Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Mwenyekiti wa NEC amtembelea Spika Wa Bunge JoB Ndungai amjulia hali,amkabidhi ripoti ya uchaguzi mkuu wa Rais

$
0
0
 
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva  (kushoto) akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhi  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.Picha na Benjamin Sawe-Maelezo

By Christina Njovu.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai nyumbani kwake  Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.

Akiwa nyumbani  kwa  spika Jaji Lubuva pia amemkabishi  Mh. Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani  ya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao. 

Kwa upande wake Mheshimiwa Ndugai ameipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo yale ya biashara SabaSaba na Nanenane katika kutoa elimu kwa wananchi.

Jaji Mstaafu Lubuva alikwenda kumjulia hali Ndugai ambaye kipindi  cha Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa matibabu  na hivi sasa afya yake imezidi kuimarika.  

WATU WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUGUSHI VYARAKA MBALIMBALI ZA IDARA YA AFYA.

$
0
0
 Baadhi ya vyeti vya kugushi vilivyokamatwa
Mihuri iliyokamatwa katika tukio hilo. 
 Kompyuta mpakato,Laptop,Printer na Scarner pamoja na mihuli  ni vifaa vilivyokamatwa katika Steshanari hiyo.

 RPC MTUI akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa ofisini kwa RPC Mtui wakipata maelezo kuhusiana na tukio hilo.


Na,Abel Daud-
KIGOMA,

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma kwa kushirikiana na wataalamu kutoka baraza la Famasia linawashikiria watu watano kwa tuhuma za kugushi vyeti mbalimbali vya idara ya afya,ambavyo vinasadikika kutumiwa kufanya kazi katika sekta ya afya.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo hii Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi wa Polisi FERDINAND MTUI,amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambapo amebainisha kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na MGENI NYABUZOKI mzanaki mwenye umri wa miaka 52 ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania mkazi wa mlole ambaye ndiye mmiliki wa stationary inayotumika kutengeneza vyeti hivyo vya kugushi.

Kamanda Mtui ameongeza kuwa wengine walio kamatwa katika tukio hilo ni pamoja na Dikson Mshahilizi (47),ambaye ni muuguzi katika Hospital ya rufaa Maweni,mkazi wa Air pot,Zawadi James  (42) muuguzi katika kituo cha afya Ujiji, mkazi wa Kazegunga Stephano Erasto (18) mkazi wa mlole na mwanafunzi wa shule ya sekondary mlole pamoja na Jonson Nyabuzoki ,ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Mlole na mtaalamu wa kutumia Kompyuta mpakato katika kutengeneza vyeti hivyo.

Kwa upande wake Mratibu wa maduka ya dawa muhimu baraza la Famasi Taifa Domick Mfoi ,amesema kuwa kutokana na huduma inayotolewa na watu ambao hawakupitia mafunzo katika sekta ya afya inapelekea madhara makubwa ya vifo kwa umma,kwani huduma watakayoipata haitaendana na huduma sitahiki kwa mgonjwa.

Ameongeza kuwa katika kudhibiti hali hiyo msako na uchunguzi wa kina utaendelea kufanyika ili kubaini kama kuna watu wengine wanaofanya kazi katika vituo mbalimbali vya afya hapa nchini.

MADAWATI 150 YAPATIKANA KUPITIA TAMASHA LA DAWATI, DAR LIVE JIJINI DAR

$
0
0
TAMASHA la wasanii wa kizazi kipya la kuchangia madawati limefanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live Mbagala ambapo jumla ya madawati 150 yamepatika.

Tamasha hilo liliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe ‘Double G’ ambapo  aliwashukuru wasanii hao kwa kujitokeza kusapoti upatikanaji wa madawati kwa watoto wa Handeni ambao ni moja ya changamoto zinazokabili Wilaya yake ukiachilia ile ya Maji.

Wasanii waliojitokeza kuunga mkono juhudi za Mkuu huyo wa Wilaya ya Handeni walisema wameamua kumsapoti Gondwe kwa kuwa wanamfahamu muda mrefu toka akiwa mtangazaji wa radio na alikuwa akiwasapoti kazi zao kwa kiasi kikubwa.


Ben Paul alisema “Wasanii kama wasanii tunatakiwa tusaidie jamii yetu kama hivi, naishi kwenye jamii hivyo naona matatizo mengi yanayokabili jamii yetu ni wajibu wangu kutumia nafasi hii kusaiii, karne hii wadogo zetu bado wanakaa chini, tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kumaliza tatizo hilo.”alisema Ben Paul anayetamba na Wimbo wake wa sasa  wa ‘Moyo Mashine’ na kuongeza.

“Vijana wa sasa wanapenda kushinda kwenye mitandao ya kijamii na kulalamikia serikali, wanataka serikali ndio iwafanyie kila kitu wakati sisi hatufanyii jambo serikali.”alisema.

Msanii nguli, Ambwene Yesaya ‘Ay’ akizungumzia tamasha hilo alisema “Double G kwanza kabisa ni mtu wa watu, ndio maana wasanii wote unaotuona hapa tumeamua kumsapoti bure kabisa, alivyotueleza wazo lake tukamwambia ni zuri na tutamsapoti, alichokifanya ni kitu kizuri ambacho kinatakiwa kiigwe na kila mtu.
“Itakuwa vizuri kila mtu akaweka nia ya kusaidia sio lazima tutengeneze madawati tunaweza tukafanya siku ya kuotesha miti ambayo naamini kila msanii akiotesha mti mmoja leo, utakuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo.”alisema Ay.

Aidha mwandaaji wa tamasha hilo Godwin Gondwe alisema kuwa Wilaya yake inakabiliwa na uhaba wa madawati 530 na anashukuru kwa kupata madawati 150 katika fedha zilizopatikana kwenye tamasha hilo la Wasanii hna kwamba bado ana upungufu wa madawati 380.

“Nawashukru sana wasanii waliojitoa kunisapoti, na wakazi wa Wilaya ya Temeke kujitokeza kumuunga mkono Rais wetu ili kutengeneza historia  za wadogo zao wasikae chini tena, na katika tamasha hili tumeweza kukusanya fedha ambazo zitatuwezesha kupata madawati 150.”alisema Gondwe.
Katika tamasha hilo, muitikio wa watu ulikuwa mkubwa na lilipendezeshwa na wasanii mbalimbali. Walioanza kufanya makamuzi mwanzoni mwa tamasha hilo ni pamoja na Bendi ya La Musica Vijana Classic, Mc wa Dar Live Brighton ‘Dalada’ na wengine wengi.

Baada ya shoo kunoga mashabiki wa Dar Live walifurahia muziki mzuri kutoka kwa Bendi ya Injili ya GWT (Glorious Worship Team), Mfalme wa Muziki wa Uswazi maarufu kama Singeli Msaga Sumu, Sterio, Ben Pol, Linex huku Fid Q, AY, Msami na Barnaba wakikamilisha listi kwa makamuzi ya nguvu.

Baada ya wasanii wote kutoa burudani ya nguvu, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ‘Double G’ aliwashukuru wote waliomuunga mkono na akaomba waendelee kujitolea zaidi kwenye masuala ya kujenga taifa.

TUKIO LA MAZISHI YA MZEE ABOUD JUMBE HUKO NYUMBANI KWAKE MIEMBENI ZANZIBAR

$
0
0

Aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mmapinduzi ya Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) MaalimSeif Shariff Hamad akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa walipohudhuria Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alhaji Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa walipohudhuria Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa walipohudhuria Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Viongozi wastaafu wakifuatilia shughuli ya Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud ukishushwa kaburini.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Gharib Bilali akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.
Aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mmapinduzi ya Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) MaalimSeif Shariff Hamad akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Mazishi wakiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe leo Mjini Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Mohamed Aboud Mohamed akisoma wasifu wa Marehemu Mzee Aboud Jumbe wakati wa Mzishi yaliyofanyika Nyumbani kwake Mjini Zanzibar.

Sheikh akisoma Duaa Mara baada ya kuuhifadhi Mwili wa Mzee Aboud Jumbe

Mtoto Mkubwa wa Marehemu Bw. Mustafa Aboud Jumbe akitoa shukrani kwa viongozi wa serikali na wananchi waliojitokeza katika kumuaga Mzee Aboud Jumbe na kuishukuru serikali kukubali kuiruhusu familia kufanya taratibu za mazishi kama alivyoelekeza Marehemu Mzee Aboud Jumbe wakati wa uhai wake.

Picha na Hassan Silayo


Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ukaguzi wa kushtukiza kituo cha CHESA

$
0
0


Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu akiwa pamojana wasaidizi wake wakifanya upekuzi katika ofisi za kituo hicho cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA), Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla.Upelelezi na Upekuzi ukiendelea ndani ya kituo hicho.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo na kuwaonyesha moja ya makablasha (file) zilizokutwa hapo ilikusadia uchunguzi kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA).Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo na kuwaonyesha moja ya makablasha (file) zilizokutwa hapo ilikusadia uchunguzi kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA)Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimweleza jambo Bwana John Kashiha wakati wa tukio hilo..Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya nyaraka za taasisi za kituo hicho
Upekuzi ukiendelea..Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha moja ya kijarida kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA).Upekuzi ukiendelea.. katika ofisi hizo. 


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo Upanga, Wilayani Ilala, jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo ya kushtukiza inafuatia baada ya hatua ya Naibu Waziri huyo wa Afya Dk.Kigwangalla kuendelea kufanya ukaguzi wa Asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zikiwemo NGO’s na CBO zenye makosa ya kiutendaji na kimfumo ambayo ni tofauti na taarifa zao katika usajili wa Serikalini na namna ya uendeshaji wa wao.

Mbali na hayo kituo hicho cha CHESA kinashukiwa kuhusika na vitendo vya uhamasishaji wa mahusiano ya mapenzi ya Jinsia moja (USHOGA), ambayo ni kinyume na mila na Desturi za kitanzania pamoja na Katiba na sharia za Nchi.

“Mahusiano ya jinsia moja si kinyume na mila na desturi zetu tu. Bali hata sheria na katiba ya nchi yetu haziruhusu mfumo huo wa kimahusiano” amesema Dk..Kigwangalla

Aliendelea kubainisha kuwa : “Sisi kama Serikali hatujawahi kusaini mikataba yoyote ya kimataifa inayoruhusu ushoga hivyo kwa taasisi yoyote hapa Nchini inayofanya hivyo ni kuvunja sheria za Nchi na inapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria na hata kufutiwa usajili wake” aliongeza Dk. Kigwangalla.

Katika ukaguzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara anayoiongoza, Bw. Julius Mbilinyi pamoja na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Hassan Selengu pia wamefanya ukaguzi katika kituo hicho ili kubaini kama kuna uwepo wa vilainishi vinavyotumiwa na watu wenye mahusiano ya jinsia moja ambavyo hivi karibuni Serikali ilipiga marufuku matumizi yake hapa nchini.

“Serikali ilikifuta kituo cha ‘SISI KWA SISI’ kwa sababu kilihusika na tuhuma za ushawishi wa mahusiano ya jinsia moja ambacho pia wewe ulikuwa Mkurugenzi wake. Sasa tumeamua kuchunguza na kituo hichi ili tujue kama mnahusika na vitendo hivyo ili tuchukue hatua endapo itabainika ama la” ameeleza Dk. Kigwangalla.

Aidha, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amemtaka Mkuu wa upepelezi Bwana Hassan Selengu afanye uchunguzi wa kina katika kituo hicho ili kubaini pesa za misaada katika kituo hicho zinatokea wapi lakini pia ni kubaini kama kituo hicho kinajihusisha na ushawishi wa watu kujiunga na mahusiano ya jinsia moja.

“Tunawasiwasi kuwa mnapokea pesa nyingi na misaada mingi kutoka katika Taasisi mbalimbali lakini pesa hizo zinatumika kuhamasisha mapenzi na mahusiano ya jinsia moja.

Mbali na hayo. taarifa za usajili wa kituo hichi zinakinzana na malengo na miradi inayofanyika hapa. Pia ipo miradi mbalimbali ambayo haijasajiliwa wala hujaitaja katika maelezo yako lakini inafanyika katika kituo hichi” alihoji Dk. Kigwangalla huku akimtajia baadhi ya miradi hiyo ambayo Serikali inaitambua.
 
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).

Tazama hapa MO TV, kuona tukio hilo:

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamis Kigwangalla akiwasili katika ofisi za kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo Upanga, Wilayani Ilala, jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiandika maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA) Bw. John Kashiha wakati alipotembelea katika kituo hicho chenye maskani yake Upanga, Ilala, Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 15.2016Mkurugenzi wa kituo COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA) Bw. John Kashiha akielezea miradi mbalimbali ya kituo hicho kwa Naibu Waziri. (Hayupo pichani).Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA).

Mhe. Samia Suluhu Hassan: Mzee Jumbe alikuwa baba wa Maendeleo na Baba wa Demokrasia.

DC MTATURU: SERIKALI IPO TAYARI KUCHUKIWA NA WAVIVU

$
0
0
Dc Mtaturu (Kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa APEC Respicius Timanywa zawadi ya kuku iliyotolewa na wahitimu wa mafunzo hayo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza juu ya umuhimu wa mafunzo ya usalama barabarani.
Dc Mtaturu akionyesha kuku aliyokabidhiwa kama zawadi baada ya kukubali kuwa mgeni rasmi  wakati wa kufunga mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani wakionyesha alama za barabarani walizozichora wao wenyewe kwa ajili ya kuashiria kuelewa mafunzo waliyopatiwa
Baadhiya Bodaboda za washiriki zikiwa zimepaki bila kufanya kazi ya kubeba abiria ambapo wamiliki walikuwa kwenye mafunzo

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya waendesha pikipiki.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kupunguza umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa akiwashukuru washiriki wote wa mafunzo hayo

Na Mathias Canal, Singida

Serikali imeeleza kuwa ipo tayari kuchukiwa na wananchi wavivu wasiotaka kujishughulisha na Ujasiriamali, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Biashara ili kukuza pato la kaya zao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kufunga mafunzo ya usalama Barabarani kwa Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa Wilaya ya Ikungi yaliyohusisha Kata ya Issuna na na Kata ya Mkiwa na kufanyika JMC Hotel Kijijini Issuna B.

Katika mafunzo hayo yaliyochukua siku sita yamewakutanisha pamoja waendesha Bodaboda 84 ambao wamefundishwa Alama na sheria zote za usalama Barabarani, Upatikanaji wa leseni, Faida za kulipa kodi na somo la ujasiriamali, Polisi jamii, Ulinzi shirikishi na elimu juu ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukosefu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).

Akiwahutubia wananchi hao Mtaturu amemshukuru Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ajira ya pikipiki kwani kwa kiasi kikubwa imesaidia kupunguza uhalifu na kuandaa ajira kwa vijana wengi nchini hivyo kuachana na kujihusisha na mambo yasiyo na tija kwa jamii ikiwemo kushinda vijiweni.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la APEC yatasaidia kupunguza ajali za pikipiki zinazosababishwa na uzembe wa baadhi ya waendesha pikipiki katika Wilaya zote za Mkoa wa Singida.

Dc Mtaturu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha madereva Bodaboda waliokwepa mafunzo ya awamu hii wanasajiliwa ili wahudhurie mafunzo yatakayorudiwa kwa awamu ya pili kwa Wilaya nzima, hivyo kwa wale ambao hawatapata mafunzo hawataruhusiwa kuendesha pikipiki zao ili kuepusha ajali mpaka pale watakapopata mafunzo.

“Dereva bila elimu ni sawa na bunduki bila risasi, hivyo nakuagiza mkuu wa Polisi kutowakamata kwa kosa la kutokuwa na leseni angalau kwa kipindi cha miezi miwili wakati wanafuatilia leseni zao”  Alisema Mtaturu

Akizungumzia kuhusu alama za barabarani Mtaturu alisema kuwa tayari ameshamwagiza Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri kufanya mawasiliano na wakala wa barabara katika maeneo yote ambapo alama za barabarani hazipo.

Ili kuvunja makusudi makusudi ya kuvunja sheria Mkuu huyo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) amuelekeze mkuu wa Trafiki Wilaya (DTO) ambapo alisema kuanzia leo kila dereva wa pikipiki anapaswa kutembea na kivuli cha cheti na leseni. 

Akisoma risala iliyoandaliwa na wahitimu wa mafunzo ya udereva wa pikipiki Kata ya Mkiwa na Issuna Yohana Chawenda amezitaja changamoto zinazowakabili waendesha bodaboda hao kuwa ni pamoja na kukabwa na kuibiwa pikipiki zao, Upatikanaji wa leseni, baadhi ya abiria kukataa kuvaa kofia ngumu, Baadhi ya waendesha pikipiki kukataa kushiriki mafunzo ya usalama barabarani, Baadhi ya wananchi kuharibu alama za barabarani na Baadhi ya maafisa wa usalama Barabarani kusimamisha pikipiki sehemu isiyo rasmi jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kupunguza umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa, amesema kuwa lengo la Taasisi hiyo kutoa mafunzo hayo ni kupunguza ajali na kuwaandaa vijana kujihusisha na ujasiliamali wa uendeshaji wa Bodaboda huku wakiwa katika hali ya usalama.

Timanywa amesema kuwa mafuzno hayo yataendelea katika maeneo mengine ili kutoa fursa kwa watanzania wote wanaopenda kushiriki kwa ajili ya kujifunza kwa manufaa ya leo na kesho.

Zaidi sana amesema kuwa mafunzo hayo pia yamelenga kuwafanya vijana waweze kumiliki fursa kubwa na kutengeneza faida kubwa iliwaweze kulipa ushuru na kodi za serikali.

MKUU WA MAJESHI MKUU WA MAJESHI JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE, AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA CANADA OFISINI KWAKE, NGOME JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, akimkabidhi zawadi ya nembo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ), Waziri wa Ulinzi wa Canada,
Harjit Singh Sajjan,mara baada ya mazungumzo yao makao makuu ya jeshi Ngome, Upanga jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. (PICHA NA JWTZ) .



TAZAMA PICHAZA SHEREHE YA HARUSI YA MASANJA MKANDAMIZAJI

$
0
0
Muigizaji Maarufu wa sanaa ya vichekesho kutoka kundi la Orijino Komedi, Emmanual Mgaya a.k.a Masanja Mkadamizaji akishuhudia sebene babkubwa lililokuwa likiporomoshwa na Mkewe Bi. Monica Masatu alikuwa sambamba na Muigizaji mwenzake katika kundi hilo, Isaya Mwakilasa a.k.a Wakuvwanga, katika hafla ya Ndoa yao iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Primrose, jijini Dar es salaam.Picha zote na Joseph a.k.a Kasampaidadaily
Moja ya vitu vilivyowavutia watu wengi walioalikwa kwenye mnuso huo, ilikuwa ni hii show ya wakali hawa wa kuvunja mbavu ambao ni wafanyakazi wenza wa bwana harusi kutoka kundi la Orijino Komedi yaani hapo namzungumzia Joti, Wakuvwanja na Profesa. hawa jamaa waliiteka kabisa sherehe hiyo.
Wazazi.
Bwana Harusi Masanja Mkandamizaji akila Selfie na Mdau.
Wamekutana sasa, Bwana Harusi na Swahiba wake Joti.
Wapendezesha Harusi.

MBUNGE MAHAMOOD MGIMWA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA MUFINDI KASIKAZINI

$
0
0

Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu akiwa sambamba na mwenyekiti wa ccm wilaya ya mufindi Yohanes Kaguo.
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikagua baadhii ya maeneo ambapo michezo hiyo itafanyika


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa ameweza kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo huku akitaka michezo yote kuendelezwa.

Mgimwa ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Mufindi Kusini katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.

Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mgimwa amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye ka,a Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.

“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata. Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mgimwa.Mgimwa ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.

Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.

Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.

DC MTATURU AMALIZA MGOGORO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mang’onyi wakati wa kutatua mgogoro kati ya wananchi na muwekezaji Shanta Gold Mine
Wanachi Kijijini Mang’onyi wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mkuu wao wa Wilaya
Baadhi ya viongozi wakisikiliza maelezo ya awali katika ufunguzi wa mkutano huo uliodumukwa zaidi ya masaa matatu
Dc Mtaturu akikemea tabia ya wanasiasa kutoa matamko ya kisiasa kwa maslahi yao binafsi huku wakiwa mbali na eneo la wawakilishi wao
Wananchi wakimlaki Mkuu wao wa Wilayaya Ikungi
Dc Mtaturu akikemea tabia ya wananchi kuwachagua viongozi ambao wakipewa ridhaa tu wanahamia Dar es salaam ilihali wananchi wao wanabaki kuteseka pasina kuona umuhimu wa viongozi wao
Dc Mtaturu akitoa agizo kwa muwekezaji Shanta Gold Mine kuwalipa fidia haraka wananchi ili mradi huo uanze haraka iwezekanavyo
Nyumbani ni salamu na unyumbani ni kuongea Kinyumbani, moja ya tabasamu kati ya mwananchi na Dc wake wakizungumza kwa lugha moja baada ya mkutano
Wananchi wakielemishwa na Mkuu wa wilaya juu ya siasa zinazokwamisha maendeleo yao huku wanasiasa wenyewe wakishindwa kufanya uwakilishi katika maeneo yao badala yake wamekuwa wawakilishi wa kitaifa
Msingi wa kikao ni kusikilizana Mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Uongozi wa Shanta Gold Mine na wananchi Kijijini Mang’onyi wakiwa kwenye mkutano wa kutatua mgogoro wao

Na Mathias Canal, Singida

Mgogoro uliodumu katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi kati ya wananchi wa Kijiji cha Mang'oni na Muwekezaji Shanta Gold Mine umechukua sura mpya ya maelewano baada ya wananchi kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa uwekezekezaji na fursa watakazozipata ikiwa ni pamoja na ajira kwa wananchi wenyewe na maendeleo ya Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Akiwa katika kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na wananchi hao kujua kadhia iliyopelekea kutoelewana kwa kipindi chote hicho jambo ambalo limerudisha nyuma maendeleo tarajiwa kwa pande zote mbili.

Mgogoro huo umemalizika kwa Mkuu huyo kuamua kuwa wananchi walipwe fidia haraka iwezekenavyo ili kupisha uanzishwaji wa Mgodi huo ambapo tayari takribani wananchi 67 watalipwa katika awamu ya kwanza huku wengi zaidi 130 kulipwa katika awamu ya pili.

Dc Mtaturu amefanya mkutano wake wa hadhara wa mwanzo tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambapo amewaagiza wawekezaji hao kukutana na kuwa na kikao cha pamoja kati yao na wananchi waliofanyiwa tathmini kwa ajili ya makubaliano ya namna bora ya malipo yao ikiwa ni pamoja na kuwashauri kila mmoja kufungua Account Bank ili iwe rahisi na salama katika uhifadhi wa fedha zao.

Baadhi ya Wananchi katika kijiji hicho cha Mang'oni hivi karibuni walizuia njia kwa kuweka magogo na mawe barabarani kama ishara ya kuwazuia wawekezaji hao kupita katika eneo lao kwa madai ya kutolipwa fidia kwa wakati na mwekezaji kuweka alama za mipaka ya eneo lake pasina wananchi kushirikishwa.

Hata hivyo Dc Mtaturu alisema kuwa huenda wananchi walikuwa na hoja ya msingi lakini kutolipwa fidia hakumfanyi mtu kupata uhalali wa kuharibu mali za muwekezaji kwani kufanya hivyo ni sehemu mojawapo inayochelewesha ulipaji wa fidia.

Mtaturu ameonyesha kukerwa na viongozi wanaowapotosha wananchi hao ilihali wakiwa wamejificha ama wanaishi mbali na kijijini hapo na kusema kuwa hiyo ni nidhamu ya woga kwani muwakilishi mzuri wa wananchi ni yule anayetanguliza maslahi ya wananchi mbele kuliko masalahi ya kisiasa, Chama ama maslahi yake binafsi.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kiongozi mzuri daima ni yule anayetatua changamoto za wananchi sio kuzipinga kwani siasa safi na nzuri ni ile inayoleta maendeleo sio kupinga maendeleo.
Amewataka wawekezaji hao kuwa na mahusiano mazuri na wananchi kwani unapokuwa na mradi wako katika Kijiji chochote nchini usipokuwa na mawasiliano mema na wananchi wa eneo husika ni dhahiri kuwa mradi wako utakuwa hauna tofauti na mradi mfu.

Hata hivyo pamoja na faida kwa wananchi kulipwa fidia na serikali kupata pato lake lakini wananchi 60 kutoka Kijijini hapo wataajiriwa katika Mradi huo kati ya ajira 120 zilizopo ambapo wengine 60 watatoka nje ya eneo hilo ili kutoa fursa kwa watanzania wote kujipatia ajira.

KATIBU MKUU MALIASILI, MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI ATOA WITO KWA WADAU WA UHIFADHI NCHINI KUKEMEA VITENDO VYA UINGIZWAJI WA MIFUGO KWENYE MAENEO YA HIFADHI NCHINI

$
0
0
Na Hamza Temba - WMU

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ametoa wito kwa wadau wa uhifadhi nchini kukemea kwa nguvu zote tabia ya uingizaji wa mifugo ndani ya hifadhi za Misitu na Wanyamapori nchini kwakuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi na kunahatarisha ustawi wa hifadhi hizo ambazo ni muhimu kiikolojia na uchumi na wa taifa.


Milanzi ametoa wito huo juzi wakati akifunga mafunzo maalum ya kijeshi katika kituo cha Mlele ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Mkoani Katavi kwa Mameneja wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Askari wa TANAPA kwa ajili kubadilisha mfumo wa utendaji katika taasisi hizo kutoka wa kiraia kwenda wa Jeshi Usu (paramilitary) kuboresha utendaji wao wa kazi.


“Mifugo katika hifadhi zetu sio sahihi ni kinyume kabisa cha sheria za nchi, endeleeni kulikemea hili, tusipige siasa kufurahishana kwakua madhara yake ni mengi ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji, muingiliano wa magonjwa baina ya mifugo na wanyamapori na kuharibu ubora wa vivutio vyetu” Alisema Milanzi.


Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 Ibara ya 18 (2) inakataza kabisa kuingiza mifugo ndani ya hifadhi, Sheria hiyo inasema “Si ruhusa mtu yeyote kuingia na kulisha mifugo ndani ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Ardhioevu”.


Milanzi alisema kuwa hifadhi za taifa nchini zina umuhifu mkubwa kwa uchumi wa taifa kwakuwa kupitia utalii zinachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za nje (foreign currency). Aidha sekta hiyo inatoa ajira zaidi ya milioni moja na nusu kupitia huduma za kitalii nchini. 


Mbali na faida za kiuchumi hifadhi hizo pia zina faida nyingi za kiikolojia ambazo ni uhifadhi wa vyanzo vya maji, kusaidia upatikanaji wa mvua na hewa safi kwa viumbe hai ikiwemo binaadamu. Alisema kuharibu hifadhi hizo kwa kulisha mifugo ndani yake ni jambo ambalo halikubaliki kwa kuwa ni kuhatarisha pia maisha ya binaadamu ambayo yanategemea hifadhi hizo.


Alieleza kuwa Serikali inaenda kulifanyia kazi tatizo hilo pamoja na migogoro mingine ya ardhi kwa ajili ya kuyatafutia suluhu kwa kushirikisha Wizara zinazohusika ambazo ni Ardhi, Kilimo na Mifugo, Sheria na Katiba, Tamisemi, Maliasili na Utalii na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.


Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo, Milanzi alisema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uadilifu, nidhamu, ujasiri, uaminifu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa muda mfupi na hivyo kuwataka kuyatumia kuongeza ufanisi katika kulinda maliasili zilizopo kwenye maeneo yao.


Aliwataka pia wahitimu hao kutafsiri mafunzo hayo na maendeleo ya sekta ya uhifadhi nchini na kuliongezea taifa mapato kwa kuboresha huduma za utalii, kubuni bidhaa mpya za utalii na kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi aliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyoyapata kuziba mianya yote ya ujangili na kwamba jamii inategemea kuona kazi hiyo kwa vitendo.


Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UNDP kupitia mradi wa “Spanest” yalifanyika kuanzia tarehe 15 Julai hadi tarehe 13 Agosti, 2016 kwa kuwahusisha washiriki 69 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Tanapa. Mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa awamu yanatemewa kuhusisha taasisi zote za uhifadhi wa wanyamapori nchini kuelekea kwenye mabadiliko ya muundo wa utendaji kazi kutoka mfumo wa Kiraia  kwenda mfumo wa Jeshi Usu (Paramilitary).

Mahojiano na Olympian Hilal Hemed Hilal (Live) kutoka Brazil

$
0
0
Photo Credits: MissiePopular.com
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU (Jumatatu Agosti 15 2016) Mubelwa Bandio alifanya mahojiano ya moja kwa moja na Hilal Hemed Hilal. Nahodha wa Tanzania katika mchezo wa kuogelea kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro nchini Brazil.

Alikuwa mkarimu kujiunga nasi kwa njia ya Skype sambamba na kocha wake Alexander Mwaipasi
Karibu uungane nasi

NEW VIDEO FROM TANZANIA GOSPEL ARTIST BEATRICE MWAIPAJA. SONG: MUNGU UMENIHURUMIA VIDEO DIRECTED BY JACKSON JOACHIM

MBUNGE WA MKURANGA,MH. ULEGA AKABIDHI MADAWATI 537 HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA.

$
0
0

Mbunge Abdallah Ulega (katika alie simama) akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Msham Munde, mkuu wa wilaya hiyo Filberto Sanga, na mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke mara baada ya kukabidhi madawati 537 ya mbunge wilayani humo.Sehemu ya madawati ya hayo. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)


Mbunge wa Jimbo mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Njopeka mara baada ya kufanya ziara ya kuwashukuru wananchi hao baada ya kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo ambapo pia mbali na kushukuru anatumia mikutano hiyo kuhamasisha maendeleo na kuwataka kufanya kazi kwa bidii leo mkoani Pwani.
Walimu wa shule ya msingi Misasa wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega mara baada ya kuzuru shuleni hapo kwa lengo la kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii na kwamba yeye kama kiongozi wao yupo pamoja nao .
Akina mama wa kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Likanga wakimsilikiliza mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwa makini wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru uliofanyika kijiji hapo ambapo pia walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zao hususani kukosekana kwa Zahanati na maji safi.
Watendaji wa halmashauri wakimsikiliza kwa makini mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega,katika mkutano wake wa hadhara wa kushurukuru wananchi wa kijiji cha Njopeka ,kata ya Likanga ambapo katika ziara hizo amekuwa akitembea na watendaji hao ili kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwasili katika kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Lukanga ,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa kijiji waliokuja kumpokea,ulega yupo katika ziara ya kushukuru wananchi wake pamoja na kuhamasisha maendeleo ya watu.
Mbunge Abdallah Ulega akikabidhi madawati 537 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mkuranga Msham Munde ,madawati hayo yametokana na fedha zilizotolewa na bunge baada ya kubana matumizi na kukabidhiwa Rais Dkt John Magufuli ambaye naye aliagiza zitengeneze madawati.
Mdau wa maendeleo kutoka kampuni ya Hamisi Njomoke Limited akimkabidhi madawati 50 mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kauli mbiu ya rais ya kuwataka watanzania kujitokeza kuchangia ili kuondoa kero hiyo katika shule leo mokani Pwani.


AWATAKA VIONGOZI NA WALIMU KUTUZA MADAWATI HAYO

Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi madawati 537 kwa halmashauri ya wilaya hiyo, huku akiwataka viongozi wakiwamo madiwani wa kata mbalimbali kusimamia vizuri madawati hayo ili kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi alisema kuwa madawati hayo yametokana na fedha zao ambazo zilibaki baada ya kubana matumizi katika ofisi ya bunge na kwa kauli moja walikubali kumkabidhi Rais Dkt. Magufuli, ambapo naye kwa kutambua changamoto ya madawati akaelekeza fedha hizo zipelekwe kutengeneza madawati hayo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msham Munde alimshukuru Mbunge huyo na kudai kuwa uchangiaji wa madawati hayo ni mchakato endelevu hivyo wadau waendelee kujitokeza kuchangia huku akisisitiza kwamba kwa asilimia kubwa yamekwenda kutatua kero hiyo.

Wakati huohuo mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke alimkabidhi mbunge wa jimbo hilo Ulega Madawati 50 kama sehemu ya kumuunga mkono mbunge paoja na Rais Dkt Magufuli huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia ili watoto wasome katika mazingira rafiki.

Dr.Amon Mkoga Foundation wakabidhi madawati 90 kwa wilaya ya Tabora mjini.

$
0
0

Mwenyekiti wa Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation Ndugu.Amon Mkoga akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Isike kulia ni Amina Rajabu na kushoto ni na James Shija.
Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe. Sweetbert Nkuba, (kushoto) akipokea moja ya madawati 90 yaliyotolewa na Dr.Amon Mkoga Foundation na kukabidhiwa kwake na mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu.Amon Mkoga(kulia). Anayeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika ambao ni wadhamini wa kampeni hiyo iitwayo “Simama Kaa” Mwenyekiti wa Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation Ndugu.Amon Mkoga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Isike Manispaa ya Tabora.

Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation imetoa msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni 5.5 kwa shule za msingi katika manispaa ya Tabora, ikiwa ni mchango wa Taasisi hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya Tabora mjini , Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu Amon Mkoga amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya taasisi hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Dr.Amon Mkoga Foundation katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Taasisi yetu inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Mkoga.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe. Sweetbert Nkuba ambaye alisema madawati hayo 90 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Tabora na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.

Mpango mkubwa umeme nchini wazinduliwa, Kaya 500,000 kupata umeme wa uhakika

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza huku akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa mpango wa TREEP katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird .

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akielezea mikakati ya Serikali katika usambazaji wa umeme vijijini wakati alipokuwa akizindua mpango wa kupanua wigo wa upatikanaji wa umeme vijijini (TREEP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB)
Sehemu ya wakazi wa Kwedizinga wilayani Handeni mkoani Tanga wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani ) katika uzinduzi huo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga akielezea mpango wa kupanua wigo wa upatikanaji wa umeme vijijini (TREEP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) kwenye uzinduzi huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird (katikati) wakisaini makubaliano kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa kupanua wigo wa upatikanaji wa umeme vijijini (TREEP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) kwenye uzinduzi huo. Kushoto kabisa ni Kamishna Msaidizi wa Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird (kushoto) wakibadilishana nakala ya makubaliano baada ya utiaji saini wake katika uzinduzi huo. Katikati ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dk. Gideon Kaunda akielezea mpango wa TREEP katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird (kulia) akielezea mikakati ya Benki ya Dunia (WB) katika kuisaidia serikali katika usambazaji wa umeme vijijini. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Future Century Limited ya Tanzania, Hellen Masanja (wa kwanza kulia) akielezea mafanikio ya kampuni yake katika usambazaji wa umeme vijijini katika uzinduzi huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza mmoja wa wakazi kutoka katika eneo la Kwedizinga wilayani Handeni mkoani Tanga alipokuwa akiwasilisha maoni yake katika uzinduzi huo. 
 ………………………………………………………………………………..

Na Greyson Mwase, Tanga

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amezindua mpango mkubwa wa umeme nchini utakaowezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa takribani kaya 500,000 katika maeneo mengi ya vijijini.

Uzinduzi huo uliofanyika katika eneo la Kwedizinga wilayani Handeni mkoani Tanga ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Benki ya Dunia (WB), Ujerumani, Sweden, Norway, Uingereza na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Wengine waliohudhuria ni pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), watendaji kutoka katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga, wabunge, madiwani na wananchi kutoka kutoka katika maeneo mbalimbali mkoani Tanga.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Profesa Muhongo alisema kuwa mpango huo ni wa kihistoria kwa kuwa utakuwa ni mkombozi kwa Tanzania kwani umeme utakaozalishwa utakuwa ni wa uhakika na kuwezesha nchi kupiga hatua kubwa kiuchumi na kuingia katika kundi la nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Alisema kuwa, serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kubuni vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme ikiwa ni pamoja na maji, jotoardhi, upepo, gesi, jua, makaa ya mawe lengo likiwa ni kuendana na kasi ya usambazaji wa umeme vijijini

“ Tunataka kuhakikisha kuwa tunaendana na kasi ya ongezeko la miradi mipya ya umeme vijijini kwa kuhakikisha kuwa tuna vyanzo vipya vya uzalishaji wa umeme,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo aliendelea kusema kuwa serikali ina mpango wa kuzalisha umeme wa uhakika na kuuza wa ziada katika nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Zambia n.k

Wakati huo huo akielezea mpango huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alisema kuwa serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB) zilikubaliana kuanzisha mpango wa kupanua wigo wa upatikanaji wa umeme vijijini Tanzania ujulikanao kama Tanzania Rural Electrification Expansion Program;(TREEP) lengo likiwa ni kuhakikisha nishati ya uhakika inapatikana katika maeneo ya vijijini kwa bei nafuu.

Alieleza kuwa mradi huo wa miaka sita unaotarajiwa kukamilika mwaka 2022, fedha zake zinatokana na mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia (WB) wa Dola za Marekani milioni 200.

Aliendelea kufafanua kuwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 25 ambazo zinaratibiwa na Benki ya Dunia zilizotolewa kama msaada kupitia Programu ya Kuongeza Kasi ya Nishati Jadidifu kwa Nchi Zenye Kipato cha Chini (SREP), kati ya fedha hizo kiasi cha Dola za Marekani milioni tisa zimejumuishwa chini ya TREEP

Mhandisi Nyamo-Hanga, alifafanua kuwa lengo la mpango wa TREEP ni kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya umeme vijijini ikiwa ni pamoja na miundombinu ya usambazaji na ya uzalishaji hasa wa nishati jadidifu vijijini.

Aliongeza kuwa mpango wa TREEP ni wa kwanza kabisa kutumia mfumo mpya wa Benki ya Dunia unaojikita kwenye utekelezaji wa matokeo.

Alitaja washirika wengine wa mradi huu kuwa ni pamoja na Serikali ya Norway, Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (Sida), Umoja wa Ulaya (EU), Idara ya Serikali ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) ambapo miradi yake yote itasimamiwa na REA.

Alisema kuwa mpango wa TREEP utajumuisha maeneo matatu ambayo ni pamoja na eneo la kwanza litakalohusisha katika kuongeza wigo wa miundombinu ya usambazaji umeme wa gridi ambapo kiasi cha Dola za Marekani milioni 151 zitatumika katika eneo hili.

Aliendelea kusema kuwa eneo la pili litajikita kuendeleza mifumo ya umeme nje ya gridi kwa kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa sekta binafsi ili kuendeleza miradi ya nishati jadidifu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na shughuli za uzalishaji mali ambapo kiasi cha Dola za Marekani milioni 42 zitatumika.

Alisema eneo la tatu litalenga katika kuendelea kujenga uwezo wa kitaalam kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wengine ambapo kiasi cha Dola za Marekani milioni 16 zitatumika.

Akielezea mafanikio yanayotarajiwa kupatikana kutokana na mradi wa TREEP, Mhandishi Nyamo-Hanga alisema kuwa kaya zisizopungua 500,000 hadi milioni 2.5 zitaunganishwa na umeme wa gridi na nje ya gridi ikijumuisha takribani kilomita 24,000 ya miundombinu usafirishaji na usambazaji.

“Takribani watu 310, 000 watafikiwa na huduma ya umeme kupitia mifumo ya nje ya gridi pamoja na upatikanaji wa vyanzo vipya ya umeme hali itakayopelekea mabadiliko makubwa ya kiuchumi,” alisema Mhandisi Nyamo-Hanga.

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird aliipongeza serikali ya Tanzania katika juhudi zake za kupambana na umaskini kwa kuweka mikakati ya kuhakikisha nishati ya uhakika ya umeme inapatikana kwa gharama nafuu.

Bird alisema nishati ya umeme ni muhimu hususan katika kipindi hiki ambapo serikali imejikita katika uchumi wa viwanda na kuongeza kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kushirikiana na Serikali katika maeneo yote ili malengo yake yaweze kufikiwa.

Alisema kupitia mpango wa TREEP huduma za jamii zitaboreshwa ikiwa ni pamoja na shule na hospitali za kisasa na upatikanaji wa maji ya uhakika kwa kutumia pampu zinazotumia umeme.

SANLAM EMERGING MARKETS ANNOUNCES EXECUTIVE APPOINTMENTS

$
0
0
The Sanlam Group is pleased to announce key leadership appointments which will support and further strengthen the Group’s Pan-African growth. This is also in keeping with the Group’s expanded footprint on the continent following the recent acquisition of a 30% stake in Morocco-based Saham Finances. 
These appointments will result in four distinct regionally focused units within Sanlam Emerging Markets (SEM) - Southern Africa; East Africa; North and West Africa; and South East Asia.

With effect from 01 September 2016:

· Mr Julius Magabe, the Managing Director and Chief Executive Officer of Sanlam Life Insurance in Tanzania since 2011, will assume the position of Regional Executive: East Africa for SEM. Magabe will remain based in Dar es Salaam. He will join the SEM Executive Committee and will be responsible for businesses in Kenya, Rwanda, Tanzania and Uganda.
Among his successes at the helm of Sanlam Life Insurance, he is credited for growing the business and achieving 60% of the market share.
Magabe is an alumnus of the Johannesburg-based Gordon Institute of Business Science (GIBS). He also holds an MBA from the Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) and is a graduate of the Institute of Finance Management Tanzania in Insurance and Risk Management. He joined Sanlam Life Insurance in Tanzania (formerly African Life Assurance) in 2007 as Head of Corporate Business. In 2010 he was appointed as Managing Director of the company, a position he has held up to now.

· Mrs Margaret Dawes, currently SEM’s Executive Director: West and East Africa, will take up the position of Executive Director: North and West Africa. A Chartered Accountant, Dawes also holdsaBSc (Hons) Biology (London) and anHDip Tax Law (Wits). 

She joined Sanlam in 2005 as the chief financial officer for Sanlam Developing Markets (now SEM) and has held various other positions within SEM. In her new role, Dawes will be responsible for the SEM businesses in Nigeria, Ghana as well as those businesses in the North and West Africa region which are part of the recently established partnership with Saham Finances based in Morocco.

Earlier this year, the Group made the following appointments:

· Mr Gaffar Hassamas SEM’s Regional Executive: Southern Africa responsible for SEM’s businesses in Namibia, Botswana, Malawi, Zambia and Zimbabwe. 
An MBA graduate from Oxford Brookes, Gaffar is also a fellow member of Chartered Association of Certified Accountants (FCCA). Prior to his SEM appointment, Hassam was the Group CEO for Botswana Insurance Holdings Limited (BIHL) since 1 December 2011. Hassam joined BIHL in April 2003 as the Group Finance Manager and Company Secretary and held several positions within the Group, includingamong others, Head of Finance and Chief Operating Officer.

· Mr Prasheem Seebran as SEM’s Regional Executive: South East Asia responsible for all SEM’s businesses in Malaysia. 

An Actuary, Seebran is currently completing his MBA at Henley Business School. He began his career at Marsh and held various positions at Guardrisk and Telesure before joining Sanlam in June 2013. In September 2013, hemoved to Malaysia where he has been responsible for all risk and capital related areas within Sanlam’s short term insurer, Pacific &Orient (P&O). He has also been in charge of developing P&O’s actuarial capabilities and has worked with the regulator on developing the risk management function and optimisation of capital.
In June, Sanlam Group also announced the appointment of Mr Junior Ngulube as the Chief Executive Officer of SEM. Dawes, Hassam, Seebran and Magabe will report to Ngulube when he takes over from Mr Heinie Werth on 01 October 2016. Werth has been appointed the Group’s Financial Director with effect from 01 October, succeeding Mr Kobus Möller who will retire.
Commenting on the appointments Sanlam Group CEO, Mr Ian Kirk, said: “On behalf of the Sanlam Group Executive Committee, SEM and staff, I wish to congratulate these colleagues. We are confident that they will continue to add value to the SEM business and support us in our journey as a Pan-African leader in financial services.” 
“We are pleased to have been able to fill the majority of these positions from organically grown Sanlam candidates through our succession planning and leadership development programmes, while balancing that by bringing in the right type of external exposure and experience.”The Group is in the process of appointing Magabe’s successor at Sanlam Life Insurance in Tanzania and an announcement will be made in due course. 
Ends

Issued by Sanlam Group Communications

ABOUT THE SANLAM GROUP 

Sanlam is a leading financial services group listed on the JSE Limited and the Namibian Stock Exchange. Established in 1918 as a life insurance company, the South Africa-based Sanlam Group has transformed into a diversified financial services business. 
Through its business clusters – Sanlam Personal Finance, Sanlam Emerging Markets, Sanlam Investments, Santam and the newly established Sanlam Corporate - the Group provides comprehensive and tailored financial solutions to individual and institutional clients across all market segments. The Group’s areas of expertise include insurance, financial planning, retirement, trusts, wills, short-term insurance, asset management, risk management and capital market activities, investment and wealth. 

The Group operates in Southern Africa through Botswana, Malawi, Mozambique, Namibia, Swaziland, Zimbabwe and Zambia; East Africa through Kenya, Tanzania, Rwanda and Uganda; West Africa via Nigeria and Ghana and in India and Malaysia. It has an indirect presence via associate companies in Burundi, The Gambia and Lesotho. The recently announced acquisition of a 30% interest in Morocco-based Saham Group will further extend the Group’s footprint into an additional 20 countries mostly in Francophone Africa. The Group also has business interests in the United Kingdom, the USA, Australia and the Philippines. It has a stake in leading global micro-insurance specialists, UK-based Micro-Ensure Holdings Limited. For further information, visit www.sanlam.com

ENQUIRIES 

Pearl Majola, Sanlam Group Communication 

+27 11 778-6305 or +27 83 286 7476 or pearl.majola@sanlam.co.za

MAAJABU YA ZIWA NGOZI (LAKE NGOZI).

$
0
0
ZIWA Ngozi ni moja ya maziwa duniani ambayo yametokana na kulipuka kwa Volicano,ziwa hilo Lililopo Wilaya ya Rugwe Mkoani Mbeya nchini Tanzania katika kijiji cha Mbeye one au mchangani  ni la pili kwa ukubwa Afrika.

Asili ya jina Ngozi linatokana na jina la kabila la Wasafwa linalomaanisha kitu kikubwa ‘’LIGOSI’’ na ziwa hilo tangu zamani lilikuwa chini ya himaya ya kabila la wasafwa katika koo mbili za machifu ikiwemo ya Chifu Mrotwa Mwalingo (akitawala upande wa magharibi) na chifu Mlotwa Mwalupindi(aliyekuwa akitawala upande wa Mashariki).

Ziwa Ngozi lipo usawa wa  mita 2600 kutoka usawa wa bahari na limezungukwa na misitu minene ya asili  katika safu za milima ya Uporoto na kuna hekari 9,332 ambazo zimetengwa kwajili ya uhifadhi wa eneo hilo.

Ndani ya ziwa Ngozi kuna visiwa viwili vinavyovutia sana kwa muonekano na inatajwa visiwa hivyo hutumika kwajili ya mazalia ya bata pori na ndege wengine.

Ziwa hilo lina kina cha mita 74 na urefu wa kilometa  2.5  pamoja na  upana wa kilometa 1.5 na eneo lake ni km za eneo 3, na pembezoni mwa ziwa hilo kuna mabonde makubwa yenye misitu mikubwa ya miti ya asili na baadhi ya mimea hiyo ni migomba ya asili na mianzi ya asili pamoja na miti mirefu na maua ya aina mbalimbali.

Umbali wa kutoka katika Kijiji cha Mbeye one au Mchangani hadi katika ziwa hilo la Ngozi ni zaidi  masaa mawili kwa miguu,ingawa kabla ya kufika katika ziwa hilo kuna sehemu ya kupunzika ambayo kwa Lugha ya Kisafwa hufahamika kama  NZEYENZU.

Pia sehemu ya kupunzika hutumika kwajili ya watalii wenye magari na usafiri mwingine kuyaacha hapo,na umbali kutoka sehemu ya kupumzika hadi sehemu linapopatikana ziwa hilo ni  nusu saa(30 saa) ambapo wageni na watalii  hutumia muda huo kupandisha sehemu kubwa iliyoinuka.

Kuna njia nyembamba iliyotengenezwa kwa umahili mkubwa wakati wa kupandisha mwinuko huo kuelekea ziwa Ngozi,na ukiwa njiani ni kawaida kusikia milio ya ndege wa aina mbalimali pamoja na ngedere ingawa si rahisi sana kuwaona kutokana na misitu minene ya asili yenye miti mirefu na mabonde ya ajabu.

Unapofika  eneo la Ziwa Ngozi utastajabu umbo la ziwa hilo,huku maji yakionekana kuwa  chini kutoka sehemu  uliyosimama na kwa mbali ni jambo la kawaida kusikia milio ya mara kwa mara ya bata pori ndani ya ziwa hilo.

Muonekano wa ziwa Ngozi  unavutia sana bila kukuchosha wakati wa kulitazama ,ingawa ni kawaida kwa ukungu kutawala sehemu kubwa ya eneo la ziwa hilo kwa siku na  kiwango cha joto katika eneo hilo ni 18 °C.

Ukiwa eneo la ziwa hilo inahitajika uangalifu wa hali ya juu  kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na mapango yaliyopo pembezoni na ambayo ukikanyaga vibaya unaweza kuporomoka nakupoteza maisha na ni jambo la busara kuzingatia maelekezo ya watalaam.

Maajabu mengine ni kuwa maji ya Ziwa  Ngozi hubadilika rangi kila wakati zikiwemo rangi za Bluu ,nyeupe na  nyeusi na  ladha ya maji hayo ni ya chumvi na mbayo hutumika  kwa imani za kimila.

Watu mbalimbali waliyoyafikia maji ya ziwa ngozi  wanaweka wazi kuwa ni kazi ngumu ya kufika huko kutokana na kushuka chini kwa kutumia kushika mizizi ya miti kwa muda wa kati ya dk 45 hadi dk 60 na wa kupandisha kutoka chini kabisa huwa ni kazi ngumu sana.

Ndani ya ziwa hilo kuna samaki ambao ni vigumu sana kuwavua  kutokana na miundo mbinu ya Ziwa hilo ,ambapo sehemu ya samaki hao wanadaiwa kuliwa na bata wa porini na ndege wengine tofauti wanaokula samaki.

Mbali na ziwa Ngozi kuna  maziwa mengine madogo sana yenye asili ya  volkano yaliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambayo ni  Kisiba, Chungululu,Ikapu, Itamba, Masoko, Ilamba,Ndwati, Katubwi Itende,Lusanje  na  Kingili.,pia kuna  ziwa  Chala( Dschalla) ambalo lipo nje kidogo ya  mjini Moshi  mkoani Kilimanjaro  ndani ya  Mlima Kilimanjaro..

Je wajua Maziwa makubwa duniani yenye muundo wa ziwa Ngozi(a natural lake occupying the caldera),Ziwa Toba linalopatikana eneo la Sumatra nchini , Indonesia ndiyo ziwa pekee duniani linaloongoza kwa ukubwa lina urefu wa Kilometa 100 na upana wa kilometa 30 na eneo  ni km za eneo  1,130 na kina ni mita 500.

Maziwa mengine ni  Pinatubo linalopatikana nchini Ufilipino lina kina cha mita 600 na upana wa km 2.5 na ziwa Heaven linalopatikana Korea ya Kaskazini lina Urefu wa mita 213 na eneo la Km  9.82,maziwa mengine ni IRAZÚ nchini  Costa Rica,Cuicocha, nchini Ecuador na mengineyo.

Imeandaliwa na  Ng'oko Innocent.

KAIMU KAMISHNA MSAIDIZI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI KUTOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI ATUA TANGA KUANGALIA ENEO LITAKAPOJENGWA GATI KWA AJILI YA KUSHUSHIA MAFUTA GHAFI

$
0
0





Greda likisafisha eneo ambalo linatarajiwa kujengwa gati kwa ajili ya kushushia mafuta ghafi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia akiwa na viongozi kutoka Wizara ya Nishati na Madini walipotembelea sehemu ambayo litajengwa gati mpya eneo la Chongoleani jijini Tanga kushushia mafuta ghafi kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini ,Mwanamani Kidaya kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo wakati walipotembelea eneo la Chongoleani ambapo kutajengwa gati ya kushushia mafuta ghafi



Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mwanamani Kidaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kulitembelea eneo hilo leo .
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumzia namna mkoa huo ulivyojipanga na fursa hiyo mara baada ya kulitembelea eneo hilo .
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa tatu kutoka kushoto namna walivyojipanga kutokana na fursa hiyo

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mwanamani Kidaya kushoto akimuonyesha kiti Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella mara baada ya kutembelea eneo hilo




Muonekano wa eneo ambalo kutajengwa gati mpya kwa ajili ya kushushia mafuta ghafi .Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images