Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 937 | 938 | (Page 939) | 940 | 941 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda (kushoto) akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam.Wengine kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida.

  Picha na 1. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda (kushoto) akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam.Wengine kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita akizungumza na wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida.
  Wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam wakifuatilia kikao cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema, akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hamphrey Polepole na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi.
  Na.Aron Msigwa - Dar es Salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda amewataka watendaji wa mkoa huo kuhakikisha kuwa wanasimamia ubora wa madawati na vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

  Aidha, amezitaka manispaa za jiji hilo kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa mapya na kuwahamasisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitolea kufanikisha mpango huo na kutoa wito kwa madiwani kujiwekea mkakati wa kujenga walau madarasa mawili kwenye Kata zao.

  Akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC), Mhe Makonda amesema kuwa licha jiji hilo kukabiliwa na changamoto za kimaendeleo za muda mrefu kwenye sekta ya elimu, miundombinu ya Afya, maji na barabara mafanikio yameanza kuonekana kutokana na juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa huo.

  UPATIKANAJI WA MADAWATI

  Kuhusu upatikanaji wa madawati amesema kuwa toka Mhe. Rais wa Jamhuri ya Tanzania atangaze kampeni ya upatikanaji wa madawati kwa ajili ya shule za Msingi kumekuwa na mwitikio mzuri kwa viongozi wa mkoa huo kuhakikisha madawati yanapatikana kwa uhuru

  Amesema mkoa wake ulikua na upungufu wa madawati zadi ya 66,031 yaliyokuwa yakihitajika katika shule za msingi , Sekondari zikihitaji madawati zaidi ya 30,000.

  Amesema wabunge wa majimbo ya Dar es salaam tayari wametoa madawati 5000 kila mmoja katika jimbo lake na juhudi zinaendelea kufanywa na madiwani na Mameya kuendelea kutenga bajeti kwenye Halmashauri zao kwa ajili ya ununuzi wa madawati huku akiwashukuru Wakuu wa wilaya kwa kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia madawati kwa kujitolea na kufanikisha mkoa huo kuwa umepata madawati yote yaliyobaki ifikapo Agosti 31 mwaka huu.

  VYUMBA VYA MADARASA

  Amesema bado mkoa unakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na kuongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Pombe Magufuri katika ahadi zake aliupatia mkoa huo kiasi cha shilingi bilioni 2.7 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya madawati zihamishiwe kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa na kazi ya kumalizia upatikanaji wa madawati yaliyobaki ibaki kwa viongozi wa mkoa huo.

  Amesema fedha hizo zimekwishakutengwa na kuanza kusambazwa kwenye wilaya husika na kusisitiza kuwa ujenzi wa madarasa hayo unaendelea lengo likiwa kujenga madarasa 123 kwa fedha zilizotolewa na Mhe.Rais Dkt. John Magufuli.

  “Kama mkoa tunamshukuru Rais alitupatia shilingi bilioni 2 na akawabana mawaziri wake wakachanga milioni 107, tukafikisha jumla ya shilingi bilioni 2.1 fedha hizi ilikua ziende kwenye madawati, nikamwomba Mhe. Rais aturuhusu tuzitumie kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ili madawati tuendelee kupambana nayo sisi wenyewe”Amesisitiza Mhe. Makonda.

  Aidha, wadau mbalimbali kutoka ndani ya nchi wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kampeni juhudi za Serikali kwa kutoa michango mbalimbali na kufanikisha ujenzi wa madarasa kupitia uchangiaji wa mabati mabati 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa pia wadau kuchangia tani zipatazo 35 za nondo.

  USAFI WA MAZINGIRA.

  Amesema mkoa wa Dar es salaam una changamoto ya uzalishaji wa taka nyingi ikilinganishwa na maeneo mengine nchini kwa kuwa una idadi kubwa ya watu takribani wakazi zaidi ya milioni 5 ambao

  Amesema juhudi za kuendelea kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi zinaendelea kwa kuwahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kusafisha mazingira yao ili kujikinga na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu yanayosababishwa na uchafu.

  Amewataka viongozi wa mkoa huo kusimamia wajibu wa kuliweka jiji katika hali ya usafi kwa kusimamia sheria ili jiji hilo liwe katika hali ya usafi ikiwa ni pamoja na kuwaagiza wamiliki wa maduka yote katika jiji hilo kuwa na vifaa vya kutupia taka nje ya maduka yao.

  Amepongeza juhudi za watendaji wa mkoa huo kutenga fedha kwenye bajeti ya 2016/2017 kwa ajili ya kununulia magari ya kubebea taka.

  Ili kuhakikisha kuwa kampeni hiyo inakuwa endelevu na inafanywa kwa kasi na nguvu kubwa ameanzisha mpango wa utoaji wa gari (pick up) na fedha kama motisha kwa Mwenyekiti wa mtaa atakayefanya vizuri kwenye usafi kuanzia mwezi huu, huku wajumbe 5 wa Serikali ya mtaa na mtendaji wa mtaa utakaofanya vizuri wakipatiwa kiasi cha shilingi milioni 5 kila mmoja.

  "Napenda kuwajulisha kuwa mwezi huu niliahidi kukabidhi gari aina ya pick- up kwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa atakayefanya vizuri kwenye usafi,kwenye mtaaa wake na tayari nimeshainunua nalenga kutoa motisha kwa viongozi hao” Amesema.
  Amesema zawadi hizo zitatolewa kwa kwa kuzingatia vigezo vya Afya vilivyowekwa na tayari timu iliyoundwa kufuatilia suala hilo imeanza kazi ya kupita katika maeneo mbalibali kufuatilia utekelezaji wa kampeni hiyo kubaini mitaa na viongozi waliofanya vizuri na kusisitiza kwamba viongozi wa mitaa watakaozembea kusimamia usafi katika maeneo yao watatangazwa hadharani kupitia vyombo vya habari ili jamii iwajue kuwa wanakwamisha kampeni ya usafi.


  SOKO LA KARIAKOO

  Mhe. Makonda amepongeza juhudi zinazofanywa na viongozi na watendaji wa halmashauri ya Ilala na jiji kuifanya Kariakoo kuwa katika hali ya usafi na na kuwawezesha wananchi kupita kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali.

  Amesema yeye kama mkuu wa mkoa aliyekabidhiwa jukumu la kusimamia mkoa huo atahakikisha kuwa maeneo yote ya jiji la Dar es salaam ikiwemo Kariakoo na Ubungo yanabaki kuwa maeneo yanayowezesha wananchi kupita kwa huru bila hofu yoyote.

  “ Mimi nawapongeza Mameya wa jiji, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na Maafisa Biashara kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya kuifanya Kariakoo na Ubungo iweze kupitika, nawahakikishia maadam mimi ndiyo Mkuu wa Mkoa itabaki hivyo, maeneo hayo yatabaki salama kwa watu kupita na wale wanaofanya biashara na kulipa kodi wafanye kazi yao kwa uhuru ” Amesisitiza.

  WAMACHINGA KATIKATI YA JIJI.

  Amewataka wafuate sheria zinazosimamia jiji kwa kuacha kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa na kuwa tayari kwenda kwenye maeneo waliyopangiwa na kuongeza kuwa ataendelea kusimamia sheria, kanuni na taratibu zinazouongoza mkoa huo kuhakikisha kuwa maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao na halmashauri husika yanatumika kama ilivyokusudiwa ili Dar es salaam iwe mahali pazuri na salama pa kuishi.

  Mhe. Makonda amekiri kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wenye maduka eneo la kariakoo ambao wamekua wakikwamishwa na wafanyabiashara wadogo ambao wamekuwa wakipanga barabarani, nje ya maduka yao bidhaa zilezile wanazouza wao katika maduka yao huku wakiwa hawalipii kodi jambo ambalo linawasababishia hasara.

  Amewaagiza wakuu wa wilaya watangaze barabara zitakazotengwa katika kata kwa ajili ya kufungwa mwisho wa Juma (week end) ili zitumiwe na wafanyabiashara wadogo kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akiwahutubia wakazi wa jiji la Mwanza Agosti 11, 2016 na kuongeza kuwa barabara zitakazofungwa zitahusisha zile za Kata ambazo zitakuwa zinahudumiwa na Ofisi za kata ili kuwawezesha wananchi kufanya biashara kwa uhuru na kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yao.

  OMBAOMBA.
  Kuhusu ombaomba amesema kuwa mkoa wake utalishughulikia kwa nama ya kipekee kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la ombaomba ambao wamegawanyika katika makundi ya watu wazima na watoto ambao sasa wamekuwa kero kwa wakihusishwa na vitendo vya ukwapuaji wa mali za watu, kuharibu magari pindi wanapokosa fedha walizoomba kutoka kwa watumia barabara.

  Amewaagiza wenyeviti wa Kamati za ulinzi na Usalama wa mkoa huo katika kila wilaya kulifanyanyia kazi suala hilo wakishirikiana na maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha hakuna watoto wanaozunguka kuombaomba kwa kuwa walitakiwa kuwa shule na elimu sasa inatolewa bure.

  KERO YA USAFIRI.

  Amepongeza juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mradi wa Mabasi ya mwendokasi ambayo yamekuwa msaada kwa wakazi wa jiji hilo pia uwepo wa Treni za abiria za reli ya Kati katika jiji la Dar es salaam kutokea Dar es salaam stesheni hadi Ubungo na Pugu.

  Aidha, mkoa umeiomba Wizara ya Ujenzi, Mawasliano na Uchukuzi kuangalia uwezekano wa kuanzisha boti tatu za kisasa zitakazoanzia safari yake Feri kwenda Mtoni Kijichi na Mbagala na wataalam wa wizara husika wanafanya upembuzi yakinifu kuwezesha jambo hilo wakati ukisubiriwa utekelezaji wa Awamu ya pili na tatu wa ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi katika jiji hilo.

  Kuhusu msongamano wa malori ya mafuta yanayokuja katika Bandari ya Dar es salaam kuchukua mafuta, mkoa huo kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja na Wizara ya Nishati na Madini umeweka mkakati wa kuangalia uwezekano wa kujenga bomba la mafuta litakalotoka Kurasini hadi chalinze kupitia njia ya mradi wa Tazama ambalo litapunguza msongamano wa malori yapatayo 1000 hadi 1500 yanayoingia na kutoka katika jiji hilo.

  ULINZI NA USALAMA.

  Amesema kuwa Serikali ya mkoa wa Dar es salaam itaendelea kuhakikisha kuwa jiji la Dar es salaam linakuwa salama na kuvitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Jeshi la Polisi kuendelea kutekeleza sheria na majukumu yao ipasavyo ili kudhibiti vitendo vya kiharifu na uvunjaji wa sheria, ujambazi, umiliki silaha haramu, madawa ya kulevya, vitendo vya udharirishaji wa binadamu .

  “Kipindi cha nyuma silaha zilikua zinalia hovyo sasa nalishukuru Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kwa kazi nzuri, tutaendelea kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo kwa kufanya oparesheni za wamiliki silaha kinyume cha sheria kuondoa kila aina ya uharifu unaofanyika ndani ya majumba ya watu katika jiji hili” Amesisitiza Mhe. Makonda.

  0 0

   
  Mlinzi wa Timu ya Mpira wa Pete wa Tanzania Joyce Kaira (GK) akiwa katika hekaheka za kuzuia Wachezaji wa Rwanda Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Amahoro Tanzania iliifunga Rwanda 56-13

  Kocha wa Timu ya Tanzania kwa Mpira wa Pete Argentina Daudi akitoa maelekezo kwa Wachezaji wake katika muda wa mapunziko katika mchezo baina yao na Rwanda uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali ambapo Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
  Nyota Chipukizi wa Mpira wa Pete wa Tanzania Nasra Suleiman ( Mwenye Mpira)akiwa katika hekaheka za kuisaidia Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Tanzania iliifunga Rwanda 56-13
   
  Na Selemani Semunyu JWTZ 

  Timu ya Mpira wa Pete ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imedhihirisha Ubabe wake katika mchezo huo baada ya kuifunga Timu ya Jeshi la Rwanda RDF kwa Magoli 56-13 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na Timu zote tangu kuanza Mashindano hayo. 

  Tangu Mwanzo wa Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Rwanda walionekana kuzidiwa na kiwango kilichoonyeshwa na Tanzania kupitia Nyota wake Mwanaidi Hassan aliyefunga 37 na Nasra Suleiman aliyefunga 19 waliokuwa mwiba kwa Timu ya Rwanda kutokana na kupachika magoli kila wapatapo mpira. 

  Tanzania iliweza kumiliki vipindi vyote vine vya mchezo huku Rwanda wakionekana kutoelewana kutokana na idadi ya magoli waliokuwa wakifungwa tangu Robo ya Kwanza mbayo ilimalizika kwa Tanzania kuongoza kwa 13-2 huku Robo ya pili 32-6 na Robo ya tatu 42-10.
  Kwa upande wake Mchezaji Nasra Suleiman alisema mbali na kupata ushindi huo lakini hawatobweteka kwani wanawasubiri Kenya ili kutangaza Ubingwa kwa kushinda Michezo yote. 

  Kwa upande mwingine Tim u ya Mpira wa Miguu ya Tanzania wameinyamazisha Timu ya Jeshi ya Kenya baada ya kuwafunga mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Kigali Nyamirambo.
  Katika Mchezo huo Kenya Ndio walianza kupata bao Muda mchache kabla kwenda mapumziko katika Dakika ya 42 kupitia kwa mchezaji wake Private Peter Onyango kabla ya Dakika tatu Baadae Private Prosper Mkwama kusawazisha bao na kwenda mapumziko wakiwa Sare.; 

  Kipindi cha Pili kilianza huku Timu zote zikifanya mabadiliko na kosa kosa ya magoli kwa Nyakati tofauti lakini Mnamo dakika ya 77 Private Abdulrahman Musa akaiandikia Tanzania bao la Pili na la ushindi.
  Kufuiatia matokeo hayo sasa Tanzania wamebakiza Mchezo mmoja na Rwanda utakaopigwa siku ya ufungaji Agosti 17 katika Uwanja wa Amahoro huku Timu ya mpira wa Pete wanatarajia kukutana na Kenya Agosti 14.

  0 0

   Mkandarasi kutoka kampuni ya Future Century Limited  ya  Tanzania Hellen Masanja (kushoto) akielezea utekelezaji wa usambazaji wa umeme  katika jimbo la Handeni Vijijini mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) katika eneo la Kweditilibe wilayani Handeni mkoani Tanga. Profesa Muhongo  yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisikiliza maoni yaliyokuwa yanawasilishwa na mmoja  wa wakazi wa Kata ya Kamgwe wilayani Handeni mkoani Tanga. Kulia ni Mbunge wa Jimbo  la Handeni Vijijini, Mboni Mhita.

   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akipokea zawadi  ya mbuzi kutoka kwa wakazi wa eneo la Kweditilibe wilayani Handeni mkoani Tanga
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisani kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika  kata ya Kwamgwe wilayani Handeni mkoani Tanga.
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea mikakati ya usambazaji wa umeme vijijini itakavyotekelezwa na  Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya  Tatu katika eneo la Kweditilibe wilayani Handeni mkoani Tanga

  Na Greyson Mwase, Tanga 

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa hakuna fidia yoyote itakayotolewa kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme vijijijni unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). 

  Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi kutoka katika vijiji vya Kweditibile na Kamgwe vilivyopo katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga. 

  Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi. 
  Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imetenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya usambazaji wa umeme vijijini ambapo iwapo fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kulipa fidia, inaweza kuathiri utekelezaji wa miradi ya REA .

  “Mkumbuke kuwa iwapo fedha hizi zitatumika kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha miradi ya umeme vijijini, fedha nyingi zitatumika na kukwamisha utekelezaji wa miradi ya REA,” alisema Profesa Muhongo 
  Aliendelea kusema kuwa miundombinu ya umeme haihitaji eneo kubwa hivyo haiwezi kuathiri mazao kwenye mashamba kama inavyoaminika na watu wengi .

  Alifafanua kuwa nishati ya umeme ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuongeza kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote nchini vinapata huduma ya umeme na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi Alisema kuwepo kwa nishati ya uhakika vijijini kutapelekea wanavijiji kuanzisha viwanda vya kusaga na kukoboa nafaka, kilimo cha kisasa na kuongezeka kwa ufaulu darasani. 

  Hata hivyo Profesa Muhongo alitoa agizo kwa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha kuwa wananchi waliostahili kuunganishiwa umeme kupitia REA Awamu ya pili wanaunganishiwa kabla ya mwezi Oktoba mwishoni kwa gharama ya shilingi 27,000. 

  Wakati huohuo Mbunge wa Handeni Vijijini, Mboni Mhita aliishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kasi kubwa ya usambazaji wa umeme vijijini na kuwataka wananchi wa jimbo lake kuchangamkia fursa hiyo.


  0 0  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwalusembe kweye hafla ya uziduzi wa kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe, ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani.
  .Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani.

  Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwasil katika kijiji cha Mwalusembe kwa ajili ya kuziduzi kisima cha Maji ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo mkoani Mpwani.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amezindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ,ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation
  Mara baada ya uzinduzi huo,Mh. Ulega aliwashukuru wafadhili hao na kuwaomba kuendelea kusaidia wilaya hiyo ili kukabiliana na uhaba wa Maji uliopo na kuwa Wilaya ya Mkuranga ni moja ya maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya Maji.
  Mh.Ulega Pia aliwataka wananchi wa kijiji hicho kutumia Maji hayo vizuri ikiwa pamoja na kulinda miundombinu yake ikiwamo solar na vinginevyo ili visiibiwe,Mh Ulega tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge wa jimbo hilo tayari ameshachimba visima katika vijiji zaidi ya vitano huku akisaidia kutatua mbalimbali ya wananchi ambayo yamekuwa kero kwao

  0 0


  Baadhi ya wanachama wa Comfort Zone waliopo Dodoma wakitoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Hasene kilichopo eneo la Chang'ombe wilaya ya Dodoma mjini.

  Misaada iliyotolewa ni vitu mbalimbali ikiwemo mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wajenzi wa madarasa na bweni la kulala watoto.
  Wanachama wa Comfort Zone wakiwa wamebeba baadhi ya Misaada kabla ya kuikabidhi kwa Watoto yatima wa kituo cha Hasene kilichopo eneo la Chang'ombe wilaya ya Dodoma Mjini.
  Wanachama wa Comfort Zone wakiwa wameketi na Watoto yatima Baada ya Kuwakabidhi Misaada mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia.

  0 0


  Wanafunzi wa darasa la nne wakionesha vipaji vyao vya kucheza nyimbo za asili


  Hapa ni katika shule ya msingi Little Treasures iliyopo eneo la Bugayambelele katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumamosi,Agosti 13,2016 kumefanyika sherehe ya maadhimisho ya miaka Mitano tangu kuanzishwa shule hiyo Julai mwaka 2011.

  Sherehe ya maadhimisho ya miaka mitano ya shule hiyo imefanyika katika eneo la shule hiyo na kuhudhuriwa na wazazi na walezi wa watoto,walimu,wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu.

  Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa alisema siku mbili kabla ya kilele cha maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, wanafunzi wa shule hiyo walitembelea Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija,Hospitali ya rufaaa ya mkoa wa Shinyanga na kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto soma <<HAPA>>.

  Nchagwa alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi wanne na sasa ina jumla ya wanafunzi 540.

  Naye Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic aliwataka wazazi na walezi kuendelea kushirikiana na shule hiyo ili kuhakikisha kuwa watoto wanaosoma katika shule hiyo wanatimiza ndoto zao huku akisisitiza kuwa mazingira ya shule hiyo ni rafiki kwa elimu bora ya wanafunzi.

  Aliongeza kuwa ni wajibu wa wazazi na walimu kushirikiana pamoja katika kuwalea watoto hivyo kuwasisitiza wazazi na walezi wa watoto kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao ili wakue katika maadili mema.

  Michezo mbalimbali kutoka kwa wanafunzi,wazazi na wafanyakazi wa shule hiyo ilikuwepo katika kunogesha sherehe hiyo. Mwandishi wetu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametusogezea picha 60 za matukio yaliyojiri..Tazama hapa chini

  Nje ya geti la shule:Bango likionesha kile kilichokuwa kinaendelea katika shule ya Little Treasures ambayo pindi tu ufikapo lugha ya kawaida zinazotumika ni Kiingereza,Kifaransa na Kiswahili kidogo

  Mbele ya jengo la utawala shule ya Little Treasures

  Muonekano halisi wa shule ya Little Treasures

  Keki maalum kwa ajili ya sherehe ya kuadhimisha miaka mitano ya shule ya msingi Little Treasures yenye wanafunzi zaidi ya 500 na walimu wa kutosha

  Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic akiwasalimia wageni mbalimbali waliofika katika sherehe hiyo ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule yake mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi wanne na sasa ina zaidi ya wanafunzi 500 kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga
  Wazazi wakiwa eneo la tukio wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

  Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akizungumza wakati wa sherehe ya miaka mitano ya shule hiyo.Kushoto ni wanafunzi wa shule hiyo

  wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

  Wageni waalikwa na wazazi wakiwa eneo la tukio

  Wanafunzi wa darasa la watoto (Baby Class) wakitoa burudani ya wimbo

  Wanafunzi wa shule ya awali daraja la pili (Middle Classa) wakiimba wimbo

  Wanafunzi wakiwa eneo la tukio

  Wanafunzi wa Middle Class wakitoa burudani ya wimbo

  Mmoja wa wanafunzi wa Middle Class akifundisha wazazi waliofika katika sherehe hiyo namna ya kutamka maneno
  Tunafuatilia kinachoendela hapa....

  Wanafunzi wa shule ya awali daraja la tatu/daraja la mwisho (Pre -Unit) wakiimba wimbo
  Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiunda umbo la muonekano wa shule yao ya Little Treasures

  Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiimba wimbo

  Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
  Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiendelea kutoa burudani

  Wazazi wakifurahia burudani

  Wazazi wakiwa eneo la tukio

  Wanafunzi wa darasa la pili wakitoa burudani

  Wanafunzi wa darasa la tatu wakikariri shairi

  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akisoma risala ambapo alisema pamoja na shule hiyo kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma kwa kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali,kuwa na mabasi ya kusafirisha wanafunzi hadi majumbani mwao sasa shule hiyo imefanikiwa kujenga bweni kwa ajili ya wanafunzi huku ikiendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa samaki,ng'omben.k

  Wazazi wakiwa eneo la tukio

  Pamoja na wanafunzi kuonesha michezo mbalimbali wazazi nao hawakuwa nyuma kushiriki katika michezo...Mchezo wa wazazi kukimbiza kuku ulichukua nafasi

  Wanafunzi wakishuhudia wazazi wao wanavyokimbiza kuku

  Mshindi wa shindano la kukimbiza kuku akiwa ameshikilia kuku wake

  Wanafunzi wa darasa la nne wakiimba na kucheza muziki

  Wazazi wakiwa chini ya mti wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

  Wanafunzi wa darasa la nne wakicheza Ngoma ya asili kutoka kabila la Kikurya
  Wazazi wakiwa eneo la tukio

  Wanafunzi wa kwaya ya shule wakitoa burudani

  Wanafunzi wa darasa la tano wakiimba wimbo wa Kifaransa

  Wanafunzi wa darasa la tano wakicheza

  Wanafunzi wa darasa la tano wakiendelea kutoa burudani

  Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Little Treasures Tilulindwa Sullusi akizungumza katika maadhimisho ya miaka mitano ya shule hiyo.Sullusi aliwataka wazazi kushirikiana na shule hiyo ili kuhakikisha kuwa watoto wanatimiza ndoto zao

  Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic akizungumza katika sherehe hiyo ambapo alisema wataendelea kushirikiana na wazazi,jamii inayowazunguka kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki ya elimu katika mazingira rafiki zaidi.

  Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic pia alihamasisha wazazi kuwasimamia watoto wao majumbani badala ya kuwaachia walimu pekee
  Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic alisema shule yake inaendelea kuibua vipaji vya watoto na kuomba jamii kupeleka watoto wao katika shule hiyo kwani ina mazingira rafiki ya elimu kwa watoto

  Washindi wa shindano la kusaka mtoto wa mfalme wa kiume na wa kike wa shule ya Little Treasures (Prince na Princess) wakiwa jukwaani

  Prince wa shule ya Little Treasures akipunga mkono kwa wazazi

  Wazazi wakiwa eneo la tukio

  Tunafuatilia kinachoendelea

  Wanafunzi wa darasa la sita wakionesha michezo mbalimbali
  Burudani inaendelea

  Wanafunzi wa darasa la sita wakionesha michezo yao

  Wanafunzi wakiimba na kucheza ngoma

  Wafanyakazi wa shule ya Little treasures wakijiandaa na shindano la kuvuta kamba.Shindano hilo lilikuwa kati ya wafanyakazi wa shule hiyo na wazazi wa wanafunzi

  Wazazi wakijiandaa kuvuta kamba...ambapo hata hivyo waliibuka washindi

  Keki maalum kwa ajili ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule ya Little Treasures

  Mzazi na wanafunzi waliozaliwa Agosti 13 wakikata keki kwa ajili ya wanafunzi,wafanyakazi wa Little Treasures,wazazi na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe ya kutimiza miaka mitano ikiwa pia ni sehemu ya kusherehekea siku zao za kuzaliwa

  Mzazi,watoto wakilishana keki

  Wanafunzi wakilishana keki

  Wazazi wa wanafunzi waanzilishi,wanafunzi waanzilishi na wafanyakazi wa shule ya msingi Little Treasures wakilishana keki

  Zoezi la kulishana keki linaendelea
  Mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic akifurahia jambo la wazazi

  Baada ya kufungua Shampen.... mzazi anagawa kinywaji kwa wanafunzi
  Mzazi akigawa kinywaji meza kuu

  Meneja wa shule ya msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akizungumza wakati wa kufunga sherehe hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alisema wanategemea kufungua shule ya sekondari mwaka 2018 .Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  Bofya <<HAPA>> Kuona matukio zaidi ya shule ya Little Treasures

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Mkoa, Makatibu Tawala Wasaidizi, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, baada ya kufungua Mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa viongozi hao wa Wilaya Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji. (wa pili kushoto)Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (kushoto)Mkuu wa Wilaya Busega, Tano Mwera na( kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo (hawapo pichani), katika Mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa viongozi hao Mjini Bariadi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini(kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka (kulia) kufungua Mafunzo elekezi kwa viongozi hao Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji.Mstari wa Kwanza kutoka kushoto Wakuu wa Wilaya,Tano Mwera (Busega), Seif Shekalaghe (Maswa), Joseph Chilongani (Meatu), Benson Kilangi (Itilima) na Festo Kiswaga (Bariadi). Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji. Kutoka (kushoto) Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Afisa Uhamiaji, Kamanda wa Zimamoto na Mkuu wa TAKUKURU 
   
  Na Stella Kalinga, SIMIYU

  Serikali Mkoani Simiyu imesema haiko tayari kuwavumilia na kuwaacha katika vyeo na majukumu waliyonayo watendaji wanaotoa takwimu zisizo za kweli.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyofanyika jana Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji, kwa kuwa baadhi ya viongozi hao wametoka katika sekta binafsi ambazo zina mifumo tofauti ya kitendaji na mfumo wa Serikali.


  “Tunawezaje kukaa na Mtendaji ambaye ukimwomba taarifa za upungufu wa madawati anadanganya, idadi ya wanafunzi anadanganya, walimu anadaganya tutamchukulia hatua tu. Lazima tupeleke ujumbe kwamba taarifa za uongo hazina nafasi tena katika Mkoa wa Simiyu. Namwagiza Katibu Tawala Mkoa, aanze kuchukua hatua stahiki dhidi ya watendaji wote waliotoa taarifa zisizo za kweli hususani katika takwimu za wanafunzi, walimu, madawati na vyumba vya madarasa”, alisema Mtaka.

  Mtaka amesema azma ya Serikali Mkoani humo ni kuhakikisha Nafasi za watendaji wasio waadlifu zinajazwa na watumishi waadilifu, wenye sifa na elimu ya kutosha waliopo katika Halmashauri za Mkoa huo.

  Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi hao wa Wilaya kubaini watumishi wenye sifa na uwezo wa kutekeleza majukumu ya Serikali katika maeneo yao na wawape fursa watumie talanta zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Pamoja na kubaini watumishi wenye sifa, viongozi hao wameelekezwa kuwachukulia hatua watumishi wanaopenda kufanya kazi kwa mazoea, ikiwa ni pamoja na kuwapangia majukumu yanayoendana na uwezo wao wa kufanya kazi.

  Katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, Mtaka ametoa wito kwa viongozi hao kuibua vyanzo vipya vya mapato na kusimamia ukusanyaji wa Mapato hayo kwa kuzingatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutowabugudhi wananchi wanyonge na akawataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya kuimarisha vikundi vya uzalishaji vya vijana na wanawake

  Sanjari na hilo Mtaka amewataka Viongozi hao wa Wilaya kutambua fursa za maendeleo katika maeneo yao na kuzitekelezafursa hizo kwa manufaa ya Wananchi walio katika maeneo yao.

  Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe, Tano Mwera alisema mafunzo hayo yamemsaidia kumpa mwanga na dira ya utendaji katika nafasi yake hasa katika utaratibu wa mawasiliano na mahusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa Mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi, Nafasi yake kama Kiongozi wa Serikali Wilayani pamoja na Sheria na Miongozo ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

  Mafunzo hayo ya siku moja kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambayo yaliongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini. yaliendeshwa na Makatibu Tawala Wasaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.

  0 0
 • 08/13/16--21:56: CLEZENCIA AMEREMETA
 • Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Tanzania Daima, Clezencia Tryphone akiwa amepozi kwa picha kabla ya kufunga ndoa na Joseph Singano katika Kanisa la Mt. Nicholaus Parokia ya Kunduchi jijini Dar es Salaam  Agosti 13 2016. (Picha na Francis Dande) 
  Akiwa ndani ya Gari.
  Akiwa mepozi kwa picha
  Tabasamu.
  Akiwa na furaha.
   Kuingia Kanisani.
  Maharusi wakiingia kanisani.
  Ibada ikiendelea.
   Joseph Singano akimvisha pete mke wake.
   Clezencia Tryphone akimvisha pete mume wake. 
  Clezencia Tryphone akiibusu pete baada ya kumvalisha.
  Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Tanzania Daima, Clezencia Tryphone akiwa na furaha baada ya kufunga ndoa na Joseph Singano katika Kanisa la Mt. Nicholaus Parokia ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Joseph akisaini cheti cha ndoa.
   Clezencia akisaini cheti cha ndoa.
   Wakipokea cheti cha ndoa.
   Wakionyesha
   Wakitoka kwa furaha.
   Pongezi
  Wakipita juu ya khanga wakati wakitoka kanisani.  

  0 0
 • 08/14/16--23:24: TANGAZO


 • 0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea maua ya ukaribisho
  Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akiwasili kanisani hapo kwa viongozi wa dini na wageni waalikwa
  Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akiwasili kanisani hapo kwa viongozi wa dini na wageni waalikwa
  Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akiwasili kanisani hapo kwa viongozi wa dini na wageni waalikwa
  Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akiwasili kanisani hapo kwa viongozi wa dini na wageni waalikwa
  Baadhi ya waumini wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kuingia ukumbini
  Baadhi ya waumini wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kuingia ukumbini
  Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akitoa neno la shukrani katika tukio hilo
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla katika kongamano hilo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga rasmi kongamao hilo la Shiloh 2016
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani
  Zoezi la kuwafariji Wamama Wajane likiendelea
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa nyuma ni baadhi ya Akina mama Wajane waliofarijiwa wakati wa kongamano hilo  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa nyuma ni baadhi ya Akina mama Wajane waliofarijiwa wakati wa kongamano hilo  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa salamu kwa Akina mama hao  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiondola baada ya kumalizika kwa kongamano hilo

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza machache kwa wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kongamano hilo.
   
   


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaomba viongozi wa taasisi za Dini na viongozi wa dini hapa Nchini kuhakikisha wanaendeleza maombi kwa kuliombea Taifa suala la Amani ili Nchi kubaki katika misingi yake mikuu ya kuwaletea wananchi wake Maendeleo pamoja na kudumisha amani iliyopo.

  Naibu Waziri Dk. Kigwangalla ameyasema hayo leo Agosti 14.2016 wakati alipokuwa mgeni rasmi kwa kumuakilisha Waziri wa Wizara hiyo. Mh. Ummy Mwalimu katika kufunga kongamano la Kimataifa la siku nne la SHILOH 2016, lililoandaliwa na Kanisa la Victorious Church Of Tanzania (VCT) lenye makao Makuu yake, Tabata Bima Jijini Dar es Salaam.

  Katika tukio hilo, Naibu Waziri aliweza kufunga rasmi kongamano hilo sambamba na kutoa sadaka kwa akina Mama Wajane sadaka zilizoandaliwa na kanisa hilo ilikuwasaidia akinamama Wajane mbalimbali.

  Akitoa neno la kupongeza kwa uongozi wa kanisa hilo, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa, hatua ya kanisa hilo kuwajali Wanamama Wajane ni la kuungwa mkono kwani ni miongoni mwa mambo yanayopaswa kuigwa na watu wote ambapo pia kwa hatua yao ya kuliombea amani Taifa pamoja na viongozi wake ndilo jambo jema katika Nchi.

  “Tunafanya kazi hii ya uongozi ni kwa uwepo wake Mungu kwani uongozi wetu sie ni Mungu ndiye aliyetaka tutumike na ndiye aliyetuita. Hivyo kufika kwangu hapa ni kuitika wito wa kuwatumikia watu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa neno kwa waumini huku akinukuu moja ya vifungu vya kwenye Biblia.

  Ambapo pia amewataka viongozi hao kuendelea kuzidisha maombi kwa kuimbea Serikali ya Tanzania kwani kwa kipindi hiki ili Taifa liwe na amani pamoja na wananchi wake wafanye mambo ya kimaendeleo.

  Aidha, katika hatua hiyo Dk. Kigwangalla alipata kuwafariji Wanawake Wajane ikiwemo kukabidhi baadhi ya zawadi kwa akina mama hao mchango uliotoka kanisani hapo.

  Kwa upande wake, Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Bishop Elis Musa Chessa amemwelezea Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla kuwa ni miongoni mwa Mawaziri wenye upeo mkubwa hivyo katika dhama za sasa ni kati ya viongozi wanaohitajika katika kuinua Taifa kwani vigezo alivyo navyo vinatosha kabisa kwa kipindi hiki na kuendelea kwa miaka ya baadae.

  “Tunaiombea Serikali yetu ya Tanzania kuwa na amani pamoja na viongozi wetu akiwemo Rais Dk. John Pombe Magufuli. Viongozi wote wa Serikali pamoja na Jamii nzima ya Tanzania” aliomba Bishop Elias Chessa.

  Kongamano hilo la Kimataifa la Shiloh 2016, lilianza Agosti 11 na kufikia tamati siku ya leo Agosti 14 huku likikusanya waumini mbalimbali kutoka ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania.

  Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokelewa wakati wa kuwasilia kwenye kanisa hilo la Victorious Church of Tanzania kufunga kongamano la siku nne la Kimataifa la Shiloh 2016, mapema leo Agosti 14.2016

  0 0

  The Sanlam Group is pleased to announce key leadership appointments which will support and further strengthen the Group’s Pan-African growth. This is also in keeping with the Group’s expanded footprint on the continent following the recent acquisition of a 30% stake in Morocco-based Saham Finances. These appointments will result in four distinct regionally focused units within Sanlam Emerging Markets (SEM) - Southern Africa; East Africa; North and West Africa; and South East Asia.

  With effect from 01 September 2016:

  · Mr Julius Magabe, the Managing Director and Chief Executive Officer of Sanlam Life Insurance in Tanzania since 2011, will assume the position of Regional Executive: East Africa for SEM. Magabe will remain based in Dar es Salaam. He will join the SEM Executive Committee and will be responsible for businesses in Kenya, Rwanda, Tanzania and Uganda.

  Among his successes at the helm of Sanlam Life Insurance, he is credited for growing the business and achieving 60% of the market share.

  Magabe is an alumnus of the Johannesburg-based Gordon Institute of Business Science (GIBS). He also holds an MBA from the Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) and is a graduate of the Institute of Finance Management Tanzania in Insurance and Risk Management. He joined Sanlam Life Insurance in Tanzania (formerly African Life Assurance) in 2007 as Head of Corporate Business. In 2010 he was appointed as Managing Director of the company, a position he has held up to now.

  · Mrs Margaret Dawes, currently SEM’s Executive Director: West and East Africa, will take up the position of Executive Director: North and West Africa. A Chartered Accountant, Dawes also holdsaBSc (Hons) Biology (London) and anHDip Tax Law (Wits).

  She joined Sanlam in 2005 as the chief financial officer for Sanlam Developing Markets (now SEM) and has held various other positions within SEM. In her new role, Dawes will be responsible for the SEM businesses in Nigeria, Ghana as well as those businesses in the North and West Africa region which are part of the recently established partnership with Saham Finances based in Morocco.

  Earlier this year, the Group made the following appointments:

  · Mr Gaffar Hassamas SEM’s Regional Executive: Southern Africa responsible for SEM’s businesses in Namibia, Botswana, Malawi, Zambia and Zimbabwe.

  An MBA graduate from Oxford Brookes, Gaffar is also a fellow member of Chartered Association of Certified Accountants (FCCA). Prior to his SEM appointment, Hassam was the Group CEO for Botswana Insurance Holdings Limited (BIHL) since 1 December 2011. Hassam joined BIHL in April 2003 as the Group Finance Manager and Company Secretary and held several positions within the Group, includingamong others, Head of Finance and Chief Operating Officer.

  · Mr Prasheem Seebran as SEM’s Regional Executive: South East Asia responsible for all SEM’s businesses in Malaysia.

  An Actuary, Seebran is currently completing his MBA at Henley Business School. He began his career at Marsh and held various positions at Guardrisk and Telesure before joining Sanlam in June 2013. In September 2013, hemoved to Malaysia where he has been responsible for all risk and capital related areas within Sanlam’s short term insurer, Pacific &Orient (P&O). He has also been in charge of developing P&O’s actuarial capabilities and has worked with the regulator on developing the risk management function and optimisation of capital.

  In June, Sanlam Group also announced the appointment of Mr Junior Ngulube as the Chief Executive Officer of SEM. Dawes, Hassam, Seebran and Magabe will report to Ngulube when he takes over from Mr Heinie Werth on 01 October 2016. Werth has been appointed the Group’s Financial Director with effect from 01 October, succeeding Mr Kobus Möller who will retire.

  Commenting on the appointments Sanlam Group CEO, Mr Ian Kirk, said: “On behalf of the Sanlam Group Executive Committee, SEM and staff, I wish to congratulate these colleagues. We are confident that they will continue to add value to the SEM business and support us in our journey as a Pan-African leader in financial services.”

  “We are pleased to have been able to fill the majority of these positions from organically grown Sanlam candidates through our succession planning and leadership development programmes, while balancing that by bringing in the right type of external exposure and experience.”

  The Group is in the process of appointing Magabe’s successor at Sanlam Life Insurance in Tanzania and an announcement will be made in due course.

  0 0  0 0

  Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji mafunzo kwa askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi
  Askari na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakipokea salamu za heshima kwa kupiga saluti wakati gwaride likipita mbele kwa heshima wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa Ngorongoro.
  Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi ,Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
  Askari na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
  Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witness Shoo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko wakifuatilia maonesho ya matumizi ya silaha kutoka kwa wahitimu hao.
  Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akisherehesha wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na Maafisa wa Hifadhi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.

  Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya jeshi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ,Freddy Manongi wakifuatilia maonesho hayo.

  Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitizama matundu ya risasi zilizolengwa na mmoja wa askari wa uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi. Wakufunzi wa Mafunzo ya kijeshi kwa maofisa na askari wa Hifadhi za Taifa wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi,(hayupo pichani). Mhifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Lilian Magoma akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa askari na maafisa wa uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
  Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Getrude Lyatuu akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
  Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Freddy Manongi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Alexander Songorwa akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuzungumza na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maofisa wa Hifadhi za Taifa . Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari na maofisa wa Hifadhi za Taifa. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika pichaya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.

  Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog ,Kanda ya Kaskazini.

  0 0


   Baadhi ya mafundi wa kampuni ya kutengeneza ndege ya Bombardier ya nchini  Canada wakiendelea kuipaka rangi moja ya ndege mpya za Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) nchini humo hivi karibuni. Ndege hizo zinatarajiwa kuingia nchini wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Septemba mwaka huu zikipishana kwa wiki moja.


  Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) limesema ujio wa ndege zake mpya mbili aina ya Bombardier Q400 zinazotarajiwa kuingia hapa nchini siku chache zijazo, utaleta mapinduzi makubwa kihuduma na kiutendaji kwa shirika hilo, huku shukrani zaidi zikielekezwa kwa Rais John Joseph Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kufufua shirika hilo.

  Akizungumza kupitia taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la hilo Muhandisi Patrick Itule alisema ujio wa ndege hizo utalirejesha shirika hilo kwenye biashara ya ushindani dhidi ya makampuni mengine ya ndege hapa nchini.

  Ndege hizo zinazotengenezwa na kampuni ya Bombardier ya nchini Canada zinatarajiwa kuingia nchini wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Septemba mwaka huu zikipishana kwa wiki moja.

  “Baada ya ujio wa ndege hizi hatuoni tena sababu ya sisi kukwama na tutakuwa tumeingia rasmi kwenye biashara ya ushindani kwa kuwa changamoto kubwa ya uhaba wa ndege ambayo imekuwepo kwa miaka kadhaa sasa itakuwa imeanza kutatuliwa,’’ alibainisha Muhandisi Itule huku akisisitiza kuwa shirika hilo halitakuwa tayari kuwavumilia wafanyakazi watakaoshindwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya sasa.

  Alisema shirika hilo tayari limeunda kikosi kazi kinachosimamia masuala mbalimbali likiwemo suala la mafunzo ya watendaji wake mbalimbali ili kuendana na matakwa ya biashara hiyo kwasasa.

  “Tumejipanga kuboresha mfumo mzima wa utendaji kazi na hiyo ni kuanzia mfumo wa ukataji tiketi na huduma zote muhimu kwa wateja ndio maana kwasasa tunawekeza zaidi kwenye ubora wa rasilimali watu ili kuwavutia zaidi wateja…uvutiaji ambao utaambatana na utoaji huduma kwa gharama nafuu,’’ aliongeza.

  Akizungumzia uwezo wa ndege hizo, Afisa Biashara wa shirika hilo Bw Josephat Kagirwa alisema zina uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na kwamba ujio wake utaongeza njia za kusafiri kwa shirika hilo kutoka njia mbili za sasa hadi kufikia njia zaidi ya kumi.

  “Tutakuwa na madaraja mawili yaani daraja la uchumi (Economy Class) litakalohusisha abiria 70 na daraja la biashara (Business Class) litakalohusisha abiria sita kwa kila ndege. Kwa ujio wa ndege hizi tutaweza kuongeza safari za ndani na baadae mwakani itakapopatikana ndege ya tatu kama Mheshimiwa Rais alivyoahidi ndipo tutaanza safari za nje ya nchi tukianza na nchi jirani,’’ alibainisha.

  Alitaja baadhi ya mikoa ambayo shirika hilo litaboresha zaidi safari zake kuwa ni pamoja na Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma, Tabora, Mpanda, Kilimanjaro, Mtwara, Zanzibar, Pemba, Bukoba pamoja na Visiwa vya Comoro. Hata hivyo alisisitiza kwamba safari hizo katika maeneo tajwa na kwingineko zitaanzishwa baada ya kufanyika kwa upembuzi yakinifu.

  “Lengo ni kuhakikisha tunakuwa tayari kutoa huduma nje ya nchi ndani ya muda mfupi iwezekanavyo ili tuweze kutimiza wajibu wetu kama shirika la ndege la taifa kwa kutangaza nembo ya taifa letu nje ya nchi, kusafirisha watanzania sambamba na kukuza utalii kwa kuwaingiza na kuwasambaza watalii ndani na nje ya nchi kwa urahisi,’’ alisema.

  Hata hivyo Bw Josephat alisema mabadiliko hayo yanaambatana na changamoto kadhaa huku akizitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na uhaba wa wataalamu wa kutosha kuendana na kasi waliyojiwekea, gharama kubwa katika uwekezaji wa teknolojia ya kisasa na gharama za vipuri na mabadiliko ya mara kwa mara yanayochangiwa na ushindani katika biashara ya anga.

  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk.
  Aggrey Mlimuka (kulia), akisalimiana na  Msaidizi wa Balozi wa China
  nchini Tanzania, Gou Hao Dong wakati wa semina iliyoandaliwa na ATE
  kwa kushirikiana na Ubalozi wa China pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu,
  Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kuhusu sheria za kazi,
  vibali vya kuishi na taratibu za kuingia nchini yenye lengo la kukuza
  mahusiano ya China na Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
  Salaam mwishoni mwa wiki.
   Meneja Kitengo cha Sheria wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),
  Suzanne Ndomba (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kisheria
  wakati wa semina iliyoandaliwa na ATE  kwa kushirikiana na Ubalozi wa
  China pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
  wenye Ulemavu kuhusu sheria za kazi, vibali vya kuishi na taratibu za
  kuingia nchini yenye lengo la kukuza mahusiano ya China na Tanzania.
  Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Msaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania,  Gou Hao Dong
  (kulia), akizungumza   wakati wa semina iliyoandaliwa na ATE  kwa
  kushirikiana na Ubalozi wa China pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,
  Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kuhusu sheria za kazi, vibali vya
  kuishi na taratibu za kuingia nchini yenye lengo la kukuza mahusiano
  ya China na Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam
  mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia maelezo mbalimbali
  ya watoa mada  wakati wa semina iliyoandaliwa na ATE  kwa kushirikiana
  na Ubalozi wa China pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,
  Ajira na Watu wenye Ulemavu kuhusu sheria za kazi, vibali vya kuishi
  na taratibu za kuingia nchini yenye lengo la kukuza mahusiano ya China
  na Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
  wiki.

  0 0


   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya ofisi yake ilivyojipanga katika kusimamia takwimu za taifa wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi leo jijini Dar es salaam.  Warsha hiyo inashirikisha wadau wa ndani na nje ya nchi.
   Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima akiongea na wadau wa takwimu wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi leo jijini Dar es salaam. Warsha hiyo inashirikisha wadau wa ndani na nje ya nchi.
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Afrika Kusini, Bw. Pali Lehohla akitoa maelezo kuhusu ofisi yake inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kausimamia takwimu za taifa hilo wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi leo jijini Dar es salaam.
  Washiriki wa warsha wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akitoa taarifa ya ofisi yake wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia leo jijini Dar es salaam.
  (picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO)

  Na May Simba na Eleuteri Mangi, MAELEZO
  SERIKALI kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imezindua mpango wa kuboresha matumizi ya takwimu sahihi katika kutekeleza malengo 17 ya dunia kwa maendeleo ya nchi.

  Akizungumza na wadau wa takwimu jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima amesema kuwa matumizi ya takwimu sahihi yataisaidia Serikali kutekeleza sera na mingo ya ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

  Malengo hayo ni pamoja na kutokomeza umasikini, njaa, kuimarisha afya na ustawi, Elimu bora, usawa wa jinsia, maji safi na salama, nishati mbadala kwa gharama nafuu, kazi zenye staha na ukuzaji uchumi, viwanda, ubunifu na miundombinu, na jamii endelevu.

  Malengo mengine ni matumizi na uzalishajinwenye uwajibikaji, kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, kuendeleza uhai katika maji, kulinda uhai katika ardhi, amani, haki na taasisi madhubuti pamoja na ushirikiano ili kufanikisha malengo.

  Dkt. Mlima amesema kuwa mpango huo uliozinduliwa utaisaidia Tanzania kufikia malengo ya maendeleo endelevu kulingana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025.

  Aidha, Serikali inaendelea kusimamia kuwekeza zaidi katika ukusanyaji wa takwimu sahihi kwa lengo la kuweka, kufuatilia na kutekeleza mipango yake kwa kulingana na malengo iliyojiwekea. 

  “Hatua hii itasaidia kuendeleza malengo ya SDG kupitia upatikanaji wa takwimu kwa njia ya uwazi ambayo itakuwa ya haraka kutuonyesha mapungufu na hivyo kutatua changamoto zinazoikabili jamii” Dkt. Mlima
  Dkt. Mlima amezitaka Wizara, Taasisi na Mashirika mbalimbali kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha uwepo wa usimamizi thabiti katika kupima matarajio ya maendeleo yanayokusudiwa. 

   Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kuja na mipango ambayo itahusisha matumizi sahihi ya takwimu zitakazoisaida Serikali kutatua changamoto zilizopo na kutoa mwelekeo katika kutekeleza sera za nchi.

  Vilevile, Dkt. Albina amesema kuwa, mpango huo utahusisha wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ambapo wamependekeza kuwepo kwa kamati itakayohusisha viongozi wa juu wa Serikali na kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi kwa kuwa wapo kwenye ngazi ya maamuzi.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Afrika Kusini, Bw. Pali Lehohla amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika suala la takwimu na kushauri mataifa mengine ya Afrika kujifunza namna  Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyopaswa kuongozwa na uongozi bora na imara.

  0 0


  Richard Owiti kutoka nchini Kenya akionesha kombe lake la ushindi mara baada kushika nafasi ya kwanza kwa wachezaji wa ridhaa,kwenye mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye (wa pili kulia).Kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango wakishuhudia kwa pamoja.


  Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi vifaa vya mchezo huo wa Gofu mshindi wa kwanza wa wachezaji wa ridhaa katika Mashindano ya Gofu ya wazi ya Tanzania,Richard Owit kutoka nchini Kenya,yaliofungwa jana jioni katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha,pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango. Mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko mkubwa yalishirikisha washiriki wapatao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Kenya na Unganda.
  Mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa kulipwa wa mchezo huo wa Gofu kutoka nchini Kenya,Jacob Okelo akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni sita,kwenye hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania ,yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya USA River na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye.
  Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja Afisa Maendeleo ya jamii na Uhusiano,Justine Kesi ikiwa ni sehemu ya kiasi cha fedha kilichotolewa na Wadhamini waliodhamnini mashindano hayo ya Gofu kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya huduma za jamii mbalimbali kwa vijiji vinavyozunguka viwanja vya Kili Golf,jijini Arusha.

  Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jana jioni wakati wa kufunga mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf- USA River  jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa kulipwa na ridhaa wa mchezo huo walishiriki.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA
  Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

  Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

  Wazir Nape (wanne kulia) akiwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wa Gofu hapo jana kabla ya kuhitimisha mashindano hayo
  Baadhi ya Wadau nao walikuwepo kufuatilia kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya Gofu jana jioni jijini Arusha

  Waziri Nape pia alikutana na wadau ambao walidhamini mashindano hayo ya Gofu

  Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimsikiliza Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA),Mh Godbless Lema,kwenye viwanja vya Kiligolf,USA-River jijini Arusha,ambapo Mh Nape alikuwa mgeni rasmi katika kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania.Pichani kulia ni Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
  Waziri Nape (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Gofu kwenye viwanja vya Kiligolf jijini Arusha,kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania,Chris Martin,Mkurugenzi wa viwanja vya Gofu (KiliGolf),Jerome Bruins,Mmoja wa wasimamizi waku wa kampuni ya Group Six International LTD,Janson Huang,na kushoto kwa Waziri ni Mke wa Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nassari,Mh Joshua Nassari,Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango pamoja na Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
  Waziri Nape akishiriki kucheza mchezo wa Gofu

  Waziri Nape akipata maelezo mafupi kuhusiana na uwanja huo wenye viwango vyote kimataifa cha Kiligolf.
  Waziri Nape akifurahia jambo na Mhe Nassri,kulia ni Mke wa Mh Nassari


  Waziri Nape pia alipata wasaa wa kutembelea mashimo ya mchezo huo wa Gofu yapatayo 18 ndani ya uwanja wa Kili Gofu,uliopo USA River jijini Arusha.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya Wastaafu, Ramadhan Maneno, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Jackline Liana, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
  Waziri Simbachawene akitoa hotuba yake
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Gerald Guninita, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba yake kuelezea huduma na fursa mbalimbali zilizopo kwenye Mfuko, wakati wa Mafunzo hayo
  Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea, ambaye pia ni Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa wakuu wa wilaya wastaafu
  Baadhi ya washiriki
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji kupitia mpango wa PSS
  Maafisa wa PSPF, wakifuatilia mafunzo hayo
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, (kulia), akiongozana na Meneja Masoko, na Mawasiliano wa PSPF, Costantina Martin, wakati wa mapumziko
  Waziri Simbachawene akitoa hotuba yake.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (katikati), akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Katibu wa Wakuu wa Wilaya Mstaafu, Betty Mkwasa, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Gerald Guninita, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
  Mkuu wa wilaya mstaafu Manju Msambya, akitoa neno la shukrani
  Waziri Simbachawene, akkimsikiliza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Omar Mangochie(kulia)
  Washiriki wakifuatilia kwa kusoma vipeperushi na kusikiliza

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili kwa wakuu wa wilaya wastaafu iliyoandaliwa na PSPF na kufanyika Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Wenine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji,Mwenyekiti wa Wakuu haoi wa Wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, George Yambesi, na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji, (katikati), wakionyesha fomu za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), mara baada ya waziri kufungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakuu wa Wilaya wastaafu, na Wanachama wastaafu wa Mfuko jijin Dar es Salaam, jana Agosti 15, 2016. Wazuru alimwakilisha Rais John Magufuli kufungua mafunzo hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu

  Mtaalamu wa Saikolojia Dkt. Chris Mauki, akitoa mada juu ya kudhibiti Stress
  Picha ya pamoja na viongozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, viongozi wa PSPF, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na kamati tendaji ya wakuu wa wilaya wastaafu
  Wakurugeni wa PSPF
  Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng' Issa, akitoa mada juu ya fursa zilizopo za uwezeshaji kwa watanzania
  Dkt. Kijaji akiteta jambo na Mkuu wa wilaya mstaafu, Betty Mkwasa

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia), akifurahia jambo baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi. Waziri Simbachawene, alijiunga na Mfuko huo mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wakuu wa wilaya wastaafu na maafisa wastaafu wa serikali kwa niaba ya Rais John Magufuli jijini Dar es Salaam Agosti 15, 2016.

  0 0

   Mchezaji  Mpira wa  Kikapu wa  Tanzania Mwaipungu  (mwenye Mpira) akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilifungwa
   
   Mchezaji  Mpira wa Mikono wa  Tanzania Bonnerge Kasanga (mwenye Mpira) akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilifungwa 26-15
   Mchezaji  Mpira wa Mikono wa  Tanzania Bonnerge Kasanga (mwenye Mpira) akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilifungwa 26-15(
   
   
  Na Selemani Semunyu JWTZ
   
  Timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kwa Mpira wa Pete wametangaza ubingwa wa michuano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki kwa mchezo huo yanayoendelea katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.
   
  Tanzani]a ilifikia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Kenya  39-33 katika Mchezo uliokuwa vuta nikuvute ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Timu hiyo kushinda na hivyo kupata alama ambazo haziwezi kufikia na Timu yeyote.Katika Mchezo huo Tanzania ilianza vyema tangu Robo ya Kwanza ambapo ilitoka 17-13 wakati robo ya pili 20-16 huku robo ya Tatu wakitoka 31 kwa 24 na mwisho Tanzania kuibuka Washindi.
   
  Nahodha wa Tanzania Dorita Mbunda alisema wanafuraha kwa kurejesha ubingwa walioupoteza mwaka jana na kuchukuliwa na Uganda.Nahodha wa Uganda Carlo Alepo alisema walikuwa na wachezaji wachanga amabao ni wageni katika mashindano hivyo wanajiandaa kwa michuano ijayo kwani wachezaji wao watakuwa na uzoefu Tayari wa Mashindano.
   
  Kikosi cha Tanzania kilichoibuka na Ushindi huo  ambacho kilicheza Mwanzol had Mwisho wa mchezo huo ni  Dorita Mbunda,Faraja Malaki,Joyce Kaira,Veronica Patric,Mwanaidi Hassan,Nasra Suleiman Na Lulu Joseph.Kwa upande wake  MaKocha wa Timu hiyo Grace Mgyabuso na Argentina  Kienzevya kwa Nyakati tofauti walisema  ahadi waliyoitoa kwa Watanzania na Mkuu wa majeshi wameitimiza kilichobaki ni kusubiri kukabidhiwa kombe. 
   
  Naye Kanali  Mary Hiki wa Tanzania  aliwapongeza wachezaji na kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao yaliyowawezesha kuibuka na ushindi huo ambao aliuita ni muhimu kwa Taifa.Awali Timu ya Tanzania iliifunga Timu ya Rwanda ambayo ni mabingwa wattezi kabla ya Kuwafunga Wenyeji Rwanda kwa matokeo ambayo hayajafikiwa na Timu yeyote katika Michuano hii.

  0 0
 • 08/15/16--08:39: Pangani Wapata Kivuko Kipya
 •  Kivuko cha Pangani II pamoja na kivuko kipya MV. Tanga
   Abiria, Magari pamoja na mizigo kwenye kivuko kipya cha pangani MV. Tanga
    Kivuko Kipya cha Pangani MV. Tanga baada ya kuwasili katika eneo la Pangani,Tanga.
  MV. Pangani II, ambayo imekuwa ikihudumia wakazi/wasafiri kati ya pangani na Bweni mkoani Tanga.
   
  Wananchi wa Pangani/Bweni mkoani Tanga wamepata kivuko kipya cha MV. Tanga, ambacho sasa kitasaidiana na MV. Pangani II kutoa huduma katika eneo la Pangani/Bweni. 

  MV. Tanga iliwasili Pangani siku ya ijumaa saa moja jioni, ikitokea katika bandari ya Dar es salaam ambako ndiko ujenzi wake ulifanyika. Ujenzi wa kivuko cha MV. Tanga umefanywa na Kampuni ya kitanzania iitwayo Songoro Marine Company Ltd.

  Akiongea na wananchi wa Pangani Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Lazaro Vazuri alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kivuko kipya cha MV. Tanga ni muendelezo wa sera ya Serikali ya kuboresha huduma kwa wananchi wake.

  Nae Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Lekujan Manase alisema “TEMESA imejipanga kuhakikisha kuwa vivuko vyake vyote vinafanyiwa matengenezo ya kinga kwa wakati, ili kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi wanaotumia vivuko hivyo inapatikana kwa wakati muafaka hivyo MV. Pangani II sasa itakwenda kwenye ukarabati na baada ya ukarabati huo vivuko vyote viwili vitabakia katika eneo la Pangani/Bweni ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.”

  Wananchi wa Pangani/Bweni wamekipokea kivuko cha MV. Tanga kwa furaha kubwa na kuiomba Serikali kutoa huduma ya kivuko kwa saa 24 kwa siku ili kuwasaidia wananchi hasa wa eneo la Bweni kupata huduma hiyo nyakati za usiku wanapohitaji kupata huduma za kijamii upande wa Pangani.

  MV. Tanga ina uwezo wa kubeba tani 50 ambazo ni sawa na kubeba abiria 100 na magari 6 kwa pamoja. Uwezo wa MV. Tanga unalingana na uwezo wa kivuko cha MV. Pangani II.
   
  Imetolewa na,
   Kitengo cha Habari na Mawasiliano TEMESA.
   

older | 1 | .... | 937 | 938 | (Page 939) | 940 | 941 | .... | 1897 | newer