Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Muhimbili Yafanya Upasuaji kwa Watoto Wenye Tatizo Mfumo wa Hewa na Njia ya Mkojo

$
0
0
Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na Profesa Saber M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.
Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.
Profesa Saber M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo LEO.
Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa upasuaji na kutenganishwa.
Kutoka kushoto ni Eliudi Joel na Elikana Joel wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakisubiri kufanyiwa upasuaji LEO.
Profesa Dk. Saber M. Waheeb akifanya utafiti mdogo kwa mtoto ambaye amelazwa kwenye Jengo la watoto katika hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kushoto) akimkaribisha Profesa Saber M. Waheeb katika hospitali hiyo LEO.
Profesa Lawrence Museru (kulia) akizungumza na madaktari na wataalamu wa kada nyingine LEO katika hospitali hiyo kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji.
Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi za Mashariki ya kati akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk. Julieth Magandi LEO wa hospitali hiyo.
……..
Na John Stephen 

Dar es Salaam, Tanzania. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO imeanza upasuaji kwa watoto wanane na wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakula ili kuwa sawa na watu wengine ambao hawana matatizo hayo. 

Madaktari wa hospitali hiyo wanafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Misri ambao wamewasili leo wakitokea Misri kwa ajili ya kushiriki shughuli hiyo. 

Madaktari wa Muhimbili ni Dk. Zaitun Bokhary, Dk. Yona Ringo Madaktari, Dk. Herman Wella, Dk. Victor Ngolta, Dk Mwajabu Mbaga, Dk. Joachim Angela, Dk. Hashim Lituli na Dk. Gertrud Mollel wakati madaktari na wataalamu wa kada nyingine kutoka Misri ni Mahamed Malak, Saber Waheeb, Amr Alaa, Tamer Ghoneim, Ragia Mohamed Awad, Sherouk Saad Ayoub, Hazem Ahmed. 

Wataalamu hao wametembelea watoto waliolazwa kwenye Jengo la Watoto na kujadiliana na madaktari wa hospitali hiyo jinsi watakavyotoa huduma za upasuaji kwa watoto hao.
Kwa mujibu wa Dk Julieth Magandi, watoto wengine sita watafanyiwa upasuaji huo kesho. Dk Magandi amesema Leo madaktari hao wameanza kwa mtoto mwenye tatizo la mfumo wa chakula na hewa na kwamba watoto pacha wawili waliungana na kutenganishwa kutoka Mbeya nao watafanyiwa upasuaji wa kuweka sawa mfumo wa njia ya mkojo. 

Baadhi ya watoto wanaofanyiwa upasuaji ni; Nasra Rashidi, Hughes Khalid, Fahad Selemani, Elikana Joel, Eliudi Joel, Hasna Hamis Kalemea, Ibrahim Haji na Sofia Ramadhani.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 18

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA KWA WAJASILIAMALI VIJIJINI KUPITIA MRADI WA MADAWATI.

$
0
0
Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia) na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale. Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang'wale. Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano. Fursa ya ajira iliendelea kusambaa kwa dereva wa trekta Bw ,Machibya aliyepata tenda ya kusafirisha Madawati kwenda katika shule zilizokusudiwa kupata Madawati hayo. Lakini pia wakati wa shughuli za utengezaji wa Madawati hayo mafundi walihitaji kupata chakula na hii pia ikawa Fursa kwa Mama Nitilie Devotha Sonda wa Sonda ambaye alikuwa akitoa huduma ya chakula kwa mafundi hao.


Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetengeneza mamia ya ajira kwa vijana na wanawake wanaoishi maeneo mbalimbali mkoani shinyanga na Geita kupitia mpango wa kutengeneza madawati elfu sita katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 200.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana wamesema neema ya kujiingizia vipato kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali katika zoezi la kutengeneza madawati imebadili maisha yao hasa katika msimu huu wa kiangazi ambao wengi wao ajira zao zimesimama kwani walio wengi wanategemea mvua kwenye ajira yao ya msingi ya kilimo.

“Tunashukuru sana msimu huu wa kiangazi, tumepata nafasi ya kupata kazi za ambazo zinatupatia kipato kupitia utengenezaji wa madawati, mimi hapa ni fundi chuma, nachomelea vyuma na kazi yangu hii huku vijijini wateja ni wachache sana, muda mwingi huwa tuko doro kwenye kijiwe chetu lakini sasa hivi tuna kazi nyingi sana za kutengeneza madawati hapa imebidi niajiri vijana wengine watano kuweza kunisaidia kukamilisha kazi ya kuunganisha vyuma kwa ajili ya madawati mia tano ambayo tumepata tenda na Kampuni iliyoshinda tenda ya kutengeneza madawati kwa gharama ya mgodi wa dhahabu ya Bulyanhulu.” Anasema Abbas Mbua mkazi wa kata ya Msalala wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.

“Sisi wapiga msasa tunajipatia shilingi elfu kumi na tano kwa kila dawati 5 hii si haba, kiasi hiki kimenisaidia sana maana sikupata vizuri mazao mwaka huu kwa hiyo pesa niliyoingiza kwenye kazi ya kupiga msasa imebadili kabisa hali halisi nyumbani, nimenunua gunia za mahindi, maharage na mchele, hali imetulia kwa kweli siwezi kusema uongo” anasema Maige Deus mkazi wa Kahama.

“Ninaiomba sana serikali yetu iendelee kuvumbua miradi mingine ili sisi vijana tuendelee kuchapa kazi, maana vinginevyo tunakaa vijiweni kazi hamna, lakini mradi huu wa madawati ulivyokuja hatuna hata muda wa kuvuta sigara, tuko bize kutwa nzima tunatengeneza madawati, hapa mimi ndiyo fundi mkuu kwenye hiki kiwanda naunganisha mbao na kuhakikisha madawati yako vizuri kwa ajili ya wanafunzi.” Anasema Abdul Karim Ramadhani akiwa katika kiwanda cha Zacharia and Deus Timber Supply cha Nyang’wale mkoani Geita.

Halikadharika mama nilitie nao wanasema si haba mradi wa kuchonga madawati umeongeza idadi ya wateja katika migahawa yao, Devotha Sonda wa Sonda Mama Nitiliea katika kijiji cha Msalala anasema “ Kabla ya mradi wa madawati vyakula hapa tulikwa tunapika kidogo na wateja walikuwa ni wa kubangaiza tu lakini sasa hivi kutokana uchongaji wa madawati vijana ni wengi sana na binafsi nimepewa tenda kabisa ya kupikia vijana wanaotengeneza madwati na ninalipwa vizuri na kwa muda, naomba miradi kama hii iendelee tu hadi madawati yatoshe na sisi mitaji itakuwa imekua. Mwaka huu maswala ya ada kwa watoto, mavazi sasa ni jambo rahisi.”

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya kizawa ya Zacharia and Deus Timber Supply Deus Mlela iliyopo Nyang’wale kilomita hamsini kutoka mgodi wa Bulyanhulu amesema, “Tenda ya kutengeneza madawati mia tano kutoka Bulyanhulu kwetu tumepata faida mara mbili kwanza imetuongezea mtaji na pili imetupa uwezo na kujulikana kwa wadau wengine, sasa hivi tumepatiwa tena tenda na Halamashauri ya wilaya kutengeneza madawati mengine elfu moja na kampuni nyingine imetupa tenda na madawati mia mbili, bila kazi ya Bulyanhulu kutufungulia mlango ingekuwa vigumu kuweza kupokea tenda hizo kwa sababu mtaji ulikuwa mdogo. Tunaomba wadau waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa vijana ambao hawana ajira.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama amesema, “Kimsingi kuwa karibu na Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu imewafanya watu wa Nyang’wale ule uzito wa kazi ya madawati kuwa tofauti na sehemu nyingine, japo hatujamaliza kabisa tuna mapungufu kidogo, faida ya mradi wa madati faida yake ya kwanza ni kwa watoto wa shule ambayo ni walengwa, wanapata madawati wake vizuri na waweze kuelewa masomo yao vizuri, kwa njia nyingine mpango huu umetengeneza ajira, wale watengeneza mawadaati wamepata kazi ya kufanya na kipato, wanajipatia mahitaji wengine wananunua mifugo, kwa mfano katika mradi huu bulyanhulu imedhamini madawati yenye thamani ya shilingi million thethini na tano na hii pesa imezunguka kwa watu wote, mafundi seremala, waendesha mikokoteni, mama nitilie, na wengine wengi wamejipatia kipato na hata mitaji.”

Mwaka 2013 Mgodi wa Bulyanhulu ulitoa madawati 1329 kwa ajili ya shule 10 za msingi zinazozunguka mgodi wa Bulyahulu.Mwaka huu 2016 Madawati 1380 kwa halmashauri ya Msalala madawati 500 kwa wilaya ya Nyang’wale 500, madawati 2000 yatatolewa hivi karibuni kwa mkoa wa Shinyanga na pia Bulyanhulu itaipatia dola za kimarekani elfu 6000 shule ya msingi ya binafsi ya St. Josephine Bhakita iliyoko km 12 kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika kijiji cha Ilogi kata ya Bulyanhulu.

BALOZI WA ISRAEL NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI MAKAMBA.

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh. Yahel Vilan alimpomtembelea Waziri Makamba  Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba wakijadiliana jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh Yahel Vilan alimpomtembelea Waziri Makamba  Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam. Wengine ni Maafisa toka Wizara ya mambo ya nje waliongozana na Balozi huyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisoma Nakala za machapisho  alizopatiwa na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh . Yahel Vilan.


Chindo ft. Wakazi, Fid Q & Dully Sykes - TORATI YA MTAA #NewTanzaniaHipHop

$
0
0


Torati Ya Mtaa is a brand new single from Chindo Man, and the lead single off his new Album also titled "Torati Ya Mtaa". He features two Hip Hop heavyweights (Fid Q & Wakazi), with the hook sung by the Legendary Bongofleva Artist, Dully Sykes (who by the way, also did the production of the song). Torati Ya Mtaa is the Swahili phrase which means "Street Laws/Codes" and throughout the song, the three emcees reiterate the codes that run their respective streets, with Chindo hailing from Kijenge Juu (AR City), Fid Q from Mwanza (Rock City) & Wakazi from Stakishari Ukonga (Dar City). Such street tales and guidelines are artistically embroidered over the Typical bongofleva style beat that is so reminiscent of the "P Funk Majani Era", and the familiarity of the sound along with the clever wordplay & rhyme schemes of the rappers, has made TORATI an instant TZ Hip Hop Classic. The Video was directed & edited by Shebuge (Wanene ENT) & Shot on location in Dar Es Salaam, Tanzania (Tandale, Magomeni & Wanene Studios). Color grading done by Lui Arts.

For more info:

www.africanmusicnow.com
www.wakazimusic.com

Twitter:
@Umbwax
@wakazi
@FidQ
@Dully_Sykes

Pepo wa Bongo Dansi bado anasumbua washabiki ulaya !

$
0
0

NGOMA AFRICA BAND AKA FFU ndio walipeperusha !

Utamu wa muziki wa dansi wa kiafrika umegeuka kuwa pepo asiye sikia
ubani wala uvumba mbele ya washabiki wa muziki wa kiafrika kule ughaibuni,kwa takribanimiaka 23 sasa Ngoma Africa band imekuwa katika medani ya muziki katika majukwaa ya kimataifa kule ughaibuni na kufanikiwa kujizolea umaarufu kwa kuwanasa washabiki wa kimataifa katika kila kona. urimbo wanaoutumia kuwanasa washabiki wao ni "Muziki wa dansi" au Bongo dansi kutoka uswahilini na jirani mwa afrika mashariki. 
 
bendi hiyo mashughuli iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake mwanamuziki mtanzania Ebrahim Makunja kwa majina ya usanii Kamanda Ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens, bendi ya Ngoma Africa band na muziki wake imegeuka kuwa pepo aliyewaganda washabiki wa kila umri na kila jinsia, na kuifanya bendi hiyo kujiwekea historia ya bendu pekee ya kiafrika katika majukwaa ya kimataifa ,bendi ambayo mara nyingine usababisha ulinzi kuwa mkubwa kila wanapotumbuiza.bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya utani na washabiki wake,majina kama vile FFU-Ughaibuni,aka "Viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kutoka "Special Planet Bongo land".

Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kinapokwea jukwaani kinakuwa na kazi moja tu hakuna kuremba remba bali kushambulia kwa muziki moto mpaka

washabiki wanachanganyikiwa.

usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

uungana nao at www.facebook.com/ngomaafricaband

jarida moja la ujerumani limeitaja bendi ya ngoma africa kuwa yenye mafanikio na imeshinda mapambano kwa kuwa bendi pekee ya kiarika kuteka soko la muziki ujerumani na ulaya som at http://www.afrikaportal.eu/portraet-ngoma-africa-band/

Serikali yampongeza Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko (katikati), Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri wakiwa wameshikilia Kamusi hiyo mara baada ya Uzinduzi 17 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko (katikati) akiwa ameonyesha juu Kamusi ya Ukristo iliyoandikwa na Padre Jordan Nyenyembe (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri 17 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko (katikati) akikata utepe kuzindua Kamusi ya Ukristo iliyoandikwa na Padre Jordan Nyenyembe (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri 17 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHSUM.

Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Serikali imempongeza Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe pamoja na wadau wengine waliohusika katika kufanikisha uandishi wa Kamusi hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Mhe. Waziri Nape Nnauye wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Kamusi hiyo.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Mhe. Waziri Nape Nnauye, Bibi. Beleko amesema kwamba Padre Jordan Nyenyembe anapongezwa kwa uandishi wa Kamusi hiyo kwani kunaonyesha juhudi za kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili.

Alisema kwamba uandishi wa Kamusi ni kazi ngumu na endapo maneno ndani ya Kamusi hayatafsiriwi sawa sawa basi kuna uwezekano wa kusababisha chuki, ghasia na hata mapigano na hasa maneno yanayohusiana na masuala ya imani ya dini Fulani.“Ni matumaini yangu kwamba, Kamusi hii itahamasisha na kurahisisha uelewa wa vitabu na maandiko mbalimbali kwa usahihi na ufasaha kwa jamii na kuleta upendo, utulivu na amani”, alisema Beleko.

Aliongeza kuwa Wamisionari wa mwanzo wa imani ya kikristo walisaidia katika usahihishaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia vitabu na nyaraka mbalimbali, aidha walishiriki katika kuandika sarufi za Kiswahili, kamusi za kiswahili na kutafsiri Biblia kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine hali ambayo ilisaidia kukuza dini ya Ukristo na kukuza lugha ya Kiswahili.

“Lugha yetu ya Kiswahili kila kukicha inazidi kukua na kupitia Kamusi hii tunaamini kwamba wasomaji wataongeza maarifa na ufasaha na kudumisha umoja, amani na uzalendo”, alisema Beleko.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri ambaye aliliwakilisha Baraza hilo alieleza kwamba, ushirikiano kati ya serikali na taasisi za kidhni ni jhambo mhimu katika kusukuma maendeleo ya taifa.

“Katika Kanisa la Katoliki Tanzania linaunga mmkono jitihada zote za Wasomi na Wataalam wote wanaowezesha ujuzi na maarifa mbalimbali kidini na hata kielimu kuwafikia Wananchi katika kukabiliana na changamoto, hivyo nachukua nafasi kwa niaba ya Baraza, kumshukuru na kumpongeza Padre Jordan kwa jitigada zake za kubuni na kufanya kazi hii njema kwa Watanzania”, alisema Padre Ubadius.

Naye Mwandishi wa Kamusi hiyo, Padre Jordan Nyenyembe alisema kwamba Kamusi hiyo inakamilisha kazi iliyoanza mwaka 2004 kama Makala katika Gazeti la Kiongozi iliyoitwa ‘Kiswahili cha Mwanakanisa’.

Alisema kwamba, wasomaji watakaokuwa wanaitumia Kamusi hiyo wawe huru kumshirikisha kwa kutoa maoni yao mbalimbali ili aweze kuboresha katika matoleo yajayo.“Mtakaoisoma Kamusi hii msisite kutoa maoni yenu ambayo yataniwezesha kuboresha katika matoleo yajayo”, alisema Padre Jordan.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Mkuki na Nyoka, Bw. Walter Bugoya alieleza kwamba, kuandaa kamusi kama hiyo kunahitaji mtu kufahamu masuala mengi ambayo anatarajia kuyaandika, hivyo anakuwa na kazi kubwa ambayo inahitaji umakini, kutafuta maana sahihi ya maneno.


“Pia katikia suala la uhalili Mwandishi anahitaji kusaidiwa na Wahariri ili kazi yake iwe rahisi kwa wasomaji kwa kupata maana sahihi ya maneno ndani ya kitabu husika”, alisema Bw. Bugoya.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi alisema kuwa, suala la lugha kwenye Makanisa ni muhimu sana kwani litasaidia kukuza uelewa wa mafundisho ya imani ya dini hiyo, hivyo amepongeza kazi ya uandishi wa Kamusi hiyo.

WAZIRI MKUU AWAWEKA SAWA WATUMISHI WA OFISI YAKE

$
0
0
*Asema safari imeiva, ataka wajipange kuhamia Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya kuhamia Dodoma imeiva na amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wajipange kisaikolojia.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Agosti 18, 2016) alipokutana na kuzungumza na watumishi wa ofisi yake kutoka taasisi, idara na vitengo mbalimbali waliopo Dar es Salaam.

Waziri Mkuu aliwataka watumishi hao watambue kuwa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.

“Tangu wakati huo kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizofanyika ili kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo,” alisema.

“Pia tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,” alisema.

“Napenda kuwatoa hofu, mambo yanaenda vizuri ila mtambue kuwa safari imeiva sasa. Kikubwa ni kwamba tutakwenda kwa awamu kama ambavyo imepangwa,” alisema.

Aliwataka watumishi hao wazidishe mshikamano miongoni mwao huku wakitambua kuwa wana dhamana ya kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu na uaminifu. “Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu tunapaswa tutambue dhamana tuliyonayo. Tufanye kazi kwa bidii. Tuhakikishe kila kilichopangwa kinafanyika kwa ufanisi na kinafanikiwa,” alisema.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AWAVUA MADARAKA WALIMU 12 WA SHULE YA MSINGI,WAKUU WA SHULE 11 ZA SEKONDARI NA WARATIBU WA ELIMU 10

RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA ARUSHA FELIX NTIBENDA,AMTEUA MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na Rais,kuapishwa kesho ijumaa Ikulu jijini Dar
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA SSRA ILIPOTOA MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA TABORA, MKOANI TABORA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uhusino na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi.Sarah Kibonde akimkabidhi madawati Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora, Sweetbert Nkuba, kwa ajili ya Shule za Msingi za Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora.Mkuu wa Kitengo cha Uhusino na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi.Sarah Kibonde (aliyekaa kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Manispaa, Walimu Wakuu wa Shule za Manispaa ya Tabora pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi za manispaa hiyo, mara baada ya kukabidhi madawati kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora, Sweetbert Nkuba.Mkuu wa Kitengo cha Uhusino na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi.Sarah Kibonde (kulia), akiwa amekaa kwenye moja ya madawati aliyomkabidhi Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora, Sweetbert Nkuba (kushoto), kwa ajili ya Shule za Msingi za Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora. Baadhi ya wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi za Manispaa ya Tabora, wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na SSRA na kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusino na Uhamasishaji wa SSRA, Bi.Sarah Kibonde kwa ajili ya Shule hizo za Msingi mkoani Tabora.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi za Manispaa ya Tabora, wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na SSRA na kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusino na Uhamasishaji wa SSRA, Bi.Sarah Kibonde kwa ajili ya Shule hizo za Msingi mkoani Tabora. Mkuu wa Kitengo cha Uhusino na Uhamasishaji wa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi.Sarah Kibonde, akiwa amesimama mbele ya wanafunzi waliokaa kwenye madawati yaliyotolewa na SSRA kwa ajili ya Shule za Msingi za Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MKUU MSAIDIZI WA UMOJA WA MATAIFA DKT. NATALIA KANEM PIA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI BALOZI LIBERAT MFUMUKEKO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya nae mazungumzo.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akizungumza na Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni  Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem wapili kutoka (kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitazama vitabu alivyopewa na mgeni wake Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni  Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem wapili kutoka (kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza (kulia) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiangalia vitabu hivyo.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem watatu kutoka kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga watatu kutoka (kushoto). 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya  mazungumzo. 
PICHA NA IKULU.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2016 amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Balozi Liberat Mfumukeko Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumsihi ahakikishe Jumuiya inajielekeza kukabiliana na matatizo ya wananchi na kupunguza matumizi ya fedha yasiyo ya lazima.

Dkt. Magufuli amesema ni vema Jumuiya hiyo itilie mkazo katika kuziwezesha nchi wanachama kukabiliana na matatizo muhimu ya wananchi yakiwemo upatikanaji wa maji, uboreshaji wa miundombinu kama vile barabara na reli, kuimarisha huduma za afya, kujenga viwanda vitakavyozalishaji ajira na kuongeza mapato, na kukuza biashara na uwekezaji.

"Itakuwa ni manufaa zaidi endapo nyie watendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mtafanya juhudi kubwa kuhakikisha nchi wanachama zinajikita kukabiliana na matatizo ya wananchi, mkifanya hivyo na mkaepuka matumizi makubwa ya fedha kwenye mambo yasiyo ya lazima tutanufaika zaidi" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amempongeza Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, aliyeshika wadhifa huo kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu (2016) kwa mipango na mikakati mizuri aliyoanza nayo katika kutekeleza malengo ya Jumuiya ikiwemo kupunguza matumizi, kuvutia wawekezaji na kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi na programu iliyo chini ya Jumuiya hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko pamoja kumshukuru Rais Magufuli kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa kwake ameahidi kutekeleza wajibu wake vizuri na kwa manufaa ya wana Afrika Mashariki.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na aliyekuwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya idadi ya watu hapa nchini (UNFPA - Tanzania) Dkt. Natalia Kanem ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UNFPA.

Dkt. Magufuli amempongeza Dkt. Natalia Kanem kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na amesema anaamini kuwa Dkt. Natalia Kanen atakuwa Balozi mzuri wa Tanzania hususani katika kuongeza mkazo kwa Umoja wa Mataifa kuisadia Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo ongezeko la wakimbizi, umasikini na huduma za mama na mtoto.

Kwa upande wake Dkt. Natalia Kanem ambaye amekuwa hapa nchini kwa kipindi cha takribani miaka miwili ameishukuru na kuipongeza Tanzania kwa kuwa nchi ya amani na jinsi ilivyojitoa kuwahudumia wakimbizi kutoka mataifa mbalimbali yanayokumbwa na matatizo ikiwemo mapigano.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Agosti, 2016

Msimu wa pili wa kambi tiba ya GSM Foundation wafungwa rasmi Iringa, maisha ya watoto 37 yaokolewa

$
0
0

Kambi tiba ya GSM iliyokuwa imeingia katika msimu wake wa pili tangu Agosti mosi mwaka huu, imefungwa rasmi mkoani Iringa, huku watoto 37 wakiwa wamefanyiwa upasuaji, na wengine zaidi ya 300 wakipata ushauri nasaha kutokana na afya zao kutoruhusu kufanyiwa upasuaji, huku suala la uimara wa afya likiwa kipaumbele cha kwanza.

Awali akiongea kabla hajamkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Amina Masenza kuongea, Msemaji wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba alisema kila kukicha wanashukuru kuona maisha ya watoto ambao ilikuwa wapate mtindio wa ubongo ama kupoteza maisha yanaokolewa kupitia mchango wao pamoja na madaktari kutoka Taasisi ya ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili, MOI.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI kwa mwaka 2002, unasema zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na migongo wazi, na kati yao ni 500 tu wanaoweza kufika hospitali na kupata matibabu kutokana na changamoto kuu tatu.

Ya kwanza ni uhaba wa madaktari bingwa wa upasuaji wa vichwa vikubwa na vikubwa na migongo wazi ambapo kwa tanzania nzima, kwa sasa wamebaki saba tu, huku sita wakiwa ni waajiriwa wa Taasisi ya MOI na mmoja akiwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.

Kutokana na uhaba huo wa madaktari, ambao wanapatikana katika mikoa miwili tu ya Tanzania, Mikoa mingine ambayo watoto wa aina hii huzaliwa wagonjwa hupata changamoto ya pili ya kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu ambapo hata hivyo, wakifika huko hupata changamoto ya kukuta foleni ya wagonjwa kutoka mikoa mingine wanaokuwepo kutoka mikoa mingine.

Kuna imani pia za kishirikina ambapo watoto wengi hupelekwa kwa waganga, wakihisi labda wamelogwa, wakati hili ni tatizo la kiafya ambalo mtoto akiwahishwa anaweza akawahishwa hospitali na akapona,

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza amewaomba GSM Foundation warudi tena iringa kwani anahisi wagonjwa waliotibiwa kutoka mkoa wake ni wachache sana, ukilinganisha na idadi anayoijua ya watoto waliomo mkoani humo.

Mkuu huyo ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kwamba wanajua idadi ya wagonjwa waliomo katika wilaya zao ili waeze kuwatayarisha kwa ajili ya matibabu kabla hajawasiliana na wataalamu ili kulimaliza tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa.

PICHANI JUU: Msemaji wa GSM Foundation, Khalfan Kiwamba `Kiwadinho',(Kulia) akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Meneja wa Meneja wa Taasisi hiyo Shannon Kiwamba(Wa kwanza kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Robert Salim(wa Pili kutoka kushoto, na Kibwana Matukio kutoka GSM Foundation(Mwenye Miwani).
 Mkuu wa Mkoa wa iringa, akimjulia hali mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na Kambi tiba ya GSM Foundation.
Dk Mwanaabas Sued kutoka Taasisi ya MOI, akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Afisa Miradi kutoka GSM Foundation Kibwana Matukio(wa Kwanza kushoto) Dk John Mtei kutoka MOI,(wa Pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto).

MHE. UMMY MWALIMU AMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA IDADI YA WATU DUNIANI (UNFPA) LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) mara baada ya kufika Ofisini kwake kumuaga leo jijini Dar es salaam.Wengine alioambatana nao ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) kuhusu machapisho mbalimbali ya Umoja yanayoelezea Maendeleo ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.)akiangalia moja ya chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 alilokabidhiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (katikati) , Mwakilishi Mkazi wa UNFPA anayemaliza muda wake hapa nchini Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.


Na. Mwandishi Wetu - Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amemuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo. 

Akizungumza na mwakilishi huyo Ofisini kwake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy ameeleza kuwa Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera, miongozo na sheria mbalimbali zinazohusu usawa wa jinsia na haki za watoto hususan watoto wa Kike.

Amesema Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na UNFPA pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Tanzania.

Ameleza kuwa wizara yake itaendelea kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya watoto linalohusisha ndoa na mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti kwa watoto linamalizika katika jamii ya watanzania

Aidha,amesema kuwa wizara yake itaendelea na juhudi za kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa kuweka miundombinu na mazingira bora ya kujifungulia huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuelimisha na kuhamasisha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kuzingatia uzazi wa mpango.

Kwa upande wake Dk. Natalia Kanem ambaye alikua ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyompatia katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini na kuahidi kuendeleza kudumisha mashirikiano hayo atakapokuwa Makao Makuu ya Shirika hilo.

MKUU WA WILAYA KINONDONI,HAPI ATEMBELEA HOSPITALI MWANANYAMALA.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi alipotembelea katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.

*Abaini gharama ya kadi ya wagonjwa kupandishwa hadi 10,000/= bila kufuata utaratibu.
*Aagiza kusitishwa mara moja
*Mganga mfawidhi kuchukuliwa hatua

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi leo asubuhi amefika katika hospitali ya Mwananyamala akiambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni na mganga Mkuu wa Kinondoni. Hapi amefika hospitalini hapo na kuongoza moja kwa moja kwenye dirisha la malipo ambapo imebainika kuwa gharama za kadi ya mgonjwa zimepandishwa bila kufuata utaratibu na kufikia shilingi 10,000 kwa mgonjwa kumuona daktari.  

Hapi ameyabaini hayo licha ya taarifa ya uongo iliyotolewa na msimamizi wa dirisha la malipo kuwa wamesitisha kutoza kiasi hicho .

Mkuu huyo wa wilaya alimuagiza mtaalam wa Max Malipo kufungua kompyuta yake na kuangalia ni kiasi gani ambacho wagonjwa waliofika saa 1 asubuhi leo walitozwa. Baada ya mtaalam huyo wa Max Malipo kufungua ikabainika kuwa wagonjwa wote walitozwa shilingi 10,000/=.

"Hivi wewe dada kwanini ulikua unanidanganya? Unadhani mimi ni mjinga? Unadhani nimekuja hapa kwa bahati mbaya? Najua kila kitu mnachofanya hapa. Ndio maana nikaitwa Mkuu wa Wilaya. Usirudie kunidanganya tena..." alisema Mh Hapi.

Baada ya kuzungumza na wagonjwa walioeleza kilio chao kuwa bei za vipimo pia zimepandishwa kinyemela, mkuu wa wilaya ameagiza Mkurugenzi na mganga mkuu kupitia maamuzi yote ya upandishwaji wa gharama bila kufuata utaratibu na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili watu masikini wasishindwe kupata huduma.

"Wananchi masikini hawawezi kumudu gharama ya shilingi 10,000/= kwa kadi. Hii ni hospitali ya serikali na sio binafsi. Naagiza utaratibu ufuatwe na bei hii isitishwe kutumika mara moja. Badala yake bei ya awali iendelee. Huu ni uchonganishi mkubwa unaolenga kuwafanya wananchi waichukie serikali yao. Hatuwezi kuvumilia."

Naye Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni bwana Aron Kagurumjuli alieleza kuwa tayari amechukua hatua ya kumvua wadhifa wake mganga mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala kuanzia leo hii. Gharama mpya za daktari kuona mgonjwa zinatajwa kupandishwa kutoka shilingi 6,000 hadi 10,000/= kwa mgonjwa kuanzia tarehe 1 Ogasti mwaka huu.

Singida yazindua huduma tembezi za madaktari bingwa

$
0
0
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amezindua huduma tembezi za madaktari bingwa humo na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa.

Huduma zilizozinduliwa Wilayani Iramba katika hospitali ya Kiomboi zitahusisha huduma za za upasuaji, meno, macho, upasuaji wa mifupa, huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto, wanawake na huduma za mionzi.

Mhandisi Mtigumwe amesema matarajio ya mkoa huo ni kuwa huduma tembezi za kibingwa zitasaidia kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali kabla hayajafikia hatua ya usugu na kupunguza gharama za rufaa za wagonjwa kwenda nje ya mkoa.

“Huduma tembezi za kibingwa zitawasaidia wananchi kutambua uwepo wa huduma za kibingwa katika mkoa wa singida na kupata matibabu kwa gharama nafuu” alisema Mhandisi Mtigumwe.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. John Mwombeki akisoma taarifa ya hali ya afya Mkoa wa Singida amesema wazo la kuanzisha huduma tembezi za kibingwa limetokana na idadi kubwa ya operesheni zilizofanyika kwa mwaka 2015/2016 na pia mkutano wa wadau wa afya mkoani hapa kuafiki wazo la kuanzisha huduma hiyo.

"Kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 jumla ya operesheni kubwa na ndogo 4,836 zimefanyika katika hospitali mbalimbali mkoani hapa, aidha Idara ya macho katika hospitali ya Mkoa imefanya jumla ya operesheni kubwa na ndogo 2,020" ameongeza Dkt. Mwombeki.

Dkt. Mwombeki amesema uwepo wa madaktari bingwa 11 mkoani Singida pia umekuwa chachu ya utekelezaji wa huduma hiyo huku Mkoa ukifanya jitihada za kuazima madaktari wengine katika mikoa jirani ya Dodoma na Manyara.

Baadhi ya wagonjwa waliohudhuria katika siku ya kwanza ya zoezi hilo huku huduma hiyo ikitarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tano wilayani hapo wameeleza shauku na furaha yao ya kusogezewa huduma za kibingwa katika halmashauri zao.

"Nilikuwa naumwa jino ambalo limeota vibaya, niliambiwa nitaweza kufanyiwa operesheni katika hospitali kubwa kama Muhimbili lakini hawa madaktari wametusaidia , nimepata huduma haraka na kwa gharama nafuu, nawasihi wenzangu waje kwa wingi" amesema Bi Neema Josseph Mkazi wa Kijiji cha Kizaga Wilayani Iramba.

Naye Mzazi wa mtoto Jonas Masaka amesema huduma za kibingwa zitamsaidia mtoto wake mwenye matatizo ya macho na hiyo kumpunguzia gharama ya kumpeleke katika hospitali kubwa kutibu tatizo la macho linalomsababisha mtoto huyo kushindwa kusoma vizuri.


Huduma ya tembezi za kibingwa Mkoani Singida zitafanyika katika Wilaya zote tano za Mkoa nwa Singida na hvyo kupunguza wagonjwa wa rufaa watakaopelekwa hospitali za Bugando, KCMC na Muhimbili.

Madaktari Bingwa waendelea kuwahudumia wananchi Singida

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa Iramba waliojitokeza siku ya siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa.
. Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akihutubiwa wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma tembezi za madaktari bingwa Mkoani Singida.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida John Mwombeki akisoma taarifa ya hali ya afya Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa huduma tembezi za kibingwa
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho akimhudumia mteja siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Meno akimhudumia mteja siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amezindua rasmi huduma tembezi za madaktari bingwa Mkoani Singida, na kuwasihi wananchi Mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa. 

Huduma hizo za kibingwa zilizozinduliwa Wilayani Iramba katika hospitali ya Kiomboi zitahusisha huduma za kibingwa za upasuaji, meno, macho, upasuaji wa mifupa, huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto, wanawake na huduma za kibingwa za mionzi. 

Mhandisi Mtigumwe amesema matarajio ya Mkoa ni kuwa huduma tembezi za kibingwa zitasaidia kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali kabla hayajafikia hatua ya usugu na kupunguza gharama za rufaa za wagonjwa kwenda nje ya mkoa. 

'Huduma tembezi za kibingwa zitawasaidia wananchi kutambua uwepo wa huduma za kibingwa katika mkoa wa singida na kupata matibabu kwa gharama nafuu' amengeza Mhandisi Mtigumwe. 

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki akisoma taarifa ya hali ya afya Mkoa wa Singida amesema wazo la kuanzisha huduma tembezi za kibingwa limetokana na idadi kubwa ya operesheni zilizofanyika kwa mwaka 2015/2016 na pia mkutano wa wadau wa afya mkoani hapa kuafiki wazo la kuanzisha huduma hiyo. 

"Kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 jumla ya operesheni kubwa na ndogo 4,836 zimefanyika katika hospitali mbalimbali mkoani hapa, aidha Idara ya macho katika hospitali ya Mkoa imefanya jumla ya operesheni kubwa na ndogo 2,020" ameongeza Dokta Mwombeki. 

Dokta Mwombeki amesema uwepo wa madaktari bingwa 11 mkoani Singida pia umekuwa chachu ya utekelezaji wa huduma hiyo huku Mkoa ukifanya jitihada za kuazima madaktari wengine katika mikoa jirani ya Dodoma na Manyara. 

Baadhi ya wagonjwa waliohudhuria katika siku ya kwanza ya zoezi hilo huku huduma hiyo ikitarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tano wilayani hapo wameeleza shauku na furaha yao ya kusogezewa huduma za kibingwa katika halmashauri zao. 

"Nilikuwa naumwa jino ambalo limeota vibaya, niliambiwa nitaweza kufanyiwa operesheni katika hospitali kubwa kama Muhimbili lakini hawa madaktari wametusaidia , nimepata huduma haraka na kwa gharama nafuu, nawasihi wenzangu waje kwa wingi" amesema Bi Neema Josseph Mkazi wa Kijiji cha Kizaga Wilayani Iramba. 

Naye Mzazi wa mtoto Jonas Masaka amesema huduma za kibingwa zitamsaidia mtoto wake mwenye matatizo ya macho na hiyo kumpunguzia gharama ya kumpeleke katika hospitali kubwa kutibu tatizo la macho linalomsababisha mtoto huyo kushindwa kusoma vizuri. 

Huduma ya tembezi za kibingwa Mkoani Singida zitafanyika katika Wilaya zote tano za Mkoa nwa Singida na hvyo kupunguza wagonjwa wa rufaa watakaopelekwa hospitali za Bugando, KCMC na Muhimbili.
 

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MISITU KIHOLELA

$
0
0
Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongoakitoa ufafanuzi leo, Mpingo House jijini Dare Salaam, kuhusu upigaji marufuku usafirishaji wa magogo ya miti kwenda nje ya nchi, magari kubeba mbao yakiwa yamefunikwa, pikipiki na baiskeli kubeba mkaa kwenda sehemu moja hadi nyingine mijini na vijijini. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo (Kulia) wakizungumza na Waandishi wa habari leo, Mpingo House jijini Dare Salaam, kuhusiana na utaratibu kusafirisha mazao ya misitu ikiwemo mkaa ambapo mfanyabiashara anayefanya biashara hiyo, atapaswa kuwa na vigezo ambavyo Serikali inavihitaji, tofauti na hapo sheria itachukua mkondo wake

……………………………………………………………………

WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) imepiga marufuku usafirishaji wa mazao ya misitu ikiwemo mkaa ambapo mfanyabiashara anayefanya biashara hiyo, atapaswa kuwa na vigezo ambavyo Serikali inavihitaji, tofauti na hapo sheria itachukua mkondo wake.

Imesema zuio hilo linakwenda sambamba na kupiga marufuku usafirishaji wa magogo ya miti kwenda nje ya nchi, magari kubeba mbao yakiwa yamefunikwa, pikipiki na baiskeli kubeba mkaa kwenda sehemu moja hadi nyingine mijini na vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, alisema uamuzi huo ni moja ya mikakati ya kukusanya maduhuli stahiki ya rasilimali za misitu na kuwabana wakwepa ushuru.

Alisema moja ya majukumu ya TFS, ni kuhakikisha inaanzisha na kusimamia rasilimali za misitu ili zisaidie ustawi wa taifa kwa kizazi cha sasa na kijacho, hivyo ni lazima wananchi wafahamu kuwa ni kosa kuvuna hovyo misitu na bidhaa zake bila kibali.

Mtendaji huyo alisema kila zao linalotokana na misitu ni lazima lilipiwe ushuru stahiki na kukatiwa risiti, hivyo kukwepa kufanya hivyo kwa kutumia njia mbalimbali zinazokatazwa ni kuvunja sheria na kuiibia serikali mapato.

“Mazao ya misitu, ikiwemo mikaa ni kosa kuuzwa na kusafirishwa bila kuwepo kibali na risiti. Muuza mkaa lazima uwe na risiti, na wewe mnunuzi tukikukamata na gunia la mkaa na huna risiti utawajibika.

“Tunataka kuhakikisha maduhuli ya mazao ya misitu yanakusanywa ili kupata matumizi endelevu ya rasilimali za misitu hivyo ni biashara hii ya miti, mkaa na mazao ya nyuki inatakiwa iwe wazi.

“Ni marufuku kusafirisha mazao ya misitu usiku, kama mtu ana vigezo vyote tunavyovihitaji kusafirisha mazao ya misitu anatakiwa kusafiri kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni, ikipita hapo, weka pembeni gari mpaka asubuhi,” alisema.

Aidha alisema TFS chini ya Wizara ya Maliasili ina Meneja miti kwenye kila wilaya, ambao wanafanya kazi kwa karibu na Maofisa Watendaji wa vijiji ambao hushirikiana kutoa vibali kwa kuvuna miti stahiki kisheria na kutoa risiti.

Alisema risiti hizo pamoja na vigezo vingine ikiwemo kuwa na usajili wa TFS, leseni ya biashara na namba ya utambulisho wa mfanyabiashara (TIN), hati ya kusafirisha mazao ya misitu humfanya mfanyabiashara kuruhusiwa kuendelea na biashara ya mazao ya miti nchini.

Profesa Silayo alisema TFS wataendelea na majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipozungumza na watumishi wa wizara hiyo mapema mwezi uliopita.

Baadhi ya maagizo hayo likiwemo la kupunguza vizuio kwenye maeneo mbalimbali ya nchi, Silayo alisema wanafanya utafiti kujua kizuizi gani kitolewe na kipi kibaki sambamba na kubana uvunaji holela wa misitu.

Alisema lengo lao si kukamata magogo baada ya kuvunwa bali ni kuzuia misitu isiharibiwe hivyo inapotokea, hutumia vizuio hivyo kukagua na kukamata nyara hizo za serikali ili kuongeza maduhuli kwa mujibu wa sheria.

“Tumeanza kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, ambayo kiuhalisia yana ukweli mkubwa kwa hiyo tunataka kuondoa vizuizi visivyo na tija lakini pia kuwasisitizia watu wetu kule vituoni kuzingatia weledi.

“Tayari tumeanza kutumia mashine za kielektroniki za malipo yaani EFD kwenye vizuio vyetu mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro na tutaendelea kuzisambaza maeneo mengine mara tu TRA watakapoziingizia program yao ya malipo,” alisema.

Alisema wana changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa vitendea kazi hususan magari lakini wanafanya jitihada mbalimbali kuhakjikisha wanazitatua ili misitu iwe na mchango kwenye pato la taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali Misitu wa TFS, Mohammed Kilongo, alisema kitakwimu asilimia 94 za kaya zote takriban milioni tisa nchini zinatumia mkaa kama nishani kuu, huku maeneo ya mijini pekee ikiwa na asilimia 38 za watumia mkaa.

“Mahitaji ya miti ni mita za ujazo 62.3 huku uwezo ukiwa ni mita za ujazo 42.8 hivyo uharibifu wa misitu unafika hekta 372,000 kwa mwaka sawa na asilimia 1.1 ya eneo lote lenye miti,” alisema Kilongo.

Alisema kwa takwimu hizo, miti na misitu nchini imekuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa na kusababisha uhitaji wa hekta mpya 185,000 za misitu inayotakiwa kupandwa maeneo mbalimbali ya nchi.

“Upungufu huu ni kichocheo cha uvunaji haramu na holela ndani ya misitu ya hifadhi, mapori ya akiba na hata ndani ya hifadhi za taifa hivyo suala la kuilinda ni jukumu letu sote, kila gunia lazima lilipiwe ushuru,” alisema.

Pia alisema katika jitihada za kurudisha misitu iliyopotea, upo mkakati wa kitaifa wa kupanda miti ambapo kwa kila wilaya imepewa jukumu la kupanda miti milioni moja na nusu kwa mwaka chini ya uangalizi wa Meneja misitu wa wilaya husika.

Wiki kadhaa zilizopita, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam, alisema nchi inageuka jangwa kutokana na misitu mingi kukatwa kiholela huku maduhuli ya serikali yakipotea.

Kauli hiyo inaonekana kuanza kuzaa matunda baada ya TFS kuamua kuongeza kasi ya usimamizi wa rasilimali za misitu na nyuki nchini kwa siku za hivi karibuni hatua ambayo inadaiwa kuwa endelevu.

TFS inasimamia jumla ya misitu 506 nchini ikiwemo ya asili na kupandwa, pamoja na kusimamia jamii takriban milioni 9.2 za nyuki walioko kwenye misitu hiyo maeneo mbalimbali ya nchi.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA UFAFANUZI WA HABARI ILIYOANDIKWA NA GAZETI LA JAMHURI "PROF MUHONGO AVURUNDA"!

$
0
0


Tunapenda kutoa maelezo kutokana na taarifa iliyotolewa katika gazeti la Jamhuri la Jumanne tarehe 16 – 22, 2016. Toleo na. 255 iliyokuwa na kichwa cha habari Prof. Muhongo avurunda.

Watanzania na Taifa kwa jumla wanashuhudia jinsi Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Muhongo na viongozi wengine wote wa Wizara ya Nishati na Madini wanavyofuatilia majukumu yao kwa karibu ikiwemo sekta ya mafuta. Mhe. Prof. Muhongo na viongozi wa Wizara wamekuwa wakitoa miongozo na maelekezo juu ya sekta ya mafuta ambapo kumeendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta nchini kwa wakati wote. Ni imani yetu kuwa Mhe. Prof. Muhongo ataendelea kutekeleza majukumu yake vizuri na hivyo kuendelea kutimiza matumaini ya Mhe. Rais na Taifa kwa jumla katika mambo yote yanayohusu wizara ya nishati na madini ikiwemo sekta ya mafuta.

Tunapenda pia kueleza kuwa maagizo yote aliyotoa kuhusiana na mafuta ya ndege yaliyokuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli yalitekelezwa kwa ukamilifu. Maagizo hayo yalikuwa ni Kampuni ya Sahara kuondoa mafuta yaliyochanganyika kutoka katika maghala na mabomba na pia kusafisha maghala na mabomba hayo ili kuwezesha kupokea mafuta mengine safi. Kampuni ya Sahara ilitekeleza kwa ukamilifu maagizo haya. Usimamizi wa maagizo haya ulikuwa kwa PBPA na EWURA ambapo taasisi hizi zilisimamia utekelezaji wake. Hivyo si kweli kwamba Prof. Muhongo ameshindwa kusimamia maagizo yake.

Zuio la Kampuni ya Sahara kushiriki katika zabuni lilitolewa na PBPA kwa kutumia mamlaka yaliyo katika Kanuni. Zuio hili lilitolewa na PBPA ili kuhakikisha mafuta yaliyochanganyika yanaondolewa katika maghala na kusafishwa kwa maghala hayo na mabomba ikiwa ni pamoja na kukamilishwa kwa uchunguzi ili kutambua kuwa mafuta haya yalichanganyika sehemu gani. Ifahamike kuwa mara baada ya meli iliyokuwa imeleta mafuta haya (mafuta ya ndege na mafuta ya petroli) kufika hapa, mafuta hayo yalipimwa na TBS. 

TBS walithibitisha kuwa mafuta yote katika meli hii yako katika kiwango cha ubora unaotakiwa. Aidha, TBS walitoa idhini ya kuteremshwa kwa mafuta hayo. Meli ilianza kuteremsha mafuta haya tarehe 4/5/2016 na kumaliza kuteremsha tarehe 8/5/2016. Meli hii iliruhusiwa kuondoka mara baada ya kumaliza kupakua mafuta na taratibu zote kukamilika. Taarifa ya kuchanganyika kwa mafuta haya ilitolewa tarehe 12/5/2016 wakati meli tayari ilikuwa imekwishaondoka. Hivyo kulazimu kufanyika uchunguzi wa kujua ni wapi mafuta haya yalichanganyika.

Suala la uchunguzi wa wapi mafuta yalichanganyika lilikataliwa na makampuni ya mafuta kama ilivyokuwa imependekezwa na kampuni ya Sahara. Makampuni ya mafuta yalisimamia katika taarifa ya uchunguzi ya awali iliyofanywa na pande zote husika. Taarifa hii ilikuwa na mapendekezo tofauti kati ya makampuni ya mafuta na kampuni ya Sahara. Hivyo, kwa kuzingatia hatua hii kilichokuwa kimebakia ni kufuata mkataba kati ya pande mbili hizi.

Kuondolewa zuio la Kampuni ya Sahara kushiriki katika zabuni kulitolewa pia na PBPA kwa kutumia mamlaka yaliyo katika Kanuni. Hii ilikuwa ni baada ya kuhakikisha kuwa mafuta yaliyochanganyika yameondolewa, usafi wa maghala na mabomba umefanyika na kampuni ya Sahara imelipa thamani ya mafuta yote yaliyoondolewa katika maghala.

Sheria ya Petroli (Petroleum Act, No. 21) ya mwaka 2015 imetoa adhabu kwa yule atayaleta mafuta ambayo hayakidhi viwango vya vya ubora unaotakiwa. Aidha, Kanuni ya uagizaji wa mafuta kwa pamoja (The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations) ya mwaka 2015 nayo imetoa adhabu juu ya kosa la kuleta mafuta yasiyokidhi viwango vya ubora. Kutokana na mazingira haya ya adhabu katika kosa tajwa, PBPA iliomba kupata mwongozo kutoka katika Mamlaka za kisheria ili kuhakikisha kuwa adhabu inayotolewa iko katika misingi sahihi ya ki-sheria.

Ni vyema ikafahamika kuwa hakuna sehemu ambapo PBPA imedanganya Taifa. Ni kweli kabisa kuwa Sheria, Kanuni na Mikataba inaeleza juu ya mafuta yaliyoletwa na kukutwa hayajafikia viwango vya ubora unaotakiwa. Mafuta haya hayateremshwi na hutakiwa kurudishwa na yule aliyeyaleta, ikiwa ni pamoja na kutekelezwa kwa taratibu zingine kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Mkataba. Lakini, Sheria, Kanuni na Mkataba havina sehemu inayoeleza juu ya mafuta yaliyofika, yakapimwa na kuthibitika kuwa yako katika viwango vya ubora unaotakiwa, yakaruhusiwa kuteremshwa, meli ikaoondoka na baadae kutambulika kuwa mafuta yaliyo katika maghala yamechanganyika.

Suala la ubora wa meli hushughulikiwa na TPA. Taarifa za meli inayotakiwa kuleta mafuta hutumwa TPA ambao huthibitisha kama meli hiyo inaruhusiwa au hairuhusiwi kuingia katika bandari zetu zinazotumika kuteremsha mafuta.

Hitimisho, ni vyema ikafahamika kuwa utaratibu wa uagizaji mafuta kwa pamoja hapa nchini umeanza tangu 2011. Utaratibu huu umekuwa na mafanikio makubwa, hasa ikizingatiwa kuwa umejengwa katika misingi ya uwazi na ushirikishwaji. Nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikifika kujifunza kwetu. Aidha, hata taasisi zingine ndani ya nchi yetu ziko katika kutekeleza manunuzi yao kwa kutumia utaratibu unaotumiwa na PBPA. Hii ni baada ya kujifunza kutoka PBPA. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani wadau mbali mbali wanaona mafanikio ya utaratibu huu.

PBPA inapenda kuufahamisha umma kuwa itaendelea kusimamia uagizaji wa mafuta kwa pamoja kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu. Shughuli hizi zitafanywa kwa uwazi zaidi na kushirikisha wadau wote wanaohusika. Tutabuni njia mbali mbali ili kuwezesha makampuni ya Watanzania kuweza kushiriki katika biashara ya mafuta. Tunaamini kuwa tutaungwa mkono na watu wote ili kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Imetolewa na

Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji
Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA)
DAR ES SALAAM

TIC YATEMBELEA NA KUKAGUA SHUGHULI ZA UWEKEZAJI WA MAKAMPUNI NCHINI

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akisikiliza na kuandika maelezo ya Pastory Mroso Meneja Mkuu wa Mlimani City Group wakati alipotembelea mradi mpya wa ujenzi wa kumbi mpya za mikutano na kujionea maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi huyo amefanya ziara hiyo ili kuona maendeleo na shughuli za uwekezaji wa kampuni hiyo nchini hapa nchini ili kutambua changamoto na mafanikio yaliyopo katika uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, waliosimama nyima kutoka kushoto ni Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC , Phina Lyimo Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Veronica Mrema Afisa Uhamasishaji na Uwekezaji TIC.
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kituo hicho kutoka kulia ni Phina Lyimo Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Veronica Mrema Afisa Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC wakati Kaimu Mkurugenzi huyo alipotembelea ujenzi wa kumbi mpya za Mlimani City.
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akiteta jambo na Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC leo alipotembelea na kukagua ujenzi kumbi mpya za Mlimani City.Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akionyeshwa picha ya kumbi mpya za Mlimani City zinazoendelea kujengwa hazipo pichani na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mlimani City Group Pastory Mroso wakati alipotembelea mradi huo ili kuona maendeleo ya uwekezaji wa kampuni hiyo nchini.
Meneja Bidhaa Mwandamizi wa Kampuni ya Super Doll .inayotengeneza matela ya maroli iliyo chini ya kampuni mama ya Super Star Group Bw. Ibrahim Juma akiwaelezea wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wakati walipoitembelea kampuni hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ili kuona tija na changamoto za uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, Ziara hiyo iliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC.
Meneja Bidhaa Mwandamizi wa Kampuni ya Super Doll .inayotengeneza matela ya maroli iliyo chini ya kampuni mama ya Super Star Group Bw. Ibrahim Juma akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wakati walipoitembelea kampuni hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ili kuona tija na changamoto za uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, Ziara hiyo iliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images