Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MOI YAPOKEA MSAADA WA MIGUU BANDIA TAKRIBANI 600 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 60

$
0
0
Mkurugenzi wa Mradi wa Watoto Kwanza Bi. Janeth Kiwia kulia akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo mapema hii leo katika taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dkt. Othman Kiloloma.
leg2
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji waTaasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu  Dkt. Othman Kiloloma (kushoto) akionesha moja ya mguu wa bandia ambao umotolewa msaada na Taasisi ya Legs 4 Afrika ya nchini Uingereza kwa kushirikiana na Asasi ya Mohamed Punjani pamoja na Taasisi ya Watoto Kwanza ikiwa ni sehemu ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo mapema hii leo katika taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu, kulia ni Mkurugenzi wa Mradi wa Watoto Kwanza Bi. Janeth Kiwia.
leg3
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mohamed Punjani Foundation Bw. Gulam Punjani kulia akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo mapema hii leo katika taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu, katikati ni  Mkurugenzi wa Mradi wa Watoto Kwanza Bi. Janeth Kiwia na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji waTaasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu  Dkt. Othman Kiloloma.
leg4
Mtaalam wa kutengeneza viungo vya miguu toka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Soud Ramadhan akionesha namna ya utengenezaji wa miguu bandia kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo mapema hii leo katika taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu.
leg5
Mtaalam wa kutengeneza viungo vya miguu toka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Geofrey Mwakasungula akionesha namna ya utengenezaji wa miguu bandia kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo mapema hii leo katika taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu.
leg6
Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji waTaasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu  Dkt. Othman Kiloloma (kulia) akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya viungo bandia wakati wa makabidhiano ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo mapema hii leo katika taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu.
leg7
: Mkurugenzi wa Mradi wa Watoto Kwanza Bi. Janeth Kiwia kulia akisoma pamoja na wanafunzi ambao wanamataizo ya viungo wakati wa makabidhiano ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo mapema hii leo katika taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu.
(Picha zote na Benjamin Sawe – Maelezo)

Mayanja atamba kuisambarataisha Azam FC Jumamosi

$
0
0
Benchi la Ufundi la klabu ya Simba limesema hakuna kitakachowazuia kuibuka na ushindi dhidi ya Azam FC katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru.

Timu hizo mbili zitakuwa zinakutana kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu na mpaka sasa hakuna timu iliyopoteza mchezo. Simba na Azam FC mpaka sasa zimekusanya jumla ya pointi 10 kutokana na mechi nne na zimefungana kwa kila kitu kwenye msimamo huo.

Mbali ya kuwa sawa katika idadi ya mechi za kucheza, kila timu imeshinda mechi tatu, kutoka sare mechi moja, kufunga mabao saba, kufungwa mabao mawili na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kutokana na hali hiyo, mchezo huo ndiyo utaamua nani atakuwa katika mstari mnyoofu wa kuongoza ligi na timu ipi itapoteza mwelekeo. Hii inatokana na ukweli kuwa mechi ya Simba dhidi ya Azam, Yanga dhid ya Simba na Yanga dhidi ya Azam ndizo zinazotoa hali halisi ya nani anaweza kutwaa ubingwa msimu huu.

Mayanja alisema kuwa wanajua mchezo huo utakuwa mgumu na wamejiandaa vilivyo ili kufanya vyema. Alisema kuwa Azam FC ni timu ngumu, lakini wamejidhatiti ili kuitwaa kushinda na kufuta aibu ya miaka mine ya kutotwaa ubingwa wa Tanzania Bara wala kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa kwa kushika nafasi ya pili.

“Tunajua tutakacho kifanya katika mchezo huo, tumejiandaa na jambo zuri kwetu ni kuwa tuna kikosi kipana na hakuna majeruhi hata mmoja, nawaomba mashabiki wa Simba waje kwa wingi kuipa sapoti timu yao,” alisema Mayanja.

Aliongeza kuwa wamedhamiria kukata kiu ya mashabiki wao katika mechi hiyo ambayo anaamini itakuwa njia pekee ya timu yake kufanya vyema msimu huu.

Zaidi ya wafanyabiashara 100 wa Tanzania na Kongo kushiriki kongamano la Biashara

$
0
0
 Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna  Msonsa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba 22 Jijini Lubumbashi, Congo. Kushoto ni Afisa Miradi wa Kampuni ya Uhusiano ya 361 Tanzania, Bi. Naomi Godwin.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Louis P. Accaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba 22 Jijini Lubumbashi, Congo. Kushoto ni Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna Msonsa.
Meneja wa Masoko wa Kampuni ya GSM Group Bi. Farida Rubanza (kushoto) akielezea jambo wakati wa mkutanio wao na  waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Louis P. Accaro, Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna Msonsa na Afisa Miradi wa Kampuni ya Uhusiano ya 361 Tanzania, Bi. Naomi Godwin.Picha na Frank Shija, MAELEZO.

Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Zaidi ya wafanyabiashara 100 kutoka Tanzania na Kongo wanatarajia kushiriki kongamano la biashara litakalofanyika Lubumbashi Kongo Septemba 22 mwaka huu.

Lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuongeza kiasi cha mauzo ya nje na kuboreshwa mazingira mazuri ya biashara kati ya nchi hizo mbili.

“Wafanyabiashara wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kupata soko nchini Kongo, kutokana na nchi hiyo kutegemea bidhaa nyingi kutoka Tanzania kama vile samaki wabichi na wakavu kutokana na nchi hiyo kutokuwa na bahari,” alifafanua Afisa biashara wa TANTRADE Bi. Getrude Ngwesheni.

Aliendelea kwa kusema kuwa Kongo wanaongea lugha ya kiswahili kuwasiliana, lugha ambayo inatumika na watanzania wengi, hivyo itarahisisha mawasiliano katika shughuli za biashara.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kongamano hilo kutoka Chama cha wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bi. Anna Msonsa amesema kuwa kongamano hilo linatoa fursa kwa wafanyabiashara wote kuanzia wa chini mpaka wale wakubwa na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo.

Akitoa maelezo ya namna ya kushiriki Kongamano hilo Afisa Miradi kutoka Kampuni ya 361 Bi. Naomi Godwin amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kujaza fomu ambazo zinapatika katika ofisi za 361 digrii zilizoko Msasani pamoja na ofisi za TCCIA na TANTRADE au kwa kutembelea tovuti ya www.tanzaniadrc.com.

Aidha, kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Kongo, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Chama cha wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Shirikisho la wafanyabiashara wa Kongo (FEC), Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Taasisi ya Sekta Binafsi Nchi Tanzania (TPSF), Kampuni ya 361 Degrees na mdhamini mkuu ambaye ni Taasisi ya GSM Foundation.

CHINA YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 100 KWA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meje Jenerali mstaafu Salimu Kijuu akimshukuru Naibu Balozi wa China Zhang Biao baada ya kupokea msaada kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi

 Baadhi ya Madaktari wa kichina waliokuja bukoba kutoa huduma za matibabu kwa wahanga wa tetemeko la ardhi wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Sehemu ya misaada iliyotolewa na serekali ya china kwa wahanga wa tetemeko Mkoani Kagera


 Lori lililoleta msaada wa serekali ya china Mkoani Kagera kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi


Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

UBALOZI wa china nchini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya china na wananchi wa china wametoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni mia moja kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea septemba 10 Mkoani Kagera.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa niaba ya Balozi wa China ambaye yupo likizo nchini China Dk. Lu Youqing, Naibu balozi wa china Zhang Biao alisema kuwa wamewatembelea wahanga wa tetemeko hilo na kujionea jinsi wananchi walivyohathirika.

"Ndugu zetu bado wanahitaji misaada kwani tetemeko limewaathiri sana kwani wapo waliopoteza makazi,waliojeruhiwa tumeona huzuni sana tulipoona hali hiyo,tunawapa poleni nyingi sana na tupo pamoja katika kipinfi hiki Kigumu"alisema Naibu Balozi huyo

Alivitaja vitu walivyotoa kwaajili ya wahanga wa tetemeko kuwa ni mahema,madawa,chakula na mablanketi.

Alisema Nchi ya china na Tanzania ni marafiki wanaoshirikiana katika sekta mbalimbali katika kujenga Taifa la Tanzania watazidi kusonga mbele.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu  baada ya kupokea msaada huo aliushukuru Ubalozi wa China kwa ushirikiano wao na kuguswa na maafa hayo ya tetemeko la ardhi kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.

Kijuu alisema kuwa msaada huo utawafikia walengwa kwa wakati na kamati ya maafa iliyoundwa itasimamia kwa karibu.amesema mpaka sasa kuna shilingi milioni 460 kwenye akaunti ya maafa ya kagera zilizotumwa  na wananchi wote Tanzania

"Ninawahakikishia kuwa msaada huu utawafikia walengwa na hakuna ujanja ujanja wowote utakaotokea,na misaada hii tutaanza kuwagawia walengwa walioathirika zaidi kama waliopoteza makazi,wazee na wajane"alisema Kijuu.

Mabaki yaliyopatikana Pemba nchini Tanzania ni ya shirika la Malaysia Airlines iliyotoweka mwaka 2014

$
0
0
 
Mabaki ya ndege yaliyopatikana katika pwani ya visiwa vya Pemba nchini Tanzania yalitoka kwa ndege ya shirika la Malaysia Airlines iliyotoweka mwaka 2014, maafisa wa Malaysia wamethibitisha.

Waziri wa uchukuzi wa Malaysia Liow Tiong Lai amesema kupitia taarifa, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kwamba baada ya uchunguzi imebainika kwamba kipande hicho kikubwa cha bati kilichopatikana mwezi Juni ni cha ndege hiyo safari nambari MH370.

Amesema uamuzi huo ulifikiwa na wataalamu kutoka Idara ya Usalama wa Safari za Ndege ya Australia (ATSB) na wale wa kuchunguza usalama wa MH370.

Mapema Julai, waziri wa uchukuzi wa Australia Darren Chester alikuwa amedokeza kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa mabaki hayo yalikuwa ya ndege hiyo.Alisema muundo wa mabaki hayo, ukubwa wake na muonekano wake viliashiria kwamba yalikuwa ya ndege hiyo ya Malaysia.

Mabaki hayo pia yalikuwa na muhuri wa kuonesha tarehe ya kuundwa kwake ambayo ilikuwa Januari 23, 2002. Ndege hiyo ya Malaysia iliwasilishwa kwa shirika hilo 31 Mei, 2002, kwa mujibu wa tovuti ya shirika la Channel News Asia.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilitoweka Machi 2014, ikiwa na abiria 239 baada ya kupaa kutoka Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia kuelekea Beijing.
Bw Liow amesema mabaki hayo yatachunguzwa zaidi kubaini iwapo kutapatikana ufumbuzi kuhusu kilichotokea hadi ndege hiyo ikatoweka.

Image copyrightSerikali, Tanzania
 Awali, wachunguzi walikuwa wamethibitisha kwamba mabaki yaliyopatikana visiwa vya Reunion mwezi Julai 2015 yalitoka kwa ndege hiyo.
Mabaki mengine yanayodhaniwa kutoka kwa ndege hiyo yamepatikana Msumbiji, Afrika Kusini na visiwa vya Rodrigues, Mauritius.

CHANZO BBC SWAHILI

UVCCM YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU VURUGU ZA JIJINI ARUSHA,YAMSIMAMISHA KAZI KATIBU WA UVCCM ARUSHA

$
0
0
Jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM imemsimamisha kazi aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel kwa kutotiii agizo la Makao Makuu linalomtaka kuhama na kusibabisha mvutamo na malumbano yasio na tija kwa chama cha Mapinduzi mkoani Arusha.

Pia Jumuiya imewataka vijana wa uvccm kutambua kuwa shughuli za uendeshaji wa umoja huo zinafanyika kwa kufuata taratibu za kikanuni chini ya misingi ya nidhamu na utii.

Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka Hamdu Shaka amewaeleza wandishi wa habari katika ofisi za UVCCM mkoa wa Arusha mara baada ya kumaliza mzozo ulioibuka na kusababisha baadhi ya vijana kufunga ofisi wakimkataa Ezekiel asiendelee kubakia mkoani hapo.

Shaka alisema tokea tarehe 25 August makao makuu ilimuandikia barua Mollel kumuhamishia Makao Makuu Dar Es Salam lakini cha ajabu kwa muda wote amekuwa akikaidi kuhama kwa sababu zake binafsi.

Alisema kikao cha sekreterieti ya Taifa kilichoketi jijijini Dar es salaam 14 September kimeamua kumsimamisha kazi katibu huyo na kumtaka ampishe katibu wa mkoa mpya Said Goha aliyehamia Arusha akitokea lindi

"Mollel amekuwa akidai kuwa Arusha kuna harufu ya ubadhirifu wa mali na miradi ya Jumuiya, Makao makuu haijapinga dai hilo , kuhama kwake si kikwazo cha kuzuia kubaini nani amehusika na tuhuma hizo, amehamishwa kwa sababu za kawaida pia kutokana na sintofahamu iliopo "alisema shaka.

Alipoulizwa iwapo ni mpango wa kukuondoa ili kuficha ukweli wa ufujaji wa miradi alisema kuhama kwake hakuwezi kuzuia ukweli usijukikane, kwani Jumuiya inafanya uchunguzi wa miradi na rasilimali zake pia vyombo vya serikali vimeombwa viingiliie sakata hilo ili kupata ukweli wa mambo.

"Mtumishi unapohamishwa toka kituo kimoja kwenda kingine na kukataa huo ni uvunjaji wa taratibu, ukiukaji wa kanuni na kutoonyesha nidhamu ya kazi, amesimamishwa kazi hadi jambo lake litakapifikishwa katika vikao vya kitaifa vyenye mamlaka ya uteuzi wake wa mwisho kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM"alieleza shaka

Akijibu swali la mwandishi kwamba katibu huyo amekuwa akikaidi kuondoka kwa sababu analindwa na baadhi ya wakubwa wa makao Makuu pia makao makuu ikitaka kumlinda kiongozi mmoja wa juu asihusishwe na ubadhirifu huo, shaka alikana na kusema wanaoeneza maneno hayo ni mashabiki wa kisiasa..

"Nasema vijana wenzetu wa Arusha wafahamu uendeshaji wa kazi zetu ni uzingatiaji wa taratibu na kikaanuni, makao makuu haiwezi kumkingia kifua mwizi na kumtetea , kumlinda na kumtetea mvunja taratibu husika "alisema.

Aidha Kaimu huyo Katibu mkuu alisema kazi ya ufuatiliaji miradi, mikataba , mapato na matumizi yake yatafuatiliwa hatua kwa hatua na ukweli wa jambo hilo utaanikwaa bila mtu kulindwa na kuogopwa.

Hata hivyo shaka alipoulizwa kwamba makao makuu imeshindwa kumchukulia hatua za kinidhamu mwenyeikiti wa mkoa huo Lengi Sabaya anayedaiwa kufanya hadaa na kukutwa na vitambulisho feki , alijibu kuwa madai hayo ni binafsi yenye mwekeleo wa jinai na iwapo kweli anakabiliwa na tuhuma hizo vyombo vya dola vipo na vinapaswa kuchukua hatua haraka UVCCM haitamlinda mtu katika jambo lolote lililo kinyume na maadili ya Chama.

Pia akiwataka wana Jumuiya kuacha tabia ya kubuni au kubashiri mambo ambayo mtu hana ushahidi nayo akidai kwamba kiongozi fulani anamlinda mtu fulani wakati hakuna kiongozi makini anayeweza kumlinda mtu anayekiuka kanuni na kuvunja taratibu halali

"chama chetu kina Katiba jumuiya yetu ina kanuni toleo la 2012 tuna kanuni ya utumishi kanuni ya fedha na maadili iyo ndio miongozo yetu katika kutekeleza majukumu ya kila siku hatutafumbia macho mtu yoyote atakaepindisha mstari mmoja wa kanuni au taratibu kwa vile hakuna aliye juu ya miongozo hiyo" alisema shaka

Amewataka vijana wa Arusha kuwa watulivu kwani viongozi wote wako makini katika kila jambo na jumuiya Arusha itaendelea kubaki salama.

Shaka amewasili mkoani arusha jana kufuatia kuibuka kwa mzozo uliosabanisha baadhi ya vijana kumfungia ofisi katibu aliyehamishwa Ezekiel molel ambae anaungwa mkono na Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa huo kwa madai amempa kazi afanye na hajakamilisha.

WATAALAMU WAOMBWA KUTOA ELIMU YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA ASILI.

$
0
0
 
 Na. Sheila Simba,MAELEZO.
 
Jumuiya ya Wanataluma wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDASA) imesema kuwa itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na majanga ya asili yanayotokea katika maeneo mbalimbali nchini, kutoa msaada wa kitaalam na kuwasaidia waathirika wa majanga hayo.

Aidha, itaendelea kuwahamasisha wadau mbalimbali waendelee kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo vyakula, maji safi na salama, makazi ya muda na madawa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera ili kuwaepusha na magonjwa ya kuambukiza.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wanajumuiya hao leo jijini Dare Es Salaam na Mtaalamu wa Jiologia wa chuo hicho Dkt.Elisante Mshihu amesema kuwa jumuiya yao itaendelea kutoa elimu na taarifa sahihi kwa umma kupitia tafiti mbalimbali zinazohusu matetemeko ya ardhi kama nyenzo muhimu ya kukabiliana na majanga hayo.

“Matetemeko ni hali ya kawaida duniani na kwa hapa kwetu yamekua yakitokea katika mikoa ya Dodoma,Arusha,Bukoba na Singida ndani ya miaka kumi hivyo ni vyema wananchi wafahamu namna ya kukabiliana nayo yanapotokea”alisema Dkt Mshihu

Dkt.Mshihu amesema elimu na taarifa sahihi ni nyezo madhubuti ya kukabiliana na majanga ya asili kokote Duniani,na kuongeza kuwa uwekezaji katika elimu ni jambo linalohitajika kwa sasa hapa nchini.

“Itabidi elimu ya juu na vyombo vya habari vijengewe uwezo wa kifedha na kitaaluma ili kutimiza majukumyu yake wakati wa kukabiliana na majanga haya ya asili ”alisisitiza Dkt.Mshihu. Ameongeza kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inapaswa kuelekeza nguu zake katika eneo hilo kwani kijiografia na kijiolojia inaonyesha Nchi zote wanachama ziko katika hatari ya kukubwa na majanga ya asili.

Aidha jumuiya hiyo imefungua akaunti katika bank ya NBC yenye jina la UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM SELF INSURANCE,akaunti namba 040103001175 katika tawi la Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam,na kuomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia waathirika wa tetemeko lilitokea mkoani kagera hivi karibun

BANK OF AFRICA (BOA) YAZIDUA KADI MBILI AMBAZO NI TOUCAN VISA NA PROXMA VISA JIJINI DAR.

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Huduma za Kibenk Kidigital wa Bank of Africa (BOA), Bw. Emmanuel Mshindo akionyesha kadi aina ya TOUCAN iliyotolewa na benki ya Afrika (BOA). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo, Bw. Kaisha Boge. Meneja Masoko, Utafiti na Maendeleo wa Bank of Africa (BOA), Bw. Muganyizi Bisheko akionesha card aina ya PROXIMA iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Benki ya Afrika (BOA) imezindua kadi mbili TOUCAN VISA CARD na PROXMA VISA CARD ambazo zinasaidia kulinda usalama wa mteja tofauti na zilizokuwa zimetolewa mwanzo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Huduma za Kibenki Kidigital wa Bank of Africa (BOA), Bw. Emmanuel Mshindo. Picha na Emmanuel Massaka wa Blogu ya Jamii. Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo, Bw. Kaisha Boge (katikati) akizielezea kadi hizo zilizotolewa nabenki ya Afrika (BOA) mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

SERIKALI KUFUTA UJINGA IFIKAPO MWAKA 2030

$
0
0

 Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (katikati), akisoma hutuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kusoma Vitabu chini ya Hema Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwale, iliyoratibu maadhimisho hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Haki Elimu, John Kalaghe.
 Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kulia), akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Mradi wa Usomaji Room to Read, Mkurugenzi wa Mradi, Room to Read, Juvenalius Kurulatera na Mkurugenzi Mkuu, Haki Elimu, John Kalaghe.
 wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wanafunzi wakishiriki maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Wadau wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mbaruku kutoka wilayani Bagamoyo wakiigiza Igizo la Almas na Jitu kwenye maadhimisho hayo.
 Wanafunzi wakiwa makini kusikiliza mada.
 Wanafunzi kutoka kituo cha kujisomea cha Early Lead Club wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wadau na raia wakigeni wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Ofisa wa Room to Read kutoka Mikocheni, Veronica Mahenge (kulia), akitoa zawadi ya vitabu kwa wanafunzi waliosoma vizuri vitabu mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.

Na Dotto Mwaibale

OFISA Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda kwa niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawe, amesema serikali itashirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mwaka 2030 wawe wamefuta ujinga nchini.

Mapunda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya usomaji vitabu kwenye hema yanayoadhimishwa duniani kote. 

Alisema moja ya shabaha iliyopo kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuhakikisha kila mtoto nchini anapata elimu bure kuanzia darasa la kwaza hadi kidato cha nne.

"Nafahamu shirika lenu la Room to Read limekuwa likitumia mbinu mbalimbali katika kuendeleza elimu bora kwa kuweza kujenga maabara katika shule zetu, kutoa vitabu na mambo mbalimballi katika kupambana na elimu," alisema.

Alisema takwimu za kitaifa za sensa ya makazi na watu katika mwaka 2012 zinaoonesha kuwa asilimia  22 ya watanzania hawezi kusoma na kuandika kwa ufasa, 81.7 ni wenye ya msingi 14.4 ndio wenye elimu ya sekondari na asiimia 2.3 elimu ya  chuo. 

Alisema kiwango hicho kidogo kinasababisha watoto kutokuwa na msingi imara katika kipindi cha mwazoanapoanza shule.

"Kwa mfumo unaofanywa na Room to Read katika kuhakisha wanafunzi wanajua kusomma na kuandika afikapo darasa la tatu ni wazi kuwa serikali tunapaswa kujifunza ili kuhakisha hadi ifikapo 2030 tunakuwa tumefanikiwa kufuta ujinga," alisema Mapunda.

Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inayosema 'Kuandika yaliyoita, Kusoma yajayo' itumike kutafakari kufuta ujinga.

Awali Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwale alisema siku ya usomaji duniani ni siku muhimu kwa wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi wenyewe, wazazi, walimu, mashirika yasio ya kiserikali na serikali.

Alisema siku hiyo huadhimishwa kila mwaka  ifakapo Sepemba 9, ikiwa ni kutimiza azimio la Tehrani lilipitishwa mwaka 1965 ambapo kwa mwaka huu wanaadhimisha miaka 50 tangu kuazshwa kwake mwaka 1966.

"Kutokana na kuwepo kwa mitiani ya Taifa ya darasa la saba, sisi Room to Read  na washiriki wezetu tuliona ni vyema kuadhimisha siku hio leo ili kupisha tukio muhimu la wadau wetu," alisema.

Mwakabwale alisema takwimu za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) za mwaka 2015 zinaonesha hali ya usomaji duniani katika nchi saba Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Tanzania ni ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha watazania wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha kwa asilimia 80.3.

Alisema Nchi ya Burundi inaongoza katika nchi za ukanda huo kwa asilimia 85.6 ya wananchi wake wanajua  kusoma na kuandika kwa kiwango cha juu ukilinganisha na nchi nyingine.

Maadhimisho hayo yalinogeshwa na Taasisi ya Room to Read kwa kufanya maonesho ya vitabu na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kupata fursa ya kusoma vitabu na kuulizwa maswali pamoja na kupata zawadi za vitabu

Waganga Wakuu wa Mikoa waagizwa kuhakiki takwimu za chanjo

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
15/09/2016 .

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa kuhakiki takwimu za chanjo na kuzitawanya wilaya kwa wilaya ili kuhakikisha vituo vyote vinapata chanjo zilizopo. 

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo mjini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kuhusu upungufu wa baadhi ya chanjo katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Waziri Ummy amesema kuwa licha ya kuwa na uhaba wa chanjo, kuna baadhi baadhi ya wilaya ambazoo chanjo ya aina moja haipo wakati wilaya nyingine chanjo hiyo ipo. 

“Licha ya uhaba wa chanjo, kuna baadhi ya wilaya ambazo chanjo ya aina moja haipo ila wilaya nyingine chanjo hiyo ipo, kwa mfano chanjo ya kifua kikuu kwa manispaa ya Dodoma, kuna chanjo dozi 6540 wakati wilaya za Bahi, Chamwino na Chemba hakuna kabisa chanjo hiyo”, amefafanua Waziri Ummy.. 

Hata hivyo Waziri Ummy amewataka Waganga hao Wakuu wahakikishe wanapitia takwimu hizo ndani ya mikoa yao ili kuweza kuzitawanya chanjo hizo kwenye wilaya zote ambazo hazina au zenye upungufu. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa ili kukabiliana na upungufu chanjo nchini, Wizara hiyo imenunua na inategemea kupokea chanjo kiasi cha dozi milioni mbili za kinga dhidi ya Kifua Kikuu (BCG) Septemba 28, mwaka huu, chanjo ya Polio dozi milioni mbili Septemba 19, 2016 na chanjo ya Pepopunda dozi 1,240,000 Septemba 26, mwaka huu. 

Pia Waziri Ummy amesema kuwa Wizara imepokea fedha kutoka Hazina kwa ajili ya ununuzi wa chanjo nyingine za Surua na Rubella na zitategemewa kutumwa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) mbao ndio wanunuzi wa chanjo nchini. 

Mbali na hayo Wizara hiyo inaendelea kuwahimiza wananchi hasa wazazi na walezi wenye watoto wa umri wa kupata chanjo, kuwa mara wapatapo taarifa ya uwepo wa chanjo zilizokosekana wawapeleke watoto wao ambao hawakupata chanjo au kukamilisha chanjo kulingana na ratiba ili kuweza kukamilisha chanjo zao na kuwahakikishia usalama wa afya watoto wao. 

Zaidi ya hayo, Serikali inawahakikishia wananchi wote kuwa huduma za afya ikiwemo chanjo zinaendelea kutolewa nchini bure, hivyo wananchi waendelee kutumia huduma hizo wakati wote kwani chanjo ni haki ya msingi kwa kila mtoto. 

Chanjo ambazo zilikuwa na upungufu nchini ni pamoja na chanjo kwa ajili ya kukinga ugonjwa wa Surua na Rubella (MR) Kifua Kikuu (BCG), Polio (OPV) na Pepopunda (TT) ambazo hutumika kwa watoto kuanzia wanapozaliwa hadi miaka miwili na kina mama wajawazito kulingana na mwongozo wa chanjo uliotolewa na Wizara ya Afya ili kuwakinga na magonjwa hayo

Wananchi wahamasishwa kushiriki matembezi ya hisani kuchangia wahanga wa tetemeko la Kagera

$
0
0


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO



Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na  Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa matembezi ya hisani ili kusaidia wahanga waliokumbwa na maafa ya  tetemeko  la ardhi  lilitotokea  Septemba 10 mwaka huu, huko mkoani  Kagera.


Akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga amesema kuwa, matembezi hayo ya hisani ya kilomita tano yataongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.


   Aliongeza kuwa Matembezi hayo yatafanyika siku ya Jumamosi Septemba17 mwaka huu, ambapo yataanzia Bwalo la Polisi Osterbay (Polisi Officer’s Mess) kuanzia saa 12 asubuhi.


Aidha amesema kuwa, matembezi hayo yana lengo la kuhamasisha wafanyabiashara, taasisi za fedha, kampuni mbalimbali pamoja na  jamii ya watanzania, wanadiplomasia waliopo nchini kuchangia kwa kutoa misaada mbalimbali ili kusaidia wahanga maafa ya tetemeko la ardhi la mkoani  Kagera.


“Tunafanya kampeni hii ya tembea kwa ajili ya Kagera, kwa lengo la kuwahamasisha watanzania, wafanyabashara na jumuiya ya wanadiplomasia waliopo nchini ili kila mtu aweze kushiriki kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha kitakachosaidia wenzetu waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Kagera” alisema Kasiga


Hivyo basi, Wizara hiyo imeeandaa daftari maalumu la michango kwa jumuiya ya mabalozi  katika nchi zote zenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, ili kuunga mkono zoezi la kuwasaidia wahanga wa maafa ya tetemeko la ardhi lilitokea mjini Bukoba.


Pia Serikali imefungua akaunti rasmi kwa jina la Kamati Maafa Kagera katika benki ya CRDB ya  mkoani Kagera yenye namba 0152225617300 ambayo itakayotumika kupokea  michango kutoka kwa watu mbalimbali.

POLISI JIJINI DAR YAWAKAMATA BEACH BOYS 33 KWA TUHUMA ZA KUWAHADAA WASICHANA KIMAPENZI

$
0
0
Polisi jijini Dar es Salaam wamewakamata watu 33 wakiwamo vijana wanaopenda kukaa ufukweni maarufu ‘beach boys’ kwa tuhuma za kuwahadaa wasichana kimapenzi.Vijana hao, wanadaiwa kuwarubuni wasichana kuwa watawafundisha kuogelea lakini baadaye huwalazimisha kufanya ngono wakiwa majini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya askari kufanya msako na kukutwa wakifanya mapenzi kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA SARPCCO EXTRA ORDINARY MEETING KESHO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mkuu wa mkoa wa Arusha Ndugu Mrisho Gambo  mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa  Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) utakaofanyika mkoani Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Lekule Laiza (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) utakaofanyika mkoani Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbali mbali waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) utakaofanyika mkoani Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

Denmark, Ujerumani yaonesha nia uzalishaji wa mbolea

$
0
0
 Naibu  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe (aliyekaa mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha mabalozi kutoka katika nchi  za Ujerumani na  Denmark pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika  hivi karibuni jijini  Dar es Salaam
 Sehemu ya mabalozi na wawakilishi  kutoka katika nchi za Denmark na  Ujerumani  wakifuatilia kwa makini maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe ( hayupo pichani)
 Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen akieleza jambo katika kikao hicho.
 Naibu  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe  akielezea fursa za uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini
 Naibu  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini, James Andelile (kulia) wakifuatilia  maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen (hayupo pichani)
 Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (kulia) kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen (kushoto) akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Naibu  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo jijini Dar es Salaam
Kutoka kulia Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen, Naibu  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo,  Mwakilishi kutoka kampuni  ya Ferrostaal Industrial Projects, Wilfried Wiemann na mwakilishi kutoka  Ubalozi wa Denmark, Mette Melson wakiwa katika picha ya pamoja.
 
Na Greyson Mwase

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe amekutana na mabalozi kutoka nchi za Ujerumani na Denmark ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kumilikiwa na kampuni za Ferrostaal Industrial Projects ya Ujerumani, Haldor Topsoe ya Denmark na Fauji Fertilizer Limited ya Pakinstan kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)

Akizungumza katika kikao hicho kilichokutanisha pia watendaji kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati naMaji (EWURA) na TPDC, Balozi wa Denmark Nchini Einar Jensen alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa kiwanda cha mbolea, Tanzania itapata manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na ajira, fedha za kigeni kutokana na kuuza mbolea nje ya nchi na hivyo kuinua uchumi wa nchi.

Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho bado yanaendelea ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali.

Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 za kiasi cha matumizi ya kemikali haribifu

$
0
0
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO, Dodoma.
 
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86 ya kiasi cha matumizi ya kemikali haribifu chini ya programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali hizo.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo mjini Dodoma kuelekea kilele cha   maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni Septemba 16, mwaka huu.
Waziri Makamba amesema kuwa upungufu huo umetokana na jitihada za utekelezaji wa mpango wa usimamizi wa vipozi uliowezesha uwekaji wa mtambo wa kunasa na kurejeleza kemikali uliopo katika kituo cha Tanzania cha uzalishaji bora na teknolojia endelevu.

Aidha, Waziri Makamba alisema kuwa mpango huo uliwezesha ununuzi na usambazaji wa mashine 20 za kunasa na 5 za kunasa na kurejeleza gesi katika karakana 20 na vituo vitano vya kanda vya kunasa na kusafisha gesi chakavu za majokofu na viyoyozi katika vyuo vya VETA vya Mwanza, Dar es Salaam, Kigoma, Mbeya na Mkokotoni Zanzibar.

Mbali na hayo, Waziri Makamba ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika kupunguza na kuondosha madhara ya Tabaka la Ozoni yanayosababishwa na bidhaa zinazotumika majumbani au sehemu za biashara.

Waiziri Makamba amesema kuwa ili kuhifadhi tabaka la Ozoni nchini, jamii kwa ujumla inapaswa kuepuka kuingiza gesi zilizopigwa marufuku nchini sambamba na vifaa vinavyotumia gesi haribifu ikiwemo majokofu na viyoyozi vilivyokwishatumika na ambavyo vinatumia vipoozi aina ya R11 NA R12.

Aidha, wananchi wametakiwa kuepika kutupa ovyo majokofu ya zamani ama vifaa vya kuzima moto vyenye kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni aina ya CFCs na halon na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mafundi ama mamlaka husika.

Kila mwaka, Septemba 16 Tanzania inaungana na Jumuiya ya kimataifa huadhimisha siku ya Kimataifa ya Hifadhi la Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Ummoja wa Mataifa katika Azimio nambari 49/114 la 19 Desemba 1998 ikiwa kumbukumbu ya kutiwa saini Mkataba wa Montrel kuhusu kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni angani

Shilingi bilioni 6.6 zatumika kunufaisha kaya maskini Dar es Salaam.

$
0
0
Na: Abushehe Nondo & Frank Shija

MAELEZO

JUMLA ya kaya 26,248 zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) kwa kupatiwa jumla ya shilingi Bilioni 6.6 katika mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando wakati akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Mmbando amesema kuwa utambuzi wa kaya maskini ulianza mwezi Januari 2015 kwa kushirikisha wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala ambapo jumla ya kaya 26,248 zilizoandikishwa na kupokea ruzuku kila baada ya miezi miwili kwa kuzingatia mzunguko wa malipo.

Aliongeza kuwa wanufaika wa mpango huo wamepatikana kutokana na ushirikishwaji wa jamii husika ambapo jamii yenyewe ilibainisha majina ya walengwa katika maeneo yao.

Aidha Mmbando amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo kuna baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza mpango huo ikiwemo baadhi ya kaya zilizokidhi vigezo kukataa kuandikishwa, kuandikishwa kwa kaya zisizokuwa na sifa, pamoja na kupokea ruzuku pungufu.

Katika kukabiliana na changamoto hizo, Mmbando amesema mpaka sasa jumla ya kaya 609 zimeondolewa katika kwenye mpango huo ikiwemo kaya 141 (Ilala), kaya 296 (Kinondoni) na kaya 172 (Temeke).

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Mkoa wa Dar es Salaam, Esterine Sephania amesema kuwa suala la udanganyifu wa kuandikishwa kwa walengwa wasiokuwa na sifa linaanzia katika ngazi ya serikali za mitaa ambapo huko ndiko wanaleta majina.

Aliongeza kuwa kutokana na udanganyifu uliojitokeza katika zoezi hilo takribani shilingi milioni 2.2 zimepotea kupitia udanganyifu uliotokana na uandikishwaji kwa watu wasiokuwa na vigezo.

ASILIMIA 96 YA WANANCHI WAKUBALI UTENDAJI KAZI WA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.

$
0
0

Na Daudi Manongi,MAELEZO.

Dar es Salaam

TAKWIMU zilizotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza imeonyesha kuwa asilimia 96 ya wananchi wanakubali hatua za kiutendaji kazi za Rais John Pombe Magufuli ikiwemo uondoaji wa wafanyakazi hewa na sera ya elimu bure.

Taarifa iliyotolewa leo katika vyombo vya habari na Mshauri Mwandamizi wa Mawasiliano wa Twaweza, Risha Chande alisema asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo mpaka mwisho wa awamu yake ya kwanza ya uongozi.

“Utafiti huu unaonyesha kuwa asilimia 69 ya wananchi walifuraishwa na juhudi za Rais za uondoaji wa wafanyakazi hewa, wakati asilimia 61 walipongeza sera ya elimu bure wakati asilimia 61 walifurahishwa na usimamishwaji wa watumishi wa serikali” alisema Chande.

Chande alisema kuwa katika utafiti huo unaonyesha wananchi wengi kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano ya kufanya maboresho katika huduma za umma ikiwemo mamlaka ya mapat (asilimia 85), mashuleni (asilimia 75),vituo vya polisi (asilimia 74),mahakama (asilimia 73), vituo vya afya (asilimia 72).

Aliongeza kuwa kwa upande wa huduma zinazotolewa katika utumishi wa umma, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 95 ya wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na madaktari, walimu, na maofisa tawala katika ofisi za umma.

“Pamoja na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa Serikali ya wamu ya Tano wananchi wamesema suala la umakini na kanuni za demokrasia na haki ni vyema zifuatwe ambapo wananchi nane kati ya kumi wanasema watendaji waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu” alisema Chande.

Akifafanua zaidi Chande alisema utafiti huo pia umeonyesha kubadilika kwa matarajio ya wananchi ambapo katika kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya kutojali miongoni mwa wananchi kulikotokana na utendaji duni kutoka kwa watendaji.

Serikali ina uwezo wa kugundua barabara iiliyojengwa chini ya kiwango

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma

Serikali ina uwezo wa kugundua barabara iiliyojengwa chini ya kiwango kwa kukagua miradi inayotekelezwa wakati wote wa ujenzi wa miradi hiyo hata baada ya kukamilika kabla ya muda wa ukaguzi wa mwisho kupita.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani alipokuwa akijibu swali la Miza Bakari Haji Mbunge wa Viti Maalum lililohoji kama Serikali inaweza kugundua ni barabara ngapi zilizotengenezwa chini ya kiwango nchini.

Mhandisi Ngonyani alizitaja barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami ambazo zilikuwa matatizo mbalimbali kabla ya muda uliotarajiwa kuwa ni pamoja na Kilwa ambayo inaanzia Mbagala Rangi Tatu hadi Bendera Tatu, Sekenke hadi Shelui, Kyamorwa  hadi Buzirayombo na Nangurukuru hadi Mbwemukulu.

Barabara hizo zilipokamilika yalijitokeza matatizo mbalimbali kabla ya muda uliotarajiwa yanayotokana na mapungufu kwenye ubora kama mashimo katika barabara hizo na kuharibika kwa tabaka mbili za juu.

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa ujenzi wa barabara hutengenezwa kwa kuzingatia mikataba kati ya TANROADS na Mkandarasi na kati ya TANROADS na Mhandisi Msimamizi na viwango vinavyotakiwa kwenye ujenzi wa mradi huo wa barabara vimetajwa kwenye mkataba husika.

“Endapo kunatokea tatizo lolote kuhusu ubora wa kazi, kwa mfano barabara kujengwa chini ya kiwango, vipengele vya mkataba husika vitatumika kubaini nani aliyesababisha mapungufu hayo kati ya Mkandarasi, Mhandisi Msimamizi au mwajiri na hatimaye kuwajibika” alisema Mhandisi Ngonyani.

Katika kudhibiti nidhamu ya kuheshimu mikataba, Mhandisi Ngonyani alisema kuwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mradi wa ujenzi wa barabara husika hatua zilichukuliwa kulingana na vipengele vya mikataba husika na Mkandarasi wa miradi hiyo walirekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika barabara hizo kwa gharama zao wenyewe.

Wingi wa magari nao umeainishwa kuwa ni sababu nyingine ambayo inasababisha uharibifu wa barabara kutokana na wingi wa magari makubwa ya mizigo yanayotumia ekseli zenye tairi moja.

Ili kuhakikisha uthibiti wa uzito wa magari, Serikali inafanya utaratibu wa kufanya mabadiliko ya kanuni za usalama barabarani za mwaka 2001 ziweze kuoana na Sheria ya Uthibiti wa uzito wa magari ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambayo imeweka kiwango cha uzito wa tani 8.5 kwenye ekseli zenye tairi moja.

Akijibu swali la Mbunge wa Nanyumbu Mhe. Dua William Nkurua aliyehoji ni lini Serikali itatekeleza miradi ya barabara wilaya ya Nanyumbu, Mhandisi Ngonyani alisema kuwa Wakala wa Barabara Tanzania imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Nangomba hadi Nanyumbu hatua ambayo itasaidia kujengwa kwa barabara hiyo. 

Madereva wa malori wa Tanzania na Kenya waliotekwa DR Congo waokolewa

$
0
0
Madereva wa malori kutoka nchini Tanzania waliokuwa wametekwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hatimaye waokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo.

Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ambaye ameiambia BBC kuwa wote wapo salama.Mwandishi wa BBC wa eneo la mashariki mwa Congo Byobe Malenga ana taarifa zaidi.CHANZO BBC SWAHILI

Vijana nchini wahimizwa kuunga mkono kampeni ya Uchumi wa Kijani.

$
0
0

Mkutano Vijana na Uchumi wa Kijani
Baadhi ya picha kutoka katika mkutano huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Raleigh Tanzania, Bw Alistar Mackay akizungumza na washiriki wa mkutano


Washiriki wa mkutano huo
Wawakilishi wa taasisi na ofisi za serikali
Mgeni Rasmi akizungumza na waandishi wa habari

Ms Clara Makenya kutoka United Nations Environment Programme akizungumzia uchumi wa kijani katika mkutano huo.

Vijana nchini Tanzania wahimizwa kujiunga na kampeni ya Vijana kwa Maendeleo ya Kijani ili kulinda mazingira kwa kuyafanya endelevu sambamba na kujiiinua kiuchumi.

Hayo yalibainishwa na Afisa Mawasiliano wa shirika la kimataifa la Raleigh Tanzania Bw. Kennedy Mmari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Uchumi wa Kijani kwa Vijana iliyofanyika kwatika ukumbi wa British Council.

Bwana Mmari alisema kuwa wao kama shirika linalojihusisha na vijana wamekuja na kampeni hii ya kitaifa kwakua wanaamini uwezo walionao vijana katika kuleta mabadiliko endapo watapewa nafasi.

“Sisi kama vijana tunahitaji sana maendeleo ya kiuchumi ila lazima maendeleo hayo yalinde mazingira yetu hivyo basi tunahitaji uchumi wa kijani, uchumi ambao utazingatia vilivyo shughuli za kiuchumi kwaajili ya kupunguza umasikini lakini ukijikita pia katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mazingira endelevu” alielezea Bw. Mmari.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Injinia Ngosi Mwihava alisema wao kama Serikali wametoa Baraka zote kwa kampeni hiyo kwani athari za mabadiliko ya tabia nchi zimedi kuongezeka siku hadi siku.

“Sisi kama serikali ni jukumu letu kuhakikisha wananchi wanayatunza mazingira na kuyafanya yawe endelevu, na ndio maana leo tupo hapa na vijana ili kuhakikisha elimu ya mazingira endelevu inawafikia na wao wanaisambaza” alisema Injinia Mwihava.

Aidha Injinia Mwihava alisema kuwa serikali itahakikisha mazingira yanalindwa na kuwa endelevu hivyo wataanza na kupiga marufku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Januari mwakani kama njia mojawapo wa kuzuia uchafuzi wa mazingira.

“Serikali sasa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaandaa kanuni za kudhibiti mifuko ya plastiki nchini na hata kama mgeni akija nayo toka nje akifika mpakani lazima aambiwe kuwa hatutumii tena mifuko ya plastiki” alisisitiza Injinia Mwihava.

Naye mmoja wa vijana waliohudhuria hafla hiyo Pius Matunge alisema ni wakati sasa kwa vijana kushika hatamu kwenye kulinda mazingira.

"Kila kijana lazima ajione yuko mbele kwenye kulinda na kuyatetea mazingira ili yaweze kutumika kwenye kuinua uchumi wa nchi yetu" alihitimisha Bw. Pius.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na shirika Raleigh Tanzania ilikutanisha pamoja vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini na mashirika mbalimbali na wadau wa mazingira kujadili jinsi gani vijana wanaweza kuwa mawakala wa maendele ya Uchumi wa Kijani.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images