Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAANZA MCHAKATO WA UJENZI WA JENGO LAKE MKOANI DODOMA

$
0
0
Wahandisi wa Kampuni ya Norplan Tanzania wakiendelea na kazi ya upimaji wa udongo kwa ajili ya upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika eneo itakapojengwa ofisi hiyo inayopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo la ofisi hiyo itakuwa na ghorofa 6 na inatarajiwa kukamilika mwaka 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akipewa  maelezo na Mhandisi wa kampuni ya Norplan Tanzania, Magesa Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa jengo la ofisi hiyo linalopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18. 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea eneo litakapojengwa jengo la ofisi hiyo linalopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18. 

Picha zote na Emmanuel Ghula. 

……………….. 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma kwa kuanza kujenga jengo lake mkoani humo. 

Jengo hilo litakalokuwa nyuma ya Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya ujenzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema jengo la NBS lilipangwa kujengwa jijini Dar es Salaam lakini kutokana na agizo la Rais imebidi jengo hilo lijengwe mkoani Dodoma. 

“Kabla ya agizo la Mhe. Rais, jengo la NBS lilipangwa kujengwa Dar es Salaam na tayari maandalizi yalikuwa yameshafanyika lakini kutokana na agizo hilo imetupasa kujenga jengo letu hapa mkoani Dodoma,” amesema Dkt. Chuwa. 

Kwa upande wake Mhandisi wa kampuni ya Norplan Tanzania, Magesa Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa jengo hilo amesema atahakikisha anafanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa. 

“Nimepewa siku 12 za kumaliza suala zima la upimaji wa udongo katika eneo hili na mpaka sasa hali ni nzuri na nina uhakika kuwa kampuni yangu itamaliza kazi hii ndani ya muda uliopangwa,” amesema Mhandisi huyo. 

Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu utaanza rasmi mwezi Novemba 30 mwaka huu na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.

Serikali inachukua hatua dhidi ya malalamiko ya ukiukwaji wa maadili dhidi ya viongozi wa Umma na matumizi ya TEHAMA sarikalini

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said wakati wa kikao kuhusu masuala ya kiutumishi na viongozi wa Mkoa wa Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela. (Picha ya Maktaba)

…………………………………………………………………..

Makala iliyopita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) aliongea kuhusu hatua zinazochukuliwa kuondoa Watumishi wasiostahili kuwepo katika orodha ya malipo ya Serikali (payroll). Aidha, alieleza hatua zinazochukuliwa kwa wote waliobainika kusababisha malipo yasiyostahili. Waziri Kairuki aliongea hayo katika Runinga ya Taifa (TBC), makala ya leo inaangalia suala la Maadili kwa viongozi wa Umma, Nyaraka za Serikali na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini.

Usimamizi wa Maadili kwa viongozi wa Umma ukoje?

Waziri Kairuki alieleza kumekuwepo na malalamiko ya ukiukwaji wa maadili dhidi ya viongozi wa Umma na hadi kufikia Agosti 2016, malalamiko 200 yalipokelewa ambapo kati ya malalamiko hayo, malalamiko 142 yalihusu Sheria ya Maadili na malalamiko 58 hayakuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Uchunguzi wa awali umefanyika kwa malalamiko 11 yanayohusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili. Aidha, malalamiko 58 ambayo hayakuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma walalamikaji walipewa ushauri na mengine yalielekezwa kwenye mamlaka zinazohusika. Malalamiko hayo yalihusu pamoja na mambo mengine masuala ya rushwa na migogoro ya ardhi” Mhe. Kairuki alifafanua katika kipindi cha TBC.

Aliongeza, hatua zinazochukuliwa dhidi ya Viongozi wa Umma wanaothibitika kukiuka Sheria ya Maadili ni pamoja na kufikishwa katika Baraza la Maadili lililoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kufanya uchunguzi wa kina.

Kuanzia mwaka 2010/11 hadi 2015/16 jumla ya mashauri 69 ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalifanyiwa kazi na Baraza la Maadili, kati yake mashauri 38 yalithibitika kukiuka Sheria ya Maadili na Viongozi na wahusika kupewa adhabu mbalimbali ikijumuisha Onyo (12), Onyo Kali (19), Faini ya shilingi milioni moja (1), kushushwa cheo (3) na kuondolewa katika wadhifa (3).

Waziri Kairuki mwenye dhamana na Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini alisema miongoni mwa mashauri hayo yalihusu kutowasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni, kutoa tamko la uongo, matumizi mabaya ya madaraka na mali ya Umma na mpaka wakati huu Sekretarieti ya Maadili ina malalamiko 12 yakufikisha mbele ya Baraza la Maadili.

Pamoja na hayo, alisema ipo mikakati ambayo Serikali inaitumia katika kukuza maadili ya viongozi wa umma nchini ikiwamo kutoa elimu kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo katika mwaka wa fedha 2015/16, Viongozi wa Umma 7,442 walipatiwa elimu kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mgongano wa Maslahi na Maadili ya Utumishi wa Umma.

Hali ikoje kuhusu Nyaraka na Siri za Serikali?

“ Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 na Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Mwaka 2002 ni kosa la Jinai kwa mtu yeyote kutoa au kuvujisha taarifa zenye zuio kwa wasio walengwa” Waziri Kairuki alisema.

Aliainisha kuwa Serikali imekuwa ikichukua hatua kuhusu hilo ikiwamo kuwashitaki wahusika mahakamani kwa kuvunja sheria, Kuwachukulia hatua za kinidhamu Watumishi wa Umma na hatimaye kufukuzwa kazi, kushushwa cheo na kupunguziwa mshahara.

Aliongeza mengine yanayofanyika ni pamoja na kutoa elimu kwa Watumishi na wananchi juu ya Sheria na Kanuni zinazosimamia masuala ya utoaji wa taarifa, nyaraka na siri za Serikali.

Mhe. Kairuki alisema hatua nyingine zinazochukuliwa ni kuendelea kusimamia Sheria ya Usalama wa Taifa Na. 3 ya mwaka 1970 na Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Mwaka 2002, Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa vya TEHAMA wa mwaka 2012 na Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma za mwaka 2005, pia kuimarisha matumizi na usalama wa mifumo ya TEHAMA ili kudhibiti uvujaji wa nyaraka na siri za Serikali kupitia mitandao ya kijamii.

Matumizi ya TEHAMA yakoje Serikalini?

Waziri Kairuki alisema matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamepunguza gharama za uendeshaji wa kazi mbalimbali za Serikali akitolea mfano wa uendeshaji wa semina na mikutano kwa njia ya mawasiliano ya video (Video Conference) ambapo mikutano ya Serikali hufanyika kwa gharama nafuu kwani haimlazimu mshiriki kusafiri; na uendeshaji wa mafunzo ambapo mwezeshaji mmoja anaweza kuendesha mafunzo kwa watendaji katika zaidi ya kituo kimoja.

Alisema hadi sasa huduma hiyo ipo katika Mikoa yote isipokuwa mikoa ya Geita, Katavi, Njombe, Simiyu na Songwe ambayo Serikali ipo katika mkakati wa kufikisha huduma hiyo, pamoja na hilo taasisi 77 zimeunganishwa kwenye Mtandao wa Mawasiliano ya Serikali (GovNet) hivyo kufanya mawasiliano kulipia muda wa maongezi.

“Azma ya Serikali ni kutatua kero zinazowakabili wananchi katika kupata huduma mbalimbali katika Taasisi za Umma” Waziri Kairuki alisema na kuelezea utekelezaji wa miradi kama Mawasiliano ya ndani ya ofisi (electronic Office) kupitia Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka (electronic Records) kupitia Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao (e-Procurement system) kupitia PPRA na MSD, na Huduma za Kitabibu kwa njia ya mtandao (Telemedicine system) kupitia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

***Itaendelea – Sehemu ijayo itahusu suala la mapambano ya rushwa na mpango wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi.

WILDAF YAWASILISHA MAPENDEKEZO KUFUTA SHERIA ZA KIMILA ZINAZOSIMAMIA MIRATHI

$
0
0

Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF) limewasilisha mapendekezo kwa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria likitaka kufutwa kwa sheria mbalimbali za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo zinalalamikiwa kuwakandamiza wanawake nchini . 

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga amesema mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwakanadamiza wanawake na kuwanyima haki ya kumiliki mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na waume zao. 

Amesema katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba Serikali itunge sheria moja ambayo pamoja na zile za kidini itashughulikia masuala ya mirathi na kuweka usawa wa kisheria katika urithi wa mali kati ya mwanamke na mwanaume ikiwa ni pamoja na watoto wa kiume na wa kike kuwa na usawa katika kurithi mali inapotokea mzazi wa kiume amefariki. 

“Tulipoonana na Mhe Waziri Dkt Mwakyembe alituagiza kama tunataka kuwasaidia wanawake nchini basi tuwasilishe wizarani mapendekezo yetu juu ya nini kifanyike, sasa leo tumekuja hapa kutekeleza agizo la Mhe Waziri, tunampatia Katibu Mkuu mapendekezo husika, ambayo kwa asilimia kubwa yanapendekeza kufutwa kwa sheria zote za kimila ambazo zinamkandamiza mwanamke na mtoto wa kike na kutungwa kwa Sheria moja itakayoshughulikia masuala yote ya mirathi nchini na tuna imani kuwa yatafanyiwa kazi na kufanikisha azma ya WILDAF ya kuwasaidia wanawake nchini, alisema Mwenyekiti wa WILDAF Bi. Judith Odunga 

Akipokea mapendekezo hayo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam amewapongeza na kuwashukuru WILDAF kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ili kuwasaidia wanawake na Serikali kwa ujumla wake kwani kitendo hicho kitasaidia sheria husika kufanyiwa marekebisho yatakayostahili ili ziendane na wakati, zikidhi mahitaji na kutafsiriwa katika lugha ambayo wananchi wengi ambao ndio walengwa wazielewe sheria hizo 

Amesema sasa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa sheria zote nchini zinatafsiriwa na zile zinazotungwa zitakuwa kwa Kiswahili na Kingereza, uamuazi ambao utawawezesha watanzania wengi kuzielewa sheria hizo. 

Prof Mchome alaiwashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaadi kuwa wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yaoi ili kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia wananchi wengi na kuwataka wadau wengine kuja wizarani kuzungumza pale watakapoona kuna haja ya kufanya hivyo kwani wizara ipo tayari kuwasilikiza na kuyafanyia kazi mapendekezo yao. 
Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo hayo yanayotaka kufutwa kwa sheria za kimila nchini ambazo zinadaiwa kuwakandamiza wanawake kwa kuwanyima haki sawa ya kumiliki mali pindi wanapofiwa na waume au wazazi wao anaeshuhudia kushoto ni Bibi Thabita Siwale Mwenyekiti wa Kikosi cha kupambana na haki za mirathi Tanzania- KIKUHAMI.
Wajumbe mbalimbali wa WILDAF walioambatana na Mwenyekiti kushuhudia uwasilishaji wa mapendekezo yao wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome Ofisini kwa jijini Dar es Salaam

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA OZONI DUNIANI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akiongea na waandishi wa Habari juu ya Siku ya Kimataifa ya tabaka la Ozoni. Siku hii huadhimishwa Septemba 16 kila mwaka. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bw. Richard Muyungi. (Picha kwa hisani ya Idara ya Habari Maelezo)
…………………………………………………………..
Tarehe 16 Septemba mwaka huu tutaungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Azimio lake nambari 49/114 la tarehe 19 Desemba 1998 kama kumbukumbu ya tarehe ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol – 1987) kuhusu kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni angani.

Ozoni ni hewa iliyoko kwenye angahewa ya juu, takribani kilometa 10 hadi 50 juu ya ardhi. Kazi yake kubwa ni kuchuja sehemu kubwa ya mnururisho wa mionzi kama “Ultraviolet B” isifike kwenye uso wa dunia. Ujumbe wa mwaka huu ni “Kuhuisha Tabaka la Ozoni na Tabia-Nchi kwa pamoja Duniani”. Ujumbe huu umeambatana na Kauli mbiu isemayo “Kukabiliana na ongezeko la gesi Joto Duniani HFCs chini ya Itifaki ya Montreal”. 

Tabaka la Ozoni linapoharibiwa huchangia kuruhusu mionzi zaidi ya “Ultraviolet B” kufika kwenye uso wa dunia na hivyo kusababisha kuongezeka kwa magonjwa kama vile saratani ya ngozi, uharibifu wa macho yaani “mtoto wa jicho” unaosababisha upofu, upungufu wa kinga dhidi ya maradhi na kujikunja kwa ngozi. Aidha, madhara mengine ni kuharibika kwa mimea hasa mazao ya kilimo kutokana na kuathirika kwa maumbile na mifumo ya ukuaji. 
 
Vile vile, baadhi ya kemikali hizi husababisha kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.
Ili kulinda tabaka la Ozoni, Serikali za mataifa mbalimbali zilikubaliana kuunda Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa Hifadhi ya Tabaka la Ozoni mwaka 1985. Mkataba huu unasisitiza ushirikiano katika utafiti, usimamizi na ubadilishanaji wa taarifa za hali ya Tabaka la Ozoni kutokana na kupungua kwa matumizi yake. 
 
Vile vile ulianzishwa Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol) unaohusu udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni na Mkataba huu ulipitishwa tarehe 16 Septemba, 1987. Lengo kuu la Mkataba huu ni kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hili. 

Hadi sasa Mkataba wa Montreal umepata mafanikio makubwa ya kupunguza zaidi ya kiasi cha asilimia 98 (takribani tani 1.8) ya uzalishaji wa matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni. Punguzo hilo la matumizi ya kemikali hizi limechangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa sababu baadhi ya kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni pia husababisha kuongezeka kwa joto duniani. 
 
 
Kwa mfano, kiasi cha kemikali kilichoondolewa katika matumizi ni takriban tani bilioni 135 za hewa ukaa na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi. Aidha, matokeo ya tafiti yanathibitisha kwamba kiwango cha kemikali zinazoharibu tabaka la Ozoni angani kinaendelea kupungua na inakadiriwa kuwa iwapo jitihada za utekelezaji wa Mkataba huu zitaendelea, Tabaka la Ozoni litarudi katika hali ya kawaida ifikapo katikati ya karne hii. 

Ili kufanikisha utekelezaji wa Mkataba wa Montreal, mwaka 1996 Serikali iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali hizi. Mikakati ya kitaifa ndani ya Programu hii ni pamoja na:
i) Kujenga uwezo wa Taasisi zinazosimamia utekelezeji wa Mkataba;
ii) Kuweka takwimu za kemikali hizo; 

iii) Kutoa elimu kwa wadau na kwa umma wa Watanzania kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili;
iv) Kusambaza habari kuhusu kemikali na tekinolojia mbadala;
v) Kubadilisha tekinolojia katika viwanda vinavyotumia kemikali haribifu;
vi) Kutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha ujuzi katika sekta ya kuhudumia viyoyozi na majokofu;
vii) Kuimarisha mbinu za upunguzaji wa matumizi ya kemikali husika kwa kuanzisha mtandao wa kunasa, kusafisha na kurejeleza vipoza joto;
viii) Kuhamasisha na kuhimiza matumizi ya kemikali na tekinolojia mbadala na rafiki kwa tabaka la Ozoni; na
ix) Kuweka taratibu za kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali zinazodhibitiwa na Mkataba wa Montreal. 

Hatua hizi zimewezesha Tanzania kuondosha kemikali hizi kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na Mkataba. Kwa mfano, Viwanda vitatu vilivyokuwa vinatumia kemikali haribifu vimebadilisha teknolojia hiyo. Aidha, wafanyabishara wengi ambao ni wauzaji wa kemikali husika wamekuwa na uelewa mkubwa na hivyo biashara ya kemikali mbadala imeendelea kukua mwaka hadi mwaka. 

Chini ya Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu, Serikali iliandaa Mpango wa Usimamizi wa Vipozi (Refrigerant Management Plan) ambao utekelezaji wake umefanyika kama ifuatavyo:
Kuandaa Kanuni za Usimamizi wa Kemikali Zinazomong’onyoa Tabaka la hewa ya Ozoni na zilianza kutumika tarehe 7 Desemba 2007;
Jumla ya mafundi mchundo wa viyoyozi na majokofu 500 wamepatiwa mafunzo kuhusu njia bora za kuhudumia vifaa hivyo bila kuathiri Tabaka la hewa ya Ozoni;
Kusambazwa kwa Vitambuzi vya kemikali hizi vipatavyo 18 kwa ajili ya usambazaji katika vituo vilivyo mipakani mwa nchi yetu;
Mashine 20 za kunasa na 5 za kunasa na kurejeleza gesi chakavu zimenunuliwa na kusambazwa kwa karakana 20 na Vituo vitano vya Kikanda vya kunasa na kusafisha gesi chakavu za Majokofu na Viyoyozi katika vyuo vya VETA vya Mwanza, Chang’ombe – Dar es salaam, Kigoma, Mbeya na Mkokotoni-Zanzibar;
Mtambo wa kunasa na kurejeleza kemikali umewekwa katika Kituo cha Tanzania cha Uzalishaji Bora na Tekinolojia Endelevu (Cleaner Production Centre for Tanzania);
Utekelezaji wa Mpango wa Kusimamia Usitishaji wa Matumizi ya Kemikali hizi (Terminal Phase-out Management Plan (TPMP).
Jumla ya maafisa forodha na wasimamizi wa sheria 172 wamepatiwa mafunzo kuhusu udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la hewa ya Ozoni.

Hadi sasa Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86 ya kiasi cha matumizi ya kemikali hizi cha mwaka 1999. Hapa nchini maadhimisho haya yatafanyika kwa njia ya uelimishaji umma kuhusu Tabaka la Ozoni, faida zake, madhara ya kuharibika kwa Tabaka hili na matumizi salama ya bidhaa zenye kemikali rafiki kwa Tabaka la ozoni. 
 
Hivyo kupitia kwenu wanahabari naamini elimu hii itaendelea kutolewa kwa jamii ya Watanzania ili kuongeza ushiriki wao katika kutekeleza jukumu hili muhimu la kulinda sayari hii. Makala zimeandaliwa ili muweze kuzitumia katika kuwafikishia Wananchi elimu hii muhimu. 

Ni muhimu tuzingatie kwamba juhudi za kila mmoja wetu zinatakiwa ili kupunguza na kuondosha madhara katika Tabaka la Ozoni yanayosababishwa na bidhaa tunazonunua na kutumia majumbani au sehemu za biashara. Natoa wito kwa kila mwananchi kushiriki katika 
 
kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
Kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku na vifaa vinavyotumia gesi haribifu kama vile majokofu na viyoyozi vilivyokwishatumika (mitumba) na ambavyo vinatumia vipoozi aina ya R11 na R12.
Kuingiza nchini vipoozi mbadala na rafiki kwa tabaka la Ozoni kama vile R22, R134a, R407, R404 na R717. 

Kununua bidhaa zilizowekwa nembo rasmi isemayo “Ozone friendly” yaani “sahibu wa Ozoni” au “CFC-free” ikiashiria haina wala haikutengenezwa na kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni.
Kuepuka kutupa ovyo majokofu ya zamani ama vifaa vya kuzima moto vyenye kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni aina ya “CFCs” na “halon”. Pata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mafundi ama mamlaka zinazohusika.

Kuepuka matumizi ya kemikali aina ya “Methyl bromide” kufukizia udongo, na badala yake kutumia mbinu mbadala na salama pamoja na mbinu tungamanishi za udhibiti wa wadudu waharibifu yaani “integrated pest management”.

Mafundi wa majokofu na viyoyozi wahakikishe kuwa wananasa na kutumia tena vipoozi (refrigerants) kutoka kwenye viyoyozi, na majokofu wanayohudumia badala ya kuviachia huru visambae angani. Aidha, mafundi watoe elimu kwa wateja wao juu ya njia rahisi za kutambua uvujaji wa vipoozi kutoka katika majokofu na viyoyozi wanavyotumia.
Nawatakieni maadhimisho mema ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni.

JANUARY Y. MAKAMBA (MB.)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS

MUUNGANO NA MAZINGIRA

MBUNGE RIDHIWANI ASAIDIA MATIBABU YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani kikwete atembelea Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha Mkoani Pwani, kufunga mpango wa kusaidi watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa zoezi hilo linalofadhiliwa na Gsm foundation wakishirikiana na Moi.
Mbunge wa Chalinze akiwa katika wodi ya watu waliopata ajali na matatizo mengine ya viungo wakisubiri kupatiwa huduma na wale waliopatiwa huduma ya mifupa kuwajulia hali na kuwapa pole.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani kikwete akipata maelezo toka kwa madaktari wa Moi waliokuwa wanawapokea na kuwaaangalia watoto walikua na matatizo.

Mbunge Ridhiwani akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ufungaji wa mafunzo ya usalama wa barabarani kwa waendesha bodaboda wa Wilaya ya Chalinze

Mbunge Ridhiwani akizungumza na vijana walio maliza mafunzo katika ufungaji wa mafunzo kushoto ni Diwani wa kata ya Bwilingu Ndg. lufunga na wengine ni Ocd wa Chalinze na mkufunzi mkuu wa trafic Chalinze Kamanta Gontako.

Mbunge akimpa cheti cha kuhitimu mafunzo mmoja kati ya wahitimu aliyesimama kushoto ni Diwani wa kata ya Bwilingu Ndg. lufunga na wengine ni Ocd wa Chalinze na mkufunzi mkuu wa trafic Chalinze Kamanta Gontako.

Baadhi ya vijana waliofuzu mafunzo na kupatiwa leseni ya udereva wa bodaboda msaada wa Ofisi ya Mbunge wa Chalinze wakifuatilia kwa makini yanayotokea katika kikao hicho

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ameshirikiana na Gsm Foundation na MOI kusaidia kutibu watoto nane wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Katika matibabu hayo watoto wapatao 23 walifanyiwa vipimo na 8 kati yao walikutwa na matiatizo hayo na kufanyiwa upasuaji,na kuongeza kuwa watoto wengine walikutwa na matatizo tofauti na hayo,na kupelekwa katika hosptali ya taifa Muhimbili na wengine walipelekwa kwa madaktari bingwa wa magonjwa kwa matibabu.

“Watoto wote waliofanyiwa operesheni tuliwakuta wanaendelea vizuri wakiwa na wazazi wao wakiendelea kuwapatia huduma za mwisho kabla ya kuruhusiwa”,alisema Kikwete

Aidha,Mbunge huyo amewaomba wazazi kutowaficha watoto wenye matatizo kama hayo kwani yanatibika na kuacha kuendekeza Imani potofu za kuwafungia ndani na badala yake kuwapeleka katika vituoa vya afya ili kupata matibabu.

“Nawashauri wazazi kutowafungia ndani watoto wenye matatizo kwa kufanya hivyo ni kuwanyima watoto nafasi ya kupona na kuishi maisha kama watoto wengine”,alisema Kikwete.

Kikwete amewaomba wadau katika sekata ya afya kujitokeza kuungana na Gsm Foundation katika kusaidia katika sekta hiyo ili kumkomboa mtanzania kuondoka na matatizo ya kiafya yanayowakabili.

“Nawashukuru sana Gsm kwa kujitoa kusadia watoto hawa kupata matibabu kwa ni jambo la kupigiwa mfano na wadau wengine katika kusaidia jamii”,alisema Kikwete

Mbunge huyo ameshukuru madaktari kwa kujitolea muda wao na kuwatibu watoto hao na kutoa wito kwa Gsm Foundation kuondelea kusaidia katika Mkoa wa Pwani ili kuwafikia watoto wengine katika maeneo ya Mkuranga,Kibiti,Mafia na Rufiji.

Katika hatua nyingine Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa polisi Mkoa wa Pwani,polisi Wilaya ya Chalinze na kituo cha udereva wa vyombo vya moto cha Winners Driving School wameendesha mafunzo ya udereva kwa vijana 160.

Mafunzo hayo ya udereva yamewezesha vijana hao kupatiwa leseni mara baada yakumaliza mafunzo yatakayo wasaidia katika shughuli zao za kila siku za kujitafutia kipato,mafunzo hayo yamegharimu shilingi milioni 20.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SARPCCO)

$
0
0


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu ambaye amekabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Dos Santos JANE (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo mara baada ya kukabidhiana Uenyekiti katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimpa mkono wa pongezi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SARPCCO kwenye mkutano wa  Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni akihutubia kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za kusini mwa Afrika.
                               ..........................................................................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Bara la Afrika kuweka mipango na mikakati madhubuti ya kukabiliana na vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyotokea katika ukanda huo kama hatua ya kuhakikisha wananchi wanafanya kazi zao kwa amani na utulivu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 16-Sep-2016 wakati anafungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika  katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni chachu katika kuibua changamoto mbalimbali za kihalifu na kuzifanyia kazi ipasavyo kwa manufaa ya ukanda huo.
Amesema ni wajibu wa wakuu hao wa majeshi ya polisi ya kusini mwa Afrika kujiepusha na malalamiko yasiyo ya msingi kutoka kwa raia ambayo yanasababishwa na vitendo vya urasimu, uzembe na rushwa ili kujenga uwazi na uwajibikaji.

Makamu wa Rais pia amehimiza kudumishwa kwa ushirikiano miongoni mwa wakuu wa majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika kubadilishana mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kuvuka mipaka.
Katika mkutano huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini –IGP- Ernest Mangu amekabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Nchi ya Msumbiji Dos Santos JANE.

Shirikisho la SARPCCO lilianzishwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika ukanda huo.

Shirikisho hilo linaundwa na nchi wanachama 15 ambapo baadhi ya nchi hizo ni Angola, Botswana, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DCR-,Malawi, Zambia, Zimbabwe, Madagascar,Swaziland, Afrika Kusini,Lesotho, Syshelles na Tanzania ambayo ni mwenyekiti mpya wa SARPCCO.

Tanzania imekabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO wakati ndio Mwenyekiti mpya wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika inayojulikana kwa jina la (SADC TROIKA).


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MSAADA WA SH. MIL. 121.679

$
0
0
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokea kiasi cha Shilingi Milioni 1.6 kutoka kwa Mratibu Taifa wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Bi. Mariam Kilembe wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa ajili ya Kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, leo Bungeni Mjini Dodoma.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 121.679 ili kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.Msaada huo umetolewa leo (Ijumaa, Septemba 16, 2016) na wadau mbalimbali wakiwemo Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Caspian, Bw. Omid Karambech aliyetoa sh. milioni 100.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bordar Limited, Bw. Wu Yahui aliyetoa sh. milioni 20 pamoja na Bi. Mariam Kitembe aliyetoa sh. milioni 1.679 kwa niaba ya Wauguzi walioshiriki mafunzo ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).Akipokea msaada huo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu amewashukuru kwa michango yao ya fedha na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.

Jumapili, Septemba 11, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kagera ili kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo pamoja na kujionea madhara yaliyojitokeza.

Pia aliongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba kuaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko hilo. Aliwaomba wananchi wawe watulivu na kuwaahidi kuwa Serikali itakuwa pamoja nao.

Jumanne, Septemba 13 mwaka huu Waziri Mkuu aliongoza hharambee ya kuchangia waathirika wa teteme hilo na kupokea zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania.

Mbali na kusababisha vifo, watu wengine 253 walijeruhiwa na maelfu ya wananchi walikosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
  1. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, SEPTEMBA 16, 2016

Waziri Mkuu Majaliwa ahitimisha Mkutano wa Bunge.

$
0
0
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akilihutubia Bunge kabla ya kutoa kauli ya kuliahirisha bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016 ambapo mbali na mambo mengine amesema serikali itaendelea kutekeleza yale iliyoyaahidi na kuwashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kujitolea kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 
Na Beatrice Lyimo na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehitimisha Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Mbili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Akihitimisha Bunge, Waziri Mkuu ameainisha mambo mbalimbali ambayo yamefanyika wakati wa Mkutano huo ikiwa ni pamoja na mijadala mbalimbali inayohusu miswada ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza, mara pili na kwa mara ya tatu.
Waziri Mkuu amesema kuwa mijadala ya mkutano huo ilikuwa ya uwazi na hoja zilizotolewa zililenga katika kuleta maendeleo nchini.
“Nawapongeza sana wabunge wote kutokana na michango yenu mizuri na yenye tija hatua ambayo ilibidi mara kadhaa vikao vyetu kuendelea hadi usiku ikiwa ni nje ya muda wa kanuni za Bunge” amesisitiza Waziri Mkuu.
Katika kuhitimisha mkutano huo, Waziri Mkuu amebainisha baadhi ya matukio mbalimbali yaliyotokea nchini ikiwemo janga la tetemeko la ardhi, shughuli za bunge, mwenendo na mwelekeo wa hali ya uchumi, mwenendo wa ukusanyaji mapato ya Serikali, mpango wa Serikali kuhamia Dodoma, hali ya upatikanaji wa chakula nchini, maboresho katika tasnia ya Ushirika, Sekta ya elimu, suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi, kuimarisha usafiri wa anga, hali ya amani na utulivu nchini pamoja na suala la michezo nchini.
Akizungumzia kuhusu janga la tetemeko la ardhi lililotokea mikoa ya Kanda ya Ziwa, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi, Sekta binafsi na Jumuiya za Kimataifa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia waathirika wa tetemeko hilo.
“Serikali inaendelea kukusanya michango kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali, waliotayari kuchangia wanaweza kutumia akaunti ya maafa iliyofunguliwa benki ya CRDB yenye namba 0152225617300 kwa jina la Kamati ya Maafa Kagera na kwa njia ya simu michango hiyo inaweza kutumwa pia kupitia M-pesa 0768-196669, Airtel Money 0682-950009 na Tigo pesa 0718-069616” amesisitiza Waziri Mkuu.
Kwa upande wa mwenendo na mwelekeo wa hali ya uchumi nchini, Waziri Mkuu amesema kuwa kwa ujumla hali ya uchumi nchini inaridhisha na inaendelea kuimarika.
Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) hali ya uchumi umeimarika ambapo pato la Taifa lilikua asilimia 5.5 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa mwaka 2015, ukuaji huo unatoka na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme, huduma za mawasiliano, utangazaji na huduma za intaneti na kuongezeka kwa uchimbaji wa madini.
Katika suala la ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa mwezi Julai na Agosti, Waziri Mkuu amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi hicho mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yalikuwa shilingi Trilioni 2.168 ikilinganishwa na makadirio ya kukusanya shilingi trilioni 2.113 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 103 ya lengo la Serikali.
Waziri Mkuu amesema kuwa, katika mpango wa Serikali kuhamia Dodoma ni dhamira ya Serikali ya Awamu ya tano ya kukamilisha mchakato na ahadi ya Serikali ya kuhamia katika Mji wa Makao Makuu Dodoma ambapo utekelezaji wake utakuwa wa awamu sita.
Vilevile katika sekta ya Kilimo, Waziri Mkuu amesema kuwa hali uzalishaji na upatikanaji wa chakula nchini umefika tani 16,172,841, ambapo Serikali imetoa ruzuku za pembejeo za kilimo kwa ajili ya mazao ya chakula hususani mahindi, mpunga na mtama, kwa upande wa mazao ya biashara ruzuku hiyo hutolewa katoka mazao ya korosho, pamba, chai, kahawa na alizeti.
Pia Serikali itafanya marekebisho ndani ya tume ya maendeleo ya Ushirika na kuchukua hatua za kinidhamu kwa watakao bainika na ubadhirifu wa mali za ushirika.
Katika Sekta ya Elimu, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali imeamua walimu wapya watakaoajiriwa wapangiwe vituo vya kazi moja kwa moja na kwa kuzingatia maeneo yenye upungufu wa walimu.
Kuhusu uhakiki wa vyeti vya watumishi, Waziri Mkuu amesema kuwa, Serikali inaendelea na zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi na kuwaagiza wagurugenzi wa halmashauri kuandaa vituo maalum ambavyo vipo jirani na vituo vya kazi ili kuwapunguzia watumishi gharama na adha wakati wa zoezi hilo.
Katika kuboresha usafiri wa anga nchini, Waziri Mkuu amesema kuwa  Serikali imenunua ndege mbili aina ya Dash 8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zitakazotumika kutoa huduma za usafiri wa anga kwa soko la ndani na chi jirani.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa vyombo vya usalama na ulinzi nchini vimeendelea kulinda na kudumisha amani na utulivu nchini kwa manufaa ya ustawi wa nchi ili kufanikisha lengo la kukuza uchumi na kuondoa umaskini.
Aidha, Waziri Mkuu ameipongeza Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya Kimataifa.
Mbali na hayo Waziri Mkuu Majaliwa amepokea michango mbalimbali iliyotolewa na Kampuni ya Caspian shilingi milioni 100, Ofisi ya Taifa ya Takwimu shilinhi milioni 1.6 na kampuni ya Bordar Ltd shilingi milioni 20 kwa ajili ya waadhirika wa tetemeko lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa

Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari wasomwa Bungeni.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi na Beatrice Lyimo, MAELEZO, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewataka wadau wa habari na wananchi kwa ujumla kutoa maoni juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari wa mwaka 2016 uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni leo mjini Dodoma.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhairishwa Bunge, Waziri Nape amesema kuwa muswada huo unalengo la kuboresha tasnia ya habari ili kuweza kurahisha utendaji kazi wa wanahabari na kuifanya tasnia hiyo kuheshimika nchini.
 
“Ombi langu kwa wadau wa tasnia hii wausome vizuri muswada huo na  kujitokeza kwa wingi na kutoa maoni yao ili tuwe na sheria itakayoleta magezuzi na kukuza tasnia ya habari” amesema Waziri Nape.
 
Waziri Nape amewataka wadau wa habari kuendelea kusoma muswada huo ili kuweza kupata mapendekezo ya namna ya kuifanya sheria hiyo kuwa bora kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.Aidha, Waziri Nape amewaahidi wadau wa habari kukutana nao mara kwa mara wakati wa kutoa maoni na mapendekezo yao yatakayosaidia kuboresha mazingira ya wanahabari nchini ili waweze kufanya kazi yao ipasavyo wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma.
 
Vile vile, Waziri Nape amewapongeza waandishi wa habari kwa kushiriki vema katika kuhabarish umma kuhusu mkutano wa Bunge uliohitimishwa leo na kuahidi kuendelea kushirikiana nao wakati wote.

SENSEI MTSHALI (7TH DAN) ATUA KATIKA SEMINA YA KARATE, MITIHANI KUFANYIKA KESHO JUMAMOSI

$
0
0

Sensei Mtshali akirekebisha mkanda wa Sensei Florence Kieti kutoka Mombasa, Kenya.

Sensei Mtshali (kulia) akitoa maelekezo.

Wakati semina ya kimataifa ya Shotokan Karate imeingia katika siku ya tano leo hii hapa kwenye ukumbi wa Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam, tunashuhudia ujio wa mwalimu mkongwe kabisa wa mchezo huo barani Afrika, Edward Mtshali Sensei (7th Dan) kutoka nchini Afrika Kusini.

Sensei Mtshali (68) amewasili nchini juzi usiku na kuanzia jana amekuwa darasani akiwaonyesha makarateka wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini uzoefu wake katika semina hii ambayo inawahusisha makarateka kutoka Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Tanzania Bara na Zanzibar.Sensei Mtshali ndiye ameshika darasa kwa leo ambapo zaidi ya makarate-ka 50 wanahudhuria.

Mbali ya Mtshali, lakini pia Mkufunzi Mkuu wa JKA/WF-Kenya, David Mulwa Sensei naye ametua nchini kuhudhuria semina hiyo.Hii siyo mara ya kwanza kwa walimu hao wawili kuja nchini, kwani wamekuwa chachu kubwa ya maendeleo ya karate kutokana na msaada wao mkubwa kwa vijana wa Tanzania.

Wasifu wake Edward Mtshali Sensei, au Ed kama anavyoitwa kila mahali, ndiye Mbantu wa kwanza kupewa hadhi ya kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini wa Japanese Karate Association (JKA) World Federation (WF). Pia ni Mbantu wa kwanza kupewa hadhi ya rangi za taifa la Afrika Kusini mara tano mfululizo. Mara ya kwanza ilikuwa alipocheza dhidi ya timu ya Uingereza mwaka 1977. Timu ya taifa ya Afrika Kusini ilikuwa ikichaguliwa kutoka katika timu nne tofauti, Timu ya Wahindi, Machotara, Wabantu na Makaburu (maarufu Springbok) na Sensei Ed alikuwa karate-ka pekee Mbantu kuchaguliwa.

Mwaka 1978, alikuwa mmoja wa wachezaji wa timu rasmi ya Springbok ambayo ilishindana na timu za Ujerumani na Marekani, ambapo timu ya Marekani ilikuwa na mchezaji, ambaye kwa sasa ni maarufu katika filamu, Billy Blanks.

Ilikuwa ni katika kipindi hiki ambapo alianza kucheza akiwa chini ya Sensei Stan, muasisi na Mkufunzi Mkuu wa South Africa JKA, akiwa pamoja na wanandugu wakungwe wa Geyer. Mwaka uliofuata alikuwemo kwenye timu ya taifa ya Afrika Kusini ambayo ilikwenda Marekani. Katika mashindano hayo, alitwaa tuzo maalum kama mshiriki wa muda mrefu.

Mwaka 2006, katika mashindano ya ShotoCup nchini Australia, Sensei Ed alikuwa Mbantu wa kwanza kutwaa Dan ya 7 akisimamiwa na timu ya majaji Wajapani wote kutoka makao makuu ya Japanese Karate Association (JKA) World Federation (WF). Mpaka sasa yeye ni Mbantu pekee barani Afrika kuwa na rank hiyo ndani ya JKA. Kwa sasa Sensei Ed ndiye anayesimamia JKA/WF katika nchi 26 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alizaliwa Aprili 26, 1948 na mwaka huu ametimiza miaka 68, lakini ukimtazama unaweza kudhani ana miaka 45 kwa jinsi alivyo mkakamavu. Amekuwa akicheza karate kwa miaka 50 sasa na amekumbana na changamoto nyingi. 

Mwaka 1968, mkufunzi wake wa kwanza alikuwa Samuel Maimane, ambaye alikuwa na mkanda wa bluu ambapo walikuwa wakicheza Shotokan karate. Sababu ya kusema kwamba alifahamu hiyo ni Shotokan ni kwa vile kitabu walichokuwa wanakitumia kilikuwa kile kilichoandikwa na Sensei Nishiyama. Ilikuwa ni vigumu wakati huo kwa Wabantu kupata ujuzi na kupata waalimu wa kuwapandisha madaraja.
Huyo ndiye Sensei Mtshali, japo kwa ufupi tu.

Imeandaliwa na mtandao wa www.maendeleovijijini.blogspot.com

WATU TANO WANAODAIWA MAJAMBAZI WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi wa Habari juu opreresheni ambazo zimefanyika na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha Bunduki aina ya Gobole kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam. 04.Kamanda wa Polisi Kanda Maalu

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha Bastolaaina ya Browning TZCAR No.87881 kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha namba za usajili bandia zinazotumiwa na wahalifu pikipiki kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha magari yaliyoibiwa sehemu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam 1 kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu jamii)
…………………………………………………………………………………………
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Kikosi Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum ya Dar Es salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es salaam. 

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kamada wa Polisi wa Kanda Maalum,Kamishina Simon Sirro amesemaa askari Polisi wakiwa katika ufuatiliaji maeneo ya Goba Wilaya ya kipolisi Kawe Mkoa wa Kinondoni walimkamata mwanamke mmoja mkazi wa Goba, baada ya kupata taarifa kuwa anawafahamu majambazi wanaojihusisha na uvamizi kwenye maduka makubwa.  Amesema Katika na mwanamke huyo mahojiano aliwataja washirika wake watano ambao walifuatiliwa na kukamatwa katika upekuzi walipatikana na silaha moja Bastola aina ya Browning TZCAR No.87881 ikiwa na risasi 17. 

Sirro amesema katika mahojiano zaidi watu hao walikiri kufanya matukio ya ujambazi wa kutumia silaha jijin Dar es Salaam na mmoja wao alitaja silaha nyingine amezifichwa kwenye majaruba ya Chumvi maeneo ya Ununio na kuwaongoza askari hadi kwenye eneo husika. walipofika maeneo hayo mtuhumiwa alianza kukimbia kuelekea kichakani ndipo
Askari walirusha risasi iliyompata mguu wa kushoto na kufanikiwa kumkamata. 

Hata hivyo mtuhumiwa alifariki akiwa njiani kuelekea hosptalini kutokana na kuvuja
damu nyingi kutokana na jeraha la risasi.  Aidha kati ya watuhumiwa wengine waliobaki mmoja aliwaongoza askari hadi eneo la gongolamboto anakoishi ambapo katika upekuzi  alipatikana silaha nyingine aina ya Shotgun Pump action ambayo imefutwa namba za usajili, msumeno mmoja na tupa moja ya kunolea misumeno na visu. Watuhumiwa wote wanne wanaendelea kuhojiwa mara ya upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani. 

Katika tukio lingine Polisi kanda Maalum Dar es salaam huko magomeni mtaa wa
makumbusho askari wakiwa doria waliwatilia mashaka watu wawili wakiwa
wamepakizana kwenye Pikipiki na begi dogo mgongoni ndipo askari
waliwasimamisha hawakutii amri hiyo, Polisi walifuatilia ili kuwahoji lakini watu hao
baada ya kugundua kuwa Polisi wanawafuatilia walianza kukimbia kwa kasi mara wakatupa begi hilo, askari waliliokota baada ya kulipekua begi hilo walikuta Bastola mbili aina ya Browning No, NE984517CAT5802 Ikiwa na risasi 11 na nyigine yenye No. CZ 2075 aina ya RAMI ikiwa na risasi 21 na magazine mbili iliyotengenezwa CZECH REPUBLIC jitihada ya kuwasaka watu hao zinaendelea. 

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam anatoa wito kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa kupitia kamati za ulinzi na usalama za mitaa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao na kutimiza wajibu wao, amewataka wamiliki wote wa nyumba jijini kuhakikisha kuwa wanaweka kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu jijini. 

Aidha amewataka kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na wao kuwa na
picha za wapangaji wa nyumba hizo, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuweza
kuwabaini wahalifu mbalimbali katika maeneo yao, atakayeshindwa kutekeleza
wajibu wake atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani. 

Kikosi Maalum cha Kupambana na wezi wa magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam ililipokea taarifa toka kwa raia mwema kuwa kuna gari aina ya Toyota Carina T 289 DFL imeibiwa jijini DSM maeneo ya Kimara na kupelekwa mafichoni Mjini Mbeya. Baada ya taarifa hizo kupokelewa ndipo ufuatiliaji ulianza na mtuhumiwa Mzawari Ahmad (29) mkazi wa mwananyamala alikamatwa jijini MBEYA akiwa na wenzake wawili na alikiri kuhusika na tukio hilo. 

Jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa raia mwema kwamba huko Mkoa wa
Kilimanjaro kuna gari nyingine aina ya Suzuki Carry T234 DAJ ambayo
iliibwa maeneo ya Tandale jijini DSM mali ya NURDIN MPELEMBE. Askari walisafiri
mkoa tajwa tarehe 05/09/2016 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Serafin
Valerian(46), mfanyabiashara, mkazi wa Himo Kilimanjaro akiwa na magari matatu ya
wizi nyumbani kwake. Magari hayo ni: SUZUKI CARRY T935 CPC rangi nyeupe
namba zake halisi ni T139 DEK mmiliki ni BRAYAN LYIMO wa Ilala mtaa wa Arusha Dsm,gari nyingine ni TOYOTA RAV 4 rangi ya silver T732 CHP ambayo iliibwa kimara
jijini Dsm tarehe 11/01/2016 nyumbani kwa CECULAR JAMES LAURICH namba halisi ni
T440CAW. 

Mtuhumiwa baada ya kupekuliwa alipatikana na hati
mbalimbali za magari na pikipiki ambazo ni: kadi za bajaji, bima za magari
mbalimbali yaliyopata ajali na kulipwa, plate namba za pikipiki, motorvehicle
licence na TIN namba zenye majina mbalimbali. 

watuhumiwa wote wakiwemo madalali wa magari haya ya wizi wanaendelea
kutafutwa na mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano mara upelelezi
utakapokamilika atapelekwa mahakamani. polisi kanda maalum d’salaam yakusanya milioni tsh 882,570,000/= tozo za makosa ya usalama barabarani kuanzia
Septemba 6 hadi septemba 16.

WAREMBO 16 KUWANIA TAJI LA MISS TEMEKE 2016

$
0
0

Washiriki wa Miss Temeke 2016 wakifanya mazoezi ya kujiandaa na shindano lao jijini Dar es Salaam. Shindano hilo, litakalofanyika Viwanja vya Sigara TCC Chang'ombe Septemba 24 mwaka huu.


Na Dotto Mwaibale

WAREMBO 16 wanatarajia kupanda jukwaani katika shindano la kumpata Miss Temeke 2016 litakalofanyika Septemba 24 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam katika mazoezi yao, Mwalimu wa warembo hao Neema Honest alisema warembo wote wapo fiti na wanaendelea vizuri na mazoezi Chang'ombe Sigara TCC.

"Washiriki wote wapo katika hali nzuri na sasa wanaendelea na mazoezi tayari kwa shindano hilo litakalofanyika Chang'ombe Sigara TCC" alisema Honest.Aliwataja warembo kuwa ni Jesca Nassary, Diana Nyaki, Juliet Pallangyo, Irene Tomitho, Macrina Kudema, Anitha Mugisha, Khadija Masoud na Sia Kiweru.

Aliwataja wengine kuwa ni Sara Bigambo, Nancy Mushi, Mwantum, Esther Mnaki, Anitha Kisimba na Clara Premsinga

Mashine ya MRI Yaanza Kazi, Uongozi Muhimbili Wapongezwa

$
0
0
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa wakati Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akieleza jambo kwa waandishi wa habari leo.
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya mashine ya MRI kuanza kufanya kazi. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Joshua Job na Daktari Bingwa wa Mionzi, Mussa Ndukeki wa hospitali hiyo.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano uliofanyika leo kwenye hospitali hiyo.
Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Medadi Mallaya akimuhudumia mgonjwa leo.

……………………………………………………………………..
Na John Stephen, MNH

Dar es Salaam, Tanzania. Mashine ya MRI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepona baada ya kuharibiika tarehe 24/08/2016. Mashine hiyo iliharibiika baada ya kutokea hitilafu ya umeme. Tangu mashine hiyo imepona tayari wagonjwa 52 wamepatiwa kipimo cha MRI. 

Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare amesema baada ya mashine hiyo kuharibiika, mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wa Muhimbili walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hiyo.
“Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi,” amesema Dk Lwakatare. 

Mmoja wa ndugu wa wagonjwa, Lazaro James, mkazi wa Singida amesema kwamba tangu kuharibiika kwa mashine ya MRI alikuwa akiisubiri na kwamba amefurahi baada ya kurejea kwa huduma hiyo. “Tunashukuru huduma za MRI zimerejea hapa Muhimbili, gharama zake ni nafuu kuliko kuliko kupata matibabu nje. Jambo lingine napenda kuwapongeza madaktari na wauguzi kwa utendaji bora. 

Naye Hawa Hussein mkazi wa jijini Dar es Salaam, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma bora kwa wagonjwa. Hawa ameuopongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya juhudi za kuiwezesha mashine hiyo kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa. Amesema kwamba madaktari wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hivyo wana imani wataendelea kupata huduma bora na kwa wakati.

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AWAASA WAJUMBE WA ALAT KUTATUA KERO ZA HALMASHAURI.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akiwaasa wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote
saba Mkoani Singida  katika kikao cha Jumuiya za Serikali za mitaa Tanzania (ALAT).
Wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida  wakiendela na katika kikao cha Jumuiya za
Serikali za mitaa Tanzania (ALAT).
……………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Singida
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewaasa
wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida kutumia vikao vya mafuzo ya Jumuiya za Serikali za mitaa (ALAT) kutatua kero za halmashauri.
 
Mhandisi Mtigumwe ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya ALAT
mkoa wa Singida na kuwasisitizia kuwa mafunzo hayo yawe na tija na sio kukaa vikao visivyo na matokeo chanya.
 
Ameongeza kuwa katika kipindi cha miezi sita tangu ateuliwe na
Mhe Rais amebaini halmashauri zina changamoto za ukusanyaji hafifu na
usioridhisha wa mapato ya ndani pamoja na mikataba mibovu inayosainiwa na halmashauri na hivyo kuiletea hasara serikali.
 
Mhandisi Mtigumwe amesema kumekuwa na migogoro ya ardhi
inayosababishwa na maafisa ardhi wasio kuwa waadilifu, watumishi na madiwani,kujimilikisha ardhi na vibanda kinyume na utaratibu pamoja na kutotengwa kwa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana.
 
“Halmashauri hazijatenga maeneo ya viwanda vidogo na vya kati,
uchafu umekithiri katika maeneo mengi, watumishi wanaokiuka taratibu
hawachukuliwi hatua za kinidhamu na mawasiliano hafifu kati ya viongozi na watumishi, viongozi na viongozi na hata watumishi wenyewe, hizi ni baadhi ya changamoto ambazo kikao cha ALAT kitumike kuzitafutia majibu, alisisitiza.
 
Mhandisi Mtigumwe amewasisitiza wakurugenzi kuunda mabaraza ya
wafanyakazi na halmashauri zenye mabaraza hayo basi vikao vifanyike ili kero na changamoto za watumishi zisikilizwe na kutafutiwa ufumbuzi.
Kwa upande wao meya, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri
wamemshukuru mkuu wa Mkoa kwa nasaha alizowapa na kuahidi kuyatumia mafunzo ya ALAT katika kuleta mabadiliko katika halmashauri zao.
 
Wajumbe walipata fursa ya kujifunza juu ya Mfumo ya serikali za
mitaa Tanzania bara, ukusanyaji wa mapato ya ndani kwenye halmashauri,
utaratibu wa manunuzi katika serikali za mitaa , uwazi na uwajibikaji na
mawasiliano kwa viongozi.

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA BALOZI MTEULE WA UINGEREZA NCHINI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uingereza Mhe. Sarah Cooke na kufanya mazungumzo naye. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 16 Septemba, 2016.
Dkt. Mahiga akizungumza na Balozi Mteule wa Uingereza nchini, Mhe. Cooke mara baada ya kupokea Nakala zake.



Balozi Mteule Mhe. Sarah Cooke akizungumza huku Dkt. Mahiga akimsikiliza.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki Bw. James Bwana (wa kwanza kulia) akielezea jambo kwa Dkt. Mahiga na Balozi Cooke .
Mazungumzo yakiendelea.

RATIBA RASMI YA SERIKALI KUHAMIA DODOMA HII HAPA

$
0
0
Ratiba rasmi ya serikali kuhamia Dodoma iliyosomwa na Waziri Mkuu bungeni: https://t.co/BgoJiCUo7E

Leo Septemba 16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne wa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya serikali kuhamia Dodoma.

Kufuatia ratiba hiyo iliyogawanyika katika vipengele sita, itaishia Juni 2020 ambapo serikali yote itakuwa imehamia Dodoma. Ratiba hiyo imegawanyika katika vipengele vifuatavyo


1. Septemba 2016 – Februari 2017.

Katika kipindi hiki, Waziri Mkuu, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara, na baadhi ya watumishi wa Idara katika wizara watahamia Dodoma.


2. Machi 2017 – Agosti 2017.

Wizara zitafanya uchanganuzi wa gharama zinazohitajika kuhamisha watumishi wengine kutoka Dar es Salaam ili kuwekwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18.


3. Septemba 2017 – Februari 2018.

Watumishi wa Idara za Wizara na taasisi mbalimbali za serikali watakuwa wakihamia Dodoma.


4. Machi 2018 – Agosti 2018.

Kuhama kwa watumishi mbalimbali wa serikali.


5. Septemba 2018 – Februari 2020.

Kuhama kwa watumishi wa serikali.


6. Machi 2020 – Juni 2020.

Katika kipindi hiki, Ofisi ya Rais na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitahamia Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitumia wasaa huu kuwataka wakazi wa Dodoma kujenga nyumba mbalimbali za makazi ili watumishi wa serikali watakapohamia Dodoma, pamoja na watu wengine, wapate maeneo ya kuishi.

MATUKIO MBALIMBALI BUNGENI WAZIRI MKUU AKILIAHIRISHA BUNGE MPAKA NOVEMBA 1, 2016

$
0
0
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiimba wimbo wa taifa baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma. 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali itahkikisha inaipa kipaumbele miradi ya maji ambayo haikutekelezwa kwa awamu ya kwanza, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdalah Ulega (katikati)akiwaeleza jambo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe. James Mbatia akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu swali Bungeni na kuwataka wananchi kufuata kanuni sheria na taratibu za nchi, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akijibu swali wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akilihutubia Bunge kabla ya kutoa kauli ya kuliahirisha bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016 ambapo mbali na mambo mengine amesema serikali itaendelea kutekeleza yale iliyoyaahidi na kuwashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kujitolea kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakibadishana mawazo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe. Said Kubenea, baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja: Christopher Bageni ahukumiwa kunyongwa hadi kufa, zombe na wenzie wawili waachiwa huru

$
0
0
 Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ilala Christopher Bageni amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutengua hukumu iliyomwachia huru na kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja.
Kadhalika mahakama hiyo imewaachia huru  Mkuu wa Upelelezi wa zamani (wakati huo Mkoa wa Dar es Salaam) (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi  mstaafu Abdallah Zombe na wenzake wawili baada ya ushahidi wa rufaa hiyo kushindwa kuwatia hatiani.

Mara baada ya hukumu kusomwa, ghafla Bageni aliduwaa wakati wenzake wakimkumbatia huku  wakibubujikwa na machozi wakiwa kizimbani. 
Wanaodaiwa kuwa wanafamilia wa washtakiwa hao waliangua vilio huku washtakiwa wenzake walisikika wakieleza masikitiko yao. Wengine walisikika wakisema angejua asingekuja mahakamani kusikiliza hukumu hiyo.
“Namshukuru Mungu...Lakini nasikitika kwa Bageni kukutwa na hatia sina raha kabisa....” alisema ASP Makele wakati akitoka katika ukumbi namba moja wa mahakama hiyo. 

Akizungumza baada ya hukumu hiyo,  ACP mstaafu Zombe alisema anamshukuru Mungu na kuhusu Bageni alisema hana cha kuzungumzia.
Hukumu hiyo imesomwa leo na Msajili wa mahakama hiyo Mhe. John Kahyoza baada ya rufani iliyokatwa na upande wa Jamhuri  kusikilizwa na jopo  la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Bernard Luanda, Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.

Msajili alisema awali Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Salum Massati (wakati huo kabla ya kupanda kuwa jaji wa rufani), ilimuona Zombe na wenzake hawana hatia na kwamba haiwezi kuwahukumu kwa kosa la kusaidia kufanyika mauaji hayo.
Alisema Mahakama ya Rufani inakubaliana na Jaji Massati  kwamba mtuhumiwa hawezi kutiwa hatiani bila kuthibitisha mtu aliyetenda kosa hajashtakiwa na kutiwa hatiani.

TCU yaongeza muda wa udahili wa vyuo vikuu

$
0
0
 Na: Lilian Lundo - MAELEZO

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa udahili wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu mwaka wa masomo 2016/2017 ili kuwapa fursa  waombaji ambao wana sifa lakini hawakupata vyuo kutokana na ushindani wa vyuo na kozi walizozichagua.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Eleuther Mwageni alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo mzima wa udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017, leo  Jijini, Dar es Salaam.

“ Tume imekamilisha awamu ya kwanza ya udahili kwa waombaji wenye sifa ya kidato cha 6, ambapo jumla ya waombaji wote ilikuwa 55,347, waombaji wenye sifa ni 47,203 sawa na asilimia 85.3 ya waombaji wote. Katika waombaji hao wenye sifa waliopata vyuo ni 30,731 sawa na asilimia 65 na waombaji 16,472 ambao wana sifa sawa na asilimia 35 hawajapata vyuo hadi sasa, waombaji waliokosa sifa ni 8,144,” alifafanua Prof. Mwageni.

Amesema kuwa Tume imeamua kuongeza muda wa udahili kuanzia Septemba 12 mpaka Septemba 23, 2016 ili kuwapa nafasi waombaji wenye sifa, fursa ya kuomba tena vyuo na kozi zenye nafasi kutokana na  wengi wao kuomba vyuo na kozi za aina moja.

Prof. Mwageni alivitaja vyuo ambavyo vimeombwa na waombaji wengi na tayari vimeshajaa kuwa ni Chuo cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi, Chuo Kikuu cha Kikristo cha Tiba Kilimanjaro(KCMUCo) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

Pia alizitaja kozi ambazo zimechaguliwa na waombaji wengi kuliko nafasi zilizopo kuwa ni kozi ya Ualimu, Udaktari wa Binadamu, Ufamasia, Uhandisi, Sayansi ya Uthamini wa Ardhi na Sheria. Alitoa mfano wa kozi ya Ualimu Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam ilikuwa na waombaji 15,803 wakati nafasi ni 1,000.

Hivyo amewashauri waombaji waliokosa nafasi kuomba vyuo na kozi zisizo na ushindani ili waweze kupata nafasi kwa awamu hii ya pili.

Aidha Tume hiyo imepunguza viwango vya udahili kwa waombaji wenye sifa ya stashahada kutoka GPA 3.5 mpaka 3.0. Hivyo wamewataka waombaji wenye vigezo hivyo kuomba vyuo na kwa wale waliomba awamu ya kwanza hawatatakiwa kuomba tena bali kusubiri matokeo ya waombaji wenye sifa ya stashahada.

WAZIRI NAPE ATOA WITO KWA WADAU KUTOA MAONI ILI KUUBORESHA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WA MWAKA 2016.

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo alitoa wito kwa wadau mbalimbali katika sekta ya habari kutoa maoni ili kuuboresha
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa Mwaka 2016(The Media Service Bill, 2016) uliosomwa kwa mara ya kwanza leo Bungeni Mjini Dodoma, Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas.

Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Michezo Mhe. Nape Nauye (MB) katika mkutano aliufanya na kutoa wito kwa wadau kuboresha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa Mwaka 2016(The Media Service Bill, 2016) uliosomwa kwa mara ya kwanza leo Bungeni Mjini Dodoma. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live


Latest Images