Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza wakati wa kikao na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha Kimataifa (IMF) nchini, Bw. Jens Reinke (hayupo pichani) kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia)akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha Kimataifa (IMF) nchini, Bw. Jens Reinke (kushoto) katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha Kimataifa (IMF) nchini, Bw. Jens Reinke akizungumza kuhusu namna shirika hilo litachangia kuinua uchumi wa nchi wakati wa kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza wakati wa kikao na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo akizungumzia utayari wa benki hiyo wa kufadhili miundombinu nchini, katika kikao cha benki hiyo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Amina Khamis Shaaban wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), baada ya kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo baada ya kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
********************************
Na Farida Ramadhan, WFM – Dodoma
Serikali imeanza utekelezaji wa maelekezo ya kikao cha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Kimataifa (IMF), Bi. Kristalina Georgieva kilichofanyika kwa njia ya mtandao mwanzoni mwa mwezi huu ambacho pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu atheri za kiuchumu na kijamii zilizotokana na changamoto za janga korona (Covid- 19).
Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini, Bw. Jens Reinke katika ofisi za Wizara hiyo.
Alisema wamekutana ili kutafsiri maelekezo hayo katika utekelezaji ili kuiwezesha IMF kushirikiana na Tanzania katika kujenga uchumi ambao umekumbana na misukosuko inayoendelea duniani inayotokana na changamoto za janga la korona (Covid- 19).
“Tumekutana na IMF pamoja na Wataalam wa Wizara pamoja na baadhi ya taasisi zake kujadili namna ya kuandaa taarifa ya maeneo yaliyoathirika zaidi na misukosuko hiyo pamoja na kuangalia kiwango cha athari katika maeneo husika”, alisema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema athari za misukosuko hiyo ya uchumi zinatofautiana kisekta kwa kuwa kuna sekta ambazo zimeathirika moja kwa moja kama biashara, utalii na makusanyo, na kuna zile ambazo haziathiriki moja kwa moja.
Alisema wataangalia athari za misukusuko hiyo katika huduma za jamii kwa upana wake kama huduma za Afya hususani kuboresha miundombinu, dawa na upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na suala la upatikanaji wa maji.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini, Bw. Jens Reinke alisema shirika hilo lipo tayari kushirikiana na Tanzania na kubainisha kuwa yeye binafsi yupo tayari kufanya kazi na wataalam wa Tanzania ili kusaidia nchi na kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa kwa kasi kama ilivyopangwa.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo kuhusu namna bora ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na benki hiyo.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema Serikali itaufanyia kazi ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na benki hiyo ili kuhakikisha kuwa miradi yote inayofadhiliwa inatekelezwa kwa haraka kama ilivyopangwa.
“Benki ya Maendeleo ya Afrika ni miongoni mwa benki ambazo zinatoa fedha nyingi katika hudumia miradi nchini hususan miradi ya miundombinu, na kesho Mwakilishi wa Benki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha watasaini mkataba kule Dar es Salaam kwa ajili ya miradi”, alibainisha Dkt. Nchemba.
Alisema kwasasa benki hiyo inafadhili miradi ya miundombinu takribani 22 ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko mkoani Dodoma na mradi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.
Afafanua kuwa Serikali inangojea utekelezaji wa benki hiyo kuwezesha Tanzania kunufaika zaidi na madirisha ya mikopo inayotolewa ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali.
Alisema benki hiyo iko tayari kuyafanyia kazi mambo yote muhimu waliyojadili ikiwa ni pamoja na kuwezesha Tanzania kunufaika zaidi na madirisha ya mikopo inayotolewa.
Aidha, Bi. Nwabufo alimpongenza Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kupata nafasi hiyo na kutoa salam za pole kutokana na msiba mzito ulioikumba nchi kwa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
SERIKALI YAANZA UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA NA IMF
KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET, INAKUPA FURSA YA KUTAMBA NA BAHATI NASIBU YA KENO!
*Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa.
Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet imekusogezea bahati nasibu kupitia mchezo wa Keno. Keno ni mchezo wa namba ambao mchezaji anachagua namba 10 kutoka kwenye orodha ya namba 1 mpaka 80. Huu ni mchezo wa bahati nasibu, ukiwa na bahati sana utashinda pesa nyingi zaidi. Keno ni moja ya mchezo unaopendwa na wachezaji wengi wa Meridianbet.
Namna ya Kucheza Mchezo wa Keno
Ukiingia kwenye upande wa bahati nasibu ya Meridianbet, utaona ubao unaoonesha namba 1 mpaka 80. Mteja ataamua anataka kuweka dau la kiasi gani? Kumbuka, kila dau utakaloliweka, linaweza kukupatia faida stahiki kulingana na dau hilo.
Baada ya mteja kuweka dau, atachagua namba zake 10 za bahati anazoamini zitatolewa kwenye mzunguko unaofuata, baada ya kukamilisha hatua hizi, mteja atasubiri matokeo ya droo husika kutokea.
Namna ya Kupata Ushindi Kwenye Mchezo wa Keno
Ushindi waKeno ya Meridiabetunategemea idadi ya namba ulizochagua na zile zilizotokea kwenye droo husika! Kama ukipatia namba mbili basi ushindi wako utakuwa ni mara 2 ya dau lako! Kama ukichagua namba zote na zikatokea katika ile droo kabambe ya "Zote zitokee" basi utakuwa miongoni mwa mamilionea! Jiunge sasa na Meridianbet na ufaidi odds, bonasi na promosheni kabambe!
Vigezo na masharti, kuzingatiwa!
Serikali yatoa msaada Vifaa vya Uvuvi na Uchakataji Samaki kwa Chuo cha VETA Chato.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO VYAMA VYA USHIRIKA YATAKAYOFANYIKA JULAI 3 MKOANI TABORA


Akizungumza leo Mei 26,2021 jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania(TFC) Florian Haule amesisitiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndio anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na katika maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli mbalimbali ambazo zitafanywa na vyama hivyo vya ushirika.
Amesema miongoni mwa shughuli ambazo ziatafanyika kutakuwa na maonesho lakini kutakuwa na uchangiaji damu utakaofanywa na wana ushirika na mwaka huu kitaifa yatafanyika Viwanja vya Nane Nane mkoani Tabora.
"Shughuli zitakazofayika kutakuwa na maonesho ya bidhaa na huduma za vyama na wadau , kongamano la wanaushirika na wadau wake, shindano la isha ya wanafunzi wa shule ya msingi, sekondari na vyuo vikuu, kutoa damu kwa wahitaji, kupanda miti ili kuhifadhi mazingira.
"Pia kutakuwa na kutoa misaada mbalimbali katika vituo vya afya na hospitali , kupata huduma za afya kutoka kwa madaktari bingwa watakaopiga kambi katika viwanja vya maonesho.Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali nchini."Amesema Haule.
Aidha amesema kauli mbiu kwenye maadhimisho hayo itakuwa inasema "Ushirika tujijenge upya kwa ubora na tija" huku akifafanua kauli mbiu hiyo imekuja kutokana na changamoto ya janga la Corona ambayo dunia imepitia.Hivyo tumeona tusimame na tujijenge upya."
Akielezea zaidi maadhimisho hayo, Haule amesema pia kutakuwa na uzinduzi wa tuzo maalum kwa viongozi mbalimbali ambao wametoa mchango wao kwa kiasi kikubwa katika vyama vya ushirika nchini.
Akizungumzia kwa kifupi kuhusu muelekeo wa ushirika, Haule amesema Serikali ya Awamu ya Sita inajipanga kuipandisha nchi yetu iweze kufikia kuwa nchi yenye uchumi wa kati kupitia uendelezwaji wa sekta ya viwanda na nyinginezo.
"Mazingira hayo yanatosha kueleza mwelekeo ushirika wa vyama vya ushirika vitajipanga pamoja na vyama vya ushirika kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.Aidha vyama vya ushirika vinatarajiwa kuwa chombo cha uzalishaji wa malighafi za viwandani na nyinginezo.
AfDB YAIKOPESHA TANZANIA BILIONI 323 KUJENGA MRADI WA UMEME MTO MALAGARASI
Saidina Msangi na Ramadhani Kissimba, Dar es SalaamSerikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika zimesaini mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.4) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa nguvu ya maji - Malagarasi.Mikataba ya mkopo huo wenye masharti nafuu imesainiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya Afrika Mashariki.Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa Mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo utaijengea TANESCO uwezo wa usambazaji wa vifaa vya kuunganisha wateja 4,250 katika Wilaya za Kigoma, Kibondo na Kasulu ikiwemo kaya 1,000 zenye kipato cha chini, zahanati 4 na shule za msingi 6.“Mradi huu utahusisha ujenzi wa kituo kipya cha uzalishaji wa umeme wa gridi ya 49.5 MW chenye uwezo wa kuzalisha wastani wa GWh 181 za umeme kwa mwaka ili kuboresha usambazaji wa umeme na kupunguza utegemezi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta mazito ”, alisema Bw. TutubaAlieleza kuwa mradi huo unatarajiwa kugharimu takribani dola za Marekani milioni 144.1 ambapo Benki ya Maendeleo ya Afrika itatoa dola za Marekani milioni 140 na Serikali ya Tanzania itachangia dola za Marekani milioni 4.14 zilizobaki.“Kati ya fedha hizo, dola za Marekani milioni 120 zitatolewa kupitia dirisha la Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na dola za Marekani milioni 20 kupitia Africa Growing Together Fund”, alifafanua Bw. Tutuba.Aidha, Bw. Tutaba alisema kuwa mradi huo utajumuisha ujenzi wa njia ya usafirishaji wa umeme, upanuzi wa mtandao wa kusambaza umeme wa 132kV na ununuzi wa transfoma mpya 15 ili kuongeza uwezo wa kusambaza wa umeme kwa wananchi.Aliongeza kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo kutaongeza kiwango cha fedha kilichotengwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya kufadhili miradi ya sekta ya nishati nchini Tanzania kutoka takriban dola za Marekani milioni 325.19 hadi kufikia dola za Marekani milioni 465.19 (takriban shilingi trilioni 1.07).
Aliongeza kuwa mradi huo pia ni sehemu ya utekelezaji wa vipaumbele vya Benki ya Benki ya Mandeleo ya Afrika vya kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya nishati ya umeme ili kuchochea maendeleo ya viwanda na kuboresha maisha ya watu barani Afrika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Nnenna Nwabufo alisema kuwa mradi huo ni moja ya miradi sita iliyoidhinishwa na benki hiyo katika kipindi cha miaka mitatu.Aliitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma wenye thamani ya dola za Marekani milioni 180, Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato (dola 271m), barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (dola 256m), barabara ya Bagamoyo – Horohoro – Lunga – Malindi (dola 150m) na Mradi wa usambazaji umeme wa Nyakanazi – Kigoma (dola 123m)B1. Nnenna alisema kuwa uwekezaji wa Benki yake nchi Tanzania imefikia thamani ya dola za Marekani bilioni 2.33 zilizowekezwa katika sekta za miundombinu ya usafiri na usafirishaji, nishati ya umeme, maji na usafi wa mazingira, kilimo, utawala bora na fedha.Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya AfrikaMashariki, wakisaini mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.4) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Mto Malagarasi, Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya Afrika Mashariki, wakibadilishana hati za mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki, wakionesha hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Nnenna Nwabufo, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba (wa pili kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo (wa tatu kulia walioketi), baada ya hafla ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Vodacom Tanzania yajiandaa na siku ya Mazingira Duniani
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia akisalimiana na Waziri wa Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo wakati alipomtembelea ofisini kwake ikiwa ni maandalizi kuelekea siku ya kimataifa ya mazingira duniani, Vodacom ilipofanya ziara fupi ya miradi ya mazingira mkoani Dodoma, Vodacom ni mojawapo ya wadau katika miradi endelevu inayolinda mazingira nchini.
Mwakinyo kumpa asante Rais Samia kwa kumchapa Mayala
Bondia Hassan Mwakinyo ameahidi kumpa kipigo kikali mpinzani wake Antonio Mayala kutoka Angola ikiwa asante kwa Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
Mwakinyo ambaye atawania mkanda wa Afrika (ABU) wa uzito wa Super welter atapanda ulingoni kesho kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.
Alisema kuwa amejiandaa vyema na kwa vile atakuwa anapigana kwa mara ya kwanza chini ya uongozi wa Rais Samia, hatofanya makosa zaidi ya kushinda katika raundi za mwanzoni tu katika pambano hilo lililodhaminiwa na KCB Bank, Plus TV, Multichoice Tanzania, Tanzania Tourism Board, Onomo Hotel, Precision Air, Prestine Logistics, Urban Soul na washirika wa kimataifa Global Boxing Stars na Epic Sports Entertainment.
“Nitakuwa napigana kwa mara ya kwanza chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Sitamwangusha Rais na watanzania kwa ujumla, nawaomba mashabiki kufika kwa wingi ili kunipa sapoti,” alisema Mwakinyo.
Wakati Mwakinyo anasema haya, mpinzani wake Mayala amesema kuwa pamoja na kupata taarifa za muda mfupi, amejiandaa vyema ili kuonyesha kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa.
“Nimekuja kwa ajili ya kushinda na si kupoteza, nilikuwa nafanya mazoezi kwa sababu ngumi ni kazi yangu na siwezi kuruhusu Mwakinyo kushinda na kuchukua mkanda wa Afrika,” alisema Mayala.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema kuwa mbali ya pambano hilo, pia bondia Daniel Matefu atazichapa na bondoa kutoka Bulgaria Pencho Tsvetkov huku bondia wa kike Leila Yazidu atazichapa na bondia wa Bulgarian Joana Nwamerue.
Pia bondia Hamisi Palasungulu atazichapa na bondia wa Congo Brazzaville Ardi Ndembo huku Imani Daudi Kawaya akionyeshana kazi na bondia kutoka Afrika Kusini Chris Thompson.
Pambano lingine la ABU litakuwa kati ya bondia Shabani Jongo chini ya Mnigeria Olanrewaju Durodora ambao watawania uzito wa juu na nyota mwingine Ibrahim Class atazipiga na bondia wa Afrika Kusini, Sibusiso Zingange.
Mabondia wa kigeni na makocha mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kupambana na wapinzani wao wa Tanzania katika pambano la Rumble in Dar 2 lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.
Mikopo ya NMB Masta Boda sasa yatua rasmi kanda ya kaskazini

Kutoka Kushoto: Mwendesha bodaboda wa Jijini Arusha Stella Nguma, Mkuu wa kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB Alex Mgeni, Mwenyekiti wa chama cha pikipiki za miguu mitatu Twaha Mpera, Mwenyekiti wa chama cha pikipiki za miguu miwili Okero Costantine, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Allan Rushokana, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa ndani Benki ya NMB Benedicto Baragomwa na Meneja Mwandimiz wa Bidhaa, Clara Mwichumu, wakizindua kampeni ya Miliki Chombo jijini Arusha inayowawezesha waendesha bodaboda na bajaji kupata mikopo nafuu. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika leo jijini Arusha katika Ukumbi wa Lush Garden.

Baadhi ya waendesha boda boda na bajaji wa jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Allan Rushokana na wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kufanyika uzinduzi wa Mikopo ya NMB Masta Boda leo.
……………………………………………………………………………….
Kutokana na changamoto ya madereva boda boda na pikipiki aina ya miguu mitatu kutomiliki vyombo vyao vya kazi, Benki ya NMB imekuja na njia ya kuwakomboa na hali ya utegemezi kwa kuwapatia mikopo nafuu ya umiliki wa vyombo hivyo.
Hakimu Saimon ni katibu wa bodaboda mkoa wa Arusha alisema anaishukuru taasisi hiyo kwani wamekuwa wanaendesha pikipiki za wengine kwa muda mrefu hali inayopelekea kuwa tegemezi katika umiliki wa vyombo hivyo kwa kuwarejeshea wamiliki wao fedha waliopangiwa.
“Kwa kufanya hivyo wamekuwa wakiingia mikataba ya kurejesha sh.10,000 kila siku ndani ya miezi 13 ilikuwa ni mateso lakini kupitia benki ha NMB kila mmoja wetu atanufaika na mkopo huu na kuweza kumiliki chombo chake na kujikwamua kiuchumi katika kujiletea maendeleo,”alisema Katibu huyo.
Alisema ni jambo la furaha kwao kutumia fursa ya mkopo huo katika kumiliki vyombo vyao kwani wao watatoa asilimia 20 na 80 wataongeza Benki ya NMB hivyo watafanya juhudi katika marejesho hawatakuwa na mchezo katika kutumia fursa hiyo.
Kaimu Afisa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa alisema baada ya uzinduzi huo waendesha bodaboda na bajaji watapata fursa ya kupata pikipiki za miguu mitatu na miwili ikiwa zoezi hilo lilianzia Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na sasa Arusha ikiwa mkoa unaofuata ni Mbeya.
Baragomwa alisema benki hiyo imetenga Sh. bilioni 5 kwa kuanzia kwa mwaka huu ambapo zitawanufaisha waendesha bodaboda zaidi ya milioni mbili nchini.
“Kwa kuwa bodaboda wengi ni vijana na hawana dhamana, NMB imekuja na njia ya kuwakopesha kwa mikopo nafuu. Ni vyema wakatumia fursa hii ili kila mmoja amiliki chombo chake,”alisema.
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi katika uzinduzi huo, Afisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Allan Rushokana alisema swala la kuwakopesha mikopo hiyo madereva hao itawasaidia kuwaletea maendeleo yao na kujikwamua kiuchumi.
“Lengo kubwa la taasisi ya fedha ya NMB ni kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kwani suala la ajira nchini limekuwa changamoto lakini kujiajiri kuna nyanja pana hivyo wazingatie utaratibu wa kupata mikopo ili kila mmoja aweze kumiliki chombo chake na mpango huu ukatoe matokeo mazuri katika kuleta maendeleo na kujikwamua kiuchumi,”alisema Mwakilishi huyo.
Kagame, Elumelu leads UBA Africa Conversations 2021
UBA then went further to introduce UBA Africa Day conversations with its third edition of its annual discussions this year, UBA invites reknown African leaders familiar with the continent heritage to discuss various social, economic and political issues impacting Africa as a continent and this year’s panel included African leaders such as Mrs. Ngozi Okonjo-Iweala, Director-General of the World Trade Organisation(WTO), Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Director-General of the World Health Organisation(WHO), Rwanda’s President H.E. Paul Kagame and Makhtar Sop Diop, Managing Director, International Finance Corporation(IFC). Taking into consideration the current challenges of COVID 19 it has taken further safety measures by conducting these conversations online where the entire African continent can follow through, learn and engage in the conversations.
Speaking during the conversation which mostly featured the effects of Covid 19, President Kagame said that Covid 19 has affected many African countries economically due to lockdowns and therefore urged called other African leaders to come together and discuss ways of moving to the next stage. “The effect of Covid 19 has both been felt by the government and private sector. We should learn from this shock to invest more of our budget in our national health system. This is not the last global crisis and the next one should not catch Africa unprepared”.
President Kagame added, “I think it is important for African leaders to come together and discuss this crisis, we can discuss about the causes of conflicts and poverty. It is not about who is doing this or that, I think mutual respects is the best form of relationship between Africa and rest of the world, we talk of problems in Africa, deprivation and poverty, but this is not our identity”.
UBA Group Chairman and Founder of the Tony Elumelu Foundation – Tony Elumelu said ‘We have seen how our youth despite Covid 19 have leveraged their talents expertise network and technology to create wealth and support the communities they live. We must therefore make sure that the gains these youths have made are not erased’.
On his part, The World Health Organization Director Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus said that WHO is working day in day out to bring immediate solutions for the equitable distribution of vaccine doses. However, it is clear that Africa cannot rely solely on the importation of vaccines from the rest of the world. We must build capacity not only for Covid vaccines but for other vaccines and medical products’.
He added, more than anything else, the pandemic has demonstrated that health is not luxury item or simply an outcome of development but its human right and a prerequisite for social and economic development.
Ngozi Okonjo-Iweala, Director-General of the World Trade Organisation(WTO) said that if Africa wants to recover from Covid epidemic, the discussion of restricting debt is most important and giving Africa economies space of breathe so that they can invest only in the health sector but also on economic sector and we are going to recover. ‘It is important for the world that we reverse this vaccine inequality and Africa benefits from it. We cannot recover sustainability without it. So we have to fight for it, whether by getting more vaccines in or by manufacturing our own, said Iweala.
Africa Day has been celebrated since 1963 on May 25th across the African continent and worldwide. The day was inaugurated by the Organisation of African Unity, in celebration of the unity, diversity and beauty of Africa and its people and the theme for this year was ‘Bringing Africa to the World’

UBA Bank Tanzania staff lead by their Managing Director Mr Kingsley Ulinfun cuts a cake to celebrate UBA this year’s UBA Africa Day. Being a Pan African bank of choice, UBA has since been celebrating this day for years, the bank coelebrates this day by decorating their offices with traditional African themes and even staff are encouraged to research and represent various African heritage through clothing, food and aesthetics.
KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA (NARCO) INAWATANGAZIA MWALIKO WA KIKAO WAWEKEZAJI WOTE WENYE MIKATABA YA MUDA MREFU KATIKA VITALU VYAKE
MAWAZIRI BIASHARA, VIWANDA, FEDHA NA UWEKEZAJI KUKUTANA KESHO JIJINI ARUSHA





Mwakinyo, Mayala kuwania ubingwa wa ABU jioni ya leo Next Door Arena Masaki,jijini Dar
Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa Tanzania, Hassan Mwakinyo jioni leo atapanda ulingoni kuwania ubingwa wa uzito wa super welter wa Afrika wa shirikisho la ngumi za kulipwa Afrika (ABU) dhidi ya bondia wa Angola, Antonio Mayala.
Pambano hilo limepangwa kuanza saa 12.00 jioni kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki na mabondia wote wametamba kutwaa mkanda huo ambao upo wazi.
Mwakinyo ambaye ana rekodi ya kushinda mapambano 18 na kupoteza mawili, ametamba kushinda pambano hilo kabla ya raundi ya tano katika pambano hilo la raundi 12.
“Nimejiandaa zaidi ya raundi 12 kwa lengo la kuwa imara muda wote, lengo langu ni kushinda raundi za mwanzoni, lakini nimeamua kumpa nafasi mpaka raundi ya nne au ya tano ili kutoa burudani kwa mashabiki wangu,” alisema Mwakinyo.
Alisema kuwa Mayala hakuwa lengo lake, lakini kwa sababu ameingilia ugomvi wa bondia Brendon Denes wa [MO1] Zimbabwe ambaye ameumia, atatoa kichapo cha hali ya juu.
“Kamwe sitamdharau Mayala kwani ameingilia ugomvi ambao haukuwa wake, atajuta kukubali kupigana na mimi, nitamnyoosha kisawasawa,” alisema.
Alisema kuwa amedhamiria kuwapa furaha mashabiki wake na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwani atakuwa anapigana kwa mara ya kwanza chini ya uongozi wake.
Mbali ya pambano hilo, bondia mwingine wa Tanzania, Shabani Jongo atawania ubingwa wa uzito wa juu wa ABU dhidi ya bondia kutoka Nigeria Olanrewaju Durodora.
Pambano hilo limepangwa kuwa la raundi 12 na Jongo ametamba kufanya vyema. Katika kusindikiza mapambano hayo mawili, bondia nyota wa Tanzania Ibrahim Class atazichapa na bondia wa Afrika Kusini, Sibusiso Zingange katika pambano la uzito wa light yaliyodhaminiwa na kampuni ya KCB Bank, Plus TV, Multichoice Tanzania, Tanzania Tourism Board, Onomo Hotel, Precision Air, Prestine Logistics, Urban Soul, Global Boxing Stars, M-BET na Epic Sports Entertainment.
Mapambano mengine ya utangulizi yatawahusisha bondia wa Tanzania Daniel Matefu ambaye atazichapa na bondia wa Bulgaria Pencho Tsvetkov ambapo bondia wa kike Leila Yazidu atazichapa dhidi ya bondia mwingine wa Bulgaria Joana Nwamerue.
Pia bondia Hamisi Palasungulu atazichapa na bondia kutoka Congo Brazzaville Ardi Ndembo huku Imani Daudi Kawaya atapigana na bondia kutoka Afrika Kusini Chris Thompson.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa alisema kuwa pambano hayo yataonyeshwa katika nchi zaidi ya 32 Afrika kupitia Plus TV ambayo inapatikana kwenye king’amuzi cha DStv.
“Tunajivunia sana kuwa mstari wa mbele kuendeleza vipaji hasa vya ngumi za kulipwa hapa nchini na kushirikiana na serikali. Rumble in Dar 2 ni alama ya maendeleo ya ngumi za kulipwa nchini kwa mujibu wa malengo yetu, tunaomba ushirikiano kutoka kwa wadau, ” alisema Twissa.
Meneja Maendeleo ya Biashara na Miradi wa kampuni ya Jackson Group Sports, Levis Paul akiwatambulisha mabondia Hassan Mwakinyo wa Tanzania (kulia) na Antonio Mayala wa Angola ambao jioni ya leo watapanda kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki kuwania ubingwa wa Afrika wa uzito wa Super Welter. Pambano hilo limeandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.
FAINALI YA UEFA LEAGUE WIKIENDI HII
Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!
Meridianbet haijawahi kukuacha kinyonge. Baada ya Fainali ya Europa League iliyokuwa na Odds bomba. Sasa, unaweza kufurahia Wikiendi yako ukibashiri mechi ya Fainali ya UEFA na mechi nyingine kibao na kuwa kwenye familia ya mabingwa. Meridianbet imekuandalia Odds za kijanja sana kwenye mechi ya fainali ya EUEFA na nyingine kibao, bashiri sasa!
Ijumaa hii, Kule Denmark, Superliga itaendelea ambapo, kutakuwa na mchezo kati ya Aarhus vs Aalborg, Meridianbet imekuwekea odds ya 1.95 kwa Aarhus.
Jumamosi, kule porto patachimbika, Fainali ya ligi ya mabingwa ulaya itapigwa, Chelsea watakuwa kibaruani kuvaana na Manchester City, bashiri kombe litaenda London au Manchester, kwan City wamewekewa Odds ya 2.00 ili ufaidi Zaidi.
Siku hiyo hiyo kule Bundesliga, Koln watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Holstein Kiel, ambao wanapambana ili kuingia Bundesliga. Ukichagua kubashiri na Meridianbet, basi utakuta ya kijanja ya 2.25 kwa Koln ili ikufaidishe!
Jumapili, Katika La Liga 2, Sporting Gijon watakuwa nyumbani kucheza na Almeria, na Meridianbet imekuandalia Odds ya 2.00 kwa Gijon ili kukupa ushindi mkubwa Zaidi.
Siku ya jumatatu, Kutakuwa na mechi ya kupanda daraja ligi ya Wales, Morecamble watakuwa nyumbani kucheza Newport County, na Meridianbet tumeweka Odds ya 2.65 kwa Newport kwa ajili yako.
Ni rahisi sana kuwa bingwa wikiendi hii, cha kufanya changamkia fursa. Piga *149*10# kujiunga au tembelea www.meridianbet.co.tz na ujiunge na familia ya mabingwa!
RAS SENEDA WATUMISHI WA UMMA IRINGA JENGENI NYUMBA ACHENI KUNUNUA GARI KWANZA
WATUMISHI wa UMMA mkoa Iringa wametakiwa kuwa mfano kwa wananchi kwa kuhakikisha wanakuwa na mashamba ya kimkakati yatakayowasaidia wananchi kujifunza ikiwa ni pamoja na wao kujiinua kiuchumi .
Akizungumza kwenye kikao cha wakuu wa taasisi za UMMA za mkoa wa Iringa cha kujitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya Queen Sendiga,katibu tawala wa mkoa huo Happiness Seneda alisema kuwa mkoa wa Iringa umebarikiwa kuwa na ardhi ambayo inafaa kwa kilimo cha mazao yoyote yale
Seneda alisema kuwa watumishi wengi wa umma wamekuwa na hali ngumu kutokana na kutowekeza kipato chao katika ardhi jambo linalowaletea ugumu hasa pale wanapopata matatizo ya kufiwa au kufariki wao wenyewe.
Aliongeza kusema kuwa watumishi wengi wa Umma wamekuwa wakijikita katika vitendo vya anasa kama ulevi na uzinzi hali inayosababisha mishahara yao kutumika bila malengo na kuzifanya familia zao kuishi katika mazingira magumu.
“Watumishi wenzangu wa sekta za umma tunajisahau kwa sababu tunakuwa na uhakika wa kupata mishahara na malupulupu basi tumekuwa ni wanywaji pombe wa kupindukia tumekuwa wazinifu mwisho wasiku tunapata tabu pale mnapofariki maana unakuta nyumbani hakuna hata kitu cha kuanzia” alisema Seneda
Awali akizungumza mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Queen Sendiga alisema mkoa umejipanga kuja na kilimo mkakati kitakachowainua wananchi kiuchumi hivyo watumishi wa umma wanatakiwa kuwa mfano kwa kuwa na mashamba ya kilimo cha biashara.
Alisema ni aibu kwa mkoa wa Iringa kuonekana wananchi wake wanalia umasikini wakati mkoa umebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba inayozalisha mazao ya aina mbalimbali kama alizeti, nyanya, palachichi, mpunga mahindi na mengineyo.
Sendiga alisema mkakati walionao ni kuona kila kaya inakuwa na mashamba ya kulima na katika mashamba hayo eka moja ni lazima liwe shamba la kilimo maalumu cha biashara ili kuwainua wananchi wake.
‘’Niseme wazi ninachukizwa na hali ya wananchi wa mkoa wa Iringa wakati wamerikiwa ardhi yenye rutuba nyingi ya kilimo mkoa sasa umekuja na mkakati wa kuhakikisha kila kaya inakuwa nae ka moja ya kilimo maalumu cha zao la biashara na nitafuatilia hilo ukiona umelima kilimo kile cha mazoea hakikisha una eka moja ya kilimo biashara”alisema Sendiga.
Wakizungumza baadhi ya wakazi wa mkoa wa Iringa wamesema kuwa mkakati aliokuja nao mkuu wa mkoa ni mzuri na utawainua wananchi wa mkoa wa Iringa ambao wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea japo changamoto huwa katika suala la pembejeo.
Manaibu waziri wa Tanzania, Sweden wajadili Mabadiliko ya Tabia Nchi, Nishati jadidifu na uchumi wa blue
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande (kulia), akutana na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Nchini Sweden Mhe. Janine Alm Erickson kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya Sweden na Tanzania katika masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, Nishati jadidifu pamoja na uchumi wa blue. Kikao hicho kimefanyika leo 28/5/ 2021 katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es salaam na kimehudhuriwa na Balozi wa Sweden Anders Sjoberg, maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na NEMC

POLISI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI WATOA MAFUNZO KWA MADEREVA WA MABASI KITUO CHA MBEZI LUIS MKOANI DAR
JESHI la Polisi kitengo cha Usalama barabarani, limetoa mafunzo kwa mafundi magari waliyokuwa ndani ya Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Luis, Dar es Salaam kwa lengo la kuwafundisha namana ya kutambua vifaa ambavyo vipo kwenye magari hayo.
Mafunzo hayo yalitolewa kwa siku mbili na Mkuu wa Usalama Barabarani, ASP Ibrahim Samwix kwa lengo la mafundi hao kutambua mfumo wa injini ya gari unavyofanya kazi ili kuwarahisishia namna ya utengenezaji wa magari.
Pia,Mkuu huyo aliwafundisha kuhusu kifaa cha aina ya turbo kinavyofanya kazi, na namna ya kukitambua kama kikiwa kibovu, kwa sababu mafundi wengi wamekuwa wakifanya masuala ya ufundi kwa mazoea.
ASP Samwix alitoa pia mafunzo katika kifaa cha mfumo wa rejeta namna kinavyofanya kazi, kwa sababu mafundi wengi na madereva wamekuwa wakishindwa kutunza mabasi wanayopewa kutokana na mapungu madogo madogo.
Kabla ya mafunzo hayo, Mkuu huyo alianza na madereva kwa kuelimisha jinsi ya kufuata sheria za barabarani na kuendesha gari kwa mwendo ambao unatakiwa ili kuepusha ajali na kuokoa maisha ya wananchi.
Kwa wa upande wa madereva hao ambao walikuwa zaidi ya 40, walilishukuru Jeshi la Polisi kwa mafunzo hayo, kwa sababu yanawakumbusha kufuata sheria za barabarani, kutokana na kwamba wengi wanafanya kazi hiyo kwa mazoea.
Pia, wanasema ni mara yao ya kwanza kupatiwa mafunzo, kwa hiyowao wameona ni bahati kubwa kwa sababu wamejifunza mambo mengi kwa wakati mmoja kwa sababu wakati mwingine wanahisi kuwa wamesahaulika.
Aidha wameomba elimu hiyo na mafunzo hayo yawe endelevu kwa manufaa yao na kwa manufaa ya watumiaji wa barabara, wao wapo tayari muda wowote na pia wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Kwa upande wa abiria, Athuman Omary ambae ni Mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alitoa shukrani kwa jeshi hilo kwa elimu ambayo walikuwa wanaitoa kwa dereva na wamiliki wa mabasi kwa sababu inaonesha ni jinsi gani wanajali maisha ya abiria.
Pia, Mkazi wa Ubungo, Mwajuma Juma aliwata madereva hao kutumia mafunzo waliyoyapa kwa kupunguza ajali za usalama barabarani kwa sababu kuna baadhi ya madereva hawafuati sheria hizo kwa makusudi.
Wakati huo huo wawamiliki wa mabasi, wamelipongeza jehi hilo kwa mafunzo ambayo wamepewa madereva wao pamoja na mafundi wa mabasi, wanasema hiyo itaondoa ajali za barabarani, itasaidia ulinzi wa magari yao na pia ushirikiano baina ya askari na wao utakuwa wa manufaa.
Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi Luis Dar es eslaam, ASP Ibrahim Samwix akizungumza na mafundi wa magari waliyokuwa ndani ya Kituo cha Mabasi cha kwa lengo la kuwafundisha namna ya kutambua vifaa ambavyo vipo kwenye magari hayo.
Mafunzo hayo yalianza kutolewa Mei 27 mpaka Mei 28, 2021 jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi luis Dar es eslaam ASP Ibrahim Samwix akiendelea na kazi kama anayoonekana pichani(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
NAIBU KATIBU MKUU DKT MDOE ASHANGAZWA NA MSICHANA ALIYEBUNI KIFAA KINACHOTOA TAARIFA SEHEMU IVUJAYO GESI KWENYE BOMBA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Mdoe akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika Banda la Nacte kabla ya kuanza kutembelea maonesho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Nacte, Profesa Kondoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Mdoe (kulia) akitembelea banda la Chuo cha Taifa cha Utalii wakati wa maonesho hayo.
Dkt. Mdoe akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Mipango ya Muda Mfupi wa Benki Kuu (BoT), Tulla Mwigune kuhusu alama mbalimbali muhimu zilizomo kwenye noti alipotembelea banda hilo.
Dkt. Mdoe akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza NACTE, Profesa Kondoro.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Kemmy Product, Penina Kaminyonge (kushoto) akimueleza Dkt. Mdoe kuhusu bidhaa zao mbalimbali wanavyosindika ambazo wanauza kwenye maonesho hayo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE (TAWLA) CHAFANYA MKUTANO MKUU WA 31 WA MWAKA

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson Mwansasu akizungumza katika mkutano wa 31 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaofanyika kwenye Hoteli ya Coral Beach Masaki mkoani Dar es Salaam jana Jumamosi Mei 29,2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson Mwansasu akizungumza katika mkutano wa 31 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaofanyika kwenye Hoteli ya Coral Beach Masaki jijini Dar es Salaam jana Jumamosi Mei 29,2021 Katikati ni Lulu Ngw'anakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWLA na kushoto ni Mwanachama wa TAWLA Flaviana Charles Rwechungura.
Balozi Mwanaidi Maajal Mwanachama wa (TAWLA) akiongoza mjadala katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Coral Beach Masaki jijini Dar es salaam
Lulu Ngw'anakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TAWLA) akimkaribisha mgeni rasmi ili kuzungumza na wanachama wa taasisi hiyo katika mkutano huo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson Mwansasu kushoto, Lulu Ngw'anakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWLA na Mwanachama wa (TAWLA) Flaviana Charles Rwechungura wakishiriki katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tike Mwambipile akipiga makofi wakati mgeni rasmi Mh. Dk. Tulia Ackson hayupo pichani alipokuwa akizungumza.
Mwanachama wa (TAWLA) Flaviana Charles Rwechungura akizungumza katika mkutano huo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson Mwansasu kushoto akifuatilia mada katika mkutano huo.
Picha mbalimbali zikionesha wanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) wakiwa katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Coral Beach jijini Dar es salaam.


SHAMBA LENYE EKARI 100 LINAUZWA,LIMEPIMWA.
EURO 2020 KUKARIBISHWA NA MECHI KALI ZA KIMATAIFA
Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!
BAADA ya kumaliza mishemishe za vilabu na odds kubwa sana, sasa Meridianbet inakupa ushindi wa kibingwa sana katika mechi za kimataifa. Wachezaji wakubwa duniani wanaenda kuwakilisha nchi zao na Meridianbet tunakuhakikishia kuwa odds kubwa na za kijanja sana zipo katika mechi hizo, bashiri sasa!
Jumanne hii, kutakuwa na mechi ya kirafiki kabla ya michuano ya EURO 2020, Poland watakuwa nyumbani kuwaalika Russia. Meridianbet imekuwekea Odds ya kirafiki ya 2.35 kwa Poland ili kukupa ushindi mnono.
Siku ya jumatano, kutakuwa na mchezo kuchukua bingwa wa U-21, ambapo Ujerumani watakuwa nyumbani kucheza na Denmark, kwa upendo mkubwa kabisa, Ujerumani wamewekewa Odds ya 2.25 na Meridianbet kwa ajili yako!
Na siku ya Alhamis sasa, michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia 2022 itaendelea, Venezuela watakuwa ugenini kuvaana na Bolivia. Kwa kuthamini ushindi wako, Meridianbet imekuandalia Odds ya 2.00 kwa Bolivia.
Ni rahisi sana kuwa bingwa wiki hii, cha kufanya nikuchangamkia fursa tu. Piga *149*10# kujiunga au tembelea www.meridianbet.co.tz na ujiunge na familia ya mabingwa!