Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LILILOKUWA NA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA, AONGEA NA WAAKAZI WAKE.

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  alipotembelea na kuongea na wakaazi wa  Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni  jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi Mhe John Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Ali Hapi na viongozi wengine akitembelea eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
 Wananchi wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi  wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
 Kiongozi wa wakazi wa  nyumba za Magomeni Kota Bi Mwajuma  Sama akiongea machache na kuomba dua  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli   alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akimfariji  Bi. Mwajuma  Sama  kwa taabu walizopata  yeye kiongozi na wakaazi wenzie  wa   Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli   akimshukuru wakili Twaha Taslima wa Law Chambers kwa kusimamia vyema maswala ya mgogoro wa eneo iliyokuwa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
PICHA NA IKULU.

WAFANYAKAZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATINGA MAHAKAMANI.

$
0
0
Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat
Mfumukeko.

Na Woinde shizza,Arusha.
Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
wamefungua kesi kumshtaki Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo
kwa madai ya kuvunja mikataba ya ajira.

Kesi hiyo wameifungua katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EACJ) kitengo cha awali.

Wafanyakazi watatu kutoka Idara ya Amani na Usalama
wanadai Juni 17, Katibu Mkuu huyo alivunja mikataba yao ya
ajira kinyume na agizo la Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki waliyoyatoa kwenye mkutano wa nyongeza
wa 31 na kwa kuzingatia Kanuni ya 96 ya taratibu za
wafanyakazi wa EAC ya mwaka 2006.

Wanadai kuwa walipokea barua kutoka Masjala ya EAC yenye
notisi ya miezi mitatu ya kusitishwa kwa ajira zao iliyowekwa
saini na katibu mkuu huyo, huku ikieleza kuwa EAC haina
fedha za kuendeleza mradi wa APSA unaopata fungu kutoka
Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Umoja wa Afrika (AU).

WATANZANIA 30 WAFAIDIKA NA KAMPENI YA FNB KWA KUJIZOLEA MILIONI 30

$
0
0
Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdul (kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha wateja wa rejareja wa First National Bank (FNB), Francois Botha (kushoto) kwa niaba ya washindi kumi wa kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es salaam leo. Meneja Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachang’a akiwapigia simu washindi wa droo ya kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi ambapo washindi kumi walijipatia shilingi milioni moja kila mtu. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Sheria wa benki hiyo, David Sarakikya (kushoto), Mtaalamu wa Mfumo wa Habari na Mawasiliano wa FNB, Bi. Ilakiza Hezwa na Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdul (kulia).


KAMPENI ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba iliyoendeshwa na First National Bank Tanzania imefika mwisho baada ya miezi mitatu ambapo. Kupitia droo ya mwisho ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam leo washindi kumi wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja. 

Akiongea kwenye makabidhiano ya zawadi ya fedha hizo kwa washindi wa mwezi Agosti, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha alisema: “Kampeni ya Mama imekuwa na mvuto kwa watu wengi na wameweza kuitumia kujiwekea akiba benki. Sisi kama benki ni jukumu letu kuwatunuku wateja wetu kwa uaminifu wao kwetu na kuwapa nafasi ya kujiwekea akiba ya badae. Hii kampeni imekuwa na mafanikio makubwa na tumefurahia kuona wateja wetu wanajitokeza kwa wingi kushiriki.”

Kampeni ya Mama ilizinduliwa mwezi Juni ambapo katika muda wa miezi kampeni hiyo imetoa fursa ya kujishindia mamilioni ya fedha taslimu kutokana na kila shilingi elfu hamsini waliyokuwa wakijiwekea kwenye akaunti zao. 

Botha alitaja washindi wa droo hiyo kuwa ni. Adolph Kalyelibwa wa Mwanza , Halima Mohamed wa industrial branch, Devotha Muttakywa wa Mwanza, Alvin Kamoyo wa Mwanza, Gilbert Mosha wa Mwanza, Denis Mazige wa Dar es salaam, Isiaka Said wa Mwanza, Gladys Cafrica wa Dar es salaam, Geradina Chipala wa Mwanza na Sumbuko Chipanda wa Dar es salaam. 

Benki ya FNB ilianzisha kampeni ya Mama kwa lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiwekea akiba ambapo kupitia droo za kampeni hiyo kwa muda wa miezi mitatu jumla ya washindi 30 wamejishindia zawadi. 

Botha alisema kwamba kampeni hii imejenga msingi mzuri kwa kuijengea jamii utamadani wa kuweka akiba kwa ajili ya badae na vilevile ni msingi mzuri wa kupata maisha bora kutokana na kuwa na akiba ya kuwekeza katika maendeleo na kuboresha maisha.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ajibu kilio cha muda mrefu cha wakazi waliokuwa wakiishi nyumba za Magomeni Kota Dar es salaam, Aahidi kuwajengea nyumba za kisasa.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika nyumba za Magomeni  Kota ambazo zilivunjwa kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa za makazi na Biashara ambao walitelekekezwa kwa muda mrefu na manispaa ya Kinondoni na kuwafanya waishi maisha magumu. Katika hotuba yake Mhe. Rais ameahidi kuwajengea nyumba  za kisasa wakazi hao  644 ambapo wataishi  bure kwenye nyumba hizo  kwa muda wa miaka 5 kabla ya kuandaliwa kwa utaratibu wa kuwamilikisha nyumba hizo. 
 Baadhi ya wakazi wa nyumba za Magomeni Kota wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli mara baada ya kuahidi kuzipatia majibu kero zao za muda mrefu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza jambo na viongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kuwasili eneo la Magomeni Kota zitakapojengwa nyumba za kisasa za wakazi 644   watakaojengewa nyumba hizo na Serikali. Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa unatarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu.
Waziri wa Ardhi ,Nyumbana Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) wakati akikagua eneo zitakapojengwa nyumba za kisasa za wakazi 644 wa eneo la Magomeni Kota ambao watajengewa nyumba na Serikali. Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa unatarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu. Wengine Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi, Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Paul Makonda 9wa pili kutoka kulia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wazee waliokuwa wakazi wa nyumba za Magomeni Kota mara baada ya kuzungumza nao leo jijini Dar es salaam. Mhe. Rais pamoja na mambo mengine ameahidi kuzishughulikia kero zote za wazee hao ikiwemo kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ambazo watakaa bure bila kulipia kwa muda wa miaka 5 na baadaye kufanyika utaratibu wa kuwamilikisha nyumba hizo kwa gharama nafuu.
 Baadhi ya wananchi wa jiji la Dar es salaam wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Magomeni Kota leo.
Msemaji wa Wazee wa Magomeni Kota Mchungaji John Raymond (wa pili kutoka kushoto) akiwa na uso wa furaha akiwa  na Wakazi wenzake 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota ambao wameahidiwa kujengewa nyumba zao na Serikali.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota ambao ambao nyumba zao zilivunjwa kupisha ujenzi wa mradi wa kisasa wa Makazi na Biashara chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni. Serikali  imeahidiwa kuwajengea  nyumba wakazi hao kufuatia agizo la Rais.
 Baadhi ya akina Baba waliokuwa wakazi wa nyumba za Magomeni Kota wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kufuatia kero na Hoja zao za muda mrefu kupatiwa majibu.
  Baadhi ya Wazee waliokuwa wakazi wa nyumba za Magomeni Kota wakimwombea dua ya Afya njema na Utumishi mwema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia  Hotuba kufuatia hotuba aliyoitoa mara baada ya kuwatembelea eneo la Magomeni Kota kuji kero na Hoja zao za muda mrefu huku akiahidi kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ambazo watakaa bure kwa muda wa miaka 5 kabla ya kufanyika utaratibu wa kuwamilikisha kwa gharama nafuu.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza
Wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alipowatembelea wakazi hao kwa lengo la kuzungumza na kujibu kero zao za muda mrefu leo jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi akizungumza na Wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi akizungumza na Wakazi 644 wa zilizokuwa nyumba za Magomeni Kota.Picha/Aron Msigwa.

NHC YAVAMIA WADAIWA SUGU UPANGA NA KUWATOLEA VYOMBO NJE

$
0
0

Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Mzizima Auction Mart wakitoa vyombo vya Winfrida Nkungu Mpangaji wa shirika la nyumba NHC nyumba namba 838 Mtaa wa Senegal Upanga jijini Dar es salaam kutokana na kudaiwaBgharama ya Pango miezi tisa kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tatu 2,300,000. Shirika la Numba la Taifa NHC liko kwenye kampeni kubwa ya kukusanya madeni yake maeneo mbalimbali nchini.
2
Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Mzizima Auction Mart wakikusanya nguo na vitu mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwenye nyumba hiyo.
34
Wakiendelea kutoa vyombo nje.
5
Vyombo vikiwa nje baada ya kampuni hiyo kukamilisha kazi ya kutoa vyombo hivyo nje.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA HOTEL YA NYOTA TANO KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la funguzi wa hotel ya Ramada Encore  yenye hadhi ya nyota 5 jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo Bw. Abdul Ismail.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa hoteli ya Ramada Encore iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli Ramada Encore  Bw. Abdul Ismail wakati wa halfa fupi wa uzinduzi wa Hotel ya Ramada Encore jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua hoteli ya nyota 5 ya Ramada Encore katikati ya jiji la Dar es salaam.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Serikali ya Tanzania haiwezikufuta michezo nchini.

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
06/09/2016
Serikali ya Tanzania haiwezi na haina nia ya kufuta michezo nchini kwa sababu yeyote ile.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa akijibu swali la Mhe. Venance Mwamoto ambaye alihoji kutaka kujua kwa nini Serikali isifute Michezo nchini.

Akijibu swali hilo Mhe. Nape alisema kuwa nia ya Serikali ni kuendeleza Sekta ya Michezo kwa maendeleo ya Taifa kwa kuwekeza katika miundombinu ya michezo, Elimu ya Michezo na kushirikiana na wadau wengine na kuhakukisha sekta ya michezo inaendelezwa.

“Naamini kuwa swali lake limelenga kupata maelezo ya kwanini michezo haiendelei kwa kasi wanayotamani wanamichezo wengi hapa Tanzania na wala siamini kuwa anayo nia ya kutaka Serikali ifute michezo kwa kuwa anafahamu fika umuhimu wa michezo kwa Taifa pamoja na wananchi kwa ujumla”, Alisema Mhe. Nape.

Waziri Nape aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake itaendelea kutenga fedha kupitia Bajeti ya Wizara na vyanzo vingine kadri iwezekanavyo ili kuendeleza michezo katika ngazi mbalimbali.

Aidha, alitoa wito kwa wadau wa michezo, ikiwemo Serikali za Mitaa, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, waheshimiwa wabunge, Sekta binafsi na wadau wengine kuibua vipaji vya michezo kwa watoto kuanzia umri mdogo na kuviendeleza.

Akizungumza kuhusu mpango wa Serikali kudhibiti mavazi yasio na staha kwa baadhi ya wasanii nchini, Waziri Nape amesema kuwa Wizara kupitia Baraza la Sanaa la Taifa imekuwa ikitoa elimu kwa wasanii mara kwa mara juu ya umuhimu wa maadili katika sanaa na namna ya kubuni kazi za sanaa zenye ubora unaozingatia maadili ya nchi na jamii.

Pia Waziri Nape ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wasanii nchini wanazingatia nidhamu katika mavazi wanayoyatumia katika kazi zao za sanaa na kuwataka Watanzania kutunza na kulinda maadili na utamaduni wa Mtanzania.

“Ikiwa jamii inayakataa mavazi hayo ili kulinda maadili itapelekea wasanii hao kuona mavazi hayo hayatakiwi, endapo jamii itaonyesha kuyakuwali mavazi hao itapelekea wasanii hao kuona ni kitu cha kawaida na kuzidi kutozingatia maadili,” alifafanua Waziri Nape.

Mavazi ni moja ya utambulisho unaozingatiwa katika Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayomtaka Mtanzania ana wajibu wa kulinda mila na desturi sambamba na kuhakikisha maadili yanalindwa na wanawake hawadhalilishwi kupitia kazi za sanaa.

Rais John Pombe Magufuli akagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam asubuhi hii

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kukakagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam asubuhi hii,Rais Magufuli aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh,Paul Makonda pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako .

 Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akizungumza jambo wakati Rais Dkt Magufuli alipokwenda kukagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam asubuhi hii,Rais Magufuli aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh,Paul Makonda pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako .

KIVUKO CHA MV.MAGOGONI CHAANZA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI

$
0
0
 Magogoni kikiwa majini mara baada ya ukarabati wake kukamilika.
mv1
Mkuu  wa Jeshi la Majini (Navy, Meja Jenerali Rogastian Laswai (kulia) akitoa maelezo Kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa kwanza kushoto) kuhusu huduma za usafiri wa majini katika Kivuko cha Mv. Magogoni.
mv2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Majini (Navy) Meja Jenerali Rogastian Laswai kabla ya ufunguzi wa Kivuko cha Mv. Magogoni, jijini Dar es salaam.
mv3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kivuko cha Mv. Magogoni mara baada ya ukarabati wake kukamilika, Jijiji Dar es salaam.
nav
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa nne kushoto) akiwa pamoja na watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakivuka kuelekea upande wa Kigamboni kwa kutumia usafiri wa Mv. Magogoni.
mv4
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan (Kushoto), akitoa maelezo ya moja ya kifaa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) mara baada ya ufunguzi wa Kivuko cha Mv. Magogoni.
mv5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Kivuko cha Mv.Magogoni, Jijini Dar es salaam.
mv6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa nne kushoto) akiwa pamoja na watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakivuka kuelekea upande wa Kigamboni kwa kutumia usafiri wa Mv. Magogoni.
mv8
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akishuka kutoka katika kivuko cha Mv. Magogoni.
mv9
Wakazi wa Kigamboni wakielekea kupanda  kivuko cha Mv. Magogoni mara baada ya kuanza kutoa huduma za usafiri kati ya Magogoni  na Kigamboni.
Muonekano wa Kivuko cha Mv.

Picha Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA BURUNDI NA SUDAN KUSINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Burudi uliowasilishwa kwake na Aime Laurentine Kanyana Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
mge1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Aggrey Tisa Sabuni Mjumbe maalum wa Rais wa Sudani Kusini aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kuwasilisha ujumbe kutoka kwa Rais huyo wa Sudan kusini.


Serikali yapongeza Sekta Binafsi kwa kuwekeza katika Utalii

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Hoteli ya Ramada encore Abdul Ismail (kushoto),wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Hoteli hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi (kulia) wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Hoteli hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Nimrod Mkono (kushoto) walipokutana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Hoteli ya RAMADA encore leo Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akielezea jambo wakati alipotembelea chumba cha mazoezi kilichopo katika Hoteli ya RAMADA encore alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Hoteli hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msaidi wa Msimamizi Msaidizi wa Mapokezi katika hoteli hiyo Bi. Janeth Leornard.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi wa Hoteli ya RAMADA encore, Abdul Ismail (kulia) wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi Hoteli ya RAMADA encore leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Uongozi wa Hoteli ya RAMADA encore wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hoteli hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija, MAELEZO.

NAIBU WAZIRI MPINA AKAGUA MIUNDO MBINU YA DAWASCO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akisisitiza jambo kwa kaimu mkurugenzi wa Uzalishaji na usambazaji wa maji  Dawasco Injinia Aroun Joseph mara baada kufanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya dawasco.                           
Naibu Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akitoa maelekezo kwa Mwanasheria kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira Nchini NEMC  Manchare Heche jinsi ya kuweza kushughulikia tatizo la utririshaji maji taka.                          
 Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji maji kutoka Dawasco injinia  Aroun Joseph akielezea jambo mbele ya naibu waziri Mh.Luhaga  Mpina mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya Dawasco

Source East Africa B2B Trade platform for craft products in offing

$
0
0


Sanaa za Mikono....



Sanaa za Mikono....













Mratibu wa Maonyesho ya Sanaa za Mikono kwa Afrika Mashariki Bi. Nakaaya Sumari akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) na baadhi ya wadau waliokuja kwenye uzinduzi wa Maonyesho hayo kwa vyombo vya habari, vinavyotarajiwa kufanyika mwezi septemba 23 hadi 25 2016, Jijini Arusha


















Sanaa za Mikono....



Sanaa za Mikono....



Sanaa za Mikono....









































































Ramadhani Mvungi (Star Tv ) na Ihucha Adam (EABC-PR)wakiteta jambo....


Mpiga Picha Kapigwa Picha Akionyesha Picha kwa wapigwa picha na mpiga Picha...
Mtangazaji Maarufu wa AZAM TV (Idd Uwesu ) katika Ubora wake....

ADAM IHUCHA,

CRAFTS producers in East Africa will soon be able to sell their products to international markets following the plans to establish an annual professional for Business-to-Business (B2B) trade fair for Home Décor, Fashion Accessories and Lifestyle products in the region.

Currently, there is no B2B trade platform for the crafts sector in the whole of East African region.


he Africa and Middle East World Fair Trade Organization (WFTO) regional director, Mr Bernard Outah said there is need to establish B2B so that producers could easily sell their products to any country of their choice without problem.

He said, at the moment, the only option for producers to reach regional or international buyers is to travel around the region in search of potential buyers or to participate in trade fairs in South Africa, West Africa or International trade fairs in Europe or the US. He said the high cost of participation fails most of African crafts producers from attending international trade fairs.

“Failure to access market opportunities is one of the key challenges that face most of African crafts producers in East African region,” he said. According to Mr Outah, the establishment of B2B will enable East African crafts producers to excel in the area and boost their businesses at both local and international levels.

Meanwhile, the public has been urged to recognize the crafts sector as a key economic sector in the region and offer required support so that it can unfold its potentiality. CBI programme manager for the export coaching programme in East Africa Ms Heiydy van der Ploeg said there is need to promote and give support to craft sector so that it could help in building up East African countries economies.

According to UNESCO, the crafts sector is the second largest employer in the developing world behind agriculture. Most of those engaged in crafts are majority women with little or no education.

The global crafts sector is valued at USD 34bn/- per annum and 65 percent of global crafts exports come from developing countries. East Africa is one of the most important crafts producing regions on the African continent.

Its geographical location has made it a melting pot of different cultures, resulting in a rich diversity of crafts skills and products. The Chief Executive Officer (CEO) for TradeMark East Africa (TMEA), Mr Frank Matseart said crafts are important part of the East African trade story but it receives little input from various stakeholders.

He added that a growing tourism sector in the region offers the potential to sell products to tourists through souvenir and gift shops. “Many hotels and lodges, besides sourcing products for their own in-house gift shops also look for interior decoration products to decorate their houses,” he said.

For the first time, professional craft trade fair is scheduled to take place in the country from September 23rd to 25th, this year. --

MAHAKAMA YAWAHITAJI WENYE MAJINA HAPO CHINI.

$
0
0
Tunaomba kutoa taarifa kuwa, wenye majina na anuani hapo chini ambao ni watumishi/walikuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanahitajika kupata taarifa muhimu na maalum juu ya masuala yahusuyo Utumishi wao: Wafike na kuonana na Bibi. Agatha Ng’ingo – Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Utawala na Utumishi, namba ya simu (0673 – 001 773) ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.

S/N

JINA KAMILI

CHEO

KITUO CHA KAZI

C/N

1

BW. ROBERT WILLIAM CHAGAKA

DEREVA II

MAHAKAMA YA WILAYA IRAMBA

111824992

2

BW. GODLISTEN MOSES MWANRI

DEREVA II

MAHAKAMA YA WILAYA KISHAPU

111827839

3

BI. AGNES AUDAX RWEGOSHORA

HAKIMU MKAZI II

MAHAKAMA YA MWANZO UJIJI KIGOMA

111838464

4

BI. HAPPINESS ELIAS MISHWARO

HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO MWANDAMIZI

MAHAKAMA YA WILAYA MBARALI

10915901

5

BW. BARAKA JAFARI MUKAMA

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA WILAYA ILALA

9927780

6

BW. RAMADHANI MOHAMED KILYOUSUNGU

MLINZI

MAHAKAMA YA WILAYA RUFIJI

9496501

7

BI. REHEMA SAMWEL PANDAPANDA

HAKIMU MKAZI II

MAHAKAMA YA WILAYA MPWAPWA

9927919

8

BI. HAWA GODREY MKUMBO

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA WILAYA KASULU

8203232

9

BW.CHRISTINA JOHN MAYILA

MSAIDIZI WA OFISI MWANDAMIZI

MAHAKAMA YA WILAYA KAHAMA

7758540

10

BW. YASSINI WAZIRI MASELE

MLINZI

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA

111400187

11

BW. JOSEPH FRANCIS BOMA

MLINZI

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA

111397724

12

BW. BRUTON RABIEL KIMARO

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MANYARA

7203497

13

ABIHUDI GILLIARD MASEU

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA KUU ARUSHA

5187924

14

HUSSEIN HASSAN BACHOO

AFISA UGAVI I

DAR ES SALAAM

5529186

15

ASHA MAGOMBA ABDALLAH

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA WILAYA MONDULI

111827925

16

BW. AMRI MUSSA RASHIDI

MLINZI

MAHAKAMA YA WILA

YA TANDAHIMBA

9544435

Imetolewa na,
MTENDAJI MKUU.

Benki ya TIB Corporate yatoa msaada wa Sh 10 million kwa taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

$
0
0
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TIB Corporate Bw Frank Nyabundege (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi y ash milioni 10 kwa Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dk. Julius Mwaiselage (kulia) kuiwezesha taasisi hiyo kukabiliana na mahitaji mbalimbali katika matibabu ya wagonjwa wa saratani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Charles Singili (wa pili kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Charles Singili (kushoto) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 
Benki ya TIB Corporate imetoa msaada wa sh mil 10/- kwa taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ikilenga kuiwezesha taasisi hiyo kukabiliana na mahitaji mbalimbali katika matibabu ya wagonjwa wa saratani.Msaada huo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo katika kuisaidia jamii kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mteandaji wa benki hiyo Bw Frank Nyabundege alisema taasisi hiyo ina uhuru wa kuchagua mahali inapoweza kuelekeza matumizi ya pesa hizo kulingana na vipaumbele vyake.

“Tunaunga mkono jitihada zinazofanywa na ORCI katika kukabiliana na saratani hapa nchini na ndio maana na sisi tukaona tuna wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia kiasi hiki cha pesa ili kisaidie kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili taasisi hii muhimu zikiwemo,’’ alibainisha Bw Nyabundege.

Alisema uwepo wa taasisi hiyo ni fahari kwa taifa kwa kuwa imekuwa ikisaidi mapambano dhidi nya ugonjwa huo ambao umekuwa kikwazo katika uzalishaji kwa kuwa umekuwa ukishambulia nguvu kazi ya taifa.

“Matibabu ya ugonjwa huu pia yamekuwa yakihusisha gharama kubwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi katika ngazi za kifamilia,’’ aliongeza.Alitoa wito kwa watu binafsi na mashirika mengine kujitokeza na kusaidia taasisi hiyo ya Serikali kwa kiasi chochote.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage alisema kwa sasa taasisi yake inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa huku akikabiliwa na uhaba wa miundombinu na dawa na vifaa tiba vinavyoendana na ongezeko hilo na hivyo kutoa wito kwa mashirika, taasisi na watu binafsi kuisaidia taasisi hiyo.

“Kwa takwimu za mwaka jana tulipokea wagonjwa zaidi ya elfu tano ikilinganishwa na wagonjwa 1500 kwa mwaka tuliokuwa tukiwapokea miaka ya nyuma wakati taasisi inaanza,’’ alisema huku akitaja baadhi ya sababu za ongezeko la ugonjwa kuwa ni pamoja na aina ya vyakula vinavyoliwa na kwa sasa, matumzi ya tumbaku na ukosefu wa mazoezi miongoni mwa wana jamii.

MUWSA YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI MANDELA MJINI MOSHI.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq Madawati kwa ajili ya shule ya Msingi Mandela iliyopo Manispaa ya Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq (katikati) akiwa ameketi kwenye Dawati na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru pamoja na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mandela. Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandea wakiwa wameketi katika madawti yaliyotolewa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikabidhi madawati kwa mkuu wa shule ya msingi Mandela ,Pegi Michael.




Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.Said Mecky Saidiq akiwasili katika shule ya msingi Mandela iliyopo kata ya Bomabuzi wilaya ya Moshi kwa ajili ya kupokea msaada wa Madawati yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).

Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiimba nyimbo wakati wakipokea wageni waliofika katika tukio la kukabidhi madawati.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq alipowasili katika shule ya msingi Mandela kwa ajili ya kukabidhiwa Madawati.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (kushoto) pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya (kulia) wakati wa makabidhiano ya Madawati kwa ajili ya shule ya msingi Mandela.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ,Joyce Msiru akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msing Mandela.

Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Wananchi Babati wazinduliwa mradi wa maji na mwenge wa uhuru

$
0
0

Mkimbiza mwenge kitaifa Lucia Kamafa akimtwisha ndoo ya maji Mariam Mollel mkazi wa Gunge Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambpo ukiwa Mkoani humo ulitembelea miradi yenye thamani ya sh7.7 bilioni.

Mwenge wa uhuru ukikimbizwa kwenye Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambapo ulizindua miradi yenye thamani ya zaidi ya sh1 bilioni.


Wakazi 2,986 wa Kijiji cha Endanachan Wilayani Babati Mkoani Manyara, waliokuwa wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji, wameondokana na changamoto hiyo baada ya kuzinduliwa mradi wao utakaozalisha lita 144,000 kwa siku.

Akizindua mradi huo, kiongozi wa mbio za mwenge uhuru kitaifa George Mbijima aliwataka wakazi hao kuuchunga na kuutunza mradi huo kwani serikali imetumia gharama kubwa hadi kufanikisha kuwapatia maji wananchi wake.

Mbijima alisema maji ni hitaji kubwa la jamii hivyo itakuwa jambo la ajabu endapo baada ya muda mfupi, miundombinu ya mradi huo ukaharibika kwani haitakuwa sifa nzuri kwa jamii kususiana na tukio hilo.

Ofisa mtendaji wa kijiji cha Endanachan Amos Gurti alisema mradi hadi kukamilika mradi huo umegharimu sh286 milioni, ikiwemo sh29 milioni za wananchi, sh600 milioni za halmashauri na sh256 milioni za wahisani wa Water aid na Kanisa katoliki jimbo la Mbulu, (DMDD).

Alisema kupitia mradi huo wananchi wengi zaidi watapata huduma bora kwani una vituo tisa vya kuchotea maji ya bomba, bomba za usafirishaji kilometa 1.2 bomba za usambazaji kilometa 7.1 na tenki moja lenge ujazo wa lita 50.

“Usimamizi na uendeshaji wa mradi huu unategemea zaidi mapato yanayotokana na ankara za maji yanayochotwa na wananchi wa hapa ambapo ndoo moja ya maji yenye ujazo wa lita 20 huuzwa kwa sh25,” alisema Gurti.

Mmoja kati ya wakazi hao Martha Lowri alisema awali walikuwa wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma ya maji ila baada ya huduma hiyo kuanzishwa watakuwa wamerahisishiwa kazi ya kufuata maji mbali.

Lowri alisema hivi sasa hata mahusiano yao ya ndoa kwenye nyumba za wanawake wa eneo hilo utakuwa mzuri kwani hawatatembea tena umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma hiyo mbali na majumbani mwao.

MATUKIO MBALIMBALI LEO BUNGENI MJINI DODOMA.

$
0
0

Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha 2 cha bunge la kumi na moja  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Margaret Sitta akimueleza Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wito kwa waajiri nchini kuwasilisha nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii miezi mitatu hadi sita kabla ya kustaafu kwa wateja wao ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni Mjini Dodoma.

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA MSUMBIJI

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio  mara  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Bibi, Monica Patricio Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais leo,(katikati) Balozi Mdogo wa Msumbiji anyefanyia kazi zake Zanzibae Bw. Jorge Augusto Menezes.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio (wa pili kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana nao mara  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
[Picha na Ikulu.]

MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA TANZANIA KIPINDI CHA OKTOBA - DESEMBA 2016

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images