Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 91 | 92 | (Page 93) | 94 | 95 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Takwimu za wahamiaji haramu zinaonekana kupungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na takwimu za mwaka jana,  ambapo wahamiaji 200 walipatikana  na  takwimu za  mwaka huu ni wahamiaji 21 ndio waliokamatwa mkoani Iringa hadi hivi sasa.

    
  Akiongea  Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Iringa ALLY  NASSOR,amesema kuwa mkakati uliopo sasa ni  kuimarisha ulinzi na wanaendelea kupambana na wimbi la wahamiaji  haramu ambao wanatoka nchini Ethiopia.


  NASSOR  amesema kuwa kwa sasa wanahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi  wa maeneo ya ruaha mbuyuni na maeneo mengine, na kuwataka wananchi kuacha kuwaficha  wahamiaji hao haramu kwa kuwa ni kinyume cha sheria.

  Aidha ametaja changamoto ambazo zinawakabili kuwa ni pamoja na  upungufu wa vitendea kazi kama magari pamoja na rasirimali watu.

  0 0

  Watu 11 wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa kutokana na makosa mawili yanayo wakabili likiwemo la uvunjifu wa amani katika manispaa ya Iringa.


  Akiwasomea mashtaka watuhumiwa hao wakili wa serikali KASANA MANZIKU Mbele ya Hakimu mkazi mahakama ya mkoa SALOME KAYOMBO, amesema kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa mawili ambapo kosa la kwanzwa ni kufanya maandamano  bila kibali jambo ambalo ni kinyume na sheria na kosa la pili ni kuharibu gari yenye namba za usajili S.N 9323 mali ya kikosi cha zimamoto mkoa wa Iringa, kufuatia vurugu zilizotokea mnamo tarehe 19 ya mwezi huu katika eneo la mashine tatu Manispaa ya Iringa.


  Washitakiwa wote wamekana tuhuma hizo na  washitakiwa 10 wako nje kwa dhamana na mmoja kukosa dhamana,aidha kesi hiyo  imepangwa kusikilizwa tena juni 3 mwaka huu.


  washitakiwa hao walikamatwa kufuatia vurugu za wafanyabiashara wa soko la mashine tatu zilizotokea tarehe 19 mwezi huu zilizokuwa zikimuhusisha mbunge wa Iringa mjini MCHUNGAJI PETER MSINGWA.
  0 0

  Albert4
  R.I.P Mangwea
  Taarifa zilizotufikia katika chumba chetu cha habari zinasema kuwa msanii maarufu wa Bongo Fleva Albert Mangwea amefariki dunia leo hii katika hospitali ya St Hellen iliyoko South Africa, sababu za kifo chake hazijatajwa mpaka sasa, ingawa redio nyingi jioni hii zinaeleza kuwa chanzo cha kifo chake ni kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya.

  Lakini taarifa hizi hazijathibitishwa mpaka sasa, Mtandao huu unafanya jitihada ya kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Ngwea ili kujua ukweli wa taarifa ya kukumbwa na umauti.


  Taarifa hizi zimepokelewa kwa huzuni kubwa na watanzania nchini kote, jiji la Dar es salaam limeshtushwa na taarifa hizo zinazotangazwa kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii yaani blogs, Twita, n.k.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

  0 0

  Mtaalam wa sheria za kimataifa na Haki za Binadamu kutoka mtandao wa kimataifa wa wabunge wanaotetea Haki za Binadamu, Amani na Utawala wa Sheria duniani Bw. Peter Barcroft (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkutano wa wabunge walio kwenye mtandao huo jijini Dar es salaam kujadili namna watakavyounganisha nguvu zao katika kuzihamasisha na kuzishawishi nchi mbalimbali duniani kupinga na kuzuia silaha kuangukia mikononi mwa makundi ya wahalifu kwa kusaini mikataba inayozuia hali hiyo.
  Mbunge kutoka Ghana Bw. Alban Bagbin akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mkutano wa wabunge walio katika mtandao wa Kimataifa wa kutetea amani, maendeleo, utawala wa sheria na Haki za Binadamu duniani watakavyopanga mikakati mbalimbali ya kuzishawishi nchi wanazotoka kusaini mikataba inayozuia uagizaji , uingizaji na usambazaji wa silaha katika nchi zao kuyafikia makundi yasiyohusika ambayo yamekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani duniani. Takribani wabunge 22 kutoka nchi za Afrika wanashiriki mkutano huo.
  Mbunge kutoka Sierra Leone Bernadette LAHAI akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) athari zinazosababishwa na silaha kuangukia katika mikono ya wahalifu hasa katika bara la Afrika na kuwa chanzo cha machafuko na kukwamisha maendeleo ya wananchi. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

  0 0

  Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule  ya msingi migori katika kijiji cha migori, aliyefahamika kwa jina la GANJA TWANGA (12), amefariki baada ya kutumbukia katika bwawa la mtera.


  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa MICHAEL KAMUHANDA amesema kuwa mtoto huyo amefariki dunia mnamo tarehe 25 mwezi huu, majira ya  saa 11:30 jioni wakati akichunga ngombe pembezoni mwa bwawa hilo.


  Katika tukio jingine KAMUHANDA amesema kuwa mnamo tarehe 24 mwezi huu majira ya saa 5:25 mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi mangalali CONJESTA KINDOLE (13), amefariki dunia baada ya kuchapwa viboko na STEPHANO  KUNOGELA (52) mwalimu wa shule hiyo.


  KAMUHANDA ameongeza kuwa mtoto huyo amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa manispaa ya iringa na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo.

  0 0

  Wakizindua program ya Airtel Rising Stars 2013 Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Dar es Saalam Almasi Kasongo wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars 2013.
  Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo , wengine ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo(katikati) na Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu.
  Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo akikazija jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye halfa ya uzinduzi wa program ya Airtel 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni
  Baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012 wakisalimiana na Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo

  Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012.


  ========  ======= ========
  Airtel yazindua michuano ya Airtel Rising Stars 2013

  Airtel Tanzania leo imezindua michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Airtel imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kudhamini mashindano hayo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) pamoja na serikali kukuza vipaji vya soka nchini Tanzania.

  Huu ni mwaka wa tatu mfululizo tangu kampuni ya airtel ianze kudhamini mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo huanzia ngazi ya mkoa hadi Taifa. Fainali za Airtel Rising Stars Taifa hufatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa kwa wachezaji nyota chini ya ukufunzi wa makocha mahili wa vijana kutoka klabu ya Manchester United.

  “Nafurahi kwamba tumepiga hatua na leo tunazindua msimu wa tatu wa Airtel Rising Stars ambao bila shaka utakuwa wa ushindani na wa kusisimua”, alisema Beatrice Singano, Mkuu wa Idara ya mawasiliano ya Airtel Tanzania. Uzindinduzi huo ulifanyika katika ofisi za TFF. Singano alisema: “Airtel imevutiwa na mwitikio wa vijana wengi waliojitokeza kujiandisha na kushiriki katika mashindano ya Airtel Rising Stars katika miaka iliyopita. Ni matumaini yetu kwamba vijana wengi zaidi watajitokeza kushiriki mwaka huu”.

  Singano alisema mpango huu kabambe unawalenga wasichana na wavulana nchi nzima ili kuwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwa mawakala wa soka, makocha na mamlaka nyingine zinazohusika na programu za kuendeleza vipaji vya soka. Mwaka huu Airtel Rising Stars itajumuisha jumla ya timu 24 za wasichana na wavulana kutoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Morogoro, Ilala, Kinondoni Temeke, Kigoma, Tanga na Ruvuma ambao baadhi yao watateuliwa kuunda timu za mikoa yao katika fainali za Taifa. Vile vile mashindano ya Taifa yatatumika kuteua timu itakayoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa (inter-country tournament)

  Akizunguma katika hafla hiyo, mgeni rasmi Mkurugezi wa Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na Airtel kuwekeza kwenye programu ya soka ya vijana ambao ndiyo nguzo mhimu kwa maendeleo ya mchezo wa soka nchini. Kauli yake iliungwa mkono na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF Bw Basibu Ramadhani ambaye alisema program za soka za vijana ndio njia pekee ya kuinua kiwango cha soka nchini.

  “Tumeshudia vipaji vingi katika mashindano yaliyopita na bila shaka michuano ya mwaka huu yataendelea kutoa vipaji vingine vingi. Natowa wito kwa timu kubwa hapa nchini kutumia fursa hii kupata wachezaji chipukizi kwa ajili kuimarisha timu zao. Nawatakia washiriki wote mashindano mema na wazingatie nidhamu na taratibu ya mchezo wa soka.” alisema Thadeo. Programu hii ya Afrika inaungwa mkono na klabu kubwa ya Manchester United kwa lengo la kubaini vipaji vya soka na kuviendeleza ili kuweza kuonekana kwa mawakala, makocha na kupata nafasi ya kutambulika kitaifa na kimataifa.

  Ushirikiano wa Airtel na Manchester United katika kuendeleza soka ya vijana ni utekelizaji wa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya pande hizo mbili mwezi Disemba 2010 ambayo yanaiwezesha Airtel kutumia hazina ya ufundi wa soka kutoka klabu hiyo kubwa duniani kuendeleza vijana chipukizi barani Afrika. Vijana wanaoshiriki Airtel Rising Stars mwaka huu hapa nchini wanatajiwa kuanza kujiandikisha mwezi ujao na jumla ya timu 24 kutoka mikoa 9 zitashiriki. 

  Airtel ni kampuni ya simu za mikononi inayofanya biashara barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Democratic Republic of Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Tanzania, Uganda, na Zambia.


  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti Steve Gannon, katika picha ya pamoja na viongozi wa mtaa wa Chang`ombe `B’ baada ya kutembelea kiwanda cha bia cha Serengeti jana jijini Dar es Salaam.  
    Mtaalamu wa mtambo wa kudhibiti maji taka Simon Peter kutoka kampuni ya bia ya Serengeti akitoa maelekezo kuhusu namna mtambo huo unavyofanya kazi katika namna ya utunzaji wa mazingira

   Mtambo wa kudhibiti maji taka na kuua kemikali.
    Mfanyakazi wa kiwanda cha Serengeti akimuonesha mwenyekiti wa Chang’ombe` B’ aina ya ngano inayotumika katika utengenezaji wa vinywaji vinavyozalishwa kiwandani hapo.
    Mwenyekiti wa mtaa wa Chang`ombe `B’ Ahmad Khadil akizungumza na wana habari kwa niaba ya viongozi wenzake mara baada ya kutembelea mtambo wa kusafisha maji taka na kuua kemikali ndani ya kiwanda cha Bia cha Serengeti jana jijini Dr es Salaam.

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM, kwenye Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo May 28, 2013. Kinana ambaye yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katiobu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.


  Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Mei 28, 2013 katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoani Njombe.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo May 28, 2013. Kinana ambaye yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katiobu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
  Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Ludewa na Vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, uliofanyika  katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo Mei 28, 2013. 
  Sehemu ya umati wa watu wakishangilia jambo wakati Nduhu Kinana alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo Mei 28, 2013.
  Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikujombe akizungumza na wananchi  wa Ludewa na vitongoji vyake waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo May 28, 2013.Mbunge huyo aliwaeleza wananchi kuwa kwa sasa jimbo lake limepata fedha kwa ajili ya kujenga minara mitatu ya mawasiliano kwa ajili ya kuepuka kero ya mawasiliano mkoani humo,aidha aliyataja maeneo hayo kuwa ni Lupingu,Makonde pamoja na Madope .Mh Deo aliongeza kufafanua suala la ujenzi wa barabara,alibainisha kuwa suala la ujenzi wa barabara unaendelea vizuri kwani tayari serikali imekwisha mtengea fedha kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 10 za lami kwa ajili ya Wilaya ya Ludewa,akaongeza kuwa Serikali imemtengea kiasi cha fedha Bilioni 1.2 kwa ajili ya kutatua tatizo la maji kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa. 
  3Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa mpira wa mjini Ludewa .
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa shina la CCM tawi la Itunda kata ya Malangali mapema leo,alipotembelea mashina kadhaa kwa kuzungumza nao mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.
  Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia katika kijiji cha Malangali mapema leo mchana.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amembatana na ujumbe wake wakitembelea mashina ya chama hicho sambamba na kuzungumza na wanachama katika tawi la Itunda kata ya Malangali mapema leo,kwa madhumuni ya kuyakagua mashina hayo na kuimarisha chama.
  Baadhi ya Wanachama wapya wapatao 60 walijiunga na CCM katika kijiji cha Malangali,pichani baadhi yao wakila kiapo.

  0 0  Mabomba ya  usambazaji maji katika jiji la dare s salaam, na Pwani umeanza kutoka mtambo wa ruvu chini Bagamoyo  hadi katikati ya jiji la Dar es salaam, mradi ambao utagharimu shilingi bilioni  184. 05 ili kuongeza lita milioni 756 kutoka lita 300 za sasa katika Jiji Dar es Salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo katika huduma ya maji. Picha na Athumani Shomari

  0 0  Kutokana na habari za kufariki kwa mwanamuziki Albert Mangwair, msanii ambaye ni mmoja kati ya wana Hip Hop maarufu nchini, Mwanamuziki mwingine pia wa Hip Hop Hamis Mwin'jumah, a.k.a MwanaFA (Pichani) na ametangaza kuahirisha show yake ya The Finest iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii May 31, 2013.


  MwanaFA ameiambia Mdimuz Blog kwamba kuguswa kwake na taarifa hizi kumesababisha ajisikie kuomboleza kwanza, kabla maisha mengine hayajaendelea, kwa hiyo amewaomba radhi mashabiki, hasa wale waliokuwa wameshanunua tiketi, na kuwaomba wawe na subira, tarehe ya show itratangazwa tena baada ya mwili wa marehemu kuletwa na kupumzishwa.Habari kwa hisani ya Mdimuz Blog.

  0 0
 • 05/28/13--15:48: DONT MISS THE SHOW.!


 • 0 0
 • 05/28/13--20:00: haya ni majangaaa sasa .!


 • 0 0

  Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo linalotarajia kufanyika Juni 7,mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya kawaida ni Sh. 10,000. Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa www.sufianimafoto.com, kinywaji cha Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.

  0 0

  IMG_0267   

  Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.
  IMG_0269Mgeni rasmi Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara huo.
  IMG_0271
  Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akielekea kuweka shada la maua kwenye maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
  IMG_0274
  Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiweka shada la maua kwenye mnara huo.
  IMG_0281
  Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa kwa niaba ya Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka Askari wa kulinda Amani wa Umoja wa mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
  IMG_0284
  Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akitoa heshima zake mara baada ya kuweka shada la maua.
  IMG_0224
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye Mnara wa Mashujaa viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja viongozi wa dini. (Picha na Dewji Blog).
  IMG_0169
  Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiwasili kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam kushiriki kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.
  IMG_0231
  Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi, Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan na Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwa wimbo wa mataifa kwenye maadhimisho hayo.
  IMG_0259
  Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi akielekea kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka askari wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.
  IMG_1145
  Mmoja wa askari wa JWTZ akipendisha bendera ya Umoja wa Mataifa kama ishara ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja huo wanaolinda Amani katika nchi mbalimbali za Afrika.IMG_0433
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya kuwakumba Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
  IMG_0374
  Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Kazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dk. Alberic Kacou kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.


  IMG_0389
  Zainab Abdallah moja ya Vilabu vya Umoja wa Mataifa akighani shairi wakati wa maadhimisho hayo.
  IMG_0406
  Baadhi ya Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.
  IMG_0407IMG_0192 
  Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania Bw.George Otoo (wa pili kulia) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (kulia) wakiwa na baadhi ya maafisa mbalimbali wa jeshi la Tanzania wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho hayo.
  IMG_0394
  Kushoto ni Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na baadhi ya mabalozi na maafisa mbalimbali wa jeshi nchini.
  IMG_0330 
  Baadhi ya Askari Wanawake wa Vikosi vya Kulinda Usalama wa Tanzania wakiimba wimbo maalum wa kuhamasisha Amani katika maadhimisho hayo.
  IMG_0464
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akipeana mikono na Askari Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani kutoka Tanzania kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
  IMG_0487
  Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akisalimiana na Askari wa Kulinda wa Umoja wa Mataifa waliohudhuria maadhisho hayo leo jijini Dar es Salaam.
  IMG_0542
  Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani kutoka Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
  IMG_0248
  Wananchi wakitazama yaliyokuwa yakiendelea wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya askari wa kulinda usalama wa Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
  IMG_0554
  Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akibadilishana mawazo na mmoja wa askari wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.
  ====== ======== ======
  Tanzania imesema shughuli ya operesheni za kulinda amani katika mataifa yenye mvutano wa kivita barani Afrika zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upelekwaji wa wanajeshi na udhibiti wa rasilimali na utoaji wa maamuzi.

  Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar e s Salaam, Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi amesema tunapoadhimisha siku hii pia tunawakumbuka raia, askari na wapiganaji zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha tangu mwaka 1948 wakiwa katika zoezi la kulinda amani.

  Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alberic Kacou amepongeza vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania na Polisi wa Usalama wa Raia kwa kuandaa tukio hilo la kumbukumbu ya walinda amani wa Umoja wa mataifa wake kwa waume waliopoteza maisha yao.

  Amesema katika siku hii ya kimataifa, tuitumie kuwakumbuka walinda amani zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha na kuwaunga mkono askari zaidi ya 111,000 waliopo na wanaoendelea kulinda amani katika nchi mbalimbali zilizo na migogoro.

  0 0

  Kutokana na vitendo vya kikatili wa kijinsia vya mauwaji ya wazee kwa fikra potofu za kishirikina vinavyoendelea nchini,Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Iringa  GASPEL NSANYI akemea vikali  tabia hiyo.


  Akiongea na nuru fm afisa maendeleo ya jamii NSANYI amesema kuwa watu wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi kwa kuhisi mtu flani mchawi kwa kigezo cha macho mekundu na uzee.


  NSANYI amesema kuwa matukio ya mauaji ya kikatili kwa vikongwe kwa sasa hayapo katika manispaa ya iringa ila manispaa inakabiliwa na tatizo la unyanyaswaji wa watoto .


  SANYI ameitaka  jamii kuachana na vitendo hivyo kwani kila binadamu ana haki ya kuishi na kupata haki zote zamsingi.
  0 0

  Afisa elimu wa shule za msingi katika manispaa ya Iringa ANGELUSI KISIGA  amezitaja changamoto ambazo zinawakabili katika kukuza kiwango cha ufaulu kwa shule za msingi kama ufuatiliaji duni wa walimu wakuu katika mchakato wa kujifunza na kufundisha walimu na wanafunzi.


  Akizungumza leo,Afisa huyo amesema kuwa walimu kuwa na mlundikano wa vipindi vingi vya kufundisha,mchakato wa kujifunza na kufundisha kutotekelezwa ipasavyo kati ya walimu na wanafunz,wazazi na mazingira ya shule ni chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu.


  Amesema kuwa kutokana na hali hiyo walimu wa shule za msingi katika manispaa ya Iringa waliamua kujiendeleza na Kiwango chao cha  elimu kufikia daraja la tatu A na wengine wamejiendeleza kufikia kiwango cha stashahada na shahada ambapo hupelekea ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa shule za msingi.


  Amesema kuwa walimu wa shule za msingi wanashindanisha wanafunzi kitaaluma kuanzia ngazi ya shule,kata na wilaya mpaka  mkoa ili kuweza kupima uwezo wa wanafunzi wao.  Pamoja na hayo amesema kuwa wanamikakati ya kupunguza changamoto hizo ikiwemo kufanya ukaguzi na kuendesha mafunzo ya mbinu bora za ufundishaji wa masomo ya kiingereza na hisabati na kufanya uchambuzi wa mihtasari na maada ili kubaini maeneo magumu ya kufundisha na kujifunza kwa walimu na wanafunzi.  WAKATI HUO HUO.....

  Serikali kupitia wizara ya elimu imeahidi kutangaza matokeo ya kidato cha nne hivi karibuni kutokana na matokea mabaya kwa mwaka huu wa 2012.


  Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Tanzania MH: PHILIPO AGUSTONO MULUGOamesema kuwa watoto hao hawajachelewa masomo yao kwani serikali ina mipango mizuri katika kuboresha secta ya elimu hapa nchini. Mulugo ameyasema hayo katika kata ya mbalamaziwa wilaya ya mafundi alipokuwa anapita kuelekea jimboni kwake chunya mkoani mbeya.

   Ameongeza kuwa serikali kupitia wizara hiyo ya elimu ipo katika mikakati ya kuboresha miundombinu kwa waalimu ili kurahisisha utendaji wao wakazi na kuhakikisha secta ya elimu inasonga mbele hapa nchi.

  0 0  0 0


  Tarehe kama hii, miaka mitano uliyopita,mama mpendwa Adelina Mapango, uliagana nasi. Nikisema 'uliagana nasi' inaweza kutafsiriwa kana kwamba ulipata nafasi ya kutuaga.Nilikuja huko nyumbani kukuuguza Februari 2008, lakini tangu nilipokuona pale Muhimbili hadi tarehe 29 Mei 2008 hukuwahi japo kuniambia neno moja la mwisho.Nakumbuka ulivyokuwa ukiniangalia kwa upendo wako mkubwa,nakumbuka pia tabasamu lako licha ya maumivu makubwa uliyokuwa nayo.Lakini kila nilipojaribu angalau kusikia neno lako moja tu,haikuwezekana hadi siku unafariki.

  Mama mpendwa, kabla ya kifo chako sikuwahi kuelewa maana ya kufiwa na mzazi au mtu wa karibu.Sasa sio tu naelewa bali kila siku ya Mungu tangu siku ulipotutoka imekuwa kama ndoto mbaya ambayo natamani iishe ili hali irejee kuwa kama zamani.Kwa bahati mbaya, ndoto hiyo mbaya ni ukweli (hali halisi), na hadi sasa matarajio kuwa kuna siku nitaamka na kukuona au kukusikia ukiwa hai yanazidi kufifia.Kwa kifupi,mama mpendwa,hadi leo bado napata shida kuamini na kukubali kuwa haupo nasi.

  Nyakati mbili ngumu zaidi kwangu ni wakati ninapofanya sala kabla ya kulala ambapo wakati wa uhai wako nilikuwa nikisali "Ee Bwana uijalie familia yangu yani Baba na Mama..." lakini sasa inabidi nimtaje Baba pekee.Pia wakati wa uhai wako,nilijenga utaratibu kwamba nikipiga simu naanza kuongea na Baba kisha anapitisha simu kwako tunaanza kutia stori mbalimbali.Sasa,mama,nikimaliza kuongea na Baba huwa najikuta nasahau kuwa haupo hapo nyumbani,na kumwambia Baba akupe simu...then nakumbuka haupo.Naishia kutoa machozi.

  Nikiwa mbinafsi,nitaangalia tu jinsi ninavyopata shida kukabiliana na ukweli kuwa hauko nasi.Lakini kuna rafiki yako kipenzi Baba Mzee Chahali ambaye yeye amekuwa mtu tofauti kabisa tangu ulipoondoka.Kama unavyokumbuka,baba ni mtu mkimya,mwenye marafiki wachache, na rafiki yake mkuu ulikuwa wewe.Sasa tangu uondoke,baba amekuwa mnyonge kupita kiasi.Kibaya zaid, ameendelea kudai labda yeye ndio angestahili kutangulia mbele ya haki kwa vile alikuwa amekuzidi kiumri.Kwa hakika, baba ameendelea kuwa katika wakati mgumu sana licha ya sapoti kubwa tunayompatia.

  Lakini pia kuna rafiki zako wapenda Kulwa na Doto (Peter na Paul). Pengine kwa vile wao ni last borns, walikuwa wakikuchukulia zaidi ya mzazi, ulikuwa kama bibi yao, shangazi yao, na kikubwa zaidi, rafiki yao.Kila ninapoongea na wadogo zangu hawa najiskia kutokwa na machozi.Kimsingi, sidhani kama waliwahi kuwaza kuwa na maisha bila ya uwepo wako mama.

  Familia yote kwa ujumla inakukumbuka sana mama.Nina mkanda wa video niliowarekodi wewe na baba mlipokuwa mnaadhimisha miaka 50 ya ndoa yenu mwaka 2005,lakini kila nikijaribu kuuangalia najikuta nabubujikwa na machozi.Katika mkanda huo uliongea mambo mengi ya msingi kuhusu maisha.Kuna nyakati nataka kuuangalia ili nirejee wosia wako lakini nashindwa kwa sababu ya uchungu.

  Mama nilikupenda sana,ninakupenda sana,na nitaendelea kukupenda milele.Kwangu, japo hupo nasi kimwili,lakini unaendelea kuishi nasi kiroho.Nitazidi kukukumbuka kwa sala kila siku,na ninaamini huko uliko unapata faraja kila ninapotenda mambo kwa kuzingatia mafundisho yako.

  WE MISS YOU SO MUCH MAMA MPENDWA

  PUMZIKO LA MILELE AKUPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE AKUANGAZIE UPUMZIKE KWA AMANI AMINA

  0 0   Mambo  PUBLISHERS  ni  waandishi,watayarishaji  na  watoaji  wa
  vitabu  mbalimbali  vya  ziada  na  kiada. Tunapenda  kuwatangazia
  vijana  wa  kitanzania, nafasi  za  kazi  ya  usambazaji  wa    vitabu
   kwa  wateja  wetu wa  jumla  na  reja  reja  waliopo  katika   kata
  na  vitongoji  vyote    jijini  Dar  Es  salaam.

  SIFA  ZA  MWOMBAJI:
  1. Umri  kuanzia  miaka  18  hadi  45.

  2. Elimu  Kuanzia   kidato  cha  nne, sita  na  kuendelea.

  3. Awe  mkaazi  katika  mojawapo  kati  ya  kata  zilizopo  jijini
  Dar  Es  salaam.

  4. Awe maridadi, mwaminifu, anaye  jituma   na  anaye  weza  kufanya
  kazi  kwa  kujisimamia.

  5. Awe  na  uwezo  wa  kuchukua   kuanzia  nakala  TANO na  kuendelea
  kwa  bei  ya  jumla  ya  SH. ELFU  TATU  NA  MIA  TANO ( Tshs. 3,500
  /=)   kwa  nakala.


                                               MAJUKUMU   YA  KAZI

  Kuchukua  vitabu   kwetu  na  kuviwasilisha  katika  duka  la  vitabu
  , duka  la  bidhaa  ama  kituo  chochote  cha  mauzo   kilichopo
  katika  kata  anayoishi.

                                              MALIPO  KWA  MAWAKALA

  Mawakala  watakuwa  wakilipwa  kamisheni   kwa  kila    kitabu
  kitakacho  wakilishwa   kwenye  duka  husika  ama  kituo  cha  mauzo
  husika.

                                                     UTARATIBU   WA  KUANZA  KAZI
   Fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI
  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  kuanzia  siku  ya  Alhamisi  ya  kesho
   tarehe  30 MEI  2013  saa  tano  kamili  asubuhi  ukiwa  na  barua
  yako   ya  maombi, CV, passport  size  mbili  za  rangi   na  kiasi
  cha  kuchukua  kuanzia  nakala  tano  kwa  bei  ya  jumla  kwa  bei
  ya  sh. ELFU  TATU  MIA  TANO ( Tshs. 3,500/=) kwa  nakala.

                                                   AU

  Tuandikie  maombi  yako  kwa  njia  ya  barua  pepe  yetu  ambayo  ni

  Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  10 JUNI  2013.  Kwa  maelezo  zaidi, wasiliana  nasi  kwa   SIMU   0782405936.


  KWA   MAELEZO  ZAIDI  KUHUSU  MRADI  HUU, TAFADHALI  TEMBELEA ;


  0 0


  Abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi la kampuni ya Ukinga maarufu kama Japanese lililokuwa likitoka mkoani Mbeya kwenda Ikonda Makete wameonja adha ya safari yao kwa mshituko mkubwa mara baada ya askari wa usalama barabarani waliokuwa njia panda ya Matamba kufyatua risasi hewani muda mchache baada ya kulisimamisha basi hilo

  Tukio hilo la aina yake limetokea baada ya askari kutoka kituo kidogo cha polisi Matamba wilayani Makete mkoani Njombe kulisimamisha basi hilo kama ilivyo kawaida ili kufanya ukaguzi ambapo baada ya ukaguzi ilionekana basi hilo lenye namba za usajili T 446 CHG limebeba abiria kupita kiasi

  Kufuatia hali hiyo, askari alilazimika kuzuia basi hilo kuendelea na safari huku akitaka abiria waliozidi kushuka na kutafutiwa usafiri mwingine pamoja na wahusika wa basi hilo(dereva na kondakta) kulazimika kulipa faini kutokana na kosa la kuzidisha abiria walilolifanya, ambapo kuliibuka malumbano kati ya dereva na askari hao wa usalama barabarani

  Akijitetea mbele ya askari kuhusu kosa la kuzidisha abiria alilolifanya dereva huyo ambaye jina lake mwandishi wetu hakufanikiwa kulipata kutokana na hali halisi iliyokuwa eneo hilo, alimsikia dereva huyo akikiri kupakia abiria zaidi ya kiwango lakini akisema miongoni mwa abiria hao waliozidi ni wagonjwa pamoja na wengine walikuwa wanawahi msibani

  “afande kutokana na hali hiyo tunatambua kweli tumekosea abiria tumewajaza na kama unavyojua mazingira ya huku Makete abiria ni wengi lakini magari ni machache na kama tusingewabeba ni ngumu kwao kufika Ikonda hospitali kwa matibabu kwa kuwa gari ni hili moja tu” alisema

  Maelezo hayo hayakufua dafu mbele ya askari na badala yake aliwataka kulipa faini ya kosa hilo ili iwe fundisho kwa wengine hali iliyowalazimu abiria waliokuwa kwenye basi hilo kushuka chini kujua kulikoni huku wakiwataka askari kuwaruhusu kuendelea na safari, na ndipo askari hao walipofyatua risasi hewani kama njia mojawapo ya wao kujihami kutokana na wingi wa abiria hao.

  Akizungumza na ripota wetu mmoja wa abiria aitwaye Ester kutoka Tukuyu aliyekuwa akielekea Ikonda hospitali kwa matibabu amesema wao kama abiria walimfuata askari na kumwambia kuwa wanaomba wawahishwe kutibiwa wao wachukue namba za gari waje kuwaadhibu baadaye lakini alishangazwa na askari kuanza kufyatua risasi hewani

  Mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi anaruhusiwa kufyatua risasi pale anapoona maisha yake yapo hatarini kama njia mojawapo ya kujinasua na hatari iliyopo mbele yake

  Amesema kilichosababisha mtafaruku huo ni kitendo cha askari huyo kumtoza faini ya shilingi 30,000/= dereva na kondakta wa basi hilo, ambapo kondakta alidai kuwa hana hela jambo ambalo halikuwaingia kichwani askari hao, na kugoma kuliruhusu gari hilo hadi pale watakapolipa faini ya kosa la kuzidisha abiria

  “Katika hali ya kawaida si rahisi kondakta kusafiri na gari tena la abiria bila kuwa na hela, hivyo kutokana na kukaa muda usiozidi dakika 15 wa mabishano abiria waliposhuka na kutaka kumfuata askari Yule mwenye silaha, aliwakataza abiria wasimfuate lakini alipoona wanazidi kumfuata, aliamua kufyatua risasi hewani kama njia ya kuwatawanya, na baadaye kondakta alilipa faini hiyo na gari likaruhusiwa kuondoka” alisema SP Kaiza

older | 1 | .... | 91 | 92 | (Page 93) | 94 | 95 | .... | 1897 | newer