Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

Benki ya Diamond Trust Bank Yakabidhi Msaada wa Viti kwa Kituo cha Aga Khan Madrasa

$
0
0



Mkuu wa Kitengo cha Fedha Benki ya DTB Tawi la Zanzibar Ndg Shahr Mohammed kushoko akimkabidhi msaada wa Vitu kwa ajili ya Madrasa hiyo inayotowa Elimu ya Mafunzo kwa Walimu wa Skuli za Maandalizi Zanzibar, akipokea msaada huo wa Vitu 40 kwa ajili ya Taasisi hiyo ya Programu ya Makuzi na Maendeleo ya Watoto Madrasa Ndg Khamis Said Abdallah hafla hiyo imefanyika katika Kityuo hicho kiponda Zanzibar wakishuhudia Wafanyakazi wa DTB na Kituo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Benki ya DTB Ndg Shahr Mohammed akikabidhi msaada wa Vitu vilivyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya matumizi ya Kituo hicho akipokea msaada huo Mkurugenzi wa Programu ya Makuzi na Maendeleo ya Watoto na Madrasa Ndg Khamis Said Abdalla.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Benki ya DTB Tawi la Zanzibar Ndg Shahr Mohammed, akizungumza na wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi viti hivyo 40 kwa ajili ya Kituo hicho ni moja ya misaada yao kwa jamii kutumia faida wanayoipata kusaidi miradi ya Jamii.Hafla hiyo imefanyika katika Kituo chaMadrasa Kiponda Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Programu ya Makuzi na Maendeleo ya Watoto na Madrasa Ndg. Khamis Said Abdallah akitowa shukrani kwa Benki ya DTB kwa msaada wao huo wameotowa wakati muafaka wakati kituo hicho kina upungufu wa thamanin kwa walimu wanaopata mafunzo katika kituo hicho.

Airtel FURSA, VETA YAWAFANIKISHA VIJANA ELFU 18 KUSOMA UFUNDI STADI KWA SIMU

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na VETA imeingia mkoani Arusha kuendelea kutoa uelewa kwa vijana kukamata FURSA na kusomo kozi mbalimbali toka VETA kupitia mfumo wao wa simu ujulikanao kama VSOMO. hadi sasa zaidi ya vijana elfu kumi na nane nchini wamejisajili kusoma kwa mfumo huo wa simu za mkononi huku mikakati yao ikiwa ni kuongeza kozi 10 zaidi ili wanafunzi kuendelea kujisomea.

Hayo yamebainishwa na  Mkuu wa mauzo kanda ya kaskazini  Bw, Brighton Majwala wakati alipoongea na wajasiliamali na madereva bodaboda  waliokusanyika stand kuu  Arusha jana,   

“Airtel na Mamlaka ya ufundi stadi VETA lengo letu ni kuwafikishia elimu ya ufundi vijana wengi nchini, upande wetu Airtel tunahakiksha mtandao upo vyema ili vijana waweze kusoma bila kukwama, hadi leo hii tayari vijana zaidi ya milioni 18 wameshakamata FURSA hii kwa kupakua aplikesheni au mfumo huu wa VSOMO katika simu zao” alieleza Bw Majwala

Majwala aliendelea kusema kuwa “mpango wetu Airtel na VETA ni  kuongeza uelewa kwa  vijana ili wasome kozi zilizopo sasa ikiwemo ya  ufundi piki piki, umeme wa nyumbani, ufundu simu, ufundi wa aluminium, utaalam wa masuala ya urembo, pamoja na ufundi wa kuchomea vyuma”.

kwa upande wake Meneja  Uhusiano wa Airtel alisema “kutokana na VSOMO kuwa na idadi kubwa ya vijana waliojisajili  tayari Airtel kwa kushirikiana na wadau wetu VETA tuko katika utekelezaji wa kuongeza kozi zingine zaidi ya kumi ili kuongeza wigo wa kuchagua pamoja na kuongeza  idadi ya wanaosoma na kuhitimu”. alieleza mmbando

“tunampango wa kuongeza kozi zingine 10 kabla ya mwezi wa 12 ambapo sasa hivi tayari VETA wako katika utaratibu wa kuzifanyia kazi kozi hizo ili ziweze kuingia katika mtandao” alisema Mmbando

 “Mradi wa VSOMO ni sehemu ya mpango wa Airtel FURSA wenye lengo la kuwawezesha vijana pamoja na kutimiza kauli mbiu ya  “Airtel the smartphone network” kwa kujipatia elimu ya ufundi stadi toka VETA kwa smartphone zao” alisisitiza Mmbando

Airtel kwa kushirikiana na  VETA nchini ilizindua mfumo wa masomo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao VSOMO mwezi Julai 2016 ambapo mpaka sasa  tayari mfumo huu umetambulishwa  katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Morogoro na Mwanza lakini kutokana na uhitaji mkubwa kwa  vijana tayari mfumo huo umepokea maombi ya vijana toka mikoa 25  kwa kupakua mfumo/aplikesheni hiyo hiyo na kuomba kusoma kwa njia ya simu za Airtel.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (katikati) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airte jana.
Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala na wafanyakazi wengine wa Airtel kwa pamoja wakizungumza na baadhi ya wajasiliamali na watoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel jana.
Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala akitoa maelekezo kwa baadhi ya wajasiliamali wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel mkoani jana.

WAZIRI ANGELLAH KAIRUKI AFUNGUA MKUTANO WA KAZI WA MFUKO WA TASAF MKOANI ARUSHA.

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Angellah Kairuki akiwaongoza Wakuu wa mikoa kutoka kushoto,Mhandisi Mathew Mtigumwe(Singida),Dk Joel Bendera(Manyara),Said Meck Sadick(Kilimanjaro)na Martine Shighela(Tanga).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Angellah Kairuki akifungua mkutano wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(Tafas)walioketi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo,Ladislaus  Mwamanga na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadick.

Wakuu wa wilaya kutoka mikoa mitano ya Singida ,Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga wakiwa kwenye mkutano wa Kazi wa kupata uelewa zaidi wa mfuko wa Tasaf.

Wakuu wa mikoa Mhandisi Mathew Mtigumwe wa Singida,Dk Joel Bendera wa Manyara(katikati) na Martine Shighela wa Tanga.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Tasaf ,Ladislaus  Mwamanga akizungumza katika mkutano huo.

Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha akizungumza jambo katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga,Godwini Gondwe  akizungumza  katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba  akizungumza  katika mkutano huo.

WATOTO PACHA WAFANYIWA UPASUAJI KATIKA NJIA MKONO.

$
0
0
 Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH, Dk Victor Ngotta (kushoto) akimfanyia upasuaji Eliudi leo kwa kushirikiana na Profesa Saber Waheeb (katikati) na Dk Mohamed Malak kutoka Misri (kulia).
  Daktari Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary akizungumza jambo baada ya kumfanyia upasuaji mtoto Elikana aliyekuwa na tatizo la mfumo wa njia ya mkojo Leo.
 Dk Bingwa wa Upasuaji, Dk Yona Ringo akiwa ofisini baada ya kumfanyia upasuaji mtoto Elikana ambaye alikuwa na tatizo la mfumo wa njia ya mkojo Leo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Na John Stephen
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Leo imefanikisha kuwafanyia upasuaji watoto pacha ambao walikuwa wana tatizo katika njia mkojo.

Watoto hao wametoka katika chumba cha upasuaji salama na sasa wanaendelea vizuri baada ya kurejeshwa wodini. Watoto hao ni Eliudi Joel na Elikana Joel ambao wana umri wa miaka mitatu kila mmoja.

Daktari Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary na Dk Bingwa wa Upasuaji, Dk Yona Ringo wamefanikisha upasuaji wa Elikana wakati Eliudi amefanyiwa upasuaji na Profesa Saber Waheeb na Dk Mohamed Malak kutoka Misri kwa kushirikiana na Dk Victor Ngotta na Dk Mwajabu Mbaga wa Muhimbili.

Dk Bokhary amesema kuwa upasuaji wa watoto hao umechukua saa moja na nusu na kwamba hivi sasa wanaendelea vizuri baada ya shughuli hiyo.

“Watoto hawa wataendelea kuwapo wodini hadi watakapopona vizuri ndio tutawaruhusu,” amesema Dk Bokhary.

Dk Bokhary amesema kuwa watoto wengine wawili leo wamefanyiwa upasuaji ambao walikuwa na tatizo kama hilo.

Jana madaktari wa hospitali hiyo walianza upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakul

WAFANYAKAZI WA KITUO CHA TIC WATEMBELEA MIRADI MBALIMBALI ILIYOWEZESHWA NA KITUO HICHO.

$
0
0
.
4
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akionyeshwa picha ya kumbi mpya za Mlimani City zinazoendelea kujengwa hazipo pichani na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mlimani City Group Pastory Mroso wakati alipotembelea mradi huo ili kuona maendeleo ya uwekezaji wa kampuni hiyo nchini.
001
Meneja Bidhaa Mwandamizi wa Kampuni ya Super Doll .inayotengeneza matela ya maroli iliyo chini ya kampuni mama ya Super Star Group Bw. Ibrahim Juma akiwaelezea wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wakati walipoitembelea kampuni hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ili kuona tija na changamoto za uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, Ziara hiyo iliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC.0001
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akisikiliza na kuandika maelezo ya Pastory Mroso Meneja Mkuu wa Mlimani City Group wakati alipotembelea mradi mpya wa ujenzi wa kumbi mpya za mikutano na kujionea maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi huyo amefanya ziara hiyo ili kuona maendeleo na shughuli za uwekezaji wa kampuni hiyo nchini hapa nchini ili kutambua changamoto na mafanikio yaliyopo katika uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, waliosimama nyima kutoka kushoto ni Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC , Phina Lyimo Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Veronica Mrema Afisa Uhamasishaji na Uwekezaji TIC.
0002
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kituo hicho kutoka kulia ni Phina Lyimo Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Veronica Mrema Afisa Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC wakati Kaimu Mkurugenzi huyo alipotembelea ujenzi wa kumbi mpya za Mlimani City.
002
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akiteta jambo na Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC leo alipotembelea na kukagua ujenzi kumbi mpya za Mlimani City.Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari.
1
Meneja Bidhaa Mwandamizi wa Kampuni ya Super Doll .inayotengeneza matela ya maroli iliyo chini ya kampuni mama ya Super Star Group Bw. Ibrahim Juma akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wakati walipoitembelea kampuni hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ili kuona tija na changamoto za uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, Ziara hiyo iliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC.

 Wafanyakazi wa Kituo cha uwekezaji cha TIC wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi waliotembela vituo vya uwekezaji vinavyowezeshwa na kituo hicho.



DONDOO ZA HABARI MAGAZETINI LEO.

WAZIRI ANGELLAH KAIRUKI AFUNGUA MKUTANO WA KAZI WA MFUKO WA TASAF MKOANI ARUSHA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora,Angellah Kairuki akiwaongoza Wakuu wa mikoa kutoka kushoto,Mhandisi Mathew Mtigumwe(Singida),Dk Joel Bendera(Manyara),Said Meck Sadick(Kilimanjaro)na Martine Shighela(Tanga).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora,Angellah Kairuki akifungua mkutano wa Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii(Tafas)walioketi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo,Ladislaus
Mwamanga na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadick.
Wakuu wa wilaya kutoka mikoa mitano ya Singida   ,Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga wakiwa kwenye mkutano wa Kazi wa kupata uelewa zaidi wa mfuko wa Tasaf.

Wakuu wa mikoa Mhandisi Mathew Mtigumwe wa Singida,Dk Joel Bendera wa Manyara(katikati) na Martine Shighela wa Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Tasaf ,Ladislaus Mwamanga akizungumza katika mkutano huo.

Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha akizungumza jambo katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga,Godwini Gondwe akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akizungumza katika mkutano huo.

FANYENI UKAGUZI KUBAINI WANAFUNZI HEWA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Maofisa Elimu nchini wafanye ukaguzi katika shule ili kubaini wanafunzi hewa kwenye mpango wa elimu bure.

“Kila mwezi Serikali inapeleka shule zaidi ya shilingi bilioni 18 kugharamia elimu bure na sasa tumeanza kuona udanganyifu katika sekta ya elimu kwa kuwa na wanafunzi hewa. Wakuu wa Wilaya na Maofisa Elimu nendeni mkafanye ukaguzi ili mpate takwimu sahihi,“ amesisitiza.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 18, 2016) alipokutana na watumishi na viongozi wa Manispaa ya Ilala katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

 “Wakuu wa Wilaya na Maofisa Elimu mkiona takwimu ziwachanganya, ni lazima mtoke maofisini na kwenda katika shule zilizo kwenye mpango wa elimu bure mkafanye uhakiki wa idadi ya wanafunzi,” ameonya.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema maamuzi yanayotolewa kwenye  vikao vya madiwani lazima yawe na tija na ameitaka halmashauri hiyo kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinatumika kuboresha shunghuli za maendeleo badala ya kujilipa posho.

“Lazima mjipange vizuri na kupunguza changamoto zinazoikabili wilaya yenu. Malipo yote ni lazima yawe yale yaliyoainishwa katika waraka na si vinginevyo.Mtu wa Ilala unadai nauli ya sh. 200,000; hivi unakuwa unatoka wapi hata mimi wa Lindi silipwi nauli hiyo,” amehoji.

Waziri Mkuu amesema ni lazima halmashauri zote nchini zizingatie sheria za Mamlaka ya Serikali za Mitaa na watendaji wake wajiulize kama mambo wanayoyafanya yana tija na wanawatendea haki watu wanaowatumikia.

Amesema Serikali inataka kuwa na watumishi wanaotambua nafasi zao na watakaofanya kazi kwa uadilifu, uaminifu pamoja na uwajibikaji mkubwa hivyo kila mtu ahakikishe anafanya kazi vizuri na yenye matokeo chanya.

“Kuna watu wanaona ukuu wa idara ndiyo kila kitu, hata yule anayekimbiza mafaili hathaminiwi, hili si jambo jema! Ninyi wote ni kitu kimoja, ni watumishi wa Serikali, hivyo kila mmoja amthamini mwenzake,” amesema.

Waziri Mkuu amesema: “Mkurugenzi yeyote asikubali kuwa na wakuu wa Idara wasiokuwa na ushirikiano na watumishi wengine kwa sababu hataweza kupata mafanikio ya kiutendaji ndani ya eneo lake,”.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM. 
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.

Article 6

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI.

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini, Bi. Bella  Bird  kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 18, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Maajliwa akizungumza  na  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini, Bi. Bella  Bird, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 18, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA SEKTA YA UCHUKUZI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo kuhusu uboreshwaji wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa alipokagua chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua moja ya darasa linalotumika kufundishia Marubani wa ndege alipokagua Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akiongea na wanafunzi wanaosoma kozi ya udereva alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam. Kushoto (mwenye tai nyekundu) ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akibadilishana uzoefu na makapteni wa meli ya Azam aliposafiri na boti hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akiongea na mmoja wa abiria wanaotumia usafiri wa boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, na kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili abiria hao ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi hivi karibuni.

…………………………………………………………………………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imejidhatiti kufanya maboresho makubwa ya kimiundombinu na rasilimali watu katika sekta za uchukuzi ili kuiwezesha sekta hiyo kuongeza ajira na kukuza uchumi wa nchi.

Prof. Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kusafiri wa boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikiwa ni mkakati wa kupata taarifa sahihi kuhusu hali ilivyo sasa kutoka kwa abiria na waendeshaji wa vyombo vya majini.

Amesema Serikali itaboresha Bandari ya Dar es Salaam ili kupunguza urasimu usio wa lazima na kuwawezesha abiria na boti kukaguliwa kwa haraka na kuondoka kwa muda unaotakiwa.

‘Tutahakikisha kuwa idadi ya manahodha na wahandisi wa vyombo vya majini wazalendo inaongezeka ili mkakati wa kuboresha usafiri wa majini hapa nchini uwiane na uwepo wa wataalam wa uhakika’ amesema Prof. Mbarawa.

Waziri huyo wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema Serikali ina mpango wa kujenga meli mpya za kisasa katika Ziwa Victoria ili kuhamasisha wasafirishaji katika sekta ya usafiri majini kuwa na vyombo vya kisasa na hivyo kupunguza gharama za usafiri.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambapo amesisitiza kuwa Serikali itaunga mkono juhudi zinazofanywa na Chuo hicho katika kutoa mafunzo wa marubani wa ndege ili kuongeza idadi ya marubani wazalendo.

‘Mpango wetu wakukunua ndege mpya unaendana na kuwezesha Chuo hiki chenye kufundisha marubani ili tuwe na marubani wazalendo wa kutosha’ amesisitiza Prof. Mbarawa.

Amewataka wafanyakazi wa Chuo hicho kufanya kazi kwa uzalendo, ubunifu na kuzingatia matokeo ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayokwenda haraka.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zacharia Mganilwa amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa chuo hicho kitashirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Kampuni hodi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) katika kupata utaalam wa kisayansi katika mradi wa ujenzi wa reli ya kati ya Kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

Serikali imejipanga kujenga chuo cha kisasa cha Usafirishaji kwa kushirikiana na Jamhuri ya Watu wa China ikiwa ni mkakati wa kukifanya chuo hicho kuwa chuo mahiri katika upande wa Afrika Mashariki na Kati.

Zaidi ya Shilingi trilioni 4 zimetengwa na Serikali katika bajeti ya mwaka huu ili kuimarisha miundombinu ya usafiri wa Angani, barabarani, relini na majini.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA RAIS WA TEC

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalalekumtwa kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 18, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, Renatus Nkwande (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalekumtwa kabla ya mazungumzo yao , Ofisini kwake jijini Dar es alam Agosti 18, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalekumtwa (kushoto kwake), Askofu Renatus Nkwande wa Jimbo Katoliki la Bunda (wapili kulia) na katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Raymond Saba (kulia), Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalekumtwa (kushoto kwake), Askofu Renatus Nkwande wa Jimbo Katoliki la Bunda (wapili kulia) na katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Raymond Saba (kulia), Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 18, 2016.

MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO AJA NA MIKAKATI YAKE MIPYA ITAKAYOLENGA KUWAPATIA WANANCHI TAARIFA ZA KILA MARA

$
0
0
 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Abbasi akifafanua mikakati yake mbalimbali kuhusiana na Idara hiyo,kwenye mkutano wake wa kwanza wa kujitambulisha na pia kuzungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo mapema leo asubuhi jijini Dar,Mkurugenzi huyo kwa mara ya kwanza leo amekutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali tangu kuteuliwa kwake hivi karibu.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Abbasi akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa kuhusiana na mikakati yake ambayo aliitaja,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Vicent Tinganya.
Baadhi ya Waandishi kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Hassan Abbasi alipokuwa akielezea mikakati yake mipya kuhusiana na Idara hiyo,mapema leo katika ukumbi wa Idara hiyo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.



                         
MKAKATI WA KUWAELEZA WANANCHI UTEKELEZAJI WA AHADI ZA SERIKALI

Dar es Salaam, Ijumaa, Agosti 19, 2016:

Serikali kupitia Idara ya Habari-MAELEZO itaanza kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuwapatia wananchi taarifa za kila mara kuhusu utekelezaji wa ahadi zake.  Mikakati hiyo itakayosaidia kuongeza uwazi na ushirikishaji, pamoja na mambo mengine, itahusisha hatua zifuatazo:-

Mosi, kuboresha mfumo wa mawaziri na watendaji waandamizi Serikalini kuzungumza na wananchi ili kuainisha utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti, sera na mipango ya Taifa. Kuanzia Agosti 25 mwaka huu, mawaziri wataanza kuzungumza na umma kupitia vyombo vya habari kueleza vipaumbele vya bajeti zao na utekelezaji wake hadi kufikia sasa.

Pili, kuanzisha utaratibu wa Idara ya Habari-MAELEZO kueleza kwa umma kila mara, na haraka iwezekanavyo, utekelezaji wa sekta zote katika ngazi ya kitaifa. Msemaji Mkuu wa Serikali atakuwa akitoa taarifa hizo kuanzia hivi karibuni.

Tatu, Serikali itaimarisha ushirikiano zaidi na wadau mbalimbali katika kutekeleza mikakati yake ya mawasiliano kwa umma. Pamoja na wadau wengine, Serikali itahakikisha inafanyakazi kwa karibu na vyombo vya habari ili vishiriki vyema katika ujenzi wa Taifa.

Mwisho, wakati huu Idara ikiendelea kufanyiakazi mikakati mingine ili kuboresha mawasiliano kwa umma, naomba wadau wote kutoa ushirikiano kwangu binafsi, Idara niliyopewa kuiongoza hivi karibuni na zaidi tumuunge mkono Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ajenda yake ya mageuzi kupitia HapaKaziTu.

Imetolewa na:

Hassan Abbasi,
Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO.

WAAJIRI WATAKIWA KULINDA AFYA ZA WAFANYAKAZI WAO.

$
0
0
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi akizungumza wakati wa mkutano wa wadau kuhusu usalama wa Afya mahali pa kazi jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa Timu ya wataalamu wa Afya ya Jamii na Mazingira kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani, Geneva, Dk. Ivan Ivanov akizungumza wakati wa mkutano wa wadau kuhusu usalama wa Afya mahali pa kazi jijini Dar es salaam. 

Na. Aron Msigwa – Dar es Salaam.
Waajiri kote nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kisheria kwa wafanyakazi waliowaajiri kwa kuhakikisha kuwa wanaweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kuwapatia vitendea kazi muhimu vya kuwakinga na madhara ya kiafya katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau kuhusu usalama wa Afya mahali pa kazi jijini Dar es salaam, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi amesema kuwa waajiri wana wajibu huo kwa kuwa maeneo ya kazi ni sehemu muhimu katika maisha na uhai wa wafanyakazi kote nchini.

Amesema watumishi wamekuwa wakitumia muda mwingi kwa siku wakiwa mahali pa kazi kwenye viwanda, mashamba, maeneo ya kutolea huduma za Afya, migodini na kwenye shughuli mbalimbali hivyo mazingira hayo lazima yawe salama kwa afya zao.

Ameongeza kuwa wafanyakazi katika maeneo mbalimbali nchini karibu kila siku wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zenye athari kwa afya zao hasa athari za kibiolojia, Kemikali, ajari za viungo vya miili yao, matatizo ya usikivu yanayotokana na mazingira yenye kelele na changamoto mbalimbali ambazo wakati mwingine husababisha vifo.

“Wapo baadhi ya waajiri hawatimizi wajibu wao wa kisheria wa kuhakikisha wanalinda afya za watumishi wao kwa kuwawekea mazingira safi na salama, jambo hili halikubaliki” Amesisitiza Prof. Mohammed.
Amesema Serikali kupitia wizara ya Afya ikishirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya itaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi katika sehemu zao za kazi kazi ili kulinda afya zao.

Kwa upande wake kiongozi wa Timu ya wataalamu wa Afya ya Jamii na Mazingira kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani, Geneva, Dk. Ivan Ivanov amesema kuwa Tanzania ina wafanyakazi zaidi ya milioni 16 , wengi wao wakiwa kwenye sekta isiyo rasmi ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa na chanzo cha kipato kwa jamii na Taifa.

Amesema utafiti uliofanywa na mtaalamu aliyeteuliwa na WHO umebainisha changamoto mbalimbali ambazo zinapaswa kufanyiwa kazi na Serikali ili kuboresha maslahi na mazingira ya kufanyia kazi kwa kundi hilo.

“Ninajua wafanyakazi nchini Tanzania wamekuwa chanzo cha mapato, uzalishaji na ni tegemeo kwa jamii na Taifa, wanapougua au kupata ajali kwa sababu ya mazingira yasiyo salama hasara kwao wenyewe na kwa Taifa kwa kuwa hali hii inaongeza idadi ya wafanyakazi wagonjwa” Amesema Dk. Ivanon.

Amesema WHO inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuweka msisitizo katika kuboresha mazingira ya wafanyakazi katika sekta zote ili kudhibiti mazingira yenye viashiria hatarishi kwa afya za wafanyakazi maeneo ya viwanda, Sekta ya Afya, migodini na mashambani.

Amesema kuwa mchango wa WHO ikishirikiana na Tanzania ni kuboresha Mpango mkakati kwa ajiri utakaowezesha uboreshaji wa Afya za wafanyakazi kuanzia ngazi ya ngazi ya kijiji hadi Taifa ili kuwalinda wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mazingira hatarishi kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo watoto na wazee. 

Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya na Usafi wa Mazingira wa wizara hiyo Dk. Halid Masa akiuelezea mkutano huo wa wadau wa Afya na Usalama wa kazi amesema kuwa unakusanya wadau wote nchini ili kupitia taarifa ya utafiti uliofanywa na mtaalam aliyeteuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Amesema kufanyika kwa utafiti huo kunatokana na Azimio la mkutano wa Afya wa dunia (World Health Assembly) lililotoka mwaka 2007 ambao ulizitaka nchi zote zitengeneze mpango wa utekelezaji kuhusu masuala ya Afya kazini.

Amesema kupitia Azimio hilo Tanzania ilianza kufanya utafiti mwaka 2005 na ripoti ya utafiti huo imekamilika tayari kwa majadiliano yanayowahusisha wadau ili waweze kutoka na mkakati wa utekelezaji wa kukabiliana na changamoto za afya kazini.

“Mwaka 2005 utafiti huu ulianza kufanyika sasa umekamilika, kwenye mkutano huo wameitwa wadau ili kupata taarifa hii, kuijadili na kutoka na mkakati wa pamoja wa kukabiliana na changamoto zote za masuala ya Afya Kazini” Amesema.

Amesisitiza kuwa suala la Afya kazini ni mtambuka kwa kuwa linahusisha wadau mbalimbali pamoja na changamoto mbalimbali ikiwemo ufanyaji wa kazi katika mazingira yasiyo salama.

HAPA KAZI TU.

$
0
0
 
Rais John Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TAMWA YAWAKUTANISHA WANAHABARI KANDA YA ZIWA KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU.

$
0
0

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini, TAMWA, kimewakutanisha wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, kujadili namna mafunzo yaliyotolewa na chama hicho kwa wanahabari hao wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, kwa kuangazia usawa wa kijinsia kati ya Wanawake na Wanaume katika mchakato wa uchaguzi huo.

Pichani ni wanahabari hao wakiwa kwenye semina ya siku mbili kuanzia leo, inayofafanyika Jijini Mwanza, ambapo imelenga kujadili namna mafunzo yaliyotolewa mwaka jana na TAMWA kwa kushirikiana na taasisi ya INTERNEWS yalivyosaidia katika suala la usawa wa kijinsia kabla na baada ya uchaguzi mkuu pamoja na changamoto zilizojitokeza.

Na George Binagi-GB Pazzo

Mkufunzi wa semina hiyo, Deodetus Balile, ambaye pia ni Mhariri gazeti la Jamuhuri.
Semina kwa Wanahabari Kanda ya Ziwa
Godfrida Jola (kulia) akiteta jambo na Edson Sosten (kushoto), wote ni Maafisa Miradi TAMWA.
Baadhi ya Wanahabari Kanda ya Ziwa, wanaoshiriki Semina ya TAMWA Jijini Mwanza
Wanasemina

Tazama Hapa Semina ya Mwaka Jana

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO YALIVYORAHISISHA MCHAKATO WA AJIRA NA KUPUNGUZA GHARAMA ZA SERIKALI

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi  akizungumza na baadhi wa Watendaji wakuu wa Wakala wa Serikali (hawapo pichani) wakati akifungua  jukwaa la kujadili uimarishaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kutumia TEHAMA.

 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yalivyorahisisha mchakato wa ajira na kupunguza gharama za serikali.

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi (katikati) pamoja na baadhi ya Watendaji wakuu wa Wakala za Serikali baada ya kumaliza majadiliano kuhusu uimarishaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kutumia TEHAMA.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akiongea na baadhi wa Watendaji wakuu wa Wakala wa Serikali (hawapo pichani) wakati akifungua jukwaa la kujadili uimarishaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kutumia TEHAMA. 


Baadhi ya watendaji wakuu wa Taasisi wakitoa mchango wao wakati wa majadiliano kuhusu uimarishaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Baadhi ya watendaji wakuu wa Taasisi wakitoa mchango wao wakati wa majadiliano kuhusu uimarishaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) 



 Picha zote kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano Serikalini Sekretarieti ya Ajira Karika Utumishi wa Umma.


SERIKALI KUWAELEZA WANANCHI UTEKELEZAJI WA AHADI ZAKE

VODACOM YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SARATANI HOSPILI YA MUHIMBILI

$
0
0

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania katika picha ya pamoja  muda mfupi baada ya kushiriki katika kazi za kijamii za kusafisha mazingira  ya hosteli wanazoishi watoto wanaotibiwa Saratani katika hospitali ya Muhimbili ambapo pia waliwatengenezea lishe na kucheza nao,vilevile walijitolea fedha zao kununua mahitaji mbalimbali ya watoto hao.
Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo akiongea na wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani (Hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili,(kushoto) ni Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza na (kulia) ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza akiongea na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa kusaidia watoto wanaotibiwa ugonjwa wa Saratani  katika hospitali ya Muhimbili.Wafanyakazi wa Vodacom pia walitoa msaada wa fedha taslimu,vyakula na vitu mbalimbali vya kuwasaidia ambapo pia walitenga muda wao kusafisha maeneo ya hosteliwanazoishi watoto hao na walishiriki kuwatengenezea lishe na kucheza nao kwa ajili ya kuwapatia faraja.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakishiriki kusafisha  mazingira  ya hosteli wanazoishi watoto wanaotibiwa Saratani katika hospitali ya Muhimbili
 Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza na (kulia) akiongea na wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani (Hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili (katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo na kulia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan
 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan (Kulia) akiongea na wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani (Hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili (katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo na (kushoto ) ni Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza.
 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan (Kulia) akipokea baadhi ya vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi wa Vodacom kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza (wa nne kutoka kulia) wengine pichani wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo (Wa tatu kutoka kushoto).Wengine ni maofisa wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na Saratani.
 .Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakicheza na watoto.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakishiriki kutengeneza lishe wakati walipojitolea muda wao kusaidia watoto wahanga wa ugonjwa wa Saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya saratani ambao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepatiwa msaada wa milioni 20 kutoka taasisi ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya kufanikisha  matibabu yao na kuwapatia lishe bora.

Mbali na msaada wa fedha wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania wametenga muda wao kushiriki kusafisha maeneo ya hosteli wanaoishi watoto hao ikiwemo kucheza nao,kuwatengenezea lishe pia wametoa msaada wa vyakula na fedha taslimu kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto hawa.

Msaada huo  umetolewa leo  katika hosteli wanazoishi watoto hao zilizopo katika  hospitali ya Taifa Muhimbili  kupitia Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwahudumia watoto wenye maradhi ya Saratani linalojulikana kama Tumaini la Maisha ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo.

Akitoa pongezi kwa niaba ya serikali,Dk.Msemo amesema kuwa serikali inafarijika inapoona makampuni  ya biashara kama Vodacom yanajitoa kusaidia jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali hususani katika sekta ya afya ambako kunahitajika uokoaji wa maisha ya watu.
“Nawapongeza  sana wafanyakazi wa Vodacom na taasisi yake yake ya kusaidia masuala ya kijamii ya Vodacom Tanzania Foundation pia nimefurahishwa kuona wafanyakazi mmejitoa kuchangia kusaidia watoto hawa wenye matatizo ya saratani na kutenga muda wenu kuja kusafisha mazingira eneo hili wanaloishi,kushiriki kuwatengenezea lishe na kujumuika nao kwa kucheza nao kwa ajili a kuwapatia faraja”.Alisema.

Akiongea wakati wa kupokea msaada huo Mkurugenzi wa Shirika la Tumaini la Maisha,Dk. Trish Scanlan alishukuru kwa msaada huo kutoka Vodacom Tanzania Foundation kwa watoto utakaowafikia na kuwanufaisha walengwa kupitia  shirika hilo lisilo la kiserikali linaloshughulika na kuwasaidia watoto wahanga wa ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 Alisema kuna idadi kubwa ya watoto zaidi ya 300 wanaolazwa hospitalini hapo wakiwa wanakabiliwa na saratani ya aina mbalimbali na kutokana na umri wao  na wanahitaji misaada ya  madawa ya kuwatibu ikiwemo lishe bora na mahitaji mengine mengi ya kila siku.

Kwa upande wake Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza alisema kuwa siku zote taasisi hiyo itakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali katika kusaidia jamii hususani katika nyanja za Afya na Elimu.

“Afya ni moja ya suala ambalo tunalipa kipaumbele na ndio maana tumekuwa tukivalia njuga kutokomeza magonjwa mbalimbali mojawapo ikiwa ugonjwa huu wa saratani ambao siku hadi siku umekuwa ukiongezeka na kusababisha vifo vya watu wengi ”Alisema.

Alisema Vodacom Foundation imetoa kiasi cha shilingi milioni 20 kupitia taasisi ya Tumaini la Maisha ili kuwawezesha watoto hawa kupatiwa  madawa,lishe  bora na mahitaji mbalimbali hususani katika kipindi hiki kigumu wanachoendelea kupata matibabu na aliwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia wenye matatizo mbalimbali kwenye jamii.

 Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake anaendelea na matibabu ya Saratani Grace Nyambisu kutoka mkoani Dodoma akiongea kwa niaba ya wenzake alishukuru Vodacom Tanzania Fondation kwa msaada huu muhimu wa lishe na madawa kwa watoto wao katika kipindi hiki kigumu ambacho wanaendelea kupata matibabu.

Alisema kwa msaada huo  taasisi hiyo imethibitisha usemi wa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki kwa kuwa umetolewa katika muda mwafaka ambao watoto wanahitaji kupata lishe bora na madawa wakati huohuo wazazi wengi wakiwa wanakabiliwa na changamoto ya kutomudu kuwahudumia  kutokana na kukabiliwa na ugumu wa maisha ambao unasababishwa na kutumia muda wao mwingi kuuguza watoto badala ya kujishughulisha na kazi za uzalishaji kwa ajili ya kuwaingizia vipato.

AMH AFRICA OPENING THE FIRST NISSAN TANZANIA SHOWROOM

$
0
0
3N
AMH Africa Managing Director South Africa Tim Jaques Speaks to reporters in Dar es salaam yestarday during the official opening of the first Nissan Tanzania showroom centre,is the Nissan Tanzania Managing Director Mr Christopher Henning and left is Nissan Tanzania Commercial Manager Mr Ash Ramraj
IMG_1227
Nissan Tanzania Managing Director Mr Christopher Henning speaks to the reporters in Dar es salaam yestarday during the official opening of the first Nissan Tanzania showroom, right is the AMH Africa Managing Director South Africa Tim Jaques and Nissan Tanzania Commercial Manager Mr Ash Ramraj.
...........................................................................................
Associated Motor Holdings (AMH) is a vehicle distribution and dealership company. It is part of the South African listed Imperial Group. Imperial is a proud a representative of NISSAN in Tanzania, and also proudly represents Nissan in Kenya, Zambia and Malawi.
Imperial is the largest motor vehicle distributor and retailer in sub Saharan Africa and in South Africa, and is also present in various other markets globally including Europe and Australia.

Imperial has extensive automotive expertise, with over 250 dealerships on the African continent, and vehicle sales of close to 200 000 units per year in Africa alone.
Imperial operates in 40 African countries with its various businesses ranging from logistics and pharmaceutical to vehicle dealerships. It employs over 50 000 people, and has globally renowned technical and non-technical training centres. Imperial is committed to sustainable development throughout Africa.

According to Tim Jaques, Managing Director - AMH Africa“, NISSAN is a world class brand that has allowed us to strategically move forward into East Africa. To support this, we have invested extensively into the region, there will be much further investment to ensure long term, sustainable growth of the brand in the Tanzania market.”

“This will be not only in dealership infrastructure but also in employment, training, people development and social initiatives. So in joint collaboration with NISSAN, we intend on using our combined capabilities, to offer our customers in Tanzania world class products and service.”
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images