Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

HOSPITALI ZA DAR ES SALAAM KUNUFAIKA NA PROGRAMU YA 5'S KAIZEN

$
0
0
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana pamoja na Hospitali ya Mwananyamala kupitia programu ya 5’S-KAIZEN zimefanikiwa kuboresha huduma ya afya kwa wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika hopspitali hizo.

Programu ya 5’ S- KAIZEN inafadhiliwa na Serikali ya Japan chini ya Shirika la ushirikiano wa kimataifa JICA inalenga kumuandalia mfanyakazi wa afya hatua nzuri ya kutumia kiwango cha juu cha ujuzi na maarifa ikiwemo Sasambua, Seti, Safisha, Sanifisha pamoja na Shikilia (5’ S-KAIZEN).

Akizungumza kuhusu program hiyo msimamizi kutoka Ofisi ya Mradi wa Maendeleo ya Rasilimali watu wa JICA, Hisahiro Ishijima alisema kuwa lengo la programu hiyo ni kukuza na na kuanzisha maarifa ya njia ya uboreshwaji wa huduma za afya katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania.

Amesema kuwa usimamiaji wa mifumo ya utoaji huduma hospitalini unakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na ukosefu wa rasilimali tiba, na kuongeza kuwa changamoto hiyo inayopaswa kutatuliwa ili kuboresha huduma bora za matibabu.

“kanuni ya S Tano(5’S) ni nyenzo ya usimamiaji inayotumika kama njia ya msingi na inayotekelezeka hatua kwa hatua ili kuimarisha ubora na usalama katika aina zote za mpangilio ya kazi ikiwemo sekta ya afya”Alisema

Kwa upande wake Afisa Muuguzi Mwandamizi katika hospitali ya Amana, Evelyne Rwezaura alisema kuwa Hospitali hiyo inatekeleza programu ya 5’ S-KAIZEN ambapo kwa sasa hospitali hiyo imefanikiwa kuwa na mazingira mazuri ikiwemo upangaji mzuri wa mafaili ya wagonjwa na dawa.

“Tangu kuanza kwa mkakati huu wa mpango wa 5’S mazingira ya hospitali yamebadilika ukilinganisha na mazingira ya awali kwani kwa sasa kumekuwa na mpangilio mzuri kuanzia mafaili ya wagonjwa, dawa na usafi kwa ujumla ikiwemo utupaji wa taka hatarishi” aliongeza Rwezaula.

Naye Idrisa Mintanga, ambaye ni mgonjwa aliyelazwa katika hospitali hiyo alisema kwa sasa hospitali hiyo ya Amana kumekuwa na mabadiliko makubwa ukilinganisha na awali kuanzia mapokezi, usafi wa mazingira kwa ujumla, muda wa kusubiria umeimarishwa na kuuomba uongozi wa hospitali hiyo kuzidi kuimarisha huduma zake kwani kunamfanya mgonjwa kuona kuwa anadhaminiwa.

Aidha, Afisa Muuguzi katika wodi ya Kibasila katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alisema mbali na pamoja na changamoto zilizopo za vitendea kazi, upungufu wa mafunzo kwa wafanyakazi, mpango wa KAIZEN umeweza kutatua changamoto za usimamiaji ubora kwa ujumla katika hospitali hiyo.
 
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
DAR ES SALAAM
10/08/2016

RC MAKALA AFAGILIA VIPAJI AIRTEL RISING STARS.

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amoss Makalla aliye simama akizungumza na wachezaji kabla ya kuzindua michuano ya Airtel Rising Star kwa Mkoa wa Mbeya iliyo anza kutumia vumba jana katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kushirikisha timu sita.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akisalimiana na wachezaji wa timu ya Dable 'A' ya jijini Mbeya kabla ya kuzindua rasmi michuano ya Airtel Rising Star Mkoa wa Mbeya iliyoanza jana katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa kushirika timu sita za vijana.



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akisalimia na mchezaji Alvira Zaibu wa tatu kushoto, kutoka timu ya soka ya watoto ya Mbeya Talent wakati wa ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star iliyonza kutimua vumbi jana katika dimba la Sokoine kwa kushirikisha timu sita za Mkoa Mbeya.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipiga mpira golkini ishara ya ufgunguzi rasmi ya michano ya mpira wa miguu kwa vijana chini miaka 17 Airtel Rising Stara iliyonza jana katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akifatalia mchezo wa ufunguzi wa michuano ya vijana chini ya miaka 17 Airtel Risin Star kati ya Mbaspo Academy dhidi ya Dable A zote kutoka jijini Mbeya uliomazika kwa Mbaspo kuibka na ushindi wa bao 4-0 ndani ya Uwanja wa Sokoine jijini mbeya

Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Airtel Mkoani Mbeya wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars mkoani hapo.
Wachezaji kutoka timu sita zinazo shiriki Michuano ya Airtel Rising Star chini ya miaka 17 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amsos Makalla hayupo katika picha kabla ya kuzindua rasmi michuano hiyo kimkoa jana katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amefungua rasmi mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya na kuvitaka vilabu vya soka kutumia vipaji vinavyoibuliwa na programu hiyo ya vijana. Ufunguzi huo ulifanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo Agosti 9, 2016.

“Hii ndio njia pekee ambayo inaweza kutuletea maendeelo ya soka na kuiwezesha nchi yetu kuondokana na matokeo mabaya katika mashindano mbali mbali ya kimataifa”, alisema. Aliishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kubuni programu hii ambayo imekuwa ikiwapa vijana fursa ya kuonyesha na kuviendeleza vipaji vyao.

Makala amewataka vijana kucheza kwa kujituma na kufahamu kwamba hatma ya mchezo wa soka hapa nchini iko mikononi mwao. Alilitaka Shirikisho la soka nchini (TFF) kufanya kazi kwa karibu na wadau wengine ili kuhakikisha kuwa vijana wanaoibuliwa kupitia Airtel Rising Stars wanaendelezwa.

Amewataka viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya (MREFA) kuyatumia vizuri mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa na kuchagua vijana nyota watakaounda timu za mkoa kushiriki kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 6 hadi 11 jijini Dar es Salaam.

Michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa inaendelea katika mikoa minginge ambapo timu za wavulana za Makongo Sekondari na Kawe United zilitoshana nguvu baada ya kutoka suluhu katika uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Fainali za Taifa zitashirikisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Timu nyingine zitatoka Morogoro, Mwanza, Mbeya, Arusha, Lindi na Zanzibar.

MAFUNDI TEMESA WAPIGWA MSASA

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama (mwenye koti jeusi) akisikiliza maelezo kuhusu namna kifaa cha kukagua taa za magari kutoka kwa mmoja wa mafundi wa Kituo cha Ukaguzi wa Magari cha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.


Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt. Mhandisi Prosper Mgaya akifafanua jambo mara baada ya kumpokea Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama(aliyevaa tai) alipowasili Chuo hapo kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi 25 wa TEMESA yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo mafundi hao katika Nyanja za matumizi ya vifaa vya kisasa, utambuzi wa vilainishi halisi, na ubora wa matairi. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Vazuri Lazaro Mbise.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo mafundi hao katika Nyanja za matumizi ya vifaa vya kisasa, utambuzi wa vilainishi halisi, na ubora wa matairi ambapo jumla ya mafundi 25 wanashiriki. Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt. Mhandisi Prosper Mgaya, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi. Sylivester Semfukwe na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Vazuri Lazaro Mbise.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Le Kujan Manase akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt. Mhandisi Prosper Mgaya akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Le Kujan Manase, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Vazuri Lazaro Mbise na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi. Sylivester Semfukwe.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ufundi kutoka TEMESA na wadau wa mafunzo hayo wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) hivi karibuni.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama (watatu mwenye tai) akiangalia hatua za ukaguzi wa gari katika Kituo cha Ukaguzi wa Magari kilichopo Chuo cha Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) hivi karibuni wakati wa hafla uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Meneja wa Kituo hicho Mhandisi. Hans Mwaipopo.
Na: 
Frank Shija, MAELEZO

Mafundi wa TEMESA watakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu yao ili kupunguza malalamiko ya wateja wao.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama wakati akifungua mafunzo ya mafundi hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Nshama aliosema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani yataongeza ufanisi kwa mafundi wa Serikali hivyo kuongoa malalamiko ambayo yamekuwapo kuwa TEMESA imekuwa ikifanya kazi za matengenezo ya magari na mitambo chini ya kiwango.

“Kupitia mafunzo haya ni matumaini yangu kuwa mafundi wa TEMESA watakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi zao kwa weledi ikiwemo uwezo wa kutumia vifaa vya kisasa katika kutambua vipuli halisi na feki, na kubaini mchanganuo wa gharama halisi za matengenezo ya magari ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara”. Alisema Dkt. Nshama.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Le Kujan Manase amesema kuwa kutokana na mafunzo hayo kushirikisha mafundi 25 kutoka karakana mbalimbali zilizo chini ya TEMESA ni dhahiri kuwa zitaongeza ufanisi katika kutoa huduma ya ufundi kwa wateja ambao kwa kiasi kikubwa ni magari na mitambo inayomilikiwa na Serikali pamoja na taasisi zake.

“Hapa kuna jumla ya mafundi 25 maana yake ni kwamba kila karakana nchini ina wataalam waliopata mafunzo ya kutumia vifaa vya kisasi, mkishirikiana kazi zenu zitakuwa na tija”. Alisema Mhandisi Manase.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt.Mhandisi Prosper Mgaya amesema kuwa Chuo chake kitanendelea na jitahada za kuhakikisha kinaendesha program mbalimbali kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini ikiwemo kuandaa mafundi kwa ajili ya vyombo vya usafiri wa aina mbalimbali.

Mafunzo haya ya mafundi wa TEMESA yanafanyika kwa ushirikiano baina ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),Kampuni ya Superdoll Trailer na TEMESA yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo mafundi katika Nyanja za matumizi ya vifaa vya kisasa, utambuzi wa vilainishi, ubora wa matairi na ukaguzi wa magari.

ACTIVISTA TANZANIA WAADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI.

$
0
0
Mkurugenzi wa DOT Tanzania, Dawson Luogard akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya vijana leo katika ukumbi FES Oyster Bay jijini Dar es Salaam.
Mtandao wa Vijana wa Activista Tanzania wakishirikiana na Tanzania Youth Vision Association(TYVA) wameadhimisha siku ya Vijana Duniani kwa kuwakutanisha vijana zaidi ya 120 kutoka maeneo mbalimbali na kujadili mada mbalimbali kuhusu Kodi, Kilimo na Maendeleo Endelevu ya malengo ya millenia.(Picha na Geofrey Adroph)
Mkurugenzi wa Jielimishe Kwanza, Henry Kazure akitoa mafunzo kwa vijana waliofika katika maadhimisho ya siku ya vijana katika ukumbi wa FES yaliyoandaliwa na Activista Tanzania wakishirikiana na TYVA.

Katibu wa Actvista Tanzania, Maria Kayombo ambaye alikuwa mshereheshaji akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya vijana yaliyofanyika katika ukumbi wa FES Oyster Bay jijini Dar es Salaam
Baadhi ya vijana wakifuatilia mada
Mratibu wa Kwanza wa Activista Tanzania, Elly Ahimidiwe akizungumza na vijana waliofika katika maadhimisho ya siku ya vijana yaliyoandaliwa na Mtandao wa vijana wa Activista Tanzania wakishirikiana na TYVA.
Baadhi ya Vijana waliofika katika maadhimisho ya siku ya Vijana wakisikiliza mada zinazoendelea katika ukumbi wa FES Oster Bay jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Activista Tanzania, Hatibu Kilenga akifunga mafunzo kwa vijana yaliyoandaliwa na Mtandao wa Vijana wa Activista Tanzania wakishirikiana na Tanzania Youth Vision Association(TYVA) katika maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani.
Picha ya Pamoja

RAIS DKT MAGUFULI AHUTUBIA MAELFU YA WANANCHI WA JIJI LA MWANZA UWANJA WA FURAHISHA LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha eneo la Kirumba jijini humo.APICHA NA IKULU

Baadhi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara,wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia
Wananchi wakimsikiliza Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye uwanja wa Furahisha,jijini Mwanza

DC KAKONKO AKABIDHI MAGARI MAWILI YA WAGONJWA KITUO CHA AFYA MGAZA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Kakonko Col. Hosea Maloda Ndagala akikabizi funguo za magari mawili ya kubebea wagonjwa (hayapo pichani)kwa Mganga Mkuu wa kituo cha afya Mgaza Wilayani Kakonko Dkt Selemani Fadhiri. Wanaoshuhudia wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya KakonkoLusubilo Mwakabibi na kushoto ni Diwani wa Kiziguzigu, Renatus Daniel.
Mkuu wa Wilaya akijaribu moja ya magari hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Col. Hosea Ndagala akiongea na Madiwani. Watumishi wa Hospital wakati wa hafla ya kukabidhi magari ya wagonjwa katika kituo cha afya Mgaza Wilayani Kakonko
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko akitoa shukrani wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo.


**********

Cosmas Makalla, Kakonko

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Maloda Ndagala amekabidhi magari mawili mapya ya kubebea wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser Hard top Ambulance yenye thamani ya dola za kimarekani 18,000 kwa gari moja kwa vituo vya afya viwili Wilayani Kakonko hivi karibuni.

Kanali Hosea Ndagala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla iliyofanyika katika kituo cha afya Mganza amesisitiza magari hayo kutumika kubebea wagonjwa kama ilivyokusudiwa.

“Naagiza magari haya ya wagonjwa yatumike vizuri kwa kubebea wagonjwa hasa wanawake wanaokwenda kujifungua na kutunzwa vizuri ili baada ya miaka mitano ya mkopo yaonekane yakiwa katika hali nzuri. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Aidha ametoa wito kwa watumishi wa afya hususani wahudumu kutumia lugha nzuri wanapowahudumia wagonjwa ili kuondoa malalamiko miongoni mwa wananchi ambao baadhi wamekuwa wakilalamika kuwa hawapati lugha nzuri kutoka kwa wahudumu.Katika hafla hiyo walihudhuria viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri, makamu Mwenyekiti na waheshimiwa madiwani.

Akitoa wito kwa watumishi Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Maganga ameeleza kuwa Wilaya ya Kakonko imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa magari ambapo gari lililokuwa likitumika kubebea wagonjwa lilikuwa moja tena chakavu.

“Tunalishukuru shirika la UNICEF kwa msaada mkubwa walioutoa wa magari mawili ya wagonjwa kwani itakuwa ni msaada mkubwa kwa akina mama wanokwenda kujifungua na wale wanaoishi maeneo yenye umbali mrefu”.

Mheshimiwa Juma Maganga ameonya watumishi ambao watayatumia magari hayo vibaya kwa ajili ya shughuli zao binafsi watachukuliwa hatua za kinidhamu mara moja. Aidha amewaomba waheshimiwa madiwani kutoa taarifa wanapoona magari hayo yanatumika vibaya katika maeneo yao ya Utawala.

Vilevile ameliomba shirika la UNICEF kuendelea kusaidia sekta ya afya katika Wilaya ya Kakonko kwani bado inachangamoto ya vifaa tiba pamoja na miundo mbinu ya hospitali.

Mkurugenzi Mtendaji Lusubilo Joel Mwakabibi ambaye ndiye msimamizi wa magari hayo ya wagonjwa amesisitiza watumishi wa afya kuyatunza magari hayo na kuyatumia kwa mujibu wa maelekezo. Ameahidi kuyafanyia service mara kwa mara na kuyawekea mafuta wakati wote.

Shirika la UNICEF limetoa magari hayo kwa Halmahsuri ya Wilaya ya Kakonko kama mkopo utakaolipwa katika kipindi cha miaka mitano. Magari haya yatakuwa ni ukombozi kwa wakazi wa Wilaya ya Kakonko kwani wataweza kupiga simu na kufuatwa pale walipo ili kukimbizwa katika kituo cha afya kwa lengo la kupata huduma ya afya kwa haraka.

NBS YAPOKEA MSAADA WA BIL 25 KWA AJILI YA WATOTO

$
0
0

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akionyesha Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania mbele ya wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa taarifa hiyo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa takwimu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania jijini Dar es salaam.


Na Ally Daud-Maelezo

Tume ya Taifa ya Twakimu (NBS) imepokea msaada wa shilingi bilioni 25 kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kusaidia kuboresha tasnia ya takwimu kuhusu haki za watoto nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji amesema kuwa amepokea msaada huo kwa nia ya kuendeleza tasnia ya takwimu nchini na kusaidia malengo ya nchi ya miaka mitano.

“Tumepokea msaada huu kwa furaha na hamasa kubwa katika kufikia lengo letu la kuboresha na kukuza tasnia ya takwimu nchini ili kuweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya miaka mitano ya nchi yetu”. Alisema Mhe. Kijaji.

Aidha Mhe. Kijaji amesema kuwa Wizara yake imewapa kipaumbele watoto kwa kutenga shilingi. Bilioni 18 kila mwezi ili kuwasaidia katika mambo muhimu ya kila siku hususani elimu bora, makazi na malazi.

Mbali na hayo Mhe. Kijaji ameshukuru na kuwapongeza Umoja wa ulaya kwa msaada huo na kuwataka wasichoke kuwa nao pamoja katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Balozi wa Umoja wa Ulaya Bw. Eric Beaume Amesema kuwa msaada huo sio mwisho wao kwani wanapenda kazi ya NBS na matokeo yake hivyo wapo tayari kutoa kiasi kikubwa zaidi ili kuwezesha tume hiyo kutoa takwimu zenye uhakika kwa maendeleo ya Tanzania.

Bw.Beaume amesema kuwa Umoja wao utakua bega kwa bega na Tanzania katika kutoa misaada ili kusaidia haki zote za watoto ili kujenga taifa lenye tija na muamko wa kimaendeleo kutokana na takwimu zitokanazo na tume hiyo.

Aidha Bw. Beaume ameongeza kuwa Umoja wao upo tayari kusaidia Nyanja za kilimo, Nishati katika maeneo ya vijijini ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa miaka mitano ijayo.

Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa amesema kutokana na msaada huo wamepata hamasa kubwa kwa tume hiyo kuweza kupambana na kupata takwimu yakinifu zitazopelekea kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yahusuyo jamii nchini na kufikia malengo ya miaka mitano.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MZEE ALLY MTOPA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa (kushoto) ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza masuala mbali mbali ya kisiasa na ya kijamii na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

SULUHU YA MAGWANGALA YAPATIKANA,NI BAADA YA KUPATIKANA MAENEO YA KUHIFADHIA MAGWANGALA

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na watendaji kutoka Mkoa wa Geita, Wizara ya Nishati na Madini, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) (hawapo pichani) Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Selestine Gesimba na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga
Sehemu ya watendaji kutoka Mkoa wa Geita, Wizara ya Nishati na Madini, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akifafanua jambo katika eneo la Lwenge, Nyamikoma ambalo ni moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuhifadhi magwangala


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kulia ni mkuu wa mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (mbele) akisoma taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kubaini maeneo kwa ajili ya kuhifadhia magwangala mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Halmashauri ya Geita.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (hayupo pichani) Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Uchimbaji Mdogo, Julius Sarota
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho
Sehemu ya watendaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)

Na Greyson Mwase, Geita

Mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika mkoa wa Geita kuhusu upatikanaji wa magwangala na eneo la kuhifadhi magwangala hayo, umepatiwa ufumbuzi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kukutana na mkuu wa mkoa wa Geita, uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), watendaji wa halmashauri ya mkoa huo na wawakilishi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Profesa Muhongo alifanya ziara katika mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Magufuli lililotolewa Julai 31 mwaka huu la wachimbaji wadogo kupatiwa magwangala pamoja na maeneo ya kuhifadhi magwangala hayo ili kuchenjua na kupata dhahabu.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha watendaji kutoka Mkoa wa Geita, Wizara ya Nishati na Madini, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Profesa Muhongo alisema maeneo ya awali yaliyopatikana kwa ajilli ya kuhifadhi magwangala hayo ni pamoja na Lwenge- Nyamikoma, Kasota B na Samina B yaliyopo mkoani Geita.

Aliagiza Ofisi ya Madini Mkoani Geita kutoa leseni za uchenjuaji madini mara moja kwa vikundi vyote vya wachimbaji madini ili waanze kazi mara moja ya uchenjuaji madini kwa kutumia magwangala hayo.

“Ninaagiza Ofisi ya Madini Mkoani Geita kutoa leseni za uchenjuaji madini kwa vikundi vilivyoundwa kupitia halmashauri mara moja bila vikwanzo vyovyote ili waanze na shughuli za uchenjuaji madini mara moja,’ alisema Profesa Muhongo.

Akizungumzia suala la usafirishaji wa magwangala katika maeneo hayo Profesa Muhongo alisema ni jukumu la vikundi vilivyopewa magwangala hayo kusafirisha kutoka kwenye mgodi hadi kwenye maeneo yaliyoainishwa.

Aliongeza kuwa iwapo vikundi vitakosa uwezo wa kusafirisha magwangala hayo, halmashauri inaweza kufanya mazungumzo na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa ajili ya gharama ya kusafirisha magwangala hayo.

Aidha katika kikao hicho Waziri Muhongo alikubaliana na uongozi wa Mgodi wa Dhahabu (GGM) kwa ajili ya kusafirisha tani 10 kwa kila eneo kwa kuanzia kama njia ya kuonesha nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo.

Profesa Muhongo alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wa madini wananufaika na sekta ya madini kupitia shughuli za uchenjuaji madini na kuwataka kuomba ruzuku pindi zinapotangazwa.

Awali akiwasilisha taarifa ya mkoa wa Geita kuhusu utekelezaji wa mpango wa uainishaji wa maeneo ya kuhifadhia magwangala, mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alisema kuwa suala la magwangala limekuwa la muda mrefu ambapo wananchi wa Geita wamekuwa wakihitaji magwangala hayo ili wafanye shughuli za uchenjuaji kwa lengo la kujipatia kipato.

Kyunga alisema kuwa ili kutekeleza azma hiyo ya kuwapatia wananchi magwangala, jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kwa kushirikisha viongozi wa serikali, taasisi za kimazingira pamoja na wadau mbalimbali.

Alisema katika utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli alilolitoa Julai 31 mwaka huu la kuwapatia wananchi magwangala tayari mkoa umefanya hatua za awali kwa kutafuta maeneo tisa yatakayofaa kwa ajili ya uhifadhi wa magwangala

Aliainisha maeneo yaliyopatikana ni pamoja na Magogo, Lwenge-Nyamikoma, Kasota A, Kasota B, Bugulula A, Bugulula B, Manga- Saragulwa, Mgusu, Samina A na Samina B.

Aliongeza kuwa maeneo yaliyopewa kipaumbele cha kwanza ni pamoja na Lwenge-Nyamikoma, Samina A, Manga-Saragulwa, Kasota B na Mgusu. Aliongeza maeneo yaliyopewa kipaumbele cha pili ni pamoja na Samina A, Samina B (Mpomvu), Bugulula A na Bugulula B

“Kipaumbele cha tatu ni Magogo, pamoja na mapendekezo hayo bado tuliona maeneo mawili ya Manga- Saragulwa na Mgusu ambayo yanaweza kutumika kwa kuanzia kwa kuzingatia suala la usalama, idadi ya askari waliopo kulingana na changamoto ya uhalifu unaoweza kujitokeza na kufanya tathmini ya uendeshaji wa shughuli hiyo,” alisisitiza Kyunga.

Akielezea matokeo ya uwepo wa shughuli za magwangala mkoani Geita Kyunga alieleza kuwa ni pamoja na ongezeko la watu katika maeneo hayo na kuhitaji uimarishwaji wa ulinzi.

SERIKALI ZA TANZANIA NA UTURUKI ZASHIRIKIANA KUPATA TAARIFA KUHUSU SHULE ZA FEZA

$
0
0
Serikali imesema kwamba inaendelea kushirikiana na Serikali ya Uturuki ili kupata taarifa zaidi kuhusu wamiliki wa shule za Feza kuhusishwa na jaribio la kuipindua serikali ya Uturuki kama ambavyo imeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga alisema wanaendelea kuwasiliana na Serikali ya Uturuki kuhusu taarifa hizo ili kupata ukweli.

Balozi Mahiga alisema kuwa kumekuwepo na taarifa zinazohusisha wamiliki wa shule hizo na baadhi ya wafanyabiashara ambao walifadhili na kuongoza jaribio la mapinduzi lililoshindwa Julai 15, mwaka huu nchini humo.

“ Serikali inaendelea kufanya mawasiliano na Serikali ya Uturuki kupitia ubalozi wake hapa nchini ili tuweze kupata taarifa kuhusu kuhusishwa kwa wamiliki wa shule za Feza na baadhi ya wafanyabiashara katika jaribio la kuipindua serikali ya uturuki,” alisema Balozi Mahiga.

Aliongeza kuwa kwa sasa serikali ya Tanzania haiwezi kufanya uamuzi wowote kuhusu wamiliki wa shule ya Feza na wafanyabiashara wa uturuki waliopo hapa nchini.

Kuhusu wanafunzi wa kitanzania wanaosoma nchini humo, Balozi Mahiga alisema kuwa wamemuagiza afisa ubalozi wa Tanzania aliyepo Roma nchini Italia kufuatilia hatma ya wanafunzi katika vyuo vilivyopo kwenye miji ya Ankara na Instanbul baada ya kufungwa kwa shule na vyuo kufuatia jaribio hilo la mapinduzi.

Kwa upande wake, Balozi wa Uturuki nchini Bw. Yasemin Eralp, hivi karibuni alisema kuwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini mwake katika vyuo na shule zilizofungwa watahamishiwa vyuo vingine kuendelea na masomo yao.

Balozi Eralp alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kufungwa kwa baadhi ya vyuo na taasisi za kielimu zilizobainika kuwa na uhusiano na kikundi cha kigaidi cha Fetullah Terrorist Organization(FTO) kinachotajwa kufadhili na kuongoza jaribio la mapinduzi lililoshindwa hivi karibuni nchini humo.

Hivi karibuni Serikali inatarajia kukutana na balozi wa Uturuki nchini ili kujua ni vyuo vingapi vilivyofungwa nchini humo ikiwa ni pamoja na idadi ya wanafunzi wa kitanzania wanaosoma katika vyuo hivyo ili kupatiwa msaada zaidi. 
 
Na. Abushehe Nondo na Immaculate Makilika - MAELEZO

Dar es Salaam 

BALOZI MAHIGA AELEZA MGOGORO WA UTURUKI UNAVYOHUSISHWA NA SHULE ZA FEZA

NETBALL TANZANIA YAANZA VYEMA MASHINDANO YA MAJESHI

$
0
0

Mchezaji Faraja Malaki wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27
Mchezaji Nasra Suleiman wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 (Picha na Selemani Semunyu).
Mchezaji Veronica Patrick wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27.
Mchezaji Veronica Patrick wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 (Picha na Selemani Semunyu)

Na Selemani Semunyu JWTZ .

Timu ya Mpira wa Pete Netball ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ime3rejesha heshima yake baada ya Kuwafunga mabingwa Watezi wa Michuano hiyo kwa Mpira wa Pete Uganda kwa magoli 29 kwa 27.

Katika Mchezo huo uliokuwa wa Vuta nikuvute na rabsha za hapa na pale zilizizojitokeza kabla wakati na Baada ya Mchezo huo ambao ulikuwa na Upinzani Mkali kutokana na historia ya Timu hizo.

Katika Robo ya Kwanza Tanzania ilimaliza ikiongoza kwa magoli saba kwa Sita huku Timu zote zikicheza Mchezo wa kuviziana lakini uliojaa nguvu na kukamiana miongoni mwa Wachezaji. Katika Robo ya Pili Tanzania pia ilimalizai ikiwa mbele kwa mabao 13 kwa 11 kukiwa na tofauti ya magoli mawili tofauti na robo ya kwanza ambayo ilimalizika kwa tofauti ya goli moja.

Robo ya Tatu Uganda walikuja na kusawazisha na kasha kuongeza na hivyo kumaliza kwa ushindi wa magoli 20 kwa 19 ya Tanzania na kuwafanya Tanzania kwenda kujiuliza. Hatimaye robo ya Mwisho ikamalizika na Timu ya Tanzania kuibuka na Ushindi na hivyo kuwatisha Mabingwa wa mwaka uliopita pengine utarejea kwa Tanzania .

Kwa Upande wa Nahodha wa Timu hiyo Dorita Mbunda alisema mechi yao na Uganda wamecheza kama fainali kutoka na historian a kuahidi kujipanga kwa ajili ya kuwakabili Kenya.

Kwa upande wake Nahodha Uganda Lilian Ajio amelalalimika Waamuzi kutoelewa Sheria Mpya za Mchezo huo hali iliyopelekea wakati mwingine kutokuwa na maamuzi sahihi.

WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA NA SERIKALI KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA UHUSIANO

$
0
0

Mwenyekiti wa mkutano wa wadau wa Washirika wa Maendeleo Dkt. Donald Kaberuka akifafanua jambo kwa wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria mkutano wa kutafuta njia bora ya kuhuisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau hao wa maendeleo na serikali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka meza kuu akichangia jambo wakati wa mjadala kuhusu namna bora ya Tanzania kuhuisha na kuimarisha ushirikiano na wadau wake wa maendeleo, mkutoano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam. Kulia kwake anaonekana Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile.
Mtaalamu Mshauri James Adams, akichokoza mada ya namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na wadau wake wa maendeleo, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa mkutano unaojadili kuhusu namna ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB-Dkt. Donald Kaberuka (kushoto), akifafanua jambo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu, Jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kuhusu namna ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa mkutano, aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB-Dkt. Donald Kaberuka (kushoto), katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kulia ni Bw. Steve Kayizzi Mugerwa wakisikiliza hoja ya mdau wa Maendeleo (hayupo pichani) wakati wa mjadala kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano wa Maendeleo nchini Tanzania, mkutano umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (kushoto) akisikiliza kwa makini hoja ya mjumbe wa Mkutano kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kutafuta njia bora ya kuhuisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau hao wa maendeleo na serikali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kutafuta njia bora ya kuhuisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau hao wa maendeleo na serikali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.

WANAOSAFIRI NJE YA NCHI WATAHADHARISHWA KUHUSU UPATAJI WA KADI ZA CHANJO HOMA YA MANJANO.

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu Chanjo ya Homa ya Manjano na vitendo vya baadhi ya watumishi wa afya wasiowaaminifu ambao hulipwa fedha ili waweze kuwatengenezea wasafiri kadi za Chanjo ya Homa ya Manjano na kisha kuzitumia nje ya nchi jambo ambalo kinyume cha sheria na hatari kwa usalama wa Afya zao. Picha/Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Aron Msigwaa- MAELEZO.

11/8/2016. Dar es Salaam.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewatahadharisha wananchi wanaopanga kusafiri kwenda nje ya nchi kuhakikisha kuwa wanafika katika vituo vya afya na kuchanjwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya Homa ya Manjano badala ya kuwalipa fedha baadhi ya watumishi wa afya wasio waaminifu ili watengenezewe kadi hizo kinyume cha sheria.

Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo leo jijini Dar es salaam amesema baadhi ya wasafiri wamekuwa wakishirikiana na watumishi wa afya wasiowaaminifu kwa kuwalipa fedha ili waweze kuwatengenezea kadi hizo na kisha kuzitumia nje ya nchi jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Afya zao.

“Kumekuwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu ambao hupokea fedha na kisha kutengenezesha kadi za wasafiri zinazoonesha kuwa wamepatiwa chanjo, Jambo hili ni hatari kwa afya ya msafiri, sasa tunaona mlipuko wa ugonjwa huu ukitokea katika nchi za karibu ni muhimu mtu kuchanja ili kuepuka kuwa chanzo cha kuleta ugonjwa huu” Amesisitiza Dk.Neema.

Amesema ni jambo lisilokubalika kwa msafiri kuwa na kadi ya chanjo ya Kinga ya Homa ya Manjano akijua kabisa hajapatiwa chanjo hiyo na kuongeza kuwa jambo hilo linamuweka muhusika katika hatari ya kupata maambukizi akisafiri kwenye nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo.

“Napenda kusisitiza kuwa ni muhimu sana msafiri akachanjwa chanjo hii kwa ajili ya kinga ya afya yake mwenyewe, kupata kadi bila kuchanjwa na kwenda mahali ambapo kuna ugonjwa huu ni kujidanganya, epuka kuwa chanzo cha kusambaza ugonjwa huu” Amesisitiza Dk. Neema.

Kuhusu gharama za chanjo hiyo amesema kuwa msafiri anayetaka kupata chanjo hiyo anatakiwa kulipia gharama ya Elfu Ishirini (20,000/=) ikiwa ni malipo halali ya Serikali na mlipaji hupatiwa stakabadhi halali.

Aidha, amesema mbali na hatua zinazochukuliwa kudhibiti hali hiyo, Wizara inakamilisha utaratibu wa kuwa na kadi maalum ambazo zitakuwa tofauti, zenye nembo maalum ambazo mtu hataweza kughushi wala kufanya udanganyifu wa aina yoyote.

TAMKO KUTOKA WIZARA YA AFYA


RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA MALI ZA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA NYANZA ZIRUDISHWE.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza na kuchukua hatua za kurejesha mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha Ushirika cha Nyanza ambazo zilinunuliwa na kutwaliwa na watu binafsi kwa njia za ujanja ujanja.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 11 Agosti, 2016 alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Dkt. Magufuli amesema Serikali yake haipo tayari kuwafumbia macho watu wachache waliovifilisi vyama vya ushirika vya wakulima kwa kujimilikisha mali za ushirika yakiwemo majengo, viwanda na mashamba na ametaka mali hizo zirudishwe mikononi mwa wananchi.

"Hata kama walichukua miaka 20 iliyopita, vyombo vya dola vichukue hatua na mali hizo zirudishwe kwa umma" Amesema Rais Magufuli.

Katika Mkutano huo Rais Magufuli pia amesema Serikali itafanya oparesheni kubwa ya kuteketeza Makokoro katika ziwa Victoria ikiwa ni juhudi za kukabiliana na tatizo la uvuvi haramu uliosababisha kupungua kwa samaki na kuathiri shughuli za uvuvi na usindikaji wa minofu ya samaki katika viwanda.

Amebainisha kuwa lengo la kuchukua hatua hiyo ni kuwezesha samaki wengi kuzaliana ili lengo la Serikali la kujenga viwanda vya kusindika mazao ikiwemo viwanda vya kusindika minofu ya samaki lifanikiwe.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha linalokatiza barabara ya Uwanja wa Ndege kwenda katikati ya Jiji la Mwanza.

Daraja hilo litakuwa na urefu wa meta 46, upana wa meta 3.6 na kimo cha meta 5.5 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Mwezi Desemba Mwaka huu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6.455

Akizungumzia ujenzi huo Rais Magufuli amemtaka Mkandalasi anayejenga Daraja la Furahisha kukamilisha kazi hiyo Mwezi Desemba Mwaka huu kwa mujibu wa mkataba, na pia ameagiza Mkandalasi aliyekuwa akifanya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuendelea na kazi hiyo ndani ya wiki moja kwa kuwa Serikali imejipanga kumlipa fedha za kazi hiyo.

Pia Dkt. Magufuli ameahidi kuongeza fedha katika ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Katikati ya Jiji la Mwanza hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza ili barabara hiyo ifike hadi uwanjani badala ya kuishia eneo la Pasiansi.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Mwanza
11 Agosti, 2016

WATANZANIA ZAIDI YA 1000 WANUFAIKA NA MAFUNZO NCHINI JAPANI

$
0
0

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo
Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu YOSHIDA akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi (12)waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (03), mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
Watumishi (12) waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (waliosimama) wakijitambulisha mbele ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ( wa pili kulia mstari wa mbele) na Waandishi wa Habari (kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama (wa kwanza kushoto) akiuliza swali kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama (wa kwanza kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.

Mahusiano yaliyodumu kwa muda mrefu baina ya Serikali ya Tanzania na Japani yamewezesha watanzania zaidi ya 1000 kupata mafunzo katika vyuo mbalimbali nchini Japani kwa kipindi cha miaka 8 ambayo yamesaidia kuwa na rasilimaliwatu yenye tija katika maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menentimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro kwenye hafla fupi ya kuwaaga watanzania 12 waliopata fursa ya mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani kwa ufadhili Serikali ya Japani kupitia Mpango wa ABE initiative, iliyofanyika leo nyumbani kwa balozi wa Japani nchini Tanzania .

“ Kati ya mwaka 2008 hadi 2015 zaidi ya watanzania 1000 wamepata mafunzo katika vyuo mbalimbali nchini Japani kupitia ufadhili wa Shirika la kimataifa la Maendeleo la Japani ( JICA) na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuwajengea uwezo watumishi wa umma na watumishi walio katika sekta binafsi” alisema Dkt. Laurean Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro alifafanua kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendelo la Japani limewawezesha vijana wengi wa kitanzania kupata mafunzo ya shahada ya Uzamili kupitia Mpango wa ABE initiative,ambao baada ya kumaliza mafunzo , wanarudi nchini Tanzania na kuanza kujenga ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Japani na pia kuchangia katika maendeleo ya sekta ya viwanda nchini” alisisitiza Dkt. Ndumbaro

“ Katika awamu ya kwanza mwaka 2014 walienda vijana 29 na awamu ya pili ambayo ni mwaka 2015 walienda vijana 32 kwa ajiri ya kupata mafunzo nchini Japani, ambapo mpaka sasa idadi ya wanufaika wa mafunzo hayo imefikia 73” alifafanua Dkt. Ndumbaro. Aidha Dkt. Ndumbaro aliwataka vijana waliopata fursa ya mafunzo hayo nchini Japani kusoma kwa bidii na kutumia elimu na ujuzi watakaoupata kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.

Alisema, ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Japani umeanza tangu mwaka 1960 ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania ilipata fursa ya kupeleka watanzania nchini Japani mwaka 1962 kwa ajili ya kupata mafunzo katika vyuo mbali mbali nchini humo. Kwa upande wake Balozi wa Japani nchini Mhe. Masaharu Yoshida alisema, Japan itaendelea kudumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya nchi hizo mbili ili kila upande unufaike kupitia ushirikiano huo.

Naye Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani nchini (JICA) Bw. Toshie Nagase amesema, vijana 12 waliopata nafasi ya mafunzo nchini Japani kupitia Mpango wa ABE initiative ni kati ya 52 walioomba nafasi hiyo, hivyo hawanabudi kuitumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii kwa ajili ya manufaa ya nchi.

Mpango wa ABE initiative wa miaka 5 ulianzishwa nchini Japani mwaka 2013 na Waziri Mkuu wa Japani Mhe. Shinzo ABE ambaye alitambua umuhimu wa kusaidia uwezeshaji wa maendeleo endelevu ya kiuchumi barani Afrika, mpango huo ulilenga kunufaisha vijana 1000 wa kiafrika.

WALIMU KUSAFIRI BURE USAFIRI WA GARI MOSHI -RC MAKONDA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa suala la walimu wa serikali kusafiri bure zinaendelea mpaka vyombo vyote vya usafiri kukubali kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makonda amesema walimu lazma warahisishiwe maisha katika utendaji wao kazi ikiwa ni kupata usafiri bure katika vyombo vya usafiri vilivyopo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika maombi yake walimu watasafiri bure katika usafiri wa gari moshi za Pungu -Stesheni na Ubungo -Stesheni kwa kutumia vitambulisho ambavyo viko katika utaratibi wa daladala.

Makonda amesema kuwa ameomba Waziri wa Tamisemi juu ya walimu kusafiri bure wa mabasi ya mwendo haraka na baada ya hapo kazi ya kupigania walimu katika vyombo vyote usafiri ili waweze kufundisha watoto na wawe na viwango vya juu vya ufaulu kuzidi mikoa yete nchini.

Aidha amesema kuwa haitakuwa busara suala la walimu kusafiri bure haliwezi likaachwa bila kuwa ufumbuzi kutokana kuamini kuwa walimu wakipata usafiri wanaweza kufika mapema shuleni na kufundisha.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa wanaunga mkono jitihada za Rais katika elimu na kama taasisi ya serikali wanachokufanya katika ysafiishaji wa walimu.

Kadogosa amesema kuwa kama kampuni wamechelewa sana kuanza kutoa huduma hiyo na kuongeza kuwa kwa wanafunzi watatumia usafiri huo kwa kulipa sh.100.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA DARAJA LA FURAHISHA JIJINI MWANZA PIA AHUTUBIA WAKAZI WA MWANZA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard Ndassa wakipiga makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara baada ya kukamilika.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara baada ya kukamilika.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu wa Wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake mara baada ya kuzindua ujenzi wa Daraja la Furahisha jijini Mwanza





Wanachi wakishangilia wakati Rais Dkt. Magufuli alipokuwa akihutubia.

Mwanamuziki Christian Bella akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutumbuiza katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ,Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli pamoja na Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula wakiomba dua kabla ya kuhutubia maelfu wa wakazi wa jiji la Mwanza.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Waziri wa Kilimo Mhandisi Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuhutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza. PICHA NA IKULU

Tanzania kuwa mwenyekiti TROIKA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema Tanzania imepokea nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya TROIKA ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inayosimamia masuala ya Ulinzi na Usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Balozi Mahiga alisema Tanzania imepata nafasi hiyo wakati wa Mkutano wa SADC uliojadili masula ya Ulinzi na Usalama uliofanyika hivi karibuni mjini Maputo, Msumbiji.

“Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli atapokea nafasi hiyo ya kuwa mwenyekiti wa TROIKA kutoka kwa Rais wa sasa wa Msumbiji, Filipe Nyusi, nafasi inayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja” alisema Balozi Mahiga.

Aliongeza kuwa Mkutano huo wa TROIKA unatarajiwa kufanyika Agosti 29 na 30 mwaka huu huko Mbabane nchini Swaziland.

Aidha, Balozi Mahiga alisema kuwa SADC ni jumuiya iliyopiga hatua katika kusimamia masuala ya ulinzi, usalama na diplomasia jambo ambalo haliko katika jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kusaidia kutatua masuala yanayohusu hali tete za usalama katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa Waziri Mahiga alisema mkutano wa TROIKA ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika kinachotarajiwa kufanyika baadae mwezi huu ambapo, taarifa ya hali tete ya usalama ya nchini Lesotho itatolewa.

Waziri Mahiga, alisema katika mkutano wa SADC uliofanyika mapema mwezi huu Maputo Msumbiji uliitaka nchi ya Lesotho kutekeleza masuala kadhaa katika kutafuta suluhu ya matatizo nchini humo, ikiwemo kufanya mageuzi ya katiba, mageuzi ya sekta ya ulinzi na usalama pamoja na kufanya marekebisho katika sekta ya utawala. Mkutano huo wa SADC, vilevile unatarajiwa kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jumuiya hiyo ikiwemo mgogoro wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia kuibuka kwa makundi mbalimbali yanayohatarisha amani mashariki mwa nchi hiyo
 

Na. Immaculate Makilika na Abushehe Nondo- MAELEZO
Dar es Salaam
11.8.2016 
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images