Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48915 articles
Browse latest View live

MHANDISHI MASAUNI: SERIKALI ILITOA MSAMAHA KWA WADAIWA WA KODI

$
0
0

  Na, Saidina Msangi na Josephine Majura, WFM, Dodoma

SERIKALI imesema kuwa katika Mwaka wa Fedha 2018/19 ilitoa msamaha kwa wadaiwa wa Kodi (Tax Amnesty) uliohusisha riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma ili kuongeza makusanyo.


Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Henry Maganga Nicodemus, Mbunge wa Mbogwe aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kufuta madeni ya muda mrefu kwa wafanyabiashara wa ndani yatokanayo na ukosefu wa elimu juu ya matumizi sahihi ya mashine za EFD wanayodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. 

 

Mhe. Masauni alisema kuwa msamaha huo ulilenga kusamehe malimbikizo ya nyuma ya riba na adhabu (Interest and Penalties) kwa kiwango cha asilimia 100 kwa wafanyabiashara wote hapa nchini ambao walikuwa na malimbikizo ya madeni hayo ya kodi.

Msamaha huo ulitolewa kwa kipindi cha miezi sita (6) kilichoanzia tarehe 1 Julai 2018 mpaka tarehe 31 Desemba 2018, kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wake, Serikali iliongeza muda wa msamaha huo kwa miezi sita ili wafanyabiashara waliokuwa na madeni hayo wakamilishe malipo husika”alieleza Mhe. Masauni.


Aidha Mhe. Masauni alisema kuwa hatua hiyo ya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi SURA 438 ilitarajiwa kuongeza mapato ya Serikali na kukusanya malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi (Principal Tax) pamoja na kuinua kiwango cha ulipaji kodi kwa hiyari kwa zaidi ya asilimia 10.


Mhe. Masauni aliongeza kuwa licha ya nia nzuri ya Serikali ya kufuta riba na adhabu ili kuwawezesha walipakodi wenye madeni sugu ya kodi kuyalipa kwa awamu ili kurahisisha mwendelezo wa biashara zao wengi wao hawakulipa kodi hizo hata baada ya kuingia mikataba na TRA na hata baada ya Serikali kuongeza muda wa ziada wa kufanya malipo ya kodi husika yaliyotokana na msamaha huo.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akijibu swali bungeni kuhusu msamaha kwa  wadaiwa wa  kodi jijini Dodoma.


MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AITAKA SERIKALI KUANZISHA MAHAKAMA YA FAMILIA “FAMILY COURT”

$
0
0

 

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo.
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo.

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira amesema ipo haja ya Serikali kuanzisha Mahakama ya Familia yaani Family Court kama ilivyofanya kwenye Mahakama za Ardhi ili kusaidia kuondosha changamoto zinazojitokeza ikiwemo Masuala ya Matunzo ya Watoto.

Amesema ili Matunzo ya Watoto yaweze kubebwa kwa uzito unaostahili na kupanua wigo mpana wa haki ili kuhakikisha changamoto za namna hiyo zinaondoka kwenye jamii badala ya kuendelea kuwepo kila wakati.

Aliyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati alipouliza Maswali Mawili ya Nyongeza baada ya Serikali kuwasilisha Majibu ua Swali lake la Msingi lililouliza "Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwakomboa Wanawake wanaobebeshwa mzigo mkubwa wa kugharamia matunzo ya Watoto bila msaada wa Baba?" 

Mbunge Neema alisema pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini hata kwa Sheria zilizopo bado kuna changamoto kubwa kwenye eneo hilo.

Mbunge Neema Lugangira alisema ndio maana hata Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ilani yake ya Uchaguzi 2020/2025 imeliona hilo na imeahidi kuielekeza Serikali kwenye Ukarasa wake wa 145 unaosema "CCM itaelekeza Serikali kuimarisha huduma za usuluhuhi wa migogoro ya ndoa na matunzo kwa watoto" na kwa msingi huo aliuliza maswali yake  mawili ya nyongeza.

Katika maswali yake ya nyongeza Mbunge Lugangira aliishauri Serikali iboreshe Sheria zilizopo ili gharama za matunzo ya watoto iendani na hali ya uchumi wa sasa na maisha ya sasa kutokana na maisha kuwa juu kuliko ilivyokuwa awali.

Akijibu Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Mhe Mwanaidi Khamisi amesema "Serikali imetoa maelekezo wazazi kuhakikisha mtoto anapata matunzo yote stahiki, na kama wazazi wa mtoto hawaishi pamoja na mtoto anaishi na Mama yake basi Baba atawajibika kugharamia malezi ya mtoto kulingana na kipato alichonacho". Swali hili pia lilimnyanyua Mhe Waziri Dkt Dorothy Gwajima ambae alisema "Nakiri tatizo Watoto kutelekezwa ni kubwa na ipo haja ya Serikali kufanya harakati za ziada ili kulidhibiti. 

Kwa upande mwingine Mbunge Neema Lugangira aliishauri Serikali ianzishe Mahakama ya Familia yaani Family Court na kwa upande wa Serikali, Mhe Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis alisema Serikali imekubaliana na ushauri wa Mbunge Neema Lugangira na ipo haja ya kuwa na chombo maalumu ambacho kitakuwa kinashughulikia masuala la familia hivyo wameupokea ushauri wa Mbunge Lugangira na wataufanyia kazi  kulingana na Sheria zilizopo.

RAIS DK. MWINYI AWAAHIDI MAHUJAJI CHANJO

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itawawezesha Mahujaji wake wote kupata chanjo ya maradhi ya COVID 19 ili kuweza kwenda kutekeleza  ibada ya Hijja nchini Saud Arabia mwaka huu. 

Alhaj Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa salamu zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wote mara baada ya Sala ya Ijumaa huko katika Masjid Omar bin Khatab, Msumbiji kwa Mabata, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.


Akitoa salamu zake hizo kwa waumini hao na wananchi kwa jumla, Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba mwaka jana waumini hawakuweza kwenda kutekeleza ibada hiyo tukufu kutokana na kuwepo kwa maradhi hayo duniani lakini mwaka huu upo mwelekeo kwamba ibada ya hija inaweza kuruhusiwa lakini kwa masharti. 


Hivyo, alieleza kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshajipanga kuwapatia Mahujaji wake wote chanjo hiyo itapatikana na kwa wale wote walioweka nia waendelee na maandalizi ya kwenda kufanya ibada ya Hijja mwaka huu.


Alhaj Dk. Mwinyi alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepata mwelekeo kwamba chanjo hiyo itapatikana kwa uhakika na haitokuwa na kikwazo cha aina yoyote na wale wote wanaopaswa kupata huduma hiyo kwa ajili ya kwenda kutekeleza ibada hiyo tukufu watapatiwa.


Aidha, Alhaj Dk. Mwinyi alisisitiza haja ya kuendeleza umoja na mshikamano na kueleza kwamba dini ya Kiislamu inawataka na kuwafunza waumini wake wote kuwa wamoja.


Alisema kwamba mifano mingi imetolewa katika hadithi za Mtume Mohamad (S.A.W), juu ya suala zima la umoja na kueleza kwamba kwa upande wa Zanzibar amani, utulivu na umoja vyote hivyo vipo na lililobaki hivi sasa ni kujitafutia maendeleo. 


Aliongeza kwamba lililobaki hivi sasa ni kuhakikisha kila mtu anafanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo yanayohitajika huku akiahidi kwa upande wake kufanya yale yote aliyoyaahidi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kuomba ushirikiano ili kuleta maendeleo nchini.


Alisema kwamba pale panapokemewa watu hufanya hivyo kwa nia njema kabisa na hatafutwi mtu wa kulaumiwa bila sababu na hufanywa hivyo ili wanaofaidika wawe wengi na sio wachache.


Sambamba na hayo, Alhaj Rais Dk. Mwinyi alilipokea ombi la msiikiti huo la kuwapatia zulia jipya na kusema kuwa ombi hilo atalifanyia kazi kwa haraka na kuwaahidi kuwafanyia mengine zaidi kwani milango yake iko wazi.


Mapema akisoma hotuba ya Sala ya Ijumaa Khatibu wa Msikiti huo Sheikh Othman Othman Hussein aliyaeleza mafunzo ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuimarisha umoja.


Katika hotuba yake hiyo Sheikh Othaman alisisitiza haja ya kuimarisha na kuendeleza umoja miongoni mwa waislamu kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na neema kubwa katika wanaadamu ni kuwa wamoja.


Aidha, Sheikh Othman aliueleza kwamba msingi mwengine unaoimarisha umoja ni kuwa na subira jambo ambalo waumini walijifunza sana katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Sheikh Othman alisisitiza subira na kutoa mifano ya aya za Qur-an tukufu pamoja na hadithi za Mtume Muhamad (S.A.W) zinazosisitiza suala zima la subira.


Nao waumini wa msikiti huo walieleza jinsi walivyofarajika kwa kusali pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi katika sala hiyo ya Ijumaa katika msikiti wao huo.


Pamoja na hayo, waumini hao walimueleza Alhaj Dk. Mwinyi ombi lao la kutaka kupatiwa zulia jipya la msikiti wao ili kuweza kufanya ipada zao ipasavyo, ombi ambalo Alhaj Dk. Mwinyi alilipokea na kulikubali mikono miwili. 

MAHAKAMA YA AFRIKA KUADHIMISHA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA

$
0
0

 

Rais wa Mahakama ya Afrika ya watu na haki za binadamu Jaji Silvain Ore akizungumza na waandishi wa habari  mkoani Dar es Salaam leo Mei 21, 2021 kuhusu maadhimisho ya miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya watu na haki za binadamu. Kulia ni Afisa Habari wa mahakama ya ya Afrika ya watu na haki za binadam, Sukhdev Chhatbar.
Afisa Habari wa mahakama ya ya Afrika ya watu na haki za binadam, Sukhdev Chhatbar akifafanua jambo kuhusu kuweka majina ya Mwalimu Nyerere  na Rais wa Afrika Kusini kutumika katika mahakama na ukumbi wa mahakama ya Afrika. kushoto ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya watu na haki za binadamu Jaji Silvain Ore
Afisa Itifaki wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ( African Court on Human and Peoples Rights), Tamambele Simba akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar es Salaam leo Mei 21, 2021.

KATIKA kuadhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ( African Court on Human and Peoples Rights), mahakama hiyo imesema itawaenzi  viongozi wawili mashuhuri wa Afrika, mwasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Mwasisi wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Mandela kwa kuyatumia majina yao katika ukumbi wa mahakama hiyo na maktaba yake.

Rais wa Mahakama hiyo Jaji Silvain Ore ameyasema hayo leo Mei 21, 2020  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 15 ya mahakama hiyo tangu kuanzishwa kwake yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Amesema, lengo kubwa na kufanya maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii pamoja na kuifahamu mahakama hiyo ili waweze kujua shughuli zake na kuitumia.

"Katika maadhimisho hayo kutokuwepo na kongamano maalumu la majaji kutoka nchi mbali mbali za Afrika, mashindano ya wanafunzi na mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari wa nchi za Afrika.

Naye,  Afisa Habari wa mahakama hiyo, Sukhdev Chhatbar ameeleza kuwa jina la Mwalimu Nyerere litatumika katika jengo la Maktaba kubwa ya mahakama hiyo lililojaa vitabu mbali mbali vya sheria na haki za binadamu huku jina la Nelson Mandela likitumika katika ukumbi wa kusikiliza kesi wa Mahakama hiyo ambao kwa sasa unaitwa Kibo.

Akijibu swali la iwapo mahakama hiyo ina mpango wowote wa kuja kutumia lugha ya kiswahili katika kutoa maamuzi yake, Afisa Itifaki wa mahakama hiyo, Tamambele Simba amesema mahakama  kuwa Mahakama hiyo huendesha shughuli zake kwa kutumia lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili.

Amesema, Kiswahili ni miongoni mwa lugha za Umoja wa Afrika (AU) na kwamba hata mahakamani hapo wanatumia lugha ya kiswahili.....mfano anapokuja mtu anayejua kiswahili basi kesi yake itaendeshwa kiswahili ama kwa kutumia mkalimani ama la."  Amesema Simba

“Mbali na kiswahili kule zinatumika pia lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kiswahili pia, Tunao wakalmani wazuri wa kutafsiri." Amesema Simba

 Mahakama ya kikanda iliyoanzishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kudumisha na kulinda haki za watu barani Afrika.

 Ilianzishwa kutokana na itifaki na mkataba wa Afrika wa watu na haki za Binadamu chini ya Ibara ya kwanza inayohusu  uanzishwaji wa Mahakama ya Afrika ya watu na haki za Bianadamu. 

Mkataba huo ilikubaliwa mwaka Juni 9,1998 na utekelezaji wake ukaanza Januari 25, 2004, lakini mahakama hiyo ilianza rasmi shughuili zake Novemba 2006.

Mpaka sasa ni nchi wanachama wa umoja wa Afrika (AU) 30 tu kati ya 55 ambazo zimesharidhia itifaki hiyo ikiwemo Tanzania.

Kati ya nchi hizo ambazo zimesharidhia itifaki hiyo ni nchi hadi kufikia Juni 2019 ni nchi tisa tu ndizo zilikuwa zimeshatoa tamko, la kuridhia itifaki hiyo ikiwemo Tanzania, hatua ambayo huwawezesha mtu binafsi na asasi zisizo za kiraia (NGO) kufungua kesi katika mahakama  hiyo kabla ya Tanzania kujitoa katika hatua hiyo  mwaka jana.

Serikali yasisitiza Kuendelea Kushirikiana na Sekta zenye tija kwa Taifa

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapo na Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Wadau wa Sekta ya Usafirishaji. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 21, 2021 Mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Wadau wa Sekta ya Usafirishaji katika mkutano uliofanyika leo Mei, 21,2021 Mkoani Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati katika mkutano uliofanyika leo Mei, 21,2021 Mkoani Dar es Salaam.

Picha ya pamoja.



SERIKALI yasisitiza Kuendelea Kushirikiana bega kwa bega na Sekta zenye tija kwa Taifa.

Akizungumza Mara baada ya Kufungua rasmi Kamati ya Ushauri wa Wadau wa Sekta ya Usafirishaji Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Leonard Akwilapo iliyofanyika Dar es salaam amesema Serikali imeridhika na utendaji wa kazi unaofanywa na chuo Cha Usafirishaji nchini (NIT).

"Ni chuo pekee ambacho tunaendelea kuona wataalam wakizalishwa siku Hadi siku kutokana na progamu zinazotolewa nakupatikana wahitimu hatimae hao hao wanakua wataalam hivyo kwa namna moja au nyingi inasaidia Serikali kutotumia pesa nyingi kutafuta wataalam wakigeni badala yake wazawa wanaimarishwa na kuwa wataalam wabobezi."

Hata hivyo ameeleza Malengo ya Serikali katoka kusaidia chuo hicho ni pamoja na kutoa Mafunzo ya kinadharia yatakayokidhi Mahitaji ya nchi katika sekta ya Usafirishaji.

Vilevile amesema kutokana na Sekta hiyo ya Usafirishaji Kuendelea Kupanuka ataimarisha na kununua Meli pamoja na ndege.

Pia amewataka wanakamati hiyo waweze kujadili Mambo yatakayowezesha Chuo hicho Kupiga hatua ya Kimaendeleo ili Kusaidia Sekta ya Uchukuzi.

Kwa Upande wa Mkuu wa chuo hicho Pro. Zacharia Mganilwa amesema Kuna baadhi ya Miradi inaendelea Kutekelezwa ikiwemo Kujenga Majengo 9 na katika Kampasi yatajengwa Majengo matano.

"Majengo mengine ambayo tulitegemea yangekaamilika ni pamoja na Uwanja wa ndege kwa Dar es salaam Kwa ajili ya Wanafunzi kufanya Nadharia na kutokana na changamoto imepelekea ujenzi huo kuchelewa tunategemea hivi punde utaanza rasmi."

Mbali na ujenzi ametaja Mitaa mitano mipya ambayo tayari imeshadahili Wanafunzi na kupata ithibati kutoka Nacte.

"Miongoni mwa Mitaala hiyo ni pamoja na Uhandisi katika Reli ya Kisasa (SGR)".

Ameomba Mashirika ambayo Wanafunzi watafika Kama sehemu ya Mazoezi yani Mafunzo kwa vitendo waendelee kutoa Ushirikiano.

"Baadhi ya Wanafunzi tayari wameshahudhuria Mafunzo kwa vitendo sehemu mbalimbali Kama Latra, TLC, Sumatra kwa takribani Mwezi mmoja hivyo ningependa kuwasihi watoe Ushirikiano wadhati katika Hilo kusudi tuwapatie Wanafunzi wetu Elimu ya Usafirishaji katika kila nyanja "

Pia ameweka wazi kuwa kuna watumishi 8 wako nchini za Uingereza, Singapore pamoja na China wenye Shahada ya uzamivu Wamepelekwa huko Kwa ajili ya kuendelea na masomo.

"Serikali ina nia ya dhati kuzalisha wataalam kutoka nchini kwetu ambao tutajivunia kuwa nao hivyo tumeona ipo fursa ya kupeleka watu ambao baadae wataendelea kuzalisha wataalam wengine."

TUNAFANYIA KAZI MAONI YA WADAU WA SEKTA NDOGO YA UTANGAZAJI KUHUSU UBORESHAJI WA SEKTA HIYO-SERIKALI

$
0
0

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi akizungumza na wadau mbalimbali  wakati wa kufungua kikao cha Majadiriano ya Jinsi ya Kuboresha Huduma za Utangazaji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari akitoa maeleylzo kuhusiana na Sekta ya utangazaji katika kikao cha Majadiriano ya Jinsi ya Kuboresha Sekta ya Utangazaji, kilichofanyika jijni Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Leseni wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akitoa maelezo katika kikao cha Majadiriano ya Jinsi ya Kuboresha Huduma za Utangazaji, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Habari Dkt.Jimmy Yonazi akisikiliza maoni ya wadau katika kikao cha majadiriano ya jinsi kuboresha Sekta ya Utangazaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi akiwa picha ya Pamoja na wadau Mara baada ya kufanyika kikao cha majadiriano ya jinsi kuboresha huduma ya Sekta ya Utangazaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

SERIKALI imeahidi kufanyia kazi maoni ya uboreshaji wa huduma za Utangazaji   yaliyotolewa na wadau katika kikao cha mashauriano ya jinsi ya kuboresha huduma za Utangazaji nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, ambacho kiliunganisha wadau kutoka maeneo mbalimbali  ya Tanzania,  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi amesema Serikali  iko tayari kujifunza kutoka kwa wadau hivyo washiriki wawe huru katika kuchangia.

Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kimekusanya maoni katika maeneo matano ambayo ni pamoja na tozo za leseni za Redio, Televisheni, Maudhui mtandaoni na Masafa ya Utangazaji.

Maeneo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na mfumo wa biashara kwenye urushaji wa matangazo ya televisheni yanayorushwa bila kulipia na mfumo wa biashara kwenye matangazo ya televisheni ya kulipia.

Aidha, matumizi ya kisimbusi kimoja ili kupata maudhui kutoka kwa watoa huduma tofauti; mikataba ya kibiashara kati ya vituo vya utangazaji na wasambazaji wa matangazo; na wajibu wa vituo hivyo katika leseni pia vimejadilidiwa.

Hii ni mara ya sita kwa mwaka huu 2021 ambapo TCRA imekuwa ikiandaa mikutano ili kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kuboresha huduma za Mawasiliano.

WANAFUNZI WATEMBELEA KIWANDA CHA SBL MOSHI

$
0
0

Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imeendelea kutoa mchango wake katika kusaidia kuimarisha sekta ya kilimo nchini  kwa kuwapa wanafunzi wa kilimo fursa ya mafunzo viwandani

 Ikiwa ni muendelezo wa kuwapa fursa wanafunzi wa taaluma ya kilimo kujifunza kwa vitendo, kampuni hiyo ilitoa nafasi kwa wanafunzi wa chuo cha Kilimo na mifugo cha Kilacha Kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro kutembelea kiwanda chake kilichopo Moshi mjini.

 Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, alisema, “programu ya Kilimo-Viwanda inawajengea wanafunzi wa kilimo uwezo wa kuelewa kwa vimatendo. Kupitia ziara hii wanafunzi wameza kujionea namna malighafi za mashambani zinavyotumika kutengeneza bia’’.

 Ocitti alifafanua kuwa ufadhili hchini ya Kilimo Viwanda unajumuisha malipo yote ya chuo na gharama zingine katika kipindi chote cha masomo kwa wanafunzi wanaochaguliwa na kuongeza kuwa programu hiyo inawalenga wanafunzi wanaotoka katika familia maskini ambazo haziwezi kumudu kugharamia masomo kwa Watoto wao.

 Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa program hiyo imelenga kusaidia juhudi za serikali kuongeza idadi ya maafisa  kilimo. “SBL ni mzalishaji wa bia mkubwa nchini kwa kutumia nafaka za ndani katika utengenezaji wa bia. Hadi sasa SBLinafanya kazi na mtandao wa wakulima 400 kwenye mikoa nane nchini ambapo tunanunua nafaka kama shayiri, mahindi na mtama kwa ajili ya uzalishaji bia. SBL inatumia takribani tani 17,000 sawasawa na asilimia 70 na mahitaji yao kwa mwaka.,” alisema

 Programu ya ufadhili wa masomo ya Kilimo Viwanda ilianzishwa mwaka 2020 na julma ya wanafunzi 71 wamenufaika nayo kwa kupata fursa ya kusomea kozi za diploma ya kilimo katika vyuo vingine vitatu ambavyo ni Kaole Wazazi College of Agriculture (Bagamoyo), cha Igabiro Training Institute of Agriculture (Bukoba) na St. Maria Goretti Agriculture Training Institute (Iringa).

 Katika upande wake, meneja msaidizi wa chuo hicho, Padre Jerome Silayo aliipongeza kampuni ya bia ya SBL kwa msaada wao wa katika kusaidia maendeleo ya kilimo na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano katika kuwasaidia wanafunzi kutoka familia masikini nchini.

Mtaalam anayehusika na malighafi zinazotumika kutengeneza bia wa SBL, Deogratius Adam (kushoto) akiwaelezea wanafunzi wa chuo cha Kilacha shughuli za ufungaji wa nafaka zinazozalisha bia ya Serengeti kwenye kiwanda cha SBL, Moshi.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti (kulia) na meneja wa Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kilacha Padre Jerome Silayo (kushoto) pamoja na wanafunzi wa chuo hicho waliotembelea kiwanda cha SBL cha Moshi ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo.

Mtaalam anayehusika na malighafi zinazotumika kutengeneza bia wa SBL, Deogratius Adam (kushoto) akiwaelezea wanafunzi wa chuo cha Kilimo na na Mifugo Kilacha hatua mbali mbali ambazo hupitiwa wakati wa utengenezaji wa bia wakati wanafunzi hao walipotembelea kiwanda cha SBL kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kampuni ya bima ya Strategis yajitosa kuhudumia Arusha

$
0
0
KAMPUNI ya Bima ya Strategis, ikiwa ni kampuni binafsi ya bima ya pili kwa ukubwa nchini na moja ya makampuni ya mwanzo kusajiliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za Bima Tanzania (TIRA) na ambayo imekuwa ikifanya biashara kwa zaidi ya miongo miwili, imezindua rasmi ofisi yake jijini Arusha.

Akiongea katika uzinduzi huo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Utafiti wa TIRA ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, Zacharia Muyengi, alisema kuingia kwa kampuni hiyo jijini Arusha kutanufaisha wakazi wa jiji hilo na maeneo jirani na hivyo kuchangia kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za bima kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 15.

“ Ni asilimia 15 tu ya Watanzania ndio wanatumiahuduma za bima, mkakati wetu ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 50 ya watu watakuwa wanatumia huduma hizo,, na wakati huo huop kiwango cha uelewa wa maswala ya bima kitaongezeka kutoka asilimia 30 ya sasa hadi asilimia 80, “ alisema Muyengi.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kuwezesha makampuni ya bima kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, tunategemea watoaji wa huduma hizo nao wataitikia wito wa serikal kwa kulipa wateja wao kwa muda muafaka. Nachukua fursa hii kutoa wito kwa makampuni ya bimakuja na bidhaa zinazokizi mahitaji ya Watanzania,kama vile wavuvi,wafugaji na wakulima.”

Vilevile aliipongeza kampuni ya Strategia na kuiomba kuendeleza utamaduni wakewea kulipa madai ya wateja wake kwa muda unaofaa. Alisema:” Sisi TIRA kwa upande wetu tunafurahishwa na namna kampuni ya Strategis inavyofanya kazi, wana uwezo wa kifedha wa kutosha na wanafanya malipo kwa haraka”

Uzinduzi wa ofisi hii ya mauzo ni sehemu ya uamuzi wa kimkakati wa Strategis kuboresha ufanisi na manufaa ya shughuli zake katika jiji la Arusha na kanda nzima ya kaskazini.

Katika mwaka uliopita,kampuni ya Strategis iliimarisha ukuaji wake na kukua kwa asilimia 20 hadi kushika nafasi ya kampuni binafsi ya bima ya pilli kwa ukubwa nchini Tanzania kwa kuzingatia umiliki wa soko. Wakati kampuni hii inaendeela kuongoza katika bima ya afya kwa sekta ya binafsi, shughuli zake zisizo za afya zimekua kwa asilimia 40 kwa mwaka 2020. Ukuaji huu unatokana na marekebisho ya kimuundo yaliyofanywa na kampuni hiyo kuimarisha nafasi yake katika sekta ya bima, pamoja na kuungwa mkono na wadau mbalimbali.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis ( Kitengo cha Tiba) ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni la Strategis, Dr. Flora Minja,alisema kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatilia mkazo katika kukuza wigo wa huduma zake, kuzindua huduma mpya na kutumia teknolojia na ubunifu katika utoaji wa huduma.

“ Hivyo basi mkakati wetu ni kuhakikisha kuwa tunakwenda sambasamba na maendeleo ya teknolojia ambayo zinaongeza ufanisi na usahihi katika kutunza za taarifa za wateja, na tutahakikisha kuwa tunakwenda na wakatina maendeelo ya teknoloji yanayotokea kwenya sekta ya bima na kuwasiliana na wadau mbaliombali kwa muda muafaka.”

“ Kampuni ya Strategis inaunga mkono ajenda ya huduma ya bima kwa wote,na inaunga mkono lengo la serikali na watoa huduma za bima lakuhakikisha kuwa ifikapomwaka 2030 angalau asilimia50 ya wananchi watakuwa wanatumia huduma za bima. Ili kufaniklisha hili,kampuni yetu inanui kupanua eneo lakelaklutoa huduma, na ofisi hii ya Arusha ni miongoni mwa mikakati ambayo inatarajiwa kuhakikisha kuwa tunafikia kila kikundi nchini,” Alisema Dr. Flora.

Awali akiongea katika uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis ( huduma zisizo za tiba), Jabir Kigoda,alisema kampuni hiyo imejizatiti kutoa huduma za kiwango cha juu kwa mkoa wa Arusha, mkakati ambao utaimarshwa na uzinduzi wa bidhaa zinazolenga sekta ya utalii, pamoja na sekta nyinginezo za uchumi kama viwanda na uzalishaji.

Uzinduzi wa ofisi yetu ya Arusha ni kiashirio cha namna gani tumejiandaa vyema kuhudumia soko labima na kunga mkono harakati za serikali za kuongeza uelewa na matumizi ya huduma za bima nchini,’ akisema Kigoda.

Aliongeza Kigoda : “ Uzinduzi hu unaofanyika leo ni zaidi ya ufunguzi wa ofisi jijini Arusha. Kwetu sisi uzinduzi huu unaonyesha nia namna gani tupo makini kuhudumia wateja wetu, ambao tunawapa kipaumbele. Tunaamini uwepo wa ofisi hii utaleta ushindani wenye manufaa sokoni na kusaidia kufikisha huduma kwenye sekta zilizoachwa nyuma na huduma za bima kama utalii, kilimo bishara na viwanda.

“ Tuna uhakika kuwa uwepo wetu hapa Arusha utakuwa na manufaa katika mkoa mzima na kwamba huduma zetu hapa zitakuwa na kuwa bora zaidi. Tutaendelea kujenga na kuimarisha ushirika dhabiti kwa kutoa viwango vya juu vya malipo ya bima, huduma za ushauri wa majanga mbalimbali na kufupisha muda wa kulipa wateja”

Sekta ya bima nchini imekuwa ikikua kwa asilimia 17.7 kwa mwaka, huku mapato ya bima yakipanda hadi kufikia Tsh 814.5bn kwa kipindi cha mwaka wa 2019-2020, kutoka mapato ya Tsh 691bn mwaka uliotangulia. Vilevile katika kipindi hicho,TIRA imesajili makampuni ya bima 31, madalali 10 na mawakala 780.

Kampuni ya Strategis inamilikiwa asilimia 100 na wazawa na wafanyakazi wake asilimia 100 wanatoka nchini humu. Mbali na ofisi iliyozinduliwa Arusha,kampuni hii ina ofisi nyingine Zanzibar na Dar es Salam..
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko na Utafiti wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Zakaria Muyengi (katikati), akipozi kwa picha na kutoka kushoto; Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Strategies, Dennis Bimbo, Ofisa Mwwndeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Dr. Malav Manek,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Strategies (kitengo cha tiba), Dk. Flora Minja, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategies (kitengo kisicho cha tiba), Jabir Kigoda na Meneja wao Mkuu, Nirmal Sheth muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategies (kitengo kisicho cha tiba), Jabir Kigoda, akizungumza katika hafla hiyo mjini Arusha jana

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategies (kitengo cha tiba), Dr. Flora Minja, akihutubia wakati wa uzinduzi huo mjini Arusha jana.

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Zakaria Muyengi (kutoka kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Strategies (kitengo cha tiba), Dk. Flora Minja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategies (kitengo kisicho cha tiba), Jabir Kigod,a wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya ya kampuni hiyo jijini Arusha jana. kulia ni Meneja Mkuu wa Strategies, Nirmal Sheth.




Jezi mpya za Meridian Bet zaipa mzuka LCL kwenye ligi Kuu ya Walemavu

$
0
0

Kampuni ya Meridian Bet yatoa  msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya kubashiri  matokeo ya Meridian Bet umeipa mzuka timu ya Lenster senior  league (LCL) wa kushinda ubingwa tena wa Ligi Kuu ya walemavu itakayoanza Juni mwaka huu.

Timu hiyo yenye wachezaji saba wa timu ya taifa imekabidhiwa msaada wa jezi, vikinga ugoko, njumu, mipira na soksi vilivyotolewa na Meridian Bet.

Meneja wa Meridian Bet, Ernest John  na Meneja Mwendashaji Mkuu  Tanzania, Corrie Borman walikabidhi msaada huo katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Meridian Bet na kueleza kuwa ni muendelezo wa kampuni yao kusaidia jamii yenye uhitaji nchini.

Nahodha wa LCL, Alphan Athuman aliyeambatana na wachezaji wengine na uongozi wa timu amesema msaada huo ni chachu kwao kufanya vizuri na kuuahidi uongozi wa Meridian Bet kurejea na kombe mwishoni mwa msimu baadae mwaka huu.

Waziri Mwambe akutana na Wafanyabiashara Jumuiya ya Ulaya.

$
0
0

 

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Godfrey Mwambe akizungumza na wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuhusiana na fursa zilizopo za Uwekezaji nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi-Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza fursa zilizopo katika sekta ya Mifugo kwa Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt.Godwill Wanga akizungumza kuhusiana na mikakati ya baraza hilo katika ukuzaji wa biashara nchini.
Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Manfredo Fanti akizungumza kuhusiana na na majadilioano kati ya Serikali ya Tanzania  na Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam.

*Awahakikishia fursa za Uwekezaji nchini na milango iko wazi .

*EUBG wafurahishwa kukutana na viongozi wa Serikali ya Tanzania kufanya majadiliano.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 
 WAZIRI wa Nchi Ofisi Waziri  Mkuu Uwekezaji, Godfrey Mwambe amesema kuwa Tanzania ina fursa  za Uwekezaji na kutaka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuja kuwekeza na milango iko wazi.

Mwambe aliyasema hayo wakati alipokutana katika kikao cha majadiliano na Wafanyabiashara wa Jumuiya  Umoja wa Ulaya kilichofanyika  jijini Dar es Salaam.

Mwambe alisema kuwa Serikali ya Tanzania kuwezesha taratibu kwa wafanyabiashara kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Nae Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi-Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema sehemu ya Uwekezaji ni Sekta ya mifugo kwani Tanzania  kwa upande wa Ngozi na nyama ambapo Masoko wanaweza kufanyia katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

Profesa Ole Gabriel amesema kuwa nchi za jumuiya za Ulaya wana akiba fedha ambao wanaweza kuwekeza na nchi ikaweza kupata fedha za kigeni pamoja kuongeza ajira.

Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EUBG), Cikay Richards alisema ujio wa Umoja huo ni kufanya majadiliano na Serikali ya Tanzania katika kuangalia namna ya fursa ya za Uwekezaji zilizopo Tanzania.

Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Manfred Fant amesema kuwa majadiliano na Serikali ya Tanzania yanafungua milango kwa wafanyabiashara kuwekeza Tanzania.

Amesema kuwa katika Uwekezaji huo wataongeza Maendeleo ya nchi katika ukuaji wa uchumi kupata fedha za kigeni.

Kwa  upande wa Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga amesema kuwa TNBC ni kutaka kuongeza biashara nyingi ambapo EUBG wakiwekeza wanakuwa wameongeza ajira pamoja na kuongeza fedha za kigeni.

Dkt.Wanga amesema kuwa kumekuwa na hatua mbalimbali za serikali katika kutatua changamoto ziliopo katika sekta binafsi.

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA ALIKO DANGOTE

$
0
0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Mei, 2021.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Mei, 2021.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Mei, 2021



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Mei, 2021. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Masauni, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata pamoja na wajumbe wengine waliombatana na Alhaji Aliko Dangote.



Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU



WAHUKUMIWA JELA KWA RUSHWA

$
0
0

  Na Mwandishi wetu, Simanjiro

MWENYEKITI wa soko la Mirerani, Mkoani Manyara, Yesaya Songelael Yindi amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la kutoa rushwa ya shilingi 407,000 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Simanjiro, Yefred Myenzi

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu, ameyasema hayo ofisini kwake mjini Babati, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Makungu amesema pia, Mahakama hiyo ya Wilaya ya Simanjiro, imemuhukumu kifungo cha kwenda jela miezi 12  au kulipa faini ya shilingi milioni moja mfanyabiashara wa mji mdogo wa Mirerani Antipas Benedict Ngelesh kwa kosa la kukaidi amri halali ya Mkurugenzi huyo ya kubomoa kibanda.

Amesema wafanyabiashara hao wamehukumiwa kwenye kesi hiyo ya jinai namba 47/2020 na Hakimu wa mahakama ya wilaya ya hiyo ya Simanjiro Nicodemo Onesmo.

Amesema kwenye hukumu hiyo mstakiwa Songelaeli amefanya kosa hilo kinyume na kifungu cha kuzuia rushwa cha 15 (1) (b) na 15 (2) ya cha sheria ya kuzuia rushwa namba 11/2007.

Amesema awali, mawakili wa TAKUKURU, Martin Makani na Evelin Makani waliwasilisha ushahidi usioacha shaka mahakamani hapo na kusababisha adhabu hizo kwa washtakiwa hao.

Amesema Mahakama hiyo iliridhika kupitia ushahidi huo na vielelezo kuwa Songelaeli ambaye ni Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Mirerani alimtumia Myenzi rushwa kwa njia ya mtandao ili asivunje kibanda hicho cha kuoshea magari kilichojengwa na Ngelesh nje ya utaratibu.

Amesema Songelaeli mwenye ushawishi mkubwa kwenye eneo hilo alimtumia Myenzi fedha hizi kwa njia ya rushwa ili amshawishi kubadili amri ya kuvunja kibanda hicho cha Ngelesh ambaye naye hakukivunja ili kutekeleza agizo hilo hadi walipokamatwa na TAKUKURU na kufikishwa Mahakamani.

Amesema Mahakama iliwatia hatiani washtakiwa wote wawili kama walivyoshtakiwa huku wakili wa utetezi Shirima akiwaombea huruma washtakiwa hao kwa kutokuwa na taarifa za uhalifu huko nyuma, matatizo ya kiafya na watoto wanaowategemea huku mawakili wa TAKUKURU wakiiomba Mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria.

"Ni rai yetu watumishi wa umma mkoani Manyara, kukataa rushwa kwa kutoa taarifa TAKUKURU kama alivyofanya Mkurugenzi wa Simanjiro Myenzi, ikiwa wote tutashirikiana na kuzingatia misingi ya uadilifu tuliyojiwekea katika utumishi wa umma vita dhidi ya rushwa itakuwa nyepesi na watoa rushwa nao hawatatoa watahofia sheria kuchukua mkondo wake." amesema Makungu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati.

VIJANA ZAIDI YA 200 WAPATIWA MAFUNZO NA BENKI YA NMB JIJINI DODOMA

$
0
0
Zaidi ya vijana 200 wa Jiji la Dodoma wanaojishughulisha na usafishaji wa abiria kwa bodaboda na pikipiki za miguu mitatu, jana walipatiwa mafunzo na Benki ya NMB ya jinsi gani wanaweza kujiongezea kipato na pia kuchangamkia fursa pale zinapopatikana.

NMB vile vile iliwapa elimu juu ya mikopo mbalimbali inayotolewa na benki hiyo ikiwemo ya bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu kupitia mpango wao wa ‘Miliki Chombo na NMB’ – ambao kwa mwaka huu, imetenga Sh. bilioni 5 kwa ajili ya kuwakopesha kundi hilo.

Mpango huu wa Miliki Chombo na NMB umelenga kuwafikia vijana wengi nchini kote, kama njia ya kuwapa ajira vijana ambao bado hawajaingia katika mfumo wa ajira ili na wao waweze kupata kipato cha kujikimu kimaisha.

Akizungumza katika hafla ya uzunduzi wa mpango huu wa Miliki Chombo na NMB, Meneja wa NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi alisema mpango huo ni fursa tosha kwa vijana wenye nia ya kujiajiri, kwani pia masharti yake ni nafuu na kuwaasa vijana wengi kuchangamkia fursa hiyo. Lakini pia, aliwataka watembelee matawi ya NMB ili kupata ushauri zaidi ni namna gani wanaweza kuupata huo mkopo na wakutane na watalaam ili kujadili watakavyoweza kuendesha biashara hiyo kiurahisi.

Kwa upande wake Naibu Meya wa Jiji la Dodoma – Emmanuel Chibago aliiishukuru benki ya NMB kwa mpango huo, kwani ni mojawapo ya juhudi za kuiunga Serikali Mkono katika juhudi zake za kuongeza ajira kwa vijana.

Bwana Chibago aliwataka vijana watakao chukua mkopo huo kuwa waaminifu kwa NMB ili waweze kufikia malengo yao. Mpango huu Miliki Chombo na NMB umeshafika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma




Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Miliki Chombo na NMB Jijini Dodoma inayolenga kuwakopesha vijana bodaboda na pikipiki za miguu mkitatu, Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi na mwisho kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kadi NMB – Philbert Casmir, Mkuu wa Idara ya Biashara- Alex Mgeni(mwenye fulana ya bluu) pamoja na Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Dodoma – Kenneth Chimoti.



Mameneja wa NMB matawi ya mjini Dodoma wakiashiria kuwa tayari kuelimisha vijana kuhusu mkopo wa bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu ‘Miliki Chombo na NMB’ baada ya uzinduzi wa mpango huo Jijini Dodoma.

Waendesha bodaboda na pikipiki za miguu mitatu wakifurahia uzinduzi wa Miliki Chombo na NMB uliofanyika katika ukumbi wa Dear Mama – Jijini Dodoma.

Zantel yamtangaza msanii ‘Zuchu’ kuwa balozi wa Zantel 4G

$
0
0
· Ni kupitia kampeni yake ya Pasua Anga Ki Zantel 4G ambayo imelenga kutoa elimu juu ya matumizi yenye tija ya mtandao wa 4G

Zanzibar.21 Mei 2021. Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel leo imeingia makubaliano na msaniI wa muziki kutoka kundi la Wasafi ‘WCB’ Zuhura Othman Soud maarufu kama ‘Zuchu’ kuwa balozi wa mtandao wa Zantel 4G.

Tukio la utiaji saini makubaliano hayo lilifanyika katika makao makuu ya Zantel yaliyopo eneo Amani-Zanzibar na kushuhudiwa na menejimenti ya Wasafi pamoja na waandishi wa habari.

Mkuu wa Biashara wa Zantel, Aneth Muga alisema kampuni hiyo ina imani kubwa na msanii huyo kutokana na ukweli kuwa ni moja ya kipaji kutoka Zanzibar na anaufahamu vema mtandao wa Zantel.

“Zantel kwa sasa tunaendesha kampeni yetu inayojulikana kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ ambayo inalenga kufanya uelimishaji juu ya matumizi yenye tija ya mtandao wa 4G.Zuchu amekuwa mfano mzuri wa namna anavyotumia mtandao wa 4G kuendeleza kipaji chake na ameweza Kupasua Anga kitaifa na Kimataifa,” alisema Muga.

Aliongeza kuwa mbali na uelimishaji, kampeni hiyo imelenga kuinua na kutambua vipaji mbalimbali kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo za michezo, muziki pamoja na uchekesahji ‘comedy’.

“Sote ni mashahidi juu ya namna gani msanii huyu alivyoweza ‘Kupasua Anga’ na kuwa mmoja ya msanii wa kike mashuhuri hapa nchini.Zuchu anakwenda kuwa balozi wa Kampeni yetu hii ya Pasua Anga Ki Zantel 4G ambayo itafanyika kwa muda wa miezi 6 mfululizo,” alisema.

Katika ulimwengu huu wa kidigitali, simu ya mkononi imekuwa sehemu muhimu sana ya maisha yetu.Kupitia simu tu,unaweza kufanya mambo mengi sana kwa haraka na urahisi zaidi. Mfano, kukata tiketi za safari mbali mbali kama ndge au boti, kununua na kuuza bidhaa mbali popote ulimwenguni,kujiendeleza kielimu, kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki na mengine mengi.

Kwa kutambua hilo, Kampuni ya Zantel tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtu anafikiwa na mtandao wetu hasa intaneti yenye kasi ya 4G ili kuishi maisha ya kidigitali.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Zuchu alisema “Nimefurahi sana kuwa balozi wa kampeni hii ya Pasua Anga Ki Zantel 4G, ukizingatia mimi ni moja ya wasanii kutokea Zanzibar hivyo naifahamu vizuri Zantel,” alisema na kuongeza

“Intaneti ni kitu muhimu sana kwangu, siwezi kukaa masaa 24 bila kuwa na mtandao hasa mtandao wa 4G ambao utaniwezesha kufanya mambo mbalimbali kwa haraka zaidi,” alisema Zuchu.

Zuchu anakuwa balozi wa kampeni hiyo ambayo itadumu kwa miezi sita ambapo atafanya mambo mbalimbali ya uelimishaji kupitia matamasha ya muziki pamoja na mitandao ya kijamii.

Mkuu wa Biashara na Masoko wa Zantel, Bi.Aneth Muga (wa pili kushoto) na Msanii wa Bongo flava kutoka lebo ya WCB Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ wakisaini mkataba wa makubaliano ambapo msanii huyo atakuwa balozi wa mtandao wa Zantel 4G.Kushoto ni Mkuu wa Zantel-Zanzibar Mohamed Khamis Mussa pamoja na menejimenti ya kundi la Wasafi.


Mkuu wa Biashara wa Zantel, Bi.Aneth Muga (wa pili kushoto) na Msanii wa Bongo flava kutoka lebo ya WCB Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ wakionesha mkataba wa makubaliano ambapo msanii huyo atakuwa balozi wa mtandao wa Zantel 4G.Kushoto ni Mkuu wa Zantel-Zanzibar Mohamed Khamis Mussa pamoja na menejimenti ya kundi la Wasafi.

Bondia Jongo atamba kutwaa ubingwa wa ABU wa uzito wa Juu

$
0
0
Bondia wa uzito wa juu wa ngumi za kulipwa nchini, Shaaban Jongo ametamba kumsambaratisha mpinzani wake kutoka Nigeria, Alanrewaju Durodoro katika kuwania ubingwa wa Afrika (ABU) lililopangwa kufanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Next Door Arena.

Mabondia hao watapinana katika pambano la utangulizi la raundi 10 ambapo siku hiyo bondia Hassan Mwakinyo atazichapa na bondia kutoka Angola, Antonio Maiala kuwania ubingwa wa Afrika wa ABU wa uzito wa super welter katika pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya The Jackson Group Sports chii ya Afisa Mtendaji Mkuu Kelvin Twissa.

Jongo alisema kana kuwa amejiandaa vizuri na pambano hilo na kamwe hata mdharau mpinzani wake kufuatia ushindi wake wa mfululizo dhidi ya bondia Alphonce Mchumiatumbo wa Tanzania na Mmarekani, Shawn Miller.

Alisema kuwa rekodi za Durodoro zinaonyesha jinsi gani bondia huyo alivyo na uzoefu mkubwa katika ngumi za kulipwa kwa kushinda mapambano 34 na kupoteza manane. Jongo mpaka sasa ameshinda mapambano manane, kupoteza moja na kutoka sare mara mbili. Alisema kuwa pambano hilo litamfungulia njia yake ya kucheza kwenye mikanda ya ubingwa wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) na hivyo lazima ashinde.

“Nipo tayari kwa pambano, najua uwezo wa mpinzani wangu na kamwe sitampa nafasi, natarajia upinzani mkali sana,” alisema Jongo. Durodoro aliyewasili jana alisema kuwa amekuja kuendeleza rekodi yake ya ushindi dhidi ya Jongo.

“Nimekuja kwa ajili ya ushindi na siyo kushinda, nimejiandaa vyema na najua nini cha kufanya siku ya pambano,” alisema Durodoro. Mbali ya kuwasili kwa Mnigeria huyo ma mabondia wawili wa Bulgaria Pencho Tsvetkov na mwanadada Joana Nwamerue waliwasili mapema zaidi tayari kwa mapambano hayo.

Tsvetkov atazichapa na Mtanzania Daniel Matefu katika pambano la uzito wa juu wakati Joana atazichapa na Mtanzania Leila Yazidu katika pambano la uzito wa super-light.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Jackson Group Sports, Kelvin Twissa alisema kuwa mabondia wengine Sibusiso Zingange, Antonio Maiala na Chris Thompson watawasili leo wakati bondia wa Congo Brazzavile Ardi Ndembo atawasili kesho. Twissa alisema kuwa tiketi zinauzwa kwa sh50,000 kwa viti za kawaida na Sh200,000 kwa viti maalum. Tiketi hizo zinauzwa kwa njia ya ontapp na Nilipe katika pambano hilo lililodhaminiwa na KCB Bank, Tanzania Tourist Board, DStv, Onomo Hotel, M-Bet na Plus Networks Ltd.


Bondia wa Nigerian Alanrewaju Durodoro (wa pili kushoto) na kocha wake Adefemi Babafemi (wa pili kulia) wakiwasili uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa pambano la Ijumaa dhidi ya Shaaban Jongo wa Tanzania katika Rumble in Dar 2 kwenye ukumbi wa Next door Arena. Wengine katika picha ni maofisa wa kampuni ya Jackson Group Sports. 





RC MAKALLA AKUTANA NA WAZEE WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo May 24 ameanza rasrmi majukumu yake kwa kukutana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam ambapo ameweka utaratibu wa kufanya kikao nao kila baada ya miezi mitatu.

RC Makalla amesema anatambua hamani na Mchango wa Wazee Katika jamii hivyo ameona ni vyema kuanza majukumu yake kwa kukutana nao ili kuchota busara na Baraka zao kwani anatambua Wazee ni hazina Muhimu.

Aidha RC Makalla amesema Katika kutatua kero na changamoto za Wananchi amepanga kuanza ziara ya utatuzi Kata kwa Kata hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anayo dhamira ya dhati kuzipatia majibu kero zao.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwakuwa Mkoa wa Dar es salaam ni Mkoa mkubwa na Wenye kutoa taswira ya nchi nzima kwenye kila nyanja mbalimbali, amejipanga kuhakikisha Jiji linakuwa shwari na watu wanafanya shughuli zao pasipo usumbufu wowote Kama maono na mategemeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho kwanza Wamemshukuru na Kumpongeza RC Makalla kwa namna anavyoheshimu Wazee na wamemuahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha Katika majukumu yake.

Aidha Wazee hao wamesema Wana Imani kubwa na RC Makalla kwakuwa *wasifu wake wa uongozi unaonyesha kila alipopita amekuwa akiacha alama hivyo wanaamini atafanya Mambo makubwa na Mazuri Katika Mkoa wa Dar es salaam.

FAINALI YA EUROPA LEAGUE KUPIGWA WIKI HII

$
0
0

 

*Meridianbet, NyumbaYenye Odds Bora naBonasiKubwa! 

MWISHO wa safari moja nimwanzowanyingine! Hukuligimbalimbalizikitamatika,liginyinginezimeanzanafainalikubwakibaokupigwa wiki hii. Meridianbetimekuandalia Odds za kijanjasanakwenyemechi za fainalihizo, bashiri sasa!

Jumannehii, kule Red Star Stadium kutakuwanafainaliyaSerbian Cup, ambapoCrvena Zvezdawatakuwanakibarua cha kuchezanaPartizan. Mechihiinikubwasanahuko Serbia, naMeridianbetkutambuaukubwa wake tumekuwekea Odds ya 2.45 kwaCrvena Zvezda.

Siku yaJumatanokutakuwanakilele cha Ligiya Europa. Manchester UnitedwatakuwakibaruanikupambananaVillareal, katikafainaliya Europa League. UkichaguakubashirinaMeridianbet, Odds ya 1.93 imewekwakwa Manchester Unitedkwaajiliyako!

Na Alhamis, kule Norway, kutakuwanamechiyakukatanashokakatiyaSandefjord vs Rosenborg. LigiyaEliteserien ndo kwanza imepamba moto. Merididianbetwameweka Odds ya 1.65 kwaRosenborgilikukufaidisha,bashiri sasa!

MKUU WA MAJESHI APONGEZWA UJENZI WA UWANJA GOFU DODOMA

$
0
0
Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara (katikati ) akiwa na baadhi ya wachezaji na wachezaji wasaidizi kwenye Kibanda cha Kupumzikia wachezaji wakati wa zoezi kuzindua kibanda hicho katika Uwanja wa Gofu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara (Katikati) akizindua jiwe la msingi kwenye Uwanja wa gofu wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo Dar es Salaam wanaomtazama ni Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo wa kwanza kulia , balozi Ombeni Sefue, Profesa Wineaster Anderson na wakwaza kushoto ni Dk Edmund Mdolwa.
Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara (wapili kulia) akikata Utepe kwenye Kibanda cha Kupumzikia wachezaji kulia kwake ni Mwenyekiti wa Klabu ya Golf Lugalo Brigedia jenerali Mstaafu Michael Luwongo ,Balozi Ombeni Sefue, Nahodha wa Lugalo Kapteni Japhet Masai na Wakwanza kulia ni Joseph Kitani Mchezaji wakati wa zoezi katika uwanja wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalio Jijini Dar es Salaam jana.

Na.Kapteni Selemani Semunyu JWTZ
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amepongwezwa kwa Jitihada za Kujenga Uwanja wa Golf Jijini Dodoma.

Hayo yalisemwa Jana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara wakati akizindua kivuko na kibanda cha kupumzikia Wachezaji wakati wa Mazoezi katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

" Mwanzo tulipata eneo yatakapojengwa Malao Makuu ya Jeshi Dodoma lakni ilikuwa mbali lakini kwa Kilimani ni eneo sahihi, " Alisema General Waitara.

Jenerali Mstaafu Waitara aliongeza kuwa uwanja huo kujengwa itamfanya Mkuu huyo wa Majeshi kuacha kumbukumbu kubwa kati ya kumbukumbu za Heshima alizoziacha.

"Jeshi ni mfano na linaongoza katika kuhamasisha Michezo yote nchini na halijawahi kushindwa hivyo ni mwendelezo huo ni mzuri. alisema Jenerali Mstaafu Waitara.

Aliongeza kuwa Ujenzi wake sio mgumu na kinachotakiwa kufanyika ni kuchukua kilichofanyika klabu ya golf ya Lugalo kuhamishia Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alipongeza Wanachama wanaojitoa kutatua changamoto za Uwanja.

Aidha alitoa Wito kwa Wachezaji wengine wwnye nia njema kujitokeza kusaidiana kutatua Changamoto mbalimbali zinazojitokeza Uwanjani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu ya Majenerali na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dk Edmund Mndolwa amewaomba viongozi wa Selikali kucheza Mchezo huo.

Alisema Golf ndio Mchezo Pekee unaoweza kucheza kwa Muda Mrefu bila kujali Umri na idadi.

Ujenzi wa Kidaraja umefanikishwa kwa hisani ya proffesa Wineaster .......na Kibanda cha Pumzikia ni Mike Laizer.

AIRTEL MONEY YAZINDUA “AIRTEL MONEY TUNAKUUNGANISHA NA DUNIA” KUPANUA SEKTA YA HUDUMA ZA KIFEDHA NCHINI

$
0
0

 Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money leo imezindua kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money.

Akizungumza jijiji Dar es Salaam leo wakati wa kuitangaza kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema “huduma ya kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya 200 itajulikana kama Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia” hakuna mipaka wala changamoto ya kupokea fedha kutoka nje ya nchi ukiwa na Airtel Money sasa”

“Huduma hii ni inadhihirisha dhamira yetu ya kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta suluhisho la huduma za kifedha hapa nchini ili kuwafikia Watanzania wengi ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki. Tunaelewa ya kwamba tunao ndugu, jamaa na marafiki walio nje ya nchi ambao wangependa kutuma fedha kwa ndugu zao watanzania lakini wanakumbana na vikwazo kutokana na hatua nyingi zinazotakiwa wakati wa kutuma fedha nje ya nchi. Airtel Money imekuja na suluhisho, mteja wa Airtel Money anatakiwa kuw na laini ya simu ya Airtel ambayo imesajiliwa tu”. Nchunda alisema.

Nchunda aliongeza kuwa Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia itaboresha uchumi shirikishi kati ya familia na marafiki waliopo nje ya nchi kwa kuwa itaongeza uhuru wa kuchangua njia rahisi na ya haraka pale inapohitaji kupokea fedha au kwa wanaotaka kutuma fedha hapa nchini kwa haraka, huku sisi Airtel tukiwa tumejipanga kikamilifu kuendelea kutoa huduma nafuu, salama, haraka bila mipaka.

Nchunda alizitaja baadhi ya nchi ambazo mteja wa Airtel Money ataweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Airtel Money ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Uswizi, Swedeni, Uholanzi, Italia, Norway pamoja na nchi zote za Afrika Mashariki.

“Mnamo mwishoni mwa mwaka jana, Airtel kwa kushirikiana na WorldRemit, ambayo ni kampuni ya kimataifa ya malipo walizindua mfumo huu wa malipo kwa kuwawezesha wateja wa Airtel Money kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money kwa nchi Zaidi ya 50. Huu ni muendelezo wa kuhakikisha wateja wetu wanaishi kwenye dunia ya kisasa pamoja na kwenda na mabadiliko ya teknolojia kwenye upande wa kutuma na kupokea fedha kimtandao’, alisema.

“Lengo letu kama kampuni siku zote imekuwa ni kutoa huduma na bidhaa ambazo ni za kipekee na ambazo zinapatikana kwa unafuu ili kuendana na maisha ya kila siku ya wateja wetu. Kwa kuzindua pokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200, tunaileta pamoja jamii kwa kuondoa mipaka kwani wote wataweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money kutoka mataifa mbalimbali’, Nchunda aliongeza.

Airtel Money ni moja ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi ambayo inakuwa kwa kasi huku ikiwa hapa nchini ikiwa imeunganisha na makampuni ya malipo ya huduma mbalimbali zaidi ya 1000, pamoja na kuunganisha na taasisi za fedha zaidi ya 40. Vile vile, Airtel Tanzania inazidi kupanua wigo kupitia Airtel Money Branch karibu yako ambapo kwa sasa ina maduka ya Airtel Money Branch zaidi ya 1200 ambayo yanatoa huduma na bidhaa zote za Airtel nchni.

Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando kulia akiwa na  Mkurugenzi wa Airtel Money Isack pamoja na Mkuu wa Chapa wa Airtel Money bi Gilian Rugumamu wakizindua rasmi kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money.

 Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo  wakati kuzindua kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money. Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money.

NMB yaendesha semina ya walimu kuwapa elimu ya fedha

$
0
0

  Walimu wametakiwa kujiendeleza kwa kukopa mikopo nafuu, yenye tija na kuwawezesha kutatua  changamoto zinazowakabili ili kuweza kunufaika na kufurahia kazi wanayoifanya.

 

Akizungumza wakati wa mafunzo ya walimu wa mkoani Arusha yaliyoandaliwa na Benki ya NMB, Afisa elimu sekondari wa mkoa huo, Khalifani Omary alisema mafunzo hayo yatawajenga walimu katika kujiwekea kipato na kufahamu fursa mbalimbali zilizoko benki ili kuweza kujiendeleza kimaisha.

 

"Mafunzo haya yatawasaidia katika kuwaongezea ufahamu namna wanavyoweza kunufaika na benki ya NMB ikiwa jitihada hizi zitaleta matokeo chanya nakuleta faraja kwa jamii,"alisema Omary.

 

Afisa elimu alisema jitihada hizo ni nzuri na  zinaunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha watanzania walio wengi wanajumuhishwa katika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua  vipato vyao hivyo ametoa rai kwa taasisi nyingine za kifedha nchini kufanya jitihada hizo kama NMB.

 

Alisema anashukuru huduma za kibenki zimeboreshwa na kusogezwa karibu na wateja wake kwani hapo awali walimu walipata taabu kutembea umbali mrefu hivyo benki ya NMB imekuwa chachu ya maendeleo katika jamii kwa kuwanufaisha wateja wake.

 

Kwa upande wake Mkuu wa biashara ya Kadi wa benki ya NMB, Philbert Casmir  alisema  wameandaa mafunzo yanayoitwa siku ya walimu ambapo wameanza mkoani Arusha kwa kutambua mchango wa mwalimu katika jamii na kutoa suluhisho ya changamoto zao katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mikopo nafuu na bima mbalimbali.

 

"Tunatambua mwalimu ni mwezeshaji katika jamii hivyo NMB tumekuja na suluhisho mahususi kwa walimu ikiwemo mikopo nafuu ya kujenga au kununua nyumba,"alisema Mkuu huyo.

 

Casmir alisema pia kuna bima za walimu na watanzania kwa ujumla zinazoweza kuwasaidia kupata nafuu wakati wa majanga mbali mbali.

 

Baadhi ya walimu hao walisema wanashukuru benki ya NMB kwa kuwapa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuwekeza fedha nakutumia katika matumizi sahihi ya kujiendeleza kiuchumi na kuwaletea maendeleo.

 

Mwalimu  mkuu wa shule ya msingi Daraja mbili, Zukra Kalunde alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kufahamu umuhimu wa kadi pamoja na kujifunza namna ya kupata mikopo nafuu ya benki hiyo itakayowasadia kujiendeleza kiuchumi kama ujenzi wa nyumba zao za kuishi na biashara.


Mkuu wa kitengo cha biashara ya kadi Benki ya NMB, Bw. Philbert Casmir akihutubia katika shughuli hiyo.


 

Meneja wa  wateja binafsi Benki ya NMB, Bi.Nyamisinda Manyonyi akitoa elimu ya Mikopo kwa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Arusha. 


Washiriki wa Semina ya walimu wakuu wa Shule za msingi na wakuu wa Shule za Sekondari zilizopo Mkoa wa Arusha, wakisikiliza hotuba ya mgeni rasimi kwenye uzinduzi wa semina ya  mafunzo ya bidhaa za NMB. Semina hiyo yenye lengo la kutoa elimu ya fedha na bidhaa mbalimbali za NMB ilifanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na walimu zaidi ya 300.

 

Viewing all 48915 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>