Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WANANCHI WAJITOKEZA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU JIJINI ARUSHA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru uliopokelewa leo katika Jiji la Arusha eneo la Kisongo kwaajili ya kukimbizwa kwa siku moja katika urefu wa Kilometa 81.19 katika Tarafa tatu.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia akipokea Mwenge wa Uhuru ambao utakimbizwa ukiwa unaelimisha na kueneza ujumbe wa "Washirikishwe na Kuwezeshwa" ujumbe huo ukiwa umeambatana na kauli mbiu "Vijana ni Nguvukazi ya Taifa Washirikishwe na Kuwezeshwa"
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,George Mbijima akizindua Kituo cha Afya  katika Kata ya Elerai jijini Arusha kitakachowahudumia wananchi wa Kata hiyo,Sombetini na Ngarenaro.Miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh 1.5 ambayo Soko,Afya,Maji,Elimu,Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi makundi maalumu,Ujenzi wa daraja na usafi na utunzaji wa mazingira.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,George Mbijima akiwagawia Vyandarua ukiwa ni mpango wa Jiji kupiga vita ugonjwa wa Malaria baada ya kuzindua Kituo cha Afya  katika Kata ya Elerai jijini Arusha.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,George Mbijima akizindua Soko la Mazao mchanyiko   katika Kata ya Elerai jijini Arusha .
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kimandolu ambako mradi wa maji ulizinduliwa

DRC yaonesha nia na Bomba la Mafuta, Afrika Mashariki

$
0
0
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese amesema Serikali ya Kongo iko tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania kwenye Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.

Mhe Lusa- Diese aliyasema hayo katika kikao kilichokutanisha ujumbe wake na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa lengo la ziara yake lilikuwa ni Serikali ya Kongo kuomba kushiriki na kuwa sehemu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kutokana na kwamba sehemu ya Kongo ina mafuta.

Alisema kuwa nchi ya Kongo kupitia wataalam wake ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini ili kufanikisha mradi mkubwa wa bomba la mafuta ambalo litanufaisha nchi zote za Afrika Mashariki.

Naye Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli alisema kampuni yake ina uzoefu kwenye utafiti na uchimbaji wa mafuta na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki, kampuni yake itakuwa na uwezo wa kusafirisha kuanzia mapipa 30,000 hadi 100,000 kwa siku kulingana na mahitaji.

Aliishukuru serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa tayari kushirikiana na Kongo kwenye mradi wa bomba la mafuta na kuongeza kuwa kupitia mradi huu nchi zote kwa pamoja zitapata mapato na kukua kwa uchumi wake.

Awali akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na Kongo katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki na kuelekeza wataalam kutoka nchi zote mbili kuanza kukutana kuanzia sasa kwa ajili ya kujadili mpango wa ujenzi wa bomba hilo na kumwalika Waziri wa Mafuta wa Kongo, Mhe Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese kwenye kikao cha Mawaziri wa Nishati na Madini kutoka nchi za Tanzania na Uganda kinachotarajiwa kufanyika Tanga mapema mwezi Oktoba.

Katika hatua nyingine Profesa Muhongo alisema kuwa nchi ya Kongo imeonesha nia kwenye utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na kuongeza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na nchi ya Kongo kupitia kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa mafuta katika ziwa hilo lenye viashiria vya mafuta.

Aidha alisisitiza kuwa mara baada ya ugunduzi wa mafuta katika Ziwa Tanganyika, nchi za Tanzania, Kongo na Burundi zitanufaika kupitia mapato pamoja na kuongezeka kwa ajira.


Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichoshirikisha Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese na ujumbe wake, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi mbele ya waandishi wa habari. Kushoto ni Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese.
Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli akisisitiza jambo katika kikao hicho.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipeana mikono na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto)

HAL yafanya kazi miaka 8 bila kibali cha TBS

$
0
0
KAMPUNI inayojulikana kama Hanspaul Automechs Limited (HAL) iliyopo Arusha imekuwa ikifanya kazi nchini kwa takriban miaka nane sasa bila kuwa na idhini ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS). 

HAL ilianzishwa mwaka 2007 ikijishughulisha na utengenezaji na uuzaji ndani na nje ya nchi mabodi ya magari maalumu kwa safari za kitalii maarufu kama ‘Safari’. 

Hayo yamefahamika hivi karibuni baada ya TBS kuthibitisha kuwa haijawahi kuipa HAL cheti cha ubora kwa ajili ya mabodi hayo, hivyo kuliweka njiapanda shirika hilo katika vita vya kusaka haki ya kutengeneza mabodi hayo yanayofahamika pia kwa jina la ‘War Bus’. 

Kesi ya kutafuta haki hiyo ipo mahakamani kwa muda mrefu sasa kati ya HAL na kampuni nyingine ya utengenezaji mabodi ya aina hiyo iliyopo Mjini Moshi, RSA Limited, ambao wanadai wao ndio wabunifu wa awali wa mabodi hayo. 

Wiki iliyopita, kilifanyika kikao kwenye Makao Makuu ya TBS jijini Dar es Salaam chini ya Mwanasheria wa Shirika hilo, Humphrey Shonga, kati ya maofisa wa TBS na wanasheria wa RSA Limited. 

Katika kikao hicho cha Agosti 18 mwaka huu, wanasheria wa RSA Limited walihoji sababu za TBS kuruhusu bidhaa zisizokuwa na cheti cha ubora kuingizwa katika soko la Tanzania na pia kuuzwa nje ya nchi zikitokea Tanzania. 

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya kikao hicho, ili TBS iweze kuwapa HAL cheti cha kuthibitisha ubora wa bidhaa zao, waliwaagiza kuwasilisha vielelezo na michoro ya utengenezaji wa mabodi hayo ambavyo haviendani na vya mshindani mwingine yeyote. 

“HAL wameshindwa kuwasilisha vielelezo hivyo hadi leo,” alisema mmoja kati ya watu waliohudhuria kikao hicho ambaye hakupenda jina lake liandikwe na kuongeza: 

“Hata hivyo, pamoja na kutotambuliwa na TBS, HAL imekuwa ikipata upendeleo wenye shaka wa kutengeneza na kuuza ndani na nje ya nchi bidhaa hizo.” 

Barua ya Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA) kwa wanasheria wa RSA Limited ya Julai 25 mwaka huu, inaweka wazi kuwa, Februari 24, 2016, HAL ilipewa leseni ya muda (Temporary Industrial License) namba 00000928 ikitakiwa kuwasilisha taarifa ya maendeleo za kila mwaka huku bidhaa zinazozalishwa zithibitishwe ubora na TBS. 

“Hii inathibitisha kuwa kwa miaka nane, HAL imekuwa ikibadili na kutengeneza mabodi ya magari ya kitalii bila kuwa na leseni huku mamlaka husika zikishindwa kuchukua hatua,” alisema mtoa habari wetu. 

Kwa mujibu wa kanuni za TBS na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), magari yote yenye dhamana ya kubeba abiria lazima yathibitishwe na TBS kabla ya kuingia barabarani. 

“Lakini hadi sasa TBS haijaonyesha nia ya kutekeleza kanuni hiyo kwa walau kuionya HAL kwa kosa la kuingiza bidhaa zake sokoni bila kibali chao, au kuuambia umma kwmba mabodi yao (Safari Tourist Bodies) ni salama na halali kubeba abiria au la,” alisema. 

Ukimya wa TBS unazidisha shaka kwa sababu ni wazi kuwa maofisa wao waliopo kwenye mipaka kama Namanga, Sirali au Mutukula na wengine wanaofanya ukaguzi maeneo mbalimbali nchini wamewahi kukutana na bidhaa za HAL. 

“Au basi hata barua za RSA Limited za mwaka 2008, 2014, 2015 na 2016 (nakala zake tunazo) kuitaarifu TBS suala hili, zingetosha kuwaamsha wakaguzi wa shirika hili muhimu kwa afya na usalama wa Watanzania na kuchukua hatua,” alisema. 

Alipotafutwa jana kwa njia ya simu kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi, Afisa habari wa TBS, Bi Rhoida Andusamile alisema hawakuwa tayari kuizungumzia swala hilo kwani shirika hilo ilikuwa katika maandalizi ya kutoa taarifa rasmi hapo baadaye, bila kutaja ni lini taarifa hiyo itatoka. 

Kwa upande mwingine, HAL pia imekuwa ikipata mauzo makubwa kwa kuungwa mkono na Toyota Tanzania Limited (TTL) inayotambua bidhaa hizo wakati ubora wake haujathibitishwa. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa HAL Group, Satbir Hanspaul, kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha kati ya mabodi (war bus) 30 na 35 kwa mwezi lakini hutengeneza mabodi aina ya Winnebago kwa oda maalumu. 

Mwaka jana, Hanspaul aliwaambia waandishi wa habari kuwa Kenya, Uganda na Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zinazoagiza 'War Buses' kutoka Arusha kwa ajili ya kusafirisha watalii kwenye mbuga zao. 

Zipo taarifa kuwa mataifa mengine ya ughaibuni huagiza mabodi yaliyotengenezwa maalumu na kampuni hiyo kwa ajili ya kutumiwa na majeshi ya huko.

TEA KUFADHILI UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU KATIKA MAENEO YASIO RAHISI KUFIKIKA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Joel Laurent (wa kwanza kushoto) akijadiliana suala na viongozi wa Halmashauri ya Kilosa, Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kutekeleza na kufadhili mradi wa kujenga nyumba za walimu kupitia Watumishi Housing Ltd katika Ujenzi katika maeneo yasio rahisi kufikika, katika shule ya Sekondari Uleling'ombe iliyopo Wilaya ya Kilosa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Laurent akiongea na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, kamati ya shule ya Uleling'ombe,uongozi wa kijiji cha Uleling'ombe wakijadilana utekelezaji wa Mradi wa kujenga nyumba za walimu katika maeneo yasio rahisi kufikika, katika shule ya Sekondari Uleling'ombe iliyopo Wilaya ya Kilosa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Laurent akioneshwa eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Uleling'ombe mradi unaotekeleza na kufadhili na Mamlaka ya Elimu Tanzania ikiwatumia Watumishi Housing Ltd katika Ujenzi katika maeneo yasio rahisi kufikika.
Picha ya pamoja.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent amesisitiza kuwa taasisi yake itaendelea kutafuta rasilimali ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanosoma katika maeneo ambayo ni magumu kufikika wanajengewa miundombuni ili kupata elimu bora.

Mkurugeni Mkuu huyo alisema hayo wilayani Kilosa wakati akikagua eneo la ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya sekondari ya Uleling’ombe utakaogharimu zaidi ya 148m/- ambayo walimu sita watakaa katika nyumba hiyo.

Alisema mamlaka hiyo imetiliana saini mkataba na Watumishi Housing wa ujenzi wa nyumba za walimu 40 nchi nzima katika maeneo ambayo ni magumu kufikika ili kuhakikisha kuwa walimu wapya wanaopangiwa katika maeneo hayo ambao wengi wamekuwa wakikimbia kufundisha wanapata sehemu nzuri za kuishi.

Aliongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha mamlaka yake imetenga bajeti ya kujenga nyumba 30 mwaka huu ambapo ujenzi wa kila nyumba ni miezi mitatu.“Nyumba hii itakapokuwa tayari na tunategemea ikamilike ifikapo Desemba mwaka huu, itakuwa na uwezo wa kuwaweka walimu sita kuishi katika nyumba hiyo ila tunazitaka halmashauri kuangalia uwezekano wa kuwawekea samani za ndani” alisema.

Na pia alisisitiza juu ya umuhimu wa ushiriki wa wananchi na halmashauri hizo katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hizo unazingatia ujenzi ili ziweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kuwanufaisha wanafunzi wengi zaidi.TEA ilibuni mradi huo baada ya kugundua kuwa kuna uhitaji maalum wa makazi ya walimu katika mazingira ambayo ni vigumu kufikika ambapo wengi ambao wamekuwa wakipangiwa kufundisha hutafuta uhamisho na hivyo wanafunzi wa maeneo hayo ufaulu wao umekuwa mdogo kutokana na kukosa walimu.

“Walimu wanaokusudiwa kuishi katika nyumnba hizi ni wale wanaoanza kazi ndiyo maana ni chumba na sebule kwa kila mwalimu kwani tunaamini baada ya muda watakuwa wameishazoea na kuweza kujipatia makazi uraiani pale watakapokuwa tayari kuanza familia” Alisema Bw Laurent.

Aliongeza kuwa mamlaka hiyo inajadiliana na wadau mbali mbali ili kuona kama wataweza kuwezesha upatikanaji wa internet na ving’amuzi katika sebule ya pamoja ya nyumba hizo ili wale watakaopangiwa maeneo hayo wasijione kuwa wamepangiwa katika mazingira ambayo si rafiki au wameonewa.

Akizungumza katika ukaguzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Bw Rwegerela Katabaro alisema kuwa wako tayari kushirikiana na TEA japo rasilimali fedha imekuwa ni changamoto kubwa.

Aliomba kuwa katika miradi mingine halmashauri zipewe taarifa za awali ili ziweke kutenga fungu katika bajeti zaona hivyo kuchangia katika juhudi za maendeleo.Alimhakikishia Mkurugenzi Mkuu huyo juu ya ushiriki wa halmashauri kusimamia kwa karibu ujenzi wa nyumba hiyo ili kupata nyumba ambayo inalingana na thamani ya fedha zilizotengwa.

Aidha ili kuondoa mgongano alishauri TEA itoe muongozo ili kila taasisi ijue jukumu lake katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hiyo unakuwa bora na kwa viwango walivyokubaliana.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Uleling’ombe, Magashi Shimba alishukuru kwa kupatiwa mradi huo kwani walimu wengi wanaopangiwa huko huwa hawarudi kutokana na mazingira hasa upatikanaji wa makazi.

Rais Magufuli amteua Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2016 amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Bw. Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2016

MFUKO WA PSPF WATOA ELIMU YA KUJIUNGA KATIKA MFUKO WA KUJICHANGIA KWA HIARI KWA WANANCHI WASIO KATIKA SEKTA RASMI ZANZIBAR

$
0
0

Afisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Fadhila akizungumza wakati wa Mkutano Taasisi zisizo rasmin za Wavuvi, Madereva wa gari za mchanga, Kifusi na Wakulima wa mbogamboga kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari ya Mfuko wa PSPF uliofanyika katika ukumbi wa Betilyamin Malindi Zanzibar.

Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakimsikiliza Afisa wa Mfuko wa PSPF akitowa maelezo kuhusiana na Mfuko huo.
Afisa wa Idara ya Uvuvi na Maendeleo Zanzibar Ndg Mohammed Chum akitowa maelezo wakati wa mkutano huo na Mfuko wa PSPF kwa Wavuvi wa Zanzibar kujiunga na Mfuko huo.

Waziri wa Kilimo Maliasili Uvuvi na Mifugo Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akifungua mkutano wa Wavuvi na Wananchi wasio kuwa katika Sekta Rasmin kujiunga na Mfuko wa PSPF katika Mafao ya Hiari ili kupata huduma muhimu za maendeleo kupitia mfuko huo.

Waziri wa Uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohammed akisisitiza jambo wakati wa kufungua Mkutano wa Wadau Wasiokuwa katika Sekta Rasmin kujiunga na Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiara ili kupata fursa mbalimbali zinazotolewa na PSPF kwa Wanchi wa Tanzania.

Afisa wa PSPF Zanzibar Bi Faidha Katavi akitowa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi kujiunga na Mfuko huo baada ya kufungua mkutano huo wa kuwahamashisha Wananchi wasio kuwa katika Sekta rasmin kujiunga na Mfuko wa Kujichangia kwa Hiara Mafao yao na kupata fursa zinazotolewa na PSPF kwa Watanzania.
Mhe Hamad Rashid akijaza fomu ya Kuchangia kwa Hiari Mfuko wa PSPF baada ya kuufungua Mkutano huo na Wavuvi.

Afisa wa PSPF Bi. Faidha Katavi akitowa maelezo jinsi ya kujiunga na Mfuko wa PSPF Kujichangia kwa Hiara Mafao katika mfuko huo.

Afisa PSPF Ndg. Hadji Jamadari akitowa maelezo jinsi ya kujiunga na Mfuko wa PSPF kwa mafao ya kujichangia kwa hiari kupitia mfuko huo kwa Wananchi wasio katika Sekta rasmin jinsi wanavyoweza kunufaika kupitia kuchangia mafao kwa hiari.



Afisa wa PSPF Ndg Hadji Jamadari akitowa maelekezo kwa Wananchi wanaojiunga katika Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiari wakati wa mkutano huo kutowa Elimu ya Mfuko kwa Wananchi wa Zanzibar wasio kuwa katika Sekta Rasmin.


Afisa wa PSPF Ndg. Hadji Jamadari akitowa maelezo ya moja ya fomu ya kujiunga na Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiara kwa Wananchi wasiokuwa katika Sekta rasmin, mkutano huo umewashirikisha Wavuvi, Wachimba Mchanga, Magari ya Mizigo ya Mchanga na Kifunzi na Umoja wa Jumuiya wakulima wa mbogamboga Zanzibar.

RC SIMIYU ATOA UFAFANUZI SAHIHI WA TAARIFA KUHUSU WALIMU WAKUU KUVULIWA MADARAKA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka,
Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema(kulia) akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) wa kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.



Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa ufafanuzi wa agizo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata mkoani humo, ambalo Serikali ya Mkoa ililitoa tarehe 17 Agosti ,2016 katika kikao ambacho alipokea Vishikwambi (tablets) 637 kutoka EQUIP Tanzania (Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini) kwa ajili ya Walimu wakuu na Waratibu wa Elimu Kata

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshaji wa agizo hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii., kuwa Mkuu wa Mkoa ametangaza kuwavua madaraka Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata wote wa Mkoa huo; hali iliyopelekea baadhi ya Walimu wakuu na Waratibu kukosa ari ya kufanya kazi, kwa kigezo cha kusubiri kuvuliwa madaraka.

Mtaka amesema Mkoa ulipokea taarifa za takwimu za wanafunzi hewa, vyumba vya madarasa, idadi ya walimu na idadi ya madawati, baada ya kupokea taarifa hizo ulionekana utofauti mkubwa wa takwimu hizo ndipo Serikali mkoani humo, ikaahidi kupitia mapungufu ya udanganyifu wa takwimu hizo kwa kila shule na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha Walimu wakuu na Wakuu wa Shule waliodanganya idadi ya wanafunzi.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu umepata bahati ya kuwa na Mradi wa EQUIP Tanzania ambao umewawezesha waratibu kupata pikipiki na posho, walimu wakuu wamepewa vishikwambi kwaa jili ya utunzaji wa takwimu, hivyo Serikali inao wajibu wa kuangalia mahitaji ya Mkoa katika elimu ambapo alielekeza yafanyike mabadiliko ya Walimu wakuu Msingi, Sekondari na Waratibu wa mkoa mzima.

“Nililisema mwanzo na leo nalirudia tutafanya mabadiliko makubwa kwa Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari na Waratibu Elimu kata kwa kujiridhisha na maendeleo ya shule zetu, idadi ya walimu waliopo,idadi ya wanafunzi, kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na mazingira ya shule ; lakini tutatoa upendeleo kwa shule 10 bora katika kila wilaya kwa Mitihani ya Kitaifa ya Darasa la IV, VII Kidato cha II na IV , hiki ni kipimo kimojawapo cha walimu wa kuendelea nao. Nasisitiza hakuna mtu atakayeonewa wala kufedheheshwa”, alisema Mtaka.

Mtaka amesema azma ya Serikali ni kuibua vipaji vipya vya viongozi wa Elimu katika ngazi ya Wilaya ambapo alisema ameshaagiza Maafisa Elimu wa Wilaya kuwasilisha taarifa ya walimu waliojiendeleza katika ngazi shahada ya kwanza na shahada ya uzamili ili watakaokuwa na sifa waweze kuteuliwa katika nafasi za Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata ambao watafanyiwa upekuzi (vetting) na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Sanjari na hilo , Mkuu huyo wa Mkoa amesema Walimu wakuu na Wakuu wa shule wa zamani ni tofauti na wale wa sasa, kwa kuwa sasa hivi wamekuwa maafisa masuuli wa shule zao ambapo wanapokea fedha za Elimu bila malipo kupitia akaunti za shule zao, hivyo ni lazima wapatikane watu waadilifu, wenye sifa na uwezo wa kuongoza shule na kusimamia fedha za Serikali.

Akichangia katika kikao hicho Afisa Elimu (Msingi) Wilaya ya Meatu, George Lowasa ameshauri Uchambuzi wa watu watakaoteuliwa ufanyike katika umakini mkubwa ili wapatikane watendaji wazuri na kuhusu utoaji wa takwimu sahihi alishauri kuwe na utaratibu wa kuziboresha kila (robo) baada ya miezi mitatu ili kuwa na takwimu sahihi pale zinapohitajika.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesema Uteuzi huo utazingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uteuzi ambapo hakuna mtu atakayeonewa au atakayependelewa.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amesema atawachukulia hatua Maafisa wale wanaolalamikiwa na walimu kwa kuwatolea lugha mbaya kila wanapotoa huduma kwa walimu hao katika Halmashauri za Mkoa huo.

Naye Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema ameshauri baada ya mabadiliko ya wakuu wa shule na Waratibu wa Elimu Kata kufanyika wale ambao wataonekana hawana sifa za kuendelea kushika nafasi hizo waondolewe kwa staha, ambapo aliomba Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa ikishirikishe chama hicho katika masuala yote muhimu ya kuendeleza sekta ya Elimu, kwa kuwa wanamsaidia mwajiri katika usimamizi wa utendaji kwa walimu.

Kikao hicho cha wadau kilichofanyika mjini Bariadi na kimewahusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Maafisa Elimu kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ngazi ya Mkoa na Wilaya.

WAZIRI MKUU ATOA SIKU MBILI KWA MAOFISA ARDHI KUMALIZA KERO ZA WANANCHI

$
0
0



 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Miundombinu wa mkoa wa Rukwa pamoja na Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Sumbawanga kutatua matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa Manispaa hiyo.



“Ijumaa kuanzia saa 3.00 asubuhi wenye kero za ardhi wote waende kwenye ukumbi wa Manispaa mkuu wa idara atakuwa na watumishi wote na hapa mtasikilizwa kero zenu na kupatiwa ufumbuzi. Nasiku hiyo hakuna kazi nyingine ni kusikiliza wananchi tu,” alisema.



Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza na maelfu ya wakazi Mji wa Sumbawanga waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela katika jimbo la Sumbawanga mjini ambapo aliwasisitiza watendaji hao kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao.



Alisema tangu alivyoanza ziara yake katika mikoa ya Rukwa na Katavi kila eneo alilopita amekutana na wananchi wakiwa na mabango yanaeleza changamoto na hii inatokana na viongozi wa mikoa hiyo kushindwa kutenga siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero hizo.



Waziri Mkuu alibainisha kwamba baadhi ya mikoa na halmashauri mbalimbali nchini zimeshaanza utaratibu huo wa kutenga siku maalumu katika wiki na kusikiliza matatizo yanayowakabili wananchi jambo ambalo limeanza kuonesha mafanikio ya utatuzi wa kero hizo.



Awali akizungumza katika mkutano huo mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly alisema wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya migogoro mikubwa ya ardhi, hivyo alimuomba Waziri Mkuu kuwasaidia katika kuipatia ufumbuzi.



Mbunge huyo alisema migogoro hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu imewasababishia usumbufu mkubwa wakazi wa jimbo hilo kukosa haki  zao na muda mwingi wamekuwa wakiutumia kufuatilia hatma ya ardhi yao bila ya mafanikio hivyo kurudi nyuma kimaendeleo.



Pia mbunge huyo alimuomba Waziri Mkuu kuwaondolea zuio la kuuza mazao yao nje ya nchi kwa sababu kitendo hicho kimesababisha kushuka bei ya mahindi na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima ambao wametumia gharama kubwa katika kuandaa mashamba.



Akizungumzia zuio hilo Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali kuzuia uuzwaji wa mazao nje ni kutaka kujiridhisha na uwepo wa chakula cha  kutosha nchini ili kuepuka kukumbwa na baa la njaa na kisha kwenda kuomba msaada kwenye nchi tuliowauzia.



 Kuhusu suala la soko la mahindi Waziri Mkuu alisema Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) watanunua kwa bei ya soko na kwamba wataruhusiwa kuuza nje ya nchi baada ya Serikali kujaza maghala yake huku wataalam wakimalizia kufanya tathmini ya hali ya chakula nchini.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Jenista Mhagama kufungua Maonesho ya wajasiriamali.

$
0
0


Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa wa kwanza kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali yataofanyika Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali yataofanyika Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa.



Habari/Picha Na Ally Daud.

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama anatarajiwa kufungua maonesho ya wajasiliamali yatofanyika Septemba 26 katika viwanja vya Mlimani City ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Ujasiriamali na ushindani Tanzania(TEEC) kwa kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ili kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng’i Issa amesema kuwa maonesho hayo yatalenga kuwawezesha wananchi kuwa wabunifu katika sekta ya biashara ili kupiga hatua kufikia uchumi wa kati.

“Maonesho ambayo yatafanyika kesho ni kwa ajili ya wajasiriamali wote wakubwa, wa kati na wadogo ili kuwawezesha kiujuzi na kiushindani katika soko la biashara” alisema Bi. Issa.

Aidha Bi. Issa amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na kliniki ya biashara kwa watu wote kutoka kwa wataalamu wa biashara ili kuweza kuwapatia mafunzo wajasiriamali wakubwa na wadogo ili waweze kupata mafanikio yao na jamii kwa ujumla kupitia biashara zao.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye amesema kuwa maonesho hayo yatawajengea wajasiriamali fursa za masoko kwa biashara nchini na Afrika kwa ujumla.

“Kupitia maonesho hayo wajasiriamali watapata fursa ya kutengeneza masoko ya biashara zao kwa ubora zaidi nchini na afrika kwa ujumla ili waweze kujitangaza kimataifa” alisema Bw. Simbeye.

Aidha Bw. Simbeye amesema kuwa wana mpango wa kuwaelimisha wajasiriamali kwa wingi zaidi ili waweze kuwa wabunifu na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya biashara ndani na nje ya Tanzania.

Mbali na hayo Mkurugenzi Simbeye amesema kuwa anawakaribisha watu wote wajasiriamali wakubwa na wadogo kufika katika maonesho hayo ambayo hayana kiingilio ili waweze kupata ujuzi wa kutosha kwa maendeleo ya biashara zao na kuinua uchumi wa nchi.

MAABARA ZA GST, TIRDO ZATEULIWA KUTHIBITISHA UBORA WA MAKAA YA MAWE

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (kushoto kwa Waziri), wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa Mkutano baina ya Wizara na wachimbaji pamoja na watumiaji wa makaa ya mawe, uliofanyika Agosti 24 wizarani, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo katika mkutano na wachimbaji pamoja na watumiaji wa makaa ya mawe (hawapo pichani) uliojadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Mkutano huo ulifanyika Agosti 24, mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.
Wajumbe mbalimbali walioshiriki Mkutano baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Wachimbaji pamoja na Watumiaji wa Makaa ya Mawe, wakifuatilia mijadala mbalimbali katika Mkutano huo uliofanyika Agosti 24 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.


Veronica Simba na Devota Myombe

Serikali imeziteua maabara za Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Shirika la Umma linalojishughulisha na tafiti mbalimbali pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu Viwanda (Tanzania Industrial Research and Development Organization – TIRDO), kupima na kuthibitisha ubora wa makaa ya mawe yanayozalishwa nchini.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema Maabara hizo za GST na TIRDO zitatumika kupima na kuthibitisha ubora wa makaa hayo pale inapotokea mgogoro wa kutokukubaliana kuhusu ubora wake baina ya wazalishaji na watumiaji wake. Aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam alipokutana na kuzungumza na wazalishaji na wamiliki wa Viwanda vinavyotumia makaa ya mawe nchini kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo.

Maelekezo hayo ya Waziri Muhongo yalitokana na wasiwasi walioonesha baadhi ya wajumbe wa kikao hicho, hususan watumiaji wa makaa ya mawe, ambao wamekuwa wakilalamika kuwa madini hayo yanayozalishwa nchini hayana ubora unaotakiwa na hivyo kuagiza kutoka nje ya nchi, kabla ya hivi karibuni kuzuiwa na Serikali na kuwataka wanunue yanayozalishwa hapa nchini.

Akitoa maelekezo kuhusu utaratibu utakaotumika, Profesa Muhongo alisema kuwa, pande zote mbili, yaani wazalishaji na watumiaji wanapaswa kuwa na maabara zao ambazo zitatumika kupima ubora wa makaa husika. Alielekeza kuwa, kabla ya kupeleka mzigo wa makaa ya mawe kwa watumiaji, wazalishaji wanapaswa kupima ubora wake katika maabara zao na kuweka alama inayoonesha ubora husika juu ya mzigo.

Aidha, kwa upande wa watumiaji, Waziri Muhongo alielekeza kuwa, wanapopokea mzigo husika, wanapaswa kuupima katika maabara zao, kabla ya kuutumia ili kujiridhisha kuhusu ubora wake kama ambavyo utakuwa umeainishwa katika alama iliyofungwa juu ya mzigo.

“Mkijiridhisha kuwa makaa ya mawe mliyopokea yana ubora unaotakiwa, mtapaswa kusaini kuthibitisha hilo na endapo mkigundua kuna tofauti, mna haki ya kutokusaini na kutokuyatumia makaa hayo,” alifafanua. Waziri Muhongo aliongeza kuwa, endapo itatokea mgogoro wa kutokuelewana kuhusu ubora wa makaa yaliyowasilishwa na mzalishaji kwa mtumiaji, pande hizo mbili zitapaswa kutoa taarifa serikalini kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa kushughulikia migogoro katika sekta husika.

Alisema kuwa, suala husika likifikishwa serikalini, Mwenyekiti atasimamia zoezi la upimwaji wa makaa husika katika moja ya maabara zilizoteuliwa, ambazo ni GST na TIRDO ili kuthibitisha ubora wake na hivyo kufikia muafaka. Waziri Muhongo aliwataka wazalishaji na watumiaji wa makaa ya mawe kuacha manung’uniko yasiyo na tija na kila upande utimize makubaliano yaliyofikiwa katika vikao vyote vya awali na kwamba, Serikali kwa upande wake, itatimiza wajibu wake ipasavyo.

WAJUMBE WA BODI STAMICO WATEMBELEA MGODI WA TANZANITEONE

$
0
0

Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la madini nchini (STAMICO) wakiwa na baadhi ya watumishi wa kampuni ya TanzaniteOne na STAMICO walipotembelea mgodi wanaoumiliki kwa ubia na kampuni hiyo uliopo mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


Wajumbe wa bodi ya shirika la madini nchini (STAMICO) wakiwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Balozi Alexiander Muganda, (mwenye nguo ya rangi ya buluu) baada ya kutembelea mgodi wanaoumiki kwa ubia na kampuni ya TanzaniteOne uliopo mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la madini nchini (STAMICO) Zena Kongoi akizungumza na waandishi wa habari, kwenye mgodi wanaoumiliki kwa ubia na kampuni ya TanzaniteOne.

Wajumbe bodi ya STAMICO wakipanda scip kwa ajili ya kuingia kwenye mgodi wa madini ya Tanzanite uitwao CT.


MFUKO WA PSPF WATOA ELIMU YA KUJIUNGA NA MFUKO WA KUJICHANGIA KWA HIARI KWA WANANCHI WASIO KATIKA SEKTA RASMI ZANZIBAR

$
0
0

Afisa wa Idara ya Uvuvi na Maendeleo Zanzibar Ndg Mohammed Chum akitowa maelezo wakati wa mkutano huo na Mfuko wa PSPF kwa Wavuvi wa Zanzibar kujiunga na Mfuko huo.
Afisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Fadhila akizungumza wakati wa Mkutano Taasisi zisizo rasmin za Wavuvi, Madereva wa gari za mchanga, Kifusi na Wakulima wa mbogamboga kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari ya Mfuko wa PSPF uliofanyika katika ukumbi wa Betilyamin Malindi Zanzibar.
Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakimsikiliza Afisa wa Mfuko wa PSPF akitowa maelezo kuhusiana na Mfuko huo. 
Waziri wa Kilimo Maliasili Uvuvi na Mifugo Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akifungua mkutano wa Wavuvi na Wananchi wasio kuwa katika Sekta Rasmin kujiunga na Mfuko wa PSPF katika Mafao ya Hiari ili kupata huduma muhimu za maendeleo kupitia mfuko huo. 
Waziri wa Uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohammed akisisitiza jambo wakati wa kufungua Mkutano wa Wadau Wasiokuwa katika Sekta Rasmin kujiunga na Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiara ili kupata fursa mbalimbali zinazotolewa na PSPF kwa Wanchi wa Tanzania.
Afisa wa PSPF Zanzibar Bi Faidha Katavi akitowa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi kujiunga na Mfuko huo baada ya kufungua mkutano huo wa kuwahamashisha Wananchi wasio kuwa katika Sekta rasmin kujiunga na Mfuko wa Kujichangia kwa Hiara Mafao yao na kupata fursa zinazotolewa na PSPF kwa Watanzania.  
Mhe Hamad Rashid akijaza fomu ya Kuchangia kwa Hiari Mfuko wa PSPF baada ya kuufungua Mkutano huo na Wavuvi.
Afisa wa PSPF Bi. Faidha Katavi akitowa maelezo jinsi ya kujiunga na Mfuko wa PSPF Kujichangia kwa Hiara Mafao katika mfuko huo.
Afisa PSPF Ndg. Hadji Jamadari akitowa maelezo jinsi ya kujiunga na Mfuko wa PSPF kwa mafao ya kujichangia kwa hiari kupitia mfuko huo kwa Wananchi wasio katika Sekta rasmin jinsi wanavyoweza kunufaika kupitia kuchangia mafao kwa hiari.
Afisa wa PSPF Ndg Hadji Jamadari akitowa maelekezo kwa Wananchi wanaojiunga katika Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiari wakati wa mkutano huo kutowa Elimu ya Mfuko kwa Wananchi wa Zanzibar wasio kuwa katika Sekta Rasmin. 
Afisa wa PSPF Ndg. Hadji Jamadari akitowa maelezo ya moja ya fomu ya kujiunga na Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiara kwa Wananchi wasiokuwa katika Sekta rasmin, mkutano huo umewashirikisha Wavuvi, Wachimba Mchanga, Magari ya Mizigo ya Mchanga na Kifunzi na Umoja wa Jumuiya wakulima wa mbogamboga Zanzibar. 
Picha ya Pamoja.

Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi ( LTSP ) Kupunguza Migogoro ya Ardhi, MOROGORO

$
0
0
Na Salum Mwinyimkuu, Morogoro.

Zaidi ya hatimiliki 300,000 za Ardhi zinatarajiwa kutolewa kwenye Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA mkoani Morogoro kupitia mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi wa LTSP, ili kupunguza Migogoro ya Mipaka kwenye Vijiji.

Miongoni mwa Changamoto inayofifiza Juhudi za Serikali kumaliza tatizo la Migogoro ya Ardhi katika Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA ni Rushwa kwa Baadhi ya Watendaji wasio waaminifu.

Wilaya ya KILOMBERO yenye vijiji 99 imejizolea Umaarufu kwa kuwa na maeneo mengi yenye Utata wa Ardhi,ikihusisha migogoro ya Mipaka baina ya kijiji na kijiji, hifadhi na kijiji pamoja na wakulima na wafugaji.
Godfrey Machabe Mratibu wa Program ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi (kushoto), Renit Halimba Diwani Viti maalum Wilaya ya Kilombero (wa pili kushoto) Lucas Mwaisaka Katibu tawala msaidizi Wilaya ya kilombero (kulia) Alicie Libenanga (wa pili Kulia) na Syabomi Mwaipopo (katikati) Dkt Steven Nindi Wakikabidhiana Mpango wa matumizi Bora ya Ardhi Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

Wajumbe na Viongozi wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kushiriki Semina ya Uhamasishaji wa Ujenzi wa Masjala za Ardhi zaVijiji, Kukabidhi Mpango wa matumizi Bora ya Ardhi wa Wilaya na kutambulisha timu ya upimaji Mipaka iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro.

Ili kuhakikisha Changamoto hiyo inabaki Historia, mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi umetua Wilayani Kilombero, ukiwa na Shabaha ya kupima mipaka ya Vijiji 20,na kupatiwa Hatimiliki ya Ardhi ili kuondoa Migogoro hiyo.

MARY MAKONDO ni Kaimu kamishna wa Ardhi nchini akizungumza Wilayani humo, ameeleza umuhimu wa Mradi huo unaofadhiliwa kwa Dola Milioni 15.2, wenye lengo la Kurasimisha Ardhi ili imnufaishe Mwananchi wa Masikini na kuondoa Migogoro isiyo na tija.

Zoezi hilo la Urasimishaji Ardhi na Utoaji wa Hatimiliki za Kimila litaenda sambamba na Ujenzi wa Masjala za Ardhi kwenye Vijiji vilivyopo kwenye mpango wa LTSP,lengo likiwa ni kuweka sawa kumbukumbu za Mikataba inayohusu Ardhi.

Itakumbukwa Mradi huu ni matokeo ya Mkutano wa wakuu wa nchi zenye Uchumi Mkubwa Duniani, ambapo Tanzania ilialikwa kuhudhuria kama mshiriki, ambako kulizinduliwa Ushirikiano kati yake na Kundi la G8 kuhusu uwazi kwenye sekta ya ardhi.
Kiongozi wa Urasimishaji kutoka Mpango wa Land Tenure Support Programme, Swagile Msananga akifafanua Jambo kuhusu Masjala za Ardhi za Vijiji katika Semina ya uhamasishaji wa Ujenzi wa masijala hizo iliyofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
Kaimu mkurugenzi mkuu tume ya taifa ya Matumizi ya ardhi Dkt Stephen Nindi (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Ardhi Bi Mary Makondo wakikabidhi mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya wilaya kwa kaimu Mkurugenzi wa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Gerald Kauki (Kulia) wakati wa Semina ya Uhamasishaji wa Ujenzi wa Masijala za Ardhi za Vijiji, Sambamba na kutambulisha timu ya upimaji Mipaka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Morogoro.
Timu ya Maafisa kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Waliosimama) iliyowasili Mkoani Morogoro kwa kazi ya Kupima na kumilikisha Ardhii takayofanyika katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

BENKI YA BARCLAYS WAZINDUA MKOPO WA NYUMBA KWA WANANCHI.

$
0
0
BENKI ya Barclays Tanzania wazindua mkopo wa Nyumba kwa wananchi mkopo ambao utaanzia shilingi Milioni 30 hadi Mkopo wa Milioni 50 ambao utakuwa na riba ya asilimia 19.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za rejareja wa Benki ya Barclays, Oscar Mwafwagasi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema Mkopo huo ni kwa waajiliwa wa kudumu.

Amesema kuwa Mkopo utakopeshwa kwa wazawa wa Tanzania(Raia wa Tanzania) tuu pia unaatakiwa kulipa kuanzia  mwaka wa kwanza wa mkopo hadi miaka 20.
 Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za rejareja wa Benki ya Barclays, Oscar Mwafwagasi akizungumza wakati wa kuzindua Mikopo ya Nyumba kwa  wananchi hapa nchini ambao utaanzia shilingi Milioni 500 ambao utakuwa na riba ya asilimia 19. Kulia ni Meneja wa Masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera.

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za rejareja wa Benki ya Barclays, Oscar Mwafwagasi, Meneja wa Masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera na Mkurugenzi wa biashara na wateja wa rejareja wa benki ya Barclays, Kumar Pather wakisikiliza kwa makini swali kutoka kwa mwandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani , ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi ifikapo mwezi Februari, mwakani. Kikao kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati), katika kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani , ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi ifikapo mwezi Februari, mwakani.Wa kwanza mkono wa kulia kwa Naibu Waziri ni Katibu Mtendaji wa baraza ambae pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani , Mohamed Mpinga. Kikao kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Henry Bantu, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani , ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi ifikapo mwezi Februari, mwakani. Kikao kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ASP Deus Sokoni, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani, ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi ifikapo mwezi Februari, mwakani. Kikao kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Moro Kids yatwaa ubingwa Airtel Rising Stars Morogoro

$
0
0
Wachezaji wa timu ya moro kids wakishangilia baada ya kunyakua kombe la mashindano ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ya Angrikana 1-0 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro jana.
Kapteni wa timu ya Moro Kids Abdul Rashid akipokea kombe la mshindi wa kwanza wa mashindano ya Airtel Rising Stars kutoka kwa mgeni rasmi ambae ni Meya wa Manispaa ya Morogoro pascal kihanga, Moro Kids imenyakua kombe hilo baada ya kuifunga timu ya Angrikana 1-0.
Mchezaji wa timu ya Moro Kids Ibrahimu Ally mwenye jezi nyeupe wakiwania mpira na mchezaji wa timu ya Angrikana Baraka Omary katika mchezo wa fainali ya Airtel Rising Starkwenye uwanja wa Jamhuri Morogoroo. Moro Kids ilinyakua kombe hilo kwa ushindi wa 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Angrikana Saidi Mohamed akidhibitiwa kikamilifu na beki wa timu ya Moro Kids Ibrahim Yohana katika pambano la fainali ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo moro kids ilinyakua kombe hilo baada ya kushinda 1-0.

Timu ya vijana ya Moro Kids imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kufanya kazi ya ziada na kuishinda timu ngumu ya Angrikana 1-0 katika mchezo wenye upinzani mkali uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana.

Goli hilo la ushindi liliwekwa kimiani na mshambuliaji machachari Nyamawi Juma katika dakika ya 22 baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Angrikana na kuachia shuti kali lililotinga wavuni. Goli liliibua nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.

Angrikana walijibu mapigo kwa kufanya mashambulizi mfululizo ambayo hata hivyo hayakuweza kuzaa matunda. Kipingi cha pili walikianza kwa matumaini ya kupata goli la kusawazisha lakini hadi dakika ya mwisho matokeo yalibaki kuwa 1-0.

Akikabidhi kikombe kwa washindi, Meya wa manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwapongeza Morogoro Kids kwa mafanikio makubwa na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwa kujituma huku wakifuata maelekezo ya walimu wao. “Kwa kufanya hivyo kutawaweka katika nafasi nzuri ya kutimiza ndoto zenu za kufanikiwa katika maisha kupitia soka”, alisema.

Aliwataka viongozi wa soka mkoani Morogoro pamoja na makocha kuhakikisha wanachagua vijana wenye vipaji ili kuuwakilisha vyema mkoa wa Morogoro kwenye fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi to 11.

Wakati wa mechi hizo za mkoa makocha walipata fursa ya kuwatathimini uwezo wa kila mchezaji na kuchagua vijana wenye vipaji kuunda kombaini ya mkoa. Mikoa mingine ambayo tayari imeshaunda vikosi vyake ni kwa fainali hizo ni Ilala, Kinondoni, Temeke and Mwanza.

Fainali hizo za kila mwaka itazikutanisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Washiriki wengine watatoka Mwanza, Morogoro, Mbeya, Lindi, Arusha na Zanzibar.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA: TATIZO LA MAJI SUMBAWANGA KUWA HISTORIA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa inatarajiwa kupata huduma ya maji safi na salama kuanzia mwezi ujao baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji uliokuwa unajengwa.
 

Mradi huo unajengwa kwa usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, Manispaa ya Sumbawanga (SUWASA), kwa ufadhili wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Ujerumani kupitia benki yake ya Maendeleo (KfW), sh. bilioni 31 utakapokamilika.


Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana  (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati na akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga na kuitaka kampuni ya kampuni ya Techno Fab Gammon Joint Venture ya India kumaliza ujenzi wa mradi huo haraka iwezekanavyo.


Alisema mradi huo ambao tayari umekamilika kwa asilimia 85 unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu, hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanashirikiana na Manispaa katika kulinda miundombinu ya mradi huo mara utakapokamilika pamoja na kutunza vyanzo vya maji.


“Pamoja na Serikali kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maji inayojengwa katika maeneo mbalimbali nchini,changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo imekuwa kubwa kutokana na baadhi ya visima vimeanza kukauka hali inayosababishwa na uharibifu wa mazingira,” alisema.


Alisema kumekuwa na uvamizi mkubwa katika maeneo ya vyanzo vya maji ambapo wananchi wanajishughulisha na shughuli za ulimaji, uchungaji wa mifugo, ujenzi wa nyumba za makazi na uchomaji misitu hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira na hatimaye vyanzo hivyo hukauka.


Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wote wa wilaya na wenyeviti wa vijiji nchini kuyasimamia maeneo yenye vyanzo vya maji na kuwaondoa watu wotewalioyavamia kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kuwafikisha mahakamani.


Naye Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye alimuwakilisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge katika hafla hiyo alisema aliishukuru Serikali ya Ujerumani na Umoja wa nchi za Ulaya kwa kufadhili mradi huo.


Hata hivyo Mhandisi Kamwelwe alisema suala la kuhifadhi mazingira ni msingi endelevu wa upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo aliwaomba wananchi kujiepusha na uchafuzi wa vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira ili kuepuka athari ya Taifa kukubwa na janga la ukame.


“Wananchi wanatakiwa kuacha kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kulima, kufuga ndani ya mita 60 kutoka katika mito, maziwa na vyanzo vingine vya maji ili kuepusha uharibifu wa mazingira ambao madhara yake ni makubwa kwa viumbe wote,” alisema.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

ALHAMIS, AGOSTI 25, 2016

VODACOM YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA TAMASHA LA MZIKI MNENE

$
0
0

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati kampuni ya Vodacom Tanzania ilipokabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wengine pichani ni waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (kulia) na Gerald Hando.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akionyesha moja ya T-shirt wakati kampuni ya Vodacom Tanzania ilipokabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaoangalia ni waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (katikati) na Gerald Hando .
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaopokea ni waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (katikati) na Gerald Hando.
Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni ya Channel ten,Said Makala(kulia)akiuliza swali wakati wa Uongozi wa kampuni ya Vodacom Tanzania ilipokuwa ikikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.

Katika juhudi za kuendeleza sekta ya michezo nchini,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imekabidhi jezi za michezo kwa Uongozi wa Tamasha la Mziki Mnene na Vodacom ulioandaa tamasha mahusisi kwa timu mbalimbali zitakazoshiriki katika mpira wa miguu wa maveterani katika tamasha hilo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani wakati wa tamasha hilo lililoandaliwana kituo cha EFM linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi ijayo chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi kwa uongozi huo,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema Vodacom Tanzania inafurahi kudhamini tukio hili muhimu lenye lengo la kutoa burudani kwa jamii kupitia tasnia ya muziki na michezo

“Vodacom tunafurahi kushiriki katika tukio hili la kuleta burudani kwenye jamii na ndio maana kampuni imekuwa mstari wa mbele kudhamini michezo na Sanaa kwa kuwa inaamini kupitia sekta ya michezo watanzania wengi wanaweza kupata burudani wazipendazo na kupumzisha akili pia kupitia tamasha hili wananchi watapata fursa ya kupata na kununua bidhaa mbalimbali za mawasiliano kutoka Vodacom popotelitakalofanyika tamasha hili huduma zetu zitakuwepo na tutaendelea kudhamini matukio ya burudani kwa ajili ya kuinua vipaji vya Sanaa na michezo kama ambavyo kwa sasa tunavyoendelea kudhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara na mashindano ya kucheza muziki wa dansi ya Dance 100% na tuzo za wasanii ya EATV”Alisema.

Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo vya michezo Mratibu wa tamasha hilo,Denis Sebbo amesema kuwa tamasha la muziki mnene mwaka huu, litafanyika kwa kipindi cha muda wa wiki 12 ambapo muziki utapigwa katika baa 12 za Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.

Baadhi ya wasanii ambao watapamba tamasha hilo aliwataka kuwa ni Machupa,Msaga Sumu,Dula Makabila,Easy Man,Khalid Chokoraa,Mc KKoba,Shoz Dear,Peter Msechu,AT,Majid Migoma,Dogo Niga na Rublay.

Alisema tamasha la muziki mnene mwaka huu litaenda sanjari na kampeni ya NJE NDANI ambapo vipindi vinne mbalimbali vya redio hiyo viratushwa live naaliwataka wapenzi wa michezo na burudani kuhudhuria tamasha hili ambalo ni mwisho wa burudani na tayari limeishaanza kuwa gumzo ya jiji

JESHI LA POLISI ZANZIBAR KUPAMBANA NA WANAOTUMIA KAZI ZA WASANII BILA YA LESENI YA HAKIMILIKI

$
0
0

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame akizungumza na wandishi wa habari kuhusu wajibu wa Jeshi la Polisi katika usimamizi wa kazi za wasanii, hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar. Picha na Mkame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Jeshi la Polisi Zanzibar limedhamiria kupambana na uharamia wa kazi za hakimiliki kwa kudhibiti maeneo ya uingizaji hakimiliki haramu katika maeneo ya bandarini na uwanja wa ndege .

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omari amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kuhusu usimamizi na wajibu wa Jeshi la Polisi katika usimamizi wa hakimiliki .

Amewataka wananchi kuelewa kwamba kutoa kopi ,kuuza vinasa sauti na picha za kieletroniki vikiwemo CD,DVD na vyenginevyo bila ya leseni ya hakimiliki ni miongoni mwa makosa ya jinai.

Aidha alisema kutumia hakimiliki biila ya ridhaa ya mwenye haki kama vile kurudufu kusambasa na kuonyesha kazi kwa umma ama kuibadilisha kazi na kuwa kwa mtindo mwengine ni kosa kwa mujibu ya sheria ya hakimiliki No. 14 ya mwaka 2003.

Amesema hakimiliki ni mali ya anaemiliki ,ni kazi yake inaestahili ulinzi kwani kuitumia bila ya ridhaa ya mwenye haki ni kosa kisheria

Katika kusimamia sheria ya hakimiliki Jeshi la Polisi limetoa taaluma kwa askari wake wakiwemo makamanda wa mikoa yote ya Zanzibar katika mwaka 2008 -2009 ofisi ilianzisha kikundi kazi cha hakimiliki .

Alieleza kuwa jumla ya polisi 100 wa Unguja na Pemba walipatiwa mafunzo ya utambuzi wa makosa ya hakimiliki kupitia mtalamu wa utambuzi wa jinai za hakimiliki SP Omar Muwowo kutoka jeshi la polisi Zambia na Interpol.

Kamishna huyo alieleza kuwa Jeshi la Polisi lilifanikiwa kupambana na uharamia wa hakimiliki kwa kushirikiana na Afisi ya hakimiliki kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya Unguja na kukamata nakala haramu za vinasa sauti na picha vya kielektroniki vikiwemo CD , DVD‘S na MP3 zenye uzito wa tani mbili . Aidha alisema nakala haramu hizo ziliangamizwa kwa kushirikiana na Idaraya Mazingira Zanzibar .

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MKOANI RUKWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wafipa wakati walipowasili kwenye kijiji cha Mtowisa mkoani Rukwa kuzungumza na wanachi Agosti 24, 2016.
 Wananchi wa kijiji cha Mtowisa mkoani Rukwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo Agosti 24, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wafipa wakati walipowasili kwenye kijiji cha Mtowisa mkoani Rukwa kuzungumza na wanachi Agosti 24, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa Kijiji cha Mtowisa  baada ya kuwasili kijijini hapo wakiwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa Agosti 24, 2016

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images