Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 935 | 936 | (Page 937) | 938 | 939 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi juu ya utozwaji wa kodi za misaada inayotolewa na wadhamini kusaidia Sekta ya Maendeleo ya Michezo Nchini.

  Ufafanuzi huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo kutokana na habari iliyochapishwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Serikali kukosa mabilioni ya fedha kwa sababu ya kutokukusanya kodi ya fedha zinazotolewa na wadhamini kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  “Fedha zinazotolewa kama msaada kutoka kwa wadhamini huwa hazikatwi kodi lakini TRA hupata mapato yake kutokana na matumizi ya fedha hizo hasa pale wahusika wanapozitumia katika shughuli za kiuchumi”,alisema Kayombo.

  Kayombo ametaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazoweza kuwaingizia mapato kutoka kwenye misaada hiyo kuwa ni; kodi za waajiriwa wakiwemo makocha na wachezaji, makusanyo ya uwanjani ,kupewa huduma za kitaalam pamoja na majengo ya kupangisha au kupanga.

  Amefafanua kuwa kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) linakodisha jengo basi fedha wanazopata lazima walipe kodi ya asilimia 10 kutoka kwenye fedha hizo na kama wao ndio wamekodi jengo kwa ajili ya matumizi yao wanatakiwa kutoa kodi ya asilimia 5.

  Kwa upande wa kodi kutoka kwa waajiriwa, Mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimu kwa vilabu vya michezo kuwa michezo ni ajira kama ajira zingine hivyo mishahara yao inatakiwa kukatwa kodi kulingana na kiasi wanacholipwa.

  Zoezi la kuwatoza kodi makocha na wachezaji limeanza rasmi mwaka huu.
   
  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  0 0

  Mbunge Abdallah Ulega wa Jimbo la mkuranga akiwa sambamba na watendaji na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo akikagua mradi wa ufugaji wa samaki unaondeshwa na kikundi cha ufugaji samaki katika kijiji cha kibewa.Mh Ulega anaendelea na ziara zake za kushukuru wananchi wake.

  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akimsikiliza Mganga wa Zahaniti ya Kijiji cha Sotele,Emily Bugingo kilichopo kata ya Dondo bara baada ya kutembelea Zahanati hiyo leo Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,Globuya jamii)
   

  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibewa kilichopo kata ya Dondo mkoani Pwani ,ambapo katika mkutano huo Mh.Ulega aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kisha akatumia fursa hiyo kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi .

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Juma Abed akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Kijiji cha kibewa ambao aliwataka kumtumia mbunge wao Ulega na kwamba ni muda wao sasa kumbebesha majukumu yao kwani ndio kazi waliyompa,na zaidi kuacha siasa na kujikita kufanya kazi.

  Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Jumbe Kazenga wa kijiji cha Kibewa Kata ya Dondo akitoa ya moyoni kwake kwa mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah ulega ambapo pamoja na mambo mengine alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoianza,ulega yupo katika ziara ya kushukuru kwa wananchi wake baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
  Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Jumbe Kazenga wa kijiji cha Kibewa Kata ya Dondo akitoa ya moyoni kwake kwa mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah ulega ambapo pamoja na mambo mengine alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoianza,ulega yupo katika ziara ya kushukuru kwa wananchi wake baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga wilayani Pwani Abdallah Ulega amewaondoa hofu wananchi wake na kuwaeleza kuwa wasiwe na wasiwasi kwani Rais Dkt.Magufuli ana nia njema kwa watanzania
   
  Mh.Ulega ametoa kauli hiyo wilayani Mkuranga katika mkutano wake wa kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Sotele kilichopo kata ya Dondo wilayani humo. Amesema kuwa hakuna haja ya kumchukia Rais kwani anayoyafanya Rais leo yamesababishwa na watu wachache ambao Kazi yao ilikuwa ni kujijali wenyewe tu na si vinginevyo na pia waliwasahau wananchi kuzisikiliza shida na kero zao na kuzifanyia kazi.
   
  ."Mnajuwa Rais anadhamira ya dhati kabisa na watanzania na katika bajeti ya mwaka huu ndio maana ametenga  fedha nyingi ambazo zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi hivyo kinachotakiwa ni kumuunga mkono na kuzidi kumuombea tu"amesema Ulega.
   
  Akizungumzia maendeleo ya jimbo la Mkuranga alisema amejipanga kikamilifu kuwaletea maendeleo wananchi wake na ndio.maana anapita kuwashukuru na kuhimiza maendeleo.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema siku ya Agosti 11.2016 amekutana na wadau wa Sekta ya Afya kutoka taasisi Touch Foundation kuangalia namna ya kusaidia sekta ya Afya hasa kwa maeneo ya pembezoni mwa Nchi ili kuimalisha hudumm hizo.

  Ugeni huo kutoka katika Taasisi ya Touch Foundation ya nchini Marekani umeonyesha nia yake ya dhati ya kuendelea kusaidiana na Wizara ya Afya ya Tanzania ikiwemo huduma za akina mama Vijijini.

  Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amekutana na ugeni huo ofisini kwake ukiongozwa na Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Touch Foundation ambae pia ni mstaafu kutoka katika kampuni ya McKinsey, Bwana. Lowell Bryan ambaye pia alishawai kuwa mshahuri kwa miaka mingi huko kipindi cha nyuma katika masuala ya Afya ya Tanzania.

  Ujumbe wa ugeni huo una miradi mbalimbali kama kuzalisha wataalam wa afya, kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto kwa kuboresha mfumo wa rufaa kutoka kijijini kuja mpaka mahala watakapopata huduma na kwa sasa wameanza na wilaya mbili za Sengerema na Shinyanga Mkoani Shinyanga.

  Akielezea muda mfupi baada ya majadiliano na ujumbe huo Dk. Kigwangalla alibainisha kuwa Wameonyesha nia ya kuendelea kuisaidiana na Tanzania katika masuala ya Afya hivyo mikakati ya itaendelea kuwa endelevu hasa katika miradi ya kusaidia kupunguza vifo kwa akina Mama Wajawazito.

  “Mradi wao wa kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito pamoja na watoto, unatekelezwa kwa kuboresha mfumo wa rufaa kutoka kijijini kwa wakinamama wajawazito kuja mpaka wanapoweza kupata huduma za kiafya hii ni pamoja na Kituo cha Afya ama Hospitali kubwa.

  Wametengeneza utaratibu wa usafiri, mawasiliano ya simu na kuwapatia wahudumu posho katika Wilaya ya Sengerema na shinyanga wakishirikiana na Vodafone Foundation.

  Watatusaidia kutengeneza mikakati ya kiufundi ya namna ya kuboresha huduma za afya ya msingi, huduma hizi za msingi ni kama vituo vya afya na zahanati ikiwa ni pamoja na kutupa utaalam katika eneo la kufanya tathmini ya rasilimali watu katika sekta ya afya, kuanzia gharama za kuajiri madaktari ama kada za chini” aliongeza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla.

  Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza jambo kutoka kwa wageni (Hawapo pichani) wakati wa mazungumzo juu ya uwekezaji wa katika sekta ya Afya.
  Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Touch Foundation ambae pia ni mstaafu kutoka katika kampuni ya McKinsey, Bwana. Lowell Bryan akimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
  Ugeni katika mkutano huo.
  Majadiliano yakiendelea.Bwana. Lowell Bryan akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati wa mkutano huo uliofanyika ofisini kwa Naibu Waziri, Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Abushehe Nondo (MAELEZO).

  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema kuwa bado inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa usafiri wa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es Salaam.

  Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA, Bw. David Mziray ambaye alibainisha kuwa kwa sasa bado wanaendela kupokea maoni kutoka kwa wadau kama sheria ya mamlaka hiyo inavyoelekeza kabla ya kuja na kiwango rasmi cha nauli ya usafiri huo.

  “Tumetoa muda mpaka Agosti 19 mwaka huu iwe ndio mwisho wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusiana na bei elekezi ya nauli kwa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu” Alisema Mziray.

  Pia, Mziray alifafanua kuwa kwa kipindi hiki ambacho wanapokea maoni wameielekeza Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) waendelee kutoza nauli ya shilingi 400 kwa watu wazima na shilingi 200 kwa watoto na wanafunzi mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo.

  Alieleza kuwa tangu usafiri huo wa treni uanze huduma zake imeonekana kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri muda mrefu njiani na sasa wanaweza kuwahi katika maeneo yao ya kazi na biashara wakiwemo wanaokwenda kwenye soko la Kimataifa la samaki la Ferry.

  Aidha, aliongeza kuwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya usafiri pasipo na matatizo yoyote kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inatarajia kuongeza mabehewa kutoka 15 yaliyopo sasa hadi kufikia mabehewa 20.

  Akizungumzia baadhi ya changamoto walizoziona tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo ya usafiri wa Treni alisema kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma ya vyoo na maji katika baadhi ya vituo.

  “Tunatarajia hivi karibuni Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) itajenga vituo vipya na kufanya ukarabati kwenye vituo vya zamani ili kuweza kuwaondolea usumbufu wananchi kwa kuweka huduma mbalimbali ikiwemo vyoo na maji kwenye vituo hivyo” Alisema Mziray.

  Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu ilizinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam hasa wakazi wa maeneo ya Gongolamboto, Pugu na Chanika.

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Aziz Ponary Mlima akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi wakati akifungua warsha ya kimataifa kuhusu mpango wa takwimu za malengo ya maendeleo endelevu uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Alibina Chuwa (kushoto), akihutubia katika warsha hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (katikati), akipitia nyaraka kwenye warsha hiyo. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
  Warsha ikiendelea.
  Wadau wa maendeleo wakiwa kwenye mkutano huo.

  Wadau wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.

  Wanahabari wakiwa kwenye warsha hiyo.
  Warsha ikiendelea.
  Taswira ya meza kuu kwenye warsha hiyo. Kutoka kulia Dk. Verena Knippel, Mratibu wa Shirika la Global Partinership, Sanjeev Khagram, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Alubina Chuwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Aziz Ponary Mlima, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban, na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

  0 0

  Na Georgia Misama – MAELEZO

  Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imejipanga kutoa huduma bora kwa mashirika na taasisi zinazotarajia kuhamia Mjini Dodoma.

  Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano TTCL Bw. Nicodemus Thom Mushi leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa miaka mitatu wa mageuzi ya kibiashara wa Kampuni hiyo.

  Mushi ameeleza kuwa, katika mpango huo TTCL imejipanga vyema kufanikisha azma ya Serikali ya kuhamia mjini Dodoma kwa kutoa huduma bora kwani tayari kampuni hiyo ina rasilimali watu, vifaa na wataalamu wa kutosha katika kutoa huduma za Mawasiliano.

  “Nitumie fursa hii kuwaomba taasisi zote za Umma zinazohamia Dodoma na Taasisi zote kwa ujumla kutumia huduma za TTCL ambazo zote zimethibitika kuwa ni huduma bora na za uhakika na zenye gharama nafuu,” amefafanua Mushi.

  Aidha, kampuni hiyo imeboresha njia ya kusikiliza wateja ambapo hivi sasa malalamiko ya wateja hushughulikiwa ndani ya masaa matatu toka mteja anapotoa taarifa katika kituo cha huduma kwa mteja.

  Akiongelea juu ya maboresho, Mushi amesema kuwa, kampuni hiyo imeleta huduma mpya ya 4G LET ambayo inapelekea intaneti yenye kasi zaidi, vile vile imeboresha miundo mbinu ya mitandao ya simu na data na kuondoa mitambo chakavu.

  Sambamba na hayo Mushi amewahakikishia wateja kuwa TTCL ni kampuni pekee ambayo ni suluhisho la huduma bora na ya uhakika wakati wote na mahali popote iwe ni nyumbani, sehemu ya kazi na hata kwenye vyombo vya usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine

  0 0

  §  Wateja watashuhudua huduma za ubora wa hali ya juu kutoka kwa watoa huduma.
  §  Itaongeza asilimia 27 ya ongezeko la ukuaji kibiashara kati ya Shanghai-Abu Dhabi.
  §  Abu Dhabi inaunganisha zaidi ya mataifa 40 eneo la Ghuba, Ulaya, Afrika na Amerika Kusini.

  Shirika la Ndege la Etihad limeanzisha safari mpya ya ndege yake ya kisasa ya Boeing 787 Dreamliner kwenda Shanghai kutoka Abu Dhabi. Ndege hiyo yenye ubora wa kiwango cha juu kwa daraja la kati na kwanza pamoja na wahudumu waliobobea, ina jumla ya viti 299 ambapo daraja la kwanza ina viti 28 na daraja la kati kuna viti 271 ikiwa na uwezo wa kufanya safari nane ikiwakilisha ongezeko la asilimia 14 katika safari zake

  Ndege ya Etihad EY862 kutoka Abu Dhabi iliondoka saa nne na dakika 25 Agosti 02 ikitokea Mashariki ya kati na kuwasili Shanghai saa tano na dakika kumi asubuhi ya tarehe 03 Agosti. Ndege hiyo iliyozindua safari zake iliondoka tena Agosti 03 saa sita kamili mchana siku hiyo hiyo. Sherehe hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na wadau wa usafiri wa anga waliopo nchini China.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema,”Tangu kuzinduliwa usafiri wa anga kati ya Shanghai na Abu Dhabi katika kipindi cha miaka minne iliyopita, tumeshuhudia ukuaji mkubwa katika sekta ya utalii nchini China na kuongezeka kwa wateja.”

  Uamuzi wa kuongeza ndege ya kisasa ya Boeing 787 inatokana na umuhimu wa sekta ya anga kati ya Shanghai na Abudhabi. Shanghai ni mji wa kisasa unaokua kwa kasi kiuchumi, kibiashara, usafirishaji kwa bandari jambo ambalo limeisukuma Shirika la Etihad kuwa kiungo muhimu kwa kuanzisha ndege mpya ya kisasa katika eneo hili.

  Bwana Baumgartner aliongeza, “Huduma za Ndege mpya ya Boeing 787 itasaidia kuvutia na kukuza utalii ndani na nje ya Shanghai na miji inayoizunguka mashariki mwa China. Kwa kuongeza hii itawezesha ukuaji wa biashara China na wateja kufurahia huduma bora ya usafiri wa ndege ya kisasa kwa kuwaunganisha na Abu Dhabi na mataifa zaidi ya 40 Ukanda wa Ghuba, Ulaya, Afrika na Amerika Kusini.

  Kwa mujibu wa Global Business Travel Association, China ndiyo taifa linaloongoza katika soko la kibiashara ukiacha Marekani ambapo iliwekeza zaidi ya Dola za kimarekani milioni 291.2 katika mwaka 2015. Ndege hiyo ya kisasa itawezesha Shirika la Ndege la Etihad kuimarika kibiashara katika jamii ya China kwa kuanzisha ndege ambayo itawavutia wateja wa aina mbalimbali kwenye soko la usafiri wa anga.

  Wateja watajipatia huduma zote muhimu wanapokuwa kwenye sehemu za mapumziko na baada ya ndege kutua. Kuna huduma ya mapumziko inayopatika kwenye miji zaidi ya 30 ikiwamo Beijing na Shanghai. Wawapo katika Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi, wageni hupatiwa huduma bora zenye ubora wa hali ya juu kupitia sehemu maalumu walizotengewa kupumzika huku wakifurahia huduma inayotolewa kupitia eneo maalumu kwa wateja wa daraja la kwanza na  kutoka kwa wakala wa huduma wa Shirika wa Etihad (EAP).

  Katika ndege hiyo mpya, kwenye daraja la kati kuna eneo ambalo litamwezesha mteja kupata huduma mbaliambali ikiwamo runinga yenye ukubwa unaomwezesha kuona vyema, pia kuna nafasi ya kutosha kumwezesha mteja kuwa huru.

  Pia, kuna viti ambavyo vinampa uhuru wa kukaa na kuna mifumo ambayo inamwezesha mteja kusogeza kiti kwa kadiri anavyohitaji. Na kila chumba maalumu kwenye ndege hiyo kuna runinga ya kisasa ikiwa na vidhibiti sauti.

  Wageni wanaotumia usafiri wa daraja la kati, wanayo fursa ya kuchagua chakula wanachotaka jambo linalowapa nafasi kuchagua wanachotaka wawapo safarini. Kila daraja lina huduma maalaum ya kutoka kwa watoa huduma wa Etihad. Aidha wateja wanakuwa na wigo wa kuchagua chakula wakipendacho kutoka wa wasimamizi wa vyakula na watoa huduma hao hutoa msaada wa karibu kwa  wazazi ambao huwa wanasafiri na watoto.

  Mathalan kwenye ndege hiyo, burudani inapatikana. Kuna mfumo wa muziki wa kisasa wa Panasonic eX3 IFE ambao unapatikana kwenye ndege ya Boeing 787s na Airbus A380s.

  Mteja ataweza kufurahia mfumo wa bure wa intanteti kwa ajili ya simu na kumwezesha pia kutazama chaneli mbalimbali za runinga kipitia satellite ikiwa ni matangazo ya moja kwa moja.

  Kwa wateja wa daraja la kati, ndege hiyo ina viti vyenye ubora ambavyo kuna vifaa maalumu vya kusikilizia muziki, pia viti vyake vikiwa na nafasi ya kutosha kwa kila mtu kukaa kwa uhuru huku akiburudika na televisheni inayopatikana kwa kila kiti.

  Ndege imetengenezwa ikiwa na vifaa vya kudhibiti unyevunyevu pamoja na mgandamizo wa hewa ili kumfanya mteja ajisikie vyema awapo safarini.

  Shanghai ni sehemu ya saba kufikiwa na huduma ya ndege hiyo ya kisasa ya B787-9 Dreamliner. Maeneo mengine ambako ndege ya aina hiyo inafanya safari zake ni Perth, Brisbane, Singapore, Washington DC, Zurich na Düsseldorf.
  Shirika la Ndege la Etihad kwa mara ya kwanza lilizindua safari zake mara tano kwa wiki  kwa kutumia ndege ya A330-220 kwenda Shanghai tangu Machi 2012.

  Ratiba kwa ndege za Abu Dhabi-Shanghai:

  NAMBA YA NDEGE.
  MAHALI INAPOTOKA
  KUONDOKA
  INAPOKWENDA
  KUWASILI
  KIPINDI
  AINA YA NGEGE
  EY862
  Abu Dhabi
  (AUH)
  22:25
  Shanghai
  (PVG)
  11:10 next day
  Daily
  B787-9
  EY867
  Shanghai
  (PVG)
  00:30
  Abu Dhabi (AUH)
  06:15
  Daily
  B787-9


  Zingatia: Safari zote za kuondoka na kuwasili zimewekwa kulingana na muda wa eneo husika.

  0 0

  WANAWAKE wapata mafunzo ya kuwajengea uwezo kiuchumi pia wamehimizwa kutambua fursa za kiuchumi, kupambana na changamoto mbalimbali zinazomzunguka pamoja na kujihusisha katika shuguli za vikundi ili  kujiletea maendeleo na kupunguza umaskini.

  Hayo yamabainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi  ya MIBOSCO, Moses Emena  wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha Wanawake Kiuchumi  lililofanyika leo kunduchi Mtongani jijini Dar es salaam leo. 

  Jukwaa hilo limewakutanisha Wanawake wapatao 150 likiwa na lengo la kuwapa elimu wezeshi Wanawake katika  harakati za  kutokomeza umaskini na kupambana na unyanyasaji wa aina zote ndani ya jamii zetu kwa kuendeleza elimu, haki na uhifadhi wa mazingira .

  Moses Emena  amesema “ Jukwaa hili limedhamiria kuleta mwamko na hamasa chanya kwa Wanawake wa eneo hilo katika harakati za kujikomboa kiuchumi.” ameongeza kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo, katika harakati za kupamba na umaskini.

  Emena  pia  amewashkuru wawezeshaji wa mafunzo hayo  Kampuni Trumark kwa kukubali kujitolea kutoa mwongozo wa maandalizi na kutoa elimu wezeshi kwa Wanawake na kushirikiana nasi bega kwa bega katika kufanikisha siku ya leo.

  Vile vile aliwashuru kwa dhati wadhamini na wadau wa maendeleo ya Wanawake Kampuni ya Vodacom Tanzania na Shirika la  Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kujitoa kwao kuwezesha,  bila kuwasahau wangeni waalikwa kutoka taasisi za fedha Akiba Commercial Bank, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, waandishi wa habari na wengine wote.
    Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba akizungumza na wanawake 150 katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililofanyika Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi wa Trumark, Agnes Mgongo akitoa somo la fursa kwa wanawake wapatao 150 waliohudhulia katika ufunguzi wa jukwaa la wanawake kuwezeshwa kiuchumi jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MIBOSCO, Moses Emena akizungumza na wanawake wapatao 150 kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi.
   Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa NSSF, Stella Kabyemere akizungumza na wanawake wapatao 150 kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi.
   Afisa  utafiti wa NSSF, Musa Chande akitoa somo kwa wanawake 150 jinsi ya kujiunga na NSSF katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa Mikopo wa Benki ya ACB akizungumza .
  Mwakilishi wa VODACOM Tanzania akizungumza  na wanawake wapatao 150 kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

  Meza Kuu.
   Wafanyakazi wa Trumark Tanzania.
    Mfanyakazi wa Trumark Tanzania akitoa somo kwa wanawake leo jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa VODACOM Tanzania akizungumza  na wanawake wapatao 150 kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi.   Wanawake wakisikiliza somo likiendelea.
   Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi  ya MIBOSCO, Moses Emena akiteta jambo na Mc wa shughuli ya Leo.
   Mwanamke akichangia maada leo.
   Kwaya ikitumbuiza.

  Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi  ya MIBOSCO, Moses Emena na wafanyakazi wa Trumark Tanzania wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mesigwa Baregu (kulia), akizungumza katika kongamano la Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha), ikiwa ni maadhimisho ya siku ya vijana duniani lililofanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Mtoa mada katika kongamano hilo, David Kafulila.
   Mtoa mada katika kongamano hilo, David Kafulila akichangia mambo mbalimbali.
   Meza kuu katika kongamano hilo.
   Mkutano ukiendelea.
   Mada zikiendelea kutolewa.
   Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali.
  Usikivu ukiwa umetawala katika ukumbi huo.


  0 0


  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliofika kumlaki mara baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiendelea kuwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa chama hicho Rais Dkt John Pombe Magufuli,mara baada ya kuingia ofisini kwake na kusaini kitabu cha wageni na kisha kuwasalimia Wanachama na Wananchi waliofika kumlaki mapema leo Nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akizungumza kama Mwenyeji wa mapokezi ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk, John Magufuli.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akimkaribisha Kinana kumkariisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli kuzungumza na wana CCM na wananchi, Nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam, leo
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa kabla ya kumkaribisha Dk. Magufuli
  Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi na wanachama wa CCM mbalimbali waliofika kumlaki Mwenyekiti mpya wa chama hicho,Rais Dkt John Pombe Magufuli .

  Wananchi wakifuatilia ujio wa Mwenyekiti Mpya wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli

  Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Johnn Magufuli akipokewa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika katika ofisi hiyo, akiwa Mwenyekiti wa Chama. Kulia ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda mara baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo


  Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga tumba baada ya kuongea na wana-CCM nje ya Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016,huku umati mkubwa wa Wanachama na wananchi wakifuatilia. 

   Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiteta na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipokaribishwa kwenye Ofisi ndogo ya CCm jijini Dar es salaam na kuzungumza na Wana CCM na wananchi Agosti 12, 2016
   Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiteta na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipokaribishwa kwenye Ofisi ndogo ya CCm jijini Dar es salaam na kuzungumza na Wana CCM na wananchi Agosti 12, 2016.

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisaini kitabu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), kumuonyesha Ofisi yake Mwenyekiti huyo, alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Wazir Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia na Mweyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akitoa maneno ya kumkaribisha rasmi kwenye Ofisi yake ya Uenyekiti wa CCM, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.


  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi mpira Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga ikiwa ni ishara ya Naibu Waziri huyo kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini humo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waendesha Pikipiki/Boda Boda (hawapo pichani) kabla ya kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini humo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Kulia ni Wafadhili wa Mashindano hayo.

  Sehemu ya waendesha Boda Boda jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati kiongozi huyo alipokuwa anazungumza na madereva hao kabla ya kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini humo. Mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini Dar es Salaam na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akilionyesha Kombe ambalo Mshindi wa Kwanza atakabidhiwa mara baada ya kumalizika Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ameyazindua mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiijaribu pikipiki mpya ambayo atakabidhiwa Mshindi wa Kwanza mara baada ya kumalizika Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ameyazindua mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti) akimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga wakati alipokuwa anazungumza na Waendesha Boda Boda (hawapo pichani), kabla ya Naibu Waziri Masauni kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Kamanda Mpinga alisema Mashindano hayo ambayo yameshirikisha Wilaya za Temeke, Kinondoni na sasa Ilala yanatarajiwa kumalizika Septemba 18, 2016. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aonyesha zawadi ya Saa aliopewa na Wahandishi Wanawake (TAWESE) kwenye Kongamano la Pili la Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mhandisi Mshauri Bi. Warda Ester Mash'mark alipotembelea banda lake wakati wa Kongamano la Pili la Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Anifa chingumbe wa TTCL namna ambavyo mtandao wa 4G LTE unavyofanyakazi alipotembelea banda la TTCL kwenye Kongamano la Pili la Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Kongamano la Pili la Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
  Sehemu ya Waandishi waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais.
  Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Steven Mlote akihutubia kwenye Kongamano hilo la Wahandisi Wanawake.
  Mwakilishi wa Balozi wa Norway akihutubia kwenye Kongamano hilo la Wahandisi Wanawake lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam.
   
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wahandisi wanawake nchini kufanya kampeni maalum ya kushawishi watoto wa kike kujenga ari ya kusoma masomo ya sayansi na hisabati kama hatua ya kuongeza maradufu wahandisi wanawake nchini.

  Makamu Rais ametoa kauli hiyo 12-Aug-16 wakati anafungua kongamano la maonyesho ya kitengo cha wahandisi wanawake cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

  Amesisitiza kuwa kampeni hiyo itasaidia kuelimisha wasichana,kuwaunganisha na kuwaendeleza watoto wa kike ili waweze kujitambua na kuithamini nafasi yao katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia fani za sayansi na teknolojia.

  Makamu wa Rais amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa wahandisi katika maendeleo ya nchi hususani katika sekta za nishati,madini,barabara,maji,uvuvi na kilimo imeendelea kuweka mipango madhubuti ya kuinua na kuimarisha fani ya uhandisi hapa nchini.

  Ameeleza kuwa serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuongeza vyuo vya uhandisi kutoka chuo Kimoja mwaka 1970 mpaka vyuo Tisa hivi sasa na kuongeza maabara katika shule za umma ili kuwavutia wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amepongeza baadhi ya halmashauri nchi ambazo zimekamilisha ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari na kuweka vifaa vyote vya kujifunzia.

  Kuhusu wakandarasi wa ndani ya nchi, Makamu wa Rais amesema serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa wenye uwezo katika ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ili kuwajengea uwezo.

  Amesisitiza kuwa matumizi ya wakandarasi wazawa wenye uwezo wa kufanya kazi yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania kuliko kutumia wakandarasi wa nje ambao mara nyingi baadhi yao wanaajiri watalaamu kutoka kwenye nchi wanazotoka kuliko kuajiri Wataalamu wa hapa nchini.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameshauri Taasisi ya Wahandisi Tanzania iendelee na jukumu la kuwaunganisha wahandisi wote watanzania ndani na nje ya nchi kwa manufaa ya taifa na ameishukuru serikali ya Norway kwa mchango wao wa shilingi bilioni 4.3 ili kuchangia mpango wa miaka Mitano kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 ambao utasaidia kuwajengea uzoefu wahandisi wanawake ili waweze kusajiliwa na bodi ya usajili ya wahandisi nchini.

  Makamu wa Rais amesema mpango huo pia unatarajiwa kunufaisha wanafunzi wa kike 150 nchini na utaisaidia serikali kufanikisha lengo la kufikia uchumi wa viwanda na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya ameiomba serikali ihakikishe inakamilisha mpango wa kuweka vifaa kwenye maabara za shule za sekondari kote nchini kama hatua ya kuwavutia wasichana wengi kusoma masomo ya sayansi.

  Kulingana na takwimu za Kitengo cha Taasisi ya Wahandisi Wanawake Tanzania idadi ya wahandisi wanawake imeongezeka kutoka wanawake 35 mwaka 2005 hadi wanawake wahandisi 298 mwaka 2015.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi Akizungumza na Maafisa mipango miji jijini Dar es salaam leo. Kulia Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Michael Mwalukasa.
  Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na maafisa wa mipango miji.

  WAZIRI wa Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewataka watendaji wa  wizara hiyo kuendelea kujenga nyumba za makazi za watumishi wa serikali mkoani Dodoma.

  Akizungumza na maafisa wamipango miji jijini Dar es salaam leo Waziri Lukuvi amewataka watendaji hao kuweza kujipanga kujenga nyumba za makazi  za watumishi wa Serikali ilikuweza kuwahudumia watumishi hao wanaotarajia kuhamia mjini Dodoma.

  ''Lengo la kikao hiki ni kuwataka mjipange ili kuweza kujipanga ni namna gani mtaweza kuhudumia watumishi wa serikali wakati wakiwa mjini Dodoma''amesema Waziri Lukuvi.

  Amesema kuwa sambamba na wizara mbalimbali kuhamia katika jiji la Dodoma amewataka watendaji hao kuweza kuboresha ramani ya mipango miji ilikuonesha namna gani mji unavyotakiwa kukaa ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo .

  ''Tumeshamaliza mastar Plan tangu mwaka 2010 ya Dodoma kwani maeneo mengi yakuishi yameshaainishwa nilazima maafisa mipango kufanya biashara ikiwemo viwanja vyandege.

  Nae Katibu wa Wizara hiyo, Michaeli Mwalukasa amesema kuwa serikali inaandaa sera ya nyumba ikiwemo muswada wa uendelezaji miliki katika miji mbalimbali hapa nchini.

  0 0

  Mkurugenzi wa Jamani Foundation, Nirmala Pabari (kushoto) akikabidhi madawati Mameneja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa (kulia), Anne Mlimuka (wa pili kulia). Katikati ni Mwalimu Kasyupa kutoka Shule ya Msingi Yombo akiwakilisha kwa niaba ya waalimu wa shule zilizopokea msaada wa madawati 100.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiwa wamekaa katika madawati waliyokabidhiwa na taasisi ya Jamani Foundation. Kutoka kushoto, Mkurugenzi wa Jamani Foundation, Nirmala Pabari, Meneja wa TEA, Tito Mganwa na Anne Mlimuka.
  Meneja Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuk (kushoto), akikabidhi madawati yaliyotolewana JAMANI Foundation kupitia TEA kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Umoja, Juto Komba.

  Meneja Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuk (kushoto), akikabidhi akizungumza katika hafla yakupokea madawati 100 kutoka taasisi ya Jamani Foundation.Mkurugenzi wa Jamani Foundation akizungumza katika hafla ya utoaji wa madawati 100 kwa Shule ya Msingi Yombo. 
  WanafunziwashuleyaMsingiyaMsingiUmojawakichezangomayaasili, kutumbuiza katika hafla ya makabithiano ya madawati.

  JAMII imetakiwa kujenga utaratibu wa kutunza vifaa vya misaada vinavyotolewa kwa ajili ya shule ili viweze kudumu na kusaidia wanafunzi kwa muda mrefu.

  Ushauri Huo ulitolewa jana na Meneja wa Uhamasishaji na Wateja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa wakati wakikabidhiwa madawati 100 yaliyotolewa na Jamani Foundation kwa shule za msingi Umoja na Yombo za jijini Dar es Salaam.

  Alisisitiza umuhimu wa shule na wazazi kuwajengea watoto utaratibu wa kuthamini na kutunza vifaa wanavyopewa ili viweze kuduma na kunufaisha wanafinzi wengi zaidi kwa muda mrefu.

  “Madawati haya 100 yamegharimu 12m/-, hii inaonyesha ni jinsi gani wenzetu wa Jamani Foundation wanathamini mahitaji yetu nasi basi kuonyesha shukrani yetu tunapaswa kuyatunza ili yadumu na wenzetu wengine wafaidike pia na msaada huu” alisema Mganwa.

  Aliishukuru Jamani Foundation kwa ushirikiano wao na Mamlaka ya Elimu katika kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili kuhakikisha ubora wa elimu unazingatiwa.

  Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiano nayo katika kukabiliana na kero ya upungufu wa madawati na kwa sasa wanategemea kuanza ushirikiano katika mradi wa ujenzi wa vyoo ili kutunza afya za wanafunzi mashuleni.

  Akizungumza wakati wa kuwakabidhi TEA madawati hayo, Meneja wa huduma za jamii wa Jamani Foundation, Bi Nirmala Pabari alisisitiza umuhimu wa mashirika na asasi mbalimbali kusaidia jamii ili kuboresha maisha.

  Alisema wataendelea kushirikiana na serikali katika maeneo mbali mbali kulingana na mahitaji na uwezi wao lengo lao likiwa ni kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika mazingira bora ya upatikanaji wa huduma muhimu za jamii.

  Akipekea madawati hayo, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Umoja, Bw Dyuto Komba alisema watatumia utaratibu wa kugawa kila dawati kwa mwanafunzi na kuandikishana na wazazi wao ili kujenga dhana ya uwajibikaji.

  “Kama tulivyofanya kwenye kugawa kitabu, na kwa madawati hivyo hivyo, yatapewa namba na majina ambapo kila mwanafunzi atapaswa kulitunza na likiharibika mzazi au mlezi atawajibika kwa matengenezo” alisema.


  Alisema baada ya msaada huo, shule yake haina tena shida ya madawati na kusema changamoto waliyonayo ni uhaba wa madarasa hasa kutokana na kuongezeka kwa usajili wa wanafunzi wa shule ya awali na msingi.

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Usajili Wanachama Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Msafiri S. Mugaka, akimkabidhi Bw. Kenny Rodgers, kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari,(PSS), wakati wa maonyesho yaliyoandaliwa na kampuni ya simu za mikononi, Airtel, yaliyopewa jina la Airtel Bazaar yaliyolenga kuwakutanisha wateja wa kampuni hiyo na kampuni nyinhione zinazotoa huduma na kufanyika makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam, Agosti 12, 2016.(PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)
  Bw. Kennedy akijaza fomu tayari kujiunga na mpango wa PSS wa PSPF
  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akipatia maelezo, mfanyakazi wa Airtel alipotembeela banda la Mfuko huo
  Mfanyakazi huyu wa Airte, akisoma kipeperushi kabla ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, PSS
  Hadji Jamadari, Afisa Mkuu wa Matekeelzo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko huo kupitia PSS, Bw.Anthony S. Masha, baada ya kujiunga

  Afisa Matekelezo msaidizi wa PSPF, Penzila Kaisi, akimpatia maelezo juu ya huduma mbalimbali ambazo Mfuko unatoa, kwa mwanachama
  Herman F. Laswai, (kushoto), akikabidhiwa kadi yake ya kujiunga na uanachama wa PSPF, kupitia Mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Matekelezo msaidizi wa Mfuko huo, Angelina Kombe
  Angelina Kombe, Afisa Matekeelzo Msaidizi wa PSPF, akimpatia maelezo kwa umakini mkubwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la PSPF
  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akimsikilzia kwa makini mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ambapo baadaye alijiunga baada ya kuelewa huduma za Mfuko huo
  Wananchi wakipatiwa huduma na maafisa wa PSPF
  Elimu ikiendelea kutolewa kuhusu huduma za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo
  Penzila Kaisi (kulia), Afisa Matekelezo msaidizi wa PSPF, akimuelimisha mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ili kujua shughuli zake.
  Mkuu wa kitengo cha kuandikisha wanachama cha Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msafiri S. Mugaka, akiwapatia maelezo wanachama hawa wa PSPF, kuhusu mafao na faida nyingi ambazo mwanachama anaweza kupata ikiwa ni sehemu ya huduma zitolewazo na Mfuko
  Angelina akitoa somo kwa mwananchi huyu
  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akimsikilzia kwa makini mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ambapo baadaye alijiunga baada ya kuelewa huduma za Mfuko huo
  Mkuu wa kitengo cha kuandikisha wanachama cha Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msafiri S. Mugaka, akiwapatia maelezo wanachama hawa wa PSPF, kuhusu mafao na faida nyingi ambazo mwanachama anaweza kupata ikiwa ni sehemu ya huduma zitolewazo na Mfuko
  Mwanachama mpya akijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS


  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


  MFUKO wa Pensehni wa PSPF, umeendelea kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS, wakati wa Maonyesho ya taasisi na makampuni ya kutoa huduma yaliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mikononi, Airtel na kwenda na jina la Airtel Bazzar na kufanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco jijini Dar es Salaam, Agosti 12, 2016.

  Akizungumza na waandishi wanhabari kwenye banda la Mfuko huo, Mkuu wa Kitengo cha Usajili nwa Wanachama cha Mfuko huo, Bw. Msafiri S. Mugaka, alsiema, PSPF kupitia mpango wake wa PSS, imefanikiwa kusajili wanachama wapya kadhaa, ambayo ilikuwa ni moja ya huduma walizokuwa wakizitoa kwenye maonyesho hayo ya siku moja.

  "Pia wanachama wetu waliweza kuja na kupatiwa huduma za taarifa za michango yao, wanawezaji kufaidika na mafao mbalimbali ya yatolewayo na Mfuko kama vile fao la Elimu, Uzazi, mikopo kwa wafanyakazi wapya, na mafao mengine kadhaa,"alisema.

  Maonyesho hayo yalishirikisha makampuni kadhaa ya kibinafsi na taasisi za umma na yalilenga kuwakutanisha wateja wa Airtel, na taasisi hizo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenyewe wa Airtel kutembelea taasisi hizo na kupatiwa huduma mbalimbali wakiwa hapo hapo kazini.

  0 0


  Naibu Waziri Jafo akiwa na Mbunge wa vitimaalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hamad walipotembelea mradi wa maji ulioanza kutoa maji katika kijiji cha Tinde Mkoa wa Shinyanga.
  Jafo akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Tinde Mkoa wa Shinyanga.
  Jafo akizungumza na wananchi na watumishi katika mradi wa maji kijijin cha Tinde.
  Naibu Waziri Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama wa Wilaya ya Shinyanga.

  Jafo akikagua barabara mradi wa ujenzi wa barabara za lami katika Manispaa ya Shinyanga zinazojengwa chini ya Tamisemi. 
   
  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amewataka wakuu wa idara kwenye Halmashauri nchini kuacha kufanya kazi kimazoea kwa kuishia kukaa maofisini bila kwenda maeneo ya vijijini ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

  Jafo ametoa kauli hiyo ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi katika Halmashauri za Singida, Shinyanga, Uyui na Sikonge mkoani Tabora. Akizungumza na watumishi katika halmashauri hizo, Jafo amesema imekuwa ni mazoea kwa wakuu wa idara kujifungia maofisini bila kufika vijijini kukutana na wananchi ili waweze kutatua kero zao.

  Hata hivyo amewaonya baadhi ya wakuu wa idara wanaowanyanyasa watumishi wa kada za chini kwa kuwapendelea baadhi yao katika mchakato wa upandishaji wa madaraja. Amewaagiza wakurugenzi kupangiana malengo na wakuu wa idara kuwa ni kitu gani kila mmoja wao atakifanya ndani ya mwaka mmoja kwenye eneo lake la kazi.

  Aidha amesema na wakuu wa idara wafanye hivyo hivyo kwa watu wao wa chini ili kila mtu apimwe kiutendaji ndani ya mwaka mmoja. Jafo amekemea tabia ya wakurugenzi wa Halmashauri kupitisha malipo ya miradi ambayo inakuwa imejengwa chini ya kiwango na kwamba ni ubadhirifu wa fedha za wananchi kwa kuwa haifikii malengo yaliyokusudiwa.

  “Hali kama hii imejitokeza kule halmashauri ya kondoa mkoani Dodoma serikali imefanya uchunguzi na tayari hatua zimechukuliwa kwa watendaji 8 ambao wamesimamishwa kazi na wengine kufikishwa mahakamani kutokana na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo…Serikali itaendelea kuchukua hatua kwa yeyote atakayefanya vitendo kama hivi,”amesema Jafo

  Naibu Waziri huyo kwa takriban wiki mbili amefanikiwa kutembelea halmashauri 15 na kutembelea miradi 63 ikiwemo miradi ya hospitali, vituo cha afya na zahanati, miradi ya elimu, maji, na miundombinu ya barabara.

  Miongoni mwa Halmashauri alizozitembelea ni pamoja na Halmashauri ya Kilolo, Mufindi, Mafinga, Iringa, Chemba, Kibaha, Korogwe mji, Halmashauri ya Korogwe, Jiji Arusha, Kisarawe, Singida, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Uyui, na Sikonge .

  Jafo bado anaendelea na ziara yake katika mikoa ya Katavi na Rukwa kwa lengo kutimiza matakwa ya watanzania. 

  0 0


  Na. Immaculate Makilika

  Hivi karibuni Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini ambapo aliahidi kushirikiana na Tanzania katika uimarishaji wa sekta ya viwanda hapa nchini.

  Ujio wa Waziri Mkuu Modi nchini umekuwa fursa muhimu kwa watanzania kuongeza ushirikiano na wenzao wa nchini India kuwekeza kwenye kilimo , afya, viwanda na biashara kwa ajili ya kukuza fursa mbalimbali ikiwemo ajira na kuongeza mapato ya wananchi na Serikali kwa ujumla.

  Ziara hiyo ya Waziri Mkuu wa India nchini imeonesha nia ya dhati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda kama alivyokuwa akiahidi wakati wa Kampeni.  Moja wapo ya ahadi ambazo zimetokana na ziara ya kiongozi huyo wa Serikali ya India ni kuanzisha Viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu zitakazotibu magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria, figo na kisukari.

  Viwanda vingine ni vile vya kutengeneza vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali mbalimbali nchini, uanzishwaji wa viwanda hivyo utasaidia kupunguza gharama ya kununua vifaa hivyo nje ya nchi ambavyo vinaigharimu Serikali fedha nyingi.  Kazi nyingine muhimu zilizofanyika kwenye ziara ya Waziri Mkuu huyo India na Tanzania zilisaini mkataba wa pamoja kati ya Shirika la Viwanda Vidogo India (NSIC) na Shirika la Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO) kwa ajili ya ushirikiano utakaowasaidia wajasiliamali wadogo na wakati.

  Mkataba huo unatarajiwa kuiwezesha SIDO kubadilishana uzoefu na NSIC, kufanya utafiti, kushauri kuhusu miradi na sera ya uendeshaji wa viwanda vidogo vidogo.  Hii yote ikiwa ni katika kuanzisha vituo vya atamizi (incubators). ambapo kupitia atamizi hizo, wananchi watapatiwa mafunzo ya uzalishaji wa bidhaa na mafunzo ya biashara yatakayowawezesha kuanzisha biashara zao za viwanda vidogo vya uzalishaji.

  Aidha, atamizi hizo zitawasaidia wabunifu kunufaika na mafunzo na teknolojia ya India. Mpango ambao unadhamiria kutafuta ubia kwenye sekta ya viwanda vidogo pamoja na uratibu wa maonesho ya viwanda hivyo.  Kuhusu hatua ya Shirika la Viwanda Vidogo la nchini India kushirikiana na SIDO, Rais Magufuli amesema itaisaidia Tanzania kufukia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

  Akizungumza wakati wa ziara ya Waziri Mkuu huyo wa India Rais Magufuli anasema kuwa Tanzania ni mnunuzi mkubwa wa aina mbalimbali za pikipiki, bajaji na Tata kutoka India hivyo ipo haja ya nchi hiyo kuwekeza nchini kwa kujenga kiwanda kitakachokuwa kinatengeneza vyombo hivyo vya usafiri wa bei rahisi ili kurahisisha biashara ya nchi hizi mbili.

  Kufuatia ombi la Rais Magufuli kuiomba Nchi ya India kujenga Viwanda hapa nchini , Waziri Mkuu huyo amekubali ombi hilo na nchi yake inatarajia kuanza zoezi hilo wakati wowote. Kujengwa kwa kiwanda hicho nchini kutasaidia kwa vyombo hivyo kuuzwa bei nafuu na hivyo kuongeza idadi ya watumiaji na ajira nchini, hatua itakayosaidia kuchangia mapato ya Serikali kwa njia ya kodi kwa bidhaa.

  Rais Magufuli amemuoamba Waziri Mkuu huyo wa India kuangalia uwezekano wa kuhamishia baadhi ya viwanda vya pikipiki, bajaji na trekta hapa nchini ili watanzania wapate ajira na Serikali ijipatie kodi kutokana na shughuli hizo.  Aidha, Tanzania na India zinatarajia kushirikiana katika sekta ya Afya kupitia Kampuni ya Appolo Group kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii( NSSF) kujenga hospitali ya kisasa katika eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam itakayotoa huduma za afya kwa wakazi wa jiji na nchi nzima kwa ujumla.

  Hatua hiyo inalenga kusaidia Tanzania kupunguza gharama ya fedha inazozitumia kwa ajili ya kugharimia ununuzi wa vifaa tiba toka nje ya nchi, ambapo asilimia 80 ya fedha ununulia dawa na asilimia 100 inatumika kwa ajili ya kununulia vifaa tiba kutoka nje ya nchi.

  Katika kuimarisha kilimo, India imeendelea kuipa mikopo Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inakusudia kuimarisha sekta ya kilimo nchini. Miradi hiyo ambayo inatarajiwa kugharimu dola za marekani milioni 178.125 inatarajiwa kunufaisha sekta hii nchini.

  Mwaka 2015, India ilinunua mbaazi na choroko kutoka Tanzania zenye thamani ya dola za marekani milioni 200. Hii ni wazi kuwa endapo wakulima na Serikali kwa ujumla wakitilia mkazo suala hili zinaweza kupatikana faida nyingi kupitia mazao haya.

  Aidha, katika kuhakikisha hili linafanikiwa Rais John Magufuli anasema  nchi ya India ina uhitaji mkubwa wa mazao ya kilimo hasa jamii ya kunde hivyo akawataka wakulima kutumia fursa hiyo kuzalisha mazao hayo kwa wingi. “India inauhitaji wa tani 200 za mazao jamii ya kunde, wakulima mnatakiwa kuzalisha mazao hayo kwa wingi kwa vile tayari kuna soko la uhakika, na tutahakikisha madalali hawatakuwepo ili mkulima asinyonywe” .

  Kwa lengo la kuona mkulima haendelei kunyonywa, Serikali itaomba Serikali ya India kupitia taasisi yake Natioanal Seeds Cooperation kuipatia mbegu bora na mafunzo ya namna ya kuzimea ili uzalishaji uwe mkubwa na kutumia sehemu ndogo ya ardhi ili wakulima wengi waweze kuanza kuzalisha bidhaa hiyo. Kilimo hicho kinaweza kuzalisha ajira 1,000,000 kwa watanzania, kwa sasa mazao hayo yanalimwa mikoa ya Arusha, Dodoma, Shinyanga na Mtwara.

  Aidha, India ni mtumiaji mkubwa mazao ya mbaazi na choroko ambapo kwa mwaka inatumia kiasi cha tani milioni 23 lakini kiasi kinacholimwa nchini humo ni tani milioni 17 ikiwa ni pungufu ya tani sita. Kufuatia hali hiyo wakulima wa Watanzania wanayo fursa ya kupata masoko ya mazao hayo kwa kuwa soko lake lipo nchini India

  Katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), India imeipatia Tanzania msaada wa ujenzi wa kituo mahiri cha mfano wa cha masuala ya TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichopo jijini Arusha na ujenzi wa mradi wa Pan African e-Network unaounganisha hospitali na vyuo nchini (Ocean Road Cancer Institute, MUHAS na taasisi dada za India).

  Katika ziara yake nchini Waziri Mkuu wa India Mhe. Modi aliahidi kusaidia Tanzania katika masuala ya TEHAMA ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizi mbili “Lengo letu ni kusaidiana na kuimarisha mahusianao yetu katika kukuza uchumi na kutengeneza fursa mpya za ajira kwa wananchi wetu” anasema Waziri Modi.

  Katika sekta hii, India itasaidia Tanzania katika kusomesha wataalamu wa kitanzania nchini mwao, ambao wataweza kufanyakazi mbalimbali zikiwemo katika sekta ya viwanda nchini. Hatua hiyo inatazamiwa kuifanya Tanzania kuwa na uwezo wa kutengeneza programu zake yenyewe badala ya kununua nje ya nchi, kuweza kutunza usiri wa taarifa utakaosaidia usalama wa nchi, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma kwa urahisi zaidi na kutengeneza mifumo ya ukusanyaji mzuri wa mapato.

  Katika sekta ya nishati, Kampuni ya Bajaj ya India, imeeleza nia yake ya kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya mafuta nchini kwa kujenga kinu cha kusafirishia mafuta, tayari kuna mawasiliano yanaendelea baina ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Bajaj Group kuhusiana na uwekezaji huo.

  Aidha, kampuni za Shapoorji Pallonji na Kamal Industries, zinajenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi wa MW 250 katika eneo la Zinga, Mkoani Pwani. Uwekezaji huo, unalenga kuzalisha umeme utakaotumika katika eneo la viwanda la Kamal Industries na umeme mwingine utauzwa kwenye gridi ya Taifa ili kuweza kuuzwa kwenye maeneo mengine ya viwanda huko Bagamoyo na kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani.

  Mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na India yamechukua muelekeo mpya, ambapo makampuni kadhaa ya India yakitarajiwa kuanzishwa ndani ya miaka michache ijayo ambapo chini ya mpango huu, Tanzania itakuwa kitovu cha viwanda vya India.

  0 0


  Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi wa Baraza hilo kilichokutana kujadili hali ya siasa Jijini Dar es Salaam.
  Bi. Georgia C. Mtikila, Mjumbe wa Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
  Bw.Constantine B. Akitanda, Mjumbe wa Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa, Bw.Vuai Ali Vuai akizungumza na Wajumbe wa Kamati (hawapo pichani) wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya Baraza. . Secretarieti kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakifuatilia kwa makini wakati wa Kikao cha Kamati ya Uongozi.


  Na Monica Laurent, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

  Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa wamekutana leo Jijini Dar es Salaam kujadili hali ya Siasa nchini.

  Katika kikao hicho ambacho kilikuwa cha dharura kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ,wajumbe wamekubaliana kwa pamoja kuwa, ipo haja ya kuitishwa kwa kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kujadili hali ya siasa nchini.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Bw. Vuai Ali Vua ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa amesisitiza kuwa Kamati ya Uongozi inalo jukumu la kuimarisaha na kudumisha hali ya amani nchini pamoja na kujadili changamoto zilizopo katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi .

  Aidha, wajumbe wa kikao cha Kamati ya Uongozi wameazimia kuonana na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kwa lengo la kujitambulisha, kuelezea umuhimu wa Baraza la Vyama vya siasa katika mfumo wa vyama vingi na kubadilishana mawazo kuhusu hali ya siasa nchini.

  Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa huundwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Baraza ambao huchaguliwa na wajumbe wa Baraza, Katibu wa Baraza akiwa ni Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye yuko kisheria na pia wenyeviti wa kamati nne za Baraza.

older | 1 | .... | 935 | 936 | (Page 937) | 938 | 939 | .... | 1898 | newer