Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live

JUMUIAYA YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR YAISHUKURU TAASISI YA KUJITOLEA YA KUTOA HUDUMA KWA KUWAFADHILI MRADI WA KILIMO CHA MATUNDA NA MBOGA MBOGA.

$
0
0
MAIDA HAMZA/MCC   .
                    
Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar imeishukuru Taasisi ya kujitolea ya kutoa huduma (VSO)  kwa kuwawapatia  ufadhili wa mradi wa  kilimo cha matunda na mbogamboga .

 Mwenyekiti wa Jmumuiya hiyo Nd.Ali Omari Makame amesema Taasisi hiyo pia imewapatia  mabwanashamba kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wanaojishughulisha na kilimlo hicho kwa lengo la kujiongezea kipato.

Ndugu Makame  ameeleza hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari Makao makuu ya Umoja huo Wireles Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Amesema Umoja huo pia unaendesha programu ya kutoa taaluma  na mikopo ya fedha kwa wakulima wa mbogamboga na matunda  pamoja na wafanya biashara wadogowadogo wa maduka, mitumba, tungule, mkaa  ili kupata pesa ambazo zinaweza kuendeleza maisha yao ya kila siku

 Mwenyekiti wa Umoja wa watu wenye ulemavu ameongeza kuwa katika kuwasaidia vijana  walemavu ambao hawana   uwezo wa kujiendeleza katika  elimu ya juu wanawasidi vifaa na  fedha  ili kuhakikisha nao wanapata fursa hiyo kama wanayopata vijana wengine.

Ndugu Makame  ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa kuwapatia  madaktari wa  kushirikiana na maafisa wa  walemavu  vijijini   kuwatambua watoto  wenye  ulemavu na kuwapatia visaidizi.

 Ameongeza kuwa katika kuimarisha  Jumuia yao,  wameanzisha darasa la lugha za alama na  watu wote wanaopenda kushiriki  wanakaribishwa kujiunga  katika darasa hilo ili kuimarisha mawasiliano kati yao na watu wa kawaida.

Amelalamikia watu wenye ulemavu kukosa nafasi ya  kushirikishwa katika kamati za sheha na udiwani hali  inayopelekea kukosa utetezi wa  maslahi ya walemavu  katika ngazi za shehia na wadi.

Aidha amesema jumuia yao  imekuwa ikichukua hatua ya kusimamia kesi za udhalilishaji wa kijinsai kwa walemavu kwa kuandaa   taratibu  katika kutoa ushahihidi inapohitajika.

Ametoa wito kwa jamii  kuliona suala la walemavu  ni suala la wananchi na sio lao peke yao ama  taasis  zinazowasaidia  ili kujenga   jamii iliyobora   na kupunguza tofauti baina ya walemavu na wasio walemavu.

TSN Kudhamini Pambano la Kuchangia waathirika wa Tetemeko la Ardhi.

$
0
0
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kushoto ni Kapteni wa Timu ya Bongo Movie Jimmy Mafufu.
 Mwakilishi wa Timu ya Bongo Fleva, Kalapina (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, wakati makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy na Mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Movie Jimmy Mafufu, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kulia ni mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Fleva M2 the P, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akiwakabidhi vifaa vya michezo wawakilishi wa Bongo Movie na Bongo Fleva  kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.

Picha na Frank Shija, MAELEZO.


TSN Kudhamini Pambano la Kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi.

Na Daudi Manongi,MAELEZO


Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) imejitolea kudhamini pambano la kuchangia wahanga wa tetemeko la Ardhi Kagera litakalofanyika siku ya Jumapili saa tisa kamili kati ya Wasanii wa Bongo Movie na Bongo Fleva katika uwanja wa Taifa.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara wa kampuni hiyo Bw.Jahu Mohamed Kessy wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

“Sisi kama Tanzania Sisi Nyumbani(TSN) tumejitolea kudhamini pambano hili kwa kushirikiana na wasanii hawa kwa kuwa tumeguswa na janga hili na hivyo mbali na michango mbalimbali tukaona ni vyema tujitolee kuwapa Mipila na Jezi kwa wasanii hawa ili kuhamasisha uchangiaji huu ”Aliongeza Bw.Kessy.

Aidha Bwana Kessy alisema kuwa wao kama TSN wanaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika tasnia hizi mbili tofauti, kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji huu kwa pamoja.

Pia amewataka wananchi,mashirika na makampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa kagera waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo la Ardhi.

Kwa upande wake mwakilishi wa Bongo Movie Bw.Steve Nyerere amesema kwamba wao kama bongo movie wameguswa na jambo hili na ndio maana wamejitokeza kutumia vipaji vyao ili kile kitakachopatikana ili kiweze kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Kagera.

PPF YAWATAKA WASTAAFU KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UHAKIKI LINALOENDELEA NCHINI.

$
0
0

Meneja Kiongozi wa Pensheni na Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni PPF, John Mwalisu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki wa wanachama wastaafu wa mfuko huo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa PPF Bibi. Lulu Mengere.
Meneja Uhusiano wa Uhusiano wa PPF Lulu Mengere akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki wa wanachama wastaafu wa mfuko huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bi. Janeth Ezekiel na Meneja Kiongozi wa Pensheni na Huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo, John Mwalisu.
Waandishi wa habari wakimskiliza Meneja Uhusiano wa PPF Bibi. Lulu Mengere (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija, MAELEZO.
 
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

MFUKO wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) umewataka wanachama wastaafu wa mfuko huo PPF kujitokeza katika zoezi la uhakiki linaoendelea na kumalizika nchini kote tarehe 28 Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandsihi wa habari leo jijini Dar es salaam Meneja Kiongozi wa Shughuli za Pensheni na Huduma kwa Wanachama, John Mwalisu alisema uhakiki huo hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi za wanachama wanaolipwa pensheni kupitia mfuko huo.

Mwalisu alisema zoezi hilo la kuhakiki wa wastaafu lililoanza Septemba 12 hadi Septemba 23 mwaka huu katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar ni endelevu na linatarajia kuendelea mikoani kuanzia Septemba 26 hadi octoba 28 mwaka huu.

Alisema katika zoezi hilo kila mstaafu anatakiwa kwenda na nyaraka kamili za uanachama ikiwemo Kitambulisho cha mstaafu cha PPF, picha ndogo ya rangi, nakala ya kati ya kitambulisho cha Taifa au kadi ya mpiga kura, hati ya kusafiria au leseni ya udereva.

Aliongeza kuwa awamu ya pili ya zoezi hilo litahusisha mikoa ya kanda ya kati ambayo ni Morogoro, Dodoma na Singida kati ya tarehe 26 hadi 30 Septemba mwaka huu, wakati katika mikoa ya kanda ya Ziwa zoezi hilo litaanza Octoba 3 hadi octoba 7 ikihusisha mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera.

Katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini zoezi hilo la uhakiki wa wastaafu litaanza octoba 17 hadi octoba 21 mwaka huu na katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro zoezi hilo litaanza Octoba 24 hadi Octoba 28” alisema Mwalisu.

Aidha ,alisema kuwa zoezi la ukakiki wa wastaafu hao kwa mikoa ya ya Dar es salaam, Pwani na Zanzibar limemalizika Septemba 23 mwaka huu na kutoa wito kwa wanachama wastaafu katika mikoani inayofuata kuonyesha ushirikiano katika zoezi hilo la uhakiki.

Naye Meneja Uhusiano Mfuko huo, Lulu Mengele alisema kuwa katika kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi, PPF imeanzisha mfumo maalumu wa kuchangia (WOTE SCHEME) unaohusiha sekta rasmi na isiyo rasmi kwa lengo la kukidhi mahitaji na kutambua mchango wa wanachama katika uchumi wa nchi.

Aliongeza kuwa mfumo huo pia unatoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi kuweza kunufaika ili kuweza kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Akizungumza kuhusu mfuko wa Wote Scheme, Mengele alisema wanachama wa mfuko huo kuwa ni pamoja na wakulima, mama lishe na wajasiriamali wadogowadogo ambapo kiwango cha chini cha kuchangia kwa kila mwezi ni Tanzania shilingi 20,000.

Muhimbili, MUHAS, EMAT Waendesha Mafunzo ya Kuokoa Maisha ya Wagonjwa wa Dharura na Ajali Leo

$
0
0
 Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Otilia Gowelle akizindua Mkutano Mkuu wa kwanza wa wataalamu wa tiba ya dharura Tanzania ambao unafanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umelenga kutoa mafunzo kwa vitendo kwa washiriki mbalimbali kutoka katika sekta ya afya nchini. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Juma Mfinanga,  Mkurugenzi wa ABBOT Fund nchini, Natalia Lobue, Rais wa Chama cha Madaktari na Wataalamu wa Tiba ya Dharura Tanzania (EMAT), Dk Hendry Sawe, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi na Mkuu wa Kitivo cha Tiba, MUHAS, Profesa Sylvia Kaaya. 
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi leo katika mkutano unaoendelea katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Madaktari na Wataalamu wa Tiba ya Dharura Tanzania (EMAT), Dk Hendry Sawe akiwasilisha mada kwenye mkutano huo leo.

DIWANI WA CHADEMA ARUMERU MASHARIKI ASWEKWA RUMANDE KWA SAA 48,AACHIWA KWA DHAMANA

$
0
0

Katibu wa CHADEMA jimbo la Arumeru Mashariki Elisa Stephen Mungure (Kulia) akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Embaseny Gadieli Mwanda (kushoto) nje ya Mahakama ya Mwanzo ya Enaboishu jana mara baada ya kuwekwa rumande kwa saa 48 na mkuu wa wilaya ya Arumeru ambapo jana alifikishwa mahakamani na kupewa dhamana

Na Woinde Shizza,Arusha

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Wilaya ya Arumeru Mashariki kimelaani vikali kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexender Mnyiti kumuweka rumande Diwani wa Kata ya Embaseny Gadieli Mwanda kwa saa 48 na kudai kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya madaraka.

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru Elisa Stephen Mungure amesema kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji dhidi ya viongozi wa upinzani ambao wamekua wakikamatwa mara kwa mara na kuwekwa rumande . Mungure alisema kuwa mbinu hiyo imekua ikitumika kwa hila ili kudhoofisha na kuua upinzani hivyo chama chake kimejipanga kukabiliana na hila hizo za kisiasa. 

“Diwani wa Kata ya Embaseny alitakiwa kuripoti katika kituo cha polisi cha
Usariver septemba 20 mwaka huu ndipo alipokutana na Amri ya Mkuu wa Wilaya ya kuwekwa ndani kwa masaa 48 bila kuhojiwa ,jana alifikishwa mahakama ya Mwanzo ya Enaboishu na kutuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mradi wa Kuku Kukua ambao Diwani huyo siyo muhusika ,tunamshukuru Mungu amepata Dhamana” Alisema Mungure

Akizungumza baada ya kupata Dhamana katika mahakama hiyo Diwani huyo Gadiel Mwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Arumeru Mashariki alisema kuwa Mkuu wa Wilaya alifanya ziara katika kata yake na kuzungumza na Wananchi ,baadhi ya watu ambao wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM walimshutumu kuwa anahusika na mradi huo alipotaka kujitetea alinyimwa nafasi hiyo na kuamriwa kufika kituo cha polisi asubuhi na mapema ndipo alipokutwa na masaibu hayo.

Mwanda alisema kuwa misigano ya kisiasa inayotekea inalenga kuzorotesha
juhudi za maendeleo ambazo amekua akizifanya kwa kushirikiana na wananchi jambo ambalo litawaathiri wananchi wengi hivyo amewataka wananchi kuendelea na juhudi hizo ikiwemo ujenzi wa zahanati ya kisasa.

Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo Ester Swai na Agnes Elia wamesema kuwa kukamatwa kwa viongozi kila mara kunazua hali ya taharuki miongoni mwa wananchi hivyo wamezitaka mamlaka husika kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa.

PANAFRICAN ENERGY YATOA MSAADA KWA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu akimshukuru Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni ya PanAfriacan Energy Tanzania Limited Bwana Andrew baada ya kukabidhiwa msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 yasaruji kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu akizungumza jambo na uongozi wa kampuni ya PanAfriacan Energy Tanzania Limited baada ya kukabidhiwa msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 yasaruji kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu akimshukuru Patrick Rutabanzibwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Pan African Energy baada ya kukabidhiwa msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 yasaruji kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera

Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya PanAfrican Energy Tanzania imekabidhi msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 saruji kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Kagera. Msaada huo uliokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu ofisini kwake ni kutoa mkono wa pole kwa wana Kagera kwa maafa yaliyowakumba takribani siku kumi zilizopita. 

Akikabidhi msaada huo Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni ya PanAfriacan Energy Tanzania Limited Bwana Andrew Kashangaki alisema, “Kwa niaba ya Kampuni ya PanAfrican Energy tunatoa pole kwa watanzania wenzetu wana Kagera kutokana na janga lililowakumba ndugu zetu na kuwahakikishia tupo pamoja katika hili.Kwa uzalendo mkubwa tumeguswa na yaliyowapata wenzetu na hasa kupata uharibifu mkubwa wa mali na mbaya zaidi kupoteza uhai wa baadhi ya watanzania wenzetu pia kupata majeruhi. 

Hili ni janga letu sote kwa kuguswa na hili tumekabidhi mifuko 5000 ya saruji na mabati 1900 ambayo tunaamini yatasaidia kufanyia marekebisho baadhi za nyumba zilizoathiriwa na tetemeko. Kwa hiki kidogo tunaomba kiwe kama faraja kwenu na tunawahakikishia hatutaishia hapa tutaendelea kusaidia kadiri ya mahitaji ya wenzetu hasa katika elimu yaani kufanyia ukarabati baadhi za shule zilizoharibika vibaya. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PanAfrican Energy Patrick Rutabanzibwa aliushukuru uongozi wa mkoa wa kagera kwa namna wanavyozidi kujaribu kutatua changamoto wanazopitia waathirika wa tetemeko ardhi. Alielezea namna wanavyojitokeza kusaidia shughuli za kijamii, “Kampuni yetu inashughulika na utafutaji, uchimbaji, uendelezajii na usambazaji wa gesi asili ya Songo Songo.

Kampuni ilianza shughuli hizi mnamo Mwaka 2001 na uzalishaji ukaanza 2004. PanAfrican Energy (Tanzania) inafanya miradi ya maendeleo ya kiuchumi, kisheria na kimaadili, katika kutatua matatizo ya jamii zetu na kujitolea uwezo wetu, rasilimali na watu katika kujenga maisha bora ya baadaye kwa wote. Miradi ya PanAfrican Energy (Tanzania) itatathiminiwa na kukubaliwa katika misingi ya kudumu kwenye sekta ya elimu, afya na uwezeshwaji wa jamii. 

Tunaamini huu ni mwanzo wa kushirikiana na wewe. Tumeweza kutembelea sehemu mbali mbali na kuona shule zilizopata uharibifu mkubwa na tunaahidi kwamba tukirudi Dar es Salaam tutawasilisha ujumbe huu na kwamba bado msaada unahitajika kurudisha shule zetu kwenye hali ya kawaida.” 

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu aliishukuru Kampuni ya PanAfrican Energy kwa msaada wa vifaa vya ujenzi waliowapatia na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kusaidia. 

“Hii inadhihirisha ni jinsi gani watanzania tulivyo na umoja na upendo, kwa niaba ya wana Kagera na Serikali kwa ujumla natoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa msaada huu mkubwa militupatia wa vifaa vya ujenzi. Bado tunahitaji msaada zaidi kwani athari iliyotokea ni kubwa sana kuachilia vifo vya wenzetu 17 bado majengo mengi yameathirika vibaya kwani majengo 2072 yamebomoka kabisa, zaidi ya 40,000 yapo katika uharibifu hatarishi na 9000 yana mipasuko”. 

Msaada huo ulitolewa mara baada ya mkoa wa Kagera kupatwa na tetemeko la ardhi lililotokea takribani siku kumi zilizopita.

LOWASSA AISIFU SERIKALI URATIBU MAAFA KAGERA

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu alipomtembela leo ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari ya tetemeko la ardhi katika mkoa wake


Na Mwandishi Wetu-KAGERA.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.


Bw. Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari zilizotokana na tetemeko hilo.


“Napenda nikupongenze mkuu wa mkoa kwa namna ulivyokabili tukio hili, wala hatukuwa na mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwa hiyo jambo hili limempata mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.


Adha Mhe. Lowassa alisema kuwa suala hili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa hivyo watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.


Katika kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na serikali katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo.


“Tunashukuru watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema  Meja Generali Salum Kijuu.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MAFIA, AIPA SIKU 10 TAASISI YA HIFADHI YA BAHARI KULIPA DENI LA SH. MILIONI 100

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku 10 kwa Taasisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu kulipa deni la sh. milioni 100 inayodaiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mafia. 

Deni hilo linatokana na malimbikizo ya miaka mitatu ya maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na taasisi hiyo katika maeneo ya hifadhi ya bahari wilayani humo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo katika ukumbi Caltas akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi siku mbili. 

“Waandikieni barua na muitume leo hii kwa njia ya mtandao (email) kuwajulisha kuwa wanatakiwa kulipa deni hilo ndani ya siku 10. Hakikisheni wanalipa deni hili ili Halmashauri iweze kufanya kazi zake vizuri,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona Halmashauri hiyo ikinufaika kutokana na vyanzo vyake vya mapato, hivyo haitakuwa tayari kuona ikihangaika.

Mbali na agizo hilo, Waziri Mkuun amesema atafuatilia kuona wajibu wa taasisi hiyo na mipaka yao ikiwa ni pamoja na kujua mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.

Awali mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili wilaya hiyo ni kutolipwa kwa wakati fedha za maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na Taasisi ya Hifadhi ya Bahari.

Mkuu huyo wa wilaya ameiomba Serikali kuangalia upya majukumu ya taasisi hiyo na nafasi ya halmashauri katika kuendesha shughuli za uwekezaji pamoja na kupata mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, SEPTEMBA 23, 2016.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kwa ziara ya kikazi wilayani humo Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mafi2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Pwani baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia  kwa ziara ya kikazi Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
maf3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya Ijumaa kwenye Msikiti Mkuu wa Mafia akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Pwani Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
maf4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye Msikiti Mkuu wa Mafia bbada ya kushiriki  sala ya Ijumaa akiwa katika siku ya kwanza na ziara  ya mkoa wa Pwani Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
maf5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye Msikiti Mkuu wa Mafia bbada ya kushiriki  sala ya Ijumaa akiwa katika siku ya kwanza na ziara  ya mkoa wa Pwani Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


MAFUNZO YA MWONGOZO WA UWEKEZAJI WA UMMA MBEYA YAFUNGWA

$
0
0
Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma, Mhandisi Happiness Mgalula akifunga mafunzo ya Maafisa Mipango na Wachumi Kanda za Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika katika jijini Mbeya. Kushoto kwake ni Dkt. John Mduma, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kushoto kwake ni Dkt. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia klasta ya Uchumi Jumla. Mafunzo hayo yalijumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Songwe na Mbeya
uwe1
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Mwongozo wa Uwekezaji wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Sinene akichangia hoja katika mafunzo hayo yalifanyika jijini Mbeya
uwe2
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Mwongozo wa Uwekezaji wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Sinene akichangia hoja katika mafunzo hayo yalifanyika jijini Mbeya
uwe3
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mwongozo wa Uwekezaji wa Umma wakifurahia jambo wakati wa mafunzo hayo
uwe6
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakipiga makofu wakati wa kufunga mafunzo hayo

WANANCHI KYERWA WAHIMIZWA KULIMA MAZO YANAYOKOMAA KWA MUDA MFUPI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akitembelea eneo la kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa kujionea ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulivyoathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera na kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista akiwa ziarani wilaya ya Kyerwa na kujionea mazo la viazi ambalo pia linaweza kulimwa wilayani humo.

(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera).

………………………………………………………………….

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera

Ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulioathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera umemlazimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.

Athari hiyo ya ukame imemlazimu Waziri Mhagama kuwataka wananchi wa wilaya hiyo na mkoa wa Kagera kwa ujumla w0aanze kulima mazao mengine yanayokomaa kwa muda mfupi yaweze kuwapunguzia adha ya upungufu wa chakula unaotokana na kutegemea zao la ndizi pekee.

Akiwa katika kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa Waziri Mhagama aliongea na wananchi wa kata hiyo ambapo alisema “Mabadiliko ya tabia nchi ni makubwa, msiendelee kutegemea zao moja tu la chakula la ndizi, ni lazima mkubali sasa tuende kwenye mazao mengine ya chakula, limeni mihogo, limeni mahindi. Nendeni kwenye mazao yanayokomaa kwa muda mfupi, vinginevyo tukisema kila kila mwaka tuendelee kutegemea kahawa na ndizi kwa hali ya hewa ilivyo sasa tutaendelea kukosa chakula”.

Waziri Mhagama aliyataja mazao hayo kuwa yanaweza kukomaa kwa muda mfupi kuanzia miezi mitatu ndiyo yanaweza kuwa mkombozi wa katika kukabiliana na upungufu wa chakula na kuwahakikishia wananchi chakula cha kutosha hatua ambayo itawafanya waendelee na shughuli zenye tija kwa maendeleo yao.

Mkulima wa kata hiyo Shakiru Issa anathibitisha kuwa upo uwezekano wa kulima mazao mengine zaidi ya ndizi na kahawa ambayo yanamuongezea kipato ambapo yeye analima pia zao la viazi mviringo kwa ajili ya chakula pamoja na kuuza hatua inayomsaidia kumuongezea kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Waziri Mhagama amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha tabia ya kuchoma mapori moto mara moja kwa kuwa tabia hiyo huhatarisha maisha ya watu, kupoteza mazao shambani,miti na hifadhi ya misitu ambayo ndiyo kivutio kikuu cha mvua.

Aidha, ziara hiyo wa Waziri Mhagama imekuwa faraja kwa wananchi wa Kata ya Itera ambapo amemwagiza Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya aende kufanya tahmini ya hali ukame ilivyo athiri wilaya hiyo na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo.

Katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha wilayani Kyerwa, Waziri Mhagama ametoa wito na kumuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Mstaafu Shaban Lissu pamoja kulima zao la ndizi, aanza haraka kampeni ya kuwahamasisha wananchi hao kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ambayo yataweza kuwapatia chakula cha kutosha kwa mahitaji yao ya kila siku.

AMOS AND JOSH RELEASE "KUPE" OFFICIAL VIDEO FT BEN POL, APIO & MOHAMMED AMIN.

MH. SUBIRA MNGALU AKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA AJILI YA UJENZI WA VYOO CHUO CHA MAENDELEO KISARAWE.

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikabidhi mifuko ya saruji na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vyoo kwa Bw.Herry Mjengelaungu Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Kisarawe katika hafla iliyofanyika chuoni hapo leo kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe Bw. Mtera Mwampamba na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Happiness Saneda.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akizungumza na wakufunzi na wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Kisarawe kabla ya kukabidhi vifaa katika chuo hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Happiness Saneda.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akipiga picha na mkuu wa chuo hicho pamoja na wakufunzi mara baada ya makabidhiano.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani kupitia CCM Mh. Subira Mngalu akizungumza na Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Happiness Sanneda wakati wakikagua maeneo ya chuo hicho kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Bw. Herry Mjengelaungu.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikagua chumba cha kompyuta.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo angalia.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikagua mabweni ya chuo hicho kutoka kwa mkuu wa chuo Bw. Herry Mjengelaungu. 
 
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu(CCM) ametoa msaada wa vifaa za ujenzi wa vyenye thamani ya sh. milioni moja kwa Chuo
Maendeleo ya Wananchi(FDC) Kata ya Kazimzumbwi, Kisarawe mkoani
Pwani.

Subira alimkabidhi msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni
saruji,mchanga,mbao, matofali, nondo na kokoto kwa ajili ya kusaidia
ujenzi wa choo cha wavulana baada ya cha awali kubomoka na wanafunzi
kulazimika kutumia choo kimoja cha wasichana.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo jana, Subira alisema
anaamini ujenzi wa choo hicho utakamilika mapema kwa kuwa unafanywa na nguvu kazi ya vijana wenyewe chini ya usimamizi wa wakufunzi wao.

Mbunge huyo alisema kwamba anatambua kwamba ana wajibu wa kuhakikisha afya za vijana wanaosoma chuoni hapo zinakuwa salama hivyo ametoa kama kiongozi na mzazi wa watoto hao.

Alisema aliguswa baada ya kutembelea chuo hicho mwezi mmoja uliopita
na kuona changamoto nyingi zinazowakabili wanafunzi na watumishi wa
chuo hicho ambapo alihidi kusaidia na kuhamasisha viongozi wengine
wafike chuoni hapo.

Subira alisema vyuo hivyo na vyuo vya ufundi vilivyopo chini ya VETA
ni muhimu hususan wakati huu ambao nchi inaelekea kwenye uchumi wa
viwanda,vyuo hivyo ndivyo vitakavyozalisha wataalamu watakaofanya kazi
kwenye viwanda.

Alisema vyuo hivyo ambavyo kwa Mkoa wa Pwani vipo Kibaha, Kisarawe na
Ikwiriri wilayani Rufiji, miundombinu yake ni chakavu na wanakabiliwa
na changamoto nyingi hivyo wakati serikali inaangalia namna, viongozi
na wadau wanapaswa kusaidia.

Mbunge huyo alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happines Senada na uongozi wa halmashauri kuwatumia vijana wa chuo hicho kuwapa kazi
hususan za ujenzi wa vyoo vya shule za msingi ili kusadia vyuo hivyo
na kwamba sheria ya manunuzi imeruhusu kutumia makundi maalumu ya
vijana na wanawake.

Awali akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho Mkuu wa
Wilaya, Happines alisema chuo hicho kina umuhimu mkubwa hivyo
atahakikisha changamoto zinazowakabili zinatatuliwa kwa kushirikiana
na wadau.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Heri Mjengelaungu, alisema chuo
hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu chakavu,
tatizo la maji, umeme, vifaa vua kufundishia kwa vitendo , haina
magari.

Alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wake wa vifaa vya ujenzi wa choo
hicho kwa kuwa hali ni mbaya hivyo watahakikisha kwa kushirikiana na
wanafunzi na wakufunzi choo hicho kinakamilika mapema zaidi kwa kuwa
shimo limeshachimbwa.

KILELE CHA SHEREHE ZA ELIMU BILA MALIPO ZANZIBAR 2

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimvalisha medali Hassan Aswahi kutoka skuli ya Paje akiwa mshindi wa tatu katika mbio maalum za Vijiti(relay) mita 100×4 wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila malipo leo ,katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]23/09/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi Kikombe Nd,Abdalla Makame Makame Afisa Elimu na Mfunzo ya Amali Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa washindi kiujumla wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila malipo leo ,katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,(kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma,[Picha na Ikulu.]23/09/2016.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila malipo leo ,katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja, [Picha na Ikulu.]23/09/2016.

Waaalimu na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila malipo leo ,katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja
 
Watoto wa Maandalizi wakiwa katika mashindano mbio za Riadha wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila malipo katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Watoto wa Maandalizi wakiwa katika mashindano mbio za magunia wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila malipo katika Uwanja wa Amaan Studium leo,[Picha na Ikulu.]23/09/2016.

Watoto wakicheza Ngoma aina ya Bomu wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila malipo katika Uwanja wa Amaan Studium leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]23/09/2016.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa slamu zake na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuzungumza na Walimu pamoja na Wanafunzi katika maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu Bila malipo, sherehe zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]23/09/2016.
………………

NA TAKDIR ALI- MAELEZO ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuifanyia ukaguzi mitaala ya Skuli za binafsi ili kwenda sambamba na mitaala ya Skuli za Serikali.

Hayo ameyasema leo huko Uwanja wa Amani mjini Zanzibar wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya miaka 52 ya elimu bila malipo.

Amesma mitala ya skuli za binafsi haiendi sambamba na ile ya serikali kitu ambacho hakipaswi ,hivyo amesema ikohaja ya Wizara ya elimu namafunzo ya amali Zanzibar kushirikiana katika kuangalia mitaala miataala hiyo ya ufundishaji ili iende sambamba na skuli za serikali.

Aidha amesema mashirikiano ya pamoja yapande hizo mbili yatapelekea wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya majaribio na ile ya mwisho wa mwaka.

Dkt. Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vyema katika kuhakikisha kwamba inakabiliana na changamoto mbalmbali zinazoikabili sekta ya elimu hapa Zanzibar ili kuhakikisha inafikia dhana ya Raisi wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alioitangaza Elimu bila malipo mwaka 1964.

Akiwazungumzia Wazazi juu ya suala zima laelimu kumpatia mtotoDkt. Ali Mohamed Shein amesema suala la elimu kwa mtoto hali mlazimu mwalimu pekeyake bali ni jambo la wote ambalo linahitaji ushirikiano kati ya mwalimu wazazi na wanafunzi.

Amesema wasiachiwe walimu pekeyao kufundisha na kuwaongoza bali wae na ushirikiano wa pamoja.

Pamoja na hayo Dkt.Ali Mohamed Shein alisema kabla ya Mapinduzi ya Mwaka1964 ilimu Zanzibar ilikuwa ikitolewa kwa misingi ya ubaguzi kituambacho kiliwafanya wonyonge kuikosa hakihiyo ya elimu kitu ambacho kwa sasa Zanzibar imepiga hatua kubwa mbele kwani upatikanaji wa elimu ni wakila mmoja ambae kafikia umri wa kwenda skuli.

Ameseama haki hiyo sasa imefikiwa kukua nakwasaa kua na vyuo vikuu vitatu kwa ujumla wake mbapo kwa kiasi ya miaka 20 iliopita Zanzibar haikuwa na hata chuo kikuu kimoja na kupelekea wanaotaka kusoma kuenda nje ya Tanzania.

TAZAMA VIDEO MPYA KUTOKA THE HURICANE SOUNDS-UPO VIZURI

TEA YASHIRIKI MAONESHO KATIKA MKUTANO MKUU WA ALAT

$
0
0
 Kaimu Meneja Miradi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuka akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita Simon Berege katika maonesho yanayofanyika mkoani humo katika Mkutano Mkuu wa ALAT.
Ofisa Mawasiliano TEA, Sophia Asad akitoa maelezo katika maonesho wakati wa Mkutano Mkuu wa ALAT.
  Kaimu Meneja Miradi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuka akitoa ufafanuzi baadhi ya watu waliotembelea banda la TEA katika maonesho yanayofanyika katika Mkutano Mkuu wa ALAT mjini Musoma. 
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Sylvia Lupembe akimweleza jambo Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene kwenye maonesho yaliyofanyika katika  Mkutano Mkuu wa ALAT mjini Musoma.

DC MPWAPWA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI (FDC)-CHISALU

$
0
0
Na Mathias Canal, Dodoma

Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC)-CHISALU amekalia kuti kavu mara baada ya kubainika kuwa ameruhusu udahili wa wanafunzi wanaosoma fani ya utaalamu wa Kilimo na Mifugo ilihali chuo hicho ni maalumu kwa ajili ya mafunzo ya utaalamu wa Maendeleo ya jamii (Community Development).

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu huyo kutokana na kupokea malalamiko ya baadhi ya wanafunzi chuoni hapo ambapo malalaniko yao yamekuwa na hoja za msingi zilizopelekea kuibuka kwa kadhia mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho.Katika kutaka kubaini udhaifu unaohusu utendaji wa uongozi wa chuo hicho Dc Shekimweri alisikiliza hoja za wanafunzi chuoni hapo ambapo walitaka kujua sababu zinazopelekea wao kufanya mtihani unaoandaliwa na Chuo cha Ufundi VETA ilihali mtaala wao sio wa VETA.

Mbali na kadhia hiyo wanafunzi hao wamehoji pia fani ya kilimo wanafunzi hao wanayosoma ya Kilimo na Mifugo ambayo haitakiwi kwa mujibu wa taratibu pia haina namba ya mtihani (Exam Code) hivyo ni kwa kiasi gani wanafunzi hao watahakikishiwa ajira kama maafisa Mifugo pindi wamalizapo masomo yao.

Dc Shekimweri alizuru Chuoni hapo kwa lengo la kutaka kujua hatma ya wanafunzi wa chuo hicho kufungwa pasina sababu ndipo alipobaini uongo uliotumiwa na Mkuu wa Chuo hicho kwa kudai kuwa chuo kimefungwa kwa sababu ya kujiandaa na mitihani ambapo hata hivyo mtihani huo unataraji kufanyika Oktoba 10, 2016.

Mkuu wa chuo hicho alieleza kuwa chuo hicho kitafungwa hadi Tarehe 9/10/2016 siku moja kabla ya kufanyika kwa mitihani ambapo janja hiyo ilibainiwa na Mkuu wa Chuo kwa kudanganywa ratiba ya mtihani huo ambayo inaonyesha kuwa tarehe 26/09/2016 ndipo ambapo mtihani huo unataraji kuanza.

Hata hivyo Mkuu huyo wa chuo hicho amefunga chuo hicho pasina kushirikisha Bodi ya Chuo ambapo pia alihoji sababu za kudanganywa kufungwa chuo hicho bila maamuzi ya kusitisha kufanyika kwa mitihani ambapo ratiba yake imekwisha tolewa jambo ambalo lilimuacha mdomo wazi Mkuu huyo wa Chuo hicho.

Kutokana na kadhia hizo Dc Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu wa chuo hicho kwa kutumia uongo wakati wa kujitetea na kushindwa kitekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo kutoitisha vikao vya Bodi, Kutosikiliza kero za wanafunzi hata alipojulishwa kwa maandishi na wanafunzi hao, kufunga chuo kwa dharula ilihali tatiba ya mtihani inaendelea na kuwashauri vibaya wanafunzi kuhusu hatima yao kutokana na mkanganyiko wa mtaala.

Dc Shekimweri alisema kuwa serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inahubiri zaidi uwajibikaji hivyo maamuzi hayo yanatuma salamu ili mamlaka ya uteuzi ifuatilie na kushughulikia tuhuma dhidi yake na kuchukua stahiki za kisheria.

Mkuu huyo wa Wilaya amesitisha Bodi ya chuo na kumtaka mwenye mamlaka nanuteuzi wa Bodi aivunje Bodi hiyo kwa kushindwa kukutana hata mara moja tangu bodi hiyo ilipoanzishwa Mwaka 2013hivyo kushindwa kitafsiri na kusimamia Dira kwenye mpango mkakati (Strategic Plan) pia kutokuwa na kalenda ya mwaka wa taaluma.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya pia alihoji pasina kupatiwa majibu kuhusu uidhinishwaji wa mpango wa bajeti wa chuo kuhusu anayeufanya ilihali Bodi haikutani kwa ajili ya vikao.

Dc Shekimweri alienda mbali zaidi kwa kutaka kujua vipi vipaombele vya chuo, mabadilko na mitaala, mafanikio na changamoto za chuo vinajadiliwa na kufikiwa maamuzi na watu gani iwapo Bodi haikutani kujadili.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpwapwa alisema Changamoto za mitaala, Udahili na mtihani pamoja na vyeti vya kuhitimu litafanyiwa kazi kwenye Mamlaka husika (VETA) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri Mhagama atembelea taasisi za elimu Bukoba mjini.

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akimueleza Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda Renatusi Nkwande (wa pili kushoto) namna ya kutumia jengo la kanisa lililoathiriwa na tetemeko la ardhi lililopo ndani ya shule ya sekondari Ihungo. wa pili kulia ni Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama na Mhadhiri wa Seminari Kuu ya Ntungamo Padre Benedict Bigirwamungu (wa kwanza kulia).

mhg9
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro katika eneo la shule ya msingi Mugeza Mseto iliyopo Manispaa ya Bukoba wakati wa ziara ya kujionea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na tetemekola ardhi.

mhg6
Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda Renatusi Nkwande (wa pili kushoto) akionesha Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama (wa pili kulia) maeneo ya kanisa lililopo ndani ya shule ya sekondari Ihungo  lililoharibika kwa athari za tetemeko la ardhi. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya na Mhadhiri wa Seminari Kuu ya Ntungamo Padre Benedict Bigirwamungu (wa kwanza kulia).
mhg7
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiongea na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya Elimu Sekondari Mwl. Rubaiyuka (kulia) leo mjini Bukoba mara baada ya kutembelea ghala la vifaa vinavyokusanywa kabla ya kugawiwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya.
mhg8
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro katika eneo la shule ya msingi Mugeza Mseto iliyopo Manispaa ya Bukoba wakati wa ziara ya kujionea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na tetemekola ardhi.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)
mhg1
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mugeza Viziwi iliyopo manispaa ya Bukoba alipowatembelea leo shuleni hapo.
mhg2
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mugeza Mseto iliyopo manispaa ya Bukoba alipowatembelea leo shuleni hapo.
mhg3
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akisalimiana na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya msingi Mugeza Mseto iliyopo Manispaa ya Bukoba Joseph Rubago.
mhg4
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akieleza Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda Renatusi Nkwande (wa pili kushoto) namna ya kutumia jengo la kanisa lililoathiriwa na tetemeko la ardhi lililopo ndani ya shule ya sekondari Ihungo. wa pili kulia ni Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama na Mhadhiri wa Seminari Kuu ya Ntungamo Padre Benedict Bigirwamungu (wa kwanza kulia).

(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)

KANUSHO: PROFESA MUHONGO KUCHANGISHA SHILINGI 40,000 KWA AJILI YA TETEMEKO KAGERA

$
0
0

Gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Septemba, 2016 katika ukurasa wake wa Tano imeandikwa habari yenye kichwa cha habari “Harambee ya Profesa Muhongo yakusanya Sh 40,000 Bukoba”.

Mwandishi wa Habari hiyo ameandika kuwa ziara aliyoifanya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika Kata ya Hamugembe, Bukoba wakati akikagua miundombinu ya umeme, iligeuka kuwa harambee baada ya waathirika wa tetemeko la ardhi kudai msaada wa chakula na mahema.

Tunapenda kuuarifu Umma wa Watanzania kuwa, siyo kweli kwamba Profesa Muhongo aliitisha harambee ya kuchangia maafa hayo kama ilivyoandikwa na Mwandishi ambaye kwa sababu zake binafsi aliamua kupindisha ukweli na kueleza kuwa, “ilimlazimu Profesa Muhongo kuitisha mchango wa fedha kutoka kwa maofisa aliokuwa ameambatana nao na kufanikiwa kupata shilingi 40,000 na kuwakabidhi wakazi hao”.

Ikumbukwe kuwa Waziri wa Nishati na Madini alikuwa mkoani Kagera kukagua shughuli za kiutafiti zinazofanywa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi tarehe 10 Septemba, 2016 na kusababisha athari mbalimbali ikiwemo kwa miundombinu ya umeme.

Hivyo, taarifa kuwa Profesa Muhongo aliitisha harambee ya kuchangisha fedha za kusaidia waathirika wa maafa siyo sahihi kwani Profesa Muhongo hakuomba wala kuagiza Maofisa alioambatana nao kuchangia fedha kama ambavyo mwandishi anataka kuwaaminisha wananchi.

Akiwa katika kata ya Hamugembe mkoani humo ambapo alikwenda kukagua nyumba ambazo zimekatiwa huduma ya umeme kwa sababu ya kuathiriwa na tetemeko hilo, baadhi ya wananchi walidai kuwa shida yao ni chakula na malazi, na mmoja wa wananchi alisema kuwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kagera aliyeambatana na Profesa Muhongo, alishafika kata hiyo na kuwasaidia kiasi cha fedha.

Hata hivyo, Profesa Muhongo aliwaeleza wananchi hao kuwa, yeye alikwenda hapo kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kitaalam anayoyasimamia na kwamba kilio chao kuhusu kucheleweshewa huduma atakifikisha kwenye Kamati inayoshughulikia Maafa aliyokutana nayo tarehe 22 Septemba, 2016.

Baada ya wananchi kumtaja Meneja wa TANESCO wa Mkoa Kagera aliyewahi kuwasaidia wananchi hao fedha kutokana na tetemeko hilo, Meneja huyo aliamua kuongeza kiasi cha Fedha na kumpa mmoja wa wananchi hao, tofauti na ilivyoandikwa kwenye gazeti kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye aliyekabidhi pesa kwa wananchi.

Tunawaasa waandishi wa habari kuzingatia ukweli na usahihi katika uandishi wa habari ili kupeleka habari sahihi kwa wananchi.

Imetolewa na;

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

23 SEPTEMBA, 2016

CDF TROPHY YAANZA KWA KASI LUGALO GOLF CLUB

$
0
0
Mwenyekiti wa Klabu ya golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo (Katikati) akiangalia mazoezi ya wachezaji wa Klabu hiyo wanaotaraji kushuka Uwanjani kuwania CDF Trophy ( Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akikata utepe kuzindua Daraja la Kiwanja namba Tisa cha Golf Lugalo ikiwa ni sehemu ya kuboresha uwanja huo na kuwa na sifa zaidi kwa mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kimataifa (Picha na Luteni Selemani Semunyu).

……………………………………………………………………
SelemaniSemunyu JWTZ
Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa Mchezo wa Golf CDF Troph imeanza kwa Michezo ya awali ambapo Wapiga mikwaju wa kulipwa wamechuana vikali huku Geofrey Reverian na Klabu Lugalo na Farai Chitengwa wa Zimbambwe wakilazimika kurudia mchezo baada ya kufungana. 

Katika mashindano hayo yanayofanyika katika Uwanja wa Lugalo Golf Club Jijini Dar es salaam wamefungana mikwaju ya jumla (gross) 72 kwa kila mmoja na kulazimika kutakiwa kurudia mchezo kwa kucheza viwanja vitatu hali itakayoamua nani kuibuka mshindi katika kundi la wapiga mikwaju wa kulipwa. 

Katika nafasi ya tatu ya Wapiga Mikwaju hao wa kulipwa imechukuliwa na Salim Mwenyenza aliepata mikwaju ya Jumla 74 ikiwa ni kati ya wachezaji wa kulipwa 20 walioshiriki katika kinyanganyiro hicho ambacho mshindi atajulikana jumamosi Septemba 23 mwaka huu. 

Katika hatua Nyingine wacheza Golf wa kundi la Wachezaji Wasaidizi (Carde) 30 walipambana kupata mbabe wa kundi hilo ambapo Richard Mtweve aliibuka na ushindi kwa kupata Net 69 baada kupigaMikwaju ya Jumla 76 huku akicheza kwa kiwango cha Saba. 

Nafasi ya pili imechukuliwa na Rasuri Shaban baada ya kupata Net 70 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 79 huku kiwango cha Uchezaji kikiwa ni Tisa na Mwanamke pekee kwa kundi hilo Rose Nyenza kushika Nafasi ya tatu baada ya kupata net ya 87 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 111 na kiwango cha Uchezaji kikiwa ni 24. 

Michezo hiyo ya Kombe la Mkuu wa majeshi ya Ulinzi CDF Trophy yanatarajiwa kuendelea na kufikia tamati Jumamosi Septemba 24 katika Uwanja wa Golf wa Lugalo ambapo wachezi wa makundi matatu watachuana. Makundi hayo ni Senior,Junior, Ladies na Daraja la A Daraja B na daraja C ambapo mbapo pia mshindi wa Jumla atapatikana kutoka katika Makundi hayo. 

Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo ya Kombe la Mkuu wa majeshi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda.

Serikali kushirikiana na Korea ya Kusini kuendeleza sekta za Habari ,Michezo na tasnia ya filamu.

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea zawadi ya jezi maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee kutoka Korea ya Kusini, jezi hiyo ni zawadi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kutoka kwa klabu hiyo Septemba 23,2016 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia zawadi ya kitabu aliyoipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa TCN kutoka Korea ya Kusini Bw. Soon Young-Soon Septemba 23,2016 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka klabu ya ya Soka ya Seongnam na kampuni ya TCN kutoka Korea ya Kusini leo Spetemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na ujumbe kutoka Korea ya Kusini ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na Utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na ujumbe kutoka Korea ya Kusini ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na Utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016.
Katibu Mkuu Wizara wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa maelezo kuhusu sekta zilizopo katika Wizara hiyo kwa ujumbe kutoka Korea ya Kusini katika kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bi Suzana Mungy akitoa maelezo ya utendaji wa Shirika hilo na fursa zilizopo kwa wawekezaji kuwekeza katika sekta ya hiyo kwa ujumbe kutoka Korea ya Kusini katika kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016.
Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee kutoka Korea ya Kusini akimueleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na ujumbe wa Wizara(hawapo pichani) kuhusu mpango wa klabu yake kuwekeza katika soka la vijana kwa kuanzisha Shule ya Michezo nchini katika kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Korea ya Kusini ukimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam.

Ujumbe kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ukimsikiliza mmoja wa viongozi wa ujumbe kutoka Korea ya Kusini Bw. Soon Young-Soon (Hayupo Pichani) katika kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

………………………………………………………………..

Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Dar es Salaam, Tanzania

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kutoka Korea ya Kusini wamekubaliana kushirikiana kuendeleza sekta za Habari, Michezo na filamu kwa kuwekeza katika miundombinu na wataalamu.

Pande hizo mbili zimekubaliana kushirikiana katika sekta hizo katika kikao kilichojumuisha ujumbe kutoka Kampuni ya TCN na Klabu ya Soka ya Seongam kutoka Korea Kusini na ujumbe kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amesema kuwa kuja kwa ujumbe huo kutoka Korea ya Kusini ni fursa nzuri kwa Tanzania kuendeleza sekta za Habari, Michezo na Filamu kupitia wadau mbalimbali na wawekezaji kutoka nje ya nchi ambapo Serikali ipo tayari kushirikiana nao katika kuleta ufanisi na maendeleo katika sekta hizo.

“Ni matumaini yangu kuwa mazungumzo haya yataleta matunda kwani tayari tumeshazungumza nao kuhusu fursa zilizopo na kilichobaki ni wao kutuandikia rasmi ili tuanze sasa mchakato na matunda yataanza kuonekana hivi karibuni” Alisema Nnauye.

Aidha Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee kutoka Korea ya Kusini amesema klabu yake ipo tayari kuwekeza katika shule ya michezo kwa vijana ili kuongeza kasi ya maendeleo ya soka kwa vijana.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCN kutoka Korea ya Kusini Bw. Soon Young-Soon alisisitiza kuwa kampuni yake imejiandaa kuja Tanzania kuwekeza katika utengenezaji wa Filamu kwa kuleta wataalamu na kutengeneza miundombinu ya kisasa katika utengenezaji wa filamu bora na utengenezaji wa vipindi mbalimbali nchini.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Suzana Mungy ameushukuru ujumbe kutoka Korea ya Kusini na kuahidi kuwapa ushirikiano wataalamu kutoka Korea ya Kusini na kuwakaribisha kuwekeza katika sekta ya Habari hasa utengenezaji wa vipindi bora.

Korea ya Kusini ni moja ya nchi rafiki wa Tanzania na kwa miaka mingi wamekuwa wakishirikiana katika sekta mbalimbali zikiwemo Habari, Michezo Utamaduni na Sanaa kwa ujumla.
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live




Latest Images