Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 982 | 983 | (Page 984) | 985 | 986 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu wataalamu saba wakiwamo madaktari wanakwenda India Septemba 25, mwaka huu kwa ajili ya kujifunza upandikizaji wa kifaa cha usikivu ( COCHLEA IMPLANT).


  Baadhi ya wataalamu wanaokwenda India Septemba 25, mwaka huu kujifunza upandikizaji wa kifaa cha usikivu wakimsikiliza mkurugenzi.

  Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Pua, Koo na Sikio, Dk Edwain Liyombo wakati akizungumza leo kuhusu watoto wenye matatizo ya usikivu na kuzungumza.
  …………………………………………………………………
  Mafunzo kugharimu shilingi milioni 528
  ·Ujenzi, ukarabati na vifaa vipya kugharimu shilingi Bilioni 3.4

  Na. Neema Mwangomo (MNH)
  Hospitali ya Taifa Muhimbili inaendelea kutekeleza azma ya Serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ambao mara nyingi walikuwa wakifuata matibabu yasiyopatikana hapa nchini ama kutokana na kutokuwepo wataalamu au ukosefu wa vifaa vya kutolea huduma husika.

  Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar Es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema katika kutekeleza hilo, Septemba 25, 2016, Hospitali itapeleka watalaamu saba nchini India katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi ili wakajifunze kwa njia ya vitendo jinsi ya kufanya upasuaji na upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto.

  “Wataalamu hao ni pamoja na madaktari bingwa wawili wa upasuaji wa pua, koo na masikio, wauguzi wawili wa chumba cha upasuaji, mtalaam mmoja wa kupima usikivu pamoja na watalaam wawili wa kufundisha jinsi ya kuongea hususani kwa watoto waliozaliwa na tatizo hilo” amesema.

  Prof. Museru amesema kuwa takwimu za Hospitali ya Taifa Muhimbili zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya wagonjwa ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa kifaa cha usikivu ni watoto wadogo na kusisitiza kuwa huduma hii itasaidia watoto wengi hapa nchini na pia kujenga uwezo kwa wataalamu wa ndani ya nchi.

  “Gharama za kupandikiza kifaa cha usikivu kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi milioni 80 hadi 100 anapopelekwa nje ya nchi wakati mgonjwa mmoja anayepandikizwa figo nje ya nchi pia hugharimu kiasi cha shilingi milioni 40 hadi 60. Uwepo wa huduma hizi hapa nchini utawezesha watanzania wengi kupata huduma hii na kwa gharama nafuu zaidi na kupunguza mzigo kwa Serikali wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwani gharama za matibabu zitapungua kwa zaidi ya asilimia 50” amesisitiza.

  Amesema wataalam hawa wanatarajia kurejea hapa nchini Oktoba 28, 2016 tayari kuanza kutoa huduma hiyo. Mapema mwezi huu Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipeleka nchini India wataalamu 18 wa fani mbalimbali kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upandikizaji figo kwa watu wenye matatizo ya figo ambapo timu hiyo inatarajia kurejea mwishoni mwaka huu.

  Prof. Museru amesema gharama za kupeleka timu zote mbili ya upandikizaji wa figo pamoja na upandikizaji wa kifaa cha usikivu ni shilingi milioni 528 zikijumuisha gharama za mafunzo, nauli, fedha za kujikimu pamoja na gharama nyingine za mafunzo. Fedha hizi zote zitalipwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kujenga uwezo wa watalaamu wake.

  Katika hatua nyingine Prof. Museru amesema Hospitali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 3.4 ili kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 12 hadi 20, na sasa hivi tunavifanyia ukarabati viliyokuwepo 12 na kuweka vifaa vipya katika vyumba vya upasuaji vipya nane vitakavyoongezwa.

  Kuhusu upanuzi wa huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo Prof. Museru amesema eneo linalotumika kwa sasa linapanuliwa kwa kuongezewa vitanda kutoka 17 vya sasa hadi vitanda 42 sambamba na kuongeza mashine zake kufikia 42 na kuweka mtambo wa kuchuja maji (water-treatment plant).
  Prof. Museru amesema Hospitali itaongeza pia vyumba vya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu vipya vinne (ICUs) vikiwa na jumla ya vitanda 40 na kuviwekea vifaa vipya pamoja na vyumba vinne vya kupokea wagonjwa baada ya kutoka ICU (step-down ICU) na kabla ya kwenda kwenye wodi za kawaida navyo vitakuwa na vitanda 40. Aidha Ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu hii unaendelea na unatarajiwa kuwa umekamilika ifikapo mwishoni mwa Disemba 2016

  0 0


  Na Ally Daud-Maelezo,Dar es Salaam.

  HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imetenga Tsh. Bilioni 3.4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba, ukarabati  wa majengo ununuzi wa vifaa katika jengo la upasuaji na jengo la wagonjwa mahututi (ICU).

  Akizungumza hayo wakati Wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari watakaosafiri  kwenda nchini India Septemba 25 mwaka huu Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa MNH Prof. Lawrence Museru alisema mradi huo unatarajia kuanzia Januari mwaka 2017.

  "Tumetenga Bilioni 3.4 ili kuweza kuongeza na kukarabati vyumba vya upasuaji kutoka 12 hadi kufikia vyumba 20 pamoja na kuongeza vyumba vya ICU vinne na vitanda 40 pamoja na vifaa vipya ili kutoa huduma bora" alisema Prof. Museru.

  Aidha Prof. Museru alisema kuwa hospitali hiyo pia inatarajia kuwapeleka nchini wataalamu 7 wakiwemo madaktari bingwa wa fani za pua, koo na masikio  ili kujifunza kwa njia ya vitendo jinsi ya kufanya upasuaji na upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watu wazima na watoto.

  Prof. Museru aliongeza madaktari hao wanaenda kuhudhuria mafunzo ya mwezi  mmoja katika hospitali ya Appolo iliyopo nchini humo ili kupunguza gharama ya za kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

  Akifafanua zaidi Prof. Museru alisema kuwa tayari hospitali hiyo imepeleka timu ya wataalamu 18 India ili kupata uwezo wa upandikizaji figo ambapo mafunzo hayo yanatarajiwa kukamilika miwshoni mwa mwaka huu. 

  Kwa upande wake Mkuu Wa Idara ya Pua na Masikio wa Hospitali hiyo, Dkt.Edwin Liombo alisema kuwa mafunzo hayo yakikamilika watakuwa wameokoa zaidi ya asilimia 50 ya gharama za upasuaji na upandikizaji wa masikio, pua na figo.

  Aidha Dkt. Liombo aliongeza kuwa gharama za kupandikiza kifaa cha usikivu kwa mtoto mmoja ni kati ya Tsh. milioni 80 hadi Tsh. Milioni 100 na kiasi cha Tsh. Milioni 40 hadi 60 ikiwa ni gharama za kupandikiza figo kwa mtu mmoja nje ya nchi.
  MWISHO

  0 0

   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  na nahodha wa timu ya Kilimanjaro Queens, Sophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati), akimpongeza Nahodha wa timu ya mabingwa wa Kombe la Challenge la Afrika Mashariki na Kati 2016, Kilimanjaro Queens, Sophia Mwasikili wakati timu hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Asilimia kubwa ya wachezaji wa Kili Queens ni matunda ya mashindano ya Airtel Rising Star. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi wakati timu ya mabingwa wa Kombe la Challenge la Afrika Mashariki na Kati 2016, Kilimanjaro Queens, ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma na (wa pili kulia), ni Nahodha wa timu hiyo,  Sophia Mwasikili.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati), Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda (kushoto) na nahodha wa timu yaKilimanjaro Queens, Sophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam .
   Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam . Asilimia kubwa ya wachezaji wa Kili Queens ni matunda ya mashindano ya Airtel Rising Star.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam. wakishuhudia ni  Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (katikati) akifatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda
   wachezaji 8 wa Kilimanjaro Queens ambao ni matunda ya Airtel Rising Stars wakiwa katika picha ya pamoja wakati timu  hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel.  wachezaji hawa waliibuliwa kutoka katika michuano ya Airtel Rising Stars iliyopita
   Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (aliyeshikilia kombe) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji 8 wa Kilimanjaro Queens ambao ni matunda ya Airtel Rising Stars pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel Tanzania. 
   wachezaji wa Kili Queens wakiingia katika ofisi za Airtel  wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel na kushukuru kwa mchango wa Airtel katika kuinua vipaji vya vijana kupitia program ya Airtel Rising Stars.
   Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akiwapokea wachezaji  wa Kili Queens  wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel makao makuu leo
  Timu ya wanawake Tanzania ya Kilimanjaro Queens ikiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Airtel na TFF wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel leo
  Airtel yaipongeza Kilimanjaro Queens

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imeipongeza Timu ya wanawake Tanzania ya Kilimanjaro Queens kufatia ushindi wa walioupata katika michuano ya Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 maarufu kama CECAFA

  Timu ya kili Queen iliyosheheni vijana kutoka Airtel Rising Stars imeibuka washindi wa michuano hiyo baada ya kuichapa harambee Queens ya Kenya bao 2-1

  akiongea wakati wa timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel leo , Mwenyekiti wa soka la wanawake Tanzania , Bi Amina Karuma alisema" Tumekuja hapa Airtel leo na kuleta kombe hili kwani tunadhamini sana mchango mkubwa unaofanywa na Airtel kupitia program ya Airtel Rising Stars ambayo imetuwezesha kupata wachezaji mahiri na waliotuwezesha kuleta ubingwa huu nchini. 
  Tunajisikia faraja kuona Airtel iko bega kwa bega na sisi katika kuhakikisha soka la wanawake linaendelezwa na kukua kwa kasi, juhudi hizi zilizofanywa kwa miaka sita sasa zimezaa matunda kwa timu ya wanaume ya Serengeti boys na sasa kwa timu yetu ya Kilimanjaro Queens. napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwaomba waendelee kushirikiana nasi katika kukuza, kulea na kubaini vipaji chini ya mpango wa Airtel Rising Stars ambao umekuwa tija skwa maendeleo ya soka nchini"

  kwa upande wake Mkurugenzi Mkuuwa Airtel Bwana Sunil Colaso aliwapongeza wachezaji wa Kili Queens kwa ushinid wa kishindo kikubwa na kuahidi kuendelea kudhamini michuano ya Airtel Rising Stars ili kubaini vipaji vipya zaidi na kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao ili kutimiza dhamira ya kampuni yake chini ya Mpango wake kabambe wa Airtel FURSA

  kufatia ushindi huo Airtel imewazawadia wachezaji hao kila mmoja kiatu cha mpira ikiwa ni motisha kwa wachezaji kuchezea na kuendelea kufanya vizuri na kupata vifaa bora vya michezo

  wachezaji wa Kili Queen walitoka katika michuano ya Airtel Rising Stars ni pamoja na Stumai Abdallah, Sherida Boniface, Anna Ezron , Anastazia Antony, Amina Ally, Donisia Daniel, Najiat Abbasi na Maimuna Khamis

  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini kuwa tayari kwenda kufanya kazi kokote watakakopangiwa na Serikali kulingana na mahitaji ya eneo husika.

  Amesema moja ya wajibu wa watumishi wa umma ni kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania sehemu yoyote walipo ili kuwaletea maendeleo na atakayeshindwa ni vema akatafuta shughuli nyingine nje ya ajira za Serikali.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana  jioni (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mkunguni wilayani Mafia.

  Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

  Waziri Mkuu alisema kila awamu inakuwa na mkakati wake, watumishi wa umma wanatakiwa kubadilika na kufanya kazi kutokana na awamu iliyoko madarakani inavyotaka

  “Hii ni awamu ya kazi zaidi. Hata kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu! si neno la kufurahisha bali lina malengo yanayowataka Watanzania wote wafanye kazi,” alisisitiza.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mganga Mkuu wa mkoa wa Pwani, Dk. Beatrice Byarugaba kuimarisha huduma katika hospitali ya wilaya ya Mafia na kupeleka madaktari bingwa ili kuwapunguzia wananchi gharama za  kufuata huduma nje ya wilaya hiyo.

  Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuimarishwa kwa kitengo cha (TEMESA) kwa kupeleka mafundi watakaomudu kufanya matengenezo ya magari wilayani huko ili kupunguza gharama za kusafirisha magari hadi makao makuu ya mkoa wa Pwani kwa matengenezo pale yanapohitaji matengenezo.

  “Namna nyingine mnayoweza kufanya ni kuomba kibali maalumu cha kuruhusiwa kufanya matengenezo ya magari hayo kwenye karakana za watu binafsi zenye mafundi wenye sifa zinazotambulika na Serikali ili badala ya kuyapeleka Kibaha kwa matengenezo,” alisema.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Ndikilo ameiomba Serikali kuipa kipaumbele hospitali ya wilaya hiyo yenye kuhudumia wananchi zaidi ya 50,000 ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa wataalamu, dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

  “Kwa wilaya ya Mafia mgonjwa anapokosa dawa au vipimo maana yake aende Dar es Salaam au Rufuji au Mkuranga kufuata huduma hizo. Jambo hili linawagharimu sana wananchi hasa wa hali ya chini. Naiomba Serikali ituangalie  kwa jicho la huruma,” alisema.

  Mkuu huyo wa mkoa alitaja changamoto nyingine inayowakabili wananchi wa wilaya hiyo kuwa ni usafiri wa majini kutokuwa na uhakika kutokana na kukosekana kwa meli rasmi ya abilia yenye usalama na staha.

  Alisema kwa sasa wananchi wengi wanasafiri kwa kutumia majahazi na boti ndogo ambazo si salama na kwa sababu hiyo aliiomba Serikali kutafuta namna ya kutatua tatizo hilo linaloikabili wilaya hiyo kwa muda mrefu.

  Naye Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi 469 katika kada za afya, elimu barabara, maji na utawala.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, SEPTEMBA 24, 2016

  0 0

  Maandalizi ya Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika kesho Septemba 25 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika huku ushiriki wa wa wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu kwenye mbio hizo ukitajwa kuwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio hizo.

  Mbio hizo zinazofanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza zikiwa na baraka zote kutoka Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) , zikilenga kilenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini, kutangaza utalii na vivutio vilivyoko kanda Ziwa pamoja na kupambana na ujangili.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Msemaji wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema kamati ya maandalizi ya mbio hizo imejiandaa vilivyo na maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.

  Alisema wanatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1200 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka mashirika mbalimbali, walemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na wanafunzi.

  “Rock City Marathon inahusisha mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake, mbio za Kilometa tano zitakazohusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, mbio za Kilometa tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee, mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 pamoja na mbio fupi za mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi,’’

  “Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB, New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door,’’ alitaja.

  Kuhusu barabara zitakazohusisha mbio hizo zitakazoanza saa 12:00 asubuhi Bw Kasonta alisema; “Kwa washiriki wa mbio za km 21 wataanzia Uwanja CCM Kirumba, kwa wale wa Km 5 wataanzia barabara ya Nyerere eneo la Polisi Mabatini, kwa wale wa Km 3 ambazo ni mbio za wazee wataanzia Barabara ya Nyerere eneo la Makaburi ya Wahindi na kwa mbio za watoto yaani Km 2 wao wataanzia eneo la Mwaloni kuelekea CCM Kirumba,’’

  Kwa upande wa zawadi kwenye mbio hizo Bw Kasonta alisema washindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. mil 1.5/- kila mmoja, sh. 900,000/- kwa washindi wa pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.

  “Kwa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa makampuni huku pesa zilielekwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi.,’’

  Akizungumzia usalama katika tukio hilo ambalo litahusisha maelfu ya watu, Mwenyekiti Msaidizi wa kamati yam bio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu zaidi na jeshi la polisi na jeshi la hilo limeshajipanga vilivyo kwa ajili ya tukio hilo ili kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama wakiwemo watazamaji na washiriki mbio hizo.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Spika wa Bunge Job Ndugai, wakati Spika alipofika kumsalimia, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Septemba 24, 2016. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Aron Msigwa akimsainisha kitabu cha wageni mkazi wa Nyakanga Pius Rigamba wakati alipotembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.Katikati na mwandishi wa redio Victoria ya mjini Musoma.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akiwasilisha mada kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara. 

  Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Mchanga Mjaka akifuatilia mada akiwa na wageni waalikwa wenzake kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
   
  Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi akumuuliza swali Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
  Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Overblessing Msuya akitoa maelezo kuhusu Mashine ya Kielektroniki ya Usajili wa Mpigakura (BVR) wananchi waliotembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
  Mtoto anayesoma darasa la tano shule ya Msingi Kaminyonge aliyefahamika kwa jina moja la Salvatory (10) akimueleza Mhasibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Hubert Kiata kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi wakati alipotembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.Katikati na mwandishi wa redio Victoria ya mjini Musoma. 


  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani (wa pili kushoto) akishiriki sala ya kuanza kikao kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kinachofanyika mjini Musoma mkoani Mara.Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Agsotino Mbogella, Katibu Mkuu wa ALAT Habraham Shamumoyo na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Stephen Mhapa.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akiwasilisha mada kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara. 

  0 0


  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri (Kulia)
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru

  Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Tabora wakiulaki mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Mkoani humo
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru

  Kutoka Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Bw Dandala Mzunguor, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Fute Martin, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe, na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakijadili jambo muda mchache kabla ya makabidhiano ya Mwenge wa uhuru


  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanriakimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe john Mwaipopo kwa ajili ya kushirikiana na wakimbiza Mwenge Kitaifa kuukimbiza Wilayani humo

  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji jumanne Mtaturu, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe,Mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Uhahula, Mkuu wa wilaya ya Iramba, Injinia Masaka John Masaka, Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Choro Tarimo

  Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe, kulia ni Mkimbiza Mwenge Kitaifa George J. Mbijima
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akimuaga Mkimbiza Mwenge Kitaifa lucia Vitalis kutoka Manyara mara baada ya kumaliza ziara ya Mwenge katika Mkoa wa Singida na kuanza ziara Mkoani Tabora

  Na Mathias Canal, Tabora

  Mwenge wa Uhuru umewasili Mkoani Tabora ambapo unatarajiwa kuzindua miradi 45 yenye thamani ya shilingi Bilioni ishirini na tatu, Milioni nne, laki nne elfu na arobaini na saba mia tano sitini na sita 23,004,447,566/= ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 40% ukulinganisha na miradi ya mwaka 2015 iliyokuwa na thamani ya shilingi 9,207,720,213.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mgongolo, Kata ya Igunga, Wilayani Igunga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri amesema kuwa sera ya Vijana Tanzania ya Mwaka 2007 inatambua kuwa vijana ni watu wote wenye umri wa miaka 15-35 ambapo kulingana na sensa ya Mwaka 2012 inaonyesha kuwa Mkoa huo una jumla ya vijana 439,455 hivyo hekari 681 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za vijana ili kukidhi kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.

  Mwanri alisema kuwa Mwaka 2015 Mwenge wa Uhuru mkoani Tabora ulikimbizwa katika Halmashauri 7 zilizokuwepo ambapo Mwaka huu utakimbizwa katika Halmashauri 8 ambazo ni Igunga, Nzega Mji, Tabora Vijijini (Uyui), Sikonge, Urambo, Kaliua, Tabora Manispaa na Nzega Vijijini.

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Aggrey Mwanri mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo naye amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo ili aukimbize katika Miradi iliyopangwa ukiwemo wa kuzindua Mradi wa maji Vijijini, Kufungua vyumba viwili vya madarasa na choo cha matundu 10 katika Shule ya Sekondari Mwayunge, Kuweka Jiwe la msingi katika Hoteli ya Mjasiriamali Zengo T. Kija, Kuzindua mradi wa Kilimo cha bustani na Ufugaji wa samaki wa kikundi cha Vijana cha Msongela, na Kuzindua zahanati ya Kijiji cha Igogo.

  Miradi mingine ambayo Mwenge wa Uhuru utazuru ni pamoja na kugawa kadi za CHF kwa wanachama wapya, Kugawa vyandarua kwa wananchi na baadaye utazuru katika Shule ya Sekondari Nanga.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Singida kwa kujitokeza kwa wingi kutokana na juhudi na ushiriki wao kwenye kuibua, Kutekeleza na Kusimamia miradi mbalimbali ambapo pia amewataka wananchi hao kwa umoja wao kuitunza miradi hiyo.

  Mtigumwe alisema kuwa tangu Mwenge wa Uhuru ulipokabidhiwa Mkoani Singida ukitokea Mkoani Dodoma Septemba 17, 2016 umepita kwenye miradi 61yenye thamani ya Shilingi 14,266,628,518 iliyopo katika Halmashauri saba ambayo ni pamoja na Mradi wa elimu, Afya, Maji, Barabara, Biashara, Mazingira, Kilimo, Mifugo, Ushirika na programu mbalimbali za mapambano dhidi ya Rushwa, Dawa za Kulevya, Ukimwi na Malaria.

  Mtigumwe alisema kuwa mbali na Mwenge wa Uhuru kupita kwenye Miradi mbalimbali Mkoani Singida Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa amewaongoza wakimbiza Mwenge wenzake kitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2016 ambao ni “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa” Vile vile, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amesisitiza umuhimu wa vijana na wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya Rushwa, Dawa za kulevya, Kuchukua hatua dhidi ya tabia hatarishi zinazoweza kuchochea maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria.

  0 0

   TAREHE 23.09.2016 MAJIRA YA SAA 19:45 USIKU KATIKA MTAA WA NYAKATO MECCO WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, WATU WANAOZANIWA KUWA MAJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA INAYOZANIWA KUWA AINA YA SMG / SAR WALIVAMIA DUKA LA VIFAA VYA UJENZI MALI YA ELIKANA NGAGAYA MIAKA [38] MKAZI WA KANGAE NA KUPORA FEDHA PAMOJA NA SIMU NNE ZA AINA MBALIMBALI, AMBAPO BADO HAIJAFAHAMIKA KIASI CHA FEDHA KILICHOIBIWA NA THAMANI YA SIMU ZOTE.

  INADAIWA WAKATI MAJAMBAZI HAO WANAONDOKA ENEO LA TUKIO WALIFYATUA RISASI TATU ZILIZOMPATA GRACE MAEGA MIAKA [36] KWENYE BEGA LA MKONO WA KUSHOTO WAKATI AKIZIMA TAA NDANI YA DUKA LAKE LILILOPO JIRANI NA DUKA TAJWA HAPO JUU, KISHA WAKATOKOMEA GIZANI, NDIPO MAJERUHI ALIKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA MATIBABU LAKINI ALIFARIKI DUNIA MASAA MACHACHE BAADAE KWA KUVUJA DAMU NYINGI.

  JESHI LA POLISI BADO LIPO KATIKA MSAKO PAMOJA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, HADI SASA HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA UCHUNGUZI ZAIDI.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATA WATULIE HUKU WAKIENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI, LAKINI PIA AMESEMA MAJAMBAZI HAO WATASAKWA POPOTE WALIPO HADI KUTIWA NGUVUNI, HIVYO WANANCHI WASIWE NA MASHAKA.

  IMETOLEWA NA:
  DCP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akitazama samaki aina ya pweza wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha TANIPESCA eneo la Kilindoni wilayani Mafia, Mkoani Pwani.  Septemba 24, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akiwa ameshika moja ya samaki aina ya pweza wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha TANIPESCA eneo la Kilindoni wilayani Mafia Septemba 24, 2016.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dk Beatrice Byalugaba kufanya uchunguzi na kubaini madaktari wa hospitali ya wilaya ya Mafia wanaomiliki maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo na kuwachukulia hatua.


  Amesema ameshangazwa kukuta maduka ya dawa yanayomilikiwa na madaktari nje ya hospitali hiyo kwani tayari Serikali ilishaagiza kuondolewa kwa maduka ya madaktari karibu na hospitali wanazofanyia kazi.

  Waziri mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Septemba 24, 2016) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Mafia katika siku ya pili ya ziara yake wilayani mafia. 


  Kuhusu tatizo la upungufu wa dawa hospitalini hapo amemuagiza Dk. Beatrice kufanya utafiti wa aina ya magonjwa yanayowasumbua wananchi wa wilaya hiyo ili wanapoagiza waagize dawa nyingi za kutibu magonjwa hayo.Pia aliwataka watumishi wa hospitali hiyo wajitahidi kuwahudumia vizuri wagonjwa licha ya uchache wao. Lengo ni kuhakikisha wanapunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.


  Wakati huo huo Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kuwa na uhakika wa kupatiwa matibabu bure kwa kipindi cha mwaka mzima.


  Awali Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Joseph Mziba alisema mwamko wa wananchi kujiunga na mfuko wa CHF ni mdogo jambo linalokwamisha upatikanaji wa huduma za afya wilayani Mafia. Jumla ya wananchi waliojiunga na CHF ni  watu 6,000 kati ya watu 50,000.


  Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Eric Mapunda ameiomba Serikali kutoa kibali kwa halmashauri kununua dawa ambazo zinakosekana MSD kwenye soko moja kwa moja bila ya kupitia utaratibu wa manunuzi.


  "Kuna wakati tunakosa dawa MSD na kulazimika kununua kwa mawakala kwa kufuata taratibu ya manunuzi. Tunalazimika kununua boksi moja la ambapo boksi moja la panadol linauzwa sh. 20,000 na tukinunua moja kwa moja sokoni bila ya kufuata utaratibu huo boksi hilo hilo tunalipata kwa sh. 8,000,”alisema


  Baadhi ya wananchi waliokuwepo hospitalini hapo walieleza malalamiko yao kuhusu lugha chafu na dharau inayotolewa na baadhi ya madaktari na wauguzi.
                                                                                

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  JUMAMOSI, SEPTEMBA 24, 2016

                    

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kulia) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe wilayani Kasulu. Kulia ni Mbunge wa Kasulu, Daniel Nsanzugwanko na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wananchi wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo
  Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi. 
  *************
  WANANCHI wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, wanataraji kuanza kufaidi umeme wa REA pindi awamu ya pili ya mradi huo itakapo kamilika mwishoni mwa  Octoba 2016.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, alipotembelea miundombinu ya Umeme wa REA katika Wilaya ya Kasulu.

  Waziri Muhongo yupo katika ziara ya siku tano mkoani Kigoma kuangalia utekelezaji wa awamu ya pili ya miradi ya REA mkoani humo na Wilayani Kasulu aliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Martin Mkisi.

  Prof Muhongo, akiambatana na Wahandisi wa Tanesco, REA na Wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo, wamezungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe na Heru Juu Wilayani Kasulu.

   Aidha katika awamu ya tatu, vijiji vipatavyo 29 vitakamilishiwa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa za kufunga umeme wa bei rahisi na kujitokeza kwa wingi kwenye  mafunzo yatakayotolewa na Tanesco kuhusu umeme wa REA.

  Pia amewaagiza wakandarasi kukamilisha usambazaji wa huduma hiyo ifikapo Octoba 30 mwaka huu bila kuongeza siku hata moja.

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa (katikati) akiingia kwenye ukumbi wa Nyantale kwa ajili ya kufungua semina ya ujasiriamali ya wanawake eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
  Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.

  Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.

  Katibu wa Ofisi ya Jimbo la Segerea,Jacqueline,akizungumza na akinamama wa jimbo hilo kwenye semina ya ujasiriamali.
  Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka Benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio wa mapato na matumizi jinsi inavyosaidia kwa wajasiriamali kukua kibiashara kwenye semina hiyo.
  Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Erica Sendegeya,akizungumza na wanawake wajasiriamali umuhimu na faida ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwenye semina hiyo.
  ,akitoa mojawapo ya mada ya kuwawezesha wanawake wajasiriamali kukua kiuchumi kupitia biashara zao.

  Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka Benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio wa mapato na  Mama mjasiriamali akichangia mada katika semina hiyo
  Semina ikiendelea.
  Wanawake wajasiriamali wa Jimbo la Segerea wakisikiliza kwa makini wakufunzi waliokuwa wakizungumza kwenye semina ya ujasiriamali ya kuwainua kiuchumi wanawake. PICHA ZOTE na SHUNDA BLOG
  Mwenyekiti wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali wa Jimbo la Segerea,Salma Fumbwe,akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa (kushoto) katika semina ya ujasiriamali ya wanawake iliyofanyika ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima,jijini Dar es Salaam,leo. Kauli Mbiu ni Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi”.

  Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
  Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
  Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.  Na Elisa Shunda

  WANAWAKE washauriwa kutenganisha fedha ya msingi wa biashara na fedha ya matumizi mbalimbali ya nyumbani ili kuboresha na kusonga mbele kiuchumi tofauti na wakichanganya watakuwa wanadumaza biashara zao na matokeo yake kupata hasara inayopelekea kusimamisha biashara anayoifanya.

  Hayo yamezungumzwa na wakufunzi mbalimbali waliokuwa wakitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake kwenye semina yenye ujumbe wa kauli mbiu ya Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.

  Akizungumza kwenye semina hiyo mbunge wa jimbo hilo,Bonnah Kaluwa,alisema kuwa ameamua kuandaa semina ya ujasiriamali ya wanawake kwa ajili ya kuwapatia elimu mbambali za ujasiriamali pamoja na elimu ya utunzaji wa fedha za biashara kwenye sehemu yenye uhakika pasipokuwa na shaka wala wizi kwa kuwaletea benki ya Equity na Mfuko wa hifadhi ya Jamii ya PPF ambao watawasaidia kuwahifadhia fedha zao pamoja na kuwapatia bima ya afya na fao la kustaafu endapo watakidhi vigezo.

  “Wakinamama nimefurahi kwa jinsi mlivyojitokeza kwenye semina hii natumaini tukimaliza hapa kila mmoja wetu atakuwa amepata elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya ujasiriamali likiwemo la kutofautisha fedha ya matumizi ya nyumbani na fedha ya biashara kwa kuwa ukipata elimu ya kutenganisha vitu hivyo utaendelea kwenye biashara yako huwezi kutoa fedha ya biashara kununua chakula au kumsomesha mtoto lazima utayumba hivyo ni bora kila mtu ategeshe sikio lake vizuri kusikiliza elimu itakayotolewa hapa ambayo itatufumbua kutofautisha masuala ya nyumbani na biashara ambayo itatusaidia sana kufikia kwenye malengo yetu” Alisema Kaluwa

  Aidha akitoa elimu ya ujasiriamali kwenye semina hiyo,mkufunzi wa kujitegemea,Albert Magonga,alisema kuwa huwezi kuwa mjasiriamali halafu huweki mazingira ya kuonyesha bidhaa zako kwa majirani yako wanaokuzunguka na pia ni vyema mjasiriamali kuwa mbunifu wa kutambua eneo unaloishi ni kitu gani ambacho ni adimu ili uanzishe upate wateja wako ambao watanunua biashara yako kutokana na jinsi unavyokiandaa.

  Naye Mkufunzi wa utunzaji wa fedha kutoka benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,alisema kuwa watu wengi wanaokopa fedha katika taasisi mbalimbali nchini wana mapungufu ya kutokuwa na elimu ya fedha jinsi ya kuitumia akatolea mfano benki yao wanakopesha hadi maprofesa ambao wanaaminika wana upeo mkubwa wa kufikiri lakini kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha wanashindwa kutumia vizuri fedha walizokopa mwisho wanauza nyumba yake ili kurudisha kiasi cha fedha walizomkopesha.

  “Unapotaka kwenda kukopa katika taasisi yoyote ya fedha ni lazima uwe na elimu ya matumizi ya fedha la sivyo utaishia pabaya kwa mfano benki yetu ya Equity tunakopesha hadi maprofesa ambao tunaamini wana upeo mkubwa wa akili ila kutokana na kutokuwa na elimu ya utunzaji na utumiaji wa fedha wanashindwa kurudisha fedha zetu tunauza nyumba yake kwa ajili ya kurudisha kiasi cha fedha tulizomkodisha,hivyo ninyi leo mnapata elimu ya kujua bajeti yako na mapangilio wa mapato na matumaini ikiwemo na daftari la biashara zako ili kujua mahesabu yako” alisema Mwashilindi.

  Akaongeza kwa kusema mjasiriamali bora anapaswa kupata taarifa sahihi kutoka kwenye vyombo vya habari ni fursa kwake akatolea mfano ukipata taarifa ya habari kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mwezi wa kumi kutakuwa na joto kali wewe kama mfanyabiashara kutokana na taarifa hiyo lazima apange biashara ya kuuza vitu vinavyoendana na kipindi hicho kwa kufanya biashara kama Soda,Maji na Juice.

  Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Erica Sendegeya,aliwashauri akinamama wajasiriamali kujiunga na mfuko huo utakaowasaidia mambo mbalimbali ikiwemo la masuala ya afya kwa kupata vitambulisho vya NHIF kwa bei nafuu na kuwaambia mfuko wa PPF ukichangia kwa takribani miaka 15 kwa kila mwezi shilingi 20000 unaingizwa kwenye fao la pensheni hivyo aliwataka wakinamama hao kujiunga na mfuko huo.

  Semina hiyo ya ujasiriliamali kwa wanawake wa jimbo la Segerea itawezesha kuwapatia elimu ya utunzaji wa fedha akinamama zaidi ya 500 ambao wapo kwa kanda mbili ambapo mkutano huu wa mwanzo ulifanyika kwenye jimbo hilo kwa kanda ya A ambapo baadae kanda B nao watapatiwa elimu hiyo kupitia ufadhili wa benki ya Equity na Mfuko wa Hifadhi ya jamii kushirikiana na ofisi ya jimbo la Segerea.

  0 0

  “Tumedhamilia kulipiza kisasi katika mchezo huo, tunajua utakuwa mgumu, ila tumejiandaa kwa ajili ya mechi hiyo na ushindi ni lazima,” alisema Barnabas.
   Kikosi cha Kijitonyama Veterans
  Kikosi cha Warioba Veterans

  Timu ya Kijitonyama Veterans, kesho Jumapili, itapambana na timu ya Warioba Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Kijitonyama maarufu kwa jina la uwanja wa Bora au “Emirates" jijini Dar es salaam.

  Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mratibu wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto Omary.

  Mbali ya mechi hiyo ya asubuhi, Kijitonyama Veterans pia jioni itapambana na timu ya Sinza Veterans katika mchezo mwingine wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye uwanja huo huo.

  Majuto alisema kuwa mechi zote mbili  ni sehemu ya kujiweka fiti kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya ligi ya timu za veterans iliyopangwa kuanza baadaye mwezi huu kwa  Manispaa ya Kinondoni. Alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo na kuahidi ushindi.
  “Tupo vizuri kwa ajili ya mechi zote mbili na hii inatokana na kuwa na kikosi kikubwa ambacho , tumejiandaa vyema na tunaahidi kufanya vyema katika mchezo huu,” alisema Majuto.

  Kocha mchezaji wa timu ya Warioba Veterans, Barnabas Emilio alisema kuwa wamejiandaa kulipa kisasi kwa Kijitonyama Veterans ambao katika mechi ya mwisho walifungwa mabao 3-0.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurian Ndumbaro na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulkisho vya Taifa (NIDA), Mohammed Khamis Abdallah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba . Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Seerikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari.Picha na: Frank Shija, MAELEZO.

  Na Frank Shija, MAELEZO
  SERIKALI inatarajia kufanya zoezi la utambuzi na usajili wa taarifa za watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba ili kutoa vitambulisho vya Taifa vilivyo na taarifa zote muhimu za mtumishi husika.

  Hayo yamebainisha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.

  Kairuki amesema kuwa zoezi hilo la utambuzi na usajili wa wananchi ambalo linaanza na watumishi wa umma ni muhimu na litasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na kuondoa usumbufu kwa wananchi kwani taarifa zao zote muhimu zitakuwa sehemu moja hivyo kupunguza kero ya kuulizwa taarifa kila uendapo.

  Waziri Kairuki amesema kuwa zoezi hilo litashirikisha Wizara yake pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ambapo taarifa zitakazotumika ni zilizilizopo katika vitambulisho vya mpiga kura.

  “Kama mnavyofahamu kuwa Serikali ipo katika maboresho makubwa ya utendaji wake, hivyo ili kuendana na hali hiyo tutaanza zoezi la utambuzi na usajili wa watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba, zoezi litakalochukua takribani wiki mbili, zoezi hili ni muendelezo wa Serikali kukabiliana na matatizo ya kutokuwa na taarifa sahihi.”

   Alisema Kairuki.
  Aidha Kairuki amewata watumishi wote wa umma kushiriki zaoezi hilo wakiwa na taarifa zote muhimu zinazowatambulisha ambazo ni pamoja na Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu, kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Mzanzibar Mkazi, hati ya malipo ya Mshahara, hati ya kusafiria na kadi ya mpiga kura.

  Waziri huyo ametoa wito kwa waajiri kuweka mazingira wezesha ili kufanikisha zoezi hilo ikiwemo kutenga ofisi itakayotumiwa na kwa kazi hiyo pamoja na kusisitiza waajiri wahakikishe watumishi wao wanasajiliwa bila kukusa na taarifa ya zoezi hilo iwasilishe Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawabora ndani ya siku 14 tangu zoezi hilo kukamilika kwake.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro amewataka watumishi wote wa umma kulipa umuhimu mkubwa zaozi hilo na kusisitiza kuwa Serikali haita sita kucghukua hatuia za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma kwa mtumishi yeyote atakaye kaidi zoezi hilo.

  Awali akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu namna zoezi hilo litakavyotekelezwa nchi znima kwa muda wa wiki mbili tu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mohammed Khamis Abdallah amesema kuwa zoezi hilo litafanikiwa kwani wanao wafanyakazi zaidi ya 460 nchini nzima ambao wapo katika Ofisi za Halmashauri.

  Pia aligusia suala la vifaa na kusema kuwa tayari wamewasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo imewapa mashine za BVR kwa ajili ya kuzitumia katika zoezi hilo la utambuzi na usajili.

  Zoezi la utambuzi na usajili wa wananchi hasa watumishi wa uuma kukabiliana na vyanzo vya watumishi hewa kwa kuunganisha mifumo ya utambuzi wa watu na mifumo mingine ikiwemo usimamizi wa rasilimali watu na mishahara katika utumishi wa umma ambapo kuunganishwa kwa mifumo hiyo kutawezesha mifumo hiyo kuwasiliana na kutumia taarifa zilizo kwenye kanzi data ya NIDA suala litakalokuwa limerahisisha upatikanaji wa taarifa.


  0 0  0 0  NA HERIETH SEMGAZA


  Wafanyabiashara katika soko la kariakoo lililopo jijini Dares salaam wameombwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwachangia wahanga wa tetemeko la Bukoba mkoani Kagera leo katika harambee iliyofanyika katikati ya soko la Kariakoo jijini Dar es salaam

  Hayo yamesemwa na Philimin Romano Chonde Mwenyekiti wa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo(JWK) ambapo alitaja jumla ya pesa na thamani ya vifaa mbalimbali vilivyochangwa katika kampeni ya hiyo ,ambayo bado inaendelea amesema mpaka sasa wamepokea Jumla ya shilingi milioni 60 laki saba na mia Tano zimekusanywa  Philimin Romano Chonde amesema tunaendelea kupokea mchango wenu ili tuweze kuwasilisha kwa Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa katika siku itakayopangwa, Aidha amewapongeza wanachama,wafanyabiashara wote waliojitokeza kutoa michango yao na kuwataka waendelee kujitoa katika shughuri mbalimbali za Kitaifa.

  Nae SILVER MANDE mhazini Wa JWK amesema kuwa taasisi na wafanyabiashara wengine waendelee kujitokeza kwa wingi ili kutoa michango yao na kufanikisha kazi hiyo ambayo ni muhimu sana katika jamii yetu hasa kwa hawa wenzetu ambao walipata jamnga la Tetemeko la Ardhi huko Bukoba na kuathiri maisha yao na shughuli zao za kila siku.
  Taasisi mbalimbali na wafanyabiashara tunaomba muwe mstari wa mbele kutoa michango na kwa yeyote atakaye kuwanacho alete ili tuweze kujumuisha rambirambi zetu na kuwasilisha kwa Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

  0 0

    Kipa wa Timu ya Maji Maji ya Songea "Wana Lizombe", Amani Simba akiruka bila mafanikio wakati akijaribu kuudaka mpira uliopigwa kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji wa Simba, Jamal Mnyate na kuiandikia timu hiyo bao la kuongoza, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
   Mshambuliaji wa Timu ya Maji Maji, Enyima Darlington akiruka sambamba na Beki wa Simba kuwania mpira wa juu katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
   Mshambuliaji machachari wa Timu ya Simba, Laudit Mavugo akiondoka na mpira baada ya kumtoka Beki wa Maji Maji, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
   Mshambuliaji wa Timu ya Maji Maji, Enyima Darlington akitoa pasi nzuri ya kichwa kwa Mchezaji Mwenzake, Alex Kondo, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
   Ibrahim Ajib wa Simba akimpiga chenda maridadi, Luhanga Mapunda wa Maji Maji, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.

  0 0


  Naibu waziri wa Nchi ofis ya makamu wa rais muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina akifanya usafi na wananchi wa wilaya ya kigamboni katika kutekeleza agizo la Mh. rais la kila mwisho wa mwezi kufanya usafi.
  Naibu Waziri wa Nchi ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa na wananchi wa kigamboni waliojitokeza kwaajiri ya kufanya usafi katika fukwe za kigamboni
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari,hawapo pichani mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika fukwe za wilaya ya kigamboni.


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa kuhakikisha fukwe zote za kigamboni zinafanyiwa usafi na kuwa katika hali ya kuridhisha.

  Naibu Waziri Mpima ameseyasema hayo leo katika maeneo ya fukwe za kigamboni aliposhiriki katika siku ya usafi kitaifa ya mwezi wa September.

  Amesema fukwe za kigamboni ni chafu sana na usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni hauridhishi, “pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kusafisha mazingira leo fukwe ni chafu na wengine wanatuangalia tunavyosafisha huku wakiendelea na shughuli zao, Angalia wale wavuvi kwenye mitumbwi yao wanaendelea na kazi zao na wao ndo wachafuzi wakubwa huko baharini na nchi kavu. “Alisema.

  Mpina amemtaka mkuu wa wilaya hiyo kuwawajibisha viongozi walioko chini yake kwa kosa la uzembe wa ufuatiliaji wa sheria ya mazingira kabla hajawajibishwa yeye. “kiongozi mzembe afukuzwe kazi kabla haujafukuzwa wewe na kuingia kwenye matatizo.” Alisisitiza naibu waziri Mpina.

  Hata hivyo Naibu Waziri Mpina alimpongeza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha kampeni ya upandaji miti maarufu kama ‘’MTI WANGU’’ na kuwashauri wakazi wa jiji kushiriki Katika siku ya uzinduzi na kuahidi kuwa pamoja nao siku hiyo.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa ameelezea jitihada za usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni ikiwa ni pamoja na mashindano ya usafi wa mazingira na kuwataka wakazi wa kigamboni kuongeza jitihada za kutosha kuiweka kigamboni safi.

  Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi ni siku maalum ya usafi ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Rais la Usafi wa mazingira ambapo mwezi huu kitaifa imefanyika Kigamboni.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge Mhe. William Ngeleja akipokea hundi ya shilling million kumi kutoka kwa Mwakilishi wa Mwananchi Communications LTD Bw. Francis Nanai kwa ajili ya msaada kwa msadaa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
  nge8
  Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge Mhe. William Ngeleja akipokea hundi ya shilling millioni tano kutoka kwa  Mwakilishi wa Jubilee Insurance Bi. Elieth kileo kwa ajili ya msaada kwa msadaa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
  nge9
  Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge Mhe. William Ngeleja akipokea hundi ya shilling millioni tano kutoka kwa  Mwakilishi wa Jubilee Insurance Bi. Elieth kileo kwa ajili ya msaada kwa msadaa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
  nge1
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw Alex Nkenyenge akifafanua kuhusu maandalizi ya Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies itakayofanyika kesho.
  nge2
  Mwenyekiti wa Bunge Sports Club  Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga na Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies katika  Uwanja wa Taifa na kutangaza kuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe Kassim Majaliwa.
  nge3
  Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Mhe. William Ngeleja akionesha moja ya kikombe kwa waandishi wa Habari(hawapo pichani) kitakachotolewa kwa mshindi katika mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga na Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies katika  Uwanja wa Taifa.
  nge4
  Mwakilishi wa wasanii wa Bongo Movie Bw.William Mtitu akizungumza kuhusu maandalizi ya timu yao kabla ya mchezo wao wa kesho na wasanii wa Bongo Flava utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa kwa dhumuni la kuchangisha fedha kwaajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
  nge5
  Mwakilishi kutoka Mwananchi Communications LTD Bw. Francis Nanai akizungumzia mchango wao walioutoa wa kutoa taarifa kwa watanzania kuhusu hali ilivyo mkoani Kagera na kutoa nafasi kwa makampuni yatakayojotokeza kufanya harambee kuwasaidia waathirika wa tetemeko watatoa matangazo bure kwa ajili yao katika vyombo vyao vya habari.
  nge6
  Mwakilishi kutoka Shirika la Bima ya Afya Taifa NHIF Bw. Baraka Maduhu akitoa ufafanuzi kuhusu huduma za kiafya zitazotolewa kwa wachezaji na wananchi kwa ujumla kesho katika mchezo kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies.

  nge10
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo.
  nge11
  Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge Mhe. William Ngeleja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge wakiwa katika picha ya pamoja na wabunge, wasanii wa bongo movie na bongo flava, wawakilishi wa Mwananchi Communications Ltd, Jubilee Insurance,Shirika la Taifa la Bima ya Afya na Selcom Tanzania mara baada ya mkutano wa kuhamasisha wananchi kushiriki kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kupitia michezo.
  (Picha Zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.) 

older | 1 | .... | 982 | 983 | (Page 984) | 985 | 986 | .... | 1898 | newer