Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

NEWZ ALERT:Naibu waziri Tamisemi,Selemani Jafo anusurika kifo ajalini Mbeya

$
0
0

Gari la Naibu Waziri wa Tamisemi likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo.

Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.

Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.


Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.

Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguz alisema hakuumia popote ni wazima.

Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge
 
Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUWASILISHA MAONI KUHUSU MPANGO KAZI WA UENDESHAJI WA SERIKALI KWA UWAZI KABLA YA TAREHE 10 SEPT. 2016

$
0
0
 
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar es Salaam
5.9.2016

SERIKALI imeanza kupokea maoni na ushauri kutoka kwa asasi za kiraia, sekta binafsi na wananchi kuhusu maboresho ya rasimu wa mpango kazi wa kitaifa wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi wa Awamu ya tatu (2016/17 -2017/18).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Susan Mlawi Ilisema mwisho wa kuwasilisha maoni na ushauri huo ni tarehe 10 Septemba mwaka huu saa 9:30 alasiri.

Mlawi alisema mpango kazi huo utahusisha vipaumbele katika maeneo saba ambayo ni pamoja na upataji taarifa, takwimu huria, bajeti za wazi, uwazi kuhusu ardhi, uwazi kuhusu tasnia ya uziduaji, uwazi katika masuala ya afya, na mifumo ya utendaji kazi.

Aidha aliongeza kuwa maoni, ushauri na mapendekezo hayo yanaweza kuwasilisha Serikalini katika njia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo  tovuti rasmi ya wananchi (www.wananchi.go.tz), tovuti ya ogp (www.opengov.go.tz), government open data portal (www.opendata.go.tz).

 Mlawi alizitaja njia nyingine za kuwasilisha maoni hayo ni katika barua pepe ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (ps@utumishi.go.tz ) pamoja na njia ya barua kupitia sanduku la posta 2483 Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mlawi alisema rasimu ya mpango kazi inapatikana katika tovuti  ya wananchi (www.wananchi.go.tz), tovuti ya ogp (www.opengov.go.tz), government open data portal (www.opendata.go.tz), tovuti ya ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma (www.utumishi.go.tz), pamoja na mitandao ya kijamii ya facebook (utumishi week) na blog (http://utumishiweek.blogspot.com).

“Moja ya vigezo na matakwa ya utekelezaji wa mpango huu kwa nchi mwanachama ni kuandaa mpango kazi wa kitaifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za kiraia, sekta binafsi na wananchi, hivyo Serikali inawahimiza wadau kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao” alisema Mlawi.

Mpango wa uendeshaji wa Serikali kwa uwazi ni jitihada za kimataifa katika kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji huduma bora kwa wananchi. Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2012.

MTANDAO HATARI WA MAJAMBAZI WATATU WAKAMATWA,WAKUTWA NA SILAHA 23,RISASI 835,PINGU 48,REDIO CALL 12,BULLET PROOF 3 NA SARE ZA POLISI

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionesha moja ya kifaa walichokuwa wakitumia majambazi hao kuangalia wakati wa kufanya uhalifu,mbele ya waandishii wa habari (hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika na majambazi.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha bunduki  kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya bunduki zilivyokuwa zikitumika na majambazi sugu .
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam  na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya operesheni walioifanya na kuwakamata majambazi watatu.
 
 




BUNGENI MJINI DODOMA LEO KATIKA PICHA.

$
0
0
                 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye                (MB) akieleza mipango ya Serikali katika kuimarisha michezo nchini                   na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidiana na Serikali                                                                      kuwekeza katika Michezo. 


 Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiingia kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuendesha mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai Akiwaongoza Wabunge wa kuimba wimbo wa Taifa wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika ukumbi wa bunge wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma
 .Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Selemani Said Jafo (MB) akieleza mpango wa kuendelea kuimarisha hospitali za Serikali Nchini.
 Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akiwaeleza jambo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju na Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana,Wazee na Wenye Ulemavu wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Chemba Mhe. Juma Nkamia akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (MB), wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma. 
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

MKURUGENZI ILEJE HAJI MNASI ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA

$
0
0





Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.
baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi.


Na fredy mgunda,ileje

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.

Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa zidi yake.

“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo,kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na kuwaambia hayupo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu za wasimamizi”alisisitiza Mnasi.

Hata hivyo Mnasi aliwataka wasimamizi hao kuwa makini katika kufanyakazi hiyo na kama kuna jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.

“hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.“Nawaasa wasimamizi wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisema Mnasi.

Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichpo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.

Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.

Lakini mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.

TTCL yatoa huduma ya intaneti bure mkutano wa wanasayansi Dar

$
0
0
Mmoja wa maofisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kushoto) akimwelezea mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission. TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali. Mmoja wa maofisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kushoto) akimwelezea mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission. TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali. Timu ya mauzo ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ikiwa katika banda lao nje ya mkutano wa Tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission. TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' ulioandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission wakiwa katika banda la maonesho ya bidhaa mpya za TTCL Baadhi ya wateja (kushoto) wakipata huduma katika banda la Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) lililokuwa nje ya mkutano wa Tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission wakishiriki katika mkutano huo. TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' ulioandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission wakiwa katika banda la maonesho ya bidhaa mpya za TTCL wakipokea vipeperushi vya kampuni ya TTCL vinavyoelezea bidhaa na huduma zao mpya.

INTRODUCING NEW VIDEO: DAWA

JPM akagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam asubuhi hii


UNESCO KUTUMIA BILIONI 3 KUSAIDIA WATOTO WA KIKE KURUDI SHULE

$
0
0

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akizungumza kuhusu mradi ambao una malengo ya kurejesha watoto wa kike shuleni. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum akizungumzia sababu ya watoto wa kike kutokuwepo shuleni na jinsi ambavyo UNWOMEN watashiriki katika mradi wa kusaidia watoto wa kike kurudi shuleni.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watu Duniani (UNFPA), Maria Karadenizli akielezea takwimu za watoto wa kike ambao hawapo shuleni. 
 Mkuu wa Ofisi wa Shirika hilo la Maendeleo la (KOICA), Joosung Park akielezea ushiriki wa KOICA katika kusaidia mradi huo kukamilika sawa na mipango iliyowekwa.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi akizungumza kuhusu mipango ya serikali kukabiliana na tatizo la watoto wa kike kukatishwa masomo.

Na Mwandishi wetu

Katika kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa shuleni na hatimaye kumaliza masomo yao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetenga Dola 1,605,000 ambazo ni zaidi ya Bilioni 3 za Kitanzania ambayo zitatumika kuwasaidia watoto wa kike nchini kurejea katika shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo.

Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodriguez alisema kuwa Tanzania bado inaonekana kuwa na tatizo la watoto wa kike kuachishwa masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo kupata mimba za utoto na ndoa za utotoni hivyo kupitia mradi huo wataweza kuwasaidia watoto hao kuendelea na masomo.

Bi. Rodriguez alisema UNESCO imeamua kushirikiana na serikali ili kuwasaidia watoto wa kike kurejea masomoni na utafanyika kwa uhakika bila kumwacha mtoto yoyote na wana matumaini utaweza kusaidia watoto wa kike ambao wamekatishwa ndoto zao kimaisha kutokana na kukatishwa masomo.

“Tanzania kuna tatizo la watoto wa kike kusahaulika katika elimu na UNESCO imejitoa kushirikiana na serikali ya Tanzania ili kusaidia kukuza elimu ya watoto wa kike, “Baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuchangia ni pamoja na mambo ya asili, wamekuwa wakiwaozesha ndoa za utotoni na na watoto wengine wamekuwa wakipata mimba za utoto na hivyo kuacha masomo … mradi huu ni wa uhakika na utasaidia kukuza elimu,” alisema Bi. Rodriguez.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi alisema serikali inafahamu kuwepo kwa changamoto hizo na imekuwa ikifanya jitihada ili kuhakikisha kuwa matatizo ya watoto wa kike kukatishwa masomo yakimalizika.

Alisema kuwa makabila mengi ya Tanzania yamekuwa yakiwaona watoto wa kike kama watu wa kukaa nyumbani na kulea watoto lakini kama jamii ikiwa na mtizamo tofauti na kuwawezesha watoto wa kike basi wanaweza kusaidia nchi kukuza uchumi.

“Tumeona kazi ambayo wameifanya UNESCO hata machifu huko Ngorongoro wameanza kuelewa umuhimu wa watoto wa kike kuwa shuleni na kwa mpango huu matarajio ya serikali ni kumaliza changamoto iliyokuwepo awali,

“Serikali inafahamu kuna changamoto nyingi ambazo zinawakuta watoto wa kike na sio katika elimu pekee bali ni maeneo mengi … serikali inataka kukuza thamani ya elimu kwa watoto wa kike ambao wengi wao wanakatishwa kwa sababu ya mimba na ndoa za utotoni,” alisema Bi. Tarishi.

Nae Afisa Mradi wa Maswala ya Afya ya Uzazi kwa Vijana (UNFPA), Fatina Kiruviya alisema mradi una malengo ya kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa shuleni na kwa kuanza wanataraji kufanya mradi Ngorongoro, Pemba, Geita na Sengerema.

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WAKABIDHI MADAWATI KWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ,Bi Zainab Telack (aliye vaa ushungi) akiongozwa na Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila (kushoto kwake) wakati wakielekea uwanja wa Taifa wa mjini Kahama kwa ajili ya makabidhiano ya Madawati kutoka kampuni ya Acacia. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akihutubia wananchi katika uwanja wa Taifa Kahama wakati wa zoezi la Kukabidhiwa madawati kutoka kwa kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia, Bulyanhulu. Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,kutoka kushoto ni Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Elias Kasitila, Afisa Miradi Mzee Hamisi, Afisa Mahusiano ya Jamii William Bundala Chungu pamoja na Afisa Mahusiano ya Jamii David Magege, wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kabla ya zoezi la Kukabidhi Madawati . Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga wakichukua taarifa kwa ajili ya kuuabarisha umma juu ya tukio la makabidhiano ya Madawati.
Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia kwa ajili ya shule katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi,Zainab Telack akikata utepe kuashiria kupokea madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia.

Na Dixon Busagaga,Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amekabidhiwa madawati 2,000 yenye thamani ya Shilingi 240,800,000/= na Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Makabidhiano yamefanyika leo mjini Kahama.

Akimkabidhi madawati hayo Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, “hii ni awamu ya nne kwa mgodi wa Acacia Bulyanhulu kukabidhi madawati ndani ya mwaka huu katika kipindi ambacho taifa linaendelea kutekeleza kampeni ya kitaifa ya dawati kwa kila mwanafunzi iliyoagizwa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa lengo la kuboresha mazingira ya elimu nchini Tanzania.”

Ameongeza kuwa, “licha ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kuchangia madawati pia inachangia miradi mingine kwenye jamii lakini kwenye sekta ya elimu mgodi unashirikiana na jamii kuitekeleza miradi kama vile ujenzi na ukarabati wa nyumba, ofisi za walimu madarasa, maabara za sayansi na udhamini wa masomo kwa wanafunzi.”


Miradi ya Madawati 2016 kutoka Mgodi wa Acacia Bulyanhulu

Mei tulikabidhi madawati 380 kwa Halmashauri ya Msalala yenye thamani ya shilingi 28,500,000/=
Juni tulikabidhi madawati 1,000 kwa Halmshauri ya Msalala yenye thamani ya shilingi 88,500,000/=
Julai tulikabidhi madawati 500 kwa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita yenye thamani ya shilingi 37,500,000/=
Na hii leo Agosti tunakabidhi madawati 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga yenye thamani ya shilingi 240,800,000 /=
Aidha mwaka 2013 mgodi wa Acacia Bulyanhulu pia ulikabidhi dawati 1,389 kwa Wilaya ya Kahama

Mchango wa Miradi ya Madawati Kwenye Ajira
Katika kipindi cha miezi minne, utengenezaji wa madawati yenye thamani ya shilingi 393,800,000 umewezesha kutolewa kwa tenda za kutengeneza madawati kwa vikundi vya wajasiliamali wadogo na kuwawezesha vijana kujipatia ajira.

Wanafunzi ambao Wamenufaika
Mradi wa Madawati wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu umewaondelea adha jumla ya wanafunzi 5,040 ya kuketi sakafuni wakati wa kupokea masomo yao, baada ya kupata madawati 3,880 bora ya kudumu ambayo yametengenezwa kwa awamu nne hadi sasa.

Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu na Sekta ya Elimu Nchini

Mgodi wa Bulyanhulu unaamini kwamba elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii na unaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine wa maendeleo katika ngazi mbalimbali kuendeleza shughuli za uboreshaji wa elimu hapa nchini kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mgodi kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kampuni ya ACACIA, (ACACIA Maendeleo Fund).

Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi Zainab Telack amesema, “ Tukio hili la kukabidhiwa madawati ni tukio kubwa, nimefurahi sana na ninajua furaha ya watoto watakaotumia madawati haya itakuwa mara mbili yake, kwa hivyo kwa niaba ya Mkoa wa Shinyanga nawashukuru sana Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kwa kututengenezea madawati elfu mbili, mkoa wa Shinyanga ulikuwa na upungufu wa Dawati elfu 7000 lakini sasa kupitia mchango wa leo kutoka Bulyanhulu na wadau wengine sasa mkoa wetu unamaliza kabisa upungufu wa madawati.”

JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI YA JUHIWANGUMWA YATAMBULIWA KISHERIA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi akizungumza kwenye mkutano kabla ya kukabidhi rasmi hati mbili kwa pamoja ya kuitambua Jumuiya ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la serikali Na. 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika kijiji cha Utete Wilayani Rufiji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi akikabidhi rasmi hati kwa kiongozi wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA Bw. Shaban Dinongo ya kuitambua Jumuiya hiyo kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la serikali Na. 204. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika kijiji cha Utete Wilayani Rufiji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi akioneshwa ramani na Mratibu wa mradi Kitaifa wa KILORWEMP Bw. Pellage Kauzeni unaotenganisha kati ya eneo la hifadhi ya Jumuiya ya JUHIWANGUMWA na kijiji cha Utete Wilayani Rufiji kabla ya kukabidhi rasmi hati ya kuitambua Jumuiya hiyo kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la serikali Na. 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika kijiji cha Utete Wilayani Rufiji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi akiwa kwenye picha ya pamoja na na Kamati Endeshi ( Steering Committee) inayosimamia Mradi wa KILOWEMP katika kikao kilichofanyika jana Wilayani Rufiji . Kamati hiyo ndiyo iliyosaidia kuratibu mpaka kufikia hatua Serikali kuamua kukabidhi hati mbili kwa pamoja katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( katikati) akiwa kwenye kikao cha Kamati Endeshi ( Steering Committee) inayosimamia Mradi wa KILOWEMP cha kujadili miradi inayotekelezwa katika maeneo ya Wilaya ya Rufiji. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Ubelgiji ( BTC), Bw. Ton Snis na kushoto na upande wa kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori. Bw. Herman Keryaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi alipotembelea Kambi ya Watalii jana iitwayo Trackers inayopatikana katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kukabidhi rasmi hati mbili kwa pamoja ya kuitambua Jumuiya ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la serikali Na 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili.

Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi, imekabidhi rasmi hati ya ya kuitambua Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo la Jumuiya hiyo, Rufiji mkoani Pwani.

Pia, imekabidhi hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili hususani wanyamapori kwa kuwapa wananchi mamlaka ya kusimamia na kutumia rasilimali hizo kwa kuwa na uhifadhi na maendeleo endelevu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho katika maeneo yao, Taifa na Dunia kwa ujumla.

Akizungumza jana katika kijiji cha Utete wilayani Rufiji wakati akikabidhi hati hizo mbili kwa pamoja kwa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya JUHIWANGUMWA , Milanzi amewatahadhalisha Viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa na waadilifu wawazi hususani katika masuala ya pesa na mikataba watakayoingia na wawekezaji ili kuweza kuepuka migogoro isiyo ya lazima kutoka kwa Wananchi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika jumuiya nyingine.

‘’Tunataka fedha zitakazopatikana kupitia utalii wa Picha na utalii wa uwindaji ( photographic and tourist hunting) zitumike katika huduma za kijamii kwa kuboresha miundombinu, shule, hospitali na huduma nyinginezo za kijamii na sio pesa hizo zitumike kuwaneemesha watu wachache’’ alisema Milanzi

Aliongeza kuwa, Serikali kuu ( Wizara) itaendelea kuwasaidia pale inapohitajika kufanya hivyo katika masuala ya Uhifadhi, ‘’hatutaki kuwaingilia katika masuala yenu mfano katika masuala ya mapato na matumizi hivyo nawataka mshirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili msiweze kutumbukia kwenye migogoro ya namna hiyo’’ alisisitiza Milanzi

Aidha , Maj.Gen. Milanzi amewataka Wakuu wa Wilaya ya Rufiji, Malinyi, Kilombero na Ulanga ambazo ni Wilaya zinazounda jumuiya hiyo ya JUHIWANGUMWA yenye ukubwa wa kilomita za mraba 496.5 Kuhakikisha kuwa wanashirikiana na wananchi kuzuia mifugo isiingie ndani ya hifadhi kwa kuwa ni kinyume cha sheria ya uhifadhi kulisha mifugo hifadhini.

Milanzi alisema ‘’ Suala la kuingiza mifugo kwenye hifadhi lisiwe la kisiasa ni lazima kila mwananchi atambue kuingiza mifugo ndani ya hifadhi ya wanyamapori ni kuvunja sheria ya Uhifadhi hivyo atakayebainika lazima sheria ifuate mkondo wake’’

Pia, Milanzi alishukuru Serikali ya Ubelgiji kwa kusaidia kuanzishwa kwa hifadhi hiyo tangu mchakato ulipoanza mwaka 006 chini ya mradi wa ‘’ Eastern Selous Conservation Project’’ kwa juhudi wanazofanya kusaidia uhifadhi na hasa kwa kushirikisha wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Rufiji,Bw.Juma Njwaya alisema atahakikisha Hifadhi ya JUHIWANGUMWA inakuwa mfano katika masuala ya uwazi na uwajibakaji ili kuwawezesha wananchi kunufaika na rasilimali zao hususani wanyamapori.

Naye , Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Shabani Dihongo alisema wanajisikia fahari kwa hatua ambayo Serikali imefikia ya kuweza kupewa mamlaka kamili katika kuisimamia hifadhi yao

‘’Tutahakikisha tunafanya doria za kutosha na pia kila mwananchi atashirikishwa ili aweze kuona faida ya hifadhi hii ambayo tumeipigania kwa muda mrefu hatimaye leo tumeweza kupewa mamlaka kamili ya kuweza kuisimamia’’ alisema

Wizara ya Elimu yawaasa vijana kutumia elimu kujiajiri

$
0
0

Kaimu Kamishna wa Elimu Bw. Nicholaus Bureta akinyanyua juu nembo ya African Youth Leadership Transformation Summit (AYLTS) kuashiria uzinduzi wa nembo ya taasisi hiyo wakati wa hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Kamishna wa Elimu Bw. Nicholaus Bureta akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa Mkutano wa Vijana wa Afrika juu ya changamoto za ukosefu wa ajira na rushwa pamoja na suluhu za changamoto katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF ulioko Millenium Tower jijini Dar es Salaam.(Picha Na: Lilian Lundo – MAELEZO) .


Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bw. Nicholaus Bureta akizungumza wakati mkutano wa Vijana wa Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulijadili changamoto za ajira kwa vijana na suala la rushwa.
Washiriki wa Mkutano wa Vijana wa Afrika wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano wa Vijana wa Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulijadili changamoto za ajira kwa vijana na suala la rushwa

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imewaasa vijana waliomaliza shule kuacha kujibetweka bali watumie elimu waliyoipata kujitafutia ajira ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Nicholaus Bureta wakati wa ufunguzi wa mkutano wa vijana wa Afrika unaojadili changamoto zinazowakabili vijana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Bureta alisema kuwa Serikali inatoa elimu bora ili kuhakikisha vijana wanapata uwezo na maarifa yatakayowasaidia kujiajiri hata wasipopata nafasi za kuajiriwa katika taasisi na ofisi za umma pamoja na kuitumia elimu hiyo katika kupambana na vitendo vya rushwa.

“Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inatutaka tuwe na watanzania walioelimika na wenye mtazamo chanya ambao utahakikisha jamii yetu inabadilika kufikia uchumi wa kati hivyo vijana msikae kusubiri ajira bali mjifunze jinsi ya kujiajiri kutokana na elimu mliyoipata mashuleni”, alisema Bureta.

Kwa upande wake Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa (UN), Stellah Vuzo amewapongeza vijana hao kuamua kukusanyika kuchangia mawazo yao juu ya matatizo yanayowakabili kwani vijana wana nafasi kubwa ya kuhakikisha malengo mbalimbali yanatekelezeka.

Aidha, aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa umemteua balozi kijana ambaye anashughulikia ajira za vijana hivyo amewaomba vijana walioshiriki katika mkutano huo kuyafikisha mawazo hayo kwa balozi huyo ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.

Naye Mkuu wa Utafiti kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCB), Daniel Pundu alisema kuwa tatizo la rushwa haliwezi kuisha endapo vijana hawatashirikishwa hivyo amewasisitiza vijana kushirikiana na Serikali kuchukua hatua za kupambana na rushwa ili kuhakikisha rushwa inaondoka.

“Tunajua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa na ndio sababu tunawasisitiza kupambana na rushwa, kwa kulitambua hilo Serikali imeanzisha vilabu vya wapinga rushwa katika shule za sekondari na vyuo vikuu vikiwa na lengo la kuhakikisha vijana wanahusika kwenye mapambano hayo”, alisema Pundu.

TANZANITEONE YAJIPANGA KUENDELEA KUDHAMINI MICHEZO

$
0
0
Kampuni ya TanzaniteOne ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kuunga mkono michezo mbalimbali ili kuhakikisha wanamichezo wanapiga hatua.

Ofisa mahusiano wa kampuni hiyo Halfan Hayesh alisema japokuwa TanzaniteOne imedhamini michezo mingi hadi sasa, itaendelea kujitolea mara kwa mara kuwasaidia wanamichezo.

Alisema hivi karibuni walimdhamini mwanamichezo wa mbio za magari na pia wakazifadhili timu nne za soka za mkoa wa Manyara, kwa kuzipatia vifaa vya michezo ikiwemo suti na sare za michezo, mipira, na sare za waamuzi.

“Tunawaahidi wapenzi wa michezo kuwa tutaendelea kuwadhamini wanamichezo kwani hivi karibuni tulidhamini gari moja kwenye mbio za magari na kuwakilishwa na dereva Shanbhai na msaidizi Mwangi,” alisema Hayesh.

Alisema pia walishadhamini michezo mingine ya burudani ikiwemo ya miss kanda ya kaskazini, miss Arusha, Miss Manyara na Miss Mirerani na wataendelea na udhamini wa michezo tofauti ili kusaidia maeneo yote.

Alisema anatambua kupitia michezo kuna vipaji vingi vitagunduliwa hivyo kampuni hiyo itaendelea kuthamini suala hilo kwani michezo ni ajira, afya, upendeo, furaha, burudani na kujenga mshikamano na jamii inayowazunguka

NGOMA AFRICA BAND KUKINUKISHA MONACO JUMAMOSI 10SEPT 2016

$
0
0

"Kutumbuiza mabwanyenye wa umoja wa Yacht Club"
Na mbwa domobaya lao limeonekana

Bendi Maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni wanatarajiwa kutuo katika kisiwa cha Monaco kufanya showmaalumu kwa mwaliko wa Yacht Club ya Monaco,bendi hiyo itawatumbuizamabwanyeye hao katika kisiwa hiko cha kuponda raha siku ya jumamosi 10 September 2016 usiku hadi asubuhi.

Pia habari za uhakika zinasema kuwa
yule mbwa wao aina ya Bulldog aliyepotea amepatika na kurudishwa kwa mkuu wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja.
Usikose kupata muziki at www.ngoma-africa.com

au jiunge nao at www.facebook.com/ngomaafricaband
 Ebrahim Makunja aka Kamanda ras Makunja Kiongozi wa Ngoma Africa Band
 
 
 
 
 

OFISI YA MTAKWIMU MKUU YATOA TAARIFA YA BEI ZANZIBAR.

$
0
0

-Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Hamis Ahmada Shauri akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mfumuko wa Bei ambapo kwa mwezi wa Nane unaonesha kushuka.hapo katika ofisi yao Mwanakwereke Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Hamis Ahmada Shauri akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mfumuko wa Bei ambapo kwa mwezi wa Nane unaonesha kushuka.hapo katika ofisi yao Mwanakwereke Mjini Zanzibar.
Mwandishi mwandamizi wa I,T,V Farouk Karim akiuluza maswali kwa Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Hamis Ahmada Shauri kuhusiana na Mfumuko wa Bei ambapo kwa mwezi wa Nane unaonesha kushuka.hapo katika ofisi yao Mwanakwereke Mjini Zanzibar.
Meneja wa Uchumi katika Benki kuu Tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele lugobi akitolea ufafanuzi wa maswala katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mfumuko wa Bei ambapo kwa mwezi wa Nane unaonesha kushuka.hapo katika ofisi yao Mwanakwereke Mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Balozi Kijazi kuzindua Bonanza la SHIMIWI

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi


Na May Simba-MAELEZO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Bonanza la Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambalo litafanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shimiwi. Bw. Moshi Makuka, bonanza hilo litafanyika tarehe 10, Septemba mwaka huu katika uwanja wa Taifa (Uhuru) kuanzia saa 12:30 asubuhi.

“Bonanza litawashirikisha watumishi wote wa Serikali kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salam” alisema ndugu Makuka.

Aidha Bw. Makuka alisema kwamba bonanza hilo ni maandalizi ya michezo ya Shimiwi ambayo yamepangwa kufanyika Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 14 mpaka 27 Octoba mwaka huu.

Michezo ya mwaka huu ina lengo la kuunga mkono agizo la Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli la kuhamishia Makao Makuu yake mkoani Dodoma.

Mbali na hayo Bw. Makuka alisema michezo hiyo itawapa fursa watumishi wa umma kufahamu mazingira na kufanya maandalizi muhimu kwa ajili ya kuhamia mkoani humo

Bw. Makuka aliongeza kwamba walipanga michezo hiyo kuanza Octoba 14 ili kuadhimisha kumbukumbu muhimu ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere na kuenzi agizo lake la Serikali kuhamia Dodoma linalotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

“Michezo ya mwaka huu itaanza na ibada maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa na kumtakia afya njema Mhe. Rais Dkt. John Magufuli sanjari na kushiriki upandaji miti katika maeneo yatakayopendekezwa na Serikali ya mkoa”aliongezaBw. Makuka

Michezo ya Shimiwi hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwaunganisha wafanyakazi wote na kuimarisha afya zao ili kuepuka maradhi ya mara kwa mara.

SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI.

$
0
0
Wachimbaji Wadogo Wadogo


Na Daudi Manongi-MAELEZO-Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imepanga kuwapatia ruzuku wachimbaji wadogo wa madini ili kuongeza mchango wa madini katika pato la taifa kutoka asilimia 3.5 ya sasa hadi 10.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha Tunatekeleza kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Taifa(TBC).

“Sekta ya Madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa,lakini dhamira yetu ni kwamba wakati tunaingia kuwa nchi ya kipato cha kati madini yanapaswa kuchangia si chini ya asilimia kumi”

Aidha aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025, hivyo adhma ya Wizara yake ni kuongeza kasi ya pato linalotokana na sekta ya madini na 

Aliongeza kuwa ili mafanikio hayo yafikiwe Serikali imekusudia kupandisha hadhi ya wachimbaji wadogo ili wafikie ngazi ya kuwa wachimbaji wa kati na hivyo sekta hii itachangia pato la Taifa kwa kiasi kikubwa.

Aidha Waziri Muhongo alisema kuwa Serikali imepokea pesa mkopo wa Tsh. Bilioni 3 kutoka Benki ya Dunia na imepanga kutoa ruzuku ya vifaa kwa wachimbaji hao wakati wowote kuanzia sasa.

“Serikali imeshaanza kutoa maeneo na kufikia tarehe 15 septemba tutaanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji hao” alisema Prof. Muhongo.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuzuia utoroshaji wa madini nje ya nchi Profesa Muhongo alisema kuwa tangu mwaka 2012 Wizara yake iliweka madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vya ndege vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,Kilimanjaro na Mwanza na wakafanikiwa kukamata madini zaidi ya tani kumi.

MSAADA WA MATIBABU KWA MGONJWA DANIEL MANOTA.

$
0
0
Daniel Manota ni mhitimu wa mafunzo ya ualimu Ilonga Tc mwaka 2015.anasumbuliwa na maradhi ya FIGO tangu mwezi wa 10/2015, kwa sasa yuko Muhimbili hospitali, hari yake inazidi kuwa mbaya kwa kukosa pesa za kununua dawa, hivyo kama ndugu, jamaa na rafiki unaombwa kumchangia ili aweze kununua dawa zake zinazogharimu kiasi cha sh.milion 1 kwa wiki.

 Tunaomba tumuunge mkono kijana mwenzetu ambaye anapata maumivu makali. 
MUNGU HUMBARIKI ATOAYE KWA MOYO WA UKUNJUFU.
Tuma mchango kupitia namba hii, tuunganishe nguvu zetu kwa lengo la kuokoa maisha yake.
hii.
0659656970. NEEMA URASA
076818874 .DANIEL MANOTA.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6,2016. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwenye jengo la Utawala  la Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKANUSA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII

$
0
0

Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan

  
YAH: KUKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE

MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII



Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.



Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.



Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.



Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.



Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dar es Salaam
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images