Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 954 | 955 | (Page 956) | 957 | 958 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumitomo Corporation ya Japan, Bw. Kunihuru Nakamura  katika Mkutano wa TICAD 6 uliofanyika Nairobi Kenya, Agosti 28, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sumimoto Corporation ya Japan katika mkutano wa TICAD 6 uliofanyika jijini Nairobi Agosti 28,2016.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumimoto ya Japan, Bw. Kanihuru Nakamura  (kushoto kwake) baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi Agosti 28, 2016. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa James Mdoe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt.Adelhelm Meru.  Wanne kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia  Masuala ya Wakimbizi, Fillipo Grand kabla ya mazungumzo yao jijini Nairobi, Agosti  28, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (kushoto) wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. 
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   
    
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka Japan na kusema kwamba kufanyika kwa Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Bara la Afrika (TICAD VI) jijini Nairobi kumetoa fursa kwa Tanzania na nchi nyingine kukutana na wafanyabiashara wakubwa wenye nia ya kuwekeza barani humo.

  Ametoa kauli hiyo jana (Jumapili, Agosti 28, 2016) alipokutana faragha kwa nyakati tofauti na viongozi wa makampuni makubwa ya Japan ambao walikuwa wakihudhuria mkutano huo uliofanyika katika kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Jomo Kenyatta (JICC) jijini Nairobi, Kenya.

  Mkutano wa sita wa TICAD ambao umemalizika jana, ulilenga kuiwezesha Afrika katika sekta ya uchumi na uwekezaji. Ili kufikia lengo hilo, mkutano huo umewashirikisha wadau wa sekta binafsi zikiwemo kampuni binafsi zaidi ya 300 kutoka Japan.

  Katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Rais wa kampuni ya Sumitomo, Bw. Kuniharu Nakahura, alisema kampuni hiyo imeanza utekelezaji wa mradi wa Kinyerezi II wa kuzalisha umeme wa MW240 kutoka gesi asilia (Gas Fired Combined Cycle Gas Power Plant). Mradi huo ulioanza kutekelezwa Machi 2016, unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.

  Bw. Nakahura ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, alisema kampuni yao inajishughulisha zaidi na utengenezaji wa bidhaa za vyuma, kemikali, ujenzi wa miundominu, na usafirishaji.

  Naye Makamu wa Rais wa kampuni ya Toyota Tshuso, Bw. Yasuhiko Yokoi alikutana na Waziri Mkuu na kumweleza jinsi kampuni hiyo kubwa duniani inavyoweza kushiriki na kuchangia maendeleo nchini Tanzania.

  Alisema kampuni yao inajishugulisha zaidi na masuala ya miundombinu ikiwemo kuzalisha mitambo ya umeme na mitambo ya bandari. Pia inazalisha bidhaa za kilimo (matrekta, mashine za viwanda vya mbolea na nguo, ujenzi wa maghala ya nafaka), mitambo ya nguvu za umeme wa joto-ardhi na uzalishaji wa magari ya aina mbalimbali.

  “Kwa mfano hapa Kenya, tumeweza kutengeneza mitambo midogo ya kisasa ambayo inazalisha mbolea tofauti kulingana na hali halisi ya udongo wa mahali husika. Huwezi kuzalisha mbolea ya aina moja na kuamua kuisambaza kwa nchini nzima. Tunapima udongo wa sehemu moja na kuzalisha mbolea inayofaa kwa udongo ule,” alisema.

  Naye Rais wa kampuni ya Marubeni, Bw. Fumiya Kokubu alimweleza Waziri Mkuu kwamba maeneo ambayo wangependa kuwekeza ni kwenye viwanda vya nguo, mbolea, saruji, uzalishaji wa sukari, umeme wa gesi na hasa miradi ya LNG.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa Serikali iko tayari kushirikiana nao na akawashauri watume timu za maafisa wao ili wakutanishwe na wadau wa sekta husika.

  Alisisitiza kuwa Tanzania hivi sasa imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na kwa sababu hiyo inahitaji kuwa na nishati ya kutosha ili iweze kumudu kuendeleza sekta hiyo. “Serikali ya awamu ya tano imeamua kujenga uchumi wa viwanda, tunahitaji kujenga viwanda vya kutosha ili tuweze kusindika mazao ya wakulima ambao wanafikia asilimia 80 ya Watanzania wote. Tunahitaji masoko ya uhakika kwajili ya mazao wanayozalisha,” alisema.

  Akiwa kwenye mkutano huo, Waziri Mkuu pia alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya wakimbizi, Bw. Filippo Grandi; Meya wa Jiji la Yokohama, Bibi Fumiko Hayashi; na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Sudan, Jenerali Bakri Hassan Saleh.

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu alitembelea Maonesho ya Biashara ya Afrika na Japan (Africa-Japan Expo 2016) ambapo Mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TANTRADE) na wadau wengine kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) walishiriki.

  Akiwa huko alitembelea pia mabanda ya Uganda, Rwanda, Sénégal, Kenya, Japan na UN Habitat. Pia alitembelea banda la wajasiriamali wa nguo kutoka Tanzania ambao walishiriki maonyesho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Jomo Kenyatta (JICC) jijini Nairobi, Kenya.

  Waziri Mkuu alirejea jijini Dar es Salaam jana usiku.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMATATU, AGOSTI 29, 2016.
   

  0 0

  Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wakiteta jambo leo kwenye Uwanja wa Kagera Sugar kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi karibuni. Na sasa ukiwa tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange ya Ligi Kuu Vodacom. Kagera Sugar wanajifua kujiandaa kwa Mchezo wao wa tarehe 3 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui kutoka Shinyanga ambapo nmchezo huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa tayari kwa Viwango vya Fifa. ‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia wamefanya usajili wakiwemo makipa. Leo wameanza kujifua kwenye Uwanja wao kwa ajili ya kuhakikisha hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.
  Wakiomba kabla ya kufanya Mazoezi leo hii jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
  Mwenyekiti wa kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama ambaye pia ni Katibu wa KRFA (katikati) kulia ni Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), WALLACE KARIA nao walikuwepo Uwanjani hapo kujionea Uwanja huo ambao umemalizika kwa kusuasua.


  Mecky Meximeakitoa maelekezo kwa wachezaji wake leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba, Wakijiandaa kuikaribisha Timu ya Mwadui hivi karibuni.
  Kwa Makini Wachezaji wa Kagera Sugar wakisikiliza Viongozi wao

  Wachezaji wa Kagera Suga wakijifua leo hii hioni kwenye Uwanja wa Kaitaba
  Kocha mpya wa Kagera Sugar Mecky Mexime  Dokta wa Timu ya Kagera Sugar(kulia) akiteta jambo na Mwamed (kushoto)

  Walinda mlango wa Kagera Sugar wakijifua Vikali leo hii
  Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangaru
  Mashabiki wamejitokeza kwa Wingi kuwakaribisha Kagera Sugar ambao walichezea Misimu miwili nje ya Uwanja wa Kaitaba. Msimu ulopita Kagera waliwapa presha kubwa wapenzi wao hadi dakika za mwisho ambapo walikuwa wanapigania kutoshuka daraja.


  Mashabiki wakiwacheki Kagera Sugar leo wakati wa Mazoezi Kaitaba


  Mashabiki wa Kagera Sugar leo wamejitokeza kwa wingi kuwaona wenzao 'Wanankurukumbi' wakati wa mazoezi

  Mashabiki na Wapenzi mbalimbali wa timu ya Kagera Sugar wamejitokeza kwa Wingi hii leo kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kupita kwa ujenzi wa uwanja huo.
  Mazoezi makali kujiandaa na Mzunguko wa Tatu wa Ligi kuu Vodacom

  Makipa wa Kagera Sugar wakijiuliza jambo leo wakati wa mazoezi yao kwa mara ya kwanza tangu Uwanja huo umalizike kujengwa hivi karibuni. Kagera Sugar wanajiandaa na Mchezo wao wa Ligi kuu Vodaom tarehe 3.  Mapumziko, Wachezaji wa Kagera Sugar wakipata maji ya kunywa.Kocha Mkuu wa Kagera Mecky Mexime
  Shabiki wa Kagera Sugar
  Straika wa Bukoba Veteran Salum Bonge nae alikuwepo Uwanjani hapo
  Mecky Mexime

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza na waandishi kukemea hatua ya kuahirishwa Baraza la Madiwani leo kwasababu za kutotimia akidi.

  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro amekemea kitendo cha kuahirishwa kikao cha Baraza la Madiwani katika jiji la Arusha kuwa kinawanyima wananchi haki ya kuwakilishwa katika baraza hilo linalojadili maendeleo.

  Kikao hicho kimeshindwa kufanyika baada ya madiwani 14 pekee kuhudhuria katika ya madiwani 36 ambao ni wajumbe halali wa kikao hicho.Meya wa Jiji hilo,Kalist Lazaro amesema amelazimika kuahirisha kikao hicho baada ya akidi kushindwa kutimia huku akidai baadhi ya madiwani wamejificha wakiogopa kukamatwa na polisi kwa kuhamasisha maandamano ya Septemba Mosi.

  Mkuu wa wilaya amepinga kauli hiyo ya Meya na kusema akiwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amewasiliana na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD)ambaye alikanusha taarifa za kutafutwa madiwani hao.

  Aliwataka madiwani hao watimize wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi waliowachagua badala ya kutoa sababu zisizo na mashiko huku wakifahamu vikao vya baraza la madiwani vipo kisheria na vina gharama kuviandaa.

  0 0

  Agosti 22, 2016 Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na dunia kwamba ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija, ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.

  Msimamo na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza awali yaani Agosti 31 mwaka huu.

  Jumuiya yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka UVCCM tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.

  Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi wake hakui, hana jeuri wala ubishi.

  Mtoto au watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM si watukutu, hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi. Tumezingatia kutii maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.

  Sambamba na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa na maandamano nchi nzima.

  Jambo jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni taarifa ya kintelejinsia iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza  suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.

  Pia jambo jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake. 

  Wanajeshi wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya la usafi wa mazingira. 

  UVCCM tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka na si wakati huu.

  Tunaelewa kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa masuala ya kiutawala.

  Tulishusha maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD, washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama tulivyokusudia.

  Watendaji wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.

  UVCCM kwa wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa vitendo.

  Tumewataka Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo huko Ihemi.

  UVCCM tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe nyingine katika wakati ujao badala ya kufanyika Agosti 31 mwaka huu kama tulivyotangaza hapo awali.

  UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

  KAIMU KATIBU MKUU.

  0 0  0 0

  Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.

  Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanznia, ni kumhusu Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.
  Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa mausala ya siasa na mwanasheria
  KARIBU

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha afya Mlali

  DcNdejembi alipotembelea wodi wa wagojwa
  Dc Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali

  Na Mathias Canal, Singida

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha Mlali kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani humo kusikiliza kero wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini kupatiwa tiba.

  Huu ni muendelezo wa ziara za kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya kupunguza na kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na wananchi wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya hususani sekta ya Afya.

  Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo mbalimbali, wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.

  Licha ya jengo hilo kujengwa chini ya kiwango chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhudumu katika Wilaya hiyo.

  Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake mwenyewe.

  Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu wa Kituo cha afya Mlali  kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya umma ili kuendelea kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila Mtanzania anayefika katika Zahanati hiyo.

  Kwa upande wa wananchi waliofika kupatiwa huduma kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani wamesema kuwa huduma zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina ahueni kubwa huku changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za chanjo kwa watoto kwani hawapati huduma hiyo kwa wakati.

  Sambamba na hayo Dc Ndejembi ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi wafurahie huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia na kuimarisha Afya zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana ya HapaKaziTu kwa vitendo.

  0 0

  Na Mathias Canal, Singida

  Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Mkoa wa Singida wamekabidhiwa jumla ya madawati 90 kwa kila Halmashauri ili kuondoa adha waliyokuwa wanakumbana nayo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipowaagiza wakuu wa mikoa yote nchini wakati akiwaapisha Ikulu, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.
  Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa chini wakiwa darasani.
   Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
  Mtigumwe amesema kuwa Hali ya Madawati katika Mkoa ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500 hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika Halmashauri za Singida na Manyoni.

  Alisema kuwa mwanzoni mwa mwezi June mwaka huu aliteua kamati ndogo ya uratibu wa madawati kwa kushirikisha wadau mbalimbali katika Mkoa baada ya kuona juhudi za serikali kupitia mamlaka za Halmashauri yaManispaa na Wilaya.
  Ameeleza kuwa kamati hiyo iliweza kukusanya Jumla ya shilingi milioni 42,626,500/= kutoka kwa wadau 67 (Pesa taslimu ikiwa ni 29,046,500) wadau watano walitoa madawato 60 yenye thamani ya shilingi 3,580,000/= na madawati 100 kutoka bonite Bottles Ltd yenye thamaniya shilingi 10,000,000/= ambapo jumla ya madawati yaliyotengenezwa ilikuwa ni 470.
   Akisoma Taarifa ya utengenezaji wa madawati Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Afisa Mifugo wa mkoa wa Singida Elias Donaty Seng’ongo amesema kuwa kupitia kamati ya kuratibu madawati walishirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi za serikali (TBA,Gispa, Tanroads, Sido, Veta, Temesa, Sekretarieti ya Mkoa (RS), Takukuru na TRA, Mashirika ya huduma (NHC, Tanesco, Suwasa, Posta, Taasisi za fedha (NMB, na CRDB), Mifuko ya hifadhi ya jamii (NHIF, NSSF, na PSPF), Mashirika yasiyo ya serikali (NGO’s, SEMA, HAPA, TUNAJALI, na HELVETAS).
  Amewataja wadau wengine waliochangia kuwa ni Vyuo vya idara za serikali (NAO, Madini, Hazina Ndogo, Chuo cha Uhasibu, TIA, Utumishi wa Umma, Chuo cha walimu Singida, Abet English Medium School, Maasai English medium  School, Lake School, Viwanda vya usagishaji mafuta (Mount Meru na Umoja wa wakamuaji mafuta Mkoa wa Singida, Wafanyabiasharambalimbali, wauzaji wa vinywaji baridi) Bonite Bottles Ltd, Wauzaji wa vipuri vya magari, Makandarasi, Wakala wa huduma za misitu TFSAmaduka ya vifaa vya ujenzi, Hoteli na Baba na Mama Lishe Mkoani humo.
  Seng’ongo alisema kuwa kupitia taarifa kutoka Ofisi ya Elimu Mkoa uliweza kufikia lengo la utengenezaji wa madawati kwa asilimia 98% ambapo juhudi bado zinaendelea kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakuwa endelevu kwa siku zijazo.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa wa Singida amewashukuru wadau wote waliochangia fedha Taslimu ama Madawati yakiwa tayari yametengenezwa huku akiwasihi wadau wote kuendelee kujitolea katika kuchangia shughuli za maendeleo katika Mkoa huo.
  Pia amesema kuwa madwati hayo ana imani yatatunzwa vizuri ili wanafunzi waweze kusoma vizuri wakiwa wamekaa kwenye madawati kwani mwanafunzi akiketi kwenye dawati hata mwandiko na ufahamu wake unakuwa mzuri tofauti na mwanafunzi ambaye atasoma akiwa amekaa sakafuni hivyo kupitia upatikanaji wa madawati hayo ana imani kubwa kuwa mkoa wa singida utaimarika kielimu na kuimarisha ufaulu wa wanafunzi.
  Naye Mfanyabiashara, Mkulima na Mfugaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akizungumza kwa niaba ya wadau wote waliochangia amesema kuwa Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amebuni njia nzuri ya kuwapa motisha kwa kutoa Hati kwa wadau wote waliochangia jambo ambalo litaamsha ari zaidi katika kuchangia shughuli za Maendeleo ya Mkoa na taifakwa ujumla.
    Tati alisema kuwa anasikitika sana pale anaposikia kuwa mkoa wa Singida unashika nafasi ya Tano kwa umasikini katika Mikoa yote nchini ilihali ni mkoa wenye rutuba ya kutosha na eneo pana katika uwekezaji hivyo amewasihi wananchi na wadau kwa pamoja kushirikiana kwa pamoja katika kukomesha umasikini huo.  0 0

  1
  Bw . Mohamed Seif Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume hiyo akikabidhi kwa Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mgahawa wa Mokka City Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam.
  2
  Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 mara baada ya kukabidhiwa rasmi.
  3
  Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015

  0 0


  Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia Dk Bernald Achiula akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo wakati akishukuru wanafunzi wa chuo hicho kwa michango yao waliyochanga ili kumsaidia mwanafuzni mwenzao Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ana matatizo ya kusikia, wanafunzi hao wamechanga Fedha na kumnunulia mwenzao Vifaa vya kumsaidia kusikia vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano, Kulia ni Mwanafuzni Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ameelezewa kuwa ana uwezo mkubwa katika masomo yake darasani pamoja na kutokuwa na uwezo wa kusikia, na Katikati ni Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.
  Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia akielezea kwa waandishi wa habari kuwa kitu kilichowafanya wanafunzi wa chuo hicho kumchangia mwanafunzi mwenzao Shinuna Salum Kulia ni kutokana na uwezo wake katika masomo pamoja kuwa tatizo la usikivu linalomkabili
  Mwanafuzni huyo Shinuna Salum Nyamkokwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea kuhusu msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema awali kichwa kilikuwa kinamuuma sana lakini kwa sasa hakiumi tena.
  Gordian Kilave Mkuu wa Idara ya Lugha Chuo cha Diplomasia akielezea matatizo yaliyokuwa yakimkuba na kumsumbua mwanafunzi Shinuna Salum kabla ya kupatiwa vifaa hivyo ambavyo ninamsaidia kusikia kwa sasa.

  0 0


  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote jijini Dar es Salaam leo.
   Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumi na nne ya Siku ya Wahandisi yatakayofanyika Septemba mosi hadi pili jijini Dar es Salaam.

  Maadhimisho hayo ya siku mbili yanatarajiwa kukutanisha zaidi ya wahandisi elfu mbili kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata fursa ya kufanya majadiliano ya kitaaluma, kufanya maonesho ya kiufundi na kibiashara, kuwatambua na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo yao ya mwisho na kuwaapisha wahandisi waliokidhi vigezo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote amesema mada kuu katika maadhimisho hayo itakuwa ni “TANZANIA KUELEKEA KUWA NCHI YA UCHUMI WA KATI NA KUWA NCHI YA VIWANDA: NINI JUKUMU LA WAHANDISI”.
  “Tumejipanga Siku ya Wahandisi mwaka huu iwe na mvuto wa pekee kwa sababu mada yake ni ya kitaifa ikiangalia Dira ya Maendeleo ya Taifa na mwelekeo wa nchi kuwa nchi ya viwanda” amesema Eng. Mlote.


  Maadhimisho ya wahandisi Tanzania yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2013, lengo likiwa ni kuiwezesha jumuiya ya wahandisi nchini kuionesha jamii kile ambacho wahandisi wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi.

  Takribani wahandisi elfu 17 wanakadiriwa kuwepo nchini katika sekta mbalimbali, lengo likiwa ni kuwa na wahandisi elfu 83 ili kukidhi mahitaji ya nchi kuwa ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  JIJI la Dar es Salaam linatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa awamu ya nne wa hoteli za Africa ambapo wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wapatao 200 wanatarajiwa kuhudhuria kuzugumzia masuala muhimu katika sekta ya ukarimu.

  Mkutano huu umeandaliwa na kuratibiwa na kampuni ya kimataifa ya LNoppen na HD Partnership ambapo wameingia katika makubaliano ya kuandaa mkutano huu. Wadau na wamiliki wa hoteli wanaweza kuhudhuria katika mkutano huu kwa kujiandikisha kabla ya tarehe 6 Septemba kupitia tovuti ya africa.hotelandresortsummit.com.

  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya LNoppen Group amesema, “ Tanzania ni nchi iliyo juu kwa kutembelewa na wageni mbalimbali kutoka barani Afrika na mataifa mengine. Kampuni nyingi za kimataifa zimewekeza nchini Tanzania na nchi inazidi kuimarika katika kanda ya Afrika. Tumeona ni vyema mkutano wa mwaka huu tuufanye nchini Tanzania kutokana na fursa zilizopo hapa hasa katika sekta ya Utalii na Ukarimu”.

  Nchi zilizoandaa mkutano huu katika miaka iliyopita ni Ghana 2014, Sengal 2015 na Nigeria Januari 2016.
  Katika siku mbili za mkutano huu mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya ukarimu na utalii yatajadiliwa ikiwa pamoja na usimamizi wa mapato, marejesho ya mtaji, rasimali watu na ajira, huduma bora kwa wateja na ushindani katika sekta ya Utalii Afrika. Majadiliano yatafanyika katika paneli ambapo tafiti zitajadiliwa kwa kina. Mkutano utafunguliwa na Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye atatoa utambuzi wa sera za serikali na vichocheo kwa wawekezaji nchini Tanzania.

  Akiongelea umuhimu wa Mkutano huu, Meelis Kuuskler, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa HD Partnership amesema, “ Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa namna hii, mkutano huu hautatangaza Tanzania kama kitovu cha Utalii peke yake bali utatangaza nchi kwa wawekezaji na jumuiya ya maendeleo kwamba Tanzania ipo wazi kwa biashara''
  Wadau mbalimbali wa sketa ya Utalii na Ukarimu wanasisitiziwa kuwa watapata fursa ya kuhudhuria mkutano kwa kujiandikisha kabla ya tarehe 6 Septemba 2016. Kujiandikisha na kupata taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya africa.hotelandresortsummit.com.

  0 0

  Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA ya sasa na ile tuitakayo.
  Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kutoa maoni kulingana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania na ukuaji wa Demokrasia ya nchi yetu.
  KARIBU

  0 0

  Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake


  Familia ya marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo (pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi, kwa ajali ya gari.
  Familia inapenda kuwashukuru kipekee Wakwe wa marehemu - familia ya Mzee Edriss Mavura;  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Prof Elifas T. Bisanda pamoja na uongozi wa chuo na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT); 

  Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Afya duniani (WHO) Uganda na Tanzania; Dr Harvinder Palaha wa Aga Khan Hospital, na madaktari wenzie, wauguzi na wafanyakazi wote wa Aga Khan Hospitali kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU); 

  Mzee wetu Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi; Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania na Bw. Ziya Kaharan, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki; Prof. Fatmahan Atalar, Mkurugenzi wa MUHAS Genetic Laboratory ya Chuo Kikuu cha Muhimbili; Wanajumuiya wa Ikungi Development Association (IDEA); Umoja wa Wanafunzi waliosoma Uturuki, Masheikh wa Dar es Salaam na Ikungi; na Majirani wote wa Dar es Salaam na Singida.

  Kwa kuwa si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja, tunaomba wote mlioguswa na msiba huu mpokee shukrani zetu za dhati.

  Tunapenda kuwataarifu kuwa Dua ya arobaini (40) ya marehemu itasomwa Jumamosi, tarehe 03 Septemba 2016, Makiungu-Ikungi, Singida, saa 5 asubuhi Wote mnakaribishwa.


  INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUUN


  0 0

   
  (Na Jovina Bujulu, MAELEZO)
   
  Hivi karibuni Serikali imetangaza kununua ndege nne katika kipindi cha mwaka huu wa fedha kwa ajili ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL)  ili kuimarisha sekta ya usafiri wa anga hapa nchini zitakazogharimu Dola za Kimarekani milioni 46.

  Serikali kwa kuanzia imetoa asilimia 40 ambazo ni sawa shilingi bilioni 39,937,939,200 kwa ajili ya ununuzi wa ndege mbili za awali .ambazo zimelipwa Kampuni ya Bombadier Inc ya nchini Canada.

  Azma hiyo ya Serikali ya kununua ndege mpya inatokana na ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutaka kufufua Shirika la Ndege Tanzania na kulipatia mtaji ili lianze upya kutoa huduma hiyo kwa Watanzania.

  Ujio wa ndege hizo utaimarisha huduma za usafiri wa anga na kuongeza ushindani katika utoaji wa huduma za anga hapa nchini kati yake na kampuni binafsi za ndege zinazotoa huduma hiyo kwa sasa.

  Mara baada ya ndege hizo kuwasili hapa nchini zitaanza kutoa huduma ya usafiri wa anga hapa nchini kabla ya kupanua wigo wake wa utoaji wa huduma katika ngazi  ya ukanda wa Afrika Mashariki na baadaye katika anga.nyingine za Kimataifa.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (MB) aliwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha hivi karibuni alisema kuwa Shirika la ATCL  lina ndege moja aina ya Dash 8-Q300 na ndege ya kukodi aina ya CRJ 200.

  “Kwa sasa ATCL  ina ndege moja na ndege nyingine ni ya kukodi  ambazo zinawezeshwa na Serikali kutoa huduma za usafiri wa anga kati ya Dar es salaam, Mwanza, Mtwara, Kigoma na  Moroni Comoro” alisema Profesa Mbarawa.

  Aidha,  Prof. Mbarawa aliongeza kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na kampuni ya ATCL  na wadau wengine imekwishaainisha ndege mbili zinazofaa kununuliwa ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 78  na  baadaye ndege nyingine mbili kubwa zitakazokuwa na uwezo wa kubeba abiria 155 ambazo zitanunuliwa kwa kipindi cha mwaka huo fedha.

  Mchakato wa ununuzi wa ndege hizo mbili ambazo zitanunuliwa katika awamu ya kwanza ulihusisha wawakilishi wa viwanda vya ndege vya Boeing ya Marekani, Airbus ya Ufaransa, Embraer ya Brazil  na Bombadier ya Canada.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani alisema kuwa ndege hizo ambazo zinatarajiwa kununuliwa zitatumia anga la Tanzania ambapo hivi sasa anga hilo linatumiwa na ndege zinazotoka nje ya Afrika, hivyo upatikanaji wa ndege hizo utasaidia kutoa fursa kutua kwenye anga za nchi jirani.

  “Muda si mrefu tutapata ndege mbili mpya, mwakani tutaongeza nyingine mbili, Serikali imejipanga kufufua Shirika la Ndege na kubadilisha mfumo wa uendeshaji ili liweze kujiendesha lenyewe” alisema Mhandisi Ngonyani.

  Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Mawasiliano) William Budoya , amesema kuwa msukumo wa kununua ndege hizo ni jambo la muda mrefu kuanzia Serikali ya Awamu wa Nne 2005-2015,na katika kuendeleza utekelezaji wa juhudi hizo Serikali ya Awamu ya Tano imetoa msisitizo na kulipa  kipaumbele suala hilo.

  Aidha, Afisa Mawasiliano huyo amesema kuwa ndege zitakazonunuliwa ni aina ya Bombadier kutoka kampuni ya Bombadier Inc ya nchini Canada.

  Serikali ilichagua kampuni ya Bombadier Inc kwa sababu iliainisha mchanganuo wa biashara ambao ulishauri kuanza na ndege ndogo, kwa kuangalia soko la ndani baadaye ndege zinaweza kuongezwa kwa kuangalia soko la kimataifa.

  Aliongeza kwa ndege hizo zinatarajia kufika nchini ifikapo mwezi Septemba mwaka huu, na kwa kuanzia zitaanza kutoa huduma kwa safari za ndani ya nchi.

  Aidha alisema kuwa Serikali imemteua  mshauri mwelekezi ambaye ataweka manejimenti imara katika uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuajiri wafanyakazi walio na weledi na wenye utayari wa kufanya kazi kwa ufanisi.

  Shirika la ndege la Tanzania (ATC) lilianzishwa mwezi Machi, 1977 chini ya sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1969 na baada ya kuvunjwa kwa lililokuwa Shirika la ndege la Afrika Mashariki.

  Katika kutekeleza sera ya  ubinafsishaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa Mashirika ya Umma ya mwaka 2002,  Shirika la ndege la Tanzania (ATC) liliundwa upya huku Serikali ikimiliki   asilimia 49 ya hisa zake kwa Shirika la ndege la Afrika Kusini hatua ambayo  ilipelekea kuundwa upya kwa kampuni ya ndege Tanzania (ATCL).

  Pamoja na kuwepo kwa kampuni ya ndege ya ATCL, kwa sasa kuna kampuni binafsi zinazojihusisha na huduma za usafiri wa anga nchini na nje ya nchi.Kampuni hizo ni Precision Air, Fastjet, Auric na Coastal Air.

  Akizungumzia mpango wa Serikali wa kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikiikabili kampuni ya ATCL , Budoya alisema kuwa mshauri mwelekezi aliyeteuliwa na Serikali  atatayarisha mpango madhubuti wa kibiashara utakaoifanya kampuni ya ATCL kujiendesha kwa faida na kuweza kuteka soko la ndani na nje ya nchi.

  Majukumu ya sekta ya uchukuzi yanasimamiwa Sera ya Taifa ya Uchukuzi ya mwaka (2003) na utekelezaji wake ambao unahusu usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga, kusimamia viwanja vya ndege na usalama katika usafirishaji nchini

  0 0

  Meneja wa Bendi ya Dar Music, Khamis Maero (Katikati)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha wasanii wapya wa bendi hiyo pia amesema kuwa wafanya uzinduzi wa Albamu yao Septemba 16 mwaka huu katika ukumbi wa Mango Gaeden Jijini Dar es salaam.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  BENDI ya Dar Music inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 16 huku uzinduzi huo ukisindikizwa na Malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na bendi ya Msondo.

  Uzinduzi huo utaenda sambamba na utambulisho wa albamu ya bendi hiyo iliyobeba nyimbo 6 pamoja na video ya wimbo wao wa Chozi la Maskini.

  Akizungumza na waandishi wa habari  Meneja wa bendi hiyo Khamis Maero amesema kuwa uzinduzi huo mkubwa unafanyika kwa mara ya kwanza toka Rais mpya Jado Fideforce aingie madarakani na kutambulisha wanamuziki wapya waliojinga na bendi hiyo.

  Kwa upande wake Fide Force amesema kuwa nyimbo zitakazotambulishwa katika uzinduzi huo ni pamoja na wimbo uliobeba albamu yao ya Chozi la Maskini pamoja naSalmaga.

  Nyimbo nyingine ni Bongo mchango, Maisha Upendo, Mtu Box, Jibebishe  na Ama zao Ama zangu.

  "Ndani ya bendi yangu nimeamu kuchukua wanamuziki wazuri ili kuhimili ushindani uliopo katika tasnia ya muziki kutokana na ushindani uliopo" amesema Fideforce.

  Fideforce kuwa ana uzoefu mkubwa na kile kinachopelekea bendi nyingi kuvunjika hivyo hawawezi kuruhusu kitu hicho kitokee ndani ya bendi yao.

  "Uzuri ni kwamba ninaelewa muziki wa bongo ulivyo na nini huwa kinafanyika na kipi cha kuepuka ili bendi kutovunjika" , amesema Fideforce.

  0 0

  Meneja Msimamizi wa masuala ya Usalama wa Vodacom Tanzania, James Wawenje (kulia) na Ofisa Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Jehud Ngola (kushoto),wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati) akiwasilina na Hassan Mfaume Mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/- katika droo ya wiki ya promosheni ya ‘Kamata Mpunga’inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla ya washindi 224 wamepatikana tangu kuanza kwa promosheni hiyo.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.


  0 0

  Meneja wa Bendi ya Dar Music, Khamis Maero (Katikati)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha wasanii wapya wa bendi hiyo pia amesema kuwa wafanya uzinduzi wa Albamu yao Septemba 16 mwaka huu katika ukumbi wa Mango Gaeden Jijini Dar es salaam.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  BENDI ya Dar Music inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 16 huku uzinduzi huo ukisindikizwa na Malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na bendi ya Msondo.

  Uzinduzi huo utaenda sambamba na utambulisho wa albamu ya bendi hiyo iliyobeba nyimbo 6 pamoja na video ya wimbo wao wa Chozi la Maskini.

  Akizungumza na waandishi wa habari  Meneja wa bendi hiyo Khamis Maero amesema kuwa uzinduzi huo mkubwa unafanyika kwa mara ya kwanza toka Rais mpya Jado Fideforce aingie madarakani na kutambulisha wanamuziki wapya waliojinga na bendi hiyo.

  Kwa upande wake Fide Force amesema kuwa nyimbo zitakazotambulishwa katika uzinduzi huo ni pamoja na wimbo uliobeba albamu yao ya Chozi la Maskini pamoja naSalmaga.

  Nyimbo nyingine ni Bongo mchango, Maisha Upendo, Mtu Box, Jibebishe  na Ama zao Ama zangu."Ndani ya bendi yangu nimeamu kuchukua wanamuziki wazuri ili kuhimili ushindani uliopo katika tasnia ya muziki kutokana na ushindani uliopo" amesema Fideforce.

  Fideforce kuwa ana uzoefu mkubwa na kile kinachopelekea bendi nyingi kuvunjika hivyo hawawezi kuruhusu kitu hicho kitokee ndani ya bendi yao.

  "Uzuri ni kwamba ninaelewa muziki wa bongo ulivyo na nini huwa kinafanyika na kipi cha kuepuka ili bendi kutovunjika" , amesema Fideforce.

  0 0

  Na Abushehe Nondo na Sheila Simba - MAELEZO.

  Serikali imesema kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini. 

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani katika chuo cha Taifa cha usafirishaji(NIT) 
  Mbarawa alisema kuwa Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

  “Serikali imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali halisi ya Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa baadhi, huku lengo ni kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa Mbarawa.

  Mbarawa aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni kuhudumia wananchi hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani zimezingatia mambo mbalimbali ikiwemo suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.

  Aliongeza kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini kwani zinaweza kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ndio vingi nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.

  Prof. Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa ndege hizo katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani 1.7 za mafuta tofauti na aina nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa safari moja.

  Waziri Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha kuwa suala hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na nchini nyingi ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400 zilizotengezwa na  Kampuni hiyo.

  Mpaka sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa asilimia 40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19 septemba mwaka huu ambapo zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe 15 septemba mwaka huu kupitia nchini Uingereza.

  Akizindua mafunzo hayo ya wakufunzi wa  marubani, Waziri Mbarawa aliwaasa Marubani ambao watahitimu mafunzo hayo  kuhakikisha wanazingatia suala na nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.

  “Hatutaki kuwa na marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio waadilifu,hakikisheni mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya anga ambapo wakati mwingine Rubani anajijua anakasoro lakini bado anang’ang’ania kurusha ndege” alisema Prof.Mbarawa.

  Aidha amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za urubani ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini. 

  0 0

   Katibu wa Chama hicho, Jafari Makatu (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni wasanii wa chama cha Waigizaji cha Mkoa wa Kinondoni (STDFAA).

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
  CHAMA cha Waigizaji cha Mkoa wa Kinondoni (STDFAA) wamemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye kuiharakisha Sera ya filamu ili iwasaidie katika mambo mbalimbali hususani ya kisheria.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Chama hicho, Jafari Makatu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na kuzungumzia changamoto zinazowakabili katika tasnia ya filamu nchini.

  Makatu amesema kuwa Sheria ya Filamu ni muhimu katika tasnia hiyo hivyo ikiharakishwa itasaidia wadau wa tasnia hiyo kufanya kazi kwa uwazi na usalama wa hali ya juu kwa kuwa watakua wanalindwa na sheria.

  “Tunamuomba Waziri wetu Mhe. Nape atuharakishie Sera ya Filamu kwa sababu sheria hiyo itatusaidia kuoanisha mambo mbalimbali ya kisheria kuanzia kwenye uandaaji wa kazi zetu hivyo, kupelekea kufanya kazi kwa  ufanisi na kutoa kazi bora zaidi”. Alisema Makatu.

  Ameongeza kuwa sheria hiyo pia itawasaidia katika suala zima la Haki miliki na Haki shiriki, malipo stahiki kwa kila kazi, masoko, madaraja ya waigizaji na wadau wote wa tasnia ya filamu pamoja na ulazima wa kila msanii kujiunga katika vyama husika vitakavyowasaidia katika mambo mbalimbali.

  Aidha, Katibu huyo ameiomba Serikali kuwekeza kwenye sanaa ili kuwawezesha kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuchangia katika Pato la Taifa pia amemuomba Mhe.Nape kuwatafutia eneo maalum la ardhi ambalo litawasaidia katika kufanyia shuhuli zao za kurekodi filamu.

  Ametoa rai kwa wasanii kujiunga katika vyama mbalimbali vinavyowahusu ili kuleta umoja, mshikamano na tija katika kazi za sanaa,amesisitiza wasanii kujiunga na Bima za Afya.

  Naye Mdhamini wa Chama hicho, Ahmed Olotu amewaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kuwasaidia wasanii kupambana na wauzaji  wa filamu feki kwa kuwa wanarudisha nyuma maendeleo ya wasanii na kupunguza pato la Taifa.

older | 1 | .... | 954 | 955 | (Page 956) | 957 | 958 | .... | 1897 | newer