Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 956 | 957 | (Page 958) | 959 | 960 | .... | 1897 | newer

  0 0

   
   KASI ya Rais Magufuli katika kuhakikisha Tanzania inajitegemea kwa kila mhusika kulipa kodi imeanza kulipa kufuatia takwimu kuonesha kwamba watalii wameongezeka nchini na hivyo kuongeza mapato zaidi Serikalini.
  Ukweli huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Mghembe alipokuwa akizungumza kuhusu mikakati mbalimbali iliyotekelezwa na Wizara yake.
  “Pamoja na kelele za sekta ya utalii baada ya Serikali kuanza kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika sekta ya utalii, lakini nakuhakikishia hivi sasa watalii wameongezeka nchini na mapato yamekua kwa asilimia 22 zaidi,” alisema Waziri Maghembe.
  Waziri Maghembe ametanabaisha kuwa tofauti na mtazamo wa wadau wa sekta ya utalii ongezeko la kodi hiyo halijaathiri watalii wengi hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania inabaki kuwa na vivutio vya kipekee duniani.
  “Nchi yetu ina vivutio vingi ambavyo havipo nchi nyingine yoyote. Hii ikijumlishwa na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini, hakuna mtalii atakayeshindwa kugharamia ongezeko la dola nane tu,” alisema Waziri Maghembe.
  Alitumia muda huo pia kueleza kuwa utafiti wake katika nchi za nje unaonesha kwamba Balozi za Tanzania zinaongoza kutoa viza kwa watalii mbalimbali ikilinganishwa na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki hasa katika miji mikubwa kama Berlin.
  Akizungumzia vita dhidi ya ujangili, Waziri Maghembe amesema juhudi za Serikali kuwekeza katika mafunzo na vifaa vya kisasa zimezaa matunda pia baada ya  ujangili kupungua nchini kwa kiasi kikubwa.
  Alisema tayari watuhumiwa wakubwa wa mtandao wa ujangili wameshakamatwa na baadhi wamehukumiwa vifungo jela. Alimtaja mmoja wa watuhumiwa wakubwa wa mtandao huo raia wa kigeni ajulikanaye kwa jina la “Malkia wa Pembe za Ndovu” naye yuko mahabusu kwa sasa.
  “Katika vita hii tumeamua kuuchukulia ujangili kama ugaidi au uhujumu uchumi. Tumekamata majangili wakubwa na wafadhili wao na bado vigogo zaidi tunaendelea kuwafuatilia na muda wowote tutawakamata,” alisema.
  Aliongeza kuwa Serikali pia imepiga marufuku uvunaji wa mazao ya misitu hasa magogoro bila leseni na kwamba atakayefanya hivyo atakamatwa, mali na gari husika vitataifishwa na wahusika kufikishwa mahakamani.
  Takwimu za kuongezeka watalii nchini zinaipa nguvu Serikali ya Rais Magufuli kwa sababu tangu alipoingia amekuwa akisisitiza sana katika umuhimu wa kukusanya kodi ili nchi ijitegemee. Tofauti na mtazamo huo, baadhi ya watu wamekuwa hawaamini kama hilo linawezekana.

  0 0

   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimkaribisha kuketi  Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimsindikiza Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016. 
    "Hapa kazi tu..." anaonekana kusema Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yake na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016.

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimia na Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mkoba walipokutana katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO)yaliyofanyika Agosti 30,2016.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikilza Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mkoba walipokuwa wakijadiliana maswala mbalimbali ya kimichezo katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) uliofanyika Agosti 30,2016.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) akizungumza na viongozi wa Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) katika ufunguzi ya mashindano ya michezo ya Umoja huo uliofanyika Agosti 30,2016.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Yahya Msugwa(kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) walipokutana katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) uliofanyika Agosti 30,2016.
  Rais wa Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) Bw. Henry Kapenda akielezea jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) walipokutana katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) uliofanyika Agosti 30,2016.
  PICHA na  Raymond Mushumbusi WHUSM

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
  Dar es Salaam.
  31/08/2016.

  RAIS Dkt. John Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika  kongamano la tatu la kitaifa la afya  litakalofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 14-15 Novemba, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Rais wa Taaasisi ya Tanzania Health Summit (THS) Dkt. Omary Chillo alisema kuwa kongamano hilo litahudhuriwa na  wadau 500 wa afya kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo watoa huduma za afya, watunga sera, watafiti wa magonjwa ya afya, wachumi, na wadau wa maendeleo.

  Alisema kongamano hilo litalenga kuongeza nguvu za Serikali za kuboresha afya za Watanzania kupitia kupashana habari na ujuzi, majadiliano ya changamoto na kufikia muafaka wa njia bora za utatuzi wake ili kuimarisha huduma za afya nchini.

  Aidha, alisema kuwa mkutano huo utahusisha vipengele mbalimbali ikiwemo vikao vya mashauriano yatakayogusa mada mbalimbali za maendeleo ya afya, taarifa kutoka kwa wataalamu wabobezi wa afya, pamoja na kuwasilisha matokeo ya uchunguzi.

  Pia aliongeza kuwa katika kongamano hilo pia kutakuwa na maonyesho ya huduma na bidhaa kutoka kwa wasambazaji wa huduma za afya ya mashirika ya umma na binafsi.

  Dkt. Chilo alitoa wito kwa wadau wa afya nchini kutoka Serikalini, mashirika binafsi, mahospital, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za kitaaluma, wasambazaji, na washirika wa maendeleo kushiriki kikamilifu katika kongamano hilo.

  0 0

  -Zaidi ya shilingi milioni 300 kushindaniwa
   -Mshindi wa zawadi kubwa kujinyakulia kitita cha shilingi milioni   100

  Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushiriana na benki ya CBA imezindua promosheni kubwa ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia fedha taslimu kutoka kwenye kitita cha milioni 300 zilizotengwa kwa ajili ya promosheni hii na mshindi mmoja wa zawadi kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.

  Promosheni hii inayojulikana kama ‘Jiongeze na M-Pawa’ itatoa washindi wa siku wa shilingi milioni 1/- kila mmoja,washindi wa wiki  shilingi milioni 20/- kila mmoja na wateja wapatao 200 wataongezewa mara mbili ya akiba zao walizojiwekea kwenye akaunti zao za M-Pawa kila siku.
                                                          
  Promosheni hii ambayo imeanza leo Agosti 31 itadumu kwa kipindi cha wiki 6 na itafikia mwishoni mwezi Oktoba ambapo itafanyika droo ya kumpata mshindi wa zawadi kubwa.Katika kipindi chote cha promosheni mabalozi wa bidhaa za Vodacom na maofisa wa kampuni watatembelea sehemu mbalimbali za Tanzania kwa ajili ya kuwaelimisha  faida za kujiwekea akiba kupitia huduma hii hususani wanaoishi maeneo ya vijijini.
                                                                                        
  Ili kushiriki kwenye promosheni anachotakiwa kufanya mteja ni kujiwekea akiba kwenye akaunti yake ya M-Pawa kwenye simu yake katika kipindi cha promosheni.Kwa kujiwekea akiba mojamoja kutawawezesha wateja kujipatia pointi za kuingia kwenye promosheni na kuwa na uwezekano wa kujishindia fedha taslimu kila siku,kila wiki na zawadi kubwa ya promosheni.Kadri mteja anavyojiwekea akiba kwenye akaunti yake ya M-Pawa ndivyo anakuwa na nafasi kubwa ya kushinda .
    
  Kwa mfano kwa kujiwekea akiba kati ya shilingi 1,000/-mpaka 19,000/-mteja anajipatia pointi 20,wakati akijiwekea  akiba kati ya shilingi 20,000/-mpaka shilingi 99,999/-mteja anajipatia pointi 40 na kadri anavyoweka akiba ndivyo pointi zinaongezeka  zaidi na  kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.
                                  
  Kuweka akiba kwenye akaunti ya M-Pawa na kuwa kwenye  nafasi ya kushinda mteja anaweza kupiga  *150* 00#  kisha kwenda kwenye menu ya  M- Pawa, chagua Weka  kwenye M-pawa, weka kiasi cha fedha kisha weka namba yako ya siri ya  M-Pesa  .

  Wateja watakaojishindia shilingi milioni 1/-na wale  watakaoongezewa fedha zaidi ya mara mbili ya akiba zao fedha zao zitaingizwa kwenye akaunti zao za M-Pawa moja kwa moja ambapo watafahamishwa kuwa wameshinda kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS).Washindi wa wiki wa shilingi milioni 20/- na mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni watakabidhiwa zawadi zao  na maofisa wa Vodacom watakaochaguliwa kufanya kazi hiyo kulingana na mikoa watakayotokea washindi.
             
  Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwahamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba na kunufaika kwa mikopo yenye riba nafuu ya kati ya asilimia 2% hadi 5% kulingana na akiba ya mteja aliyojiwekea.”Promosheni inawakumbusha watanzania kuwa kuweka akiba kwenye M-Pawa ni chaguo la busara hususani kwa wajasiriamali kwa kuwa inawezesha kupata mikopo nafuu yenye riba ndogo”.amesema Ian Ferrao,Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania .

  “Huduma ya M-Pawa ni akaunti ya benki kwenye ncha ya kidole chako ambayo imebuniwa kuboresha maisha ya wateja!Zaidi ya watanzania milioni 4.8 wanaendelea kufurahia huduma hii na natoa wito kwa watanzania wengi wajiunge zaidi na kufurahia huduma hii ya M-Pawa.Unavyojiwekea akiba zaidi ndivyo kiwango cha kukopa kinavyoongezeka”.Alisisitiza Ferrao.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam kuajadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu. Kulia kwake ni Rais wa chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akimuonyesha Rais wa chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano na ujumbe wake taarifa ya maendeleo ya Miundombinu
  nchini, walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam.

  Rais wa chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano (wa nne kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es salaam kuajadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Rais wa chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano, wakati Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea Ofisini kwake kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Rais wa chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano wakati Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea Ofisini
  kwake kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu. 

  PICHA NA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (W-UUM)

  0 0


  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO) , Kulia ni Mkurugenzi wa shirika hilo, Askofu Nason Ngoy Ngoy. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 31, 2016katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”,

  Mkurugenzi wa Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO). Askofu Nason Ngoy Ngoy, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO). Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
  Washiriki wa uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Goodluck Ole Medeye, mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”.Hafla hiyo imefanyika leo.
   
  (PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI) 

  0 0


  Wanafunzi wakiwa katika sehemu ya mapokezi ya uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuanza safari jana mjini Zanzibar.

  Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, akizungumza na waandishi habari mjini Zanzibar juu ya safari wanafunzi 70 wanaokwenda kusoma nchini India.
  Wanafunzi wakiingia katika feri ya Zanzibar kwa ajili ya safari ya kwenda vyu vikuu vya nchini India kupitia uwanja wa ndege wa zanzibar jana mjini Zanzibar
  Wanafunzi wakipata historia katika makumbusho ya soko la watumwa wakati wa ukoloni ambalo lilifanyika Zanzibar.
  Wanafunzi wakiingia katika basi kwa safari ya uwanja wa ndege wa Zanziabar kwa safari ya kwenda kusoma katika vyuo vya nchini India.

  Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel (Mwenye Bag) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na baadhi ya wazazi waliowasindikiza watoto kwa ajili safari ya nchini India Jana Mjini Zanzibar
  Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel (Mwenye Bag) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa GEL katika uwanja wa Zanzibar.

  Wanafunzi wakiingia katika boti ya kwenda Zanzibar kwa kwenda kusafiri kwa ndege kwa kutumia uwanja wa ndege wa Zanzibar.


  MKURUGENZI wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa kati ya 10 Wazazibar saba wanajua vyuo vya nje na tofauti ya Tanzania Bara hivyo kunahitajika kuwepo kwa ofisi ya kuratibu wanafunzi wanaotaka kusoma vyuo vya nje.

  Mollel ameyasema mjini Zanzibar wakati alipokuwa anasafirisha wanafunzi 70 kwenda vyuo vya India kwa kupitia uwanja wa ndege wa Zanzibar, amesema kuwa kati ya sehemu ya kuongeza ofisi ni Zanzibar,Mwanza pamoja na Dodoma kutokana na serikal kuhamia huko .

  Mollel amesema kupitia Zanzibar ni pamoja na kutaka wanafunzi hao wajue historia ya Zanziba katika makumbusho yalipokuwa Soko la watumwa ili wakifika huko waweze kuitangaza Tanzania uwepo wa vivutio hivyo.
  Amesema wazazi wanatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa na serikali na kuacha kutumia mawakala kwa kupeleka wanafunzi wanaokosa vigezo na mwisho wa siku wanakuwa hawana chakufanya nje na kuwa wazurulaji na kuipa doa nchi.

  Aidha Mollel ameshauri wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi ambao hawana sifa ofisi za balozi ziwanyime viza katika kuleta heshima ya nchi kuwa watu wanaosoma nje ya nchi wanasifa za kujitosheleza na si vinginvyo.

  Mollel amesema kuwa wanafunzi wanaopita GEL wanafuata taratibu zote ikiwa na vyuo wanavyokwenda vinatambulika ndani pamoja na bodi za nchi husika.Hata hivyo amesema wanafunzi wanaondoka vyuo vya nje vimeshafunguliwa tofauti ndani hivyo nafasi bado zipo kwa ajili wanafunzi wanaotaka kutimiza ndoto zao.

  Mollel amesema ada ya vyuo vya nje na vyuo binafsi vya ndani ni sawa hivyo wazazi waache kuogopa hilo kutokana na mfumo uliowekwa baina ya Global Education Link na vyuo vya nje mzazi anaweza kulipa kwa awamu.

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe, amesitisha shughuli za maandamano zilizokuwa zimepewa jina la (UKUTA) kwa Muda wa mwezi mmoja,kwa kile alichodai baada ya kuombwa na viongozi wa Dini na taasisi Mbalimbali, ambapo maandamano hayo yalitarajiwa kufanyika kesho Septemba Mosi nchi nzima.

  Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha kwa maandamano hayo mapema leo mchana wakati akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara za viongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa kutafuta Suluhu
  Viongozi mbalimbali wa kidini pamoja na Taasisi mbalimbali za kiraia hatimaye wamesaidia kutokomeza UKUTA kwa kuuomba uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuahirisha Oparesheni hiyo iliyopangwa kufanyika Septemba mosi nchi nzima. 

  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya CHADEMA Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,  Freeman Mbowe amesema  Viongozi hao wakuu wa kidini wamewaomba na kuwasihi katika vikao mbalimbali walivyokaa pamoja nao na kusema tunaheshimu viongozi hao. 

  Mbowe amesema wanawapa muda wa wiki mbili au tatu ili waonane na Rais Magufuli kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu wa kisiasa na kuliepusha taifa na machafuko ya kisiasa. 

  Pia amesema Viongozi wa Taasisi za kiraia kama vile Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Wahariri na Jukwaa la Katiba nao wamewasihi kuahirisha UKUTA kwa muda ili kutoa fursa kwa jitihada za mazungumzo na majadiliano kufanyika. 

  "Sisi CHADEMA tunatambua na kujali haki zetu za kisiasa kama zilivyofafanuliwa katika Katiba na Sheria za nchi yetu. Hata hivyo tunajali na kuheshimu kwa kiasi kikubwa zaidi haki za Watanzania ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yao" amesema Mbowe

  Amesema wanawaomba kuwatangazia viongozi weo wa ngazi zote CHADEMA, pamoja na wanchama,wafuasi na Watanzania wote kuhairisha kwa mwezi mmoja mikutano na maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho Septemba Mosi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Doto M.James aliyeteuliwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.

  0 0


  Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kupambana na Trakoma (ITI) akizungumza na washiriki wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma kuhusu uendelezaji wa juhudi za kuwaelimisha wananchi na kutoa tiba katika maeneo  yanakabiliwa na ugonjwa Trakoma kwa nchi washiriki wa mkutano huo kutoka Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Eritrea, Sudani na Sudani Kusini.
  Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Upendo John Mwingira akiwasilisha kuhusu mkakati wa kukabiliana na Trakoma kwa kuyafikia maeneo yasiyofikika kirahisi ya jamii za wafugaji nchini Tanzania wakati Mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo  unaofanyika  jijini Arusha. Wananchi kutoka Jamii za wafugaji kutoka nchi washiriki wa mkutano huo bado wanakabiliwa na changamoto ya ugonjwa wa Trakoma.

  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Frida Mokiti akichangia wakati wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma jijini Arusha.
  Mshiriki wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma Kutoka nchini Kenya Dkt. Rebecca Oenga akitoa uzoefu wa nchi ya Kenya katika kukabiliana na Trakoma  kwenye maeneo ya mipakani  ya jamii za wafugaji.
  Afisa Afya kutoka Kaunti ya NAROK nchini Kenya Daniel Sironka akitoa mchango wake kuhusu namna anavyowaelimisha wananchi wa eneo lake kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Trakoma wakati wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma jijini Arusha.
  Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Sightsavers, Michael Kelly (katikati) akisisitiza jambo kuhusu ushiriki wa Sightsavers katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma wakati wa mkutano wa pili wa
  mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma jijini Arusha.
  Washiriki wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Arusha.
   Washiriki wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Arusha.


  Washiriki wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma kutoka Tanzania wakiwa katika majadiliano kabla ya kuwasilisha taarifa ya pamoja kuhusu maeneo ya utekelezaji katika mapambano dhidi ya Trakoma.
  Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.

  0 0

  Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilimu Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu (kushoto),akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fasta Fasta, Prasada Acharya waandaaji wa Tamasha la Pamoja Carnival linalotarajiwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, wakati wa utambulisho wa huduma ya usafiri wa haraka na salamakwa njia ya mtandao jana


  Viongozi wa ambao ni waandaaji wa Tamasha la Pamoja Carnival wakifuatilia maelezo kuhusu tamasha hilo, wakati yakiwasilishwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.


  0 0


  Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia), akirejesha kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo katika ofisi za CCM hii leo.

  Na BMG

  Nzwalile ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe Baraza Kuu Chadema Taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Chadema Mkoa wa Mwanza, amefikia uamuzi huo baada ya jana kujivua vyeo hivyo.

  Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na kwamba Chadema imepoteza mwelekeo kwani kimekuwa kikiibuka na oparesheni za kuichonganisha serikali na wananchi huku pia demokrasia ikikosekana ndani ya chama hicho.

  "Kama ni udikiteta basi mimi niseme Chadema ndiko kuna udikiteta kwani zaidi ya mara tatu nimemsikia Lowasa (Edward Lowasa, aliyekuwa mgombea urais 2015) akisema yeye ndiye mgombea urais mwaka 2020, kwa kikao gani". Amesema Nzwalile na kuongeza kwamba yale mambo yote mabaya yaliyokuwa yakifanyika ndani ya CCM yamenyooshwa hivyo hakuna haja ya yeye kuendelea kukaa Chadema.

  Amesema atazunguka Wilaya zote ili kuhakikisha anawarejesha wengine ndani ya CCM huku akiwa na jukumu moja la kuubomoa Ukuta unaoelezwa kujengwa na Chadema kwani ni ukuta wa tope hivyo atatumia tu maji kuubomoa.

  Nzwalile amekaribishwa ndani ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo, ambaye pia amewakaribisha makada wengine wa upinzani kuhamia CCM akisema kwamba chama hicho kinaendesha mambo yake kidemokrasia.
  Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akipokea kadi ya Chadema ya aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (katikati).
  Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia).

  Soma HAPA Taarifa ya awali.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC). Bw. Gerson Partinus Msigwa,aliyethibitishwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC).

  Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika wadhifa huo.

  Kabla ya uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015.

  Jaffar Haniu
  Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi.
  Dar es Salaam
  31 Agosti, 2016

  0 0

  Mapema asubuhi ya leo, watu wanaodaiwa kuwa ni Madalali wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) wamefika ofisi za Gazeti la kila siku la Tanzania Daima zilizopo katika makutano ya Mtaa wa Mkwepu na Indraghand na kuwatolea vyombo vyote nje kufuatia deni la muda mrefu la kodi ya pango wanalodaiwa bila kulipwa. Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Neville Meena amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wako kwenye Msukosuko mkubwa sana sasa ila wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unaendelea kufanyika kama kawaida. 
  Sehemu ya Wafanyakazi wa Gazeti hilo wakiwa nje ya Ofisi huku wakitafakari namna ya kufanya.
  Vyombo vya Ofisi hiyo vikiwa nje.


  0 0

  .
  Mkuu wa Kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC Silas Matoi akifafanua kuhusu matumizi ya kadi ya benki hiyo ya ‘Visa travel Money’ inayomwezesha mteja kufanya malipo mitandaoni kwa urahisi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini.
  (Toka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi Silas Matoi wakionyesha tuzo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliyopewa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania. Mkutano na waandishi wa habari umefanyika katika makao makuu ya benki hiyo mapema leo jijini Dar es salaam.
  (Toka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi Silas Matoi wakionyesha Tangazo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) lenye maelezo kamili kuhusiana na tuzo ya Visa waliyopewa hivi karibuni baada ya benki yao kuongoza katika miamala mitandao.


  Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi. Joyce Malai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Kushoto) ni Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini. Mkutano huo umefanyika katika makao makuu ya benki hiyo mapema leo jijini Dar es salaam.


  Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC Silas Matoi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi.Joyce Malai na (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini.
   Jitihada za BancABC katika ubunifu,kuendeleza na kufanikisha usalama wa miamala  matandaoni nchini Tanzania, imetambuliwa kwa tuzo ya Visa kuthibitisha ubora wa huduma yake mitandaoni.
  Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo, Bi. Joyce Malai alithibitisha taarifa hiyo alipozungumza na vyombo vya habari mapema leo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

  “Tunafurahi kupokea tuzo hii licha ya ushindani wa masoko uliopo, hii inaonyesha ni jinsi gani tumejidhatiti kuhudumia wateja wetu na kuwarahisishia kufanya miamala ya kifedha,” alisema Bi. Malai.

  Aliongeza kuwa katika jitihada hizi za kuboresha miamala salama mitandaoni,  mtu yeyote anaweza kumiliki  kadi hii  ya Visa bila kujali kama anayo akaunti ya BancABC au la. Bi. Malai alifafanua kwamba kadi ya Visa ya BancABC ni rahisi kutumia kwani humhakikishia mteja ulinzi wa fedha zake na pia huondoa usumbufu wa kutembea na pesa taslimu.

  Kadi hii inaweza kutumika kufanyia miamala mbalimbali ya kifedha kama vile kulipia tiketi za ndege pia kulipa posho na mishahara kwa wafanyakazi, kulipa ada za shule na kujikimu kwa wanafunzi, mikopo na misaada kwa serikali na mengineyo.ili kupata kadi hii mteja anahitajika kuwa na  kitambulisho halisi na kisha kujaza fomu zinazopatikana katika tawi lolote la benki hii.

  Aliongeza kwamba wateja wanaweza kuweka fedha kwenye kadi hiyo kwa kutumia huduma mbalimbali za kutuma pesa kama vile TIGOPESA, AIRTELMONEY au M-PESA pamoja na benki zingine zilizopo Tanzania.

  “Tunaamini kwamba upekee wa huduma hii ndicho kilichowavutia wateja na hivyo kusababisha ushindi wa tuzo ya Visa,” alisema. Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini alisema, kadi hiyo inaweza kutumika pia kwa fedha za mataifa mbalimbali kama Shilingi ya Tanzania, Dola ya Kimarekani, Euro na Randi ya Afrika Kusini.

  “Licha ya kuwawezesha wateja kufanya biashara mitandaoni, Mteja anaweza kutumia pesa zake kwenye Visa ATM Zaidi ya 400 nchini au Visa ATM Zaidi ya 1.3milioni duniani kote.

   Zaidi ya hapo Visa inamawakala Zaidi ya 1000 Tanzania na mawakala Zaidi ya 35 milioni duniani kote. Kupata kadi hii tutumie barua pepe customercaretz@bancabc. com.
   
  Atlas Mara iliinunua BancABC Juni 2014 huku ikizidi kujitanua Tanzania, Botswana, Mozambique, Zambia na Msumbiji. Baada ya hapo ilinunua benki mbili nchini Rwanda (BR Commercial na BPR ambazo zinaendelea kukamilisha mchakato wa kuungana).

  Atlas Mara iliorodheshwa katika Soko la Hisa London, mwezi Desemba 2013. Ndoto za kampuni hii ni kuanzisha taasisi kubwa ya kifedha Kusini mwa Sahara kupitia uzoefu wake, umahiri na upatikanaji wa mitaji, ukwasi na uzalishaji fedha. Malengo yakiwa ni kujumuisha ujuzi wa taasisi za dunia nzima na mitazamo ya kina ndani ya Afrika, hivyo kusaidia kukuza uchumi katika nchi zinazo hudumiwa na Kampuni hii.

  0 0

  A spacious office space is available for rent at Hugo House Kinondoni (Plot no 22).

  It has 5 rooms which are well partitioned and suitable for any executive office setting with space of 72 SQM. 
  The office is fully carpeted and has Split units air conditioners.
  Available for immediate occupancy.

  For inquiry please contact 0713 465 336 or 0713 274 535

  0 0

  OR-TAMISEMI inatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016. Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza. 

  Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740 sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara. 

  Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2015 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii. 

  Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
  Imetolewa na Katibu Mkuu,
  OR-TAMISEMI


  Tumia link hii kupata matokeo : >> Waliochaguliwa kidato cha tano awamu ya pili 2016
  Link ya Matokeo ya awali : >> Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016

  0 0  0 0

   Maneja Usambazaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Robert Noel (kulia) akionesha kwa mmoja wa wateja baadhi ya bidhaa za mawasiliano ya intaneti zinazotolewa na kampuni hiyo katika maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za TTCL, kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wateja waliotembelea maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akihudumiwa kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Kikosi cha wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kilichofanya maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa wadau kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akitoa ufafanuzi kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa wadau kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya kikosi cha wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kilichofanya maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa wadau kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam kikiwa katika picha.

older | 1 | .... | 956 | 957 | (Page 958) | 959 | 960 | .... | 1897 | newer