Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

HAPPY BIRTHDAY BLOGGER MC BARAKA

$
0
0

Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, Aug 23. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. Ni neema ambayo sistahili,Napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana, niitumie kwa mambo mema,Nizingatie wajibu wa kuvitumia kikamilifu vipaji alivyonipa Mungu kwa manufaa ya wanadamu.

Siwezi kujivunia chochote nilichoweza kufanya, bali ni kumshukuru Mungu na kuendelea kumtegemea na kila ninaposherehekea kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa kwangu, fikra zinanituma kufananisha mchango wangu Kimkoa na Kitaifa sawa na ule wa watu maarufu,Ukweli ni kwamba ninajitahidi lakini mchango wangu bado ni hafifu sana. Mengi nimefanya kupitia Bukobawadau Blog Media ninachoweza kusema ni kwamba changamoto ni kubwa sana!

I will always praise God

MBUNGE AOMBWA KUVISAIDIA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA ILI KUIPUNGUZIA MZIGO HOSPITALI YA MKOA WA TANGA BOMBO

$
0
0

Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) ambaye alikwenda kuitembelea hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kuangalia changamoto zinazowakabili.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita



Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza, Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF), Mussa Mbaruku ameombwa kuangalia namna ya kuweka mkakati wa kuvisaidia vituo vya afya na Zahanati zilivyopo ndani ya Jiji la Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo inayohudumia wagonjwa wa mkoa mzima.

Ombi hilo lilitolewa jana na Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Asha Mahita wakati Mbunge huyo alipoitembelea hospitali ya alisema kuwa msongamano unaoikabili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa unatokana na kutokuwepo na ubora katika zahanati na vituo vya afya jambo ambalo linalowafanya wanachi kukimbilia katika Hosptiali hiyo.

Hatua hiyo inatokana na zahanati na vituo vya afya vingi Jijini Tanga kukakabiliwa na changamito nyingi zinazo sababisha kukosa ubora hali inayochangia kwa asilimia kubwa wananchi wengi kukimbilia katika hospital ya Rufaa ya Bombo na kuongeza msongamano wa wagonjwa.

Mahita alisema ipo haja ya kuvisaidia vituo hivyo ambavyo havina nyumba za watumishi, uzio, miundombinu mibovu na vingine kukosa umeme jambo ambalo linakuwa si rafiki kwa wahudumu na linakwamisha shughuli za kiafya hasa nyakati za usiku.

Alisema kuwa iwapo kutakuwepo na mabororesho katika vituo hivyo huku Serikali na wadau mbalimbali wakiweka nguvu zao katika swala la kumalizia Hospitali ya wilaya ambayo mpaka sasa inajengo moja la ghorofa kwa ajili ya utawala ikimaliziwa na kuanza kutumika kutapunguza kwa asilimia kubwa msongamano kwenye hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Mbunge Mussa Mbaruku alihaidia kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo kwani wananchi afya zao zinapokuwa zimeimarika inawasaidia kuweza kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

“Ndugu zangu huu si muda wa kupiga porojo kuhusiana na masuala ya afya ambalo ndio uti wa mgongo wa wananchi hivyo lazima viongozi wajenge umoja na kutafuta njia ya kuweza kuviboresha vituo hivyo ambavyo vitawasaidia kwa asilimia kubwa wananchi kupata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi “Alisema

Aidha alisema pamoja na changamoto zinazozikabili zahanati na vituo hivyo lazima Serikali itenge fedha za kutosha ili kuweza kuimalizia Hospitali ya Wilaya iliyopo Masiwani Shamba ambayo mpaka sasa bado hakuna majibu sahihi ya kukwama kwa umaliziwaji wa Hosptili hiyo.

“Bado nashindwa kupa majibu ni kitu gani kinachokwamisha kumalizika kwa Hospitali ya Wilaya ambayo tayari inajengo zuri la utawala tena la ghorofa serikali inawajibu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Hospitali hiyo inamalizika na inakuwa na kiwango bora katika sekta zote za matibabu.

Mbaruku alifanya mazungumzo hayo na mganga mkuu wa Mkoa alipo watembelea madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza, Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

SUMMER FIESTA THIS SUNDAY 28TH AUG, BANK HOLIDAY WEEKEND @CLUB 20 READING UK RG1 7JL

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA: FANYENI UKAGUZI KUBAINI WALIOKULA FEDHA ZA USHIRIKA NA KUWACHUKULIA HATUA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Mkoa Katavi, Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga kupeleka wakaguzi wilayani Mlele na kubaini watu waliokula fedha za chama cha ushirika cha Ukonongo na kuwachukulia hatua.

“Watakaobainika watiwe hatiani. Licha ya bodi ya ushirika huo kuvunjwa, hatuwezi kuacha suala hili limalizike kwa kuvunja bodi kwa sababu walioingia wanaweza kuiba kwa mategemeo ya kuvunjwa bodi,“ amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumatatu, Agosti 22, 2016) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Inyonga wilayani Mlele.

Amesema kila mtumishi afanye kazi na awajibike kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kwa mujibu wa taaluma yake ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwani hilo ndilo lengo la kuajiriwa kwake.

“Haiwezekani hapa kuna Ofisa Ushirika halafu Waziri Mkuu analetewa mabango ya kumtaka atatue tatizo la chama cha Ushirika. Hali hii inaonyesha hapa hakuna kazi inayofanyika,“ amesema.

Waziri Mkuu amesema wanahitaji watumishi watakaosikiliza maelekezo yanayotolewa na Serikali na kuyafanyia kazi kwa sababu malengo ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli ni kuona nchi hii inabadilika hivyo wasioweza ni vema wakaandika barua za kuacha kazi.

“Msikubali kuhamasishwa kufanya mambo yatakayowaletea madhara. Fanyeni kazi ili tupate maendeleo. Hatuwezi kufananishwa na nchi ndogo ndogo, wenzenu wanafanya kazi nasi tupunguze maneno tufanye kazi,“ amesema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamilia kumaliza changamoto ya upatikanaji wa umeme nchini ambapo imetenga zaidi ya sh. trilioni moja kwa ajili ya kumalizia kazi ya usambazaji umeme nchi nzima ikiwemo wilaya ya Mlele.

Amesema watapeleka jenereta kubwa mbili zitakazofungwa katika kijiji cha Utende ambazo zitasambaza na kuwasha umeme katika kata ya Inyonga na maeneo mengine.

“Mwezi Novemba mwaka huu umeme utakuwa umewaka wilayani Mlele. Mkakati ni kuunganisha mkoa wa Katavi na gridi ya Taifa kutoka Tabora, kupita Sikonge hadi Inyonga,“ amesema.  

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na mbunge wa jimbo la Katavi, Mhandisi Isack Kamwelwe amemuomba Waziri Mkuu kuwasaidia kupandishwa hadhi kwa kituo cha afya cha Inyonga na kuwa Hospitali ya wilaya kwa sababu wilaya yao haina hospitali.

Pia ameomba wilaya hiyo ipatiwe umeme wa Tanesco ili kupunguza gharama kubwa za kununua umeme kutoka kwa mfanyabiashara ambaye amefunga jenereta na anawauzia unit moja sh. 1000 wakati Tanesco wanauza sh. 100 kwa unit moja.

Awali Mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel Kassanda alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa nyumba za watumishi hali inayosababisha mkuu wa wilaya na Katibu tawala wa wilaya kuishi kwenye nyumba za kupanga.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 23, 2016.
                     

WAZRIRI MKUU MAJALIWA: ONDOENI WATU WALIOVAMIA MAENEO YALIYOHIFADHIWA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kuhakikisha unawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi na ushoroba  wa wanyama  wa Lyamgoroka.

Agizo hilo limetolewa jana jioni (Jumatatu, Agosti 22, 2016) na Waziri Mkuu  wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha  Majalila wilayani Tanganyika.
                          
Waziri Mkuu alisema wilaya hiyo inatakiwa kuendelea kuwaondoa watu wote waliovamia na kujenga makazi  ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi  ili kuepuka uharibifu wa mazingira.

“Hakikisheni mnatunza mazingira. Msiache wakate miti hovyo kwa sababu wanakausha vyanzo vya maji na kusababisha eneo kuwa hatarini kukumbwa na ukame, hivyo ni vyema wakaondolewa mapema,” alisema.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka Maofisa Ushirika na Kilimo katika mkoa wa Katavi kuwasaidia wakulima wa tumbaku kwa kuhakikisha wanapata soko la uhakika na kulipwa kwa wakati.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kupitia mabango waliyokuwa wameyabeba ambayo yalikuwa yakiwalalamikia maofisa hao kwa kushindwa kuwatafutia masoko na  badala yake wanawakumbatia wabadhilifu wa fedha za ushirika.

"Hatuwezi kuwa na Ofisa Kilimo ambaye hajui masoko ya mazao ya wakulima wake.Mnakaa ofisini tu! Hamfanyi kazi. Lazima mfuatilie masuala ya kilimo katika maeneo yenu, sasa chukua mabango yote yanayohusu zao la tumbaku na ukalete majibu kwa wakulima,” alisema.

Awali Waziri Mkuu alitembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za halmashauri na wilaya Tanganyika ambapo aliwapongeza wakazi wa kijiji cha Majalila kwa kutoa bure ardhi yenye ukubwa wa ekari 500 ili Serikali iweze kujenga ofisi hizo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 23, 2016.

DSE yakuza mauzo ya hisa kwa asilimia 57

$
0
0

Na Ally Daud-Maelezo

Idadi ya mauzo katika soko la hisa Dar es salaam (DSE) imekua kwa asilimia 57 na kufikia shilingi bilioni 3.3 kutoka shilingi bilioni 2.1 wiki iliyopita kutokana na ukubwa wa idadi ya mauzo.

Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Mwandamizi wa Masoko DSE Bi. Mary Kinabo imesema kuwa idadi ya mauzo hayo yamekua kutokana na kupanda kwa idadi za hisa zilizouzwa kutoka shilingi milioni 1.6 hadi kufikia shilingi milioni 2.2.

Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa Benki ya CRDB imeendelea kuongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa asilimia 49 ikifuatiwa na Soko la hisa DSE ikiwa na asilimia 43 na ya tatu ni kampuni ya Bia nchini TBL yenye asilimia 4.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa asilimia 0.67 na kufikia shilingi trilioni 23.4 kutoka trilioni 23.2 wiki iliyopita na ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwa shilingi trilioni 8.4.

Mbali na hayo taarifa hiyo imeeleza kwamba licha ya mauzo kupanda lakini viashiria vya soko katika sekta ya viwanda vimeshuka kwa alama 19.47 baada ya bei za hisa kutoka TBL kushuka kwa asilimia 0.66 huku sekta ya huduma za kibenki kupanda kwa alama 29.89 kutokana na kupanda kwa kaunta ya DSE na NMB.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa viashiria vya soko katika sekta ya huduma za kibiashara wiki hii imebaki kwenye hali yake ya wiki iliyopita baada ya bei za hisa za Swissport kubaki kwa shilingi elfu 3.543.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU HALI YA MHE JOSEPH MICHAEL (MB) BAADA YA KUPATA AJALI

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA WILAYA YA KASKAZINI ''B'' UNGUJA

$
0
0
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 22/08/2016.

Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema hapendelei kuona wauguzi wanatumbuliwa majipu kutokana na uzembe wao lakini hayuko tayari kutumbuliwa yeye kwa ajili yao .

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea vituo mbali mbali vya Afya Wilaya ya Kaskazini B Unguja vikiwemo Kituo cha Kiwengwa na Kituo cha Bubwini Misufini kutaka kuona changamoto zinazopo vituo hapo.

Alisema kuna baadhi ya wauguzi huwafanyia dharau wagonjwa au wajawazito wakati wa kujifungua jambo ambalo halipaswi kuona linafanyika, kitu ambacho kinaweza kuwapeleka pabaya na kutumbuliwa majibu.

“Sitoona vizuri kuona mfanyakazi anatumbuliwa jipu kwa ajili ya uzembe wake na pia siko tayari kutumbuliwa mimi kwa ajili yake “Alisema Harusi .

Aidha alisema kwamba wauguzi wawetayari kukamilisha majukumu yao ya kikazi na waache lugha chafu ambazo zitawasumbuwa wagonjwa na kuonekana kuwa wao wakorofu katika kutoa huduma .

Hata hivyo Naibu Waziri alieleza kuwa wauguzi waelewe kuwa awamu iliopo hivi sasa ni awamu ya uwajibikaji na ufatiliaji na ni rahisi mawasiliano kufika kwa haraka na kuweza kuharibu malengo ya baadae hivyo wasiwe tayari kuchokozwa wakachokozeka.

Nae Muuguzi wa kituo cha afya cha Kiwengwa Khadija Ali Juma alieleza matatizo mbali mbali ambayo wanakabiliana nayo kituoni hapo ikiwemo kutokuwa na uzio katika eneo hilo, wananchi kuchafua katika kwa makusudi katika maeneo ya vyoo pamoja na kufanya maskani katika kituo hicho .

Aidha alisema kutokuwa na friji katika kituo hicho kunachagia usumbufu mkubwa wa kuhifadhia dawa za chanjo za mama na watoto ambazo zinahitajika kuhifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi ili zisiharibike .

Alisema ushirikiano mdogo uliopo baina ya kituo cha afya na kamati ya sheha hawaufurahikii wauguzi ,kwani sheha wa sehemu hiyo haonyeshi ushirikiano mzuri na wauguzi waliopo katika kituo hicho .

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya alitembelea katika Kituo cha Afya cha Bumbuni Misufini ambacho kilitokezea matatizo ya kutofahamiana kati ya Wauguzi wa serikali na Wakunga wa Jadi .

aliwataka wauguzi ambao ni waajiriwa wa serikali kutoa mashirikiano ya pamoja na wakunga wa jadi ili kuepusha tofauti miongoni mwao na kuweza kutatua changamoto ambazo zitaweza kujitokeza kwa wazazi .

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA WILAYANI MLELE

$
0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda wakati Waziri Mkuu, alipohutubia mkutano wa hadara kwenye kijiji cha Majimoto wialayani MleleAgosti 23, 2016. Wapili kulia ni Mbunge wa Kavuu, Dkt.Pundeciana Kwembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati walipokutana katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu,   kwenye kijiji cha Majimoto wilayani Mlele Agosti 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WAGANGA WAKUU WANAOWATOZA FEDHA ZA MATIBABU WAJAWAZITO, WAZEE NA WATOTO CHINI YA MIAKA 5.

$
0
0
Waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto ) akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa waganga Wakuu wa Hospitali za Umma kusimamia utekelezaji wa Sera na miongozo ya Afya katika  maeneo yao ya kazi.

Na. Aron Msigwa - Dar es salaam. 


Serikali imesema kuwa haitamvumilia Mganga mkuu yeyote wa Hospitali ya Umma atakayebainika kuwatoza fedha wananchi walio katika kundi la watu wanaotakiwa kupata matibabu bure  wakiwemo wazee wasiojiweza, wajawazito na watoto  walio na umri chini ya miaka 5.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo jijini Dar es salaam kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya wananchi walio katika makundi hayo katika maeneo mbalimbali kudaiwa fedha katika hospitali hizo.

Serikali hatutamvumilia Mganga Mkuu yeyote wa hospitali ya umma anayetoza fedha kwa mwanamke mjamzito, kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka 5 na mzee asiyejiweza, hatujabadilisha Sera " Amesisitiza Mhe.Ummy.

Amesema kwa mujibu wa Sera ya Afya ya 2007 mama wajawazito, wazee wasiojiweza na watoto walio na umri chini ya miaka 5 wanatakiwa kupata matibabu bure na kusisitiza kwamba kuwatoza fedha ni kinyume cha Sera hiyo.

Amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa ambao ndio wasimamizi wa Wakuu wa utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya mikoa kutimiza kikamilifu majukumu yao kwa kushughulikia haraka kero na malalamiko ya wananchi kuhusu huduma za Afya katika maeneo yao ili wananchi waweze kufurahia huduma bora za afya.

Amesema Serikali inaendelea kuzishughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo changamoto ya uhaba wa dawa ili kuhakikisha kuwa hospitali za umma zinakuwa na dawa za kutosha kukidhi mahitaji ya wagonjwa wanaohudumiwa.

Katika hatua nyingine Mhe. Ummy Mwalimu ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha mara moja vitendo vya baadhi ya madaktari wa hospitali hizo kuwaandikia wagonjwa kwenda kufanyiwa uchunguzi wa vipimo katika hospitali binafsi.

 Kuanzia sasa MOI wasimamishe kupeleka wagonjwa kwenda kupima MRI katika hospitali binafsi, pale itakapotokea na tukajua na kujiridhisha kuwa MRI ya Muhimbili imekufa na haifanyi kazi wataruhusiwa kufanya hivyo

Amesisitiza kuwa kitendo cha madaktari hao kuwaandikia wagonjwa kwenda kupima vipimo vya MRI nje ni kuhujumu na kuzikosesha mapato hospitali hizo.

 

SINTOFAHAMU YA VYAMA VYA SIASA INATATULIWA KWA KUKAA NA KUZUNGUMZA PAMOJA-JAJI MUTUNGI

$
0
0
MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi 

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii .

MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi amesema masuala yote ya  sintofahamu kwa wa vyama vya siasa yatatuliwa katika meza ya majadiliano na si vinginevyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesema kuwa kuna taharuki au hofu ambayo inajengwa kwa wadau wa siasa ambayo inahitaji kuwepo mazungumzo kutokana na taratibu zinazohusu utawala bora.Amesema kuwa utawala bora ni kuheshimu miundombinu iliyowekwa kwa kufuata sheria zake na bila kufanya hivyo miundombinu haitakuwa imetendewa haki kwa watu kufanya chochote bila kuangalia misingi iliyowekwa katika miundombinu hiyo.

Amesema kuwa Baraza la vyama vya siasa limeandaa mkutano wa wadau wa vyama vya siasa pamoja na watu wengine kuweza kuzungumza masuala mbalimbali ambayo yamejitokeza katika kipindi hiki na kupatiwa ufumbuzi wa sintofahamu miongoni mwa  wadau.

Jaji Mutungi amesema kuwa baraza la vyama vya siasa linatarajia kukaa  Agosti 29 na 30 kutaka wadau wote waweze kushiriki ili kutafuta suluhu kwa yale ambayo yamejitokeza sambamba na kuyatafutia suluhu katika kuendelea kulinda amani ya nchi yetu.

Amesema  siku zote watu wanatafuta mwafaka wa jambo lolote katika meza ya mazungumzo na kupata suluhu katika kulinda amani ya nchi yetu.

Aidha amesema suala la Chama cha Wananchi (CUF) anaangalia na kuona jinsi gani anaweza kushauri kutokana na kuwa mlezi wa vyama vyote ambavyo vimepata usajili katika ofisi yake.

NAIBU WAZIRI (OR) KATIBA, SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ATOA TARIFA YA MGAO WA TATU WA MIRABAHA

$
0
0



Afisa Mtendaji Mkuu wa Hakimiliki Zanzibar Bi. Mtumwa Khatib Ameir akimkaribisha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Mwalim kwenye Mkutano na wandishi wa Habari juu ya taarifa ya mgao wa tatu wa Mirabaha uliofanyika Ofisi ya Wizara Mazizini Mjini Zanzibar.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Mwalim akitoa taarifa ya mgao wa tatu wa Mirabaha inayotolewa na Ofisi ya Hakimiliki kwa wasani na wabunifu kutokana na watumiaji wa sanaa hizo.
Mwandishi wa habari wa Star Tv Abdallah Pandu akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma (hayupo pichani) katika Mkutano na wandishi wa Habari juu ya taarifa ya mgao wa tatu wa Mirabaha inayokusanywa na Ofisi ya Hakimiliki Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Mwalim akijibu maswali ya waandishi wa Habari.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ATEMBELEA VITUO VYA AFYA WILAYA YA KASKAZINI ''B'' UNGUJA

$
0
0
 ibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman wapili Kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkunga wa Kituo cha Afya cha Kiwengwa Khadija  Ali Juma Wakati alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya Afya Kaskazini  B Unguja.
 Naibu Waziri wa Afya  Harusi Saidi Suleiman katikati akiangalia shimo la Uchomwaji Taka linalotumiwa na Kituo cha Afya cha Kiwengwa baada ya kufanya ziara katika vituo vya Afya Kaskazini  B Unguja .kushoto ni  Mkunga wa Kituo cha Afya  Kiwengwa Khadija  Ali Juma.

 aibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akisaini Kitabu cha Wageni mara baada alipofika katika kituo cha Afya cha Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini B Unguja.

 Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman wakwanza kulia akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Bumbwini Misufini  Dk, KHamisi akitoa maelezo ya  Kumkaribisha  mara baada ya kufika katika Kituo hicho Mkoa wa Kaskazini B Unguja.
Mhudumu wa Afya  wa Kijiji  cha Bubwini Misufini Riziki Kiongwe Debe akitoa maelezo kuhusu changamoto zinazo wakabili kwa Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman (Hayupo pichani )mara baada ya kufika katika Kituo kilichopo kijijini hapo Mkoa wa Kaskazini B Unguja .


Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akifafanua jambo alipokutana na Wauguzi wa kituo cha Afya cha Bumbwini Misufini Mkoa wa Kaskazini B Unguja.kulia ni Afisa wa Afya Wilaya Mosi Kali Makame.PICHA NA MIZA OTHMAN-MAELEZO ZANZIBAR.

Hati za viwanja vya Bayport zaendelea kutolewa kwa wahusika

$
0
0
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akimkabidhi hati mteja wao Mary Simon, baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinapatikana kwa njia ya fedha taslimu na mikopo maalumu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Kulia ni Meneja Mikopo wa taasisi hiyo, Nasibu Kamanda. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Wateja wa Bayport wafurahia hati zao za viwanja

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana imeendeleza utaratibu wake wa kugawa hati kwa wateja wao walionunua viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa njia ya mikopo na fedha taslimu.

Mradi huo wa Vikuruti ulizinduliwa mwaka jana, ambapo baada ya kufanikiwa kwake, taasisi hiyo ikaanzisha miradi mingine mitano ambayo ni Kigamboni, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha na Kilwa, huku ikiweka utaratibu rahisi na nafuu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, alisema kwamba kugawa hati kwa wateja wao ni mwendelezo wa huduma nzuri zinazotolewa na taasisi yao kwa ajili ya kuwakomboa wananchi katika suala zima la ardhi.

Alisema kwamba makubaliano yao ni kuhakikisha taasisi inasimamia sualaa la hati ili wateja wao wasisumbuke kutokana na mchakato mzima wa utendaji kazi wao unaotoa urahisi juu ya upatikanaji wa viwanja vyao vyenye hati.

“Tunaendelea na kutoa hati kwa wetu walionunua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, ambapo Watanzania wengi walichangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo, ambavyo ukiacha vya Vikuruti, wateja wetu pia wanaweza kukopa fursa hii ya ardhi kwa miradi yetu ya Kimara Ng’ombe (Bagamoyo), Msakasa (Kilwa), Tundi Songani (Kigamboni), Boko Timiza (Kibaha), Kibiki na Mpera (Chalinze) na Kitopeni (Bagamoyo).
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akizungumza jambo baada ya kumkabidhi hati mteja wao Mary Simon kushoto baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Mikopo wa Bayport Financial Services, Nasibu Kamanda.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services katikati akisisitiza jambo.
Mteja wa Bayport Financial Services Sixtus Kilenga kushoto akisaini kama sehemu ya kukabidhiwa hati ya kiwanja. Hati hizo kwa wateja walionunua viwanja vinavyopatikana kwa njia ya mkopo na fedha taslimu zinaendelea kutolewa kwa waliokamilisha taratibu zao.


Naye mteja wa Bayport aliyopewa hati yake, anayejulikana kwa jina la Mery Simon Anthony aliipongeza Bayport kwa kutoa huduma nzuri kiasi cha kumfanya amiliki kiwanja chenye hati, huku kikiwa hakina mlolongo wowote.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu nimepata hati yangu kwa haraka na sijapata usumbufu wowote, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi katika miradi hii ya viwanja vya Bayport kwa sababu ni rasilimali nzuri,” Alisema.

Naye Sixtus Francis Kilenga alisema kwamba amefurahishwa na utaratibu mzima wa kupata kiwanja chenye hati, huduma zinazotolewa na Bayport, ambapo mteja hana jukumu lolote la kufuatilia hati katika maeneo yanayohusika.

“Utaratibu wa kununua kiwanja kasha ukapewa hati bila kufuatilia wizarani ni mpya, hivyo binafsi nimeufurahia na unaweza kuifanya Bayport kuwa moja ya ofisi zenye kujali muda na gharama za kiutendaji wa wateja wao,” alisema.

Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo ya bidhaa ikiwamo viwanja pamoja na fedha taslimu isiyokuwa na amana wala dhamana, huku taasisi hiyo ikiwa na matawi zaidi ya 82 nchi nzima kwa ajili ya kuwapatia Watanzania huduma bora.

TAZAMA HAPA LIVE MECHI YA TP MAZEMBE NA YANGA


MBUNGE WA ILEJE JANET MBENE ATAKA WALIOKULA FEDHA ZA MRADI WA HOSPITALI WACHUNGUZWE

$
0
0
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene, akiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo  akikagua sehemu ya juu ya jengo jipya la Hospitali ya Wilaya ya Ileje Ksata ya Itumba inayojengwa kwa pesa za Serikali ya Tanzania

 Mganga mkuu wa Hospitali ya  Ileje akitoa maelezo kwa  Mbunge wa Jimbo hilo Mh Janet Mbene alipokuw akaikagua ujenzi wa jengo jipya la Hospitali hiyo
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akitoa pole katika wodi ya Wanawake amabao walibahatika kujifungua kwa Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje.
  Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akitoa pole katika wodi ya Wanawake amabao walibahatika kujifungua kwa Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje.
  Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akiwa amembeba mmoja ya watoto waliozaliw akatika hospitali ya Wilaya ya Ileje

  Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akikagua mashine ya X -Ray  katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje
  Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akipita katika moja za wodi za Hospitali ya Wilaya ya Ileje


    Na Mwandishiwetu,  Ileje

 MBUNGE wa Ileje  Mh Janet Mbene,  amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo  kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika ubadhilifu wa fedha za mradi wa ujenzi wa Hospitlai ya Wilaya ya Ileje.

Mh Mbene alisema hayo alipofanya ziara katika Hospitali hiyo na kubaini upungufu mkubwa juu ya muda wa ujenzi wa Hospitali hiyo na kiasi cha pesa kilichotolewa na Wizara ya fedha katika kaukamilisha ujenzi huo ambao kwa sasa umekwama.

"Naomba Mkurugenzi afikishe swala hili kwa TAKUKURU, hili waweze kubaini ni kiasi gani ambacho kimeibiwa na wale wote waliohusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria hasa kwa mujibu wa sheria za utumishi wa Umma na kushtakiwa katika Mamlaka zinazo husika" alisema Mbene.

aliweka wazi kuwa inaonyesha wazi kuwa wakati wa kuvunja bara za la madiwani kiasi cha pesa zaidi ya milioni 100 kilikuwepo kwenye akaunti kwa jaili ya ujenzi wa jengo jipya la Hospitali ya Wilaya ya Ileje lakini mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi na kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani fedha hizo azionekani zilipokwenda.

anataja kuwa kumekuwa na utamaduni wa watendaji kutumia fedha kinyume na mipango hali inayfanya kukwama kwa miradi mingi katika Halmashauri hiyo.

alitoa wito kwa wananchi kuwa na imani na serikali walioichagua kwani sasa yeye kama mbunge yupo begakwabegakuakikisha anakomesha ufisadi ndani ya wilaya hiyo

KIKAO CHA EDWARD LOWASSA CHAZUIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

$
0
0
 

 Kikao cha ndani cha Mh.Edward Lowassa na wanachama wa Chadema wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kimezuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi asubuhi ya leo.
  Kikao cha ndani cha Mh.Edward Lowassa na wanachama wa Chadema wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kimezuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi asubuhi ya leo.

 Baadhi ya Wananchi wakitazama tukio hilo
 Kikao cha ndani cha Mh.Edward Lowassa na wanachama wa Chadema wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kimezuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi asubuhi ya leo.

DC GABRIEL DAQARRO AAPISHWA. AAHIDI MAKUBWA ARUSHA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akiapa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa wilaya mpya ya Arusha,Gabriel Daqarro(kulia)wanaoshuhudia ni Katibu Tawala mkoa,Richard Kwitega na Afisa wa Itifaki,Mukhsin Khasim.
Viongozi mbalimbali katika Jiji la Arusha wakifatilia tukio hilo.
Mwenyekiti wa CCM na Mbunge mstaafu wa Longido,Lekule Laizer(kushoto) akimskiliza Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Arusha DC,Mathias Manga.
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa.
Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

UFUNGUZI WA MAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA

$
0
0
 Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue mafunzo hayo ya siku tano.  Waliokaa ni Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uzalishaji, Tume ya Mipango (katikati) na Bw. John Mduma, Mhadhiri Mwanamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Jijini Mwanza katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta).
 Mgeni Rasmi Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uzalishaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa hotuba kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Rasilimali za Umma kwa washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita and Simiyu. Wengine ni Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (kushoto) na Bw. John Mduma, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia).
 Washiriki wakisikiliza na kufuatilia kwa makini mafunzo waliyokua wakipata kutoka kwa muwezeshaji.
 Washiriki wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Rasilimali za Umma kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita and Simiyu pamoja na wawezeshaji wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

Picha zote Na: Thomas Nyindo,Tume ya Mipango

Muwezeshaji Dr. Kenneth Mdadila, Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akishusha nondo kwa washiriki wa mafunzo hayo.

DC STAKI ATENGA SIKU YA JUMATATU KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki shughuli za maendeleo kwa kufyeka baadhi ya vichaka
 Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza na viongozi wa Kijiji na Kata ya Gonja Maore na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya
Dc Senyamule akishiriki zoezi la kupanga matofali yaliyofyatuliwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani humo.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ametenga Siku moja katika Juma ili kushiriki shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.

Huu ni utaratibu ambao Mkuu huyo wa Wilaya ameuanzisha kwa muktadha wa kuchochea ari katika utendaji Kazi na uwajibikani kwa kila mwananchi ili kuimarisha na kusukuma kwa vitendo juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa vitendo na utekelezaji wa utendaji kazi ili kuakisi dhana nzima ya serikali hii ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu.

"Nimeamua kutenga siku hii ya jumatatu kwani naamini italeta hamasa kwa wananchi kupenda kazi za maendeleo, itawatia moyo na kuona kuwa serikali ipo karibu nao ". Alisema Staki

Akizungumzia kuhusu kuanza kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Dc Staki amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaoishi kwa mazoea ya kuyumbishwa na siasa zisizo na manufaa kwao lakini huu si wakati tena wa kurudi nyuma badala yake watanzania wote wanapaswa kushirikiana katika kufanya Kazi na kulifanya Taifa Letu kufika mbali zaidi kimaendeleo.

Hii imekuwa ziara ya mwanzo ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki kwa kushiriki kufanya kazi za Jamii akiwa na dhamira ya kuwatia Moyo wananchi ili kupunguza lawama zisizo na lazima kwa serikali na badala yake kujituma katika kufanya kazi.

Ziara hiyo katika kushiriki Kazi za jamii imefanyika katika kijiji cha Mheza na Maore vilivyopo kata ya Gonja Maore huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kuishauri na kushirikiana na serikali.

Kwa upande wawananchi wa maeneo hayo walionyesha kufurahishwa na utaratibu huo ambao haujawahi kufanyika na kiongozi yeyote katika Wilaya ya Same tangu kuumbwa kwa msingi ya ulimwengu.

Wananchi hao wamemuakikishia Mkuu hiyo wa Wilaya hiyo kuwa watashirikiana nae katika shughuli za maendeleo kwani kwa kiasi kikubwa udini na uzembe wa watendaji wengi umesababisha kuendelea kuzorota kwa maendeleo ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Pamoja na hayo pia Dc Staki Ametoa onyo kwa wananchi hususani Vijana ambao ni wavivu katika kushiriki shughuli za Jamii kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu kW kila mwananchi atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake.

Viewing all 46340 articles
Browse latest View live


Latest Images