Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

PATA HABARI ZA UHAKIKA ZA KUPATWA NA JUA KUPITIA TOVUTI ZA DAILYNEWS NA HABARILEO ONLINE KUTOKA RUJEWA

$
0
0
Kaa tayari kupata habari na matukio motomoto yatakayo kua yakijiri kutoka eneo la Rujewa, Wilayani Mbararali mkoani Mbeya ambako tukio kubwa la kihistoria Duniani linakwemda kushuhudiwa hapo kesho kwa JUA KUPATWA KIPETE.

Kampuni yako ya magazeti ya Serikali (TSN) ambao ni wachapaji magezti ya Daily News, Habarileo, Spotileo, Sunday News na Habaroleo Jumapili itakuwa ikikurushia matukio hayo kupitia  mitandao yake ya http://www.dailynews.co.tz na http://www.habarileo.co.tz 

HAPA KAZI TU.....HAKUNA KULAZA HABARI.

MIPAKA YA TANZANIA IKO SALAMA-WAZIRI DKT MWINYI

$
0
0
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa-Dkt Hussein Mwinyi 

Na: Lilian Lundo - MAELEZO
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia watanzania kwamba mipaka ya Tanzania ni salama.

Mhe. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) alipokuwa akieleza mikakati ya wizara hiyo katika kuhakikisha mipaka ya Tanzania iko salama.

“Nchi iko salama, mipaka ya nchi iko shwari, ziko changamoto chache za nchi zinazotuzunguka kuwepo katika machafuko mfano Burundi hivyo wananchi wake kukimbilia Tanzania,” alifafanua Mhe. Dkt. Mwinyi.

Amesema Tanzania sio kisiwa, imejiunga na jumuiya mbali mbali kama Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa hivyo kupitia Jumuiya hizo Tanzania hupata maelekezo ya kuwapokea wakimbizi kutoka nchi zenye machafuko.

Hata hivyo Mhe. Dkt. Mwinyi amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inahakikisha wakimbizi wanaoingia nchini wanafuata utaratibu unaotakiwa bila kuvunja sheria za nchi.

Pia ameeleza kuwa Tanzania inaendelea na mazungumzo ya amani na nchi ya Malawi juu ya mgogoro wa umiliki wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo mbili ili kupata ufumbuzi wa amani, ambapo mazungumzo hayo ya yanaongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa. 

Aidha, Mhe. Dkt. Mwinyi amesema kuwa kutokana na Wizara hiyo kufanya vizuri katika Ulinzi na Amani ya Nchi, Jumuiya ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa imeiomba nchi ya Tanzania kutoa Ulinzi wa wa Amani kwa nchi za Sudani, Kongo na Lebanoni kutokana na machuko yanayoendelea katika nchi hizo.

Vile vile ameeleza kuwa, ushiriki wa Jeshi la Tanzania katika nchi zenye machafuko kunaisaidia Jeshi hilo kupata mafunzo ya kivita kutokana na Tanzania kuwa ni nchi ya amani hivyo kufanya baadhi ya wanajeshi kutoshiriki mafunzo ya uhalisia ya kivita tangu wanapoajiriwa mpaka kustaafu.

Maandamano ni lazima yafuate sheria”- Kamanda Mstaafu Tibaigana

$
0
0
 Kamanda Mstaafu Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuanzia mwaka 2001 hadi 2008, Alfred Tibaigana amesema kuwa maandamano ya aina yoyote ni haki ya mwananchi na yanaruhusiwa kisheria lakini maandamano hayo lazima yafuate sheria na taratibu zilizobainishwa katika Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kamanda Tibaigana alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu akisisitiza kuwa kila jambo linalofanyika hapa duniani ni lazima liongozwe kwa Sheria na Kanuni.

Ingawa sheria nyingi za nchi mbalimbali duniani zinafanana lakini kila nchi imejiwekea sheria na kanuni za kufuata katika kufanya jambo lolote au katika kutafuta suluhu ya migogoro mbalimbali ikiwemo ya kisiasa, kidini, kijamii pamoja na ya kiuchumi.

Tanzania ni nchi mojawapo inayoongozwa kwa Sheria na Kanuni mbalimbali na ndio sababu hata katika Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa nchi imeeleza wazi kuwa hakuna aliye juu ya sheria wala hakuna anayeruhusiwa kuzivunja sheria hizo.

Anasema kuwa ili Taifa litengemae ni lazima wananchi wafuate Sheria na Kanuni zilizowekwa kwa sababu kutofuata sheria ni kosa kubwa.

Tibaigana anaongeza kuwa Sheria ni msumeno, ni vema kila pande ikaheshimu sheria na kanuni hasa kwa kutambua madaraka ya kila mmoja yanaanzia wapi na yanaishia wapi ili kuzuia tatizo la muingiliano wa majukumu ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa sheria na kanuni zilizowekwa na nchi husika.

Aidha, Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeelezea kwa undani pamoja na kuweka sheria na kanuni zinazohusu maandamano ya aina yoyote ,yawe ya kisiasa, kidini, kijamii au ya kiuchumi.

“Sheria inamtaka mwananchi au kundi la wananchi wanaohitaji kufanya maandamano kutoa taarifa kwa maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa eneo husika kabla ya masaa 48 ya kuanza kwa maandamano hayo ikieleza dhumuni la maandamano hayo, pia wahusika wanatakiwa wawe tayari kwa jibu lolote kutoka kwa mkuu huyo kwa kuwa chochote watakachojibiwa  lazima kiwe na sababu”, anasema Tibaigana.

Tibaigana anafafanua kuwa kama wahusika watakataliwa kufanya maandamano na hawatoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi kuna hatua mbili muhimu zinazotakiwa zifuatwe na sio wahusika kujiamulia kuandamana kilazima kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Hatua hizo muhimu zinazotakiwa kufuatwa ni kuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kumueleza kuwa hawajaridhika na sababu zilizotolewa na  Mkuu wa Polisi ili waziri naye kwa upande wake aamue kuruhusu au kukataza, endapo wahusika hawatoridhika na majibu ya waziri, watatakiwa kwenda Mahakamani ambapo ndipo uamuzi wa mwisho utatolewa.

Anasisitiza kuwa hakuna sheria inayotambua maandamano ya nchi nzima kufanyika kwa siku moja kwa sababu kila eneo lina Mkuu wa Polisi mwenye haki ya kukubali au kukataa ombi la kufanya maandamano kulingana na hali halisi ya eneo lake.

Kila jambo lina faida na hasara zake lakini kuna mambo ambayo faida huwa chache kuliko hasara, maandamano yana athari kubwa kiuchumi na kijamii kwa sababu maandamano yoyote ni lazima Jeshi la Polisi liwajibike katika kuongoza na kulinda maandamano hayo, hivyo kupelekea wanajeshi wengi kusitisha kazi zingine kwa ajili ya kuzuia vurugu zisitokee.

Athari zingine ni kusitishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za usafiri , kufungwa kwa maduka na masoko pamoja na athari zitokanazo na vurugu zinazoweza kutokea kwa sababu ya maandamano hayo.

Aidha, Kamanda Tibaigana anatoa ushauri kwa vyama vya siasa vinavyotumia maandamano kama njia ya kupata usuluhishi wa migogoro yao kufata sheria na kanuni zilizowekwa kwani maandamano mengi ya aina hiyo yanasababishwa na kutaka nafasi ya kuongoza nchi kwahiyo kama chama hakitoheshimu sheria za nchi lazima kiwe mfano mbaya kwa wananchi watakaowaongoza.

Watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa maandamano sio njia pekee ya kusuluhisha migogoro yao bali njia bora ni kukaa chini na kuelewana kwa njia ya mazungumzo, huo ndio utamaduni wa nchi yetu kwani hali hiyo ya kutii sheria na kanuni umepelekea nchi kuendelea kuwa na amani wakati wote.

“Sisi ndio walinzi wa amani hiyo kwahiyo yatupasa kuzitii sheria zetu ili kuitunza amani yetu daima”.

Rais Magufuli ni Rais aliyesubiriwa tangu kuanza kwa uhuru-Cheyo

$
0
0
 Mzee Cheyo.
 
Na: Lilian Lundo - MAELEZO.

Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amesema kuwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Rais aliyesubiriwa kwa muda mrefu tangu kuanza kwa Uhuru.

Cheyo ameyasema hayo jana alipokuwa akielezea juu ya utendaji wa Rais Magufuli tangu ameingia madarakani Novemba, 2015.

“Utendaji wa Rais Magufuli umewashtusha watu wengi kwani hawakutegemea kwa muda mfupi aliokuwa madarakani kama angeweza kuchukua hatua kubwa kama vile kupambana na mafisadi, jambo ambalo limekuwa likiongelewa na viongozi waliopita lakini kulikuwa hakuna matunda ya moja kwa moja,” alifafanua Cheyo.

Ameendelea kwa kusema kuwa Rais Magufuli amekuwa na adhima ya kupambana na Mafisadi na kutatua kero za Taifa tangu akiwa kwenye kampeni huku akisimamia kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

Vile vile Cheyo amesema kuwa kero ambazo amekuwa akizitatua Rais Magufuli zikiwemo ufisadi, uchumi tegemezi, mapato madogo na ukosefu wa vifaa mahospitalini ni kero ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na kambi ya upinzani kwa muda mrefu.

Hivyo kuingia kwa Rais Magufuli madarakani kumeleta utatuzi mkubwa kwa kero hizo ambazo zimekosa utatuzi kwa muda mrefu kutokana na viongozi waliopita kutozichukulia uzito mfano Rais Magufuli alivyoweza kutatua tatizo la vitanda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kipindi kifupi ambapo hivi sasa hakuna mgonjwa anayelala nchini katika hospitali hiyo.

Akielezea suala la ufisadi nchini, Cheyo amesema kuwa ufisadi ni ugonjwa wa muda mrefu ambao umepoteza fedha nyingi za nchi kutokana na mikataba mibovu iliyokuwa ikisainiwa na viongozi wa juu.

Aidha amempongeza Mhe. Rais kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na kuona tatizo hilo lishughulikiwe kisheria na kwa njia maalum ili kukomesha ufisadi nchini.

Cheyo amewataka watanzania kugeuza mawazo yao na kuchukia rushwa kwa kukataa kupokea na kutoa rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na inarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

WIZARA YA AFYA KUFANYA UZINDUZI WA KONDOMU MPYA MKOANI MWANZA.

$
0
0
Baada ya juzi Agost 30,2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuzindua aina mpya ya Kondomu iitwayo Zana Kondomu mkoani Mbeya, Uzinduzi kama huo unatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza Septemba 05,mwaka huu.

Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni (pichani), jana alisema mkoa wa Mwanza unatarajia kupokea ugeni kutoka wizara hiyo ambao utajumuisha wataalamu mbalimbali wa afya watakaokuwa wakitoa semina na elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia vyombo vya habari, wakielezea juu ya uzinduzi wa kondomu hiyo.

Alisema miongoni mwa dhumuni la kuzindua aina hiyo mpya ya Kondomu, ni kusaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukwimwi ambapo Wizara itakuwa ikigawa bure kondomu hizo zenye ubora kwa wananchi, kote nchini.
Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni
Baadhi ya Wanahabari mkoani Mwanza, wakimsikiliza Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza.

TANZANIA YATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA ASASI MUHIMU NA NYETI YA SIASA,ULINZI NA USALAMA SADC

$
0
0
Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali umemalizika katika mjini Mbabane Swaziland ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi muhimu na nyeti ya Siasa, Ulinzi na USalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC- (SADC Organ On Politisc, Defence and Security Cooperation) ambapo nchi ya Angola imeteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa asasi hiyo.

Jukumu kubwa la asasi hiyo litakuwa ni kuangalia masuala yote yanahusiana na Siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Lesotho.

Akizungumzia mambo muhimu yaliyojiri kwenye Mkutano huo wa 36 wa SADC mjini Mbabane - Swaziland, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia  Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na amehimiza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa nchi wanachama wa SADC kwa sasa zinatakiwa kuongeza juhudi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka kama hatua ya kujenga ustawi bora wa wananchi wa kanda hiyo.

Kuhusu Mpango wa Mfalme wa Swaziland wa III wa kujenga Chuo Kikuu cha SADC nchini mwake kabla ya mkutano ujao wa SADC hapo mwakani chuo ambacho kwa kuanzia kitatoa ufadhili wa masomo ya Sayansi,Ugunduzi na Utafiti kwa wanafunzi wanaotoka kwenye nchi wanachama wa SADC, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema mpango huo ni mzuri na utasaidia kutoa wataalamu wengi hasa wanasayansi katika ukanda wa SADC na serikali ya Tanzania inaunga mkono mkakati huo.

Kuhusu Tanzania kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi za SADC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga amesema Tanzania itahudumu katika asasi hiyo kwa mwaka MMOJA na anaimani kuwa changamoto za kisiasa zilizopo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lesotho zipatiwa ufumbuzi.

Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC pia umeiteua nchi ya Swaziland kuwa mwenyekiti wa SADC na Jamhuri ya Afrika Kusini imeteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC.

Katika mkutano huo wakuu wa nchi na serikali wametia saini rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali ya jumuiya hiyo ikiwemo mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbabane
Swaziland
1-Sep-16

TAZAMA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA LEO HUKO RUJEWA MKOANI MBEYA LEO,RC WA MBEYA NA SONGWE WAONGOZA WANANCHI KUSHUHUDIA TUKIO HILO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Kanali Mstaafu Chiku Galawa pamoja na Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) , Pascal Shelutete wakiangalia tukio la kupatwa kwa Jua kutumia vifaa maalum muda huu, katika eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya. Tukio hilo limeonekana vizuri zaidi katika eneo hilo kuliko maeneo mengine nchini. Watu kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia wako katika eneo hilo, kushuhudia kwa uzuri tukio la kupatwa kwa Jua.
Hivi ndiyo jua lilivyoanza kuonekana baada ya kupatwa, Hapo ni eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya, eneo lililotengwa kwa ajili ya kutizamia tukio hilo kwa uzuri zaidi.
Na hata kina sie huku Mjini Dar es salaam tumelishuhudia tukio, japo tulitandwa na wingu zito. ila si haba tumebahatika kuiona kwa namna hii.
 
 Baadhi ya wananchi wakiendelea kushuhudia kupatwa kwa jua
 Muonekano wa kupatwa kwa jua huko Rujewa leo
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amoss Makala akizungumza na wakazi wa mji wa Rujewa waliojitokeza kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua mkoani Mbeya
 Jua jinsi linavyoonekana kwa kutumia karatasi maalumu ambayo unaweza kuona jua katika mandhari mbalimbali.
 Kikundi cha ngoma wakitumbuiza katika eneo ambapo kupatwa kwa jua kumetokea na kuonekana kwa kutumia kifaa maalumu Rujewa Mkoani Mbeya.
Biashara zikiendela katika eneo la Rujewa Mkoani Mbeya kama ijulikanavyo Mkoa wa Mbeya kwa Kulima Mpunga hapo biashara ya Mchele ikiendelea.
Mamalishe nao hawakusita kuona fursa iliyojitokeza katika eneo Lujewa Mkoani Mbeya kuhudumia wananchi wanaoenda kutazama kupatwa kwa jua.
Mwananchi akijiandaa kuangalia jua kwa kutumia karatasi maalumu.
Picha na Fadhili Atick na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MAADHIMISHO YA 14 SIKU YA WAHANDISI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Meza Kuu,Pichani tatu kushoto ni Rais Dkt John Pombe Magufuli akishiriki kama Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 14 ya Wahandisi,yaliyofanyika leo Mlimani City,jijini Dar, 
Baadhi ya Wahandisi wakiwa kwenye maadhimisho ya 14 ya siku ya Wahandisi, kwenye ukumbi wa MlimaniCity jijini Dar es Salaam asubuhi hii.Rais John Pombe Magufulindiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayoambao kauli mbiu yake ni "Kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda"

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA RIPOTI YA HALI YA HEWA BARANI AFRICA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Kutoka kwa Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Neville Isdell na Katikati ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa ICF, Ris Mstaafu, Benjamin Mkapa katika hafla ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Neville Isdell na Katikati ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa ICF, Ris Mstaafu, Benjamin Mkapa katika hafla ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016.
Picha ya pamoja.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Afrika wajiulize wanaweza kuchangia kitu gani katika kuboresha maisha ya mamilioni ya wakazi wa bara hilo.

Ametoa kauli hiyo jana usiku (Alhamisi, Agosti 31, 2016) wakati akizungumza na wawakilishi wa taasisi za kimataifa waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya Taasisi ya Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji barani Afrika (ICF) uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alisema taasisi hiyo imesaidia kukuza uwekezaji kupitia miradi katika nchi mbalimbali za Afrika kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi, usajili wa biashara za wajasiriamali na upatikanaji wa leseni za biashara.

“Kutokana na kazi inayofanywa na taasisi hii, hali ya uwekezaji katika nchi nyingi imeimarika na bara la Afrika limekuwa mbia kwa wawekezaji kutokana na ushirikiano baina ya Serikali za nchi husika na sekta binafsi. Uchumi wa nyingi za Afrika umeimarika kuliko hapo awali,” alisema.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema zaidi ya wajasiriamali 500 kutoka Tanzania walipatiwa mafunzo kwa ushirikiano baina ya ICF, Serikali na ESAURP ili kuwajengea uwezo waweze kufanya biashara zao kwa tija zaidi. “Mafunzo hayo yaliwalenga wajasiriamali wadogo na wa kati ambao wanajihusisha na uvuvi, biashara za rejereja na jumla kutoka mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam”.

“Kupitia mafunzo hayo, wajasiriamali hao waliweza kusajili biashara, kurasimisha biashara zao, kuongeza mitaji na kujua namna ya kutunza taarifa za biashara zao,” alisema.

Mapema, Mwenyekiti Mwenza wa taasisi hiyo ambaye pia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin Mkapa alisema kuna haja ya wananchi kubadili mitazamo yao juu ya sekta binafsi kwani nayo ni muhimu katika ujenzi wa uchumi kwa nchi yoyote ile.

“Watu wengi wanahisi kwamba wawekezaji ni wabaya. Hii si kweli. Tunapaswa kujenga mazingira ya kuwakubali kwa sababu wanakuja na mitaji yao na wao wanawakilisha michango kutoka kwa mamilioni ya wafanyakazi kutoka kwenye nchi zao. Hatupaswi kuwaona kwamba ni maadui,” alisema.


Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa kukubali kuiruhusu taasisi hiyo ya ICF iweke makao yake makuu hapa nchini wakati ilikuwa imeshakataliwa kufanya hivyo katika nchi nyingi ambako ilipeleka maombi yake.

Aliwataka viongozi mbalimbali watumie uzoefu uliowekezwa na taasisi hiyo kwenye uboreshaji wa mifumo ya mahakama na ukusanyaji kodi, utoaji wa leseni, urasmishaji wa biashara za wajasiriamali wadogo.

“Tunayo maeneo mengi ambayo tumefanya vizuri iwe ni katika TEHAMA, miundombinu, mahakama au mambo ya forodha. Uamuzi ni wenu juu ya jambo lipi muanze nalo katika kuboresha huduma ili kuharakisha maendeleo ya bara hili,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, SEPTEMBA MOSI, 2016

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KUWAIT AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA UMOJA WA MAKAMPUNI YA FOUAD ALGHANIM

$
0
0



Mhe. Dkt. Mahadhi J. Maalim, akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Fouad Alghanim, Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim. Kushoto kwa Mhe. Dkt. Mahadhi ni Bw. Sami M. Al-Farhan, Makamu Wa Rais wa Umoja huo wa Makampuni ya Fouad Alghani anayeshughulikia masuala ya uwekezaji wa Kimataifa na mwanzo upande wa kulia ni Bw. Iman Njalikai, Mkuu wa Masuala ya Utawala katika Ubalozi wa Tanzania Kuwait.
Katika picha Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akiwa katika mazungumzo na Bw. Fouad Alghanim, Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim. 
 
 Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim, unajumuisha zaidi ya Makampuni ishirini ambayo yanajihusisha na masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji, nishati, mafuta na gesi, usafirishaji, miundombinu, biashara ya magari, masuala ya anga na ndege, mawasiliano, ujenzi wa makazi ya kisasa, masuala ya ulinzi, utalii na afya.

Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti huyo alieleza matarajio yake juu ya ziara atakayofanya hivi karibuni kutembelea Tanzania ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana. Mwenyekiti huyo alimfahamisha mheshimiwa Balozi kuwa licha ya kutokuwa na shughuli za kiuchumi nchini Tanzania, Umoja huo unatekelezaji miradi mbalimbali katika nchi za jirani za Uganda, Rwanda na kwingineko. Aliongeza kuwa, Umoja huo una nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali Tanzania hususan miundombinu.

Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Maalim, alimshukuru Mwenyekiti huyo kwa kuonesha nia ya kutembelea Tanzania na kuona fursa mbalimbali za uwekezaji. Vilevile, alimshauri kuangalia namna ambavyo Umoja huo unaweza kushirikiana na Serikali pamoja na Sekta binafsi hususan katika suala la ujenzi wa makazi ya kisasa katika Makao Makuu mapya ya Serikali mjini Dodoma.

Aidha, Mhe. Dkt. Maalim, alipongeza kitendo cha Mwenyekiti huyo kuamua kufanya ziara Tanzania na kumuahidi kuwa Ubalozi wa Tanzania Kuwait upo tayari kutoa ushirikiano utakaohitajika ikiwepo kuwapatia taarifa muhimu kuhusu uwekezaji nchini Tanzania, pamoja kuwakutanisha na wadau muhimu katoka sekta binafsi na ile ya umma.

TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

$
0
0

USAJILI: FIFA YALETA WARAKA MPYA

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukisema mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.

FIFA limeleta mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine lakini kabla ya kufanya hivyo utasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji huyo na shabaha kuu ni kurahisisha mawasiliano ya TMS Managers nchi nzima, klabu na mashirikisho mbalimbali duniani.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


MALINZI AMPONGEZA RAIS MPYA WA EFA

Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongeza kwa Hani Abou-Reida kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri (EFA) katika uchaguzu mkuu uliofanyika juzi Jumanne Agosti 30, 2016 jijini Cairo.

Katika salamu zake, Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa Hani Abou-Reida katika wadhifa huo ni kilelelezo cha familia ya mpira wa miguu ya Misri kuona umuhimu wake katika kutumikia shirikishi hilo sambamba na kuwa mwakilishi FIFA.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

MAKOCHA KILIMANJARO QUEENS WATAJWA

Shirikisho la Mpira Miguu Tanzania (TFF) limemteua Sebastian Nkoma kuwa Kocha Mkuu wa timu ya soka taifa ya wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens ambayo kwa mara ya kwanza inakwenda kushiriki mashindano ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.

Uteuzi huo wa Nkoma unakwenda sambamba na wasaidizi wake, ambao ni Hilda Masanche na Edna Lema wakati Meneja wa timu hiyo, Furaha Francis. Mtunza vifaa ni Esther Chabruma maarufu kwa jina la Lunyamila.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


SEMINA YA KLABU ZA WANAWAKE LIGI KUU

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa semina elekezi kwa klabu za Ligi Kuu za wanawake inayotarajiwa kuanza baadaye mwaka huu.

Semina hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, itafanyika Jumamosi Septemba 3, 2016 kwenye Ukumbi wa Hosteli za TFF zilizopo ofisi za Makao Makuu ya shirikisho hilo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, makutano ya barabara za Shaurimoyo na Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

YONDAN ABAKI, STARS IKIIFUATA NIGERIA

Sentahafu wa Young Africans, Kelvin Yondani si miongoni mwa wachezaji 18 walioondoka leo Septemba mosi, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Taarifa ambazo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipata ni kwamba Yondani ana matatizo ya kifamilia ambako hajayaweka sawa hadi timu hiyo inaondoka kwenda Nigeria na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa hajajaza nafasi hiyo.

TFF YATEUA KOCHA WA KILIMANJARO QUEENS

$
0
0
Kocha Wa timu ya Kilimanjaro Queens Sebastian Nkoma alipotambulishwa leo na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa wanawake Amina Kaluma (kulia)

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Mpira Miguu Tanzania (TFF) limemteua Sebastian Nkoma kuwa Kocha Mkuu wa timu ya soka taifa ya wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens ambayo kwa mara ya kwanza inakwenda kushiriki mashindano ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.

Uteuzi huo wa Nkoma unakwenda sambamba na wasaidizi wake, ambao ni Hilda Masanche na Edna Lema wakati Meneja wa timu hiyo, Furaha Francis. Mtunza vifaa ni Esther Chabruma maarufu kwa jina la Lunyamila.

Kabla ya uteuzi huo, Nkoma alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ambayo kwa sasa ipo kambi ndogo ya kwenye hosteli za TFF kujiandaa na kambi kubwa itakayofanyika Shelisheli kabla ya kuivaa Congo – Brazzaville kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo. Fainali hizo zitapigwa Aprili mwakani, nchini Madagascar.

Kilimanjaro Queens inatarajiwa kuanza mazoezi ya leo, Septemba mosi, 2016 ambako wachezaji watakuwa wanakwenda mazoezini Uwanja wa Karume, Ilala  na kurudi nyumbani hadi Jumapili ambako Jumatatu itasafiri kwenda Uganda kupitia Bukoba mkoani Kagera itakakoweka kambi tena ya siku nne.

Kwa mujibu wa CECAFA, michuano hiyo itafanyika jijini Jinja na Tanzania ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango vya Mpira wa Miguu kwa nchi za Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa pamoja na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na mwenyeji Uganda.

Tanzania itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, 2016 kabla ya kucheza na Ethiopia Septemba 16, 2016. Rwanda na Ethiopia zitacheza Septemba 14, 2016 wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.

Kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya zitakazocheza Septemba 13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza na Uganda. Septemba 15, Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.

Nusu fainali itafanyika Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na nne.

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA WAHANDISI, ATEMBELEA KIKOSI CHA ANGA MAJUMBA SITA UKONGA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Septemba 1, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya  pamoja na Wanajeshi wa JWTZ Kikosi cha Anga 603 KJ Majumba Sita Ukonga jijini Dar es salaam  alikotembelea kuwapongeza kwa kusherehekea miaka 52 ya Jeshi la Wananchi leo Septemba 1, 2016

Rais Magufuli awataka wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu

Na Sheila Simba-MAELEZO 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka  wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.

Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.

“mkiamua nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.

Aidha amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.

“Tumemsikia waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli

Akimkaribisha rais Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.

“serikali inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.

Aidha Mhandisi Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini.akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.

“Katika kuhakikisha miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda

SERIKALI YA RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI IENDELEE NA MIKAKATI YAKE YA KUJENGA NCHI KWA SASA-UVCCM

$
0
0
Pichani kulia ni Kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Taifa ,Shaka Hamdu Shaka akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma,shoto ni kaimu katibu wa hamasa,sera,utafiti na mawasiliano wa UVCCM Taifa Chief Silvester Yeredi

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema  hakuna mazungumzo, majadiliano wala mijadala inayostahili kufanyika kati ya Serikali ya CCM na Chadema na kuiomba Serikali ya Rais Dk John Magufuli iendelee na mikakati yake ya kisera ili kuimarisha maendeleo ya kiuchumi.

Pia umoja huo  umeeleza kuwa  dunia inajua, ulimwengu unaaelewa na Chadema wanafahamu kuwa Tanzania hakuna mgogoro wa kisasa zaidi ya serikali kupigania mabadiliko, nchi kuwa ya viwanda na kutokomeza  maadui umasikini, ujinga na maradhi.

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mluu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Mkoani hapa.

Shaka alisema UVCCM ilijua, ilielewa na kutambua mapema  Chadema na viongozi wake walikuwa wakifanya maigizo katika  siasa, hawakuwa na ubavu wala jeuri ya kuandamana kwa madai aliyoyaita ni ya  kipuuzi ambayo hayana msingi kwa mustakabali wa nchi na maendeleo yake.

Alisema viongozi na wafuasi wa Chadema  walishindwa kuandamana Septemba Mosi, hawataweza na wala hawatajaribu kufanya hivyo  Oktoba Mosi kwa sababu wanachotaka kukifanya ni utoto wa kisiasa  baada ya kushindwa kubuni mkakati wa kukiendesha chama chao ili kiaminike na kukubalika.

"Tunazo habari  wabunge wa Chadema wamechachamaa na kumbana Mbowe  kwa  hoja wakitaka kurudi bungeni ili kushiriki vikao kwa kuwa hawaeleweki kwa wapiga kura wao majimboni lakini pia wanakabaliwa na 'waya mkali',   hawaoni kwa nini wasishiriki vikao vya Bunge huku baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho wakiwa na utajiri na wengine  wafanyabiashara,"alisema Shaka.

"Cha ajabu hata na wale wazee tuliokuwa tukiwaheshimu bila soni wanashiriki kuudanganya ulimwengu wakitoa madai ati kuna mgogoro wa kisiasa  unaohitaji suluhu, yafanyike mazungumzo na majadiliano,"alisema Shaka.

Alisema UVCCM imeshangazwa na madai ya Chadema na kusema  kwamba chama hicho na viongozi wake wamekuwa wakikutana na viongozi wa madhehebu ya dini na mashirika ya kiraia, kisheria  yaliyowataka ati wasiteshe maandamano kwa muda hadi Oktoba Mosi mwaka huu.

"Tumekuwa tukijiuliza bila kupata majawabu ya kina pale Mbowe na Chadema wanaposema wameshauriwa na viongozi wa madhhebu ya dini na taasisi  zingine. Je hapo awali pia walishirikiana na viongozi hao  kupanga na kuitisha maandamano yenye lengo la kumdhihaki Rais na kumwita dikteta?" alihoji Kiongozi huyo wa Vijana.

Hata hivyo, alisema si jambo linaloingia akilini na mtu alazimike kuyamini maneno ya Chadema kama kweli viongozi wa dini na taasisi zilizotajwa, walihusika na kushiriki mpango wa uitishji maandamano ya vurugu na sasa  wahusike tena kuwakataza Chadema wasifanye  maandamano.

"UVCCM,  wananchi wema, wapenda amani na utulivu, viongozi wa mashirika ya kiraia na madhehebu ya dini, hatuwezi kusimama  hadharani kuitbitishia dunia kama Tanzania kuna mgogoro wa kisiasa  unaohitaji yafanyike mazungumzo, majadiliano hadi kufikia mapatano," alieleza Shaka.

Alisema ulimwengu mzima  unafahamu,  mashirika na jumuia za kimataifa nazo zinaelewa  kwamba katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, wananchi walitekeleza wajibu wao wa kikatiba  na  kupitia demokrasia ya uchaguzi  walimchagua kwa kura Rais Dk. Magufuli kuwa Rais wao na matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa na chombo chenye dhamana ya kisheria na kikatiba ambacho ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Shaka, alisisitiza kuwa wananchi wote, mashrika ya Kimataifa na ulimwengu unaelewa  Dk. Magufuli baada ya kuchaguliwa, serikali yake bila kupoteza wakati imekuwa ikihimiza kwa nguvu zote mpango wa uwajibikaji,  utendaji wenye  ufanisi, nidhamu, huku serikali yake ikipiga vita ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma  pia   ikikusanya kodi na kuongeza mapato ya taifa.

"Chadema na UKUTA wao  wanachotaka ni  siasa za mitaani na maandamano haramu. Wanataka kukithiri kwa malumbano na mabishano yasiyo na maana badala ya wakulima, wafanyakazi, wavuvi na wafugaji wafanye kazi kwa bidii, kujituma ili wazalishe mali na kujienga uchumi na kimaendeleo alisema,"alisema Shaka .

Shaka alieleza kuwa haipendezi na  haiwapi hadhi au heshima mbele ya jamii watu  wanaojiita viongozi wa kisiasa wa Chadema kuwa na uhodari wa kutunga uongo, wakauamini, kuueneza na kuutetea kwa misuli ya unafiki na upotoshaji.

"UVCCM tunawaasa viongozi wa Chadema waache mara moja  siasa za utoto na tabia ya kuwatia hofu wananchi, wasiwafanye waishi kwa wasiwasi kwa siasa zao uchwara ambazo zimekosa afya  na wala haiwapi heko au heshima mbele ya dunia,"alisema Shaka.

LIJUE JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA MAJUKUMU YAKE KATIKA KUTEKELEZA DHIMA YA KUOKOA MAISHA NA MALI ILI KUKUZA USALAMA KWA UMMA

$
0
0
Kamanda wa mkoa wa Njombe wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkaguzi Joseph Mwasabeja akitoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Njombe.
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakifanya ukaguzi wa mifumo ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto katika moja ya majengo marefu hapa jijini.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa ameambatana na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo wakikagua moja ya kisima (Fire Hydrant) kinachoweza kutoa msaada wa maji katika matukio pindi magari ya zimamoto yanapoishiwa maji.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionyesha jinsi ya uzimaji moto na kiasi cha maji yanayotumika (Pressure) wakati wa matukio.

(PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE AND RESCUE FORCE ACT”. Majukumu makubwa ya Jeshi ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengineyo.

HUDUMA YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI INATOLEWA.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii. Hivyo basi mtu yeyote anastahili kupata huduma hiyo kwa kupiga namba ya simu 114. Pia kuna huduma nyingine zitolewazo na Idara.

HUDUMA ZITOLEWAZO NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajukumu kubwa la kutoa huduma kwa jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Kuokoa maisha ya watu na mali zao, Kuzima moto, Kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga moto, Kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto, Kusoma ramani za majengo na kutoa ushauri, Kutoa huduma ya kwanza katika majanga na ajali barabarani, Kutoa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto, Kufanya uchunguzi kwenye majanga ya moto na Kutoa huduma za kibinadamu.

KUFIKA KWENYE TUKIO BILA YA VITENDEA KAZI (MAJI)

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wote huwa limejiandaa kwa magari yake kuwa na vitendea kazi vya kuzimia moto na kufanyia maokozi pia magari huwa yamejazwa maji wakati wote yanapokuwa vituoni yakisubiri matukio. Changamoto iliyopo ni wananchi wengi kuwa na dhana kuwa magari ya Zimamoto huenda kwenye matukio bila maji.

AINA YA GARI LA ZIMAMOTO, VIFAA, UWEZO WA KUBEBA MAJI (UJAZO), NA JINSI YA UFANYAJI KAZI

Gari la Zimamoto linapofika kwenye tukio hufanya kazi kama mtambo wa kuzimamoto, magari hayo yanamatanki ya maji yenye ujazo kuanzia lita 1,500 hadi lita 7,000 (kuna moja linabeba lita 16,000) ili maji hayo yatoke kwa nguvu na kuweza kuzimamoto, magari ya Zimamoto yamefungwa pampu zenye uwezo wakusukuma lita 2,000 hadi lita 6,000 kwa dakika.

Kwa kawaida tunapofika kwenye tukio hutumia mipira yenye kipenyo cha milimeta 70 na kufunga kifaa cha kumwagia maji (branch pipe) chenye kipenyo cha milimeta 20 na pampu husukuma maji kwa nguvu ya bar 7, kwa vipimo hivyo huwa tunamwaga lita 1,000 kwa dakika kwa njia moja ya kutolea maji hivyo kwa gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha ndani ya dakika saba, kwa kawaida tunatumia njia mbili za kutolea maji hivyo huwa tunamwaga lita 2,000 kwa dakika, na gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha baada ya dakika 3½ nasisi hulazimika kuondoka eneo la tukio kwenda kutafuta maji.

Huku nyuma wanaweza kuja waandishi wa habari na kuwauliza wananchi mbona moto unawakana Zimamoto hawapo? Wananchi hujibu kuwa wamekuja lakini baada ya muda mfupi wameondoka na kusema kuwa wanakwenda kuchukua maji, hapo ndipo dhana ya Zimamoto wamekuja kuangalia kwanza ukubwa wa moto na sasa ndio wamekwenda kuchukua maji hujengeka. Ki uhalisia si kweli kuwa magari ya Zimamoto hufika kwenye tukio bila ya maji.

Maji yanayobebwa na magari ya Zimamoto husaidia kuanzia kazi, kabla maji ya kwenye gari kwisha gari la Zimamoto hutegemea kupata maji kutoka kwenye vituo maalum vya maji kwa ajili ya Zimamoto (Fire Hydrants) ambazo katika miji yetu mingi huwa hazifanyi kazi kutokana na sababu zifuatazo:-
Kutokuwa na maji
Kufukiwa na vifusi au mchanga au kufunikwa kutokana na ukarabati wa mitaa au barabara.
Kung’olewa na kubadilishwa matumizi.
Kung’olewa kwa alama za utambulisho (H sign)
Kuibiwa kwa mifuniko kutokana na biashara ya chuma cha kavu.
Miradi mingi ya maji katika miji kutoshirikisha ufungwaji wa vituo vya maji (Fire Hydrants).

MBUNGE MUFINDI KASKAZINI MAHMOUD MGIMWA ATOA MSAADA WA AMBULACE JIMBONI KWAKE

$
0
0






MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi huku wananchi wakiwa kwa pembeni

MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akifurahia jambo na viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa na viongozi wa wilaya ya mufindi wakiangalia muonekano wa wa gari hilo la kubebea wagonjwa
na hii ndio sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa alilokabizi mbunge wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi.

na fredy mgunda,iringa


Gari la kubebea wagonjwa [Ambulance] lenye thamani ya mill.80 lakabidhiwa katika kwa mkurugenzi na mkuu wa wilaya wa Mufindi na MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Mgimwa alikabidhi gari hilo ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiomba kura kwa wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini katika kampeni ya uchaguzi mkuu 2015,ambapo alisema kutokana na changamoto ya uhaba wa gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati na vituo vya afya katika jimbo hilo, endapo atapewa ya kuwa mbunge atahakikisaha gari ya wagonjwa linapatikanaili wagonjwa waweze kufika hospital kwa wakati.

Akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi gari hilo,mbunge Mgimwa alisema muda wa kupiga siasa umeshapita na kazi iliyopo hivi sasa ni kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.

Alisema pamoja na kuongeza gari ya wagonjwa atahakikisha anaboresha vituo vya Afya vilivyopo katika jimbo lake ili kupunguza wimbi kubwa la msongamano wa wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika Hospitalini ya wilaya.

‘’’Nipo kwenye mchakato wa kuboresha vituo vyote vya Afya ndani ya jimbo langu,na nitahakikisha huduma muhimu zinapatikanaikiwa pamoja na dawa za kutosha na vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wananchi wangu waweze kuhudumiwa bila usumbufu katika vituo hivyo,hii itasaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya’’’’’alisema Mgimwa

Aidha katika mkutano huo mbunge alisisitiza swala la uaminifu kwa watumishi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wahakikishe wanajikinga na vitendo vinavyoashiria rushwa ,vinavyoweza kuwaharibia sifa ya utendaji kazi zao na kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao.

‘’’Sisi wabunge,madiwani na mtumishi yeyote aliyepewa dhamana na wananchi anatakiwa ajiepushe na swala zima la rushwa ili aweze kutenda haki kwa kuwatatulia changamoto wananchi wake waliomchagua. Tunatakiwa tuwatumie wananchi kuwaletea maendeleo ipasavyo na si vinginevyo’’’alisema

Jamhuri William ni mkuu wa wilaya ya Mufindi,akipokea msaada wa gari hilo kutoka kwa mbunge Mgimwa alisema gari hilo litaweza kusaidia kuokoa vifo vya wanamufindi hasa mama na mtoto ambapo hapo awali kuliwa na gari moja tu.

Williamu alisema kutokana na uwingi wa wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya kwa mwezi ni zaidi ya 500 aliosimia kubwa ni akina mama wajawazito na wengi wao wanafikishwa wakiwa katika hali mbaya kutokana na gari la wagonjwa kuwa moja na kushindwa kumudu.

“Tunamshukuru mbunge kwa kuliona hili na na kuokoa maisha ya watu hasa mama na mtoto ingawa bado hitaji lipo kutokana na uwingi wa wagonjwa endapo tutapata gari la tatu itasaidia sana”alisema

Williamu ameongeza kwa sasa gari hilo litahudumiwa na wilaya kuanzia kuwalipa wafanyakazi wa gari hilo,kulifanyia marekebisho ya gari hilo endapo litatokea kuharibika kwa aina yoyote ile.

Wananchi nao walitoa malalamiko yao kwa mbunge Mgimwa,ambapo Markusi Chusi alimuomba mbunge aweze kusiomamia swala la utapikananji wa vibali vya kuvuna miti,kwa kumtaka ahakikishe wazawa wa eneo husika wanapewa kipaumbele ili waweze kunufaika mali alisi hiyo ilipo kwako.

‘’’’Tumelia kwa muda mrefu,sisi tunanyanyasika kwa kuwapendelea wageni na kutuacha sisi wenyeji tuliopo hapa.Nimeomba mara tano hivi sasa na ukizingatia mimi ni mjane lakini naachwa na pesa yangu inaliwa wageni wanapewa hali inayotukatisha tama wananchi tuliouzunguka msitu huu.’’’’alisema

TTCL washiriki maonesho ya Mkutano 14 wa wahandisi Mlimani City Dar.

$
0
0


 Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kitengo cha mauzo (katikati) wakiwahudumia wateja kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.  Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.Baadhi ya wakandarasi wakitembelea mabanda anuai kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Baadhi ya wakandarasi wakitembelea mabanda anuai kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao.Baadhi ya wakandarasi wakitembelea mabanda anuai kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Baadhi ya wakandarasi wakitembelea mabanda anuai kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao.Baadhi ya wakandarasi wakipata huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao.  Baadhi ya wakandarasi wakipata huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao.Baadhi ya wakandarasi wakipata huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao.  Baadhi ya wakandarasi wakipata huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao.Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kitengo cha mauzo wakiwahudumia wateja kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kitengo cha mauzo wakiwahudumia wateja kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kulia) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi. Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kulia) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.  Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.

RAIS DKT MAGUFULI AWAFUNDA WAHANDISI,AWATAKA WACHAPE KAZI

WATANZANIA WALIVYOTUMIA FURSA YA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA RUJEWA MKOANI MBEYA

$
0
0
Wafanyabiashara wa tikiti maji wakitumia tukio la kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali kuuza matunda hayo kwa wananchi waliofika katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa Jua. 
Wafanyabiashara wa Mchele wao pia hawakubaki nyuma wakatumia fursa hiyo kuuza Mchele kwa wananchi waliofika kushuhdia tukio hilo.
Mama lishe pia hawaubaki nyuma kuhakikisha wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo .
Benki ya NMB pia walitoa huduma ya kufungua Akaunti kwa wananchi waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yaiendelea katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Amosi Makala akizungumza juu ya fursa za kiuchumi zilizojitokeza kutokana na tukio la kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Songe Luteni Mstaafu ,Chiku Galawa akizungumza na wananchi waliofika katika eneo hilo kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA ,Pascal Sheluetete akizungumza na wanahabari ambapo shirika hilo limetangaza kufungua lango la Ikoga kwa ajili ya kuingia Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa upande wa Bonde la Ihefu.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Luteni Mstaafu ,Chiku Galawa walipokutana kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amosi Makala,(katikati) ,Mkuu wa Mkoa wa Songwe ,Chiku Galawa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete wakitizama tukio la kupatwa kwa jua ka kutumia miwani maalumu za kutizamia.
Hatua ya mwanzo ya tukio la kupatwa kwa jua ,baada ya mwezi kuanza kupita mbele ya Jua na kuanza kuzuia mwanga usifike katika uso wa Dunia.
Mwezi ukiwa umebakiza kipande kidogo wakati ukipita mbele ya jua.
Mwezi ukiwa katikati ya jua na kutengeneza kipete.
Mwezi ukiwa umeanza safari  ya kuliachia jua.
Baadhi ya wananchi wakitizama tukio hilo .
Wengine walilazimika kutumia miwani maalumu kwa ajili ya kuchomea vyuma kutizama tukio hilo. 

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali ,Mbeya.

KUTANA NA CHOO SAUNDI PRUFU

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images