Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAPOKEA MSAADA WA FEDHA KUTOKA SERIKALI YA UJERUMANI.

0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava akikaribisha ujumbe toka Serikali ya Ujerumani uliofika Ofisi kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kusaini mkataba wa makubaliano ya  kuisaidia Ofisi ya Makamu wa Rais kiasi cha fedha yuro laki nne kwa ajili ya shughuli za mabadiliko ya tabia Nchi.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava akiongea jambo na Mwakilishi wa Balozi wa Ujerumani Bi. Lena Thiede kabla ya kuanza shighuli ya kusaini mkataba huo.
 Sehemu ya Watumishi ya Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Richard Muyungi(wa kwanza kulia) wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava (hayupo pichani) wakati anatoa neno la shukurani kwa Serikali ya Ujerumani  kabala ya kusiani mktaba huo.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava pamoja na Mkuu wa program ya Maji toka Ubalozi wa Ujerumani Bw. Ernst Doring wakisaini hati za makubaliano ya Serikali ya Ujerumani kuisaidia Ofisi ya Makamu wa Rais kiasi cha fedha yuro laki nne  kwa jaili ya kuendesha program  za mabadiliko ya tabia Nchi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava na Mkuu wa program ya Maji toka Ubalozi wa Ujerumani Bw. Ernst Doring  wakibadilishana hati za makubaliano mara baada ya kusaini  mkataba huo.

RC MTWARA AZUNGUMZIA AJALI YA MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MAAMA SAMIA SULUHU HASSAN

0
0

DC Kati atoa wiki daktari kuhamia Unguja Ukuu

0
0
Na Salum Vuai, MAELEZO

MKUU wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa Said, ametoa muda wa wiki moja kwa daktari wa kituo cha afya Unguja Ukuu kuhamia katika nyumba anayopaswa kuishi kijijini humo kuanzia jana Septemba 9, 2016.

Amesema kama kuna matatizo yoyote yanayosababisha daktari huyo ashindwe kuhamia kwenye nyumba hiyo, afike ofisini kwa kiongozi huyo kabla ya Septemba 15, mwaka huu kumueleza ili hatua za kurekebisha zichukuliwe.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya alisema nyumba hiyo imekamilika ikiwa na huduma zote muhimu, maji, umeme na pia iko safi, lakini anashangazwa kwa nini haijahamiwa hadi alipotoa agizo.

Amri hiyo ni ya pili kutolewa na Bi. Mashavu, ambapo wiki chache zilizopita alifika katika kituo hicho, akakikagua na kujiridhisha kwamba hakina tatizo na kuagiza kwa watendaji wa afya wilayani kuhakikisha daktari husika anahamia mara moja.

Alieleza kushangazwa kwake kuona hadi sasa hakuna daktari aliyehamia katika nyumba hiyo.

Alilazimika kurejea kutoa agizo hilo, baada ya suala hilo kutajwa na baadhi ya wakaazi wa Unguja Ukuu juzi kuwa ni kero, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mabaraza ya vijana wa shehia za Kaepwani, Tindini na Kaebona iliyofanyika kijijini hapo.

Alisema si vyema kwa daktari kuishi mjini na kuiacha nyumba hiyo bila kukaliwa, hali aliyoeleza kuwa ni usumbufu kwa wananchi wa huko hasa pale kunapotokezea dharura ya kuugua wakati wa usiku.

“Nyumba hii imejengwa ili daktari awepo karibu na wananchi na aweze kuwahudumia pale kunapokuwa na mgonjwa mwenye hali mbaya nyakati za usiku. Nataka ndani ya wiki moja daktari awe amehamia, na kama kuna tatizo waje wanione tutafute ufumbuzi,” alisisitiza.

Alieleza kuwa iko haja kwa daktari kuhamia haraka katika nyumba hiyo, kwani mbali na Unguja Ukuu, kituo hicho kinategemewa na shehia nne ikiwemo jirani ya Kikungwi.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, walikaririwa wakisema kwamba hakuna sababu ya kukosekana daktari wa kuishi kijijini hapo, kwani nyumba hiyo iko katika hali nzuri.

“Hali hii inatusumbua sana kwani mara nyingi akitokezea mgonjwa usiku na hulazimika kutafuta gari kwa ajili ya kwenda ama Makunduchi au mjii. Ni Tunaomba muhusika atekeleze agizo la DC kwa ajili ya kuwahudumia wananchi,” alifahamisha Salama Abdalla, mkaazi wa shehia ya Tindini.

Hata hivyo, akizungumzia suala hilo, sheha wa shehia ya Tindini Haroun Rashid Haroun, amesema ingawa nyumba hiyo imekamilika kiujenzi, lakini haina samani yoyote kama vile vitanda na vifaa vyengine vya matumizi.

Alisema, kwa mujibu wa daktari huyo, anachosubiri ni kupatiwa kwa vifaa hivo ili aweze kuhamia.

Aidha, alisema daktari huyo alikuwa likizoni na kwamba sasa ni wiki ya pili tu tangu aliporipoti kazini, lakini ukosefu wa samani ndio uliomzuia kuhamia katika nyumba hiyo.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

MRADI WA KUONGEZA UJUZI NA IDADI YA WAKUNGA MAENEO YA VIJIJINI NCHINI WATAMBULISHWA MKOANI MWANZA

0
0

Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Projestus Rubanzibwa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, kwenye kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi, kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.

Amesisitiza kwamba Wakuu wa Vyuo vya vya Ukunga nchini wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba wanatoa mafunzo bora kwa wahitimu wa vyuo hivyo ili watakapohitimu masomo yao waweze kusaidia kutoa huduma bora afya.

Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini, unatekelezwa na Shirika la Jhpiego kwa kushirikiana na Taasisi ya Wakunga nchini Canada, Shirika la Amref, Serikari ya Canada, Taasisi ya Wakunga Tanzania na Wizara ya Afya nchini, lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwa akina mama na mtoto ili kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi maeneo ya Vijijini nchini.

Na BMG
Kaimu Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dr.Silas Wambura, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, ambapo amesema mkoa wa Mwanza unakabiriwa na upungufu mkubwa wa idadi wa wakunga pamoja na vifaa tiba hali ambayo inasababisha kuwepo kwa vifo vya akina mama na watoto.
Dr.Dustan Bishanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la Jhpiego, amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha unaongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga maeneo ya Vijijini hapa nchini ambapo wahitimu wa masomo ya Sayansi katika maeneo hayo watakuwa wakipewa ufadhiri wa masomo kwa makubaliano ya kurudi kwenye maeneo yao ili kutoa huduma za afya. Mradi huo unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2021.
Kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza ujuzi na idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Dr.Dustan Bishanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la Jhpiego, akizungumza na wanahabari kwenye kikao hicho.
Martha Rimoy ambaye ni Mratibu wa Taifa wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), amesema bado maeneo mengi nchini yanakabiloiwa na upungufu wa Wakunga kutokana na idadi ya Wakunga wanaohitimu vyuoni kutoendana na idadi ya ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya huku wengine pia wakishindwa kwenda kufanya kazi maeneo ya Vijijini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mazingira duni.

Gustav Moyo ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amesema hali ya upungufu wa Wakunga nchini hususani maeneo ya Vijijini si nzuri hivyo Serikali inatumia jitihada mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili kutatua changamoto hiyo.

Amesema asilimia kubwa ya mikoa ya Kanda ya Ziwa inakabiliwa na upungufu huo na kwamba Serikali itakuwa ikitolea kipaumbele kwenye mikoa hiyo pindi inapotoa ajira kwa Wakunga.
Kikao hicho kimewajumuisha wadau mbalimbali wa afya wakiwemo Wakunga, Waganga Wakuu wa Wilaya na Maafisa Elimu ambao watakuwa na wajibu wa kuwahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili kuongeza idadi ya Wakunga.

Wadau wa afya kutoka Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora, Kigoma na Mara wameshiriki kwenye kikao hicho.

RC SHIGELLA ATEMBELEA BANDARI YA TANGA

0
0

Kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa kwanza kulia aliyekaa kwenye boti wakati alipofanya ziara ya kuitembelea bandari hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa kwanza kulia akitazama maeneo ya bahari akiwa kwenye boti wakati alipoitembelea kuona namna ya utendaji wao katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari wa Tanga Henry Arika
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika wa pili kutoka kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia wakati alipofanya ziara ya kuitembelea Bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi kwa ufanisi,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akishuka kwenye boti la Bandarini akisaidiwa kushuka wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliyoitembelea bandari hiyo kuona namna inavyofanya kazi zake
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga Bandari ya Tanga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella ambaye aliitembelea Bandari hiyo anayefuatia ni Mkuu huyo wa mkoa .
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akipanda ngazi kuelekea kwenye meli iliyotinga nanga baharini wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella juzi kuona namna inavyofanya kazi zake
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga bandari ya Tanga wakati wa ziara yake ya kuitembelea Bandari hiyo .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akipanda ngazi kuelekea kwenye meli hiyo akifuatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella .
Kaimu Meneja wa Bandari wa Tanga Henry Arika akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga kwenye bandari ya Tanga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kuitembelea Bandari hiyo kuona shughuli zake anayefuatia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akiteta jambo na PRO wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Moni Jarufu wakati wa ziara yake

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa kwanza kushoto akionyeshwa kitu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,(Ras) Mhandisi Zena Saidi wakati wa ziara yake ya kuitembelea Bandari hiyo jana
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi wakiteta jambo wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa kuitembelea Bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi zake kulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu

Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiwa ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kushoto wa kwaza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakifurahia jambo wakati wakiwa kwenye ziara ya kuitembelea Bandari ya Tanga




Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha Blog

PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

0
0
 Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya  Idara ya Nishati katika kikao hicho.
Kutoka kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini kutoka  Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo, Profesa Mark Mwandosya na mwakilishi kutoka katika kampuni ya Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakiwa katika picha ya pamoja.

Waziri Makamba awabeba vijana Unguja Ukuu

0
0
Mh.Januari Makamba.

Na Salum Vuai, MAELEZO

WAZIRI wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mambo ya muungano Januari Makamba, ameyachangia mabaraza ya vijana Unguja Ukuu shilingi milioni tatu na kuyataka yaelewe kuwa mustakbali wa taifa la Tanzania umo mikononi mwao.

Makamba, alikuwa akizungumza na vijana wa shehia tatu za kijiji cha Unguja Ukuu wakati wa uzinduzi wa mabaraza ya vijana wa shehia hizo uliofanyika juzi katika uwanja wa mpira wa Tindini katika jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati.

Mabaraza yaliyozinduliwa ni yale ya shehia za Kaepwani, Tindini na Kaebona.

Hata hivyo, Waziri huyo aliyepangwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, aliwahutubia vijana hao kwa kuunganishwa na teknolojia ya mtandao akiwa mjini Dodoma ambako ametingwa na vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamba aliwataka vijana hao kutojiingiza katika siasa chafu zinazoweza kuwafarakanisha na kurudisha nyuma jitihada zao na za serikali katika kuleta maendeleo nchini.

Badala yake, aliwaeleza kuwa siasa nzuri ni zile zilizojikita katika kuwaunganisha watu, kuimarisha upendo, na kujenga taifa kwa lengo la kuwakomboa na umasikini.

Waziri huyo pia aliwashauri vijana kutoendekeza mihemko kwa kujiingiza kwenye vitendo viovu ikiwemo biashara au matumizi ya dawa za kulevya, uvutaji bangi, uasherati na uporaji, ambavyo alisema havina hatima njema kwao na kwa taifa.

Alieleza kuvutiwa kwake na ubunifu wa vijana hao katika kujishughulisha na miradi mbalimbali ya kuwaendeleza kimaisha na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

Mapema, Mwakilishi wa jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said, na kwa niaba ya mbunge Khalifa Salum Suleiman, aliwapongeza vijana hao kwa kuitikia wito wa serikali kuunda mabaraza yao ambayo ndiyo njia inayoweza kuwainua.

Aliwahakikishia kuwa viongozi wa jimbo wako pamoja nao kwa kuwasafishia njia ya kutimiza mipango yote ya maendeleo wanayoipanga, huku akiwataka wasiyumbishwe na watu wasiokuwa na nia njema, ambao wamelenga kuwarejesha nyuma.

Aidha aliyachangia mabaraza hayo kwa pamoja shilingi laki tano.

Katika risala yao, vijana wa mabaraza hayo walisema wamejidhatiti kuupiga vita umasikini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji nyuki, kuku, mbuzi na ng’ombe, pamoja na kilimo ingawa wanakabiliwa na changamoto kadhaa za uhaba wa vitendea kazi walizoomba wasaidiwe kuzipatia ufumbuzi.

Hafla ya uzinduzi huo iliyopambwa kwa burudani za sarakasi, muziki, tenzi, ngongoti na maigizo, ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa Said, madiwani wa wadi za jimbo la Tunguu, masheha na wananchi mbalimbali.

SILOAM: SIYO KUPATWA WA JUA NI ' JUA LA HAKI'

0
0
Na Mwandishi Maalum

Tukio la kupatwa kwa jua lililotarajiwa na Dunia na kujiri katika mji mdogo wa Rujewa, Mbalali mkoani Mbeya nchini Tanzania, limeacha simulizi na dhana katika maono na imani mbalimbali zikiwemo za dini.

Mwandishi wa Kanisa la The Pool of Siloam, akieleza mtazamo wa kiimani wa Kanisa hilo, anaeleza kuwa Kanisa hilo linaliona tukio hilo kuwa si la kupatwa kwa jua, bali ni tukio lililogeuka kuwa la 'jua la haki' kuzuka na kufunika sehemu kubwa ya nchi kama ilivyoand ikwa katika Biblia, katika Malaki 4:1-4.

Anaeleza kuwa, watu wengi kutoka mataifa mbalimbali walilitarajia kwa hamu tukio hilo la kupatwa kwa jua lakini ikawa ni tofauti na matarajio hayo hata kwa wanasayansi na wanajimu kwa jinsi ilivyotokea jua la siku hiyo ya Septemba 1, 2016.

"Tukio la kuzuka kwa Jua la Haki kwa mara ya kwanza hapa Tanzania siku ya 12 adari, 3 (Novemba 16, 2014), ikiwa ni siku ya unyakuo wa Mjumbe wa Mapenzi ya Mungu, Eliya Ad2 (miaka 1000), Mungu wa Majeshi nyumbani kwake Bagamoyo mkoani Pwani ambapo Kanisa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walihudhuria", anaeleza mwandishi huyo.

Wakili wa Mungu Elisha Eliya (Ad2) miaka 1000, anayezungumziwa na mwandishi huyo, ndiye Kiongozi wa Kanisa hilo la The Pool of Siloam, ambalo katika miaka ya hivi karibuni limejizolea wafuasi wengi na kuwa na Makanisa yake katika maeneo mbalimbali hapa Tanzania.

Miongoni mwa taratibu za Kanisa hilo, kila muumini hutakiwa kuvaa mavazi nadhifu, maeupe anapokuwa katika shughuli mbalimbali za ibada kanisani au kwingineko.

Akieleza zaidi mwandishi huyo anasema, "Pia kumekuwa na mwendelezo wa matukio hayo mara kwa mara tangu hiyo 12 Adari, 3 (Novemba, 16 2014) katika matukio mbali mbali yaliyohusisha shughuli za Kanisa la Siloamu", anaandika Mwandishi wa Kanisa hilo na kuongeza:-

"Kuzuka kwa jua hilo la Haki kulitokea katika matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na tukio la safari ya Kanisa kwenda jiji la Eliya (Kigoma) Januari 10, mwaka huu wa 2016, lakini pia lilizuka siku Wakili wa Mungu alipofanya ziara katika mkoa wa Ararati (Kilimanjaro) ambapo aliwaambia wa mkoa huo kuwa aliyesikia Sauti ya Mungu, kizazi cha nne alizaliwa katika mkoa huo".

Anaeleza zaidi kwamba, Januari 26, mwaka huu(2016), akiwa katika mkoa wa Kigoma, ambao kwa mtazamo wa The Pool of Siloam ni jiji la Kigoma, Kiongozi wa Kanisa hilo, anayetajwa kwa hadhi ya Wakili wa Mungu Elisha Eliya miaka 1000(Ad2), aliwaambia wananchi wa mkoa huo wakati akihubiri, kuwa Kigoma ndio mahali ambapo sauti ya Mungu kizazi cha nne ilipitia hapo kwa kuwa ndipo alipoisikia Sauti ya Mungu akiwa hapo (Kigoma), mwaka 2003.

"Lakini pia katika ibada ya 23 shebati, 5 (Septemba 1, 2016) wakati akiahirisha ibada iliyoitwa ya Majibu Wakili wa Mungu Elisha Eliya, aliahirisha ibada hiyo kwa kusema yeye (Kiongozi wa Kanisa hilo), anakwenda kuangalia jua la haki na ndivyo ilivyotokea katika sehemu kubwa ya nchi", ameeleza mwandishi huyo.

WAZIRI MKUU KUFUNGA AIRTEL RISING STARS.

0
0
 Mchezaji wa Kinondoni Salum Yohana  (nyekundu) akimpiga chenga mlinda mlango wa Mbeya ma kuifungia timu yake bao la pili  wakati wa fainali za taifa za mashindano ya Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1. 
 Beki wa Kinondoni Haji Mohammed Haji  (nyekundu) akipinga mpira kichwa kuondoa hatari golini kwake huku akisongwa na washambuliaji wa Mbeya wakati wa fainali za taifa za Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.

 Mchezaji wa Kinondoni Hassan Kipera (nyekundu) akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Mbeya Ernest Kamange wakati wa fainali za taifa za mashindano ya Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.
 Mchezaji wa Kinondoni SalumYohana  (nyekundu) akijiandaa kuifungia timu yake bao la pili  wakati wa fainali za taifa za mashindano ya Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.
Mshambuliaji wa timu ya Mbeya (nyeupe) akichuana vikali na beki wa timu Kinondoni wakati wa fainali za taifa za Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa atakuwa mngeni rasmi wakati wa kufunga fainali za taifa za michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Jumapili 11 Septemba mwaka huu kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Salum Madadi amesema hiyo ni heshima kubwa kwa vijana, viongozi na wadhamini wa mashindano hayo. “Ujio wa Waziri Mkuu utaamusha ari ya wachezaji”, alisema Madadi. 

Fainali za mashindano hayo zilifunguliwa Jumanne 6 Septemba na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Jumla ya timu 12 zinashiriki mashindano hayo huku sita zikiwa za wavulana na sita wasichana. Mikoa inayoshiriki niTemeke, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Morogoro na Mwanza kwa wavulana na Temeke, Ilala, Kinondoni, Arusha, Lindi na Zanzibar kwa wasichana.

Katika hatua nyingine, timu za mkoa wakisoka wa Kinondoni za wavulana na wasichana zimekuwa za kwanza kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya Airtel Rising Stars baada ya mechi zilizochezwa asubuhi, Alhamsi Septemba 8 kwenye uwanja wa Karume. Timu ya wasichana Kinondoni waliwafunga Lindi 10-0 huku wavulana wakishinda 2-1 dhidi ya Mbeya.

Wasichana Kinondoni walianza vyema mashindano hayo baada ya kuwafunga Arusha 4-0, kwa hivyo waliingia uwanjani wakiwa wakitaka sare ya aina yeyote kutinga hatua ya nusu fainali. Iliwachukua dakika tano kupata goli la kwanza likifungwa na Aisha Juma. Mchezaji nyota wa mechi hiyo Prisca Bahela aliifungia timu yake mabao matano peke yake kati ya dakika ya 16, 20, 25 kipindi cha kwanza na 30 na 31 kwenye kipindi cha pili. 

Magoli mengine yalifungwa na Isabela John dakika ya 7 na 19 kipindi cha kwanza huku Mwantum Ramadhani na Veronica Mapunda wakifunga dakika ya 23 na 29 kipindi cha pili.

Kwenye mechi kati ya wavulana Kinondoni na Mbeya, timu hizo ziliingia uwanjani kila moja ikiitaji ushindi ili kusonga mbele. Hali hiyo ilisababisha mechi kuwa kali na ya kuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu. 

Timu ya Kinondoni ndio iliyokuwa ya kwanza kupata goli kwenye dakika ya 14, goli likifungwa na Shaban Maguli  aliyewashinda nguvu mabeki wa Mbeya na kuruka juu kufunga akiunganisha krosi nzuri kutoka kwa mshambualiaji mwenzake Marco Muhiru. Baada ya kupata bao, kasi ya mchezo iliongezeka huku Mbeya wakitafuta goli la kuzawazisha na Kinondoni wakitaka kuongeza bao kujihakikishia ushindi. Mpaka kipindi kwa kwanza kinamalizika Kinondoni 1 Mbeya 0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ileile lakini walikuwa ni Kinondoni waliowafurahisha mashabiki wake kwenye dakika ya 57 baada ya kiungo Salum Yohana kupokea pasi nzuri kutoka kwa Hassan Kipera na kufanya kazi nzuri ya kuwachambua  mabeki watatu pamoja na mlinda mlango na kuiandikia timu yake bao ya pili. 

Baada ya bao hilo, Mbeya waliongeza kasi iliyosababisha kupata bao dakika ya 77 likifungwa na Pius Crinton akiunganisha mpira wa kona uliopingwa na Ernest Kamange. Matokeo yalibakia hivyo mpaka mwisho wa mechi na kufanya Kinondoni wavulana na wasichana kusonga mbele. 
Robo fainali za michuano hiyo zitachezwa Jumamosi Septemba 10 huku zikihitimishwa na kilele cha fainali Jumapili 11 Septemba.

Profesa Ndalichako: Sreikali imeshalipa madai ya walimu yasiyokuwa ya mishahara

0
0
Prof.Joyce Ndalichako

Na: Frank Shija, MAELEZO

SERIKALI imewataka walimu wa shule za msingi na sekondari nchini kuwasilisha madai yao yasiyo kuwa ya Mishahara ikiwemo stahili za likizo ili waweze kulipwa madai hayo kwa wakati. 

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1).

Profesa Ndalichako alisema kuwa Madeni ya Walimu yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni madai yatokanayo na mishahara na yasiyokuwa ya mishahara ambayo yamekuwa yakilipwa na Serikali kupitia Wizara yake ambapo hadi hivi sasa hakuna mtumishi ambaye hajalipwa.

“Hakuna jalada la madai ya walimu yasiyokuwa ya mishahara na kama yapo madai walete ili walipwe kwani fedha zipo”. Alisema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa madai ya mishahara yamekuwa yakishughulikiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambapo nayo yamekuwa yakifanyika.

Kwa mujibu wa Profesa ndalichako alisema Serikali imekuwa ikipata ufadhili kutoka Serikali ya Sweden kwa ajili ya kusaidia katika kulipa stahili mbalimbali za walimu ili kuboresha weledi wa taaluma yao.

Kwa upande wa ubora wa Elimu, Ndalichako alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika sekta elimu, ubora wa Elimu ya Tanzania umekuwa ukifanyiwa kazi kupitia program mbalimbali zikiwemo za mpango wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Akitolea mfano Waziri Ndalichako alisema kuwa kumekuwapo na maboresho makubwa tokea enzi za mpango wa UPE miaka ya 1970 ambao lengo lake lilikuwa kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kujiunga na elimu ya msingi.

Waziri Ndalichako mwaka 2013 Serikali iliendelea kufanya maboresho kwa kuongeza sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu ili kupata walimu wenye ubora ndipo udahili wa ikiwemo ufaulu wa daraja la tatu kwa wahitimu wa kidato cha nne na ufaulu wa masomo mawili katika kidato cha sita.

“Serikali ilianzisha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilibainisha kuwa elimu ya msingi na mafunzo mwanafunzi atatakiwa atasoma darasa la kwanza hadi la 6 kwa msingi na mafunzo ni kuanzia darasa la 7 hadi la 12”.

EAC YAHITAJI MIEZI 3 KUTOA MAAMUZI KUHUSU MKATABA WA EPA

0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
 
Immaculate Makilika na Abushehe Nondo-MAELEZO
Dar es Salaam.

WAKUU wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kutumia kipindi cha miezi 3 hadi Januari mwakani ili kuupitia upya mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA) kabla ya kukubaliana na baadhi ya vipengele vya mkataba huo.

Akizungumza katika mkutano wa 17 wa Jumuiya hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema hatua hiyo imetokana na mjadala na majadiliano ya kina kutoka kwa Wakuu wa Jumuiya hiyo.

Rais Magufuli alisema kwa mujibu wa mkataba huo, Umoja wa Ulaya ulitaka mkataba huo usainiwe mwaka huu, ambapo hata hivyo kwa kuzingatia maslahi na ustawi wa jumuiya hiyo, Viongozi wa nchi wanachama wamehitaji muda zaidi wa kufanya maamuzi juu ya mkataba huo.

Dkt. Magufuli alisema kufuatia uamuzi huo, Viongozi hao wameitaka Sekretarieti ya Jumuiya hiyo kuandaa utaratibu wa kusimamia masuala ya mahusiano kuhusu mkataba huo kwa kufanya mawasiliano na Umoja wa Ulaya.

“Tumewaomba wenzetu wa Umoja wa Ulaya wasiiadhibu nchi ya Kenya kwa kuwashinikiza kusaini mkataba wa EPA ifikapo oktoba mosi mwaka huu, ni vyema nchi zote wanachama tujiridhishe na vipengele vya mkataba huo kabla ya kuweka saini ya makubaliano” alisema Rais Magufuli.

Akitolea mfano baadhi ya sababu zinazoifanya nchi za Jumuiya hiyo kuhitaji muda zaidi wa majadiliano kuhusu mkataba huo ni pamoja na uhakika wa kulinda viwanda vya ndani vya nchi wanachama, njia bora za kulinda maslahi ya wakulima, namna bora ya makusanyo ya kodi za bidhaa kutoka nchi za Ulaya.

Kwa upande wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema katika ulimwengu wa sasa suala la utengamano wa jumuiya unahitaji zaidi wingi wa watu na uwezo wa kujitosheleza kwa uzalishaji na masoko yatakayoyosaidia ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama.

“Mwaka 1960 idadi ya watu katika nchi za Afrika Mashariki ilikuwa na takribani watu Milioni 40 ukilinganisha na watu Milioni 165 waliopo sasa ambapo uwezo wa uzalishaji na masoko umeongezeka, hivyo hatuna budi kuwa na jumuiya yenye uwezo wa kuzalisha bidhaa kwa wingi na kutoa huduma” alisema Museveni.

Aidha Museveni aliutaka Umoja wa Ulaya kukubaliana na uamuzi wa wakuu wa jumuiya hiyo kuwapa muda zaidi wa kufanya maamuzi kuhusu mkataba huo ambao umebeba maslahi mapana zaidi kwa wananchi wa jumuiya.

Naye Naibu Rais wa Kenya, William Ruto alisema maamuzi kuhusu mkataba huo yanalenga usawa na kuimarisha umoja baina ya nchi wanachama hivyo ili dhana hiyo iweze kwa wananchi ni wajibu wa Viongozi kuweka maslahi ya wananchi wao.

Aidha katika mkutano huo, Wakuu wa Jumuiya hiyo walipokea ripoti mbalimbali ikiwemo ripoti ya mgogoro wa Burundi, ripoti ya mabaraza la mawaziri wa jumuiya hiyo kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini Sudan Kusini pamoja na uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

TAMKO LA WAZIRI UMMY KWA WANAFUNZI WALIOHITIMU DARASA LA SABA.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAMKO LA MHESHIMIWA UMMY MWALIMU (MB) WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU WATOTO WALIOMALIZA ELIMU YA MSINGI LILILOTOLEWA TAREHE 09/09/2016

Ndugu Wanahabari, Nitumie fursa hii kupitia kwenu kuongea na watoto wa Tanzania, wazazi / walezi na jamii kwa ujumla katika kipindi hiki muhimu ambacho watoto wetu wamemaliza Elimu ya Msingi.  Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza watoto wote waliomaliza mtihani wa Taifa wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka huu, Hongereni sana!. Ni jambo la ufahari kwetu sisi wote kama wazazi/ walezi na Taifa kwa ujumla kwani hii ni fursa adhimu kwa ustawi na maendeleo ya mtoto na ni moja ya njia ya kutimizwa kwa haki ya msingi ya mtoto ya kuendelezwa ambayo inamjengea mtoto msingi imara wa maisha yake ya baadae. Pongezi zangu nyingi kwa watoto wote wa kike na wa kiume walioweza kufikia hatua hii muhimu kwa maendeleo na ustawi wao.

Ndugu Wanahabari, Takwimu zinaonyesha kuwa, wanafunzi 795,761 (wavulana 372,883 sawa na asilimia 46.86 na wasichana 422,878 sawa na asilimia 53.14) wamesajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu. Hivyo ningependa kutumia fursa hii kuwaasa watoto waliomaliza darasa la saba kutojihusisha na tabia au vitendo vyovyote vinavyo hatarisha afya, usalama na maendeleo yao, kama vile kujihusisha kwenye masuala ya ngono, matumizi ya madawa ya kulevya na vileo katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo ya mitihani yao.

 Watoto wetu wa Kike na Kiume wajitambue, na wajue kuwa wao ni hazina ya pekee katika maendeleo ya nchi yetu. Kipindi hiki wakitumie vizuri kwa kuwa waadilifu, waaminifu, wenye bidii na kuzingatia kanuni za nidhamu na tabia njema huku wakijiandaa kwa ajili ya kuendelea na elimu ya Sekondari. Tukumbuke kuwa Serikali imekusudia kumpa kila mtoto nafasi ya kupata elimu ya Sekondari. Msingi tayari umeshawekwa na Rais wa Awamu ya tano, Mheshimiwa John Pombe Magufuli wa kutoa Elimu ya Sekondari bure. Hivyo tusingefurahi mmojawapo kati ya watoto hawa waliomaliza elimu ya msingi jana akaikosa nafasi hii kwa sababu zinazoweza kuzuilika. Nawaasa watoto wote kutumia kipindi hiki kwa kukataa kurubuniwa, kushawishiwa na kujiingiza katika mambo yenye kuhatarisha afya, usalama na maendeleo yao.

Ninawataka Wazazi wenzangu, Walezi na jamii kwa ujumla:-
Kutowaozesha watoto wote wa kike waliohitimu darasa la saba mwaka huu wakati wa kipindi hiki cha kusubiria matokeo yao, iwe ni kwa sababu yoyote ile au kwa lengo la kujipatia mali kwa njia ya mahari. Kila Mzazi/Mlezi anapaswa kutambua umuhimu wa mtoto wake kuendelea kielimu, na kukua kimwili na kiakili kabla ya kuingia katika ndoa. Ieleweke kuwa Elimu ya watoto wa kike ni moja ya njia bora za kupunguza umaskini katika mataifa yanayostawi. Kila mwaka wa elimu kwa mwanamke utaongeza mapato yake ya baadae kwa asilimia 15, ikilinganishwa na asilimia 11 kwa wanaume. Aidha, Kila mwaka wa mtoto wa kike kuwa shule humuepusha na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) mara 7. 

Pia, uzoefu unaonyesha kuwa, kila mwaka wa kuelimika humsaidia msichana kufanya maamuzi bora yake na ya familia yake. Benki ya Dunia ilibainisha ya kwamba kila mwaka wa elimu huzuia vifo 2 vya uzazi katika wanawake 1000 kila mwaka!. Kwa hiyo kumpa mtoto wa kike fursa ya elimu inamsaidia sio yeye tu kukua kiakili na kimwili lakini pia inamnusuru na ndoa na mimba za utotoni na kuchangia maendeleo yake, ya familia yake na jamii kwa ujumla. Ni vyema jamii hasa wazazi na walezi wafahamu kuwa ndoa kwa wasichana sio njia muafaka ya kutatua changamoto za kifedha za wazazi/walezi. Bali elimu ndio njia bora ya kutatua changamoto hizo.

Kuwalinda watoto wote wa kike na wa kiume waliohitimu darasa la saba mwaka huu dhidi ya vitendo vyote vya Ukatili, hasa kwa watoto wa kike kupewa mimba au kuwahusisha katika mahusiano ya kimapenzi. Kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 ambayo imefanyiwa marekebisho na kuhuishwa kwenye Makosa ya Jinai (Penal Code Cap 16)  inaelekeza kuwa ni kosa la jinai  kwa mtu yoyote kumlaghai mtoto wa chini ya miaka  18 kwa kumpa mimba au kufanya nae mapenzi. 

 Kifungu cha 130 (e) cha Sheria hii kinaeleza wazi kuwa “Ni kosa kwa mtu wa jinsia ya kiume kumbaka msichana au mwanamke; kwa ridhaa au bila ya ridhaa akiwa chini ya umri wa miaka kumi na nane. Mtu yeyote atakayetenda kosa la kubaka atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha au kifungo kisichopungua miaka thelathini. Aidha, Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009 Kifungu cha 83 kinaelekeza kuwa ni kosa kumuhusisha mtoto katika kazi, biashara au mahusiano yoyote yenye mlengo wa kingono iwe ni kwa malipo au bila malipo. 

Mkono wa Serikali ni mrefu. Tutahakikisha tunawakamata na kuwafikisha Mahakamani wale wote watakao kwenda kinyume na sheria hizi.

Aidha, natoa Rai kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa kwa mamlaka husika za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata, Wilaya na hata katika Madawati ya Jinsia na Watoto yaliyopo Polisi, pale watakapobaini mzazi au mlezi au taasisi anaenda kinyume na jitihada za serikali za kumuendeleza mtoto kielimu hasa katika kudhibiti ndoa za watoto waliomaliza Elimu ya Msingi hususan katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo yao.

Vunja ukimya toa taarifa kwa maendeleo ya watoto wetu.
Nawatakia kila la kheri watoto wote wa Tanzania katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo yao ya mtihani wa Elimu ya msingi.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watoto wa Tanzania.

Imetolewa na:-
UMMY A. MWALIMU (MB)
WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, 
WAZEE NA WATOTO
DODOMA
09/09/2016

WAENDELEE WAIRWANA WAMKABIDHI MKUU WA MKOA WA SINGIDA MADAWATI ELFU MOJA.

0
0

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilongero Wilayani Singida wakiwa wameketi katika madawati yaliyotolewa na asasi ya WAENDELEE.
Baadhi ya ndogo kati ya madawati 1055 yaliyotolewa na asasi ya WAENDELEE.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Eliya Digha akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew J. Mtigumwe (aliyevaa miwani) mara baada ya kuyapokea madawati hayo yaliyotolewa na asasi ya WAENDELEE, katikati yao ni Mwenyekiti wa asasi hiyo Bw. Joseph J. Kijeruda.

Asasi isiyo ya Kiserikali ya wakazi wa tarafa za Ilongero, Mtinko na Mgori ya WAENDELEE yenye mkusanyiko wa watu wenye jamii ya Wairwana wamemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe mchango wa madawati 1055 yenye thamani ya shilingi milioni 97,125,000.

Akiongea kabla ya kukabidhi mchango huo wa madawati Mwenyekiti wa WAENDELEE Joseph Jingu Kijeruda amesema asasi hiyo imeona umuhimu wa kutoa mchango huo ili kuunga mkono nitihata bza serikali katika kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini.

Kijeruda amesema asasi hiyo yenye lengo la Kuhamasisha na kushiriki katika maendeleo ya Wilaya ya Singida, imeguswa na changamoto za sekta ya Elimu zinazosababisha ufaulu duni kwakuwa wanafunzi wengi wa tarafa hizo tatu wamekuwa wakikaa chini wakati wa masomo.

Ameongeza kuwa makubaliano na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida ni kuyagawa madawati katika shule zenye upunguzu zaidi kuliko nyingine huku akiomba madawati hayo yawekwe kwenye kumbukumbu ya mali za serikali na kutunzwa vizuri.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew J. Mtigumwe ameishukuru na kuipongeza Asasi ya WAENDELEE kwa kuunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania la kuhakikisha kila mwanafunzi ana kaa kwenye dawati ifikapo June 2016.

Mtigumwe amesema hadi kufikia Juni mwaka 2016 halmashauri za Iramba, Mkalama, Itigi, Ikungi na Halmashauri ya Manispaa zilikuwa zimekamilisha utengenezaji wa madawati huku Manyoni ikiwa bado haijakamilisha madawati 1,229 na halmashauri ya Wilaya ya Singida ikiwa haijakamilisha madawati 667.

Amewasisitiza na kuwaagiza wakuu wa Wilaya na wakurugenzi kufanya uhakiki wa madawati, viti na meza kwa shule za msingi na sekondari, kufanya tathmini ya mahitaji ya matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari, kufanya uhakiki wa mali zote za shule na kuhakikisha kuwa maeneo yote ya shule yanapimwa na kupatiwa hati.

Mwanzoni mwa mwaka 2016 mahitaji ya madawati kwa halmashauri ya wilaya ya Singida yalikuwa 16,556 huku upungufu ukiwa 6,122.

Hadi sasa kupitia jitihada mbalimbali kama vile harambee mbalimbali, mchango ya mfuko wa jimbo, mchango wa chama cha mapinduzi wilaya ya Singida, nguvu za wanakijiji na asasi ya WAENDELEE, halmashauri imefanikiwa kuvuka lengo na kupata madawati17,384 ikiwa na ziada ya madawati 828.

Rais Magufuli ateua Makatibu Tawala wa Mikoa ya Rukwa na Mara

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.

Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
09 Septemba, 2016

CHADEMA KUFUNGUA KESI KUOMBA MAHAKAMA KUU KUAMURU JESHI LA POLISI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAFUASI WAKE WANAOSHIKILIWA KATIKA VITUO MBALIMBALI

0
0


Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70 wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga Udikiteta (Ukuta), bila ya kufikishwa mahakamani. Kushoto ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70 wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga Udikiteta (Ukuta). Kulia ni Mwenyekiti Baraza la Umoja wa Vijana Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na kushoto ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

 
  CHADEMA KUFUNGUA KESI KUOMBA MAHAKAMA KUU KUAMURU JESHI LA POLISI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAFUASI WAKE WANAOSHIKILIWA KATIKA VITUO MBALIMBALI 
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinakusudia kufungua maombi katika Mahakama Kuu ya kuiomba mahakama hiyo kuiamuru Polisi kuwafikisha mahakamani watu wanaoshikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na chama hicho kudai kuwa kuna watu 10 ambao wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) na Kituo cha Oysterbay vya Dar es Salaam kwa zaidi ya wiki mbili bila kupewa dhamana ya polisi au kufikishwa mahakamani.

Kauli hiyo ya Chadema imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu yake yaliyo mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo mchana.

Akifafanua kuhusu Habeas Corpus alisema, ni mamlaka iliyonayo Mahakama Kuu ya kuamuru mamlaka yoyote ya kiserikali inayomshikilia mtu kumpeleka mtu huyo mahakamani.

Lissu alisema, vijana hao walikamatwa katika mikoa mbalimbali kwa makosa aliyodai kuwa ni kujihusisha na haraka za kinachoitwa Umoja wa Kupambana na Udikteta (UKUTA) pamoja na masuala mengine ya kisiasa.

“Kama ikifika Jumanne hawajapelekwa mahakamani au hawajapewa dhamana ya polisi, tutakwenda Mahakama Kuu kufungua maombi ya habeas corpus, imuite IGP au DCI au Ma-RPC au wakuu wa vituo wanakoshikiliwa hao waeleze kwanini wanawashikilia hao watu kwa zaidi ya wiki mbili,” alisema Lissu.

Lissu alisema tayari wameshaanza maandalizi ya hati hizo ambazo zitapelekwa Mahakama Kuu ili iweze kuwaita kati ya Mkuu wa Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Makamanda wa Polisi wa Mikoa au Wakuu wa Vituo vya Polisi wanakoshikiliwa watu hao.

Alifafanua kuwa alionana na watu hao ambao wamedai mbali na kushikiliwa lakini pia wamepigwa na kuteswa huku wakidai kuwa wamekuwa wakichukuliwa usiku na kupelekwa katika eneo lililopo Mikocheni ambako wanateshwa na kurudishwa polisi.

Alisema jeshi la polisi linakiuka sheria na haki za binadamu kwa kuwashikilia watu hao kwa muda mrefu bila kuwapa dhamana au kuwafikisha mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashitaka.

TPSF, TBS KUSHIRIKI KAMPENI ENDELEVU YA FAHARI YA TANZANIA PAMOJA NA UTOAJI TUZO KWA BIDHAA 50 ZA KITANZANIA

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini, Gofrey Simbeye akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea uzinduzi wa Kampeni endelevu ya Fahari ya Tanzania pamoja na utoaji tuzo kwa Bidhaa 50 za Kitanzania, sherehe zitakazofanyika tarehe 20 Septemba 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Conference. Kulia ni Msimamizi wa Kampeni hizo, Emmanuel Nnko. Msimamizi wa Kampeni za endelevu ya Fahari ya Tanzania pamoja na Utoaji Tuzo kwa Bidhaa 50 za kitanzania.

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na Taasisi ya Viwango Tanzania TBS kwa pamoja wanakaribisha wazalishaji wa bidhaa nchini kushiriki katika uzinduzi wa kampeni ya Fahari ya Tanzania'-Proudly Tanzania Campaign' ambayo itakwenda sambamba na utoaji tuzo wa Bidhaa 50 bora za Kitanzania-Top 50 Tanzania Brands Awards 2016.

Kampeni hizi na utoaji tuzo utahudhuriwa na Mh. Samia suluhu Hassani, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Viwanda, Biaashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage Viongozi mbalimbali pamoja wageni waalikwa wapatao 400 sherehe zitakazofanyika Tarehe 20 Septemba 2016 katika ukumbi wa Mlimani City.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya uzinduzi wa kampeni hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Sembeye amesema Fahari ya Tanzania ina malengo makuu manne ambayo ni kuhamasisha uzalishaji unaotumia viwango vya ubora ili kukidhi matakwa ya soko.

Amesema kuhamasisha utumiaji wa bidhaa za nchini zilizokidhi ubora na viwango stahiki, kuhamasisha wazalishaji kuongeza dhamani ya bidhaa au kuzalisha kwa kutumia malighafi za Kitanzania. Pia amesema kuhamasisha ushindani wa kuuza kwenye masoko ya nje.

Simbeye amesema kuwa katika kuzindua kampeni hii TPSF, TBS na washirika wao waliona kuanza kwanza na utambuzi wa Bidhaa 50 bora za Kitanzania.

Kwa upande wa Msimamizi wa Kampeni hizo, Emmanuel Nnko amesema kwenye tuzo hizo zitakuwa na madaraja mawili ambayo ni Premier linalohusu Wafanyabiashara au Makampuni makubwa na daraja la wajasiriamali wadogo kama special category.

TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZNAIA (TFF)

0
0


NAPE KUZURU TFF JUMAMOSI, KUTETA NA MALINZI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) kesho Jumamosi Septemba 10, anatarajiwa kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

 KOZI YA MAKOCHA WANAWAKE YAFUNGWA

Kozi ya makocha wa Mpira wa Miguu imefungwa leo Septemba 9, 2016 saa 5.00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine ndiye aliyefunga kozi hiyo ambako pamoja na mambo mengine, alitoa shukrani za pekee kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) akisema: “Tunajivunia kwa upendeleo huu, bila shaka ni kwa sababu hata wanafunzi wanaofanya kozi hii, wanafanya vema.”

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA SIKU TATU MFULULIZO

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo mitano ya Mzunguko wa Nne.

Miongoni mwa michezo hiyo, itakuwa ni ile ya upinzani wa jadi kati ya JKT Ruvu itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini


KOCHA MOHAMMED MSOMALI AZIKWA

Kocha na mchezaji mahiri wa zamani wa Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mohammed Msomali amezikwa leo Septemba 9, 2016 kwenye makaburi ya Kola yaliopo barabara ya zamani ya Dar es Salaam-Morogoro.

Mbali ya wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) waliohudhuria mazishi hayo kwa upande wa TFF iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi katika maziko hayo ya Msomali aliyefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 74.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

 
KILIMANJARO QUEENS YAENDA UGANDA

Baada ya jana Septemba 8, 2016 kuilaza Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’, inatarajiwa kuondoka leo kwenda Jinja, Uganda kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) maarufu kama Kombe la CECAFA itafanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

DK. SHEIN AKUTANA NA WATENDAJI WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS KATIBA,SHERIA,UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mkutano Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2015-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.
Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika mkutano Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2015-2020,chini ya Mwenyekiti Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kulia) akiwa na Viongozi wengine wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mkutano Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2015-2020,chini ya Mwenyekiti Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.

NCHI INA CHAKULA CHA KUTOSHA-SERIKALI

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.

Serikali imetoa kauli kuhusu hali ya chakula nchini na kusema kuna chakula cha kutosha pamoja na ziada ya asilimia 123. Ziada hiyo ya chakula inatokana na uzalishaji wa msimu wa mazao mwaka 2015/2016 ambao unapelekea upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2016/2017.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba leo mjini Dodoma alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu hali ya chakula nchini.“Takwimu zinaonesha upatikanaji na mahitaji ya chakula nchini ni wa kuridhisha kwa kiwango cha utoshelevu wa ziada kwa asilimia 123” Dkt. Tizeba.

Katika kufafanua hali hiyo, Dkt. Tizeba amesema kuwa kulingana na takwimu zilizopo hali ya upatikanaji na mahitaji ya chakula nchini inautoshelevu wa ziada kwa asilimia 123 ambapo nafaka ni asilimia 113 na mazao yasio ya nafaka ni asilimia 140 ambapo viwango vya ziada kwa mazao yote ya chakula ni tani 3,013,515.

Dkt. Tizeba ameongeza kuwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) inauwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 246,000 ambapo kufikia Septemba 6, ilikuwa na akiba ya tani 67,506.920 za chakula kinachojumuisha mahindi, mpunga na mtama.

Pia amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango wake wa kuiongezea NFRA uwezo wa kuhifadhi chakula katika kanda sita baada ya kupata mkopo wa dola za Kimarekani million 55 kutoka Serikali ya Poland ambazo zitatumika kujenga vihenge vyenye uwezo wa kihifadhi tani 190,00 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000.

Kuhusu muda wa Serikali wa kutoa vibali vya kuuza chakula nje ya nchi, Dkt Tizeba amesema kuwa lengo ni kutoa nafasi kwa Serikali kukamilisha taarifa ya tathimini ya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2015/2016 na hali ya upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2016/2017. 

Mbali na hayo, Dkt Tizeba amesema kuwa katika kuboresha hali ya usalama wa chakula nchini, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inapitia upya mfumo wa utoaji wa vibali vya kusafirisha chakula nje ya nchi ili kuwezesha ufuatiliaji wa karibu kuliko ilivyo sasa.

Aidha, Dkt. Tizeba amesema kuwa utoaji wa vibali vya kusafirisha mazao nje umejitokeza baada ya kuona chakula kinasafirishwa nje bila kufuata utaratibu maalumu ambapo wafanyabiashara wa nchi jirani walijihusisha kununua vyakula vikiwa bado mashambani kabla ya kuvunwa.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhifadhi chakula cha kutosha kwa matumizi katika kaya ambapo ameitaka sekta binafsi kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na kuuza mazao katika maeneo yenye uhaba.

Kuhusu hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inayoikabili dunia ikiwamo upungufu wa mvua , Dkt Tizeba amesema kuwa Serikali itaendelea na juhudi za kuhimiza na kupanua kilimo cha umwagiliaji mashambani kwa kuimarisha miundombinu iliyopo na uvunaji wa maji ya mvua ili kuongeza uzalishaji wa mazao wenye tija. 

Hata hivyo, Serikali inaendelea kuhamasisha na kuelimisha wafanya biashara kuuza unga nje ya nchi badala ya mahindi au mchele badala ya mpunga ili kuendana na Sera ya kuendeleza Viwanda nchini na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

YALIYOJIRI BUNGENI LEO September 9, 2016

0
0

SIMU.tv: Serikali inampango gani wa kutatua changamoto katika vyama vya ushirika wilaya ya Karagwe? Naibu waziri  Antony Mavunde anatoa ufafanuzi.https://youtu.be/sDFyQYjoiaM.

 SIMU.tv: Serikali yatolea  ufafanuzi juu ya kuzisaidia hospitali zinazomilikwa na taasisi za dini ili kuziwesha kutoa huduma bora za afya kwa jamii;https://youtu.be/ootCiuZuO2s
 SIMU.tv: Serikali inampango gani wa kutatua shida ya maji wilayani Bagamoyo? Naibu waziri wa maji Mhe.Isack Kamwelwe anajibu swali la Mhe.Kawambwa;https://youtu.be/0Jzm1N6FQ60
 SIMU.tv: Serikali inamkakati wa kuiwezesha TRA kupata rekodi za moja kwa moja kutoka kwa wafanyabiashara? Naibu waziri Ashatu Kijaji anafafanua.https://youtu.be/WIObrtoO74c
 SIMU.tv: Hii hapa kauli ya serikali kuhusu vigezo inavyotumia kutoa mikopo kwa vyama vya  ushirika pamoja na Vicoba; https://youtu.be/_Irp-ehjY6E
 SIMU.tv: Je,Serikali inampango wa kuwamilikisha ardhi wakazi wa Nachingwea? Naibu waziri wa ardhi Mhe.Mabula akijibu swali la Mhe.Masala;https://youtu.be/abDHp4qkgs4
 SIMU.tv: Je, serikali inampango gani wa kuweka sheria kali kwa watu wanaohusika kuwanyanyasa watoto? Haya hapa ni maelezo ya serikali. https://youtu.be/HDCpoL-reJI
 SIMU.tv: Fahamu kauli ya serikali kuhusu kuboresha miundombinu ya mawasiliano katika vijiji vya Kichelu, kiasi na Mbwela. https://youtu.be/J6U8KgVgyY8
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images