Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

MZEE YUSUF AACHANA NA MUZIKI,AVITAKA VITUO VYOTE VYA TELEVISHENI NA REDIO KUACHA KUPIGA NYIMBO ZAKE

$
0
0
Aliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.

Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)

Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).

Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.

Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)

Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.

Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.

KILA KIJIJI KUPATIWA UMEME IFIKAPO 2020

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na sehemu ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na wakandarasi wanaosimamia miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mara baada ya kuwasili wilayani Handeni mkoani Tanga.Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 kila mwananchi anapata umeme wa uhakika na kupelekea uchumi wa nchi kukua kwa kasi.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Tanga Mhandisi Abdulrahman Nyenye akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wengine kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Wilaya ya Handeni, Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akielezea mafanikio ya miradi ya usambazaji wa umeme vijijini iliyotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Pili (REA II).


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (kushoto) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA Awamu ya Pili (REA II) iliyokuwa inasomwa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Tanga Mhandisi Abdulrahman Nyenye (hayupo pichani) 




















Na Greyson Mwase, Tanga



Profesa Muhongo aliyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Pili (REA II) kutoka kwa watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Tanga. Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na REA pamoja na kuzungumza na wananchi.

Profesa Muhongo alisema kuwa kwa kutambua mchango wa nishati ya umeme katika ukuaji wa viwanda nchini, serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa kasi ya usambazaji wa umeme vijijini inaongezeka ili ifikapo mwaka 2020 mgawo wa umeme uwe ni historia.

Alieleza kuwa serikali imeamua kuweka nguvu katika usambazaji wa umeme hususan katika maeneo ya vijijini ili kufuta umaskini kwani kupitia nishati ya umeme wananchi waishio vijijini wana uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuongeza ajira na kupunguza wimbi la vijana wengi kukimbilia mijini kwa ajili ya kutafuta maisha.

Akielezea mpango wa utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini itakayosimamiwa na REA Awamu ya Tatu (REA III), Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imetenga zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika maeneo yote kipaumbele kikiwa ni katika vijiji vilivyokosa umeme REA Awamu ya Pili. (REA II)

Hata hivyo Profesa Muhongo alieleza kuwa wakandarasi waliokwamisha miradi ya REA Awamu ya Pili hawatapewa kazi ya kusambaza umeme vijijini katika REA Awamu ya Tatu.

“Serikali iko makini katika kuhakikisha kuwa wakandarasi wenye sifa wanapewa kasi ya kusambaza umeme vijijini, hatuhitaji wakandarasi wasiotekeleza miradi kwa wakati,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo aliwataka wakandarasi wa kitanzania wenye vigezo kujitokeza na kuchangamkia fursa ya kusambaza umeme vijijini kupita REA Awamu ya Tatu.

Aliongeza kuwa kupitia REA Awamu ya Pili wakandarasi wa kitanzania walionyesha uwezo mkubwa sana katika kusambaza umeme vijijini.

Ili kuendana na mahitaji ya umeme nchini Profesa Muhongo alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linaongeza Megawati 200 za ziada ndani ya miezi 18.

Alisema wakati serikali kupitia REA ikiendela na kasi yake ya kusambaza umeme nchi nzima, shirika la TANESCO linatakiwa kuhakikisha nishati ya uhakika inapatikana ikiwa ni pamoja na ubunifu wa vyanzo vipya vya umeme.

Awali akielezea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania mkoani Tanga, Mhandisi Abdulrahman Nyenye alisema kuwa miradi ya umeme vijijini chini ya ufadhili wa REA imekuwa ikitekelezwa katika wilaya zote nane za mkoa wa Tanga ambazo ni pamoja na Tanga Mjini, Muheza, Korogwe, Handeni, Kilindi, Lushoto, Pangani na Mkinga ambazo zinapata umeme wake kutoka Gridi ya Taifa kupitia vituo vya Hale, Kange na Tanga (Majani Mapana)

Alisema kundi la kwanza lilihusisha wilaya za Korogwe, Lushoto, Handeni na Kilindi ambapo mradi wa wilaya hizi ulitekelezwa na mkandarasi STEG International Services Ltd ya Tunisia na kusimamiwa na TANESCO.

Alifafanua kuwa gharama za mradi huo ilikuwa ni Dola za Marekani 9,463,502 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 14.6 na kuendelea kusema kuwa kundi la pili lilihusisha wilaya za Muheza, Mkinga, Tanga Vijijini na Pangani na kutekelezwa na mkandarasi Sengerema Engineering Group Ltd ya Tanzania na kusimamiwa na TANESCO.

Alisema kuwa mradi huu uligharimu shilingi bilioni 15.6 na kusisitiza kuwa miradi yote kwa mkoa wa Tanga imekamilika kwa asilimia 99 ambapo jumla ya vijiji 178 vimepatiwa huduma ya umeme

Akielezea changamoto katika utekelezaji wa miradi hiyo Mhandisi Nyenye alieleza kuwa ni pamoja na tatizo la wananchi kuzuia upitishwaji wa laini za umeme kwenye maeneo yao kwa kudai fidia ili kuruhusu mazao yao yakatwe na hali ya hewa ya mvua isiyotabirika hasa maeneo ya wilaya za Muheza na Lushoto.

Alitaja chagamoto nyingine kuwa ni pamoja na ubovu wa miundombinu hasa ya barabara kwenye maeneo mengi , hali duni ya kiuchumi ya wananchi inayopelekea wananchi kushindwa kulipa gharama za kuunganishiwa umeme na gharama kubwa za ukaguzi wa miundombinu ya ndani (wiring) zinazotozwa na wakandarasi ambazo zimekuwa ni kikwazo kwa wananchi wanaohitaji huduma ya umeme.

TUPO TAYARI KUWAHUDUMIA WANAOHAMIA DODOMA – TTCL.

$
0
0
 Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Nicodemus Thom Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa maofisa habari kutoka idara ya Habari. Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Nicodemus Thom Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa maofisa habari kutoka idara ya Habari. Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Nicodemus Thom Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa maofisa habari kutoka idara ya Habari. Mkutano wa waandishi wa habari na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ukiendelea. Kulia ni baadhi ya wanahabari wakifuatilia mazungumzo hayo.

Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imesema ipo tayari kutoa huduma za Mawasiliano za kisasa kwa Taasisi za Umma zinazohamia mkoani Dodoma kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa taasisi hizo jijini Dar Es Salaam kuzisaidia kutekeleza majukumu yao. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Meneja Mawasiliano wa TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelelezo) ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kwa Taasisi zake kuwasiliana na Umma na kutoa ufafanuzi wa hoja mbali mbali.

“TTCL imejipanga vyema kufanikisha azma hii ya Serikali ya kuhamia Dodoma. Tupo tayari na tunao uwezo mkubwa wa Rasilimali watu, vifaa na utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za Mawasiliano.

Tunawahakikishia wateja wetu wote kuwa, watakapochagua kuitumia TTCL, watakuwa wamefanya uchaguzi sahihi. Nitumie fursa hii kuziomba taasisi zote za Umma zinazohamia Dodoma na taasisi zote kwa ujumla kutumia huduma za TTCL ambazo siku zote zimethibitika kuwa ni huduma bora, za uhakika na zenye gharama nafuu,” alisema Bw. Thom Mushi. Akizungumzia kuhusu mipango ya Kampuni hiyo kuboresha huduma zake, Bw. Mushi alisema, kwa kutumia fursa iliyopo katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, TTCL inaendelea kutekeleza kwa vitendo wajibu wake kwa Umma kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunganisha Kampuni, Taasisi, Ofisi za Serikali, Mashirika ya Umma na binafsi wateja waliopo nchi jirani ili waweze kupata Mawasiliano ya uhakika wakati wote. 

Kwa sasa tunao Mpango Mkakati wa Biashara wa miaka mitatu(Strategic Business Plan 2016-2018) unaolenga kuboresha na kuleta huduma mpya katika soko, kuongeza jita na uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa Wateja wetu hasa tukizingatia kuwa, TTCL ni mhimili mkuu wa mawasiliano nchini Tanzania.

Akifafanua kuhusu hatua muhimu zilizochukuliwa na TTCL hadi sasa kutekeleza mpango wa mabadiliko, alisema ni pamoja na kuboresha miundombinu ya mtandao wa Simu na Data, kuondoa mitambo chakavu, kuleta huduma bora na zenye kukidhi mahitaji. Aidha aliongeza kuwa TTCL imeboresha miundombinu ya simu za mezani na Mkononi kwa kuleta teknolojia ya GSM -2G, UMTS-3G na 4G LTE sokoni ili kwenda sambamba na ushindani wa soko la mawasiliano. 

Teknolojia hii itasaidia kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya simu za mezani, simu za mkononi na huduma ya intaneti yenye kasi zaidi. “…TTCL inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya Data nchi nzima (IP Core Network, IP transport Network, Metro Network). Hii itaongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wetu kama vile Wizara, Idara na Taasisi za Umma, Serikali za Mitaa, Taasisi za fedha, Kampuni za Umma na binafsi na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi. Kufanikiwa kwa mpango huu kutaleta mabadilko chanya katika huduma za kijamii kama vile Elimu, Afya, Biashara, Uwekezaji, Ujasiriamali, Kilimo, Ufugaji na huduma nyingine ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji mawasiliano ya uhakika ili kufanyika kwa ufanisi.” Wakati huo huo, kampuni ya TTCL imempongeza mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari (Maelezo) Mwanahabari Mwandamizi, Ndugu Hassan Abbas, kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo. 

“Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kumpongeza Ndugu Hassan Abbas, kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.” “Wasifu wa Ndugu Abbas unatupa imani kubwa kwamba, chini ya uongozi wake, pamoja na utekelezaji wa Majukumu mengine, Idara ya Habari Maelezo itaendelea kutoa mwongozo thabiti kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali pamoja na kuhakikisha kuwa, Umma unapata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka kuhusu utendaji wa Serikali katika kuwatumikia,” alisema Bw. Thom Mushi.

Kampuni ya Anuflo yazindua karatasi maalum ya kuzuia maambukizi ya UTI

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus akimuelezea Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Shekha Nasser (wa pili kulia) jinsi ya matumizi ya karatasi maalum ya kutandika kwenye sinki la choo ijulikanyo kwa jina la Believe Toilet Seat cover mara baada ya uzinduzi wa bidhaa hiyo.Kushoto ni mmoja wa mdau wa bidhaa hiyo akishuhudia.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Shekha Nasser (katikati) akiitambulisha karatasi maalum ya kutandika kwenye sinki la choo ijulikanyo kwa jina la Believe Toilet Seat cover mara baada ya uzinduzi wa bidhaa hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus na kushoto ni mmoja wa mdau wa bidhaa hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus wa pili kulia akimuelezea mmoja wa mdau, Shumbana Wawa ambaye anafanyakazi kampuni ya MultiChoice Tanzania, jinsi ya kutumia karatasi maalum ya kutandika kwenye sinki la choo ijulikanyo kwa jina la Believe Toilet Seat cover. Akifuatilia maelekezo hayo ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Shekha Nasser (wa pili kushoto)

Tatizo sugu la ugonjwa wa UTI na magonjwa ya ngozi yanayosabishwa na uchafu chooni, limepatiwa tiba baada ya kampuni ya Anuflo Industries Limited kuzindua karatasi maalum za kuzuia tatizo hilo lijulikanalo kwa jina la ‘Believe toilet seat cover’ ambazo huzuia maambukizi hayo.

Mbali ya karatasi hizo, kampuni hiyo pia imezindua karatasi maalum ya ‘kuondoa mafuta kwenye uso ijulikanayo kwa jina la “Believe blotting paper’ ambayo ni maalum kwa warembo, ma-bibi harusi na wanawake wenye tatizo hilo kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus alisema kuwa ameamua kutengeneza bidhaa hizo kutokana na matatizo ambao yameanza kuwa sugu na kero kwa jamii.

Flora alisema kuwa tatizo la ugonjwa wa UTI na ugonjwa wa ngozi vimekuwa kero kubwa kwa jamii na hii inatokana na matumizi mabaya ya choo iwe nyumbani, kazini, sehemu za starehe na maeneo mengine kama Baa nk.

Alisema kuwa kuna watu si wastaharabu katika matumizi ya vyoo na usababisha kujisaidia haja ndogo kwenye sinki la choo na kumpa shida mtu mwenye lengo la kujisaidia haja kubwa.

“Inafikia hatua mtu anaamua kupanda juu ya sinki la choo ili kuepuka kukalia mkojo ambao umetokana na matatizo ya matumizi mabaya, matokeo yake ni uharibifu wa choo au kuhatarisha kuvunjika miguu kutokana na kuepuka ugonjwa wa UTI na magonjwa mengine ya ngozi,”

“Kwa kutambua tatizo hilo, tukaamua kuzalisha bidhaa hii ambayo inaingia sokoni kwa mara ya kwanza Tanzania tena kwa bei nafuu kuliko kutibu ugonjwa wa UTI ambao gharama yake ni kubwa na uhatarisha matatizo mbalimbali ya kiafya,” alisema Flora.

Alisema kuwa bidhaa hiyo itapatikana kwenye maduka ya Shear Illusions na kwenye supermarket mbalimbali za jijini na kuwaomba wadau kununua ili kujikinga na matizo hayo.Kuhusiana na karatasi maalum za kuondoa mafuta usoni, Flora alisema kuwa nazo zimeingia zenye ubora wa hali ya juu na kuondoa tatizo la mtu kujifuta kwa njia ya leso na ‘tissue’ ambazo si matumizi sahihi.

“Mabibi harusi, warembo na wanawake kwa ujumla,karatasi hizi ni sahihi kwa kuondoa mafuta usoni, tuache kutumia vitambaa, bidhaa hii imetengenezwa kwa ajili ya kuondoa tatizo hilo,” alisema.

TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarufa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.

Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani Richard Muyungi

TANZANIA inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka 2030 ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchi.

Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.

“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.

Ambapo alisema katika kushiriki juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .

Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa nchini.

“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.

Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia wizara za kisekta.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

CHRISTIAN BELLA ALIVYONOGESHA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI JIJINI MWANZA

$
0
0
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akikonga nyoyo za maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akitumbuiza  maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akiimba mbele ya maelfu ya wananchi wa  jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akipongezwa kwa kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwanamuziki nyota Christian Bella baada ya kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016

WAENEDLEZA SEKTA YA MILIKI WAOMBWA KUWEKEZA DODOMA.

$
0
0


Jonas Kamaleki, MAELEZO

Waendelezaji sekta za miliki nchini wameombwa kuwekeza Dodoma ili kuweka mazingira safi ya Serikali kuhamia mjini hapo.

Akizungumza na Waendelezaji sekta za miliki (Real Estate Developers) leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amewakaribisha waendelezaji hao kuanza uwekezaji wa majengo mjini Dodoma.

“Sisi tuhahamia Dodoma tunawaomba nanyi watu wa sekta binafsi kuwekeza mjini hapo ili kushirikiana na Serikali katika zoezi hilo. Dodoma kuna fursa nyingi za biashara hivyo nawataka mkazichangamkie”,alisema Lukuvi.

Aidha, Lukuvi amesema kuwa Dar es Salaam itakuwa ni kitovu cha biashara na si kwa ajili ya shughuli za kiserikali, hivyo itakuwa na sura tofauti ambayo itaakisi kuwa ni kweli ya kibiashara.

“Tunatengeza mpango kamambe (Master plan) wa jiji la Dar es Salaam ili kiwe kweli kitovu cha biashara, hiyo ni fursa nyingine kwenu kuitumia”,alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, mpango huo wa Dar es Salaam mpya utakamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu (2016) na utaenda sanjari na wa jiji la Mwanza na Arusha.

Akiwakaribisha waendelezaji wa sekta za miliki, Lukuvi amesema Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) imeshapima na kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli mbali mbali mjini Dodoma. Ameainisha maeneo hayo kuwa ya makazi, shule, viwanda, Hospitali, Mahoteli na sehemu za starehe.

Rai ya Waziri Lukuvi inakuja siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipotoa kauli kuwa Serikali itahamia Dodoma ndani ya kipindi chake cha uongozi kilichobaki cha miaka mine (4) na miezi mine (4).

Tamko la Rais Magufuli alilolitoa wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Julai 23, 2016, lilifuatiwa na la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye alisema kuwa yeye atahamia Dodoma Septemba, 2016. Baada ya hapo mawaziri kadha wa kadha wameonyesha kuunga mkono tamko hilo na kuanza kujiwekea malengo ya kuhamia Dodoma.

Tangu nia ya kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali itolewe mwaka 1973 na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, maandalizi ya kuhamia huko ndipo yalianza. Majengo kwa ajili ya ofisi za serikali yalianza kujengwa na kuthibitisha hilo baadhi ya wizara zilionyesha nia ya kuhamia Dodoma. Mpaka sasa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko Dodoma na nyingine zinafuata.

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAANDAA SEMINA KWA WAHARIRI WAKUU WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa James Mlowe akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali na wageni waalikwa kwenye mkutano ulioandaliwa na LAPF,uliofanyika mapema leo jijini Dar Es Salaam.Mkutano huo uliokuwa na wawasilishaji mada mbalimbali walioelezea Mafanikio ya mfuko huo,Dira ya mfuko huo,mambo ya uwekezaji,nini ufanye ukipata pensheni yako mara baada kustaafu,mafao yanayotolewa na mfuko huo sambamba na pensheni mbalimbali ikiwemo pensheni ya Urithi,pensheni ya ulemavu na nyinginezo .
Meneja wa Kanda ya Dar Es Salaam kutoka mfuko wa Pensheni wa LAPF.Bi.Amina Kassim akiwasilisha mada iliyohusu Maandalizi ya kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu namna ya kutumia pensheni yako mara tu baada ya kustaafu katika mkutano kwa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania,mkutano huo wa siku moja uliondaliwa na LAPF umefanyika leo jijini Dar .

Bi Amina alieleza kuwa kuna tafiti zinabainisha kuwa baadhi yao wakishapata fedha za kustaafu mara nyingi wamekuwa wakikosa nidhamu ya kuzitumia fedha hizo,wamekuwa wakinunua vitu vya anasa wasivyokuwa na ulazima navyo ,wamekuwa wakikosa ndoto kuhusu Maisha watakayoishi baada ya kustaafu,hivyo amewataka Wastaafu kuwa na mambo muhimu ya kufanya ikiwemo maandalizi ya kiuchumi,kuwa na nidhamu ya fedha,kuwekeza fedha zao katika mambo mbalimbali,kufanya uwekezaji wa biashara binafsi. 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri,Bwa.Theophil Makunga akitoa mwongozo mfupi kwa wageni waalikwa wa mkutano kwa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania,mkutano huo wa siku moja uliondaliwa na LAPF umefanyika leo jijini Dar,ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo nashughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF.
Meneja Matekelezo Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa.Victor Kikoti akiwasilisha mada kwa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania, iliyokuwa ikihusu mambo mbalimbali ya mfuko huo ulioanzishwa mwaka 1944,ikiwa na Dira ya kuwa mfuko bora wa Pensheni unaopendwa zaidi hapa nchini.
Afisa Mwandamizi Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Bi. Rehema Mkamba akitoa maelekezo mafupi kwa washiriki wa mkutano wa Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania katika mkutano huo uliondaliwa na LAPF,uliofanyika jijini Dar.
Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano huo uliondaliwa na LAPF .

HANDBALL TANZANIA YAWIKA MBELE UGANDA

$
0
0

Mshambuiliaji wa Timu ya Tanzania Ally Hamisi (Mwenye Mpira ) akitafuta namna ya kuwatoka walinzi wa Timu ya Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23
Mshambuiliaji wa Timu ya Tanzania Ally Hamisi (Mwenye jezi namba 11) akipambana na walinzi wa Timu ya Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23
Baadhi ya mashabiki wa Timu ya Tanzania Wakishangilia wakati Timu yao ikipambana na Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23.
Mchezaji wa Timu ya Tanzania Mtumwa JUma akipambana na walinzi wa Timu ya Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23


Na Selemani Semunyu JWTZ
Timu ya mpira wa Mikono ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imefanikiwa kurejesha nguvu yake baada ya kuifunga Timu ya Jeshi la Uganda UPDF kwa 24-23 katika Mchezo wa Pili wa Timu hiyo uliokuwa na ushindani mkali baina ya Timu hizo.

JWTZ imeifunga UPDF Timu zote zilianza Mchezo taratibu huku wakijaribu kusomana wachezaji wa timu hizo hali il;iyokuwa ikibadioli mchezo huo katika kila dakika inayomalizika huku tanzani awakionekana kuwazidi wenzao wa Uganda.

Hadi Nusu ya Kwanza ya Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro ilimalizika huku Timu ya Tanzani ilikuwa ikiongoza kwa magoli 12 -9 dhidi ya Uganda ambao walionekana kupoteana katika kipindi hicho chwa kwanza.

Kipindi cha pili Uganda waliingia kwa Nguvu huku wakionyesha kufaidika na Kipindi cha mapunziko kwani walifanikiwa kupunguza idadi ya Tofauti ya magoli na kuibana Tanzania kutokuwa na tofauti kubwa na hatimaye kufanikiwa kutoka uwanjani wakiwa wamefungana kwa tofauti ya Goli Moja.

Nahodha wa Timu ya Tanzania Sedrick Damiano alisema kipingon walichopata katika Mchezo wa kwanza kutoka kwa Rwanda kimewafanya kubadilika na kurekebisha makosa yaliyojitopkeza sambamba kuwa makini na Waamuzi.

Pia Alisema ni mategemeo yake ushindi huu utakuwa salamu tosha kwa Wapinzani wao Kenya ambao watakutana nao katika mchezo unaotarajiwa kufanyika Agosti 14 katika uwanja wa Amahoro. Kwa Upande wake mkurugenzi wa Michezo wa JWTZ Brigedia Jenerali Martin Busungu alisema ushindi huo umewapa nguvu ya kuhakikisha wanashinda katika michezo iliyosalia.

Katika Mchezo Mwingine katika Mpira wa pete Tanzania inatarajiwa kukutana na Wenyeji Rwanda wakati katika Mpira wa Miguu Tanzania inatarajia Kukutana na Kenya katika Uwanja wa Kigali Nyamirambo.

WAZIRI NAPE ATAKA WATU KUTUMIA FURSA ZA UONESHAJ MBASHARA WA MASHINDANO YA LIGI KUU BARANI ULAYA

$
0
0

Waziri wa Habari,Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye akizungumza jana katika uzinduzi wa uoneshaji mbashara wa mashindano ya ligi kuu Barani uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye akipokea zawadi ya king'amuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi wa TV 1,Balozi Paul Lupia katika uzinduzi wa uoneshaji mbashara wa mashindano ya ligi kuu Barani uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye akiteta jambo na Mkurugenzi wa TV I,Joseph Sai katika uzinduzi uoneshaji mbashara wa mashindano ya ligi kuu Barani uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 
WAZIRI wa Habari,Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye amesema kuwa uoneshaji mbashara wa mashindano ya ligi kuu Barani Ulaya
yanayoanza kutimua vumbi leo na kuonyeshwa mbashara na TV 1 ni fursa kwa wachezaji wa ndani kujifunza mbinu mbalimbali katika kuboresha ligi za ndani.

Nape amyesema hayo jana wakati wa uzinduzi wa uoneshaji wa mbashara wa TV 1 wa mashindano ya Ligi kuu Barani Ulaya yanayoanza kutimua vumbi leo amesema kuwa TV 1 kuonesha mashinadano hayo yanaongeza fursa kwa wizara yake katika wananchi kuweza kupata habari za michezo.

Amesema kuwa ni fursa ya kwa watu kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani kupitia oneshaji huo kutokana na watu wa nje wanaamini Mlima Kilimanjaro uko Kenya na wakitaka kufika lazima wafanye hivyo wakati haiko hivyo.

Amesema kuwa sekta ya Wizara yake ni kubwa hivyo wananchi wanafursa ya kufanya matangazo mbalimbali katika mashindano hayo ya ligi kuu barani Ulaya.

Nape amesema kuwa hata yeye ni shabiki wa timu wa Manchester United na anatabiri kuwa wataingia fainali katika mshindano hayo na kuweza kuibuka kuwa mabingwa barani ulaya.

Aidha amesema sekta ya utalii wanatakiwa kutumia fursa ya mashindano ya kuhamasisha utalii ikiwa ni pamoja na kuelezea mlima kiliimanjaro uko Tanzania na Sio Nchini Kenya na watalii wakisafiri wafike Tanzania kwa kufanya hivyo watakuwa wameisadia serikali kupata mapato ya moja kwa moja.

Aidha ametaka kuanza kwa mashindano hayo kuongeza ujuzi wa wachezaji katika kuweza kubadili soka la ndani kuwa na ushindani wenye tija wa kusonga mbele katika mchezo wa miguu.

HOJA YA HAJA: WAZIRI WA MAWASILIANO NA WAHUSIKA TAFADHALI ANGALIENI BEI ZA INTERNET KWA MAKAMPUNI YA SIMU NCHINI TANZANIA

$
0
0
Imekuwa ni kawaida kwa makampuni ya simu za Mikononi za Tanzania katika kufanya maamuzi binafsi katika kupanga bei za internet bila ya kumuangalia mtumiaji wa mwisho ambae ni Mtanzania Masikini.

Napata ugumu kuamini Tanzania inayotafuta maendeleo kwenye nyanja hii kwanini iweze kukubali na kuwaachia makampuni ya simu kufanya Price Fixing watakavyo huku wakishusha viwango vya internet (MB) na kuongeza thamani ya gharama kwa watumiaji wa Tanzania ambao ni masikini huku wizara husika ipo, Competition Commission, Competition And Consumer Protection Policies zipo na wahusika wapo wanafumbia macho tu.

Tukitaka Tanzania iendane na dunia inavyokwenda na kuongezeka kimaendeleo katika nyanja hii na tukitaka kwenda sambamba na Mtazamo madhubuti na ulio mzuri wa Mheshimiwa Rais wetu Magufuli wa kuiletea Tanzania maendeleo kwenye kila nyanja na kutaka kufanya Tanzania liwe Taifa lenye nguvu duniani na lenye watu walio elimika ni vyema wahusika wakahakikisha haya makampuni ya simu hayafanyi Price Fixing maana ukiangalia kwa undani viwango vyao vya kuuza internet vyote vimepangwa sawa sawa na vyote wamevishusha kwa wakati mmoja bila ya kutoa sababu ya msingi inayo wafanya kuongeza gharama na kushusha viwango vya internet wakati Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umepita Tanzania.

Wahusika kama mkishindwa kuwatetea Watanzania walio wanyonge, Mheshimiwa Rais Magufuli hili ni jipu tunaomba uanze kutumbua kwenye sekta hii ya mawasiliano.

Ni matumaini yetu wahusika na wadau wote watakutana na kuweza kulitafutia mchakato madhubuti kwa kuwatetea watumiaji wa simu na internet nchini Tanzania na vile ili kuweza kuleta maendeleo nchi nzima na kuwawezesha ata Mtanzania aliyepo Chato au Sumbawanga aweze kupata fursa ya kuunganishwa na dunia kwa kupata viwango vya bei iliyo nzuri na viwango vikubwa vya internet. Vile vile kuanzia sasa haya makampuni ya simu kamwe yasifumbiwe macho kwa bei wanazozipanga kwenye huduma ya mawasiliano kwa maana yanawanyonya Watanzania ambao ni masikini kwa manufaa yao!

RAIS MAGUFULI AISIFIA 'SIZONJE 'YA MRISHO MPOTO,ATENGUA FUMBO LA MASHAIRI YAKE

$
0
0
Utunzi mahiri wa mashairi na ughani uliotukuka wa Mrisho Mpoto, umeligusa sikio la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameeleza kuwa shabiki mkubwa wa kazi za msanii huyo hususan wimbo wake ‘Sizonje’.

Akizungumza na Mpoto jana, muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli alimueleza msanii huyo kuwa anazifahamu vizuri kazi zake na kwamba anaupenda sana wimbo wake wa ‘Sizonje’ huku akichambua baadhi ya mistari iliyomo kwenye beti za wimbo huo.

Mpoto alikuwa msanii pekee aliyeongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Wakuu wote wa Wilaya za Dar es Saalam pamoja na viongozi wengine waliofika katika uwanja huo wa ndege kumpokea Mkuu huyo wa nchi.

“Nasikiliza nyimbo zako sana, ila huu wimbo wako wa Sizonje nimeuelewa sana na nausikiliza kila siku, kwangu umekuwa kama wimbo wa taifa, mwanzoni nilipata tabu kuuelewa lakini sasa hivi… aaaah, nimeuelewa vizuri sana. Halafu Sizonje namjua, nimtaje?,” yalisikika baadhi ya maneno ya Rais Magufuli kwa Mrisho Mpoto.

Akielezea tukio hilo lililoleta msisimko wa aina yake uwanjani hapo, Mpoto alisema kuwa baada ya kumsikia Rais ameanza kuusifia wimbo wake alishtuka na kujawa na furaha ya aina yake kwani kwa msanii ni jambo la thamani kubwa kusifiwa kazi yake na Mkuu wa Nchi.

Alisema kuwa pamoja na kuusifia wimbo huo, Rais alionesha kuufahamu vizuri zaidi baada ya kuanza kuipitia baadhi ya mistari na kuahidi kumfumbulia fumbo lililofichwa kwenye wimbo huo watakapokutana tena.

“Unapopata thamani kutoka kwa Mkuu wa Nchi inaleta faraja sana," amesema Mpoto. "Kwahiyo, mheshimiwa Rais leo kuniambia kwamba yeye ni shabiki wa kazi zangu na kwamba anapenda sana wimbo wa Sizonje, na akafunguka kwa mistari ‘minane’ ya Sizonje ikiwa ni pamoja na ile inayosema ‘huyu mgeni anayepitia madirishani wakati milango ipo!’ Na akaniambia siku tukikutana ataniambia vile vyumba vitatu kwanini havifunguki,” ameongeza.

Msanii huyo amemshukuru Rais Magufuli kwa kuthamini mchango wake katika sanaa kwakuwa anaamini kuthaminiwa ni hitaji kubwa la kila msanii.

“Kwakweli leo ni siku yenye furaha sana. Najisikia furaha sana. Asante sana mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. Umenifanya nimekuwa na siku nzuri sana,” Mpoto amefunguka kwa furaha.

Mwaka huu mwanzoni, Mrisho Mpoto aliachia audio na video ya ‘Sizonje’ aliomshirikisha Banana Zorro ambapo kwa muda mfupi tu, wimbo huo uligeuka kuwa mkubwa na kufanya vizuri. Kutokana na ufanisi wa kazi zake, Mpoto ameendelea kukubalika akipata mikataba ya ubalozi wa mashirika na taasisi kubwa nchini ikiwa ni pamoja na mfuko wa pensheni wa PSPF.

VIONGOZI WA CUF WAKIONGOZWA NA MAALIM SEIF WAMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI NYUMBANI KWAKE LEO JIJINI DAR

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo leo Agosti 13, 2016 .
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam.
Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe. Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakimwombea dua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) ili aendelee kuwa na afya njema ya kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu walipomtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto) akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Viongozi wa CUF wamefika nyumbani kwa Mhe. Spika, Job Ndugai kumjulia hali baada ya kurejea hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.

SHILINGI BILIONI 7.56 ZAPATIKANA MNADA WA MADINI YA TANZANITE

$
0
0

Mhandisi Juma Lunda( kulia)akitoa bahasha katika sanduku maalum la kuhifadhia maombi ya zabuni za kununua madini ya Tanzanite katika mnada. 


Na Zuena Msuya Arusha

 Serikali yakusanya Mrabaha wa Zaidi ya Milioni 331

Serikali imekusanya mrabaha wa zaidi ya shilingi milioni 331 katika mnada wa madini ya Tanzanite yaliouzwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 7.56 kutoka kampuni mbili za uchimbaji madini hayo katika eneo la Mirerani mkoani Manyara.

Akitangaza washindi wa zabuni za kununua madini ya Tanzanite mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, Mkurugenzi wa kitengo uthaminishaji Almas na madini ya vito(TANSORT), Ardhard Kalugendo alisema kuwa katika mnada huo kampuni tano zilijitokeza, mbili kati ya hizo ziliuza madini yake kwa wanunuzi mbalimbali; Kampuni tatu hazikuweza kuuza kutokana na kutokubalina bei na wanunuzi.

Kalugendo alifafanua kuwa mnada huo ulifanyika kwa njia ya uwazi na kushirikisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera alisema kuwa mnada huo umeiwezesha Serikali kupata mrabaha pamoja na kuzuia utoroswaji wa madini hayo nje ya nchi uliokuwa ukiikosesha Serikali mapato yake kwa maendeleo ya taifa.

Katika hatua nyingine Bendera aliwatoa hofu wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika migodi ya Mirerani mkoani Manyara kuwa kwa Serikali imeimarisha ulinzi kwa usalama pamoja na mali zao; Pia wafanyabiara wa Tanzanite watoe ushirikiano kwa vyombo vya usalama pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.

Aidha aliwasihi wanunuzi na wachimbaji wa Tanzanite kufuata sheria na taratibu za uchimbaji na ununuzi ili kuhakikisha kuwa madini hayo adhimu yanayopatikana nchini tanzania pekee duniani yanawanufaisha watanzania wote.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe,( kushoto) akishuhudia uchambuaji wa barua za maombi ya zabuni ya kununua madini ya Tanzanite wakati wa mnada.

Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe alisema kuwa pamoja na manufaa yaliopatikana katika mnada huo, Serikali itaendelea kuboresha mnada huo kwa kuongeza muda zaidi ili kutoa fursa kwa kila mfanyabiasha wa Tanzanite kushiriki; Vilevile kuwepo na majadiliano zaidi kati ya wauzaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Profesa Mdoe aliongeza kuwa lengo la Serikali katika mnada huo ni kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite kupata matokeo chanya na yenye tija katika shughuli zao, pia Taifa linufaike kutokana na matokeo hayo kwa njia mbalimbali.

Mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Tanzanite, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzaniteone Faisal Shuhbhai aliipongeza Serikali kwa kuweka utaratibu huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini kwakuwa utawawezesha wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao kwa ufanisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Faisal alisema kuwa utaratibu wa mnada utawawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite waliokuwa wakikwepa kodi, kulipa mirabaha kwa wakati baada ya kuwepo kwa mpango huo ambao haukuwepo hapo awali; Aidha utawasaidia wafanyabiara kupata bei elekezi inayoendana na soko la dunia na hivyo kuacha kutorosha madini ya Tanzanite nje ya Tanzania kwa madai ya kutafuta masoko.

Baadhi ya wauzaji na wanunuzi na madini ya Tanzanite walioshiriki katika mnada,Mkurugenzi wa Kampuni ya TanzaniteOne Faisal Shahbhai,(kulia) Hussein Gonga( wa pili kulia) mchimbaji, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VGL Group ,Sunil Agrawal( wa pili kushoto), na Mmoja wa Wakurugezi wa Kampuni ya TanzaniaOne, Rizwan Ullah ( kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera( aliyesimama)akisoma hotuba wakati wa kumtangaza mshindi wa zabuni ya kununua madini ya Tanzanite, katika mnada wa madini hayo uliofanyika mkoani Arusha, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe(wa pili kushoto), Mkurugenzi wa kitengo cha uthaminishaji Almasi na madini ya vito,Archard Kalugendo( kulia) na Kamishna Msaidizi wa Madini, Salim Salim( kushoto).
Mkurugenzi wa kitengo cha uthaminishaji Almasi na madini ya vito,Archard Kalugendo( kulia)akitangaza washindi wa zabuni za kununua madini ya Tanzanite,mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera( wa pili kulia) Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe(wa pili kushoto).

Mkurugenzi wa Bunda apokea madawati 90 kutoka kwa Mbunge Ester Bulaya

$
0
0

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jimbo la Bunda Bi. Janeti Mayanja amepokea madawati 90 yalitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi. Ester Bulaya, ambapo hapo awali madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo walikataa kupokea madawati hayo baadaya ya kuwa yameandikwa jina la mbunge huyo pamoja na kuwa yamenunuliwa na fedha za Mfuko wa Jimbo.

Akizungumza leo kwa njia ya simu, Mkurugenzi Mayanja alisema kuwa amepokea madawati hayo jana Agosti 12 kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Ester Bulaya baada ya kufutwa jina lake, ambapo madawati hayo tayari yamewasilishwa katika shule tatu zilikuwa na uhaba.

“Tulifanya kikao na Mbunge Bulaya na tukakubaliana kuwa ni vyema majina yake yakafutwa katika madawati hayo kwa vile yalinunuliwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo, lakini endapo mbunge atapenda kutupa madawati atakayonunua kwa fedha zake binafsi na kuandika majina yake hapo tutapokea kwa vile bado kuna tunauhitaji katika jimbo letu” alisema Mkurugenzi Mayanja

Alifafanua kuwa fedha zilizotumika kununua madawati hayo zilikuwa ni fedha za Mfuko wa Jimbo zinazotokana na ruzuku ya Serikali ambazo matumizi yake hupangwa na Ofisi ya Mbunge.

Madawati hayo 90 yalisambazwa katika shule tatu za Msingi zilizopo katika Jimbo la Bunda zilizokuwa na uhaba wa madawati ambazo ni Nyatwali, Nyerere na Ligamba, zilizopewa madawati 30 kwa kila moja.

MBUNGE VITI MAALUM KAGERA ATOA ZAWADI MBALIMBALI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA KAGERA

$
0
0
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Oliver Semuguruka akisikiliza maelezo kutoka kwa ofisa muuguzi wa wodi ya wazazi Mkoa wa kagera kabla hajatoa zawadi kwa wodi hiyo. 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Oliver Semuguruka akiwa amembeba mmoja wa watoto aliyezaliwa kwenye hospital ta Mkoa wa Kagera alipoenda kuwasalimia na kuwapatia zawadi. 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera akiwa na wajumbe wa umoja wa UWT Mkoa wa Kagera wakiwa nje ya wodi ya wazazi kabla ya kwenda kutoa zawadi kwao


Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Kagera Oliver Semuguruka ametoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospita ya Mkoa wa Kagera.

Ametoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wanawake waliojifungua,watoto na wanawake wajawazito wanaosubiria kujifungua alisema kuwa akiwa kama kiongozi wa jamii anaguswa na masuala mbalimbali hasa yanayohusu wanawake.

"Mimi ni kiongozi wa jamii hasa wanawake,ninaguswa sana na matatizo ya wanawake wenzangu siyo wa hapa Kagera tu wanawake wa Tanzania nzima leo nimekuja kuwapa pole na nimewaletea zawadi za sabuni za kufulia,kuogea,juisi na biscuti "alisema Mbunge huyo

Akizungumzia zawadi hizo Ofisa muuguzi msaidizi wa zamu wa wodi ya wazazi Evelyne Lugabandana alimshukuru Mbunge huyo kwa msaada alitoa kwa wagonjwa.

"Tunamshukuru mbunge wetu kwa moyo wake wa upendo wa kuwakumbuka wanawake wenzake na watoto na kuamua kuja kuwapa pole na kuwapatia zawadi pia"alisema Muuguzi huyo

Baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye wodi hizo ambazo Mbunge ametoa zawadi walimshukuru mbunge kwa zawadi na kumtaka awasaidie kutatua kero waliyonayo ya kulala wawili kitanda kimoja na kwenda na vifaa vya kujifungulia.

ZAIDI YA WAVUVI TISA WALIOKUWA WAKIFANYA UVUVI MTO KAGERA WAFARIKI DUNIA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

$
0
0

Mwenyekiti wa wavuvi wa mwalo wa kitwe akimuelezea waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba jinsi wavuvi wanavyouwawa katika mto kagera  wanapoenda kuvua samaki.
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba akiwa kwenye mmoja wa mtumbwi unaotumiwa na wavuvi wa mwalo wa kitwe Mkoani Kagera.

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera Karlo,Kagera

ZAIDI ya wavuvi tisa waliokuwa wakifanya shughuli zao za uvuvi ndani ya mto Kagera wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa nyakati tofauti.

Akisoma taarifa ya Wilaya kwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchini Lameck Mwigulu Nchema,Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kanali mstaafu Shaabani Lissu alisema kuwa wavuvi hao wanatokea katika mialo ya Rubwela,Kanyika,katwe na Ruko katika ziwa ngoma.

Alisema matukio hayo ya vifo vya utata yameanza kutokea kuanzia mwezi wa pili mwaka huu wakati wavuvi hao wanapoenda kuvua ndani ya mto Kagera unaotenganisha nchi ya Rwanda na Tanzania.

"Mara nyingi wavuvi wakienda kuvua ndani ya Mto Kagera huwa hawarudi,huwa wanatekwa na kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani ya Rwanda"Alisema Mkuu huyo wa Wilaya

Alisema hivi karibuni wavuvi wawili walienda kuvua ndani ya mto Kagera na mmoja aitwaye Emanuel Kahonda alipigwa risasi na kufariki dunia huku mwenzake Yoha Misago akinusurika katika tukio hilo na kukimbia na kwenda kutoa taarifa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

"Mhe.Waziri ni juzi tu kuna mvuvi alipigwa risasi ndani ya mto Kagera hata msiba kwake bado upo, mwenzake aliyeshuhudia na kufanikiwa kuwatoroka wauaji hao yeye kunusurika ndiyo alikuja kutoa taarifa ofisini kwangu"alisema

Naye mwenyekiti wa mwalo wa Kitwe Ustadhi Hakimu alimthibitishia Waziri kuwa wavuvi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kuuwawa kikatili na askari wa nchi jirani ya Rwanda.

"Hapa kijijini kuna wajane wengi,waume zao walikuwa wakienda kuvua samaki ndani ya mto Kagera hawarudi,wanadai tunavua samaki kwenye maji yaliyopo nchi mwao,na mto kagera wameufanya wao peke yao,Tunaomba utusaidie Mhe.Waziri hili tatizo liishe

Upande wa kule kwao kuna misitu sana na huwa wanajificha humo,yaani wakikuona tu wala hawakusemeshi wanakupiga risasi tu humo humo majini,na maiti zimekuwa zikipotelea mtoni humo humo"alisema Mwenyekiti huyo.

Naye waziri wa mambo ya ndani ya nchini Mwigulu Nchemba aliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kyerwa kukutana na viongozi wa mialo ili wapate taarifa rasmi ya chanzo cha matukio hayo na kuipatia wizara ili waweze kutoa tamko rasmi juu ya mauaji hayo ya wavuvi.

"Hali hii imenistua sana,hatuwezi kuruhusu watanzania wenzetu wawe wanauwawa kikatili kiasi hiki,nikipata taarifa rasmi nitafuatilia jambo hili hata kwa kuwasiliana na wenzetu ili nijue kama ni msimamo wa serekali yao au ni uhalifu"alisema Nchemba.

MAANDALIZI YA MAHAKAMA YA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI YAIVA

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (Kushoto) na Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi wakizungumza jambo walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya uanzishwaji wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) akiwa pamoja na wadau wengine wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuangalia Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria Sinza leo jijini Dar es salaam. Baadhi ya Wadau wa Mahakama waliotembelea Mahakama hiyo ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mawasiliano, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) akiwaelezea jambo baadhi ya Makatibu Wakuu na watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi za Serikali ambao ni Wadau wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuwa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es salaam. Anayetazamana na Kattanga ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) wakiwaonyesha jambo wadau wengine wa Mahakama walipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo jijini Dar esa salaam
Makamu Mkuu wa Shule ya Sheria (Fedha na Utawala) Dkt. William Pallangyo na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga wakielezea jambo kwa wadau wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo Sinza jijini Dar es salaam.

YANGA YAIKUNA 1-0,YAJIPA MATUMAINI MAKUBWA YA KUIBAMIZA TP MAZEMBE

$
0
0






Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiachia shuti la hatari kwa kipa wa Bejaia  . Yanga wameibuka kidede kwa goli 1-0 dhidi ya Bejaia
 Golikipa wa Yanga akiokoa mpira wa hatari uliokuwa ukitinga nyavuni kwake
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga Simon Msuva akikokota mpira kuelekea lango la Bejaia.
kipa wa Bejaia akiokoa moja ya hatari iliyoelekezwa langoni mwake na Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva. Yanga wameibuka kidede kwa goli 1-0 dhidi ya Bejaia.

BAADA ya Kupata ushindi wa kwanza walioupata Yanga, Koch mkuu wa Hans Van De Pluijm amesema ushindi huu umempa nguvu katika kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe.

Yanga imefanikiwa kushinda goli 1-0  lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka Zimbabwe Thaban Kamosoku dakika ya tatu dhidi ya Mo bejaia mechi iliyofanyika kwenye dimba la uwanja wa Taifa.

Pluijm amesema kuwa, wachezaji wake wamecheza vizuri sana na wameweza kulinda goli katila dakika zote ingawa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza ila anawapa hongera kwa jitihada walizozifanya.

Naye Nahondha wa Yanga, Vicent Bossou amesema wamefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha wanatoka ushindi na wamecheza timu nzuri sana yenye uzoefu wa muda mrefu wa michuano ya kimataifa ila anawapongeza pia wachezaji wenzake kwa jitihada walizozifanya.

Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku mchezo kati ya Mazembe na Medeama ukitarajiw kuchezwa kesho nchini Ghana.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHITIMISHA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIZIMKAZI (KIZIMKAZI DAY), ZANZIBAR

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Ndugu Idrisa Kitwana wakati wa kilele cha sherehe za siku ya Kimkazi (Kizimkaziday) kwenye kijiji cha Kizimkazi Mkunguni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Mashindano ya kuzuta kamba

Vijana wa Kiume wakishindana kukuna nazi ikiwa sehemu ya mashindano ya Siku ya Kizimkazi (Kizimkazi Day).
Wakina Mama wakishindana kufunga kamba kwenye kilele cha sherehe za Kizimkazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano dhidi ya rushwa,ufisadi kama hatua ya kukomesha tabia hiyo ambayo inarudisha nyumba maendeleo ya wananchi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 13-Aug-16 wakati anahitimisha kilele cha sikukuuu ya Kizimkazi katika kijiji cha Kizimkazi Mkunguni wilayani ya Kusini Unguja – Zanzibar ambaye yeye ni mwasisi wa sikukuu hiyo ambayo inatumiwa na wakazi wa maeneo hayo kufanya michezo mbalimbali ya jadi pamoja na kujadili na kuweka mipango na mikakati ya kujiletea maendeleo kwa ushirikiano na viongozi wao.

Makamu wa Rais amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa watendaji wanaorudisha nyuma maendeleo ya wananchi ikiwemo ubadhirifu wa fedha za umma ili kukomesha tabia hiyo. Amesema kuwa ili wananchi waweze kupata maendeleo ya haraka ni muhimu wananchi wakaimarisha ushirikiano miongoni mwao katika kubaini changamoto zinazowakabili na kushirikiane na viongozi wao katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema yeye kama kiongozi wa kwanza kupata wadhifa huo kutoka kwenye kijiji cha Kizimkazi - Zanzibar ataendelea kushirikiana wananchi hao kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hao ikiwemo tatizo la upatikanaji wa maji.
Makamu wa Rais pia amehimiza wananchi wa Kizimkazi kutafuta eneo haraka kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali ambayo bado ni tatizo kubwa katika eneo hilo ili aweza kuwasaidia katika ujenzi wake kama hatua ya kuondoa kero ya watoto kushindwa kupata elimu ya awali.

Katika Risala maalum ya wananchi wa kijiji cha Kizimkazi na Katibu wa Sherehe hizo Said Ramadhani Mgeni kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wamewapongeza viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada wanazofanya za ukusanyaji wa mapato ya serikali na wamesema wanaimani kubwa kuwa fedha zinazopatikana zitatumika katika kuinua uchumi na kujenga ustawi wa Jamii bora wananchi.

Wananchi hao wameahidi kuwa watadumisha na kuimarisha ushirikiano kati yao na serikali hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Baadhi ya Viongozi wa wilaya na Mkoa wa Kusini Unguja waliopata nafasi ya kuzungumza katika hafla hiyo ya hutimisha sikukuu ya wakizimkazi wamewaomba wananchi kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao. Katika kilele cha sherehe hizo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi ambao walishiriki kwenye mashindano ya siku ya Kizimkazi zikiwemo fedha taslimu.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images