Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

TUMEDHAMIRIA KUWASAJILI WATOTO WOTE NCHINI – WAZIRI MWAKYEMBE

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua mpango huo kwa ajili ya mikoa ya Iringa na Njombe katika viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa
Asante kwa ushirikiano

……………………………………………………

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasajili watoto wote nchini wenye umri chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.

Dhamira hiyo ya Serikali inalengo la kuiondoa nchi katika takwimu zinazoonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho barani Afrika ambazo watoto hawana vyeti vya kuzaliwa.

Dkt Mwakyembe amesema hayo mjini iringa alipokuwa akizindua kampeni ya uandikishaji watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Iringa na Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.

Dkt Mwakyembe ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kuwa miongoni mwa nchi ambazo watoto wake hawajasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa na kusema kuwa ndio maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikaamua kuendesha kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano.

Amesema serikali imedhamiria kuiondoa Tanzania katika hali hiyo kwakuwa sio sahihi kwa nchi kuwa katika nafasi hiyo sawa na Somalia

‘Hali hii sio sahihi, Tanzania haistahili kuwepo katika kundi hilo tumedhamiria kuiondoa nchi huko, tunataka Tanzania iwe juu ktk usajili wa watoto kama ilivyo juu kwa chanjo mbalimbali kwa watoto wetu’ alisema.

Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitano wanasajiliwa na kuwa ma vyeti vya kuzaliwa unaendeshwa kupitia Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi RITA chini ya ufadhili wa UNICEF.

BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA RAIS LAKUTANA LEO IKULU

$
0
0
Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo (wa nne kutoka kulia) akiongoza kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
iku2
Katibu Msaidizi Tume ya Maadili (Kanda ya Kusini) Be. Muhuwa R. Kapangawazi akitoa mada kuhusu Maadili ya Utumishi wa Umma na Tamko la Ahadi ya Uadilifu wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
iku3
Kaimu Mshauri wa Kitaalamu Ofisi ya ushauri wa Mafuta na Gesi ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Emma Msaky, akitoa mada kuhusu utendaji wa ofisi yake wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
iku4
Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo (wa nne kutoka kulia) na viongozi wengine pamoja na wajumbe wakipata picha ya pamoja baada ya  kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
PICHA NA IKULU

MTAA WA MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM WAANZISHA TOVUTI YAKE KWA AJILI YA MAENDELEO

$
0
0
 Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence Sakafu (katikati), akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni, aliyekuwa mgeni rasmi, kuashiria uzinduzi rasmi wa tovuti hiyo. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta, Mwenyekiti wa mtaa huo, Kimweri Mhita, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Masaki, Richard Mwakyulu na Mjumbe wa Kamati ya Mtaa huo, Rose Mkisi.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita (kulia), akizungumza katika na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya mtaa huo iliyofanyika Hoteli ya Best Western Plus Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta. 
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita, akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya tovuti hiyo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea kabla ya uzinduzi huo.
 Wajumbe wa kamati ya mtaa huo wakishiriki kwenye uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo,  Peter Mkongereze akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
 Mmoja wa waendeshaji wa tovuti hiyo, Benjamin Chaula (kulia), akielezea jinsi itakavyokuwa ikifanya kazi.Kushoto ni Norbert Baranyikwa.
 Makofi yakipigwa baada ya uzinduzi wa tovuti hiyo.
Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence Sakafu (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.


Na Dotto Mwaibale

SERIKALI ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam imezindua tovuti yake ili kurahisisha mawasiliano na shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tovuti hiyo Dar es Salaam leo asubuhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Masaki, Kimweri Mhita alisema tovuti hiyo imeanzishwa kwa lengo la  kuwasiliana na kuwashirikisha katika shughuli za maendeleo raia wa kigeni wanaoishi katika mtaa huo.

"Kutokana na jiografia ya eneo letu kulikuwa na changamoto kuwa ya kuwashirikisha wenzetu katika masuala mbalimbali kutokana na kutokuwa na mawasiliano tukaona tuanzishe tovuti yetu itakayosaidia kuondoa changamoto hiyo" alisema Mhita.

Alisema kupitia tovuti hiyo itasaidia kuwatambua wafanyabiashara waliopo katika mtaa huo ambao wameanza kujisajili pamoja na wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Tarafa wa Kata ya Magomeni, Fullgence Sakafu alisema kuanzishwa kwa tovuti hiyo katika wilaya hoyo wilaya hiyo mtaa huo umeonesha njia hivyo akaomba mitaa mingine kuiga mfano huo.


Alisema tovuti hiyo itasaidia kuweka wazi mipango ya maendeleo katika mtaa huo pamoja na kuhimizana kwenye kampeni ya kufanya usafi inayoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuwa.

TANZIA

WILAYA YA KASULU WABUNI MKAKATI WA KUDHIBITI AJIRA ZA WATOTO.

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col Martin Mkisi, akifungua Kikao kazi cha Kudhibiti Utumikishwaji wa watoto.

Col Mkisi, akishiriki ktk kikao kazi na wadau wengine.

Mkuu wa Wilaya Col Mkisi ktk picha ya pamoja na washiriki ktk kikao kazi cha Kudhibiti Utumikishwaji wa Watoto. 

*****************
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Col Martin Mkisi amefungua na kushiriki katika kikao kazi cha kubuni mikakati na usimamizi wa utekelezaji wa sheria za kudhibiti tatizo sugu wilayani hapa la utumikishwaji wa watoto.


Mpango huo umeshirikisha watekelezaji wa sheria Wilayani( Law enforcers) kama vile: watendaji ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara, Mahakimu, polisi,Usalama na Maafisa Magereza.


Mpango huo unaofadhiriwa na WEKEZA chini ufadhiri wa USAID,pamoja na mambo mengine, unalenga katika kupinga utumikishwaji wa watoto, ajira za watoto, utoroshaji wa watoto kwenda kufanya kazi hatarishi na mimba za utotoni, katika mikoa ya Tanga na Kigoma.


Aidha,Washiriki ktk mpango huo, wameondoka na azimio la kwenda kukomesha tatizo hili sugu hasa ktk kata za Kagerankanda, Heru -Ushingo, Kitagata na Nyamidaho Wilayani Kasulu.

Mkurugenzi wa Afrika akutana na Mabalozi wa Afrika nchini kuzungumzia ushirikiano

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo (kushoto) akizungumza katika kikao na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Afrika hapa nchini. Mazungumzo yao yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na nchi zao. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Slipway iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba, 2016
Sehemu ya Mabalozi kutoka nchi za Afrika wakia kwenye Mkutano wao na Balozi Shelukindo. Kutoka kulia ni Balozi wa Uganda hapa nchini, Mhe. Doroth Samali Hyuha, akifuatiwa na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Yasser El shawaf na Balozi wa Msumbiji, Mhe. Monica Patricio Mussa

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Bw. Suleiman Saleh wakati wa mkutano kati ya Wizara na Mabalozi wa Afrika waliopo nchini
Mkutano ukiendelea.

Jaji amkabidhi Lukuvi ripoti ya Mgogoro wa Mabwegere

$
0
0

Jonas Kamaleki- MAELEZO

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jacob Mwambejele amemkabidhi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ripoti ya uchunguzi baada kukamilika kwa uchunguzi huo.

Tukio hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo ripoti iliyohusu uchunguzi wa Mgogoro wa muda mrefu kuhusu kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani, Kilosa, mkoani Morogoro.

Katika makabidhiano hayo Jaji Mwambejele amesema kwa kushirikiana na timu yake, Wizara ya Ardhi, Vijiji vya wilayani Kilosa na uongozi wa Mkoa wa Morogoro wamekamilisha ripoti hiyo ndani ya siku 60 kama adidu za rejea zilivyowataka.

Jaji Jacob Mwambejele amesema uchunguzi huo uliangalia baadhi ya mambo ikiwemo kama uanzishwaji wa kijiji cha Mabwegere ulianzishwa kisheria na sheria zilifuatwa katika uanzishwaji huo, kama ulikuwepo usahihi wa kisheria katika upimaji wa eneo hilo na kama wanavijiji walishirikishwa, alisema Lukuvi.

Jaji huyo ameyataja maeneo mengine ya uchunguzi huu kuwa yalikuwa pamoja na kuchunguza kama upimaji ulizingatia mipaka, kuchunguza maeneo mengine yenye migogoro na kuchunguza jambo jingine lolote ambalo litasaidia katika kuleta suluhu ya mgogoro huo.

Kwa upande wake, Waziri Lukuvi ametoa shukrani zake kwa Jaji Mwambejele na timu yake, waziri Lukuvi amesema ripoti hiyo imekalika kwa wakati na inataraji kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 25.

“Mapendekezo yaliyotolewa ndani ya ripoti ya Jaji, tutayafanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kumaliza mgogoro wa Mabwegere ambao umedumu kwa miaka mingi,” alisema Lukuvi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi mapema mwaka huu alimteua kwa mamlaka yake chini ya kifungu 18 (1) cha Sheria ya Ardhi sura 113 Jaji Jacob Mwambejele wa Mahakama Kuu- Kitengo cha Biashara kuchunguza mgogoro wa Kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mfuru, Mbigiri, Mandengwa, Dumila , Matongolo na Maboiga vilivyopo Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro ili kupata suluhisho la kudumu la mgogoro huo.

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL C. MAKONDA KUHUSU KAMPENI YA AFYA CHEKI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari LEO jijini Dar es Salaam kuhusu kampeni ya kupima afya bure ambayo inaratibiwa na ofisi yake kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali za rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam na Afya Check ya Clouds FM pamoja na wadau wengine. Kampeni ya kupima afya itafanyika Septemba 24 na 25, mwaka huu kwenye viwanja vya Mnazi mmoja siku ya Jumamosi na Jumapili.
kod2
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Onesmo Kisanga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) LEO akizungumzia kuhusu umuhimu wa kupima afya mara kwa mara ili kuzuia uwezekano wa mtu kupata matatizo makubwa ya magonjwa ya figo.
kod3
Baadhi ya waandishi wa habari na madaktari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akiwahamasisha wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kupima afya Septemba 24 na 25, mwaka huu.
kod4
Kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ilala, Victoria Ludovick, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Onesmo Kisanga wa Muhimbili na Mshauri Mtaalamu wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Figo, Dk Omar Sherman wa Hospitali ya Aga Khan wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda LEO.
kod5
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweo amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya hasa kina mama kupima endapo wanaviashiria vya kansa au la.
kod6
Mganga Mkuu wa Kinondoni, Dk Aziz Msuya akizungumza katika mkutano wa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya kupima afya ambayo itafanyika Septemba 24 na 25, mwaka huu. 
kod7
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya wa jijini Dar es Salaam Leo. Kutoka kulia ni Mshauri Mtaalamu wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Figo, Dk Omar Sherman wa Hospitali ya Aga Khan, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Onesmo Kisanga wa Muhimbili, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dk Hedwiga Swai, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Muhimbili, Dk Juma Mfinanga na Mganga Mkuu wa Kinondoni,  Dk Aziz Msuya.
…………………………………………………………………..
TAARIFA  YA MKUU WA MKOA MH. PAUL MAKONDA
Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha kuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa zoezi la kiafya kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam linalotarajia kufanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 24/09/2016 siku ya Jumamosi na tarehe 25/09/2016 siku ya Jumapili kuanzia saa mbili kamili asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
 
Ndugu Wananchi,
Napenda kuwajulisha kuwa hii ni habari njema kwetu kwani huduma zote za vipimo zitatolewa bure bila gharama yoyote hivyo tunaombwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hili la kuzijua vema afya zetu kwani itatuwezesha kijikinga na magonjwa yanayoweza kijitokeza, kuepuka matumizi ya gharama kubwa za matibabu, na kuzuia vifo visivyo vya lazima kwani kuna wengine huenda hospitali pindi hali imekua mbaya sana.
 
Ndugu Wananchi,
Napenda kuwajulisha kuwa KILA AINA YA UGONJWA KATIKA MAGONJWA KUMI MAKUBWA kama vile Shinikizo la Damu, Kisukari, Saratani ya Matiti, Saratani ya Shingo ya Uzazi, Tezi Dume, Saratani ya ngozi kwa albino na Magonjwa mengine mengi yatapimwa.
 
Hivyo wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam mnahamasishwa kufika kwa wingi kwani MADAKTARI BINGWA kutoka HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD, TAASISI YA MOYO YA JAKAYA MRISHO KIKWETE, HOSPITALI ZA RUFAA ZA MKOA WA DAR ES SALAAM, HOSPITALI YA AGAKHAN, TAASISI ZA CCP MEDICENE wote kwa pamoja watakuwa tayari kuwahudumia.
 
Ndugu Wananchi,
Ninaimani ya kuwa kila mmoja wetu anajua umuhimbu wa AFYA YAKE kwani utakapoijua vema afya yako itakusaidia kuwa salama kila iitwapo leo na kukupelekea kuwa na nguvu ya kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha kila siku sambamba na kuinua uchumi wa Taifa letu la Tanzania.
 
CHEKI AFYA YAKO KWA UBORA WA MAISHA YAKO
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
 
Paul C. Makonda
MKUU WA MKOA WA
DAR ES SALAAM

WATALAAM WA TEHAMA WAPASWA KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza wakati akifunga mkutano wa wadau wa sekta ya mawasiliano wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Mhandisi Clarence Ichwekeleza akitoa mada wakati wa Mkutano wa wadau wa sekta ya mawasiliano wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016
Baadhi ya wadau wa sekta ya mawasiliano wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) akizungumza wakati akifunga mkutano wa wadau wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016

………………………………………………………………………….

Na Ally Daud-Maelezo

Wataalamu Wa tehama wamepaswa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ya tehama ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo iliyopo kwa sasa ulimwenguni.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustin Kamuzora katika mkutano wa wadau wa tehama uliojadili utekelezaji wa mkakati wa Sera ya Tehama ya mwaka 2016

Aliongeza kuwa wataalamu wa tehama wanapaswa kutumia njia mpya na za kisasa ili kukuza uchumi kama zinavyofanya nchi zilizoendelea duniani.

“Wanatehama mnatakiwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ili kuweza kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati kwa kupitia teknolojia hiyo kama zifanyavyo nchi nyingine zilizoendelea duniani kote” alisema Prof. Kamuzora.

Aidha Prof. Kamuzora alisema katika mkutano huo wanatarajia kupata mbinu mbadala za kupambana na uhalifu kwa kutumia mitandao katika kutekeleza mkakati wa Sera ya tehama ya mwaka 2016- 2020 ili kutekeleza mpango huo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza alisema kuwa moja ya mkakati wa mkutano huo ni kutengeneza miundombinu ya tehama kwa Watanzania waweze kufikiwa kirahisi.

Aidha mhandisi Ichwekeleza alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2018 inaandaa mkakati maalum wa kuwalinda watoto kutokana na madhara ya Tehama ili kuweza kuwasaidia watoto kukua katika misingi bora inayoendana na jamii ya Tanzania.

Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali Wa mitandao ya simu pamoja na wataalamu Wa tehama nchini ili kujadili mkakati wa Sera ya Tehama ya mwaka 2016.

JESHI LA POLISI MKOANI PWANI KWA KUSHIRIKIANA NA MAOFISA WA MALIASILI WAKAMATA VIROBA VIWILI VIKIWA VIMEJAA BANGI

$
0
0

Askari polisi wa kituo cha polisi cha Chalinze akionesha viroba viwili vya bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja vilivyokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa mazao ya Misitu yasiyo na kibali katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro wakitokea Tunduma wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland ( Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii)
Viroba viwili vya bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja vilivyokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa mazao ya Misitu yasiyo na kibali katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro vikitokea Tunduma vikiwa kwenye gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland ( Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii)

Kaimu mkuu wa Kanda ya Pwani wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Jonathan Mpangala akiwaonesha waandishi wa habari gari lililokuwa limebeba magunia mawili ya mkaa ambayo ndani yake kulikuwa na viroba viwili vilivyojaa bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja ( Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii)

Moja ya Kiroba kilichojaa bangi chenye uzito wa kilo 50 kilichokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa mazao ya Misitu yasiyo na kibali katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro kikitokea Tunduma kikiwa kwenye gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland (Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii)

………………………………………………………….

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inamshikilia Dereva Bw. Emanuel Bisama (37) ambaye ni mkazi wa Kimara Suka Dar es Salaam,kwa kosa la kusafirisha magunia mawili ya mkaa ambayo baada ya kupekuliwa ndani yake kulikutwa na viroba viwili vyenye uzito kilo 50 kila kimoja vikiwa vimejaa bangi.

Akizungumza jana na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani , ACP. Bonaventura Mushongi alisema Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland Bw. Emanuel Bisama (37) alikamatwa Septemba 21 saa 4.00 asubuhi katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro akitokea Tunduma na kwa sasa yupo mbaroni kwa mahojiano licha ya kukana kuwa hakujua kilichomo ndani ya magunia hayo.

Kamanda Mushongi alisema walifanikiwa kumkamata wakiwa katika Operesheni ya Ukaguzi wa mazao ya Misitu katika Barabara kuu ya Morogoro hadi Dare Salaam, aliongeza kuwa Dereva huyo wa gari amefunguliwa kesi CHA/RB/3039/2016 kwa kosa la kupatikana na bangi

Kwa upande Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania (TFS) Kaimu wa Kanda ya Pwani Bw. Jonathan Mpangala alisema kuwa Mtuhumiwa huyo amefunguliwa kesi ya pili yenye CHA/RB/5113/2016 kwa kosa la kumiliki na kusafirisha mazao ya misitu bila kibali kwa sheria ya misitu namba 14 ya 2012 kifungu 88 na 89.

Alisisitiza kuwa Operesheni ya kukamata usafirishaji wa mazao ya misitu bila vibali itakuwa ya kudumu baada ya kuona magari mengi hasa makubwa yakiwa yamepakiwa magunia ya mkaa kuanzia mawili hadi matano ambayo yamekuwa yakioneka waziwazi hata ukiwa barabarani namengi yakiwa hayalipiwa ushuru wa Serikali kuu na hata magari mengine yakiwa hayajalipiwa ushuru wa Halmashauri

Naibu Waziri Mhe.Anastazia afungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa TBC

$
0
0
  Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyevaa Kitenge cha Kijani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika uliyofanyika Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam.Aliyevaa Suti ya Bluu ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt.Ayoub Ryoba. Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyevaa Kitenge cha rangi ya Kijani ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo uliyofanyika Jijini Dar es Salaam Septemba 22,2016.Aliyevaa Suti ya Bluu ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt.Ayoub Rioba. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) (hawapo pichani) katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt.Ayoub Ryoba. Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) (hawapo pichani)katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa Kanda ya Kusini Bw.Asheri Chilewa akimwomba Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) kupitia Wizara yake kuandaliwe mkakati wa kufundisha lugha ya Kiswahili fasaha kwani kumekuwa na makosa mengi yanayojitokeza katika matumizi ya Kiswahili, katika mkutano na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) uliyofanyika Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali ya wafanyakazi. Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)Dkt. .Ayoub Ryoba akizungumza namna walivyoweka mikakati ya kutatua changamoto za wafanyakazi wa Shirika hilo kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) katika mkutano na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) uliyofanyika Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi RAAWU Taifa Bw.Felician Maige akimuomba Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa kwanza kulia) kuzungumza na Uongozi wa Shirka la Utangazaji la Taifa kwa kuwapatia ajira za kudumu wafanyakazi waliyokuwa hawana mikataba kwa muda mrefu,katika Mkutano na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) uliyofanyika Jijini Dar es Salaam Septemba 22,2016.

………………………………………………………….
Na Anitha Jonas – WHUSM- Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amewaahidi Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufuatilia malimbikizo ya mishahara yao na kuhakikisha wanalipwa. 

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC ) uliyolenga kujadili bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyopitishwa na Bunge na kuweka mikakati ya namna Shirika litakavyoweza kupata pesa nakuweza kujiendesha pamoja na namna ya kuboresha huduma ya matangazo.
“Natambua TBC ina wafanyakazi zaidi ya mia sita (600) nawasihi mtakapotoka hapa mkawarejeshee wenzenu mliyojifunza na mkawaeleze mipango mliyoamua kwa niaba yao,”alisema Mhe.Anastazia. 

Akiendelea kuzungumza katika Mkutano huo Mhe.Anastazia aliupongeza uongozi wa TBC kwa kuandaa Harambee ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera kwani wameonyesha uzalendo wao wa kuona changamoto zilizopo katika kurekebisha miundombinu iliyoharibika pamoja na kuwasaidia wakazi walioathirika mahitaji muhimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Ryoba alisema shirika lina malengo ya kuwafikia Watanzania wote na kuhakikisha linawaunganisha kwa Taarifa mbalimbali,pamoja na kuandaa vipindi vyenye maudhui yanayogusa watu wote.

Pamoja naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU Taifa Bw.Felician Maige alimuomba Mhe.Naibu Waziri kuzungumza na uongozi wa Shirika hilo kuhusu kuwapatia ajira za kudumu au mikatabu baadhi ya wafanyakazi waliyofanya kwa muda mrefu kama vibarua. 

Kwa upande wa mmoja wa Wafanyakazi wa TBC Bw. Asheri Chilewa alimuomba Naibu waziri huyo kupitia Wizara yake na Taasisi yake ya Kiswahili kuundwe mkakati utakaosaidia kufundisha jamii lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwani kwa hivi karibuni kumekuwa na upotoshwaji wa matumizi ya lugha hiyo kwa kiasi kikubwa na maneno kutumika isivyo sawa .
Huku akitoa mfano wa namna watu wanasema mtu amepoteza maisha pale anapofariki ambapo siyo sahihi kwani maisha ya mtu hayapotei.
Hata hivyo Naibu Waziri aliueleza Uongozi wa TBC kuwa Serikali inaelewa changamoto wanazopitia na kwa sasa inashughulikia suala hilo kwa kuona ni namna gani kupitia mapato ya Kampuni ya Startimes yatakavyoweza kuchangia uendeshaji wa shirika hilo na mpaka mwakani mkakati huo utakuwa umekamilika.

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA STENDI KUU UBUNGO NA KIBAHA, AGUNDUA MABASI MABOVU, AYAZUIA KUSAFIRI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akishuhudia Dereva wa Basi la Tahmeed (kulia) akipimwa kilevi na Trafiki Nuru Mvungi kabla ya Basi lake kuruhusiwa na safari. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa7
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari, Picha ya Ndege Kibaha, Pwani, mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua mabasi mabovu na usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa8
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akihoji usalama wa mtoto baada ya kugundua siti moja kukaa watoto wawili jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa9
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwasalimia wananchi wa Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani mara baada ya kumaliza ukaguzi wa mabasi mabovu pamoja na madereva ambao hawana leseni. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akielekea Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi ya Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba za usajili T419 BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwauliza abiria wa Basi la Harambee linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, maswali mbalimbali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wakati wanaposafiri. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua mikanda katika Basi la Shambalai wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akioneshwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, tairi la Basi la Shambalai ambalo halina ubora kwa ajili ya kusafirisha abiria. Hata hivyo Masauni aliagiza basi hilo lizuiwe kufanya safari na pia kuchukuliwa hatua kali kwa Mmiliki wa basi hilo pamoja na Dereva. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akizungumza na madereva wa Basi ya mikoani pamoja na wa magari madogo ya mizigo yanayopaki Stendi Kuu Ubungo, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani. Hata hivyo, madereva hao walilalamika kuwa hawana mikataba ya kazi zao. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi hiyo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

DARAJA LA SALENDER KUANZA UJENZI JUNI MWAKANI-RAIS MAGUFULI

$
0
0
Ujenzi wa Daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo Agha Khan kupitia baharini Jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza Mwezi Juni Mwakani baada ya Serikali ya Tanzania kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa fedha za ujenzi kutoka benki ya Exim ya Korea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 Septemba, 2016 muda mfupi baada ya kufanya Mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Song Geum-Young, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema ujenzi wa daraja hilo litakalokuwa na urefu wa kilometa 7 zikiwemo kilometa 1.4 zitakazopita baharini, unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na daraja hilo litasaidia kupunguza adha ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

"Mchakato wa kulijenga hili daraja la Salender unaendelea vizuri kwa sababu hivi sasa kampuni ya Kikorea ambayo inafanya usanifu ipo kwenye hatua za mwisho na zabuni zinategemewa kutangazwa mwezi wa tatu Mwaka kesho na zitakwenda haraka, kwa hiyo mambo yakienda vizuri ujenzi unaweza kuanza mwezi wa sita, bahati nzuri fedha zote zipo na zimeshatolewa na Benki ya Exim ya Korea"Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Dkt. Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi alizozifanya zilizowezesha kujengwa kwa hospitali ya Mloganzila  kwa ufadhili wa Jamhuri ya Korea na kwamba hospitali hiyo itakuwa ya kisasa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema ujenzi wa Hospitali hiyo unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu na kwamba tayari Madaktari na Wataalamu takribani 100 waliopata mafunzo nchini Korea na wenye ujuzi wa namna ya kutumia teknolojia inayowekwa kwenye hospitali hiyo wapo hapa nchini.

Rais Magufuli ambaye ameelezea nia ya Serikali ya Tanzania kufungua ofisi za Ubalozi Mjini Seoul nchini Korea ameongeza kuwa Serikali yake imedhamiria kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi kwa lengo la kuwaletea manufaa wananchi ikiwemo kutumia teknolojia na ujuzi wa nchi ya Korea katika ujenzi wa Meli.

Kwa upande wake, Balozi wa Korea hapa nchini Mhe. Song Geum-Young ametoa salamu za pole kufuatia maafa ya tetemeko la Ardhi yaliyotokea Mkoani Kagera na mikoa jirani, na ameahidi kuwa Korea itatuma timu ya wataalamu kuja kuona namna ya kusaidia.

Balozi Song Geum-Young pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Korea itaendeleza na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania na kwamba itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini ikiwemo ujenzi wa Daraja la Salender, Meli, Hospitali ya Mloganzila na mingineyo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Urusi hapa nchini Mhe. Yuri Popov ambapo viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo huku wakitilia mkazo katika kukuza biashara na uwekezaji.

Pamoja na hayo Balozi Yuri Popov amepongeza na kuelezea kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli katika kuimarisha uchumi huku akibainisha kuwa kwa hatua hizi anaamini ajenda ya kujenga uchumi wa viwanda itafanikiwa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea taarifa ya hali ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na katika mazungumzo yake na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele, amemtaka kuendelea kuimarisha utendaji kazi wa maabara hiyo ili kuongeza ufanisi wa majukumu yake ambayo ni kufanyia uchunguzi vielelezo vya makosa ya Jinai na usimamizi wa sheria za udhibiti wa kemikali na udhibiti wa vinasaba vya binadamu (DNA).


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
22 Septemba, 2016

MAMBO YANAZIDI KUIVA ATCLA,SAFU YAKE YA JUU YA UONGOZI YAKAMILIKA

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA JAMHURI YA KOREA HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kuhusiana na ujenzi wa daraja hilo jipya la Salenda kutoka kwa  Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa  nchini Song Geum-Young mara baada ya kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini  hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele Ikulu jijini Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU.

Masauni apanda mabasi ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiingia ndani ya Basi la Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na basi hilo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam akitoka kituo cha Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitelemka katika moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam katika kituo cha Nyerere, Posta. Masauni alipanda basi hilo akitokea Ubungo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiondoka katika Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi cha Nyerere, Posta, mara baada ya kusafiri na usafiri huo akitokea Ubungo, jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Katikati ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.




Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata tiketi ya mabasi ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga naye akiwa mmoja wa wasafiri wa mabasi hayo. Masauni aliyapanda basi la Mwendo kasi mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiigusisha tiketi yake katika mashine ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam ili mruhusu kuingia ndani ya stendi hiyo kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………………………………………………………….

Felix Mwagara, MOHA

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameupongeza Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT wa jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi waendelee kuyatumia mabasi hayo wanaposafiri sehemu mbalimbali jijini humo.

Mhandisi Masauni ameyasema hayo jana mara baada ya kusafiri na mabasi hayo kutoka kituo cha mabasi hayo cha Ubungo mpaka katikati ya jiji kwa lengo la kujionea jinsi mabasi hayo ya mwendokasi yanavyohudumia abiria pamoja na kuwapa moyo wananchi kuwa usafiri huo unatumiwa na mwananchi wa aina yeyote.

Akizungumzia usafiri huo, Masauni alisema mradi huo umerahisisha sana usafiri kwani ametumia dakika chake akitokea Ubungo hadi Posta katikati ya jiji bila usumbufu wowote, hivyo mradi huo ameomba uendelee kulindwa pamoja na kutunzwa na UDA-RT na wananchi wenyewe kwa ujumla.

“Mimi kwa kweli nimeufurahia sana usafiri huu, Serikali imefanya jambo kubwa sana kwa wananchi wake, kwa kuwajali wananchi kwa kuuleta mradi huu ambao unarahisisha safari kwa uharaka zaidi na pia unapendezesha jiji kwa jinsi magari yalivyo nadhifu,” alisema Masauni ambaye pia alilipa nauli kwa kupanga foleni kama wananchi wengine wanavyofanya wanapotaka kusafiri na usafiri huo.

Masauni aliongeza kuwa; “Nimefarijika sana na lugha ya adabu na tulivu ambayo wanaitumia madereva wa mabasi hayo wanapowatangazia wananchi vituo mbalimbali vya kushuka na kuingia kwenye mabasi hayo, hii inasaidia kuwa na mawasiliano mazuri na abiria, pia inaonesha madereva hao wamefunzwa vizuri na wanaipenda kazi yao.”

Hata hivyo, Masauni alitoa ushauri kwa uongozi wa mabasi hayo, kuruhusu wananchi waingie ndani ya mabasi hayo kwa idadi ambayo haitaleta kero kwa abiria wengine ili kupunguza wingi wa abiria hao kwa lengo la kuepuka mbanano mkubwa wa abiria.

Pia aliwataka wananchi wa jiji hilo kuyatunza mabasi hayo, na pia kukubali maelekezo ya madereva wanapotoa matangazo wanapokuwa safarini kuelekea maeneo mbalimbali ya jiji.

Naibu Waziri huyo alipanda mabasi hayo akitokea Ubungo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza kwa kutembelea Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kwa lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria wanaosafiri na mabasi hayo. Masauni pia alifanya ziara hiyo ya ghafla kwa kutembelea Stendi ya Kibaha, mkoani Pwani.

Serikali Kununua Ndege Jet mpya mbili Mpya Mwakani

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawsiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akitoa maelekezo kwa Bodi mpya ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) wakati alipoitambulisha Bodi hiyo, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Eng. Leonard Chamriho.

Na. JAMVI LA HABARI .

Taarifa iliyotolewa  na Kitengocha Habari na Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Inasema kuwa waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi mitatu kwa Bodi mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kusuka upya uongozi uliopo ili kuweza kuleta ufanisi wa utendaji kazi wa Shirika hilo.

Akizungumza jijini Dar es salaam mara baada ya kuitambulisha Bodi hiyo, Waziri Mbarawa amesema kuwa Uteuzi wa Bodi hiyo utasimamia kuleta tija na ufanisi wa shirika hilo ambalo kwa kipindi kirefu lilikuwa na changamoto nyingi.

“Nataka kuona mabadiliko makubwa kuanzia kwenye Menejimenti hadi uongozi wa chini, hakikisheni mnaweka uongozi amabao utafuata maadili, utakuwa na ufanisi, ubunifu na kasi katika utendaji kazi” amesema Profesa Mbarawa.

Aidha, ameitaka Bodi hiyo kusimamia na kuboresha mpango wa kibiashara wa usafirishaji (Business Plan) katika Shirika hilo ili kuweza kumudu soko la ushindani na kuweza kuongeza mapato ya Shirika hilo.

“Kama mnavyojua usafiri wa anga una ushindani mkubwa, hivyo ili Serikali iweze kupata faida katika biashara hii ni lazima tuboreshe mpango wa kibiashara unaoendana na wakati”, amesisistiza Waziri Mbarawa.

Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kuipa ATCL mifumo imara, makini na mahiri ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili Shirika hilo ikwemo wizi wa mafuta ya ndege na upotevu wa mapato. Ili kupima ufanisi wa utendaji wa Shirika hilo Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kuandaa mkataba kwa kila mfanyakazi kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

Katika hatua nyingine Waziri Mbarawa amesema kuwa Serikali ina mpango wa kununua ndege mbili mpya aina ya Jet ifikapo mwaka 2017 kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji wa
anga nchini.

Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ameitaka Bodi hiyo kutumia fursa walioipata katika kufanya kazi vizuri ili kufufua shirika
hilo na kuwapatia watanzania huduma sahihi na bora za usafirishaji.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Emmanuel Korosso, ameahidi kushirikiana na wajumbe wa bodi yake katika kutekeleza maelekezo ya Waziri haraka iwezekanavyo ikiwemo
kubadilisha menejimenti ya shirika hilo.

Tume ya Mipango yatoa Elimu juu ya Mipango ya Maendeleo ya Kimataifa na Kikanda

$
0
0
                       
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe  (kushoto) akiongea na wadau wa sera na Mipango kutoka tasisi mbalimbali juu ya mikakati na mipango ya maendeleo ya Kimataifa na Kikanda. Katikati ni Balozi Innocent Shiyokutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na kulia ni Bw. Maxwell Mkumba kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Wadau wa sera na mipango wakisikiliza moja ya mada zilizotolewa katika warsha hiyo.
                  Washiriki wakiwa wanasikiliza mada juu ya Mpango wa maendeleo wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).        

Na Adili Mhina.
Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) imeendesha warsha ya kujenga uelewa juu ya Dira na mipango ya maendeleo ya  kimataifa na kikanda.

Warsha hiyo imewakutanaisha wakurugenzi wa mipango na sera kutoka sekta mbalimbali, idara na mashirika ya Umma, wawakilishi wa asasi zisizo za kiraia, wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na wataalam kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Paul Sangawe alisema warsha hiyo imekusudiwa kujenga uelewa juu ya Sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kimataifa na kikanda hususani malengo ya maendeleo endelevu 2030, Agenda ya maendeleo ya Afrika 2063, na mpango mkakati wa nchi za kusini mwa Afrika 2016/17-2010/21.

Alieleza kuwa walengwa katika warsha hiyo watapata uelewa juu ya kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kimataifa na kikanda.

Warsha hiyo inayoendelea katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam itasaidia wadau kupata uzoefu kutoka nchi zingine wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

MHE. JANUARY MAKAMBA AKIWAFARIJI WAATHIRIKA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA

RAIS MAGUFULI HAJAKATAA KUONANA NA VIONGOZI WA DINI:SHEIKH ALHAD

$
0
0
Na.Sheila samba & Abushehe Nondo,Maelezo

Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi hao ambao wamemuomba kukutana naye, kama inavyoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Akizungumza leo jijini, Dar es Salaam na waandishi wa habari Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima la Septemba 21 ISSN 0856 9762 toleo na.4310 sio za kweli.“taarifa hizo sio za kweli, taarifa hizo zimelenga kumgombanisha Rais na Viongozi wa Dini na watanzania kwa ujumla na hilo halitafanikiwa,” alisema Sheikh Alhad

Aidha Viongozi hao wamesema uamuzi wao wa kumuomba Rais kuonana naye, haujatokana na kuagizwa na UKAWA, bali umetokana na maono waliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Amefafanua kuwa Rais MAGUFULI anawaheshimu Viongozi wa dini na mara zote amekua akiwaomba wamuombee na kusema leo ni siku ya tano tangu wamuandikie barua ya kumuomba kukutana naye na wanaimani Rais atakutana na Viongozi hao.

Ameeleza kuwa Barua hiyo imeandikwa Septemba 19 na kupelekwa siku hiyo hiyo Ikulu, ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata, Katibu Mkuu wa CCT na Katibu Mkuu wa TEC.“Naomba watanzania wasisikilize maneno hayo kwasababu hayana nia njema kwa Taifa letu, naamini Mh Rais tutaonana nae na tutaongelea mustakbali wa nchi katika mambo mbalimbali,” alisistisa Sheikh Alhad

Akizungumzia utendaji wa Serikali ya Rais MAGUFULI, Sheikh ALHAD amesema Rais amerejesha nidhamu Serikalini, ukusanyaji mapato umeimarika na pia pengo kati ya wasionacho na walionacho linaanza kupungua. caption.Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akionyesha gazeti la Tanzania Daima kwa waandishi wa habari,liloandika taarifa sio za kweli.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images