Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 930 | 931 | (Page 932) | 933 | 934 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Mbeya baada ya kupokea taarifa ya mkoa Agosti 7, 2016 kwenye  Ikulu ndogo ya mbeya .  Agosti 8, 2016 atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wakulima Nanenane. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu).

  *Awataka wafanyabiashara kuwaripoti watendaji wanaoongeza kiwango kikubwa cha kodi kuliko inavyostahili kulipwa

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuimarisha kitengo cha tathmini ili kuweka viwango halali ambavyo havitawagandamiza wafanyabiashara na uwepo uwazi kuhusu viwango stahili vya kodi wanavyotakiwa kulipa.

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 07, 2016) wakati alipozungumza na viongozi wa mikoa ya Mbeya, Katavi, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa na Njombe mara baada ya kuwasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya maonyesho ya nane nane kwa mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika mkoani Mbeya.

  ‘‘TRA waendelee kukusanya mapato vizuri ila kuna wakusanya kodi wanaotaka kuharibu mkakati wa Serikali kwa kufanya mambo ya hovyo kwa kuwaongezea viwango vikubwa vya kodi kuliko kodi stahili wanavyotakiwa kulipa na kufanya suala hili liwe kama tatizo au adhabu kwao jambo ambalo si sahihi. Naagiza watendaji wa TRA wanaofanya hivyo wasakwe na wachukuliwe hatua“, alisema.

  ‘‘Wafanyabiashara mnaoonewa kwa chuki binafsi na watendaji wa TRA toeni taarifa ili muweze kufanya biashara zenu kwa uhakika bila ya wasiwasi lengo ni kuwafanya muweze kulipa kodi sahihi kwa mujibu wa sheria“, alisema.

  Ili kufanikisha mpango huo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuwasikiliza wafanyabiashara ambao wana malalamiko ya kweli ya kutotendewa haki katika kutozwa kodi kwa sababu mchango kupitia kodi ni kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa Taifa.

  Katika hatua nyingine ameitaka idara ya Uhamiaji ijikite katika kudhibiti watumishi wasiokuwa waaminifu ambao wamekuwa wakichukua rushwa kutoka kwa wageni wanaotoka nje ya nchi na kuwaingiza nchini bila ya kuwa na vibali maalumu.

  ‘‘Ni lazima tuhakikishe hakuna uingiaji holela ndani ya nchi na hasa kwa wanaoingia bila vibali maalumu kwani bila ya kudhibiti suala hilo tunaacha mianya ya kuingia watu wasiokuwa na nia njema na Taifa letu. Watu watakaobainika wameingia nchini bila ya vibali wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria,“ alisema.

  Alisema kitendo cha mipaka kushindwa kudhibitiwa na kuruhusu uingiaji holela wa watu wasiokuwa na vibali chini kunasababisha Serikali kushindwa kuteleza ipasavyo mipango yake ya kuwahudumia wananchi kulingana na idadi halisi.

  Mbali na kuiagiza Idara ya Uhamiaji pia Waziri Mkuu alisema wakuu wa mikoa ya mipakani wana jukumu la ziada la kuhakikisha wanadhibiti mipaka yote na kuhakikisha hakuna watu wanaoingia nchini bila ya kuwa na vibali.

  Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wakuu wa mikoa kote nchini kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yao na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu ili Watanzania waweze kutekeleza shughuli zao za maendeleo kama walivyojipangia.

  “Natambua kuwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama katika maeneo yenu, endeleeni kuimarisha hali ya ulinzi na usalama. Nchi hii tunahitaji iwe tulivu na salama na ni wajibu wenu kuhakikisha kwamba lolote linalotokea mnalikabili vilivyo“, alisema.

  Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Makalla alipokuwa akisoma taarifa ya mkoa huo kwa Waziri Mkuu alisema mkoa huo una jumla ya viwanda 1,653 kati yake vikubwa ni tisa, vya kati 19 na vidogo 1,625 na bado wanaendelea kuzisimamia halmashauri kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya kuongeza na kupanua viwanda.

  Mhe. Makalla alisema katika eneo hilo la viwanda mkoa una kiwanda kimoja cha kusindika nyama cha Tanganyika Pachers kilichopo wilayani Mbeya ambacho hakijawahi kufanya kazi tangu kilipojengwa na kufungwa mitambo mwaka 1975.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema usimamizi wa kiwanda hicho uko chini ya Masajili wa Hazina na kwamba tayari kuna muwekezaji amepatikana kwa ajili ya kukiendesha hivyo ameiomba Serikali kuharakisha taratibu za mikataba ili kiweze kuanza kufanya kazi.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATATU, AGOSTI 08, 2016.

  0 0  Wananchi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Yefred Myenzi akizungumza nao.Diwani wa kata ya Endiamtu Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Philemon Oyogo akizungumza na wananchi wa kata hiyo, baada ya viongozi wa wilaya hiyo kuwatembelea.

  Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imejipanga kuanzisha mnada wa madini ya vito ya Tanzanite katika eneo maalumu la kibiashara ili kusaidia kuongeza pato la ushuru wa huduma kwa jamii.

  Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Yefred Myenzi, akizungumza na wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani, alisema uimarishaji wa ukusanyaji wa mapato ni moja ya maagizo ya kitaifa ya kusogeza huduma karibu na jamii. Myenzi alisema msukumo wa mbunge wa jimbo hilo James Ole Millya unahitajika kubadili sheria ili ushuru wa huduma uongezeke kutokana na kukosekana kwa mfumo madhubuti wa kuwabana walipa kodi wakubwa kama wa migodi ya madini.

  Alisema inasikitisha kuona utajiri mkubwa wa rasilimali zilizopo Simanjiro hauakisi maisha ya wakazi wake, wala miundombinu yake na huduma za kijamii kama elimu, afya, maji umeme na huduma za kifedha na mawasiliano.“Simanjiro ina jina kubwa nchini na duniani kutokana na madini ya vito aina ya Tanzanite yanayopatika eneo la Mirerani pekee duniani na mtu ana matarajio ya kushuhudia maendeleo yanayoshabihiana na utajiri huo,” alisema Myenzi.

  Alisema wigo wa eneo la kijiografia haliwiani na idadi ya wataalamu wa halmashauri kukusanya mapato pale wanapotakiwa na ukwepaji kodi unaohusisha ukosefu wa uadilifu wa watumishi, wafanyabiashara na wananchi.“Naamini Simanjiro ya leo siyo ya jana na sivyo itakavyokuwa kesho, wenzetu waliotangualia walifanya walichoweza kwa nafasi yao nasi tumepewa fursa hii tuitumie kuandika historia na tuache urathi usiofutika,” alisema Myenzi.

  Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jackson Sipitieck alisema wanamatarajio makubwa na mkurugenzi huyo mgeni na watahakikisha wanampa ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya maslahi ya jamii.

  Mbunge wa jimbo hilo Ole Millya alisema kutokana na elimu ya shahada mbili alizonazo Myenzi anatarajia jamii ya Simanjiro kwa namna moja au nyingine watanufaika naye kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, afya, na maji.

  0 0

  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga (wa pili kushoto), akizungumza na wamiliki wa shule za udereva (hawapo pichani), wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta), Hoteli ya Dreamers Buguruni Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla na Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati
  Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla (katikati), akimkabidhi risala yao Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni. 
  Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati (kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.
  Mjumbe wa chama hicho, Cosmas Munuo (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
  Mjumbe wa chama hicho, Regina Sulle akiuliza swali kwenye mkutano huo. Kushoto ni mjumbe Fatma Somji na kulia ni Santos Akyo.
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga (kushoto), akisisita jambo wakati akijibu maswali ya wanachama wa chama hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla.
  Mjumbe wa mkutano huo, Leonard Mtandika akiuliza swali. Kutoka kulia ni Pascol Mtandika na Ibrahim Nyato.
  Mjumbe wa Mkutano huo kutoka mkoani Dodoma, Robert Mwinje (kulia), akichangia jambo kwenye mkutano huo.. Kushoto ni mjumbe mwenzake,kutoka mkoani Mwanza, Mussa Ramadhan.


  Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni (kulia), akifafanua baadhi ya vifungu vya sheria katika mkutano huo.
  Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

  Mgeni rasmi, DCP Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo ambao ni wanachama wa Chashubuta.
  Hapa DCP Mpinga akiagana na wajumbe hao baada ya kufungua mkutano huo.

  Na Dotto Mwaibale

  JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na sifa.

  Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es Salaam leo.

  "Kuanzia sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali na hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema Mpinga.

  Mpinga alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E 2002) mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo zitategemewa kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na kuwa chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa na madereva.

  Alisema jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havisa sifa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

  Mwenyekiti wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya Mpinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya changamoto waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na usafirishaji kutoona mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya serikali pekee.

  Mkolla alimuomba Kamanda Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili kwenda na mahitaji ya barabara, vyombo na wakati na shule hizo ziwe zinashirikishwa katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala hiyo.

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band yenye makao yake kule Ujerumani,wanatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival litakalo fanyika jumamosi hii 13 August 2016 katika viwanja vya Rebstock Park,jijini Frankfurt,Ujerumani ambapo wapenzi wa muziki watapata burani ya aina yake kutoka kwa bendi hiyo iliyofanikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani,kikosi cha Ngoma Africa band kinachoongozwa na mkuu wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kinadumu katika gemu la muziki kwa takribani miaka 23 sasa na kuwekwa katika rekodi ya kimataifa kuwa ndio bendi ya kiafrika inayodumu kwa muda mrefu barani ulaya.

  usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com
  wape Hi at www.facebook.com/ngomaafricaband
   
  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia kwake) wakikagua vipando vya kabeji wakati walipotembelea banda la Magereza kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti8, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama jiko banifu linalotumia gesi ya pumba wakati alipotembelea banda la Magereza kwenye maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. (Picha na Ofiasi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananachi wakati lipotembelea maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia picha yake iliyochorwa na kutolewa kwake na Chama cha Wandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania mkoani Mbeya (TAJATI) katika kilele cha sherehe za Maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwaja wa wa John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8, 2016. Watatu kulia kwake ni mkewe Mary na wapili kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
  Baadhi ya viongozi waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016.
  Baadhi ya viongozi waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016.
  Baadhi ya viongozi waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua vipando vya alizeti katika eneo la banda la Chuo cha Kilimo cha Uyole kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha karoti zilizostawi vizuri wkati alipotembelea banda la Mapanda Mkoani Katavi katika maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vitunguu vilivyopandwa kwenye gunia namna ya kilimo ambacho ni muafaka kwa watu waishio mijini hasa magorofani. Alikuwa akitembela maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa Maonyesho wa John Mwakangale wa jijini Mbeya
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipata maelezo kuhusu jiko banifu kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Nkansi, Saidi Mtanda (kushoto) kuhusu jiko banifu lililobuniwa na kutengenezwa na Samuel Msigale (watatu kulia) ambaye ni mjasiliamali kutoka Nkansi mkoani Rukwa. Alikuwa kitembelea maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa maonyesho ya wakulima Nanenane wa John Mwakangale Agosti 8, 2016.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na askari magereza wa mkoa wa Mbeya baada ya kutembelea banda lao kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Mbeya Julius Sang’unda
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kujitolea kutoka Uingereza ambao Agosti 8, 2016 walitembelea maonyesho ya wakulima Nannane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya. (Picha na Ofisi ya wairi Mkuu)  0 0

  Waziri wa Fedha Dr.Philip Mpango (Kushoto) akisalimiana na Bw. Simon Migangala Kaimu Mkurugenzi mkuu UTT AMIS wakati alipotembelea banda la wizara ya fedha katika viwanja vya NaneNane Ngongo mkoani Lindi.


  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akipata maelezo ya kina kuhusiana na mifuko ya uwekezajiwa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS.Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga akitoa Maelezo hayo.
  Bi. Surah Twaakyondo, Afisa kutoka UTT-AMIS akitoa maelezo ya jinsi ya kuwekeza kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wananchi waliotembelea banda wakati wa maonyesho ya NaneNane yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi.
  Bi Ashura Kassim wa UTT AMIS akiwasaidia wananchi wa mkoa wa Arusha kujiunga katika uwekezaji wa pamoja
  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya uwekezaji ya UTT AMIS ndugu Daudi Mbaga akitoa elimu kwa wananchi kwenye viwanja vya Nane Nane Arusha.
  Ni furaha iliyoje kuwekeza na UTT AMIS ..mteja Nane Nane Arusha baada ya kujiunga na UTT AMIS

  UTT AMIS ni kampuni inayoendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. Mpaka sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 253.

  Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.

  Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Wawekezaji wote wananufaika kwa kupata faida shindani hivyo kuweza kukuza mitaji yao, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu mkubwa wa gharama na uwazi ni vichocheo vinavyofanya UTT AMIS kuwa kimbilio lao.

  UTT AMIS - Mshirika hakika katika uwekezaji.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisalimiana na Mkuu wa Wiliya Mjini Bi. Marina Joel Thomas (katikati) aliekuwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
  Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” (kulia) Silima Haji Haji akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud katika sherehe ya kumpongeza kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa.
  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akizunguza na wafanyakazi wa Wilaya ya Magharibi “B” na walikwa katika sherehe ya kumpongeza na kuwaaga wafanyakazi waliostaafu iliyofanyika viwanja vya Skuli ya Urafiki Wilaya ya Magharibi “B”.
  Aliekuwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.​
  Sehemu ya walikwa katika sherehe ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa Mjini Ayoub Mohammed Mahmoud na kuwaaga wafanyakazi waliostaafu.
  Sehemu ya walikwa katika sherehe ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa Mjini Ayoub Mohammed Mahmoud na kuwaaga wafanyakazi waliostaafu.
  Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” (kulia) Silima Haji Haji akiwakaribisha walikwa kwenye sherehe ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa Mjini na kuwaaga wafanyakazi waliostaafu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.

  Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya NANE NANE kitaifa katika uwanja wa NGONGO Manispaa ya LINDI mkoani LINDI kwa naiba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI. 

  Katika hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya NGONGO, Makamu wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia iwapo tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii, kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

  “Napenda kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini au itikadi za vyama vyenu.”

  Kuhusu uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema maadhimisho ya sikukuu ya NANE NANE ni moja katika ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi kote nchini.

  Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla. 

  Makamu wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.

  Aidha amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.

  Kwa Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dakta PHILIP MPANGO amehimiza wananchi kote nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami huku Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi katika hatua ya kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais 
  8-Aug-16

  0 0


  Mhe Mavunde alipotembelea banda la ushonaji la Jeshi la kujenga Taifa JKT katika Maonesho ya Nane nane kabla ya kuyafunga rasmi
  006 Mhe Mavunde alipotembelea banda la maonesho ya wanyama aina ya mbuzi, Ng’ombe na Kondoo la kampuni ya Ranchi za taifa (NARCO LTD)
  Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akipokea zawadi ya mboga za majani kutoka kwa vijana wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kutembelea banda hilo
  Mhe Mavunde alipotembelea banda la Maonesho ya kilimo cha Vitunguu
  Mhe Mavunde akisalimiana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma marabaada ya kutembelea banda la maonesho la Wilaya hiyo .
  Mhe Mavunde akitazama ubora wa matrekta yaliyofikishwa katika Maonesho ya wakulima ya Nanen nane .

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Maonesho ya wakulima Nane nane kwa ajili ya kufunga maonesho hayo
  Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini maelekezo ya namna ya kuchakata mihogo kutoka kwa mkulima wa zao hilo tangu mwaka 1980 kutoka Kijiji cha Nzuguni Josiah Malogo Ndoya
  Mhe Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini namna ya kulima mahindi kwa mbinu bora na za kisasa ili kuwa na mavuno yenye tija.
  Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza maelekezo katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuhusu umuhimu wa matumizi ya dawa katika kilimo cha kisasa 

  Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki katika maonesho ya Nane nane katika uwanja wa Nzuguni Kanda ya kati Dodoma .
   
   
  Na Mathias Canal, Dodoma

  Maonesho na Mashindano ya mifugo Kitaifa sanjari na Maonesho ya Kilimo yametoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde wakati akifunga maonesho ya wakulima Nane nane Kanda ya Kati Dodoma yaliyokuwa yanafanyika katika uwanja wa Nzuguni kwa kauli mbiu ya "Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya Maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).

  Amesema kwa kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli inatekeleza azma ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma ameishauri Wizara ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi na ile ya Biashara na masoko kuangalia uwezekano wa kuanzisha rasmi maonesho ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ya Kimataifa (International Agriculture Trade Fair) katika uwanja wa Nzuguni ambao ndio uwanja wenye eneo kubwa kwa maonesho ya Kilimo hapa nchini.

  Aidha ametoa wito kwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo kuendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.

  "Naomba niwaambie wakulima na wafugaji wetu kuwa maonesho ninayoyafunga hii leo ni muafaka na fursa nzuri kwao hususani vijana kwenda kuanza mara moja kutumia mlichojifunza na kuleta mapinduzi yenye maendeleo chanya yanayotarajiwa kiuchumi, hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuzikumbusha Halmashauri za serikali za mitaa zote kuwahamasisha wakulima, Wafugaji na wadau wengine kutumia teknolojia zilizooneshwa hapa kuongeza ufanisi wao katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi” Alisema Mavunde

  Naibu waziri huyo pia ametoa zawadi kwa washindi katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma na Singida, Wizara za serikali, Taasisi za uzalishaji wa serikali, Makampuni ya pembejeo za Kilimo na Mifugo, Makampuni ya zana za Kilimo na Mifugo, Taasisi za serikali na Mashirika ya Umma, Taasisi za fedha na Mabenki, Taaisisi za mafunzo na utafiti, Taaisisi zisizo za kiserikali (NGOs na CBOs), Taasisi za mawasiliano ya kibiashara, Mamlaka za udhibiti, Vyombo vya habari, na Kampuni za nishati mbadala kwa kufanya vizuri katika maonesho hayo.

  Pia zawadi hizo zimetolewa pia kwa watu wenye mashamba makubwa ya ufugaji ng'ombe wa maziwa, Wafugaji wadogo wa ng'ombe wa nyama, Wafugaji bora, na Wakulima bora.

  Sambamba na hao pia Jeshi la Kujenga Taifa JKT limeibuka kidedea kwa ushindi wa jumla likifuatiwa na Jeshi la Magereza ambapo nafasi ya tatu imechukuliwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvu.

  Akitoa maelezo ya awali kuhusu maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa Malengo ya maonesho hayo ni utoaji elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi.

  Mtaturu alisema kuwa mpaka tarehe 7 hapo jana jumla ya watu waliokuwa wametembelea inakadiriwa kuwa 40,000 huku matarajio ya siku ya ufungaji ikitarajiwa kuongezeka watu 12,000 na kufikia idadi ya watu 52,000.

  Dc Mtaturu amesema kuwa Teknolojia/Bidhaa zilizooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa (JKT Kondoa) Taasisi za kitafiti ambazo zimeonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa ya kanda ya kati na udhibiti wa magonjwa.

  Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, Taasisis za elimu zimeonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.

  Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji wa Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amemshukuru mgeni rasmi Antony P. Mavunde kwa kuitikia wito wa kufunga maonesho hayo ambapo pia ameishukuru Benki kuu ya Tanzania (BOT), Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, LAPF, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Chuo kikuu cha Dodoma kwa uwakilishi na uchangiaji kwa ajili ya maonesho hayo.

  Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane Kanda ya kati Dodoma yaliyohusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yalifunguliwa tarehe 03 Agosti 2016 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ngao ya Ushindi wa pili katika kundi la Tasisi na Mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali, Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Mbeya, Julius Sang'unda wakati alipofunga Maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos makalla na wapili kulia kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Kulia ni Mwenyekiti wa TASO wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Crispin Mtono . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ngao ya ushindi wa tatu katika kundi la Tasisi na Mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Uendelezaji Kilimo katika Eneo la Ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geofrey Kirenga wakati alipofunga Maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos makalla na wapili kulia kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Kulia ni Mwenyekiti wa TASO wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Crispin Mtono

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Luteni Joseph Benedict Lyakurwa wa Suma JKT alipotembelea eneo lao na kujionea shughuli mbali mbali za kilimo na ufugaji kwenye kilele cha maadhimisho ya 23 ya sikukuu ya wakulima ya Nanenane mkoani Lindi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo Daraja la kwanza Halima Kikwega wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane , Ngongo Lindi.

  Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho 23 ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Sehemu ya Wakazi wa mkoa wa Lindi na Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Lindi.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi mikono wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho ya Wakulima Nane nane mkoani Lindi.

  ...............................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.


  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane kitaifa katika uwanja wa Ngongo Manispaa ya Lindi mkoani Lindi kwa naiba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

  Katika hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya Ngongo, Makamu wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia iwapo tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii, kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

  “Napenda kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini au itikadi za vyama vyenu.”

  Kuhusu uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane ni moja katika ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi kote nchini.

  Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.

  Makamu wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.

  Aidha amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.

  Kwa Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amehimiza wananchi kote nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami huku Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi katika hatua ya kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0

  NA VICTOR MASANGU, PWANI 

  WAFANYAKAZI wametakiwa kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanachapa kazi kwa bidii bila ya kutegeana kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo. 

  Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti mpya wa chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na afya (Tughe)Mkoa wa Pwani Catherine Katele,wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho ulioambatana na uchaguzi wa viongozi.

  Mwenyekiti huyo alisema kwamba wafanyakazi wa Mkoa wa Pwani wanapaswa pia kuachana na makundi ambayo hayana maslahi yoyote kwa taifa kwani serikali iliyopo madarakani haipo tayari kumvumilia mtumishi mzembe anayeshindwa kutimiza wajibu wake.

  “Mimi kwanza napenda kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa kuweza kuniamini na kunichagua kuwa mwenyekiti wao mpya wa Tughe Mkoa wa Pwani, lakini kitu kikubwa nawaomba tuachane na kufanya kazi kwa mazoea hii ni hatari sana na kitu cha msingi ni kila mmoja wetu atekeleze majukumu yake ipasavyo,”alisema Catherine.

  Katele,alisema kwamba katika uongozi wake atahakikishe anaweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwasaidia wafanyakazi kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuwapa moyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Aidha aliongeza kuwa ataweza mpango kazi wake wa kupita katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwapa elimu wafanyakazi kuhusina na uwajibikaji pamoja na utawala bora.

  Alisema,Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr.John Magufuli haitaki kuona mtumishi au mfanyakazi yeyote analeta masihara katika utekelelzaji wa majukumu yao hivyo ni vema kuhakikisha wanajenga misingi imara katika kucha kazi na sio vinginevyo.

  “Ni vema wafanyakazi sasa tubadili tabia zetu na tuendana na kasi ya Rais wetu, nadhani mnatambua serikali ya wamu ya tano haitaki kuona mtumishi ambaye ni mzembe kwa hivyo na sisi tujifunze ii kuepukana na kutumbuliwa,”alisema Mwenyekiti.

  Katele,alisema anatambua kuwepo kwa changamoto nyingi kwa wafanyakazi na wanachama wa Tughe kiujumla lakini kamwe wasitumie migomo na maandamano yasiyo na tija katika kudai haki zao ila ni vyema watu wakafuata utaratibu ulio sahihi.

  Alisema,mara nyingi watu wanadhani kufanya migomo ndio suluhu ya kupata haki zao jambo ambalo sio sahihi na kwamba madhara ya kufanya hivyo ni makubwa kwani wanaweza kupoteza kazi bila sababu ya msingi.

  Alisema ,kwasasa atatumia nafasi yake kushirikiana na wakuu wa idara ili kuona jinsi ambavyo wanaweza kuchukua hatua sahihi za kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki na maslahi yao kwa wakati.

  Hatahivyo,Katele amewataka wafanyakazi kutii sheria za kazi huku akiwaomba watumishi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi ili waweze kusaidiana kwa pamoja kutatua changamoto zinazowakabili.

  Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwenyekiti huyo mpya Catherine Katele alichaguliwa na kuwa mshindi baada ya kupata idadi ya kura 38.

  0 0

  Mkutano wa Kimataifa kuhusu ugonjwa wa Hemophilia limemalizika Orlando, nchini Marekani Julai 24-28, 2016. Lilikutanisha zaidi ya wadau 6,000 kutoka takribani nchi 130 duniani chini ya World Federation of Hemophilia (WFH). Hemophilia ni ugomjwa wa damu wa kurithi ambapo damu inakosa uwezo wakuganda pale mshipa unapodhurika. Huwapata zaidi watoto wa kiume. Malengo makuu yalikuwa kuboresha tiba na maisha ya wagojwa.

  Pamoja na mambo mengine, kongamano ni jukwa la kutambua jitihada zinazofanyika duniani kote hususani utafiti wa kupata tiba na uangalizi bora kwa wagonjwa. Hutengeneza jukwa na mtandao kwa wagonjwa, wazazi /jamaa, madaktari bingwa, wahudumu, watengeneza sera na watafiti wa dawa na kujenga mahusiano na baraza la kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa washiriki toka sehemu mbalimbali duniani.

  Moja ya mafanikio ni ugunduzi wa dawa (factors) zenye uwezo wa kufanya kazi mwilini kwa muda mrefu zaidi (longer half-life drugs) na hivyo maisha bora kwa wagonjwa. Pili ni upatikanaji wa misaada (donations) ya dawa kutoka makampuni yanayotengeneza dawa kwa nchi maskini. Ikumbukwe nchi hizi hazimudu kununua dawa kwa wagonjwa kutokana na bei yake kuwa kubwa. Tanzania imewakilishwa na Raisi wa Chama cha Hemophilia Bw. Richard Minja

  0 0

  With the large number of safari destinations, Tanzania has also been the best place for diving and snorkeling Its endless coral reefs in the crystalline waters of the Indian ocean offer some of the best water sport which every individual would like to enjoy during his / her tour to Marine park destinations.

  If you planned to explore the deep at the Indian Ocean, Jumia Travel shares the best Marine parks in Tanzania that would make your tour complete.

  Chumbe Island Marine Sanctuary
  It is only found in Zanzibar. The coral reef is a protected sanctuary which is famous for its coral diversity, holding 90% of the coral diversity found in East Africa. The reef is shallow enough to see everything very clearly by snorkeling or in a water mask. Chumbe has more than 200 species of hard corals which act like trees in the forest, they provide home, shelter and food to more than 440 identified fish species. You can only enjoy the park by getting a tour guide who can explain in details about all other treasures found around the areas.

  Dar es Salaam Marine Reserve
  This includes (Mbudya Island, Bongoyo and Pangavini Island).
  Dar es Salaam Marine Reserve has the potential biodiversity and richness, diving sports, snorkeling sites and Dolphin reserves. Most of the tourists enjoy these places during the weekend; a tourists can either take a small motor boat ride to Mbudya (only 20 Minutes from the mainland) or to Bongoyo which also takes 30 minutes from the mainland.

  Mnazi Bay Marine Park
  The Mnazi Bay - Located in Ruvuma, Southern Tanzania on the Mozambique Border is a home of Whales, Dolphins, Turtles and different species of Birds. The area is rocky with sandy shores and is also recognized as being internationally important due to its biodiversity with mangroves, seagrass beds and coral reefs.

  Mafia Marine Park
  Mafia Island is located 120 km South of Dar es Salaam. Mafia’s best diving is at the depth, less than 30m where you can see most kinds of tropical marine habitats. It is also surrounded by some of the richest reefs in the world, with over 50 types of corals and 400 species of fish.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Laubit Mavugo akishangilia mara baada ya kuipatia timu yake bao la Nne dhindi ya Wageni wao, AFC Leopards ya Nchini Kenya, wakati wa Mtanange wao wa kirafiki ulioambatana na sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya tangu kuanzishwa wa timu ya Simba a.k.a Wekundu wa Msimbazi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Hadi kipenda cha mwisho kilipolizwa na Mwamuzi, Heri Sasi, Simba ilikuwa ishaichakaza AFC Leopards kwa Bao 4 - 0. 
  Nahodha wa Timu ya Simba, Jonas Mkude akiangalia namna ya kumtoka Mchezaji wa Timu ya AFC Leopards ya nchini Kenya, Bernard Ongoma, wakati wa Mtanange wao wa kirafiki ulioambatana na sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya tangu kuanzishwa wa timu ya Simba a.k.a Wekundu wa Msimbazi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.Simba imeshinda 4-0.
  Mgeni Rasmi katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya Simba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiongozana na viongozi mbali mbali wa Timu ya Simba kuingia uwanjani kuwasalimia Wachezaji pamoja na Washabiki waliofurika kwa wingi uwanjani hapo.
  Msemaji wa Timu ya Simba, Haji Manara akitoka kuwasabahi mashabiki wa Simba waliofurika uwanja wa Taifa leo.
  Wanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta wakitoa Burudani uwanjani hapo.

  TIMU ya Simba imeibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya AFC Leopards kutoka nchini Kenya, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka 80 ya tangu kuanzishwa kwa timu ya Simba.

  Simba iliweza kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa ambapo dakika ya 38 Ibrahim Ajib aliipatia Simba bao la kuongoza baada ya kupokea pasi safi toka kwa Jonas Mkude na kuachia shuti la chini chini umbali wa kama mita 25.

  Kipindi cha pili Simba iliwaingiza Muzamir Yassin, Jamal Mnyate na Laudit Mavugo ambao walibadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza mashambulizi na kuwafanya mabeki wa Leopards kuwa 'bize' muda wote kupambana na washambuliaji wa simba jambao ambalo lilishindwa kufua dafu mbele ya washambuliaji hao.

  Dakika ya 55 Ajib tena anaifungia Simba goli la pili baada ya Mavugo kuichambua vyema safu ya ulinzi ya Leopards na kumrahisishia mfungaji.

  Dakika kumi baadae Kichuya alifungia Simba goli la tatu baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa kiufundi na Mavugo.

  Ilichukua kama dakika saba hivi baada ya goli la tatu, pale Mavugo alipoifungia timu yake goli la nne baada ya kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na Kichuya ambaye aliwafanya mabeki wa Leopards kuwa nae macho muda wote.

  Mashabiki wa Simba waliohudhuria mchezo huo wameonesha imani kubwa kwa kikosi chao hicho kilichosukwa chini ya Omog kwa ushirikiano na Jackson Mayanja.


  0 0


  0 0

  Mgeni Rasmi katika Shehere za kuadhimisha Miaka 80 ya Wekundu wa Msimbazi "Simba SC", Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa tano kushoto), akiwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) pamoja na Baadhi ya viongozi wa Timu ya Simba, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukata keki ya Hepi Besdei ya Simba, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Wachezaji wa Zamani wa Simba, wakiongozwa na aliewahi kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo, Mzee Hassan Dalali (kati) wakikata keki ya Hepi Besdei ya Simba, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
  Mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji "MO" akimlisha kipande ya Keki, Mgeni Rasmi katika Shehere za kuadhimisha Miaka 80 ya Wekundu wa Msimbazi "Simba SC", Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
  MO akisalimiana na Mashabiki wa Simba.


older | 1 | .... | 930 | 931 | (Page 932) | 933 | 934 | .... | 1898 | newer