Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 964 | 965 | (Page 966) | 967 | 968 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Harrison Mwakyembe akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (Kushoto) Mhe. Ruth Mollel na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi. Wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Mjini Dodoma.
  MWA2
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania
  MWA3
  Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu swali wakati wa Wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Mjini Dodoma.
  MWA4
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akijibu swali wakati wa Wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Mjini Dodoma.

  0 0

   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji 


  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.

  Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa inaendelea na mikakati ya makusudi katika kudhibiti ongezeko la deni la taifa.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Saed Kubenea Mbunge wa Ubungo lililouulizwa kwa niaba yake na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe lililohusu deni la taifa.

  Naibu Waziri huyo aliitaja mikakati inayosaidia kupunguza deni la taifa ambayo ni pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuendelea kutafuta misaada na mikopo nafuu na kukopa mikopo michache ya kibiashara ya miradi yenye kuchochea kwa haraka ukuaji wa pato la taifa.

  Mikakati mingine ni kudhibiti ulimbikizaji wa madai ya kimkataba kwa wakandarasi na watoa huduma na kudhibiti madeni yatokanayo na dhamana za Serikali kwenye mashirika ya umma kwa kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mikataba inayoweza kusababisha mzigo wa madeni kwa Serikali.

  Naibu Waziri Dkt. Ashatu alisema hadi kufikia Juni 2016 deni la taifa lilikuwa dola za kimarekani bilioni 23.2 ikilinganishwa na dola bilioni 19.69 kwa mwezi Juni 2015 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.

  Dkt. Ashatu alifafanua kuwa kati ya kiasi hicho, deni la Serikali ni dola za Kimarekani bilioni 20.5 na deni la sekta binafsi ni dola za Kimarekani   bilioni 2.7 na kuongeza kuwa deni la Serikali linatokana na mikopo ya ndani na nje kwa ajili ya kugharimia miradi ya maendeleo.

  Baadhi ya miradi ya maendeleo iliyoainishwa ambayo imetumia fedha za maendeleo ni pamoja na ujenzi wa barabara na madaraja, mradi ya kimakakati wa kuboresha majiji, ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kv 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga na mabasi yaendayo haraka.
   
  Miradi mingine ni ujenzi wa bomba la gesi na mitambo ya kusafisha gesi, upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dar es salaam na mradi wa maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini.

  Aidha, Dkt. Ashatu amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011, Serikali ilipokea mikopo yenye masharti nafuu na ya biashara kiasi cha sh trilioni 1.3 na mwaka 2014/2015 Serikali ilipokea mikopo ya kiasi cha Sh. trilioni 2.3 mikopo ambayo haikufikia trilioni 15 kwa mwaka 2011 na trilioni 9 kabla ya mwaka 2015.

  Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi alipokuwa akichangia hoja hiyo amewatoa hofu Watanzania na kusema kuwa haitatokea hata siku moja wagongewe milango kwa kudaiwa deni la taifa na kuongeza kuwa deni la taifa linapimwa kutokana na ukusanyaji wa mapato hatua ambayo Serikali inaendelea kuitekeleza kwa vitendo.

  Waziri Mwigulu aliongeza kuwa Serikali haikopi kwa ajili ya miradi ya kawaida isipokuwa inakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa lengo la kuwahudumia wananchi.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Dodoma.

  Serikali katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti 2016 imefanikiwa kulipa jumla ya sh. bilioni 511.86 ikiwa ni malimbikizo ya mwajiri kwa watumishi waliostaafu.

  Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mary Chatanda Mbunge wa Korogwe Mjini aliyehoji kuhusu changamoto inayowakabili wastaafu ya kucheleweshewa mafao yao na Mfuko wa pensheni wa PSPF katika mwaka wa fedha 2015/2016.

  “Kucheleweshwa kwa malipo ya wastaafuhakutokani na Serikali, isipokuwa waajiri ndio baadhi ya nyaraka zinazohusika ili kuaandaa malipo ya wastaafu hao alisema Dkt. Kijaji.

  Naibu Waziri Dkt. Kijaji amesema kuwa nyaraka zinazomhusu mtumishi ziwasilishwe ndani ya muda wa miezi mitatu hadi sita kabla ya muda wa kustaafu ili malipo yake yaweze kuandaliwa kwa wakati na kupata stahili zao ili waweze kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

  Aidha, jumla ya sh. bilioni 83.25 zimelipwa ikiwa ni malipo ya deni kabla ya mwaka 1999 hali inayoonesha kuwa Serikali inaendelea kulipa malimbikizo ya madai ya wastaafu na mafao mengine yanayotolewa na Mfuko huo ili waweze kuendesha maisha yao baada ya kustaafu.

  Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai 2016 Mfuko umelipa mafao ya pensheni ya mwezi kwa kiasi cha sh. bilioni 117 ambapo kwa sasa mfuko huo unaendelea kulipa malimbikizo ya mafao ya mkupuo kwa wastaafu wapya na mafao mengine.

  Katika kudhihirisha dhamira hiyo ya kulipa mafao ya wastaafu, Dkt. Kijaji amesema kuwa tangu Julai 2015 bodi za mifuko ya hifadhi za jamii zinaendelea kufanyia kazi mafao ya wastaafu na kuwalipa stahili zao kwa asilimia 50 kulingana na maelekezo ya Serikali.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama ameliarifu Bunge kuwa mfumo na sheria vimeunganishwa na kutoa fursa kwa mtumishi anapohama kutoka ajira moja kwenda nyingine anaruhusiwa kuhama kutoka mfuko moja kwenda mfuko mwingine.

  0 0

  KIMONDO

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.

  07/09/2016

  Serikali inaendelea kutangaza Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya ikiwa ni kivutio muhimu na adimu nchini na duniani kwa ujumla.
   
  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Kamani leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasungu lililohusu mpango wa Serikali katika kuhamasisha watalii wa ndani na nje kuja kuangalia Kimondo hicho.

  Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali imekuwa inaendelea kuhamasisha kwa kukitangaza Kimondo hicho kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya runinga na nakala za machapisho mbalimbali.

  “Uhamasishaji umefanyika kwa kutumia njia mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na vipindi vya runinga vya ZAMADAMU na Utalii wa ndani na kutumia machapisho ya Tanzania ya “The land of great Heritage Sites” na “Tanzania Cultural Heritage Resources” ambapo nakala zake husambazwa katika maonesho mbalimbali na Balozi zetu pamoja na jarida la “Ifahamu Idara ya mambo ya kale”” na jarida la Maliasili,” alifafanua Naibu Waziri huyo.

  Aidha, Mhandisi Kamani aliongeza kuwa juhudi hizo limepelekea ongezeko la idadi ya watalii na mapato ambapo kati ya mwaka 2012/2013 na 2014/2015 watalii waliongezeka kutoka 990 hadi 1,681 pamoja na mapato kuongezeka kutoka shilingi 811,000 hadi 2,426,00.

  Mbali na hayo, Mhandisi Kamani alitoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na wadau wengine kujitokeza kuboresha mazingira na miundombinu ya eneo la kimondo hicho ili kuweza kuzidi kuvutia watalii wengi na kuongeza pato la taifa.

  Kimondo hicho kinaendelea kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia katika masuala ya utalii ambapo kinaaminiwa kuwa ni kati ya vimondo nane vikubwa zaidi duniani kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 12, urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo – MAELEZO, Dodoma

  07/09/2016

  Serikali imetoa wito kwa wanasiasa kutotumia masuala ya Muungano katika masuala yao ya kiasisa kwani watu wa pande mbili za Muungano hawawezi kufarakana kwa sababu ya umiliki wa eneo.

  Akijibu swali la Mhe. Jaku Hashim Ayoub lililohusu umiliki wa kisiwa cha Latham (Fungu Mbarak), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba amesema kuwa katika orodha ya changamoto 14 za Muungano zilizoshughulikiwa na zinazoendelea kushughulikiwa hakuna suala lolote linalohusu umiliki wa eneo.

  Waziri Makamba amesema hakuna mgogoro wowote unaohusu umiliki wa eneo lolote baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa tafsiri na suala zima la mipaka ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Zanzibar limewekwa wazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya Zanzibar.

  Waziri Makamba amesema kuwa kuhusu suala la mafuta na gesi hakuna mgogoro wowote kwani leseni za utafutaji wa mafuta zilitolewa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika eneo hilo kwa mujibu wa Sheria ya Utafutaji Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 1980.

  “Hakuna mgogoro wowote wa mafuta na gesi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, huko nyuma leseni za utafutaji mafuta zilitolewa na TPDC katika eneo hilo kwa mujibu wa Sheria ya utafutaji mafuta na gesi asilia,” amefafanua Waziri Makamba.

  0 0


  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
  07/09/2016

  Serikali imeunda timu ya wataalamu inayoendelea na kazi ya kutatua na kupatia suluhisho migogoro mbalimbli ya ardhi nchini.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Kamani alipokuwa akijibu swali la Mhe. Dkt Shukuru Kawambwa lililohusu mpango wa Serikali katika kumaliza mgogoro kati ya TANAPA na vitongoji vya Kitame, RAZABA Gama-Makani katika kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo.

  Mhandisi Kamani amesema kuwa mgogoro baina ya kijiji cha Makarunge na hifadhi, unaonesha wananchi hawakushirikishwa katika zoezi la uwekaji mipaka ambapo zoezi hilo liliwashirikisha kikamilifu kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa mkutano na wanakijiji hao.

  Aidha, Mhandisi Kamani amesema kuwa mgogoro wa baina ya shamba la RAZABA na hifadhi umetokana na utata wa eneo la takribani hekta 3,441, ambapo juhudi za kutatua mgogoro huo zinaendelea kufanyika kwa kushirikisha ngazi za vijiji, wilaya, mkoa na wizara husika na kutolewa maelekezo ikizingatia athari za mazingira.

  Kwa upande wa mgogoro baina ya Gama-makani na hifadhi, Mhandisi Kamani amesema kuwa mgogoro huo unatokana na malalamiko ya wananchi kuwa baadhi yao walifidiwa wakati wa uanzishwaji wa hifadhi ambapo hawakuwa wamiliki wazawa wa maeneo hayo.

  “Mgogoro huu unatokana na malalamiko ya wananchi kuwa baadhi ya wananchi ambao walifidiwa wakati wa uanzishwaji wa hifadhi katika eneo hilo, hawakuwa wamiliki wazawa wa maeneo hayo, ingawa taarifa zinaonesha kuwa mchakato wa malipo ya fidia ulifuata taratibu muhimu ikiwemo ushirikishwaji wa karibu wa uongozi wa wilaya ya Bagamoyo, Serikali za kata na Serikali za vijiji husika,” amefafanua Naibu Waziri huyo.

  Migogoro yote iliyoainishwa inahusiana na hifadhi ya taifa Saadani iliyoanzishwa kisheria kwa tangazo la serikali (GN) Na. 281 la mwaka 2005.

  0 0

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kushoto)  wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuhusu ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu, kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia  kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Badhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. Katikati ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa  makazi mapya ya Waziri Mkuu katika eneo la Mlimwa na kuagiza umalizike kwa wakati ili aweze kuhamia kama alivyoahidi.

  Katika ziara hiyo aliyoifanya leo mchana (Jumatano, Septemba 7, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na namna kazi ya ujenzi inavyofanyika.“Nimekuja kukagua makazi mapya na mahali pa kufanyia kazi. Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri, nimejionea mwenyewe na naamini katika kipindi kifupi watakuwa wamekamilisha,” amesema.

  Amesema kutokamilika kwa ujenzi huo hauwezi kukwamisha azma yake ya kuhamia Dodoma kwa sababu tayari inafahamika kuwa  Makao Makuu ya Ofisi ya Waziri Mkuu yako Dodoma.

  Amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa bali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.

   “Tangu wakati huo Serikali zote ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo,” amesema.

  “Pia tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,” amesema.

  Amesema uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kuhamia Dodoma unakuja baada ya kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu na maeneo ya kutolea huduma za kijamii kwa wageni na wenyeji ikiwemo Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yenye uwezo wa kutibu magonjwa makubwa kama ya moyo na figo.

  Waziri Mkuu amesema tayari Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina mpango kamambe (master plan) na ina viwanja vya kutosha kujenga makazi na ofisi mbalimbali.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMATANO, SEPTEMBA 7, 2016.     


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposimama Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
  Sehemu ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia alipowasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.

  ..........................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari ili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016 wakati akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku NNE mkoani huo.

  Makamu wa Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo.

  Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.“Bahari yetu ndio mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”

  Kuhusu uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi zote.

  Amesema mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

  Katika ziara yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua jengo la ofisi za Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

  Makamu wa Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki.
   

  0 0


  Na Ally Daud -Maelezo,Dar es Salaam

  Hospitali za Muhimbili, Amana, Mwananyamala na Kairuki za Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuwekwa kwenye mradi maalum wa kudhibiti taka hatarishi ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha usafi wa mazingira katika huduma za afya nchini.

  Mradi huo wa kudhibiti taka hatarishi ikiwemo sindano, gloves, nyembe na bandeji unasimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mazingira uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya aAfya na Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Neema Rusibawengile alisema kuwa lengo la mradi huo una lengo la kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika maeneo ya hospitali nchini.

  “Mkutano huu umelenga kuandaa na mradi utaodhibiti taka hatarishi amabao utanza kufanya kazi katika hospitali za Muhimbili,Amana,Mwananyamala kairuki na baadaye kuendelea nchi nzima” alisema Dkt Rusibawengile.

  Dkt. Rusibawengile alisema kuwa mkutano huo pia umewakutanisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na Mazingira watakaojadili mbinu mpya za kutunza mazingira kwa ajili ya kupeuka magonjwa ya maambukizi nchini yanayotokana na taka hatarishi.

  Kwa mujibu wa Dkt Rusibawengile alisema mkutano pia huo unalenga kupata njia mbadala za kupunguza uzalishaji wa mekyuri katika hospitali, zahanati na vituo vya afya ili kuondoa utumiaji wa vifaa vyenye nishati hiyo.

  Kwa upande wa mratibu wa udhibiti wa taka hatarishi za Hospitali Dkt. Honest Anicetus alisema wadau wa mkutano huo pia wamepanga kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya afya katika utunzaji wa mazingira.

  0 0

  Makamu wa Rais akiwasalimia wananchi katika mji wa Nangurukuru Wilaya ya Kilwa waliojitokeza kwa wingi wakati akipita kuelekea Mkoani Mtwara kwa ziara ya kiserikali.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amesema serikali itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari ili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.

  Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016 wakati akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku NNE mkoani huo.

  Makamu wa Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo.

  Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.

  “Bahari yetu ndio mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”

  Kuhusu uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi zote.

  Amesema mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa la kwanza hadi kidato cha NNe.

  Katika ziara yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua jengo la ofisi za Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

  Makamu wa Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki.


  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Mtwara
  7 Septemba, 2016

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko akizungumza na wadau mbalimbali walio katika Mapambano dhidi ya Ukimwi leo jijini Dar es salaam. Mkurugenzi huyo amekutana na wadau hao kwa mara ya kwanza kuzungumza nao kuhusu mikakati mbalimbali ya kudhibiti Ukimwi.

  Wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko alipokuwa akizungumzanao leo jijini Dar es salaam.

  Na. Aron Msigwa –  Dar es salaam.

  Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imewataka baadhi ya wadau, mashirika na taasisi zilizo katika mapambano dhidi Ukimwi kuzingatia malengo ya awali ya kuanzishwa kwa taasisi hizo  na kuepuka kujiingiza katika shughuli za uanaharakati ambazo ni kinyume cha sheria.

  Akizungumza katika kikao chake cha kwanza na wadau mbalimbali walio katika mapambano dhidi ya Ukimwi leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa baadhi ya wadau, mashirika na taasisi zimekuwa zikifanya shughuli nje ya malengo ya awali ya kuanzishwa hali inayosababisha mgongano katika jamii.

  "Zipo baadhi ya taasisi zinazofanya shughuli nje ya malengo, tunatambua Serikali haijakataa jitihada za makundi mbalimbali ya kupambana na UKIMWI, sisi kama TACAIDS tutaendelea kuungana na Serikali kuhakikisha kuwa zile taasisi zilizo kwenye mapambano zinasimamia malengo ya kuanzishwa kwake na si vinginevyo" Amesisitiza Dkt. Maboko.

  Amewataka wadau na mashirika hayo kuendelea kujikita na kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ,uhamasishaji wa wananchi kupima kwa hiari VVU kwa lengo la kujua hali zao  ili waweze kujikinga na maambukizi  mapya ya  ugonjwa huo.

  Pia amewata wadau hao kuangalia namna bora ya kuwafikia, kuwaelimisha na kuwafuatilia wananchi walio katika makundi maalum kwenye mazingira hatarishi pia kuongeza shughuli za utafiti zitakazoisaidia nchi kufikia lengo la maabukizi sifuri.

  Amesema hali ya uelewa wa wananchi juu ugonjwa wa Ukimwi imefikia asilimia 90 kwa kuwa watanzania sasa wanauelewa kuhusu ugonjwa huo na hali zao . Aidha, wengi wana uelewa iwapo wamepata maambukizi au la kutokana na kuongezeka kwa kampeni za uhamasishaji na elimu ya kujikinga na maambukizi.

  Kwa upende wake Mkurugenzi wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Lulu Ng’wanakilala amesema Taasisi zinazosajiliwa kutoa huduma za kuzuia na kupunguza maambukizi dhidi ya Ukimwi nchini Tanzania na kuanza kujiingiza kwenye shughuli za uanaharakati zinakwamisha na kupunguza juhudi za Serikali na wadau wengine wenye mapenzi mema walio kwenye mapambano dhidi ya Ukimwi.

  ‘Sisi kama wadau wa hizi taasisi tunaongea lugha moja, NGOs zinazosajiliwa kutoa huduma na kuanza kufanya uanaharakati kupitia masuala ya Ukimwi zinakwenda kinyume cha maelengo,sisi tupo kwa lengo moja kuhakikisha maambukizi yanafikia sifuri kwa kuhakikisha wote wanaotakiwa kupata huduma wanafikiwa na huduma zetu hasa makundi yanayochangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Ukimwi’ Amesisitiza.

  NayeAfisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOFA) Bw. Deogratius Peter, akizungumzia hatua ya baadhi ya taasisi kuenenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake amesema

  ‘Serikali imeshatoa Sera na miongozo mbalimbali inayosimamia shughuli za utoaji wa huduma za mapambano dhidhi ya Ukimwi kwa taasisi, makundi na wadau mbalimbali,  Sisi pamoja na Serikali tunakubali na kuheshimu juhudi za makundi haya katika mapambano dhidi ya Ukimwi, suala la uanaharakati halikubaliki maadili lazima yazingatiwe katika utoaji wa huduma zetu tufuate sheria za nchi ile kuepusha migongano isiyo ya lazima’ Amesisitiza.

  Ameongeza kuwa taasisi zote zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi lazima zikajikite katifa tafiti pia kuyafuatilia makundi yote yaliyo katika mazingira hatarishi ambayo yanachangia  kwa kiwango kikubwa kueneza maambukizi ya VVU.       

  0 0

  Wanafunzi wa shule ya Msingi Mahembe Manispaa ya Singida wakifanya mitihani ya kumaliza elimu ya Msingi.

  Wanafunzi elfu 21, 417 wa shule za Msingi 514 katika halmashauri saba za Mkoa wa Singida leo wameanza mitihani ya kumaliza elimu ya msingi inayofanyika nchini kote.

  Wanafunzi hao mabao wavulana ni elfu 9,639 wasichana ni elfu 11,778 wamefanya mitihani ya masomo ya kiswahili, hisabati na sayansi kwa siku ya leo huku wakimalizia na masomo ya kiingereza na maarifa ya jamii.

  Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian Kimolo amesema mitihani inafanyika kwa amani na utulkivu kutokana na kufanya maadalizi mapema kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na halmashauri zote za Mkoa wa Singida.

  Kimolo ameongeza kuwa Mkoa ulitoa semina nelekezi kwa waalimu wasimamizi 2158 ambao wanasimamia mitihani katika shule 511 zenye wanafunzi wanaofanya mitihani hiyo ikiwa shule za serikali ni 504 na za binafsi 7.

  Amesema kuwa wanafunzi wasioona wanaofanya mitihani ni 8 wavulana watano na wasichana watatu huku wenye uoni hafifu ni 49 wavulana wakiwa 23 na wasichana 26.

  Akiongea baada ya kuanza kwa mitihani katika shule ya Msingi Mahembe iliyopo Manispaa ya Singida Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwana Patrick Masong amesema mitihani inafanyika kwa utulivu na watahiniwa wote wamehudhuria.

  Masong amesema hakuna matatizo yoyote yaliyojitokeza tangu waanze mitihani na wana imani zoezi hilo litakamilika kwa usalama huku akisema ufaulu utakuwa mzuri kutoka na walimu kuwafundisha vizuri wanafunzi hao.

  0 0


  0 0


  Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani  kupuuza  taarifa za sauti  zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni. 

  Taarifa hizo za uvumi  zinazoendelea kuzagaa  kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu  ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni  kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

  Kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), majambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

   Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.

  Niwajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo,  kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa. Sheria ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77 iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo. 

  Sambamba na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu, kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale watakapomtilia mashaka mteja yeyote watoe taarifa kituo chochote cha polisi. 

  Pia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la  Dar Es salaam.

  DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU

  S.N.SIRRO - CP
   KAMISHNA WA POLISI
  KANDA MAALUM
  DAR ES SALAAM

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na kuwachukulia hatua kisheria na za kinidhamu viongozi na watumishi wa umma ambao wanakiuka taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara wakati anafungua jengo la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi bilioni MBILI.

  Makamu wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni watendaji hao.

  Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

  Makamu wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na wahakikishe walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.

  Makamu wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia mienendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawaleta madhara kwa serikali na jamii kwa ujumla.

  Makamu wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa kazi ya kuhakiki mali na madeni ya viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini na mwaka huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote nchini.

  Naye Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kwa nchi nzima.

  Imetolewa na 
  Ofisi ya Makamu wa Rais 
  Mtwara.
  8-Sep-2016.

  0 0


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
  Jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
  Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kagandaakihutubia kwenye hafla hiyo
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akihutubia kwenye hafla hiyo.
   

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda mara baada ya kuwasili kwenye halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo macho, haijalala na haijashindwa kuongoza nchi bali imejipanga kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa.

  "Serikali haijashindwa kuongoza nchi. Nataka niwahakikishie waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kwamba tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa na kazi hiyo imeanza kwa marekebisho makubwa kwa maeneo ambayo tunadhani yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa,” amesema.

  Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, ambaye alitaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kunusuru mdororo wa uchumi uliopo nchini.

  Bw. Mbowe alidai kwamba hali ya uchumi imeshuka na kwa mujibu wa taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) uagizaji wa bidhaa kutoka nje umepungua, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na sekta ya ujenzi imesimama hali inayoashiria kudorora kwa uchumi.

  Kuhusu suala la kupungua kwa mizigo katika bandari na vituo vya forodha, Waziri Mkuu amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bahari umeshuka duniani kote kwa sababu ya kushuka kwa hali ya uchumi kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta na gesi.

  Hata hivyo Waziri Mkuu amesema tayari wafanyabiashara wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameihakikishia Serikali kwamba mizigo yao yote itakuwa inapitia Bandari ya Dar es Salaam hasa kwa mkakati wa pamoja wa ujenzi wa reli ya standard gauge inayoanzia Dar es Salaam-Tabora - Isaka.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuimarisha amani na ulinzi kwenye maeneo yote nchini na kwamba vyombo vya dola viko macho. “Watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji watakamatwa popote walipo na kuchukuliwa hatua za kisheria,; amesema.

  Amesema hatua hiyo inatokana na matukio ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni ambapo raia wasiokuwa na hatia na askari waliuawa katika maeneo ya Vikindu mkoani Pwani, Tanga na Mwanza. Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani

  Katika swali lake, Bw. Ngonyani alitaka kujua ya Serikali kuhusu kukomesha mauaji hayo, yanayotokea kwa watu wasio na hatia pamoja na askari, ambapo Waziri Mkuu, alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi na familia, ambazo ndugu zao walipoteza maisha katika mauaji hayo.

  Pia ametoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha wanawafichua watu ambao wanawatilia shaka na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili waweze kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA. JUMATANO, SEPTEMBA 8, 2016

  0 0  0 0

   Mchezaji wa timu ya Temeke Ismail Kovu (no 4) akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Mbeya Pius Griton (no 15) wakati wa mashindano yanaoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Mbeya ilishinda 1-0. 
   Mchezaji wa timu ya Temeke Ismail Kovu (nyeupe) akitafuta jinsi ya kuwatoka mabeki wa timu ya Mbeya wakati wa mashindano yanaoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Mbeya ilishinda 1-0.
  Beki wa timu ya  Temeke Ismail Kovu (nyeupe) akichuana na kiungo wa timu ya Mbeya Salum Luhinda wakati wa mashindano yanaoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Mbeya ilishinda 1-0.

  Kinondoni yaipunguza kasi Arusha.
  Timu ya Temeke ya wavulana imeshindwa kutamba mbele ya Mbeya baada ya kumkubali kichapo cha 2-0 kwenye mashindano yanayoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa zinazochezwa kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

  Kwenye mechi ya kwanza ya michuano hiyo iliyochezwa leo, Jumatano 7 Septemba – timu ya wasichana ya Kinondoni iliifunga Arusha 4-0. Kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa jana Jumanne 6 Septemba, Arusha waliwafunga Lindi 2-0. Magoli ya Kinondoni yalifungwa na Anna Audela dakika ya 35 kwa njia ya penati. La pili likifungwa na Maimuna Abasi dakika 39, la tatu Aisha Juma dakika ya 41 na la nne likifungwa na Vaileth Tadeo dakika ya 60.

  Kwenye mechi ya Mbeya na Temeke, timu ya Temeke ndio walianza na kasi baada ya kuwa wameshinda mchezo wa kwanza 4-1 dhidi ya Kinondoni, lakini mabeki wa Mbeya walisimama imara na kudhiti washambualiaji wa Temeke. Kwa dakika takribani 20 za kipindi cha kwanza, timu ya Temeke waliweza kuwadhiti vizuri Mbeya na hivyo kusababisha mpira kuchezwa nusu ya uwanja.

  Hata hivyo, kadri muda ulivyokuwa unaenda, timu ya Mbeya iliweza kuanza mashambulizi taratibu na ilipofika dakika ya 45, Mbeya waliweza kuonana vizuri na kucheza pasi za uhakika ambapo Lameck Juma alitoa pasi nzuri kwa Ernest Kamange ambaye alimpiga beki wa Temeke na kuachia shuti lililomshindwa mlinda mlango wa Temeke na hivyo kuiandikia timu yake bao la kwanza. Timu zilienda mapumziko Mbeya ikiwa inaongeza 1-0.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Temeke wakitafuta bao la kuzawazisha. Hata hivyo kwenye dakika ya Ernest Kamange alifanyiwa madhambi kwenye nje kidogo na eneo la penati ambapo mwamuzi wa mchezo aliamuru ipingwe foul. Alikuwa na Lameck Juma ambaye alienda kucheza hiyo foul ambapo aliachia shuti lililoenda moja kwa moja hadi kimiani. Baada ya bao hilo, Temeke waliendeleza mashambulizi lakini yote yaliishia au kwa mabeki au kwa mlinda mlango ambaye alionyesha mpira wa kuvutiwa. Mpaka dakika ya 90 Temeke 0 Mbeya 2.

  Fainali za Airtel Rising Stars 2016 zilifunguliwa jana Jumanne 6 Septemba na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mkuu huyo wa Ilala alitoa Shukrani kwa kampuni ya Airtel Tanzania kuweza kuwekeza kwenye soka la vijana. ‘ Nataka nitoe pongezi za dhati kwa wenzetu wa Airtel kwa kudhamini mashindano haya. Hii inasaidia vijana kuweza kujipatia ajira kwani kwa wale watakaofanya vizuri watachanguliwa kujiunga na timu yetu ya vijana ya Serengeti Boys pamoja na Twiga stars, alisema Mjema.  Aliongeza kuwa Wazazi wanatakiwa wawape watoto uhuru wa kuchangua fani zao na kusimamia bega kwa bega kuwaunga mkono.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema huu ni mwaka kwa Airtel kudhamini mashindano ya Airtel Rising Stars hapa nchini na kuhaidi kuendeleza udhamini huo.

older | 1 | .... | 964 | 965 | (Page 966) | 967 | 968 | .... | 1903 | newer