Mashindano ya mchezo wa gofu maarufu kama TM Cross Country Golf Challenge jana yalimalizika katika viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es Salaam kwa hafla ya washindi kukabidhiwa zawadi za vikombe.
Mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mwaka wa nne, yamefadhiliwa na kinywaji cha Johnnie Walker kinachosambazwa na kampuni ya bia ya Serengeti na yaliweza kuwaleta pamoja wachezaji wa gofu wa madaraja mbali mbali.
Jumla ya washindi kumi na tatu wa madaraja tofauti tofauti walifakiwa kujiondokea na vikombe baada ya kuibuka vinara.
Akizungumzia kuhusu mashindano hayo ambayo huusisha kucheza kwenye viwanja mashimo tisa badala ya 18, mwazilishe wake Terence Mwakaliku alisema mashindano hayo hutoa fursa kwa wachezaji wa gofu kucheza mchezo huo kwa namna ya tofauti na walivyozoea.
“Badala ya kucheza kiwanja kimoja baada ya kingine, mashindano haya yanahusisha kuchanganya viwanja na mashimo pia na hivyo kumfanya mchezaji kupata uzoefu wa tofauti,” alisema Mwakaliku
Mwakaliku aliishukuru Johnnie Walker kwa kufadhli masindano hayo na kuongeza kuwa udhamini umesaidia kuboresha mashindano na pia umesaidia kuwavutia wachezaji wengi zaidi kushiriki.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndiyo walikuwa wadhamini wakuu wa kupitia Johnnie Walker alisema kinywaji hicho kinajivunia kuwa sehemu ya mashindano hayo ya aina yake.
“Katika mashindano haya kinachofanyika ni kubadilisha uwanja wa kuchezea gofu ili tuweze kucheza kwa namna tofauti na tulivyozoea na hivyo kufurahia kucheza kwa namna tofauti kabisa. Kinywaji chetu cha Johnnie Walker ni kinywa ambacho kinatoa ladha Pamoja na uzoefu tofauti kwa watumiaji na tuna furahi kudhamini mashindano haya,” alisema.
Johnnie Walker ni moja kati pombe kali zenye ubora wa hali ya juu na hadhi ya kimataifa. Kinywaji hiki kina jumla ya aina tano ambazo zimeshinda tuzo za ubora wa kimataifa. Aina hizo ni pamoja na JW Red Label, JW Black Label, JW Green Label, JW Gold Label, na JW Blue Label kila moja ikiwa na historia yake ya kipekee.
Mkurugenzi Mtedaji wa kampuni ya bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akimkabidhi kikombe mshindi wa Daraja C katika mashindano ya Johnnie Walker TM Cross County Challenge 2021 Danstan Kolimba. Wa pili kushoto ni mwanzilishi wa mashindano hayo Terence Mwakaliku na kulia ni James Mwambona kutoa Simba Courier ambao ni mdhamini mwenza wa masindano.

Baadhi ya washindi wa mashindano ya Johnnie Walker TM Cross County Challenge 2021 wakifurahia ushindi wao mara baada ya kukabidhiwa vikombe katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtedaji wa kampuni ya bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akicheza wakati wa mashindano ya Johnnie Walker TM Cross County Challenge 2021 yaliyofanyika katika viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es Salaam. Kulia ni mchezaji ambaye pia ni mwanzilishi wa mashindano hayp, Terence Mwakaliku.