Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 985 | 986 | (Page 987) | 988 | 989 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa(kulia) wakati alipotembelea Mtambo wa  kutengenezea lami katika Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group leo wakati  alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi (wa pili kulia) Mtaam wa Mtambo N.P.Singh.
  bak1
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(kulia ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud.
  bak2
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis,akifuatiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohamed.
  bak3
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipanda ngazi ya moja ya nyumba zinazojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo   Bw.Said Salim Bakhresa  wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo.
  bak4
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa mashine za kutengenezea lami katika Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group N.P.Singh (wa pili kulia) wakati  alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum,(katikati) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa na (kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis,[Picha na Ikulu.]26/09/2016.


  0 0


  Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud
  Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wa leo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Mkoani Tanga
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano huo
  Waandishi wa Habari wa Mkoani Tanga wakichukua habari leo
  PRO wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA)Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari wa mkoani Tanga

  MAMLAKA ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imekusudia kuanzisha mpango mkakati maalumu wa udhibiti uchafuzi wa mazingira baharini (NMOSCRP) unaosababishwa na umwagaji wa mafuta unaofanywa bila ya kufuata taratibu za mazingira zilizowekwa na kuharibu mazingira.

  Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini Taifa Capt Mussa Hamza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wiki ya bahari dunia inayofanyika Kitaifa Mkoani Tanga kwenye viwanja vya Tangamano kesho Jumanne.

  Ambapo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yatakayokwenda sambamba na maonyesho mbalimbali na warsha itakayofanyika Septemba 28 mwaka huu.Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari wame lazimika kuanzisha mpango huo ili kukabiliana na uchafuzi huo ambao unaweza kuchangia utoekaji wa viumbe vya vilivyopo.

  Aidha alisema kuwa kutokana na uchavuzi huo wa mazingira uliopitiliza unachangia kwa kiasi kikubwa kuhatarisha mazilia ua samaki katika bahari na viumbe vingine vilivyomo baharini.Alisema Tanzania imeingia katika shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo usafiri mkubwa wa mafuta ni kwa njia ya bahari hali ambayo inalazimika kuanzisha sheria maalumu ambayo inaweza kulinda mazingira ya bahari.

  “Hakuna vyombo vinavyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kama vyombo bya baharini hivyo imetulazimu kuanzisha mpango maalumu ambao tunategemea kesho kuuzindua ili kuweza kukabilia na uchavuzi wa mazingira katika bahari yetu ya Hindi”Alisema.

  Hamza alitumia fursa hiyo kueleza kuwa miongoni mwa sababu za kufanya maadhimisho hayo Kitaifa Mkoa wa Tanga ni kutokana na mkoa huo kuingia katika mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bomba kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga ambapo kutakuwepo na fursa kubwa ya kuitangaza Tanga kwa wawekezaji.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafirishaji wa Majini Zanzibar (ZMA) Suleiman Masoud alisema kufanyika kwa maadhimisho hayo katika mkoa wa Tanga ni tija kwa bandari ya Tanga,kupitia maadhimisho hayo lengo ni kuitangaza bandari hiyo kwa wafanya biashara wakubwa ndani na nje ya nchi.

  Alisema Tanga inaweza kuwa ni sehemu kuu ya kitovu cha biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari na hata nchi kavu ikiwa itawekewa mipango madhubuti ya kuifufyua bandari ya Tanga.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya (wa pili kushoto) akipewa maelezo kutoka kwa Sista Edeline Jacob baada ya Dk Ulisubisya kuitembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) LEO. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru na kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari Kambi.
  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Ulisubisya akiwa kwenye wodi mpya wakati alipoitembelea hospitali hiyo leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru na katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi, Mhandisi Gaudence Aksante.
  Mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Ulisubisya wakati alipotembelea Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili leo.
  Mkurugenzi wa Tiba, Dk Hedwiga Swai wa hospitali ya Muhimbili,Mkurugenzi wa Tiba Dk Magreth Mhando kutoka wizara afya na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi wakitoka katika idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili baada ya katibu mkuu kuitembelea idara hiyo leo.
  Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akiwaeleza wageni wa Wizara ya afya jinsi mashine ya CT scan inavyofanya kazi.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Ulisubisya. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari Kambi na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali MUHAS, Henry Sawe.

  Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

  ……………………………………
   
  Na Neema Mwangomo
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya ameupongeza Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kupanua maeneo ya kutolea huduma za afya. 

  Dkt. Ulisubisya ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hospitali hiyo ambako ameona shughuli mbalimbali za maendeleo na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo.
  “ Nimefarijika sana na utendaji kazi wenu kwa kweli mnastahili pongezi na muendelee kufanya kazi, kwani asiyefanya kazi hapa si mahali pake,”amesema Katibu Mkuu Dkt Ulisubisya. 

  Baadhi ya maeneo ambayo yanapanuliwa kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za afya ni Sewahaji Wadi 18,Idara ya Magonjwa ya Dharura na ICU Wadi moja , wadi ambayo tayari inafanya kazi hivi sasa. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru amemuhakikishia Katibu Mkuu kwamba MNH itaendelea kutoa huduma bora na za kibingwa ili Watanzania wanunufaike na huduma zinazotolewa na hospitali hiyo. 

  “Mpango uliopo ni kuhakikisha MNH inaonyesha njia na kuwa mfano, tutafanya kila tuwezalo ili kutatua changamoto zilizopo ili kuendana na dira ya serikali,” amesema Profesa Museru. 

  Maeneo aliyotembelea ni Mwaisela ICU Wadi Moja, wadi tatu, Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Idara ya Radiolojia, Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Wadi 18 Sewahaji , Maabara Kuu na jengo la Watoto.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
  ban2
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,  Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
  ban3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,  Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
  ban4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
  ban5
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu   chumba cha mitambo ya  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
  ban6
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
  ban7
  Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimlaki kwa furaha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
  ban8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
  ban9
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016ban10
  Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Bandarini Bw. akieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
  ban11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa   Kampuni ya  Ushushaji Mizigo Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
   PICHA NA IKULU

  0 0


  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass2
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass3
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yanafanyika Kitaifa katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita, yalipokuwa yanaingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki hiyo. Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass4
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa zawadi ya Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza katika uchorani wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo zilipambanishwa katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita. Masauni aliyazindua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo yanafanyika Kitaifa, katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita. Masauni katika hotuba yake aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass5
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika Kitaifa katika Viwabya vya CCM Kalangalala mjini Geita. Maadhimisho hayo yalizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia).
  mass6
  Washiriki wa maonesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki ajali tunataka kuishi salama”. Maadhimishjo hayo yalinduliwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Katika hotuba yake Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.
  mass7
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha ushiriki, Mwakilishi wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Amanda Walter.  toa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0  Fatma Makame/ MCC

  Wananchi wa kijiji cha Chaani Wilaya ya Kaskazin ‘A’ Unguja wamelalamikia ubovu wa barabara inayoelekea Mkwajuni ambayo imekuwa kero kubwa kwao na wananchi wengine wanaotumia barabara hiyo.

  Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Bi. Neema Mchezo Bakari amesema tatizo hilo ni la muda mrefu na bado halijapatiwa ufumbuzi jambo ambalo linapelekea usumbufu katika harakati zao za kutafuta maendeleo.

  Amesema wananchi wanapata usumbufu mkubwa kutokana na kuwepo mashimo katika barabara hiyo na kupelekea baadhi ya madereva kukataa kupita na wengine kuendesha gari kwa kasi bila kujali mashimo hayo na kusababisha ajali.

  “Inafika wakati wajawazito kujifugulia njiani kwenye gari wakati wanapopelekwa hospitali kutokana maumivu wanayoyapata kutokana na mashimo yaliyomo katika barabara hiyo”, amefahamisha mwananchi huyo.

  Nae Chum Juma Simai amesema ubovu wa barabara hiyo umechangia baadhi ya madereva wa gari za abiria kutoza nauli kubwa kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali na kuitaka mamlaka husika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

  Nae Mkandarasi Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara Nd. Jafeti amesema serikali tayari inalishughulikia tatizo la barabara hiyo na ujenzi utaanza baada ya kukamilika hatua za kumpata mkadarasi na kuwataka wananchi kujenga subira na ustahamilivu.

  0 0

   Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,. Anastazia Wambura akiwasisitizia jambo mshindi wa kwanza hadi wa tatu baada ya kuwakabidhi tuzo zao.
   Washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili,  Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa Ubalozi wa China nchini,  Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,  Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
   Washindi hao 10 wakifurahia baada ya kukabidhiwa  tuzo.

  Na Dotto Mwaibale

  STARTIMES  imefanya Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za Beijing ya mwaka 2016 kwa mara ya pili jijini Dar es Salaam kwa lengo lakuendelea kukuza ushirikiano wa iutamaduni baina ya China na Tanzania.

  Akizungumza wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa kwa muda mrefu serikali ya China na Tanzania zimekuwa na mahusiano mazuri katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

  “Mahusiano mazuri ya kiutamaduni ndiyo yaliyopelekea serikali hizi mbili kuendelea kushirikiana na kuwa marafiki mpaka hivi leo. Uhusiano huo si tu unatunufaisha katika masuala ya kiuchumi bali pia kijamii. 

  Kupitia kazi za sanaa kam vile tamthiliya za michezo ya kuigiza na filamu watu huweza kujua na kujifunza tamaduni za kila upande. 

  Nawapongeza StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kutuletea maonyesho haya ambayo nina hakika yatakuwa na manufaa makubwa kwa tasnia yetu.” Alisema . Wambura

  “Pia ningependa kuwapongeza StarTimes kwa juhudi zao za dhati katika kukuza utamaduni wetu kuipa nafasi lugha ya Kiswahili kuwa mojawapo inayotumika kutafsiri filamu na tamthiliya hizi za 
  michezo ya kuigiza. Nimesikia mlifanya shindano la vipaji vya sauti ambapo watanzania kumi walipatikana na watakwenda kufanya kazi katika makao yenu makuu yaliyopo Beijing. 

  Hii ni hatua nzuri na jambo la kuigwa kwa kukipa Kiswahili nafasi kubwa. Ninegependa kumalizia kwa kutoa wito kwa washindi waliopatikana kwenda huko China kutuwakilisha vema kama mabalozi wetu na kukifanya Kiswahili kiendelee kutambulika zaidi.” alisema Wambura

  Akielezea umuhimu wa maonyesho hayo Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,. Guo ZiQi amebainisha kuwa kihistoria China imedumisha kwa dhati urafiki na mataifa ya Afrika na kushirikisha tamaduni ndio njia madhubuti itakayoenzi mahusiano hayo.

  ‘’Utofauti ndio unaofanya dunia pawe mahala pazuri pa kuishi na China na Tanzania kwa muda mrefu zimedumisha utamaduni wao unaovutia zaidi. Katika kilele cha mkutano wa jukwaa la ushirikiano baina ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya watu wa China, 

   Xi Jinping alionesha nia ya kujizatiti katika kudumisha mahusiano mazuri ya kiutamaduni, kuimarish mafunzo baina ya China na Afrika ili kusonga mbele kwa pamoja na vilevile kuhakikisha mustakabali wa ukuaji wa urafiki baina ya China na Afrika.’’Alisema  ZiQi

  ‘’Kwa kuendelea kukua kwa mahusiano ya maingiliano ya kiutamaduni baina ya watu wa China na Waafrika, michezo ya kuigiza ya runinga na filamu za Kichina imezidi kujizolea umaarufu na kuwa kichocheo muhimu katika kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili. Kwa hivi sasa Beijing inaongoza China katika uzalishaji wa michezo ya kuigiza ya runinga na filamu. 

  Mpaka hivi sasa ina taasisi takribani 3,400 zilizojikita katika uzalishaji wa filamu na vipindi vya uninga na uendeshaji, vikiwa tayari vimekwishazalisha zaidi ya mfululizo wa vipindi vya runinga 3,000 na karibuni filamu 300 kwa mwaka.’’ alisema ZiQi

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia na Ufundi ambaye alizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Wang Xiabo alisema kuwa,‘’mnamo mwaka 2014, Halmashauri ya Mamlaka ya Uandishi wa Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Runinga ya Beijing ilishirikiana na StarTimes kuzindua msimu wa Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za Beijing katika nchi za Kiafrika. Lengo kubwa lilikuwa ni kuleta simulizi nyingi za Kichina barani Afrika na kukuza uhusiano katika tasnia za filamu na runinga baina ya pande mbili.’’

  ‘’Maonyesho haya yamefanyika kwa mafanikio makubwa kwa miaka ya 2014 na 2015 mfululizo. Filamu maarufu za Kichina na mfululizo wa michezo ya kuigiza ya runinga  ambayo imeingizwa sauti kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa na lugha nyinginezo tano za Kiafrika zilionyeshwa na StarTimes kwa miaka hiyo iliyopita,’’ alisema Wang Xiabo kuwa,‘’Katika kipindi hiko tamthiliya kama zilipata mapokezi makubwa sana kutoka kwa hadhira ya barani Afrika.

  Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji waTaifa (TBC),  Ayoub Riyoba, ambao ni washirika wa kampuni ya StarTimes katika urushaji wa matangazo ya dijitali nchini Tanzania amebainisha umuhimu wa filamu hizo hususani katika ukuzaji wa tamaduni baina ya nchi hizo mbili.

  ‘’Tanzania na China zina historia ndefu ya mahusiano tangu enzi hizo za waasisi wa mataifa haya. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Sisi kama chombo cha habari cha taifa tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tunasaidia jitihada za 
  serikali kukuza na kuutangaza utamaduni wetu hususani lugha ya Kiswahili. Kwa takribani miaka miwili iliyopita TBC imekuwa ikionyesha tamthiliya za Kichina zilizoingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili. 

  Kwa kufanya hivyo hivyo tamthiliya hizo zimeonyesha kupokewa vizuri na kupendwa sana na watanzania kwani wamekuwa wakielewa kinachoonekana.’’ alisema Riyoba

  ‘’Mbali na kukuza lugha yetu ya Kiswahili nchini na nje yanchi, hii pia ni fursa kwa tasnia yetu ya filamu kujifunza kutoka kwa wenzetu ambao wamepiga hatua zaidi. Tasnia yetu bado ni change na inahitaji mengi ya kujifunza ili kusonga mbele na kufikia pale walipo wenzetu na kuwa inazalisha kazi nyingi zaidi za sanaa. 

  Ningependa kuchukua fursa hii kuipongeza na kuishukuru serikali ya China kwa jitihada zao wanazozionyesha katika kukuza filamu na lugha yetu ya Kiswahili. Na ningependa kuwaahidi kutokana na ushirikiano huu watazamaji wa TBC wataendelea kupata burudani ya tamthiliya 

  na filamu nzuri zaidi ya zilizopita.’’  alisema Meneja Mkuuwa TBC katika maonyesho hayo Ubalozi wa China nchini Tanzania pia ulikabidhi mfano wa hati za makubaliano ya kwenda kufanya kazi jijini Beijing kwa washindi 10 waliopatikana katika shindano la vipaji vya sauti lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

  Washindi hao 10 waliopatikana ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Saiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa (DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao (DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard (DSM).


  0 0

   Mmoja wa watoto wa  wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, Beatrice Moses akifurahia mchezo wa kuraka ndani ya bwawa la kuogelea katika bonanza la siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Afisa Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara wa Kampuni ya Simu za Mkononi YA Airtel (kulia), akimpa zawadi Beatrice Nalingigwa baada ya kuibukas kidedea katika shidano la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel,Warren Kanga (kushoto) na Umilkheri Matata wakichuana wakifanya vitu vyao katika shindano la kucheza muziki ikiwa ni sehemu ya burudani kusherehekea siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, wakifurahia ndani ya bwawa la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
    Baadhi ya wafanyakazi na familia zao wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha upendo na mshikamano wao ambao ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
   Mwanafamilia wa Airtel akiwapa chakula watoto ikiwa ni ishara ya upendo ulio ndani ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania yasherehekea siku ya wanafamilia mwishoni mwa wiki hii Kunduchi Wet n Wild .

  Ni muda muafaka kwa familia mbali mbali kuwezakujuana na  kujumuika kwa pamoja na kuweza kubadilishana mawazo na hata kufurahia mafanikia ya matunda waliyoyapata kwa mwa huu.

   Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao. "Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya.

  Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia  600 walishiriki katika bonanza hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki, kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea.  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana.

  0 0

  Na Abushehe Nondo, MAELEZO.

  Wadau wa habari nchini wameipongeza Serikali kwa kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za habari wa mwaka 2016.

  Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Bw. Theophil Makunga wakati akitoa taarifa kuhusu muswada wa Sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  “Tunaishukuru Serikali kwa kuanza mchakato wa kuiondoa sheria ya habari ya mwaka 1976 kwa kupeleka bungeni muswada mpya wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016” Alisema Makunga.

  Alisema kuwa muswada huo ambao umesomwa bungeni kwa mara ya kwanza na Waziri wa habari ,Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Nnauye utamaliza kilio cha siku nyingi cha waandishi na wadau wa habari kuhusu sheria ya mwaka 1976 ambayo ilionekana kuwabana katika utendaji wao wa kazi.

  Ameongeza kuwa katika muktadha huo, taasisi mbalimbali za kihabari na wadau wa habari wanatakiwa kushiriki katika kutoa maoni yao ili kazi ya uandishi wa habari isiwe na matatizo.

  Makunga amesisitiza kuwa muswada huo siyo mali ya wamiliki wa vyombo vya habari , wahariri, au vyumba vya habari vilivyopo Dar es Salaam pekee bali unagusa maslahi mapana ya sekta nzima ya habari nchini.

  Aidha, katika kukusanya maoni hayo ya wadau wa habari wamewekewa mpango utakaowawezesha kukusanya maoni yao nchi nzima kupitia klabu zao za waandishi wa habari zilizosambaa nchi nzima.

  Wadau wa habari nchini wataweza kusoma muswada huo na kufanya uchambuzi wa maudhui yake na hatimaye kutoa maoni yatakayowezesha kupatikana kwa sheria bora.

  Muswada wa Sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016 kwa mara ya kwanza umesomwa bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katika Mkutano wa Nne wa Bunge la 11 lililomalizika Septemba 16 mwaka huu.

  0 0

  Bonde la Mto Rufiji linavyoonekana.


  *Asema inaendeshwa kwa ubabaishaji

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itapitia upya sababu za kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) kufuatia mamlaka hiyo kuendeshwa kwa ubabaishaji.

  Hatua hiyo imekuja baada ya mamlaka hiyo kushindwa kusimamia uendelezaji wa bonde hilo na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ikwiriri mkoani Pwani. Alisema baada ya mapitio hayo shughuli za mamlaka hiyo zitahamishiwa kwenye mamlaka nyingine za serikali kwani RUBADA imeshindwa kufanyakazi hiyo kwa muda mrefu.

  “RUBADA wamepewa ardhi lakini wameshindwa kuiendeleza, tutafanya upya mapitio ya kuanzishwa kwake,” alisema. Akizungumzia kuhusu Kampuni ya Agro Forestry Plantation inayotaka kujenga kiwanda cha sukari wiyani Rufiji aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha asilimia 60 ya watumishi watakaowaajiri wawe ni vijana wa wilaya hiyo.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, kwenda wilayani Rufiji kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Mkuranga na Ikwiriri. Waziri Mkuu amelitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Ikwiriri kuhusu kutotatuliwa kwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.

  Naye Mkurugenzi wa halshauri ya wilaya hiyo, Rashidi Salum alimweleza Waziri Mkuu kuwa, mgogoro huo umeshatatuliwa kwa ngazi ya wilaya hivyo hatua iliyosalia ni kwa uWaziri wa Ardhi kufika na ramani ili kutoa uamuzi.

  0 0


  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi jiji la Dar es Salaam, Leo Komba (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu anachofahamu juu ya wananchi wawili kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo
  " Sasa hapo mimi sima la ziada, Wewe si ndiyo Mkurgenzi?" Sawa kuanzia mda huu, nakuagiza ukafute umilikishwaji ardhi uliofanywa katika eneo la makaburi haya", alisema Waziri Lukuvi na kuongeza " Na wale waliomilikishwa hapa nitafutieni kesho waje kwangu wanieleze ilikuwaje hata wakapata kumilikishwa eneo hili, na wale wote walioshiriki kwa namna yoyote katika kufanya hili uniletee majina yao mara moja".
  Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine, akimshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, William Lukuvi baada ya kutoa uamuzi wa kufuta umilikishwaji wa eneo hilo la makaburi kwa watu wawili.

  Waziri Lukuvi akifuatana na DAS wa wilaya ya Ilala wakati akiondoka kweneye eneo hilo la makaburi ya Kinyerezi, ambako amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wananchi na watu wawili waliokuwa wamemikishwa eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi Grayson Celestine. 
   
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi akisalimia na DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, kufuatia mgogoro wa wananchi wawili kumilishwa eneo hilo la makaburi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja.

  Katika sakata hilo, Waziri Lukuvi ameagiza kufutwa kwa umiliki huo mara moja ifikapo leo jioni, na pia kugiza kusakwa Pascal Kyonya Kazungu na Ntitonda Chukilizo waliomilikishwa eneo hilo watafutwe na kufikishwa ofisini kwake kesho.

  Kadhalika amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam, Leo Komba, kuorodhesha majina ya maofisa ardhi wote walioshiriki kuwamilikisha ardhi hiyo ya eneo la makaburi ili aweze kuwashughulikia kwa kuwachukulia hatua za kisheria. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Segerea Bona Kalua
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akipatiwa maelezo na Mbunge wa Segerea Bona Kalua alipowasili kwenye eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo. Kushoto ni DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo.
  Waziri Lukuvi akiwa na Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine alipowasili leo kutatua mgogoro wa kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni Dar es Salaam,.Kushoto ni Dar wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo
  Waziri Lukuvi akihoji jambo kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo.
  Waziri Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo. Kulia ni Mbunge wa Segerea Bona Kalua
  Wananchi wa eneo la Kinyerezi Sokoni wakiwa wamemzunguka Waziri Lukuvi alipowasili kwenye eneo la Makaburi hayo leo.
  PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0


  0 0

  Kila mwaka shirika la Four Corner Culture Program (4CCP) huandaa tamasha la kiutamaduni ili kukuza na kuenzi tamaduni halisi za kitanzania . Tamasha la mwaka huu limekuwa lakipekee sana kutokana matukio mablimbali ya kimaendeleo na kiutamaduni yaliyofanyika .Ambapo Shirika la Norwegian Church Aid kwa kushirikiana na 4CCP Hydom walizindua miradi mbali mbali ya maendelea katika sekta ya maji (Visima)ili kupunguza tatizo kubwa la maji linalo wakumba wananchi wa wilayani Mbulu mkoani Manyara na mkoa jirani wa Singida.
   Naibu Balozi Norway bwana TRYGVE BENDIKSBY .akizindua kisima cha maji kijiji cha ENDAGAW wilayani Mbulu. kutoka kulia ni TALE HUNGNES Mwakilishi Mkazi wa Shirika la NCA Tanzania,Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh.Flatey Massay, Balozi Msaidizi TRYGVE BENDIKSBY, Bwana Abeli Mfanyakizi wa NCA na Afisa Mradi wa WASH NCA Tanzania Bwana.Zakayo Makobelo.PICHA ZOTE NA IMANI NSAMILA.


  Bwana Zakayo Makobelo akitoa ufafanuzi Juu ya kisima hiki kitumiacho Nishati ya Jua.

  Mbunge wa Jimbo la Mkalama Mh.Allan Kilawa akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa kijiji cha Munguli wilayani Mkalama Mkoani Singida.

  Mkuu Wa wilaya ya Mkalama Mkoani Singida na Mbunge wa Mkalama wakionyweshwa Vifaa vifaa hivi vya kuzilisha nishati ya jua kwa ajili ya kusaidia Usamabazaji wa maji kijjijni.

  Naibu Balozi wa Norway Tanzania TRYGVE BENDIKSBY alipotembelea banda la NCA NA 4CCP HYDOM wakati wa Tamasha la Utamaduni Hydom.

  Vijana wa YouthCAN wakitoa elimu YA MAZINGIRA,AFYA NA MAJI SALAMA kupitia muziki wakati wa Tamasha la kiutamaduni.

  0 0  Bw. Ndirosy Mlawa akizungumza katika moja ya mikutano ya chama hicho.
  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  27/09/2016

  Dar es Salaam.
  CHAMAcha Viziwi Tanzania (CHAVITA)chaiomba Serikali kuandaa mkakati wa kuwawezesha walimu wa lugha ya alama kupata utaalamu wa kuweza kufundisha watoto viziwi kutumia lugha hiyo.


  Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Nadrosy Mlawa aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya wiki ya viziwi duniani ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Tanga.


  Bw. Mlawa  alisema kuwa mbali na hali ya maendeleo ya viziwi kuimarika kutokana na kukua kwa  mwamko katika jamii na Serikali kwa ujumla pamoja na  ushiriki wa wadau mbalimbali katika harakati za watu wenye ulemavu ambao  wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwa na wataalamu  wa kufundisha watoto viziwi nchini.


  “Kwa sasa hali ya maendeleo kwa viziwi inazidi kuimarika kutokana na kukua kwa mwamko katika jamii na serikali kwa ujumla, ushiriki wa wadau mbalimbali katika harakati za watu wenye ulemavu umesaidia kuimarisha hali hii tofauti na miaka ya 1990” alisema Bw. Mlawa


  Aidha, aliendelea kufafanua kuwa jamii imekuwa ikiunga mkono juu ya matumizi ya lugha ya alama na kupenda kujifunza lugha hiyo ya viziwi, pia kumekuwa na baadhi ya taasisi ambazo zinajali mahitaji ya viziwi na kuchukua hatua ya utekelezaji wa mahitaji hayo.


  Mbali na hayo, Mwenyekiti huyo alisema kuna changamoto nyingi wazipatazo viziwi kutegemeana na hali halisi ya mazingira, umri na shughuli wazifanyazo ikiwemo kutofundishwa kwa lugha ya alama katika ngazi zote za upatikanaji wa elimu.


  Vilevile ukosefu wa huduma ya ukalimani kwenye maeneo na matukio nyeti yanawafanya viziwi kufadhaika na kuonekana kuwa hawawezi, hawaelewi, wagumu na kutowajibika licha ya baadhi yao kuwa na taaluma mbalimbali.


  Bw. Mlawa aliendela kwa kusema kuwa kutotambuliwa kirahisi na utamaduni wa kiziwi anayetumia lugha ya alama na kubambikiwa majina yanayodhalilisha utu ni miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo katika jamii.


  Kwa upande wake Mratibu kutoka Chama cha Walimu wenye Uziwi Tanzania Francis Mbisso alisema kuwa pamoja na uwepo wa mikakati, sheria, kanuni na programu zenye matamko chanya bado utekelezaji wake unasuasua kwa baadhi ya maeneo nchini.


  Alisema kuwa shule za viziwi na vitengo vya viziwi zimekuwa zikikosa ufundishaji wa watoto viziwi kwa kutumia lugha ya alama ikiwa na sababu kubwa ya walimu kukosa utaalamu wa lugha hiyo na kutegemea kujifunza kutoka kwa wanafunzi wao.


  Mbali na hayo alitoa wito kwa jamii kwa ujumla wakiwemo waandishi wa habari kujifunza lugha ya alama ili kuweza kuwasaidia na kuwapasha habari zinazohusu jamii na huduma nyingine.


  Wiki ya viziwi duniani huadhimishwa kila mwaka  mwezi Septemba ikiwa na lengo la kuonyesha jamii uwezo wa viziwi na kuelemisha jamii changamoto wazipatazo kutokana na hali ya ulemavu wao na jisni ya kuzishughulikia

  0 0

  Balozi wa Korea nchini Mhe. Geum-Young Song akimsikiliza Katibu  Mkuu wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome alipomtembelea ofisini kwake jijini Dsm leo .
  bako2
  Katibu  Mkuu wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome akizungumza na Balozi wa Korea nchini Mhe. Geum-Young Song alipomtembelea ofisini kwake jijini Dsm leo .
  bako3
  Balozi wa Korea nchini Mhe. Geum-Young Song akimkabidhi zawadi Katibu  Mkuu wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome Ofisini kwake jijini Dsm leo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao

  0 0

   
  Na Lilian Lundo-MAELEZO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzindua ndege mbili za Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) zilizonunuliwa kwa kutumia kodi za wananchi.

  Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Septemba, 28 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1).

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamuriho leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa ndege hizo.

  Dkt. Chamuriho alisema kuwa ndege ya kwanza iliwasili nchini tarehe 20/09/2016 na ndege ya pili inatarajiwa kuwasili nchini leo tarehe 27/09/2016 kuanzia saa 6:00 mchana.

  Vile vile Katibu Mkuu huyo alisema kuwa ndege hizo zimenunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhudumia wananchi wa ndani ya nchiya Tanzania na nchi jirani.

  “Ndege hizo aina ya Dash 8 Q400 zimetengenezwa na kiwanda cha Bombadier nchini Canada ambapo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 76 na zitatumika katika kuhudumia soko la ndaniya Tanzania na nchi jirani,” alifafanua Dkt. Chamuriho.

  Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawakaribisha wananchi wote kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo unaotarajiwa kuanza saa mbili kamili (2:00) asubuhi.

  0 0

  Mkuuwa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipokea moja ya mfuko wa saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT-CCM) Sophia Simba ukiwa ni miongoni mwa mifuko 200 sa saruji iliyotolewa na UWT kusaidia maafa Kagera.
  Baadhi ya wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT-CCM) wakipakia mifuko ya saruji kwenye gari tayari kwa kupelekwa kwenye ghala la kukusanyia misaada inayyotolewa ili kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi.

  ………………………………………………………………..

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.

  Mkoa wa Kagera bado unaendelea kupokea misaada kutoka taasisi, mashirika ya dini, mashirika binafsi, vyama vya siasa pamoja na nchi mbalimbali ili kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililoathiri maeneo mbalimbali ya mkoa.

  Katika kuhakikisha wakazi wa mkoa huo walioathiriwa na tetemeko la ardhi, wadau nchini wanendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii ikiwemo vifaa vya ujenzi, vyakula pamoja na vifaa tiba.

  Akikabidhi msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT-CCM) Katibu wa umoja huo Amina Makiragi amesema kuwa mchango ni chachu inayolenga kupaza sauti ili kuhamasisha wananchi na wadau wengine kuendelea kutoa misaada yenye lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

  Katibu huyo wa UWT-CCM ameipongeza Serikali kwa hatua walizochukua katika kutatua la tetemeko la ardhi kwa umahiri mkubwa na kuanza kuchukua hatua za kurejesha miundombinu mbalimbali ya kutolea huduma za kijamii ikiwemo shule, vituo vya afya na barabara.

  Aidha, Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Sophia Simba amesisitiza kuwa katika maafa yeyote, wanawake na watoto mara kwa mara ndio wamekuwa waathirika wakubwa wa majanga yanayoikumba jamii.

  Ili kuhakikisha misaada inayotolewa na wadau mbalimbali nchini, Mwenyekiti Sophia ametoa wito kwa Kamati ya maafa kusimamia misaada hiyo ipasavyo na kuigawa kwa wakati kwa walengwa hasa wahitaji ambao wameathiriwa na tetemeko hilo na kuongeza kuwa ni fahari kuona ghala lipo wazi baada ya misaada iliyokusanywa kupelekwa kwa wahusika.

  Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ametoa shukrani kwa UWT kwa moyo wa kuwajali waathirika wa maafa yaliyotokana na tetemeko la ardhi mkoani humo. Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amewaasa wadau wengine kuendelea kutoa misaada na michango yao na kuwahakikishia kuwa misaada hiyo itatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa

  0 0

  kar1
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia  waathirika wa Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Wakwanza (kushoto) ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima wakishuhudia tukio hilo.
  kar2
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatazama mfano wa hundi hiyo na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  Ikulu jijini Dar es Salaam
  kar3
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam.
  kar4
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni  Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima.
  kar5
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya aliyeiwasilisha kwa niaba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ili fedha hizo zitumike kuwasaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
  kar6
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  kar7kar8
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 985 | 986 | (Page 987) | 988 | 989 | .... | 1898 | newer