Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

ASASI YA FEDHA YAAMSHA FIKRA KWA VIJANA WA CHUO CHA KILIMANJARO ILI KUFIKIA UHURU WA KIPATO

$
0
0

Muanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Asasi ya FEDHA Jafari Selemani akizungumzia changamoto za vijana na watanzania kwaujumla juu ya kutokufikia Uhuru wa kifedha (financial freedom) ikiwemo ukosefu wa elimu ya usimamizi fedha binafsi ambapo inapelekea umasikini wa watanzania wengi, pia alitumia nafasi hiyo kuzindua progranu ya FEDHA KLABU ambayo itakayowapa fursa vijana kupata elimu ya udhibiti fedha binafsi buree kila jumamosi chuoni hapo.
Ni mshauri wa vijana pia ni Meneja Masoko wa Taasisi ya FEDHA Abdalah Kipinga akiongea na wanafunzi wa chuo ch Kilimanjaro ambapo alizungumzia juu ya maisha ya wanavyuo na changamoto zake na jinsi ya kuzikabili.

Mhamasishaji wa vijana Elly David akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro (hawapo pichani) ambapo alizungumza kuhusu siri ya mafanikio kwa vijana na kuwaasa kusimamia ndoto zao lkatika kongamano lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita chuoni hapo

Wanafunzi wa chuo cha kilimanjaro wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo lililowezeshwa na Taasisi ya Fedha mwsihoni wa wiki iliyopita

Baadhi ya washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji katika kongamano hilo lilifnayika mwisho wa wiki iliyopita chuoni hapo Sinza Mapambano ,Jijini Dar es salaam.

RC PAUL MAKONDA AWAPONGEZA KATAA UNENE FAMILY KWA KUADHIMISHA MIAKA 3

$
0
0
 
Wakifurahia jambo kwa pamoja
Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi (katikati) akiwakaribisha wanachama wenzake wa Kataa Unene Family wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya KUF yaliyofanyika Jumapili Agosti 7, 2016 jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Nidhani ya KUF, Bi. Etty Kusiluka na Bi. Mariam Sagini (kushoto) Mshindi wa shindano la kupunguza kilo 10 kwa muda wa miezi mitatu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akizungumza na wanachama wa Kataa Unene Family (KUF) jumapili Agosti 7, 2016 wakati wa maadhimisho ya miaka 3 tokea umoja huo kuanzishwa. Pembeni kulia ni Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi. Angela Msangi na Bi. Mariam Sagini Bi. Mariam Sagini (kushoto) Mshindi wa shindano la kupunguza kilo 10 kwa muda wa miezi mitatu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akimsikiliza kiongozi wa KUF.
---
Kundi la Kataa unene (KUF) linalojihusisha na kupunguza unene kwa mazoezi na kula vyakula bora limeadhimisha miaka 3 kwa na kuweka mikakati mipya ya kuwasaidia wengine.
Akizungumza katika sherehe hiyo iliyofanyika Epidor Masaki, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ambaye alipita kuwasalimia alilipongeza kundi hilo huku akisema kuwa afya ni msingi wa maendeleo yoyote duniani, hivyo hatua ya kutambua kujiweka imara mapema ni njema.
"Nawapongeza sana kwa moyo mlionao wa kufanya mazoezi si jambo dogo maana linahitaji nidhamu ya hali ya juu kujisimamia mwenyewe bila kushinikizwa na mtu,' alisema Mhe. Makonda.
Aidha, alieleza kuwa viwanja vya michezo jijini Dar es Salaam vipo vingi, maeneo ya wazi pia hivyo kuwasihi wananchi kujihusisha katika mazoezi, huo wao kama viongozi wakiwaunganisha na makundi mengine ya michezo kwa mashindano kama Toto cup, Ndondo cup na mengineyo, hasa wanafunzi wa vyuoni na shule za msingi.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi alisema katika miaka mitatu, tayari watu zaidi ya 40 wamepunguza kuanzia kilo 15 hadi 25, ambapo tayari watu 10 wamefikia malengo ya kilo zinazohitajika kutokana na urefu wao na wanaendelea kujidhibiti.
Angela alisisitiza kuwa, kupungua kwa kufanya mazoezi na kula vyakula vinavyofaa na kushauriwa kunawezekana endapo tu mtu ataamua kujikana na kudhamiria,akiwaondoa watu fikra potofu kuwa wanaopungua wanatumia dawa.
Shughuli hiyo ya Kataa Unene ilienda sambamba na kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri katika shindano la kupungua la miezi mitatu iliyopita, lililopewa jina la Sagini challange,ambapo aliyeibuka kinara wa shindano hilo ni muasisi wa shindano Mariam Sagini, aliyepunguza kilo 10 tangu mwezi Mei mwaka huu.
Wanachama wa KUF wakimpongeza Mjumbe wa Kamati ya Nidhani ya KUF, Bi. Etty Kusiluka wakati akiwapa ujumbe.
Bi. Mariam akiwaonyesha wenzake jinsi gauni lake lilivyomkaa vyema baada ya kupungua kilo 10 kwa muda wa miezi mitatu.
"Yani mwenzako nimejaribu mara hiziiii"
Wanachama wa KUF wakibadilisha mawazo.
Wanachama wa KUF wakipongezana.
Wajumbe wa Kamati ya Nidhamu ya KUF, Bi. Etty Kusiluka (kushoto na Bi. Ester Ulaya Cathbert (kulia) wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu.
Wanachama wa KUF wakipongezana.
 
 
Kila mwanachama aliweza kupata nafasi ya kuelezea changamoto na mafanikio yake.
Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu Bi. Eter Ulaya Cathbert akitoa machache.
Wanachama wa KUF wakipeana zawadi.
Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi akitoa shukrani kwa wanachama wote walioweza kufika katika maadhimisho hayo.
.
Wanachama wa KUF wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda.

Vijuso vyote vya Magazeti ya leo jumanne viko hapa

BANDA LA KILOLO LAVUTIA MAONYESHO WAKULIMA NANE NANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

$
0
0
mtaalamu  wa   kilolo kilolo  akitoa  maelekezo  kwa  wananchi  waliofika  banda  la  Kilolo kupata  elimu juu  ya  zao  la  mahindi
Wakuu wa  idara  Kilolo wakiwa  katika banda  la Kilolo
DC Kilolo Bi Asia  akitazama  nguo  zilizokuwa  zikiuzwa  kwenye banda  la  Kilolo toka  kwa  wajasiliamali wa Ruaha mbuyuni
Mkurugenzi  Kilolo  Bw  Aloyce Kweziakionyesha  mbuga  iliyopandwa  kwenye  bustani ya  aina  yake
Mkurugenzi Kilolo Bw , Aloyce Kwezi kushoto  akiwa  na  wataalam  wake  kwenye  banda  la Kilolo
Wananchi  wakitazama banda  la  ufugaji 
Bw Aloyce Kwezi akiwa katika  picha  ya  pamoja  na washiriki wa  maonyesho hayo kijana  Remi Sanga  mtaalam wa  maua na wengine
, Aloyce Kwezi mkurugenzi  Kilolo  akitembelea banda  la  Kilolo
wananchi  wakitazama  bidhaa  mbali  mbali  katika  banda  la  Kilolo
Mkurugenzi  Kilolo na  viongozi  mbali  mbali  wakitoka katika  banda  la  Kilolo
Mbunge Mary  Mwanjelwa  na  Dc  Asia  Abudalah  wakiwa  katika  maonyesho  ya  nanenane  kanda ya nyanda za  juu kusini jijini Mbeya
Dc  Kilolo Bi  Asia  na  viongozi  mbali  mbali  wakimsubiri  waziri  mkuu
Mkuu  wa  mkoa  wa Njombe Dr  Rehema Nchimbi na  mkuu  wa wilaya  ya  Kilolo Bi Asia  Abdalah  na  mbunge wa  Mbeya Mary  Mwanjelwa  wakiwa  katika  picha  ya  pamoja na MC  Charlesi Mwakipesile na meneja  wa NMB Mbeya
Mbunge  wa  Iringa  mjini Mchungaji Peter Msigwa  akifurahia nyama  choma  ya Mtanga ambae  ni mmoja  wa  wadau  wa  maendeleo Kilolo
Mkurugenzi  wa Halmashauri  ya  Kilolo Bw Aloyce Kwezi akiwa na mkuu  wa  wilaya ya Kilolo Bi Asia Abdalah katika  viwanja  vya nane  nane    jijini Mbeya  mara  baada ya waziri  mkuu kumaliza  kufunga maonyesho  hayo
Diwani  wa kata ya  Ilula Bw  Raymond Francis (Chadema)  akifurahia ushirikiano  wa viongozi na  uzuri  wa banda  la Kilolo
mkurugenzi  Kilolo  , Aloyce Kwezi kushoto akipongezana  na  viongozi  wenzake




Wananchi  wakitembelea banda  la Halmashauri  ya  Kilolo  wakati  wa  kilele cha maonyesho  hayo Picha na MatukiodaimaBlog

NAIBU WAZIRI MPINA AMUWAKILISHA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA SIKU YA KIZIMKAZI

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliyevaa suti akishika na kuangalia nishati ya mkaa unaotengenezwa na malighafi itokanayo na taka za miwa na karatasi mjini Unguja, alipomuwakilisha Makamu wa Raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kampuni ya Blue Spot, inayotengeneza nishati hiyo bila kuharibu Mazingira.
Mabinti Mapacha Sabra na Sabrina Hassan wa shule ya sekondari makunduchi wakitumbuiza kwa utenzi kwa meza kuu haipo pichani, wakati wa mkutano wa Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Hayupo pichani, kijijini Kizimkazi wakati wa siku ya kizimkazi ambapo Naibu waziri Mpina alimuwakilisha Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la makunduchi.
Aliyesimama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na baadhi yaViongozi mbali mbali wa jimbo la Makunduchi mkoa wa kusini Unguja, akizungumza na wanachi (hawapo pichani) wa jimbo hilo katika kijiji cha kizimkazi .katika siku ya kizimkazi maarufu kama kizimkazi day, alipomuwakilisha mhe. Mkamu wa Rais Mama Samia Suhulu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Aliyesimama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na baadhi yaViongozi mbali mbali wa jimbo la Makunduchi mkoa wa kusini Unguja, akizungumza na wanachi (hawapo pichani) wa jimbo hilo katika kijiji cha kizimkazi .katika siku ya kizimkazi maarufu kama kizimkazi day, alipomuwakilisha mhe. Mkamu wa Rais Mama Samia Suhulu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Naibu Waziri Mpina aliyesimama kati kati akishika chembe za malighafi inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki kwa mazingira, alipotembelea kiwanda kidogo cha Ble Spot Mjini Unguja kumwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aliyekaa katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Ris Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Picha ya Pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi, Pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya kutengeza nishati ya Mkaa rafiki wa mazingira, katika kiwanda cha Blue Spot. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.) 
 

Wakazi wa kijiji cha Kizimkazi kilichopo katika jimbo la Makunduchi Mkoa wa kusini unguja, kimekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya kizimkazi, maarufu kama kizimkazi day ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa nane.

Siku hiyo maarufu katika kijiji hicho ambayo imeanzishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo la Makunduchi mhe.Samia Suluhu Hassan ambae sasa ni Makamu wa Rais wa JAmuhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikiadhimishwa kijijini hapo kwa namna ya kipekee ya burudani, mashairi na michezo mbali mbali ambapo pia wana kizimkazi wamekuwa wakipata nafasi ya kuainisha changamoto mbali mbali zinazo wakabili kagtika kijiji hicho.

Akimuwalisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa RAis Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amehaidi kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Makunduchi mhe. Haruna Suleiman ambae pia ni Waziri wa Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia mifuko 100 ya simenti na mabati 100, na matofali 2000 ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimeanishwa kuwa moja ya changamoto kijijini hapo.

Aidha, amehaidi wana kizimkazi kuwa kwa kushirikiana na mbunge na uongozi wa serikali uwanja wa mpira ambao umekuwa ukihitaji matengezo nao utaanza kusawazishwa kwa ajili ya michezo kijijini hapo.

Wana Kizimkazi wamebainisha kukabiliana na changamoto itokanayo na mapato na matumizi ya rasilimali ya bahari, pamoja na kupungua kwa nishati ya umeme kutokana na ongezeko la mahitaji litokanalo na mji huo kupanuka.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Mpina Pia alimuwailisha Makamo wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kampuni inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki wa mazingira inayotumia malighafi itoknayo na taka za maganda ya miwa na makarati na kuwapongeza kwa jitihada kubwa za utunzaji wa mazingira kwa kutokukata miti ovyo na ubunifu wa nishati hiyo.

Ziara ya naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar ni Sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Pamoja na kumuwakilisha Mhe, Makamu wa Rais katika siku maalum ya Kizimkazi. Kizimkazi Day.

ANAWAZA ATOKE VIPI KWA SPEED YA JPM.

WANANCHI WA WILAYA YA MISSENYI WAMTAKA MBUNGE KAMALA KUTATUA MATATIZO YAO

$
0
0
 
Mbunge wa jimbo la Nkenge Deodarius Kamala akiongea na wananchi wa kijiji cha Bulembe kata Minziro wakati wa ziara yake kwenye mkutano wake wa hadhara wa kujua kero za wananchi .
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya missenyi Projestus Tegamaisho akiongea na wananchi wa kijiji cha Bulembi wakati wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Nkenge
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Bulembi na viongozi wa kijiji hicho wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Nkenge katika mkutano wake wa hadhara kijijini hapo.
Akina mama wa kijiji cha Bulembi wakimkabidhi mbunge wao zawadi.
 
EdithaKarlo wa blog ya jamii,Missenyi.

WANANCHI wa kijiji cha Bulembe Kata ya Minziro Wilaya ya Missenyi wamemtaka Mbunge wao kutatua changamoto walizonazo kijijini hapo.

Wananchi hao walimweleza mbunge wao Diodarus Kamala,Mbunge wa jimbo la Nkenge kuwa kijiji chao kina changamoto ya miundombinu ya barabara,shule na zahanati."Sisi huku hatujawahi kuona kiongozi yeyote wa serekali anakuja kututembelea yaani wewe Mbunge ndo kiongozi wa kwanza kufika hapa kijijini kwetu na umejionea mwenyewe changamoto zetu"alisema Beatus John mmoja wa wanakijiji

Alisema changamoto zilizopo kijijini hapo ni barabara kwani huwa wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 16 huku wakipita katikati ya hifadhi ya msitu wa minziro wenye wanyama wakali, kufuata huduma za kijamii kijiji cha jirani."Hapa wanafunzi nao hupata shida ya kutembea umbali mrefu kwebda shule,akitokea mgonjwa akitaka huwa ni shida,tunawabeba na kutembea nao kufuata huduma sababu hapa kijijini hatuna zahanati wala shule"alisema

Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dkt Diodorus Kamala akijibu changamoto za wakazi wa kijiji hicho amewahakikishia kuwa ataendelea kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili wanakijiji hao kwa kushirikiana nao.Kamala aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo wakati akiwa kwenye ziara yake ya kuwatembelea wapiga kura wake jimboni kwake.

Alisema kijiji hicho kina changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara,afya na elimu na atafanya kazi kwa kushiriana na wananchi hao ili kuhakikisha changamoto hizo zinaisha.Alisema watendaji wengi hawafiki kijiji hapo kwaajili ya kutatua kero zao sababu ya miundombinu ya barabara,badala yake wengi wanaishia kijiji cha ng'ambo.

Akionyesha kukerwa na ubabaishaji unaofanywa na baadhi ya watendaji Kamala alisema ataweka daftari la mahudhurio kijijini hapo."Nitaweka daftari la mahudhurio kwa mwenyekiti wa kijiji kila mtendaji wa serekali akifika huku asaini kitabu hicho na baada ya miezi sita nitarudi kuona hali ipoje,wasipofika wajiandae kushughulikiwa hii serekali ya sasa ni kazi tu"alisema

"Pamoja na sura za furaha ninazo wanaona nazo,mtu hawezi kuamini kama mnaishi na hizi changamoto zote hizi kwakweli nawapongeza sana kwa hili"alisema Kamala huku wananchi wakimshangiliaNaye Diwani wa kata ya Minziro Twaha Lubyai alisema watafanya kazi kwa kuenda na kasi ya serekali iliyopo madarakani kwa kutembelea mtaa kwa mtaa ili kujua kero za wananchi na kuziwekea mikakati ya kuzitatua.

Diwani huyo aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wao ili kuleta maendeleo katika kijiji chao.

TAMASHA LA FAMILY DAY YA BENKI CBA TANZANIA LAFANA JIJINI DAR.

$
0
0
  Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CBA Tanzania, Paul Nganga akiongea na wafanyakazi waliofika kuhudhuria Tamasha la Family Day iliyofanyika katika hoteli ya Ndoto Pole Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Benki ya CBA Tanzania, Solomon Kawiche akimtambulisha Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CBA Tanzania, Paul Nganga wakati wa Tamasha la Family Day iliyofanyika katika hoteli ya Ndoto Pole Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CBA Tanzania, Paul Nganga akiwapa zawadi watoto wa wafanyakazi wa CBA Tanzania walishonda katika michezo mbali mbali.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CBA Tanzania, Paul Nganga akiwa na washindi.
Watoto wakigawiwa zawadi.
Wafanyakazi wa Benki ya CBA Tanzania wakishindana katika mchezo wa pete.
Wafanyakazi wa Benki ya CBA Tanzania wakimenyana kukimbia huku wakiwa wamevaa mafunia.
Mshindi wa kukimbia na magunia upande wanawake akiwa amedondoka kwa furaha. 
Ilikuwa ni vuta nikuvute... mpaka team White aliponyakua ushindi.
Nderemo na vifijo vilitawala.
Team White.
Team Red.
Kipa wa team White akiokoa.
Piga nikupige. 
Gooo.... oooooooooo!
Wafanyakazi wa Benki ya CBA Tanzania na watoto wao wakilisakata lumba. 
Team White ikishangilia mara baada ya kuibuka washindi wa michezo mbalimbali katika tamasha la  CBA Tanzania Family Day lililofanyika katika hoteli ya Ndoto Pole Kunduchi Beach, Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Team Red ikishangilia pamoja na watoto wao katika tamasha la CBA Tanzania Family Day lililofanyika katika hoteli ya Ndoto Pole Kunduchi Beach, Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Team Black wakifurahia mara baada ya kumaliza tamasha la CBA Tanzania Family Day lililofanyika katika hoteli ya Ndoto Pole Kunduchi Beach, Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Click here to Reply or Forward 2.02 GB (13%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 27 minutes ago Details Cathbert Kajuna's profile photo Cathbert Kajuna Show details

MRADI WA AIRTEL NA VETA UJULIKANAO KAMA VSOMO WAENDELEA KUELIMISHA WATANZANIA MTAANI.

$
0
0
 Mabalozi wa Airtel kupitia mradi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, wakitoa elimu ya mafunzo hayo kwa wananchi jijini Dar Es Salaam.
 Abu Ally,Balozi wa Airtel kupitia mradi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, akitoa elimu ya mafunzo hayo kwa wananchi jijini Dar Es Salaam.
  Fatuma Abdallah ,Balozi wa Airtel kupitia mradi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, akitoa elimu ya mafunzo hayo kwa wananchi jijini Dar Es Salaam. 

Mnada wa Tanzanite kufanyika Arusha wiki hii.

$
0
0

Mhandisi Juma Lunda( kulia) akimuelekeza mmoja wa wanunuzi wa madini ya Tanzanite kujaza fomu za kushiriki zabuni ya kununua madini hayo.
Vifaa vinavyotumika kuhifadhi Madini ya Tanzanite.
Sehemu inayotumiwa na wauzaji pamoja na wanunuzi kujiridhisha kwa kupima thamani ya madini ya Tanzanite kabla ya kufikia muafaka wa bei.
Mkurugenzi wa Uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo( wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite wakati wa zoezi la kumpata mshindi wa zabuni ya kununua madini ya Tanzanite.
Mnunuzi wa madini ya Tanzanite Macmillan Njau( kulia) akijiridhisha kwa kupima thamani ya madini hayo kabla ya kununua, Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Franone Mining & Gem Company, Onesmo Mbise(katikati) ambaye ni muuzaji wa madini ya Tanzanite na Elia Benyamin( kushoto) Mnunuzi wa Madini.
Mthaminishaji Madini ya Almasi wa Serikali Edward Rweyemamu (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau wa Madini ya Tanzanite( kushoto), Sekretari wa kituo cha Jimolojia ( TGC)Halima Hussein( wapili kulia) na Zainab Napacho(kulia)kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania( TMAA)


Na Zuena Msuya, Arusha

Wizara ya Nishati na Madini inafanya mnada wa madini ya Tanzanite kwa mara ya kwanza yaliochimbwa kutoka migodi ya kampuni tano za wafanyabiasha wa madini hayo katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiko Mkoani Manyara.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo wakati wa mchakato wa kupata wafanyabiashara watakaoshinda zabuni ya kununua madini hayo kutoka Mataifa mbalimbali Duniani wakiwemo watanzania.

Kalugendo alisema utaratibu wa kufanya mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei halisi inayoendana na soko la dunia.

Aidha mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki ili kuchangia pato la taifa; vilevile kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji , wanunuzi pamoja na mali zao. Akizungumzia mnada huo, Kalugendo alisema zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha wachimbaji, wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa( STAMICO) pamoja Wizara ya Nishati na Madini, kwa lengo la kusimamia haki ya kila mhusika wa madini hayo.

" Madini ya Tanzanite yanathamani ya fedha nyingi sana,kwa usalama wa wanunuzi na wauzaji, Serikali imeimarisha ulinzi wakati wa zoezi hilo ili kujihadhari na watu wasio waaminifu," alisema Kalugendo. Alifafanua kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utaratibu huo ili uweze kuleta tija zaidi kwa Watanzania.

Utaratibu huo ni wa kaiwaida kwa nchi zenye madini ya namna hii kama vile Zambia( emerald),Zimbabwe( Almasi) pamoja na Afrika kusini( almasi). Washindi wa zabuni za ununuzi wa madini ya Tanzanite wanatarajiwa kutangazwa Agosti 12 mwaka mkoani Arusha.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JULAI, 2016 WAPUNGUA KWA ASILIMIA 5.1

$
0
0

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwekisigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa za mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016. Kushoto ni Kaimu Meneja, Idara ya Takwimu ya Ajira na Bei, Ruth Minja
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2016 umepungua hadi asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwekisigabo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016.

"Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2016" alisema Kwesigwabo.

Kwesigabo alisema kuwa Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.50 Mwezi Julai, 2016 kutoka 98.48 mwezi Julai 2015 na kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Julai 2016 umepungua hadi asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.1 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016.

Kwesigabo aliongeza kuwa kupungua kwa mfumuko huo wa bei wa mwezi Julai 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Julai, 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Julai 2015.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za samaki kwa asilimia 6.6, mafuta ya kupikia kwa asilimia 4.9 na maharage kwa asilimia 1.9.

Aliongeza kuwa kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa ziliso za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa kwa asilimia 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3

Alisema pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 kuna baadhi ya bidhaa zilionesha kuongezeka katika kipindi hicho zikiwa ni pamoja na bei za mchele kwa asilimia 4.7, mahindi kwa asilimia 31.6, unga wa mahindi kwa asilimia 24.1, vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 15.6 na mkaa kwa asilimia 16.0.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA SOKO LA MWANJELWA MKOANI MBEA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya Agost9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili wenye soko kuu la kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya kulikagua
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 9, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 9, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kutembelea soko jipya la kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya, Agosti 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na viongozi wa serikali kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya kurejea Dar es salaam Agosti 9, 2016. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe na wapili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Stephene.

UTEUZI WA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO

MASHINDANO EAC YAANZA KIGALI, TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TATU RIADHA

$
0
0

Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda Picha na (Selemani Sem unyu).
Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James kabarebe (wa pili Kulia) akifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali nchini Rwanda (Picha na Selemani Semunyu).
Wanamichezo wa Tanzania Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Wanarianda walioshiriki mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki wakichuana wakati wa Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo Tanzania imeshika nafasi ya Tatu
Baadhi ya Askari wa JWTZ wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Wanariadh walioshiriki mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki wakichuana wakati wa Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo Tanzania imeshika nafasi ya Tatu

Na Seleamani Semunyu JWTZ.

Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yameingia Siku yake ya kwanza baada ya kuzinduliwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu katika Riadha kwa wanawake katika mbio zilizokuwa na Ushindani Mkali na kufanyika katika Uwanja wa APRC Kicukiro. .

Mtanzania Catherine Lange aliiwezesha Timu ya JWTZ kuibuka na Ushindi wa tatu huku kwa Wanaume Mwanariadha Fabiano Nelson kufanya vyema licha kukosa ushindi wa jumla kutokana na kuwa peke yake mbele nyuma ya wakenya waliochukua ushindi wa Kwanza.

Awali akifungua mashindano hayo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James Kabarebe amewapongeza Wakuu wa Majeshi Kutoka Nchi za Afrika Mashariki kwa kuendeleza michezo na kutoa nafasi kwa nchi zo kushiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yamekuwa kiungo katika kuimarisha Ushirikiano.

Aliyasema hayo leo wakati akizindua wa michezo hiyo katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Majeshi kutoka majeshi ya Nchi Nne zinazoshiriki Michuano hiyo.

“ Michezo ni Sehemu ya Majukumu ya Jeshi Lakini nawapongeza na kuyapa uzito mashindano haya kwani yamekuwa yakitusaidia katika kuimarisha ushirikiano wa Nchi hizo ili kuhakikishia inaendelea kuwa sehemu salama.

Waziri Jenerali Kabarege alitoa Wito kwa Wakuu hao kutumia nafasi ya Michezo hii kufanyia kazi changamoto kama zipo zinazokabili majeshi katika ukanda huu.

Awali Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba aliwahahakikishia Wanamichezo maandalizi Mazuri na kuwataka kuwa huru na kuchanganyika na Wanyarwanda ambao alidai wameajiandaa kuwapokea.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambaye ni Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro amesema anamatumaini makubwa kwa Timu za Tanzania kurejea na vikombe.

WAZIRI NAPE AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO YA BARA LA AFRIKA.

$
0
0


Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katikati waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (Kushoto) akijadiliana jambo na Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katika) akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Bw.Lv Youqing.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la Afrika na China.
Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadali masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la Afrika na China
Mshauri wa mambo ya Mawasiliano kutoka Tume ya Umoja wa Afrika Bibi. Doreen Apollos akisema hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) wakati wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (wa kwanza kulia) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(wa pili kulia) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye(hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(kulia) wakionyesha hundi ya shilingi milioni arobaini na tano zilizotolewa na watu wa China kwa ajili ya kuchangia madawati katika shule za msingi za Dar es Salaam.
Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.

Kennedy Uzoka Assumes Office as UBA GMD/CEO

$
0
0
Kennedy Uzoka has assumed as the Group Managing Director and CEO of pan-African banking group, United Bank for Africa (UBA) Plc. This follows the retirement of Phillips Oduoza as Group Managing Director and CEO of UBA Plc on July 31, 2016 after completing two terms of three years each.

Uzoka, the new GMD/CEO of UBA Plc, was until his appointment, the Deputy Managing Director, a position he has held in the last six years, working closely with the former GMD/CEO. His appointment as the new GMD is seen as a testimony to the strength of the bank’s succession planning process.

“Kennedy Uzoka’s is not only very hard working, but he is also a man of impeccable integrity. He is passionate and committed to UBA. The board is confident that he will take the bank to the next level” said Tony Elumelu, Chairman, UBA Plc.

Kennedy Uzoka comes well prepared for his new position. He has been leading the transformation agenda of the Bank, after returning from completing the Advanced Management Programme of Harvard Business School.

Uzoka has over two and a half decades of experience in commercial banking, strategy and business transformation. Prior to his sabbatical at Harvard, Uzoka served as Deputy Managing Director, UBA Group and was also the CEO of UBA Africa, responsible for the Group’s operations in 18 countries across Africa as well as business in New York and London.

“Uzoka brings an extremely strong skill set and a breadth of financial services experience that will help the bank execute the next phase of its growth strategy.” said Elumelu.

Speaking to staff in a video podcast after resuming on August 1, the new GMD/CEO, Uzoka who described UBA as a strong, recognizable and trusted brand across Africa, promised to build a bank based on a strong foundation of customer service.

“We will stay close to our customers and do everything possible to serve them properly. Our customers will be the beginning, the middle and the end of our strategy" he stated.United Bank for Africa (UBA) Plc, is one of Africa's leading banking Groups with operations in 19 African countries and offices in three global financial centers: London, Paris and New York.

It is a publicly quoted company listed on the Nigerian Stock Exchange (NSE) and has a well diversified shareholder base. For more information visit www.ubagroup.com

WASHINDI WA UWEKAJI WA AKIBA WA FNB WATANGAZWA LEO JIJINI DAR.

$
0
0
 Meneja Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachang’a akiwapigia simu washindi wa droo ya kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi ambapo washindi kumi walijipatia shilingi milioni moja kila mtu. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Sheria wa benki hiyo, David Sarakikya (kushoto), Mtaalamu wa Mfumo wa Habari na Mawasiliano wa FNB, Bi. Ilakiza Hezwa na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed (kulia).

Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed (kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha wateja wa rejareja wa First National Bank, Francois Botha (kushoto) kwa niaba ya washindi kumi wa kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es salaam leo. 
(Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog). 

 First National Bank Tanzania imetangaza washindi wa droo ya pili ya kampeni yake ya kuhamasisha uwekaji akiba. Kupitia droo iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam leo jumla ya washindi kumi wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja kupitia mpango huo wa kuwahamasisha Watanzania kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba benki.

 Akiongea jijini Dar es salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha wateja wa rejareja wa FNB Tanzania, Francois Botha alisema mbali na kuhamasisha uwekaji akiba, kampeni hiyo inalenga kuhimiza wananchi wote nchini ambao hawajafungua akaunti benki kujitokeza na kuweka akiba. Kupitia droo hiyo ya pili, shilingi milioni kumi imetolewa kwa jumla ya washindi kumi ambao ni Gabriel Mrosso wa Mwanza, Agnes Mndasha wa Dar es salaam, Ebenezer Moshi wa Mwanza, Amiri Mziray wa Dar es salaam, Nelis Kashanga wa Mwanza, Festo Msofe wa Dar es salaam, Daniel Kakesyo wa Mwanza, Boniface Likingo wa Dar es salaam, Michael Lusana wa Mwanza, Benedicto Makoye wa Dar es salaam.

 Botha aliwapongeza washindi hao na kuongeza kwamba benki hiyo inaendelea kufanya jitihada kubwa kuboresha huduma na kuongeza kwamba kampeni hii ni sehemu ya jitihada hizo zilizolenga pia kuongeza idadi ya watumiaji huduma za kibenki nchini. Kupitia kampeni hiyo inayofanyika kwa muda wa miezi mitatu, wateja wa FNB waliopo na wateja wapya wanaingizwa kwenye droo moja kwa moja kutokana na kila shilingi elfu hamsini wanayoweka akiba katika benki hiyo. 

Jumla ya washindi 30 watanufaika kupitia kampeni katika muda wa miezi mitatu. Click here to Reply or Forward 2.02 GB (13%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 21 minutes ago Details Cathbert Kajuna's profile photo Cathbert Kajuna Show details

TASAF YA ILALA YATOA MILIONI 292 KWA KAYA MASKINI

$
0
0

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga- Darajani, Kata ya Kimanga Manispaa ya Ilala, Chacha Mwenge akiendelea na zoezi la kuhakiki majina ya wanufaika wa mpango wa TASAF katika mtaa wake leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
 
Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mwaluma Msofe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wakunusuru kaya masikini muda mfupi kabla ya zoezi la ugawaji wa fedha hizo kuanza katika mitaa 74 ya Manispaa hiyo leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kimanga- Darajani, Kata ya Kimanga Manispaa ya Ilala wakisubiri zoezi la ugawaji wa fedha kwa kaya masikini kuanza leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wakunusuru kaya masikini, Ayubu Kabeta akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha za kujikimu leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

Mpango wa kunusuru Kaya masikini (TASAF) wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala umetoa jumla ya shilingi milioni 292 kwa ajili ya kusaidia kaya masikini 6115 za wilaya hiyo.

Fedha hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Saalam na Mratibu wa TASAF wa Halmashauri hiyo, Mwaluma Msofe ambaye amesema kuwa fedha hizo zitagawanywa kwenye mitaa 74 ya Halmashauri hiyo kwa kuwa ndiyo walengwa wa mpango huo.

Msofe ameongeza kuwa mchakato wa kuwapata wananchi wenye maisha magumu unafanywa na wananchi wenyewe katika mtaa husika ambapo baada ya kuwatambua  wanathibitishwa mbele ya mkutano wa mtaa.

“Fedha tunazowapatia wananchi hawa zimeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwa zimesaidia kaya hizo kuanzisha miradi midogo midogo inayowawezesha kuendeleza maisha yao pia fedha hizo zimesaidia watoto kupata mahitaji muhimu ya shule hivyo kupelekea mahudhurio kuongezeka”, alisema Msofe

Mratibu huyo amefafanua kuwa kuna aina mbili za ruzuku ambazo ni ruzuku ya msingi ambayo kaya masikini hupewa kwa mtu yeyote anayetambuliwa na mpango huo wakati ruzuku ya masharti hutegemea na aina ya familia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga- Darajani, Chacha Mwenge amesema kuwa anaendelea na kazi ya kusimamia na kuchambua majina ya wahusika kwa kuwa kuna baadhi ya wananchi waliingizwa katika mpango huo bila kuwa na sifa kutokana na wananchi hao kutoa taarifa za uongo wakati wa utambuzi.

“Tumegundua kuwa kuna baadhi ya kaya ambazo  zimeingia kwenye mpango huu kimakosa kwahiyo tunaen
delea kuzitoa, hadi sasa jumla ya kaya 28 za mtaa wetu tumeshaziondoa kwa sababu ya kukosa sifa”, alisema Mwenge.

Naye mmoja wa wananchi wanaonufaika na mpango huo, Ayubu Kabeta ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha za kujikimu pia ameiomba kuongeza kiwango cha fedha hizo kwa kuwa kiasi ni kidogo bado hakikidhi huduma muhimu.

CHAMA CHA KUOGELEA KINAHITAJI MILIONI 71 KWA AJILI YA MASHINDANO YA DUNIA DESEMBA NCHINI CANADA

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea nchini, Ramadhan Namkoveka akizungumzia maandalizi ya timu ya Taifa mbayo itashiriki mashindano ya Dunia yaliyopngwa kufanyika nchini Canada Mwezi Desemba.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Kuogelea, Magdalena Moshi (wa tatu kutok kushoto) na Hilal Hilal (Wa pili kutok kulia) wakiwa na kocha wao, Alex Mwaipasi (wa pil kushoto) wakiwa na wanamichezo wengine wa Tanzani mjini Rio De Janeiro, Brazil kwa ajili ya michezo ya Olimpiki. Wachezaji hao wawili ni miongoni mwa waogeleaji 11 watakao iwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia mwezi Desemba nchini Canada.
Bingwa wa Taifa wa mchezo wa kuogelea nchini, Sonia Tumiotto akiwa katika mashindano ya Taifa kwenye bwawa la Hopac.


Waogeleaji katika staili ya 'kuchupa' au Diving


Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA), kinahitaji dola za Kimarekani 32,500 (Sh 71 milioni) kwa ajili ya kuipeleka waogeleaji nane (8) wa timu ya Taifa kwenye mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Windsor, nchini Canada.

Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka alisema kuwa timu ya Taifa ya Tanzania inakuwa na jumla wachezaji 11 ambapo kati ya hao, wachezaji watatu watalipiwa na Shirikisho la Mchezo wa kuogelea duniani (Fina).

Namkoveka alisema kuwa kila muogeleaji anatakiwa kulipiwa ni dola za Kimarekani 4,100 (Sh 8.2 million). Alisema kuwa TSA kwa sasa haina fedha za kuweza kuwapeleka wachezaji wote hao kwa ajili ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa Namkoveka, gharama kubwa kuipeleka timu na kuwaomba wadau wa mchezo huo kuwasaidia ili kuweza kufanikisha lengo lao ka kuipeleka timu hiyo katika mashindano hayo.

“Tunahitaji kupeleka waogeleaji wengi zaidi katika mashindano haya ambayo ni makubwa duniani, mchezo wetu unakuwa kwa kasi na tunahitaji kupata waogeleaji wenye uzoefu katika mashindano ya kimataifa,” alisema Namkoveka.

Alisema kuwa TSA kimeunda kamati ya watu… kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo inakwenda kwenye mashindano hayo.

Alisema kamati hiyo unaundwa na Mkurugenzi wa Fedha wa TSA, Phillip Saliboko, Asma Hilal, Amina Mfaume (Mkurugenzi wa Ufundi wa TSA), Inviolata Itatiro (Katibu Mkuu wa klabu ya Dar Swim Club), Geetha Prashant , Hamisi Mhini na Katibu Mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Swim Club (DSC), Inviolata Itatiro.

Wachezaji waliochaguliwa kuunga timu hiyo ya Taifa ni Hilal Hilal, Aliasghar Karimjee, Ammaar Ghadiyali, Denis Mhini, Adil Bharmal, Joseph Sumari ambao watashiriki kwa upande wa wanaume na kwa upande wa wanawake ni Catherine Mason, Sylvia Caroiao, Sonia Tumiotto, Mariam Foum na Magdalena Moshi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA AFANYA UKAGUZI KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KATAVI

$
0
0
 
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Mh.Mwigulu Nchemba leo amewasili mkoani Katavi,na kufanya ukaguzi kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea kwa  majirani zetu Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.
 
Katika ukaguzi huo Mh.Mwigulu amesema kuwa zoezi la uhakiki linafanyika ili kuchunguza mienendo yao na uwepo wao kwenye eneo la Kambi,amesema kuwa kumekuwepo na taarifa za baadhi ya ndugu zetu ambao wamekuwa wakijihusisha na watu waovu,kufanya vitendo vya kibaguzi na kutoka nje ya kambi zao na kwenda nchi jirani bila kibali.

Mh.Mwigulu amesema kuwa mbali ya kambi ya Katumba,pia ametembelea kambi ya Mishamo na kuviagiza vyombo vya usalama na kupitia Seririkali za mitaa kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo,amaesema na kuongeza kuwa Tanzania haina tabia za kibaguzi"moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru" ,alisema Mh.Mwigulu.

"Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi,kuishi na kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na vya kibaguzi.Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani ya nchi yetu",alisema Mh.Mwigulu.

Mwigulu alibainisha pia kuwa amekutana na Askari wa jeshi la polisi na idara zake zote na pia ametembelea gereza la mpanda ikiwa ni ziara ya kupata uhalisia wa changamoto zinazokabili jeshi la polisi,Magereza,Uhamiaji na zimamoto kwa kila mkoa,ambapo tayari kwa majawabu ya kudumu.














Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images