Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Jumla ya Tsh 187 Million zapatikana mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba leo uwanja wa Taifa jijini Dar

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kukabidhi kikombe kwa washindi katika mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba ambapo Yanga wameifunga simba 5- 2 

Katika mchezo huo Jumla ya Tsh 187 Million zimepatikana ambazo zitakabidhiwa rasmi kwa waziri mkuu ili kuwasilishwa kwa waathiriwa na tetemeko la Ardhi lililotokea mjini Bukoba mkoani Kagera, na kupelekea kupoteza maisha ya wananchi 17 na kujeruhi wengine wengi na kuharibu nyumba na miundo mbinu mbalimbali.
way2
Mwenyekiti wa timu ya wabunge Mh. William Ngeleja akizungumza jambo mara baada ya mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.Katika mchezo huo wa kirafiki Wabunge washabiki wa Yanga waliibuka washindi kwa kuwafunga mashabiki wa simba goli 5-2
way3
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi kikombe kwa wabunge mashabiki wa timu ya Yanga kwenye uwanja wa taifa leo.
way4
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavundewakati akiwapongeza wabunge mashabiki wa Yanga kwa ushindi mnono wa magoli 5-2  dhidi ya Wabunge mashabiki wa Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
way5
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na MWIGULU Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani,wakati akiwapongeza wabunge mashabiki wa Yanga kwa ushindi mnono wa magoli 5-2  dhidi ya Wabunge mashabiki wa Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
way6
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi kombe kwa wabunge mashabiki wa timu ya Yanga mara baada ya ushindi wao dhidi ya wabunge mashabiki wa timu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
way7
Wabunge Mashabiki wa Yanga wakishangili na kombe lao mara baada ya kuibuka washindi wa mchezo huo leo kwenye uwanja wa Taifa.
way8
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni ya leo.
way11
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akiwavisha nishani wabunge mashabiki wa Simba mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

TRA YA WAHAMASISHA WAUMINI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA KUJENGA UTAMADUNI WA KULIPA KODI NA KUDAI RISITI.

$
0
0



Afisa Mwandamizi Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi.Rose Mahendeka akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti wakati wa manunuzi ili kodi hii isaidie kuendesha shughuli za serikali katika kutoa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na afya,elimu,maji,miundombinu,ulinzi na usalama.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akisoma jarida lenye maelezo na taarifa za ulipaji wa kodi lilitolewa na mamlaka ya mapato Tanzania wakati wa semina iliyokuwa ikitolewa na maofisa wa mamlaka ya mapato Tanzania kwa waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Ndugu Amon Mpanju na kushoto kwake ni mkewe Grace Gwajima.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwasisitiza wauminiwake kulipa kodi ili kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (mstari wa mbele) wakiwa tayari kutoa mada ya uhamasishaji wa ulipaji kodi na umuhimu wa kudai risiti kwa waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima.
Naibu Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Ndugu Amon Mpanju akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na umuhimu wa waumini hao kujua wajibu wao kwenye kulipa kodi.


Na Frank Shija ,MAELEZO

WATANZANIA wameaswa kujenga utamaduni wa kulipa kodi na kudai risiti pindi wanapofanya biasha au kununua bidhaa ili kuisaidia Serikali kukusanya mapato kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za kijamii.

Wito huo umetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bibi. Rose Mahendeka alipokuwa akitoa elimu kwa waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.

Rose alisema kuwa shughuli za Serikali katika nchi yeyote duniani, ikiwemo Tanzania zinagharamiwa na fedha zinazotokana na kodi pamoja na tozo mbalimbali.

“Katika maandiko matakatifu imeandikwa; Ya Kaisari mpeni Kaisari, vya Mungu mpeni Mungu, hivyo ni vyema tukajenga utamaduni wa kulipa kodi na kudai risiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu”. Alisema Rose.

Alisema umuhimu wa kudai risiti kuwa ni pamoja mwananchi kutambua kiasi cha kodi anayochangia Serikali yake, kutambua kodi halisi inayotakiwa kulipwa na ushahidi wa ununuzi wa bidhaa na uhalali wa umiliki wake.

Aliongeza kuwa kutodai risiti ni kwenda kinyume na matakwa ya sheria ya mlipa kodi ambapo adhabu yake ni faini ya pointi za fedha 2 hadi 100 ambazo ni sawa na shilingi 30,000 mpaka 1,500,000/=.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju aliupongeza uongozi wa Kanisa hilo kwa kuona haja ya waumini wake kupatiwa elimu ya mlipa kodi. Aidha aliwaka waumini wa kanisa hilo kulipa kodi na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania mpya kama ambavyo baba wa Kanisa hilo Askofu Josephat Gwajima amekuwa akisisitiza.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima amewahimiza waumini wake kuishika na kuitumia elimu waliyopata kutoka kwa mwakilishi wa TRA ambapo aliwataka waumini hao kujenga utamaduni wa kudai risiti kila anapofanya malipo ili kusaidia ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Watanzania wang’ara Rock City Marathon 2016,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza awa kivutio, akimbia km 5

$
0
0
Chacha Masinde kutoka mkoani Mara akimaliza Rock City Marathon na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mbio hizo zilizofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana . Chacha alitumia muda wa saa 01:03:00 kumaliza mbio hizo akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia muda wa saa 01:04:40.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella sambamba na maofisa kutoka benki ya NMB wakishiriki mbio  za za km 5.
Washiriki wa mbio za km 21 wakiondoka Uwanja wa CCM Kirumba kuanza safari ndefu.
Ushindani ulikuwa ni mkubwa!
Washiriki kutoka pande tofauti za Dunia washiriki.
Ilikuwa ni furaha tupu kwa washiriki
Watoto nao hawakuwa nyuma…mbio zilihusisha watu kutoka rika zote kwa kuzingatia vigezo na mashariti.
Suala la usalama kwa washiriki ilikuwa miongoni mwa agenda za msingi kwenye mbio hizo.
Watu wenye ulemavu wa ngozi walishiriki mbio za km 5.


Mwandishi wetu, Mwanza



Chacha Masinde kutoka mkoani Mara ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jana jijini Mwanza baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:03:00, akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia muda wa saa 01:04:40



Mbio hizo za kilomita 21 zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba kupitia Barabara ya ikulu ndogo hadi mzunguko wa samaki na kuelekea Buzuruga kisha kutokea barabara ya pasiansi na kumalizikia uwanjani Kirumba huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella akishiriki kukimbia mbio za km 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.



Nafasi ya tatu upande wa wanaume ilichukuliwa na Mkenya Moris Mosima aliyetumia muda wa saa 01:04:57, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.



Akizungumzia siri ya ushindi wake, Chacha siri ya mafanikio hayo ni kujituma kwake zaidi katika kufanya mazoezi maalum kwa ajili ya mashindano hayo ili kuhakikisha kwamba mwaka huu mshindi wa kwanza katika mbio hizo anatoka nchini Tanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo washindi walikuwa wakitoka nchini Kenya.



 “Niliweka nadhiri nikasema mwaka huu lazima mshindi atoke Tanzania zaidi niwe mimi na ninashukuru nimetimiza adhama yangu. Pamoja na hilo maandalizi ya mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi mahitaji yote muhimu yakiwemo maji tukiwa njiani yamesaidia mafanakinio hayo licha ya washiriki kuwa zaidi mwaka huu hatua ambayo iliongeza changamoto kwetu zaidi,’’ alisema.



Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mtanzania pia Faimina Abdi kutoka mkoani Arusha aliyetumia muda wa saa 01:13:12 akifuatiwa na mwenzake  kutoka mkoani Arusha Angelina Daniel aliyetumia saa 01:14:38 huku Mkenya Dorifine Omary akishika nafasi ya tatu akitumia saa 01:16:54



Washindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya nane jijini Mwanza  waliibuka na kitita cha Sh1.5 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh900,000 na washindi watatu Sh700,000.



Mashindano hayo ya kila mwaka yaliyokatika kalenda ya RT yaliandaliwa na Kampuni ya Capital Plus kwa udhamini kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB,  New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door.



Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi kwa washindi na washiriki wa wa mbio hizo Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella ambae pia alishiriki mbio hizo kwa kukimbia mbio za km 5 alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi heshima yake katika mchezo huo.



“Ndio maana tumekuwa tukisisitiza wadhamini waendelee kujitokeza kusaidia mbio hizi ili ziendelee kuwa bora zaidi,’’ aliongeza.



Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwa niaba ya Katibu tawala jana, Afisa michezo mkoa waMwanza James William alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha wetu nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi yetu heshima ya kipekee katika mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.



Alisema: “Tanzania inaweza kurejea katika ramani ya dunia kwenye michezo kama tukijikita katika maandalizi mazuri ya kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi.”



Naye Mbunge wa jimbo la Ilemema ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Ntumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula alipongeza waandaaji wambio hizo na kutoa wito kwa washiriki walioshindwa kufanya vizuri kwenye mbio hizo kutokata tama bali wajiandae na mashindano yajayo ili waweze kufanya vizuri.


Naye Makamu Mwenyekiti wa mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema mbio hizo zimeweza kufanyika kwa mafaniko makubwa na ushirikiano walioupata kutoka uongozi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani huku pongezi pia zikielekezwa  kwa jeshi la polisi kwa kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama

Bodaboda Mirerani watakiwa kujipanga kulipia leseni ya usafirishaji

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mhandisi Zephania Chaula amewataka wamiliki na madereva wa pikipiki za kubebea abiria (bodaboda) kujiandaa kulipia mapato kupitia leseni ya usafirishaji wa abiria.

Mhandisi Chaula aliyasema hayo mji mdogo wa Mirerani, akizungumza na wamiliki na madereva wa pikipiki za kubebea abiria (bodaboda) kwenye semina iliyoandaliwa na mamlaka ya udhibiti usafirishaji wa nchi kavu na majini (Sumatra).

Alisema wanapaswa kujiandaa na ulipaji wa leseni ya usafirishaji itakayoanza kutozwa hivi karibuni kwani haikwepeki, hivyo wajipange kwa ajili hiyo ili wachangie mapato ya nchi, ambayo inalenga kujitegemea.

“Hivi karibuni tutawapa taarifa ya kuanza kwa zoezi hilo ila sasa subirini kidogo kwani hii ni serikali ya awamu ya tano inayotaka kujitegemea kupitia mapato ya wananchi na siyo kuomba misaada nje ya nchi,” alisema Mhandisi Chaula.

Afisa mfawidhi wa Sumatra mkoani Manyara, Nelson Mmari alisema lengo la kukutana na bodaboda hao ni kuhakikisha kila mmiliki anakuwa na leseni ya usafirishaji inayotolewa kupitia halmashauri ya wilaya husika.

Mmari alisema Machi 2009, Bunge lilipitisha sheria ya kuruhusu pikipiki za magurudumu mawili au mitatu kubeba abiria kwa malipo au kukodisha na iliyoanza kutumika mwaka 2010 hivyo leseni ya usafirishaji inapaswa kulipiwa.

Alisema kila mtu anapaswa awe na leseni ya usafirishaji wa biashara ya kubeba abiria wa pikipiki ya magurudumu mawili au matatu na  atakayekiuka atatozwa faini ya kati ya sh50,000 au sh100,000 au kufungwa jela miezi sita au mwaka.

Alisema mkuu wa wilaya ya Simanjiro aliwaelewesha vizuri wamiliki na madereva wa bodaboda kuwa wajiandae na zoezi la ulipaji wa leseni ya usafirishaji kwani zoezi hilo linatarajia kuanza hivi karibuni kwenye eneo hilo.

Kwa upande wake, mkuu wa askari polisi wa usalama barabarani wa mkoa wa Manyara, Mary Kipesha, alisema wanasubiri taarifa ya mkuu wa wilaya hiyo ili waanze zoezi la ufuatiliaji ulipaji wa leseni ya usafirishaji kwa bodaboda.

“Tunasubiri mazungumzo hayo ila mjiandae na ninyi kwani baada ya hapo ndipo tutaanza ukamataji kwa wale ambao watakuwa hawajalipa leseni ya biashara ya kubeba abiria kwa wenye bodaboda hapa Mirerani,” alisema Kipesha.
Mkuu wa Kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ASP Evarest Makala akizungumza juzi na wamiliki na madereva wa pikipiki katika warsha iliyoandaliwa na mamlaka ya udhibiti usafirishaji wa nchi kavu na majini (Sumatra).
Wamiliki na madereva wa pikipiki za kubeba abiria (bodaboda) wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani manyara, wakiwa katika warsha iliyoandaliwa juzi na mamlaka ya udhibiti usafirishaji wa nchi kavu na majini (Sumatra).
Mmoja wa wamiliki wa pikipiki Abubakary Sadiq akizungumza juzi mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Mnayara kwenye warsha iliyoandaliwa na mamlaka ya udhibiti usafirishaji wa nchi kavu na majini (Sumatra).

TANZANIA NOMINATED FOR THE 23RD ANNUAL WORLD TRAVEL AWARDS

$
0
0


 

Tanzania has registered ten (10) entries under nine (9) categories in the World nominations 2016 for the World Travel Awards organized by the World Travel Awards that will take place on 2nd December 2016 at the Olhuveli Beach & Spa Resort in the Republic of Maldives. Under the  Africa nominations 2016, thirty two (32) entries for Tanzania have been recorded under 17 categories. 

The winner of this competition will be decided by votes. Voting for the World and Travel Technology nominations opens online on Friday, 23rd September 2016 and will end on Monday, 24th October 2016. The voters will be travel professionals and consumers with a vote cast by qualifying travel professionals carrying a weighting of two votes.
“We are delighted to inform you of your nomination in the 23rd annual World Travel Awards and I congratulate your achievement” says Graham Cooke, the President of World Travel Awards.

Tanzania’s ten entries with their categories in brackets are:  Tanzania (World’s Leading Safari Destination 2016); Zanzibar-Tanzania (World’s Leading Dive Destination 2016); Zanzibar - Tanzania (World Leading Island Destination); and Mt. Kilimanjaro-Tanzania(World’s Leading tourist attraction).

Others are: Diamond La Gemma dell’Est Zanzibar -Tanzania (World’s Leading Beach resorts 2016); Essque Zalu Zanzibar - Tanzania (World’s Honeymoon Resort 2016); &Beyond Mnemba Island Lodge-Tanzania and Singita Sasakwa Lodge – Tanzania (World’s Leading Luxury Lodge 2016); &Beyond Mnembo Island Lodge Zanzibar – Tanzania(World’s Leading Private Island Resort 2016) and Chumbe Island Coral Park – Tanzania (World’s Leading Conservation Company).

This comes five months after Mount Kilimanjaro which is the highest mountain in Africa, and the highest free-standing mountain in the world, being declared Africa’s leading tourist attraction in 2016 during the World Travel Awards Africa and Indian Ocean Gala Ceremony held in Zanziba Tanzania on 9th April 2016. 

The World Travel Awards was founded in 1993 to recognize, acknowledge and reward excellence in the travel, tourism and hospitality industry worldwide. This year’s World Travel Awards is celebrating its 23rd anniversary. Its brand is now recognized globally as the hallmark of quality, with winners setting the benchmark to which all others aspire.

Issued by:

PUBLIC RELATIONS OFFICE
TANZANIA TOURIST BOARD
Sept 26, 2016.

UTT AMIS YATOA ELIMU YA JUU YA UWEKEZAJI KWA WANACHAMA WA NAMAINGO BUSINESS AGENCY

$
0
0
Ofisa Mafunzo Kitengo cha Masoko kutoka Kampuni ya Uwekezaji UTT AMIS, Waziri Ramadhani akitoa elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wanachama wa Namaingo Business Agency kwenye uzinduzi wa Shamba la Ufugaji Sungura Majohe jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mafunzo kutoka Idara ya Uendeshaji UTT AMIS, Abbas Kandila (kulia), akiwaeleleza jinsi ya kujaza fomu za kujiunga Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja baadhi ya wanachama wa Kampuni ya Ushauri  Kibiashara ya Namaingo Business Agency wakijaza fomu kujiunga na Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja.
Ofisa Mafunzo kutoka Idara ya Uendeshaji UTT AMIS, Abbas Kandila akipitia fomu za  wanachama wa Kampuni ya Ushauri  wa Kibiashara ya Namaingo Business Agency baada ya kujiunga na Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Kampuni ya Ushauri  Kibiashara ya Namaingo Business Agency wakimsikiliza Ofisa Mafunzo wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Waziri Ramadhani (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Shamba la Ufugaji Sungura Majohe jijini Dar es Salaam..

WATANZANIA 10 KWENDA KUFANYA KAZI STARTIMES NCHINI CHINA

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (kushoto) akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa mashindano ya sauti, Hilda Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 40 kutoka kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 Mmojawapo wa washindi wa sindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akikumbatiana na majaji baada ya shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio hilo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao na kulia ni majaji na washindi wengine. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.

 Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
  Mmoja wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akionyesha uwezo wake wa kuigiza sauti mbele ya majaji jukwaani. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Rukia Hamdani akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mshiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Coletha Raymond akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika shindano.


Na Dotto Mwaibale

Hatimaye shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa watanzania 10 kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing.

Akizungumza baada ya shindano hilo Dar es Salaam juzi , Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam ambaye ndiye aliyeongoza kwa kupata alama nyingi kutoka kwa majaji alisema kuwa anashukuru sana kupata fursa hiyo ya kuonyesha kila kipaji alichonacho kwani haikuwa kazi rahisi.

‘’Kwanza kabisa nashukuru kwa ushindi huu, haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa ukizingatia washiriki walioingia hatua ya fainali wote walikuwa wana uwezo mkubwa sana. Nawashukuru majaji kwa kunipa moyo tangu awali na hatimaye kuniamini kwamba nina kitu ambacho ninaweza kukitoa kwa watanzania kupitia kipaji change cha sauti. Fursa niliyoipata mimi pamoja na washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia na kuitumia ipasavyo.’’ alisema . Malecela

‘’Napenda kuwaahidi watanzania kuwa nitaitumia nafasi hii vema kuhakikisha nafanya kazi nzuri ili wao waendelea kuburudika na kujifunza zaidi kupitia filamu na tamthiliya. Nawapongeza pia StarTimes kwa kutambua umuhimu wa Kiswahili na kuja ubunifu huu ambao haujawahi kutokea nchini. Mara nyingi tumekuwa tukiona mashindano ya kuimba, kuigiza na kucheza lakini si kwa upande wa sauti. Wamepiga hatua kubwa sana kwa kweli ambayo inastahili kuigwa na makampuni mengine.’’ alimalizia mshindi huyo aliyeongoza kwa kuwa na alama nyingi zaidi kutoka kwa majaji

Naye kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania,  Lanfang Liao amebainisha kuwa amefurahi kuona shindano la kusaka vipaji vya sauti limepokewa kwa muitikio mkubwa na watanzania sehemu mbalimbali za nchi.

‘’Hatukutegemea kama watanzania wengi wangevutiwa na shindano hili lakini imekuwa ni kinyume chake kwani imedhihirika kuwa wapo wasanii wengi sana wenye vipaji vya sauti. Sanaa ina uwanja mpana sana ni namna tu msanii mwenyewe anavyoamua anakitumia vipi kipaji alichonacho. StarTimes tumebaini kutoka kwa wateja wetu kuwa filamu na tamthiliya zilizotafsiriwa na kuingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili zinapendwa sana. Hivyo tukaona ni vema kuviibua vipaji ili tufanye nao kazi hiyo kwa manufaa ya watanzania.’’ alisema  Liao

‘’Tunaamini kupitia shindano hili tumeweza kutoa ajira kwa watanzania 10 watakaokwenda kujumuika na wenzetu waliopo makao makuu jijini Beijing, China katika kuzalisha kazi zilizo bora kabisa. Nawasihi washindi waliopata fursa hii kuitumia vema kwa kufanya kazi kwa bidii kwani ninaamini wanastahili mpaka kuchaguliwa na majaji kuwa vinara dhidi ya wenzao 18 waliofikia hatua ya fainali. StarTimes tunaahidi kuendelea na zoezi hili wakati ujao kwani bado uhitaji ni mkubwa na sisi siku zote tupo kwa ajili ya kuwapatia kile wateja wetu wanachokitaka.’’ alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTime nchini

Katika fainali hizo washindi wa kwanza, pili na watatu; Hilda Malecela - kutoka DSM,  Safiya Ahmed kutoka Zanzibar na Sadiq Kututwa - kutoka Zanzibar) walizadiwa runinga za kisasa zenye ukubwa wa inchi 40, 32 na 24 kila mmoja na StarTimes kutokana na kuongoza kwa alama nyingi katika fainali hizo huku washindi saba wakipatiwa simu za mkononi za kisasa kutoka StarTimes.

Kwa ujumla washindi kumi waliopatikana ni;  Hilda Malecela(DSM),  Safiya Ahmed(ZNZ),  Sadiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa(DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao(DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard(DSM). Na wote watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja. 

Katika mashindano hayo takribani washiriki zaidi ya 547 walijitokeza katika usaili uliofanyika katika mikoa ya Arusha (Agosti 27), Zanzibar (Septemba 3) na Dar es Salaam (Septemba 10) na hatimaye washiriki 18 tu wakabakia na kutinga hatua ya fainali.

Washiriki 18 waliotinga hatua ya fainali ni kama ifuatavyo: kwa mkoa wa Arusha ni Mathew Philip Mgeni, Dorcas Francis, Halima Hussein, Janeth N Molely na Hilda Kinabo; Zanzibar ni Safiya Ahmed Said, Sadiq Kututwa Abdalahh, Rukia Hamdan, Imatu Obeid Fabian na Mohamed Said Mohamed; na Dar es Salaam ni Hilda Malecela, Abraham Richard, Happiness Stanslaus ‘Nyamayao’, Richard Rusasa, Emanuel Landey, Coletha Raymond, Jamila Hassan na Maisala Abdul.

The city will be host to the largest religious congregation in over three decades

$
0
0
 
  Ashara Mubaraka are the first 10 days of Moharram, that mark the martyrdom of Imam HusainAS, grandson of Prophet MohammedSAW, that took place fourteen centuries ago. This is a very important religious and spiritual event in the Dawoodi Bohra Calendar.  Each year, Dawoodi Bohras across the world observe Ashara Mubaraka by attending religious sermons, mourning the tragedy of Karbala and remembering the supreme sacrifice of Imam HusainAS.   

Imam HusainASrefused to pledge allegiance to Yazeed, a tyrannical ruler who had transgressed all that Islam stood for and had established a reign of oppression after coming to power. In the battle of Karbala, Imam HusainAS along with seventy two of his followers including his family fought bravely on the scorching sands of Karbala and acquired martyrdom. 
  The oppressors had totally denied them food and water for 3 consecutive days and even Imam HusainAS’s six month old son was martyred in the battlefield of Karbala.  Imam HusainASmade this supreme sacrifice so that truth may prevail, tyranny be exterminated and the cherished human values of righteousness, piety and virtue may ever remain supreme and uncompromised.

Following the footsteps of his predecessors, each year, 53rd al-Dai al-Mutlaq, His Holiness Dr. Syedna Mufaddal SaifuddinTUS,on receiving requests and invitations from his followers from different towns and cities, chooses a venue for delivering sermons during Ashara Mubaraka.  In this Islamic year, 1438 H, the city of Dar es Salaam is blessed to have been chosen as the venue for Ashara Mubaraka, which will be from the 2nd to the 11thof October, 2016.  

With the encouragement and blessings of His Holiness’ predecessors, a few Dawoodi Bohras made their homes in Tanzania more than two centuries ago. They came here principally to carry on business and trade. Finding the country a land of opportunities and experiencing the welcoming nature of the Tanzanians, they subsequently settled and made their homes in Tanzania.  The Dawoodi Bohras of Tanzania and those of Dar es Salaam, in particular feel extremely privileged to host this event and expect to host about 30,000 guests from all over the world including East Africa.

During Ashara Mubaraka sermons, His Holiness Dr. Syedna Mufaddal SaifuddinTUS will narrate the tragic events of Karbala and shower pearls of wisdom upon his followers, mentoring them on the noble teachings of Islam and the principles of humanity that Imam HusainAS sacrificed his life for.  During these auspicious days, His Holiness will pray for the victims of the earthquake in Kagera region. 

His Holiness and his followers, the Dawoodi Bohra community, offer support and help to the efforts of the Government of Tanzania in rebuilding and providing relief to the victims of the earthquake in Kagera region.  It is also the intention and desire of Anjuman-e-Saifee (Dar es Salaam) to launch a scheme for the support of those affected by the calamity.

Wherever he travels, His Holiness reminds his loyal followers of the noble teachings of Islam that “love for the land of abode is an essential part of the faith” and that “religion is not just prayer and fast but also to strive for betterment in this world and hereafter”.  

He guides them to strive for the betterment of their neighbours and for the common good of all the people of their country.  His Holiness guides and directs his followers to invest in trade and industry in Tanzania and has dedicated resources to assist them to work hand in hand with other members of the society and for the country at large.  Following the guidance and directions of His Holiness, the Dawoodi Bohras residing in Tanzania continue to contribute to the growth and development of their country.  

The anticipated arrival of His Holiness to Dar es Salaam is on Tuesday, 27th September at 1300 Hrs.


PRESS STATEMENT RELEASED BY:
Zainuddin T. Adamjee
Vice Chairman
Anjuman-e-Saifee

MWENYEKITI PAMOJA NA MAKAMO MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR WAZUNGUMZA NA WAANDISHI.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheri kushoto akiwa pamoja na Makamo Mwenyekiti Maryam Ishau Abdalla wakionesha vyeti vyao walivyopatiwa baada ya kuchaguliwa na kuzungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
kil1
Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Maryam Ishau akisisitiza jambo alipozungumza na Waandishi wa Habari kuelezea mikakati walioiweka baada ya kuchaguliwa,katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
kil2
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa Mwenyekiti pamoja na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar kuelezea mikakati walioiweka baada ya kuchaguliwa,katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
kil3
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheri akifafanua baadhi ya maswala yalioulizwa na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa kuelezea mikakati yao walioiweka baada ya kuchaguliwa,katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

ANGALIA VIDEO MPYA KABISA YA #JIRANI TOKA KWA WITNESZ KIBONGE MWEPEC AND OCHU SHEGGY FT SNURA AND MZEE YUSSUF-JIRANI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI MAOFISA MISITU WANNE, APIGA ‘STOP’ UVUNAJI MAGOGO RUFIJI

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Maofisa Misitu wanne na kusimamisha shughuli za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Rufiji kwa muda usiojulikana baada ya kutoridhishwa na usimamizi wake.

Maofisa waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Dk. Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa Misitu Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa wilaya Seleman Bulenga.

Waziri Mkuu amefanya uamuzi huo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Rufiji kwenye ukumbi wa halmashauri kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanya jumba la maendeleo wilayani Rufiji.

 Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Njwayo kukusanya magogo yoye yaliyoko msituni na kuyapiga mnada na kuitaka  wizara ya Maliasili na Utalii kwenda wilayani Rufiji kufanya uchunguzi wa leseni za uvunaji walizozitoa kwa wilaya hiyo.

Waziri Mkuu amebainisha kwamba wilaya ya Rufiji ni moja kati ya wilaya inayoongoza kwa uvunaji wa mazao ya misitu bila ya kufuata taratibu licha ya kuwa na maofisa misitu.

“Hakuna mafanikio katika sekta ya misitu kwenye wilaya hii ya Rufiji. Nasimamisha shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu pamoja na watendaji wake kwa sababu hatuwezi kuacha watu wanakata magogo bila ya kufuata taratibu,”

“Haiwezekani Rufiji iwe shamba la bibi, nimesimamisha uvunaji wa magogo hata kwa wenye leseni hadi tuzichunguze zimetoka wapi. Hatuwezi kuruhusu maofisa wanashiriki vitendo vya hujuma kwa kuvuna misitu Rufiji na kugonga mihuli ya Kilwa kisha fedha wanatia mifukoni,” amesema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Rashid Salum kufuatilia maagizo aliyoyatoa kuhusu kizuizi cha Ikwiriri kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipokutana na watumishi wa wizara hiyo.

Julai 18 mwaka huu Waziri Mkuu alikutana na watumishi wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam  na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji.

Waziri Mkuu aliitaka wizara hiyo kupunguza idadi ya vizuizi vya ukaguzi wa mazao ya misitu kwenye  barababara  mbalimbali baada ya kukosa tija, alitoa mfano wa barabara ya kwenda mikoa ya kusini  kuanzia Dar es Salaam yenye vizuizi visivyopungua sita na kila kizuizi kinatumika kwa ajili ya kukagua mazao ya misitu na maliasili inayotoka kuvunwa.

Awali mbunge wa Rufiji Mohammed Mchengelwa alilalamikia vitendo vya dharau vinavyofanywa na watumishi wa sekta mbalimbali katika wilaya hiyo jambo linalosababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 26, 2016

Vodacom kuendeleza kuunga mkono kampeniza Usalama Barabarani.

$
0
0

 Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani, Mheshimi wa Hamad Masauni amesema kuwa bado kuna matukio mengi ya ajali za barabarani nchini zinaso sababisha vifo vya wananchi wengi hivyo kuna haja ya kuongeza nguvu katika kampeni za Usalama barabarani ili kupunguza tatizohili.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (wapilikulia), akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango mkubwa wa  wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia), wakati wa uzinduzi wahafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanjawa Kalangala la mkoani Geita, na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Geita Ezekiel Kyunga (kushoto) na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Kamanda Mohamed Mpinga.Wasanii wa maigizo wa Futuhi wa kitumbuiza kwenye viwanjawa Kalangalala mkoani Geita, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, yenye kauli mbiu” Hatuta kiajali,tunataka kuishi”.
NAIBUWaziri Masauni aliyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa mkoani Geita ambapo pia alitumia fursahiyo kuyapongeza makampuni ya kibiashara na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayosaidiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi kufadhili na kuendesha kampeni za Usalama barabarani.
“Pamoja na kuwepo na matukio mengi ya ajali serikali inafarijika kuona yapo makampuni ya kibiashara na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanashirikiana kwa karibu na serikali kupitia Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani kuendesha kampeni za Usalama barabarani kwa jamiii kiwemo kufadhili shughuli za uhamasishaji Usalama katika Wiki hii ya Nenda kwa Usalama barabarani”.Alisema Mh.Masauni.
Aliongeza kuwa jukumu hili  la kutoa elimu ya Usalama barabarani sio la Jeshi la polisi pekee bali kunahitajika ushirikiano kutoka  kwa wananchi wote kwa kuwa kila mmoja ni mtumiaji wa barabara na vyombo vya usafiri na aliwataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za Usalama barabarani.
Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha kampeni za Usalama barabarani kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Usalama barabarani na Kikosi cha jeshi la  polisi cha Usalama barabarani.
Katika miaka mitatu mfululizo Vodacom imekuwa ikifadhili Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambapo mwaka huu imetumia zaidi ya shilingi milioni 48 kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini katika uhamasishaji wa usalama katika kipindi hiki. 
pia imekuwa ikiendesha kampeni za usalama kwa madereva na makundi mbalimbali ya jamii kwa kushirikiana na wadau wengine wa masuala ya  usalama barabarani. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia,amesema kuwa Vodacom itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini. 
“Kama Kampuni ya mawasiliano tumekuwa tukiendesha kampeni inayojulikana kama ‘Wait to Send’ ambayo imekuwa ikihamasisha madereva kutotumia simu za mkononi wakati wanaendesha vyombo vya moto ikiwemo kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi”.Alisema Mworia.
Mworia pia alisema kuwa kampuni imekuja na mkakati wa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani inawafikia wanafunzi wa shule za msingi ili wawe wakiwa na uelewa wa umuhimu wa kuzingatia kanuni za usalama barabarani ambapo kwa kushirikianana Jeshi la Polisi imekuwa ikiendesha mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

$
0
0
Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai akisalimiana  na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati)  alipowasili katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kushoto ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
spi3
Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) na Naibu Spika wa Baraza hilo  Mhe Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea.
spi4
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati alipowatembelea. Wapili kulia ni Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
spi5
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kiwasalimia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar alipotambulishwa wakati wa kikao cha Baraza hilo.
spi6
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (kulia) na Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma (kushoto).
spi7
Spika wa Baraza la Wawakilishi  Mhe Zuberi Ali Maulid akimuelezea jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati wa ziara hiyo.
spi1
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasili Mjini  Zanzibar kwa kutumia Boti wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Wawakilishi mapema leo Septemba 2016.

 Picha na Ofisi ya Bunge

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Dkt. Zainabu Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Zainabu Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Zainabu Chaula mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Waziri Mhagama atoa siku saba kwa wadaiwa wa NSSF

$
0
0

 Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Bi. Jenister Mhagama akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSFProf Samwel Wangwe.
 Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia)akimpokea Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Bi. Jenister Mhagama alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe. (katikati).
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe (wa pili kushoto) akimuonyesha kitu Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Bi. Jenister Mhagama alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara pamoja na maofisa wa shirika hilo.
 Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Bi. Jenister Mhagama akiwa ameambatana na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe. (kushoto) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Bi. Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia).
 Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Bi. Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe (kushoto)



Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Bi. Jenister Mhagama ametoa siku saba kwa taasisi za serikali, wizara,makampuni na watu binafsi kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Zaidi Waziri Mhagama imeiagiza Bodi za wadhamini za mifuko mingine ya hifadhi ya jamii kuhakikisha wanawasukuma wadeni wao kulipa madeni yote wanayodaiwa ili kuiwezesha mifuko hiyo kujiendesha kwa ufanisi zaidi.

Waziri Mhagama alitoa tamko hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni huku akitumia fursa hiyo kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, Bw Erick Shitindi  kuhakikisha uongozi wa mifuko hiyo unampatia ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wote walioshindwa kulipa madeni yao.

“Ninafahamu fika kuna mikataba ambayo ilisainiwa na pande zote mbili kabla ya kutolewa kwa hiyo mikopo na makubaliano mengine hivyo naomba basi mikataba hiyo itumike kufanikisha agizo hili,’’ alisema.

Pia alimuagiza  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe kuhakikisha kwamba anampatia ripoti muafaka  ya utekezaji wa agizo hilo.“Kwa niaba ya serikali, ninataka kuona kwamba wadaiwa wote wa mifuko hii bila kujali nafasi zao kiuchumi au kisiasa wanalipa madeni wanayodaiwa…hii lazima ijumuishe makampuni, wawekezaji na taasisi za serikali,’’ alisema.

Awali,Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema licha ya mfuko wake kufanikisha utekelezeaji wa miradi mbalimbali ikiwemo majengo bado wateja wake wengi hawajalipa madeni wanayodaiwa na mfuko huo ikiwemo watu binafsi, taasisi za serikali na zile binafsi wakiwemo pia wale walionunua nyumba za shirikal hilo.

Kwa mujibu wa Prof. Kahyarara, shirika hilo bado linadai takribani sh bilioni 20 kutoka kwa wa wapangaji wake, deni linalohusisha pia dola za kimarekani milioni 1.2.Kiasi kingine cha bilioni 86 kinadaiwa kama adhabu kutoka kwa waajiri walioshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao.

Madeni mengine ni pamoja na deni la sh milioni 42 na Dola za kimarekani milioni 35.9 ambazo zilitolewa  kama mikopo kwa sekta binafsi mbalimbali huku mkopo mwingine  wa sh bilioni 38 ulitolewa kupitia SACCOS na badi hazijarejeshwa.“Hata hivyo tumeanza kuchukua hatua mahususi kwa kulingana na matakwa ya sheria kuhakikisha kwamba madeni yote yanalipwa,’’ alibainisha Prof Kahyarara.

Kwa mujibu Mkurugenzi huo kufutia mikopo hiyo shirika liwachukua hatua dhidi  wadeni wake hatua iliyosababisha baadhi ya wadeaiwa hao kwenda mahakamani kupinga huku uamuzi wa mahakama kuhusu suala hilo ulitarajiwa kutolewa leo (jumatatu).

Akiwa kwenye miradi ya shirika hilo Waziri Mhagama alionyesha kuridhishwa na miradi hiyo iliyoanza mwaka 2014 na inatarajiwa kukamilika mwisho mwa mwaka 2016 ukihusisha ujenzo wa nyumba 439 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu zikiwemo zile ambazo zitapangishwa.


WANANCHI WAILALAMIKIA TAZARA KWA KUFUNGA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam jana.
 Wananchi wakivusha relini pikipiki yao.
 Pikipiki ikivushwa.
 Waendesha bodaboda wakivusha pikipiki zao kwenye reli baada ya kufungwa kwa muda barabara katika makutano ya Reli ya Tazara na Barabara ya Mombasa Moshi Baa Dar es Salaam jana wakati mafundi wa  Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wakifanya ukarabati katika eneo hilo.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale


MAMLAKA ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) imelalamikiwa na wananchi kwa kutozingatia muda muafaka wa kufanyia ukarabati wa reli zake jambo linalowaletea usumbufu.

Malalamiko hayo waliyatoa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  kuhusu kadhia waliopata baada ya kufungwa kwa muda Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa kupisha ukarabati eneo la reli inayokutana na barabara hiyo.

"Kazi ya ukarabati wanayoifanya ni nzuri lakini wangekuwa wakiifanya nyakati za usiku ili kuepusha usumbufu huu tunao upata wa kuvusha pikipiki zetu relini" alisema Gedion Robert.

Robert  alisema katika nchi za wenzetu kazi za kusafisha miji na ukarabati wa namna hii hufanyika usiku ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia barabara kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

Mkazi mwingine kwa Diwani Stellah Urio alisema amelazimika kulipa sh. 400 kutoka kwa Diwani hadi Relini ambapo pia alilipa sh. 400 baada ya kubadilisha gari ili kufika Ukonga Mombasa na kujikuta akitumia sh.800 badala ya 400.

Jitihada za kumpata msemaji wa Tazara , Conrad Simuchile, ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kufika ofisini kwake na kuambiwa mwandishi arudi baadae alikuwa nje ya ofisi kikazi.

Rais Dkt Magufuli atembelea Bandari ya Dsm na atoa maagizo

$
0
0


  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 .
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Septemba, 2016 ametembelea Bandari ya Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bandari hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kununua mashine nne za kukagulia mizigo bandarini (Scanning Mashine).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa kati ya mashine nne za ukaguzi wa mizigo zilizopo, ni mashine mbili tu ndizo zinafanya kazi na hazina uwezo wa kukagua mizigo yote inayotoka na kuingia nchini kupitia bandari hiyo hali inayosababisha kutokuwepo kwa udhibiti wa uhakika wa udanganyifu.

"Kwa hiyo nawaagiza TPA, na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Mbarawa na Mamlaka ya Mapato mpo hapa hakikiseni mnanunua mashine za kukagulia mizigo nne ndani ya miezi miwili, na ikifika miezi mitano muwe mmenunua mashine sita, ni lazima mizigo yote ikaguliwe kwa mashine" Amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli ameiagiza (TPA) kwa kushirikiana na Wizara husika kuanza mazungumzo na kampuni ya kimataifa ya kuhudumia shehena ya makasha bandarini (TICTS) ambayo inapakia na kupakua mizigo katika gati namba nane hadi kumi na moja ili kurekebisha mkataba ambao Kampuni hiyo imeingia na Serikali kwa lengo la kuhakikisha nchi inapata manufaa yanayostahili.

Rais Magufuli aliyetembelea eneo la mita za kupimia mafuta yanayopakuliwa melini (Flow Meters) na kubaini kuwa mita hizo hazifanyi kazi, ameiagiza TPA kuharakisha mchakato wa kununua mita mpya na kuzifunga katika eneo hilo ili kudhibiti ukusanyaji wa mapato ya kodi ya mafuta.

Aidha, Dkt. Magufuli ameitaka TPA kujipanga kujenga bandari kavu (ICD) katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani  ili kuachana na bandari kavu zilizoanzishwa na watu binafsi hapa Jijini Dar es Salaam na ambazo zimekuwa zikitumika kukwepa kodi.

Akizungumza na Wafanyakazi mara baada ya kumaliza kutembelea bandari, Rais Magufuli amewatoa shaka wafanyakazi hao na wafanyakazi wengine Serikalini, kuwa zoezi la kuhakiki vyeti linaloendelea nchi nzima halina lengo la kuwafukuza kazi wafanyakazi bali linafanywa kwa lengo la kukabiliana na tatizo kubwa la wafanyakazi hewa ambao wamefikia 17,500 na pia kuondoa tatizo la wafanyakazi wanaotumia vyeti vya kufoji.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa.Katika hatua nyingine, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Deodatus Mtesiwa ambaye amestaafu.Kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula alikuwa Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Septemba, 2016

MAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UMMA KANDA YA MOROGORO YAFUMGULIWA

$
0
0
Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kikuu cha Kilimo Morogroro (SUA). 
mbs2
Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma Kanda ya Morogoro kwa Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango. Waliokaa ni Bi. Anna Kimwela, Mchumi, Tume ya Mipango na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

mbs4
Muwezeshaji Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo hayo.
mbs01
Washiriki pamoja na wakufunzi wa mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (aliyekaa wa pili kushoto) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

WAZIRI AMPA OFISA ELIMU WIKI MOJA KUPELEKA WALIMU RUFIJI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea magodoro 10 kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mendeleo ya Wananchi cha Kibiti, Bi. Cecilia Mfuko ukukiwa ni mchango uliotolewa na Chuo hicho kwa Hospitali ya Kibiti. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa michezo mjini Kibiti Septemba 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) \ Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee Abadallah Ngwele baada ya kupokea madawati 10 yaliyotolewa na wazee wa Kibiti katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti, Septemba 26, 2016. Kushoto ni mkewe Mary na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiingia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti wilayani Kibiti ambapo Waziri Mkuu alihutubia mkutano wa hadhara , Septemba 26, 2016. . Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………………

WAZIRI MKUUkuu ,Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule.

“Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.”,alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira.

“Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa.

Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa.

Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria.

“Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima”alisema Waziri Mkuu.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza zabuni ya ujenzi.

Kuhusu utengenezaji wa madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule nchini.

Aidha, alisema ipo miradi mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua.

Mtendaji Mkuu Mpya wa TTCL Atembelea Ofisi Yake

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) anayemaliza muda wake, Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akipeana mkono na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Mtangulizi wake, Dkt. Kazaura. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) anayemaliza muda wake, Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akipeana mkono na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Mtangulizi wake, Dkt. Kazaura.Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) anayemaliza muda wake, Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kushoto), leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Mtangulizi wake, Dkt. Kazaura. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) anayemaliza muda wake, Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kushoto), leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Mtangulizi wake, Dkt. Kazaura.[/caption] KAIMU Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo ametembelea Makao Makuu ya TTCL na kukutana na Mtangulizi wake, Dk. Kamugisha Kazaura. Utambulisho wa awali wa kiongozi huyo mpya umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, anaesimamia sekta ya Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora. Makabidhiano rasmi ya ofisi yatafanyika baadae. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) anayemaliza muda wake, Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akikumbatiana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Mtangulizi wake, Dkt. Kazaura. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) anayemaliza muda wake, Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akikumbatiana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Mtangulizi wake, Dk. Kazaura.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo ametembelea Makao Makuu ya TTCL na kukutana na Mtangulizi wake, Dkt. Kamugisha Kazaura. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo ametembelea Makao Makuu ya TTCL na kukutana na Mtangulizi wake, Dkt. Kamugisha Kazaura.Wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa TTCL. Wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa TTCL
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images