Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAIOMBA UONGOZI WA AGAKHAN KUJENGA HOSPITALI NYINGINE KUBWA MKOANI DODOMA

$
0
0


Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa tatu kulia akitia udongo kwenye kichanja cha nondo kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa awamu ya pili wa jengo la hospitali ya Agakhan katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan.
Wafanyakazi na wadau mbalimbali wa hospitali ya Agakhan wakimsikiliza kwa kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa sherehe ya uzinduzi wa ujenzi wa awamu ya pili wa jengo la hospitali ya Agakhan.


Habari/Picha Na Ally Daud

Serikali imeuomba uongozi Wa Agakhan kujenga hospitali nyingine kubwa katika mkoa Wa Dodoma ili kuendana na agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt.John Magufuli na kuboresha huduma bora za afya Mkoani humo.

Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya jengo la hospitali ya Agakhan Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa Agakhan wanatakiwa wajenge hospitali nyingine kubwa mkoani Dodoma ili kueneza Huduma bora za kiafya.

"Kutokana na Agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli la kuhamia Dodoma inabidi na nyinyi mjenge hospitali kule" alisema Mhe. Ummy. Mhe. Ummy ameongeza kuwa kwa kujengwa hospitali hiyo Serikali itakua iokoa shilingi billion 20 mpaka 25 kwa ajili ya wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Aidha Mhe.Ummy amesema kuwa anaushukuru uongozi Wa Agakhan kwa kuanza kujenga jengo ilo linalogharimu Billioni 112 ili kuondoa kero kwa wagonjwa Wa magonjwa yasioambukiza na kurahisiaha huduma na matibabu bora kwa wagonjwa nchini.

Mbali na hayo Mwenyekiti wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan amesema kuwa wanampango Wa kumaliza jengo hilo kwa ajili ya kutoa Huduma bora za kiafya nchini ili kutokomeza maradhi ya mara kwa mara.

"Tuna morali kubwa ya kumalizia jengo hili ili tuweze kuboresha Huduma ya afya nchini kwa kutoa tiba zenye uhakika na za kisasa" alisema Bi Zahra

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA MAGARI MAWILI YA KUBEBEA WAGONJWA YENYE THAMANI YA SH MIL 80 KUTOKA UBALOZI WA JAPAN

$
0
0


Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akionyesha funguo ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kupokea msaada wa magari mawili kutoka Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili, kulia ni Balozi wa Japan Bw. Masaharu Yoshida nae akionyesha funguo mojawapo ya gari hizo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kupokea gari la kubebea watoto katika Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili kutoka kampuni ya Bango Sangho na kulia ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Niladri Chowdhury.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyepiga katikati akifurahia jambo na watoto walio katika Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili wakati alipopokea gari la kubebea watoto katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam na kulia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Bango sangho Bw. Niladri Chowdhury.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na wajumbe ya bodi ya udhamini ya Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili wakati alipozindua bodi hiyo leo jijini Dar es salaam na wa kwanza aliyekaa kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Charles Majinge

Habari/Picha Na Ally Daud

Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa magari mawili ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi milioni 80 kutoka ubalozi Wa Japan kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Akipokea msaada wa magari hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa anashukuru kwa msaada huo kwani utarahisisha huduma kwa wagonjwa wa hospitali hiyo.

"Nashukuru kwa msaada uliotolewa na serikali ya Japan na wasichoke kutusaidia katika kuboresha sekta ya Afya nchini" alisema Mhe. Ummy.

Kwa upande wa Balozi Wa Japan Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa hawatachoka kutoa msaada kwa Tanzania ili kuboresha sekta ya afya na kuweka mahusiano bora kati ya Japan na Tanzania. " Hatutachoka kutoa msaada kwa Tanzania kwani tunaboresha sekta ya afya na kudumisha mahusiano yetu" alisema Bw. Yoshida

Kwa wakati huohuo Waziri Ummy amepokea gari lingine la kuwabebea watoto kutoka kwa kampuni ya Bango Sangho ili kurahisisha kuwapeleka katika kliniki mbalimbali jijini Dar es salaam.

Akikabidhi gari hilo Mwenyekiti wa kampuni ya Bango Sangho Bw. Niladri Chowdhury amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuwarahisishia watoto kupelekwa kliniki kwa haraka pindi inapohitajika na kuokoa maisha yao.

Mbali na hayo Waziri Ummy pia amezindua bodi ya udhamini katika hospitali ya Muhimbili amabayo itadumu kwa muda wa miaka mitatu ili kufanya huduma za ya hospitali hiyo kuwa bora zaidi kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini.

Akizungumza katika uzinduzi Wa bodi hiyo Mhe. Ummy amesema kuwa bodi hiyo iwe ya kiutendaji na kutatua matatizo ya wagonjwa na sio kua kero kwa wafanyakazi na wananchi.

Aidha Waziri Ummy ameitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana na wizara pamoja na menejimenti ya hospitali hiyo ili kuleta huduma bora za kiafya kwa maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.

Kwa upande wa Mwenyekiti mpya wa bodi ya udhamini ya MNH Dkt. Charles Majinge amesema kuwa amepokea nafasi hiyo kwa mikono miwili na kuahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini kwa kushirikiana na Wizara.

“Licha ya changamoto zilizopo nimeipokea nafasi hii kwa mikono miwili na kuhaidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini kwa mda uliopangiwa ili kuleta maendeleo ya huduma bora kwa jamii.

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (katikati), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China, Kulia ni Msaidizi wa Balozi, Wang Fang. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiangalia vipengele mbalimbali vinavyohusu ushirikiano juu ya masuala ya ulinzi na usalama, wakati wa mazungumzo yaliyomhusisha Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing(kulia). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong(kulia), Msaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania, AI Zhuan(katikati) na Katibu wa Balozi, Dong Zhenyu(kushoto), wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAZIRI NCHEMBA ATEMBELEA ENEO LA TUKIO LA MAUWAJI YA ASKARI POLISI HUKO MBAGARA, JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba usiku wa kuamkia leo, alifika eneo la Mbagara Mbande Wilayani Temeke, Jijini Dar es salaam na kujionea eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo inadaiwa kuwa watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha za vita, walivamia eneo la Benki ya CRDB - Mbande na kuwashambulia kwa risasi Askari waliokuwepo eneo hilo na kupekea vifo vya askari hao ambao walikuwa wanne wakati walipokuwa wakishuka  kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.

Waziri Nchemba pia aliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi ambao ni raia wa kawaida wawili, ambao hali zinaendelea vizuri.

Waziri Nchemba amelaani tukio hilo na matukio mengine kama haya, na kutoa rai kwa wahusika kujisalimisha wenyewe, na kuwaomba wananchi na raia wema kutoa ushirikiano wa kifichua waovu wa matukio ya namna hiyo na mengine mengi, ili kupambana na wahalifu hao wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro, wakati walipokuwa eneo la tukio.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro wakionyesha maeneo mbali mbali ya Gari la Polisi lilivyoshambuliwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimjulia hali mmoja wa Raia aliejeruhiwa katika tukio hilo.
Muonekano wa gari ya Polisi iliyokuwa ikitumiwa na Askari hao.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA RASMI WODI MPYA YA HOSPITALI TEULE YA NKASI MKOANI RUKWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mama Mary Majaliwa kwa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Zelote Stephene na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, wakikata utepe kuashiri ufunguzi rasmi wa wodi mpya ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Nkansi, katika ziara ya mkoa wa Rukwa Agosti 23, 2016. nyuma yake ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua pazia kuashiri ufunguzi rasmi wa wodi mpya ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Nkansi, katika ziara ya mkoa wa Rukwa Agosti 23, 2016. nyuma yake ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua vitanda katika wodi mpya ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Nkansi baada ya kuizindua akiwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa Agosti 23, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary na wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Zelote Stephene.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye Hospitali Teule ya wilaya ya Nkansi baada ya kufungua wodi akiwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa Agosti 23, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HAKUNA MWANASIASA ATAKAYERUHUSIWA KUVURUGA AMANI - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inalinda amani ya nchi kwa gharama zozote na kamwe haitoruhusu mwanasiasa yeyote kusababisha vurugu zitakazochochea uvunjifu wa amani.

“Hatuzuii kuwa na vyama vya siasa ila haturuhusu vurugu kupitia vyama vya siasa na hakuna jambo lisilokuwa na mipaka. Mambo ya kuhamasishana kufanya vurugu hatutayaruhusu, tunataka watu wafanye kazi,” alisisitiza.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Agosti 23, 2016) wakati akizungumza na viongozi wa dini pamoja na wazee wa mkoa wa Rukwa mara baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Nkansi akiwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa, Agosti 23, 2016.

Alisema Serikali inataka Watanzania wawe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi zao za kuwaingizia kipato na kuwaletea tija, hivyo suala la kudumisha amani ni muhimu kwani vurugu zikitokea hawatakuwa na mahali pa kukimbilia na hakuna shughuli ya maendeleo itakayofanyika.

“Suala la uhamasishaji wananchi juu ya utunzaji wa amani ni la lazima hivyo viongozi wa dini na wazee kwa pamoja tushirikiane katika kukemea vitendo vya uchochezi kwasababu vurugu zikitokea Watanzania hatuna mahali pa kukimbilia,” alisema.

Aidha, Waziri Mkuu aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa pamoja na viongozi wake kwa sababu kazi ya uongozi ni ngumu na inachangamoto nyingi.Pia aliwaagiza viongozi wa dini wa mkoa wa Rukwa kuharakisha uundwaji wa Kamati ya Amani ya mkoa huo.

Awali, Sheikh wa mkoa wa Rukwa, Sheikh Rashid Akilimali amesema madhehebu ya dini hayawezi kuvuruga amani ya nchi ila anahofu na viongozi wa vyama vya siasa kutokana na vitendo vyao vya kuhamasisha vurugu.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri na mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa St Maurus mjini Sumbawanga Agosti 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kufuatia hali hiyo Sheikh Akilimali aliwaomba wanasiasa nchini kutovuruga amani kwani machafuko yakitokea watashindwa kufanya ibada mbalimbali ikiwemo kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sheikh Akilimali alisema kwa sasa wananchi wako huru kwenda kufanya ibada misikiti na makanisani kutokana na uwepo wa amani, hivyo aliwasisitiza wanasiasa kutothubutu kuichezea amani.

“Tafadhalini wanasiasa msituharibie amani ya nchi yetu. Amani haichezewi tunaona kwa wenzetu wanavyohangaika, wanaishi kwa tabu sisi hatujazoea  kukimbia. Sisi Watanzania ni moja na tunaishi kwenye nyumba moja hivyo hatuna budi kushirikiana kuilinda amani yetu,” alisema.

Kwa upande Katibu wa Wazee mkoani Rukwa, Kanali Mstaafu, John Mzurikwao alimuomba kiongozi huyo kuwasaidia  kutatua kero mbalimbali zinazoukabili mkoa huo zikiwemo za malipo ya pembejeo kwa mawakala wa kilimo pamoja na mgogoro wa ardhi katika shamba ya Efatha.

Waziri Mkuu alisema suala la malipo kwa mawakala wa pembejeo za kilimo linafanyiwa kazi na watalipwa baada ya Serikali kukamisha zoezi la uhakiki wa madeni hayo ili kujiridhisha kama kweli wakulima wapatiwa pembejeo na kwa kiwango gani.

KOREA KUSINI YATOA BILIONI NNE KUJENGA KITUO CHA TAARIFA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI .

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bnge la Korea Kusini wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketance  akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
  Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akisalimiana na wadau wa utalii,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Zara(katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy Chamburo.(kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kibo Safari's ,Willy Chamburo (katikati) akizungumza jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema.
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha  kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa  kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa katika Hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa.
Moja ya eneo lilipo sasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo inatumika kutoa taarifa kwa njia ya picha za video za Hifadhi hiyo.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa Taifa ,Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake  Prof,Dkt Bernhard Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema.
  Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika michoro ya kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
Wajumbe wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA ) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog Kanda ya Kaskazini.
 
Hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti kwa kushirikiana na  serikali  ya  Korea  ya Kusini imeanza mchakato wa ujenzi  wa  kituo  cha  kimataifa cha kutunza tarifa za  mienendo  ya  Wanyamapori kitakachojulikana kama Serengeti Internatinal Media Centre.

Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi  shilingi bilioni nne kitajengwa katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .

Tayari  serikali  ya  Korea  Kusini   imeshatuma  wajumbe  wake  kuja  nchini  tanzania  kujionea  eneo  kitakapojengwa  kituo  hicho  na  kukamilisha  taratibu  nyingine  muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park Joosung  amesema mradi huo ni mwendelezo  wa ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.

Akizungumza  na  ujumbe  huo  mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti  Wiliam Mwakilema  amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu utalii na kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.

Naye mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance  amesema ujenzi utaanza mwezi october mwaka huu na unatarajiwa kumalizika  baada ya miezi 14.

Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla aagiza Hospitali zote nchini kufanya ukarabati wa vifaa vya Mahospitali

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza Hospitali zote nchini kuweza kufanya ukarabati wa vifaa vyote vya Mahospitali yao ambavyo wamerundika stoo, ili kusaidia kupunguza gharama za manunuzi ya vifaa vipya ambavyo ni gharama kubwa.

Dk. Kigwangalla ameyasema hayo Wilayani Meatu, Mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo amepongeza juhudi za Hospitali ya Meatu kwa hatua yao ya kuamua kufanya ukarabati wa vifaa vyote vya Hospitali hiyo huku wakiokoa mamilioni ya fedha.

“Napongeza Hospitali ya Meatu kwa ubunifu huu waliofanya. Kwani wameweza kuokoa mamilioni na hii napenda kutoa maagizo kwa Hospitali zote hapa nchini kuhakikisha wanakarabati vifaa hivyo ambavyo vingi wamekuwa wakirundika tu stoo kwa kufanya hivyo watasaidia kupunguza gharama.” Amesema Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.

Hospitali hiyo ya Meatu imeweza kufungua kalakana ya kufanyia matengenezo na ukarabati wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda vya wagonjwa pamoja na vifaa vingine vingi ambavyo kwa manunuzi yake ni gharama kubwa sana.

Naibu Waziri huyo pia amepata kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo ikiwemo sehemu za Mahabara, Chumba cha upasuaji, wodi ya Wakinamama, kitengo cha meno, mapokezi na bohari ya chanjo ya Wilaya pamoja na duka la dawa la wilaya hiyo ndani ya Hospitali huku akikuta mapungufu kadhaa ambayo amwaagiza wawe wameyashughulikia ndani ya miezi mitatu kabla ya kuchukuliwa hatua thabiti pindi watakapokiuka
Tazama Mo tv, hapa:
DSC_6137Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa baadhi ya vitanda vya Hospitali vilivyofanyiwa ukarabati
DSC_6150
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akishuhudia baadhi ya vitanda vya Hospitali vilivyofanyiwa ukarabati
DSC_6158
Baadhi ya vitanda vilivyofanyiwa ukarabati
DSC_6160
Vitanda vya kujifungulia wodi ya wazazi.. ambavyo inaelezwa kuwa kitanda kimoja kina gharimu zaidi ya milioni moja na nusu
DSC_6147
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa baadhi ya vitanda vya Hospitali vilivyofanyiwa ukarabati
DSC_6163DSC_6148
Baadhi ya vitu vya Hospitali hiyo ya Meatu
DSC_6190
Ukaguzi ukiendelea
DSC_6195DSC_6218Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua Chumba cha Upasuaji ambapo hata hivyo alikuta mapungufu mbalimbali na kuwapa miezi mitatu wawe wamerekebisha
DSC_6222
chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Wilaya ya Meatu
DSC_6268
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiingia kwenye Kituo cha Afya Mwandoya ambacho licha ya udogo wake, kimeanzisha huduma za upasuaji miezi 6 iliyopita na hadi sasa tayari wamefanya Operesheni 40, zote zimefanikiwa.
DSC_6270
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meatu namna ya kituo hicho licha ya udogo wake lakini kipo na viwango kamili namna ya Chumba cha upasuaji kinavyotakiwa kiwe. Ambapo pia ametoa wito kwa vituo vyote vya Afya kuhakikisha wanajenga ama kukarabati chumba cha upasuaji.
DSC_6282
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimjulia hali mmoja wa watoto ambaye alifanyiwa operesheni kwenye kituo cha Afya Mwandoya,Wilayani Meatu ambacho licha ya udogo wake, kimeanzisha huduma za upasuaji miezi 6 iliyopita na hadi sasa tayari wamefanya Operesheni 40, zote zimefanikiwa.
DSC_6295
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho cha Mwandoya, kilichopo Wilayani Meatu, Mkoani Sumiyu.
DSC_6297Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa amembeba mmoja wa watoto aliyejifungua siku hiyo wakati ametembelea kituo hicho cha Mwandoya ambacho licha ya udogo wake, tayari wameweza kuwa na chumba cha upasuaji na kinatoa huduma bora safi licha ya kuwa pia kipo kijijini. Wilayani Meatu
DSC_6304
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa amembeba mmoja wa watoto aliyejifungua siku hiyo wakati ametembelea kituo hicho cha Mwandoya ambacho licha ya udogo wake, tayari wameweza kuwa na chumba cha upasuaji na kinatoa huduma bora safi licha ya kuwa pia kipo kijijini. Wilayani Meatu.
DSC_6145
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Meatu akimuonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla moja ya vitanda hivyo.
DSC_6142
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Meatu akimuonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla moja ya vitanda hivyo.

MBUNGE MAHMOUD MGIMWA AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI NA NDOO KUMI ZA RANGI KWA SHULE YA SEKONDARI YA MDABULO.

$
0
0
MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa akihutubia wananchi waliofika kwenye mkutano uliyafanyika kwenye shule ya sekondary Mdabulo.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini mahamood mgimwa
 MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa akikabidhi mifuko 100 ya saruji na ndoo kumi za rangi zenye ujazo wa lita ishirini kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya ya kukarabati majengo ya shule ya sekondari ya Mdabulo kwa uongozi wa wilaya ya mufindi.

Na fredy mgunda,mufindi

MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa amekabidhi mifuko 100 ya saruji na ndoo kumi za rangi zenye ujazo wa lita ishirini kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya ya kukarabati majengo ya shule ya sekondari ya Mdabulo iliyopo Kijiji cha Mdabulo wilayani mufindi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini Mdabulo, alisema kuweza kujenga jamii imara ni lazima kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele cha pekee.

“Sina budi kuunga mkono juhudi zenu za ujenzi wa Shule ya sekondari ya Mdabulo, ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi, nami kama mwakilishi wetu ninaungana nanyi kwa dhati na katika hili napenda kukabidhi mifuko ya saruji.
huo.

Alisema lengo la kutoa msaada huo, ni kutokana na shule hiyo kuwa chakavu katika maeneo muhimu kama kwenye mabweni na bwalo ambalo hutumiwa na wanafunzi kwa ajili ya chakula.

“Baada ya kupata taarifa hizi, nimeamua kuja na mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi ili waangalie namna ya kufanya marekebisho katika madarasa pamoja na mabweni ya shule hii na nimewaagiza wahakikishe wanakarabati shule hiyo na iwe kwenye viwango vinavyotakiwa,” alisema Mgimwa.

Mgimwa aliwataka wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kufaulu na si kusoma ili kupata ajira kama ilivyozoeleka kwa watu wengi kwani serikali inafahamu changamoto ya ajira iliyopo.

Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema huku wakisaidiana na walimu kwa kushirikiana katika nyanja ya elimu ili kupanua wingo wa ufaulu kwa wanafunzi.

“Kwa kipindi cha siku kadhaa nimekuwa na ziara katika katika jimbo langu kwa lengo la kutimiza ahadi zangu pamoja na kusikiliza kero ya wananchi na kero moja wapo ni wazazi kutowajali  wanafunzi wala kutojua maendeleo ya watoto wao pindi watokapo shule”alisema Mgimwa.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Geogrge Mgomba, aliwataka wanafunzi wake kusome kwa ajili ya ajira binafsi na si kutegemea ajira kutoka serikalini kwa kuwa serikali ina mzigo mkubwa.

“Wanafunzi mnatakiwa msome kwa bidii na msitegemee ajira kutoka serikalini, mtafute ajira binafsi au kujiajiri wenyewe,”alisema

Kwa upande wake,mkuu wa wilaya ya mufindi Jamhuri Wiliamu, alimshukuru mbunge huyo kwa kuunga mkono juhudi za wananchi za kuinua sekta ya elimu katika wilaya hiyo.

WAZIRI WA AFYA AZINDUA BODI MPYA YA UDHAMINI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wakati akizindua bodi mpya ya udhamini wa hospitali hiyo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Dk.Charles Majinge na Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Michael John.
 Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Dk.Charles Majinge (kushoto), akizungumza katika uzinduzi wa bodi atakayoiongoza.
 Wafanyakazi wa Hospitali hiyo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Usikivu wakati waziri akizungumza nao.
 Maofisa uuguzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru (kushoto), akiwa kwenye uzinduzi huo. Kulia ni Mjumbe wa bodi hiyo, Esther Manyesha na Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
 Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia uzinduzi huo.

UKOSEFU WA MAARIFA YA VIPINDI VYA MABADILIKO YA MWILI KUNAATHIRI MAKUZI BORA KWA VIJANA

$
0
0
 Mwezeshaji Herman Mathias kutoka UNESCO akitoa somo kwa washiriki wa Shule za Sekondari Sengerema.


Ukosefu wa maarifa na taarifa sahihi wa vipindi vya mabadiliko maisha ya vijana husababisha uwezekano wa kupotoka kimaadili kwa kufanya mafunzo kwa vitendo na kuathiri makuzi bora.

Akitoa mafunzo kwa wanafunzi wanaounda vikundi vya kutayarisha vipindi vya redio kwa ajili kupaza sauti zao kuieleza Jamii kuhusu hali zao mashuleni, mamlaka mbalimbali, majumbani na katika Jamii wilayani Sengerema na Pangani, Afisa Mtaalam masuala ya Afya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Herman Mathias alisema kwamba changamoto nyingi zinazoathiri makuzi ya kimaadili kwa vijana ni kutopewa maarifa na taarifa sahihi jinsi ya kutumia miili yao bila kuathiri ndoto zao.

“Vijana wengi wameshindwa kufikia ndoto zao kutokana na kutomaliza shule kwa sababu hawajui namna ya kufanya maamuzi sahihi kutumia fursa walizo nazo”, alisema Herman Mathias.


Ili kufikia malengo ya ndoto zao Afisa huyo wa UNESCO alisema vijana wanahitaji kusoma kwa bidii na kuhitimisha mzunguko wa elimu, kuwa na tabia njema kwa kuepuka vishawishi vya mtaani hususan kuvuta bangi na matumizi ya vileo, utoro na matumizi ya lugha mbaya.

Alizitaja tabia njema nyingine pamoja na kuepuka tabia za kimapenzi yanayoweza kusababisha magonjwa ya zinaa, maambikizi ya virusi vya UKIMWI na ujauzito na upatikanaji wa malezi yanayojali nafasi na muda wa mtoto na kuweka mazingira rafiki ya kuishi na kusoma, afya bora kwa kutougua hovyo magonjwa mbalimbali na kuwa msafi wakati wote hali inayompa fursa kijana kushiri katika shughuli zote za kijamii na kielimu na kuwataka wazazi na walezi kufuatilia mwenendo wa kijana shuleni na katika Jamii.

Zaidi ya asilimia 52 ya vijana hawana elimu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na afya ya uzazi.

Alisema kwamba mambo hayo yote yanawezekana kuepukika kwa sababu yako ndani ya uwezo wa vijana wenyewe na wazazi pia.

Washiriki wakichangia mawazo na uzoefu wao kuhusu changamoto zinazowakabili.

Wakichangia uzeofu wao unaowakwamisha kufikia ndoto zao, vijana hao walizitaja changamoto zinaowakumba katika kipindi cha makuzi ambazo ni mimba za utotoni zinazosababishwa na ukosefu wa elimu ya uzazi kuanzia shuleni na au katika familia, umaskini unaosababisha wasichana kutoka nje na kujiingiza katika matendo ya kimapenzi kwa kutafuta mahitaji mbalimbali muhimu na matamanio kukidhi matakwa yao kimaisha na makundi rika ambayo huchangia katika kushawishiana na kufundishana mabaya.

“Zaidi wa watoto 6,000 wanaacha masomo kutokana na ujauzito na mara nyingi waalimu wamekuwa hawaripoti taarifa za mimba badala yake huripoti utoro peke yake, lakini wanafunzi wanaelewa hali halisi na kuweza kueleza ukweli”, alisema Herman Mathias.

Kijarida kilichoandaliwa kama matokeo ya nadharia kwa vitendo.

Changamoto nyingine ni tamaa inayopita kiasi kwa kuona baadhi ya marafiki zao wanakuwa na vitu vizuri ambavyo wengine huvikosa hususan simu za mkononi, viatu na nguo nzuri, kubakwa na matumizi mabaya ya mawasiliano ya utandawazi na vifaa vya kielektroniki zinazopatikana kwa njia zisizo halali.

Matumizi mabaya ya utandawazi hushawishi vijana kuiga utamaduni wa kigeni hususan kuvaa nguo zisizo na maadili na vitendo vingine vinavyoenda kinyume na maadili ya Mtanzania na malezi yanayowapa vijana uhuru mkubwa wa kufanya mambo yao bila kurekebishwa au kuingiliwa na wazazi na walezi ni changamoto inayochangia kupotosha maadili katika makuzi ya kijana.

Wanafunzi washiriki wakifanya zoezi la viungo wakishirikiana na Mwezeshaji Herman Mathias.

Ndoa za utotoni zinazosababishwa na mila na desturi zinazoendelezwa katika Jamii kwa kiasi kikubwa zinachangia kufifisha vijana kufikia malengo ya ndoto zao na mimba za utotoni husababisha ulemavu wa mwili na akili na pia vifo kwa mama na mtoto.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 179 zilizokubaliana kutekeleza Mkakati wa Utekelezaji Mkutano wa Kimataifa wa Tatu na Maendeleo wa Cairo (UNFPA) mwaka 1994 wa harakati za maendelezo ya haki za uzazi, uzazi wa mpango, uzuiaji wa maambukizi ya VVU/UKIMWI, uwezeshwaji wa wanawake na maendeleo mengine yanayohusiana na hayo kulinda utimilifu wa kibailojia, kisaikolojia wa namna ambavyo mfumo wa uzazi unafanya kazi. Haki hizo zikipotea mtoto ana haki ya kupaza sauti kudai.

UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Redio Jamii ya wilaya ya Sengerema na Pangani, iliendesha warsha za kuwajengea uwezo vijana wa shule za Sekondari wilayani Sengerema na Shule za Msingi wilayani Pangani kupitia vikundi rika maarifa na ujuzi wa elimu ya afya ya uzazi na makuzi yao kupitia redio Jamii ili waelimike kabla ya kuandaa vipindi.

Afya ya uzazi inahusisha mfumo wa uzazi wa mtu na via vya uzazi kwa watu ambao unajumuisha uzazi na ujinsia, kuingia utu uzima, mahusiano, mimba, maambukizi ya virusi vya UKIMWI/UKIMWI na dawa za kulevya.

Pamoja na elimu ya afya ya uzazi, vijana pia waliweza kupata mafunzo ya msingi ya uandishi wa habari na utangazaji ili kuandika na kutayarisha vipindi vya redio, vijarida na midahalo kwa ajili ya kuwasiliana kutoka rika moja hadi jingine kuelimishana, kukemea, kudai na kukumbushana haki zao.
Wanafunzi wa Shule za Msingi Pangani wakiwa katika ziara ya kutembelea kituo Redio Jamii Pangani FM wakati wa mazoezi.

Elimu rika kupitia vikundi vya vijana katika redio ni mpango wa majaribio katika wilaya ya Sengerema na Pangani ambao mafanikio yake yataendelezwa katika sehemu nyingine hususan Kahama, Isaka, Micheweni, Simanjiro na Loliondo.

Vikundi hivyo ni fursa ya kuwajengea misingi ya ajira ya uandishi wa habari iwapo wataitumia vizuri kwa kushirikiana na vituo vya redio Jamii vilivyoteuliwa kuandaa na kutayarisha vipindi, kushirikiana na wenzao kurekodi majadiliano na kuwa wabunifu wa kuandaa vijarida kwa ajili ya kutoa elimu rika kuhusu afya ya uzazi na malezi.
Picha ya pamoja wanafunzi wa Shule za Msingi Boza na Kikokwe Pangani, walezi, wajumbe wa kamati za shule na viongozi kutoka Wizara ya Elimu.

Airtel Money yagawa billion 3 kwa wateja na Mawakala

$
0
0
 Kulia Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi Mr Money wa Airtel Money atakavyogawa faida ya shilingi billion 3 kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wake nchi nzima ikiwa ni faida yao kutokana na kutumia Airtel Money kuanzia Januari hadi juni mwaka huu kushoto ni Meneja wa uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando jana.
 Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa kugawa gawio la faida ya shilingi billion 3 kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wake nchi nzima ikiwa ni faida yao kutokana na kutumia Airtel Money kuanzia Januari hadi juni mwaka huu. Kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa jana.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa gawio la faida la kila kiasi cha shilingi billion 3 kwa wateja wake wa Airtel Money na mawakala wakubwa na wadogo nchi nzima

Airtel imetoa gawio la faida kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi juni mwaka huu ambapo kila mteja atalipwa sehemu ya faida kulingana na kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku

Akiongea na waandishi wa habari , Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema “Tunayofuraha kutoa gawio la faida la shilingi bilioni 3 kwa wateja wetu na wakala nchi nzima. Tunaamini gawio hili la faida litawawezesha wateja wetu kutatua mahitaji yao ya kifedha na hivyo kuthibitisha dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za kifedha”

“Tumejipanga kuwawezesha wateja wetu kwa kupitia huduma na bidhaa tunazozitoa. huduma ya Airtel Money imelenga kuleta unafuu na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini hususani ya maeneo ya pembezo mwa nchi. Aliongeza Mmbando

Mpaka sasa Airtel imeshatoa kiasi cha shilingi billion 10 kwa wateja na mawakala wa Airtel money tangu  2014.

Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea pesa, kulipia bili, kununua vifurushi, kuamisha pesa na kutoa pesa kutoka benki pamoja na kutoa mikopo isiyo na dhamana kupitia huduma ya Airtel Timiza ambayo inatoa mikopo ya haraka, rahisi kwa wateja na mawakala.

Mpaka sasa mtandao wa mawakala 50,000 wa Airtel Money nchini Tanzania wanaweza kutumia huduma hii. Theluthi moja ya mawakala wote wa Airtel Money hutumia Timiza, na baadhi ya mawakala sasa hivi wanakidhi vigezo vya kupata mikopo hadi Shilingi milioni moja.

ATAKAYEVAMIA MSITU FAINI MIL. 70, JELA MIAKA SABA- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kuvunja sheria kwa kuvamia na kuharibu mazingira ya msitu wa Mfili ambao ndiyo chanzo pekee cha maji cha Wilayani Nkasi atatozwa faini ya sh. milioni 70 pamoja na kifungo miaka saba jela.

Katika kuhakikisha hatua zinachukuliwa Waziri Mkuu amemkabidhi mkuu wa wilaya ya Nkasi, Said Mtanda kitabu cha sheria kitachomuangoza katika kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kufanya uharibifu katika chanzo hicho cha maji.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Agosti 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa mji Mdogo wa Namanyere katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanya vya Sabasaba.

“Mkuu wa wilaya akishindwa kuwachukulia hatua za kuwaondoa wananchi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu na kuanzisha makazi au kufanya shughuli za kijamii naye atakuwa jipu,” alisema.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji baada ya wananchi kuvamia katika vyanzo vya maji na kufanya shughuli za kibinadamu hivyo kusababisha vyanzo vingi kukakuka

“Serikali haitakubali kuona mtu anaharibu chanzo cha maji. Wananchi mnatakiwa kuwa walinzi wa maeneo hayo na atakayekutwa anachunga mifugo, analima, kukata nyasi au kufanya shughuli zozote za kijamii ndani ya maeneo hayo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Awali Waziri Mkuu alikagua mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfili ambalo mwanzo lilikuwa na ujazo wa lita 1,500 ambapo litakapokamilika litakuwa na ujazo wa lija 248,067 hivyo kuwezesha wakazi 82,689 kunufaika.

Akizungumza kwenye eneo la mradi mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili, Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Nkasi, Julius Kaondo alisema hadi kukamilika mradi huo unatarajiwa kugharimu sh trilioni 1.011 ambapo Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetoa sh. milioni 500 na OOfisi ya Rais TAMISEMI itatoa sh. milioni 500.

Mkurugenzi huyo alisema mradi unakabiliwa na changamoto ya ukosefu umeme ppamoja na mitambo ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme, ambapo aliiomba Serikali kuipatia halmashauri hiyo sh. milioni 222.576 ikiwa ni gharama za kupeleka umeme kwenye eneo la mradi na kununua mitambo.

Mbali na kutembelea mradi wa upanuzi wa bwawa, pia Waziri Mkuu alitembelea hospitali teule ya wilaya ya Nkasi na kuzindua wodi mpya yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 72 kwa wakati mmoja

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATANO, AGOSTI 24, 2016.

KAMPUNI YA STATE GRID YAONESHA NIA MRADI WA UMEME WA MCHUCHUMA- MAKAMBAKO

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini (katikati) Profesa Sospeter Muhongo akiwaeleza jambo Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake waliofika Ofisini kwa Waziri ili kufahamu namna kampuni hiyo inavyoweza kufanya kazi katika sekta ya Nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao baina yake na Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake waliofika Ofisini kwa Waziri ili kufahamu namna kampuni ya State Grid ya China inavyoweza kufanya kazi katika sekta ya Nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya State Grid ya China upande wa Afrika, Mingu Liu, (wa kwanza kulia mbele) wakati akimweleza Waziri Muhongo azma ya Kampuni hiyo kuwekeza katika Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme ya Msongo wa kV 400 Mchuchuma hadi Makambako. Wengine wanaofuatilia ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na ujumbe wake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiangalia Makabrasha kutoka Kampuni ya State Grid ya China ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa njia ya umeme ya Msongo wa kV 400 ya Mchuchuma hadi Makambako.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikakti) na Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youging (wa pili kushoto) na ujumbe wake wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Waziri, Balozi na kampuni ya State Grid.



Kampuni ya State Grid ya China imeonesha nia ya kuwekeza katika Mradi wa Kujenga Njia ya umeme ya Msongo wa kV 400 ya kutoka Mchuchuma hadi Makambako.

Hayo yamebainika katika kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing aliyeambatana na ujumbe huo wa kampuni hiyo.

Profesa Muhongo alichukua fursa hiyo kuieleza kampuni hiyo kuhusu Hazina iliyopo nchini ya Makaa ya Mawe na kusema kuwa, bado Serikali inatafuta wawekezaji ambao watazalisha umeme kwa kutumia chanzo hicho na kuongeza kuwa, “Bado tunahitaji wawekezaji kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe”.

Aidha, mbali na kuonesha nia ya kuwekeza katika Mradi huo, Kampuni hiyo imefika Wizarani kutaka kujua maeneo mengine ya uwekezaji katika sekta ya Nishati ambayo kampuni hiyo inaweza kufanya kazi nchini.

Vilevile, kampuni hiyo ilimweleza Waziri uzoefu ilionao katika shughuli hizo na kuzitaja baadhi ya nchi ambazo inatekeleza miradi kama hiyo kuwa barani Afrika kuwa ni pamoja na Ethiopia, Egypt, Kenya na Afrika Kusini.

Watumishi Wizara ya Habari watakiwa kuwa wabunifu katika utendaji kazi.

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Watumishi wa Wizara yake wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao akiteta jambo na Watumishi wa Wizara yake (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Mkurugenzi Msaidizi Utawala Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Erast Mushi (kushoto) akitoa ufafanuzi wa mambo yanayohusu Idara yake kwa Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel, wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo Bibi. Nuru Millao na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Bibi. Magreth Mtaki.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Zawadi Msalla akijitambulisha kwa Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016. Kulia ni Afisa Michezo Mwandamizi wa Wizara Bw. Nicolas Bulamile..

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Watumishi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia mbinu mbalimbali za kiutendaji kazi ili kuweza kuifanya Wizara kujulikana na kuleta maendeleo katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokutana na wafanyakazi wa Wizara hiyo jana Jijini Dar es Salaam.

Prof. Gabriel amesema kuwa jamii itathamini kazi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kama Watumishi wa Wizara watafanya jitihada za makusudi kwa kuwa wabunifu katika utendaji kazi hivvo kuleta tija na heshima kwa Serikali.

“Ni vema kila Mtumishi akajituma katika kukamilisha majukumu ya Wizara yetu kwa kasi na kwa wakati huku tukithamini maslahi ya jamii tunayoitumikia” alisema Prof. Gabriel

Aidha Prof. Gabriel amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuheshimiana na kuishi kama ndugu kwani muda mwingi hutumia wakiwa ofisini na kuwahaidi kuwa kwa upande wake atahakikisha kuwa Watumishi wote wanaishi katika mazingira rafiki katika eneo la kazi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Magreti Mtaki amewataka watumishi wa wizara kuacha kungojea fursa zinazopatikana nje ya Wizara bali kutumia fursa zinazopatikana ndani ya Wizara kwani ni rahisi kuzisimamia na kuziendeleza kwa maendeleo ya Taifa letu.

Mazoezi ya polisi yatikisa Jiji la Mbeya

KUUAWA KWA POLISI BENKI YA CRDB MBANDE JIJINI DAR ES SALAAM JESHI LA POLISI LAHUSISHA NA UKUTA

$
0
0

Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu tukio la mauaji ya askari wanne katika Benki ya CRDB Tawi la Mbande yaliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha na waandishi wakiwa bize kupata taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

KUFUATIA mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka wahusika wote kujisalimisha.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.

Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia alipiga mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.

Aidha CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa Mbande.

"Katika tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, " alisema.

Alisema katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika mitandaoni kubeza na kukejeli mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na polisi Srptemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.

Rais Magufuli mgeni Rasmi Mkutano wa 32 wa ALAT

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikalini Bi. Domina Feruzi kulia akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 206 Makamu Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa kushoto kwa ajili ya mkutano wa 32 wa jumuiya hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam
Makamu Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu mkutano wa 32 wa ALAT utakaonza mwishoni mwa Septemba mwaka huu , kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikalini Bi. Domina Feruzi.


Habari/Picha Na Ally Daud.

Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Nchini (ALAT) ambao utafanyika mwishoni mwa mwezi ujao mkoani Musoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa amesema kuwa, katika mkutano huo wanatarajia Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi ili kufikia malengo ya mkutano huo.

“Tumeamua kumuomba Mheshimiwa Rais kuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kupata matunda mema ya mkutano huo kutokana na kauli mbiu yake ya Hapa Kazi Tu ili kuendana na kasi hiyo katika kuleta mendeleo na uongozi bora nchini,” alisema Bw. Mhapa.

Aidha Bw. Mhapa amesema kuwa uzinduzi wa mkutano huo utaendana na ukabidhishaji wa zawadi kwa mshindi wa shindano la Halmashauri bora kwa mwaka 2016 ambapo mshindi atayechaguliwa na wananchi kwa wingi atakabidhiwa Trekta yenye thamani ya shilingi milioni 56 ili kuinua shughuli za kimaendeleo.

Mbali na hayo Bw. Mhapa ameongeza kuwa mkutano huo utadhaminiwa na Benki ya NMB kwa kupokea kiasi cha shilingi milioni 206 ambazo milioni 56 zitatumika kugharamia zawadi na milioni 150 kugharamia mkutano huo.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikalini kutoka benki ya NMB Bi. Domina Feruzi amesema kuwa wameamua kufadhili mkutano huo ili kurahisisha shughuli za kimaendeleo na kupata uongozi bora kwa faida ya watanzania.

“Tumeamua kudhamini mkutano huo ili kuweza kurahisisha shughuli za kimaendeleo na kupata viongozi bora kwa kupitia mashindano ya Halmashauri Bora mwaka 2016,”amesema Bi. Domina.

ALAT imekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa Halmashauri bora kwa mwaka wa pili sasa ambapo imesaidia Halmashauri nyingi kufanya vizuri katika ukusanyaji mapato na uboreshaji wa miundo mbinu na mazingira kwa ujumla.

Rais Dkt John Pombe Magufuli ateua Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

$
0
0





 Dkt. Modestus Francis Kipilimba-Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Agosti, 2016 amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.


Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).


Dkt. Modestus Francis Kipilimba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye amestaafu.Dkt. Modestus Francis Kipilimba ataapishwa leo mchana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.


Kabla ya uteuzi huo Bw. Robert Msalika alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.


Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.Wakurugenzi na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi zao.



Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

24 Agosti, 2016




Millicom Group Chief Executive Officer Mauricio Ramos in Zanzibar

$
0
0

 Zanzibar President Dr Ali Mohammed Shein greets Millicom Group Chief Executive Officer, Mauricio Ramos, shortly before having talks in Zanzibar yesterday 23 August 2016. Right is Zantel CEO Benoit Janin.

 Zanzibar President Dr Ali Mohammed Shein greets Rachel Samren, the Deputy CEO of Millicom Group and the Chief Executive Officer of Zantel Board of Trustees. Centre is Millicon Group Chief Executive Officer Mauricio Ramos and second left is Zantel CEO Benoit Janin when they visited the Zanzibar President yesterday in State House Zanzibar.
 Zanzibar President Dr Ali Mohammed Shein in talks with the Millicom Group Chief Executive Officer, Mauricio Ramos, when he paid a courtesy call in State House, Zanzibar yesterday 23 August 2016.
Millicom Group Chief Executive Officer Mauricio Ramos in a group photo with staff of Zantel Telecommunications Company staff in Zanzibar when he paid a  working visit to the offices in Zanzibar.
Millicom Group Chief Executive Officer Mauricio Ramos in a jovial mood after receiving an award from  staff of Zantel Telecommunications Company staff in Zanzibar when he paid working visit to the offices in Zanzibar.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images