Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Serikali, wadau wakutana kujadili mapendekezo ya kulinda na kukuza Haki za Binadamu Nchini

$
0
0

Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Masuala ya Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Nkasori Sarakikya akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi mbalimbali za Kiraia mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kujadili mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi hiyo Bi. Sarah Mwaipopo.
Mjumbe kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Bi. Blandina Sembu akichangia hoja kwenye eneo la watu wenye ulemavu na masuala ya uandishi wa Habari wakati wa kikao cha kujadili mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Serikali,kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo imefanya kikao maalumu cha wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na asasi za kiraia kwa lengo la kuwafahamisha kuhusu kujadiliwa kwa Taarifa ya pili ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya Haki za Binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Period Review).

Vilevile kikao hicho kitatoa fursa ya kujadili kwa kina na kuyapatia misismamo ya awali kama wadau, mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa Serikali mnamo mwezi Mei 2016 , na kuainisha sababu ambazo zinafaa kwa mapendekezo yaliyoahirishwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu kabla ya kupitishwa rasmi kuwa taarifa ya nchi itakayowasilishwa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kabla ya terehe 9 Septemba 2016.

Akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa masuala ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali, Bi Sarah Mwaipopo ameeleza kuwa kikao hicho ni hatua muhimu kkatika mfumo wa maandalizi ya taarifa za usimamizi na utekelezaji wa haki za binadamu nchini ambao umekua ukishirikisha wadau wote kutoka Wizara,Idara na Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi zisizo za kiserikali ambapo amesisitiza wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano na kutimiza wajibu wao ipasavyo.

“Sote tutambue na kuzingatia kwamba masuala ya haki za biandamu ni mtambuka na kila mtu ana wajibu wa kutekeleza na kuyasemea katika eneo lake”alisema Bi Sarah

Halikadhalika,kwa niaba ya Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekua ikiratibu kikamilifu maandalizi na uwasilishwaji wa Taarifa zote za masuala yote ya haki za binadamu kwa kuzingatia mikataba ya Haki za Binadamu ambayo Tanzania imeridhia na utekelezaji wa jukumu hili umeanishwa katika Ibara ya 59(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Sura ya 268, kifungu cha 14(f) ambayo ni;

kuratibu masuala ya uaandaaji na utoaji wa taarifa za nchi za utekelezaji wa Mikataba ya Kikanda na Kimataifa ya haki za binadamu amabyo nchi imeridhia ikiwemo masuala yote ambayo yanahitaji utolewaji wa taarifa za aina hiyo na kuziwasilisha kwenye vyombo husika vya Kikanda na Kimataifa kwa ajili ya majadiliano.

Kikao hicho ambacho kitafanyika kuanzia tarehe 30 -31 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam kimehudhuriwa na wadau kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jukwaa la Katiba Tanzania,Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania,MISA-TAN,PINGOS’ FORUM,Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama ya Tanzania,Uhamiaji,Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora, Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Shrikisho la Watu wenye ulemavu Tanzania( SHIVYAWATA) na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Kwa upande wa Zanzibar ni Wizara ya Kilmo na Mifugo, Wizara za Afya,Mifugo, Kazi,Vijana Wazee,Ofisi ya Mwansheria Mkuu, Jumuia ya Wanawake Wanasheria,Tume ya Uchaguzi

Utaratibu wa Mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Periodic Review) wa masuala ya haki za binadamu ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2006 kwa lengo la kuzifanyia mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ikiwa miongoni, kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa masuala ya kulinda na kukuza haki za binadamu nchini mwao.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MO NA KUFANYA MAZUNGUMZO JIJINI DAR

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji wa Makampuni ya  Mohammed  Enterprises Tanzania Limited (METEL), Bw. Mohammed Dewji, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Maandamano ya UKUTA hayawezi kufanyika-Prof.Benson Bana

$
0
0
Prof.Benson Bana


Jonas Kamaleki, MAELEZO

Maandamano ya UKUTA hayawezekani kwani hii ni ndoto ya mchana na hayana msingi wowote wala tija kwa wahusika hata kwa Taifa.

Hayo yalisemwa na Muhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Benson Bana katika mahojiano maalum.

“Wanaotaka kuandamana wanajidanganya na kuwalaghai wenzao kwani kufanya operesheni ni suala la dola na si la mtu au kikundi cha watu, hivyo maandamano hayo hayawezekani kabisa, alisema Prof. Bana.

Ameongeza kuwa wanaojiita UKUTA ni kwamba Mhe. Rais John Pombe Magufuli amewanyima ajenda kwani utendaji wake umezidi fahamu zao na kuwafanya waanze kutapatapa wasijue nini la kufanya.

Prof. Bana amesema kama viongozi wa UKUTA ni waungwana inabidi watamke wazi kuwa wametafakari na kuona kuwa maandamano hayana maana hivyo wameamua kuyasitisha nchi nzima.

Kuhusu utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, Prof. Bana alisema ni Serikali yenye maamuzi ya uhakika na inayowajali watu wote bila kujali itikadi zao za vyama, dini wala makabila hivyo inabidi watanzania waipende na kuiheshimu.

“Rais Magufuli utendaji wake ni wa kuigwa na viongozi wengi Duniani kwani anafanya maamuzi ya uhakika ikiwemo kukuza uchumi kwa kukusanya kodi na kuziba mianya ya ubadhirifu wa mali ya umma, alisema Prof. Bana.

Pamoja na kuwa Rais Magufuli amekuwa madarakani kwa kipindi kifupi, viashiria vyote vinaonyesha kuwa ni kiongozi imara na shupavu kutokana na mambo makubwa ambayo ameyafanya kwa kipindi hiki kifupi. Katika kipindi hiki kumekuwepo na nidhamu katika utumishi wa umma, kodi inakusanywa kwa kiwango kikubwa na elimu ya msingi inatolewa bure kama Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala inavyosema, alisema Prof. Bana.

Aidha, Prof Bana amesema kuwa wanaomlaumu Mhe. Rais ni wale ambao hawajitambui na labda wanaona mianya ya ubadhirifu anayoendelea kuiziba, wao wanakosa mapato, vinginevyo Rais anafanya vizuri katika kuliongoza Taifa.

“Rais Magufuli yuko sahihi kwa jinsi anavyosimamia vipaumbele vya Serikali ikiwemo elimu bure, kukusanya kodi na kuzuia mianya ya rushwa pia dhamira ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda, alisema Prof. Bana.

Prof. Bana ameelezwa kusikitishwa kwake na watu wanaomkosea Rais heshima na kumwita “Dikteta Uchwara.”Amesema watu hawa inabidi wazalendo wakemee kabisa vitendo vya namna hii ambavyo ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi.

Akizungumzia uamzi wa kuhamia Dodoma, Prof. Bana alisema kuwa ni uamzi wa busara kutekeleza azma ya Serikali ya miaka takribani arobaini iliyopita. Hivyo kuhamia Dodoma kutaufanya mji huo kuendelea zaidi kimiundombinu na kiuchumi.

Aliongeza kuwa mikoa ya jirani nayo itanufaika kiuchumi kwani itakuwa karibu na makao makuu ya nchi na pia kuhama huko kutatoa fursa kwa Dar es Salaam kukua zaidi kibiashara.

Prof. Bana ameitofautisha Serikali ya Awamu ya Tano na awamu nyingine nne zilizopita kwa kutokuwa na kigugumizi katika kufanya maamuzi yake ikiwemo hii ya kuhamia Dodoma, kuondoa wabadhirifu katika utumishi wa umma na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na fedha hizo kutumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama afya, elimu na miundombinu.

TAARIFA KWA UMMA YA UTEUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO (NDC)

WAZIRI MKUU APOKEA HUNDI YA SH. MIL. 50 KUTOKA NSSF ZA UKARABATI NA UJENZI WA SEKONDARI YA LINDI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea hundi  ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu  wa NSSF,  Profesa Godius Kahyarara kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sokondari ya Lindi iliyoungua moto. Makabidhiano hayo yalifanyika  Ofisini kwa Kwaziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016.
  Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza badaa ya kupokea hundi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi ambayo iliungua moto.  Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara, Wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary Satura na wapili kushoto ni Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Meya wa manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo akizungumza baada ya  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 kwa ajili ukarabati na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua Moto . Makabidhiano ya hundi hiyo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara na wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary Satura.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa NSSF baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 50  na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara (kushoto), Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 30. 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na watumishi wa NSSF baada ya kukabidhiwa hundi ya  Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa  Godius Kanyarara  (kushoto), Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waandishi wa habari waliohudhuria katika tukio la NSSF kumkabidhi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  hundi ya sh. milioni 50 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua . Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jjini Dar es salaam Agosti 30, 2016.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 50 kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua moto usiku wa kuamkia Julai 10 mwaka huu.

NSSF imetoa msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake iliyoitoa Julai 17, 2016 katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa majengo ya shule ya hiyo iliyoendeshwa na Waziri Mkuu .

Katika ajali hiyo, shule ya sekondari Lindi iliathirika kwa asilimia 34 ambapo vyumba tisa vya madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na fizikia yaliungua na kusababishia hasara ya sh. milioni 682.78.

Akipokea msaada huo leo (Jumanne, Agosti 30, 2016) Waziri Mkuu ameushukuru uongozi wa shirika hilo na kuwaomba wadau wengine waliotoa ahadi wazitekeleze ili waweze kukamilizsha ujenzi wa majengo hayo.

“Naamini fedha hizi zitakwenda kufanya kazi ambayo NSSF wameikusudia. Na leo hii naikabidhi kwa Meya wa Manispaa ya Lindi pamoja na Mkurugenzi wake ili waende kuzifanyia kazi,” amesema.

Baada ya kukabidhiwa hundi hiyo na Waziri Mkuu, Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo amelishukuru shirika hilo kwa kutimiza ahadi waliyoitoa siku ya harambee na kwamba fedha hizo hazitapotea kwa sababu zinaenda kutumika katika malengo yaliyokusudiwa.

Meya huyo amesema baada ya kukamilisha ujenzi wa shule hiyo wataanda hafla na kuwaita wadau wote waliotoa michango yao kwa ajili ya ujenzi huo ili wakaone matumizi ya michango waliyoitoa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa shirika hilo wa kusaidia jamii katika mambo mbalimbali kwa mujibu wa sera iliyowekwa na shirika hilo.

“NSSF imekuwa kinara kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ambapo imejiwekea sera ya kusaidia katika sekta za elimu, afya na huduma nyingine muhimu za kijamii,” amesema.

Prof. Kahyarara amesema misaada hiyo haiathiri michango ya wanachama wa mfuko huo na mafao yatolewayo kwani hutokana na faida inayopatikana kwa uwekezaji makini wa mfuko huo.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMANNE, AGOSTI 30, 2016.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WA CUBA NA INDIA IKULU DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya  mazungumzo na balozi wa Cuba Mhe Jorge Lopez Tormo nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Adelhem Meru akisalimiana na balozi wa Cuba nchini Mhe Jorge Lopez Tormo kabla ya kufanya naye  mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (aliye nyuma).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza  balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016.

TANESCO KUBORESHA KITUO KIKUU CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME CHA ILALA, MAENEO KADHAA KUATHIRIKA NA UPATIKANAJI UMEME JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0






NA K-VIS MEDIA

SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuuarifu umma kuwa kutakuwepo na katizo la umeme KUANZIA Septemba 3, 2016 kwenye maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza cha Msongo wa Kilovolti 132 cha Ubungo-Ilala.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano ya Shirika hilo, Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016, katizo hilo la umeme litaanza rasmi Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.

Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni pamoja na eneo lote la katikati ya jiji (City centre), Maeneoyote ya Upanga, maeneo yote ya Kariakoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Mbagala, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Ilala, Maeneo yote ya Chang’ombe, Maeneo ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Unilever, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jamana printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate pamoja na maeneo ya jirani.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa ili jiji la Dar es Salaam lipate umeme ulio bora na wa uhakika, Shirika laUmeem Tanzania (TANESCO), limemruhusu mkandarasi, (TAKAOKA), kubadilisha vikombe na nyaya na kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa za njia mbili (Two-lines) za Msongo wa Kilovolti 132.

Kuboresha vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Ilala na Ubungo kwa kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa zaidi.

Kubadilisha vifaa vya kupima umeme kwenye njia mbili (Two-lines) za Ubungo-Ilala.

NMB yawakumbuka watoto wenye usonji, yawapa msaada wa vifaa vya masomo

$
0
0
Pamoja na kuwa bora utoaji wa huduma za kibenki lakini pia benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inakuwa pia bora katika kusaidia jamii na katika kudhihilisha hilo imetoa msaada wa vifaa vya kutumia darasani na vya michezo kwa watoto walio na usonji (autism) ambao wanasoma katika shule ya msingi Mbuyuni, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu msaada huo, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo alisema wameamua kutoa msaada kwa shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye usonji kusoma katika mazingira mazuri hasa kutokana na hali zao jinsi zilivyo.
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya shuleni kwa wanafunzi wa usonji katika shule ya Msingi Mbuyuni.

"NMB kila mwaka tunatenga asilimia moja ya faida ambayo tunaipata katika kusaidia jamii, tumeshatoa misaada mingi kama madawati na sasa tuliona tuwasaidie watoto hawa na tunaamini msaada wetu utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa," alisema Bi. Bishubo.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi aliwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia shule ya Mbuyuni na kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo kwa kutoa msaada katika shule zingine zilizo na mahitaji.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akiwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia ambao unakadiriwa kuzidi Milioni 7.

Alisema licha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali lakini bado inahitaji wadau wengine wa kusaidiana na kama kunakuwa na wadau kama NMB ambao wanajitoa kusaidia jamii basi wanakuwa wadau wa ukweli ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo.

"Kwa nia yenu ya kusaidia jamii basi nyie mnaipatia kabisa serikali sababu inajitahidi kuleta elimu bora na hata kwa watoto hawa ambao bado kuna changamoto ya vifaa kwahiyo sisi tuwashukuru kwa msaada wenu na msisite tena kutusaidia siku tukiwafata kwa kuomba msaada," alisema Mushi.

Na Rabi Hume, MO BLOG
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Dorothy Malecela akitoa neno la shukrani kwani niaba ya uongozi wa shule na wanafunzi. (Picha zote na Rabi Hume - MO BLOG)

Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akimshukuru Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo kwa msaada ambao wamewapatia.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo wakicheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.

Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mwonekano wa baadhi ya vifaa vya michezo ambavyo NMB imetoa msaada kwa Shule ya Msingi Mbuyuni.

WALIOKOPA SACCOS NA HALMASHAURI WAREJESHE MARA MOJA: MKUU WA WILAYA MUFINDI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William ametoa muda wa siku 15 kwa watu binafsi na vikundi vilivyokopeshwa kupitia Saccos pamoja na Fedha za Halmashauri Wilayani humo, wawe wamerejesha mikopo yao mara moja na kuonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wakopaji pamoja na wadhamini wao endapo watakaidi kutekeleza agizo hilo.

Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya wilaya ya Mufindi imefafanua kuwa, mkuu wa wilaya ametoa agizo hilo baada ya kubaini uwepo wa vikundi vingi pamoja na watu binafsi waliokopa kwenye mfuko wa Halmashauri na Saccos pasipo kurejesha licha ya muda wa kukamilisha marejesho ya mikopo hiyo kupita.

“Natoa fursa kwa yeyote ambaye alikopa aidha kupitia mfuko wa wanawake na vijana wa halmashauri au saccos, awe amerejesha kwa hiali ifikapo tarehe 15 ya mwezi ya mwezi wa 9, baada ya hapo haitakuwa tena suala la mkopo ilikuwa suala la uhalifu na uwizi”

Aidha, mkuu huyo wa Wilaya amesema kunahaja ya kuvitathimini upya vigezo vya utoaji mikopo kwani baadhi ya viongozi wa Saccoss wamewakopesha watu ambao hawana udhibiti nao hivyo, pesa nyingi ziko mikononi mwa watu jambo ambalo linawanyima fursa ya kukopa wananchi wengine.

Katika hatua nyingine, Mh. Jamhuri William amewataka wananchi kuzingatia na kudumisha amani iliyopo nchini huku akipiga marufuku vyama au kikundi chochote Wilayani Mufindi kujihusisha na maandamano yaliyopangwa kufanyika September mosi.

MZEE MAHOKA AWAKANYA VIJANA KUSHIRIKI MAANDAMO YA UKUTA

$
0
0


Mzee Mohamed Hamisi Mahoka ‘Mzee Chinga’ Muasisi wa Upinzani Mkuranga

Na Wilson Makubi Mkuranga

Muasisi wa chama cha Wananchi C.U.F Wilaya ya Mkuranga Mzee Mohamed Hamisi Mahoka , ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisasa Wilaya ya Mkuranga, maarufu kwa jina la Mzee Chinga amewaasa Vijana wa Wilaya Mkuranga hasa kwa Kata zilizo pembezoni mwa Mji wa Dar es Salaam kuacha kushiriki katika maandamano hayo ambayo hayana tija kwa Chama wala Taifa kwa ujumla,

Akiongea na Vijana Nyumbani Kwake Kitongoji cha Kisasa Kijiji cha Mlamleni Kata ya Tambani Wilaya Mkuranga alisema

‘kwamba baadhi ya Wanasiasa wamekosa ajenda za kimaendeleo kwa ajili ya Watanzania, hivyo wana tafuta sababu ya kujijenga kisiasa ili kujipatia umaarufu’’ pia alisisitiza kwamba wao kama Wazee wa Upinzani watafanya siasa za upinzani zenye tija ili kunusuru umma qwa Watanzania na wanamuomba Mh Rais Jonh P. Magufuli ashighulikie kero za Wananchi bila ya woga,kwa sasa sijaona Mtu anayefanana na Magufuli kwa Nafasi ya Uraisi, Yeye anatosha’’

Vijana Niwambie enzi za ukoloni hamkuwepo kiasi kwamba hamjaona vurugu za serikali sasa mnataka kuijaribu serikali yenu, nawashauri Msishiriki jambo msilolijua, Raisi Magufuli amefanikiwa kupambana na hoja ya ufisadi hivyo ambayo ilionekana kuwa ni ngao ya upinzani katika majukwaa, sasa hawana cha kusema wanatafuta sababu nyingine ili wasikike.

Mzee Chinga alimalizia kwa kusema kwamba ‘Ni vyema sasa Wabunge wanaotaka kuandamana wanapokuja majimboni mwetu watuambie wamefanya nini katika muda waliokaa madarakani na sio kututia matatizoni, wajibu wao ni kuleta maendeleo katika majimbo lakini tofauti na wabunge wa Chadema ambao wao lengo kubwa ni kubishana na serikali, hii ni dalili kwamba uwezo wao wa kushughulikia kero za Wananchi ni Mdogo.

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia. Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi. Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .
Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .



Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya .

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI ya Taifa ya Ruaha

Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu linakivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo amewataka wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.

Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .

LEO KATIKA "TUNATEKELEZA" TBC1

Maonesho ya Bashara ya Afrika Mashariki yafunguliwa rasmi Jijini Mwanza.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, hii leo akifungua Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 

Maonesho hayo yameandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, yalianza Agosti 26,2016 na yanatarajiwa kufikia tamati Septemba 04,2016 katika viwanja wa Rock City Mall.
Na BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mara, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Picha ya pamoja.

Wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamehimizwa kuchangamkia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika soko la pamoja la nchi hizo kutokana na soko hilo kuwa na idadi kubwa ya wateja.

Akifungua maonesho ya 11 ya biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza,Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema soko lililopo kwenye nchi hizo lina zaidi ya wateja milioni 140 na hivyo likitumika vizuri litatoa fursa ya kuuziana bidhaa wenyewe kwa wenyewe.

Kwenye hotuba ya ufunguzi iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt.Leonard Massale,mkuu huyo wa mkoa amesema badala  ya wafanyabiashara hao kutegemea masoko ya nje yanayofikika kwa gharama kubwa,wanapaswa kuuziana bidhaa ndani ya nchi za Afrika Mashariki na hivyo kuinua uchumi wa nchi hizo.

Aidha amewahimiza waandaaji wa maonesho hayo chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo nchini, TCCIA, kuyatangaza zaidi ili yavutie makampuni mengi kutoka nchi zingine.

Katika hotuba yake Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, amesema licha ya kuandaa maonesho hayo kwa miaka 11 mfululizo bado wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na eneo linalofaa kwa ajili ya maonesho hayo na hivyo kulazimika kuhama mara kwa mara na kuiomba serikali kuharakisha upimaji wa eneo la maonesho Nyamuhongolo ili kujenga majengo ya kudumu.

Maonesho ya mwaka huu yanashirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda, China na wenyeji Tanzania ambapo kuna mabanda ya bidhaa mbalimbali pamoja na wanyama hai.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

WAZIRI NAPE NNAUYE ALIPOFUNGUA MASHINDANO YA MICHEZO YA UMOJA WA VYAMA VYA WALIMU KUSINI MWA AFRIKA (SATO).

Yaliojiri Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Nchini Mauritius

$
0
0
Viongozi Wakuu pamoja na Sekretarieti ya Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wake, katikati  mwenye suti Waziri Mkuu wa Mauritius Sir Anerood Jugnauth. 
Ujumbe wa Tanzania walioshiki Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid katikati kulia Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mussa Zungu  na kushoto Dk Raphael Chegeni.Kutoka kushoto Maryam Rajab, Mbarikiwa Masinga, Mhe,Maria (MB) Mhe. Raphael Chegeni (MB)Mhe Juma Hamad Omar (MB) Mhe Simai Mohammed Said (BLW)  Aziza Makwai.  
 
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akibadilishana mawazo na Wajumbe kutoka Tanzania  kabla ya kuaza kwa Mkutano huo.

Mjumbe wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai Mohammed Said, akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo inayozungumzia Suala la Nishati kwa Bara la Afrika, uliofanyika nchini Mauritius Balaclava. 
Spika wa Baraza la Wawkilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa na Wajumbe kutoka Tanzania wakishirika katika Mkutano huo wakifuatilia Mada zinazowasilishwa na Wajumbe wakati wa Mkutano huo nchini Mauritius
Mtoto wa Mfalme wa Lesotho HRH Prince Seeiso B Seeiso, Raisi wa Senate na Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara kutoka Bunge la Falme ya nchi ya Lesotho akichangia mada iliyowasilishwa na Tanzania inayohusiana na nishati ya umeme. 
 Mjumbe wa Sekterieti kutoka Tanzania Aziza Mwakwai kushoto akimsaidia Spika wa Rwanda wakati wa Kikao hicho za kuwasilisha Mada kwa Nchi husika. 
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakipitia makabrasha yao kabla ya kuaza Kikao cha Kanda ya Afrika Mashariki. katika ukumbi wa Hoteli ya Meridian Mauritius

Mjumbe wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Spika wa Bunge la Mauritius na Rais wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Hon Mrs.Santi Bai Hanoomanjee. kulia kwake Katibu wa Bunge la Mauritius. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Kenya Mhe.Justin Muturi, Spika wa Uganda Mhe Rebecca Kadaga na Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu akimwakilisha Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndungai. 
 Spika la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid (katikati) akifurahia jambo wakati wakibadilishana mawazo na Wajumbe wa Mkutano huo, kushoto Spika wa Bunge la Uganda Mhe. Rebecca Kadaga na Mhe Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar, wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano la Tanzania ambaye pia Katibu wa Nchi za Jumuiya ya Madola Dk Thomas Kashillilah wa tatu kutoka kulia mwenye suti, akizungumza na Wajumbe wa Sekterieti ya Jumuiya ya Kanda ya Afrika wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano huo uliofanyika Nchini Mauritius. 
Mwakilishi kutoka Zanzibar Mhe Simai  Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano huo, pamoja na Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi mwenye kaunda suti pamoja wa Wawakilishi kutoka Kisiwa cha Rodrigues Mauritius.
Waziri wa Afya kutoka Nchini Botswana Hon Dorcas Makgato akiwa na Mjumbe kutoka Tanzania Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiwa na Mhe Simai Mohammed Said wakiwa katika eneo maarufu la Kitalii nchini lijulikanali kwa jina la Trou Aux Cerfs (Valcano in Vacoas - Phoenix, Mauritius).
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akiwa na Wajumbe wa Mkutano huo wakitembelea Kiwanda cha Kufulia Umeme na Sukari Nchini Mauritius wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kiwanda hicho cha Omnicane Limited. 
 Msanii wa Sanaa za kutengeneza Boti kwa ajili ya Watalii wanaotembelea Nchi hiyo akiwa katika harakati za kutengeza za boti zinazopatika katika eneo la Curepipe Mauritius hutengenezwa kwa mbao kama majahazi ya Zanzibar. 

 Sanamu la pili refu duniani baada la Nchini India lijukanali kwa jina Lord Shiva Nchini Mauritius likiwa katika maeneo ya Ganga Talao.
Mandhari ya kutoka juu ya bustani ya Trou Aux Cerfs.
Imetayarishwa na Zanzinews.com

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd, Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipeana mkono wa shukurani na Nd,Hassan Khatib Hassan,baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshughulikia Idara Maalum za SMZ,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

IKUNGI HALF MARATHON 2016 KUANZA KURINDIMA WILAYANI IKUNGI JUMAMOSI WIKI HII

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielezea dhamira ya kuanzishwa kwa Ikungi Half Marathon ofisini kwake.

Na Mathias Canal, Singida

Ni kama vile kuwa na kiu kizito kinachohitaji maji ya kunywa na kisha maji yakakutikana kusikojulikana, ndivyo itakavyokuwa Wilayani Ikungi Mkoani Singida mara baada ya kutangazwa mashindano ya riadha yanayojulikana kama Ikungi Half Marathon 2016.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika Vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi.Akizungumzia dhamira ya kuanzishwa kwa mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa itakuwa ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika Wilaya hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Alisema kuwa Mashindano ya mbio ndefu yenye umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30 waishio Wilayani Ikungi na yatafanyika kila mwaka ili kuinua hamasa ya Mchezo wa riadha huku yakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 200, mita 400 na mita 800.

Mashindano hayo yataanzia katika ngazi ya Vijiji Septemba 3, 2016, ngazi ya Kata itakuwa ni Octoba Mosi, Ngazi ya Tarafa ni Octoba 15, 2016 na kwa ngazi ya Wilaya itakuwa ni Octoba 29, 2016.

Dc Mtaturu alisema kuwa kuanzishwa kwa kuzinduliwa kwa mashindano hayo ni katika kuhakikisha Wilaya ya Ikungi inaibua changamoto katika sekta ya michezo nchini hivyo hiyo ni fursa muhimu kwa washiriki kujitokeza ili kuonyesha uwezo wao katika kusakata riadha.

Mtaturu alisema kuwa mwaka 2017 panapo majaaliwa wamejipanga kufanya mashindano ya Ikungi Marathon yatakayohusisha mbio ndefu za kilomita 42 ambapo jambo hili itakuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Ameeleza kuwa mashindano hayo pia yamedhamiria kuitambulisha Wilaya hiyo Kitaifa na Kimataifa kupitia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo mbalimbali hususani mashindano ya Riadha.

Aidha amewaomba vijana wote wenye umri uliofikia miaka 17 kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ili kuimarisha afya zao na kuachana na mawazo ovu yakiwemo yale ya kujihusisha na wizi na ujambazi, Ngono zembe pamoja na ubakaji.

Kwa upande wake Afisa michezo Wilayani Ikungi Abubakary Kisuda alisema kuwa mashindano ya ngazi ya Vijiji yatafanyika kwa lengo la kupata vijana watakaoshindana ili kushiriki mashindano ya ngazi ya Kata, ambapo mashindano ya Kata yatafanyika kwa lengo la kupata vijana watakaoshindana ili kushiriki mashindano ya ngazi ya Tarafa.

Kisuda alisema kuwa hili ni tukio la awali kabisa kuanzishwa Wilayani humo tangu kuanzishwa kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo miaka mitatu iliyopita hivyo litaibua hisia chanya na kuigwa na Taifa zima.

Serikali yapiga marufuku usafirishaji wanyama nje ya nchi.

$
0
0
Na Hassan Silayo, MAELEZO

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa serikali imepiga marufuku biashara ya kusafirisha wanyama hai nje ya nchi mpaka pale itakapowekwa misingi mizuri ili nchi iweze kunufaika na biashara hiyo.

Prof. Maghembe ameyasmea hayo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC 1 ambapo alisema Serikali iliamua kuangalia upya utaratibu huo wa kuuza wanyama hai na kuamua kusitisha biashara hiyo hadi pale taratibu na misingi mizuri ya biashara hiyo itakapowekwa.

“Ni kweli kulikuwa na utaratibu wa kuuza wanyama hai nje ya nchi bila kuiwezesha nchi kupata faida yoyote ile, hivyo kwa sasa kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara kwa maslahi ya taifa”.

“Haiwezekani uuze wanyama hai nje halafu anayenufaika ni yule anayenunua na kuiacha nchi bila faida yoyote ya uwepo wa maliasili hiyo, hivyo kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara hiyo hadi pale misingi mizuri ya kibiashara itakapowekwa na kuiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake, na nisisitize kwa sasa hata Chawa wa Tanzania hataweza kusafirishwa nje ya nchi”. Alisema Prof. Maghembe.

Aidha, Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na ujangili wa wanyama pori kama Tembo na Faru ikiwemo kukamata watu wote wanaohusika katika biashara hiyo na mpaka sasa wameshakamata baadhi ya watu akiwamo mwanamama anayejiita malikia wa pembe za ndovu ambaye alikuwa kinara katika biashara hiyo.

Prof. Maghembe aliongeza kuwa hatua hiyo imeonesha mafanikio kwani kwa kipindi cha hivi karibuni soko la mauzo ya pembe za ndovu nje nchi hasa bara la Asia ambao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa hizo yameshuka na hatua hiyo inatokana na mikakati iliyowekwa na Serikali.

Akizungumzia wizi katika mazao ya misitu Prof. Maghembe alisema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kupambana na wizi wa mazao ya misitu na imekubaliwa kuwa iwapo gari litakamatwa likiwa na mazao hayo bila kuwa na kibali, Serikali itataifisha gari hilo na wahusika watashtakiwa kama wahujumu uchumi.

Pia Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa utawekwa utaratibu wa magari yote yanayobeba mazao ya misitu kusafiri mchana kwenye gari lililo wazi ili kurahisisha ufuatiliaji na udhibiti wa wizi huo.

Serikali imeahidi kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki kwenye vijiji vilivyo pembezoni mwa misitu ili kuweza kudhibiti uchomaji moto kwenye kwenye maeneo hayo hali itakayowezesha pia utunzaji wa mazingira.

Magufuli Speeds tourism in Tanzania.

$
0
0
By Our correspondents-MAELEZO

THE number of tourist arrivals in Tanzania has rose rapidly despite the government’s decision to impose value added tax on tourism activities.

Critics had it that the number of tourist arrivals in the country would have gone done thanks to the decision by the government to impose VAT during the financial year 2016/17.

Minister of Tourism and Natural Resources Prof Jumanne Maghembe revealed at a live telecast “TUNATEKELEZA” aired with the cooperation between Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) and Tanzania Information Service (MAELEZO).

"Despite blames in tourism industry after the government started to levy Value Added Tax (VAT) in the tourism industry, but I can assure you, right now tourists have increased in earnings have grown by 22 percent more," said Minister Maghembe.

Minister Maghembe says, apart from different perspective of stakeholders in tourism industry tax increases that does affect many tourists especially given that Tanzania remains and unique attractions around."Our country has many tourist attractions that are not in any other country, This includes peace, hospitality and stability prevailing in the country, no tourist will be unable to cover the increase of only eight dollars, "said Minister Maghembe.

He also spent time explaining that his research in foreign countries demonstrates that Tanzania embassies leads in issuing visas for tourists compared to other countries in the regions of East Africa, especially in big cities like Berlin.Referring to the fight against poaching, Minister Maghembe said government efforts to invest in training and modern equipment also borne fruit after a decline in poaching significantly.

He said the Government has already suspected the biggest network of poaching and they have been arrested and while some have been sentenced to jail, He referred to one of the suspects of the network's biggest foreign nationals known by the name of "MALKIA WA PEMBE ZA NDOVU" and is in custody now.

"In this battle we have decided to consider poaching as terrorism or sabotage the economy. And we have arrested poacher’s bosses and their sponsors and still we continue to monitor and any time we will arrest them, "he said.

He added that the government also banned the harvesting of forest products, particularly logs without license and those would do so will be arrested, wealthy and particular car will be nationalized and the victims will be taken before court.

Statistics of tourists increased gives strength to the government of President Magufuli because since he has been in power he was stressing the importance of collecting taxes for the nation to be independent. In contrast to this attitude, some people do not believe that's possible.

CHRISTIAN BELLA KUWASHA MOTO SHINDANO LA MISS KINONDONI 2016, KESHO KUTWA UKUMBI WA DENFRANCES SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Washiriki wa shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 wakishuka kwenye gari Dar es Salaam leo walipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Mdhamini wao Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd Mikocheni.
Wanyange hao 20 wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya gari la kampuni hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Mr Rutha akizungumza na wanyange hao walipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo Mikochezni Dar es Salaam leo.
Warembo hao wakiwa mbele ya ghala zinamo hifadhiwa bia za Windhoek wakati wa ziara hiyo.
Warembo hao wakisubiri mkutano na wanahabari baada ya ziara hiyo.

Mshauri wa Miss Kinondoni, Boy George (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya shindano hilo. Kutoka kulia ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo,Constantine Mwafulilwa, Andrea Missana, Mratibu wa Shindani la Miss Kinondoni Rhamat George na Mwalimu wa warembo hao, Neema Chaky.
Maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa katika pozi. Kutoka kushoto ni, Mr Jerome, Ismail Mzava na Mr Rutha.
Mwalimu wa Wanyange hao, Neema Chaky (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanyange hao katika tabasamu.
Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Viongozim meza kuu na wanyange hao wakionesha bia ya windhoek.

Na Dotto Mwaibale


Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi hapa nchini Cristian Bella anatarajiwa kuwasha moto katika shindano la kumsaka Malkia wa Ulimbwende.

Kanda ya Kinondoni linatarajiwa kufanyika kesho kutwa Ijumaaya katika Ukumbi wa Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwa kutanisha warembo hao na wadhamini washindano hilo ambao ni Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambao ni wasambaji wa kinywaji cha Windhoek Dar es Salaam jana, Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo, Andrea Misama alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendalea vizuri ambapo aliwashukuru warembo wote waliojitokeza kwenye shindano hilo kwa mwaka huu na kuwa mwanamuziki huyo akishirikiana na kundi la sanaa la kampuni hiyo watapamba jukwaa kwa kutoa burudani la kukata na shoka.

"Mwaka huu washiriki waliojitokeza ni wengi ukulinganisha na mwaka jana, hivyo tunatoa pongezi kwa wazazi waliowaruhusu watoto wao kushiriki, malengo yetu ni kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao”, alisema.

Kwa pande wao warembo watakaoshiriki shindano hilo wameahidi kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuwaomba wadau na mashabiki waurembo kujitokeza kwa wingi siku ya shindano ili wawezekusapoti Miss Kinondoni.

Shindano hilo linashirikisha warembo 20 kutoka vitongoji mbalimbali vya Kanda ya Kinondoni ambapo kiingilio kitakuwa sh 10,000 na 20,000 kwa VIP huku shindano hilo likipambwa kwa burudani kutoka kwa mkali wa masauti Christian Bella.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images