumu yaliyo chini ya kada hiyo.

Naye Meneja wa Mradi wa Kizazi kipya Kanda ya Kati Shirika la PACT Merina Shaidi alisema lengo la mradi huo ni kutoa huduma kwa watoto waliothiriwa na walioathirika na Virus Vya Ukimwi – VVU, kutoa huduma za Afya, Elimu, lishe, uchumi, ulinzi na usalama kwa mtoto.

Meneja wa Shirika hilo . Merina amewataka Maafisa ustawi wa Jamii wakati wanapoelekea mwisho wa mradia huo kuendeleza kazi ambazo zimekuwa zikitekelezwa na mradi huo ili kuhakikisha taarifa za ustawi zilizopo kwenye kata zinahifadhiwa kwa usiri mkubwa ili ziweze kutumika wakati zitakapohitajika kama mwongozo wa Serikali unavyoelekeza.
fisa Ustawi wa Jamii wa mkoa wa Morogoro Jesca Kagunila akizumza katika mafunzo ya siku moja kwa maafisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri za mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kusirye Ukio akizungumza katika mafunzo ya siku moja kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri zote za mkoa huo mkoani Morogoro Jana.
 (PICHA NA HERI SHAABAN).

Takwimu za Wami Ruvu Zinaisaidia Serikali Kuchukua Tahadhari za Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi-Jafo

$
0
0

 WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, amesema takwimu zinazotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu ni Muhimu kwa Sababu zimekuwa zikiisaidia Serikali hususani Wizara yake kuchukua Tahadhari kuhusu suala zima la Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye vyanzo vya maji ikiwemo Mito na Mabwawa.


Waziri Jafo ametoa kauli hiyo Mjini Dodoma kwenye Wiki ya mazingira alipotembelea Banda la Maoensho la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu.

Amesema Rasilimali maji ni Muhimu kwa maendeleo na Ustawi wa Binadamu, hivyo ameitaka Bodi hiyo ya Maji katika Bonde la Wami Ruvu kuwa mstari wa Mbele kuiongoza Serikali kupitia Takwimu zake ili iweze kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na athari za Mazingira kwenye vyanzo vya Maji.

“ Ofisi yenu ni muhimu sana, lakini inatusaidia vile vile kutoa tahadhari watu wasivamie vyanzo vya maji Kwa Sababu wakivamia Mambo yote yanakuja kuharibika, kwa mfano leo hii tunajenga lile bwana la Nyerere kama watu watavamia vyanzo vya Maji lile bwana litakuwa halijai.” Alisisitiza Wazir Jafo.

Kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani kinatarajia kufikia kilele chake June 5, ambapo Serikali inatarajia kuzindua Kampeni Kabambe ya Kuhamasisha Jamii Kutunza na Kulinda Mazingira.

Waziri wan chi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Jamii wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, kuhusiana na Shughuli mbalimbali za Bonde hilo ikiwemo Utunzaji wa Mazingira na Ulinzi wa vyanzo vya Maji, Utoaji Vibali wa Matumizi ya Maji ya Visima, Mito na Mabwawa, pamoja na Utoaji Elimu kwa Jamii ili kuepusha Migogoro ya Maji.
Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akisaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Wageni Katika Banda la Maonesho la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, alipotembelea Kwenye Banda hilo ili kujionea Shughuli mbalimbali za Bodi hiyo, Pemebeni yake ni Afisa Kutoka Bodi hiyo Harold Kayoza.
Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, alipofika kwenye Banda la Maonesho la Bodi hiyo ili kujionea Shughuli mbalimbali za Bodi hiyo kwenye Suala zima Utunzani wa mazingira kwenye vyanzo vya Maji, Utoaji Vibali wa Matumizi ya Maji ya Visima, Mito na Mabwawa, pamoja na Utoaji Elimu kwa Jamii ili kuepusha Migogoro ya Maji.

SITA WAPELEKWA MJINI NA M-PESA YA VODACOM

$
0
0

 

Afisa Tarafa kutoka Manispaa ya Kinondoni Rahma Kondo (kulia,) akimkabidhi funguo ya bajaji mshindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Twende Mjini na M-PESA Nyangije Basondole (kushoto,) makabidhiano yaliyofanyika jana katika viwanja vya shule ya msingi Bunju A mkoani Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imekabidhi zawadi kwa washindi waliopatikana kupitia kampeni ya Twende Mjini na M-Pesa, kampeni inayoendeshwa kwa malengo ya kurudisha kwa jamii pamoja na kuhamasisha jamii kutumia huduma za mtandao huo ambazo zinaboreshwa kila siku.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Afisa Tarafa kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi. Rahma Kondo amesema Vodacom imekuwa sehemu ya jamii kwa kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii pamoja na kutoa huduma za mawasiliano katika maeneo mengi ya miji na vijiji.

Aidha amewataka watanzania kujiunga na mtandao wa Vodacom katika Mawasiliano na kujipatia nafasi ya kujishindia zawadi maalumu ambazo wamekuwa wakizitoa kwa wateja wanaotumia huduma mbalimbali zinazotolewa na mtandao huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya Dar es Salaam Brigitha Steven amesema  si vigumu kushinda wateja na mawakala wanaweza kushinda kwa kutumia huduma za M-Pesa kupitia *150*00# au kupitia M-Pesa App kwa kufanya miamala ya kutuma pesa, kulipa bili na huduma mbalimbali na moja kwa moja wataingia kwenye droo na kuweza kuwa washindi. 

Pia amewataka wateja wa mtandao huo kupokea namba ya huduma kwa wateja 0754 100 100 ili kutopitwa na bahati zao na wataendeleza kampeni ya  kujitambulisha kwa wateja kupitia jumbe fupi 'Sms' pamoja na mitandao ya jamii ili wateja na watumiaji wa huduma za M-Pesa wasipitwe na zawadi hizo.

Kampeni ya Twende Mjini na M-Pesa itaendeshwa kwa wiki nane ambapo kila siku mshindi wa bodaboda mpya aina ya Boxer BM 125X atapatikana na mshindi mmoja wa bajaji mpya aina ya TVS King GS atapatikana kila wiki huku katika Grand Finale ya mashindano hayo mshindi atajishindia gari jipya aina ya Toyota Corolla Cross (SUV) ya mwaka 2021.

Katika droo hiyo ya kwanza kati ya droo nane waliojishindia bodaboda ni Godfrey Mgeni (Morogoro,) Francis Kwale, Wakala wa huduma za M-Pesa (Dar es Salaam,)  Zanzibar gateway Wakala wa huduma za M-Pesa (Zanzibar,) Ramadhan Nkondo (Dar es Salaam) Pili Joseph (Dar es Salaam.) huku Bajaji mpya ikienda kwa Nyangije Basondole kutoka Dar es Salaam.






 

Meridian Bet na Global Peace Foundation zaing'arisha Tandale

$
0
0

 

KAMPUNI ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet kwa kushirikiana na Global Peace Foundation Tanzania zimeadhimisha siku ya mazingira duniani kwa kusafisha soko la Tandale na kupanda miti ya kivuli na matunda kwenye hospital ya eneo hilo, Dar es Salaam.

Tukio hilo limeanza saa 12 asubuhi kwa watumishi wa kampuni hiyo kufanya katika maeneo mbalimbali kuzunguka soko la Tandale na kisha kupanda miti ya kivuli na matunda kwenye hospitali ya Tandale.

Mkuu wa kitengo cha ustawi wa jamii cha Meridian Bet, Amani Maeda amesema kampuni yao inaungana na mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku ya mazingira.

"Mazingira ni watu na watu ni mazingira, bila mazingira kuwa safi, hatuwezi kuwa na jamii yenye afya, ndio sababu Meridian Bet tumeungana na wenzetu wa Global Peace Foundation Tanzania kufanya usafi na kupanda miti katika kuadhimisha siku ya mazingira." Amesema Amani.

Naye msimamizi mkuu wa maduka ya Meridian Bet Dar es Salaam na Pwani, Seif Simba amesema wameshiriki katika maadhimisho hayo kwa kufanya usafi katika soko na kupanda miti hospital kwani maeneo hayo yanahudumia jamii kubwa.

"Kama kawaida yetu Meridian Bet kushirikiana na jamii, ndiyo sababu tumeadhimisha siku ya mazingira kwa kusafisha soko la Tandale na kupanda miti kwenye hospitali." Amesema.

Ofisa programu wa Global Peace Foundation Tanzania, Benson Daudi amesema zoezi hilo litakuwa endelevu.

"Tutaendelea kufanya usafi na kupanda miti katika maeneo mbalimbali yanayohudumia jamii hata baada ya maadhimisho haya." Amesema Daudi.

Viewing all 48950 articles
Browse latest View live