Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel

Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels

Showcase

Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 976 | 977 | (Page 978) | 979 | 980 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akifungua mafunzo ya Mwongozo wa Uwekezaji na Usimamizi wa Miradi ya Umma yanayoendelea katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya. Kushoto kwake ni Mhandisi Happiness Mgalula Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma na Dkt. Joihn Mduma, Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi ni Dkt. Lorah Madete, Kaimu Nibu Katibu Mtendaji, anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla.
   
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgani rasmi (hayumo pichani)
  Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe, Iringa na Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi

  0 0

  Na Ismail Ngayonga
  MAELEZO
  Dar Es Salaam.

  SEKTA  ya kilimo inayojumuisha ukulima, ufugaji na uvuvi, imeendelea kuwa sekta kiongozi. katika kutoa ajira na kuwa tegemeo la maisha kwa asilimia 75 ya Watanzania wanaoishi Vijijini.

  Kujitosheleza kwa chakula ni muhimu kwa usalama na utulivu wa nchi. Taarifa ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonyesha kuwa kiwango cha kujitegemea kwa chakula kimeongezeka kutoka asilimia 95 mwaka 2005 hadi asilimia 125mwaka 2014.

  Pamoja na uzalishaji kuwa mkubwa, inaelezwa kuwa kiasi kikubwa cha mazao ya nafaka yanayozalishwa nchini  huharibika na kupotea baada ya kuvunwa. Upotevu huo hutokana na matumizi ya mbinu duni za kuhudumia mazao wakati wa uvunaji, usafirishaji na uhifadhi kwenye maghala.
   
  Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka na asilimia 80 ya nafaka huzalishwa na kuhifadhiwa vijijini, ambapo hata hivyo uwezo mdogo na maghala duni yanayotumiwa na wakulima vijijini wakati wa kuhifadhi huruhusu upotevu wa nafaka hadi asilimia 10.
   
  Takwimu za Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) zinaonyesha kuwa, asilimia 30 hadi 40 za nafaka zinazovunwa hupotea kila mwaka nchini.
   
  Mahindi ni miongoni mwa  mazao makuu ya nafaka hapa nchini yanayolimwa nchini Huzalishwa kwa wastani wa tani 2,393,000 kwa mwaka ambao ni sawa na asilimia 63 ya mazao yote ya nafaka.

  Takwimu za Wizara ya Kilimio, Mifugo na Uvuvi zinaonyesha uzalishaji wa mahindi unaongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 2011 uzalishaji wa mahindi katika nchi nzima ulifikia tani 4,341, mwaka 2012 tani 5,104 na mwaka 2013 tani 5,174.

  Taarifa kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi zinaeleza kuna uwezekano mkubwa wa kuharibika kwa tani 40,000 za mahindi yanayoendelea kununuliwa katika msimu huu na Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kutokana na uhaba wa maghala ya kuhifadhi.
   
  Wakala katika mikoa hiyo anakabiliwa na changamoto ya uwezo mdogo wa kuhifadhi chakula hicho katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mahindi na kusababisha akiba kubwa ya chakula kuhifadhiwa nje ya maghala.

  Utafiti uliofanywa na mradi wa USAID Tuboreshe Chakula umebaini kuwa kutokana na uhifadhi duni na mbinu bora za kilimo cha mazao ya nafaka kama mahindi, alizeti na maharage unasababisha ukungu kwenye mazao hayo  hali inayosababisha sumu kuvu yenye madhara makubwa kwa mlaji.

  Mhadhiri Mwandamizi wa chuo kikuu cha sayansi cha Nelson Mandela, Dk. Martin Kimanya anasema sumu hiyo haiwezi kuondolewa kwa kupika chakula na badala yake watumiaji wanapaswa kuchagua nafaka kwa kuondoa zile ambazo zimebadilika rangi na kuwa na ukungu.

  “Wakati Tanzania ikiwa katika nafasi ya nne kwa ulizalishaji wa zao la mahindi barani Afrika, imeelezwa kuwa watumiaji wa mahindi wanakula 30% ya sumu kuvu inayotokana na uhifadhi duni wa mahindi” anasema Prof Kimanya.

  Kutokana na tatizo hilo mradi wa USAID tuboreshe chakula umeanza mikakati ya kuinusuru jamii ikiwemo kwa kutoa elimu kwa wasindikaji wa vyakula pamoja na wakulima ili kufahamu sumu kuvu na madhara yake.

  Katika  kuongeza na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula nchini, Serikali kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula Nchini (NFRA) imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi.
   
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasema Serikali imejipanga katika kuondoa tatizo la upungufu wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya kuhifadhi chakula katika maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu wa chakula.
   
  “Serikali  kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa na kwa sasa ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya ” anasema Majaliwa
   
  Aidha Majaliwa anasema Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.
   
  Anasema maghala yanakayojengwa si kwa ajili ya kuhifadhi chakula tu bali hata kuweka dawa kwa urahisi, kukausha, kuondoa unyevunyevu na kusafisha kwa kiwango kinachohitajika.
   
  Waziri Mkuu anasema kuwa anasema ujenzi wa magahala hayo utaliongezea taifa uwezo wa kuhifadhi chakula tofauti na hali ilivyo sasa.

  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba  anasema Serikali imeiagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA)  kununua mahindi moja kwa moja kutoka  kwa wakulima na kuachana na mfumo wa zamani ambapo wakulima walikuwa wakipeleka mahindi kwenye wakala huo au kupitia kwa wanunuzi binafsi.

  Kwa mujibu wa Waziri Tizeba anasema mkulima atauza kuanzia tani moja hadi mbili na kiwango cha mwisho cha ununuzi kufanywa na NFRA  ni tani tano.

  Aidha Dkt. Tizeba anasema  serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya ununuzi wa mahindi kutoka kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.

  Mary Sheto kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi anasema Serikali imeweka mikakati madhubuti kwa ajili ya kuwasaidia wananchi maskini waliopo  vijijini ambao asilimia 98 hutegemea kilimo kama njia kuu ya uchumi na maisha yao ya kila siku.

  Anasema lengo la Serikali ni kuzalisha tani milioni tano za mahindi ili nchi ijitosheleze kwa chakula kwa nia ya kupunguza mfumuko wa bei ya chakula na kuongeza kipato kwa mkulima hatimaye kukuza uchumi  na kuuza ziada ndani na nje ya nchi ambako imebainika kuwa na soko kubwa la mazao hayo.

  Kwa mujibu wa Sheto anasema Serikali imefanya mazungumzo na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa ajili ya ununuzi wa mahindi hayo na wameonesha kukubali, lakini kwa masharti ya kuzingatia ubora wa mahindi husika.

  “Kwa kuzingatia hilo, Serikali katika wilaya ambazo zitaanzishiwa utaratibu huo, wakulima wataelekezwa namna ya kuandaa zao hilo kwa ubora unaotakiwa kisha kuwahimiza kuwa katika vikundi huko huko vijijini ambako ununuzi utafanyika” anasema Sheto.

  Akifafanua zaidi Sheto anasema Serikali itahakikisha maghala mapya yanajengwa na yale ya zamani yataboreshwa kwa kukarabatiwa, ili mahindi yawe katika mazingira safi kwa lengo la kumvutia mnunuzi atakayenunua zao hilo katika soko la pamoja la wakulima.

  Anaitaja Mikoa itakayofaidika na mpango huo kuwa ni Rukwa /Katavi, Ruvuma, Njombe na Iringa, mikoa ya Kanda ya Ziwa, Dodoma na lingine katika mikoa ya Tanga/Arusha na Kilimanjaro.

  0 0

  Daraja la Lumesule likiwa katika hatua ya ujenzi katika barabara ya Mangaka – Lumesule – Nakapanya (70.5km).

  Sehemu ya barabara iliyo kamilika kwa kiwango cha lami ya Namtumbo – Tunduru.
  Sehemu ya barabara iliyo katika hatua ya awali ya ujenzi ya barabara ya Namtumbo – Tunduru kwa kiwango cha lami: Lot 2: Kilimesera – Matemanga section (68.2 km).

   Barabara ya Mangaka – Mtambaswala (65.5km) iliyo katika hatua za mwisho kukamilika kwa kiwango cha lami.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga- MAELEZO.
  SEKTA  ya kilimo inayojumuisha ukulima, ufugaji na uvuvi, imeendelea kuwa sekta kiongozi katika kutoa ajira na kuwa tegemeo la maisha kwa asilimia 75 ya Watanzania wanaoishi Vijijini.

  Kujitosheleza kwa chakula ni muhimu kwa usalama na utulivu wa nchi. Taarifa ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonyesha kuwa kiwango cha kujitegemea kwa chakula kimeongezeka kutoka asilimia 95 mwaka 2005 hadi asilimia 125 mwaka 2014. 

  Pamoja na uzalishaji kuwa mkubwa, inaelezwa kuwa kiasi kikubwa cha mazao ya nafaka yanayozalishwa nchini  huharibika na kupotea baada ya kuvunwa. Upotevu huo hutokana na matumizi ya mbinu duni za kuhudumia mazao wakati wa uvunaji, usafirishaji na uhifadhi kwenye maghala.

  Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka na asilimia 80 ya nafaka huzalishwa na kuhifadhiwa vijijini, ambapo hata hivyo uwezo mdogo na maghala duni yanayotumiwa na wakulima vijijini wakati wa kuhifadhi huruhusu upotevu wa nafaka hadi asilimia 10.

  Takwimu za Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) zinaonyesha kuwa, asilimia 30 hadi 40 za nafaka zinazovunwa hupotea kila mwaka nchini.

  Mahindi ni miongoni mwa  mazao makuu ya nafaka hapa nchini yanayolimwa nchini Huzalishwa kwa wastani wa tani 2,393,000 kwa mwaka ambao ni sawa na asilimia 63 ya mazao yote ya nafaka.

  Takwimu za Wizara ya Kilimio, Mifugo na Uvuvi zinaonyesha uzalishaji wa mahindi unaongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 2011 uzalishaji wa mahindi katika nchi nzima ulifikia tani 4,341, mwaka 2012 tani 5,104 na mwaka 2013 tani 5,174.

  Taarifa kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi zinaeleza kuna uwezekano mkubwa wa kuharibika kwa tani 40,000 za mahindi yanayoendelea kununuliwa katika msimu huu na Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kutokana na uhaba wa maghala ya kuhifadhi.

  Wakala katika mikoa hiyo anakabiliwa na changamoto ya uwezo mdogo wa kuhifadhi chakula hicho katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mahindi na kusababisha akiba kubwa ya chakula kuhifadhiwa nje ya maghala.

  Utafiti uliofanywa na mradi wa USAID Tuboreshe Chakula umebaini kuwa kutokana na uhifadhi duni na mbinu bora za kilimo cha mazao ya nafaka kama mahindi, alizeti na maharage unasababisha ukungu kwenye mazao hayo  hali inayosababisha sumu kuvu yenye madhara makubwa kwa mlaji.

  Mhadhiri Mwandamizi wa chuo kikuu cha sayansi cha Nelson Mandela, Dk. Martin Kimanya anasema sumu hiyo haiwezi kuondolewa kwa kupika chakula na badala yake watumiaji wanapaswa kuchagua nafaka kwa kuondoa zile ambazo zimebadilika rangi na kuwa na ukungu.

  “Wakati Tanzania ikiwa katika nafasi ya nne kwa ulizalishaji wa zao la mahindi barani Afrika, imeelezwa kuwa watumiaji wa mahindi wanakula 30% ya sumu kuvu inayotokana na uhifadhi duni wa mahindi” anasema Prof Kimanya.

  Kutokana na tatizo hilo mradi wa USAID tuboreshe chakula umeanza mikakati ya kuinusuru jamii ikiwemo kwa kutoa elimu kwa wasindikaji wa vyakula pamoja na wakulima ili kufahamu sumu kuvu na madhara yake.

  Katika  kuongeza na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula nchini, Serikali kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula Nchini (NFRA) imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasema Serikali imejipanga katika kuondoa tatizo la upungufu wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya kuhifadhi chakula katika maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu wa chakula.

  “Serikali  kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa na kwa sasa ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya ” anasema Majaliwa

  Aidha Majaliwa anasema Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.

  Anasema maghala yanakayojengwa si kwa ajili ya kuhifadhi chakula tu bali hata kuweka dawa kwa urahisi, kukausha, kuondoa unyevunyevu na kusafisha kwa kiwango kinachohitajika.

  Waziri Mkuu anasema kuwa anasema ujenzi wa magahala hayo utaliongezea taifa uwezo wa kuhifadhi chakula tofauti na hali ilivyo sasa.

  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba  anasema Serikali imeiagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA)  kununua mahindi moja kwa moja kutoka  kwa wakulima na kuachana na mfumo wa zamani ambapo wakulima walikuwa wakipeleka mahindi kwenye wakala huo au kupitia kwa wanunuzi binafsi.

  Kwa mujibu wa Waziri Tizeba anasema mkulima atauza kuanzia tani moja hadi mbili na kiwango cha mwisho cha ununuzi kufanywa na NFRA  ni tani tano.

  Aidha Dkt. Tizeba anasema  serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya ununuzi wa mahindi kutoka kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini. 

  Mary Sheto kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi anasema Serikali imeweka mikakati madhubuti kwa ajili ya kuwasaidia wananchi maskini waliopo  vijijini ambao asilimia 98 hutegemea kilimo kama njia kuu ya uchumi na maisha yao ya kila siku. 

  Anasema lengo la Serikali ni kuzalisha tani milioni tano za mahindi ili nchi ijitosheleze kwa chakula kwa nia ya kupunguza mfumuko wa bei ya chakula na kuongeza kipato kwa mkulima hatimaye kukuza uchumi  na kuuza ziada ndani na nje ya nchi ambako imebainika kuwa na soko kubwa la mazao hayo.

  Kwa mujibu wa Sheto anasema Serikali imefanya mazungumzo na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa ajili ya ununuzi wa mahindi hayo na wameonesha kukubali, lakini kwa masharti ya kuzingatia ubora wa mahindi husika.

  “Kwa kuzingatia hilo, Serikali katika wilaya ambazo zitaanzishiwa utaratibu huo, wakulima wataelekezwa namna ya kuandaa zao hilo kwa ubora unaotakiwa kisha kuwahimiza kuwa katika vikundi huko huko vijijini ambako ununuzi utafanyika” anasema Sheto.

  Akifafanua zaidi Sheto anasema Serikali itahakikisha maghala mapya yanajengwa na yale ya zamani yataboreshwa kwa kukarabatiwa, ili mahindi yawe katika mazingira safi kwa lengo la kumvutia mnunuzi atakayenunua zao hilo katika soko la pamoja la wakulima.

  Anaitaja Mikoa itakayofaidika na mpango huo kuwa ni Rukwa /Katavi, Ruvuma, Njombe na Iringa, mikoa ya Kanda ya Ziwa, Dodoma na lingine katika mikoa ya Tanga/Arusha na Kilimanjaro.

  0 0

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa maofisa wa jeshi toka China ukiongozwa na Mkuu wa Ugavi wa jeshi hilo Luteni Jenerali liu Shengjie mara baada ya kumtembelea ofisini kwake makao makuu ya jeshi jana jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) akipokea zawadi ya nembo ya jeshi la China kutoka kwa Mkuu wa tawi la ugavi wa China Luteni Jenerali Liu Shengjie alipomtembelea  ofisini kwake jana makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa tawi la Ugavi wa jeshi la china Luteni Lenerali Liu Shengjie akipokea zawadi ya nembo ya JWTZ  kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) alipomtembelea  ofisini kwake jana makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam.(Picha na  Luteni Selemani Semunyu)

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasilikiliza wafanyakazi wa UPL alipowasili katika ofisi hizo leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

  Mkuu wa Kitengo cha kompyuta, wa UPL, Moses Makambi akimpatia maelezo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipoingia chumba cha Usanifu wa kurasa,
  Mkuu wa Kitengo cha kompyuta, wa UPL, Moses Makambi akimpatia maelezo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipoingia chumba cha Usanifu wa kurasa,

  Mkuu wa Kitengo cha kompyuta, wa UPL, Moses Makambi akimpatia maelezo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipoingia chumba cha Usanifu wa kurasa, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

  Kaimu Mharuri Mtendaji wa UPL. Ramadhani Mkoma akiongoza Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuingia katika chumba cha habari kuzungumza na wafanyakazi

  Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiingia katika chumba cha Habari cha Uhuru Publications kuzungumza na wafanyakazi

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpatia maelezo ya utangulizi, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji, wa UPL Ramadhani Mkoma

  Wafanyakazi wakiwa ukumbini

  Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini mazungumzo yao na Rais Dk. Magufuli .

  Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuliu akiandika wakati Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Ramadhani Mkoma akieleza changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika utendaji kazi wao wa kila siku

  Baadhi ya wafanyakazi wakishangilia baada ya Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli kuahidi kushughulikia kero zao kwa nafasi yake ya Ueneyekiti wa CCM.
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Magufuli akimsikiliza Kaimu Mhasibu Mkuu wa UPL huku akinukuu dondoo muhimu

  Mwenyekiti wa Chama Cha Wafayakazi wa UPL cha RAAWU, Moses Makambi akieleza changamoto kwa Dk. Magufuli

  Ukumbi wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa UPL na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Magufuli
  Katibu Mkuu wa CCM, akimfafanulia jambo Dk. Magufuli

  Wafanyakazi wakiwa wametulia kufuatilia alichokuwa akisema, Dk Magufuli

  Dk. Magufuli akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL

  Mfayakazi wa UPL Fred Majaliwa akieleza kero anazooma zinakwamisha utendaji wa kazi za UPL
  Rhoda Kangero kutoka Idara ya Rasilimali watu, akieleza kero na changamoto
  Wafanyakazi wa UPL wakimuombea dua Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiondoka ofisi za UPL baada ya kuzungumza na wafanyakazi leo Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na watatu kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshauri jambo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli nje ya Ofisi za UPL. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi kabla ya kuondoka baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa UPL

  Wafanyakzi wa UPL wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli wakati akiondoka

  Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, wakati akitoka Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, katika Mtaa huo, kwenda Ofisi za Kampuni ya Uhuru Publications Limited, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani leo. Dk. Magufuli alifika katika ofisi yake leo kufanya kazi zake za kichama kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa CCM.

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akifuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili katika Ofisi za Uhuru Publications Limited mtaa wa Lumumba, Da es Salaam, ambako baada ya kutembelea baadhi ya ofusi za kampuni hiyo alizungumza na wafanyakazi ambapo ameahidi kutatua kero zinazowakabili kwa muavuli wake wa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

  ZIFUATAZO NI SHAMRASHAMRA ZA WAFANYAKAZI WA UPL, BAADA YA UJIO WA DK. MAGUFULI KATIKA OFISI ZAO LEO

  PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Na Ally Daud-Maelezo.

  MAUZO katika Soko la Hisa Dar es salaam (DSE) yameshuka kwa asilimia 81 kutoka Tsh. Bilioni 9 mpaka kufikia shilingi bilioni 1.7 kutokana na kushuka kwa idadi ya uuzaji wa hisa kufikia shilingi 340,000 kwa wiki hii.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa Mwandamizi wa masoko wa DSE Bi. Mary Kinabo amesema kuwa mauzo hayo yameshuka kutokana na ukubwa wa mtaji wa soko kushuka kwa asilimia 2.79 kutoka trilioni 21.3 kufikia trilioni 20.7.

  Aidha  Bi. Mary amesema kuwa ukubwa wa mtaji kutoka makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha shilingi trilioni 8.2 kutoka wiki iliyopita.

  Bi. Mary amesema kuwa licha ya idadi ya mauzo kushuka pia  Benki ya CRDB imeshika nafasi ya kwanza katika kuuza na kununua hisa kwa asilimia 53 ikifuatiwa na kampuni ya Bia nchini TBL kwa asilimia 35 huku kampuni ya Swissport ikishika nafasi ya tatu ya kununua hisa kwa asilimia 3.

  Mbali na hayo Bi. Mary amesema kuwa licha ya viashiria vya soko kushuka kwa alama 36.6 baada ya bei za hisa kutoka TBL kushuka kwa silimia 1.08,  viashiria vya huduma za kibenki na kifedha vimepanda kwa alama 3.64 baada ya mauzo ya DSE kupanda kwa asilimia 11.5.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta anayeendelea kupata matibabu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mke wa Mzee Sitta, Mama Margaret Sitta. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam
   Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta akiongoza Sala mara baada ya kujuliwa hali na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Kushoto ni Mke wa Mzee Sitta, Mama Margaret Sitta.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wafanyakazi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Magazeti hayo zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wafanyakazi hao wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakwaza (kulia) pamoja na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti hayo Ramadhani Mkoma wakwanza (kushoto) wakiomba dua mara baada ya kumaliza kuzungumza na wafanyakazi hao jijini Dar es Salaam.

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali kama ifuatavyo;
  Kwanza,Rais Magufuli amemteua Prof. Jacob Philip Mtabaji kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuanzia tarehe 15 Septemba, 2016.

  Prof. Jacob Philip Mtabaji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Awadhi Mawenya ambaye uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Kamisheni ya TCU kuvunjwa.

  Pili,Rais Magufuli amemteua Prof. Mathew L. Luhanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe (MU) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Prof. Mathew L. Luhanga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Daniel Mkude ambaye amemaliza muda wake.

  Tatu,Rais Magufuli amemteua Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake.

  Nne,Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudensia M. Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.Bi. Gaudensia M. Kabaka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Augustine Mahiga ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Tano,Rais Magufuli amemteua Bi. Mariam Mwafisi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia 05 Septemba, 2016.

  Bi. Mariam Mwafisi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Deogratias Ntukamazina ambaye amemaliza muda wake.

  Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Hetson Msalale Kipsi kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  19 Septemba, 2016

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick akitunuku zawadi kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao. Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa asakari waliofanya vizuri wakati wa kutekeleza majukumu yao. Pikipiki mbili aina ya Fekon zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai kusaidia jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick akiwa ameketi juu ya pikipiki na kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Mwandamizi Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa askari 34 wa jeshi hilo mjini Moshi.Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick akitoa cheti kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akitambua mchango wa wadau kwa jeshi la Polisi.

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali waliotekeleza vyema majukumu yao.kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Wilbroad Mutafungwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidick akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mjini Moshi kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidick akihitimisha ukaguzi wakati wa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza asakari walitekeleza vyema majukumu yao. Gwaride likitoka kwa mwendo wa haraka mara baada ya kumalizika kwa ukaguzi. Ofisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 wa jeshi hilo waliotekeleza vyema majukumu yao.Baadhi ya maofisa wa jeshi la Polisi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuoneesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick baadhi ya silaha zilizokamatwa hivi karibuni zikidaiwa kutumika katika vitendo vya uharifu. Mkuu wa Kitengo cha dawa za kulevya cha jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Mkaguzi wa Polisi,Ezekiel Midala akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro sehemu ya dawa za kulevya zilizokamatwa na jeshi hilo.Baadhi ya askari waliotunukuwa zawadi kwa utendaji kazi mzuri wakisonga mbele kwa ajili ya kutunukiwa zawadi.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein akipata maelezo yautendaji kazi, kwa msaidizi Mkuu wa utangazaji ZBC Radio Salum Othman Said alipofanya ziara kuona utendaji kazi zao.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein akizungumza na watangazaji wa ZBC Radio katika Studio za Shrika hilo Raha leo mjini Zanzibar. 
   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Muhamed Shein (katikati) katika picha ya pamoja na Watangazaji wa ZBC Radio.
  Mtangazaji wa ZBC Radio Fatma Said akifanya mahojiano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein katika Studio za ZBC ambapo Dkt. Shein amefanya ziara katika Shirika hilo. Picha na Yusuf Simai /Maelezo Zanzibar.

  0 0
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, alipofanya ziara kwenye makazi ya askari ya kigoto yalipopo Kata ya kirumba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza hii leo.

  Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

  Wizara ya Mambo ya Ndani nchini imeahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazovikabili vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo uhaba wa makazi na sale za askari ili kufanikisha vyombo hivyo kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa.

  Waziri anayeshughulikia wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, ametoa agizo hilo hii leo kwenye kikao baina yake na viongozi mbalimbali wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, kilichofanyika kwenye gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza.

  Amesema jitihada za ujenzi wa nyumba za ghorofa kwa ajili ya makazi ya askari katika miji mikuu ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam zitaenda sambamba na ujenzi wa nyumba za kawaida katika wilaya mbalimbali nchini ili kutatua kero hiyo.

  Katika hatua nyingine, Waziri Nchemba ametoa onyo la kukamatwa wale wote wanaotoa kejeli kwenye mitandao ya kijamii juu ya utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini pamoja na askari wanaopata madhara wakipambana na uhalifu, kama ilivyotokea katika tukio la mauaji ya askari lililotokea hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

  Awali Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amebainisha baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na ukosefu wa makazi ya askari, uhaba wa fedha pamoja na madeni ya askari, ambazo zikifanyiwa kazi zitaboboresha zaidi utendaji wa jeshi hilo.

  Waziri Nchemba amefanya ziara ya siku moja mkoani Mwanza, akitokea mkoani Kagera alikoenda kujionea uhalibifu uliotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwanzoni mwa mwezi huu na kuzungumza na watendani mbalimbali wa taasisi za wizara yake, ambapo ametembelea makazi ya askari ya Kigoto na gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza, kabla ya kuendelea na ziara yake hapo kesho mkoani Mara.
  Mkuu wa Kituo cha Polisi Kirumba Ilemela Jijini Mwanza (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba (kulia) kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza. Katikati ni Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
  Maofisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kwenye makazi ya skari Kigoto Jijini Mwanza hii leo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akiwa amembeba mmoja wa watoto kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

  Afisa wa polisi akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
  Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmad Msangi, akizungumza kwenye kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

  Baadhi ya Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye kikao baina yao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japani nchini, Mheshimiwa Masaharu Yoshinda ambaye amemueleza kwamba Serikali yake ipo tayari kukarabati shule zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
               
  Pia imeomba kupatiwa orodha ya mahitaji ya dharura yakiwemo mahema, mablanketi, dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo.

  Balozi Yoshinda ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 19, 2016) wakati alipokutana na Waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya maafa yalitokea Kagera.

  Kwa upande wake Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Japani kwa hatua hiyo na kukiagiza Kitengo cha Maafa kilicho chini ya Ofisi yake kuwasiliana na Ubalozi wa Japan nchini na kuwasilisha orodha ya shule zilizoharibika pamoja na mahitaji ya dharura.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amepokea msaada wa tani 2.5 za mchele, magodoro 200, mablanketi 100 na fedha taslimu sh. milioni 10 ili kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko hilo.

  Msaada huo umetolewa na wadau mbalimbali akiwemo Ofisa Utumishi wa Kampuni ya Chang Qing Inernational Investiment Limited ya nchini, Bi. Anna Jiang aliyetoa magodoro 200 yenye thamani ya sh. milioni sita.

  Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, George Shumbusho aliyetooa sh. milioni 10 pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki kati ya Serikali ya Tanzania na China, Bw. Joseph Kahama aliyetoa mchele tani 2.5 pamoja na mabllanketi 100 vyote vikiwa na thamani y ash. milioni 10.

  Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.

  Tetemeko hilo lilitokea Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 wametibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.

  Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba  2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakiiitaji misaada mbalimbali.

   IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMATATU, SEPTEMBA 19, 2016

  0 0

  Waziri Mkuu, Kaassim Majliwa akipokea msaada wa mgodoro 200 yenye thamani ya sh. 6, 000,000 kutoka kwa Bi. Anna Jiang wa Kampuni ya Chang Qing Inernational Investiment Limited ya nchini ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwake jijjini Dar es salaam Septemba 19, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya EXIM, Bw. George Shumbusho (watatu kulia) ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 19, 2016. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki hiyo, Fredrick Kanga, wapili kushoto ni Chief Finance Officer wa benki hiyo, Selemani Ponda na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa benki ya Exim, Abdul Nkondo. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Msaada wa tani mbili na nusu za mchele na mablanketi 100 vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10 ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Septemba 19, 2016. Kulia ni Meneja wa Uwekezaji wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation, Bw. Le Tong, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Urafiki Kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama, na wapili kushoto ni Afisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Nice Munissy. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Na. Abushehe Nondo na Immaculate Makilika- MAELEZO

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman amesema kuwa Serikali inatarajia kuzindua mpango mkakati wa Mahakama ya Tanzania kwa miaka 5 unaolenga kuboresha huduma za kimahakama nchini.

  Aidha Jaji Mkuu alisema uzinduzi wa mpango huo utaenda sambamba na mradi wa maboresho wa huduma za utoaji haki nchini uliogharimu kiasi cha Tsh Bilioni 140.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Jaji Chande alisema kuwa mradi huo una nguzo tatu ambazo ni utawala bora na uwajibikaji , fursa ya kutoa na kupata haki na uharakishaji wa mashahuri ambapo kwa pamoja umekusudia kutoa haki kwa wote na kwa wakati.

  “Katika kujenga imani ya wananchi kwa mahakama tunataka kufikia sehemu ambapo mtu yeyote akileta shauri lake Mahakamani basi litasikilizwa kwa wakati” alisema Jaji Chande.

  Aliongeza kuwa taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa asilimia 47 ya Watanzania hawana fursa sawa ya kupata haki ya Mahakama katika maeneo waliopo hususani mikoani kwa kuwa mikoa mingi haina Mahakama Kuu, hivyo mpango huo utakaozinduliwa utalenga kuboresha utendaji na utoaji huduma za kimahakama nchini.

  Akizungumzia kuhusu mradi wa maboresho ya huduma za Mahakama ambao unaandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia Jaji Chande alisema kuwa mradi huo unalenga kuimarisha mifumo ndani ya Mahakama, kuendesha kesi na utoaji wa hukumu kwa wakati.

  Jaji Chande aliongeza kuwa mradi huo utapanua wigo wa utoaji huduma za kimahakama ambapo itatoa fursa za mafunzo endelevu kwa watumishi wa Mahakama 6400 wa ngazi mbalimbali.

  Aidha alisema mpango huo utasaidia kuimarisha Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kukijingea uwezo wa kutoa taaluma bora kwa watumishi pamoja na wadau katika masuala ya Sheria.

  Jaji Chande alisema tayari mradi huo umewezesha kujengwa kwa Mahakama tano za kisasa zilizopo katika maeneo ya Kibaha, Kawe, Kisarawe, Kigamboni na Bagamoyo ambazo zitakuwa mfano wa uanzishwaji wa Mahakama za kisasa nchini.

  Mradi huo unaogharimu bilioni 140 utazinduliwa Kibaha mkoani Pwani Septemba 21 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

  0 0

    Mmoja wa kamishna rais mstaafu Jakaya Kikwete.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/video capture).
   
  Mmoja wa makamishna wa tume ya kimataifa ya kusaka uchangishaji kwa elimu Duniani, amesema mapendekezo yao ya kuinua kiwango cha elimu yasipozingatiwa, watoto wengi zaidi hatawakuwepo shuleni ifikapo mwaka 2030.
  Jakaya Kikwete ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania ameiambia Idhaa hii jijini New York, Marekani baada ya uzinduzi wa ripoti yao kuwa,
  Mapendekezo yao ni pamoja na mbinu mpya za uchangishaji ikiwemo taasisi za kimataifa za kibenki akisema kinachohitajika..
  Ripoti hiyo inasema serikali zisipowezeka katika elimu, watoto katika nchi hususan za kipato cha chini watatwama kwenye mzungumzo wa umaskini na kusalia bila stadi zinazohitajika.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika semina ya wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka kesho kwenda vyuo vikuu vya nchini China, iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wanaokwenda nje wakichukua tiketi pamoja na viza kwa ajili ya safari kwenda katika vyuo vikuu vya nchini China iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wazazi na wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel hayupo pichani katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.

  MKURUGENZI Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel amesema wanafunzi wanaokwenda nje waliohitimu masomo katika vyuo vya nje wanatakiwa watafutwe na waajiri na sio wawe wa kutafuta ajira.

  Mollel ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina na wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka kesho katika vyuo vikuu vya nchini China, amesema kuwa kutokana na vyuo hivyo kuwa na vifaa vya kujifunzia wanafunzi wakitumia vizuri katika soko la ajira watatafutwa.

  Mollel amesema nchi haina tatizo la ajira hivyo watu wanatakiwa kuwa na uwezo binafsi ambao utamfanya mwajiri kutafuta mtu wa kumuajiri hivyo wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo wanatakiwa kutumia maarifa ya kuja kuzalisha nchini.

  Amesema wazazi watumie muda wao katika kuwafuatilia watoto wao wanaosoma nje ili kuweza kuona thamani ya fedha wanazozitoa na elimu wanayoipata.

  Aidha amesema kuwa wale ambao wanahitaji vyuo vya nje bado nafasi zipo na wanafunzi wote watafuata taratibu zote ikiwa ni pamoja Tume ya Vyuo Vikuu nchini kujiridhisha na vyuo wanavyokwenda. Mollel amesema haitakuwa tayari kuona wanafunzi wanahitimu vyuo vya nje kupitia GEL kuwa hawatambuliki.

  0 0

  0 0

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Temeke kimemvua uanachama Diwani wa Kata ya Kurasini na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Matiti Togocho kwa tuhuma za ufisadi dhidi ya wananchi wa kata hiyo.
  Makamu Mwenyekiti Chadema Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke Bernard Mwakyembe amesema kuwa Tochogo mnamo Novemba 23, 2015 na wenzie walitengeneza hati feki za nyumba tano za James Makundi na kulidanganya Jeshi la Polisi kuwa Makundi alikuwa mpangaji ambapo alifanikiwa kufanya hujuma na kuvunja nyumba hizo kwa oda ya uongo iliyotolewa na Wakili Samora Avenue badala ya oda halali ya mahakama kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwa mwekezaji zaidi ya milioni 250.

  Pia amesema diwani huyo alishiriki kudhurumu pesa kiasi cha sh milioni 138 kwa kushirikiana na msimamizi wa mirathi ya marehemu Peter Christian Kijeni huku akijua kuwa kesi iko mahakamani, pamoja na kuvunja nyumba tatu za marehemu huyo na kuiacha familia yake kukosa makazi.

  “Utapeli mwingine alioufanya ni kudhurumu kiasi cha sh. 42,000,000 ambayo ilikuwa fidia ya Paulina Shabani na wajukuu zake. Pia Mwaka 2015 aliidhinisha kutoa eneo la wazi kwa mwemezaji Kilimanjaro Cables (T) Ltd bila kishirikisha wajumbe wa seriakali ya mtaa na badala yake alitumia wajumbe feki kwa lengo la kujipatia fedha, ” amesema Mwakyembe.

  Amedai kuwa mnamo Juni 26,2016 Tochogo alihujumu uchaguzi wa ndani ya chama katika kata ya Kurasini kwa kuita polisi ili wazuie uchaguzi huo kwa lengo la kusababisha chama hicho kukosa uongozi ili kuendelea kufanya ufisadi.

  “Tukiwa kama chama ngazi ya wilaya ambao tunawajibu wa kusimamia masilahi ya chama ngazi husika leo tumefikia maamuzi ya kumfukuza uanachama Diwani wa Kata ya Kurasini Matiti Togocho baada ya kujiridhisha na makosa yote ya ufisadi aliyowafanyia wananchi wa kata hiyo, ” amesema.

  Ameongeza kuwa “Kutokana na Maamuzi ya chama baada ya kujiridhisha na makosa yake na kwa mujibu wa katiba ya chama chetu mamlaka ya mwisho ya kumwondoa nafasi yake ya uongozi ni wilaya na nafasi ya udiwani wenye maamuzi ya kumuondoa ni kamati kuu ya chama.”

  Aidha, Mwakyembe amesema kabla ya kufikiwa maamuzi hayo ya kumfuta uanachama Tochogo, kamati ya chama hicho ngazi ya wilaya kilimuita mara kadhaa kufanya mazungumzo lakini haluitika wito, na kwamba siku alioitikia wito ambayo ilikuwa jana wakati wa mahojiano hakutoa uahirikiano na kutishia kuita jeshi la polisi.

  “Tulimuita hakuitikia wito awali alipokuja akatuambia maneno ya kejeli kuwa vikao vya ndani vimeaghirishwa na kwamba ataliambia jeshi la polisi kuja kutukamata. Tochogo aelewe kuwa

  Tupo kwa ajili ya kutumikia wananchi, na tutadili na madiwani wote wanaofanya mambo kinyume cha taratibu, ni bora tuwe nao wachache waaminifu na waadilifu kuliko kuwa na wengi ambao si waaminifu, ” amesema.

  Na Regina Mkonde 

  0 0

older | 1 | .... | 976 | 977 | (Page 978) | 979 | 980 | .... | 1898 | newer