Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 975 | 976 | (Page 977) | 978 | 979 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha kiasi cha  dola laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili kutoka (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
  bub2
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam.
  bub3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akifatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
  bub4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
  bub5
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  mchango wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.
  bub6
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  bub7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara baada ya kuwasilisha mchango wa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
  bub8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kwa misaada mbalimbali ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote. PICHA NA IKULU

  0 0

   
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Septemba, 2016 amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemoko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Kagera,Geita na Mara kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na takribani Shilingi za Kitanzania Milioni Mia nne na therathini na saba (Tshs-437,000,000/-) kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

  Katika taarifa yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

  Mhe. Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwemo kupeleka chakula, huduma za matibabu na hifadhi za dharura kwa waathirika na pia inaratibu ukusanyaji wa michango kutoka sehemu mbalimbali ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni tatu nukta sita (Tshs Bilioni 3.6) zimepatikana.

  Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maafa na michango kwa ajili ya waathirika wa maafa hayo, Rais Magufuli amewashukuru wote waliojitoa kusaidia waathirika wakiwemo Marais Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda ambao wamempigia simu za kumpa pole na tayari wametoa misaada yao, na pia nchi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara, watumishi wa umma na watu binafsi na amesema michango hiyo ina umuhimu mkubwa katika kukabiliana na athari za maafa haya.

  Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania na wote walioguswa na maafa haya kuendelea kutoa misaada kwa waathirika kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akionya na kuvitaka vyombo vya dola kuwafuatilia watu wanaotaka kutumia maafa haya kukusanya michango kwa lengo la kujinufaisha.

  Rais Magufuli amebainisha kuwa Serikali itahakikisha inarekebisha miundombinu iliyoharibika zikiwemo shule, vituo vya matibabu, barabara na huduma nyingine za kijamii na pia ametaka wananchi waliokumbwa na madhara ya tetemeko hususani nyumba zilizobomoka, wajipange kurekebisha nyumba zao kwa kuwa Serikali pekee yake haitaweza kujenga nyumba zote zilizobomoka.

  Aidha, Rais Magufuli amewasihi Watanzania kuwapuuza watu wanaotaka kutumia maafa haya kueneza uchonganishi na chuki dhidi ya Serikali na ameweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna teknolojia ya kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi na kwamba tetemeko hili halikuletwa na Serikali.

  Dkt. Magufuli amesema hata mataifa makubwa yenye maendeleo makubwa ya uchumi na teknolojia yanakumbwa na tetemeko la ardhi na kusababisha vifo vya idadi kubwa ya wananchi na uharibifu mkubwa wa mali.

  "Nilikuwa najaribu kuangalia kwa mfano nchi kama China kwenye mwaka 2014 watu 617 walipoteza maisha, Mwaka 2013 walipoteza watu 193, Mwaka 2010 walipoteza watu 2,998 Mwaka 2008 China ilipoteza watu 98,712.

  Ukijaribu kuangalia Japan, nchi ambayo imeendelea na ina utaalamu wa hali ya juu sana, kwenye mwaka 2016 tarehe 14 mwezi wa nne ilipoteza watu 6, baada ya siku mbili tarehe 16 mwezi wa nne 2016 tetemeko likatokea tena na likaua watu 35, mwaka 2012 likaua watu 3, mwaka 2011 likaua watu 15,904 mwaka 2008 likaua watu 12, mwaka 2007 likaua watu 11, mwaka 2004 likaua watu 40, mwaka 1923 liliua watu 142,800 na hiyo ni Japan. Amesisitiza Rais Magufuli.

  Shughuli ya kupokea taarifa ya Waziri Mkuu na michango kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na Mikoa jirani imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Dorothy Hyuha na Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Boniface Muhia.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  17 Septemba, 2016

  0 0  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuwatahadharisha kuwa kuna watu wametumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua kwa Kampuni Binafsi na Wakurugenzi Watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi 23/09/2016"


  Mnataarifiwa kuwa barua hizo zilizotiwa saini na muhuri wa kughushi na ambazo hata maelezo yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa utapeli.


  Yeyote aliyepokea barua hizo azipuuze na achukue hatua mara moja kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.


  Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuueleza umma kuwa uendelee kupokea taarifa sahihi zinazotolewa kupitia vyombo vya habari na pale ambapo kuna mashaka juu ya taarifa zenye nembo ya Ikulu wasisite kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu zilizotajwa katika anuani ya mawasiliano hapo juu.

  Tafadhari atakayepata ujumbe huu umtaarifu na mwenzake.

  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam

  17 Septemba, 2016

  0 0

   Kipa wa Timu ya Azam FC "Wanalambalamba", Aeshi Manula akiwa chini huku Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo akijiandaa kushangilia baada ya Kipa huyo kupitwa na mpira uliopigwa vizuri kabisa na Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya (hayupo pichani) na kuingia moja kwa moja wavuni na kuifanya timu hiyo kujipatia bao la kuongoza. Mchezo huo ambao ulikuwa ni wenye kasi na wakuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu, umemalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam huku Timu ya Simba ikiondoka uwanjani hapo ikiwa kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0. Kwa ushindi huu wa leo, Timu ya Simba sasa inashikilia ushukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa na pointi 13, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 10 sawa na Azam FC.
   Mshambuliaji wa Timu ya Azam FC, John Bocco akituliza Mpira mbele ya Beki wa Simba, Novaty Lufunga, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Simba imeshida bao 1-0.
   Beki wa Azam FC, David Mwantika akindoka na mpira baada ya kumshinda maarifa, Mshambuliaji wa Simba, Fredrick Blagnon, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Simba imeshida bao 1-0.

   Kikosi cha Simba SC.
   Kikosi cha Azam FC.

  0 0

   Mwenyekiti wa Tanzania CEO Roundtable, Ali Mufuruki akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Dk. Gift Shoko wakati wa uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ jijini Dar Es Salaam hivi karibuni. Mufuruki alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana.  Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA Tanzania, Dk Gift Shoko akizungumza na wateja mashuhuri wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ uliofanyika jinni Dar es Salaam hivi karibuni. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.  Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa CEO Round Table nchini, Ali Mufuruki akizungumza na wateja mashuhuri wa benki ya CBA Tanzania katika uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ uliofanyika jinni Dar es Salaam hivi karibuni. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana.    Wageni waalikwa. 

  Benki ya CBA yaja na huduma za kisasa za kibenki Katika mkakati wake wa kuendelea kuboresha huduma zake nchini,Benki ya CBA imezindua huduma mpya kwa wateja wake binafsi zitakazowawezesha kupata huduma za kibenki kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kupata huduma za kibenki kimtandao kupitia simu zao za mkononi. Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya,Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Tanzania,Dk.Gift Shoko,alisema kuwa huduma hizi zimelenga kuwarahisishia maisha wateja na kuwawezesha kupata huduma za kibenki kulingana na matakwa yao na kwenda sambamba na mtindo wa maisha wanaoishi.

   Alisema pia wateja wa CBA Tanzania kuanzia sasa wanaweza kutumia kadi za kimataifa za kufanya mihamala ya malipo za Visa Platinum Debit Card na Visa Gold Credit Card kwa fedha za kitanzania na Dola za Kimarekani ambazo zinawawezesha kupata huduma mbalimbali wakiwa katika uwanja wa ndege wa JKIA kwenye sehemu ya kupita watu maarufu (VIP lounge).Alisema huduma hii itawawezesha wateja wa kundi hili kufanya mihamala wakiwa katika viwanja vya ndege 600 kwenye nchi 1,000 na miji mikubwa ipatayo 300 duniani kote.

   “Tunazidi kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja ili wazipate popote na kwa wakati wowote watakapokuwa bila kupoteza muda kama ilivyokuwa hapo awali”.Alisema. Kitengo cha kuhudumia wateja watakaojiunga na huduma hii kwa kuanzia itapatikana jijini Dar es Salaam katika matawi yaliyopo kwenye mitaa ya Ohio na Samora vilevile katika tawi la Arusha. Benki ya CBA Tanzania ambayo ni moja ya Benki kubwa zinazoongoza kwa ubunifu wa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wake ,moja ya huduma ambayo imeianzisha na kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya makazi ya kutoa mikopo ya nyumba inayolipwa hadi kufikia kipindi cha miaka 20. 

   Benki ya CBA Tanzania hadi kufikia sasa inayo matawi 11 nchini kote ambapo 5 yapo jijini Dar es Salaam na mengine katika miji ya Mbeya, Tunduma, Mtwara, Moshi, Mwanza, na Arusha.Pia benki ipo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki za Kenya,Uganda na Rwanda ambazo ziko chini ya mwamvuli wa CBA GROUP.

  0 0


  0 0

   
   Wateja wa Airtel wakijipatia simu za smartphone na kujiunga na team sibanduki katika smartphone bazaar iliyoko mlimani city, Smartphone Bazaar itakuwepo siku za mwisho wa wiki Jumamosi na  jumapili . simu za kijanja kama  Fero 280 na magnus z11 , Huawei Y3C na nyingine nyingi zinapatikana hapo.
   Muhudumu katika kitengo cha huduma kwa wateja akitoa elimu juu ya simu mbalimbali za kisasa kwa wateja waliotembelea Airtel Smartphone Bazaar , mlimani city

  Katika kuendeleza kampeni yake kabambe ya “Sibanduki”  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeweka gulio la simu yaani Smartphone Baazar  mwishoni mwa wiki ndani ya mlimani City jijini Dar es Saalam ili kuwawezesha wateja wake kupata simu za kisasa , origino na kwa gharama nafuu
  Airtel Smartphone Bazaar ina lengo la kuwapatia wateja wa Airtel simu za kisasa na pia kutoa nafasi kwa wateja wa Airtel kujiunga na timu Sibanduki” na kufurahia huduma lukuki ikiwemo ,kutuma na kutoa pesa bure, kujitengenezea vifurushi vya yatosha na kupata MB zaidi, SMS zaidi na intaneti zaidi,  kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana, kutoa pesa benki na kuweka kwenye akaunti zao za Airtel Money wakati wowote na kwa wateja wapya kupata vifurushi vya dakika 60, SMS 2000 na MB 200 bure bila , vifurushi hivi vitadumu kwa muda wa siku 60
  Akiongea kuhusu Smartphone Bazaar, James Kagashe, Afisa bidhaa na masoko alisema “ Tunayofuraha kuwaletea sokoni wateja wetu simu za kisasa , origino na zenye gharama nafuu hadi shilingi 24,000. Tunazo simu nyingi ikiwemo simu Aina ya fero 280 inayouzwa 24,000, simu ya smartphone aina ya Magnus Z11 inayouzwa kwa shilingi 83,000 na simu ya Huawei Y3C kwa shilingi 140,000. Pamoja na simu hizi tunazo simu aina ya Samsung, Techno pia zinapatikana hapa katika Bazaar hii.
  Natoa wito kwa wateja na watanzania kujitokeza na kutembelea hapa ndani mlimani city na kujipatia simu kwa bei poa na kujiungana timu Sibanduki kwa huduma bora za kipekee na kibunifu wakati wote
  Smartphone Bazaar itakuwepo pia wiki ijayo siku ya Jumamosi na Jumapili hapo haop mlimani City


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa vija Shaka Hamidu Shaka akichangia damu kwenye viwanja vya mashujaa Mkoani Kagera kwaajili ya majeruhi wa wahanga wa tetemeko la ardhi.
   Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamidu  Shaka akibadhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu kwaajili ya wa waathirika wa tetemeko la ardhi

   
  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

  UMOJA wa vijana wa chama cha CCM Taifa(UVCCM)wameishauri na kuiomba selikari kutumia jeshi la wananchi JWTZ  katika zoezi la kuhakiki na kutathimini pamoja na kugawa misaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Shaka Hamidu Shaka alitoa ombi hilo kwa kamati ya maafa ya Mkoa ambayo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu alisema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa waathirika wa tetemeko kuwa hawatendewi haki na wale wanaopita kufanya tathimini kwenye nyumba zao zilizoathirika.

  "Jeshi la wananchi hawana chama wala Dini hivyo hawezi kubagua mtu nina amini watatenda haki kwa kila mwananchi aliyeathirika na itasaidia kuondokana na migogoro ambayo inaweza kujitokeza kwa wale watakaokosa haki zao pia watafanya zoezi kwa wepesi na uharaka zaidi kuliko hali ilivyo sasa"alisema Shaka

  Wakati huo huo umoja huo umekikabidhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu.

  "Umoja wa UVCCM Taifa tunawapa pole sana wahanga wote wa tetemeko la ardhi,ila tunawaomba wanasiasa wasitumie tetemeko hili kama sehemu ya kutangaza siasa zao,hili ni janga za watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za vyama wala dini zao"alisema

  Baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu alisema kuwa mambo ya ubaguzi kwa waathirika wa tetemeko ameshayakemea sana na anaendelea kuyakemea ndiyo maana ameelekeza misaada yote ipitie ofisini kwake ili iwafikie walengwa kwa utaratibu mahususi uliopangwa.

  "Endapo mtu yeyote atabainika anafanya ubaguzi nitamchukulua hatua kali sababu bado misaada inahitajika sana"alisema Mkuu wa Mkoa

  0 0


  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na wachezaji wa Serengeti Boys katika hafla fupi ya kuwakabidhi Shilingi Milioni Tano kama motisha kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa maelezo juu ya maaandalizi ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
  Kocha wa Serengeti Boys Bw. Bw.Bakari Shime akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kwa kuwapa motisha wachezaji kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.

  Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame akiahidi kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kuibuka na ushindi dhidi ya Congo-Brazaville katika mechi itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimkabidhi Millioni tano Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame kama motisha kabla ya kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
  Baadhi ya wachezaji wa Serengeti Boys wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika hafla fupi kabla ya mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)


  Na Shamimu Nyaki- WHUSM.


  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa kiasi cha shilingi million tano kwa timu ya Serengeti Boys kama motisha katika mchezo wao dhidi ya Congo Brazivile utakayochezwa leo katika Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es Salaam.

  Akikabidhi pesa hizo leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Waziri Nape amewataka wachezaji hao kujituma zaidi katika mechi hiyo ili wapate ushindi utakaowawezesha kufuzu katika fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 .

  “Watanzania wote tupo pamoja na nyie endeleeni kujituma kama mlivyofanya katika hatua ya kwanza na ya pili, Sisi kama Serikali tunawaunga mkono na tunawatakia heri ili mlete heshima kwa Taifa.”Alisema Mhe. Nape.

  Kwa upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw.Bakari Shime amemuhakikishia Waziri na Watanzania kwa ujumla kuwa mechi ya leo watahakikisha wanapata ushindi kwani wamejiandaa vizuri na wachezaji wote wapo tayari kuivaa Congo Brazavile.

  Aidha Nahodha wa Timu hiyo Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata maagizo kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata ushindi.

  “Tunashukuru sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate ushindi ili tusonge mbele zaidi ” Aliongeza Nahodha Makame.

  Timu hiyo ya vijana chini ya umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys) inashiriki kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.

  0 0

   Kijana Kelvin Jackson Kalasha akitafakari kwa furaha, wakati wa Mahafali ya kumaliza kidato cha Nne katika shule ya Tusiime, Kampasi ya Tabata, Dar es Salaam, jana, Septemba 17, 2016
   Kijana Kelvin Jackson Kalasha (Kushoto) akiwa na wahitimu wenzake wa kidato cha nne, wakati wa Mahafali ya kumaliza kidato hicho katika shule ya Tusiime, Kampasi ya Tabata, Dar es Salaam, jana, Septemba 17, 2016
   "Mama Mdogo", Kijana Kelvin akimwambia Caroline Kisamo, mwanzoni mwa sherehe hiyo ya mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Tusiime, jana. Katikati ni Mama Kelvin, Ever Kalasha
  Wanafamilia wakiwa kwenye mahafali hayo. Kushoto ni Caroline Kisamo

  Viongozi meza kuu wakiongozwa na mgeni rasmi wakati wakishiriki kuimba wimbo wa taifa wakati wa mahafali hayo
   Kelvin akipongezwa wakati akipita mezakuu kupokea cheti chake cha kuhitimu kidato cha nne wakati wa mahafali hayo
   Kelvin akiwa na wazazi wake Jackson Buhulula Kalasha na Mama  Ever Kalasha wakati wa mahafali hayo
   Kelvin akiwa na wazazi wake Jackson Buhulula Kalasha na Mama  Ever Kalasha wakati wa mahafali hayo
      Mgeni mwalikwa akimpongeza Kelvin wakati wa mahafali hayo. Katikati ni Jackson Kalasha
   Jackson Kalasha akiwa na Mama Ever Kalasha wakati wa mahafali hayo
   Kelvin akilisha keki mhitimu mwenzake wa kidato cha nne wakati wamahafali hayo
   Kelvin akimlisha keki baba yake, Mzee Jackson Kalasha wakati wa mahafali hayo
   Kelvin akimlisha keki Mama yake, Ever Kalasha wakati wa mahafali hayo
   Kelvin akipewa keki na mama yake, Ever Kalasha
   Ever Kalasha akimlisha keki kwa upendo mtoto wake, Kelvin Kalasha wakati wa mahafali hayo
   Ever Kalasha akionyesha furaha kwa mwane, Kelvin baada ya kumlisha keki
   Mama Ever Kalasha akimlisha keki mumewe, Jackson Kalasha, wakati wa sherehe ya mtoto wao Kelvin kwenye mahafali hayo katika shule ya Tusiime, Tabata, jana, kama ilivyoshuhudiwa na mpigapicha wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo. Kwa picha kem-kem za tukio hili/ TAFADHALI>>BOFYA HAPA

  0 0
  Mchezaji bora wa Klabu ya Simba kwa mwezi Agosti, 2016 Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amekabidhiwa tuzo yake mbele ya mashahiki waliokujakushuhudia mchezo wa kati ya Azam Fc na Simba Sc. Pamoja na tuzo hiyo Zimbwe Jr pia amekabidhiwa Tsh 500,000/= kama sehemu ya zawadi kwa mchezaji bora. Hii ni tuzo ya kwanza kutolewa kwa msimu huu 2016/2017 ambapo ilikabidhiwa kwa Zimbwe Jr na Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group Imani Kajula pamoja na Makamu wa Rais wa Simba Geophrey Nyange kabla ya mchezo wa kuanza, mchezo ambao ulikwisha kwa Simba kuibuka kidedea kwa kuifunga Azam FC kwa goli moja bila, goli lililofungwa na Shiza Kichuya Dakika ya 68 Kipindi cha Pili.

  0 0


  Baadhi ya Vijana waliohitimu katika fani ya ufundi wa magari chini ya Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) wakifanya mazoezi ya kurekebisha magari katika gereji ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, (mwenye tisheti jekundu) ni fundi msaidizi wa gereji hiyo, Haji Faki.
  Meneja wa Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) – Tanzania, Simon Ndembeka akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uhitaji wa walimu wa mahitaji maaalum watakaoweza kukidhi idadi ya wanafunzi walemavu wanaohitaji kupatiwa elimu ya ufundi katika Chuo cha Elimu na Ufundi Stadi (VETA) chini ya mradi huo.

  …………………………………….
  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Kisarawe
  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International wameishauri Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) kuongeza walimu waliobobea katika ufundishaji wa wanafunzi walemavu ili kuhakikisha wanapata elimu sawa na wengine. 

  Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) – Tanzania, Simon Ndembeka baada ya kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaohitaji kupatiwa elimu ya ufundi katika vyuo hivyo. 

  Meneja Mradi amesema kuwa nyakati za kuwaficha walemavu majumbani zimekwisha na kwa sasa wazazi wanafahamu kuwa ulemavu sio mwisho wa maisha hivyo muamko wa walemavu wanaohitaji kusoma umekuwa mkubwa tofauti na zamani. 

  “Mradi huu umetenga asilimia 10 kwa ajili ya jamii ya vijana wenye ulemavu kupatiwa mafunzo ya ufundi katika chuo cha VETA ili baadae waweze kuendesha maisha yao lakini lengo hilo lina changamoto kubwa ya upungufu wa walimu wa taaluma hiyo hivyo, tunaishauri VETA kuongeza walimu wa aina hiyo ili kukidhi uhitaji wa idadi ya wanafunzi walemavu”, alisema Ndembeka. 

  Ndembeka ameongeza kuwa kitendo cha kuwawezesha vijana wenye ulemavu ni moja ya lengo la mradi huo kwani kundi hilo ndilo kundi lenye changamoto nyingi za kimaisha kuliko kundi lingine lolote hivyo kuwapatia elimu kutawasaidia kuweza kupata ajira au kujiajiri na hatimaye kuweza kuyakomboa maisha yao. 

  Aidha, Ndembeka ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wao wa kutoa misaada ya mikopo, elimu, maeneo ya vijana kufanyia mazoezi pamoja na ushiriki wao kama wageni rasmi katika mahafali mbalimbali za vijana wanaohitimu elimu ya ufundi chini ya mradi huo. 

  Kuhusu suala la kuwasaidia vijana kupata ajira amefafanua kuwa mara nyingi wamekuwa wakifanya vikao na waajiri wa sekta mbalimbali nchini ili kuwajengea ufahamu waajiri juu ya uwepo wa vijana hao pamoja na kujadili jinsi ya kuwasaidia kwa kuwapatia ajira. 

  Mradi huo wa miaka mitatu unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

  0 0


  Timu ya Serengeti Boys (Tanzania),katika kipindi cha kwanza ilikuwa ikiongoza  goli 2-0 ,ambapo mnamo dakika ya 40 na 42 mchezaji Yohana Oscar Mkomola aliipatia timu yake magoli mawili dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaonendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar,ambapo Brazzaville wamejipatia goli la kwanza kipindi cha pili na mpira unaendelea.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.MPaka sasa Serengeti boys wanaongoza goli 2-1 dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaondelea hivi sasa,uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Mashabiki wakimshangilia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola mara baada ya kufungua goli la pili dhidi ya timu ya Congo Brazaville.


  Mchezaji wa timu ya Congo Brazzaville Ngumbi Exau akiruka hewani kumzuia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola asiondoke na mpira.
  Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionesha kiu kubwa ya kutaka kupata magoli mapema,kila timu ilikuwa ikishambulia lango la mwenzake kwa spidi kubwa,mpaka sasa timu ya Srengeti Boys iko mbele goli 2-1 dhidi ya Congo Brazzavile.

  0 0

  Mnamo kipindi cha pili mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Issa Abdi Makamba anaipatia goli la 3 dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.Mpaka sasa Serengeti Boys wanaongoza goli 3-2 na mpira bado unaendelea,uwanja wa Taifa jijini Dar.

  Timu ya Serengeti Boys (Tanzania),katika kipindi cha kwanza ilikuwa ikiongoza  goli 2-0 ,ambapo mnamo dakika ya 40 na 42 mchezaji Yohana Oscar Mkomola aliipatia timu yake magoli mawili dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaonendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar,ambapo Brazzaville wamejipatia goli la pili kipindi cha pili na mpira unaendelea.Mpaka sasa Serengeti boys wanaongoza goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile,goli la tatu limefungw ana mchezaji Issa Abdi Makamba.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.MPaka sasa Serengeti boys wanaongoza goli 3-2 dhidi ya timu ya Congo Brazzaville,katika mchezo unaondelea hivi sasa,uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Mashabiki wakimshangilia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola mara baada ya kufungua goli la pili dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.


  Mchezaji wa timu ya Congo Brazzaville Ngumbi Exau akiruka hewani kumzuia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola asiondoke na mpira.
  Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionesha kiu kubwa ya kutaka kupata magoli mapema,kila timu ilikuwa ikishambulia lango la mwenzake kwa spidi kubwa,mpaka sasa timu ya Srengeti Boys iko mbele goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile.   

  0 0

  Mpaka dakika 90 za mchezo.
  Mnamo kipindi cha pili mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Issa Abdi Makamba anaipatia goli la 3 dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.Mpaka mpaka dakika 90 za mchezo,timu ya Serengeti Boys wameibuka washindi kwa kuiburuza timu ya Congo Brazzavile 3-2 ,uwanja wa Taifa jijini Dar.

  Timu ya Serengeti Boys (Tanzania),katika kipindi cha kwanza ilikuwa ikiongoza  goli 2-0 ,ambapo mnamo dakika ya 40 na 42 mchezaji Yohana Oscar Mkomola aliipatia timu yake magoli mawili dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaonendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar,ambapo Brazzaville wamejipatia goli la pili kipindi cha pili.Serengeti boys wameifunga Congo Brazzavile goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile,goli la tatu limefungw na mchezaji Issa Abdi Makamba.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.MPaka sasa Serengeti boys wanaongoza goli 3-2 dhidi ya timu ya Congo Brazzaville,katika mchezo unaondelea hivi sasa,uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Mashabiki wakimshangilia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola mara baada ya kufungua goli la pili dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.


  Mchezaji wa timu ya Congo Brazzaville Ngumbi Exau akiruka hewani kumzuia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola asiondoke na mpira.
  Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionesha kiu kubwa ya kutaka kupata magoli mapema,kila timu ilikuwa ikishambulia lango la mwenzake kwa spidi kubwa,mpaka dakika 90 za mchezo timu ya Srengeti Boys imeibuka kwa ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile.   

  0 0
 • 09/19/16--03:13: BEI YA MADAFU UBAONI LEO


 • 0 0

   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),akiwapungia baadhi ya Wananchi,akiwa ameambatana na katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia kwa Rais) wakielekea kwenye ofisi za kampuni ya kuchapisha Magazeti ya Uhuru Puplication Limited wanaochapisha magaezeti ya Uhuru,Mzalendo,Burudani na redio ya Uhuru FM,mapema leo jijini Dar.PICHA ZAIDI ZINAKUJA

  0 0  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame M. Mbarawa(Mb), amemteua Dkt. Musa Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). 

  Dkt. Mgwatu amechukua nafasi ya Mhandisi Marcellin Magesa  ambaye amepangiwa majukumu mengine  Wizarani.

  Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mgwatu alikuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO).

  Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amemteua Bw. Masanja Kadogosa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa RAHCO.
  Uteuzi huo unaanza mara moja.
  Imetolewa na
  Eng. Joseph M. Nyamhanga
  Katibu Mkuu (Ujenzi)
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

   Afisa Maendeleo ya Jamii – Kata ya Vingunguti, wilayani Temeke Pius Majura akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi katika Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE).
  Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali iliyopo wilayani Temeke, Engerasia Lyimo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) ulivyowanufaisha vijana katika kata hiyo.    Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) unaofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) umeisaidia Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kupunguza idadi ya wahalifu kwa kuwapatia vijana elimu ya mafunzo ya ufundi inayowawezesha kuendesha maisha yao.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Maendeleo ya Jamii – Kata ya Vingunguti, Pius Majura alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi katika Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) chini ya mradi huo.

  Majura amesema kuwa mradi huo umewasaidia vijana wa eneo hilo kuacha kufanya uhalifu na badala yake wamejikita katika shughuli za halali ambazo zinawasaidia kupata kipato cha kuwawezesha kuendesha maisha yao.

  “Kabla ya mradi huu kuanza vijana wengi walikuwa wakijihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya na wasichana wengi walikua wakifanya biashara za kuuza miili yao, madanguro yalikuwa mengi lakini baada ya vijana kupatiwa elimu na wengine kuweza kujiajiri na kuajiriwa, uhalifu umepungua kwa asilimia kubwa”, alisema Majura.

  Afisa huyo ameongeza kuwa Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupunguza utegemezi kwa kuwasaidia vijana na wanawake kuweza kusimama wenyewe kwa kufanya shughuli zao mbalimbali hivyo, wametenga fungu la fedha kwa ajili ya makundi hayo ili kuhakikisha wanajikwamua wao binafsi pamoja na taifa kwa ujumla.

  Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali iliyopo wilayani humo, Engerasia Lyimo amesema kuwa mradi huo umewafanya vijana wajielewe na kujitambua wao ni kina nani pia umepunguza idadi ya watoto wa mitaani waliokuwa wakirandaranda bila kuwa na shughuli maalum hali iliyokuwa ikiwapelekea kujiingiza katika makundi ya uhalifu.

  Ametoa rai kwa Shirika la Plan International kupanua wigo wa maeneo wanayoyasaidia kwani bado kuna kata nyingi za wilaya hiyo hazijapata fursa za kuingizwa katika mradi huo.

  Mradi huo wa miaka mitatu unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

  0 0

    Baadhi ya watoto wa Shule ya awali ya Yohane Merlin wakiwa wamefika katika ziara yao ya kujifunza na kufanya kwa vitendo kuogelea na mambo mengine ikiwa ni pamoja na Kucheza Michezo mbalimbali
   Watoto wa Shule ya Awali ya Yohane Merlin wakiwa wanacheza na kufurahi katika maji
   Baadhi ya watoto wakiwa wamepumzika kwa muda baada ya kucheza katika maji
   Mwenyekiti wa Shule ya awali ya Yohane Merlin iliyopo Mbezi Beach David Manoti (wa nne kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wazazi na Mmoja wa walimu wakati wa ziara hiyo ya mafunzo
    Watoto wa Shule ya awali ya Yohane Merlin wakiogelea kila mmoja kwa aina yake walipokuwa katika ziara ya kujifunza na kufanya michezo mbalimbali
   Mwenyekiti  Shule ya Awali ya Yohane Merlin David Manoti akicheza na watoto
   watoto wa Shule ya Awali ya Yohane Merlin wakipata maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa shule hiyo David Manoti
   Watoto wa Shule ya Awali ya Yohane Merlin wakiendelea na michezo mbalimbali
   Watoto wa Shule ya Awali ya Yohane Merlin wakipata chakula baada ya kumaliza Ziara yao ya Masomo
  Kutoka kushoto ni  Mwalimu Mkuu wa Shule ya awali ya Yohane Merlin Sr. Jenesia Thomas Baraka,Mwenyekiti wa Kamati ya Shule David Manoti, Makamu Mwenyekiti Michael Biseko na Mjumbe wa kamati Bi. Mwile Kauzeni.
   Baadhi ya Walimu, Wazazi pamoja na wanakamati wa Shule ya Awali ya Yohane Merlin wakiwa katika picha ya pamoja
   Baadhi ya wazazi na walimu wakiwa katika Michezo ya watu wazima wakiungana na wanafunzi hao wa shule ya awali ya  Yohane Merlin
   Hili ni Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni ambapo watoto wa shule ya awali ya Yohane Merline(hawapo pichani) walipata kuliona wakati wa ziara yao ya kujifunza na michezo.

  Picha na Fredy Njeje.


older | 1 | .... | 975 | 976 | (Page 977) | 978 | 979 | .... | 1903 | newer