Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA

0
0
 Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku ya kwanza walipokutana wakati wa maandalizi ya kutengeneza kipindi hicho.
Mohammed Hammie na Happy Balisidya wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kufahamu watakuwa wakiendesha kipindi cha CHUKUA HATUA.

Chukua Hatua ni kipindi kipya cha radio kitakachowashirikisha vijana, wakizungumza na kujadili kwa pamoja masuala yanayowahusu hasa ya kujikwamua na maendeleo mkoani Dodoma na maeneo jirani.

Hiki ni kipindi ambacho kinatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za ajira kwa vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa vijana wa kike na kiume.
Lengo kuu la kipindi hiki ni kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira na changamoto wanazokutana nazo katika mihangaiko yao, kipindi kitapaza sauti za vijana ambazo hazikupata nafasi ya kusikika hapo kabla.

Si kipindi tu, bali pia ni jukwaa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi, mawazo, uzoefu na pia kujifunza kutoka kwa wengine, ni mahala pekee ambapo kijana atayaona matarajio na uzoefu kutoka fani na taaluma mbalimbali.
Kipindi pia kinatarajiwa kuimarisha ujuzi na kuelekeza upya akili za vijana kufanya kazi na kuchangamkia fursa za ajira kwa ujasiriamali, kujiajiri na kuukwepa umaskini uliokithiri miongoni mwao.

Kipindi kitaanza kuruka hewani siku ya Alhamisi ya tarehe 01/09/2016 kupitia kituo cha RASI FM RADIO inayopatika masafa ya 103.7 Dodoma.
Pia kipindi kitakuwa kinapatikana kupitia mtandao wa Youtube ukurasa wa CHUKUA HATUA, pia mijadala itakuwa inaendelea kupitia ukurasa wetu wa facebook ambao ni CHUKUA HATUA, Instagram ni KIJANA CHUKUA HATUA, na Twitter ni CHUKUA HATUA1.

Kipindi hiki kimewezeshwa na mpango wa pamoja wa ajira kwa vijana wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kazi Duniani (ILO) kwa udhamini wa SIDA.

Wananchi wa Kanda ya Ziwa zaidi ya 750 wapata mafunzo Kilimo Biashara jijini Mwanza

0
0

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) na Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia) pamoja na wajumbe wengine kutoka UNDP wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano Rock City Mall lilipofanyika kongamano la Kilimo Biashara jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumzia malengo ya Kongamano la Kilimo Biashara kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) kufungua rasmi.
Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akitoa salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akitoa hotuba ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk. Charles Mahika akielezea mikakati iliyowekwa na wizara ya kuhakikisha sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo inafanikiwa.
Mwezeshaji ambaye pia ni Rais wa vijana wajasiriamali na wataalamu wa miradi ya maendeleo mkoa wa Singida, Philemon Kiemi akitoa mafunzo ya ufugaji kuku wa kisasa kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Mratibu wa Kongamano kutoka ESRF, Abdallah Hassan akizungumza jambo kwenye kongamano hilo.
Mwezeshaji Bi. Kalega akitoa mafunzo ya ufugaji Kuku na matumizi ya Azolla kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.








Baadi ya wakazi wa Kanda ya Ziwa akiwemo mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bi. Mongella waliohudhuria Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.


Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, limesema litaendela kuinua fursa za kiuchumi zinazopatikana hapa nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazoendelea kuibuliwa.

Kauli hiyo imetolewa na Programme Specilist- Inclusive Growth UNDP Tanzania, Ernest Salla wakati wa Kongamano la Kilimo Biashara kanda ya ziwa lilofanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall Agosti 27 mwaka huu Jijini Mwanza.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na UNDP/UNEP lililolenga kuzitambulisha fursa katika kilimo biashara, lilihudhuriwa na wananchi mbalimbali zaidi ya 750 kutoka mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza wenyewe.

Katika kongamano hilo Salla alisema kilimo kina fursa nyingi hivyo watanzania hawana budi kuzitumia fursa hizo kwa kuwakumbatia wataalamu ili kiwe mkombozi wa maisha yao.Akizungumza katika Kongamano hilo la siku moja, Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida alisema licha ya uchumi wa taifa kutegemea kwa kiasi kikubwa kilimo, lakini kilimo hapa nchini bado kipo nyuma hivyo kuchangia kiasi kidogo katika kumuendeleza mkulima.

“Kwa kutambua upungufu huu, ESRF ikishirkiana na UNDP/UNEP imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali ili kusaidia wananchi na taifa kwa ujumla kujikwamua katika vizingiti mbalimbali vya maendeleo ukiwemo umasikini wa kipato,” alisema Dk Kida.

Alisema kukua kwa teknolojia duniani, kumeongeza fursa nyigi za kimaendeleo ikiwamo kilimo, kwani wakulima wengi hivi sasa hawategemei mvua na hutumia eneo dogo kwa ajili ya kilimo.

Katika warsha hiyo zilitolewa mada mbalimbali; pamoja na kilimo cha Foda (Hydroponic fodder), kilimo cha mbogamboga (Hydroponic and Aquaponic Vegetables), shamba kitalu (Green house), Azolla na ufugaji wa samaki na nyuki kutoka kwa wakufunzi mbalimbali waliotoa ufafanuzi kuhusu fursa mpya za kilimo biashara.Alisema kilimo cha kisasa au “smart farming” ambacho hakihitaji maeneo makubwa kinaweza kufanyika katika maeneo ya mjini tofauti na izaniwavyo kuwa kilimo lazima kiwe vijijini.

Alisema ESRF imeshiriki katika utekelezaji wa miradi ya majaribio inayotegemea teknolojia ya kisasa katika wilaya za Bunda, Bukoba vijijini, Sengerema, Nyasa, Ikungi na Ileje kupitia miradi ya PEI na CDRBM kwa kipindi cha miaka mitatu.

Pamoja na mambo mengine, alisema matokeo ya miradi hiyo ya majaribio yamethibitisha fursa katika kilimo biashara yanayoweza kuwasadia wananchi katika kujikwamua na ndio miongoni mwa sababu ya kuandaa warsha hiyo.

Akifungua kongamno hilo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alisema kilimo pekee ndicho chenye fursa pekee rahisi kuliko sekta nyingine duniani kote.Mongela aliipongeza ESRF, UNDP, na wadau wengine wa maendeleo, kwa tafiti hizo na kwamba hatua hiyo itasaidia kuinua uchumi wa watanzania na taifa kwa ujumla.

Licha ya Mongella kupongeza hatua hizo, lakini alizitaka taasisi mbalimbali kupitia wataalamu wake kuonyesha gharama halisi za kutekeleza miradi hiyo.“Hizi tekonolojia ni rahisi, watu wakianza nazo kidogokidogo baadaye watapanda na kufika juu, tatizo la wataalamu wanasema gharama ni kubwa za teknolojia, hivyo kuwaogopesha watu,” alisema Mongella

Amoni Manyama kutoka UNDP, alisema kuzingatia maelekezo ya wataaalamu ndio njia pekee ya kufanikisha katika kubuni fursa za kilimo na biashara.Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk Charles Mahika alisema wizara yake ikishirikiana nan chi zinazozunguka Ziwa Victoria wanaandaa mwongozo wa kuanzisha ufugaji wa samaki katika vizimba na kwamba mwongozo huo unatarajiwa kukamilishwa jijini Mwanza hivi karibuni.

Katika kongamano hilo wapo baadhi ya wananchi waliotoa shuhuda mbalimbali walionza kunufaika na fursa za kilimo biashara chini ya ufadhili wa UNDP ikishirikiana na ESRF.

MSEKWA:WATANZANIA WAACHE KUFUATA MKUMBO

0
0

Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa.

Na Fatma Salum na Sheila Simba, MAELEZO

Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa amewaasa watanzania kuacha kufuata mkumbo wa kisiasa badala yake watii mamlaka ili kuepuka kuvunja sheria na kuleta madhara kwao binafsi na taifa kwa ujumla.

Msekwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu mwenendo wa siasa za hapa nchini na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Alieleza kuwa watu wengi wana hulka ya kufuata mkumbo kwenye mambo fulani bila ya kuchunguza na kufahamu ukweli wake kabla ya kushabikia.

“Ni hulka ya watanzania kushabikia mambo wasiyoyafahamu ilimradi tu yanawafurahisha masikioni au machoni mwao kwani hata huko mitaani wanakimbilia ngoma bila ya kujua inatokea wapi au inaelekea wapi, hivyo nawasihi wajaribu kuwa makini na mbinu za siasa zinazotumiwa na baadhi ya vyama kwa kuwa nyingine zina madhara ndani yake.” Alisema Msekwa.

Akifafanua mwenendo wa siasa za hapa nchini, Mzee Msekwa alisema kuwa bado wanasiasa wengi hawafuati kanuni za ushindani wa kisiasa katika kutafuta madaraka badala yake wanatumia mbinu ambazo zinavunja sheria za nchi na hatimaye wanapambana na mamlaka.

“Ushindani wa kisiasa ni jambo la kawaida na linalokubalika ingawa ushindani huo ni lazima ufuate sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kufikia lengo, hivyo kubuni vitu ambavyo vinachochea utovu wa nidhamu na uvunjifu wa amani sio jambo zuri, ' alisisitiza.

Aidha, Msekwa alieleza kuwa utendaji wa Mhe. John Magufuli ni wa kuridhisha na wa aina yake kwa kuwa amekusudia kuleta mabadiliko chanya kwa watanzania na kuondoa mfumo wa utendaji kazi kwa mazoea jambo ambalo limesaidia kurudisha nidhamu kwa watumishi wa Serikali.

Akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuongoza Bunge, alieleza kuwa tofauti ya Bunge la zamani ni kwamba lilikuwa na nidhamu kubwa na linaheshimika lakini Bunge la sasa halina utii na hicho ndio chanzo cha malumbano yanayojitokeza mara kwa mara katika vikao vya Bunge.

Aliongeza kuwa tangu awali wapinzani kazi yao ni kuipinga Serikali iliyo madarakani lakini kwenye Bunge la uongozi wake walikuwa wakipinga kwa kutumia hoja na kufuata kanuni bila ya kudharau mamlaka ya Spika wala Serikali iliyoko madarakani.

“Kanuni zinatoa nafasi kwa mbunge asiyeridhika na maamuzi ya Spika kushitaki kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge, na kamati hiyo itasikiliza na kutoa uamuzi kama mahakama inavyosikiliza lakini wabunge wa sasa hawataki kutumia utaratibu bali hutumia mbinu za tofauti ili waweze kupata sifa ambazo hazina tija kwa wananchi waliowachagua,” alisema.

Msekwa pia amewaasa vyama vya upinzani kutumia mbinu nzuri katika kutafuta madaraka bila ya kuvunja sheria au kuhatarisha amani ya nchi kwani waliowachagua wanategemea zaidi matokeo ya kazi waliyoahidi kuwatumikia kuliko malumbano yasiyo na tija kwa ustawi wao na taifa.

KAMPUNI YA MABIBO YAWAANDALIA BONANZA WASHIRIKI MISS KINONDONI 2016 ILI KUWAWEKA FITI

0
0
 Wanyange wa Lete Raha Miss Kinondoni 2016 wakionesha moja ya shoo katika Bonanza walioandaliwa na Mdhamini wao Mkuu Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd lililofanyika ufukwe wa Jangwani Sea Breeze Mbezi jijini Dar es Salaam jana lenye lengo la kuwaweka fiti kabla ya shindano lao litakalofanyikaa Septemba mbili Hoteli ya Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.
 Wanyange hao wakiwa na waandaaji wa shindano hilo litakalofanyika Septemba 2, 2016 Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
 Warembo hao wakiwa wameshika chupa za Windhoek kinywaji kinachosambazwa na kuuzwa Mdhamini wao Mkuu Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd.
 Wanyange hao wakitosti kinywaji hicho
 Mratibu wa Shindano hilo, Rahmat George ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Rahmat Entertainment iliyoandaa shindano hilo, akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya shindano hilo.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Mabibo, Abdallah Ngoma, akizungumzia udhamini shindano hilo na shabaha ya kuandaa bonanza hilo.
 Mshauri wa shindano hilo, Boy George, akizungumza na wanahabari.
 Burudani zikiendelea katika bonanza hilo.
 Wanyange hao wakishiriki kucheza mpira wa mkono kwenye bonanza hilo.
 Wadau wa Windhoek wakicheza soka la ufukweni katika 
bonanza hilo.
 Soka la ufukweni likiendelea.

Mchezo wa kuogelea ukiendelea ndani ya kiota cha Jangwani  Sea Breeze huko Mbezi jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale

MDHAMINI Mkuu wa Lete Raha Miss Kinondoni 2016 Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd imewaandalia Bonanza wanyange wa shindano hilo ili kuwaweka fiti kuelekea shindano lenyewe litakalofanyika Septemba 2 Ukumbi wa Denfrances uliopo Sinza.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa 
Kampuni hiyo, Abdallah Ngoma alisema wameamua
kuwa andalia bonaza hilo ili kuwafanya wawe fiti kabla
ya kuingia kwenye shindano lenyewe Sptemba 2.

" Katika bonaza hilo warembo hao wameweza kushiriki
mpira wa miguu, mikono na  kucheza" alisema Ngoma.

Mratibu wa shindano hilo Rahmat George alisema maandalizi
 yote yamekwisha kamilika ambapo warembo 20 watapanda
jukwaani kuwania nafasi ya Miss Kinondoni 2016.

Alisema kama kawaida warembo hao watapanda jukwaani 
wakiwa katika vazi la ufukweni, ubunifu na kujibu maswali wata
kayoulizwa na majaji.

George ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wa 
mashindano hayo kufika kupata burudani safi itakayotolewa na mwanamuziki 
nguri Christian Bela na kikosi cha promosheni cha kampuni ya
Mabibo.

NI HESHIMA UKICHINJIWA MBUZI WA SUPU MKOANI MARA

0
0
Supu hii huchemshwa kwa masaa kadhaa bila kuungwa

Sherehe hizi hazina msimu maalumu bali hufanyika kadri familia moja na nyingine ama mtu na mtu walivyokubaliana. Mfano mtoto kumchinjia mzazi wake mbuzi kwa ajili ya supu (umusuri) au dada kumchinjia kaka ama mtu yeyote kulingana na makubaliano yao ambapo inaaminika mtu akiinywa supu hiyo husafisha tumbo.

Huchukuliwa kama Heshima kubwa pindi sherehe za aina hii zinapofanyika katika familia fulani ambapo ndugu, jamaa na marafiki hujumuika pamoja kama picha zinavyoonekana katika sherehe ya Chacha Kuchenga alipoenda kumchinjia mbuzi mdogo wake, Leah Marwa Binagi (Binti Kuchenga).
Na BMG
Supu huandaliwa

Muda wa kunywa supu.
Katika supu hiyo, huchanganywa damu mbichi ili kuongeza ladha
Bonyeza  HAPA Kujua Zaidi.
Kuna Sherehe za aina mbalimbali mkoani Mara. Leo BMG inakujuza juu ya Shereze ya kuchinjiwa supu ya mbuzi. Hii hufanywa zaidi kwa wanajamii wa kabila la Wakurya mkoani humo.

Ngoma Africa Band iliyowatia kiwewe wapenzi wa muziki Frankfurt,Ujerumani

0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama FFU-ughaibuni inayoongozwa na mwanamuziki nguli Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja juzi kati ya jumamosi ya 13 Septemba 2016 ilifanikiwa tena kulitingisha jiji la Frankfurt nchini ujerumani katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival yaliyo fanyika katika viwanja vya Rebstock Park,ambapo bendi hiyo iliwatia kiwewe waudhuriaji wa onyesho hilo.Bendi hiyo maarufu na mdundo wake "Bongo Dansi" inatajwa kuwa ndio bendi imara ya kiafrika kudumu kwa muda mrefu na kuteka soko la muziki barani ulaya.
wape Hi at www.facebook.com/ngomaafricaband








Waziri Kairuki awasisitiza watumishi wa Umma kufahamu kanuni za utumishi

0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amewasisitiza watumishi wa Umma kufahamu kanuni za kudumu za utumishi wa umma ili kutambua haki zao na kuepuka kunyanyaswa na waajiri wao.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri huyo alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mipango na mikakati iliyowekwa na wizara yake katika kipindi cha uongozi wa awamu ya tano.

Waziri Kairuki amesema kuwa ni muhimu kwa watumishi wa Umma kufahamu kwa undani maadili yaliyowekwa na Serikali kwa ajili yao kwa kuwa yatawasaidia kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu.

“Inawezekana maafisa utumishi walikuwa wakizishikilia kanuni za utumishi wa umma na kuona kama ni za kwao kana kwamba mtu mwingine hatakiwi kuzifahamu lakini napenda kutoa rai kwa watumishi wote kuwa kanuni hizi ni za kwetu wote hivyo ni muhimu kuzifahamu”, alisema Mhe. Kairuki.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa kanuni za utumishi za mwaka 1994 zilirekebishwa na kwa sasa kanuni zinazotumika ni za mwaka 2009 ambazo zinapatikana katika tovuti za wizara mbalimbali hivyo upatikanaji wake umerahisishwa tofauti na zamani.

Pia amewataka watumishi kufuatilia waraka mbalimbali wa maendeleo ya kiutumishi inayotolewa na wizara hiyo kwa kuwa itawasaidia kufahamu miundo mipya ya utumishi inayotolewa, endapo mtumishi hatofahamu mabadiliko hayo atakosa taarifa muhimu.

Aidha, Waziri huyo amewakumbusha Maafisa Utumishi kuwa kazi hiyo wamesomea na watumishi ndiyo wadau wao wakubwa hivyo kwa namna moja ama nyingine kazi yao kubwa ni kuwasimamia na kuwahudumia vyema watumishi hao katika maeneo yao ya kazi.

“Napenda kutoa agizo kwa Maafisa Utumishi wote kufanya kazi zenu kwa umakini kulingana na kanuni za utumishi, kwa kuwa kazi hiyo mmeisomea basi ni lazima muwahudumie vizuri watumishi ili nao waweze kupata ufanisi zaidi wa kutekeleza majukumu yao”, alimalizia Mhe. Kairuki.

MHE. KAIRUKI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KUJIJENGEA UWEZO KATIKA MAENEO YATAKAYO HARAKISHA MAENDELEO

0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Kushoto ni muongozaji kipindi hicho Bi. Eshe Muhidin.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo katika  kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Mhe. Kairuki aliainisha kuwa wale wanaotarajia kuomba ajira Serikalini wawe na subira wakati zoezi la uhakiki wa taarifa za kiutumishi likikamilishwa. Kushoto ni muongozaji wa kipindi hicho  Bi. Eshe Muhidin waTBC.
 Muongozaji wa kipindi cha TUNATEKELEZA Bi. Eshe Muhidin (kushoto) akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Miongoni mwa aliyosema Mhe. Kairuki ni wito kwa Watumishi wa Umma kujiendeleza katika maeneo yenye tija kwa Taifa ili kufikia malengo ya nchi.
TUMEKAMILISHA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Muongozaji wa kipindi cha TUNATEKELEZA Bi. Eshe Muhidin (kushoto) baada ya kukamilisha kurusha kipindi mmbashara (live) katika studio za Runinga ya Taifa TBC-1.

Waziri Nape Nnauye awataka Watanzania kuwapa Moyo Wanamichezo nchini.

0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akimkabidhi cheti Mwanariadha Alphonce Simbu baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya tano katika Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akimkabidhi King'amuzi cha Kampuni ya DSTV Mwanariadha Alphonce Simbu baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya tano katika Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwakabidhi zawadi zao baadhi ya Washiriki wa Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, nchini Brazil.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akiongea na baadhi ya Viongozi, wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo (hawapo pichani) walioshiriki katika Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.

Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki (TOC) Bw. Filbert Bayi akiongea na baadhi ya Viongozi, wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo (hawapo pichani) walioshiriki katika Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.


Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo waliohudhuria haflaya kuwapongeza Washiriki wa Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, nchini Brazil wakifuatilia hotuba za Viongozi. 










Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akiongea na baadhi ya Viongozi, wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo (hawapo pichani) walioshiriki katika Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.
(Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewataka Watanzania kujifunza kuwatia moyo Wanamichezo wanaposhiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Wito huo ameutoa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa Hafla ya kuwapongeza na kupokea bendera ya Taifa toka kwa Wanamichezo ambao walishiriki katika Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, nchini Brazil.

Mhe. Nnauye alisema kwamba, Watanzania ni vizuri wakajifunza kusema maneno mazuri kwa wanamichezo pindi wanaporejea toka katika Mashindano mbalimbali ili kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri wanamichezo hao huku akisisitiza kuwa, ni vema ukosoaji ukaendana na ushauri mzuri wenye kujenga badala ya kulaumu.

Aliongeza kuwa, Wanahabari nchini wanapaswa kuandika mazuri yanayofanywa na wanamichezo kwani yana manufaa kwa Taifa badala ya kutafuta maneno yasiyo na tija ya kukosoa mara kwa mara kwani kuna wavunja moyo wanamichezo.

“Tukijifunza kuandika na kusema mabaya tu ya kuvunja moyo kwa wanamichezo wetu hii sio sawa sawa, tujifunze kuwatia moyo, na hii ni hatua ya kwanza na wito wangu kwa Watanzania wote”, alisema Mhe. Nnauye.

Alisisitiza kwamba, Watanzania wanapaswa kujifunza kujivunia vitu vya kwao kwa njia hiyo itakuwa ikiongeza hamasa kwa wanamichezo katika kujituma kwa manufaa yao na ya Taifa.Aidha, alisisitiza kuwepo na maandalizi ya mapema kwa Wanamichezo nchini ili waweze kufanya vizuri zaidi huku akishauri uwekezaji wa kutosha katika sekta hiyo na kuyataka Makampuni kuwa na tabia ya kuwatumia Wanamichezo nchini katika kutangaza utalii wa nchi.

Ametoa wito kwa Viongozi wazembe ambao watashindwa kufikia malengo mazuri katika tasnia hiyo ni bora wakaachia ngazi zao ili kuwapa nafasi watu wengine wenye uwezo kutekeleza kazi hiyo.“Nadhani sasa tuanze kukabana kwenye Vyama, ukichaguliwa na kukawa na mashindano kama haya, ukashindwa kupeleka hata mchezaji mmoja, kazi yako ya kwanza nadhani ni kijiuzulu”, alisema Mhe. Nnauye.

Awali akitoa taarifa ya Wanamichezo walioshiriki katika Mashindano hayo, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Gulam Rashid alisema kwamba, Tanzania ilishiriki mashindano hayo ikiwa na Wanamichezo saba, walimu wa tatu wa michezO ya kuogelea, Judo na riadha ambapo kati yao wachezaji wa nne walipata nafasi ya upendeleo (Universality).

Alifafanua kuwa, wachezaji wa nne waliofanikiwa kupata nafasi ya upendeleo ni wale ambao walishiriki katika michezo mbalimbali katika kusaka viwango, lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kufikia viwango vinavyowaruhusu wao kushiriki katika mashindano hayo, hivyo kulingana na Sera na itikadi za Olimpiki zilitaka kila nchi Duniani ambayo ni Mwanachama wa Mashindano hayo kutoa watu wake, hivyo walitoa nafasi hiyo kwa wale waliokosa kufikia viwango kuweza kushiriki.

“Nchi ambayo haikuwa na wachezaji waliofikia viwango vya Olimpiki walipewa nafasi ya upendeleo kwa wanamichezo kuweza kushiriki na kwa Tanzania tulikuwa na Waogeleaji wa tatu, mchezaji wa Judo na mchezaji wa kike wa mbio (Marathon) kwa hiyo, huo ndiyo upendeleo ambao wengi hawauelewi ni upendeleo upi”, alisema Bw. Gulam.

AIRTEL MONEY TIMIZA YAFANYA SEMINA NA MAWAKALA MKOA WA MWANZA.

0
0


Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitoa semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.
Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza kwa umakini wakisikiliza mafunzo juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.
Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitia msisitizo zaidi katika semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.
Mawakala toka viunga mbalimbali ndani ya jiji la Mwanza wamekusanyika hapa ndani ya ukumbi wa Gold Crest Hotel kwa nia ya kupata mafunzo.
Somo limekolea na Airtel Money Timiza.
Airtel Money Timiza ni mikopo nafuu isiyo na masharti magumu zaidi ya namba ya mteja ya mawasiliano na historia ya utumiaji wa huduma ya Airtel Money Timiza.
"Ili mteja apate kukopeshwa kiwango kikubwa cha fedha, Airtel Money Timiza itatizama Je ni mteja anatumia vipi mahamisho na uchukuaji wa fedha kupitia Airtel Money yake...?Kadri mteja anavyotumia Airtel Money zaidi ndivyo anavyopata nafasi ya kukopeshwa zaidi nacho kiwango kikipanda...." Somo la semina likiendelea
Washiriki kwa umakini na semina ya Airtel Money Timiza.
'MUDA NI MALI' = Jinsi Airtel Money Timiza inavyokomboa muda huku ikimkuza na kumnyanyua mwananchi toka lindi la umasikini.
Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Timiza, Rwebu Mutahaba akitoa semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.
David Wankuru ambaye ni Meneja wa Airtel Mkoa wa Mwanza akifafanua kilichofanyika ndani ya semina kwa mawakala, masharti na masuala yote juu ya Airtel Money Timiza.
Ni sifa zipi zitampa mteja fursa ya kuweza kukopeshwa na Airtel Money Timiza? Joel Laizer ambaye ni Meneja wa Mauzo Airtel Mwanza anafunguka zaidi.
Mawakala - Kalunde Kafiti na wenzake hapa wanafunguka mengi juu ya
1.Wazo la Airtel Timiza linamanufaa gani kwa wenye kufanya kazi ya miamala?
2. Nini Tahadhari kwa matapeli wanaoweza kuitumia Airtel Money Timiza kufanya yao?
3.Jeh Mikopo itawasaidiaje wajasiliamali ambao suala la mtaji limekuwa changamoto kubwa kwao?

Wadau wa Michezo washauriwa kuwekeza katika Viwanda.

0
0

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikata utepe kuashiria uzindua wa Channeli mbili za michezo ambazo ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Said Kiganja akionesha zawadi ya King’amuzi aliyopewa na Kampuni ya TING wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni hiyo Agosti 28,2016.


aibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa Michezoalipokuwa akizindua uzinduzi wa Channeli mpya za Michezo kutoka kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt .Veron Fernandez akielezea kuhusu faida za channeli mbili mpya za michezo kutoka katika kampuni yake zitakavyosaidia kukuza Michezo nchini Agosti 28,2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Fernandez wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.Picha na
Raymond Mushumbusi - WHUSM
 
Na Raymond Mushumbusi - WHUSM

Wadau wa Michezo nchini wameshauriwa kujenga viwanda kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya michezo ili kuleta maendeleo katika sekta hiyo.

Ushauri huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizindua channeli mbili za Michezo za Kampuni ya king’amuzi cha TING.

Naibu Waziri Anastazia alisema kuwa kwa kupitia uwekezaji huo kutasaidia kuinua sekta ya michezo nchini pamoja na kuondokana na changa moto ya vifaa vya michezo jezi za michezo,mipira na vifaa vinginevyo.

“Tuunge mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwekeza katika viwanda vitakavyotengeneza vifaa vya michezo” alisema Mhe. Anastazia

Aidha, Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa kuwepo kwa viwanda hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa vifaa vya michezo nchini kwani vifaa vingi vya vinatoka nje ya Tanzania hivyo huuzwa kwa bei ya juu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Frenandes ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wa Michezo nchini katika kukuza na kuendeleza sekta hiyo.

Chaneli za Michezo zilizozinduliwa katika Kingamuzi hicho ni ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 ambazo zitakuwa zikionesha michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.  

SERIKALI YAFUNGIA VITUO VYA REDIO VYA MAGIC FM NA REDIO 5 YA ARUSHA

0
0

Serikali yaahidi kutoa ushirikiano kwa TECC

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua na Meneja wa Ofisi wa TECC, Bi. Mwasiti Mkembe (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (kushoto) akimkabidhi kitabu cha Mpango Kazi wa miaka miwili cha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo, Bi. Beng’i Issa wakati wa uzinduzi rasmi wa TECC mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi. Beng’i pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bi. Beng’i Issa (wa pili kulia); mjumbe wa bodi hiyo, Dkt. Hassan Mshinda (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua (kushoto) wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi. Issa pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wakati Dkt. Mshinda pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Sehemu ya wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  

Serikali imeahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) inastawi na kufaidisha wananchi kwa kupitia miradi yake mbalimbali kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.

Akizungumza hayo katika uzinduzi rasmi wa TECC Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa watendelea kuwa pamoja na Taasisi hiyo ili kufikia malengo ya watanzania kiuchumi.

“Kwa niaba ya serikali natambua mchango wa wajasiriamali hivyo tupo pamoja na TECC kwa kila jambo watalofanya kwa ajili ya kusapoti uchumi wa nchi kupitia ujasiriamali katika kuelekea uchumi wa viwanda.” Alisema Mhe. Jenista

Mbali na hayo Mhe. Jenista amesema kuwa malengo ya TECC ni kuimarisha ubunifu na ushindani wa biashara ndogo na za kati za Tanzania kwa kuwavuta wajasiriamali waliopo ndani ya sekta isiyo rasmi, wahitimu wa vyuo na wengine wenye kutaka kuanzisha biashara zinazoongeza thamani kwa mazao na kutengeneza bidhaa nchini.

Aidha Mhe. Jenista amesema kuwa Biashara zikianzishwa nyingi na nyingi zikijipanua kiushandi ndivyo na serikali itapata mapato zaidi kupitia kodi hivyo uzalishaji uongezeke zaidi na zaidi kwa maendeleo ya nchi.

“Natoa wito kwa taasisi mbalimbali kuiunga mkono TECC,” alisema, akiongeza kuwa fursa za kusaidia ziko nyingi kama kuwajengea uwezo kina mama wajasiriamali, wazee wanaostaafu, au kupanua programu ya Kijana Jiajiri katika mikoa mingine ya Tanzania.

Mbali na hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TECC, Bi. Beng’i Issa alisema tangu kuanza kazi miaka miwili iliyopita, kwa kutumia rasilimali chache, taasisi hiyo imeweza kujipanga na kuonyesha mafanikio makubwa katika kujenga uwezo wa wananchi kumiliki uchumi.

“Tunahitaji kufanya zaidi ya hapa na uwezo huo tunao kama tutaungwa mkono na Serikali kikamilifu ili kuweza kutekeleza wajibu wa sera yetu katika kunyanyua wajasiriamali kwa maendeleo ya taifa,” alisema Bi. Beng’i

Aidha Bi. Beng’i amesema kuwa mpaka sasa TECC imeshatekeleza miradi miwili muhimu ambayo ni mradi wa Kijana Jiajiri ambao unatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Uingereza la Youth Business International (YBI) na kufadhiliwa na umoja wa makampuni yanayochimba gesi na mafuta katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Bi. Beng’i amesema kuwa Kupitia mradi wa Kijana Jiajiri na ufadhili wa shirika la International Youth Foundation ambalo limepata fedha kutoka Master Card Foundation vijana 1,250 watajengewa uwezo katika mikoa ya Mtwara, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma kuanzia mwezi ujao wa Tisa.

Kwa mujibu wa Bi. Beng’i, mradi wa pili ambao TECC imeufanya ni kwa kushirikiana na mradi wa BEST-Dialogue wa kufanya utafiti wa maoni ya wamiliki wa biashara ili kupata changamoto ambazo zinazuia ushindani kibiashara katika mradi wa Business Leaders Perception.

SERIKALI YAVIFUNGIA VITUO VIWILI VYA REDIO LEO JIJINI DAR

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, wakati akitangaza kuzifungia radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi na kuvirusha hewani ambavyo vinaashiria uchochezi.

Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akitoa ufafanuzi alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Wanahabari,wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kivifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi vyenye maudhui yenye viashiria vya uchochezi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi ambavyo vimerushwa hewani vinavyoashiria uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baaa ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda wa saa 2 usiku hadi saa 3 na kituo cha utangazji cha Radio 5 pamoja na kipindi cha Morning Magic katika kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani.

Nape amesema kuwa kufuatia hilo amevifungia kwa muda usiojulikana kwani wamekiuka masharti ya kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.

Wakati vituo hivyo vikifungiwa kwa muda usiojulikana kamati ya maudhui imepewa jukuu la kuviita na kusikiliza kwa kina Zaidi utetezi wao na ni hatua gani zaidi ya kuchukua dhidi yao kwa mujibu wa kanuni ya huduma za utangazaji.

Nape ameendelea kuvitahadhalisha vyombo mbalimbali vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda heshima ya tasnia yetu na wakati huo kuhakikisha nchi inabaki na Amani, Mshikamano na Umoja.

JUMUIYA YA WATANZANIA WALIOSOMA CHINA YAPATA UONGOZI MPYA

0
0

mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dk. Mahame Paulo akizungumza na wanajumuiya ya CAAT
Wanachama wa CAAT wakiwasikiliza viongozi wao wa mpito
Gustavu Sanga Gustavu Sanga mwenyekiti wa uchaguzi CAAT akitoa maelekezo kwa wajumbe wa CAAT

Jumuiya ya watanzania waliosoma China – CAAT wameishauri serikali kuwatumia wasomi hao katika kuhakikisha inanufaika na mikataba na masuala mbalimbali yahusuyo TANZANIA na CHINA. 

Wakizungumza katika mkutano mkuu wa kuchagua uongozi mpya wa jumuiya hiyo wanachama wa CAAT wameeleza kuwa Watanzania waliosoma China wanaijua nchi hiyo vizuri, tabia za wachina na lugha yao hivyo wakishirikishwa kabla ya kusainiwa kwa mikataba au kuingia makubaliano yeyote wanaweza kuwa chachu ya nchi kunufaika zaidi.

Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya hiyo Dk.Mhame Paulo aliyeenda kusoma china miaka ya 80 amesema, sera ya Tanzania ya viwanda inaweza kutimia ndani ya miaka mitano kwakuwa Tanzania inauwezo wa kuzalisha na kuuza katika soko la China akitolea mfano uwezo wa Tanzania kutengeneza dawa za kutibu ugonjwa na pumu na kuziuza katika soko la China na dunia kwa ujumla.

Mwenyekiti mpya wa CAAT, Dk.Liggyle Vumilia akishukuru baada ya kuchaguliwa amesema wanachama wa jumuiya hiyo wakitumika Tanzania itapata manufaa kwakuwa wanachama wake wanajua kuongea kichina, wanajua tabia za wachina na wanaielewa china vyema kiasi cha kujua kitu gani kinapatikana wapi hivyo serikali ikiwatumia itaepuka udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa wazalendo.

Uchaguzi wa jumuiya wa watanzania waliosoma China umewaweka madarakani viongozi wa masuala mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti, katibu, mwekahazina, mkurugenzi wa masuala ya bisahara na uwekezaji, mkurugenzi wa sanaa, utamaduni na utalii, mkurugenzi wa masuala ya elimu na Tehama pamoja na mkurugenzi wa takwimu , habari na mawasiliano.

Uhusiano wa Tanzania na China una zaidi ya miaka hamsini na watanzania wamenufaika na uhusiano huo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kwenda kusoma china na idadi yao kuzidi kuongezeka kila mwaka hali iliyopelekea kuundwa jumuiya watanzania waliosoma China. Tayari jumuiya hiyo ya watanzania waliosoma China imekwishapata usajili katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi tangu mwezi wa Juni 2016

TUZO YA MWAJIRI BORA 2016 YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR.

0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa NHO, Joyce Nangai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua Tuzo ya Mwajiri bora wa mwaka 2016 ambayo itakuwa ikihamasisha na kuendeleza rasilimali watu ili kuleta maendeleo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa NHO, Joyce Nangai.Baadhi ya wafanyakazi na waandishi waki msikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlimuka.
Picha na Avila Kakingo.

CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wazindua Tuzo ya Mwajiri bora wa 2016 ambayo itakuwa ikihamasisha na kuendeleza rasilimali watu ili kuleta maendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Aggrey Mlimuka amesema kuwa kwa mwaka huu hafla ya tuzo hiyo itafanyika Desemba.

Mlimuka amesema kuwa lengo la tuzo hiyo ni kutambua wanachama wenye sera nzuri za usimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na makampuni mbalimbali mwanachama hapa nchini.

Amesema kuwa tuzo hiyo itafuata mbinu za Kisayansi na kitaalamu ili kuangalia umuhimu wa Rasilimali watu katika makampuni ya Kibiashara makubwa na madogo na yale ya kati ili kuinua ujuzi wa wafanyakazi wanaofanya kazi kwa kujituma sehemu zao za kazi.

Amesema tukio lakutafuta msihindi wa tunzo hiyo limegawanyika katika makundi mawili ambapo wataanza kufanya utafiti kwa kutumia Mshauri mwelekezi pamoja na kuwa na hafla ya tuzo itakayo fanyika Desemba mwaka huu.

Amesema kuwa kwa tunzo ya mwajiri bora mwaka huu wataangalia kipengele cha ushirikishaji wa watu wenye ulemavu pamoja na hali ya kujali wafanyakazi katika sehemu za kazi.

Mlimuka amesema kuwa tuzo hio pia itajikita zaidi katika kuangalia maeneo muhimu ya rasilimali watu, uongozi,utawala, usimamizi wa Rasilimali watu, kusaidia jamii pamoja na kuwajibika katika jamii, ubora na uzalishaji, amesema kuwa wanachama ashiriki kujaza kwa mkono dodoso kwaajili ya kushiriki.

TAMASHA LA UHONDO WA ZANTEL LAKONGA NYOYO ZA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM

0
0

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetesa na wimbo wake maarufu wa ‘Unanitega Shemeji’, Selemani Jabil ‘MsagaSumu’ akifanya vitu vyake wakati wa tamasha la ‘Uhondowa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Zantel.
 Meneja Habari na Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel,Winnes Lyaro (kulia)  akitoa maelezo kwa  baadhi ya wakazi wa Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la  Dares Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu huduma mpya zitolewazo na kampuni hiyo ikiwa ni moja ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika kuboresha bidhaa zake  na kutoa huduma bora kwa wateja. Ilikuwa ni katika tamasha lililopewa jina la Uhondo wa Zantel lililodhaminiwa na kampuni hiyo.
 Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia)  akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa maswali ya papo kwa papo wakati wa tamasha la ‘Uhondo wa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Tamasha hilo lililodhaminiwa na Zantel kama sehemu ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika kuboresha bidhaa zake na kutoa huduma bora kwa wateja.

CUF YAWAVUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE 11,AKIWEMO PROF LIPUMBA NA MAGDALENA SAKAYA

0
0
Chama Cha Wananchi (CUF) kimewasimamisha uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba 
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Bara, Magdalena Sakaya,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kaliua Mkoani Tabora.


 
TAARIFA RASMI

Awali ya yote naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na uzima wa afya na tukaweza kukutana hapa asubuhi hii ya leo. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu pia kwa kuijaalia nchi yetu kuendelea kubaki katika hali ya amani na utulivu licha ya matatizo mengi yanayotukabili.

Pili, nichukue fursa hii kukushukuruni nyinyi waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu na kuja kutusikiliza. Ni imani yangu kuwa kama ambavyo mmekuwa mkitupa mashirikiano mazuri katika kuwafikishia wananchi yale ambayo chama chetu kupitia kwenu kimekuwa kikiyatolea taarifa, kwa uzito wa kipekee taarifa hii nayo mtawafikishia Watanzania wote kupitia vyombo vyenu vya habari.

Ndugu Waandishi wa habari,

Tumewaita leo hii kuwaeleza juu ya maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa katika kikao chake cha dharua kilichofanyika jana, Jumapili ya tarehe 28/08/2016 Katika ukumbi wa Makao Makuu ya Chama, ofisi za Vuga. Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa muda Mhe, Hamidu Hassan Bobali, Mbunge wa Jimbo la Mchinga kilihudhuriwa wa Wajumbe 46 katika ya Wajumbe 60.

Ndugu Wandishi wa Habari,

Kama mnavyojua tarehe 21/08/2016 Chama Cha Wananchi – CUF kilikuwa na Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa uliofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa na agenda mbili kuu, ambazo ni:-

1.    Kupokea barua ya Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ya kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti ya tarehe 05/08/2015; na

2.    Kufanya Uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi - Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Kufuatia hujuma za makusudi zilizoandaliwa kwa mashirikiano ya maadui wa ndani na nje ya chama, aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa Mkutano Mkuu Maalum, Mhe Julius Mtatiro alilazimika kuakhirisha Mkutano ule mara baada ya kumalizika kwa ajenda ya kwanza ambapo Mkutano Mkuu uliridhia kujiuzulu kwa Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba kwa azimio lililoungwa mkono na wajumbe 476 dhidi ya wajumbe 14 waliokataa. Hivyo basi agenda namba 2 haikuwahi kukamilishwa, na kwa hivyo haikufanyiwa maamuzi.

Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi, kilichokaa jana kimejadili kwa kina juu ya hujuma za kuvuruga Mkutano Mkuu Maalum wa tarehe 21/08/2016. Baraza kuu limesikitishwa sana na kitendo kile ambacho mbali ya kukisababishia chama hasara ya zaidi ya Shillingi milioni 600, pia kimepelekea kuharibu taswira ya chama ndani na nje ya nchi.

Baraza Kuu lilipata nafasi ya kupokea maelezo ya kina kutoka kwa wajumbe mbali mbali hasa wale wanaotokea Tanzania Bara walioeleza kwamba hujuma zilizofanywa kuvuruga Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016 hazikuwa za bahati mbaya au za kushtukiza bali ni matokeo ya njama na mbinu ovu na chafu ambazo zimekuwa zikipangwa na kutekelezwa chini kwa chini kwa muda mrefu. Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa walieleza kwa ushahidi jinsi baadhi ya viongozi wa Chama walioaminiwa na kupewa nyadhifa za juu walivyogeuka na kuanza kutumiwa na maadui wa nje ya Chama kukihujumu Chama.

Baraza Kuu limezingatia kuwa CUF ni chama cha kistaarabu, ni Chama cha Kidemokrasia na ni Chama chenye kutoa matumini ya mabadiliko ya kweli kwa Watanzania walio wengi. Vurugu zilizojitokeza ni aibu na fedheha kwa chama chetu mbele ya macho ya Watanzania na wapenda demokrasia.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeridhika kwamba watu hao waliokuwa vinara wa vurugu na njama hizo ovu walipewa nafasi mara kadhaa kujirekebisha dhidi ya mwendo wao huo dhidi ya Chama lakini waliendelea na vurugu na hujuma zao hizo. Kwa hatua iliyofikia, Baraza Kuu limeona halina njia nyengine ya kukinusuru Chama isipokuwa kuchukua hatua kali na madhubuti kukilinda Chama ambao ni wajibu wake kikatiba.

Kwa msingi huu basi, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa kauli moja (unanimously) limeamua kuchukua hatua za kinidhamu kwa viongozi na wanachama mbali mbali waliohusika kwa njia moja au nyengine katika kuchochea vurugu zile. Baraza kuu limechukua hatua mbili kubwa ambazo ni kutoa karipio kali, kusimamisha na kufukuza uanachama wahusika wote walioshiriki kuchochea vurugu hizo.

Viongozi waliopewa karipio kali kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 83 (5)(b) ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ni:

1.    Rukiya Kassim Ahmed na

2.    Athumani Henku

Viongozi waliosimamishwa uanachama kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 83 (5)(c), hadi hapo watakapopata fursa ya kujieleza mbele ya Baraza Kuu ni;

1.  Prof Ibrahim Haruna Lipumba
2.   Magdalena Sakaya
3.   Abdul Kambaya
4. Ashura Mustafa
5.  Omar Mhina Masoud
6.  Thomas Malima
7.  Kapasha M. Kapasha
8.          Maftaha Nachumu
9.Mohamed Habib Mnyaa
10.   Haroub Shamis
na
11.       Mussa Haji Kombo

Mwanachama aliyefukuzwa chama ambaye alipata fursa ya kujieleza mbele ya Baraza Kuu na kikao kuamua kumfukuza chama kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 83 (5)(c) ni aliyekuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wazee wa CUF (JUWACUF), Shashu Lugeye.

Kufuatia maamuzi hayo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limewateua viongozi mbali mbali kukaimu nafasi mbali mbali zilizoachwa wazi.

Kwa kuzingatia kwamba kutokamilika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016 kulipelekea kushindwa kufanyika kwa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limetumia uwezo liliopewa na Katiba ya Chama, Ibara ya 101 na 118, kuunda Kamati ya Uongozi ambayo itakuwa ikifanya kazi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hadi hapo uchaguzi wa kujaza nafasi hizo utakapofanyika. Baraza Kuu la Uongozi limewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati hiyo ya Uongozi:

1.    Mhe. Julius Mtatiro – Mwenyekiti;

2.   Mhe. Katani Ahmed Katani – Mjumbe; na

3.    Mhe. Severina Mwijage – Mjumbe.

Aidha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, kwa kufuata Ibara ya 105 (1) na (3) ya Katiba ya Chama, limemteua Mhe. Joran Bashange kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama kwa upande wa Tanzania Bara na Mhe. Mbarala Maharagande kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma hadi hapo nafasi hizo zitakapojazwa rasmi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Chama.

Mwisho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawahakikishia wanachama na wapenzi wake na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Chama Cha Wananchi – CUF kipo imara na makini na katu hakitoyumbishwa kwa hila na njama ovu na chafu zinazofanywa na maadui wa chama hichi. Tangu kuasisiwa kwake, CUF imeandamwa na maadui wa kila aina, na imepitia katika misuko suko mingi. Tunaamini hila na njama hizo ovu zimekuwa zikielekezwa CUF kwa kutambua kwamba Chama hichi ndicho kinachobeba dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli hapa nchini.

Kutokana na umadhubuti, umakini na uimara wa Katiba ya Chama na safu ya viongozi wake, CUF imeweza kuvuka salama kila ilipoingia katika misuko suko hiyo na kwa hivyo, hata wimbi hili lililoonekana kukitikisa Chama limekabiliwa ipasavyo na sasa kazi iliyopo mbele yetu ni kuendeleza harakati za kisiasa za kuwaletea Watanzania wa Bara na Zanzibar mabadiliko wanayoyataka.

 
HAKI SAWA KWA WOTE
Nassor Ahmed Mazrui- +255 777 426 975
NAIBU KATIBU MKUU CUF
Mawasiliano: Mkurugenzi Habari - Salim Biman 077414112
K/Naibu Mkurugenzi :  Mbarala Maharagande- 0784 001408

MSANII NIGERIA ATOA MSAADA KWA KITUO CHA KULELEA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU CHA KIGAMBONI COMMUNITY CENTER

0
0

Msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule(kushoto) leo Jijini Dar es Salaam Katikati ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.Msanii hyo yupo nchini kufuatia ziara yake kwa Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Mahusiano ya Umma ya LAS Consultancy. Picha na Frank Shija


Mwanzilishi wa Kampuni ya Mahusiano ya Umma, LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tinny Entertainment kutoka Nigeria Arokodare Timilehin akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE (wa tatu kutoka kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.
Msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake katika Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Uhusiano wa Umma ya LAS Consultancy ya Jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto ni Mwanzilishi wa Kampuni ya LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana, Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina ya uongozi wa LAS Consultancy walipokuwa wakimtambulisha msanii kutoka Nigeria Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE ambaye yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kutembelea Vyombo vya Habari.

Na Sheila Simba

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Omo Alhaji,Jagabana maarufu YCEE,ametoa msaada wa shilling million 1,kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Kigamboni Community Center(KCC).

Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo jijini Dar es salaam mratibu wa ujio wa msanii huyo bi Salha Kibwana amesema kuwa msanii YCEE ametoa msaaada huo katika kituo hicho kwa lengo la kusaidia watoto hao ili kujipatia mahitaji maalum ya kila siku wawapo kituoni hapo.

“Ametoa msaada huo kutokana na faaida anayopata katika kazi zake usanii ili kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu wa elimu kwa jamii hasa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,”alisema Salha

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo hicho Mbwana Msangule,amesema kuwa kituo chake kinalea watoto hao ili kuwasaidia kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.

“msaada huu utasaidia sana kwasababu kituo kina watoto 14 wanaoishi kituoni hapo na wengine wanakuja na kurudi makwao,na nashukuru sana kwa msaada huu kwani ni sanii wa kwanza kutoka msaada,nawaomba pia wasanii wa ndani kijitokeza kutoa msaada”alisema Mbwana

Kwa upande msanii huyo amesema kuwa amekuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuonana na wasanii wengine wakubwa wa Tanzania huku akiwataja Diamond na Ali Kiba,ameongeza kuwa amefurahi pia kuktana na mashabiki wake ambao amekua wakichati kupitia mitanzandao ya kijamii

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, MHE. GEORGE MASAJU AVIASA VYAMA VYA SIASA KUHESHIMU KATIBA YA NCHI

0
0
 
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua masuala mbalimbali kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo. 
 “Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”. Amesema Mh.Masaju.
 Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju alipokuwa akizungumza nao masuala mbalimbali yaliyohusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua jambo alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Waandishi wa Habari kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,jijini Dar leo.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua masuala mbalimbali kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.PICHA NA MICHUZI JR

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar leo,Masaju amesema kuwa polisi wamesema kuwa wana hali ya kuzuia mikutano na maandamano iwapo watabaini kuwa yataibuka mambo yatakayohatarisha amani ya nchi,Masaju amesema kuwa maandamano hayo yataleta madhara na athari kama maandamano hayo ya UKUTA-Septemba mosi mwaka huu.

Amesema kuwa madhara na athari ya maandamano hayo ni kubwa kutokana na siku hiyo itakuwa mahsusi kwa ajili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwao,akaonngeza kuwa siku hiyo kutakuwa na tukio muhimu la kupatwa kwa Jua huko Lujewa mkoani Mbeya ambapo ni muhimu kwa nchi kupata manufaa kwa Watalii kuja kwa wingi na kuweza kunufaika Kiuchumi. 

Masaju amesema kuwa vyama vya siasa nchini vinatakiwa kutumia vyema haki zao za msingi zilizoanishwa katika katiba badala ya kutumia, nguvu, ubabe na kupelekea kutishia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

Masaju amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya wanasiasa wanaotoa vitisho vya kuitisha mikutano kinyume na taratibu za kisheria kwa kisingizio cha haki za kikatiba jambo ambalo sio kweli.“Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”.

Masaju aliwataka Wanasiasa kuwa wakweli na kuacha kuwapotosha wananchi kuwa wananyimwa haki ya kufanya mikutano kwani wapo baadhi yao wanaofanya mikutano katika majimbo yao baada ya Jeshi la Polisi kujidhirisha kwamba kutakuwa na hali ya amani na utulivu”. Alisema Mhe. Masaju.

Aidha Masaju alipongeza juhudi zinazofanywa na viongozi mbalimbali wa dini nchini kwa jitihada wanazofanya za kushauri katika kufika muafaka wa hali ya kisiasa nchini na kuwashauri kuhubiri amani na utulivu kwa waumini wao. 

Akitoa ufafanuzi wa tamko la baadhi ya vyama vya upinzani kutaka serikali kuvifuta vyama hivyo Mhe. Masaju alisema kuwa suala hilo ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu katiba hiyo inaruhusu mfumo wa vyama vingi.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images