Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WEKEZENI KATIKA KILIMO NA MADINI ILI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA-Prof.SEMBOJA

$
0
0
Mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja.
 
Na Sheila Simba,Maelezo

Serikali meshauriwa kusimamia uwekezaji  katika sekta za kilimo,madini na viwanda ili kufikia malengo waliojiwekea ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Wito huo umetolewa na Mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja katika mahojiano na MAELEZO kuhusu hali ya uchumi nchini katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

“Muhimu sasa Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya Madini,kilimo na viwanda na hili litasaidia kufanya nchi kuzalisha bidhaa zitakazouzwa nchini kwa wingi bila kutengemea bidhaa kutoka nje ya nchi”,alisema Prof.Semboja.

Ameeleza kuwa taarifa ya hali ya uchumi iliyotolewa na Benki Kuu nchini imeweka wazi hali ilivyo kwa sasa,na kuongeza kuwa ni kweli uchumi upo imara kutokana na taarifa zilizokusanywa na Benki  hiyo kutoka vyanzo mbali mbali.

“Ni kweli kwamba uchumi wetu upo imara na kwamba uchumi wetu unapimwa kwa kuangalia vigezo vinne ambavyo  ni pato la taifa,mfumuko wa bei,urari wa biashara na upungufu wa fedha serikalini”,alisema Prof. Semboja.

Aidha,Prof Semboja amesema kuwa serikali kwa sasa imepunguza matumizi ya fedha yasiyo ya lazima na imeongeza makusanyo ya kodi kutoka vyanzo mbalimbali.  

“Serikali haina matumizi makubwa ya fedha kwani matumizi yanendana na mapato yanayokusanywa ”,alisema Semboja

Amesema kuwa wanaolalamikia kutoonekana kwa fedha mtaani ni wale waliokuwa wanapata pesa kwa njia ambazo sio halali na hivyo kupelekea kushindwa kupata kwa sasa kutokana na udhibiti uliwekwa na Serikali katika kukusanya na kusimamia kodi kwa utaratibu halali.

Ameongeza kuwa Serikali fedha inazokusanya zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na sio kwa wachache waliokuwa wakijinufaisha wenyewe.

TPSF WAKUTANA NA WADAU WA SEKTA BINAFSI KUTENGENEZA AGENDA YA BIASHARA YA TAIFA (NATIONAL BUSINESS AGENDA)

$
0
0
 .Mkurugenzi wa Uhamasishaji Sera na Utafiti wa TPSF,Gili Teri akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wakujadili Agenda maalum inayohusisha masuala mbalimbali yakiwemo ya Kilimo,Nishati,Elimu na mengineyo.
.Baadhi ya Wadau wa Sekta Binafsi na Wafanyabiashara wakiwa katika semina hiyo.

Taasisi ya Sekta Binafsi nchini(TPSF) imekutana na Wafanyabiashara pamoja na wadau wa Sekta Binafsi ili kutengeneza Agenda ya Biashara ya Taifa.

Agenda hiyo ina lengo la kukusanya maoni pamoja na matarajio ya wadau wa Sekta Binafsi hususan kuelekea katika Uchumi wa Viwanda miaka 5 na 10 ijayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika semina maalum iliyowakutanisha Wadau wa Sekta Binafsi,Mkurugenzi wa Uhamasishaji Sera na Utafiti wa TPSF,Gili Teri amesema Agenda hiyo inahusisha masuala mtambuka lakini masuala halisi ya Kisekta yakiwemo ya Kilimo,Nishati,Elimu na Sekta nyingine mbalimbali.

"Mazingira ya Biashara yanapoboreshwa mimi na wewe tunaofanya biashara tunaweza kufaidika zaidi,tukaajiri watu wengi na tukalipa kodi zaidi,"amesema Teri
Amesema wanatengeneza agenda ya pamoja ambayo itatumika kama kitu cha ambacho kitaongoza mawasiliano kati ya Sekta Binafsi pamoja na wadau wengine wakiwemo Serikali.

KUPATWA KWA MWEZI LEO USIKU SEPTEMBA 16 2016

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO, MHANDISI FELCHESMI MRAMBA ATEMBELEA BUKOBA KUTATHMINI ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI KWENYE MIUNDOMBINU YA SHIRIKA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (wapili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika hilo mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, (kulia), wakati alipotembelea kituo cha Kabeta
 Wateja wakiwa wamepanga foleni kupata huduma za umeme kwenye kontena lililowekwa nje ya ofisi za Shirika hilo mkoani Kagera, baada ya jengo hilo kuathirika vibaya

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Bukoba
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, amekagua miundombinu ya Shirika hilo iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi na kuzungumza na wafanyakazi mjini Bukoba mkoani Kagera leo Septemba 16, 2016.
Karibu jengo lote la Ofisi za makao makuu ya TANESCO, limepata nyufa nyingi na hivyo kuufanya uongozi wa Shirika hilo mkoani Kagera, kuhamishia shughuli zake nje ya jengo, ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wateja kwenye makontena mawili ambayo yamewekwa nje ya Ofisi hizo.
Mhandisi Mramba ambaye amewasili mjini Bukoba mapema leo asubuhi Septemba 16, alianza ziara yake kwa kukagua vituo vya kupoozea na kusambaza umeme vya Kabeta, Kyaka na Misenyi na kuzungumza na wafanyakazi.
“Nianze kwa kuwapongeza wafanyakazi wenzangu kwa hatua za haraka mlizochukua mara baada ya kutokea tetemeko la ardhi, kwa kuhakikisha mnazima umeme, hiyo imepelekea kuepusha vifo ambavyo vingesababishwa na umeme wakati wa tetemeko hilo,” Alisema Mhandisi Mramba, wakati akiongea na wafanyakazi nje ya jengo la makao makuu ya TANESCO mkoani Kagera.
Mhandisi Mramba, pia alisema, “Baada ya kukagua vituo vyetu vya kupooza na kusambaza umeme, tunashukuru Mungu, hakuna athari katika mifumo yetu ingawa majengo yamepata nyufa na mengine yanahitaji kufanyiwa ukarabati wa haraka,” alsiema.
Mhandisi Mramba pia aliwataka wafanyakazi wa TANESO, kuwasaidia wenzao waliopatwa na athari kutokana na tetemeko hilo ambapo yeye mwenyewe alianzisha harambee na kufanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 3.3 zikiwemo fedha taslimu na ahadi zilichangwa.
“Sisi kama shirika tumekwisha toa mchango wetu wa jumla kusaidia waathirika wa tetemeko hili kupitia Msajili wa Hazina, lakini kwa vile waathirika wa tetemeko hili ni watanzania wenzetu, ni wadau wetu wakubwa, nimeagiza ofisi zetu kote nchini kuzungumza na wafanyakazi ili tufanye mchango kuwasaidia watanzania wenzetu.” Alisema.
Naye Meneja wa TANESCO mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, aliwapongeza wafanyakazi wa wake kwa kufanya kazi kubwa katika kipindi chote tangu janga hilo litokee, na kuwataka waendelee kulitumikia taifa kwa moyo wa kizalendo na upendo. 
Watu 17 walipoteza maisha, huku wengine zaidi ya 200 wakijeruhiwa na  nyumba zaidi ya 5,000 zikiharibiwa na tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha Richa 5.7 na lililotikisa umbali wa kilomita 10 chini ya ardhi. Tetemeko hilo lilitokea majoira ya jioni ya Septemba 10, 2016.

 Mhansisi Mramba akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea kituo cha Kabeta
 Mhandisi Francis Maze
Mwangalizi msaidizi wa ofisi za Kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Misenyi

 Mhandisi Mramba, akikagua athari za tetemeko kwenye makao makuu ya TANESCO mkoani Kagera
 Mhandisi Mramba, na ujumbe wake wakitembelea kituo cha Misenyi
 Mhandisi Mramba (kushoto), akizungumza na wafanyakazi

 Mfanyakazi wa TANESCO mkoani kagera ambaye nyumba yake iliathirika akizungumza kwenye mkuytano huo

 Wafanyakazi wa TANESCO mkoani Kagera

Hili ndilo jengo linalotumiwa na TANESCO kama makao makuu yake mkoani Kagera, ambalo limepata nyufa nyingi na kupelekea huduma za umeme kwa wateja kutolewa nje ya jengo hilo ambapo wateja wanaonekana wakiwa kwenye foleni

KAMPUNI YA SHANTA GOLD MINING YALIPA FIDIA AWAMU YA KWANZA KWA WANUFAIKA SASA KUANZA MRADI WA UCHIMBAJI MADINI YA DHAHABU

$
0
0
Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamu akitoa maelekezo ya awali kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwalipa fidia wanufaika wote
Watendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd wakifanya maandalizi ya malipo hayo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
 Baadhi ya wananchi wakisubiri maandalizi yakamilike ili wakabidhiwe mlungula wao

Dear Mama Exp ndio ndinga iliyotumika kuwafikisha wananchi hao eneo la tukio la kukabidhiwa cheki za malipo kwa wanufaika wote wa Mradi huo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV Elisante Mkumbo kuhusu mchakato wa malipo utakavyo wanufaisha wananchi kupoitia mradi wa uchimbaji madini ya Dhahabu
Bi Juliana Kidamwe mkazi wa Kijiji cha Mlumbi akihakiki malipo yake kabla ya kukabidhiwa mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson
Kushoto ni mwasibu wa Shanta Gold Mining Ltd Caroline na Mwanasheria wa kampuni ya Shanta Gold Mining David Rwechungura wakikagua fomu zote za wanufaika kabla ya kuanza zoezi la kuwapatia cheki wanufaika wote wa Mradi huo
Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamu akitoa maelekezo kwa wanufaika wote ya namna mchakato mzima utakavyokwenda
Kizito Ramadhani mkazi wa Kijiji cha Mlumbi akikagua fomu za malipo yake mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson kabla ya malipo
Kutoka kushoto ni Andrea Mtarim Mwenyekiti wa kijiji cha Kinyamberu, Ramadhani Mkuki Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlumbi, Selemani Hema Mtendaji wa Kijiji cha Mlumbi,na Jumanne Gwaye Mtendaji wa Kata ya Mang'onyi wakifatilia kwa makini zoezi la ulipaji fidia
Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemam na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson wakisisitiza jambo wakati wakizungumza na wanufaika.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini maelezo ya malipo yao
Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamua akikusanya vitambulisho kwa wananchi waliofika ili kurahisisha zoezi la malipo yao
Wanufaika wakipongezana mara baada ya kukamata cheki zao kwa ajili ya malipo ya fidia

Na Mathias Canal, Singida

Katika miezi miwili ijayo kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu (Shanta Gold Mining  Limited) iliyopo katika kijiji cha Sambaru Kata ya Mang’onyi Wilayani Ikungi, Mkoani Singida huenda ikaanza uchimbaji wa madini ya dhahabu baada ya kuanza kulipa fidia ya zaidi ya Milioni mia nane (800,000,000) wanufaika awamu ya kwanza.

Malipo hayo yamekabidhiwa kwa wahusika ikiwa ni siku tatu tu zimepita tangu Meneja wa Mradi huo Philbert Rweyemamu alipotoa ahadi ya kuwalipa mwishoni mwa wiki hii ili kupisha shughuli za uchimbaji kuanza.

Wanufaika waliolipwa fedha hizo ni wale ambao wanatokanana na mazoezi mawili ya uthamini yaliyofanywa kwenye eneo la mradi kwa ajili ya upanuzi wa kambi.

Hafla ya malipo hayo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambapo wananchi 39 wamejipatia kitita chao huku wengine wakishindwa kufika hivyo watakabidhiwa malipo yao wakati watakapoyahitaji.

Malipo hayo yanakamilisha umiliki wa maeneo hayo kwa Kampuni ya Shanta Gold mining kwa ajili ya uchimbaji na kuwafanya wananchi hao kupisha mradi wa uchimbaji dhahabu pasina kinyongo chochote.

Akizungumzia mchakato huo wa malipo hayo Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamu amesema kuwa umefika wakati wa wananchi wa Wilaya ya Ikungi na taifa kwa ujumla kunufaika na mradi huo utakaoongeza Wigo ya ajira na mzunguko mkubwa wa pesa utakaotokana na wingi wa watu watakaodhuru Mkoani Singida kwa ajili ya shughuli za kazi.

Rweyemamu alisema kuwa Mradi huo utakuwa na mahusiano chanya kwa wananchi kwani pamoja na kuchelewa kuanza kwa uchimbaji lakini imeshiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi Mang’onyi ulioanza mwezi May 2013 na kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2014 na hatimaye kuzinduliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Parseko V. Kone.

Akielezea ujenzi wa Kituo hicho Rweyemamu alisema kuwa Kituo hicho kimegharimu kiasi cha shilingi milioni mia mbili ishirini na tisa, laki tisa sabini na sita elfu na mia mbili thelathini (229,976,230) huku lengola ujenzi huo likiwa ni kwa ajili ya kusogeza huduma ya usalama karibu na wananchi.

Naye Mwanasheria wa Mradi huo wa uchimbaji Madini ya Dhahabu mkoani Singida David Rwechungura amesema kuwa Hadi sasa Shanta imewekeza takribani dola za Marekani milioni ishirini na tano hapa Singida yaani bilioni hamsini za fedha za Tanzania na bado gharama za kujenga mgodi ambazo hazitapungua dola milioni mia moja.

Alisema Mgodi wa Shanta huko Chunya Mkoani Mbeya unazalisha takribani kilo 2700 za dhahabu kwa mwaka ambapo pia umetoa ajira kwa wafanyakazi 800, licha ya wale ambao wanafaidika kwa kuuza vyakula mgodini na kadhalika.

Pamoja na kushiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi Mang’onyi, lakini pia Kampuni ya Shanta imeanzisha Mradi wa maji  kijiji cha Mangonyi (Kisima kimoja kirefu kina meta 60, miundombinu ya kusambaza maji yenye urefu wa kilomita 1.3, injini na pampu ya kusukuma maji kwenda kwenye tenki la kijiji na polisi, imechangia Madawati 100, sawia na Samani (yaani vifaa vya ofisi) ya Kijiji hicho.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ameipongeza Kampuni ya Shanta kwa kutekeleza ahadi yao kwa wakati kwa kuanza kuwalipa wananchi hao fedha zao za fidia kwa wamiliki wa mashamba zaidi ya 130 ambapo zaidi ya watu 85 ndio watakaonufaika  na kuifanya leseni ya kampuni hiyo itaanza kufanya kazi.

Dc Mtaturu amesisitiza agizo lake alilolitoa la kuitaka Kampuni hiyo kuwalipa fidia wananchi 69 wakati wa kikao cha pamoja kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi ambacho kilipewa jukumu la kuhakikisha wananchi wote ambao watapitiwa na mradi huo wanalipwa fidia sambamba na kusimamia uhamishaji wa makazi.

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOANI SINGIDA

$
0
0
Askari wa Jeshi la Polisi wakiulinda Mwenge ishara ya kuwasili muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Singida

Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma walipowasili kukabidhi Mwenge katika Kijiji cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa ameushikia Mwenge ishara ya Makabidhiano mara baada ya kuwasili
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge
 Wananchi wakishuhudia kwa karibu zoezi la makabidhiano ya Mwenge
Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Singida wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
 Wengi wamefika kushuhudia Mwenge ukiwasili mkoani Singida
 Viongozi wa Mkoa wa Singida wakifanya mazoezi ya maandalizi ya kuupokea Mwenge
 Timiza wajibu wako kata Mnyoro wa Rushwa
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akisoma salamu za shukrani mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma katika Kijiji cha Lusilile

Na Mathias Canal, Singida

Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi leo ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge ambao utakimbizwa Mkoani Singida kwa siku saba katika Halmashauri saba ambapo utaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Dkt Lutambi amekabidhiwa Mwenge huo pamoja na wakimbiza Mwenge Kitaifa katika eneo la Kijiji cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni ukiwa umewaka na kuahidi kuukabidhi kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora pasina mashaka utakapomaliza muda wake Mkoani Singida.

Lutambi alisema kuwa mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani humo utalitia jumla ya miradi 61 inayohusu sekta ya ufugaji, Mazingira, Maji, Afya, Elimu, Barabara, Utawala Bora, Kilimo, Ushirika, Biashara, Ardhi na Programu za mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Malaria Rushwa na Ukimwi.

Alisema kuwa jumla ya Miradi 33 itazinduliwa, 13 itawekwa jiwe la msingi minne itawekwa jiwe la msingi na mingine mitano itatembelewa ambapo miradi yote hiyo itakayopitiwa itakuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 14.

Mbio za Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2016 zimebeba kauli mbiu ya "Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" ambapo hata hivyo kila Halamashauri nchini zimeelekezwa kutenga asilimia 5% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vijana na asilimia 5% nyingine kwa ajili ya kina mama.

Katika kumaliza mizizi wa Rushwa, Dawa za kulevya, ukimwi na Malaria Mwenge wa Uhuru umejikita zaidi katika kauli mbiu ya "Timiza wajibu wako kata Mnyororo wa Rushwa" kwenye mapambano dhidi ya Rushwa, Kauli mbiu ya "Tujenge jamii, Maisha na Utu wetu bila dawa za kulevya" kwenye Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Kauli mbiu ya "Tanzania bila maambukizi mapya, Unyanyapaa na Vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana" kwenye Mapambano dhidi ya Ukimwi na Mapambano dhidi ya Malaria, chini ya kauli mbiu ya " Wekeza katika maisha ya baadae, Tokomeza Malaria".

Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida alisema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya zote saba za Mkoa huo ambapo jumla ya Miradi 47 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 12.

Bi Madenge amewapongeza wananchi wote kwa ushirikiano na juhudi kubwa walizofanya katika kuianzisha, kuiendeleza na kuikamilisha Miradi yote.

Pia alisema kuwa katika Wilaya zote walizozuru wakimbiza Mwenge wamepata taarifa za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuelezea namna inavyoendelea kutekelezwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe wakati akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na katibu Tawala wa Mkoa wa Singida amesema kuwa Mwenge huo unataraji Kutembelea Miradi 18 ambapo hii leo utatembelea miradi 7 na hapo kesho utatembelea Miradi 11.

Miongoni mwa Mirafi itakayofunguliwa ni pamoja na uzinduzi wa Programu ya Ufuatiliaji na kuteketeza mbu, Kufungua Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu nane ya vyoo na ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa, Ufunguzi wa daraja la Makutupora, Kuzindua Klabu ya wapinga Rushwa, Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Maarifa ya kupambana na UKIMWI, Kuzindua Mradi wa Vijana wa kufyatua matofali, na Kuzindua Klabu ya Kupambana na Dawa za Kulevya.

Kwa mujibu wa ratiba za mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, unakimbizwa katika Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni Octoba 14 mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu.

Mwenge wa Uhuru unaashiria Nuru na Mwanga, Uliwashwa rasmi kwa mara ya awali juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro Disemba 9, 1961

UHIKI yatoa mafunzo kwa vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi

$
0
0

 Afisa Msimamizi wa Miradi ya Kuweka na Kukopa kutoka Shirika la Uhamasishaji Hifadhi Kisarawe (UHIKI) , Vuai Shame akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) kupata elimu ya utunzaji wa fedha pamoja na upatikanaji wa mikopo kwa ajili waweze kuimarisha biashara zao.


 Vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi  chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) wakiwa na vyeti vya utambulisho wa kikundi chao kilichosajiliwa kwa jina la YEE Tailoring and Decoration Group na Halmashauri ya Manispaa ya Kisarawe, nyuma kulia ni  Mratibu wa Mradi wa YEE Kanda ya Mashariki, Adolf Jeremiah.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Kisarawe.

Shirika la Uhamasishaji Hifadhi Kisarawe (UHIKI) limetoa mafunzo ya kuweka na kukopa fedha kwa vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) ili kuwaelimisha jinsi ya kutunza fedha zao.

Mafunzo hayo yametolewa leo katika Kijiji cha Kauzeni, Kata ya Kibuta wilayani Kisarawe ambapo vijana wamefundishwa jinsi ya kupanga, kuchagua na kusimamia shughuli yoyote inayofanywa kwa ajili ya kujiingiza kipato pamoja na umuhimu wa kujiwekea akiba.

Afisa Msimamizi wa Miradi ya Kuweka na Kukopa – Kisarawe, Vuai Shame amesema kuwa kuna umuhimu wa vijana kupata elimu juu ya utunzaji wa fedha pamoja na upatikanaji wa mikopo ili waweze kuimarisha biashara zao na kuona faida inayopatikana kutokana na biashara hizo.

“Kazi ya UHIKI ni kuwasimamia vijana ili waweze kuunda vikundi vya kuweka na kukopa fedha zitakazowasaidia kuendeleza biashara zao, mpaka sasa tumefanikiwa kuwa na vikundi 27 vya vijana vilivyopo katika kata 4 za wilaya yetu lakini bado tunaendelea kuwahamasisha vijana wengine kufanya hivyo kwani vikundi vina faida”, alisema Shame.

Afisa huyo ameongeza kuwa kwa sasa wameamua kuwasajili vijana katika  makundi kulingana na fani walizosomea ili kuwarahisishia kupata mikopo au misaada kutoka sehemu mbalimbali pamoja na kupanua uwanja wa fursa za  kupata tenda kwa wingi.

Aidha, Shame ameishukuru Serikali kwa kuwa bega kwa bega na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika kuhakikisha wanawasaidia vijana kujikwamua kutoka kwenye lindi la umasikini kwa kuwapa mikopo vijana walio katika vikundi hivyo ili waimarishe biashara zao na kujiongezea vipato.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha hisa cha Jitegemee, Yassin Omary amesema kuwa walianzisha kikundi hicho mnamo Februari 2 mwaka huu baada ya kuhitimu elimu ya ufundi chini ya mradi wa YEE ambapo hadi sasa wamefanikiwa kuwekeza jumla ya hisa 1,621,000 zinazowawezesha kujikopesha wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya kutatua changamoto zao.

“Kujiunga kwenye vikundi vya namna hii kuna umuhimu hasa kwa sisi vijana ambao biashara zetu bado changa kwani vinatupa uwezo wa kukopa fedha pale biashara inapoyumba au pale unapotaka kuongeza mtaji kwa ajili ya kuinua biashara yako”,alisema Omary.

UHIKI ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililoanzishwa mwaka 2009, ni moja kati ya mashirika yanayowasaidia vijana waliopo chini ya mradi wa YEE unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kuratibiwa na shirika la Plan International katika kuunda vikundi vya kuweka na kukopa fedha. 
                                                   

JOGGING SIO UHUNI,KUNA WATU WALITAKA KUPENYEZA MAMBO YAO NA KUTAKA KUICHAFUA JOGGING- DC ILALA -

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema (pili kulia) akiwa sambamba na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Edward Mpogolo (tatu kushoto) wakishiriki mazoezi ya pamoja ya kikundi cha klabu ya Mazoezi cha New Life Jogging,na vikundi vingine mbalimbali vya mazoezi , mapema leo asubuhi katika viwanja vya Kimanga,Tabata Mawenzi,jijini Dar,ambapo Mkuu wa Wilaya alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya kikundi cha New Life Jogging kilipokuwa kinatimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akikabidhiwa Risala na Mwenyekiti wa kikundi cha Newa Life Jogging,Baraka Urio akiwa ameambatana na wanachama wa kikundi hicho,mara baada ya kuisoma na kuelezea changamoto na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya kikundi hicho.Kikundi hicho chenye makazi yake Tabata Mawenzi leo kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akizungumza mbele ya vikundi mbalimbali vya mazoezi (havipo pichani),vilivyoshiriki kwenye hafla hiyo fupi ya kutimizwa mwaka mmoja wa kikundi cha New Life Jogging.Mh.Mjema aliwataka viongozi wa vikundi hivyo kuelezea changamoto zao walizo nazo ikiwemo na fursa zilizopo ili serikali kupitia Ofisi yake ziweze kufanyiwa kazi kwa wakati.Mh Mjema alisema kuwa Jogging sio uhuni,isipokuwa kuna watu walitaka kupenyeza mambo yao katika Jogging.

"Lakini wale waliotaka kuyapenyeza hayo,waliotaka kuingiza uhalifu,waliotaka kupenyeza madawa ya kulevya ,waliotaka kuingiza siasa,waliotaka kuingiza Panya rodi washindwe na walegee,hatutaki Jogging zetu zichafuke,tunataka Jogging zitumike kuona fursa zilizopo",alisema Mh Mjema.
Katibu Tawala wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo akiwasalimia na kuwatia moyo vikundi hivyo vya Jogging,ambaye pia aliwaeleza kuwa wakati wa kujituna na kufanya kazi ni sasa,hivyo amewaomba viongozi wa vikundi hivyo kukutana nao ili kuhakikisha fursa na changamoto walizozieleza katika risala yao zinafanyiwa kazi kwa wakati.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akikabidhiwa jezi na Mwenyekiti wa kikundi cha New Life Jogging,Baraka Urio,pichani kati ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo na wadau wengine wakishuhudia tukio hilo.
Mgeni rasmi,Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Sophia Mjema na viongozi wengine waandamizi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha New Life Jogging,ambacho leo kinasherehekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
Vikundi mbalimbali vilishiriki kwenye mazoezi hayo ya pamoja.


Walk for Kagera yachangisha shilingi bilioni 1.5

$
0
0
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Katika matembezi hayo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kimepatikana.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akizungumz wakati wa kufungua rasmi Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zilichangwa.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga akizungumza na washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zilichangwa.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga, Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Kagera, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.

 Naibu Waziri wa Nchi, OWM –Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisania ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.

Baadhi ya washiriki wa  hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= zilipatikana.
 Baadhi ya washiriki wa  hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= zilipatikana.
 Baadhi ya washiriki wa  hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= zilipatikana.
 Wawakilishi wa Jumuiya ya Wabohora nchini  wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera kwa Rasi wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Bw. William Erio na Afisa Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Waziri wa Mmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashari katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya “ Walk for Kagera” Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Busemaker akipokea cheti kwa ajili ya kutambua udhamini wa Benki hiyo katika kufanyikisha matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Kagera leo Jijini Dar es Salaam.

 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya “Walk for Kagera” Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Aziz Mlima leo Jijini Dar es Salaam.
ais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiagana na baadhi ya washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zimechangwa.Picha na Frank Shija, MAELEZO.


Na: Frank Shija, MAELEZO

TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu mjini Bukoba Mkoani Kagera.

Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.

“Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.

Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.

“Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.

Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.

Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.

Waziri Nape kutoa laki tano kwa kila goli la Serengeti Boys

$
0
0

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo Pichani) kuhusu mchezo kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville utakaofanyika Septemba 18 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Picha na May Simba WHUSM


Na Lorietha Laurence-WHUSM.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa shilingi laki tano kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Serengeti Boys katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa dhidi ya Congo-Brazzaville.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mhe.Nape amesema milango ipo wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea katika kuiwezesha timu na hivyo kufanya vizuri katika mechi hii ambayo ni muhimu sana kushinda ili kufuzu kwa fainali hizo.

“Hii timu ni yetu sote hivyo inahitajika tuimiliki, tuepe nguvu, tuiombee ili iweze kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia fainali kwa kuitoa timu ya Congo-Brazzaville” alisema Mhe. Nape.

Aidha aliongeza kuwa kesho asubuhi atakutana na wachezaji wa timu hiyo ili kuwapa maneno ya faraja kabla ya kuanza kwa mechi na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa motisha wachezaji kwa kuwashangilia na kuwatia moyo.

Mbali na hayo Waziri Nape alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya kadi za kieletroniki zilizozinduliwa hivi karibuni kwa kueleza kuwa kadi hizo bado hazijaanza kutumika rasmi ili zitaanza kutumiwa katika mchezo baina ya Wabunge wa Simba na Yanga pamoja na Bongo Fleva.

Timu ya Serengeti Boys inaundwa na vijana wa Kitanzania wenye umri chini ya miaka 17 ambapo katika mchezo wa kesho watahitaji ushindi na baadaye kufanya mechi ya marudiano mnamo Oktoba 2 mwaka huu nchini Congo-Brazzaville.

TUME YA MIPANGO YAKAMILISHA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA UMMA MIKOA YA SINGIDA, MANYARA NA DODOMA

$
0
0

Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (katikati) akitoa hotuba ya kufunga mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma kanda ya kati iliyojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara katika ukumbi wa VETA mjini Dodoma. Kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo, dkt. John Mduma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla,Tume ya Mipango, dkt. Lorah Madete.
Washiriki wanaounda kundi la nne wakijadili maswali juu ya utayarishaji na uchaguzi wa Miradi ya uwekezaji.
Washiriki kundi la kwanza wakijadili maswali waliyopewa na wakufunzi kabla ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo Septemba 16, 2016.
Washiriki kundi la pili wakifanya maswali waliyopewa na wakufunzi mara baada ya kuhitimisha somo. Washiriki kundi la tatu wakifanya maswali kutoka kwa wakufunzi katika ukumbi wa VETA mjini Dodoma.

Na Adili Mhina, Dodoma.

Tume ya Mipango imehitimisha mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma yaliyowahusisha maofisa mipango wa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kutoka Mikoa ya Singida, Manyara na Dodoma yaliyofanyika tarehe 12-16 Septemba, 2016 katika ukumbi wa VETA mjini Dodoma.

Akifunga mafunzo hayo Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri aliwasihi washiriki kutumia ujuzi waliyoupata katika kuandaa, kutekeleza miradi ya Umma kwa njia za kisasa ili kuongeza ufanisi wa miradi na kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Alisema kuwa Tume ya Mipango imefanikiwa kutekeleza wajibu wake wa kuwajengea uwezo maafisa hao katika hatua zote muhimu zinazopaswa kuzingatiwa katika kufanya maandalizi, kutekeleza, kusimamia, kufuatilia na kufanya tahmini ya miradi ya maendeleo.

“Ni matumaini yangu kuwa hizi siku tano hazijapotea, mmepata elimu ya kutosha kutoka kwa wataalamu wetu katika masuala yote muhimu yanayohusu miradi ya Umma. Jukumu mlilonalo kwa sasa ni kuhakikisha mnatumia mbinu mlizofundishwa katika kutekeleza miradi ya serikali kwa usahihi ili tufikie malengo ya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano,” Alisema.

Nao washiriki wa mafunzo hayo walieleza kuwa wamepata elimu muhimu ambayo itarahisisha utendaji katika kusimamia miradi na kutoa ushauri wa kitaalamu katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Walieleza kuwa mafunzo hayo yamewasisitiza kutumia vigezo muhimu wakati wa kufanya uchambuzi wa kiuchumi na kifedha ili kufikia uamuzi wa kutambua miradi ipi ina manufaa na inaweza kupata mikopo katika soko la mitaji.

“vigezo kama mzunguko wa mradi (project cycle) ikiwa ni pamoja na andiko la awali (concept note), mchanganuo wa faida na hasara (cost-benefit analysis) vigezo vya kuchanganua mradi kama vile uwezo wa uzalishaji (internal rate of return) na thamani halisi ya uwekezaji (Net Present Value) vimetolewa ufafanuzi mzuri na vimeeleweka na tumevielewa” Alisema mmoja wa wakufunzi aliyejulikana kwa jina la Jemsi. Tume ya mipango inaendelea na zoezi lake la kutoa mafunzo kwa walengwa wakuu ambao ni wataalam wa Sera na Mipango ambapo kuanzia Septemba 19 wataalamu wa mafunzo hayo watakuwa Mkoani mbeya kwa ajili ya zoezi hilo

MKUU WA MKOA WA MTWARA,HALIMA DENDEGO ATOA WITO KWA WANANCHI KUPANDA MITI YA MIKOROSHO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego(wapili kushoto)akiambatana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza(kushoto) Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto kwake)wakifanya usafi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoni humo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo,Zoezi hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Mdau wa habari mkoani Mtwara,Taabu Mtingita(kushoto)na Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu wakizoa taka wakati wa zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoni humo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo.Zoezi hilo lilidhamiwa na Vodacom Tanzania.
aadhi ya waandishi wa habari wa Mkoni Mtwara,wakibeba gogo wakati wa zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, wakati wa zoezi la kufanya usafi lililoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari cha mkoani humo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo.Zoezi hilo lilidhamiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego(wapili kushoto aliepiga magoti)pamoja na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza wakimshuhudia Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mtwara,Hassan Simba(kushoto)akimwagia maji mti uliopandwa na Mkuu wa Mkoa huo katika zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa huo, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoa huo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo.Zoezi hilo lilidhamiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Dkt. Khatib Kazungu,akishuhudiwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia kwake)akimwagia maji mti aliopanda wakati wa zoezi la usafi na upandaji miti katika maeneo ya wazi lililofanyika katika hospitali ya rufaa ya Mkoa huo, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoa huo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo.Zoezi hilo lilidhamiwa na Vodacom Tanzania.

.Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Mtwara pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya ligula Mkoni humo, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoa huo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo.Zoezi hilo lilidhamiwa na Vodacom Tanzania.

Wakati serikali ikihamasisha jamii kutekeleza adhma yake ya upandaji wa miti, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amesema katika mkoa huo kila kaya inatakiwa kupanda miti 30 ya mikorosho kwaajili ya kutekeleza agizo la serikali sambamba na kukuza uchumi wa kaya.

Dendego aliyasema hayo wakati aliposhiriki zoezi la usafi na upandaji wa miti katika hospitali ya rufaa ya Ligula lililoandaliwa na waandishi wa habari wa mkoa huo kwa kushirikiana na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Alisema mkoa huo kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea zao la korosho hivyo katika kutekeleza agizo la serikali wananchi wa mkoa huo hawatapanda mti ni mti bali watatakiwa kupanda miti ya mikorosho ambayo pia itawasaidia kukuza uchumi wao kwa faida.

"Wazo la waandishi wa habari kufanya usafi na kupanda miti linapaswa kuigwa na watu wote, tunataka nchi yetu iwe nadhifu na serikali imetoa agizo la upandaji miti,sisi kwa mkoa wa Mtwara hatutapanda mti ni mti tumeamua kila kaya itapanda miti 30 ya mikorosho ambapo itasaidia kuinua uchumi wa kaya,mkoa na taifa kwa ujumla lakini pia tutakuwa tumetekeleza agizo la kiserikali la upandaji miti kwa hiyo miti tutakayopanda sisi itakuwa na faida zaidi,"alisema Dendego

Akizungumza Mkuu wa taasisi ya 'Vodacom Tanzania Foundation' Renatus Rwehikiza alisema kampuni hiyo imekuwa ikijihusisha na mambo mbalimbali ya maendeleo ya kijamii kupitia taasisi ya Vodacom Foundation kwa kuhamasisha na kutekeleza kwa kufadhili pale jamii inapohamasika.

Aidha alisema suala la usafi linalenga maeneo mbalimbali ili kuboresha mazingira na kuwa na afya bora kwa maendeleo ya taifa.

"Kampuni imekuwa ikijihusisha na mambo mbalimbali ya maendeleo ya kijamii kupitia taasisi yake ya misaada kwa jamii ya Vodacom Tanzania Foundation ambayo inagusa elimu, afya,kujikimu, na mazingira katika kutekeleza adhma ya afya kwa mazingira kwani tunahamasisha watu wakihamasika wanatekeleza kwa kuwafadhili, kwasababu usafi ni wa wote,kazini na pahala popote pa kazi ili kuwa na afya bora kwa maendeleo,"alisema Rweikiza

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mtwara Hassan Simba alisema zoezi la kufanya usafi na kupanda miti litakuwa likitekelezwa kila mwaka mwezi Septemba ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha jamii juu ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.

"Sisi tulianzisha huu utaratibu mwaka jana kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania na itakuwa ni zoezi endelevu kwasababu tunapaswa kuelimisha na kuhabarisha jamii, hivyo hatuna budi tukiwa kama wanahabari ni lazima tushiriki pia,alisema Simba

KAMPUNI YA ASAS IRINGA YAPONGEZWA KWA KUJITOLEA MIRADI YA ZAIDI YA TSH MILIONI 400 HOSPITALI YA MKOA

$
0
0
  Na MatukiodaimaBlog.
SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa   imepongeza  msaada mkubwa uliotolewa na kampuni ya  Asas  ya  mkoa hapa wa ujenzi wa jengo la  kituo  cha  damu  salama  cha  kisasa na ujenzi wa  jengo la  watoto  wanaozaliwa  njiti katika  Hospitali  teule ya  mkoa  wa  Iringa pamoja miradi  itakayogharimu zaidi ya  Tsh  milioni 400

Katika  taarifa   iliyosomwa na mganga  mkuu  wa  Hospitali ya rufaa ya  mkoa wa Iringa Dr Robert salim wakati wa  hafla ya  uwekaji wa jiwe la msingi   katika miradi hiyo leo  mbele ya mgeni rasmi   mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  alisema  kuwa awali  uongozi wa hospitali  hiyo  ulimwandikia  barua  mfanyabiashara    huyo  ili  kusaidia  msaada wa kontena ambalo  lingetumika katika  kituo cha benki ya  damu salama ila mfanyabiashara   huyo alijitolea  kujenga jengo  hilo la  kisasa na kuongeza msaada wa jengo la watoto  wanaozaliwa  njiti .

“Kutokana na agizo la Serikali la kuanzisha Benki za damu salama katika Mikoa..... Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Mfadhili  Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS iliona ni vyema kujenga jengo la Kituo Kidogo cha damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kufikia azma hiyo. ...Hospitali ilimuomba Mfadhili huyo atoe msaada wa “Container” kwa ajili ya shughuli hiyo, lakini Mfadhili kwa kuona umuhimu wa huduma ya damu salama katika Mkoa aliomba apewe ramani ili ajenge kituo hicho badala ya kutumia“Container”.”alisema


Dr Salim alisema  kuwa Hospitali   hiyo kabla ya  mfanyabiashara   huyo  kujitolea  ujenzi wa  jengo  hilo  kituo cha  kidogo  cha damu  salama  ulikuwa  ukitegemea  damu  kutoka  kituo  cha kanda  kilichopo  mkoani  Mbeya  ila  sasa  wataweza  kukusanya  damu  kupitia  kituo  hicho.

Alisema  kuwa lengo la mradi huu ni Kuboresha upatikanaji wa huduma za damu salama katika Mkoa wa Iringa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya damu salama katika Vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza vifo vya Uzazi, Watoto wachanga, Watoto na Wahanga wa ajali za barabarani na kuwa lengo la Mkoa kwa mwezi ni kukusanya chupa 784 na kwa mwaka ni chupa 9,413 (units).

Hata  hivyo  alisema mahitaji ya damu kwa mwezi katika Mkoa ni chupa 700 (unit) na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni chupa 160-200 Units kwa mwezi kuwa tangu kituo kianze kutumika mwezi Februari,2016 Mkoa umekusanya chupa 2,065 (22%) hadi sasa.

“Tunakushukuru mkuu wa mkoa  kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii ya kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mfadhili wetu Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS ya Iringa. Katika hafla hii fupi tutakuomba uweke jiwe la Msingi katika Mradi wa jengo la Kituo Kidogo cha Damu Salama na Jengo la Wodi ya Watoto wachanga vyote  vikiwa ni  hisani  kutoka kwa mfadhili wetu  Salim F Abri “

Alisema kuwa ujenzi huo  unafanywa namkandarasi anayenga mradi huu ni Buyungu General Enterprise wa Iringa chini ya usimamizi wa  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye amechangia kuchora ramani za jengo hili na kusimamia mradi mpaka ulipokamilika, mchango wake kama angelipwa ni Tshs.13,939,200.00.

Na kuwa  utekelezaji wa mradi ulianza kutekelezwa mwezi Novemba, 2014 na umekamilika mwezi Agosti, 2015. Jengo limeanza kutumika mwezi Februari, 2016. Pamoja na kujenga jengo hili Mfadhili pia ametoa msaada wa samani, mafriji makubwa 4 ya kutunzia damu na Computer 1 wenye thamani ya Tshs.30,000,000.00.
`
Aidha, Hospitali ya Vicenza ya Nchili Italia ilichangia Tshs. 800,000.00 kwaajili ya kusafisha eneo la ujenzi na Meneja wa Benki ya Damu Salama ya Kanda Mbeya ametoa msaada wa Vitanda 2 vya kutolea damu, Mizani (weighing scales) za kupimia uzito chupa za damu na Mzani 1 wa kupimia watu wanaojitolea damu.

Alisema Mpaka umekamilika mradi huu wa kituo  cha damu  salama umegharimu jumla ya Tshs.154,880,000.00 bila samani na vifaa tiba kuwa  faida kuwa ya mradi huo uboresha utoaji wa huduma  za damu salama kwa kuwa na eneo kubwa la kufanyia kazi,Kupunguza malalamiko ya wananchi kwa kukosa damu salama.
Pia Kuzuia maambukizi ya magonjwa ya VVU/UKIMWI, Hepatitis B na C na Kaswende,Kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga, watoto na wahanga wa ajali vinavyotokana upungufu wa damu au kutokwa na damu nyingi,Kupunguza gharama za kufuata damu salama umbali mrefu (Damu salama Kanda Mbeya) na  kuongeza  kuwa Wanufaika zaidi ni
Watoto, Watoto wachanga, Mama wajawazito, Wahanga wa ajali za barabarani na jamii kwa ujumla.

Dr Salim alisema kupitia mradi huo wanategemea Kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya huduma isiyoridhisha ya damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Halmashauri na kukomesha tatizo la rushwa.

Kuhusu mradi wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti alisema kuwa Mpaka utakapokamilika mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya Tshs.309,210,000.00 bila samani na vifaa tiba ambazo  zote fedha za mfadhili huyo kampuni ya  Asas.

Akizungumzia  hatua ya familia  yake  kujitolea  kujenga  miradi hiyo mikubwa Asas  alisema ni kutokana na changamoto kubwa  aliyoiona  baada ya  kutembelea  Hospitali hiyo na hata  mmoja kati ya  wanafamilia  wake  kupoteza mtoto  baada ya kuzaliwa njiti na kukosa chumba  kwa ajili ya  kunusuru uhai  wake.

Mkuu wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza pamoja na kupongeza kampuni ya Asas kwa kujitolea misaada  hiyo bado  aliomba  wahisani  wengine  kuzidi  kujitolea kwa ajili ya  maendeleo  na kuwa kama mkoa  unatambua mchango mkubwa wa kimaendeleo  unaofanywa na kampuni ya Asas  pia mfanyabiashara Rajan  aliyepata  kujitolea  kujenga  chumba cha kuhifadhia maiti  hospitalini hapo .

Awali  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  akimkaribisha mkuu wa mkoa  kuweka mawe ya msingi katika  miradi  hiyo  alisema misaada anayoendelea  kutoka Asas si  tu kwa CCM na serikali yake  ila hata kwa  vyama  vya  upinzani na  wakazi mbali mbali wa mji  wa Iringa hivyo kutaka Halmashauri ya Manispaa  kutunza  miradi hiyo.



Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza (kushoto)  akimpongeza Salim Asas   (kulia) mara  baada ya  kuweka  jiwe la msingi katika miradi  mikubwa  miwili iliyofadhili   kampuni ya Asas ukiwemo  mradi wa jengo la  kituo cha  damu  salama Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa na jengo la  watoto  wanaozaliwa njiti yote yaliyofadhiliwa kwa zaidi ya Tsh milioni 400  na  kampuni hiyo ya  Asas ya  mkoa wa Iringa(picha na matukiodaimaBlog )
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  akisaini kitabu cha  wageni
Mkurugenzi wa kampuni ya  Asas ya  Iringa wa  tatu kushoto  akiwa katika Hafla  hiyo
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza akitoa  hutuba yake ya ufunguzi wa miradi hiyo
Damu  iliyochangiwa
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza ( wa  tano  kulia ) akiwa na mfadhiliwa wa  miradi ya jengo la  kituo cha  damu  salama Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa Salim Asas kutoka  kampuni ya  Asas ya  mkoa wa Iringa (kulia kwake) pamoja na viongozi  wengine walioshiriki Halfa ya  uwekaji wa mawe ya msingi katika mradi  huo  na jengo la  watoto njiti yote  ikiwa na  zaidi ya Tsh milioni 400 zilizotolewa na kampuni ya Asas wa  nne  kutoka  kushoto ni mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akizindua  majengo hayo  kwa  hotuba
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza na mfadhili wa  miradi ya  jengo la Benki ya  damu na jengo la watoto  njiti wakiweka jiwe la msingi leo anayeshuhudia ni mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela
Mkuu wa  mkoa wa Iringa  akiwa ndani ya jengo la benki ya  damu
Viongozi mbali mbali wakiwa na mkuu wa mkoa kukagua  kituo hicho
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza ( wa  nne   kulia ) akiwa na mfadhiliwa wa  miradi ya jengo la  kituo cha  damu  salama Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa Salim Asas kutoka  kampuni ya  Asas ya  mkoa wa Iringa (kulia kwake) pamoja na viongozi  wengine walioshiriki Halfa ya  uwekaji wa mawe ya msingi katika mradi  huo  na jengo la  watoto njiti yote  ikiwa na  zaidi ya Tsh milioni 400 zilizotolewa na kampuni ya Asas wa  nne  kutoka  kushoto ni mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela

DC ILALA,SOPHIA MJEMA AONGOZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUCHANGIA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

$
0
0

1
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 6 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw. Deo Senya wakati Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) walipofanya Harambee ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi kule Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo, Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Kariakoo Bw.Philimin Lomano Chonde.

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu zilikusanywa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 31564800/= jumla ya michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/= harambee hiyo leo ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea mpaka siku ya jumamosi ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi na wafanyabiashara mbalimbali wametakiwa kuendelea kuchangia kwa kupitia jumuiya yao ya wafanyabiashara mpaka siku ya jumamosi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokeamsaada wa viatu kutoka kwa wafanyabiashara wa kikundi cha Raha Square wafanyabiashara ambao wametoa mchango ubwa sana wa fedha na vitu mbalimbali katika harambee hiyo.
3
Wafanyabiashara wa Raha Square Kariakoo wakikabidhi mcahngo wao wa fedha kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
4
Raha Square wakikabidhi Magodoro , Nguo, Vikoi , Mashuka na vitu vingine mbalimbali katika harambee hiyo.
56
Wakikabidhi Suti na vitengi pamoja na mashuka katika harambee hiyo.
7
Mkuu wa wilaya ya Ilala akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo mara baada ya harambee hiyo.
89
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiwahutubia wafanyabiashara na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika harambee hiyo.
10
Mfanyabiashara Mohammed Abdallah Nofa akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wake wa shilingi 500,000/+ kwa Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema wa pili kutoka kulia . katika picha kulia ni Edward Mpogolo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala na Kushoto ni Katibu wa JWK Bw. Abdallah Mwinyi
11
Wafanyabiashara kutoka Raha Square wakikusanya michango yao ya fedha taslimu na vifaa mbalimbali kabla ya kuvikabidhi leo.
12
Kiongozi wa Wafanyabiashara wauza Simu za mkononi Bw.Stanley Mwakipesile akizungumza machache mara baada ya kukabidhi mchango wao zaidi shilingi milioni 1,500,000/= kwa mkuu wa wilaya ya Ilala katika Harambee hiyo.

LAURA KWAI ATWAA TAJI LA TTCL MISS HIGHER LEARNING INSTITUTIONS 2016.

$
0
0
 Mshindi wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai akipunga mkono kwa mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Clara Nyaki (kulia). Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL). Mshindi wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2015 (kushoto) akimvisha Mshindi mpya wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai (aliyeketi) mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo. Hellen George a.k.a 'Ruby' akitumbuiza kwenye shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL).
 Mshindi wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai akipunga mkono kwa mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Clara Nyaki (kulia). Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL). Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Beda Kinunda (kushoto) akimtangaza mshiriki Glory Gidion kuwa balozi wa TTCL kutoka katika shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016. Mshiriki huyo atasaini mkataba wa kufanya kazi na TTCL kutangaza huduma na bidhaa za kampuni hiyo. Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) na wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakifuatilia matukio anuai katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kulia) ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwasajili kupata laini baadhi ya wapenzi wa ulimbwende waliovutiwa na huduma za kampuni hiyo katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana. Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) na wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakifuatilia matukio anuai katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kulia) ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwasajili kupata laini baadhi ya wapenzi wa ulimbwende waliovutiwa na huduma za kampuni hiyo katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana. Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kulia) ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwasajili kupata laini baadhi ya wapenzi wa ulimbwende waliovutiwa na huduma za kampuni hiyo katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana. Sehemu ya wadau na wapenzi wa masuala ya urembo wakiwa katika mapozi ya picha kwenye Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 jana.
 Sehemu ya Jopo la Majaji wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakijadiliana jambo kabla ya kutoa matokeo kwenye shindano hilo jana.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwa katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana. Sehemu ya wadau na wapenzi wa masuala ya urembo wakifuatilia michuano ya Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 ukumbini.
 Baadhi ya Washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakichuana katika miondoko mbalimbali ya mavazi. Baadhi ya Washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakichuana katika miondoko mbalimbali ya mavazi. Sehemu ya wadau na wapenzi wa masuala ya urembo wakifuatilia michuano ya Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 ukumbini.
 Sehemu ya Washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakichuana katika miondoko mbalimbali ya mavazi.
 Sehemu ya Washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakichuana katika miondoko mbalimbali ya mavazi. Washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walioingia tano bora wakichuana katika kujibu maswali ya uelewa na kijamii. Msanii Navy Kenzo akifanya vitu vyake kwenye shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL). Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Beda Kinunda (kushoto) akimtangaza mshiriki Glory Gidion kuwa balozi wa TTCL kutoka katika shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016. Mshiriki huyo atasaini mkataba wa kufanya kazi na TTCL kutangaza huduma na bidhaa za kampuni hiyo.
 Mratibu wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Bi. Maya Nkiru (kushoto) akitangaza zawadi kwa washindi na washiriki wa shindano hilo. Mshindi wa taji hilo amepata udhamini wa masomo katika chuo chochote nchini pamoja na fedha taslimu milioni moja.
 Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa TTCL ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakipiga picha na Balozi wa TTCL, Glory Gidion mara baada ya kumaliziki kwa shindano hilo. 
Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa TTCL ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakipiga picha na Balozi wa TTCL, Glory Gidion mara baada ya kumaliziki kwa shindano hilo.

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOANI SINGIDA NA ISHARA YA UHURU WA TANGANYIKA

$
0
0
MWENGE wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Singida Mwenge huu ni ni kitu mfano wa kikombe chenye mpini mrefu na utambi ambacho aghalabu huwasha na kukimbizwa katika kusheherekea au kutukuza tukio fulani.
Askari wa Jeshi la Polisi wakiulinda Mwenge ishara ya kuwasili muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Singida

Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma walipowasili kukabidhi Mwenge katika Kijiji cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa ameushikia Mwenge ishara ya Makabidhiano mara baada ya kuwasili
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge
 Wananchi wakishuhudia kwa karibu zoezi la makabidhiano ya Mwenge
Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Singida wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
 Wengi wamefika kushuhudia Mwenge ukiwasili mkoani Singida
 Viongozi wa Mkoa wa Singida wakifanya mazoezi ya maandalizi ya kuupokea Mwenge
 Timiza wajibu wako kata Mnyoro wa Rushwa
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akisoma salamu za shukrani mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma katika Kijiji cha Lusilile

Na Mathias Canal, Singida
KATIBU tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi leo ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge ambao utakimbizwa Mkoani Singida kwa siku saba katika Halmashauri saba ambapo utaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Dkt Lutambi amekabidhiwa Mwenge huo pamoja na wakimbiza Mwenge Kitaifa katika eneo la Kijiji cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni ukiwa umewaka na kuahidi kuukabidhi kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora pasina mashaka utakapomaliza muda wake Mkoani Singida.

Lutambi alisema kuwa mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani humo utalitia jumla ya miradi 61 inayohusu sekta ya ufugaji, Mazingira, Maji, Afya, Elimu, Barabara, Utawala Bora, Kilimo, Ushirika, Biashara, Ardhi na Programu za mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Malaria Rushwa na Ukimwi.

Alisema kuwa jumla ya Miradi 33 itazinduliwa, 13 itawekwa jiwe la msingi minne itawekwa jiwe la msingi na mingine mitano itatembelewa ambapo miradi yote hiyo itakayopitiwa itakuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 14.

Mbio za Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2016 zimebeba kauli mbiu ya "Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" ambapo hata hivyo kila Halamashauri nchini zimeelekezwa kutenga asilimia 5% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vijana na asilimia 5% nyingine kwa ajili ya kina mama.

Katika kumaliza mizizi wa Rushwa, Dawa za kulevya, ukimwi na Malaria Mwenge wa Uhuru umejikita zaidi katika kauli mbiu ya "Timiza wajibu wako kata Mnyororo wa Rushwa" kwenye mapambano dhidi ya Rushwa, Kauli mbiu ya "Tujenge jamii, Maisha na Utu wetu bila dawa za kulevya" kwenye Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Kauli mbiu ya "Tanzania bila maambukizi mapya, Unyanyapaa na Vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana" kwenye Mapambano dhidi ya Ukimwi na Mapambano dhidi ya Malaria, chini ya kauli mbiu ya " Wekeza katika maisha ya baadae, Tokomeza Malaria".

Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida alisema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya zote saba za Mkoa huo ambapo jumla ya Miradi 47 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 12.

Bi Madenge amewapongeza wananchi wote kwa ushirikiano na juhudi kubwa walizofanya katika kuianzisha, kuiendeleza na kuikamilisha Miradi yote.

Pia alisema kuwa katika Wilaya zote walizozuru wakimbiza Mwenge wamepata taarifa za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuelezea namna inavyoendelea kutekelezwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe wakati akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na katibu Tawala wa Mkoa wa Singida amesema kuwa Mwenge huo unataraji Kutembelea Miradi 18 ambapo hii leo utatembelea miradi 7 na hapo kesho utatembelea Miradi 11.

Miongoni mwa Mirafi itakayofunguliwa ni pamoja na uzinduzi wa Programu  ya Ufuatiliaji na kuteketeza mbu, Kufungua Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu nane ya vyoo na ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa, Ufunguzi wa daraja la Makutupora, Kuzindua Klabu ya  wapinga Rushwa, Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Maarifa ya kupambana na UKIMWI, Kuzindua Mradi wa Vijana wa kufyatua matofali, na Kuzindua Klabu ya Kupambana na Dawa za Kulevya.

Kwa mujibu wa ratiba za mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, unakimbizwa katika Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni Octoba 14 mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu.

Mwenge wa Uhuru unaashiria Nuru na Mwanga, Uliwashwa rasmi kwa mara ya awali juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro Disemba 9, 1961

Kipindi cha Reggae Time Pride Fm Sept 17 2016.....Mahojiano na Innocent Galinoma

$
0
0
Karibu katika kipindi cha REGGAE TIME ya Pride Fm Mtwara Tanzania.
Na leo, ni mazungumzo yangu na Innocent Galinoma ambaye alikuwa mkarimu sana kufika Kilimanjaro Studios kwa mahojiano.

Ni kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, mbili kamili kwa Marekani Mashariki
Jiunge nasi kupitia 87.8 Fm kwa mikoa ya kusini, ama www.878pridefm.com ama kupitia TuneIn, bofya tun.in/seTTx.

DAVID KAFULILA AONGOZA MAAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA GOSHEN NURSERY AND PRIMARY SCHOOL BUNJU JIJINI DAR

$
0
0
  Mwanafunzi Eugene Kephasi, akimvika skafu, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alikuwa  mgeni rasmi katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School  Bunju jijini Dar es Salaam leo mchana.
 David Kafulila akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu wakati akipewa historia fupi ya shule hiyo kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu (hayupo pichani).
 Kafulila (katikati) na viongozi wa shule hiyo wakielekea meza kuu tayari kwa maafali hayo. Kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu, Mkurugenzi wa Shule, Nipael Mrutu, Lupi Kiyabo na Mchungaji Elisifa Kephasi.
 Wanafunzi wakiwa tayari kwa gwaride.
 Wanafunzi wa darasa la saba wakiwa kwenye maafali yao.
 Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu (kushoto), akimuongoza mgeni rasmi David Kafulila wakati wa kukagua shule hiyo.
 Skauti akionesha namna ya kupika katika kambi yao waliyoiweka katika shule hiyo kunogesha maafali hayo.
 Magari yanayotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi yakiwa shuleni hapo
 walimu wakiwa kwenye maafali hayo.
 Wahitimu wa darasa la saba wakiimba wimbo wa shule.
 Wanafunzi wa darasa la tatu wakiimba kwenye maafali hayo.
 Wanafunzi wakiimba wimbo wa kuwaaga darasa la saba.
 Majadiliano meza kuu na mgeni rasmi. Kulia ni Mchungaji Elisifa Kephasi na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu.
 wanafunzi wa darasa la pili wakitoa burudani.
 Hapa ni furaha tupu kwa wanafunzi wa darasa la pili baada ya kutoa burudani.
 
 Sarakasi zikifanyika katika maafali hayo.
 Wageni waalikwa, wazazi na walezi wa watoto hao wakijumuika na watoto wao kwenye maafali hayo.
 Sarakasi zikiendelea.
 Hapa ni Karate kwa kwenda mbele “madogo wapo vizuri sana katika mchezo huo baada ya kupata mafunzo kutoka kwa Kamanda Mduma wa Skauti”
Skauti wakionesha namna ya kumuokoa mtu aliyepoteza fahamu ambaye yupo kwenye eneo la kikwazo kumfikia. Hapa muokoaji akipita chini ya moto kwenda kumchukua mgonjwa.…………………………………………………………….
Na Dotto MwaibaleMBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila amesema urithi pekee wa watoto ni elimu na sio mali kama ilivyozoeleka.
Kafuli ametoa kauli hiyo katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School Dar es Salaam leo mchana.
“Napenda kuwaomba wazazi na walezi kuendelea kuwapa elimu watoto wenu kwani ndio msingi wa maisha yao badala ya kuwarithisha magari, nyumba na vitu vingine vya thamani” alisema Kafulila,
Kafulila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maafali hayo alitoa shukurani zake kwa uongozi mzima wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwaandaa wanafunzi hao ambao watakuja kuwa wataalamu na viongozi wa baadae.
Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu alisema shule yao imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali bila ya kujali dini wala uraia na inazingatia maadili jambo linalowavutia watu wengi kuwapeleka watoto wao wakiwemo wa kutoka nje ya nchi.
Katika maafali hayo wanafunzi wa shule hiyo walionesha burudani mbalimbali kama kuimba, gwaride, sarakasi, karate na michezo mingine ya ukakamavu waliyofundishwa na vijana kutoka chama cha Skauti Tanzania.

Jokate, GSM Foundation wasaidia wahanga wa Tetemeko Kagera

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (kushoto) akizungumza mara mara baada ya kupokea moja ya magodoro 400 yalitolewa na Kampuni ya GSM Foundation kupitia kwa Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo (kulia).
fut2
Jokate Mwegelo akizungumza mara baada ya kukabidhi magodoro hayo ambayo yametolewa na kampuni ya GSM Foundation kwa wahanga wa tetemeko la ardhi la mkoa wa Kagera.
fut3
  Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya watoto yatima ambao nyumba yao waliyokuwa wanaishi iliathirika na tetemeko la ardhi. Jokate kwa kupitia kampuni ya GSM Foundation walisaidia watoto hao baadhi ya magodoro.
fut4
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (wa pili kulia) pamoja na Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo (kulia) mara baada ya kupokeamagodoro 400 yalitotolewa na kampuni ya GSM Foundation.


Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, mbunifu wa mavazi na mwanamuziki , Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na kampuni ya GSM Foundation amesaidia wahanga wa tetemeko la ardhi wa mkoa wa Kagera kwa kukabidhi magodoro 400.

Jokate ambaye pia ni msanii wa luninga alikabidhi magodoro hayo kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja  Jenerali mstaafu, Salum Kijuu makoa makuu ya mkoa huo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Jokate alisema kuwa  kampuni ya GSM Foundation nay eye wameguswa na athari za tetemeke hilo ambalo mbali ya baadhi ya watu kupoteza maisha, kuna waathirikia mbalimbali.
Jokate alisema kuwa kuna watu wamepoteza makazi yao ya kuishi na mali zao mbalimbali, jambo ambalo limewafanya kurudi nyuma katika kimaisha.

Alisema kuwa magodoro ni moja ya mahitaji makubwa ya wahanga katika mkoa huo kuamua kukabidhi kontaina la futi 40 kwa Mkuu wa Mkoa.
“Ni janga la kitaifa kwani waliokumbwa na matatizo hayo ni watanzania wenzetu na wanahitaji msaada mkubwa, kuna majeruhi, kuna waliopoteza wazazi na jamaa zao huku wanafunzi wakikosa sehemu ya kusomea,” alisema Jokate.

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali  Mstaafu, Salum Kijuu aliwashukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huo ambao utapunguza changamoto za wahanga wa  tetemeko hilo.
 “Namshukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huu, ni msaada mkubwa, lakini bado tunahitaji misaada zaidi, bado kuna changamoto nyingi sana kwa wahanga, hivyo tunaomba mashirika, watu binafsi  na wadau wengine waunge mkono katika janga hili,” alisema Kijuu.

Alisema kuwa kama kila Mtanzania atachangia sh 100, wataweza kukusanya jumla ya Sh bilioni 5 ambazo zitawasaidia kuondoa changamoto mbalimbali na kuwafanya wahanga kurejea katika maisha yao ya kawaida.

TANESCO YATOA ELIMU KWA WANANCHI WA KAGERA KUHUSU ATHARI ZA NYAYA ZA UMEME KWENYE MAJENGO YALIYOATHIRIKA NA TETEMEKO LA ARDHI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, akitoa taarifa za athari hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba na ujumbe wake

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, (kushoto), akimkaribisha ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, alipomtembelea Septemba 17, 2016 ofisini kwake mkoani humo ili kumpa pole kufuatia athari za tetemeko la ardhi

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID, BUKOBA
SHIRIKA la Umeme Nchini Tanzania, TANESCO, limewahadharisha wananchi mkoani Kagera kutogusa  nyaya za umeme kwenye nyumba zilizoanguka au kupata athari kubwa kutokana na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera wakati wafanyakazi wa Shirika hilo wakiendelea na zoezi la kuondoa nyaya hizo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba, (anayezungumza juu), wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, Septemba 17, 2016 ili kumpa pole kutokana na maafa haayo.
Sambamba na wito huo, Mkurugenzi huyo pia alimuhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa kuwa upatikanaji wa umeme mkoani humo utakuwepo bila shaka yoyote isipokuwa tu kwenye maeneo ambayo nyumba zimeathirika vibaya ili kuepusha athari zozote zinazoweza kutokea kutokana na kuguswa kwa nyaya hizo.
“Ninachoweza kusema Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, hakuna kifo kilichotokana na madhara ya umeme wakati wa tetemeko hilo, na vijana wetu walichukua hatua mara moja za kukata umeme tatizo hilo lilipotokea,” alisema Mhandisi Mramba.
Mkurugenzi huyo Mtendaji pia alisema, kutokana na ukubwa wa janga hilo, uongozi wa TANESCO ulichukua uamuzi wa kuwapeleka wafanyakazi wengine wa Shirika hilo kutoka mkoani Mwanza ili kuwaongezea nguvu wenzao wa Kagera katika jitihadav za kuhakikisha wananchi wanakuwa salama kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya umeme kwenye majengo mbalimbali yaliyopata athari za tetemeko hilo.
Sambamba na wito huo, Mhandisi Mramba pia alimwambia Mkuu wa mkoa kuwa, Wafanyakazi wa TANESCO nchi nzima, wameanza zoezi la kuchanga fedha ili kuwasaidia wananchi wa Bukoba. “Sisi kwa upande wetu kama Shirika, tumekwisha kabidhi mchango wetu kupitia Msajili wa Hazina,” Aliongeza Mhandisi Mramba.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, alisema, tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa kipimo cha richa 5.7, lilipelekea vifo vya watu 17, na kusababisha majeruhi zaidi ya 200, na kuacha nyumba zaidi ya 2,000 zikiharibika na nyingine kubomoka kabisa.
Alsiema mkoa unaendelea na kuratibu zoezi la kukuanya rasilimali fedha na vifaa ili kuwasaidia walioathirika.
Baada ya mkutano huo na Mkuu wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, alitembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika sana na tetemeko hilo huko Hamugembe, ili kukagua zoezi la utoaji elimu kwa wananchi kuhusu athari za nyaya zilizokaa vibaya kwenye makazi yao na kuwatia moyo wafanyakazi wa Shirika hilo ambao walikuwa wanaendelea na kazi hiyo.
Mhandisi Mramba, alipata fursa ya kuzungumza na Afisa Mtendaji wa Kata ya Hamugembe, Sudi Ahmada, na kumueleza kuwa, wakati wafanyakazi wa TANESCO wakiendelea na zoezi hilo, uongozi wa Kata nao ushirikiane na wafanyakazi wa Shirika hilo katika kuwaelimisha wananchi juu ya hatua zinazochukuliwa na TANESCO kwa sasa.
“Ningeomba muwaelimishe wananchi kuwa ni bora kutokuwa na umeme kwa kipindi hiki kifupi ambacho Shirika linachukua hatua za kuhakikisha usalama wao, na waonapo au kuwa na shaka yoyote juu ya nyaya au jambo linalowatia hofu kuhusu umeme, watoe taarifa haraka TANESCO na tutachukua hatua haraka,” alimuhakikishia Afisa huyo Mtendaji.
Naye Afisa huyo Mtendaji wa Kata ya Hamugembe, aliishikuru TANESCO kwa kuchukua hatua za haraka siku ya tukio hilo na kueleza furaha yake kwa jinsi anavyoona jitihada mbalimbali za wafanyakazi wa TANESCO katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.


 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze, akitoa elimu ya namna ya kuchukua hatua endapo patatokea athari zozote za umeme kwenye nyumba moja iiyoathirika na tetemeko huko Hamugembe
 Fundi akiwa kazini, Hamugembe




 Fundi wa TANESCO mkoani Kagera, akiondoa nyaya za umeme baada ya kukata umeme kwenye nyumba moja eneo la Hamugembe, ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari
 Mhandisi Mramba, akitembelea maeneo yaliyoathirika na tetemeko hilo huko Hamugembe
 Bi Slivia Philip, akiwa ameketi nje ya nyumba yake iliyoharibiwa vibaya na tetemeko eneo la Hamugembe-Mkishenyi mkoani Kagera, Septemba 17, 2016
 Violet Anaclet, mkazi wa Hamugembe-Mkishenyi, akiwa na mawazo wakati akijipumzika kwenye eneo la wazi baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuharibiwa na tetemeko, Septemba 17, 2016
 Mhandisi Mramba, akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Hamugembe, Sudi Ahmada, Septemba 17, 2016
 Kaimu Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Kalisa, (kulia), akizungumza na fomeni wa genge la TANESCO Kanda ya Ziwa, Freddy Lusama, wakati Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Mramba alipowatembelea wafanyakazi wa Shirika hilo waliokuwa wakiendelea na kazi kwenye eneo la Hamugembe mkoani Kagera, Septemba 17, 2016
 Meneja wa TANESCO mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, (katikati), akiwa amezungukwa na wafanyakazi wa shirika hilo akiwapa maelekezo, Septemba 17, 2016


 Mhandisi Mramba, alipofika eneo la Hamugembe, kuona jinsi wafanyakazi wa Shirika hilo wakiendelea na kazi
 Kwa bahati nzuri hakuna nguzo za umeme zilizoathirika na tetemeko hilo, hata hivyo TANESCO imeamua kuchukua tahadhari kwa kukagua ili kuona kama kuna nguzo yoyote iliyoathirika na kuchukua hatua za kubadilisha, kama ambavyo lori hili lililoonekana maeneo ya Hamugembe likiwa na nguzo hizo
 Mhandisi Mramba, akiongea na waanishi wa habari kwenye eneo moja lililoathirika vibaya na tetemeko la ardhi huko Hamugembe
 Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, 9TANESCO), Leila Muhaji, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiusalama ambayo wananchi wanapaswa kuzingatia pindi waonapo nyaya zilizoanguka au kutilia shaka yoyote kuhusiana na miundombinu ya Shirika
 Genizora Magili, anayehusika na masuala ya nyaya za umeme, akiwa amebeba vifaa vya kazi


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba na ujumbe wake, mara baada ya mazungumzo yao, Septemba 17, 2016
Meja Jenerali Kijuu, akiagana na Mhandisi Mramba na ujumbe wake

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images