Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 958 | 959 | (Page 960) | 961 | 962 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 09/02/16--01:00: TAARIFA YA MSIBA
 •  
   CLARENCE CHILUMBA ENZI ZA UHAI WAKE

  TANZIA
  MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI BI.GIMBANA EMANUEL NTAVYO,ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA AFISA HABARI NDG. CLARENCE  CHILUMBA KILICHOTOKEA LEO TAREHE 02/09/2016, NDG. CHILUMBA ALIPATA AJALI YA PIKIPIKI SIKU YA TAREHE 31/8/2016 MAJIRA YA JIONI MJINI MASASI WAKATI AKITOKEA KAZINI KUELEKEA NYUMBANI KWAKE.

  BAADA YA KUPATA AJALI ALIWAHISHWA HOSPITALINI MKOMAINDO AMBAPO ALIPATA HUDUMA YA KWANZA NA BAADAYE KUPELEKWA NDANDA. AKIWA NDANDA HALI YAKE ILIZIDI KUWA MBAYA, TAREHE 1/9/2016 ALIPATA RUFAA YA KWENDA MUHIMBILI, AMEFARIKI  AKIWA NJIANI SOMANGA O2/9/2016 MAJIRA YA SAA 8:25 USIKU.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI
  AMINA.

  TAARIFA ZA MAZISHI ZITATOLEWA BAADA YA KUWASILIANA NA NDUGU WA MAREHEMU.

  IMETOLEWA NA.
  OFISI YA MKURUGENZI WA MJI
  MASASI

  0 0  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabulla (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO Bw. Hasaan Abbasi tuzo ya ushiriki wa idara hiyo katika kisaidia kutangaza shughuli mbalimbali za makumbusho na historia nchini.Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Hassan Abbasi akiangalia tuzo aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Prof. Audax Mabulla(kushoto) ya kutambua ushiriki wa idara hiyo katika kisaidia kutangaza shughuli mbalimbali za makumbusho na historia nchini.

  0 0


  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4290 la tarehe 01 Septemba 2016, ikihusisha shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika maadhimisho ya miaka 52 ya kuzaliwa kwake na shughuli za kisiasa.

  Tunapenda  kuwataarifu wananchi kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na kutetea maslahi ya Taifa na mipaka ya nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa kufuata mila, desturi, nidhamu, kanuni na sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya juu, hivyo lisihusishwe na propaganda zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye maadili ya kitaasisi ya hali ya juu.  

  Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na wanasiasa ni wakati linapotetea na kulinda maslahi ya wananchi.  Inaombwa kuwa makini katika utoaji wa maelezo au malalamiko, iachwe mara moja vyama vya siasa kuingilia ratiba za Kijeshi.   

  Ikumbukwe kwamba tarehe 25 Julai kila mwaka ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa wetu waliolitumikia Taifa hili kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta mafanikio tunayoyaona, na hii ilipitishwa mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi kutoka Uganda baada ya ushindi wa vita vya Kagera.  

  Sherehe ya mapokezi hayo yalifanyika mji wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku ya Mashujaa na kupitishwa Kisheria,  ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa ni siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana tulikuwa tunasherekea siku ya kuzaliwa JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara moja kuchanganya shughuli za Kijeshi na mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa wekeni kumbukumbu zenu vizuri. 

  Jeshi linasisitiza wanasiasa ni vizuri wakasoma vema historia ya nchi wanayotaka kuiongoza na wanayoongoza ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno yanayotolewa na viongozi wa kisiasa wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli za Jeshi na siasa zao yanatia ukakasi na kiungulia, awe makini kuongea vitu ambavyo haelewi na kutokuwa makini zaidi aelewe madhara yanayoweza kutokea kutokana na upotoshaji.

  Jeshi letu linafanya shughuli zake ki weredi.

  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
  Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akiongoza na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za ESRF kufungua warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
  Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati). Wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha na Mkurugenzi Mkazi Msaidizi wa Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Smart Daniel (wa pili kushoto).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifungua warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Jukwaa la Wazee Tanzania, Samson Msemembo (85) akizungumzia changamoto wanazokutana nazo wazee katika vituo vya huduma za afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Kaimu Kamishna Ustawi wa Jamii Bw.Rabikira Mushi kutoka Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida waliopo meza kuu.
  Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Oswald Mashindano akizungumzia nafasi ya wazee katika sera ya kitaifa kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros akishiriki kutoa maoni kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros.
  Mshauri wa Masuala ya Ushirikiano wa Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Magharibi wa Shirika la Help Age International, Roseline Kihumba akizungumzia hali ya uzee na wazee duniani na ushirikishwaji wa wazee katika maendeleo endelevu kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
  Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha akichangia mada kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mudith Cheyo akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
  Mkurugenzi wa Mtandao wa Watu Waishio na Virusi vya Ukimwi Tanzania (SHDEPHA), Joseph Katto akizungumzia changamoto zinazowakabili wazee wanaoishi na VVU katika kupata huduma mbalimbali nchini kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.  Sehemu ya washiriki waliohudhuria warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa ESRF wakati wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International
  Picha ya pamoja  SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kuhakikisha kwamba kunakuwapo na ushirikishaji wa wazi wa wazee katika sera na mipango ya maendeleo.

  Aidha imetakiwa kutoa nafasi kwa wazee katika utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo, jamii na mazingira.Kauli hizo zimetolewa na washiriki wa warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ,SDGs ambayo imeingizwa katika mipango ya maendeleo ya taifa.


  Wakiongozwa na mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu mbalimbali kama Dk Oswald Mashindano, Danford Sango, Ahmed Makbel, Dk. Ntuli Kapologwe washiriki walisema kwamba ingawa Tanzania ina sera nzuri kuhusu wazee utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kutokana na kukosekana kwa utashi.

  Aidha walisema kwamba kukosekana kwa sheria ya wazee kunawafanya wazee hao kunyanyasika hasa katika masulaa ya kiuchumi na kiafya.Joseph Kato (62) ambaye alisema kwamba amekuwa akiishi na UKIMWI tangu ujana wake hadi sasa ameingia rasmi katika rika la wazee, anasema kwamba sera za nchi hasa za afya haiztoa umuhimu kwa magonjwa kama Ukimwi.

  Aidha alisema kwamba wazee wakiwa na afya zao wamekuwa wakipuuzwa katika suala la uchumi kwani ukiwa unaishi na Virusi vya Ukimwi ukienda benki hupewi mikopo na pia ukiwa mzee hupewi mikopo.Alisema kama sera ni kuhakikisha hakuna anayeachwa katika safari za utekelezaji wa maendeleo endelevu ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba wazee hawanyanyaswi na wanasaidiwa kuwezeshwa kiuchumi.

  Mshiriki mwingine aliyejitambulisha kama Mama Koku alisema kwamba ngazi za chini za utekelezaji zimekuwa hazitoi kipaumbele kwa wazee japo serikali kuu katika mipango yake imeonesha nini kinachotakiwa kufanywa na kila mmoja katika nafasi ya kuhudumia wazee.Alisema upo mkakati wa mwaka 2007 hadi 2025 ambao umeonesha utekelezaji wa huduma kwa makundi tete lakini wakurugenzi wa halmashauri hawaweki wazee kama kipaumbele chao wakisingizia serikali kuu.

  Hata hivyo amesema wakati umefika kwa serikali kufuatilia mkakati huo kwa lengo la kuwabana wahusika ili kipaumbele kwa wazee kiwepo.Amesema maofisa mipango wengi wanakwepa kuweka kipaumbele kwa dai kuwa fedha wanazoletewa ukomo wake hauruhusu kuwaingiza wazee huku wengine wakidanganya kwamba serikali kuu ndio imeondoa msaada kwa wazee.

  Naye Ishaka Msigwa kutoka Ruvuma alisema kwamba tatizo kubwa la kuhudumia wazee sio sera kwani ipo ila dhamira ndio haipo. Alisema wazee wanataabika sana katika suala la uchumi na kwamba ipo haja sheria ya wazee ikatungwa ili kuwasaidia kuondokana na adha ya kukataliwa wakati wa kutafuta mikopo ya kuwainua kiuchumi.

  Alisema asilimia 50 ya mayatima wanakaa na wazee vijijini na kitendo cha kuwanyima ushiriki wa uwezeshaji unawatesa.Pamoja na malalamiko hayo ya wazee ambayo yalijikita katika kuwa na kipato cha uhakika na suala la upatikanaji wa matibabu, serikali ilisema imekamilisha utaratibu wa utoaji wa pensheni kwa wazee Tanzania bara na kinachosubiriwa kwa sasa ni utekelezaji wake.

  Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifungua warsha hiyo kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) alisema hata hivyo serikali itaanza kutoa posho hizo kwa wazee wa miaka 70 kwenda juu na badae watashuka hadi katika umri unaokubalika.Alisema wamejifunza kutoka Zanzibar na wanaona hapo ni eneo jema la kuanzia.

  Aidha alisema kwamba bado anaendelea na juhudi zake za kutaka sheria ya wazee itungwe kwa kuwa ipo sera inayohusu wazee.Kwa hesabu za karibuni Tanzania inawezee zaidi ya milioni 2.Pamoja na kuzungumzia suala la malipo ya pensheni ambapo alisema suala hilo kwa sasa lipo Hazina, waziri huyo alirejea msisitizo wake wa kutaka wazee watibiwe bila malipo.

  Alisema serikali ya awamu ya tano ni serikali ya utekelezaji na kwamba suala la tiba bure kwa wazee ni suala la sera na wala si utashi.Akizungumza kwa kina masuala yanayogusa wazee kama yalivyotolewa kwa sauti na mzee Samson Msemembo (85), Waziri Ummy alisema kwamba serikali inatambua changamoto zinazowakumba wazee na itazifanyia kazi kuhakikisha kwamba zinapatiwa majibu.

  Mzee Msemembo kutoka Jukwaa la wazee Tanzania, alisema kwamba wazee wamekuwa wakinyanyasika katika sekta ya afya na uchumi wakibaguliwa na kunyimwa fursa za kuishi kwa furaha.

  Akizungumza kuhusu kero zilizoelezwa katika warsha hiyo iliyoendeshwa kwa pamoja katika Taasisi za Tafiti za Kiuchumi na Kijamii nchini (ESRF) na taasisi ya kimataifa ya kusaidia wazee Help Age, Waziri Ummy alisema serikali inataka wazee wawe na kipato cha uhakika na kupewa matibabu.

  Amesema hakubaliani na suala la wazee kukosa matibabu na kutaka wakurugenzi wote wa halmashauri kuhakikisha kwamba wazee wanaingizwa katika mfumo wa matibabu wa CHF au wanapewa kadi maalumu ya matibabu bure.

  Alisema kwamba haingii akilini kuona kwamba wazee sita katika watu 100 wanakosa kutibiwa kwa dai la kukosekana kwa fedha wakati sera zipo zinazotaka watibiwe bure.Akizungumzia tatizo la Hospitali ya Taifa Muhimbili kutotibia wazee alisema kwamba atalishughulikia tatizo hilo kwani haliingii akilini mwake:“Watumishi, vifaa, kila kitu ni cha serikali inakuaje wazee wasitibiwe” alihoji Waziri Ummy .

  Akizungumzia suala la kukuza uchumi wa wazee alisema kwamba atamwandikia barua Rais Magufuli ili aweze kutoa agizo la asilimia 2 katika mapato ya ndani ya halmashauri kuchochea uchumi kwa wazee.Alisema kuna asilimia 5 zimetengwa kwa vijana na wanawake pia 5 na haoni sababu zisitengwe asilimia 2 kwa ajili ya wazee.

  Katika warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida alisema kwamba warsha hiyo imelenga kusaidia wadau mbalimbali kutambua masuala ya wazee katika mipango ya maendeleo kuanzia ngazi za chini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya dunia.

  0 0  0 0

  Nyumba za Wasanii wa Yamoto Band zikionekana kwa muonekano wa nje.
  Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.

  Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akikagua nyumba ambazo zipo kwenye hatua ya mwisho ya umaliziaji.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akionyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Yamoto Band zitakazopatikana nchi nzima.

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  MKURUGENZI wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band na kuwataka wananchi waelewe kuwa msanii anahitaji nyumba na sio magari.

  Nyumba hizo zilizojengwa nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe amesema kuwa hiyo ni moja ya maendeleo kwa wasanii ,kwani hii si mara ya kwanza kuwazawadia nyumba wasanii wake.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa ameamua kuziweka wazi hasa baada ya kusikia maneno mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa Yamoto Band hawafaidiki na Muziki wanaoufanya.

  Fella amesema kuwa nyumba hizo mpaka sasa hajajua thamani yake ila zitakapokamilika ataita watu wa tathmini kwa ajili ya kuziangalia ili kujua zimetumika kiasi gani kwenye ujenzi huo.

  Ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi kubwa sana alizozifanya katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua wasanii. Na katika nyumba hizo zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.

  Meneja wa Mkubwa na Wanawe, Amani Temba 'Mh. Temba' amesema kuwa hizi nyumba zimejengwa kwa fedha za wasanii wenyewe wanazozipata kwenye shoo za muziki wanazozifanya na sio kama hela zinazotoka mfukoni mwa kiongozi yoyote.

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka amefurahishwa na hatua hii kwani ni mara chache sana kwa viongozi wa muziki kuchukua dhamana ya kuwajengea nyumba vijana hawa wadogo na amewataka wasanii kutokufanya mzaha kwenye tasnia hii.

  Fella amezindua pia nguo aina mbalimbali zenye nembo y Yamoto Band na wamezilipia Brela,COSOTA kwa hiyo yoyote atakayejaribu kunakili watamshughulikia.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Vodacom Afrika Bw. Shameel Joosub (kushoto),ambaye aliongozana na Viongozi wengine wa Vodacom Tanzania na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam
    Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Vodacom Afrika Bw. Shameel Joosub (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Sinare Majaar (kushoto) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Vodacom Afrika Shameel Joosub.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Naibu Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jafo akihutubia wadau wa kampeni ya kuchangia Madawati Mkoa wa Geita kwenye Harambee iliyofanyika Mjini Geita.
  Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila akitoa maelezo kuhusu namna Acacia ilivyoshiriki mwaka huu kuchangia kwenye zoezi la madawati.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bwana Graham Crew akiwa amenyoosha mikono kusalimia umma wa Watanzania waliongana kwenye harambee ya madawati Geita
  Timu ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri baada ya Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila kutanga kuwa Mgodi utatoa shilingi milioni Mia Moja kwa ajili ya madawati Mkoa wa Geita.

  Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

  Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu Umetoa Tsh 100m/- kwa Ajili ya Madawati ya Shule Mkoani Geita.

  Akitangaza kiwango hicho katika hafla ya changizo iliyofanyika Desire Park Mjini Geita , Meneja Ufanisi na Mahusiano na Jamii wa Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu bwana Elias Kasitila amesema, “Bulyanhulu imebarikiwa kuwa karibu na Wilaya mbili,Halmashauri ya Msalala iliyopo Mkoa wa Shinyanga na Nyang’wale iliyopo Mkoa wa Geita.

  “ Hivyo basi tulipopokea mwaliko kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale kuhusu kampeni ya leo ya madawati tumeamua kwamba japokuwa miradi mingine ya madawati tumeifanya mkoa wa Shinyanga tumeona kuna umuhimu wa kufanya hivyo mkoa wa Geita pia.”alisema Kasitila.

  "Hivyo basi siku ya leo tunajitolea kuchangia Tsh100m/- kwa ajili ya kampeni za mikoa inayolenga kuondoa upungufu wa madawati 70,000.”aliongeza Kasitila. Elias aliongeza kuwa, “misaada ya madawati kutoka kwenye migodi iliyoko chini ya Acacia ambayo ni, North Mara, Buzwagi and Bulyanhulu,kwa mwaka huu Acacia imetumia takriban fedha za kitanzania zaidi ya Billion Moja ambayo inakadiliwa kutengeneza zaidi ya madawati 10,000.

  Mgeni rasmi katika hafla ya kuchangia madawati mkoa wa Geita alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi ,Utumishi na Utawala Bora, Mh.Suleiman Jafo.

  Akiwahutubia washika dau waliokuwa Desire park Naibu Waziri Jafo alisema “Nitapeleka salamu kwa waziri mkuu kuhusiana na mwitikio ambao nimeushuhudia leo ninaagiza kamati ya Kampeni ya madawati Geita kuorodhesha washika dau wote waliochangia leo na kuwasilisha orodha hiyo kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ili binafsi awatambue wote walioonesha kuguswa kuiondolea Geita uhaba wa madawati.”

  Katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Aacacia Bulyanhulu Graham Crew binafsi alijitolea kuchangia fedha za kitanzania shilingi 750,000/- kwa ajili ya kampeni hiyo.

  0 0


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (wa tatu kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam walipokutana kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa pili kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai na kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Iran Bw. Ali Bagiri.
  Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (wa tatu kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman akielezea azma yake ya kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Utamaduni kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 2,2016 wa pili kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai na kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Iran Bw. Ali Bagiri.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2,2016 kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kiutamaduni kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiangalia kitabu cha Utamaduni kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.

  Picha/Habari na Raymond Mushumbusi


  Serikali ya Tanzania na Iran zakubaliana kuanzishwa kwa wiki ya Utamaduni itakayowezesha kujifunza namna ya kuukuza ,kuulinda na kuendeleza sekta hiyo.

  Makubaliano hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran.

  Waziri Nnauye alisema kuwa amekubaliana na wazo la kuanzishwa kwa wiki ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran na ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwao namna ya kuukuza, kuulinda na kuuendeleza utamaduni wa mtanzania.

  “Utamaduni ni silaha ya upendo na nimefurahia wazo la kuanzisha wiki ya Utamaduni na tuko tayari kujifunza kutoka kwenu na hakika tumelipokea na tunaamini fursa hii italeta mafanikio makubwa katika sekta hii”, alisema Mhe. Nnauye.

  Kwa upande wa Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa wataendelea kushirikiana katika masuala ya Utamaduni na kuendelea kujifunza kutoka kwa watanzania namna bora ya kuenzi,kuendeleza na kuutunza Utamaduni.

  Naibu Waziri huyo wa Iran aliendelea kusema serikali yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika uandaaji wa Filamu na kubadilishana uzoefu katika masuala ya filamu kati ya nchi hizo mbili.

  Hata hivyo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nnauye alipata mwaliko kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Turkaman kwenda nchini Iran kujionea vivutio vya utamaduni

  0 0


  0 0


  Wachezaji wa timu ya New Generation wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa baada ya kuifunga Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar, zilizochezwa kwenye uwanja wa Fuoni Alhamisi 25 Agosti 2016

  Nahodha wa timu ya New Generation Amina Hali Abdallah (nyekundu) akikabidhiwa kombe na Afisa Habari wa ZFA Ali Bakari baada ya kuichapa timu ya Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar Jana 25 Agosti 2016. New Generation ilishinda 2-1.

  Naodha wa timu ya Mbaspo Academy Mbeya, Biva Steven akipokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi Katibu Tawala wa mkoa huo Alone Mbinga baada ya timu yake kuifunga Uyole Alois Academy Penati 4-3 katika mchezo wa fainali ya Airtel Rising stars ngazi ya mkoa uli0pigwa katika dimba la uwanja Sokoine juzi.
  Wachezaji wa timu ya New Generation wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa baada ya kuifunga Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar, zilizochezwa kwenye uwanja wa Fuoni Alhamisi 25 Agosti 2016.


  TIMU ya wasichana ya New Generation imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Star, Zanzibar, baada ya kuifunga Women Fighter kwa mabao 2-1 katika fainali iliyochezwa visiwani humo jana.

  Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Fuoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar na kuvuta hisia za mashibiki wengi wa soka wanawake na wanaume, hasa kwa vile timu hizo zina upinzani wa jadi.

  Mabao ya New Generation yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza ambapo bao la kwanza lilifungwa na Warda Mwinyi katika dakika ya 10 wakati bao la pili lilifungwa mnamo dakika ya 16 wakati bao la kufutia machozi la Women Fighter lilifungwa na Khadija Hassan dakika ya 27.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi kombe kwa washindi afisa habari wa chama cha soka Zanzibar ZFA Ali Bakari Cheupe kwa niaba ya rais wa chama hicho, aliipongeza kampuni ya Airtel kwa uamuzi wake wa kudhamini michuano hiyo ambayo imeweza kuleta hamasa kubwa kwa wananchi wa Zanzibar.

  Alisema kabla ya michuano hiyo Zanzibar ilikuwa nyuma katika soka la wanawake lakini kupata udhamini huo ari imeongezeka zaidi na tayari wanawake wengi wamehamasika kutaka kucheza mpira wa miguu.

  Naye Meneja Mauzo wa Airtel Muhidin Mikidad alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo hiyo kadri ya hali itavyokuwa, ambapo amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuwaunga mkono

  Jijini Mbeya, timu ya wavulana ya Mbaspo Academy imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi baada ya baada ya kuifunga Uyole Alliance 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

  Mchezo huo uliamuliwa kwa penati kufuatia timu hizo kutoka sare ya kufungana 3-3 katika muda wa kawaida wa dakika 90.

  Katika mchezo huo ulipigwa juzi katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ulishuhudia vijana wa Uyole Alliance kutoka nje kidogo ya jiji la Mbeya wakijipatia goli la kuongoza katika dakika ya saba baada ya Daniel Shaban kufunga kwa penati baada mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

  Mbaspo walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 20 kupitia kwa Albinus Haule kabla ya Claud Alex wa Uyole Alliance kuandika bao la pili timu yake dakika ya 42.

  Mabao mengine kwenye mchezo huo yalipatikana dakika 82 kwa upande wa Mbaspo mfungaji Shadraki Sape,wakati bao la Uyole Alliance lilipatikana dakika ya 88 mfungaji ni Claud Casto.

  0 0


  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
  Mtaalamu wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa maelezo kuhusu mada inayohusiana na udhibiti wa uhalifu wa mitandao wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
  Mtaalamu wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha karatasi inayoelekeza jinsi ya kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.
  Kamishna Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, akielekezwa na Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, namna ya kudhibiti uhalifu katika majengo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya nchi hizo. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

  Septemba 2,2012 Mwandishi wa Habari, Marehemu Daudi Mwangosi (hayuko pichani), aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Iringa, aliuawa na polisi akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo mkoani Iringa ambapo aliyemuua alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani julai mwaka huu.
  Na BMG
  Kufuatia mauaji hayo, Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini, UTPC ulitenga tarehe hiyo kuwa kumbukumbu ya Kifo cha Daudi Mwangosi ikiambatana pia na tuzo inayotolewa kwa mwanahabari aliyefanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kupigwa ama kuuawa kutokana na kazi yake.

  Leo UTPC imekutana na wanahabari Jijini Mwanza imekutana na wanahabari ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Mwangosi ambapo imelaani mazingira magumu ambayo wakati mwingine wanahabari na vyombo vya habari wanayapitia katika utendaji wao wa kazi ikiwemo vyombo vya habari kufungiwa.

  Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji (kushoto) amesema wanahabari wanataka mazingira huru ya kufanya kazi huku akilaani serikali kuvifungia baadhi ya vyombo vya bila kusikilizwa juu ya yale yanayodhaniwa kufanywa na vyombo hivyo kinyume cha sheria.

  Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, amebainisha kwamba tunzo ya Daudi Mwangosi mwaka huu pia haikupata mshindi kwa namna ambavyo jopo la tuzo hiyo lilivyoweka vigezo vyake ikiwemo Mwandishi anayepaswa kuichukua awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini. Mwaka 2013 tuzo hiyo ilichukuliwa na Mwanahabari Absolum Kibanda.
  Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji 
  Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, amebainisha kwamba tunzo ya Daudi Mwangosi mwaka huu pia haikupata mshindi kwa namna ambavyo jopo la tuzo hiyo lilivyoweka vigezo vyake ikiwemo Mwandishi anayepaswa kuichukua awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini. Mwaka 2013 tuzo hiyo ilichukuliwa na Mwanahabari Absolum Kibanda.
  Vingozi wa UTPC wakimkumbuka marehemu Daudi Mwangosi
  Wanahabari mkoani Mwana wakimkumbuka marehemu Daudi Mwangosi
  Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

  0 0  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na mkewe mama Janeth,wakisalimiana na wenyeji wao mara baada ya kuwasili Pemba mapema leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili visiwani humo,ambapo hapo baadae ataelekea Unguja kuendelea na ziara yake ya kikazi .
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na mkewe mama Janeth,na ujumbe mwingine aliofuatana nao wakitazama kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili Pemba mapema leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili visiwani humo,ambapo hapo baadae ataelekea Unguja kuendelea na ziara yake ya kikazi.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
  Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli akiomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma. lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa ameambatana na Mkewe,Janeth Magufuli (hawaonekani pichani) wakisubiri kuweka mashada  ya maua na kuomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma. lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Asubuhi ya leo tarehe 02 Septemba, 2016 amewasili Kisiwani Pemba ambapo majira ya Alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Pemba katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani hapa.

  Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameelekea katika kijiji cha Wawi Bigilini kilichopo katika Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba ambako amezulu Kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

  Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma na wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu iliyoongozwa na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kiislamu na Kikristo.

  Akizungumza mara baada Dua, Rais Magufuli amesema anamkumbuka Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa ukarimu wake, upendo, kutojikweza, kutobagua watu na kudumisha amani katika siku zote za maisha yake.Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kudumisha kwa vitendo amani aliyoisimamia Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

  "Mimi najua huko aliko Marehemu Dkt. Omar Ali Juma anaendelea kuliombea Taifa hili ili hiyo amani aliyoihubiri katika maisha yake, ili huo upendo aliousimamia katika maisha yake, ili huo uchapa kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote tuweze kuendeleza kwa mioyo yetu yote" Amesema Rais Magufuli.

  Aidha, Rais Magufuli amewashukuru Wanafamili wa Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa uvumilivu na ustahimilivu wao tangu walipoondokewa na mpendwa wao.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Pemba
  02 Septemba, 2016


  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuhutubia mkutano katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Pemba katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Pemba katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi wananchi wa Kisiwa cha Pemba kutokubali kurubuniwa na watu wanaowachochea kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kuwa vitendo hivyo vinarudisha nyuma juhudi za kuwaletea maendeleo na kutatua kero zinazowakabili.

  Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 02 Septemba, 2016 wakati akihutubia Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale Wilaya ya Chakechake Mkoani Kusini Pemba, ambao umehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

  Rais Magufuli amesema Kisiwa cha Pemba kina fursa nyingi za maendeleo ikiwemo Uvuvi wa baharini, Utalii na Kilimo lakini endapo wananchi wataendelea kushabikia uchochezi na vitendo vya kuvuruga amani vinavyofanywa na baadhi ya watu, hakuna mwekezaji atakayekuwa tayari kuwekeza.

  ""Hawezi akaja mtu kujenga kiwanda wakati hakuna amani, sisi vijana lazima tuwe mstari wa mbele kujenga amani ili wawekezaji waje wajenge viwanda na tupate ajira."Hapa Pemba kuna fukwe nzuri ambazo zinafaa kujenga hoteli kubwa za kitalii, nani atakuja kujenga hoteli kama hakuna amani?" Amehoji Rais Magufuli huku akisisitiza kuwa umefika wakati kwa wananchi wa Pemba kubadilika na kujikita katika masuala ya maendeleo.

  Hata hivyo Rais Magufuli ameonya kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitawafumbia macho watu wanaofanya uchochezi unaolenga kuvuruga amani na ameviagiza vyombo vya dola vianze kuwafuatilia wote walioanza kufanya uchochezi huo.

  Amesisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobaki sasa ni kwa watanzania kufanya kazi na kujenga nchi yao.

  Mapema akimkaribisha Rais Magufuli kuzungumza na wananchi hao, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewaambia wananchi wa Zanzibar kuwa tangu aingie madarakani yeye na Rais Magufuli wamefanya mambo mengi kwa manufaa ya Watanzania

  Dkt. Shein ameongeza kuwa hali ya Muungano ni nzuri na kwamba sehemu kubwa ya kero za Muungano zimetatuliwa huku akibainisha kuwa kwa sasa kazi iliyopo ni kutafuta changamoto mpya za Muungano zenye lengo la kuchochea maendeleo.

  Mkutano huo umehudhuriwa na Mke wa Rais Magufuli Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais Shein, Mama Mwanamwema Shein, Mawaziri na viongozi mbalimbali wa Siasa, Dini na Serikali.

  Jioni hii Rais Magufuli amewasili mjini Unguja ambapo kesho tarehe 03 Septemba, 2016 ataendelea na ziara yake kwa kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume, kuzuru kaburi na kutoa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi na baadaye atazungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibandamaiti Mjini Unguja.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Unguja

  02 Septemba, 2016

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba ambako aliweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Dkt Omar Ali Juma, na kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye ndege ya ATCL katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akivishwa shada la maua ya asumini baada ya kutelemka kutoka kwenye ndege ya ATCL katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na makamanda wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri  wa Ujenzi, Mawasilaino na usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni   katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwakilishi wa jimbo la Uzini Mhe. Mohamed Raza Hassanali  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na  Waziri wa Afya Mhe.  Mahmoud Thabit Kombokatika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mohamed Seif Khatib katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mratabu wa Diaspora,Ofisi ya Rais Ikulu na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Ndugu Hassan Hafidh katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na mmoja wa makada waandamizi wa CCM katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mmoja wa viongozi  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiakisalimiana na mmoja wa viongozi katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na mmoja wa wazee mashiuhuri katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia ngoma ya utamaduni ya Kilua katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiangalia ngoma ya Msewe baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba. Picha na IKULU

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akizungumza aliyeambatana na Wabunge toka Sweden walipotembelea Ofisini kwake mapema leo.
  Kiongozi wa ujumbe toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns (kushoto) akikabidhi zawadi yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
  Kutoka kushoto ni Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mashaka Gambo pamoja na Kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Bi. Matilda Irnkarns kwenye picha ya pamoja baada ya Kikao
  Katika picha ya pamoja ni kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Kwitega, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnite , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns, ujumbe toka Sweden pamoja na viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  Baadhi wa wabunge toka Sweden wakifuatilia kikaa wakati walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema leo.

  Nteghenjwa Hosseah –Arusha

  Arusha kulindwa kwa CCTV- Camera

  MKOA wa Arusha umeanza kujipanga katika utaratibu wa kulinda mji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya CCTV – Camera ili kuimarisha usalama wa mji “Safe City”, Mfumo huu utawezeshya Mji kulindwa masaa 24 dhidi ya uhalifu kwa raia, wawekezaji na watalii.

  Kauli hiyo ilitolewa leo mjini hapa na Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo ofisini kwake mara baada ya kutembelewa na Balozi wa Sweden nchini, Bi. Katarina Rangnite aliyeambatana na Ujumbe wake wa Wabunge kutoka Nchini Sweden.

  Akizungumza na ujumbe huo RC Gambo alisema, mkoa huo tayari umekwisha kuonyesha nia ya kuwekeza katika mfumo huo ili kuwaongezea wananchi na mali zao usalama zaidi.

  “Nia yetu ni kuona hali ya usalama katika mkoa wa Arusha ikiwa ya juu sana ili kuendelea kuwavutia watalii zaidi kutoka nchi mbalimbali Duniani. Malengo yetu ni kuwa na mifumo itakayoulinda mkoa wetu kwa Saa 24 na mwaka mzima,” alisema RC Gambo na kuongeza:

  “Hatua hii itaongeza ulinzi kwa raia na mali zao, pia kwa wawekezaji waliopo mkoani kwetu na watalii wanaokuja kutembelea hifadhi na vivutio mbalimbali kwani Arusha ndio kitovu cha utalii hapa nchini,” alisema.

  Kwa upande wake Balozi Rangnite ambaye kiongozi wa msafara huo uliojumuisha pia wabunge kutoka Bunge la Sweden wanaowakilisha Kamati ya Kilimo na Mazingira, alikubaliana na nia ya kuwekeza kwenye mfumo wa usalama wa mkoa wa Arusha.

  Balozi Rangnite alimueleza Mkuu wa Mkoa Gambo kwamba, nchi ya Sweden inayo wataalamu waliobobea katika mifumo hiyo ya usalama wa miji hivyo alimuomba Gambo kuwasilisha kwake maandiko ya vitu vinavyohitajika ili kuwezesha mradi huo kutekelezwa.

  “Tukipata maandiko mbalimbali ya mradi tunaweza kuangalia ni wapi Serikali ya Sweden inaweza kuwekeza ikiwamo kusaidia kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili,” alisema Balozi Rangnite.

  Aidha Gambo alitoa ombi kwa Balozi wa Sweeden kushirikiana na Mkoa wa Arusha kwenye Kampeni ya Kulinda vyanzo vya Maji ili kuwezesha mradi mkubwa wa maji unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na maji taka (AUWSA) kutekelezwa kwa mafaniko makubwa. Itakumbukwa kwamba imepatiwa Bil 476 ili kumaliza tatizo la maji Jiji hapa.

  Katika ziara ya ujumbe huo pamoja na mambo mengine ulikuwa na lengo la kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji katika Kilimo, Mazingira na maeneo muhimu kutoka mkoani Arusha.

  Ujumbe huo kutoka Sweden ukiongozwa na Balozi Rangnite uliridhishwa na kuvutiwa na maeneo ya utalii yaliyopo katika mkoa huo yakiwamo pia mazingira rafiki yanayoruhusu uwekezaji kwa jamii yao.

older | 1 | .... | 958 | 959 | (Page 960) | 961 | 962 | .... | 1898 | newer