Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

SIKU YA KUSOMA DUNIANI: ROOM TO READ WADHAMIRIA KUONDOA UJINGA KWA VITENDO

0
0
 Hii ni maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo kuna vitabu vya aina mbalimbali vya masomo kuanzia Darasa la Kwanza mpaka la Saba 
Wanafunzi wakiwa wametulia wanasoma vitabu katika maktaba yao ambapo kila mmoja anaamua asome kwa namna gani  
Wanafunzi wa Darasa la kwanza wakiwa wanaendelea kusoma.
 
 Watoto wanafunzi wa Darasa la kwanza kutoka Shule ya msingi ya Zinga wakiwa wanaweza kusoma vitabu wakiwa na miezi sita tuu ya darasani kupitia Programu ya Room to read
 Watoto wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi ya Zinga iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wakiwa wanajifunza matamshi ambapo mpaka sasa wanaelewa vizuri na hizi ni juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika la Room to Read.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Zinga Msafiri Tolla akielezea namna walivyoweza kunufaika na Programu ya Room to Read ambapo amelishukuru shirika hilo na  ameeleza mafanikio waliyo yapata kutokana na kujengewa Maktaba na Darasa ikiwa ni pamoja na kuwa imesaidia kupunguza upungufu wa Madarasa, katika Maktaba imeweza kusaidia kiwango cha usomaji kwa wanafunzi na kufanya wanafunzi wengi kupenda kusoma shuleni hapo, na imewawezesha hata wanajamii wanayo izunguka shule kuwa na utaratibu wa kujisomea katika Maktaba hiyo, mwisho alisema kuwa kwa sasa wanafunzi wanaweza kujisomea wenyewe bila matatizo
Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Bi. Ester Lumato akielezea umuhimu wa Shirika la Room to Read ambapo katika shule ya Msingi Zinga walianza kufanya nao kazi kuanzia mwaka 2015,alisema miaka ya nyuma iliyopita taaruma ilikuwa chini lakini baada ya kuanza kufanya kazi na Room to Read kiwango hicho cha taaluma kimeongezeka zaidi. Ameongeza kuwa zamani mwanafunzi alikuwa anamaliza darasa la Saba hajui kusoma wala kuandika lakini kwa sasa wanamaliza wakiwa wanajua hayo yote kwa sababu ya shirika hilo kutoa Maktaba na Vitabu vya kutosha, mwisho alitoa wito kwa Mashirika mengine kujitoa kama Room to Read
 Joackim Kawa Meneja wa mradi wa Usomaji na maktaba kutoka Shirika Room to Read akielezea miradi ambayo wanaendesha ikiwa katika shule za Msingi wanatekeleza Mradi wa Maktaba na Kusoma ambapo kuna walimu maalum  katika shule 62 za Bagamoyo wanaandaliwa kuhakikisha wanafunzi wanaweza kusoma na na kuandika vizuri,ambapo mradi huu umetekelezwa Mkoani Morogoro pia aliongeza kuwa wanampango wa kupanua wigo zaidi wa miradi yao katika maeneo mengine nchini Tanzania
 
Hapa kila mmoja anaelewa anacho kisoma hii ni kutokana na kuwa na walimu ambao wamewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo wamekuwa wanaweza kusoma na kuandika vizuri 
Wanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya ya Msingi Zinga wakiwa wanafurahia kupata Vitabu kutoka Shirika la Room to Read
 Wanafunzi wakiwa wanachambua vitabu kwa ajili ya kujisomea katika maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read.
 Hii ni Maktaba ya Shule ya Msingi ya Kiromo ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kiromo Bi. Flora Mlowe  alisema kuwa mradi wa Room to Read umeinufaisha sana shule yake kwanza wameweza kupata chumba cha kusomea amacho kimewasaidia sana wanafunzi tofauti na ilivyokuwa mwanzoni, aliongeza kuwa mradi huo umewafanya wanafunzi waweze kuongeza juhudi za kujisomea, wanasoma kwa burudani na pia wanapata maarifa mbalimbali kupitia vitabu hivyo, hiyo imesaidia kuondoa kundi kubwa la wanafunzi ambao hawajui kusoma alimaliza kwa kusema kuwa kuwepo kwa Maktaba hiyo kutaongeza zaidi ufauru katika shule yake.
 Furaha Tonya Social Mobilizer wa Shirika la Room to Read Tanzania akiwa katika Shule ya Sekondari Matibwa iliyopo Bagomoyo akielezea mradi wa Elimu kwa mtoto wa Kike Tanzania unaoendeshwa na Shirika la Room to Read ambapo moja ya mambo wanayo fundisha ni Life Skills ambapo lengo kubwa ni kuwataka watoto waweze kujitambua.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Matibwa Ally Kilasama alisema kwamba mradi huo umeweza kuwasaidia watoto wengi zaidi wa kike kuwepo katika shule hiyo, katika mradi wa life skills alisema kuwa kwa sasa watoto wa kike  wameweze kujitambua zaidi na watoto wa kike wanafanya vizuri zaidi kulipo wale wa kiume, pia kupitia mradi huo kutoka Room to Read wameweza kupata vifaa ya Sayansi na vitabu vya kutosha kwa wanafunzi na kwa sasa wanakarabati madarasa manne hii ikiwa ni juhudi za kutokomeza ujinga.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kingani wakiwa darasani wanamsikiliza mwalimu
 Kutokana na wanafunzi wakike kuelewa Elimu ya Life Skill wameweza kuwaburuza wanafunzi wa kiume katika ufauru darasani ambapo katika Kidato cha tatu Mchepuo wa Sayansi shule ya Sekondari Kingani Mwanafunzi mmoja tu wa kiume  ndiye ameweza kuingia katika kumi Bora ambapo hapa anaelezea jinsi kulivyo na changamoto ya ushindani katika darasa hilo na kukili kuwa watoto wakike wanaweza sana 
 Rose Jeremiah Ngalya Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Mchepuo wa Sayansi aliye ongoza na kushika nafasi ya kwanza akieleza namna ya Shirika la Room to Read lilivyo wasaidia katika kuhakikisha wanapata Elimu Bora.
 
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

WASHRIKI MISS KINONDONI WAPIGA JEKI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA WILAYANI KINONDONI

0
0
 
 Picha ya Pamoja
 Miss kinondoni 2016 pamoja na washiriki wengine wakikabidhi asilimia 10% ya mapato kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa  kwa mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh.Hapi ambayo yalipatikana katika hafla fupi ya kumpata mwakilishi wa miss kinondoni 2016



WAREMBO walioshiriki shindano la Miss Kinondoni 2016, wamekabidhi msaada wa fedha taslimu Sh. milioni moja kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule zilizopo katika wilaya hiyo.

Wakikabidhi fedha hizo jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi walipomtembelea ofisi kwake, mshindi wa shindano hilo, Diana Edward, alisema kuwa wamefanya hivyo wakitimiza ahadi yao waliyoitoa walipomtembelea kiongozi huyo mwezi uliopita.

“Tulipokuja ofisi kwako, tuliahidi kutoa asilimia 10 ya mapato ya viingilio kusaidia ujenzi wa madarasa na leo tumekuja kutimiza ahadi yetu ili kuwasaidia wadogo zetu waweze kupata elimu katika mazingira bora yatakayowawezesha kuelewa vizuri zaidi masomo yao,” alisema.

Akipokea msaada huo, Hapi aliwashuku warembo hao na kamati ya Miss Kinondoni kwa ujumla kwa kuonyesha kuguswa na jitihada za Rais John Magufuli za kuboresha elimu nchini, akitoa wito kwa wadau wengine kumuunga mkono kiongozi huyo wa nchi.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mh. Hapi, msemaji wa Rahmat Entertainmen, waandaaji wa Miss Kinondoni, George Yusuph, alimtaka mkuu huyo wa wilaya kuendelea kuwasapoti katika mashindano ya mwakani, huku akitamba taji la Miss Tanzania mwaka huu kutua Kinondoni.

ROOM TO READ WADHAMIRIA KUONDOA UJINGA KWA VITENDO.

0
0
.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kingani wakiwa darasani wanamsikiliza mwalimu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Room to Read, Peter Mwakabwale akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea siku ya kusoma dunia ambapo kilele chake ni Kesho Septemba 9.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Zinga Msafiri Tolla akielezea namna walivyoweza kunufaika na Programu ya Room to Read ambapo amelishukuru shirika hilo na  ameeleza mafanikio waliyo yapata kutokana na kujengewa Maktaba na Darasa ikiwa ni pamoja na kuwa imesaidia kupunguza upungufu wa Madarasa, katika Maktaba imeweza kusaidia kiwango cha usomaji kwa wanafunzi na kufanya wanafunzi wengi kupenda kusoma shuleni hapo, na imewawezesha hata wanajamii wanayo izunguka shule kuwa na utaratibu wa kujisomea katika Maktaba hiyo, mwisho alisema kuwa kwa sasa wanafunzi wanaweza kujisomea wenyewe bila matatizo
Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Bi. Ester Lumato akielezea umuhimu wa Shirika la Room to Read ambapo katika shule ya Msingi Zinga walianza kufanya nao kazi kuanzia mwaka 2015,alisema miaka  ya nyuma iliyopita taaruma ilikuwa chini lakini baada ya kuanza kufanya kazi na Room to Read kiwango hicho cha taaluma kimeongezeka zaidi. Ameongeza kuwa zamani mwanafunzi alikuwa anamaliza darasa la Saba hajui kusoma wala kuandika lakini kwa sasa wanamaliza wakiwa wanajua hayo yote kwa sababu ya shirika hilo kutoa Maktaba na Vitabu vya kutosha, mwisho alitoa wito kwa Mashirika mengine kujitoa kama Room to Read
 Joackim Kawa Meneja wa mradi wa Usomaji na maktaba kutoka Shirika Room to Read akielezea miradi ambayo wanaendesha ikiwa katika shule za Msingi wanatekeleza Mradi wa Maktaba na Kusoma ambapo kuna walimu maalum  katika shule 62 za Bagamoyo wanaandaliwa kuhakikisha wanafunzi wanaweza kusoma na na kuandika vizuri,ambapo mradi huu umetekelezwa Mkoani Morogoro pia aliongeza kuwa wanampango wa kupanua wigo zaidi wa miradi yao katika maeneo mengine nchini Tanzania
 Hii ni maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo kuna vitabu vya aina mbalimbali vya masomo kuanzia Darasa la Kwanza mpaka la Saba 
Wanafunzi wakiwa wametulia wanasoma vitabu katika maktaba yao ambapo kila mmoja anaamua asome kwa namna gani  
Wanafunzi wa Darasa la kwanza wakiwa wanaendelea kusoma
Hapa kila mmoja anaelewa anacho kisoma hii ni kutokana na kuwa na walimu ambao wamewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo wamekuwa wanaweza kusoma na kuandika vizuri.
Wanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya ya Msingi Zinga wakiwa wanafurahia kupata Vitabu kutoka Shirika la Room to Read
 Wanafunzi wakiwa wanachambua vitabu kwa ajili ya kujisomea katika maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read.
 Hii ni Maktaba ya Shule ya Msingi ya Kiromo ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kiromo Bi. Flora Mlowe  alisema kuwa mradi wa Room to Read umeinufaisha sana shule yake kwanza wameweza kupata chumba cha kusomea amacho kimewasaidia sana wanafunzi tofauti na ilivyokuwa mwanzoni, aliongeza kuwa mradi huo umewafanya wanafunzi waweze kuongeza juhudi za kujisomea, wanasoma kwa burudani na pia wanapata maarifa mbalimbali kupitia vitabu hivyo, hiyo imesaidia kuondoa kundi kubwa la wanafunzi ambao hawajui kusoma alimaliza kwa kusema kuwa kuwepo kwa Maktaba hiyo kutaongeza zaidi ufauru katika shule yake.
 Furaha Tonya Social Mobilizer wa Shirika la Room to Read Tanzania akiwa katika Shule ya Sekondari Matibwa iliyopo Bagomoyo akielezea mradi wa Elimu kwa mtoto wa Kike Tanzania unaoendeshwa na Shirika la Room to Read ambapo moja ya mambo wanayo fundisha ni Life Skills ambapo lengo kubwa ni kuwataka watoto waweze kujitambua.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Matibwa Ally Kilasama alisema kwamba mradi huo umeweza kuwasaidia watoto wengi zaidi wa kike kuwepo katika shule hiyo, katika mradi wa life skills alisema kuwa kwa sasa watoto wa kike   wameweze kujitambua zaidi na watoto wa kike wanafanya vizuri zaidi kulipo wale wa kiume, pia kupitia mradi huo kutoka Room to Read wameweza kupata vifaa ya Sayansi na vitabu vya kutosha kwa wanafunzi na kwa sasa wanakarabati madarasa manne hii ikiwa ni juhudi za kutokomeza ujinga.
 Kutokana na wanafunzi wakike kuelewa Elimu ya Life Skill wameweza kuwaburuza wanafunzi wa kiume katika ufauru darasani ambapo katika Kidato cha tatu Mchepuo wa Sayansi shule ya Sekondari Kingani Mwanafunzi mmoja tu wa kiume  ndiye ameweza kuingia katika kumi Bora ambapo hapa anaelezea jinsi kulivyo na changamoto ya ushindani katika darasa hilo na kukili kuwa watoto wakike wanaweza sana 
 Rose Jeremiah Ngalya Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Mchepuo wa Sayansi aliye ongoza na kushika nafasi ya kwanza akieleza namna ya Shirika la Room to Read lilivyo wasaidia katika kuhakikisha wanapata Elimu Bora.
  
 Watoto wanafunzi wa Darasa la kwanza kutoka Shule ya msingi ya Zinga wakiwa wanaweza kusoma vitabu wakiwa na miezi sita tuu ya darasani kupitia Programu ya Room to read
 Watoto wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi ya Zinga iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wakiwa wanajifunza matamshi ambapo mpaka sasa wanaelewa vizuri na hizi ni juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika la Room to Read.


Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa 

ZANTEL WATOA MSAADA WA MBUZI 100 BAKWATA KWAAJILI YA WATOTO YATIMA JIJINI DAR LEO.

0
0

Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuberi, Sheihk Ally Ngeruko akiwashukuru Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Zantel  kwa kutoa mchango wao katika kituo cha watoto Yatima kilichopo chini ya BAKWATA amewaombea Mungu awaongezee walipotoa kwaajili ya watoto wa Kituo hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akikabidhi Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzani, Sheihk Ally Ngeruko Mbuzi 100 kwajiili ya vituo vya  kulelea watoto yatima vilivyo chini ya BAKWATA vya jijini Dar es Salaam.

 Msaada huo umekabidhiwa kwaajili ya sikukuu ya Kuchinja ya Idd el –Adha ambayo ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza mara baada ya kukabidhi Mbuzi kwa mwakilishi wa Mufti wa Tanzania ili aweze kugawa kwenye vituo vilivyo chini ya BAKWATA.
Amesema Zantel wameona sikukuu hiyo ya Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.

Mbuzi 400 watatolewa kwa wateja wa Zantel wenye matumizi zaidi kuliko wengine na ambao watakuwa wamejisajili katika kampeni kwa kupitia *149*15# na kuchagua  “Jibwage na Mbuzi”. Kujisajili katika promosheni hii ni bure kwa wateja wote wa Zantel. Kila siku wateja 40 watakaokuwa wametumia muda zaidi watajizawadia mbuzi.

“Hii si bahati nasibu, wale wateja wa juu watakaokuwa wametumia dakika nyingi bila kuchezeshwa mchezo wa bahati watakuwa wamejizawadia moja kwa moja hivyo natumia fursa hii kuwahamasisha wateja wetu kujisajili ili kupata mbuzi na kusambaza furaha ya Eid katika familia zao” amesema  Benoit
Baadhi ya Mbuzi zilizotolewa na Kampuni ya simu za Mkononi ya Zantel BAKWATA kwaajili ya Kuawa katika vituo vya kulelea watoto yatima hapa nchini.
Iikiwa ni sikukuu ya Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza mara baada ya kukabidhi Mbuzi kwa kituo cha watoto yatima cha Daarul Maarif kilichopo chini ya BAKWATA jijini Dar es Salaam leo.
Amesema Zantel wameona sikukuu hiyo ya Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.




Baadhi ya walezi wa Kituo hicho na wafanyakazi Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Zantel wakiwa katika shule ya Kiislamu ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.



Baadhi ya Picha za Makabidhiano.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAWAMFANO WA KUIGWA KWA KUENDESHA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI.

0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Msaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada walipotoka kwenye mkutano wa 18 wa Tume za Uchaguzi katika nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara (SADC), uliofanyika Mjini Gaborone-Botswana. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Clerence Nanyaro.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ni moja ya Tume kati ya tume za Afrika ambayo imekuwa mfano wa kuifwa katika uchaguzi kutokana kila unapofanyika uchaguzi umekuwa wa huru na haki.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuonekana kwa tume hiyo ni katika mkutano wa 18 wa Tume za Uchaguzi katika nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara (SADC), uliofanyika Mjini Gaborone-Botswana,  amesema katika mkutano huo Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika usimamizi wa uchaguzi na kufanya nchi zingine zifanye mfumo huo.

Lubuva amesema kuwa Tume za Uchaguzi katika nchi za SADC zimekuwa zikifanya kwa kutumia vitambulisho vya taifa tofauti na Tanzania kutumia kitambulisho cha mpiga kura lakini uandikishaji wa muda mfupi.

Amesema kuwa Tanzania ziliwakilishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kwa pamoja zimeonekana kuendesha uchaguzi wa haki na amani.

Aidha amesema kuwa katika mkutano huo nchi za Afrika  zimeonekana kila uchaguzi ukiisha walioshindwa huwa hawakubali matokeo katika chaguzi mbalimbali.

Lubuva amesema kuwa vitambulisho vya taifa vikikamilika kwa kila mtanzania kuwa na kitambulisho kuangalia namna ya kutumia katika chaguzi zijazo.

Hata hivyo amesema mkutano huo Tanzania kupitia NEC zimeweza kujifunza baadhi ya vitu katika uendeshaji wa uchaguzi na wataendelea kufanyia kazi katika kuboresha chaguzi zijazo.

WADAU WAIKUBALI HAPA KASI TU YA VODACOM.

0
0

· Yawezesha kupakua nyimbo na picha mitandaoni fasta fasta
Kutokana na kuimarishwa zaidi kwa miundo mbinu inayotumiwa na Vodacom Tanzania kwenye huduma za intanenti kumewezesha wateja wake kufurahia huduma hii zaidi kwa matumizi mbalimbali nchini kote.

Moja ya  kundi ambalo linaendelea kufurahia matumizi  ya internet yenye kasi kubwa ni wapenzi wa muziki ambao hivi sasa wanaweza kupakua nyimbo  mitandaoni kwa kasi kubwa ikiwemo kuangalia picha za sinema kwa viwango vyenye ubora mkubwa.

Wakiongea wakati wa thathmini ya kasi na ubora wa mtandao wa Vodacom,Baadhi ya wateja walieleza kuwa hivi sasa wanaweza kupata huduma za internet kwa urahisi mahali popote na kwa wakati wowote. 

Mmoja wa wateja  Innocent Mafuru alisema kuwa akiwa mtumiaji wa mteja wa Vodacom anaweza kutumia interneti bila kupata usumbufu wowote kwa matumzi yake binafsi na matumizi yake ya  ofisini.

“Intanenti yenye kasi ya Vodacom inaniwezesha kuperuzi mitandao mbalimbali na kupakua nyaraka mbalimbali mitandaoni ikiwemo kupata  burudani za muziki na picha za sinema kutoka kwenye mitandao”.Alisema Mafuru.
Mteja mwingine Sunday John alisema kuwa interneti ya Vodacom ina kasi ya kuridhisha kwa matumizi mbalimbali ya  ofisini,kupata nyaraka kutoka mitandaoni , kutuma na kupokea nyaraka kwa kasi bila kusahau kupakua muziki na picha za sinema .

“Nimekuwa mtumiaji mzuri wa mtandao wa Vodacom na mar azote nimekuwa nikifurahia huduma zake za interneti”.Alisema.

Mtandao wa  interneti umeendea kwa asilimia 90% hivyo unawezesha idadi kubwa ya Tanzania kuufurahia kwa kupata burudani za muziki na picha kutoka mitandaoni kwa ubora na viwango vya kimataifa.
 .Mteja wa Vodacom Tanzania, Suka Keba (kushoto) akitoa maoni yake kuhusiana na kasi ya intanenti ya mtandao wa kampuni hiyo unavyofanya kazi kwa kasi ya hali ya juu ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
 Mkazi wa Dar es Salaam, Innocent Mafuru (kushoto)  akihojiwa jana jijini na waandishi wa habari kutoka Clouds FM, Herry Mijinga kuhusiana na kasi ya intanenti ya mtandao wa kampuni hiyo unavyofanya kazi kwa kasi ya hali ya juu ukilinganisha na kipindi cha nyuma hususani tangu mtandao huo uzindue huduma ya 4G.

MFUMUKO WA BEI UMEPUNGUA HADI ASILIAMIA 4.9.

0
0

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo  kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Kaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Ruth Minja.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mwenendo wa Bei za Bidhaa mbalimbali hapa nchini.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa Mwezi Agasti 2016  umepungua hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 ya ilivyokuwa mwezi Julai.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma na huduma kwa mwaka ulioshia mwezi Agasti 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi julai 2016.

Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.28  mwezi Agasti 2015 na mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Agasti 2015 umepungua hadi asilimia 7.0 kutoka asilimia 7.6  ilivyokuwa mwezi Julai mwezi 2016.

Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Agasti 2016 umechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Agasti 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Agasti mwezi 2015.

Mwenendo wa wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula ivinaonesha kupungua ni pamoja na bei ya samaki kwa asilimia 7.01 mafuta ya kupikia 7.02. na mbogamboga asilimia 6.9 

Amesema kuwa uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania kununua bidhaa na huduma umefikia sh. 96 na senti 92  ilivyokuwa mwezi julai 2016.

Mfumuko wa bei kwa nchi zingine za Afrika Mashariki, Kenya umepungua hadi asilimia 6.26  kutoka asilimia 6.39 mwezi Julai 2016, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 4.3 kutoka asilimia 5.1 mwezi Julai,2016 

TANGA UWASA YAPATA TUZO YA UBORA KWA MAMLAKA HAPA NCHINI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akipokea tuzo ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ya ubora wa kimataifa,kupitia hati ya ISO 9001:2015 ulitokana na ushindi wa kuwa mamlaka bora ya hduuma za Maji Safi na Usafi wa Mazingira nchini kwa Mwaka 2014/2015 wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte kulia akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella walioipata mamlaka hiyo ushindi wa kuwa mamlaka bora ya huduma za maji na usafi wa mazingira nchini mwaka 2014/2015

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka  hiyo,Salum Shamte kulia akimkabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akiwa na kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi ambapo kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mpya wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Salum Shamte,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Joshua Mgeyekwa wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi .

Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji
Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji
ikiwemo wafanyakazi wa Mamlaka hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga ( Tanga Uwasa) na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

MKUU wa Kitengo cha Uzalishaji Maji katika kituo cha Kusafishia Maji
Mabayani Jijini Tanga,Faraji Nyoni akimueleza mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella namna uzalishaji wa maji uzalishaji unavyofanyika
na usafishaji wake kabla ya kuwafikia wananchi.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeweza kuwa mamlaka ya kwanza nchini kufikia vigezo vya kupewa leseni ya EWURA ya Daraja la kwanza
(Class 1Lesence).

Leseni hiyo ilitolewa Juni 17 mwaka huu na Waziri wa Maji na Umwagiliaji katika mkutano wa kuzindua ripoti ya mwaka 2014/2015 ya mamlaka za maji uliofanyika Mjini
Dodoma.

Akizungumza mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ,Felix Ngamlagosi alisema kuwa leseni hiyo ilitolewa kwa Tanga Uwasa na kwa sasa ndio mamlaka ya maji pekeennchini iliyo na leseni ya EWURA ya daraja la kwanza nchini.

Alisema kuwa leseni hiyo ya daraja la kwanza imetolewa baada ya EWURA kupitia utendaji kazi wa Tanga Uwasa na kutadhimini viwango vilivyowekwa ili mamlaka ya maji kuweza kupata
daraja la kwanza na kujiridhisha kuwa vimefikiwa.

Aidha alisema vigezo ambavyo vimeangaliwa kuwa mamkala bora ni kugharamia uendeshaji wa mamlaka,kugharamia uchakavu wa miundombinu na kuweza kulipia riba za mikopo ya uwekezaji.

“Lakini pia uwezo wa Mamlaka hiyo kujitegemea kiufundi na
kiuendeshaji”Mkurugenzi huyo alisema kuwa mamlaka hiyo imeweza kuwa ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo miongoni mwa mamlaka kubwa 25 za maji zinazotoa huduma katika makao makuu ya
mikoa Tanzania bara.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema wao kama mamlaka wataendelea kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazoendena na viwango vikubwa ili kuendelea kuwa mamlaka bora nchini.

Alisema pamoja na changamoto walizokuwa nazo lakini wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wanakabiliana nazo kwa kuwawezesha wananchi waweze kunufaika ana huduma
ya Maji kwa kiwango kikubwa .

“Lakini pia sisi kama mamlaka tumejiwekea mipango kabambe ya kuhakikisha huduma za maji zinaimarika sambamba na kujiandaa na fursa ya ujio wa bomba la mafuta utakaoanzia nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ili changamoto ya maji isiwepo wakati wa ujio wa fursa hiyo.

habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Serikali yawatoa wasiwasi Watanzania kuhusu hali ya chakula nchini

0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma

Serikali imewatoa wasiwasi Watanzania kuhusu hali ya chakula nchini na kueleza kuwa kuna ziada ya chakula zaidi ya asilimia 123 ikilichozalishwa msimu uliopita.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Tate Ole Nasha alipokuwa akizindua tovuti ya Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo mjini Dodoma.

Naibu Waziri Ole Nasha amesema kuwa hali ya chakula nchini inaridhisha ambapo tafsiri ya hali ya chakula inatokana na ukweli kuwa uzalishaji wa chakula kwa asilimia 100 inaonesha kuna chakula, asilimia 101 hadi 120 kuna utoshelevu wa chakula na asilimia zaidi ya 120 hali hiyo inatafsiriwa kuwa kuna chakula cha kutosha kwa miaka mitatu hadi minne.

“Nawasihi Watanzania kutunza chakula kilichopo ili kitumike sasa na baadae, hali ya uwepo wa chakula ndani ya nchi itaonesha kuwa kuna usalama kwa wananchi na wanaweza kuendelea na shughuli zao za kila siku” alisema Naibu Waziri huyo.

Aidha, Naibu Waziri Ole Nasha amewatahadharisha Watanzania kutunza chakula kutokana na nchi jirani kutokuwa na hali nzuri ya upatikanaji wa chakula ambapo katika nchi 15 za SADC, kati ya hizo nchi 13 hazina chakula za kutosha.

Kuhusu tovuti aliyoizundua, Naibu Waziri Ole Nasha amesema kuwa tovuti hiyo itatoa taarifa zinazokwenda na wakati badala ya kutumika kama maktaba ya kutunzia kumbukumbu za Serikali na iwe na uwezo wa kuwashirikisha wasomaji ili kupata mrejesho kutoka kwa wasomaji ambao utasaidia kufanya maboresho katika utendaji na kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake Msemaji wa Serikali Hassan Abbas amesema kuwa kwa sasa mawasiliano ya haraka duniani yamehamia kwenye mitandao ya kijamii, kwa muktadha huo, Serikali imeanza kuwasiliana na wananchi kwa haraka kwa kutoa taarifa mbalimbali kwa wakati kwa njia ya mitandao ya kijamii badala ya kusubiri vyanzo vingine vya habari.

Akitolea mfano Msemaji huyo amesema kuwa dunia ina takribani watu wapatao trilioni saba ambapo zaidi ya watu trilioni tatu wanatumia mitandao ya kijamii na asilimia 91 ya makampuni yote duniani wanatumia mitandao ya kijamii zaidi ya miwili hadi mitatu.

Awali akimkaribisha Nibu Waziri, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA amesema kuwa kuanzishwa kwa tovuti hiyo itawasaidia wananchi kupata huduma mahali walipo bila kutembelea ofisi husika au kuonana na mtoa huduma.

Tovuti iliyozinduliwa leo ni www.nfra.go.tz, yenye lengo la kurahisisha utoaji taarifa za taasisi hiyo kwa wananchi.

Serikali yajizatiti kuondoa tabaka la wasiojua kusoma nchini

0
0

Na: Lilian Lundo - MAELEZO

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejizatiti kuondoa tabaka la wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa vijana na watu wazima kwa kujenga uwiano sawa wa utoaji wa elimu kwa watu wote.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Duniani, yaliyofanyika leo, katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.

“Wizara imejipanga vizuri, na lengo kubwa la wizara ni kuhakikisha tunakuwa na mtanzania aliye elimika na aliye na stadi, maarifa na uwezo wa kutumia elimu aliyoipata,” alifafanua Bureta.

Vile vile Bw. Bureta amesema kwa sasa wizara ipo kwenye mpango wa kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) ambao unaanzia chini kwa wanafunzi wa awali mpaka shule za msingi.

Katika mpango huo walimu wamekuwa wakipata mafunzo mbalimbali ya namna ya kumuwezesha mwanafunzi kujua Kusoma Kuandika na Kuhesabu katika ngazi ya elimu ya awali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Basilina Levira amesema kwamba kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, asilimia 78 ya vijana na watu wazima ndio waliokuwa wakijua kusoma na kuandika.

Akaongeza kuwa mwaka 2015 idadi hiyo ya wanaojua kusoma na kuandika ilishuka na kufikia asilimia 77 ambapo ilipelekea wizara hiyo kutoka na mikakati inayokusudia kuondoa kabisa tabaka la watu wasiojua kusoma na kuandika nchini.

Aidha, Basilina amesema kuwa Serikali ilipitisha sheria ya vyumba vya madarasa ya shule zote nchini kutumika kufundishia vijana na watu wazima ambao hawajui kusoma na kuandika muda wa jioni baada ya wanafunzi wa kawaida wanapomaliza masomo yao.

Amefafanua kwa kusema kuwa, wizara imeandaa programu ambayo iko kwenye mfumo wa Televisheni na picha za video (DVD) yenye masomo 65 ya kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu, ambapo kwa kutumia program hiyo mwanafunzi anaweza kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa muda wa miezi 4 mpaka 6.

Mafunzo hayo kwa njia ya Televisheni na Picha za Video tayari yameanza kutumika kwa wilaya za Ilemela, Dodoma Manispaa, Songea Manispaa, Bagamoyo, Mkuranga, Temeke, Ilala na Kinondoni, ambapo asilimia 65 ya vijana na watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wamejitokeza kujiunga na Elimu hiyo huku idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake.

Siku ya Kisomo Duniani huadhimishwa Duniani kote kila ifikapo Septemba 08 ya kila ya mwaka, ambapo mwaka huu 2016 maadhimisho hayo yametimiza miaka 50 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1966.

NHC YAMCHOMOA MPANGAJI WAKE MWINGINE KWA KUDAIWA MILIONI 96

0
0

nh4
Vitu mbalimbali vikitolewa ndani vikiwemo viti.
nh5
Baadhi ya vifaa mbalimbali vya kampuni hiyo vikiwa tayari vimetolewa nje.
nh7
Mmoja wa wanafamilia ambaye hakutaka jina lake litajwe akishuhudia tukio hilo wakati wafanyakazi hao wakiendelea kutoa vitu mbalimbali katika nyumba hiyo.
nh2
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimbembe Auction Mart wakitoa Samani za kampuni ya Centre Point Limited Mpangaji wa Shirika la Numba NHC Katika nyumba Plot Namba 2008/93 iliyopo Mtaa wa Indira Ghandhi jijini Dar es salaam kwa kushindwa kulipa kodi ya pango kiasi cha shilingi Milioni 96, tukio hilo limefanyika leo asubuhi.
nh3
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimbembe Auction Mart wakitoa Samani za kampuni ya Centre Point Limited Mpangaji wa Shirika la Numba NHC Katika nyumba Plot Namba 2008/93 iliyopo Mtaa wa Indira Ghandhi jijini Dar es salaam

Ukubwa wa Deni la Taifa siyo mzigo: Profesa Semboja

0
0
Na: Frank Shija, MAELEZO

 Ukubwa wa deni la taifa siyo jambo linaloweza kusababisha kuyumba kwa uchumi wa nchi, kinachooneka ni kuendela kuaminiwa kwa Tanzania ndani na nje ya nchi jambo linalopelekea tuna pata fursa ya kukopesheka kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Profesa Haji Semboja alipofanya mahojiano maalum na mwandishi kutoka Idara ya Habari, MAELEZO kuhusu hali ya uchumi ilivyo kutokana na ongezeko la deni la Taifa leo Jijini Dar es Salaam.

“Ukubwa wa deni la taifa siyo mzigo mbaya, ni mzigo wa kimaendeleo. Unnecessary devil” Alisema Profesa Semboja.

Aliongeza kuwa kutokana kwa imani waliyo nayo wahisani ndani na nje ya nchi ndiyo maana washirika wetu wanatukopesha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama ambavyo tumeshuhudia ujenzi wa Daraja la Kigamboni, hivi karibuni tutanufaika na usafiri wa ndege”. Alisema Profesa Semboja.

Aidha amempongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli kwa hatua alizochukua za kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuondoa safari za nje zisizo za rasmi pamoja na kupiga vita vitendo vya rushwa.

Semboja aliendelea kusema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni Serikali ya awamu ya Tano kulipa madeni ya watangulizi wake huku ikitekeleza miradi ya maendeleo jambo linaloongeza imani miongoni mwa wahisani.

Hata hivyo alionya juu ya matumizi mabaya ya rasilimali fedha kuwa zinasababisha kushindwa kutekeleza wajibu wa kulipa deni kwa wakati na kupelekea kulimbikiza madeni jambo ambalo si sahihi.

Alitajaa baadhi ya matumizi mabaya ya fedha kuwa ni pamoja na safari za nje na ndani ya nchi zisizokuwa na tija, ulevi, kupelekea fedha katika miradi isiyopangwa na mengine.

Wananchi wametakiwa kutoyumbishwa na waelewi kuwa kupitia fedha zinazokopwa wanufaika wakuu ni wananchi wenyewe, mfano fedha zitakazo tumika kujenga Nyumba za Magomeni ambazo Mhe. Rais amehaidi waliokuwa wakazi wake kuishi bila kulipia kwa kipindi cha miaka mitano zikitokana na mikopo hiyo wananufaika.

Serikali kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium LukuviNa 
 
 
 
Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

Serikali imesema imejipanga kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi inayotokana na wathamini kutozingatia maadili ya uthamini pamoja na kazi za uthamini kufanywa na watu wasiokuwa na sifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi leo mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini mwaka 2016 katika mkutano wa nne wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Lukuvi amesema kuwa lengo kuu la Muswada huo ni kutunga Sheria itakayoweza kusimamia taaluma na shughuli za uthamini Tanzania Bara kwa kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii na sekta ya ardhi kwa ujumla.

Aidha, Waziri huyo amesema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa itasaidia katika kuwaondolea mateso wananchi wanaothaminiwa mali zao na kuchelewa kulipwa fidia kwa kuweka ukomo wa muda ambao fidia hiyo lazima ilipwe na kuwadhibiti wawekezaji kulipa fidia kwa wakati.

Pia ameongeza kuwa sharia hiyo itasaidia kuondoa utapeli uliokuwa unafanywa na wathamini kuongeza thamani kinyume na utaratibu na kuongeza wafidiwa hewa sambamba na kuthibiti uthamini wa kifisadi ambao umekuwa ukifanywa na wathamini kwa kushusha thamani ya mali kwa madhumuni ya kukwepa kulipa kodi.

Zaidi ya hayo, katika usajili wa wathamini chini ya sheria hiyo inayopendekezwa, kutakuwa na mfumo wa kuwawajibisha wathamini ambao watakaokiuka maadili ya kitaaluma, kutoa adhabu kwa wathamini wanaokiuka sharia hiyo ikiwa ni pamoja na kifungo, faini kali na kusimamishwa au kufutiwa usajili.

Kwa upande wake Waziri Kivuli kambi ya upinzani katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wilfred Lwakatare amesema kuwa sheria hiyo ikitekelezwa itasaidia kupunguza changamoto katika sekta ya ardhi na nyumba zilizokuwa zinatokana na matatizo ya uthamini.

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo yakutana na Wajumbe kutoka WADIGLA Misri

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(katikati) akionyesha mchoro wa mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Uhuru kwa Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy leo Jijini Dar es Salaam,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa WADIDEGLA upande wa Afrika Bw.Rami Nashed.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo ya mchoro wa mradi wa kituo cha utamaduni kwa Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu (kulia)akieleza jambo kwa Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy (kushoto), baada ya kikao kilichojadili masuala mbalimbali ya namna ya kuwezesha ushirikiano wa kuendeleza sekta zilizo chini ya wizara leo Jijini Dar es Salaam. 

Wajumbe wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na wajumbe kutoka WADIGLA Misri wakifuatilia kwa makini fursa video iliyokuwa ikionyesha fursa mbalimbali zinazotolewa na WADIDEGLA Misri ikiwemo fursa katika sekta ya Michezo yenye lengo la kukuza na kuendeleza michezo mbalimbali.




Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akifafanua jambo wakati wa kikao na wajumbe kutoka WADIGLA Misri(hawapo katika picha), katika kujadiliana masuala mbalimbali na namna ya kuwezesha ushirikiano wa kuendeleza sekta zilizo chini ya wizara.
Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy akieleza jambo wakati wa kikao na wajumbe kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kilichokuwa kikijadili masuala mbalimbali ya namna ya kuwezesha ushirikiano wa kuendeleza sekta ya Michezo, leo Jijini Dar es Salaam,kulia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano kutoka Kampuni ya Montange Bibi. Teddy Mapunda
Wajumbe wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na wajumbe kutoka WADIGLA Misri wakifuatilia kwa makini fursa video iliyokuwa ikionyesha fursa mbalimbali zinazotolewa na WADIDEGLA Misri ikiwemo fursa katika sekta ya Michezo yenye lengo la kukuza na kuendeleza michezo mbalimbali.
Wajumbe wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na wajumbe kutoka WADIGLA Misri wakifuatilia kwa makini fursa video iliyokuwa ikionyesha fursa mbalimbali zinazotolewa na WADIDEGLA Misri ikiwemo fursa katika sekta ya Michezo yenye lengo la kukuza na kuendeleza michezo mbalimbali.
Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.(08/09/2016).

Serikali ya Tanzania na China zaanza mazungumzo ya mashirikiano kuwawezesha wafanyabiashara wadogo,

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma


Serikali imeanza mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya China kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati Afrika ikiwemo Tanzania.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba alipokuwa akijibu swali la Mhe. Munde Tambwe lililohusu mkakati wa Serikali kupitia diplomasia ya uchumi na nchi ya China kuunganisha wajasiriamali wadogo.

Dkt. Kolimba amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 4 barani afrika ambazo Serikali ya China imechagua kuwekeza viwanda vyake katika miaka mitatu ijayo.

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa, Serikali ya china imeanzisha mfuko maalumu wa fedha kwa ajili ya kuwezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati wa afrika ambapo Serikali ya Tanzania imeshafanya mazungumzo na Benk ya maendeleo ya China.

“Serikali imeanza mazungumzo na benki ya maendeleo ya china kwa ajili ya kuwezesha mabenki nchini yaweze kukopa fedha hizo na hatimaye kuweza kuwakopesha wajasiriamali wetu wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya viwanda kwa kushirikiana na wenzao wa china,” alifafanua Dkt. Kolimba.

Aidha, amesema kuwa matarajio ya Serikali ni kuona mabenki nchini yanakidhi vigezo na masharti ya kuchukua fedha kutoka Mfuko wa China ili watanzania waanze kupata mitaji mapema iwezekanavyo.

Mbali na hayo Balozi wa Tanzania nchini China umekuwa ukishawishi wafanyabiashara kutoka china kuwekeza nchini nan a kuandaa ziara za makampuni mbalimbali ya China kutembelea kituo cha uwekezaji (TIC) nchini.

Jamii yatakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita ndoa katika umri mdogo

0
0

Mwashungi Tahir Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar 8-9-2016

Jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita ndoa katika umri mdogo kutokana na athari ambazo zinazoweza kujitokeza na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.

Hayo yameelezwa na Mwanasheria wa Zafela Salma Suleiman huko katika jengo la malaria Mwanakwerekwe kwenye semina ya kupinga ndoa za utotoni na udhalilishaji wa wanawake na watoto iliyowashirikisha wazazi, walimu wa vya madrasa pamoja na masheha.

Amesema jamii ipewe elimu zaidi ili ndoa hizo zisiweze kuendelea ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya watoto pamoja na kuzidisha umaskini katika jamii.

Aidha watoto chini ya umri wa miaka 18 viungo vyao vinakuwa bado havijakomaa kwa kuweza kujifungua kwa njia salama hivyo kunauwezekano mkubwa wa kupata matatizo wakati wa kujifungua .

Alieleza jamii ielewe faida na hasara za ndoa hizo kwani kupelekea ongezeko la watoto wa mitaani , pamoja na maradhi ya zinaa ambayo hupelekea kupata maradhi ya maambukizi .

Pia alielezea kuwa serikali imetunga sheria ya elimu, na sheria za makosa ya jinai ya mwaka 1984 ambayo imetoa adhabu kwa mtu yeyote ambae atamfanyia mtoto suala la udhalilishaji chini ya umri huo.

“Sheria ya elimu inamfanya mtoto atakapo pata uja uzito baada ya kujifungua ndani ya miaka miwili kwa wakati wowote anaruhusika kurudi kuendelea na masomo yake , “Alisema Salma .

Vile vile kwa mzazi au mlezi ambae atachukua hatua ya kumuozesha mtoto mwenye umri mdogo ataingia hatiani kwa mujibu wa sheria ya kosa la jinai na kutozwa faini kwa mujibu wa makosa ,kisheria.

Sambamba na hayo mwanasheria huyo alisema kesi za udhalilishaji zinaongezeka siku hadi siku kutokana na uzorotaji wa kutolewa hukumu kwa kesi hizo na kuongezeka kwa malimbikizo ya kesi hizo.

Akitoa msisitizo kwa wazazi na walezi kuepuka adhabu za kuwanyima vyakula , kumpiga kupita kiasi kunaweza kukampelekea uzururaji wa mitaani na kupata udhalilishaji wa kubakwa

Nae sheha wa shehia ya Mpendae Haji Seti ameitaka jamii isivunjike moyo wakati inapotokea kesi ya ushalilishaji kwenda mahakamani kwa kila siku hadi itapotolewa hukumu ya kesi hiyo

“Wazazi pamoja na mashahidi huvunjika moyo kwa muda mwingi unaotumika kwa kutolewa hukumu kwani daktari tayari amekwisha thibitisha ushahidi wake lakini tatizo ni kwa waendeshaji mashtaka wanataka ushahidi usio na shaka jambo ambalo halitowezekana.”walisema baadhi ya wazee hao .

Amewataka wazazi wawe mstari wa mbele kwa kufatilia kesi hizo pindipo zinapotokea hadi pale mahakama inapofikia hatua ya kutoa maamuzi yaliyo sahihi.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MBUNGE WA BUYUNGU

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago kwenye vianja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAFFO:NI KINYUME CHA SHERIA KWA MGAMBO KUWANYANYASA WAFANYABIASHARA WADOGO.

0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, Dodoma

Serikali imesema ni kinyume cha sheria kwa askari mgambo kuwanyanyasa Mama Lishe na wafanyabiashara wengine wadogo nchini.

Akijibu swali la Mhe. Zaynab Vulu (Viti Maalumu) alilotaka kujua kwanini Serikali isiandae mazingira mazuri ya kufanyia kazi wafanyabiashara hao, Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jaffo amemesema kuwa askari mgambo wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu bila kuwanyanyasa wala kuwadhulumu wakati wakiwaondoa katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Naibu Waziri Jaffo aongeza kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wafanyabiashara hao walioko katika sekta isiyo rasmi katika kukuza kipato na ajira.Aidha, Naibu Waziri Jaffo amesema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa askari mgambo yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya kuwanyanyasa wafanyabiashara na Mama Lishe wanapotekeleza majukumu yao.

Mbali na hayo, Naibu Waziri amezikumbusha Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwemo Mama Lishe karibu na maeneo walipo wateja wao.

Zaidi ya hayo Naibu Waziri huyo amewataka wafanyabiashara wadogo nchini kufanya biashara katika maeneo yaliyotengwa rasmi na Halmashauri na kuacha kufanya biashara hizo katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Wakuu wa Wilaya za Arusha kusimamia Mradi wa Mabadiliko ya Hali ya hewa Na Tabia ya Nchi

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo(Kushoto) akibadilishana business card Mwakilishi Mshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais Morindat.
Mwakilishi Mshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais Morindat (aliyesimama)akiwasilisha mada ya kutambulisha mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya Nchi kwa Sekretariet ya Mkoa wa Arusha
Viongozi wa Mkoa wakifuatilia mawasilisho ya mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya Nchi ambao unatekelezwa kwa awamu ya pili katika Wilaya za Longido, Monduli na Ngorongoro
Mratibu wa Mradi kutoka Tamisemi Sanford Kway akielezea wajibu wa Wizara katika kusimamia Mradi huu wa Mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi katika halmashauri 15 Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitoa maelekezo katika kikao cha kutambulisha Mradi wa Mabadiliko ya hali ya hewa na Tabia ya Nchi.


Teghenjwa Hoseah, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe Mrisho Gambo amewaagiza Wakuu wa Wilaya tatu za Mkoa wa Arusha zinazotekeleza mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi kuwa Wenyeviti wa kamati za mradi huo ili kuharakisha utekelezaji wake katika maeneo hayo.

Akizungumza katika kikao cha kutambulisha mradi huo wa awamu ya Pili utakaofanya kazi katika wilaya za Ngorongoro, Monduli na Longido za Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 alisema kuna haja ya kuimarisha usimamizi wa mradi huu ili kuwajengea uwezo wanajamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi ili mradi huu uweze kuleta Tija iliyokusudiwa.

Alisema awali kamati hizo zilikuwa zikisimamiwa na Maafisa Mipango katika halmashauri hizo ila kutokana na majukumu yao ameonyesha wasiwasi iwapo wanaweza kuusimamia ipasavyo hivyo aliwataka Wakuu wa wilaya kuwa vinara wa kuusimamia na kuratibu kwa karibu ili kuleta mapinduzi katika maeneo ya wafugaji na kuhakikisha wanatengeneza mfumo imara na utekelezaji wa mradi huo unafanikiwa kuanzia ngazi ya kijiji.

“Nahitaji kuona halmashauri ambazo zinatekeleza mradi huu ifikapo mwezi Novemba ziwe zimeshaanza kutekeleza majukumu yake bila vikwazo vyovyote na nipate taarifa zake mara kwa mara ili fedha zilizotolewa na wafadhili zilete matokeo chanya,”alisema Gambo

Akizungumza wakati wa Kikao hicho Mwakilishi Mshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais Morindat alisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa imekua ni tishio kubwa kwa wananchi haswa wa maeneo haya ya wafugaji na ndio maana tulianza na Halmashauri hizi kutokana na athari zilizojitokeza katika jamii za wafugaji ambapo mifugo mingi katika maeneo yao ilipoteza uhai.

Aliongeza kuwa mradi huu unatofauti na miradi mingine tuliyoizoea kwa sababu Jamii inakuwa na nafasi ya kuamua jinsi Fedha za Mradi zitakavyotumika huku malengo ya mradi yakiwa ni kuijengea uwezo Ofisi ya Raisi –TAMISEMI katika maeneo makubwa mawili ambayo ni uimarishaji wa taasisi katika uratibu wa mradi na uwezo wa kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kuziwezesha mamlaka za serikali za mitaa hapa nchini ziweze kutoa elimu kwa jamii kutambua na kutekeleza Miradi ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan Shirika la Kimataifa la Mazingira na Maendeleo (IIED), Haki Kazi Catalyst (HKC), Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza (UK-aid) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) itatekeleza mradi huu katika Halmashauri 15 huku zaidi ya Bilioni 6 zinatarajia kutumika katika mradi huu.

WAZIRI UMMY MWALIMU ALIAGIZA BARAZA LA FAMISIA KUFANYA OPERESHENI YA KUHAKIKI VYETI VYA WATAALAM WA DAWA (WAFAMASIA) NCHI NZIMA

0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Baraza la Famasia nchini.

Na.Mwandishi Wetu - Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Famasia nchini kuanza kazi ya kuhakiki vyeti vya wauza dawa (wafamasia) katika maeneo mbalimbali nchini ili kudhibiti na kuwaondoa wauza dawa wasio na sifa ya kufanya kazi hiyo kwenye maduka ya dawa.

Pia ameligiza Baraza hilo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kuwafutia usajili wafamasia wanaokiuka kanuni na taratibu za Baraza hilo ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya upotevu wa dawa na uuzaji wa dawa na vifaa Tiba vya Serikali.

Mhe.Ummy alitoa maagizo hayo mjini Dodoma katika Kikao Chake cha kwanza na Bodi ya Baraza la Wafamasia nchini ambapo pamoja na mambo mengine alikemea utaratibu ulojitokeza wa kutaka kuifanya biashara ya dawa kuwa sawa na biashara nyingine za kawaida za maduka ya kuuza nguo jambo ambalo halikubaliki.

"Biashara ya maduka ya dawa lazima iheshimiwe, lazima ianzishwe kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na watu wanaoajiliwa kuhudumia maduka ya dawa kuwa na sifa zinazotakiwa, kazi ya kuuza dawa za binadamu sio sawa na biashara ya kuuza nguo au viatu", alisema Mhe Ummy.

Ameliagiza Baraza hilo kufanya operesheni nchi nzima kukagua maduka yote ya dawa kubaini mapungufu yaliyopo kisha kuchukua hatua kali dhidi ya wale wataogundulika kufanya biashara hiyo bila kufuata taratibu na kuongeza kuwa baraza hilo ni lazima liendelee kupambana na watoa dawa wasio na sifa na wale wasio waaminifu wanaotengeneza vyeti bandia vya Wataalam wa Famasi.

Pia ametoa maelekezo kwa baraza hilo kuangalia suala la mgongano wa maslahi hasa pale ambapo Mfamasia wa Wilaya anatuhumiwa kumiliki maduka ya Dawa mawili hadi matatu ndani ya Halmashauri anayofanyia kazi.

"Ni lazima suala hili tulitafutue suluhish nimefanya ziara mikoani jambo hili nimelikuta, mimi sielewi na Wananchi wengi hawaelewi pale Mfamasia wa Wilaya anapokua na maduka ya dawa hadi matatu na muda wote yana dawa wakati dawa hizo hizo hazipatikani katika vituo na Hospitali za Serikal, Kwa nini wananchi wasiwe na hisia kuwa dawa zile ni za Serikali? Baraza nileteeni mapendekezo ya kutatua hili. Alisisitiza Mhe Ummy.

Aidha, ameliagiza Baraza hilo kuweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili nchi iwe na wanataaluma wenye uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu.

Akitoa taarifa ya Utendaji Msajili wa Baraza la Famasia Bi.Elizabeth Shekalaghe alieleza kuwa zipo changamoto wànazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo maduka mengi ya kuuza dawa kuendesha biashara hiyo bila ya kuwa na vibali vya biashaa pia kuwepo kwa wauza dawa wasio na sifa ya kufanya shuguli hiyo.

Pia alieleza mikakati iliyowekwa na barza hilo ili kuhakisha changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi ili kuhakikisha huduma za uuzaji dawa zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu ili kuhakikisha unora wa huduma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Bàraza là Famasia, Legu Ramadhani Mhangwa, amesema kuwa Baraza hilo limekuwa likifanya kazi zake kwa kuzingatia sheria ili kufikia malengo liliyojiwekea na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa na Mhe Waziri pia kutatua changamoto ya uwepo wa vyuo binafsi vinavyofundisha taaluma ya famasi kutokidhi viwango pamoja na nia ya serikali ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kada za dawa nchini.


Pia Baraza hilo limeahidi kushughulikia uhaba wa wakufunzi mahususi katika vyuo vinavyofundisha kada za famasi katika ngazi ya cheti na diploma.

Kuhusu mgongano wa maslahi kwa watumishi wakiwemo watendaji wa Halmashauri na wale wanaosimamia na kutekeleza kazi za baraza katika ngazi za mikoa na halmashauri, Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Baraza litahakikisha linasimamia kikamilifu Kanuni za Maadili na Miiko ya Kitaalamu za 2015 ili kutatua changamoto hizo iliwemo upotevu wa dawa za Serikali.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images