Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

MHE. KAIRUKI AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUWA MFANO KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

$
0
0

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (kulia) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.Katikati ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akisikiliza kwa makini.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Victor Kitu (aliyesimama) akiwasilisha malalalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi Bw. Kamugisha Rufulenge.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wadau ili kujenga taswira nzuri ya Ofisi hiyo.

Mhe. Kairuki aliyasema hayo wakati wa kikao kazi cha robo mwaka na watumishi wa Ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Alisema, Ofisi ya Rais – Utumishi kama jina lenyewe lilivyo, inatakiwa kuwa kioo na mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za Serikali kwa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wadau wake. he. Kairuki aliwataka watumishi hao kuangalia ni kwa jinsi gani huduma wanazotoa kwa wadau zinazingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika utumishi wa umma.

“Tutoe huduma kwa kuzingatia taratibu zilizopo na uadilifu mkubwa,” Mhe. Kairuki alisisitiza. Aliongeza kuwa, wapo baadhi ya watumishi wana majibu ya hovyo sana kwa wateja, hivyo aliahidi kuwafuatilia, na iwapo wakibainika hatua stahiki za kinidhamu zitachukuliwa dhidhi yao.

Aidha, Mhe. Kairuki aliwataka watumishi hao kuwa na utamaduni wa kujisomea na kufanya tafiti mbalimbali katika maeneo wanayoyafanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. “Wapo baadhi ya watumishi hawana utamaduni wa kujisomea, wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na matokeo yake hujikuta wakishindwa kufanya inavyopaswa.” Mhe. Kairuki alisisitiza.

Mhe. Kairuki amejiwekea utaratibu wa kukutana na watumishi wa ofisi yake kila robo mwaka kwa lengo la kuzungumzia masuala mbalimbali ya kiutumishi na kiutendaji.

RC MONGELLA AZUNGUMZIA ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MWANZA.

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP.Clodwig Mtweve.

Judith Ferdinand, Mwanza
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, leo amesema, Rais Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia kesho agost 10 na 11, ambapo atapokelewa hiyo kesho wilayani Sengerema akitokea Chato mkoani Geita alikokuwa na mapumziko mafupi.

"Rais Magufuli atawasili kesho asubuhi katika mkoa wetu akitokea Chato mkoani Geita na ataanza ziara katika wilaya ya sengerema kwa ajili ya kuwasalimia wananchi, kuwapa taarifa za mikakati na maendeleo awamu ya tano pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi". Amesema Mongella.

Pia amesema hiyo kesho Rais Magufuli atasimama maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwasalimu wananchi kabla ya kuwasili wilayani Nyamagana.
Ametanabaisha kwamba Rais Magufuli ataitimisha ziara yake kesho kutwa agost 11, kwa kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza, pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi ambapo ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

Mongella amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia majira ya saa nanne mchana katika uwanja wa Furahisha ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi baada ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi.
Mwanahabari akiuliza swali
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

SERIKALI YAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI MOI

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) hawapo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi ha oleo jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenizi wa MOI Dkt. Othman Kiloloma akizungumza mbele ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) hawapo pichani kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi ha oleo jijini Dar es salaam.


Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) wakitoa kero zao mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi hao leo jijini Dar es salaam
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi hao leo jijini Dar es salaam.


Habari/Picha Na Ally Daud

Serikali chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku 14 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) Dkt. Othman Kiloloma kukaa na bodi ya taasisi hiyo kushughulikia matatizo ya watumishi ili kuleta ufanisi mzuri katika kitengo hiko.

Akizungumza na watumishi wa MOI Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemtaka Dkt. Kiloloma kukaa na bodi ya taasisi hiyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili wafanyakazi waweze kutoa huduma bora kwa watanzania.

“Naagiza Bodi ya MOI pamoja na Kaimu Mkurugenzi wake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili kuondoa malalamiko na kuleta ufanisi bora katika taasisi hii”alisisitiza Mhe. Ummy.

Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa amepokea changamoto zao na za taasisi hyo nakuhaidi kuzitatua ndani ya mwezi mmoja na kuwataka wasichoke kutoa huduma bora kwa watanzania ili kuokoa maisha yao na kupambana na umaskini.

Mbali na hayo Mhe. Ummy ameagiza watendaji wa Wizara yake kuleta mkakati wa kupambana na kupunguza ajari za barabarani hasa zitokanazo na bodaboda ndani ya siku 14 ili kuwapa nafuu madaktari na wauguzi wa MOI kuweza kuondoa mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi MOI Dkt.Othman Kiloloma amesema kuwa mbali na changamoto wanazokutana nazo wamefanikiwa kuunda upya wafanyakazi wataoweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa jumamosi na itaanza mara moja.

Aidha Dkt. Kiloloma ameongeza kuwa MOI imeweza kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 kwa mwezi kutoka kiasi cha shilingi milioni 400 kwa kipindi kilichopita.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA UTALII NA UWEKEZAJI MKOANI MBEYA

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya saa ya uzinduzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (wapili kushoto) baada ya kuzindua chama hicho jana Jijini Mbeya katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale. Watatu kushoto ni mke wa Waziri Mkuu mama Mary Majaliwa
Moja ya burudani iliyokua ikiendelea kati banda la Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) jana Jijini Mbeya katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) Bw. Venansi Matinya (kushoto) akielimisha umma uliotembelea banda la TAJATI baada ya chama hicho kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa jana Jijini Mbeya katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wananchi (hawapo pichani) walioshiriki maonyesho ya nanenane kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini jana Jijini Mbeya katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale.
Baadhi ya wananchi waliotembelea maonyesho ya nanenane wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa jana Jijini Mbeya katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (wapili kushoto) akizungumza na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI), alipowasili katika banda lao katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya. Chama hicho kilizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (kushoto) alipowasili katika banda la Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya. Katikati ni Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili
Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (wapili kulia) akitambulisha baadhi ya wajumbe wa TAJATI kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alipowasili katika banda la Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya kwa ajili ya kuzindua chama hicho
Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (kushoto) akimuonyesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa picha yenye sura ya kufanana naye iliyochorwa na mmoja wa wanachama wa TAJATI baada ya kuzindua chama hicho jana Jijini Mbeya katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale. Katikati ni mke wa Waziri Mkuu mama Mary Majaliwa

Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Mbeya

SERIKALI IMEJIPANGA KUONDOA MSONGAMANO KATIKATI YA JIJI -PROFESA MBARAWA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizinduwa safari za gari moshi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wakiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipanda katika gari moshi ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika usafiri wa gari moshi uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Safari ikiwa inaendelea katika mabehewa na baadhi ya watendaji wa TRL gari moshi kati ya Pugu leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Safari inaendelea


Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni leo jijini Dar es Salaam.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza juu huduma ya usafiri wa reli kwa wananchi wa Pugu leo katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni leo jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni leo jijini Dar es Salaam.

 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanakuwa na usafiri wa uhakika katika kuondoa msongamano wa magari mjini kwa kutumia usafiri wa gari moshi. 

Hayo ameyasema leo Profesa Mbarawa wakati wa uzinduzi wa gari moshi linalofanya safari zake kuanzia Stesheni hadi Pugu, amessema kuwa kuanza kwa usafiri huo umepunguza daladala 45. 

Amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha inapungaza kama sio kumaliza kabisa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Profesa Mbarawa amesema kuwa katika hatua nyingine wanaangalia usafiri kwa njia ya boti katika baadhi ya maeneo na wataalam walishafanya kazi hiyo. 

Aidha amewataka wafanya kazi kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama walivyokuwa wakifanya na watakaofanya hivyo hawatavumiliwa ikiwa ni pamoja na kufisadi mali za reli. 

Hata hivyo amesema waliojenga katika miundombinu ya reli wanatakiwa kubomolewa kwani kuwepo kwa nyumba hizo katika miundombinu hiyo ni kosa kisheria .Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es Salaam kuwa wataondokana na foleni kutokana na jitihada mbalimbali. 

Amesema moja jitihada hizo ni kuondoa malori ya mafuta ambapo mafuta yatasafirishwa kwa njia ya bomba mpaka Chalinze na kuanza kwa safari ya mikoani. Meya wa Jiji, Isaya Mwita amewataka wananchi kutumia usafiri huo kutokana na kutokwa na foleni na gharama yake kuwa nafuu. 

Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa usafiri wameanza kutokana na nguvu ya serikali kuwa karibu katika utoaji wa huduma ya usafiri huo.

JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

$
0
0

Timu ya Jamii Media ikitambulishwa mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bukoba.

Mtandao wa JamiiForums.com umezindua rasmi mradi wa unaowashirikisha viongozi wa kuchaguliwa(hususani wabunge na madiwani), Serikali(Halmashauri) na Wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.

Mradi huu unaotambulika kama "Tushirikishane" una malengo ya kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi.

Pia Tushirikishane inalenga kuzisaidia Halmashauri kuboresha utoaji huduma za jamii kwa ufanisi zaidi. Mwitikio(maoni, ushauri na kero) wa wananchi katika mnakasha wa Jimbo/Halmashauri utachukuliwa kwa umakini na viongozi hawa ili kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa wananchi.

Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums.com, Bwana Maxence Melo aliwapongeza viongozi wa Wilaya, watendaji wa Halmashauri, Madiwani na Mbunge kwa mwitikio mkubwa walioonyesha katika kuupokea mradi wa Tushirikishane.

Maxence aliwafahamisha kwamba Mradi huu utatekelezwa katika majimbo sita (6) kwa kuanzia na Bukoba Mjini limekuwa Jimbo la kwanza katika kuanza utekelezaji wake. Alifafanua kuwa mradi huu utachukua miezi 9 na hivyo Wabunge wanaohusika kwenye mradi huu wanatakiwa kukubaliana na wananchi juu ya ahadi zisizozidi 4 za kuweza kuwa sehemu ya mradi huu zinazoweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa mradi huo.

Bwana Maxence pamoja na timu yake ya wataalam walikuwa Bukoba Mjini kwa siku tano kuendesha warsha iliyowawezesha wadau kuuelewa mradi kwa ufasaha, kutambua majukumu yao na kujua njia zitakazotumika katika kutekeleza mradi kwa faida yao.

Warsha ya Tushirikishane ilifanyika Bukoba Hotel na wadau wanaowakilisha Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wapiga kura na wananchi wa Bukoba Mjini, Madiwani wa vyama vyote pamoja na Mbunge wa Jimbo walishiriki.

Malengo ya Tushirikishane

Pamoja na lengo kuu tajwa hapo juu, Mradi huu una malengo mahususi yafuatayo:

i. Kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi wa kuchaguliwa na serikali yao (kwa njia ya mtandao, magazeti, redio, televisheni na mikutano ya wazi)

ii. Kurahisisha upatikanaji wa habari na taarifa za umma zikiwa kwenye lugha rahisi

iii. Kuchochea majadiliano ya wazi, yenye tija na staha kati ya wananchi na viongozi wao

iv. Kusaidiana na viongozi wa kuchaguliwa katika kutengeneza nyenzo za muhimu katika kutekeleza ahadi.​

Matarajio ya Mradi

Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:

i. Kujengeka kwa utamaduni wa majadiliano yenye staha kati ya viongozi na wananchi kwenye mitandao ya kijamii

ii. Kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika utekelezaji wa sera na ahadi za wakati wa Uchaguzi.

iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa sera na ahadi za kipindi cha uchaguzi.​

Kufuatilia mradi huu, tembelea JamiiForums ( http://www.jamiiforums.com/threads/jamiiforums-yazindua-rasmi-mradi-wa-tushirikishane.1094133/ )

Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akimkabidhi kitendea kazi mwakilishi wa JamiiForums (Afisa Mawasiliano) katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bi. Happiness Essau
Mkufunzi akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.
Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura.

Diwani wa Kata ya Bakoba, Mhe. Mwakyoma akiwasilisha kundi lake juu ya Wajibu wa Mbunge kwa wapiga kura wake.


Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Mhe. Maxence Melo akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani Kalumuna(katikati) ambaye ni diwani wa Bilele(CCM) na Kabaju (kulia) ambaye ni diwani wa Kashai(CHADEMA).
Mbunge wa Bukoba Mjini, akishirikiana na wapigakura wa Jimbo lake katika zoezi la kuchambua kazi na wajibu wa mbunge kwa wapiga kura wake.

Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane katika Jimbo la Bukoba Mjini wakiwa katika picha ya pamoja.
Baraza la Halmashauri ya Bukoba, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Pamoja na Timu ya Jamii Media katika picha ya Pamoja

MPINGA CUP 2016 - RATIBA RASMI

VIJUSO VYOTE VYA MAGAZETI YA LEO HIVI HAPA


HOUSE FOR SALE IN MBEZI BEACH,DAR ES SALAAM

$
0
0

The house is on a 1033 sqm plot. Mbezi beach, near Afrikana.

It has 3 rooms, all en-suite. The master is large with a walk-in closet. Has outer kitchen and a outer pantry which can be used as laundry room. Has parking for 6 cars inside. Underground water storage and tanks.

If interested or know anyone who is, please email mukazikyoma@gmail.com for discussion.










NAIBU WAZIRI MPINA AIASA TAASISI YA MUUNGANO KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA KWA SERIKALI NA UMMA.

$
0
0

Kushoto Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipata Maelezo toka kwa Dkt. Mohammed Maalim Mtaalam wa Maabara ya Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo Zanzibar, moja wapo ya taasisi ya Muungano ililopo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naibu Waziri Mpina Yupo Mjini Zanzibar katika ziara ya kikazi.
Katika Picha ya pamoja aliyekaa kati kati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina pamoja na watumishi wa Taasisi ya ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyopo Buyu katika wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kati kati ni Dkt. Yohana Shebule muhadhiri wa ya Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, na Makamu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Profesa Mtolela wakitembea kukagua jengo jipya la taasisi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, pamoja na ujumbe wake wakisikiliza taarifa na changamoto za jengo jipya la za Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, toka kwa dkt.Yohana Shebuda hayupo pichani, wakati wa kukagua jingo hilo pamoja na kuzungumza na watumishi wa taasisi hiyo
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kushoto Pamoja na ujumbe wake.wakiendelea kukagua jengo la Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar. (Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.) 
 

Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luahaga Mpina Ametoa wito kwa taasisi za Muungano zinazofanya tafiti za kisayansi, kufanya tafiti hizo ziwe na tija kwa Serikali na Umma.

Mpina aliyassema hayo, alipotembelea taasisi ya Muungano ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo katika Wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar, iliyopo chini ya Wizara ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya Kukagua jengo jipya la taasisi hilo ambalo halijaanza kutumika ikidaiwa ni kutokana na changamoto mbalimbali pamoja na ukosefu wa samani, Naibu Waziri Mpina aliishauri tafiti za taasisi hiyo ziwe zenye malengo ya kusaidia watanzia wanaoishi katika ukanda wa pwani ili kuwawezesha kusaidia kuinua uchumi wao na kuongeza pato la taifa.

Aidha, Mpina aliongeza kwa kusema kuwa anategemea tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zitoe muongozo kwa serikali na namana ambavyo nchi inavyoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. “Hakikisheni serikali inapata taarifa zenu ili ziweke kutumika, mpo kimya sana na hamsikiki.” Alisisitiza Mpina.

Kwa upande mwingine taasisi hiyo imekuwa pia ikitoa nafasi kwa wanafunzi wageni toka katika nchi mbali mbali duniani kuja kujifunza na kufanya tafiti juu ya viumbe hai waishio baharini aina ya Pomboo (Dolphin)ili kuweza kufahamu mazingira na tabia za ndani za viumbe hao na kubadilishana uwezo na kuongeza kipato kwa taasisi hiyo kupitia malipo ya mafunzo hayo maalum. 
 
Naibu Waziri Mpina pia, alitoa Pongezi kwa taasisi hiyo kuwa na jengo zuri pamoja na changamoto wanazokabilana nazo na kuwashauri wahamie na kuanza kulitumia jengo hilo. Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar pamoja na kumuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mhe.Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, inahusisha pia kutembelea baadhi ya taasisi za muungano mjini humo. 


EVELYN MKOKOI

AFISA HABARI

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

HABARI KUTOKA ZANZIBAR 

BUZWAGI YAKABIDHI SHULE MPYA NA NYUMBA ZA WALIMU KWA SERIKALI WILAYANI KAHAMA.

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (Mwenye kofia ya blue) akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) wakati wa makabidhiano ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Budushi, wengine katika picha ni mbunge wa kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kahama Mhe.Abel Shija.
Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu na Mbunge wa Kahama Mhe.Jumanne Kishimba wakizindua majengo ya shule mpya ya Budushi iliyojengwa kwa ufadhili wa mgodi wa Buzwagi. Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na Mwenyekiti wa kijiji cha Budushi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo na nyumba moja ya walimu katika shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa Buzwagi na Watendaji wa Kata ya MwendakulimaMoja ya majengo ya madarasa yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Budushi chini ya ufadhili wa Mgodi wa Buzwagi. Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa kata ya Mwendakulima.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakati wa ziara ya kupokea miradi ya maendeleo. Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyeweka mkono kwenye mfuko wa suruali) akiwa na wajumbe wengine wa kamati ya ulinzi na Usalama wa wilaya ya Kahama walipofanya ziara katika mgodi wa Buzwagi wa kukabidhiwa miradi ya maendeleo. Meneja Mkuu wa Mgodo wa Buzwagi Asa Mwaipopo akieleza jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu. Kifaa maalumu cha kupoza umeme ambacho kitatumika kupeleka umeme katika mji wa Kahama na kungunguza tatizo la kukosekana kwa umeme kikiwa kimefungwa katika kituo cha Umeme cha mgodi wa Buzwagi.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi uliyoko wilayani Kahama, katika mkoa wa Shinyanga, umekabidhi kwa uongozi wa katika Halmashauri ya mji wa Kahama majengo ya shule mpya ya msingi Budushi yenye madarasa sita, ofisi ya walimu na nyumba moja ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia mbili.

Akikabidhi madarasa hayo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema ujenzi huo umefadhiliwa na Mgodi wa Buzwagi kwa zaidi ya shilingi milioni mia nne na themani kupitia mfuko wa Acacia Maendeleo Fund, ambao umelenga kuwapunguzia adha wanafunzi wa eneo hilo la Budushi na maeneo yanayozunguka eneo hilo kuondokana na adha ya kutembea mwendo mrefu kwenda shule.

Aidha, Meneja mkuu huyo wa Mgodi wa Buzwagi alikabidhi pia nyumba mbili za kisasa za walimu zenye uwezo wa kuishi familia nne kwa shule ya msingi Mwime hatua ambayo amesema kuwa itasaidia katika kupunguza tatizo la nyumba kwa walimu kwa shule hiyo. Nyumba hizo ambazo zimejengwa kwa kutumia teknolojia ya Tofali za kufungamana zimegharimu shilingi milioni mia mbili arobaini na nane (248,126,000/=)

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea miradi hiyo ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”.

Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.

VIJANA WENYE UFAULU WA G.P.A YA 2.5 WANAWEZA KUSOMA VYUO VYA NJE KUTOKANA NA UFAULU HUO KUKUBALIKA.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Link Education, Abdumaliki Mollel amesema hayo leo jijini Dar, kuwa vyuo vya nje viko tayari kupokea vijana wenye sifa hizo.

Mollel amesema kuwa vijana wasikate tamaa Global Link Education iko kwa ajili ya yao katika kuhakikisha ndoto zao hazipotei kutokana na kukosa nafasi katika vyuo vya ndani

Amesema kuwa wazazi waache kuogopa gharama za kusoma vyuo vya nje kwani gharama za kusoma nje ni sawa na vyuo vya ndani hivyo vijana watumie furssa hizo.

Mollel amesema ndani ya nchi mwanafunzi anachukuliwa kujiunga na elimu ya juu kwa sifa kuanzia alama D sawa pointi 4 kama mfumo mpya wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) na mfumo huo ndio utakaotuumika kwa mtu yeyote kwnda kusoma nje ya nchi

Amesema wazazi na wanafunzi wanachanganywa na mfumo huo na kutaka kuacha kutishika kutokana kuwa uwezo wao kusoma nje bado wanao.

Aidha amesema kuwa global link education inawaka vijana na wazazi kuchangamkia fursa zilizopo katika kusoma nje na mazingira ya vyuo hivyo vina uwezo naa ubora katika utoaji wa elimu katika fani mbalimbali.

Amesema kuwa wanafunzi kuwa kuna watu wamesoma masomo ya sayansi lakini kutokana vyuo vya udaktari kuwa vichache wanakosa nafasi hivyo wanashindwa kufurahi na masomo hayo ktika kuwaaletea matunda.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA KIWANDA CHA NGUO UBUNGO

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agosti 10, 2016. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Adelhem Meru na wapili kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016 . Kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing na kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016 . Kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing na kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016 . Kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing na kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016 . Kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo eneo la EPZ,Mabibo External jijini Dar es salaam baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza, Agosti 10,2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhem Meru na kulia kwake ni Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*Aagiza Wizara ya Viwanda iendeleze eneo la Mkulazi, Morogoro
*Awapakazi kazi maalum Wakuu wa Mikoa sita

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ihakikishe inaendeleza eneo la viwanda vya usindikaji mazao la Mkulazi lililopo Morogoro ili liwe kielelezo kikuu cha ukanda maalum wa kiuchumi (SEZ) unaoa mbaa sambamba na reli ya TAZARA.

Amesema wizara hiyo inapaswa ishirikiane kwa karibu na Mamlaka ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi (EPZA) pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Agosti 10, 2016) wakati akizungumza na watendaji wa EPZA na wafanyakazi wa kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo eneo la Benjamin William Mkapa, Mabibo External jijini Dar es Salaam.

Pia amewataka wakuu wa mikoa sita ya Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe kufanya kazi kwa karibu na EPZA kwa kuainisha maeneo yanayohitaji kuendelezwa kiuchumi ambayo yanafikika kwa urahisi kwa reli ya TAZARA.

“Wekeni mipango yenu kwa umakini ya kuanzishwa kwa kanda maalum za kiuchumi katika maeneo yenu ya kiutawala na mipango hii ijitokeze kwenye mipango ya maendeleo ya mikoa yenu, onyesheni mikakati ya uendelezaji viwanda inayoendana na Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo wa Taifa,” amesema.

Amewataka wakuu hao wa mikoa kuhakikisha wanaweka mfumo utakaoimarisha ulinzi wa miundombinu ya reli hiyo ili isiharibiwe na watu wenye nia mbaya.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amempongeza Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing kwa bidii aliyonayo ya kuleta wawekezaji hapa nchini. “Mwezi uliopita, nilienda Mlandizi kutembelea kiwanda cha nondo ambacho kinaendeshwa kwa ubia baina ya Tanzania na China. Pia nikaenda Mkuranga kwenye kiwanda cha kutengeneza marumaru (tiles), na leo hii tuna kiwanda cha Wachina ambacho kinashona nguo zinazopelekwa kuuzwa Marekani,” amesema.

“Nimefurahishwa kukuta asilimia 99 ya wafanyakazi humu ndani ni Watanzania, na asilimia moja iliyobakia ndiyo ya wageni na hawa wanafanya kazi za kitaalamu. Nimefurahi zaidi kukuta nguo zinazoshonwa na kiwanda hiki zimeandikwa MADE IN TANZANIA. Tena nimekuta jeans za kisasa za Levis na Wrangler ambazo zinapendwa na vijana wengi na zilikuwa zikinunuliwa nje ya nchi, lakini hivi sasa zinazalishwa hapa nchini,” amesema.

“Hii ni ishara kuwa lengo la Mheshimwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka Tanzania iwe nchi ya viwanda litatimia,” na kuongeza: “Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwa na viwanda ili tuuze mazao kama pamba, korosho, maharage ambayo yamesindikwa badala ya kuuza mazao ghafi”.

Amesema amepewa taarifa kwamba kiwanda hicho kimekwishaajiri wafanyakazi 1,500 na kitaendelea kuajiri hadi wafikie zadi ya 6,000 waaohitajika. Amewataka vijana walioajiriwa kufanya kazi kwa bidii.

Mapema, akimtembeza Waziri Mkuu kwenye kiwanda hicho, Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Bw. Rigobert Massawe alisema wafanyakazi hao wanafanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni wakiwa na saa moja ya mapumziko ya mlo wa mchana halafu wanarudi tena saa 12 jioni hadi saa 1 usiku ikiwa ni masaa ya ziada (overtime).

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Kanali (Mst). Joseph Simbakalia alisema mamlaka hiyo ilianzishwa ili kuanzisha, kuendeleza na kusimamia uanzishaji na urejeshaji wa viwanda hapa nchini.

Akitoa taarifa kuhusu mamlaka hiyo Waziri Mkuu, alisema mamlaka hiyo ilianza na mtaji wa dola za marekani milioni 22 lakini hivi imefikisha dola za marekani bilioni 4 kutina na makampuni 140 ambayo yamewekeza hapa nchini.

Kuhusu kiwanda cha kushona nguo cha Tooku, Kanali Simbakalia alisema kabla ya kuajiri, kiwanda hicho kinatoa mafunzo kwa vijana 400 ambao wanafanyiwa usaili kila baada ya miezi mitatu na wataendelea kufanya hivyo kwa makundi 10 -12 hadi wafikishe idadi ya wafanyakazi 6,000 wanaotakiwa.

Alipoulizwa na Waziri Mkuu wanatumia utaratibu gani kuwapata vijana hao, Simbakalia alisema utaratibu unaotumika ni kutuma barua ya maombi, nakala ya cheti cha kuzaliwa na barua ya mtendaji kutoka kwenye Serikali za Mitaa eneo analoishi muombaji. Alisema sifa kubwa ni kujua kusoma na kuandika.




IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMATANO, AGOSTI 10, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA.

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Mstaafu wa Shule ya Sekondari Sengerema Wilson Fumbuka Mbanga ambaye walifundisha naye shule hiyo tokea mwaka 1982-1985 mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Sengerema Mkoani Mwanza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Busisi wakati akielekea Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha MV. Misungwi wakati akielekea mkoani Mwanza. 
PICHA NA IKULU.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIVYOTEMBELEA KIWANDA CHA NGUO LEO JIJIN DAR


YONO YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA UBORA WA KAZI

$
0
0

Mwenyekiti wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Yono Kevela, akionesha tuzo za kimataifa ya ufanisi bora wa kazi baada ya kukabidhiwa.

KAMPUNI ya Udalali ya Yono Auction Mart, imekabidhiwa tuzo ya Mshindi wa Kimataifa ya Ufanisi na Ubora wa Kazi, baada ya kushindanishwa na kampuni nyingine 49 za nchi tofauti duniani hatua iliyotokana na utendaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza Jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Yono Kevela, alisema ushindi huo unatokana na ufanisi wao wa kazi zikiwepo za ukusanyaji madeni ya kodi kutoka kwa wadaiwa sugu wa serikali .

Kevela alisema baadhi ya kazi walizofanya baada ya kupata zabuni ya kukusanya madeni ya wadaiwa ni za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wizara mbalimbali, taasisi za fedha na wakala wa serikali pamoja na wadau wengine.

Alisema ushindi wa tuzo hiyo ni faida ya ufanisi wa kazi zao katika kukusanya kodi za serikali huku akiahidi kutobweteka katika jukumu hilo alilopewa na Serikali hadi kushinda tuzo hiyo na badala yake atazidi kuongeza juhudi ili kampuni hiyo izidi kufanya vizuri.

“Tunashukuru kazi na huduma zetu kutambuliwa kimataifa, tumekuwa mabalozi wazuri wa Tanzania, tumetumia fursa hiyo kuitangaza nchi na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza “, alisema. Kevela

Alisema Tuzo hiyo ilitolewa Ufaransa na sherehe za kukabidhi washindi tuzo hizo zilifanywa Juni 25, mwaka huu Rome Italia ambako kampuni hiyo imeshinda ikitoka sekta binafsi, huku upande wa serikali ukishinda sekta ya Utalii kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Kampuni hiyo ya Yono imejizolea umaharufu hivi karibuni bada ya kupewa kazi ya kukusanya madeni ya wadaiwa 24 wa TRA, yenye thamani ya Sh bilioni 18.95 baada ya wadeni hao kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana.

Hata hivyo baada ya kampuni hiyo kuanza kazi, baadhi ya wadaiwa walifanikiwa kulipa madeni yao huku wengine wakilipa kiasi na wengine mali zao walikubali zikamatwe na kuuzwa ili kulipa madeni hayo, ambapo hadi sasa zaidi ya Sh bilioni saba zimeshakusanywa.

Maeneo mengine ambayo kampuni hiyo inafanya kazi ya kukusanya madeni dhidi ya wadaiwa mbalimbali ni pamoja na maeneo ya ardhi, mahakama, mabenki na taasisi zingine.

WAZIRI WA ZAMANI WA HABARI WA CHINA AWAPIGA MSASA WAKUU WA VITENGO VYA MAWASILIANO SERIKALINI

$
0
0
 Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Zhao Qizheng akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas kitabu cha Shanghai Pudong Miracle kinachoonesha jinsi mji wa Shanghai ulivyotoka kuwa mji wa hali ya chini hadi kufikia mji wa kisasa na wenye maendeleo, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini baina ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini na Waziri huyo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng akiongea na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kuhusu umuhimu wa Serikali kuwasiliana kimkakati na wananchi na namna bora ya kuwasilisha taarifa kwa jamii, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas.
 Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhao Qizheng, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, Leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas akiongea na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi baina ya Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China Zhao Qizheng na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

GAZETI LA MSETO LATAKIWA KUMWOMBA RADHI NAIBU WAZIRI WA UJENZI MHE. NGONYANI NDANI YA SIKU 7

$
0
0
Na: Abushehe Nondo, MAELEZO

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Edwin A. Ngonyani amelitaka gazeti la Mseto kumuomba radhi na kumlipa fidia ya shilingi bilioni moja kutokana na kuandika habari ya kumchafua.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake Waziri Ngonyani amesema kuwa Gazeti hilo la tarehe 4 Agosti 2016 liliandika habari yenye kichwa cha Habari “Waziri amchafua JPM” ikimuhusisha na upokeaji wa fedha kutoka moja ya Kampuni ya Madini wakati akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

“Nimewaandikia notisi ya siku saba ikiwataka waombe radhi na kunilipa fidia, na wasipofanya hivyo hatua stahiki kuwapeleka mahakamani akiwemo Mwandishi Josephat Isango, Mwanahalishi Publisher na Mchapaji wa gazeti hilo”. Alisema Mhandisi Ngonyani.

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa habari hiyo siyo ya kweli na mwandishi ametumia nyaraka za kughushi ikiwemo barua iliyoandikwa tarehe 24 Julai na kutiwa saini yake akiwa Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO wakati ukweli ni kwamba tarehe hiyo yeye alikuwa ni Mkurugenzi kamili na siyo Kaimu kama barua hiyo inavyosomeka.

Ameongeza kuwa habari hiyo imewachafua watu wengi ikiwemo familia yake, wapiga kura wake wa jimbo la Namtumbo ambao walijitoa katika kumsaidia wakati wa kampeni na hali kadhalika zimemchafua Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumhusisha na fedha kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwaahidi kuwa mitaji yao nchini itakuwa salama.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli alishasema kama kuna mfanyabiashara yeyote aliyechangia kuingia kwake ikulu ajitokeze na hakuna aliyefanya hivyo, Iweje leo mtu tu anaibuka na kuandika habari za kugushi? ”. Aliongeza.

Aidha Naibu Waziri huyo ametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuwa waangalifu pindi wanapoandika habari za kutunga kwa kutotumia majina halisi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kanuni za uandishi wa hadithi (Habari za kutunga).

“Waandishi wa habari mnatakiwa kufuata maadili ya kazi yenu kwa kuandika habari zenye ukweli ili kuliepusha taifa kuingia katika machafuko na migogoro isiyo ya lazima” Alisema Naibu waziri huyo.

UDART NA MAXMALIPO ZAINGIA MKATABA WA PAMOJA

$
0
0

Msemaji wa Kampuni ya Mabasi ya Mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam (kushoto) Bw. Deus Bugaywa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, Katikati ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi na mwisho kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi akionesha moja ya kadi za mabasi ya mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Msemaji wa Kampuni ya Mabasi ya Mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam (kushoto) Bw. Deus Bugaywa
Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ya kufanya malipo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari namna ya kuongeza salio kwenye kadi za mabasi ya mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo.

 


DART na MAXCOM wazindua mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia mawakala wa Maxmalipo.


Na Eliphace Marwa -Maelezo

Kampuni ya Maxcom Africa – Maxmalipo kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka wamezindua rasmi Mfumo unaowezesha watumiaji wa Usafiri wa Mwendo haraka (mwendo Kasi) kuweka salio katika kadi za usafiri kupitia kwa Mawakala wa Maxmalipo popote hapa nchini.

Hivyo kuanzia sasa wasafiri wenye kadi maalumu za Usafiri (Dart card) wanaweza kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo kisha atampatia fedha taslimu yenye thamani na salio analohitaji kuweka ndani ya kadi yake na Wakala atamukea salio ambalo litamwezesha kusafiri katika mabasi ya mwendo haraka kwa kutumia kadi yake hiyo.

Akiongea kwenye uzinduzi huu Afisa Mwendesgaji mkuu wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi Amesema kuwa kampuni ya Maxcom imekuwa msatari wa mbele katia kujenga mifumo imara ya kieletroniki inayorahisisha ukusanyaji wa mapoato.

“ Lengo kubwa la kampuni ya Maxcom Africa ni kujenga na kutengeneza mifumo imara na madhubuti ambayo inalenga kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki pia kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki,” alisema Bw. Lussasi.

Naye Msemaji wa Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka Bw. Deus Bugaywa aliongeza kuwa Maxmalipo ikishirikiana na Uongozi wa mradi wa mabasi ya mwendo haraka wamekua mstari wa mbele katika kufanya uvumbuzi wa njia mbalimbali za kiteknolojia zitakazo warahisishia wasafiri pamoja na watumiaji wa mabasi haya kuendelea kujipatia huduma kwa urahisi zaidi bila usumbufu wowote.

“Naweza kuwadhihirishia kwa ushirikiano huu tulionao na Maxmalipo katika mradi huu umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwetu, barani Afrika na duniani kwa ujumla,” alisema Bw. Bugaywa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha biashara katika kampuni ya Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari, amesema kuwa Maxcom Africa ina Zaidi ya mawakala 15000 nchi nzima ambao wamewezeshwa kutoa huduma hii kwa watumiaji wa kadi hizi za mwendo haraka.

“Mawakala hawa wa Maxmalipo wapo jirani na makazi ya watu hivyo wasafiri wanaweza kujipatia huduma hii kabla ya kufika kwenye vituo vya mabasi ya mwendo haraka na kupunguza foleni za abiria kwenye vituo vya mabasi ya hasa wale wanaokua wakihitaji kuweka salio kwenye kadi zao,” alisema Bw. Lazari.

Maxcom Africa imekua ni Moja ya Kampuni za Kitanzania iliyofanikiwa katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato hapa Tanzania hasa katika miradi mikubwa ikiwamo huu wa mabasi ya Mwendo Kasi, TRA, Vivuko, Mahospitali (Moi) na kwenye Kodi za halmashauri.

MWISHO.

WAZIRI AWATAKA MAAFISA WA MAWASILIANO SERIKALINI KUFANYA KAZI KIMKAKATI

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye kipindi hiki cha Awamu ya Tano.
 
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali Waziri wa zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China, Mhe. Zhao Qizheng amesema ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yanalenga kuwainua wananchi wake.

“Msemaji wa Serikali inabidi uwe makini katika kazi zako kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati”, alisema Qizheng. Akifafanua Mhe. Qizheng amesema kuwa ili Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.

Katika kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi. Pia aliwataka Wasemaji wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zinazohusu Serikali na wananchi ili kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya haabari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas amesema ni dhamira ya Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea maendeleo.“Lengo letu ni Kuhakikisha kuwa tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa mawasiliano ya Serikali na wananchi ili kuwapa fursa ya kutoa mrejesho”alisema Abbas.

Katika kuhakikisha azma hiyo inatumia Abbas amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inajipanga kufanya maboresho ya mifumo ya Mawasiliano ya Serikali.Aidha Mawasiliano ya Serikali katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano yanalenga kubadilisha maisha ya wananchi kutoka hali duni kwenda kwenye hali bora.

Mkutano kati ya Waziri wa Zamani wa Habari wa China na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisis za Serikali umelenga kujenga uwezo wa Wasemaji wa Serikali ili waweze kuwasiliana na Wananchi kimkakati
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images