Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 25,NDANI NA NJE YA NCHI

$
0
0



TANZANIA
IRAN
South China Morning Post
CHINA

soma hapa mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa kushughulikia mgogoro ndani ya CUF

$
0
0


MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ANAYO MAMLAKA YA KISHERIA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO NA HOJA ZILIZOWASILISHWA KWAKE NA BAADHI YA WANACHAMA NA VIONGOZI WA CUF

UTANGULIZI

Kuna baadhi ya watu wanadai kuwa, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya chama cha siasa, hivyo msimamo wake juu ya mgogoro wa uongozi wa chama cha CUF ni batili. Napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha kuwa, Msajili wa hana mamlaka ya kuingilia uamuzi halali uliofanywa na kikao halali cha chama cha siasa, Lakini, kama uamuzi ni batili na kikao ni batili au uamuzi ni halali umefanywa na kikao batili au uamuzi batili umefanywa na kikao halali, msajili hawezi kuutambua, kwani Sheria ya Vyama vya Siasa inampa Msajili wa Vyama vya Siasa wajibu wa kusimamia utekelezaji wa baadhi ya maamuzi ya chama cha siasa ikiwamo suala la upatikanaji wa viongozi wa kitaifa wa chama cha siasa kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama husika. Ni vyeme ieleweke wazi kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Usajili wa Vyama vya Siasa uamuzi wa kufanya mabadiliko yoyote kwa viongozi wa kitaifa wa chama cha siasa ni lazima upelekwe kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ili atambue mabadiliko hayo.

Hivyo, kuhusu mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF uliojitokeza kufuatatia kujiudhuru kwa Profesa Lipumba ni kwamba, malalamiko na hoja zilizowasilishwa kwa Msajiili wa Vyama vya Siasa na baadhi ya viongozi wa CUF ikiwamo Profesa Lipumba zilikuwa za aina tatu, ambazo ni zifuatazo:-
1.    Kupinga utaratibu uliotumika kuendesha Mkutano Mkuu wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016;
2.   Kujiuzulu na kutengua kujiuzulu uenyekiti wa taifa wa CUF; na
3.   Kupinga uhalali wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi cha tarehe 28 Agosti, 2016 kilichofanyika Zanzibar na maamuzi yake.

Malalamiko na hoja zote tajwa hapo juu zinahusu hatma ya baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama cha CUF. Viongozi hao ni wafuatao:-
1.    Profesa Lipumba ambaye aliandika barua ya kujiuzulu uenyekiti wa Taifa na kuitengua;
2.    Mheshimiwa Mgdalenda Sakaya Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara aliyesimamishwa uanachama na Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa cha tarehe 28 Agosti, 2016;
3.    Bwana Abdul Kambaya, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Taifa ambaye pia amesimamishwa uanachama na Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa cha tarehe 28 Agosti, 2016; na
4.    Bwana Shashu Lugeye Katibu wa Baraza la Wazee ambaye alifukuzwa uanachama na Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa cha tarehe 28 Agosti, 2016; 

MSIMAMO WA SHERIA

Hivyo, kwa kuwa kifungu cha 10(f) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 kinahitaji chama cha siasa kuwasilisha orodha ya viongozi wake wa kitaifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kifungu 8A(1) kinampa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuhifadhi taarifa za viongozi wa kitaifa wa Vyama vya Siasa na Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Usajili wa Vyama vya Siasa toleo namba 111 la mwaka 1992, inakitaka kila chama cha siasa kuwasilisha taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa panapotokea mabadiliko katika uongozi wa taifa. Hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa anao wajibu wa kuhakikisha taarifa za mabadiliko ya uongozi anazoletewa na chama cha siasa, ni sahihi kwa maana ya kuwa, yamefanywa na mamlaka halali ya chama kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika, ili kuepuka kupokea orodha ya mabadiliko ya uongozi wa kitaifa wa chama ambayo si halali kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama.

Vifungu hivyo vinasema ifuatavyo:-

“10(f) it has submitted the names of the national leadership of the party and such leadership draws its members from both Tanzania Zanzibar and Mainland Tanzania; …”

“8A.-(1) There shall be a register of political parties into which names, addresses and other particulars of registered political parties or national leaders of political Parties shall be entered”


Kanuni ya 5(1) inasema ifuatavyo:-

“5-(1) Where an office –bearer of a registered party ceases to hold office or a person is appointed to be an office-bearer of a registered party, the party shall, within fourteen days, send notice thereof to the Registrar.”

Kwa kuzingatia ulazima wa Msajili wa Vyama vya Siasa kujiridhisha kuwa, mabadiliko yoyote katika uongozi wa kitaifa wa chama cha siasa yamefanywa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika, ndipo akubali kufanya mabadiliko katika orodha ya viongozi wa kitaifa iliyopo katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ndiyo maana ikawepo kanuni ya 13(1) na 16 zinazompa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuhitaji maelezo kutoka kwa chama cha siasa, kuhusu viongozi wa kitaifa wa chama cha siasa. Kanuni hizo zinasema ifuatavyo, nanukuu:-

       “13-(1) The Registrar may at any time require a party to submit to him a return or report relating to the constitution, objects, office-bearers or membership as well as the finances of the party.
 2) Every office-bearer and every person managing or assisting in the management of a party shall forthwith comply with any requirement made by the Registrar under paragraph (1) of this Regulation.”
  “16. In the event of a breach by a party of the provisions of Regulation 6,7,8,11,12 or 13, every office-bearer of the party concerned shall be guilty of an offence and shall be liable on conviction to a fine not exceeding thirty thousand shillings or to imprisonment for a term not exceeding six months or to both such fine and imprisonment.”
Kwa maana hiyo basi, Msajili wa Vyama vya Siasa anayo mamlaka ya kushughulikia malalamiko na hoja tatu zilizowasilishwa kwake na baadhi ya wanachama na viongozi wa CUF, kwa sababu malalamiko na hoja zote zinagusa mabadiliko katika uongozi wa kitafa wa CUF.

Inaeleweka kuwa, suala la uanachama wa chama cha siasa ni uhusiano wa kimkataba uliopo kati ya mwanachama na chama chake. Hivyo, endapo mwanachama anayechuliwa hatua za kiidhamu siyo kiongozi wa kitaifa wa chama cha siasa, basi Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia mgogoro huo wa uanachama., labda chama cha siasa na mwanachama husika kwa hiari yao wamuombe Msajili wa Vyama vya Siasa kuwasuluhisha.

Isipokuwa, endapo mwanachama husika ni kiongozi wa kitaifa wa chama, basi Msajili wa Vyama vya Siasa anayo mamlaka ya kuingilia mgogoro huo ili kujiridhisha kuwa, mwanachama husika amesimamishwa au kufukuzwa uanachama wake kwa kuzingatia Katiba na Kanuni za chama husika, kwa sababu kusimamishwa au kufukuzwa uanachama wake kunaathiri nafasi yake ya uongozi wa kitaifa.

HITIMISHO
Hivyo, kwa kuwa kifungu cha 10(f) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 kinahitaji chama cha siasa kuwasilisha orodha ya viongozi wake wa kitaifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, na kwa kuwa kifungu 8A(1) kinampa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuhifadhi taarifa za viongozi wa kitaifa wa Vyama vya Siasa na kwa kuwa pia Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Usajili wa Vyama vya Siasa toleo namba 111 la mwaka 1992, inakitaka kila chama cha siasa kuwasilisha taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa panapotokea mabadiliko katika uongozi wa taifa. 

Aidha, Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mantiki ya majukumu yanayobebwa na vifungu hivyo, anao wajibu wa kuhakikisha taarifa za mabadiliko ya uongozi anazoletewa na chama cha siasa ni sahihi, kwa maana ya kujiridhisha kuwa mabadiliko hayo ya uongozi, yamefanywa na mamlaka halali ya chama na pia yametekelezwa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika.  Hatua hiyo inafanyika, ili kuepuka kupokea na kuhifadhi taarifa ya mabadiliko katika uongozi wa kitaifa wa chama cha siasa ambayo siyo halali, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika.

Kwa mantiki hiyo basi, nikijielekeza kwenye vifungu vya Sheria nilivyoainisha hapo juu, ni dhahiri kwamba, Msajili wa Vyama vya Siasa anayo mamlaka na wajibu wa kisheria, kuchunguza mabadiliko katika uongozi wa kitaifa wa chama yaliyofanyika na masuala yote yanayohusu na mabadiliko hayo. Mfano, pale ambapo mwanachama ni kiongozi wa kitaifa wa chama cha siasa Msajili anapaswa kujiridhisha kuwa, mwanachama husika amesimamishwa au kufukuzwa uanachama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni za chama, kwa sababu kusimamishwa au kufukuzwa uanachama wake, kunaathiri nafasi yake ya uongozi wa kitaifa.

MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO – NEC

$
0
0


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama. Wengine wanaoonekana na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mwongoza wageni na Mhifadhi wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Butiama, Jacob Thomas akitoa maelezo kuhusu picha za kumbukumbu za Baba wa Taifa kwa Mkurugenzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani na watumishi wa NEC walioitembelea makumbusho hiyo eneo la Mwitongo, Butiama –Musoma.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NEC waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwitongo, Butiama.    

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi waandishi wa habari wa mkoa wa Mara waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwitongo, Butiama. Watendaji wa NEC wako mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
  
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama Musoma akiwa ameambatana na watumishi wa NEC  na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT kutoka maeneo mbalimbali  kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Mwitongo wilayani Butiama. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iko mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
 Muongoza wageni wa maeneo ya historia nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwitongo Butiama Bi. Gaudensia Waziri akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani (mwenye kofia) kuhusu Kaburi na historia ya Chifu Burito aliyekuwa chiefu wa Kabila la Wazanaki.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani (Kushoto) akisalimiana na Msemaji Mkuu na kiongozi wa familia ya Baba wa Taifa Chifu Japhet Wanzagi (kulia) mara baada ya kuwasili eneo la Mwitongo wilayani Butiama. Wa Pili kutoka Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi. Annarose Nyamubi.

Na. Aron Msigwa – NEC, Musoma.



Viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa  aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake  ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani  mara baada  kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.


Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa  vitendo hasa  uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo  na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.


“Kupitia kumbukumbu hizi sisi watumishi wa Tume tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,  wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema Kailima.


Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa  manufaa ya taifa.


“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu Nyerere kabla hajajengewa nyumba na Jeshi, kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika  eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Kailima.


Bw. Kailima amebainisha kuwa  NEC itaendelea  kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa  viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.


“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa  wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,  matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”  Ameainisha Kailima.  


Kwa upande wake Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw. Jacob Thomas amesema kuwa  watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.


Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.



“Ninyi mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho hii mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania” 

LUGALO GOLF CLUB BINGWA MASHINDANO YA MKUU WA MAJESHI CDF TROPHY

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda (kushoto )akimkabidhi zawadi ya Kikombe Mshindi wa Jumla wa Kombe la Mkuu wa majeshi CDF TROPHY mpiga Golf ambaye ni Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Watara mara baada ya mashindano katika Uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam jana Septemba 24.
Mshindi wa Jumla wa mashindano ya CDF Trophy 2016 Mkuu wa majeshi mstaafu George Waitara (wa kwanza kulia)akipokea Mfano wa Tiketi ya Ndege aliyopewa baada ya kushinda Wapili kulia ni Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Venance Mabeyo,watatu Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda na Wakwanza kushoto ni mwenyekiti wa Lugalo Golf Club Brig Gen Michael Luwongo.(Picha
Mshindi wa Jumla wa mashindano ya CDF Trophy 2016 Mkuu wa majeshi Mstaafu George Waitara (wa kwanza kulia)akipiga mpira wakati wa mashindano hayo katika uwanja wa Golf Lugalo Dar es Salaam wakwanza kushoto ni katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Mh Job Masima.

JUMLA YA WAALIMU 701 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JIJINI ARUSHA WALIPWA STAHIKI ZAO

$
0
0



Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake,mapema leo jijini Arusha
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa wilaya


Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya kiasi cha shilingi 154 milion zimetolewa kwa Waalimu 701 wa shule za msingi na sekondari kutoka kwenye fedha ambazo zilitakiwa kulipa posho za nauli na simu za madiwani wa jiji la Arusha.

Akiongea na wanahabari ofisini kwake jijini hapa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini, Gabriel Daqqaro alisema kuwa kutokana na malimbikizo ya fedha za likizo,kufiwa,nauli, uhamisho waliokuwa wanadai walimu kwa kipindi cha mda mrefu ndio maana tumeamua kuwalipa ili waweze kufanya kazi ya kufundisha watoto wetu kwa moyo.

Daqqaro alisema kuwa baada ya kikao na mkuu wa mkoa Mrisho Gambo na waalimu wa shule 48 za jiji la Arusha, na kuagizwa kuhakikisha walimu wanalipwa stahiki zao ndani ya wiki mbili na agizo hilo tumelitiza na walimu wamelipwa fedha zao zote walizokuwa wanadai.

Alisema kuwa fedha zilizolipwa waalimu hao tumezitoa kwenye fedha zilizokuwa wakijilipa madiwani posho za usafiri na posho za simu na kuzielekeza fedha hizo kutatua kero ya waalimu na mwisho wa siku vijana wetu wapate elimu stahiki bila manung'unuko kutoka kwa waalimu.

''Hapa napenda tusiingize ushabiki wa kisiasa katika hili na tuache kuzusha maneno maneno yanayaashiria uvunjifu wa amani maana tayari nimeshaanza kusikia maneno maneno yanazuka kutoka kwa madiwani, sasa nasema hivi, sisi tumeamua kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa ,na kunakili madiwani wanadai kuwa wao walikuta fedha hizi zikilipwa na ndio maana wakaendelea kupokea,hivyo nnachotaka kuesma  kama kweli walikuwa na nia njema na wananchi kwanini wasizikate mapema mpaka wasubiri mkuu wa mkoa aje aone mambo hay,na wao ndio waanze kuongea maneno maneno''alisema DC Daqqaro.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha wananchi walio wengi wanaondolewa kero zao kwa wakati na kuondosha kabisa kero mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo waalimu kupewa stahiki zao kwa wakati.

Akawataka waalimu hao kuhakikisha malengo ya mkoa kuongeza ufaulu yanafikiwa kwa kufanya kazi kwa moyo mmoja huku serikali ikiendelea kumalizia malalamiko mbali mbali ya waalimu wa mkoa huo.

Malipo hayo ya waalimu 701 yametokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwataka DC na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athman kihamia kuhakikisha malalamiko ya waalimu walioyatoa kwenye mkutano wao yanatekelezwa ndani ya wiki mbili .

NAMNA WANANCHI WALIVYOJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA AFYA ZAO BURE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA HAPO JANA JIJINI DAR

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza na Wananchi walio fika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata vipimo na kupatiwa ushauri na Madaktari kutoka Hospitali Mbalimbali Jijini Dar es Salaam 
Wananchi wakiwa na watoto wao katika viwanja vya Mnazi Mmoja 
Wananchi wakiwa katika mistari ambao hawajapata namba 
Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma Mfinanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Zoezi la kupima vipimo kwa wananchi bure lililo ratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Hospitali mbalimbali za Dar es Salaam ikiwemo, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aga Khan Hospital, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ikiongonzwa na Rais wa Chama cha Madaktari Figo Tanzania na pia ni Daktari Bingwa wa Figo Dk. Onesmo Kisanga 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grece (kushoto) Magembe akiwaonyesha jambo wananchi walio jitokeza kupata huduma ya vipimo kutoka kwa Madaktari wa Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili mkoa wa Dar es Salaam ilioratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini humo na kutokana na mwitikio wa wananchi huwenda ziku zitaongezwa baada ya Mkuu huyo kujadiliana na madaktari hao ambapo Septemba 25 hapo awali ilikuwa ndio siku ya kuhitimisha zoezi hilo
Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja 
Zuhura Shaba (54) akiwa amebebwa na baadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Afya baada ya kujikuta amepoteza fahamu mara baada ya kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam , baada ya muda na mpiga picha hizi alibahatika kuongea nae na kuanza kusema kwa utaratibu kinacho msumbua na kueleza mengi baada ya kumdadisi alisema, yeye ni Mtoto wa 7 na baba yake ezi za uhai wake miaka ya nyuma aliwahi shika nyadhifa mbalimbali Serikalini kama, Waziri wa Afya, Meneja Mkonge Tanga, aliwahi kuwa Mbunge, hivyo anamshukuru Mkuu wa Mkoa na Mungu amuongoze kwa kila anachokifanya kwa Jamii ya Kitanzania na kumshukuru Rais wa Tanzania kwa kumpa maona ya kumchagua kijana huyu, Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa na kuishukuru timu nzima ya Madaktari kwa moyo wao kuona jamii ya kitanzani bado inahali duni na kushirikiana na Mkuu wa Mkoa kutuletea zoezi hili, nashukuru baada ya kujikuta napoteza fahamu nimejikuta nipo katika chumba huduma ya haraka na kupata huduma na sasa najiona ninanafuu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi Sophia Mjema (kushoto) akishiriki zoezi la kugawa namba kwa wananchi walioitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam 
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamenyoosha mikono wakitarajia kupata namba kwa ajili ya kupatiwa huduma ya vipimo 
Askari Polisi akizungumza na baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja 
Joice Mgeta akipatiwa vipimo na Dk. Danieli Chacha (kushoto) mara baada kujikuta anaishiwa nguvu ghafla akiwa katika foleni ya kusubiri kupata namba , kulia ni Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma Mfinanga 

(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

JWTZ KUONGEZA NGUVU UPIMAJI AFYA BURE MMNAZI MMOJA,YATOA MADAKTARI WAKE NA WAUGUZI 90 KUWASAIDIA WANANCHI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza na Wananchi walio fika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata vipimo na kupatiwa ushauri na Madaktari kutoka Hospitali Mbalimbali Jijini Dar es Salaam,hapo jana,ambapo leo RC Makonda ameongeza Siku Mbili (2), zoezi la Upimaji Afya bure

Awali ya yote niwapongeze wananchi wangu wa mkoa wa Dar es Salaam walioonyesha mfano mzuri wa kujali afya zao na jamaa zao kwa kuitikia fursa ya wito wangu wa kupima afya bure, lengo likiwa ni kuhakikisha tunazijua vyema na mapema hali za afya zetu ili tuwe na nafasi nzuri zaidi ya kushughulikia changamoto zozote zinazobainika ama zinazoweza kujitokeza kwa mujibu wa maelezo ya watalaamu.

Kitakwimu, wataalamu wetu kutoka taasisi na hospitali mbalimbali ambazo ninashirikiana nazo walipokea zaidi ya wagonjwa 14,000, idadi ambayo ilitupa moyo na faraja sambamba na changamoto ndogondogo za hapa na pale kutokana na ukweli kuwa hatukuwa na matarajio ya idadi kubwa kiasi hiki, jambo ambalo kimsingi lilipelekea zoezi kushindwa kukamilika Kwa muda uliokuwa umepangwa hapo awali.

Kwa msingi na nia yangu ileile ya kuhakikisha kila mwananchi aliyefika viwanja vya mnazi mmoja anapatiwa huduma, nimeona ni vyema niongeze siku mbili (2) za muendelezo wa upimaji wa afya ili kumpa nafasi kila mwananchi aliyefika ktk viwanja vya mnazi mmoja kupata huduma. Pili, imenibidi niongeze nguvu kwa kumuomba waziri wetu wa ulinzi Dr. Hussein Mwinyi kutupatia madaktari na wauguzi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambaye amelipitisha ombi hilo na hivyo kutuongezea madaktari wengine pamoja na wauguzi wasiopungua 90 ambao wataungana nasi kesho, hivyo kukamilisha jumla ya madaktari na wauguzi 240, idadi ambayo nina uhakika itatuwezesha kumuhudumia kila mtu na kwa wakati.

Mwisho ningependa kuwaomba wananchi wote hasa waliofika Mnazi mmoja kuendelea kuwa wavumilivu ili kuwapa moyo Madaktari wetu kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya.

Mimi RC wenu naendelea kushirikiana nanyi bega kwa bega na sitawaacha.

Rais Dk.Shein akutana na Madaktari Bingwa wa Upasuaji

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu,Utiwa Mgongona Vichwa maji (NED)Dk.Jose Picer  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 24/09/2016.
zz3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu,Utiwa Mgongona Vichwa maji (NED)Dk.Jose Picer (katikati) akiwa na Makmo wa Rais wa taasisi hiyo Dk.Mohamed Qureish (kushoto) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 24/09/2016.
zz1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu,Utiwa Mgongona Vichwa maji (NED)Dk.Jose Picer akiwa na Makmo wa Rais wa taasisi hiyo Dk.Mohamed Qureish walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 24/09/2016.


BARABARA ZA ARUSHA KUKAMILIKA MWAKANI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Shin Pil Soo wakati akikagua Daraja la Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.
Muonekano wa juu wa Daraja la Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akielekea kukagua kingo za Daraja la Themi linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha. 

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Arusha Eng. Johnny Kalupale (katikati), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), alipokagua ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 na barabara ya Arusha mchepuo (bypass), yenye urefu wa KM 42.4 jijini Arusha.
Muonekano wa barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 ambayo upanuzi wake unaendelea jijini Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishiriki kikamilifu katika uwekaji wa kifusi cha tabaka la juu la zege kabla ya kumwaga lami katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 ambayo ujenzi wake unaendelea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na baadhi ya wananchi wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 ambayo ujenzi wake unaendelea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), mkoa wa Arusha Bw. Elipid Tesha namna bora ya kupunguza msongamano uwanjani hapo.
Sehemu ya eneo la kuegeshea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Arusha ambao unakabiliwa na ufinyu wa maegesho ya ndege ambapo Serikali iko katika hatua za kuuboresha.

……………………………………………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi M/S Hanil Jiangsu J/V anayejenga barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 na barabara ya mchepuo (Arusha bypass) yenye urefu wa KM 42.4 kuhakikisha barabara hizo zinakamilika ifikapo mwezi Machi na Oktoba mwakani.

Profesa Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi barabara hizo na kujiridhisha na hatua iliyofikiwa kwa barabara zote.

“Meneja hakikisha ujenzi wa barabara hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa sehemu ya barabara inayoelekea Ikulu ya mjini Arusha ili kuiunganisha vizuri barabara hiyo kwa kiwango cha lami”, amesema Prof. Mbarawa.

Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqarro kushirikiana na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo kuhakikisha maji yanayopita kwenye madaraja yaliyopanuliwa kufuatia ujenzi unaoendela hayasababishi mafuriko kwenye makazi ya wananchi.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Eng. Johnny Kalupale amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara mkoani Arusha utakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

“Tumejipanga kuhakikisha barabara ya Sakina-Tengeru na ile ya mchepuo zote zitakamilika kama ilivyopangwa ili kupunguza msongamano hali itakayovutia ongezeko la watalii na hivyo kukuza uchumi wa mkoa wa Arusha”, amesema Eng. Kalupale.

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua uwanja wa ndege wa Arusha na kusisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuupanua uwanja huo ambao ni wa nne kwa uingizaji wa mapato nchini ili kuondoa msongamano uliopo sasa.

“Wakati Serikali tunajipanga kuongeza uwanja huu na nyinyi mjipange kuongeza mapato ili jitihada za Serikali ziendane na ubunifu wa watendaji”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), mkoa wa Arusha Bw. Elipid Tesha amesema uwanja huo ambao ni kitovu cha utalii katika ukanda wa Kaskazini ukiongezwa utaruhusu ndege nyingi kutua na hivyo kuuongezea mapato ambapo kwa sasa takribani miinuko 110 ya ndege hufanyika kila siku katika uwanja huo.

“Kwa sasa uwanja wa ndege wa Arusha una barabara ya kurukia yenye urefu wa KM 1.6 hali inayosababisha baadhi ya ndege kushindwa kuutumia ila mkakati wa uwanja huo ni kuuongeza uwe na urefu wa KM 2.5”, amesisitiza Bw. Tesha.

Uwanja wa Ndege wa Arusha uliojengwa mwaka 1956 ikiwa ni mkakati wa kuboresha huduma za utalii katika mkoa huo uko KM 7 kutoka Arusha Mjini na una eneo la ekari 280 na uzio unaoimarisha usalama wakati wote.

DK SHEIN AONGOZA HARAMBEE YA MWANAHARAKATI BIBI SITI BINTI SAAD

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi picha ya kuchora Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Pennyroyal inayojenga Hoteli Kubwa ya Kimataifa huko Matemwe Kaskazini Unguja Bw.Brian Thomson (kulia) iliyonadishwa na kuinunua kwa Shilingi za Kitanzania Milioni nane(8) pia akiwa amechangia Shilingi Miliion Ishirini na tano katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Sadi,hafla ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hayat Hotel Mjini Unguja,wakati huohuo ameahidi kuanzisha Chuo cha Muziki Academy katika Mkoa wa Kaskazini,ambapo mradi huo utagharimu shilingi za kitanzania Miliioni mia sita, wakiwemo na Walimu pamoja na zana zote
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi picha ya kuchora Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Pennyroyal inayojenga Hoteli Kubwa ya Kimataifa huko Matemwe Kaskazini Unguja Bw.Brian Thomson (kulia) iliyonadishwa na kuinunua kwa Shilingi za Kitanzania Milioni nane(8) pia akiwa amechangia Shilingi Miliion Ishirini na tano katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Sadi,hafla ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hayat Hotel Mjini Unguja,wakati huohuo ameahidi kuanzisha Chuo cha Muziki Academy katika Mkoa wa Kaskazini,ambapo mradi huo utagharimu shilingi za kitanzania Miliioni mia sita, wakiwemo na Walimu pamoja na zana zote.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) na Mtoto wa Mwanahamis Ali 9years mkaazi wa Shaurimoyo Mjini Unguja akichora kaburi alilozikwa Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad (katika picha ya kuchora chini) baada ya kukabidhiwa picha hiyo Rais, wakati wa harambee ya Ujenzi wa Ofisi ya taasisi hiyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa Hayyat Hotel Mjini Unguja,

Baadhi ya Mawaziri wakiwa katika hafla ya harambee ya Ujenzi wa Ofisi ya taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad inayotarajiwa kujengwa Fumba Mkoa wa Magharibi Unguja,wakiwa katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Hayyat Hotel Mjini Zanzibar,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya muungano Mzee Mwinyi(kushoto) pia Mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bi Nasra Mohamed Hilal (wa pili kuli) wakimuangalia Mtoto wa Mwanahamis Ali 9years mkaazi wa Shaurimoyo Mjini Unguja akichora kaburi alilozikwa Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad wakati wa harambee ya Ujenzi wa Ofisi ya taasisi hiyo inayotarajiwa kujengwa Fumba Mkoa wa Magharibi Unguja,katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Hayyat Hotel Mjini Zanzibar
Kikundi cha Muziki cha Rahatul Zamani kikitumbuiza wakati wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad hafla iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hayatt Hotel Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani)

Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Pennyroyal inayojenga Hoteli Kubwa ya Kimataifa huko Matemwe Kaskazini Unguja Bw.Brian Thomson (wa pili kushoto) akiwa na msaidizi wa kampuni ya ujenzi ya Pennyroyal inayojenga Hoteli Kubwa ya Kimataifa huko Matemwe Kaskazini Unguja Bw.David Haycok (kushoto)pamoja na Wasaidi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kutoka kulia) Mzee Burhani Saadat Haji na Chimbeni Kheir wakiwa katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hayatt Hotel Mjini Unguja,

Baadhi ya Viongozi na Wafanyabishara wa makampuni mbali mbali wakiwa katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hayatt Hotel Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]25/09/2016.
Baadhi ya Viongozi na Wafanyabishara wa makampuni mbali mbali wakiwa katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hayatt Hotel Mjini Unguja
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakijaza fomu maalum za kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wakati wa harambee ya Ujenzi wa Ofisi ya taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad inayotarajiwa kujengwa Fumba Mkoa wa Magharibi Unguja, katika hafla iliyofanyika jana ukumbi wa Hayyat Hotel Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]25/09/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi picha ya kuchora ya Marehemu Bibi Siti Binti Saad Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam Marine Fasty Ferry Huseein Mohamed wakati wa harambee ya Ujenzi wa Ofisi ya taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad inayotarajiwa kujengwa Fumba Mkoa wa Magharibi Unguja, katika hafla iliyofanyika jana ukumbi wa Hayyat Hotel Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]25/09/2016.

RC KAGERA ATOA TAARIFA KUHUSU HATUA ZA SERIKALI ILIZOCHUKUA KUHUSIANA NA TETEMEKO LA ARDHI

Ujenzi upya Ihungo, Nyakato kugharimu bilioni 60.

$
0
0
 Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.



Serikali imesema gharama za kujenga upya shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ni Sh. Bilioni 60 hadi kukamilika miundombinu yake ambayo itakayoruhusu wanafunzi kupata elimu kama kawaida.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo.

Katika kukamilisha ujenzi wa shule hizo, Mkuu wa mkoa amesema kuwa hatua ya kuvunja majengo yote imeshaanza ambapo tayari Kampuni ya CHICO ya Wachina inaendelea na uvunjaji wa majengo yote ili kazi ya ujenzi uanze..

“Wataalam wote wa ujenzi kutoka idara mbalimbali za Serikali wanaendelea na uchambuzi yakinifu wa majengo mapya ya shule hizo utakaozingatia viwango vya ujenzi ambapo ghrama za awali kwa tathmini iliyotolewa na wataalamu hao ni Sh. bilioni 30 kwa shule za Ihungo na Nyakato” alisema Meja Jenerali Mstaafu Kijuu.

Uamuzi wa kuzijenga shule hizo upya zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi, ulipelekea Serikali kuzifunga na kuwahamisha wanafunzi waliokuwa wanasomea katika shule za Sekondari Ihungo na Nyakato ili waweze kuendelea na masomo wakati shule zao zinajengwa upya.

Wanafunzi wa shule hizo tayari wamepangiwa shule watakazoenda ili kuendelea na masomo kulinhgana na mihula ya mwaka na ratiba za vipindi vya masomo kila siku.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amesma kuwa katika kuhakikisha ujenzi wa majengo ya taasisi za Serikali na wananchi yanakuwa imara na salama, wataalam wa Wakala wa Jiolojia Tanzania ndio watatoa ushauri wao kabla ya ujenzi mpya haujaanza ili ujenzi wa majengo mapya ufanyike sehemu sahihi.

Kuhusu misaada inayotolewa na Serikali, nchi rafiki, wadau na wananchi, Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Kamati ya Maafa katika kukabiliana na athari za tetemeko kwa wananchi walioathirika tayari imetoa mahitaji mbalimbali kwa waathirika wa tetemeko hilo.

Mahitaji yaliyotolewa kwa wananchi ni pamoja na unga wa sembe kilo 3,450, sukari mifuko 410, mchele kilo 3,150, maharage kilo 5,753, maji katoni 850, sabuni katoni 24, mashuka 90, mablanketi ya watu wazima na watoto 2,020, vyandarua 1,274, sare za wananfunzi 570, magodoro 694, mahema 127 na matrubali 2,760.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa amezitaka Kamati za Maafa za Wilaya zikarabati miundombinu ya kutolea huduma za kijamii ikiwemo shule za sekondari na msingi, vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoharibiwa na tetemeko la ardhi ili huduma hizo muhimu ziweze kurejea mara moja na kutoa huduma kwa wananchi.

Hadi sasa wamebaki jumla ya majeruhi 13 ambapo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wamebakia majeruhi tisa, Hospitali ya Mugana majeruhi wawili na Hospitali ya Rufaa ya Bugando majeruhi wawili ambao wanaendelea kupata huduma za matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, 2016 Mkoani Kagera lilisababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, majeruhi 427 tayari wametibiwa na kuruhusiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa na vituo mbalibali vya afya kwenye mkoa

Kampuni ya CHICO yaendelea na uvunjaji wa Shule ya Sekondari Ihungo ili kuruhusu ujenzi mpya wa shule hiyo.

TCRS yatoa vifaa vya zaidi ya milioni 60 kwa waathirika wa tetemeko Kagera.

$
0
0
Mkuu wa msafara wa Shirika la Kiristo la Kuhudumia Wakimbizi Tanganyika (TCRS) Jasmine Gwamsy akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu vifaa vyenye thamani ya jumla ya Sh. milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao wa kuwafuta machozi wanakagera baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.



Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
 
Shirika la Kiristo la Kuhudumia Wakimbizi Tanganyika (TCRS) limechangia vifaa vyenye jumla ya Sh. milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao wa kuwafuta machozi wanakagera baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.

Katika kuhakikisha hali za wananchi na ttaasisi za kutolea huduma za kijamii  zinaimarika na kurudi kwenye hali ya kawaida, wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi bado michango yao inahitajika.

Akikabidhi mchango huo, Mratibu wa Miradi inayoendeshwa na TCRS Oscar Rutenge pamoja na Jasmine Gwamsy wametaja mchanganuo wa msaada huo kuwa ni pamoja na blanketi, 1680, mashuka 840, ndoo za kutumia 840, nguo za kutumia kwawanawake, wanaume na watoto box 50, sabuni katoni 1680 pamoja na vifaa vingine 2250.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amemelishukuru shirika hilo kwa mchango wao huo kwani ni wa thamani hasa baada ya tetemeko hilo kuwaaathiri wananchi wa mkoa huo.

Aidha, Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewakaribisha na kuwataka wadau wengine waguswe kwa namna ya kipekee na waendelee kutoa michango yao waweze kuwasaidia wananchi na kurudisha hali yao  na kuendelea na shughuli zao za kijamii na kimaendeleo.

TAZAMA PICHA ZA BESDEI YA ZARI THE BOSS LADY NDANI YA ZENJI ILIVYOKUWA

$
0
0
Diamond Platnumz amemfanyia pati ndogo Zari The Boss lady kati siku yake ya kuzaliwa, pati hii imefanyika visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na watu maarufu kama Mose Iyobo, Aunty Ezekiel.Mtoto wao Princes Tiffah naye alikuwepo kwenye pati hio.
1920
123567
PICHA ZOTE KWA HISANI YA SAMMISAGO.COM 

MECHI YA HISANI YA WABUNGE MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA LAFANYIKA UWANJA WA TAIFA

$
0
0
 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia uwanjani kukagua timu ya Wabunge mashabiki wa Yanga na wabunge mashabiki wa Simba katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo wakati mchezwa hisani ya kuchangishafedha kwa ajili wahanga watetemeko la ardhi, mkoani Kagera.Yanga walishinda bao 5-2

 WAZIR Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wengine na timu wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza mechi ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Wabunge mashabiki ya Yanga na wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2
 WAZIR Mkuu Kassim Majaliwaakikagua timu kabla ya kuanza mechi ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Wabunge mashabiki ya Yanga na wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2
 .Mshambuliaji wa timu ya wabunge mashabiki wa Yanga,Ridhiwan Kikwete akiwatoka wachezaji  wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2

Mshambuliaji wa timu ya wabunge mashabiki wa Yanga akiwa,Mwigulu Nchemba akiwapiga chenga wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii

WADAU WA UTALII WAIOMBA SERIKALI KUAINISHA KODI ZOTE ZA HIFADHI NA KUZIWEKA KATIKA MFUMO MMOJA

$
0
0

Mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji Wa utalii (TATO) Wilbroad Chambulo akichangia mada wakati wa mkutano
mkutano uliandaliwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wa wadau wa utalii walikutana kujadili changamoto na Tathimini zinazokabili sekta hiyo .

katika mkutano huo pia wakuu wa wilaya zote zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha walihuthuria .

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea .


Na Woinde Shizza,Arusha

Wadau Wa utalii wameitaka serikali  kuainisha kodi zote na kuweka katika mfumo mmoja ili kuepuka usumbufu unaojitokeza mara kwa mara pindi wageni wanapokuwa katika matembezi yao.

kodi hizo watatozwa katika sehemu mbali hususa ni katika mageti ambayo wanaingilia watalii mbugani kwani hivi sasa kumekuwepo na kodi nyingi ambazo zinaleta usumbufu kwa wageni ambapo wanasimamishwa kila mahali kwa mud a mrefu na kushindwa kufurahia utalii wanaoukuja kuufanya nchini hapa..

Hayo yameelezwa na mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa utalii (TATO) wilbroad chambulo wakati akiongea katika kikao cha wadau wa utalii kilichoandaliwa na mkuu Wa mkoa Wa Arusha cha kujadili changamoto na Tathimini zinazokabili sekta hiyo .

Aliongeza kuwa mgeni anapofika nchini anatakiwa kupokelewa kama mfalme sio kusumbuliwa kwa kuwekwa mda mrefu katika viwanja vyetu vya ndege kwani inawakatisha tamaa na kujutia kuja kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.

"Unakuta mgeni anakuja akifika kiwanja cha ndege anakaa zaidi ya lisaa limoja na nusu kwenye foleni akisubiria visa kweli huu ni usumbufu ,tunatakiwa mgeni akija hapa tumpokee kwa tabasamu ikiwezekana tumtandikie zulia jekundu ili akienda kwao atangaze nchi yetu na utalii wetu kwa ujumla "alisema Chambulo.

Pia aliitaka serekali ifatilie na ishughulike na utozwaji Wa ada za kodi zinazotozwa na mageti ya wilaya ya Monduli pamoja na geti la wilaya ya ngorongoro."Serekali na Wadau wote tunatakiwa kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama Wa watalii na Mali zao unaimarishwa zaidi"alisema

Kwa upande wake mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa mkutano huo ameuita ilikuwaleta pamoja kushiriki na kujadili namna gani watakuza utalii na kuboresha utalii katika mkoa Wa Arusha kwa ujumla na iwapo watashirikiana kwa pamoja itasaidia pia kukuza mapato na kuwa maradufu zaidi
.
Alisema nivizuri Wadau Wa utalii wakashirikishwa kwa mabadiliko yoyote ya ongezeko la kodi ili baadae kusiwepo na malalamiko ya kuegemea upande mmoja.Aliongeza kuwa wao kama mkoa wanamkakati Wa kifunga CCTV katika maeneo mbalimbali ya mkoa ili kuzibiti uhalifu wanaofanyiwa watalii au wageni wanaotembelea mkoa wetu pamoja na vivutio vilivyopo Mkoani hapo.

Katika mkutano huo mambo mbali mbali yaliazimiwa ikiwemo kuitaka serikali na Wadau wa utalii kuweka mikakati ya ulinzi na usalama pamoja na kuangalia jinsi ya kuzuia ujangili.

Naibu Waziri Mhe. Anastazia Wambura awaagiza Wasanii kusajili kazi zao BASATA.

$
0
0

Na Shamimu Nyaki-WHUSM  

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura ametoa agizo kwa wasanii nchini kuhakikisha wanasajili kazi zao katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili watambulike kwa mujibu wa Sheria.

Agizo hilo amelitoa jana Jijini Dar es Salaam  alipokuwa anazindua Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA) ambapo amewaahidi wasanii kuwa wakijisajili watatambulika  na itakuwa rahisi kwa Serikali kujua changamoto wanazozipata na kuzitatua kwa urahisi.

“Napenda mtambue kwamba suala la Urasimishaji linakwenda sambamba na uwepo wa Haki Miliki ya kazi za ubunifu, nawashauri mtunze Haki Miliki zenu na msiziuze na wale wabunifu  wapya na ambao hamjasajili kazi zenu nawaomba mfanye hivyo ili kuepuka uharamia”.Alisisitiza Mhe. Anastazia.

Aidha Mhe.Naibu Waziri amewaomba wadau wote wa Sanaa kutoa maoni yao katika kuboresha tasnia hii yenye kubeba maeneo kama Muziki, Filamu, Maonyesho, Ususi, na Uchoraji ili kuwezesha tasnia hii kujulikana na  kuboresha mapato ya Wasanii.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amewataka Wasanii kutunza vibali wanavyopatiwa na Baraza hilo kwani ndio utambulisho wao popote wanapokuwa na inakuwa rahisi wao kusaidiwa wanapopata changamoto.

“Wengi wenu mmejisajili lakini wale wachache ambao bado naomba mfanye hivyo ili sisi tuwatambue na Sheria ya  Haki Miliki pia iwatambue”.Aliongeza Bw.Muingereza.

Naye Msanii wa Uchongaji Bibi Hapiness Mmbaga amewashauri wanawake kupenda fani hiyo na kuacha dhana inayosema kuwa kazi hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu kwani ulimwengu wa sasa umebadilika hakuna tena kuchagua aina ya kazi ya kufanya.

Tamasha la siku ya Msanii duniani linaadhimishwa kwa mara tatu mfululizo ambalo linalenga kuthamini mchango wa kazi za Sanaa hapa nchini ambao kauli mbiu yake  ni “Nguvu ya Sanaa”na kilele chake itakuwa ni tarehe 26 mwezi oktoba mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa  uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akimkabidhi Cheti cha ushiriki  Bw.Adrian Nyangamale Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi katika uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.

HIVI NDIVYO SAFARI YA MWISHO YA MPIGANAJI MWENZETU ADOLF SAIMON KIVAMWO ILIVYOKUWA,TULIMPENDA SANA LAKINI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI

$
0
0
 
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media ambapo marehemu aliwahi kufanyika kazi kwenye Kampuni ya The Guardian Ltd akimwombea marehemu baada ya kuweka shada la maua.
Wabunge Saed Kubenea wa ubungo (kushoto), Zitto Kambwe Kigoma Mjini na Shy-Rose Bhanji wa Bunge la Afrika Mashariki wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Mwenyekiti wa 'Media Car Wash for Cancer' aliyeongoza kampeni ya matibabu ya Kivamwo, Benjamin Thomson na Mwana habari mwenzake Grace Nackso wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Mwana habari Amy Cunningham aliyewahi ufanya kazi na Kivamwo akiweka ua wenye kaburi wakati wa mazishi.
Wana habari wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Wana habari wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Wanafamilia wakiwa pamoja wafariji wao baada ya mazishi. (Imeandaliwa na robertokanda.blogspot.com)


Waombolezaji wa kipeleka jeneza nyumbani kwa marehemu, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam leo, tayari kwa shughuli ya kuagwa na hatimaye viwanja vya Leaders Club ambapo mwili wa marehemu ulikwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam leo.


Mwandishi wa Habari, Grace Nackso akimfariji mjane Frigeria Adolf Kivamwo wakati wa ibada fupi ya kuaga mwili wa marehemu Adolf Saimon Kivamwo nyumbani kwake Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam leo.


Adolf Saimoni Kivamwo enzi za Uhai wake.

Mjane Frigenia na wanawe wakiaga mwili wa marehemu Adolf Saimon Kivamwo nyumbani kwake Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafamilia na majirani wakiaga mwili wa marehemu Adolf Saimon Kivamwo nyumbani kwake Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam leo
Baadhi ya wanafamilia wakiaga mwili wa marehemu Adolf Saimon Kivamwo nyumbani kwake Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam leo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo nyumbani kwa marehemu Kivamwo, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam leo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo nyumbani kwa marehemu Kivamwo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo nyumbani kwa marehemu Kivamwo.
Wanakwaya ya Sinai wakitumbuiza katika shughuli hiyo nyumbani kwa Marehemu Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam leo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo nyumbani kwa marehemu Kivamwo.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza kulipeka kwenye gari kwa kuelekea viwanja vya Leaders Club kwa shughuli ya kuagwa.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza kulipeka kwenye gari kwa ili kuanza safari ya viwanja vya Leaders Club kwa shughuli ya kuagwa.
Waombolezaji wakeka jeneza kwenye gari tayari kwa safari ya viwanja vya Leaders Club kwa shughuli ya kuagwa.
Mjane Frigenia (kushoto) na wanawe, Arm Eliza (mwenye miwani) wakiwasili viwanja vya leaders Club.
Wanahabari wakilipokea jeneza baada ya mwili wa marehemu Kivamwo kuwasili viwanja vya vya leaders Club kwa shughuli ya kuagwa.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo.

Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo.
Wanakwaya ya Sinai wakitumbuiza katika shughuli hiyo.
Mjane Frigenia na wanawe, Arm, Eliza (mwenye miwani) na Miriam (kulia) wakiwa na huzuni wakati wa msiba huo.
Askofu Isaya Kiputa wa Kanisa la Pentekoste Holiness Mission akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media, Dkt. Reginald Mengi (kushoto) katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media, Dkt. Reginald Mengiakisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji baada ya kuwasili viwanja vya Leaders Club leo.
Mchungaji Reuben Njereka akitoa neno katiba ibada ya kuaga iliyofanyika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo.


Wana habari wakongwe walipata fursa ya kuonana katika tukio hilo. Kulia Muhidini Issa Michuzi 'Ankali' akisalimiana na Bernard Mapalala huku Hamisi Kibari (kushoto) na Charles Kayoka wakitabasamu.
John Holana akisoma risala ya marehemu.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media, Dkt. Reginald mengi akitoa salamu zake.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo.
Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo.
Mhariri wa zamani wa Gazeti la The Guardian, Evarist Mwitumba akielezea machache kuhusu maisha ya marehemu enzi za uhai wake wakifanya kazi pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa salam za faraja kwa wafiwa na kuoelezea waombolezaji namna bora ya kuenzi mema aliyotuachia marehemu Kivamwo.

Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa mawaidha yake na kusisitiza waombolezaji kutokusahau mazuri yaliyofanya na marehemu Kivamwo na kuaenzi katika maisha yetu.
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya The Guardian Ltd, Richard Mwigamba akitoa salamu zake.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Limited, Dkt. Jim Yonaz akitoa salamu na nasaa zake kwa waombolezaji.

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya MCL, Bakari Machumu akitoa pia salam kwa waombolezaji.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, pia Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini, wakili Deodatus Balile akitoa salam zake.
Mwenyekiti wa 'Media Car Wash for Cancer' aliyeongoza kampeni ya matibabu ya Kivamwo, Benjamin Thomson akitoa salamu na shukrani kwa wote waliojitoa kwa matibabu na shughuli ya mazishi ya marehemu Kivamwo.






Mwombolezaji pia shabiki wa Timu ya Simba, Ben akimpa ubani mjane Frigenia Adolf Kivamwo wakati wa shughuli hiyo.










Mwana habari Amy Cunningham aliyewahi ufanya kazi na Kivamwo akiweka ua wenye kaburi wakati wa mazishi.










Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akimpa mkono wa pole mjane na watoto wa marehemu.










Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwapa mkono wa pole na watoto wa marehemu.










Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, pia Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini, wakili Deodatus Balile






















Mhariri Mtendaji wa Mkuu wa New Habari 2006, Absalom Kibanda (kulia) akitoa mkono wa pole kwa wafiwa. Pamoja naye ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la the Citizen, Bakari Machumu (kulia) na Mhariri Mtendaji wa magazeti ya The Guardian, Richard Mwigamba.










Mhariri Mtendaji wa Mkuu wa MCL, Bakari Machumu (kulia), Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Limited, Richard Mwigamba (katikati) na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Limited, Dkt. Jim Yonaz wakitoa pole kwa wafiwa.













































Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, pia Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini, wakili Deodatus Balile.










Mjane Frigenia akifarijiwa baada ya kuaga mwili wa marehemu Kivamwo.










Mwana Habari Leah Samike (kulia) na Rechol Mkundai wakiwafariji watoto wa marehemu baada ya kuaga mwili baba yao Adolf Saimon Kivamwo.






















Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa sasa na zamani ambao waliwahi kufanya kazi na marehemu Kivamwo kwenye Kampuni ya The Guardian Ltd wakati wa shughuli hiyo.






















Askofu Isaya Kiputa wa Kanisa la Pentekoste Holiness Mission akiongoza ibada ya mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam leo.

















Mjane Frigenia Adolf Kivamwo akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe.


Wanawe Mariam (kushoto), Amy (mdogo kabisa) na Eliza wakiweka maua kwenye kaburi.








Rais Magufuli asali Ibada ya Jumapili St. Alban Posta Jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Padri Jackson Sosthenes (kushoto) na Padri Johnson Lameck wakati alipowasili katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam kushiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia waumini wa  kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
pic1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
pic2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
pic3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
pic4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.


Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images