STAMICO yachangia matibabu ya watoto wenye vibiongo
TPA YAZINDUA KITUO MAALUM KWA AJILI YA KUHUDUMIA WATEJA KWA NJIA YA SIMU
Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
MAMLAKA ya Bandari Tanzania(TPA) imeamua kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi ambao sasa imezindua rasmi kituo maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja kwa njia ya simu ya mkononi ambapo kituo hicho kitatoa huduma kwa saa 24.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho cha TPA Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho amesema hatua hiyo ni ishara ya kuendeleza kazi katika Serikali ya Awamu ya Sita chini ya kiongozi mahiri Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kuwahudumia wananchi.
Amesema ili wananchi wanaohitaji kupata huduma za TPA watatakiwa kupiga namba ya simu 0800110032 muda wowote na kisha watahudumiwa na kwamba hakuna gharama yoyote kwa watakaokuwa wakiitumia , kwani lengo ni kusogeza huduma iwe ndani au nje ya nchi.
Aidha Mhandisi Chamuriho amewapongeza TPA kwa hatua hiyo ya kujali wateja wa ndani na nje kwa kuhakikisha wanapata huduma stahiki kupitia Mamlaka hiyo."Hatua hii ya TPA ni ya kupongeza kwani tumeelezwa hapa huduma zitatolewa saa 24, mtu anapopata tatizo lolote na wakati wowote anayo nafasi ya kuwasiliana na TPA moja kwa moja."
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi ameahidi kutoa huduma kwa saa 24 kupitia Kituo hicho huku akieleza kwamba kituo hicho kinakuja kondoa changamoto ya wale ambao waliihitaji kupata huduma za TPA lakini hakuwa na njia ya haraka ya kuwasiliana nao, hivyo sasa kwa kutumia namba hiyo ya simu itakuwa rahisi kwa yoyote kuwasiliana nao.
"Namba ambayo itatumika kwa kwenye kituo hiki ni 0800110032, haina gharama kwani gharama zote zimeshalipiwa na TPA, hivyo huduma hii ni bure na tunaamini inakwenda kutatua changamoto papo kwa hapo kwa wale ambao watakuwa na changamoto yoyote na inahitaji ufumbuzi wetu,"amesema Hamissi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka(kushoto) wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa kituo maalum cha TPA kwa ajili ya huduma kwa wateja.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho(katikati aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kwa mmoja ya watoa huduma kwa wateja katika kituo hicho maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja baada ya kukizindua rasmi leo Juni 25,2021.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka.Waliokaa ni watoa huduma kwa wateja wa kituo hicho.
Mmoja ya watoa huduma kwa wateja katika kituo hicho maalum ya TPA akitoa maelezo ya jinsi wanavyoweza kupokea simu za wateja na kuwahudumia kwa Waziri Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho(katikati).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Eric Hamissi(wa kwanza kushoto)Waziri Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho(katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka(kulia) wakishangilia baada ya kuzinduliwa kwa kituo maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wa TPA kwa njia ya simu.
Waziri Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho akizungumza wakati akizindua kituo maalum kwa ajili ya huduma kwa wateja wa TPA ambao watahudumia kwa njia ya simu kokote waliko kwa kupiga namba ya simu ambayo haina gharama yoyote lengo ikiwa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Watoa huduma kwa wateja katika kituo hicho maalum wakiendelea na utoaji huduma kwa njia ya mawasiliano ya simu baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eric Hamissi akifafanua kuhusu kituo hicho maalumu cha kuhudumia wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi(kushoto) wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Sehemu ya wakuu wa idara mbalimbali za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusu kituo hicho ambavyo kitakuwa kikitoa huduma kwa wateja wakati kikizinduliwa rasmi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) kwa ajili ya kuzindua kituo maalum cha kuhudumia wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu.(PICHA NA SAID MWISHEHE)
Yara Tanzania kushirikiana na serikali kuhamasisha matumizi bora ya mbolea na ukulima wa kisasa.
KAMPUNI ya mbolea ya Yara Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa mkulima wa zao la pamba anaongeza uzalishaji na tija ili kuinua kipato chake na pia kuongeza malighafi ya pamba itakayotumika katika viwanda vya hapa nchini.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana, Meneja Biashara wa Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile alisema mafanikio hayo yataweza kupatikana endapo wakulima wa zao hilo watatumia kwa ukamilifu matumizi ya mbolea na kufuata kanuzi zote za ukulima wa kisasa.
Alisema Yara kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba Tanzania waliweka mashamba darasa 124 katika mikoa minne ya Simiyu, Mwanza, Tabora na Geita na wilaya zake 12 kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/21 ili wakulima wa zao la pamba waweze kujifunza kwa vitendo namna bora ya matumizi ya mbolea ya Yara huku kampuni hiyo ikitoa mifuko 31 ya mbolea ya kupandia na mifuko 31 ya mbolea ya kukuzia kwa mashamba darasa yote.
“Kampuni ya Yara ina furaha kubwa kuona kile ilichofanya kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba kimekamilika na ni matumaini yetu wakulima wamejifunza umuhimu wa kutumia mbolea ili kuupa mmea lishe linganifu hivyo kuongeza uzalishaji wa pamba kwa eneo.
“Hapa Miguwa tuliweka shamba darasa ekari moja lililotumia mbolea ya kupandia ya YaraMila Otesha (NPK 13:24:12) mfuko 1(50kg) na ya kukuzia kwa mbolea ya YaraBela Sulfan (CAN 24%N+6%S) mfuko 1(50kg) na ekari nyingine haikuwekwa mbolea kama kilimo cha wakulima wengi wa pamba wafanyavyo, ni matumaini yetu matokeo yake kama inavyooneka hapa yataleta hamasa kubwa kwa wakulima kutumia mbolea”, alisema.
Akizungumza mahali hapo, Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Bodi ya Pamba, Jones Bwahama alisema bodi hiyo imepanga kuhamsisha ulimaji wa zao hilo la pamba kwa kutoa elimu ya wakulima juu ya kuzingatia kanuni bora za kilimo kwa kutumia mbolea na madawa vizuri na kupanda kwa nafasi zinazostahili ambapo itawawezesha wakulima kuvuna zaidi ya kilo 1000 kwa ekari moja.
Naye Ofisa kutoka katika Ofisi ya Kilimo Mkoa wa Tabora, Modest Kaijage alisema matumizi ya mbolea ni muhimu sana kwa mafanikio ya wakulima wa mkoa huo kwani utaleta tija kwa wakulima na kwa Taifa.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Miguwa, Anjelina Nyanda alisema mashamba darasa yaliyowekwa na Yara kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika kata hiyo yamewanufaisha wakulima wa kata hiyo kuacha kilimo cha mazoea na sasa kufanya kilimo chanye tija.
Mmoja wa wakulima wa Kata ya Miguwa, Mariam Mashala alisema amefurahishwa na matumizi ya mbolea ya Yara ya kupandia na kukuzia mahindi kwa kupata mavuno mengi kuliko awali hivyo anaomba mbolea hiyo iongezwe katika msimu ujao wa kilimo.

Viongozi kutoka Kampuni ya Mbolea ya Yara na Bodi ya Pamba, viongozi wa kiserikali, wakuliwa na waalikwa wengine wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba katika Kata ya Miguwa, Nzega, Tabora jana.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile (katikati, aliyevaa kofia), wakulima wa pamba na waalikwa wengine wakiangalia zao la pamba katika moja ya mashamba darasa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba kwenye eneo lililowekwa mashamba darasa hayo kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora jana.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile (katikati) akizungumza na baadhi ya wakulima wa pamba pamoja na waalikwa wengine wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba kuhusu faida ya mbolea ya kupanda na kukuzia ya Yara katika eneo walilowekamashamba darasa kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora jana. Wa tatu kushoto ni Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Bodi ya Pamba Tanzania, Jones Bwahama.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba kuhusu faida ya mbolea ya kupanda na kukuzia ya Yara katika eneo lililowekwa mashamba darasa kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora jana.
NMB Yazidi Kuwa Karibu na Wateja Wao: Dodoma, Singida na Manyara
Benki ya NMB imeendelea kuwa karibu na wateja wake zaidi ya 700 wa mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara kupitia jukwaa la ‘NMB Business Club na ‘NMB Executive network’ kwa nyakati tofauti.
NMB imetumia majukwaa hayo kuwakutanisha wateja wao wadogo na wakubwa ili kuwapa elimu ya kuwa wabunifu katika shughuli zao za kujiongezea kipato ili kukuza biashara zao, lakini pia, wametumia fursa hiyo kuweza kupata maoni kutoka kwa wateja wao kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo ikiwa ni moja wapo ya njia ya kuwahusisha wateja wao kuwa sehemu ya ubunifu wa bidhaa zao.
Akizungumza katika NMB Business Club mkoani Singida, Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi aliwahakikishia wafabiashara hao kuwa wapo sehemu salama, kwani NMB iko tayari kukuwa nao katika kila hatua ya shughuli zao. Lakini sio hivyo tu, alibainisha kuwa NMB imeendelea kuwa kinara wa ubunifu wa huduma na bidhaa ili kukidhi matakwa ya wateja wao.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB – Alex Mgeni alisema kuwa, kutokana na kukuwa kwa mtaji, NMB imeendelea kuwa benki inayoongoza kwa faida kwa kupata TZS bilioni 206 baada ya kodi ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 45 (YoY), mwaka 2020. Lakini pia wameruhusiwa na TIRA pamoja na BoT kufanya shughuli za Bima ‘bancassurance’ kwa kushirikiana na makampuni 10 ya bima ambapo huduma inapatikana kupitia matawi yote ya NMB nchi nzima.
Siyo hivyo tu, Alex alibainisha kuwa, NMB imerahisisha ulipaji na ununuaji kupitia matumizi ya mfumo wa malipo kupitia QR code pamoja na huduma za kibenki kupitia mtandao (Internet banking) na wameingia mkataba na makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Madini (NHIF) kuleta bidhaa ya Dunduliza lengo likiwa kuwawezesha watanzania wote hasa wa vipato vya chini kama wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wajasiriamali kuwa na bima kadiri ya uwezo wao.
Kwa niaba ya wateja, mfanyabishara Neema Mandala aliishukuru NMB kwa kuendelea kuwapa kupaumbele wateja, kwani kupitia majukwaa hayo yameongeza ukaribu wao na benki yao pendwa, lakini pia imekuwa kama njia ya kuwakutanisha wateja na wenzao ili kuendelea kufahamiana zaidi, kitu ambacho kimerahisisha wao kusapotiana kibiashara.
Meneja wa NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi akizungumza na wafanyabiashara kutoka Singida, Itigi, Ikungi na Manyoni katika mkutano NMB Business Club uliofanyika Mkoani Singida.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB - Alex Mgeni akizungumza na wafanyabiashara wakubwa wa Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) waliohudhuria jukwaa la NMB Business Executive Network katika hafla iliofanyika katika hoteli ya Morena - Jijini Dodoma.
Sehemu ya wafanyabiashara walio hudhuria mkutano wa NMB Business Club uliofanyika Mkoani Singida.
BODI YA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMA PORI (TAWA) YATEMBELEA BUSTANI YA WANYAMA PORI RUHILA, SONGEA
RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI
TAASISI YA WAJIBU YAZINDUA RIPOTI ZA UWAJIBIKAJI MWAKA 2019/2020, WADAU WAPONGEZA
WADAU mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, viongozi, wabunge ,Asasi za Kiraia na wanafunzi vyuo vikuu wameshuhudia uzinduzi wa Ripoti tano za Uwajibikaji ambazo zimetokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali( CAG).
Ripoti hizo zimeandaliwa na Taasisi ya WAJIBU ambayo imeziandaa ripoti hizo za uwajibikaji baada ya kuichambua kwa kina ripoti ya CAG ambayo iliwasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan Machi 28 mwaka huu na baadae ripoti hiyo ya CAG ikakabidhiwa kwa Bunge Aprili 4 mwaka huu.
Akizungumza jana Juni 28,2021 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya WAJIBU,Bwa. Ludovic Utouh ambaye amewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), amesema ripoti hizo ni za tano tangu waanze kuandaa na kuzitayarisha kutokana na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
"Kama tunavyojua ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambazo zimewasilishwa kwa Rais Machi 28 na kuwasilishwa bungeni Aprili 4, ni ripoti zinazotayarishwa kitaalamu, ni ripoti kubwa na ripoti ambazo kusema kweli kwa Watanzania wangi huwa hawana shauku ya kuisoma kwa sababu ya ukubwa wake.
"Sasa sisi WAJIBU tunachukua ripoti zile na kuchambua kwa undani na tunachukua yale tunayoamini yanauzito na umuhimu mkubwa kwa watanzania, kwa hiyo utakuta ripoti ya WAJIBU iliyozinduliwa leo ya Serikali kuu na mashirika ya umma inatokana na ripoti mbili kubwa za CAG za Serikali Kuu na mashirika ya umma na tumeweza kuja na kitabu cha kurasa 31.
"Na utakuta katika ripoti ile kubwa tumechambua mambo 10 ambayo tumeona yana umuhimu zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu na ukienda kwenye ripoti ya serikali ya mtaa na miradi ya maendeleo ambayo nayo imetokana na ripoti mbili za CAG ambayo ina mambo 21 ina mambo nane ambayo tumeona yana umuhimu wa umma.
"Ukija kwenye ripoti ya tatu ambayo ni ripoti ya Ufanisi ile kwa kuwa imetokana na ripoti ya CAG mwaka jana aliwasilisha bungeni ripoti 15 za ufanisi, sisi katika kupitia ripoti zile tumeona zina mambo muhimu zaidi kwa maendeleo ya nchi na tumeweza kuja na ripoti yenye page 31 ambayo inajikita kwenye maeneo hayo, "amesema Utouh.
Amesema ombi lake baada ya kuzinduliwa kwa ripoti hizo za uwajibikaji, ni vema wananchi wakazisoma kwani watazisambaza katika maeneo mbalimbali na zitakuwepo kwenye Website ya WAJIBU ,pia zitapatikana kwenye taasisi.
"Tutazigawa kupitia taasisi mbalimbali ili watanzania wapate ripoti hizi na wazisome, wakati tunasherehekea siku 100 za uongozi wa Rais Samia kweli sisi kama wananchi wa Tanzania tuwe na ari ya kuungana naye na kumsaidia kwa nia yake njema aliyonayo ya kuleta maendeleo ya nchi katika kudai uwajibikaji pale.
"Ambapo tunaona taasisi ya serikali au chombo cha Serikali hakitimiza wajibu wake , ndio lengo la WAJIBU tunasema kwamba rasimali za Serikali za taifa zikisimamiwa vizuri zinakuwa za kila Mtanzania.
Kwa upande wake Mwakilishi Ofisi ya Msajili wa NGO's Charles Mpaka amewapongeza WAJIBU kwa kuja na ubunifu waliokuja nao wa kupitia ripoti ya CAG na kuziandikia taarifa fupi ."Tumeona ripoti ya CAG ni kubwa na WAJIBU wameona umuhimu wa kuichambua na kuja na taarifa fupi.Ripoti ya CAG ilikuwa na zaidi ya kurasa 250 lakini wao wamekuja na taarifa yenye 21 mpaka 31.
"Maana yake tunaongea asilimia nane mpaka 11 wamekwenda kuipunguza, hivyo itakwenda kusaidia wananchi kupata tafsiri ya haraka na uelewa mwepesi wa ripoti ya CAG,"amesema
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Naghenjwa Kaboyoka amesema wamekuwa wakifanya kazi na WAJIBU kwa karibu sana na kwamba WAJIBU wamekuwa kama Bunge nje ya Bunge, wamekuwa wakiwakilisha wananchi , maana hizo ripoti zao wanazichambua kiasi kwamba wananchi wanaweza kuzisoma na kuzielewa.
"Kwa hiyo imekuwa mkono wetu wa kulia wa kusaidia kamati zetu mbili za PAC na LAAC , unakuta wenzetu wanakwenda mbali zaidi kueleza yale ambayo hatupati muda wa kuyazungumzia bungeni lakini wenzetu WAJIBU wanayachambua na kuyaeleza kwa wadau, na hivyo wadau wanapata nafasi ya kujua kilichopo.
"Kwa mfano tukiangalia bajeti ya mwaka huu siku zote tunasema kilimo ndio uti wa mgongo lakini akangalia bajeti iliyopita nafikiri ilitolewa tu asilimia mbili na hii ndio sekta ya uzalishaji, sasa kama sekta ya uzalishaji hazitatengewa hela nyingi zikazalisha tunategemea maendeleo gani, yatakuwa maendeleo ya vitu sio watu.
"Serikali za mitaa tuna tatizo moja, tatizo linawezekana hawa wanzetu tangu wamemaliza shule hajawahi kupelekwa kozi , hajui tena taratibu za kimataifa za kutoa ripoti zimekuaje , matokeo yake inawezekana kweli hajaiba lakini akawa hajui jinsi ya kuandaa ripoti, kwa hiyo anapata ripoti chafu.
"Lakini kusema kweli ni vizuri hawa wenzetu ambao wapo katika taaluma ya kusimamia masuala ya fedha mara kwa mara wapelekwe kwenye kozi, mara kwa mara waelezwe taratibu mpya na kufundishwa ,maana unakuta wanasema hawa wamezoea kuandika vocha tu,"amesema.
Ameongeza inawekana ni wasomi wazuri lakini viwango vya kimataifa vya kuandaa ripoti ambavyo vimewekwa havijui , hivyo halmashauri inapata hati chafu, mwingine anapata hati safi na anayepata hati safi haina maana mambo yao ni mazuri kuliko aliyepata hati chafu."Lakini ina maana gani , hesabu zao hawajazifunga kwa utaratibu unaokubalika kimataifa".
Aidha amesema anashukuru kusikia kuna halmashauri ambazo zimeanza kuchukua hatua za kuwapeleka watu wao wa kuandaa ripoti kupata kozi za kuwaongezea ujuzi huku akieleza CAG anaweza kusaidia hao watu wakaelekezwa namna ya kufunga hesabu.
WADAU mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, Wabunge ,Asasi za Kiraia na wanafunzi vyuo vikuu ambao wameshuhudia uzinduzi wa Ripoti hizo,wakipitia kwamakini Ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dodoma.
WAZIRI BITEKO AZINDUA RASMI NMB MINING CLUB JIJINI DODOMA



************************************
Aipongeza Benki ya NMB kwa ubunifu wa kutafuta wateja kwenye Sekta ya Madini
Asisitiza ushirikiano kwa mabenki kwa msaada wa kitaalamu
Na. Steven Nyamiti, Dodoma
Waziri wa Madini Doto Biteko amezindua rasmi Jukwaa la Wadau wa Madini kupitia Benki ya NMB lenye lengo la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara, wachimbaji na wadau wa madini ili kuwa na sauti moja katika kujadili changamoto wanazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja.
Hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa hilo unaokwenda kwa jina la NMB MINING CLUB umezinduliwa tarehe 28 Juni, 2021 katika Hotel ya Morena Jijini Dodoma na kuhuhudhriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Biteko amesema kuwa, ili kuwarahisishia wachimbaji kupata mikopo kwa urahisi katika mabenki ikiwemo vifaa vya uchimbaji, Wataalam wa Wizara ya Madini hawanabudi kutoa ushirikiano kwa mabenki pindi yanapohitaji msaada wa kitaalamu ili yaweze kutoa mkopo kwa wateja wao kwani baadhi ya mabenki yameshindwa kutoa mkopo kwa wachimbaji kutokana na kukosa elimu ya kutosha kuhusu sekta ya madini.
” Ninatoa rai kwa mabenki nchini kuungana kwa pamoja na kutoa mikopo mikubwa kwa wawekezaji wakubwa wa madini wanaotaka kuwekeza nchini ili faida inayotokana na mikopo hiyo ibaki nchini,” amesema Waziri Biteko.
Akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watoa mada, Waziri Biteko amesema Wizara ya Madini inapokea mapendekezo yatakayowasilishwa katika kuangalia njia sahihi ya wachimbaji wa madini kukopesheka kupitia jukwaa hilo na kusisitiza njia rahisi ni kupitia vyama vyao vya uchimbaji pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambalo pia linafanya kazi ya kuwalea wachimbaji wadogo.
” Kwa kupitia STAMICO tumeanzisha mchakato wa kuangalia dhamana kwa wale wote wanaokwenda kukopa kwenye mabenki ili kujiridhisha na utaratibu huo utakamilika hivi karibuni,” amesisitiza Biteko.
Aidha, Waziri Biteko ametoa wito kwa jukwaa hilo kuendelea kutoa elimu kwa wadau wa Sekta ya Madini kuhusu umuhimu wa kupendana na kuthaminiana kwani bila upendo Sekta ya Madini haiwezi kufika popote.
Waziri Biteko ameipongeza Benki ya NMB kwa ubunifu huo kwenye Sekta ya Madini na kueleza kuwa kupitia klabu hiyo iliyoanzishwa na benki ya NMB itapata fursa ya kupata wateja wengi waliopo kwenye Sekta ya Madini.
Naye, Afisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB Daniel Mboto amesema lengo la kuandaa jukwaa hilo ni kutoa nafasi ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya wadau na benki ya NMB na kuongeza kwamba, uzinduzi huo mkoani Dodoma ni mwanzo wa kuzungumza na wadau wa Sekta ya Madini katika kutoa huduma mbalimbali ili kuwapa uelewa zaidi wa huduma za NMB.
Jukwaa hilo la NMB Mining Club lililozinduliwa leo na Waziri Biteko mkoani Dodoma, linatarajia kufanyika katika mikoa mingine saba hapa nchini .
Wengine waliohudhuria Uzinduzi huo ni pamoja na Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) John Bina, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Dodoma Chagwa Marwa, wataalam kutoka Wizara na Tume ya Madini, wafanyakazi wa Benki ya NMB na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini.
Biteko Azindua ‘NMB Mining Club’
Benki ya NMB imeendelea kuweka historia nyingine tena kwa kuzindua jukwaa la kwanza nchini mahsusi la kuwahudumia wadau wa Sekta ya Madini liitwalo ‘NMB Mining Club’.
Klabu hiyo mpya imejumuisha zaidi ya wadau wa madini 200 wa Kanda ya Kati na imelenga kutoa mafunzo kuhusu maarifa ya biashara (elimu juu ya mipangilio ya biashara na elimu ya mwendelezo wa kitaalamu wa madini) na fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.
Wadau hao ni pamoja na wamiliki wa migodi, maduka makubwa ya vifaa vya uchimbaji, viongozi kutoka kampuni za madini, Kampuni ya Taifa ya Madini (Stamico), vyama vya wachimbaji wa kada zote na madalali.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jukwaa hilo uliofanyikakatika hoteli ya Morena- Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko aliwapongeza NMB kwa ubunifu huo wa kuwafikia na kuwaunganisha wadau wa Sekta hiyo huku wakiwapa fursa ya mafunzo ya biashara na kubadilishana mawazo kwa ajili ya ufanisi wao binafsi na kisekta kwa ujumla.
Mhe.Biteko, amewahakikishia wawekezaji na wadau wengine wa sekta ya madini mazingira bora ya uwekezaji na kufanya biashara akisema hicho ni kitu muhimu kwa ustawi wa sekta hiyo na maendelo ya taifa kwa ujumla.
Awali, Afisa Mkuu wa Mikopo wa NMB, Bw. Daniel Mbotto, alisema mafunzo hayo yamekuja wakati biashara nyingi zikipata changamoto akitolea mfano wa kushuka kwa thamani ya bei ya Tanzanite kwenye soko la dunia.
Kuhusu “NMB Mining Club”, Bw. Mbotto alisema ni mpango unaolenga kufikia miji sita nchini yaani Mwanza, Chunya, Morogoro na Arusha, ukianzia Dodoma na Kahama na maeneo ya karibu kwa lengo la uwezeshaji na kutoa mafunzo ya biashara. Ubunifu huu ndio unaoifanya NMB kuendelea kuwa kinara wa huduma na bidhaa katika sekta ya kibenki. Waziri wa Madini - Dotto Biteko (kushoto) na Afisa Mkuu wa Mikopo Benki ya NMB – Daniel Mbotto wakizindua rasmi jukwaa la ‘NMB Mining Club’ katika hafla ya uzinduzi iliofanyika katika hoteli ya Morena - Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya Madini kutoka Kanda ya Kati katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa NMB Mining Club uliofanyika Jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB – Alex Mgeni akiwaelimisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini Kanda ya Kati waliohudhuria uzinduzi wa NMB Mining Club kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki ya NMB.
EURO 2020 HAINA MWENYEWE, MAMBO MAZITO!
*Meridianbet Tunakuhakikishia Faida Kwa Kila Dau
HATUA ya 16 bora kunako muendelezo wa Euro 2020, imetoa matokeo ya kusisimua na kushangaza kwa baadhi ya timu. Meridianbet, kila dau unaloweka linaweza kukupa faida kubwa! Tembelea duka lolote la Meridianbet lililokaribu nawe, kutandaza mkeka wako wiki hii. Mchongo upo hivi;
Uingereza kuwaalika Ujerumani katika dimba la Wembley Jumanne usiku. Uingereza anaingia kwenye mchezo akitoka kuwa kinara wa kundi D huku Ujerumani akijitutumua na kumaliza kwenye nafasi ya 2 kwenye kundi F nyuma ya Ufaransa na mbele ya Ureno na Hungary.
Mchezo wa Uingereza vs Ujerumani, ni miongoni mwa michezo yenye upinzani na historia nyingi. Uingereza atakumbuka machungu ya kupoteza mchezo kwa matuta wakati huo kocha wa sasa, Gareth Southgate alikuwa anaitumikia timu hiyo. Yote 9, 10 ni kwamba – Meridianbet tumekuwekea Odds ya 2.70 kwa Uingereza kwenye mchezo huu.
Kule Norway mambo yamepamba moto. Rosenborg kuvaana na Haugesund katika muendelezo wa ligi soka nchini humo. Unaweza kuifata Odds ya 1.70 kwa Rosenborg kwenye mchezo huu ukiwa na Meridianbet.
Valerenga uso kwa uso dhidi ya Sarpsborg 08. Mambo ni moto kwenye Ligi Kuu ya Norway. Meridianbet hatukuachi nyuma, tumekuwekea Odds ya 1.60 kwa Valerenga kwenye mchezo huu.
Meridianbet, Nyumba yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!
Moto wateketeza bweni shule ye sekondari Ikuwo wilayani Makete
CCM:Kama kiongozi hujafanya chochote isahau nafasi yako mwakani
Na Amiri Kilagalila,Njombe
SONGWE KUONGEZA UKAGUZI WA DAWA NA VIFAA TIBA
Mkoa wa Songwe umeweka msisitizo katika Ukaguzi wa Madawa na vifaa tiba ili kudhibiti dawa na vifaa tiba ambavyo havipo sokoni au havija sajiliwa kuwafikia watumiaji.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Hamad Nyembea ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa dawa na vifaa tiba wa halmashauri zote za Mkoa wa Songwe ambapo mafunzo hayo yameendeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Dkt Nyembea amesema Mkoa wa Songwe unapakana na Nchi mbalimbali na hivyo kuwa na njia ambazo si rasmi zinazotumiwa na wahalifu kuingiza nchini Dawa na Vifaa tiba ambavyo havijasajiliwa au havipo.
“Mafunzo haya yatasaidia kuimarisha ukaguzi wa dawa na vifaa visivyofaa visizagae sokoni na hivyo kuleta madhara kwa watumiaji”., Dkt Nyembea.
Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Anitha Mshigati amesema katika mafunzo hayo wakaguzi watakumbushwa maadili ya Ukaguzi ili waweze kuboresha kazi hiyo kwa kufuata taratibu na sharia na matarajio ni kuwa baada ya mafunzo kazi hiyo itafanyika na kuleta tija zaidi.
Naye Mtaalamu wa Maabara wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Ashura Mwinyimkuu amesema changamoto wanazo kutana nazo ni jamii kutokuwa na elimu kuhusu ukaguzi hivyo kushindwa kutoa ushirikiano na mafunzo waliyopata yamewaongezea ujuzi wa namna ya kukabiliana na hilo.
Kwau upande wake Mfamasia wa Songwe Medard Mwazembe amesema changamoto ya wakaguzi ni ukubwa wa maeneo ya kufanya ukaguzi huku wakiwa hawana vifaa vya usafiri hivyo wanaomba TMDA kwa kushirikiana na Mkoa kutoa elimu kwa viongozi wa Kijiji na Kata ili viongozi hao waweze kusaidia kutoa elimu katika maeneo yao.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Hamad Nyembea akizungumza na wakaguzi wa dawa na vifaa tiba wa halmashauri zote za Mkoa wa Songwe wakati wakipewa mafunzo yaliyo endeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Anitha Mshigati akizungumza na wakaguzi wa dawa na vifaa tiba wa halmashauri zote za Mkoa wa Songwe wakati wakipewa mafunzo yaliyo endeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Wakaguzi wa dawa na vifaa tiba wa halmashauri zote za Mkoa wa Songwe wakipewa mafunzo yaliyo endeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
BANCABC YASHIRIKI KONGAMANO LA KUCHOCHEA UCHUMI TEGEMEZI KWA WATU WENYE ULEMAVU JIJINI DODOMA




BoT IKO TAYARI KUWAHUDUMIA WANANCHI WATAKAOTEMBELEA MAONESHO YA SABASABA BARABARA YA KILWA,DAR ES SALAAM.
Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania BoT, Vicky Msina akizungumza na baadhi ya maofisa wa benki kuu katika banda lao leo kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.
Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania BoT waliotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.
Mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la Benki Kuu ya Tanzania BoT akiuliza swali kwa maofisa wa benki hiyo kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.
Baadhi ya Maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania BoT wakiwa tayari kabisa kuwahudumia wananchi watakaotembelea katika banda hilo katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.
Mbio za Rock City Marathon 2021 Zazinduliwa Rasmi jijini Mwanza
Msimu wa 12 wa mbio za Rock City Marathon zinazofanyika kila mwaka jijini Mwanza umezinduliwa rasmi hii leo jijini humo huku serikali ikiahidi kuendelea kutumia mbio hizo kuibua vipaji vya mchezo wa riadha sambamba na kutangaza utalii wa ndani.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bw Hassan Elias Masala aliekuwa akimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel alisema ni nia ya serikali kuona mashindano hayo yanakuwa chachu ya kuwezesha kupatikana wanamichezo watakaoweza kushiriki katika Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa.
“Ili agenda kuu ya kutangaza utalii wetu iweze kufanikiwa ni wazi kwamba lazima tuwe na matukio yanaweza kuwashawishi wenzetu kutoka nje waje kututembelea. Uwepo wa mashindano makubwa kama haya ndio utatuwezesha kufanikisha hili, hivyo nawasihi wadau wote tujitokeze kuunga mkono mbio hizi,’’ alisema Bw Masala ambae pia aliahidi kushiriki mbio hizo.
Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 24 kwenye viunga vya jengo la biashara la Rock City Mall, jijini humo tayari zimefanikiwa kuvutia wadhamini na wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni ya TIPER, Serengeti Breweries, Benki ya KCB, Kampuni ya Uhandisi ya Magare, Pepsi,Maji ya Uhai, Rock City Mall, Kampuni ya Ulinzi ya GardaWorld, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Azam tv na CF Hospital.
Zaidi alitoa wito kwa wadau na wakazi kutoka ndani na nje ya jiji hilo kuhakikisha wanashiriki katika matukio mbalimbali yatakayo ambatana na mbio hizo ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo kanda ya Ziwa, kushiriki mbio zenyewe pamoja na kuwa sehemu ya wadhamini wa mbio hizo.
Kwa upande wake Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw Kasara Naftal alisema maandalizi yanaendelea vizuri huku akibainisha kuwa lengo haswa ni kukimbiza washiriki zaidi ya elfu tano.
“Tunajitahidi kufanya maandalizi ya kutosha na yenye kufuata viwango vya kimataifa ili kuwawezesha washiriki wa mbio hizi wakiwemo wale wa kimataifa wapate wasaaa wa kushiriki kikamilifu bila vikwazo vya aina yoyote.’’
“Hili pia huwa tunalifanya makusudi ili washiriki hawa wakawe mabalozi wazuri wa mbio hizi pamoja na malengo ya kuanzishwa kwake kwa maana ya kutangaza utalii pindi wanaporudi katika mikoa na mataifa yao hasa kwa wale wanaotoka nje ya nchi.’’ Alisema.
Mbali na mbio za km 21, mbio za Rock City Marathon pia zinatarajiwa kuhusisha makundi mengine ya mbio ambayo ni pamoja na mbio za kilomita 10 kwa wanaume na wanawake, kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’ na watu wenye ualibino pamoja na watoto wenye umri kuanzia miaka 7.
Kuhushu usajili wa mbio hizo Bw. Naftal alisema unatarajiwa kuanza rasmi Julai mosi mwaka huu kwa njia ya mtandao.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bw Hassan Elias Masala (alieshika mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa msimu wa 12 wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Octoba 24 mwaka huu kwenye viunga vya jengo la biashara la Rock City Mall, jijini Mwanza wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika jijini humo leo. Wanaoshuhudia ni wadau mbalimbali wa mbio hizo wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa mchezo wa huo, wadhamini na waandaaji wa mbio hizo.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bw Hassan Elias Masala akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw Kasara Naftal akizungumza kwenye hafla hiyo.
Rock City Marathon mbio za makundi yote! Wadau wa Rock City Marathon.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bw Hassan Elias Masala (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mbio za Rock City Marathon wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa mchezo wa huo, wadhamini na waandaaji wa mbio hizo.
Baadhi ya wadau wa mchezo wa Riadha jijini Mwanza wakiwa kwenye uzinduzi wa mbio za Rock City Marathon msimu wa 12.
Davis & Shirtliff Tanzania yapata cheti cha Ubora cha ISO
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Davis & Shirtliff Tanzania, Benjamin Munyao (Kushoto) akipokea cheti cha Ubora kutoka Shirika la Kimataifa la ISO kutoka kwa Ofisa wa kampuni yaBureau Veritas, Charles Vunugulu (kulia) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo,jana jijini Dar es Salaam.Katikati ni wasimamizi na wakaguzi, Fausta Kusibago na Lizy Washuka. Cheti cha ISO ni uthibitisho kuwa kampuni imekidhi viwango vya ubora vya kimataifa

Kampuni ya Davis & Shirtliff Tanzania, imekabidhiwa cheti cha ISO kutoka Shirika la Kimataifa la Usimamizi wa Viwango (ISO), hatua ambayo ni kubwa kwa kampuni ya kitanzania ambayo imekuwa mstari wa mbele kuboresha maisha ya watu kupitia huduma za maji.
Cheti cha ISO 9001 ni uthibitisho kwamba kampuni imekidhi vigezo vya usimamizi wa ubora kwa mujibu wa mfumo wa usimamizi unaokubalika kimataifa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Davis & Shirtliff Tanzania, Benjamin Munyao alisema “Katika moja ya misingi yetu ‘Core Values’ ni ubora, kwahiyo cheti hiki ni msisitizo wa ubora wa wafanyakazi wetu, vifaa vyetu na utendaji kazi kwamba upo katika viwango vya juu sana.”
Alisema kupitia hatua hiyo, kampuni inaweza kufanya kazi kitaifa na kimataifa kwakuwa mashirika mengi yanahitaji kufanya kazi na kampuni ambazo zimethibitishwa na ISO.
“Kwa zaidi ya miaka 20 tumekuwa tukiendesha biashara hapa Tanzania kwa kuhakikisha tunatumia rasilimali watu, teknolojia na rasilimali mbalimbali kuboresha maisha ya watu kupitia kutoa suluhisho mbalimbali za kudumu kwenye sekta ya maji,” alisema.
Aliongeza kuwa lengo la muda mrefu ni kuhakikisha wanaleta matokeo chanya kwa jamii ili kuhakikisha rasilimali maji inatumika kwa ufanisi ili kudumu kwa vizazi vijavyo.
Davis and Shirtliff ni kampuni inayoaminika katika utengenezaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za maji nchini Tanzania na Serikali ikiwa mmoja wa wateja wake wakubwa.
Ni dhahiri kuwa, uwepo wa wazalishaji wa bidhaa ndani ya nchi ambao wanatambulika kimataifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwasababu inaokoa mud ana kupunguza gharama za kuagiza bidhaa nje ya nchi zinazohitajika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Akikabidhi cheti hicho, Ofisa wa kampuni ya Bureau Veritas, Charles Vunugulu alisema kampuni hiyo imetimiza vigezo vyote ikiwamo kupitia mafunzo mbalimbali ya namna bora ya uendeshaji wa kampuni.
“Tutakachokifanya ni kuhakikisha kila baada ya mwaka tunafanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa kampuni inaendelea kuwa bora kila mwaka,” alisema.
Kampuni ya Davis & Shirtliff inazalisha na kusambaza bidhaa mbalimbali ikiwamo pampu za maji, majenereta, mabwawa ya kuogelea, mashine za kutibu maji pamoja na mashine za umwagiliaji kwneye kilimo.
SBL yamwaga sh. Bilioni 2 kwa mabaa kupambana na Corona
Gf TRUCKS YAWATAKA WAKANDARASI KUCHANGAMKIA OFFA YA SABASABA
Akizungumza na wandishi wa habari waliotembelea waliotembelea Banda lao ndani ya viwanja vya Maonyesho ya 45 ya Biashara ya kimataifa Afisa masoko Mwandamizi wa kampuni ya GF, Lukolo Jumaa alisema kampunin ya GF imeamua kutoa punguzo maa lumu kwa wateja wetu ambao watatembelea banda letu lililopo katika maonyesho ya sabasaba
Akifafanua zaidi punguzo hilo la bei (sabasaba special) limelenga zaidi katika mitambo inayotumika kwa shunguli za ujenzi (XCMG Motor grade) ambapo wakandarasi wazalendo wenye miradi ya ujenzi hii ndio fursa yao kwani mwaka mpya wa seriklali ndio huu na wakandarasi wazalendo nio kipamumbele katika hili
Pia wanunuzi na wadau wakubwa wa mitambo hii ni Makampuni ya Ujenzi,Makandarasi pamoja na wamiliki wa migodini,Pia tuna magari makubwa ya mizigo FAW,HONG YANG (trucks) pamoja na tipper zinazotumika katika shunghuli mbalimbali zikiwepo machimbo ya mchanga na katika baadhi ya halmashauri zimekuwa zikitumiwa kwa kukusanyia takata na shughuli nyingine.
Akienda mbali zaidi Lukolo alitanabaisha magari hayo ya FAW na HONG YANG Kwa sasa yaliotengenezwa na kiwanda cha GFA kinachomilikiwa na watanzania kilichopo Kibaha mkoani Pwani hivyo katika maonyesho ya mwaka huu tunajivunia kuonyesha magari yaliotengenezwa na wataalamu wetu wakishitikiana na wataalamu kutoka nje
DKT. MWIGULU ATETA NA CHAMA CHA WATOA HUDUMA WA SIMU TANZANIA
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA), na kuwafafanulia kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayumo pichani) na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA), walipofika wizarani hapo kwa, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC Bw. Hisham Hendi, wakati wa mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMOA), jijini Dodoma.
Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc Bi. Hilder Bujiku akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayumo pichani) na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (hayumo pichani), akizungumza wakati walipofika wizarani hapo kwa mazungumzo kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (hayumo pichani), akizungumza wakati walipofika wizarani hapo kwa mazungumzo kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC Bi. Rosalynn Mworia, akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayumo pichani) na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc Bi. Hilder Bujiku.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC Bi. Rosalynn Mworia, baada ya mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA), na kuwaeleza kuwa kodi ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa na mitandao ya simu ni ya kizalendo inayolenga kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imepanga kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ya wananchi na inayohitaji fedha nyingi na kwamba jukumu la kukamilisha miradi hiyo ni la Watanzania wote wenye uchungu wa maendeleo.
“Fedha zitakazo patikana kwenye tozo hizo hazitatumika kulipa mishahara wala kugharamia matumizi mengine yoyote ya Serikali bali zitapelekwa moja kwa moja kutatua changamoto za afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara, elimu na mingine mingi ikiwemo miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli ya kisasa na Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere” alisema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba Watanzania wengi wameunga mkono kutozwa kodi hiyo kwa kutambua umuhimu wa maendeleo yao ambayo kukamilika kwake kunahitaji mchango wao mkubwa.
“Kampuni za simu msichukulie makato haya kama kodi nyingine mnazowatoza wateja wenu bali Serikali iliamua kuweka makato haya kwenye miamala ya kuweka muda wa maongezi na kufanya miamala kwa njia ya simu ili kuwafanya Watanzania na watumiaji wengine wa simu kuchangia maendeleo ya nchi”alisisitiza Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba alitoa muda wa siku 14 kuanzia tarehe 1 hadi 15 Julai, 2021, kwa watoa huduma wote wa Mitandao ya Simu kurekebisha mifumo yao na kuanza kutoza rasmi makato hayo ili Serikali ianze kukusanya fedha hizo ambazo amesema zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuwakwamua wananchi kutoka katika adha mbalimbali.
Kwa upande wao Chama cha Watoa huduma za mitandao ya simu, waliiomba Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iwape muda wa kurekebisha mifumo yao itakayotumika kukusanya tozo hizo kwa kuwa zoezi hilo linahitaji muda wa kiufundi.
Akizungumza kwa niaba ya Chama hicho, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Bi. Roselynn Mworia, alisema kuwa chama chao kimeupokea mpango huo kwa mikono miwili na kuwataka wateja wao kuiunga mkono Serikali kwa kuendelea kutumia huduma za kupiga simu na kufanya miamala ya simu.
“Lengo la Serikali la kuamua kukusanya fedha za maendeleo kwa njia hiyo ni zuri kwani litaharakisha utekelezaji wa miradi ya huduma za kijamii, kwa kweli ni kodi ya kizalendo” alisema Bi. Mworia.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi karibuni, lilipitisha tozo ya kuanzia shilingi 10 hadi shilingi 10,000 kutozwa katika kila muamala wa kutuma au kupokea pesa na kiwango cha shilingi 10 hadi 200 kwa siku kila mteja anapoongeza salio la muda wa maongezi kwenye simu ambapo kwa pamoja, Serikali inatarajia kukusanya wastani wa shilingi trilioni1.7 kwa mwaka.