Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 943 | 944 | (Page 945) | 946 | 947 | .... | 1898 | newer

  0 0


  mwalimu wa Ufundi Ricky akionyesha baadhi ya mashine zinazotumika kufundishia wanafuinzi wanaojiunga na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Kipawa.

  Picha ya pamoja kayi ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiwa na watendaji wa Chuo cha VETA Kipawa pamoja na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo
  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya mikakati ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda ambapo chuo cha VETA Kipawa inajikita zaidi kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya viwanda.

  mmoja wa wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Mlimani waliokwenda chuoni hapo kupata mafunzo kwa vitendo juu ya masuala ya TEHAMA .picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO.


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  WAZIRI wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Mamlaka ya Elimu Ufundi, Stadi (VETA) kuhakikisha vyuo vyote vya VETA vinakuwa na ubora sawa katika kuwafanya vijana kuajirika au kujiajiri wenyewe.

  Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Chuo cha Ufundi Stadi cha Kipawa, amesema kuwa hata VETA ndio wasimamizi wa vyuo vya ufundi kuhakikisha wanazalisha vijana wenye uwezo sawa na sio kutofautiana na kufanya wananchi kuhangaika katika vyuo,Amesema vijana wakipata mafunzo yenye ubora kutafanya vijana kuacha kuhangaika na vyeti kwa ajili ya kutafuta kazi hiyo inatokana na kuwa na uwezo binafsi wa kujiajiri au kuunda kampuni na kuweza kuajiri wengine.

  Amesema kuwa kuna sehemu ya vyuo ametembelea na kukuta kuna changamoto ambazo kama menejimenti ya VETA kuhakikisha wanafanyia kazi changamoto hizo ikiwemo kuwa na mitambo ya zamani hali ambayo inafanya vijana kushindwa kupata kile ambacho kinahitajika katika kuelekea uchumi wa viwanda.

  Profesa Ndalichako amesema mafunzo ya VETA yawe ya kisasa na maeneo mengi ambayo inamilki haitumiki na kutaka kubadili mtazamo wa uendeshaji katika kuendana na adhima ya serikali.
  aidha ameitaka VETA kufanya tathimini ndani ya mwezi mmoja na wapeleke ripoti hiyo juu ya uendeshaji ikiwemo changamoto zinazowakabili .

  Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA , Geoffrey Sabuni amesema chuo cha Kipawa ni maalumu kwa ajili ya ICT na kufanya vijana wanaozalishwa kuwa na utalaamu ambao unafanya waweze kujiajiri au kuajiriwa na wakitoka katika chuo hicho huwawarudi.

  Amesema kuwa wamejipanga katika utoaji wa mafunzo katika kuweza vijana kuingia katika uchumi wa viwanda wakiwa ndio wataalamu wenye uwezo wa kutosha katika sekta hiyo.

  0 0


  Waziri wa Katiba na sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano wa kupokea ripoti ya ukaguzi kutoka kwa Taasisi zote zinazofanya usajili wa asasi za kiraia leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju
  Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea ripoti ukaguzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Rita,Emmy Karomba akifafanua jambo kulia ni Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  0 0

  Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy akifafanua kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara kuhusu umuhimu wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bw. Hassan Abbasi na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa.
   Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bw. Hassan Abbasi akifungua Mafunzo kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mambo ya kuzingatia katika Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo ili kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma. Katikati ni  Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa.
  Mchambuzi Sera Kutoka Tume ya Mipango Bi. Lilian Wawa akiwasilisha mada kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara kuhusu Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, leo Jijini Dar es Salaam

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akiongea na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara (hawapo pichani) wakati wa Mafunzo kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni  Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy na Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bw. Hassan Abbasi.
  Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara wakifuatilia mafunzo kuhusu Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo yaliyotolewa kwao na Tume ya Mipango, Leo Jijini Dar es Salaam
  PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

  0 0


  Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo. Shindano hilo limezinduliwa sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya Miss Ilala tangu ianze mwaka 1996.
  Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo.
  Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo. Source: Father Kidevu Blog.
  Mwandaaji wa shindano la Miss Ilala 2016, Teddy Kitundu ambaye pia ni diwani wa viti Maalum Ilala, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa shindano hilo Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia kulia ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania , Bossco Majaliwa (kulia) na Mkuu wa Itifaki wa Kamati hiyo, Albert Makoye. Miss Ilala inafanyika ikiwa ni mwaka wa 20 tangu lianze shindano hilo mwaka 1996.
  Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akizungumza kwaniaba ya Kamati katika uzinduzi huo.
  Mmoja wa wadhamini akizungumza katika uzinduzi huo.
  Mratibu wa shindano hilo la Miss Ilala 2016, Eric akizungumza
  Warembo waliowahi kushirikishindano la Miss Ilala wakifungua shampein katika uzinduzi huo.
  Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa akigonganisha glasi na warembo wanaowania taji la Miss Ilala 2016.

  Warembo wakigonganisha glasi na wadau wa urembo waliohudhuria hafla hiyo.

  Warembo wakigonganisha glasi na wadau wa urembo waliohudhuria hafla hiyo.
  Mdau akilamba unikoni na mlimbwende wa zamani wa Miss Tanzania
  Warembo wakijiselfisha wakati wa hafla hiyo

  Wadau wa urembo wakiwa katika hafla hiyo.
  Mwandishi wa habari za michezo na sanaa ya urembo, Michael Mauruce (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo akionyesha moja ya nyaraka zilizokiukwa na Kampuni ya Usambazaji wa Filamu nchini ya Pamoja Film Company wakati wa kikao baina ya Bodi ya Filamu Tanzania na kampuni hiyo ya usambazaji wa filamu. Bi Fisoo amewaasa wadau wa filamu kufuata sheria na kanuni zinazoongoza sekta ya filamu nchini.


  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Bodi ya Filamu Tanzania imetoa siku saba kwa Kampuni ya Usambazaji wa Filamu ijulikanayo kama ‘Pamoja Film Company’ kuwasilisha nyaraka za filamu zake ili kukagua na kuhakikisha kama wamefuata sheria na kanuni zinazosimamiwa na bodi hiyo.

  Hatua hiyo imefikiwa baada ya kampuni hiyo kubainika kukiuka baadhi ya sheria na kanuni za usambazaji zikiwemo za kutowasilisha miswada ya filamu (script) kabla ya kuanza kurekodi, kuzitangaza kazi hizo kwenye mitandao ya kijamii bila ya kuzifikisha Bodi ya Filamu Tanzania Kwa ajili ya ukaguzi pamoja na kufanya kazi za utengenezaji na usambazaji wa filamu bila kibali.

  Agizo hilo limetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alipokuwa akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Lufingo Exaud kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa kukiuka sheria na kanuni zinazosimamiwa na bodi ni kosa kisheria.

  “Natoa siku saba kwa Kampuni hii kuwasilisha miswada ya filamu zake 12 alizozitangaza na kuzisambaza kinyume cha sheria pamoja na kuleta maelezo kwa maandishi ya kujieleza sababu zilizowapelekea kufanya kazi hizo bila kibali kutoka bodi”,alisema Fissoo.

  Filamu hizo zilizotolewa na Kampuni hiyo bila kufuata sheria na kanuni ni; Spompompo, Tanga Raha, Buku 10, Jirani Hafugiki, Mke Sahihi, Chanzo, Ahsante, Je Alaumiwe, Mwaka wa Tisa, Nyaraka na Kanya Boya.

  Fisoo ameongeza kuwa Bodi imefanya jitihada kubwa kutoa elimu kwa umma kupitia njia za vipeperushi, kuandaa na kushiriki mikutano na makongamano ya kitaifa na kimataifa, kushiriki maonesho na maadhimisho ya kisekta na kitaifa ikiwa na lengo la kuwaelemisha wadau wa filamu kuhusu sheria, kanuni na miongozo inayosimamia sekta hiyo nchini.

  Aidha, amewaonya wadau wote wa filamu kuacha kukiuka sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa kisheria, “tunawaonya wadau wote kuacha mara moja tabia hii” alimalizia.

  Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lufingo Exaud amekiri makosa yake na ameahidi kulipa faini za makosa yote, pia ameomba msamaha mbele ya Bodi hiyo na kuapa kuwa hatorudia tena. Kwa kumalizia ameahidi kuwa balozi mzuri wa Bodi ya Filamu Tanzania na yupo tayari kuwapa elimu wadau wengine wa filamu nchini ili waweze kufuata sheria na kanuni zinazoongoza sekta hiyo.

  Mbali na kuahidi kushirikiana na bodi hiyo, Lufingo ameusifia utaratibu wa bodi wa kurahisisha upatikanaji wa vibali kwani kwa sasa baada ya kuwasilisha muswada wa filamu kwa ajili ya ukaguzi utapatiwa kibali ndani ya muda wa siku saba za kazi.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha Sh 2,000 kwa mzunguko na Sh 5,000 kwa jukwaa kuu wakati timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 itakapocheza na Amajimbos ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Madagascar, mwakani.

  Mchezo huo utaoanza saa 9.00 alasiri Jumapili Agosti 21, 2016 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi – Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam utachezeshwa na Mwamuzi Noiret Jim Bacari wa Comoro akisaidiwa na Mmadi Faissoil na Said Omar Chebli wakati mezani atakuwa Ali Mohamed Adelaid huku Kamishna wa mchezo huo atatoka Somalia ambaye anaitwa Amir Abdi Hassan.

  Jumamosi Agosti 6, 2016, Serengeti ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini – Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Kusini ndio walioanza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na Luke Gareth kabla ya Ally Msengi kuisawazishia Serengeti Boys katika dakika ya 70.

  Penalti ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi Linamandla Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos kunawa mpira eneo la hatari. Mwamuzi wa mchezo huo alikuwa, William Koto kutoka Lesotho.

  Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi amesema: “Watanzania wakaribie Chamazi, waje kutushangilia ili tushangilie ushindi kwa pamoja kikosi change kiko vema na ninamshukuru Mungu kwa hilo, akili yangu na akili za wachezaji wangu ni kumuondoa Msauzi (Afrika Kusini).”

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya pili Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi kutoka Shirika la CDF, Kashuma Mtengeti, Mwakilishi wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane Miller na Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  Mwakilishi wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane Miller, akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Wazir Ummy Mwalimu (kulia)
  Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu (kulia), akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa taarifa ya mradi huo.
  Wadau mbalimbali na waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Mwakilishi kutoka Shirika la MBE FORWARD UK-Naana Otoo Oyortey akitoa mada kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi huo.
  Mwakilishi kutoka Shirika la CDF, Kambibi Kamugisha, akitoa mada.
  Waziri Ummy Mwalimu akihutubia kabla ya kuzindua rasmi mradi huo.

  Mwakilishi kutoka Wadada Centre, Christian Noah akitoa mada kwenye uzinduzi huo
  Mkurugenzi kutoka Shirika la CDF, Kashuma Mtengeti, akichangia jambo.
  Waandishi wa habari wakiwa kazini.
  DK. Flora Myamba kutoka Repoa akitoa mada kwenye uzinduzi huo.
  Christine Mwanukuzi kutoka shirika la UNFPA, akichangia jambo.  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI imesema hata magereza zikijaa itaendelea kuwakamata na kuwachukulia sheria kali wanaume wote wataka0 bainika kuwaoa au kuwapa mimba wanafunzi.

  Hayo yalisema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akizindua mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya pili Dar es Salaam leo.

  Mwalimu alisema kuwa hata magereza yakijaa kwa kiasi gani serikali haitasita kuwakamata watuhumiwa hao bila ya kuwaonea huruma bila ya kujali mtuhumiwa ni mtu wa namna gani.

  "Nawaagiza maofisa Ustawi wa Jamii wote katika ngazi ya mikoa, wilaya na Kata kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa nchini kote hususan mtoto wa kike. Ninataka wahakikishe wale wote wanao wapa watoto wa shule mimba na wanao waozesha au kuoza wanakamatwa na kuchukuliwa hatua haraka kwani sheria za kuwalinda watoto zipo, kinachotakiwa sasa ni utekelezaji" alisema Mwalimu.

  Waziri Mwalimu alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha ndoa za utotoni ambapo taarifa ya Demografia na Afya ya mwaka 2010 zimeonesha kuwa kwa wastani wanawake 2 kati ya watano Tanzania wa umri wa miaka 15-49 waliolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

  Aliongeza kuwa utafiti wa hali ya afya ya uzazi, mtoto na malaria wa mwaka 2015/16 unaonesha kuwa idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19 imeongezeka kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010 na kuwa tatizo hilo lipo zaidi katika mikoa ya Katavi kwa asilimia 36.8, Tabora, asilimia 36.5, Simiyu asilimia 32.1, Geita asilimia 31.6 na Shinyanga kwa asilimia 31.2.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu alisema katika kudumisha harakati za kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni vinavyoendelea kuwakumba wasichana nchini Tanzania, CDF, Chama cha Uzazi na Malezi (Umati) na Kituo cha Wadada Centre wameamua kuzindua mradi huo kwa pamoja ili kulinda haki za wasichana hapa nchini.

  0 0


  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Dkt. Akwilina Kayumba akiongea na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) kuhusu utaendesha wa zoezi maalum la upimaji afya za waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu ambao waliachishwa kazi na mgodi huo mnamo mwaka 2007 bila kupimwa afya zao kinyume na Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

  Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) utaendesha zoezi maalum la upimaji afya za waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu ambao waliachishwa kazi na mgodi huo mnamo mwaka 2007 bila kupimwa afya zao kinyume na Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.Baada ya ukikwaji huo wa sheria kuripotiwa kwa Wakala, hatua stahiki zilichukuliwa ikiwemo kufanya kaguzi maalum za usalama na afya katika eneo la mgodi na kutoa onyo kali kwa mwajiri wa walalamikaji pamoja na kugharimia upimaji afya za waathirika wote.

  Katika kushughulikia tatizo hilo, vikao vya mashauriano vilivyojumuisha serikali, mwajiri (Mgodi wa Bulyanhulu) na waathirika kupitia chama chao, TAMICO, vilifanyika na utaratibu wa kushughulikia suala hilo ukawekwa. Katika utaratibu huo, TAMICO ilipewa jukumu la kuwatafuta waathirika wote popote walipo na kuwasilisha majina yao kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi. Wakala ulikuwa na jukumu la kuyapeleka majina hayo kwa mwajiri kwaajili ya uhakiki na kuratibu upimaji afya wa waathirika hao baada ya majina yao kuhakikiwa.
   
  Hadi kufikia sasa tayari waathirika 315 kati ya 371 ambao mwajiri alithibitisha kwamba walikuwa wafanyakazi wake wameshapimwa afya zao. Waathirika 56 waliobaki hawakujitokeza wakati wa upimaji afya licha ya kupewa taarifa juu ya zoezi hilo.Waathirika watakaopimwa kwasasa ni wale ambao vipimo vyao vya awali vilionesha kwamba wanahitaji vipimo zaidi kutoka kwa madaktari bingwa.

  Maandalizi ya upimaji huu yamekamilika na zoezi hili litafanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili siku ya Jumamosi tarehe 20/08/2016 na katika hospitali ya rufaa ya Bugando mnamo tarehe 22/08-15/09/2016. Katika zoezi hili waathirika ambao orodha ya majina yao imeambatanishwa katika taarifa hii wataonana na madaktari bingwa wa magonjwa ambayo wana dalili nayo ili kubaini kama wana matatizo kiafya na hatimaye kuweza kutazama kama matatizo waliyo nayo yametokana na kazi walizokuwa wakifanya mgodini.

  Kwa waathirika ambao madaktari watathibitisha kwamba matatizo yao ya kiafya yamesababishwa na kazi walizokuwa wanafanya, Wakala utashauri namna ambavyo wanapaswa kufidiwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Waathirika ambao watakutwa na matatizo ya kiafya ambayo hayatokani na kazi, watashauriwa kuendelea na matibabu katika hospitali zilizopo karibu nao.

  Aidha kwa waathirika ambao hawatakutwa na matatizo yoyote ya kiafya watapatiwa vyeti vyao (certificate of fitness) ambavyo hutolewa kwa wafanyakazi wanaopimwa afya zao baada ya kukoma kwa ajira zao kwa mujibu wa kifungu Na.24 (2) cha Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

  Ikumbukwe kwamba, upimaji huu ni mwendelezo wa hatua mbali mbali zinazochukuliwa na serikali katika kushughulikia tatizo hili ambalo lilitokea mwaka 2007 ambapo waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu waliachishwa kazi na mwajiri wao baada ya kugoma kufanya kazi. Hata hivyo mwajiri wao (Mgodi wa Bulyanhulu) haukuweza kuwapima afya zao kama Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 inavyomtaka.Mwisho, kwakuwa suala hili ni la kisheria na serikali ina nia ya dhati ya kulishughulikia, tunaomba ushirikiano kutoka pande zote (waathirika na mwajiri) ili kuhakikisha kwamba zoezi hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.


  Imetolewa na;

  Dkt. Akwilina Kayumba

  Mtendaji Mkuu

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.


   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa  na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo wa kwanza (kushoto).
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0

    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Agosti, 2016 amemuapisha Bw. Mrisho Mashaka Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Mashaka Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

  Bwana Mrisho Mashaka Gambo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Daudi Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

  Katika Hatua nyingine, Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wataalamu huru lililoundwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kuangalia mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wadau wa Maendeleo Dkt. Donald Kaberuka, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amemshukuru Dkt. Kaberuka kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa kipindi chake cha uongozi wa Benki ya AfDB ambapo Tanzania ilipata ushirikiano mzuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa barabara.

  Dkt. Magufuli amesema anaamini kuwa Dkt. Kaberuka ataendelea kutoa ushauri mzuri kwa Tanzania katika juhudi zake za maendeleo ikiwemo ushauri utakaotolewa katika ripoti ya jopo analiloongoza kuhusu mahusiano ya Tanzania na wadau wa maendeleo.

  "Tanzania itaendelea kushirikiana na wewe na tunaamini kuwa unayo nafasi ya kutushauri katika mipango yetu mbalimbali ya maendeleo, kama vile namna tunavyoweza kunufaika na rasilimali nyingi tulizonazo yakiwemo madini mbalimbali, gesi asilia, ardhi kubwa, mifugo mingi hususani ng'ombe, bandari, maziwa na bahari na mbuga za wanyama" Amesisitiza Rais Magufuli.

  Kwa upande wake Dkt. Donald Kaberuka pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano amesema hatua zilizoanza kuchukuliwa na serikali yake katika kuimarisha ukusanyaji wa kodi, kukabiliana na rushwa na mipango ya kutumia rasilimali zilizopo ipasavyo zinaonesha Tanzania inaelekea kupiga hatua nzuri za kimaendeleo.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  19 Agosti, 2016


  0 0

   Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vilivyo karibu na marehemu, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali akakata roho. 


  Taarifa kamili tutawaletea mara tu tutapozipata.

  MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA


  0 0

  Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,2016, kulikuwa na mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa taji la MISS MWANZA 2016 ambapo warembo 16 kutoka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza walijitosa kusaka taji hilo.

  Ilikuwa ni furaha kubwa kwa mrembo, Mary Peter (katikati), pale alipotangazwa kuwa MISS MWANZA 2016. Pia mwendelezo wa furaha uliwaendea warembo, Victoria Boniphace (kushoto) aliyetangazwa Miss Mwanza nambari mbili na Winnie Shayo (kulia), aliyetangazwa Miss Mwanza nambari tatu.

  Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza 2016, kiliandaliwa na Kampuni ya "Big D Entertainment" na baada ya kinyang'anyiro hicho, unafuata mtifuano wa MISS LAKE ZONE 2016 utakaofanyika Septemba 10,2016 ambapo washiriki wa Miss Mwanza 2016 waliongia nafasi tano bora, wanashiriki moja kwa moja kwenye shindano hilo.
  Na BMG
  Miss Mwanza 2015, Donny Roberty (kushoto), akimkabidhi taji Miss Mwanza 2016, Mary Peter (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.
  Washiriki wa Miss Mwanza, walioingia nafasi tano bora
  Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
  Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016.
  Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
  Majaji walikuwa na Kazi pevu kuchagua mshindi
  Baadhi ya waliohudhuria kwenye tukio
  Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza akidondosha burudani kwenye Miss Mwanza 2016
  Burudani za kiafrika pia zilikuwepo
  Mkali wa Moyo Mashine, Ben Pol, alidondosha burudani poa sana
  Ben Pol kazini
  Kupitia BMG, Ben Pol, aliwashukuru wakazi wa Jiji la Mwanza kwa namna wanavyopenda kazi zake na kuahidi kufanya kazi nzuri zaidi.
  Miss Mwanza 2016 aliiambia BMG kwamba, maandalizi yake mazuri ndiyo yaliyompa fursa ya kunyakua taji hilo na kwamba amejiandaa vyema kwa ajili ya taji la Miss Lake Zone 2016 na pia Miss Tanzania 2016.
  Miss Mwanza 2016 nambari mbili akibonga na BMG. Anasema shauku yake ni kuongeza juhudi zaidi ili kunyakua taji la Miss Lake Zone 2016.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde  Warioba wakati   alipomtembelea nyumbani kwake, Oysterbay jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

   
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili  kulia) wakizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) na kewe Fatma Mganga Ndugai wakati wakati walipokwenda  nyumbani kwa Spika Salasala jijini Dar es salaam  Agosti 19, 2016  kumjulia hali.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakiagana na Spika wa Bunge Job Ndugai  (kulia) na mkewe Fatma Mganga Ndugai (wapili kushoto) wakati walipokwenda nyumbani kwa Spika, Salasala jijini   Dar es salaam Agosti 19, 2016 kumjulia hali.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakiagana na Spika wa Bunge Job Ndugai  (kulia) na mkewe Fatma Mganga Ndugai (wapili kushoto) wakati walipokwenda nyumbani kwa Spika, Salasala jijini   Dar es salaam Agosti 19, 2016 kumjulia hali.

  0 0


  Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wa wakiwa moja ya maozezi yao ya kupasha viungo kabla ya kuanza mazoezi ya kutuliza ghasia.
  Askari Polisi wa kikosi maalum cha polisi (CRT) wa mkoa wa Iringa wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza katika maeneo mbalimbali.
  Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa mikoa mbalimbali wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali.
  Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kutuliza ghasia na kukabiliana na matukio yoyote ya uhalifu na wahalifu.
  Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Lindi wakifanya mazoezi magumu ya kijiweka tayari kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza ikiwemo watu wasiotii amri za Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria za nchi.
  Askari Polisi wa vikosi vya kutuliza ghasia wa wa mikoa ya Lindi, Iringa, kanda maalumu ya Dar es salaam na mikoa mengine wakipokea maelekezo mbalimbali wakati wa mazoezi ya tayari katika kukabiliana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu (Picha zote na makao makuu ya Jeshi la Polisi.)

  0 0


  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Dar es Salaam

  Serikali imezimia kuachana na biashara ya kuingiza nguo za mitumba kutoka nje ya nchi ifikapo mwaka 2018.

  Maazimio hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika uzinduzi wa mafunzo ya uanagenzi ya ushonaji nguo katika kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Company, Ltd.

  Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kwamba ifikapo mwaka 2018 soko la Afrika Mashariki halitaingiza nguo za mitumba kutoka nje.

  Ameongeza kuwa kwa kutekeleza azimio hilo Serikali imeandaa  mafunzo ya kuhakikisha vijana wengi wanapata stadi za kushona nguo nchini ili kuwawezesha kufanya kazi katika viwanda vilivyopo na vitakavyojengwa kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu wenyewe na kuacha kutegemea bidhaa kutoka nje.

  “Tumejipanga kutekeleza azimio hili na kwa kushirikiana na kiwanda hiki tunategemea kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo, kukata, kushona na kumalizia nguo” alisema Mhe. Jenista.

  Aidha Waziri huyo amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwani mafunzo hayo yatawasaidia kuendana na viwango vya soko la kimataifa na mahitaji ya soko la nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika kubuni mitindo, kukata na kushona nguo zenye ubora wa kimataifa.

  “Imani yangu kuwa wataalamu waliopo katika kiwanda hiki watawapa ujuzi wa kutosha na wengine wataweza kupata ajira katika kiwanda hiki tumieni fursa hii mliyoipata ni ya pekee kwani mmebahatika kuwa miongoni mwa wanafunzi wa kwanza kupata mafunzo chini ya Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini.

  Mhe Jenista amesisitiza kuwa mafunzo hayo yatawezesha vijana kupata ajira katika Viwanda, kujiajiri na hata kutoa ajira kwa wengine hivyo vijana watumie fursa hiyo kutengeneza mtaji na kujiunga katika vikundi vitakavyowawezesha  kufungua viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza nguo na kuendelea kukuza ujuzi waliopata.

  Pia Waziri Jenista ametoa wito kwa viwanda vingine kushirikiana na Serikali kukuza ujuzi kwa vijana kupitia mafunzo ya uanagenzi na kuwahakikisha kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha Vijana kupata mafunzo ya aina hiyo.

  “Napenda niwahakikishie kuwa Serikali iko bega kwa bega nanyi, fungueni viwanda vingi sehemu mbalimbali katika nchi yetu, sisi kama Serikali tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha rasilimali watu ya kuendesha viwanda hivi inapatikana”

  Mbali na hayo Serikali inayo mipango na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na kuwa na uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

  Serikali iliingia makubaliano na kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Co. Ltd kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo, kukata, kushona na kumalizia nguo jumla ya vijana 1,089 waliomba nafasi ya kupata mafunzo hayo yatakayoendeshwa kwa awamu tatu na kwa sasa jumla ya vijana 430 wanapata mafunzo hayo.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomjulia hali jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomjulia halijijini Dar es salaam Agosti 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), linawaomba radhi wateja wake wa Mkoa wa Temeke, kufuatia katizo la umeme usiku wa kuamkia leo Agosti 20, 2016.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu, sababu za kukatika kwa umeme ni hitilafu iliyotokea kwenye njia ya umeme unaotoka Ilala kwenda Kurasini, natayari mafundi wa TANESCO kutoka mkoa wa Temeke wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo.

  Maeneo yaliyoathirika na katizo hilo ni pamoja na Mbagala yote, Kurasini yote, Mtoni yote, na baadhi ya maeneo ya Temeke.Taarifa hiyo imesema, baada yahitilafu hiyo mara moja mafundi wa TAENESCO waliingia kazini usiku huo huo na hadi kufikia majira ya asubuhi, baadhi ya maeneo kama vile Temeke, na Kurasini umeme ulirejea.

  Taarifa hiyo inasema, umeme utarejea katika hali yake ya kawaida kwenye maeneo yote muda mfupi ujao na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.Taarifa hiyo imewataka wananchi kutoshika au kukanyaga waya wa umeme uliokatika au kuanguka na pindi uonapo hali hiyo kwenye eneo lako, tafadhali wasiliana na TANESCO kupitia namba zifuatazo, :Kituo cha miito ya simu namba 2194400 au 0768-985100.

  Shirika linawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu uliojitokeza.

  0 0

  Hujafa hujaumbika! Erasto Mketo (26) ni mkazi wa Lindi kijiji cha Mtondo Kimwaga, ni mlemavu wa miguu na mikono ambaye ana ndoto nyingi za kujikwamua kimaisha kama kijana mwingine wa Kitanzania, lakini ulemavu wake umekuwa changamoto kubwa ya yeye kuweza kufanikisha ndoto zake.

  Moja ya changamoto zinazomkuta Erasto ni pamoja na unyanyapaa hasa kwenye sekta ya ajira jambo lililomfanya apaze sauti na kuwaomba Watanzania wajitokeze kumsaidia hata kwa kumpa mtaji au ajira ili aweze kujikwamua kimaisha.

  Akiongea na mwandishi wa Blogs za Mikoa Tanzania, Erasto alisema anaamini anaweza kufanya biashara yoyote kama muajiriwa au kama atapewa mtaji wa kufungua biashara yake mwenyewe.

  “Kwa huku kijijini nimekuwa nikipata tabu sana ya kupata ajira ambayo itaendana na ulemavu wangu na elimu yangu ya shule ya msingi, lakini ningependa sana nitimize ndoto zangu kwa sababu naweza sana kufanya biashara.

  “Nawaomba watanzania wenzangu mnisaidie hata kwa kuniajiri ili mradi na mimi nijikwamue kiuchumi kama wenzangu na hata niweze kuwasaidia wazazi wangu,” alisema Erasto huku akiongeza kuwa baiskeli ya kutembelea atainunua mwenyewe kupitia ajira yake ikiwa atapata mtu wa kumuajiri.

  Kutoa ni moyo si utajiri, kama umeguswa tafadhali msaidie Mtanzania mwenzako kwa hali na mali kupitia namba 0682755874, imesajiliwa kwa jina la Anastansi Ngomba.

                                                

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii wa muziki wa taarab Bi. Shakila Said kilichotokea ghafla nyumbani kwao Mbagala jijini Dar es Salaam jana Ijumaa ya tarehe 19/08/2016.

  Shakila ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa taarab nchini hasa katika kubuni kazi za Sanaa za muziki mbalimbali ambazo zilikuja kupata umaarufu mkubwa. Moja ya kazi alizobuni na kupata umaarufu mkubwa ni pamoja na 'Macho yanacheka' na 'kifo cha mahaba'.

  Mchango wake katika muziki wa taarab hasa katika kubuni na kutunga nyimbo zenye ubora, ujumbe na maadili kwa jamii hautasahaulika kamwe. Ni mwanamuziki aliyeacha misingi katika sekta ya muziki na alijitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa taarab mahali ulipo leo.

  Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Shakila hasa katika kupenda kujitolea muda mwingi katika kukuza muziki wa taarab na sekta ya muziki kwa ujumla.

  Baraza linatoa pole kwa ndugu wa marehemu, shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote wa Sanaa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

older | 1 | .... | 943 | 944 | (Page 945) | 946 | 947 | .... | 1898 | newer